Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

AIRTEL KUTOA BIL 2.1 KAMA FAIDA KWA WATEJA


BREAKING NEWZZZZ: ZAIDI YA WATU 40 WAUWAWA MISIKITINI CHRITSCHURCH, NEW ZEALAND,

STARTIMES WAJA NA BEBA BEBA KATIKA MSIMU WA HUU WA PASAKA

$
0
0
KATIKA kuelekea kwenye msimu wa siku kuu ya Pasaka Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wametangaza Promosheni na Ofa kubwa katika msimu huu wa sikukuu ya pasaka ambapo wateja wake wataweza kununua vingamuzi vya antenna kwa bei ya punguzo sambamba na kushuka bei ya baadhi ya vifurushi.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja masoko wa Startimes David Malisa amesema kuwa, "Tumejiwekea utaratibu wa kuwapatia wateja wetu na wale wanaotamani kuwa wateja sababu  kufurahia zaidi kila sikukuu zinapofika, Msimu huu wa pasaka tunawaletea Promosheni ya Beba Beba na StarTimes na katika hili tumepunguza bei ya king'amuzi cha antenna kutoka shilingi 79,000 hadi kufikia awali shilingi 69,000 tu na mwezi mmoja bure kabisa kwa kifurushi cha UHURU" ameeleza Malisa.

Mbali na kupunguza bei ya kingamuzi cha Antenna StarTimes wamepunguza bei ya Kifurushi cha UHURU ambapo Malisa amesema kuwa,
"Pia tumepunguza bei ya kifurushi cha UHURU ambacho ni cha juu kabisa kwa watumiaji wa Antenna. Awali wateja walikuwa wakilipia shilingi 24,000 lakini kuanzia leo tarehe 15 Machi bei yake itakuwa Tsh 18,000 tu na Kifurushi hiki  ndicho chenye chaneli zote za burudani, filamu, tamthiliya na michezo bila kupitwa hata na kimoja" amesema.

Aidha ameeleza kuwa 
Katika kipindi chote cha Promosheni ya Beba Beba wateja wa StarTimes watafurahia maudhui ya kiwango cha juu ikiwemo ligi ya kandanda la Ulaya, Europa League ambayo bado inaendelea, tamthiliya za kuvutia kama Wildflower na Waaris.

Promosheni hiyo itaendelea hadi tarehe 31 ya mwezi Mei mwaka huu, huku wakiamini  wateja wao watafurahia bei ya punguzo ya kifurushi cha UHURU, pia wamewataka wateja wanaotamani kujiunga na familia ya StarTimes inayokua kila siku kuwa huu ni wakati sahihi kabisa kwao kwani gharama zimekuwa nafuu kwa ajili yao.
 Meneja masoko wa Startimes David Malisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Promosheni na ofa za msimu wa siku kuu ya Pasaka ambapo wateja wake wataweza kununua vingamuzi vya antenna kwa bei ya punguzo sambamba na kushuka bei ya baadhi ya vifurushi.

SERIKALI YATOA HATIMILIKI ZA KIMILA 100 KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA MBONDO WILAYANI NACHINGWEA

$
0
0
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakitoka kukagua jengo la masijala ya ardhi kijiji cha Mbondo wilayani Nachingwea linalojengwa kupitia MKURABITA wakati wa ziara ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo mkoani Lindi.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Jason Rweikiza (Mb) akieleza umuhimu wa hatimiliki za kimila kabla ya kuwapatia wananchini wa kijiji cha Mbondo wilayani Nachingwea wakati wa ziara ya kamati yake ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Lindi.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mwanne Mchemba (Mb) akitoa wito kwa wananchi wa kijiji cha Mbondo wilayani Nachingwea kuchangamkia fursa ya hatimiliki za kimila wakati wa ziara ya kamati yake ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Lindi.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akieleza azma ya serikali ya kuwainua wanyonge kwa kuwapatia hatimiliki za kimila ili waweze kujikwamua kiuchumi.
 Wananchi wa kijiji cha Mbondo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Jason Rweikiza (Mb) alipokuwa akizungumza nao juu ya umuhimu wa hatimiliki za kimila wakati wa ziara ya kamati yake ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Lindi.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, MJason Rweikiza (Mb) akitoa hatimiliki za kimila kwa mmoja wa wananchi wa kijiji cha Mbondo wilayani Nachingwea wakati wa ziara ya kamati yake ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Lindi.
Mtendaji Mkuu wa MKURABITA, Seraphia Mgembe akizungumzia umuhimu wa wananchi wa kijiji cha Mbondo wilayani Nachingwea kumiliki hatimiliki za kimila wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo mkoani Lindi.


WAKALA WA MAJENGO TANZANIA (TBA) WAPONGEZWA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI

$
0
0
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeupongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kwa kutekeleza miradi wanayoisimamia kwa ubora na kwa gharama nafuu.

Akizungumza mara baada ya kukagua miradi inayojengwa na Wakala huo ikiwemo jengo la ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, pamoja na Jengo la Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma,  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka,  amesema kuwa kamati imeridhishwa na kazi zinazofanywa na wakala huo na hivyo kuutaka wakala huo kutobweteka na badala yake kufanya kazi kwa bidii hata kwa miradi mingine wanayoitekeleza. 

"Sisi kama Kamati ya PAC kiukweli tumefurahishwa na utekelezaji wa miradi hii tulioikagua, tunawapongeza kwa kufanya kazi nzuri na inayozingatia thamani ya fedha", amesema Mheshimiwa Mwenyekiti.

Amesisitiza kuwa Kamati inapenda kuwatia moyo TBA kwa kuendelea  kufanya jitihada katika usimamizi wa miradi iliyonayo ili kuondoa ile dhana iliojengeka ya kwamba kazi zinazotekelezwa na wakala huo zipo chini ya kiwango.

“Tunawapongeza TBA kwa kazi nzuri iliofanyika, baada ya kukagua tumeona kuwa serikali haikufanya makosa kutoa zabuni nyingi za ujenzi kwa TBA”, amesisitiza Mwenyekiti wa Kamati

Aidha, Wakala huo umepongezwa kwa kuweza kutoa fursa kwa wanafunzi walioko na wanaotoka vyuoni kupata mafunzo kwa vitendo ili kuwajengea uwezo ambao utaiwezesha Serikali kupata wataalama zaidi  katika taaluma hiyo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, amesema wizara itaendelea kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi  kutoka vyuo vikuu ili nao waweze kuja kuwa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo nchini kupitia sekta ya ujenzi.

