Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MBOWE AAMUA KUTOA YA MOYONI KUONDOKA KWA LOWASSA CHADEMA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

BAADA ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kuamua kurejea Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema kwa kuwa ameondoka basi akawe mkweli huko alikokwenda. 

Lowassa wakati wa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aliondoka CCM na kwenda Chadema ambapo wakati wa mapokezi yake Mbowe alisema amebadili gia angani. Hivi karibuni Lowassa alirejea CCM akisema amerudi nyumbani. 
Akizungumza leo Machi 16,2019 jijini Dar es Salaam Mbowe amesema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakimuuliza kuhusu msimamo wa Chadema baada ya Lowassa kuondoka. 

"Chama chochote cha siasa kina wajibu wa kujenga chama ikiwa pamoja na kuongeza wanachama na katika kuongeza huko wanachama tulimuongeza na mzee Lowasaa mwaka 2015.Nataka kulizungumza kwa kifupi sana, vyama vyetu vya siasa vinavuna watu mbalimbali, wapo wema, wapo wasio wema, wapo wanaopenda madaraka, wapo kila mmoja kwenye roho yake anajua anataka nini katika siasa, hapa mezani huenda tunaajenda tofauti. 

"Tutumie karama zetu kwa namna ambavyo Mungu ametujaalia kupinga uovu , kulaani yasiyo ya haki, kupigania haki na usawa.Ukiona kuna mambo mengi yanatokea halafu mtu yuko kimya ni bora akishindwa kuwa na sisi basi usiwe na sisi.Mheshimiwa Lowassa nilisikitika kwasababu tulimpokea kwa nia njema sana,"amesema. 

Ameongeza kwa kuwa ameondoka na kwenda CCM basi akiwa huko kwenye Chama chake kipya awe mkweli kwa kuwaambia yale yanayoonekana hayako sawa huku akifafanua Chadema haiko tayari kuona damu inamwagika kwa sababu ya kutafuta madaraka. 

RIDHWANI PANGAMAWE ALIPENDA KINANDA AKIWA ‘KINDA’.

$
0
0
Na Moshy Kiyungi

Mpenzi wa bendi ya msondo ngoma hupatwa na faraja kubwa pindi akimuona mwanamuziki Ridhwani Pangamawe, akiwa kashikilia gitaa jukwaani.


Wasifu wa Ridhwani unaeleza kuwa alianza kupiga muziki katika bendi ya Juwata, akiwa na umri mdogo wa miaka 15 mnamo mwaka 1979.

Muziki haukumuijia kama miujiza, ila yeye alizaliwa katika familia iliyokuwa ya wanamuziki.

Ridhiwan alinaeleza kwamba baba yake mzee Pangamawe alikuwa mwanamuziki katika bendi iliyokuwa maarufu pale Iringa mjini, iliyoitwa Highland Stars.Bendi hiyo ilitikisa mjini humo kwa muziki maridadi ilivyokuwa ikiporomosha, hasa mwishoni mwa miaka ya 1970.

Mazoezi ya wanamuziki wa bendi hiyo yalikuwa yakifanyika nyumbani kwao hata mama yake pia alikuwa anaweza kupiga gitaa.Pangamawe aliaanza kuonesha kipaji cha kupiga kinanda akiwa bado mdogo sana wa umri kama miaka mitano ambapo kaka yake Zuberi Pangamawe alimkuta kwa mara ya kwanza akipiga kinanda.

Alikiri kuupenda muziki tangia akiwa bado ‘Kinda’, alisema hata kaka yake, Zuberi, aliyekuwa mfanyakazi wa RTC pale Iringa, alikuwa anajua kupiga gitaa.Ridhiwani alisimulia kwamba kinanda hicho alikuwa akipenda kupiga kila aliporudi shule hata ule wakati wa mchana, alipokuwa akirudi kula chakula cha mchana, ilikuwa lazima aguse kinanda. Tabia ambayo hadi leo bado anapenda kufanya mazoezi sana.

Pangamawe baada ya kumaliza shule ya msingi Iringa, alikwenda jijini Dar es Salaam, akiwa na nia ya kuendelea na masomo ya sekondari.Wakati akiwa hapo Dar es Salaam, kaka yake aliwamtaarifu kuwa wajomba zake ambao ndio walikuwa wenyeji wake, akamwambia kuwa Ridhiwani ana uwezo wa kupiga kinanda.

Kipindi hicho hicho Waziri Ally ‘Kisinger’, alikuwa ameiacha bendi ya Juwata, nakarudi kwenye bendi yake ya awali ya The Revolutions sasa Kilimanjaro Band ‘Wana Njenje’.Bendi ya Juwata ikawa na pengo la mbofya kinanda kwakuwa takriban bendi zote kubwa zilikuwa na mpiga kinanda wakati huo.

Msondo walianza mkakakati wa kutafuta mpiga kinanda, ambapo wapiga vinanda kadhaa mashuhuri wa wakati huo walijaribu bahati zao kujiunga na bendi hii wakiwemo Kassim magati na hata Ally Tajruna ambaye alipigia bendi hiyo kwa mwezi mzima.

Wajomba zake Ridhwani, ambao walikuwa wapenzi wakubwa wa Msondo, wakiishi jirani na mzee Joseph Lusungu. Lusungu wakati huo alikuwa mmoja wa viongozi wa bendi hiyo ya Juwata na pia alikuwa mpulizaji hodari wa tarumbeta.Walimfuata mzee huyo na kumtaarifu kuwa wana mdogo wao ambae anaweza kupiga kinanda. Lusungu akawaeleza kuwa apelekwe kwa ajili ya usaili.

Ridhwani akakaribishwa Juwata ili kufanyiwa usaili chini ya msimamizi wa usaili wa mzee Kassim Mponda.Kwa kuwa hapo awali hakuwahi kugusa kinanda kinacho tumia umeme, hivyo alibabaika kidogo.Kabla ya hapo alikuwa akitumia kinanda cha kujaza upepo.Lakini hekima za mzee Mponda, zilitumika kwa kumuacha pasipo kumtilia maanani. 

wakati huohuo bendi ilikuwa ikifanya mazoezi ya wimbo wa “dunia uwanja wa fujo”. Hivyo mzee Lusungu akamuacha anaendelea kwenye chumba kimoja anapigapiga kinanda peke yake.Uhuru mkubwa alioupata ulimfanya awe jasiri akaanza kupiga nyimbo alizokuwa anazifahamu. Jambo hilo lililowavutia wanamuziki wenziwe waliomsikia kiasi cha kuacha mazoezi na kumfuata na kumtuza pesa.

Wakati huo haikuwa rahisi kutuzwa pesa kwa mwanamuziki mgeni ambaye alikuwa hajawahi hata kupigia bendi yoyote kabla ya pale, na tena wakiwa mazoezini.Mara moja wanamuziki walikubaliana kuwa ajiunge nao. Aliendelea kupiga nyimbo zilizoachwa na waziri, na kuchukuliwa rasmi kama mwanamuziki wa Msondo.

Jina la ‘Totoo’ alipachikwa kufuatia kwamba alikuwa bado mdogo ki umri na umbo. Wimbo wake wa kwanza kurekodi akipiga kinanda ulikuwa wimbo ‘Zhuleka’ utunzi wa Shaaban Dede.

