Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

TPDC YAKABIDHI KAMBI NAMBA 8 KWA SERIKALI YA KIJIJI CHA NJIA NNE WILAYA YA KILWA

0
0
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kuimarisha huduma mbalimbali za kijamii kwa Vijiji na Mitaa inayoguswa na miundombinu ya bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. Katika kufikia azma hii TPDC imekabidhi kambi Namba 8 kwa kijiji cha Njia nne Wilayani Kilwa ili Kijiji kiweze kupanga matumizi sahihi ya Kambi hiyo.

Kukabidhiwa kwa majengo ya Kambi hayo kunatokana na kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya bomba la gesi asilia kutoka Madimba-Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam, hivyo kufanya majengo hayo kutotumika tena kwa shughuli za ujenzi. 

Akikabidhi rasmi kambi hiyo kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Njia nne hivi karibuni, Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TPDC Bi. Marie Msellemu alisema kuwa “Mikoa ya Lindi na Mtwara ni wadau wakubwa katika ustawi wa miundomibinu ya bomba la gesi asilia na tumekuwa tukishirikiana katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo na ya kijamii ikiwemo afya, michezo, utawala bora na maji lengo ikiwa ni kudumisha mahusiano mema na kuboresha huduma muhimu za kijamii, na hivyo kuwataka wananchi wa mikoa hii ya kusini kushirikiana na TPDC katika kuilinda miundombinu ya gesi asilia na kwa pamoja kuboresha huduma za jamii’’.
Muonekano wa sehemu ya jengo la Kambi ya Kijiji cha Njia nne Wilaya ya Kilwa
Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TPDC Bi. Marie Msellemu akikabidhi hati ya makabidhiano ya Kambi Namba 8 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Dr. Khalfan Ilekizemba.
Hati ya Makabidhiano ya Kambi Namba 8 kati ya TPDC na Kijiji cha Njia nne, Wilayani Kilwa.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi Kambi hiyo, Kaimu Mkurugezi wa Wilaya ya Kilwa Dr. Khalfani alitoa shukrani za dhati kwa TPDC kwa kuwa mdau mkubwa na wa karibu katika shughuli mbalimbali za maendeleo Wilayani Kilwa hasa katika kuboresha sekta ya elimu na afya.

‘Tunalishukuru Shirika la TPDC kwa kutupatia kambi hii ambayo itasaidia Halmashauri na Kijiji kupanga matumizi sahihi katika nyanja ya afya, Shule au nyumba za watumishi wa umma’’. Pia, alisema kuwa tayari kambi hiyo yenye uwezo wa kuchukua kaya/familia 25 imeshaanza kutumika kwa kusaidia makazi kwa waajiriwa wapya wa Halmashauri. 
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Daktari Khalfani akiwa na jopo la wadau wa maendeleo katika hafla ya kukabidhi kambi. 

Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Tingi Bw. Bayani Saidi Mtenda katika kutoa shukrani zake alisema sambamba na TPDC kutoa Kambi hiyo , Serikali ya Kijjji na wananchi kwa ujumla wanawajibu wa kuilinda na kuhakikisha usafi wa mazingira unaimarishwa ili iweze kudumu na kuwa na tija kwa manufaa ya Kijiji. 

Aidha, alisema kwamba Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya Kijiji ndiyo utakaoamua na kupanga matumizi ya kambi hiyo ikiwa ni pamoja na kupanga Kodi/tozo kwa watakaobahatika kuyatumia majengo ya Kambi hiyo. 

Bw Bayana alitoa wito kwa TPDC na wadau wengine wa maendeleo kuendelea kusaidia shughuli za maendeleo kijijini hapo kwani Kijiji kinachangamoto kubwa hasa katika Sekta ya elimu na kuweka bayana mapungufu ya vyumba vya madarasa hali inayopelekea wanafunzi kusomea chini ya miti.

UJUMBE WA SHIRIKA LA NGUVU ZA ATOMIKI DUNIANI KANDA YA AFRIKA WAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR

0
0


Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika, Shirika la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Prof. Shaukat Abdulrazak akizungumza na uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar ulioongozwa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Asha Ali Abdalla (kushotoni kwake).

Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Nguvu Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Lazaro Busagala akisisitiza jambo katika mkutano uliowashirikisha viongozi wa Wizara ya Afya na Ujumbe wa Shirika hilo uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.

Baadhi ya wakuu wa vitengo mbali mbali vya Wizara ya Afya wakimikiliza Mkurugenzi wa Shirika la nguvu za Atomiki Duniani (hayupo pichani) Profesa Shaukat Abdulrazak.Picha na Makame Mshenga.



Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar


Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Profesa Shaukat Abdulrazak amesema Shirika hilo litaongeza ushirikiano na Zanzibar ili kuona linatoa mchango mkubwa zaidi katika kukuza maendeleo ya sekta mbali mbali.

Profesa Shaukat alieleza hayo alipofanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Asha Ali Abdalla ofisini kwake Mnazimmoja.

Alisema lengo kuu la kufika Zanzibar kwa ziara ya kutwa moja ni kukutana na watendaji wa sekta mbali mbali ili kuwaeleza juu ya nafasi kubwa iliyopo ya kuongeza ushirikiano kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar.

Alisema ushirikiano baina ya Shirika la IAEA na Tanzania ulianza tokea mwaka 1976 na linatoa ufadhili katika miradi mbalimbali inayohusisha sekta za Afya, Kilimo, Maji, Mifugo, Rasilimaliwatu, Nishati na Viwanda.

Kwa upande wa Zanzibar Profesa Shaukat alisema Shirika hilo limesaidia katika kupambana na changamoto ya kuteketeza magonjwa yote yanayoambukizwa na Mbung’o na hivi sasa magonjwa hayo sio tatizo kubwa.

Alisema pamoja na kufadhili sekta mbali mbali, Shirika hilo limeweka kipaumbele katika kuwajengea uwezo watendaji kwa kuwapa mafunzo ili kupata uelewa mpana zaidi katika kutekeleza majukumu yao.

Aliweka wazi kuwa Shirika la IAEA limeandaa mpango wa kuimarisha vitengo vinavyoshughulikia maradhi ya Saratani katika Hospitali zinazoshughulikia maradhi hayo baada ya kuonekana yanaongeza kwa kasi katika nchi nyingi zinazoendelea.