Arch. Mwakalinga, ameahidi kwa Kamati hiyo kuhakikisha kuwa wataendelea kujenga majengo ya Serikali kwa kuzingatia ubora na kwa gharama nafuu.

Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daudi Kondoro, amefafanua kuwa jengo la Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano linalojengwa hivi sasa katika mtaa wa Moshi jijini Dodoma lina ghorofa tatu zenye jumla ya vyumba 84 zikiwemo ofisi za viongozi 15 zenye maliwato ndani, maafisa waandamizi 5, Ofisi za wazi 17, masijala 3, Makatibu Muhtasi 14, vyumba vya chai 4, stoo 3, vyoo 22 na vyoo vya watu wenye mahitaji maalum.

Ameongeza kuwa mradi wa ujenzi wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma umefika asilimia 97 ambapo amesema kuwa kazi zinazofanyika kwa sasa ni kukamilisha kazi ya madirisha, milango ya nje ya jengo pamoja na kukagua na kurekebisha dosari zilizojitokeza wakati wa ujenzi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi)

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (Wa kwanza kulia), wakati Kamati yake ilipokuwa ikikagua maendeleo ya miradi ya Ofisi za Serikali inayosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), jijini Dodoma.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daudi Kondoro, akitoa maelezo ya mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kanda ya Dodoma, Arch. Humphrey Kilo, akionesha mchoro wa Jengo jipya la Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano lililopo mtaa wa Moshi jijini Dodoma kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) walipokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
 Mbunifu Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Hamis Kileo, akionesha mchoro wa Jengo la Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) walipokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mara baada ya kukagua maendeleo ya miradi inayosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), jijini Dodoma.
 Muonekano wa nje wa Jengo la Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Muonekano wa nje wa Jengo jipya la Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano lililopo mtaa wa Moshi jijini Dodoma.

RC Wangabo aonya vitendo vya Rushwa baraza la Ardhi Sumbawanga

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametahadharisha vitendo vya kuchelewesha kusikiliza  mashauri mbalimbali katika baraza la ardhi na nyumba la Wilaya ya sumbawanga hali inayowapelekea wananchi kuhisi kuhusisha ucheleweshaji huo na vitendo vya rushwa na hivyo kuwataka kushikamana na kutafakari kauli mbiu ya wiki ya sheria yam waka huu iliyowataka kutoa haki kwa wakati kwa kushirikiana na wadau.

Amesema kuwa pamoja na mkoa kuwa na baraza moja la wilaya kati ya wilaya zake tatu na hivyo kupelekea kuelemewa na mashauri yanayotoka katika wilaya nyingine za mkoa hiyo isiwe sababu ya wajumbe wa baraza hilo kuchelewesha mashauri jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu.

“Najua kuna mzigo mkubwa na mlundikano wa kesi katika baraza, naambiwa kuna mashauri 399 na mengine 36 yamekaa zaidi ya miaka miwili, lakini pamoja na hayo wananchi nao wanlalamika kuhusiana na baraza la ardhi na nyumba Sumbawanga, moja ya malalamiko makubwa ni kwamba mashauri yanachelewesha ambapo wanachi wanaona kuna mashauri mengine yasingepaswa kuchukua muda mrefu na hili linaungana na lalamiko la pili ambalo linahusishwa baraza hili na vitendo vya Rushwa,” Alisema.

Ameyasema hayo katika hafla fupi ya kumuapisha mjumbe wa baraza la ardhi na nyumba la wilaya ya Sumbawanga Bi. Leticia Sami, ambapo kwa sasa Mkoa wa rukwa una baraza moja tu la ardhi na nyumba ambalo linapatikana katika wilya ya Sumbawanga.

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Sumbawanga Bi. Frida Hamis Chinuku alisema kuwa mchakato wa kumpata mjumbe huo unaanzia kwa majina kupendekezwa na Mkuu wa Mkoa na kisha majina hayo kupelekwa kwa Waziri mwenye dhamana ambapo humteua mjumbe na hatimae mjumbe huyo kuapishwa.  

“Mjumbe yeyote kabla ya kuanza kazi anatakiwa kuapishwa na Mkuu wa mkoa katika Mkoa husika ambako baraza lipo, mchakato wa kumpata mjumbe huyu ulianza mwaka jana 2018 na aliteuliwa rasmi tarehe 5. July mwaka 2018 na kuapishwa leo. Kwa sasa baraza litakuwa na wajumbe jumla wanne japokuwa mjumbe mmoja ni mgonjwa,” Alisema.

Kiapo hicho kinatokana na maelekezo ya Kanuni za mwaka 2003 za Sheria ya namnba 2 ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ya mwaka 2002.
 Bi Leticia Sami (kulia) akitia sahihi katika kiapo chake mbele ya mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) muda mfupi baada ya kula kiapo cha kuwa mjumbe wa baraza la ardhi na nyumba la Wilaya ya Sumbawanga.  
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. joachim Wangabo (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa baraza la ardhi la Wilaya ya Sumbawanga  Frida Chinuku muda mfupi baada ya hafla ya kiapo cha mmoja wa wajumbe wa baraza hilo. 

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA RELI YA KISASA

$
0
0
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), unaoanzia Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa KM 300 na  kusisitiza kuwa Bunge litaendelea kupitisha fedha za mradi huo hadi utakapokamilika kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo  Moshi Sulemani Kakoso, ameyasema hayo eneo la Soga mkoani Pwani mara baada ya kamati hiyo kukagua na kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika mradi huo na kusisitiza  kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuusimamia kwa ukaribu zaidi ili mradi uweze kukamilika kwa wakati .

“Kamati imekagua mradi na imeridhika na hatua za ujenzi wa reli hii hivyo hakikisheni unakamilika kwa viwango vinavyokubalika na ukabidhiwe mwishoni mwa mwaka huu kama mkataba unavyoelekeza”, amesema Kakoso. Aidha, ameipongeza Serikali kwa jitihada zinazoendelea kufanyika, Kampuni ya kikandarasi na wataalamu wote wanaosimamia ujenzi wa reli hiyo kwani kazi nzuri ya usanifu imefanyika ambapo baadhi ya madaraja magari yatapita chini na reli itapita juu na mengine reli itapita chini na magari yatapita juu.