Kwa bahati mbaya baada ya muda si mrefu kinanda kikaharibika na kwa muda wa zaidi ya miaka miwili akawa hapigi tena.Pangamawe akajiongeza kwa kuamua kuhamia kwenye upigaji wa gitaa. Alianza na kupiga second solo. Ujuzi wake mkubwa unasikika katika nyimbo za Kaka Selemani na Siwema.

Kisha akawa pia alipiga zito la besi, katika wimbo “Msafiri Kafiri”. Pamoja na kupiga gita hilo la besi, ilitokea wakati Kassim Mponda akaondoka katika bendi, wiki moja kabla ya siku ya kwenda kurekodi.Nafasi yake akakabidhiwa Ridhiwani Pangamawe kupiga gita la solo. Naye hakufanya ajizi, alizichambua nyuzi za gitaa hilo vizuri kabisa.

Kati ya nyimbo ambazo aliwahi kupiga anazozipenda zaidi mojawapo ni wimbo wa Queen Kasse.Hatimaye mwaka 1994, akaanza tena kupiga kinanda baada ya bendi kupata vyombo vipya. Akarekodi nyimbo kadhaa ukiwemo wimbo wa ‘Olee’.Kama alivyo kiongozi wa bendi hiyo Said Mabera, Ridhwani Pangamawe naye hajawahi kuodoa mguu wake kwenda katika nyingine, tangu alipojiunga nayo.

Pangamawe alisisitiza kuwa hana mpango wa kuhama kwa kuwa anaona hakuna sababu kubwa za msingi za kumfanya kuhama Msondo.

KAMATI YA BUNGE YAKABIDHI HATI ZA KWA WAKILMA-LINDI

$
0
0
JOSEPH MPANGALA , NACHINGWEA LINDI

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za mitaa imekabidhi hati za Kimila za Umiliki ardhi Mia Moja{100} kwa wakazi wa kijiji cha Mbondo kilichopo Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi 

Ugawaji wa Hati hizo unakuja baada ya kujengewa Uwezo na Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania{MKURABITA} kwa kutoa mafunzo jinsi ya kupima ardhi kwa Halmashauri ya Nachingwea kwa lengo la kuongeza thamani ardhi hizo pamoja na kuondokana na Migogoro Mbalimbali inayotokana na Mipaka.

Menyekiti wa kamati hiyo Jason Rweikiza amesema ugawaji wa Hati utawezesha wakulima kuweza kukopa katika taasisi mbalimbali za kifedha kwa lengo la kuendeleza ardhi hizo kwa kulima kilimo kitakacholeta tija na mafanikio na hivyo kujiletea maendeleo.

“Tayari taasisi za kifedha zimeanza kukubali kupokea Hati hizi hivyo wakulima wananafasi kubwa ya kuweza kuendeleza mashamba yao kwa kulima kisasa zaidi na kujiletea maendeleo”amesema Rweikiza mwenyekiti wa kamati.

Naye Mratibu wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania{Mkurabita}Dkt.Seraphia Mgembe amesema kuwa Wananchii waliopokea hati wanauwezo mkubwa wa Kuondokana na Umasikini kwa Kutumia hati zao kwa kushirikiana na wawekezaji mbalimbali watakaotaka kuwekeza hasa katika zao la korosho.

“Hii hati ni htai ambayo Vyombo vya fedha na Wawekezaji wanaamini kuwa wewe ndio mmiliki halali wa Shamba hilo kama kuna mtu anataka kuwekeza kwenye shamba lako na ili ajue kuwa wewe ndio mwenye shamba lazima umuoneshe Hati hiyo na katka wakati huu wa kilimo cha kisasa cha zao la Korosho,Wanaweza wakatokea watu wengi wakitaka kulima korosho Nachingwea na ili aweze kuingia ubia na wewe lazima umuoneshe Hati’’

Koini Mwanjisi ni Mkulima wa mazao ya Korosho na mahindi katika kijijji cha Mbondo Wilayani nachingwea tayari amepima Ardhi ya Heka saba na Kupatiwa hati anasema kwa sasa ameweza kufahamu jinsi ya kupata mikopo katika taasisi za kifedha ili kweza kulima kisasa zaidi.

“Sasa nimeoneshwa milango wapi nitaingilia kuweza kupata mkopo sababu nilikuwa nalima bila ya kuwa na nguvu za ziada lakini sasa hivi nimeshaoneshwa na Mkurabita nafikiri katika mika mingine inayokuja nitakuwa juu tofauti na hatua niliyonayo sasa hivi”alisema Mwanjisi.
mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Jason Reikiza akimkabidhi Hatimiliki za ardhi kwa Koini Mwanjisi katika hafla ya kukabidhi Hatimiliki za kimila miamoja {100} kwa wakulima wa kijiji cha Mbodo Wilaya ya Nachingewa mkoa wa Lindi.
Kutoka Kushoto Mratibu wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania{Mkurabita}Dkt.Seraphia Mgembe wakifurahi jambo na Mbunge wa iramba Mashariki Mwigulu Nchemba mara baada ya kupokea taarifa ya Mkoa Kuhusu Urasimishaji wa Ardhi katika Mkoa wa Lindi.
Naibu waziri Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa uma na Utawala Bora Marry Mwanjelwa wakijadili jambo na Mratibu wa Mkurabita Dkt.Seraphia Mgembe mara baada ya kumaliza kukagua Masjala ya Kijiji cha Mbondo kwa ajili ya kuhifadhi Hati za kimila za wananchi.
Naibu waziri Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa uma na Utawala Bora Marry Mwanjelwa akijadili jambo na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa mara baada ya kumaliza kugawa hati miliki za kimila za Mashamba kwa wakulima wa Kijiji cha Mbondo kilichopo Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi. 

MBOWE AMPUUZA PROFESA LIPUMBA BAADA YA ....

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe amesema Chama cha Wananchi(CUF)kinapita katika wakati mgumu kutokana na mgogoro unaondelea kufukuta ndani ya Chama hicho.

Mbowe amesema hayo leo Machi 15,2019 jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari ambapo amedai mgogoro wa CUF umetengeneza kwa lengo la kuudhoofisha upinzani.

"CUF inapita kwenye mgogoro mkubwa na kwa bahati mbaya ni wa kutengenezwa kwa lengo la kuudhofisha upinzani.Sitaki kuwa Msemaji wa CUF ila nawashauri wamalize kile ambacho watakifanya kwa usalama,"amesema Mbowe.

Ameongeza wakati mgogoro huo unaendelea, amemsikia mara kadhaa Profesa Ibrahim Lipumba namna ambavyo anawalaumu Chadema na uamuzi wake wa kujiondoa Ukawa.

"Profesa Lipumba ni mtu ambaye nimefanya naye nyingi, naheshimu na nitaendelea kumheshimu.Kwa sasa nimuache maana ni mtu mzima na acha afanye anachoendelea.

"Kuna siku Dunia itajua na hasa muda ukifika utaongea.Naamini haki ya wananchi wa Zanzibar kupiria maalim Seif Sharif Hamadi na Chama chake itapatikana tu.Nimuombee mema Maalim Seif na watambue haya ni mapito tu na watayapita, "amesema.

Prof Lipumba

OLIVER N’GOMA FIGO ILIKATISHA MAISHA YAKE

$
0
0
Historia ya mwanamuziki Oliver N’Goma katika muziki haitasahaulika kamwe licha ya kuianga dunia miaka minane iliyopita. Alifariki dunia Juni 07, 2010 kwenye Hospitali ya Omar Bongo, jijini Libreville, Gabon.