Alisema kwa mujibu wa idadi ya Watanzania kunahitajika kuwa na mashine 55 zinazotoa huduma ya mionzi kwa wagonjwa wa Saratani hata hivyo utafiti waliofanya wamegundua zipo mashine tano tu katika Hospitali tatu zinazotoa matibabu hayo ikiwemo Ocean Road na Bugando.

Alisema kuwa mradi wa nguvu za Atomiki Duniani katika Kanda ya Afrika unahusisha nchi 45 ambapo unajikita katika uhusiano wa ushirikiano katika nyanja tofauti.

Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dk. Jamala Adam Taib aliueleza ujumbe huo kuwa Serikali itajenga Hospitali kubwa katika eneo la Binguni na Kitengo maalum cha maradhi ya Saratani kimepewa kipaumbele.

Alilishauri Shirika la IAEA kutoa msukumo zaidi suala la rasilimaliwatu na mafunzo kwa watendaji wa Kitengo cha Saratani ili baada ya kukamilika Hospitali ya Binguni kuwe na nguvukazi ya kutosha.

Akizungumza katika kikao hicho Daktari wa huduma za Saratani Hospitali kuu ya Mnazimmoja Dk. Abdulrahaman Said alisema Kitengo kinachoshughulikia maradhi hayo hivi sasa kina madaktari wawili na wengine watatu wapo masomoni na miaka michache ijayo kitaimarika kufikia madaktari watano.

Alisema hivi sasa Kitengo Saratani kinatoa huduma ya dawa na upasuaji tu kwa vile hawana mashine ya mionzi kwa wagonjwa wa maradhi hayo na hulazimika kwapeleka Hospitali ya Ocean Road Dar es salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Ali Abdalla alimshukuru Profesa Shaukat Abdulrazak kufika Zanzibar akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Lazaro Busagala na kueleza matarajio yake kuwa ziara hiyo italeta manufaa makubwa kwa Zanzibar.

RC Wangabo atoa maamuzi mazito baada ya makusanyo ya bilioni 1.34 kuwa mikononi mwa watendaji

0
0


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo

……………………………………………………

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa siku saba kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, kuhakikisha anaunda timu ya uchunguzi ili kuwabaini wadaiwa wa shilingi bilioni 1.34 za makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri na kuwachukulia hatua wahusika wote ili kuleta ustawi katika utekelezaji wa majukumu ya kiserikali.

Amesema hayo baada ya kupitia taarifa za makusanyo na kubaini tatizo la kutowasilishwa kwa makusanyo ya mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa Local Governent Revenue Collection Information System (LGRCIS) na kueleza kuwa kumekuwa na watendaji ambao sio waaminifu wanaokabidhiwa makusanyo hayo na kuyaingiza kwenye matumizi binafsi wakitegemea kurudisha na matokeo yake Bili za wakusanyaji hazikubali kutoka kwenye mfumo hadi fedha zote alizokusanya zitimie.

Akitolea mfano halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mh. Wangabo alisema kuwa “hadi kufikia mwezi Februari mwaka 2019, jumla ya Shilingi Milioni 98 zimetumika kama sehemu ya gharama za wakusanyaji baada ya kuzikata na kutumia. Matokeo yake fedha zinapelekwa Halmashauri zikiwa pungufu na kuongeza kuwa jumla ya shilingi 241 za halmashauri hiyo zilitumika kabla ya kupelekwa benki jambo hilo ni kinyume na kifungu cha 32 cha Memoranda ya Fedha za Serikali za Mitaa.”

Alitoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo elekezi kwa waheshimiwa madiwani kutoka katika halmashauri zote nne za Mkoa wa Rukwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga ambapo Mh. Wangabo alikuwa mgeni rasmi wa semina hiyo.

Akitoa neno la Shukurani kwa mgeni rasmi mstahiki Meya wa manispaa ya Sumbawanga alipongeza juhudi za mkuu wa mkoa wa Rukwa kuhakikisha anasimamia vyema maendeleo ya mkoa huo, na kumuhakikishia kuwa hawatamuangusha katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaongezeka

“ Sisi kama ALAT mkoa na nipende kuwaarifu madiwani wa halmashauri zote na itakuja kwenye vikao vyenu, tuliona kuliko kulalamika kwa kusema hatuna vyanzo vya mapato, halmashauri za mkoa wa Rukwa zina migogoro mingi ya ardhi kwa kutopanga matumizi ya ardhi, hivyo tumeamua ardhi zote ndani ya mkoa zipimwe na tumeshanunua mashine ya Alat K yenye thamani ya Shilingi Milioni 37 ili tuongeze mapato kwa kupima ardhi,” Alisema.

Hadi kufikia tarehe 12 mwezi Machi mwaka 2019 Manispaa ya Sumbawanga in wadaiwa wa makusanyo ya mapato ya ndani shilingi milioni 45.97, Sumbawanga Vijiji Shilingi Milioni 756.17, Wilaya ya Kalambo Shilingi Milioni 252.64 na Wilaya ya Nkasi Shilingi Milioni 290.95

MKOA WA KATAVI WAZINDUA MPANGO WA KUTANGAZA UTALII WAKE

0
0



Mkuu wa mkoa wa Katavi Amos Makala katikati akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mlele Rachel Kasanda, Dk Theresia Olemako kutoka taasisi ya Jane Godall, , akifuatiwa na Mkuu wa hifadhi ya Katavi Stephano Msumi na kaimu katibu tawala mkoa wa Katavi Awaryiwa Nnko pamoja na watendajiwengine wa mkoa huo.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Amos Makala akisoma moja ya bango linaloielezea mbuga ya wanyama ya Katavi.