Naye, mjumbe wa kamati hiyo Jafari Michael ambaye ni Mbunge wa Moshi Mjini, ameishukuru Serikali kwa hatua kubwa za ujenzi wa miundombinu ya reli hiyo kwa kuwa inapita katika mikoa sita yenye uzalishaji mkubwa wa mazao na chakula na pia itakuza uchumi wa nchi kwa kupata mizigo kupitia nchi jirani za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Naibu Waziri anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye, amesema kazi ya ujenzi wa tuta la reli umefikia asilimia 64 na miundombinu ya reli hiyo ishalazwa kwa zaidi ya KM 40.
Mhandisi Nditiye ametoa wito kwa wananchi kuitunza miundombinu ya reli kwani inajengwa kwa kutumia fedha nyingi na ni urithi kwa vizazi vijavyo na faida kwa Taifa.

Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea na utekelezaji sera ya kuwawezesha wakandarasi wazalendo ili kuwajengea uwezo katika ujenzi wa miradi ya kati na mikubwa ili kukuza uchumi wa nchi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iko katika ziara ya kutembelea na kukagua miundombinu inayosimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Selemani Kakoso, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, wakati kamati hiyo ilipokagua hatua za maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam - Morogoro yenye urefu wa KM 300, eneo la Soga mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Atashasta Nditiye, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, ilipotembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam - Morogoro yenye urefu wa KM 300, eneo la Soga mkoani Pwani. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati walipokagua hatua za mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam - Morogoro yenye urefu wa KM 300, eneo la Soga mkoani Pwani. 
 Meneja Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Dar es Salaam-Morogoro, Mhandisi Machibya Masanja, akielezea namna ya utandikaji wa reli hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati ilipokagua mradi wa ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa KM 300 mkoani Pwani.
Muonekano wa sehemu ya Reli ya Kisasa iliyojengwa eneo la Soga Kibaha mkoani Pwani ambapo ujenzi wa mradi huu umefikia asilimia 45.

NFRA KUJA NA MKAKATI WA KUWA NA MFUMO WA KIELEKTONIKI WA KUFUATILIA NA KUHIFADHI TAARIFA (COMMODITY TRACKING SYSTEM)

$
0
0
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia Zikankuba akizungumza kwa niaba ya watumishi wenzake Kwenye hafla ya kukabidhi mtambo wa kusafisha nafaka uliotolewa na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na kuzinduliwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Tarehe 15 Machi 2019.


Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma

Kutokana na kukua kwa Technolojia kila siku, na matumizi ya techolojia yanaongeza ufanisi, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza na unaendelea na mkakati wa kuhakikisha kunakuwa na mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia na kuhifadhi taarifa za Hifadhi ya Taifa ya Chakula (Commodity Tracking System). 

Lengo la kuwepo kwa mkakati huo ni kuongeza ufanisi kwa kupunguza mianya ya udanyanyifu na wizi na ili kufikia lengo hilo ifikapo mwishini mwa mwaka 2020, Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umekubali kusaidia kupata ufadhili wa fedha na utaalamu ili kufanikisha lengo hilo. 

Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia Zikankuba wakati akizungumza kwa niaba ya watumishi wenzake Kwenye hafla ya kukabidhi mtambo wa kusafisha nafaka uliotolewa na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na kuzinduliwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb).

Alisema kuwa WFP ni mdau muhimu wa NFRA katika kuzungusha akiba ya chakula huku Utekelezaji wa mauzo ya tani 36,000 ukiwa unaendelea. 

Zikankuba alisema kuwa mpaka sasa Tani zote zimekwisha andaliwa na WFP wamekwisha kuchukua Tani 20,400 huku Tani 15,600 zikiwa zimekwisha andaliwa na zimehifadhiwa vizuri kwa ajili ya WFP kuchukua.

“Mauzo haya moja kwa maana yake ni kwamba Mkulima hasa mdogo anapata fursa ya soko la kimataifa moja kwa moja kwa kuwa NFRA hununua mazao yake moja kwa moja kutoka kwa wakulima” Alikaririwa

Bi Zikankuba alitumia mkutano huo kuujulisha ujumbe wa WFP kuwa NFRA ipo tayari na ina uwezo wa kuuza tani nyingine zaidi baada ya mkataba unaoendelea wa Tani 36,000 kukamilika. 

“Pia tupo tayari kufanya mazungumzo na WFP ili kukusanya na kuwauzia mazao mengine ya nafakai mtama kuanzia msimu ujao wa mavuno” Alisema

Aliongeza kuwa Mikakati na programu mbalimbali zinazoendeshwa na WFP zinasaidia NFRA kupata mazao yenye vigezo kupitia vikundi vya wakulima. Mfano: Katika msimu huu, kati ya vikundi vya wakulima 216 vilivyouza mahindi yao NFRA takribani vikundi 62 vilipata mafunzo ya kutunza na huhifadhi mazao ya nafaka kupitia programu ya Farm to Market Alliance ya WFP.

Shabiki wa Simba ashinda Sh123.6million za M-Bet

$
0
0
Dar es Salaam. Shabiki wa Simba na mkazi wa mkoa wa Songwe, Willy Mwakapembe Wadson ameshinda Sh 123,614,160 baada ya kubashiriki kwa usahihi jumla ya mechi 12 katika za  mchezo wa kubahatisha wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet Tanzania.
Mwakapembe ambaye ni mfanyabiashara ndogondogo na mkulima wa Tunduma anakuwa mshindi wa tatu tokea kuanza  mwaka huu  kushinda kiasi kikubwa cha fedha ambacho amesema kitabadili maisha yake.
Washindi wengine ni Frank Kayombo  ambaye alishinda kiasi cha Sh milioni 188.4 wakati mshindi wa pili alikuwa Simon Muray aliyeshinda Sh milioni  81.
Meneja Masoko wa M-Bet, Allen  Mushi pia alisema kuwa kuna washindi wengi waliojishindia mamilioni kupitia Jackpot Bonus ya kampuni yao.
Mushi amesema kampuni yao inazidi kupata washindi na mpaka sasa jumla ya Sh milioni 500 zimetumika kuwazawadia washindi mbalimbali.
Alisema kuwa kampuni yao inazidi kuwabadili maisha Watanzania huku wakichangia pato la serikali kiasi cha Sh milioni 24.7. Alisema ili kuweza kucheza bahati nafasi hiyo unaweza kutembelea http://bit.ly/2VZCB38ili kuanza kuanza kubet.
“M-Bet inazidi kuchanja mbuga na kuinua vipato vya Watanzania na kuchangia maendeleo ya nchi chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli. Nawaomba Watanzania kucheza  ili kushinda zawadi za fedha,” alisema Mushi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Wadson alisema kuwa alianza kubeti muda mrefu kabla ya kupata ushindi huo mnono.
Alisema kuwa hakukata tamaa pamoja na kutaniwa na marafiki zake wengi kuwa hataweza kushinda fedha nyingi zaidi ya kupoteza muda wake.
“Sikukata tamaa na kuendelea kubeti, niliamini kuwa siku moja nitapata bahati ya kushinda, nashukuru Mungu kupata kiasi hiki cha fedha na nitakaa mke wangu kupanga jinsi gani ya kuwekeza na kujiongezea kipato,” alisema Mwakapembe.
Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (Kulia) akikabidhi mfano wa hundi, Willy Mwakapemba  (katikati) kutoka mkoa wa Songwe aliyeshinda Sh Milioni 123.7 za mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania. Anayeshuhudia ni  Kaimu Msimamizi wa Kitengo cha Michezo ya Kubahatisha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi, Ilala Philipo Haule. 