Kifo chake kilisababishwa na tatizo la figo yake kushindwa kufanyakazi vizuri, ugonjwa ambao alikuwa akipambana nao kwa takriban miaka miwili ya mwisho ya maisha yake.

Wasifu wake unaeleza kuwa alizaliwa mjini Mayumba, Kusini-Magharibi mwa nchi ya Gabon mwaka wa 1959. N’goma alizaliwa alikuwa vipaji vya kupiga gitaa, kutunga na kuimba nyimbo za muziki wa Afro-Zouk na Reggae.

Alipewa jina la utani la "Noli," Alifahamika sana kwa kibao chake Bane cha mwaka wa 1989, ambacho kilivumishwa sana takriban Afrika nzima.
Maisha ya N'Goma katika muziki yanaelzwa kuwa alivutiwa kimuziki kwa mara ya kwanza na baba yake, mwalimu na mpiga harmoni.
Japokuwa alipata masomo yake ya muziki kwa mara ya kwanza wakati ana umri wa miaka minane, alianza kutumbuiza mbele ya hadhara baada ya kuhamia mjini Libreville kwa ajili ya masomo.

Oliver N’goma wakati akichukua masomo ya uhasibu, alijiunga na kundi la Capo Sound, iliyokuwa ni bendi ya shule, ambapo ndipo alipojifunza namna ya kupiga gitaa.

Kundi hilo lilikuwa likipiga dansi rasmi na mipira, ambapo alijifunza sanaa ya kutumbuiza kwenye jukwaa. N'Goma alikuwa mwanafunzi maskini kabisa, aliyejizatiti zaidi kwenye muziki na sinema badala ya masomo.

Mapenzi yake ya filamu yalimuongoza hadi kufanyakazi na TV ya Gabon, ambayo iliwahi kusafiri nayo hadi nchini Ufaransa mnamo 1988 ambapo alijifunza kuwa mtu wa Kamera. Wakati wakiwa katika majira ya baridi huko Paris, alikuwa tayari amemaliza kazi yake ya muziki alioutunga akiwa Gabon.

N’Goma aliwahi kufanya kazi ya muziki kwa pamoja na Manu Lima, ambaye alikuwa mtayarishaji wa rekodi mashuhuri kwa muziki wa Kiafrika. Lima alivutiwa sana na kazi bwana mdogo, na kushikilia mwongozo wa rekodi ya kwanza ya N'Goma iliyokwenda kwa jina la Barre.

Albamu ilifurahia mafanikio ya tabu kwa mara ya kwanza, hadi hapo kituo cha redio cha Kiafrika ilipoanza kupiga nyimbo zake. Jina la wimbo huo ilipata ushindi na mafanikio mengi huko Afrika, Ufaransa, na Ufaransa na West Indies, ulienda kutamba sana katika maeneo hayo.

N’Goma alifurahia mafanikio hayo yakilinganishwa na mafanikio yalipatikana kwenye albamu za Mario ya T.P.OK Jazz, iliyokuwa ikiongozwa na Franco Luanzao Makiadi au Yeke Yeke wa Mory Kante. Albamu hiyo ilipata kuwa moja kati ya albamu zilizouza sana katika albamu za Kiafrika hadi sasa.

N'Goma alitoa albamu ya pili ya Adia mnamo Desemba 1995. Hata hivyo alifanyakazi tena na Manu Lima. Miaka mitano baadaye, albamu yake ya tatu ya Seva ilitoka. Oliver N’Goma aliwahi kuachia albamu ya Best of Oliver N'Goma, iliyokuwa imejumuisha vibao vikali ilitolewa mnamo mwaka wa 2004.

Baadhi ya nyimbo alizoachia Oliver N’Goma zilikuwa za Jump to navigation, Jump to searc, Alphonsine, Lusa, Adia, Muetse, Julie, Icole na Bane. Zingine ni Felly, Shado, Barre, Sal, Muendu, Betty, na Ng’ebe.

MADAKTARI WA CHINA WASAIDIA VITABU NA VIFAA TIBA ZANZIBAR

$
0
0
 Mtayarishaji wa kitabu cha maradhi ya njia ya mkoji Dk. Zhang Junjie akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdalla msaada wa kitabu pamoja na vifaa tiba (kushoto) Naibu Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Zanzibar Shen Qi. hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.
 Naibu Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Zanzibar Bi. Shen Qi akitoa maelezo juu ya urafiki wa China na Zanzibar katika hafla ya kukabidhi kitabu na vifaa tiba, (kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Ali Abdalla.
Mkurugenzi Kinga Dk. Fadhil Abdalla akitoa shukran kwa Timu ya Madaktari wa China kwa msaada wa kitabu na vifaa tiba walioutoa, hafla hiyo ya makabidhi imefanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Na Ramadhni Ali – Maelezo Zanzibar 
Timu ya Madaktari wa Kichina wanaofanyakazi Hospitali Kuu ya Mnazimmoja imeikabidhi msaada wa kitabu na Vifaa Tiba Wizara ya Afya Zanzibar kwa ajili ya matumizi ya Hospitali hiyo.

Mmoja wa Madaktari wa timu hiyo, mtayarishaji wa kitabu hicho Dk. Zhang Junjie  alimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdalla  msaada huo katika hafla iliyofanyika Ofisini kwake Mnazimmoja.

Dk. Zhang alisema msaada huo ni muendelezo wa ushirikiano wa miaka mingi uliopo baina ya Jamhuri ya Watu wa China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  katika kuimarisha huduma za Afya.

Alikumbusha kuwa Jamhuri ya Watu wa China ilianzisha ushirikiano wa kuleta Madaktari Zanzibar tokea mwaka 1964 na  utaratibu huo umekuwa ukiendelezwa na kuimarishwa zaidi hadi hivi sasa.

Alieleza matarajio yake kuwa  msaada wa kitabu na vifaa tiba vilivyotolewa vitasaidia katika kuimarisha huduma za afya katika Hospitali ya Mnazimmoja na Hospitali nyengine za Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Ali Abdalla aliishukuru timu ya 28 ya Madaktari wa China kwa msaada wa vitabu ambavyo vitakuwa ni chanzo cha mafunzo kwa Madaktari wa Mnazimmoja.

Aidha alisema vifaa Tiba vitaongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa katika Hospitali hiyo ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya Teknolojia na Rasilimaliwatu.

Mkurugenzi Kinga Dk. Fadhil Abdalla alisema kitabu walichokabidhiwa na Timu ya Madaktari wa China ambacho kinahusiana na matatizo ya maradhi ya njia za mkojo, ikiwemo tenzi dume, vitatumika kama muongozo na mapitio kwa madaktari wakati wa kufanya upasuaji.

Dk. Fadhil aliongeza kuwa kitabu hicho pia kitatumika kuwasomesha Madaktari wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi za Afya ya Binadamu ya SUZA iliopo Mbweni ili kuelewa kwa undani tatizo la maradhi ya njia za mkojo na tiba yake.