Baadhi ya picha zikionyesha baadhi ya wanyama wanaopatikana katika mbuga ya wanyama wa Katavi mkoani Katavi.
Mkoa Wa Katavi Umezindua Rasimu Ya Mpango Mkakati Wa Miaka Kumi Ya Kukuza Sekta Ya Utalii Mkoani Katavi Kwa Lengo La Kuongeza Watalii Kutoka Wastani Wa Watalii 3340 Waliotembelea Hifadhi Hiyo Mwaka 2018 Hadi Kufikia Watalii 6012 Mwaka 2029

Akizungumza Mara Baada Ya Kuzindua Rasimu Hiyo Bwana Makalla Amesema Mpango Huo Utawezesha Kukuza Uchumi Wa Mkoa Wa Katavi

Aidha Mkuu Huyo Wa Mkoa Wa Katavi Amewataka Wananchi Kuacha Tabia Ya Kuharibu Mazingira Ili Kuwa Na Maeneo Ya Wanyama Pori Sanjari Na Kuwataka Waandishi Wa Habari Kutumia Taaluma Yao Katika Kuutangaza Utalii Katika Mkoa Wa Katavi Kwani Ni Mkoa Wenye Vivutio Vya Kipekee

Awali Akitoa Taarifa Ya Hifadhi Ya Taifa Ya Katavi Mkuu Wa Hifadhi Hiyo Bwana Stephano Msumi Amesema Wamefanikiwa Kudhibiti Ujangili Wa Tembo Kwa Asilimia Mia Moja Ambapo Kwa Mwaka Uliopita Hakuna Tembo Hata Mmoja Aliyeuwawa

Katika Uzinduzi Huo Kaimu Mtendaji Mkuu Wa Taasisi Ya Jane Goodall Dk. Theresia Olemako Alipata Nafasi Ya Kuwasilisha Mada Juu Ya Wanyama Aina Ya Sokwe Mtu Na Kusema Mwaka 1900 Kulikuwa Na Sokwe Mtu Zaidi Ya Milioni Mbili Lakini Sasa Wamebaki Sokwe Laki Tatu Tu

Mkuu Huyo Wa Mkoa Aliambatana Na Baadhi Ya Wajumbe Wa Kamati Ya Ulinzi Na Usalama Pamoja Na Watendaji Mbalimbali Ambao Walipata Fursa Ya Kutembelea Hifadhi Ya Katavi; Ambapo Walipata Nafasi Ya Kujifunza Namna Mzimu Wa Katabi Unavyoaminiwa Na Watu Wa Jamii Ya Wabende Na Wapimbwe

Haji Manara anakwambia Njoo Taifa kibingwa Jumamosi uje uwape support Wafalme

0
0
Andika historia yako kuja Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Jumamosi hii kuwashuhudia Mabingwa wa nchi Simba SC wakifuzu kuingia Robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika. 

TBT: Gardiner G. Habash's Je wajua TV show on Michuzi online TV

LUGOLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KITUO CHA TRAFIKI BUIGIRI MKOANI DODOMA, BAADA YA KUPATA MALALAMIKO YA MADEREVA

0
0

Na Mwandishi Wetu, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha Askari wa Usalama Bararani (Trafiki) Buigiri Mkoani Dodoma, baada ya kupokea malalamiko mara kwa mara kutoka kwa madereva wanaoitumia barabara hiyo.

Lugola alifika katika kituo hicho kilichopo barabara kuu ya Dodoma-Morogoro, nje kidogo ya Jiji la Dodoma, saa kumi alasiri akiwa ameambatana na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani humo, SSP Nuru Selemani, na kuanza kutaka kujua utendaji kazi wa askari hao katika kituo hicho.

Akizungumza na askari hao, Lugola aliwataka wafanye kazi kiweledi bila kuwaonea madereva kwa kuwaomba rushwa au kuwapiga faini kwa uonevu.

“Licha ya kuwapongeza kwa kazi nzuri kwa kuyaongoza magari lakini mnapaswa kufuata sheria na si kufanya kazi kwa uonevu, nimekua napokea malalamiko mara kwa mara kutoka kwa madereva kuhusu kituo hiki, fanyeni kazi kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani zinavyoelekeza,” alisema Lugola.

Kwa upande wake SSP Selemeni, alimweleza Waziri huyo kuwa, wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utendaji wa kazi zao, lakini maelekezo ya utendaji kazi wa weledi waliopewa wameyapokea na kuahidi kuyafanyia kazi.

Lugola alisema yeye ni Waziri ambaye anafuatilia maagizo yake kila anapoyatoa, hivyo askari ambao wanachafua Jeshi la Polisi hatawavumilia, na ataendelea kufanya ziara za kushtukiza kama hizo mara kwa mara sehemu mbalimbali nchini.

Waziri huyo yupo njiani kuelekea Mjini Morogoro kwa ajili ziara ya kikazi atakayoifanya Kesho Machi 15, Tarafa ya Kimamba, Wilayani Kilosa, Mkoani humo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, SSP Nuru Selemani (katikati) katika kituo cha Trafiki Buigiri kilichopo nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Waziri huyo alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa madereva kuonewa mara kwa mara na askari katika kituo hicho. Hata hivyo, askari hao walimweleza Waziri huyo utendaji kazi wao pamoja na changamoto wanazozipata kituoni hapo. Kulia ni Askari wa Usalama Barabarani wa kituo hicho, CP Amina. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimfafanulia jambo na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, SSP Nuru Selemani katika kituo cha Trafiki Buigiri kilichopo nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Waziri huyo alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa madereva kuonewa mara kwa mara na askari katika kituo hicho. Hata hivyo, askari hao walimweleza Waziri huyo utendaji kazi wao pamoja na changamoto wanazozipata kituoni hapo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MWAKYEMBE AKEMEA UHARIBIFU WA MAENEO YA KIHISTORIA KWA LENGO LA KUTAFUTA MADINI

0
0



Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) akisoma maelezo leo kwenye sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mjini Tabora wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na wananchi leo kwenye sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mjini Tabora wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na watumishi na viongozi mbalimbali leo wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.



Baadhi ya watumishi na viongozi wa Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha ) wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.



Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe (kulia) akisalimiana na watumishi leo wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.
Picha na Tiganya Vincent

……………..

NA TIGANYA VINCENT

SERIKALI imewataka wananchi kuacha tabia ya kuharibu maeneo ya kihistoria ikiwemo majengo ya kale kwa madai potofu kuwa kwenye maeneo hayo wakoloni walificha madini ndani yake.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.

Alisema vitendo vya aina hiyo vinasababisha Serikali kutumia gharama kubwa pindi wanapotaka kukarabati na kurudisha historia ya maeneo hayo.

“Hakuna ambaye ni mjinga aweke ndani ya nyumba dhahabu halafu asiifuate…hata wangekuwa wameweka mali ndani ya majengo yao wamekuja na njia nyingine ya kutaka kuendeleza maeneo hayo kwa kuweka miradi ya kuchimba visima ili wachukue madini kama yangekuwepo” alisema.