PREMIER BET YATOA MAMILIONI KWA WASHINDI WA JACKPOT YA SOKA

$
0
0
KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya Premier Bet nchini imetoa zawadi kwa washindi wa Jackpot ya soka iliyofanyika Machi 9 mwaka huu huku washindi wawili  wakijinyakulia vitita vya milioni 42.5 kwa kila mmoja.

Akizungumza na vyombo vya habari Meneja rasilimali watu wa kampuni hiyo Amanda Kombe amesema kuwa jamii imekuwa na uelewa mzuri mara baada ya kuzindua na kuhabarisha umma juu ya promosheni hiyo ya jackpot na kueleza  kuwa katika Jackpot iliyochezeshwa Jumamosi jumla ya shilingi milioni 85 zilikuwa zikishindaniwa na washindi wawili wamepatikana ambao ni Flavian Msigala kutoka Dar es salaam na Robert Daniel kutoka Mpanda ambao kila mmoja amejinyakulia kitita cha shilingi milioni 42 na laki tano.

Amanda amesema kuwa washindi hao waliweza kubashiri kwa usahihi mechi zote 12 na wengine 15 waliweza kubashiri 11  na wengine 52 kubashiri kwa usahihi mechi 10 na hao wote wamebahatika kupata kifuta jasho. Amesema kuwa hiyo ni jackpot ya pili kutoa washindi walibaoshiri kwa usahihi zaidi na ikiwa ni jackpot ya 56 kuchezwa.

Washindi wa Jackpot hiyo wameishukuru Premier Bet nchini kwa kutoa donge hilo ambalo litawasaidia kufanya shughuli za kujiongezea kipato kwao na  taifa kwa ujumla.
 Meneja rasilimali watu wa Kampuni ya  Premier Bet, Amanda Kombe(katikati) akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa hafla ya kutoa utoaji wa milioni awadi kwa washindi wa Jackpot ya soka iliyofanyika Machi 9 mwaka huu huku washindi wawili  wakijinyakulia vitita vya milioni 42.5 kwa kila mmoja leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa  kampuni ya  Premier Bet, Benjamin Mnali.
 Meneja Masoko wa  kampuni ya  Premier Bet, Benjamin Mnali akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo wa kubahatisha pamoja na namna ya kujiunga kwenye michezo ya kampuni hiyo wakati wa hafla ya kutoa utoaji wa milioni awadi kwa washindi wa Jackpot ya soka iliyofanyika Machi 9 mwaka huu. Kulia ni Meneja rasilimali watu wa kampuni ya  Premier Bet, Amanda Kombe
 Mshindi wa Jackpot ya soka, Flavian Msigala kutoka Dar es Salaam akizungumza na waandishi bara baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi milioni 42 na laki tano leo jijini Dares Salaam.
 Mshindi wa Jackpot ya soka, Robert Daniel kutoka Mpanda akizungumza na waandishi bara baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi milioni 42 na laki tano leo jijini Dar es Salaam.

MUONEKANO WA KIKWANGUA ANGA MAENEO YA BIAFRA-MOROCO JIJINI DAR.

$
0
0
Basi la Mwendo Kasi likielekea kituo cha Morocco kushusha na kupakia abiria kuendelea na mzunguko wake wa kawaida kati kati ya jiji la Dar,Usafiri huo pamoja na changamoto za hapa na pale  ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa abiria, lakini ndio umekuwa usafiri mkombozi kwa wakazi wengi wa jiji hilo.

TUGHE MKOA WA TEMEKE WATOA MSAADA KWA YATIMA WA KITUO CHA HIARI

$
0
0
Wafanyakazi wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wa Mkoa wa Temeke, wakiwa wamewabeba watoto Yatima wanaolelewa katika Kituo cha Hiari kilichopo Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam  walipokwenda kutoa msaada leo wa vyakula na vitu mbalimbali zikiwemo nguo ikiwa ni moja ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofikia tamati Machi 8, 2019.
Mratibu wa utoaji msaada huo ambaye pia ni  Katibu wa Tughe mkoa wa Temeke, Litson Magawa, akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo.
 Mratibu wa Jinsia wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) Taifa, Nsubisi Mwasandende (kulia), akizungumza wakati wa kutoa msaada huo.
 Katibu wa Kamati ya Wanawake Tawi la Bohari ya Dawa (MSD) Theresia Mmbaga, akimkabidhi kiroba cha unga, Mama Mlezi wa Kituo hicho, Aminajati Kilemia wakati wa kukabidhi msaada huo.
  Katibu wa Kamati ya Wanawake Tawi la Bohari ya Dawa (MSD) Theresia Mmbaga, akimkabidhi fedha Mama mlezi wa kituo hicho.
 Katibu wa Kamati ya Wanawake Tawi la Bohari ya Dawa (MSD) Theresia Mmbaga, akimkabidhi dawa za meno kwa niaba ya wenzake mtoto Jamila Hiari.
 Mjumbe wa Tughe, Mkoa wa Dar es Salaam wa Kamati ya Wanawake kupitia Mkoa wa Temeke, Mawazo Lugusha (kulia), akizungumza wakati wa kutoa msaada huo.
 Mama Mlezi wa Kituo hicho, Aminajati Kilemia, akitoa neno na shukurani baada ya kupokea msaada huo.
Wawakilishi wa Wafanyakazi wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wa Mkoa wa Temeke wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada huo.

Na Dotto Mwaibale

WAFANYAKAZI wa Taasisi za Umma wametakiwa kujenga tabia ya kusaidia jamii zenye mahitaji mbalimbali badala ya kuiachia serikali kufanya hivyo.

Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Jinsia wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) Taifa, Nsubisi Mwasandende wakati wafanyakazi wa Tughe mkoa wa Temeke wakipokuwa wakitoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watoto Yatima wa Kituo cha Hiari kilichopo Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni moja ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo ilifikia tamati Machi 8, 2019.

"Wito wangu kwetu sisi wafanyakazi wa taasisi za umma tujenge utamaduni wa kusaidia jamii zenye changamoto mbalimbali badala ya kuiachia serikali kufanya hivyo" alisema Mwasandende.

Katibu wa Kamati ya Wanawake Tawi la Bohari ya Dawa (MSD) Theresia Mmbaga alisema ni muhimu kwa wafanyakazi wa taasisi za umma kuimarisha umoja wao na ushirikiano katika kusaidia jamii kama wao Tughe Mkoa wa Temeke walivyofanya.

Mjumbe wa Tughe, Mkoa wa Dar es Salaam wa Kamati ya Wanawake kupitia Mkoa wa Temeke, Mawazo Lugusha alisema sasa ni mwaka wa tatu wamekuwa wakisaidia jamii katika maeneo mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam na kuwa utaratibu huo wataendelea kuuhimarisha kila mwaka.

Katibu wa Tughe mkoa wa Temeke, Litson Magawa alisema huu ni mwanzo tu na kuwa wanajipanga kufanya makubwa miaka ijayo kwa ajili ya kusaidia jamii zenye changamoto.

Mlezi wa Kituo hicho cha Yatima Aminajati Kilemia alishukuru Tughe Mkoa wa Temeke kwa msaada huo na kuelezea kuwa umetoa faraja kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.

Alisema changamoto kubwa waliyonayo ni nyumba ya kuishi watoto hao ambapo alisema hiyo inayotumika sasa wamepanga na kila mwezi wanalipa sh.250,000 na kuwa haikidhi mahitaji kutokana na ongezeko la watoto kutoka maeneo mbalimbali baada ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia.

Alisema katika kituo hicho mahitaji halisi ni watoto 34 lakini idadi hiyo inapanda hadi kufika watoto 54. 

AUAWA WAKATI AKIJARIBU KUPORA PIKIPIKI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

OMARY Abdallah maarufu Mboweto (50) mkazi wa Kagera ,Dar es salaam aliuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi ,kijiji cha Malale kata ya Vihingo, Mzenga Kisarawe mkoani Pwani,baada ya marehemu akiwa na washirika wenzake wawili kufanya jaribio la kupora pikipiki huko Maneromango. 

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema, tukio hilo limetokea  usiku wa kuamkia march 15 mwaka huu .

Alieleza, marehemu kabla ya kuuawa akiwa na wenzake wawili wakitumia gari namba T. 613 DFG aina ya carrina walifika Maneromango na kufanya tukio hilo. 

"Baada ya wananchi kuwashtukia ndipo marehemu alikimbiza gari kwa lengo la kukimbia, 

"Walipofika katika cha Vihingo, gari lao lilipata ajali ya kuingia kwenye korongo ambapo waliacha gari hilo na kukimbia ndipo wananchi waliwakimbiza na kumshambulia marehemu kwa silaha mbalimbali za jadi na mawe na kusababisha kupoteza maisha "alifafanua Wankyo. 

Wankyo alieleza, mtuhumiwa mwingine mmoja Abdul Zuberi maarufu Mvidunda (35)mkazi wa Chamazi alikamatwa maeneo ya Sumbwi wakati akijaribu kutoroka. 

Watuhumiwa baada ya kuhojiwa wamekiri kujihusisha na matukio mawili ya uporaji tarehe 14 January mwaka huu huko Kitonga Kisarawe ambapo walipora pikipiki aina ya sanlg namba MC 324 CDL aina ya haoujue mali ya Haruna Goha. 

Wankyo alisema, tukio jingine walilolifanya ni kupora bajaji eneo la Kibuta mali ya Shukuru Ally february 13 mwaka huu. 

Aidha jeshi la polisi mkoani hapo, limewakamata Ally Said maarufu kwa jina la Sober (37)Ramadhani Hamza -Mijoke (40)na Said Ramadhani -Ubwabwa (37)wakazi wa Mwendapole wakijihusisha na uhalifu wa kushusha mizigo katika magari,yanayotumia barabara kuu ya Dar es salaam kwenda Morogoro kwa jina maarufu Lumbesa /Shushashusha. 

IGP SIRRO AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA KENYA KWENYE MASUALA YA USALAMA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akisalimiana na balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan kazungu leo wakati alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa lengo la kujitambulisha ambapo kwa pamoja wamekubaliana kuendelea kushirikiana kwenye masuala ya kiusalama baina ya nchi hizo mbili. Picha na Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimsikiliza Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu leo tarehe 15/03/2019, wakati alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha ambapo kwa pamoja wamekubaliana kuendelea kushirikiana kwenye masuala ya kiusalama baina ya nchi hizo mbili.Picha na Jeshi la Polisi

TTCL YAZINDUA ENEO LAKE LA MAPOKEZI LIKIWA NA SEHEMU MAALUM YA MAONESHO YA KIHISTORIA YA MAWASILIANO NCHINI

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (wa pili kulia) akikata utepe leo kuashiria uzinduzi wa eneo la mapokezi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) lililopo Makao Makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akishiriki uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (wa kwanza kulia) akizungumza na wageni mara baada ya kuzinduwa eneo la mapokezi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) lililopo Makao Makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam. Anayefuata ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa eneo la mapokezi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) lililopo Makao Makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu akifuatilia.
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (wa pili kulia) akikata utepe leo kuashiria uzinduzi wa eneo la mapokezi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) lililopo Makao Makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akimuonesha Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu eneo maalumu la historia ya mawasiliano lililopo eneo la mapokezi mpya ya Shirika la Mawasiliano Tanzania Makao Makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzinduliwa leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (wa kwanza kulia) akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) mara baada ya kuzinduwa eneo la mapokezi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) lililopo Makao Makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba.

Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (kulia) akiwamiminia shampeni baadhi ya wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akimmiminia shampeni kuashiria uzinduzi wa eneo la mapokezi lililozinduliwa leo Makao Makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa mapokezi hiyo ya kisasa.


SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo limezinduwa eneo la mapokezi ya shirika hilo lililopo Makao Makuu ya Shirika, jijini Dar es Salaam. Eneo hilo lililoboreshwa kwa ukarabati wa kisasa limeongezewa sehemu maalum ya maonesho na historia ya mawasiliano nchini ikiwa ni kutoa elimu zaidi kwa jamii.

Akizinduwa eneo hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja ili kwenda sambamba na maboresho makubwa yanayofanywa ndani ya shirika la TTCL.

Alisema muonekano mpya wa eneo la mapokezi katika Jengo la Makao Makuu ya Shirika hilo ni kielelezo muhimu cha jinsi gani TTCL mpya inavyo wathamini wateja wake kwa kuwapa kipaombele." Tunatambua kuwa bila wao, huduma na bidhaa zetu hazitakuwa na maana yoyote wala hatuta weza kutimiza wajibu wetu kwa Umma na Taifa letu. Hii ndio sababu ya msingi inayotufanya siku zote tuwape Wateja wetu nafasi ya kwanza katika kila mipango tunayoipanga na kuitekeleza," alisema Mhandisi Nundu.

Aliwataka menejimenti na Wafanyakazi wote wa TTCL, kuongeza ubora wa Huduma zinazotolewa na Shirika na hasa Kipengele cha Huduma kwa Wateja ili kukidhi matarajio na mahitaji ya Wateja wake.Aidha aliongeza kwa mwaka 2019, TTCL Corporation imejipanga vyema kuhakikisha kuwa Huduma za shirika hilo inasambaa zaidi kote nchini huku ikisimamia ubora na unafuu wa gharama ambazo Wananchi wote wata zimudu.

"Tunakusudia kuendelea kufanya mageuzi makubwa ndani ya Shirika ili kuliwezesha kushindana kikamilifu katika Soko la Huduma za Mawasiliano nchini sambamba na kutimiza wajibu wa kimsingi wa kuwa mchangiaji muhimu katika Pato la Taifa."Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba awali akizungumza, alisema; "Tunafanya maboresho makubwa katika majengo ya Ofisi za watumishi, Majengo ya kuhifadhia Mitambo na Teknolojia pamoja na Maduka na Vituo vyetu vya Huduma kwa Wateja Nchi nzima."

"Hadi kufikia sasa, Majengo ya TTCL katika Mikoa kumi tayari yamefanyiwa ukarabati mkubwa huku Maduka na Vituo vya huduma kwa Wateja 15," aliongeza kiongozi huyo.Pamoja na hayo Bw. Kindamba alisema kukamilika kwa ukarabati katika eneo hilo la mapokezi lililofanyiwa maboresho kunaongeza uwezo wa kuwahudumia Wateja sambamba na kukabiliana na ushindani kutoka kwa Watoa huduma wengine.
Tupo tayari kuwahudumia wateja; Sehemu ya wahudumu katika eneo la mapokezi  wakiwa katika picha ya pamoja.

Sehemu ya wahudumu katika eneo la mapokezi hiyo wakionesha baadhi ya simu za zamani zilizotumiwa kipindi cha nyuma.

Picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (mwenye koti) kwa baadhi ya viongozi walioshiriki uzinduzi huo.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria yaridhishwa na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa mahakama

$
0
0
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa (Mb.) wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipokuwa ikikagua miradi mbalimbali ya ujenzi wa mahakama Mkoani Mbeya.  “Kamati inaipongeza Wizara ya Katiba na Sheria na Uongozi wa Mahakama kwa kusimamia kwa weledi miradi ya mahakama hapa nchini.” Aliendelea kusema “Kamati inawasihi (Wizara na Mahakama) kuhakikisha mnakamilisha miradi hiyo kwa kuzingatia muda uliopangwa na viwango vyenye ubora uliothibishwa.” Alisema Mheshimiwa Mchengerwa. 

Mheshimiwa Balozi Augustine Mahiga (Mb.), Waziri wa Katiba na Sheria ameambatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa ajili ya ziara ya siku tano (13-17 Machi 2019) ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa mahakama hapa nchini. Ziara hiyo ni ya kwanza tangu Balozi Mahiga alipokabidhiwa rasmi Wizara hiyo tarehe12 Machi 2019 na Mheshimiwa Waziri Profesa Palamagamba Kabudi (Mb.) aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Akieleza ushiriki wa Waziri Mahiga kwenye ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati alieleza kuwa, ni Waziri wa kwanza kuambatana na Kamati hiyo katika ukaguzi wa miradi ya mahakama tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani. Alieleza kuwa, Kamati yake imefarijika sana na kitendo hicho na kuahidi kwa niaba ya Kamati kuendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu mbalimbali.   
Akitoa taarifa ya ujenzi wa miradi hiyo, Waziri Mahiga alieleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2018/19 Mahakama imeendelea kutekeleza miradi 35 ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Alieleza kuwa, pamoja na kukagua miradi ya Mkoa wa Mbeya,  Kamati hiyo itaendelea na ziara ya kujihakikishia utekelezaji wa miradi hiyo kwenye Mkoa wa Njombe, Arusha, na Manyara kabla ya kuanza Mkutano wa 15 wa  Bunge la Bajeti tarehe 2 Aprili 2019.
Alieleza kuwa, kwa mwaka huo wa fedha Mahakama ilitengewa kiasi cha Tshs. 35,973,722,000/= ikiwa ni fedha za maendeleo. Kati ya fedha hizo Tshs. 15,000,000,000/= ni fedha za ndani na Tshs. 20,973,722,000/= fedha za nje. Kati ya fedha zote za ndani Bilioni 5 imeshatumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Naye Kaimu Mtendaji wa Mahakama, Bw. Solanus M. Nyimbi alieleza kuwa, katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo kumekuwa na changamoto kadhaa hususan mtiririko wa fedha za maendeleo; mazingira: jiografia ya eneo, hali ya hewa na aina ya udongo katika maeneo ya mradi; na changamoto za umiliki wa viwanja hususan katika miradi viporo. Alieleza kuwa, pamoja na changamoto hizo wameendelea kujitahidi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati uliopangwa. 

RC MONGELA ARIDHISHWA NA MAANDALIZI KIKAO KAZI CHA MAAFISA MAWASILIANO

$
0
0
Na Ndimmyake Mwakapiso
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. John Mongela, imefanya ziara rasmi katika ukumbi wa BOT kukagua maandalizi ya kikao kazi cha Maofisa Mawasilino Serikali kinachotarajiwa kufungulia na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa, Jijini humo.