Makabidhiano ya Kitabu na Vifaa vya Tiba yalihudhuriwa pia na Naibu Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Zanzibar Shen Qi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria yaridhishwa na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa mahakama

$
0
0
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa (Mb.) wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipokuwa ikikagua miradi mbalimbali ya ujenzi wa mahakama Mkoani Mbeya.  “Kamati inaipongeza Wizara ya Katiba na Sheria na Uongozi wa Mahakama kwa kusimamia kwa weledi miradi ya mahakama hapa nchini.” Aliendelea kusema “Kamati inawasihi (Wizara na Mahakama) kuhakikisha mnakamilisha miradi hiyo kwa kuzingatia muda uliopangwa na viwango vyenye ubora uliothibishwa.” Alisema Mheshimiwa Mchengerwa. 
Mheshimiwa Balozi Augustine Mahiga (Mb.), Waziri wa Katiba na Sheria ameambatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa ajili ya ziara ya siku tano (13-17 Machi 2019) ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa mahakama hapa nchini. Ziara hiyo ni ya kwanza tangu Balozi Mahiga alipokabidhiwa rasmi Wizara hiyo tarehe12 Machi 2019 na Mheshimiwa Waziri Profesa Palamagamba Kabudi (Mb.) aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Akieleza ushiriki wa Waziri Mahiga kwenye ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati alieleza kuwa, ni Waziri wa kwanza kuambatana na Kamati hiyo katika ukaguzi wa miradi ya mahakama tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani. Alieleza kuwa, Kamati yake imefarijika sana na kitendo hicho na kuahidi kwa niaba ya Kamati kuendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu mbalimbali. 
  
Akitoa taarifa ya ujenzi wa miradi hiyo, Waziri Mahiga alieleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2018/19 Mahakama imeendelea kutekeleza miradi 35 ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Alieleza kuwa, pamoja na kukagua miradi ya Mkoa wa Mbeya,  Kamati hiyo itaendelea na ziara ya kujihakikishia utekelezaji wa miradi hiyo kwenye Mkoa wa Njombe, Arusha, na Manyara kabla ya kuanza Mkutano wa 15 wa  Bunge la Bajeti tarehe 2 Aprili 2019.
Alieleza kuwa, kwa mwaka huo wa fedha Mahakama ilitengewa kiasi cha Tshs. 35,973,722,000/= ikiwa ni fedha za maendeleo. Kati ya fedha hizo Tshs. 15,000,000,000/= ni fedha za ndani na Tshs. 20,973,722,000/= fedha za nje. Kati ya fedha zote za ndani Bilioni 5 imeshatumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Naye Kaimu Mtendaji wa Mahakama, Bw. Solanus M. Nyimbi alieleza kuwa, katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo kumekuwa na changamoto kadhaa hususan mtiririko wa fedha za maendeleo; mazingira: jiografia ya eneo, hali ya hewa na aina ya udongo katika maeneo ya mradi; na changamoto za umiliki wa viwanja hususan katika miradi viporo. Alieleza kuwa, pamoja na changamoto hizo wameendelea kujitahidi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati uliopangwa. 

WAKALA WA MAJENGO TANZANIA (TBA) WAPONGEZWA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (Wa kwanza kulia), wakati Kamati yake ilipokuwa ikikagua maendeleo ya miradi ya Ofisi za Serikali inayosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), jijini Dodoma.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daudi Kondoro, akitoa maelezo ya mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kanda ya Dodoma, Arch. Humphrey Kilo, akionesha mchoro wa Jengo jipya la Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano lililopo mtaa wa Moshi jijini Dodoma kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) walipokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
 Mbunifu Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Hamis Kileo, akionesha mchoro wa Jengo la Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) walipokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mara baada ya kukagua maendeleo ya miradi inayosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), jijini Dodoma.
 Muonekano wa nje wa Jengo la Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Muonekano wa nje wa Jengo jipya la Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano lililopo mtaa wa Moshi jijini Dodoma.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeupongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kwa kutekeleza miradi wanayoisimamia kwa ubora na kwa gharama nafuu.

Akizungumza mara baada ya kukagua miradi inayojengwa na Wakala huo ikiwemo jengo la ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, pamoja na Jengo la Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma,  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka,  amesema kuwa kamati imeridhishwa na kazi zinazofanywa na wakala huo na hivyo kuutaka wakala huo kutobweteka na badala yake kufanya kazi kwa bidii hata kwa miradi mingine wanayoitekeleza. 

"Sisi kama Kamati ya PAC kiukweli tumefurahishwa na utekelezaji wa miradi hii tulioikagua, tunawapongeza kwa kufanya kazi nzuri na inayozingatia thamani ya fedha", amesema Mheshimiwa Mwenyekiti.

Amesisitiza kuwa Kamati inapenda kuwatia moyo TBA kwa kuendelea  kufanya jitihada katika usimamizi wa miradi iliyonayo ili kuondoa ile dhana iliojengeka ya kwamba kazi zinazotekelezwa na wakala huo zipo chini ya kiwango.

“Tunawapongeza TBA kwa kazi nzuri iliofanyika, baada ya kukagua tumeona kuwa serikali haikufanya makosa kutoa zabuni nyingi za ujenzi kwa TBA”, amesisitiza Mwenyekiti wa Kamati

Aidha, Wakala huo umepongezwa kwa kuweza kutoa fursa kwa wanafunzi walioko na wanaotoka vyuoni kupata mafunzo kwa vitendo ili kuwajengea uwezo ambao utaiwezesha Serikali kupata wataalama zaidi  katika taaluma hiyo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, amesema wizara itaendelea kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi  kutoka vyuo vikuu ili nao waweze kuja kuwa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo nchini kupitia sekta ya ujenzi.

Arch. Mwakalinga, ameahidi kwa Kamati hiyo kuhakikisha kuwa wataendelea kujenga majengo ya Serikali kwa kuzingatia ubora na kwa gharama nafuu.

Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daudi Kondoro, amefafanua kuwa jengo la Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano linalojengwa hivi sasa katika mtaa wa Moshi jijini Dodoma lina ghorofa tatu zenye jumla ya vyumba 84 zikiwemo ofisi za viongozi 15 zenye maliwato ndani, maafisa waandamizi 5, Ofisi za wazi 17, masijala 3, Makatibu Muhtasi 14, vyumba vya chai 4, stoo 3, vyoo 22 na vyoo vya watu wenye mahitaji maalum.

Ameongeza kuwa mradi wa ujenzi wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma umefika asilimia 97 ambapo amesema kuwa kazi zinazofanyika kwa sasa ni kukamilisha kazi ya madirisha, milango ya nje ya jengo pamoja na kukagua na kurekebisha dosari zilizojitokeza wakati wa ujenzi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi)

VOA SWAHILI: Washington Bureau na SUNDAY SHOMARI

Mloganzila yapatiwa msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye vidonda.