Mwakyembe alisema maeneo hayo ni muhimu sana katika Historia ya Tanzania na pia katika ukuzaji wa utalii kwa ajili ya kulipatia Taifa fedha za kigeni. Aliongeza kuwa maeneo hayo ni muhimu katika kutoa elimu kwa vijana wa kitaifa kufahamu historia ya nchi yao kwa ajili ya kuwa wazalendo wazuri wa Tanzania. Mwakyembe alisema Wizara yake inaewndelea na utaratibu wa kuyaorodhesha maeneo yote ya kihistoria kwa ajili ya kuyahifadhi na kuyakarabati kwa ajili faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Aidha Waziri huyo alisema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni Muswada wa Sheria ambayo utafanya maeneo ya kihistoria yasiguswe na kuzuia uharibifu. Alisema baada ya muswada huo kupitishwa na hatimaye kuwa Sheria utasaidia kulinda utajiri wa urithi wa Kihistoria ulipo hapa nchini usiweze kuharibiwa na kupotea. Katika hatua nyingine Mwakyembe alisema Serikali itahakikisha inarudisha nchini Fuvu la Kichwa cha Mama Shujaa mpiga ukoloni wa Kijerumani kutoka Singida Bibi Liti.

Alisema Shujaa huyo aliweze kupambana na Wajerumani kwa kutumia nyuki hadi hapo aliposalitiwa na wenzake na hatimaye Wajerumani wakata kichwa chake na kuondoka nacho.

Mwakyembe alisema lazima fuvu la kichwa lirudishwe nchini na kuhifadhiwa katika jumba maalumu kwa ajili ya historia ya Tanzania

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Atoa Ufafanuzi Mwananchi Aliyebambikiziwa Kesi na Polisi

SERIKALI YAOKOA BILION 3.4 KWENYE MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO

0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma. Wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe na wamwisho ni Mwenyekiti wa Chama cha Magonjwa ya Figo nchini Dkt. Kisanga
Waandishi wa Habari waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.


Na WAMJW-DOM.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali imefanukiwa kuokoa kiasi cha Shilingi Bilion 3.4 ambacho kingetumika katika matibabu kwa Wagonjwa wa Figo nje ya Nchi.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo leo Machi 14 wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma ikiwa ni Siku ya Figo Duniani ambayo inaongozwa na kauli mbiu ya Afya ya figo kwa kila mmoja kila.Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu.

“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka wagonjwa nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya wagonjwa. 80 mpaka 100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.” Alisema Dkt. Ndugulile

Aidha, Dkt, Ndugulile amesema kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia magonjwa ya figo ni pamoja na uzito wa kupindukia (obesity), matumizi makubwa ya sigara, unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara,kutokufanya mazoezi na kunywa madawa kiholela hasa dawa za kupunguza maumivu.Aliendelea kusema kuwa, magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu ni magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha matatizo ya figo, magonjwa haya yakitambuliwa mapema yanaweza kudhibitiwa kwa matibabu na kuepusha madhara kwenye figo.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa Kufikia Desemba mwaka 2018, jumla ya vituo 28 vyenye jumla ya wagonjwa 1050 vilikuwa vikitoa huduma ya usafishaji damu katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro na Dodoma.Mbali na hayo, Dkt. Ndugulile amesema Serikali imepiga hatua kubwa ya kuanzisha huduma za kupandikiza figo hapa nchini katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Figo nchini Dkt. Onesmo Kisanga amesema kuwa Ugonjwa wa Figo ni tatizo kubwa nchini huku wananchi wengi wakiwa na uelewa mdogo juu ya athari na visababishi vya ugonjwa huo.

Aidha Dkt. Onesmo amewataka wananchi kuacha tabia ya kunywa dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu hivyo kuepuka kuzalisha sumu mwilini na kupelekea ugonjwa wa figo.Hata hivyo Dkt. Onesmo Kisanga ameishukuru Serikali kwa kuwaendeleza kimasomo wataalam kwenye upande wa matibabu ya figo ambao sasa wamesambazwa sehemu mbali mbali ndani ya nchi kutoa huduma za matibabu.

Naye Dkt. Grace Maghembe Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya amesema ungojwa huu umekuwa ukiwaathiri zaidi wakazi wa mijini kuliko vijijini kutoka na mfumo wa maisha uliopo sasa ambapo watu wengi wamekuwa hawazingatii mtindo bora wa maisha kwa kutofanya mazoezi pamoja na kula chakula bora.Dkt. Maghembe amesema bado ipo changamoto kwenye matumizi ya dawa za mitishamba ambazo bado hazijatambuliwa na kuthibitishwa huku akiwataka wananchi kuwa waangalifu pia kwenye matumizi ya dawa hizo.

“Serikali inatambua umuhimu wa tiba mbadala pamoja na matibabu ya tiba za asili na ndio maana zipo taasisi za serikali zinazohusika kuzitambua dawa hizo ni zipi na zina vitu gani na unatakiwa kutumia kwa kiwango gani” amesema Dkt Maghembe nakuwataka watengenezaji wa dawa hizo kufuata taratibu zilizopo ili kuthibitisha na kusajili dawa zao.

RC ARUSHA AZURU KAYA ZILIZODHANIWA KUATHIRIKA KWA MAJI SAFI KUCHANGANYIKA NA MAJI TAKA

0
0


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari katika mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kuwatembelea wananchi ili kuwasikiliza na kujua ukweli kuhusiana na sakata la maji mkoani hapo. Picha na Vero Ignatus.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,Mhandisi Ruthy Koya akiongea na waandishi wa habari ambapo amesema wataalam wamechunguza maji hayo na kubaini kuwa hayana tatizo na kusisisitiza wananchi kuendelea kuyatumia kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Ghambo, kushoto kwake ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Hospitali ya Mkoa ,Dk,Omary Chande
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimsikiliza mmoja wa wazee katika baadhi ya mitaa aliyoitembelea.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrosho Gambo akinywa maji kwenye moja ya kaya aliyoitembelea ambapo maji hayo wananchi wamekuwa akiyashuku kuwa siyo salama,na kuwahakikishia kuwa ni salama na hayana tatizo.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,(AUWSA) Mhandisi Ruth Koya akinywa maji ambayo wananchi wameyatilia shaka kwamba siyo safi na salamaamewahakikishia kuwa maji hayo hayana tatizo na kusisisitiza wananchi kuendelea kuyatumia, huku akisisitiza wayachemshe na kuyachuja vizuri
Mtaalamu wa vipimo katika kutoka wizara ya maji mahabara ya kituo Arusha ambapo ndipo maji yapimwa. na kujiridhisha kuwa maji ni safi na salama na yana dawa ya kutosha, mkuu wa Mkoa akipewa maelekezo namna inavyofanya kazi


Na. Vero Ignatus, Arusha.