Akitoa tathmini yake mara baada ya ukaguzi wa ukumbi wa mkutano huo, Mkuu wa Mkoa ameridhishwa na mandalizi yanayoratibiwa kwa pamoja na Idara ya Habari MAELEZO kwa kushirikiana na Uongozi wa Chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini TAGCO.

“Mnakwenda vizuri, naona kila kitu kipo vizuri na kwa maandalizi haya ni imani yangu kuwa mkutano huu utaenda vizuri na msisite kutufahamisha endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote”.

Mapokezi ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, yaliongozwa na Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo ambaye pia ndiye msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abasi na viongozi wa chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini TAGCO.

Kikao hicho ni cha siku tano kinachotarajiwa kuanza siku ya Jumatatu, Machi 18 hadi Ijumaa 22, mwaka huu kinachotarajiwa kuwakutanisha zaidi ya Maofisa Mawasiliano 300 kutoka Wizara, Mashirika ya Umma, Taasisi za Serikali, Tawala za mikoa na Serikali za mitaa.
Mkuu wa Mkoa huo Mhe. John Mongela,

MADAKTARI WA CHINA WASAIDIA VITABU NA VIFAA TIBA ZANZIBAR

$
0
0
Na Ramadhni Ali – Maelezo Zanzibar 

Timu ya Madaktari wa Kichina wanaofanyakazi Hospitali Kuu ya Mnazimmoja imeikabidhi msaada wa kitabu na Vifaa Tiba Wizara ya Afya Zanzibar kwa ajili ya matumizi ya Hospitali hiyo.

Mmoja wa Madaktari wa timu hiyo, mtayarishaji wa kitabu hicho Dk. Zhang Junjie  alimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdalla  msaada huo katika hafla iliyofanyika Ofisini kwake Mnazimmoja.

Dk. Zhang alisema msaada huo ni muendelezo wa ushirikiano wa miaka mingi uliopo baina ya Jamhuri ya Watu wa China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  katika kuimarisha huduma za Afya.

Alikumbusha kuwa Jamhuri ya Watu wa China ilianzisha ushirikiano wa kuleta Madaktari Zanzibar tokea mwaka 1964 na  utaratibu huo umekuwa ukiendelezwa na kuimarishwa zaidi hadi hivi sasa.

Alieleza matarajio yake kuwa  msaada wa kitabu na vifaa tiba vilivyotolewa vitasaidia katika kuimarisha huduma za afya katika Hospitali ya Mnazimmoja na Hospitali nyengine za Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Ali Abdalla aliishukuru timu ya 28 ya Madaktari wa China kwa msaada wa vitabu ambavyo vitakuwa ni chanzo cha mafunzo kwa Madaktari wa Mnazimmoja.

Aidha alisema vifaa Tiba vitaongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa katika Hospitali hiyo ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya Teknolojia na Rasilimaliwatu.

Mkurugenzi Kinga Dk. Fadhil Abdalla alisema kitabu walichokabidhiwa na Timu ya Madaktari wa China ambacho kinahusiana na matatizo ya maradhi ya njia za mkojo, ikiwemo tenzi dume, vitatumika kama muongozo na mapitio kwa madaktari wakati wa kufanya upasuaji.

Dk. Fadhil aliongeza kuwa kitabu hicho pia kitatumika kuwasomesha Madaktari wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi za Afya ya Binadamu ya SUZA iliopo Mbweni ili kuelewa kwa undani tatizo la maradhi ya njia za mkojo na tiba yake.

Makabidhiano ya Kitabu na Vifaa vya Tiba yalihudhuriwa pia na Naibu Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Zanzibar Shen Qi.
 Mtayarishaji wa kitabu cha maradhi ya njia ya mkoji Dk. Zhang Junjie akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdalla msaada wa kitabu pamoja na vifaa tiba (kushoto) Naibu Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Zanzibar Shen Qi. hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.
 Naibu Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Zanzibar Bi. Shen Qi akitoa maelezo juu ya urafiki wa China na Zanzibar katika hafla ya kukabidhi kitabu na vifaa tiba, (kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Ali Abdalla.
Mkurugenzi Kinga Dk. Fadhil Abdalla akitoa shukran kwa Timu ya Madaktari wa China kwa msaada wa kitabu na vifaa tiba walioutoa, hafla hiyo ya makabidhi imefanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA

$
0
0
 NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 
TIMU ya kitaifa ya kufuatilia na kutatua migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi wakiwemo wakulima, imeingilia kati mgogoro uliodumu kwa miaka saba baina ya wakulima na wafugaji wa Kwala,wilayani Kibaha Mkoani Pwani na kufanikiwa kuumaliza .

Mgogoro huo unabaki historia baada ya wafugaji wa bonde la mto Ruvu  ,Mwembe Ngozi kupewa agizo la kuondoka na kuhamia eneo la Waya,  ranchi ya Taifa NARCO iliyopo Ruvu ili kuwaacha huru wakulima ambao walikuwa wakipata hasara kutokana na mazao yao kulishiwa mifugo.  

Mkurugenzi msaidizi wizara ya mifugo na uvuvi, ambae pia ni mwenyekiti wa timu hiyo, Dr. Martin Ruheta, aliwataka wafugaji hao akiwemo Sauti Mbili na Masanja Kidirgo ambao wana ng'ombe zaidi ya 500 waondoke kuanzia march 18 mwaka huu. 
Aliwaomba, wafugaji hao na wengine waondoke huku serikali ikiendelea kutafuta maeneo ya kudumu, kwa wale ambao mifugo haitoenea kwenye ranchi hiyo. 

"Timu hii ilianza kazi mwezi octoba mwaka jana, mkoa wa Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya ambapo kwa mkoa wa Pwani walianzia Mkuranga, Rufiji, Kisarawe na Leo tunamaliza mgogoro huu hapa Kwala "alifafanua Ruheta. 

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alibainisha ,kwasasa hawaombi tena, bali kuanzia jumatatu ijayo waondoke na atakaekaidi akikutwa ng'ombe wake atakuwa halali kwake .

Assumpter aliyaasa, makundi hayo yaheshimiane ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima. 

Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji (CCWT) Esta Moreto alisema ameridhishwa na maagizo hayo ila anaomba wafugaji waondoe mifugo na sio makazi yao kwakuwa wengine wana wanawake wajawazito na watoto. 

UNAMKUMBUKA AHMED KIPANDE?

$
0
0
Mwanamuziki Ahmed Kipande, alishiriki kikamilifu katika uhamasishaji wa maendeleo na kupigani Uhuru wa Tanganyika akiwa na bendi yake ya Kilwa Jazz.