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 15 ambavyo vitatumika katika vyumba vya upasuaji kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye vidonda.
Vifaa hivyo Caiman Lerrafuse HF Generator (GN 200) pamoja na Infovac Therapy System vimetolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kina mama Prof. Sang Lyun Nam akiwa na Daktari Bingwa wa upasuaji ubongo na mishipa ya fahamu Prof. Seung -Kon Huh kutoka Korea Kusini.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru amesema vifaa hivyo vitasaidia utendaji kazi katika vyumba vya upasuaji, na kuongeza kuwa watalaam hao mbali na kutoa vifaa hivyo lakini pia wanafanya kazi na watalaam wa Hospitali ya Mloganzila hatua ambayo inasaidia wataalam wa hospitali hiyo kupata ujuzi zaidi.
“Wataalam hawa tupo nao hapa Mloganzila na wapo tayari kufundisha watanzania kufanya upasuaji ambao hatufanyi, hata msaada huu waliotupatia ni jitihada zao wenyewe, hivyo napenda kutumia fursa hii kuwashukuru sana kwa msaada huu wa vifaa tiba ambavyo tutatumia ipasavyo kama ilivyokusudiwa”. Amesema Prof. Museru.
Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa MNH amesema wanakamilisha mipango ya kuomba watalaam kutoka Korea ili waje kufanya kazi kwa muda na wataalam wa Muhimbili kwa lengo la kuwajengea uwezo katika maeneo mbalimbali ili kuendelea kutoa huduma bora na za kibingwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru, (wa pili kutoka kushoto) akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Prof Sang Lyun Nam, (kulia) ni Prof. Seung –Kon Huh wa Korea Kusini. kushoto ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi akishuhudia makabidhiano hayo.

 Vifaa tiba Caiman Lerrafuse HF Generator (GN 200) pamoja na Infovac therapy system ambavyo vimetolewa kwa ajili ya Hospitali ya Mloganzila.


Prof Lawrence Museru (wa pili kutoka kushoto) akitoa neno la shukrani baada ya kupokea vifaa tiba ambavyo vitatumika katika vyumba vya upasuaji kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye vidonda.

HABARI ZA UMOTA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK, MAREKANI

UTEPE MWEUPE SULUHISHO LA VIFO VYA MAMA NA MTOTO WAKATI WA KUJIFUNGUA

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus, 
Michuzi Blog, Bukoba - Kagera.

Maadhimisho ya siku ya  Muungano wa utepe mweupe na uzazi salama  katika Mkoa wa Kagera yamefanyika Kitaifa Mkoani Kagera Machi 15, 2019 huku  jamii ikihimizwa kuacha ukatiri wa kijinsia kwa wanawake na wasichana.
Awali Maadhimisho hayo yalitanguliwa na mandamano ya wananchi mamia kwa maelfu na kisha kilele chake Kufanyika katika viwanja ya Gymkana katika manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera  yakiwa na kauli mbiu "komesha  unyanyasaji kwa wanawake na wasichana,okoa maisha wakati wa uzazi".



Meneja Mawasiliano kutoka  muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama Anna Sawaki amesema maadhimisho hayo kuwa yana lengo la kupunguza vifo kwa wananwake wakati wa kujifungua. Na kuongeza
kuwa takwimu zinaonesha vifo vitokanavyo na uzazi vinaongezeka badala ya kupungua kutokana na unyanyasaji wanaoupata akina mama pindi wawapo wajawazito na wakati wa kujifungua.



Kwaupande wake Rose Mlayi  ambaye ni mratibu wa Taifa wa muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama ameiomba jamii  kukomesha ukatili kwa wanawake na wasichana, ili kuokoa maisha yao wakati wa uzazi.
Bi Rose amesema kuwa upungufu wa vituo vya afya na zahanati katika maeneo mengi ni moja ya vyanzo vinavyosababisha vifo kwa akina mama wengi wakati wa kuelekea kujifungua hasa maeneo ya vijijini kutokana na wamama hao kutembea mwendo mrefu pamoja na baadhi ya mira potofu kutoka kwa jamii ya kuwazuia wanawake kujifungulia katika vituo vya afya.



Katika hotuba ya Waziri wa afya,maeneleo ya jamii jinsia wazee  na watoto Ummy Mwalimu iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo,amesisitiza kuwa Serikali kupitia idara zake inaendelea kukomesha vitendo hivyo, ikiwemo kuendelea na mikakati yake ya kutokomeza vifo vitakavya na uzazi pingamizi.
Waziri ummy ameongeza kuwa wizara yake inaendelea kuboresha sekta ya afya hasa upande wa vituo vya afya pamoja na vifaa tiba ambapo pia ameeleza mkakati wa kuanzisha vituo vya huduma jumuishi kwa kila kituo cha afya.

 Meneja mahusiano kutoka shirika la utepe mweupe Anna kushoto akitoa maelezo juu ya kazi wanazozifanya katika kupambana na vifo vitokanavyo na uazazi
Mgeni rasmi Deodatus Kinawiro kwa Niaba ya Waziri Ummy Mwalimu akizindua mpango wa utepe mweupe katika maadhimisho yaliyofanyika Manispaa ya Bukoba 
 Mgeni rasmi Deodatus Kinawiro Mkuu wa Wikaya ya Bukoba akionesha mpango wa utepe mweupe Mara baada ya kuzindua 
 waandamanaji na wadau wa sekta ya Afya, wakitembea kwa maandamano wakikatiza maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba kuelekea viwanja vya Gymkhana.
Waendesha bodaboda na wadau wa sekta ya Afya, wakiwa katika maandamano maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba kuelekea viwanja vya Gymkhana.
Waandamanaji na wadau wa sekta ya Afya, wakitembea kwa maandamano wakikatiza maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba kuelekea viwanja vya Gymkhana.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 15.03.2019

Tanzania yashiriki katika mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika

$
0
0



Katibu Mtendaji wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Bi. Stergomena Tax, akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa  Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Council of Ministers),  unaofanyika Windhoek, Namibia, kuanzia tarehe 15 -17 Machi, 2019.  
Mkutano huu, unahudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje, Mawaziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Mawaziri wa Fedha pamoja nchi 16 wanachama wa SADC ambapo Tanzania inawakilishwa katika mkutano huu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb.);  Waziri wa Viwanda na  Biashara, Mhe. George Kakunda (Mb.); na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.). 
Masuala yanayojadiliwa katika mkutano huu ni pamoja na  Taarifa ya Utekelezaji wa mipango na mikakati ya SADC; Taarifa ya Kamati ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Kamati ya Usimamizi wa Rasilimali watu; Hatua zilizofikiwa katika mchakato wa Visiwa vya Komoro kujiunga na SADC na Mpango wa Kuanzisha chuo cha Uhawilishwaji cha SADC (SADC  University of Transformation).
Masuala mengine yanayotarajiwa kujadiliwa katika mkutano huu ni pamoja  na; Uendelezaji wa viwanda katika kanda; Utekelezaji wa Mkakati wa Kanda wa Mawasiliano; Mabadiliko ya Kitaasisi katika Umoja wa Afrika(AU); na Majadiliano ya Ubia Mpya Baina ya Nchi za Kundi la Afrika, Carribean na Pasifiki (ACP) na Umoja wa Ulaya (EU), baada ya mkataba wa Cotonou kumalizika mwaka 2020.
Mkutano huu umetanguliwa na Kikao cha Makatibu Wakuu pamoja namaafisa waandamizi  uliofanyika kuanzia tarehe 11 - 14 Machi, 2019, Windhoek. Namibia. Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo.




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki Prof. Kabudi akifuatilia hotuba ya Katibu Mtendaji wa SADC.


Naibu Waziri Mkuu wa Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la SADC, Mhe.Netumbo Nandi-Ndaitwah,  akitoa hotuba wakati wa mkutano huo.
Wajumbe  kutoka nchi za Tanzania, Zambia  na Afrika Kusini, wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la SADC, Mhe. Nandi-Ndaitwah.