Ile sintofahamu ya wakazi wa Jiji la Arusha kuendelea kupata homa ya matumbo kutokana kudaiwa kunywa maji yaliyochanganyikana na maji taka limechukua sura Mpya Mara baada ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutembelea kaya zilizoathirika huku akinywa maji hayo kwa lengo la kujiridhisha na kubaini maji hayo hayana madhara

Akiongea na wananchi katika Kata ya Themi Gambo alikiri kuwa baadhi ya wananchi wamekumbwa na tatizo la kuumwa matumbo na kuhara ndiyo maana wao kama serikali wameamua kuwatembelea na ili kujiridhisha kuwasikiliza

Katika ziara hiyo Mhe. Gambo aliambatana na wataalamu wa Afya Mkoa wa Arusha Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira ,kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa

Mitaa ambayo wameitembelea ni pamoja na mitaa ya Naura Kata ya kati ,Mtaa wa Ndarvoi kata ya Daraja mbili na Kata ya Themi ambapo wananchi walimweleza ambapo wananchi waliweza kumueleza wa mkoa jinsi walivyoathirika na kunywa maji hayo waliodai yamekuwa na harufu kali ya kinyesi.

Wananchi hao ,Boniface Chacha,Jesta John na Hawa Hasan wamesema maji ya bomba wanayokunywa ni changamoto kubwa kwao na kuitaka serikali iwasaidie kuhakikisha afya zao hazidhuriki kutokana na matumizi ya maji safi wanayotumia."Nimetembelea eneo moja baada ya nyingine kujionea tatizo la maji na nikiri kweli kunabaadhi ya watu wanaumwa matumbo na bado wataalam wanachunguza suala hili lakini nasisitiza hakuna uchafuzi wa maji safi kuingiliana na maji taka"

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Hospitali ya Mkoa ,Dk,Omary Chande amesema madaktari wamechukua sampuli za maji na wanaendelea kuzipima kwenye maabara na hakuna mgonjwa yoyote aliyelazwa hospitali ya mkoa bali Jiji kwa maana ya vituo vya afya wamepokea wagonjwa 310

Dkt. Chande amesema sampuli mbalimbali zinaendelea kuchunguzwa ili kubaini ni kitu gani kimesababisha watu kuumwa matumbo

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,Mhandisi Ruthy Koya amesema wataalam wamechunguza maji hayo na kubaini kuwa hayana tatizo na kusisisitiza wananchi kuendelea kuyatumia na wale wasiyotumia maji hayo wachemshe maji


Amesema baada ya kuoana taarifa Mamlaka waliweza kutembelea sehemu husika zinazolalamikiwa na kuchukua sampuli na kuwashirikisha wenzao wizara ya maji mahabara Arusha na kujiridhisha kuwa maji ni safi na salama na yana dawa ya kutosha

Amesema AUWSA hawajaweza kukidhi uhitaji wa maji katika jiji la Arusha kwa 100%kwani,upatikanaji wa maji ni 40%kwahiyo ile 60%inakuwa inajazilushiwa na watu binafsi kwa vyanzo vyao tofauti

Natoa shukrani nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na serikali yake shukrani kwani ametoa fedha nyingi kwaajili ya kuondoa tatizo la maji Jijini Arusha

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Shana ametoa onyo kwa mtu yeyote yule ambae atasambaza habari za uchochezi au mtu yotote atakayeeneza uvumi wa maji safi kuchanganyika na maji taka atachukuliwa hatua za kisheria kwani tayari ufafanuzi wa kina umeshatolewa na mamlaka husika 

BI.GAUDENSIA ATUA MKOA WA MJINI ZANZIBAR,ATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO

0
0




NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Ndugu Gaudensia Kabaka amewataka Wanawake kuitumia vyema fursa ya Ujasiriamali ili wajiongezee kipato na kujiajiri wenyewe.

Rai hiyo ameitoa katika ziara yake katika Mkoa wa Mjini Kichama wakati akizungumza na Wana CCM huko katika ukumbi wa Kwa Waazee Sebleni Unguja.

Alisema ujasiriamali ni nyenzo pekee ya kuwakomboa wanawake kiuchumi na wakaweza kuwa na uwezo na nguvu za kujiajiri wenyewe.

Ameeleza kwamba CCM kwa sasa ipo katika Sera na Mkakakati wa Siasa na Uchumi hatua inayotakiwa kuchangamkiwa na Akina Mama Nchini, kwa kuanzisha vikundi vya ushirika.

Kupitia ziara hiyo aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwalea wazee katika mazingira bora yanayowawezesha kupata huduma zote za msingi za kijamii.

Alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapibduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa busara zake za kuendeleza mambo mbali mbali yaliyoasisiwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Mzee Abeid Amani Karume hasa kuendeleza Vituo vya ustawi wa jamii vya kuwatunza wazee.

Aliongeza kuwa wazee ndio chimbuko la maendeleo ya Zanzibar kwani wao ndio waliotoa nguvu zao kujenga nchi katika nyanja za kiuchumi, kimaendeleo na kijamii.

Akizungumzia ziara yake katika Wilaya ya Amani aliwapongeza viongozi wa UWT kwa juhudi zao za kubuni masuala mbali mbali ya kuimarisha jumuiya hiyo na CCM kwa ujumla.

Wakati huo huo akizungumza na Akina Mama wa Wilaya ya Mjini aliwapongeza kwa ubunifu wao wa kuanzisha Kituo cha mafunzo ya Amali ya kuwajengea uwezo wa fani mbali mbali Vijana wa CCM ili wapate ujuzi na kujiajiri wenyewe.

Alielezea kufurajishwa kwake na hatua hiyo ya kuwapatia vijana wafunzo ya Ushoni, Uuguzi, Uandishi wa Habari na mafunzo ya Komputer kwani fani hizo alizitaja kuwa zinaendana na wakati wa sasa kiajira.