Bendi hiyo ilishiriki kikamilifu siku Tanganyika inapata Uhuru Decemba 09, 1961 kwa kimba wimbo wa kusifia nchi yetu kupata Uhuru toka wa Wakoloni wa Waingereza.

Aidha chini ya uongozi wake Ahmedi Kipande, bendi yao ilishiriki kikamilifu kutoa burudani wakati mikakati ya kufanya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye meneo ya Makao Makuu ya bendi hiyo jijini Dar es Salaam mwaka 1964.

Juhudi zao katika muziki zilipelekea kuteuliwa na serikali ya Tanganyika kwenda kushiriki sherehe za Uhuru wa nchi za Malawi na Uganda.

Wasifu wa Ahmed Kipande iliyoelezewa na mwanawe wa mwisho Kipande Ahmed, alesema kwamba jina kamili la  baba yake alikuwa ikiitwa Ahmed Mohammed Kipande.Mrisho alitamka kuwa baba yake alizaliwa mwaka 1937, huko Kilwa Kivinje mkoani Lindi.

Miaka michache baada ya kifo cha mama yake Ahmed Kipande alifuatana na baba yake kuja Dar es Salaam. Baada ya kufika,  na alianza masomo katika shule ya Uhuru Wavulana maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Katikati ya miaka ya 1950, Kipande alianza kupiga muziki akitumia ala iitwayo Violin, katika bendi ya Tanganyika Jazz iliyokuwa ikiongozwa na Zimbe Kidosi.Bendi hiyo ilikuwa  na makao makuu yake mtaa wa New Street ambao hivi sasa unaitwa Lumumba.

Wanamuziki wa miaka hiyo walianzisha bendi wakizipa majina ya maeneo yale  wanakotoka. Hivyo waanzilishi wa Rufiji Jazz walitoka Rufiji, na ndivyo ilivyokuwa kwa Kilwa Jazz, Ulanga jazz na kadhalika.
Ahmed Kipande aliyekuwa ametoka Kilwa Kivinje mkoani Lindi, nae akishirikiana na mwanamuziki mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Shamte, wakaamua kuanzisha bendi ya watu kutoka Kusini ya Kilwa Jazz mwaka 1958.

Kilwa Jazz ikaanza kujizolea umaarufu kwa kutunga na kuimba nyimbo mbali mbali zikiwemo za siasa, mapenzi na za uhamasishaji kupata Uhuru wa Tanganyika.Kipande alitunga na kuimba wimbo wa TANU yajenga nchi, nchi yetu,  enyi Vijana tujenga yetu Doli na It can be done, play your party.

Zingine zilikuwa za Roza waua,‘Nipate lau nafasi, Nacheka cheka Kilwa leo na ule wa  Maneno hayafai

Nyimbo hizo zote zilizotajwa hapo juu, Ahmed Kipande na wanamuziki wa bendi hiyo walifanya kukopi nyimbo toka Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo akina Tabu Ley na John Bokelo.Wimbo wa ‘Mokolo Nakokufa’ halikadhalika nyimbo za Nacheka cheka Kilwa leo na Maneno hayafai ambazo kwa ujasiri wao ‘waliukopi na kupesti’ toka wimbo wa Course au Povouir wa T.P.OK. Jazz.

Mwaka 1973 Kilwa jazz ilialikwa na kutumbuiza kabla ya onyesho la gwiji la muziki wa dansi, Franco Luambo Makiandi na bendi ya T.P.OK. Jazz  iliyefanya onyesho kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Luambo Makiadi baada ya kuzisikiliza nyimbo hizo, alimfuata Ahmed Kipande na kumpongeza kwa umahiri wake mkubwa wa ‘kokopi na kupesti’ pasipo kukosea.

Mrisho akimsifia baba yake Kipande Ahmed, alisema kwamba mwaka 1961 siku Tanganyika inapewa Uhuru toka kwa Wakoloni, bendi ya Kilwa Jazz ilikuwa Uwanja wa taifa ikiporomosha muziki ambapo ilitoka na wimbo wa  kumshukuru mungu kwa kupata Uhuru.
Mtoto huyo japom hakuwepo wakati huo, ameukariri wimbo huo wa marehemu Ahmed. Aliimba mistari michache ya wimbo huo.
 “ Ewe mola tunakuomba uibariki Tanganyika yetu na jirani  zetu, Uhuru tumepata lakini Nyoyo zina sikitika wenzetu wanateseka  Wakoloni wa mewashika…”
Bendi ya Kilwa Jazz ilikuwa na makao makuu yake katika kona ya mitaa ya Muhoro na Jangwani ambako siku moja ilipiga muziki nje ya ofisi yao, iliwashangaza watu kuona bendi hiyo ikipiga muziki mchana.
Lakini ilikuwa mipango kamambe ikipangwa maeneo hayo kwa viongozi Wanamapinduzi siku chache kabla ya mapinduzi ya Zanzibar viongozi wakipanga mikakati ya mapinduzi yaliyouondoa utawala wa Kisultani mwaka 1964 huko Zanzibar.
Bendi ya Kilwa Jazz baadaye haikuelewa na jamii. Wengine wakafika mbali zaidi wakizusha maneno kwamba bendi hiyo ni ya serikali. Sababu eti ilikuwa ikialikwa kutoa burudani katika sherehe nyingi za kitaifa!
Bendi hiyo pia ilialikwa kutoa burudani katika sherehe za ndoa ya mmoja wa mawaziri wa serikali ya Tanganyika wakati huo, Oscar Kambona.

Ahmed  Kipande katika sherehe hiyo alionesha kipaji chake kwamba si cha kubahatisha.
Alitunga wimbo wa papo kwa papo wa kuwasifia wanandoa hao Oscar Kambona na mkewe.

Yaelezwa kwamba Kambona aliinuka toka kwenye kiti cha maharusi na  kwenda kumkumbatika Kipande kisha akamtuza kwa pesa. 
Ni miaka 32 sasa tangu Ahmedi Mohammed Kipande afariki dunia  Aprili 27, 1987 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa kipindi kirefu.
Kipande alizikwa kwenye  makaburi ya Tandika Maguruwe, mkoani Dar es Salaam  Aprili 28,1987.

Mugu ailaze roho ya marehemu Ahmedi  Kipande  pahala pema peponi, amina.  

Mwisho.
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa  namba: 0713331200, 0767331200, 0736331200 na 0767331200

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images