Mawaziri wa SADC wakiwa katika picha ya pamoja.

MANYANYA-SERIKALI HAITAMFUMBIA MACHO MUWEKEZAJI YOYOTE ANAEKIUKA TARATIBU KATIKA SUALA ZIMA LA UWEKEZAJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi  Stella Manyanya amewataka wawekezaji waliobinafsihiwa baadhi ya viwanda kutumia viwanda hivyo kwa lengo husika na sio kuvitumia kwa matumizi mengine ambayo haya kukusudiwa .

Naibu Waziri aliyasema hayo jana  wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge viwanda ,biashara na Mazingira ilipotembelea katika kiwanda cha bia cha kampuni ya TBL Arusha na kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi

Alisema kuwa Serikali haita mfumbia macho mwekezaji yeyote aliyebinafsishiwa kiwanda na badala ya kukiendeleza ,akakigeuza kufanyia shughuli nyingine tofauti na ile iliyo kusudiwa .

"wale ambao wamepewa viwanda kwa nia ya kuviendeleza na hawajafanya hivyo wamefanya vitu vingine, serikali haitaona hatari ya kuvipokonya viwanda hivyo kwa wawekezaji ambao walibinafsishiwa΄΄alisema Naibu Waziri

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge viwanda ,biashra na mazingira Suleiman Saddiq aliipongeza Tbl kwa kazi wanayofanya na jinsi wanavyolipa kodi kwa serikali pia aliwahaidi kupeleka bungeni baadhi ya changamoto ambazo wamezisema ikiwemo la kuongezewa eneo la kiwanda pamoja na kupunguziwa ushuru wa mabango .

Aidha pia kamati hiyo ilipotembelea katika kiwanda cha Camatec ilitaka serikali ifanye kila iwezekanavyo kuweka fedha za maendeleo nyingi ili vitu vinavyotengenezwa na camatec viwe na ubora zaidi na pia ijitaidi kupeleka fedha za bajeti ambazo zimepangwa kwenye kiwanda hicho kwaa wakati ili kiweze kufanya kazi jinsi ipasavyo na wananchi

Aidha Kamati hiyo ya bunge imeishauri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuviunganisha viwanda vya Cametec,Temdo na SIDO kwani viwanda hivi vina tegemeana na pia ndio nguzo pekee kuelekea uchumi wa Viwanda, hivyo ni lazima kusaidiwa kupata teknolojia za kisasa ili kusaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora na zenye ushindani katika masoko 
Pichani kushoto ni Mpishi wa bia kampuni ya TBL Richard Mkojera akitoa maelezo kwa  Naibu waziri wa viwanda ,biashara na uwekezaji Mhandisi  Stella Manyanya  namna bia zinavyotengenezwa kiwandani hapo.
Pichani ni Naibu Waziri wa viwanda ,biashara na uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akitazama namna bia zinavyowekwa lebo kiwandani hapo
Mkurugenzi wa Masoko kanda ya kaskazini James Bokela akimuelekeza Naibu waziri namna mashine ya TRA inavyohesabu beer zinavyo zalishwa.

RC Kigoma: Bodi ya Mikopo mnafanya kazi kubwa

$
0
0
*Aagiza taasisi zinazodaiwa malimbikizo kulipa mara moja 

Na Eline Maronga – HESLB, Kigoma

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali (mstaafu) Emmanuel Maganga amewaagiza waajiri wote mkoani Kigoma ambao wanadaiwa malimbikizo ya makato ya mikopo ya elimu ya juu kuhakikisha wanawasilisha fedha hizo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) mara moja.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa maagizo hayo Jumanne, Machi 12, jioni wakati akikabidhi tuzo zilizotolewa na HESLB kwa waajiri watano bora mkoani Kigoma ambao wanatekeleza matakwa ya sheria ya HESLB kwa ufanisi.

“Nawapongezeni sana Bodi ya Mikopo, mnafanya kazi kubwa sana kwa taifa letu. Lakini nimeambiwa kuna baadhi ya taasisi hapa mkoani kwangu zinawakata wafanyakazi lakini hazileti kwenu fedha za makato, nimeshaelekeza wahakikishe fedha hizo zinalipwa mara moja,” alisema Brigedia Jenerali Maganga.

Kiongozi huyo, ambaye alikua mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Lake Tanganyika, aliihimiza Bodi ya Mikopo kuhakikisha kila mnufaika wa mkopo ambaye hajajitokeza anasakwa na kuaSnza kurejesha.

“Akipatikana, wewe kata tu,” alisema na kuwapongeza wawakilishi wa waajiri kutoka taasisi tano ambazo ni Danish Refugee Council inayowasilisha Tshs 10.8 milioni kila mwezi kutoka kwa wanufaika 54.

Nyingine ni Norwegian Refugee Council inayowasilisha Tshs 7.3 milioni kwa mwezi kutoka kwa wanufaika 28; Diocese of Kigoma (CARITAS) yenye wanufaika tisa na inawasilisha Tshs 1.7 milioni kwa mwezi.

Nyingine ni Baba Watoto Centre for Youth and Children yenye wanufaika wanne na inayowasilisha Tshs 1.1 milioni kwa mwezi na taasisi ya Relief to Development Society (REDESO) yenye wanufaika 13 na inawasilisha Tshs 0.9 milioni kwa mwezi. 

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru alimweleza kiongozi huyo kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018, HESLB ilikusanya Tshs 181.4 bilioni na kuwa kutoka mkoa wa Kigoma pekee, zilikusanywa Tshs 2.66 bilioni (asilimia 1.4).

“Tunadhani tunaweza kukusanya zaidi kwa sababu tuna waajiri, wengine ni taasisi za Serikali, wanakata wanufaika lakini fedha hizo hazifiki kwetu … tumekuja kutoa tuzo lakini pia kuwahimiza waajiri sugu watimize matakwa ya sheria,” alisema Badru.

Akiwa mkoani Kigoma, Bw. Badru pia alipata fursa ya kuwasilisha mada kuhusu ‘Wajibu wa Waajiri katika Urejeshaji wa Mikopo’ kwa wajumbe wa Baraza la Ushauri la Mkoa wa Kigoma linalowajumuisha viongozi wote wakuu wa mkoa na wilaya.

Katika mada hiyo, Bw. Badru aliwakumbusha viongozi hao kuhusu wajibu wa waajiri kuhakikisha kuwa wanawasilisha kwa HESLB orodha ya waajiriwa wapya ndani ya siku 28 tangu wawaajiri kama sheria inavyoelekeza. 

“Wajibu mwingine ni kukata asilimia 15 ya mshahara ghafi wa mnufaika wa mkopo, na si chini ya hapo. Baada ya kukata, kila mwajiri anapaswa kuhakikisha anawasilisha makato hayo kwa Bodi ya Mikopo ndani ya siku 15 baada ya tarehe ya mwisho wa mwezi wa makato,” alifafanua Bw. Badru na kujibu maswali mbalimbali yaliyojitokeza.

HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwaka 2005 ikiwa na majukumu kadhaa, lakini makuu mawili – kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji wa kitanzania waliopata nafasi za kujiunga na taasisi za elimu ya juu; na kukusanya mikopo iliyoiva iliyotolewa na Serikali tangu mwaka 1994/1995.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bregadia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga akipokea tuzo ya Bodi ya kutambua mchango wake kwa waajiri wa Mkoa huo kutekeleza sheria ya Bodi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Abdul-Razaq Badiri akizungumza na waajiri waliotekeleza sheria ya Bodi katika kulipa mikopo ya wanufaika mkoani Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bregadia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga akiwa katika picha ya pamoja Waajiri wa Mkoa huo na Watendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

OLE SENDEKA AAGIZA UTEKELEZAJI KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA MKOANI NJOMBE

$
0
0
 Mary Sapali, Mratibu Wa Damu Salama Kanda ya Nyanda za Juu Kusini akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Njombe.
Dionisia Simime, Mratibu Wa Damu Salama Halmashauri ya wilaya ya Njombe akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Njombe.
  Dkt.Bumi Mwamasage, Mganga mkuu Wa mkoa Wa Njombe akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Njombe.
 Mhe. Christopher Ole Sendeka, Mkuu Wa mkoa wa Njombe, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama.

Na. Vero Ignatus.

Kampeni ya 'Jiongeze Tuwavushe Salama' imezinduliwa mkoani Njombe, ambapo Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Christopher Ole Sendeka amewataka watendaji kufanya kila wawezalo kuhakikisha kampeni hiyo inaleta tija kwa kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga pindi wanapozaliwa.

Kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali kwa wakuu wote wa mikoa nchini katika kuhakikisha vifo vya wajawazito na watoto wachanga vinapungua.

Kampeni hiyo ilizinduliwa Kitaifa mwaka jana mkoani Dodoma na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuhudhuriwa na wakuu wote wa mikoa, akiwemo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.

Mhe. Ole Sendeka amesema kampeni ya 'Jiongeze Tuwavushe Salama' ni ya kitaifa, ikiwa chini ya Raisi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, hivyo watendaji wajipange kuhakikisha malengo yanafikiwa.

"Naagiza Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Njombe, Makatibu Tawala na Wakurugenzi kuhakikisha hatua za kuzuia vifo, ikiwemo kutoa huduma za kitaalamu kwa wakati na kuhakikisha vifaa tiba vinapatikana katika vituo vya Afya," alisema Ole Sendeka.

Amesema serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha mama wajawazito wanapatiwa ushauri, dawa, kuanzia kliniki hadi pale kujifungua salama

"Mhe Dkt. Magufuli, kwa kuwajali wananchi wake, ametupatia zaidi ya bilioni 3 ili tujenge vituo vya afya katika mkoa wetu, Wakuu wa Wilaya katembelea maeneo ya ujenzi kila mara ili kuhakikisha ujenzi sahihi, kwa matumizi sahihi ya fedha unafanyika," alisema Ole Sendeka. 

Dkt. Bumi Mwamasage ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Bumi amesema uwajibikaji wa kuhakikisha mama wajawazito wanajifungua salama unapaswa kuanzia katika ngazi ya familia.

"Baba na wana familia wanalazimika kuhakikisha mama anahudhuria kliniki ili apate elimu ya ujauzito wake na umuhimu wa chanjo kwa ajili ya kujilinda yeye na mtoto atakayemzaa.

Dkt. Bumi amesema Kampeni hiyo ni ya mwaka mmoja katika mpango wa 'Life Plan' wenye lengo la kuhakikisha hakuna tena vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga, hivyo inabidi jamii yote ishiriki elimu ya kutosha itolewe katika kulikabili tatizo hilo.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliahidi kuchangia shilingi 500,000 Mkuu wa Wilaya 100,000 kila Mkurugenzi, Wenyeviti wa halmashauri Waganga Wakuu wakiahidi kutoa 50,000 ikiwa sehemu ya kuchangia upatikanaji wa Damu Salama wakati wa mama anapojifungua na kutokwa damu nyingi ambao miongoni mwao hupoteza maisha

Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama  inatekelezwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo UNICEF.

Mwisho

Matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Njombe.




VYOMBO VYA UMMA VYATAKIWA KUSIMAMIA HAKI YA UPATIKANAJI TAARIFA

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika ,tawi la Tanzania (Misa-Tan) Salome Kitomary akizungumza jambo wakati wa Mafunzo kwa watumishi wa Mahakama mkoa wa Kilimanjaro .
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika ,tawi la Tanzania (Misa-Tan) Salome Kitomary akisikiliza mawazo mbalimbali kutoka kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Mkufunzi katika Mafunzo yanayowahusisha watumishi wa Mahakama,Wakili James Marenga akiwasilisha mada katika mafunzo hayo yanayofanyika Hoteli ya Leopard mjini Moshi.
Baadhi ya Washiriki katika mafunzo hayo wakifurahia jambo wakati wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wakufunzi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

VYOMBO  vya umma vimetakiwa kuwasimamia haki ya upatikanaji wa taarifa ikwa ni pamoja na kuwa wakala kwa mwananchi yoyote atakayehitaji kupata haki isipokuwa kama kuna sheria inayotoa ufafanuzi wa msingi kwanini zisitolewe.

Hayo yamelezwa na Mkufunzi katika mafunzo kwa watumishi wa Mahakama yanayofanyika katika Hoteli ya Leopard mjini Moshi,Wakili James Marenga wakati akiwasilisha mada iliyohusu Muktadha wa Kisheria kwenye haki ya kupata taarifa.

Alisema haki ya kupata habari  inapatikana kwenye mikataba ya kimataifa ambayo ndimo misingi ya uhuru wa kujielezea imejengeka na kwamba ni tamko la kimataifa la haki za binadamu la mwaka 1948.

“Ibara ya 19  ya Tamko hilo inasema kuwa  Kila mmoja ana haki ya uhuru wa kutoa na kueleza maoni yake; haki hii inahusu pia uhuru wa kutoa  maoni yake bila kuingiliwa kati, na uhuru wa kutafuta na kutoa taarifa na maoni kwa njia yoyote bila kujali mipaka.” Alisema Marenga.

Alisema katika tamko la Afrika juu ya miiko na kanuni  za watumishi wa umma na utawala limeelekeza kuwa  Utumishi wa Umma na Utawala utahakikisha kuwepo na taarifa na utaratibu wa namna ambavyo utumishi wa umma unavyotakiwa kutoa huduma.

Marenga alisema utumishi wa umma na utawala wanatakiwa kutoa taarifa kwa wananchi juu ya mambo yanayowahusu na kama kuna maamuzi juu yao yametolewa katika misingi gani na kwa sababu gani na kama kuna namna yoyote ya kukata rufaa juu ya maamuzi hayo. 

“ Utumishi wa Umma na Utawala  uweke mfumo wa mawasiliano  na mchakato  wa kujulisha umma juu ya huduma wanazozitoa  ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa  kwa watumiaji na kupata mrejesho kutoka kwao.

Mapema washiriki wa mafunzo hayo ya siku tatu wameeleza kupata mwanga zaidi kutokana na mfunzo hayo hasa katika maeneo ya utoaji huduma kwa wananchi bila kujali hali za wahusika ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa kufuata taratibu zilizoelekezwa kwa mujibu wa Sheria ya upatikanaji  taarifa.