Sambamba na hayo alitembelea Shule ya Maandalizi iliyopo katika Jengo la UWT Mkele na kuwataka Wazazi na Walezi kuwarithisha Watoto Elimu ili iwasaidie katika maisha yao ya sasa na baadae.

Aidha alitembelea Kanisa la Angilicana la Mkunazini Zanzibar na kujionea kumbukumbu za historia ya Watu ambazo ni miongoni mwa vielelezo vya historia ya Nchi.

Aliwasihi Wanawake Zanzibar bila kujali tofauti za Kisiasa wajitokeze kwa Wingi kushiriki Kongamano la Kitaifa la UWT la kupongeza Serikali ya Awamu ya Saba inayoongozwa na Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, litakalofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kimataifa ya Verde Machi 16,mwaka 2019 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:00 Mchana ambapo Mawaziri na Manaibu Waziri watazungumzia kwa upana namna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walivyotekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa ufanisi mkubwa.

Katika ziara hiyo alipokea Taarifa za Utekelezaji wa shughuli za UWT Wilaya ya Mjini, Wilaya ya Amani pamoja na Taarifa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mjini.

Bi. Gaudensia ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa aliambatana na Viongozi mbali mbali wa Umoja huo akiwemo Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwaiba Kisasi, Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mwl. Queen Mlozi,Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo, Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania Bara Ndugu Jesca Mbogo ‘Jasmini’ pamoja na Wajumbe wa Kamati Tekekelezaji wa UWT Taifa

TIMU ZA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOA NA WILAYA ZATAKIWA KUWA WABUNIFU

0
0


Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Dorothy Gwajima akiwaonyesha moja ya taarfa ya utekelezaji majukumu kwa Timu za huduma za afya Mkoa (RHMT) na Wilaya(CHMT),(hawapo pichani) katika kikao cha Mrejesho wa Utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Chamwino leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.
Mwonekano wa kwa Timu za huduma za afya Mkoa (RHMT) na Wilaya(CHMT)wakiwa katika katika kikao cha Mrejesho wa Utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Chamwino leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.
Baadhi ya wajumbe katika kikao cha Mrejesho wa Utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Chamwino leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI wakimsikiliza kwa umakiniDkt.Gwajima .

…………………………………..

Na. Majid Abdulkarim

Kamati za huduma za afya Mkoa (RHMT) na Wilaya(CHMT) nchini zimetakiwa kuwa wabunifu katika kutekeleza shughuli zake na kuhakikisha wanaboresha huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi mkoa kwa ujumla ili kuleta matokeo bora kwa watanzania.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Dorothy Gwajima katika kikao cha Mrejesho wa Utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Chamwino leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Dkt. Gwajima amesema kuwa ubunifu unaotakiwa ni kujenga mahusiano mazuri baina ya mteja na mtoa huduma za afya ili mteja awezekuwa uhuru na kujisikia faraja katika kupata huduma kutoka kituoni hapo.

“Mahusiano mazuri yanajengwa na ukarimu, lugha nzuri kwa mteja na utendaji kazi wenu kwa ujumla mnavyo hudumia wateja wenu kwa kuwa mawakili wazuri katika jamii yao kulingana na mlivyo wahudumia” Ameseama Dkt.Gwajima

Lakini pia Dkt.Gwajima amewataka watoa huduma za afya kuwa na mpango kazi utakao weza kuwaongoza vyema katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kufikia kiwango bora cha utoaji huduma za afya nchini.

Dkt.Gwajima ameeleza kuwa mpango kazi kwa mtumishi utasaidia kuweza kupata tathimini ya utekelezaji wa amjukumu ya mtoa huduma za afya na kujua matokeo yapi yamefanyikiwa , kubaini changamoto zilizojitokeza na kuzitafutia suluhisho ili kufikia malengo ya mtoa huduma aliyojiwekea katika mpango kazi wake.

“Ili kupata tathimini ya utendaji kazi wa watoa huduma za afya amesisitiza kuhakikisha kila mmoja kuwa na taarfa ya uwajibikaji wake ukiwa na takwimu sahihi ili kuweza kupata matokeo bora katika sekta ya faya”.Ameongezea Dkt.Gwajima

Aidha Dkt.Gwajima amehitimisha kwa kuwataka watoa huduma za afya kutekeleza mipango kazi yao kwa vitendo ili kuweza kupata matokeo chanya yatakayo onyesha mabadili katika sekta ya afya na hapo tutakuwa tumetimiza azma ya serikali ya kumuhudumia mwananchi.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.Samwel Seseja amesema kuwa atasimamia vyema maelekezo yalotolewa na Dkt.Gwajima ili kuhakikisha utendaji kazi na uboreshaji wa huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi mkoa zina boreka na kuimarishwa vizuri kwa faida ya watanzania.



MKUU WA IDARA ARDHI KYERWA APEWA WIKI MOJA VINGINEVYO KUTUMBULIWA

0
0


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera baada ya kutoa hati za ardhi katika halmashauri hiyo katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoka katika Masijala ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera alipokwenda kukagua majalada ya ardhi akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika Masijala ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera alipokwenda kukagua majalada ya ardhi akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi jana. Wa pili kulia ni Mkuu wa Idara ya Ardhi halmashauri ya Karagwe ambaye pia ni Afisa Ardhi Mteule katika halmashauri hiyo na ile ya Misenyi Benard Esau.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akivalishwa Scalf na Skauti baada ya kuwasili katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kuanza ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduguli ya serikali kupitia sekta ya ardhi jana



………………………………

Na Munir Shemweta, KYERWA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amempa wiki moja Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kuhakikisha anaingiza viwanja 516 katika Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki vinginevyo ataondolewe katika wadhifa huo.

Agizo hilo limafuatia Dkt Mabula kuelezwa na Mkuu huyo wa Idara kuwa katika halmashauri hiyo jumla ya viwanja 348 pekee ndvyo vilivyoingizwa katika Mfumo wa Kielektroniki huku viwanja 516 vikiwa havijaingizwa kwenye mfumo huo.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitoa agizo hilo jana tarehe 15 Machi 2019 wakati akiwa katika mfululizo wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi katika wilaya za mkoa wa Kagera.

Dkt Mabula alisema kuna uzembe mkubwa kwa Mkuu huyo wa Idara ya Ardhi ambaye pia ni Afisa Ardhi Mteule wa halmashauri ya wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kusimamia uingizaji viwanja kwenye mfumo ambao ndiyo unaosaidia kuongeza mapato ya serikali.