“moja ya mambo tunayojifunza ni pamoja na kuacha changamoto za nyumbani mara baada ya kuingia katika maeneo yetu ya kazi ,na hii husaidia ufanisi katika kumuhudumia mwananchi ambaye ni mteja wetu “alisema Massawe mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika –Misa Tan kwa kushirikiana na taasisi ya kijerumani ya Friedrich Ebert Stiftung  yamelenga  kuwakumbusha watumishi hao wa Mahakam juu upatikanaji wa taarifa na maadili kwa utumishi wa umma pamoja na utoaji huduma kwa wateja.

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA UTALII YAPANIA KURUDISHA HADHI YA CHUO CHA MWEKA

$
0
0

Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii wakipewa maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Hashimu Paschal kuhusiana na matumizi ya silaha za moto aina ya AK-47 i wanapofanya doria wakiwa Hifadhini wakati wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge walipotembelea chuo hicho mjini Moshi. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shabani Shekilindi (wa pili kulia) akiwa na Wajumbe wa Kamati hiyo wakipewa maelezo huku wakiangalia baadhi ya taswira za wanyamapori mbalimbali wanaotumika kwa ajili ya kuwafundishia wananfunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro wakati kamati hiyo ilipofanya ziara Chuoni hapo.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii wakipewa maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Judith Mwela kuhusiana na handaki lililotengenezwa na kabila la Wachaga mnamo karne ya 18 kwa ajili ya kujihami dhidi ya maadui kabla ya Wajumbe hao kuingia ndani ya Handaki hilo kwa ajili ya kujionea , Handaki hilo lipo katika Chuo hicho

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shabani Shekilindi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na watumishi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shabani Shekilindi akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwasalimia na baadhi ya Watumishi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara Chuoni hapo.

Baadhi ya magari maalum yAnayotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka wakati wanapofanya mafunzo kwa vitendo katika Hifadhi nchini. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII) 

…………………………………………………………………………………………
Wizara ya Maliasili na Utalii imesema imeanza kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto zinazokikabili Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka ili kiendeleze hadhi yake ya kuwa Chuo cha Kimataifa. 

Hatua hiyo inakuja kufuatia kupungua kwa idadi ya wanafunzi wa kigeni wanaojiunga na Chuo hicho kila mwaka. 

Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii iliyotembelea Chuo hicho mkoani Kilimanjaro, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema shabaha ya Wizara ni kukiona chuo hicho kikiendelea kuwa na hadhi ya Kimataifa. 

Amewaeleza Wajumbe hao kuwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Wizara kuendelea kufanya mazungumzo na vyombo vya udhibiti na Usimamizi wa Elimu hapa nchini ( TCU na NACTE) ili viangalie namna ya kuondoa masharti magumu yanayosababisha baadhi ya masomo yanayotolewa na nchi nyingine yasitambuliwe chuoni hapo. 

Mhe.Kanyasu ameiambia kamati hiyo kuwa sababu nyingine ya idadi ya Wanafunzi wa kigeni kupungua ni baadhi nchi kama Malawi na Kenya kuanzisha vyuo vyao tofauti na ilivyokuwa mwanzo. 

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Shabani Shekilindi amesema Chuo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za uhaba wa wahadhiri pamoja na uchakavu wa miundombinu. 


Amesema kupitia Kamati anayoiongoza atahakikisha kuwa changamoto zote zinapatiwa majibu ili chuo hicho kiendelee kutoa huduma bora. Amekishauri chuo hicho kiendelee kuzitangaza kozi zake ndani na nje ya nchi. Naye Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Boniphace Getere amekishauri chuo hicho kiingie mkataba na watu binafsi kwa ajili kujenga mabweni yatayokayosaidia kutatua changamoto ya wanafunzi 228 kati ya 600 wanaolazimika kupanga nyumba nje ya Chuo hicho.
Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori , Mweka kilianzishwa mwaka 1963 kikiwa na wanafunzi 25 kutoka Kenya, Uganda Malawi , Cameroun na Tanzania.

Utoji wa Taarifa za Miradi ya Maendeleo kwa Wananchi ni Takwa la Kisheria- Dkt. Abbasi

$
0
0
Na Frank Mvungi- Mwanza

Watendaji Wakuu wa Serikali katika ngazi mbalimbli wametakiwa kutoa taarifa za miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa maslahi ya wananchi wa maeneo husika ili kuendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza ushirikishaji.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalum jana Jijini Mwanza, Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inawataka Viongozi wote kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

“Kutoa taarifa kwa wananchi ni takwa la Kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria Na 12 ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, hivyo kila Kiongozi ahakikishe kuwa wananchi wanapata taarifa za utekelezaji wa sera na miradi yote inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi” Alisisitiza Dkt. Abbasi.

Akizungumzia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano Dkt. Abbasi amesema kuwa kwa sasa dhamira ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na maisha bora kutokana na dhamira safi ya Serikali ya Awamu ya Tano kulenga kuwakwamua wananchi wanyonge kiuchumi.

Serikali inatekeleza miradi ya kimkakati ya; mradi wa kufua umeme wa mto rufiji, ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa hospitali za Wilaya 67, ununuzi wa ndege sita (06) ambazo tayari zimenunuliwa ili kuhakikisha maendeleo endelevu yanafikiwa kwa maslahi mapana ya Taifa na wananchi wote.

Mkurugenzi Abbasi ameitaja miradi mingine ya ujenzi wa vivuko, meli mpya na za kisasa ambapo tayari bilioni 20 zimetolewa na Serikali kwa ajili kutekeleza kujenga meli, ujenzi wa uwanja changamani na wa kisasa kwa ajili ya kukuza sekta ya michezo eneo la Nane nane jijini Dodoma.

“Miradi yote inayotekelezwa na Serikali imekuwa chachu ya maendeleo na imekuwa chanzo cha kuzalisha ajira kwa wananchi hasa Vijana lengo ni kuhakikisha kuwa wanaiunga mkono Serikali ili azma yakuwaletea maendeleo itimie kwa wakati”. Alisisitiza Dkt. Abbasi.

Katika Kuboresha sekta ya Elimu Serikali ya Awamu ya Tano inatoa zaidi ya bilioni 23 kila mwezi kugharamia elimu bure ili kusaidia kuongeza kasi ya maendeleo hapa nchini kwa kuzingatia umuhimu wa suala la elimu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Paschal Shelutete amesema kuwa Maafisa Habari wote Tanzania wanakutana Jijini Mwanza kwa mkutano mkuu wa Mwaka utaoanza Jumatatu Machi 18 hadi 22, 2019 kwa lengo la kujengewa uwezo Maafisa hao ili kuisemea Serikali katika kuwaeleza wananchi utekelezaji wa miradi inayetekelezwa na Serikali katika maeneo yao.

“Naipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kujali na kuona umuhimu wa Kada ya Mawasiliano Serikalini na kuweka mkazo katika kuimarisha sekta hii kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla” Alisisitiza Shelutete.

Akifafanua hayo, Shelutete amesema kuwa wakati wa mkutano huo Maafisa Habari watajengewa uwezo na kupewa mbinu za kisasa katika kuisemea Serikali katika maeneo yao zikiwemo Wizara, Mikoa, Wilaya, Majiji, Halmashauri, Taasisi, Wakala, Idara zinazojitegemea kote nchini.

Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano kitafanyika Jijini Mwanza kuanzia machi 18-22, 2019 na kinatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa. Mahojiano na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbasi pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) yamefanyika leo machi 15, 2019 Jijini Mwanza wakati wa ziara yao ya kutembelea vyombo vya habari Jijini humo.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images