Naibu Waziri alishangazwa na Mkuu huyo wa Idara kushindwa kuingiza idadi hiyo ya viwanja kwenyea mfumo wa kielektroniki katika kipindi cha mwaka mzima wakati alieleza kuwa kwa siku moja anao uwezo wa kuingiza viwanja ishirini.

‘’Kuna uzembe katika kusimamia idara hii ya ardhi na kama mzigo ni mkubwa kwako kusimamia idara hii basi chagua kuachia nafasi moja katia ya Ukuu wa idara ya ardhi au Afisa Ardhi Mteule ili uweze kuifanyia nafasi moja kwa ufanisi’’ alisema Mabula.

Akigeukia suala la utoaji hati katika halmashauri hiyo ya Kyerwa, Dkt Mabula aliiagiza halmashauri ya Kyerwa kuhakikisha maeneo yote yaliyochukuliwa kwa ajili ya matumizi ya umma yanapatiwa hati ili kuepuka migogoro ya ardhi.

Alisema, migogoro mingi kwenye taasisi za umma inasababishwa na taasisi hizo kutokuwa na hati kwenye maeneo yake na kutolea mfano moja ya maeneo yanayovamiwa sana ni yale ya wazi na kuzitaka idara husika kusimamia suala hilo kwa makini.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu alisema viwanja vingi katika wilaya yake havina hati jambo alilolieleza kuwa wakati mwingine linawapa ugumu wa kuchukua hatua kwa wamiliki wake ambao aliwaeleza kuwa wengi wameacha maeneo yao kuwa mapori.

Kwa mujibu wa Mwaimu wilaya hiyo imetoa miezi sita kwa wamiliki wote wa viwanja ambao hawajaviendeleza na kuviacha mapori kuviendeleza vinginevyo watafutiwa umiliki wake.

Katika hatua nyingine Dkt Mabula ametaka halamashauri ya wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera kulitumia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kujenga nyumba kwa ajili ya watumishi wake ili kuondoa uhaba wa makazi kwa watumishi wa halmashauri hiyo.

Alibainisha kuwa, hata kama halmashauri hiyo haihitaji nyumba kwa ajili ya watumishi wake basi inaweza kujengewa nyumba na shirika hilo kwa ajili ya kuutengeneza mji wa Karagwe na wakati huo kuzitumia nyumba hizo kama rasilimali ambapo nyumba hizo zinaweza kupangishwa na kuiwezesha halmashauri kujipatia kipato.

‘’Halmashauri badala ya kutegemea kuingiza mapato katika baadhi ya vyanzo kama vile kituo cha mabasi wanaweza kulitumia shirika la nyumba kuongeza hadhi ya mji na mapato kwa halmashauri’’ alisema mabula.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 15,2019


DPP AKIZUNGUMZIA MALALAMIKO YA MUSA ADAM SADIKI KUBAMBIKIZIWA KESI YA MAUAJI TABORA

0
0
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw.Biswalo Mganga akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari juu ya malalamiko ya Musa Adam Sadiki ya kubambikiziwa kesi ya mauaji katika mahakama ya Tabora. Kulia kwake ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw.Edson Makallo na Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari-MAELEZO Bi.Zamaradi Kawawa.

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw.Biswalo Mganga akisoma moja ya nakala ya mashtaka wakati akizungumzia malalamiko ya Musa Adam Sadiki ya kubambikiziwa kesi ya mauaji katika mahakama ya Tabora. Kulia kwake ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw.Edson Makallo na Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari-MAELEZO Bi.Zamaradi Kawawa. Picha na Daudi Manongi,MAELEZO
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw.Biswalo Mganga akizungumza na waandishi wa habari juu ya malalamiko ya Musa Adam Sadiki ya kubambikiziwa kesi ya mauaji katika mahakama ya Tabora.Kulia kwake ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw.Edson Makallo na Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari-MAELEZO Bi.Zamaradi Kawawa.

Maandalizi ya ujenzi mradi wa umeme wa Rufiji yafikia zaidi ya asilimia 40

0
0

Na Teresia Mhagama, Pwani

Imeelezwa kuwa, kazi mbalimbali za maandalizi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji ( MW 2115) zinazofanywa na Mkandarasi kampuni ya ubia ya Arab Contractors na Elsewedy Electric zimefikia zaidi ya asilimia 4O.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mradi huo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambao walitembelea eneo la mradi lililopo wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.

Kamati hiyo ya Bunge pia ilikagua miundombinu wezeshi iliyotekelezwa na Serikali ikiwemo Barabara, umeme, nyumba za Wafanyakazi na sehemu maalum ya kushushia mizigo katika Stesheni ya Tazara katika Kituo cha Fuga.

Dkt. Kalemani, alisema kuwa, Mkandarasi huyo ameanza kazi za maandalizi mara baada ya kukabidhiwa eneo hilo la mradi mwezi wa Pili mwaka huu. 

Alisema kuwa, miongoni mwa kazi ambazo Mkandarasi anaendelea kutekeleza kwa sasa ni ujenzi wa kambi ya muda ya Wafanyakazi, uletaji wa vifaa na mitambo itakayotumika wakati wa ujenzi pamoja na kazi za kuchukua sampuli za udongo na maji kwa ajili ya utafiti.

Aliongeza kuwa, mara baada ya kukamilisha kazi hizo za maandalizi Mkandarasi huyo anatakiwa kumaliza kazi ya ujenzi ndani ya miezi 36.

Alieleza kuwa, pamoja na kuridhishwa na hatua hiyo ya maandalizi, bado Serikali kupitia Wizara ya Nishati itaendelea kumsimania mkandarasi ili amalize kazi ndani ya muda uliopangwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula, baada ya kukagua miundombinu iliyotekelezwa na Serikali pamoja na kazi za maandalizi zinazofanywa na Mkandarasi, aliipongeza Serikali kwa kuamua kuutekeleza mradi huo na kuusimamia kikamilifu.

Alisema kuwa, Kamati hiyo pia inafuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati kutokana na umuhimu wake nchini ambapo pia alitoa wito kwa Wizara kutorudi nyuma katika usimamizi wa mradi.

Pia, alitoa wito kwa wafanyabiashara hapa nchini kuchangamkia fursa zinazopatikana katika mradi kwani Serikali itatumia takribani shilingi Trilioni 6.5 kutekeleza mradi huo hivyo ni muhimu watanzania wafaidike na fedha hizo.

Katika ziara hiyo, viongozi mbalimbali waliambatana na Kamati hiyo akiwemo Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt Tito Mwinuka pamoja na wataalam kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo.
 Moja ya nyumba inayojengwa na mkandarasi anayetekeleza mradi wa umeme wa Rufiji ambapo katika eneo hilo kunajengwa  kambi ya muda ya Wafanyakazi wa mradi huo.

 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, pamoja na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa nne kutoka mbele) wakiwa  katika eneo ambalo litatumika kutekeleza mradi wa umeme wa Rufiji (MW 2115) mara baada ya kufanya  ziara katika eneo la mradi huo.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula (katikati), Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Gulamali (wa Pili kulia) wakimsikiliza mtaalam kutoka kampuni ya ubia ya Arab Contractors na Elsewedy Electric wakati akizungumzia mradi wa umeme wa Rufiji (MW 2115).

 Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt Tito Mwinuka (katikati) wakikagua eneo kutakapotekelezwa mradi wa umeme wa Rufiji (MW 2115), wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, (katikati), akizungumza na Wataalam wanaosimamia na wanaotekeleza mradi wa umeme wa Rufiji (MW 2115) mara baada ya kufika katika eneo la mradi huo akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) akiwaongoza baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini mara walipofika katika eneo kutakapotekelezwa mradi wa umeme wa Rufiji (MW 2115), wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.

ASILIMIA 80 YA WANANCHI SIMIYU KUTUMIA BIMA YA AFYA

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa huo umejiwekea malengo ya kuhakikisha zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wake kuwa na kadi za bima ya afya ili kujihakikishia upatikanaji wa huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini.

Mtaka ameyasema hayo wakati ufunguzi wa Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.

Amesema yeye kama Mkuu wa Mkoa atafanya vikao na wanachama wa AMCOS na makundi mbalimbali ya wananchi katika wilaya zote mkoani hapa na kuzungumza nao kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kila mwananchi kuwa na Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu.

Aidha, amesema atawaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwa katika Vyama vya Ushirika Vya Msingi ambavyo vinawapa nafasi ya kupata Bima ya afya na kupata matibabu makubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya vya binafsi na vya umma kwa gharama nafuu ya shilingi 76,800/= kwa mtu mmoja(mwanachama wa ushirika).

“Nitafanya vikao na wanachama wa AMCOS zote, wakulima, wafugaji, wajasiriamali, makundi yote ya wananchi kwenye mkoa wetu wa Simiyu, tuweze kuwaelimisha faida ya mwananchi wa mkoa wa Simiyu kuwa na bima ya afya, kubwa zaidi umuhimu wa kuwa kwenye ushirika ambao utamwezesha kupata matibabu makubwa kwa bei nafuu” alisema

Katika hatua nyingine Mtaka amesema katika kipindi cha msimu wa pamba kila kituo cha kununulia pamba NHIF itaweka Afisa wake kwa ajili ya kusajili wakulima na wanachama wa vyama vya ushirika walio tayari, hivyo akatoa wito kwa viongozi walioshiriki jukwaa la ushirika afya kutoa taarifa na elimu kwa wenzao juu ya umuhimu wa suala hilo.

Mtaka pia ametoa wito kwa wakulima wote wa pamba kulipa kipaumbele suala la afya kwa kuchukua hatua ya kuwa na bima za afya ili waweze kuona manufaa ya Serikali kuboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na kujenga Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Hospitali za wilaya kwa kila wilaya na Vituo vingine vya kutolea huduma za afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernad Konga amesema NHIF ni wadau wakubwa mkoani Simiyu, hivyo wako tayari kutoa huduma bora na watawafikia wananchi wa makundi yote mkoani hapa na watahakikisha wanatoa kadi za bima ya afya kwa wakati kwa wanachama wote watakaojiunga.

Katika jukwaa hili washiriki wamepata nafasi ya kuchangia michango mbalimbali huku wanachama wa AMCOS wakiunga mkono mpango huo wa kupata bima ya afya kwa gharama ya shilingi 76,800/= ili waweze kumudu gharama za matibabu.

“Mpango huu nimeupokea vizuri ila ninashauri elimu iendelee kutolewa zaidi na zaidi ili wanachama wote wajue umuhimu wa kuwa na kadi za bima ya afya na namna zitakavyowasaidia” Lucas Ephraim mshiriki kutoka AMCOS ya Dutwa Bariadi.

“ Binafsi niko tayari kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili nipate hiyo kadi itakayonifanya niweze kutibiwa popote hapa Tanzania, lakini naomba tutakapolipia hiyo 76,800/= kadi zetu tuzipate mapema” Mmoja wa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya msingi, Bw. Magwashi Gandila

Mkoa wa Simiyu una vyama vya Ushirika Vya Msingi(AMCOS) zaidi ya 379 vyenye wanachama zaidi ya 300,000 na Jukwaa hili limeazimia wanachama wa AMCOS wakawe mabalozi wazuri kuwahamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani humo katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi. 
Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Benard Konga akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani humo, katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) aizungumza na Meneja wa Wanachama kutoka NHIF(kushoto) na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Benard Konga, mara baada ya kumalizika kwa Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa Serikali na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yakiwasilishwa katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa dini, viongozi na watumishi wa Serikali na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yakiwasilishwa katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mwanachama wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Dutwa wilayani Bariadi, Bw. Lucas Ephraim akichangia hoja katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa taarifa ya utangulizi katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.

QNET inaleta bidhaa zake za kuboresha maisha nchini Tanzania

0
0
· Dar es salaam inakuwa mwenyeji wa siku 2 za maonyesho ya Absolute Living (Kuishi kikamilifu) ya bidhaa QNET 

· Watu wote wanakaribishwa kuhudhuria na kuelewa bidaa za QNET, huduma na mtindo wake wa biashara. 

Tarehe 13 Machi 2019, Dar es salaam: Kampuni yenye asili ya Asia ya mauzo ya moja kwa moja QNET itaendesha maonyesho ya bidhaa na huduma zake jijini Dar es salaam siku ya tarehe 16 na 17 Machi 2019 katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 1 Jioni. 

Maonyesho yenye jina la Absolute Living, (Kuishi Kikamilifu) sambamba na falsafa ya bidhaa za kampuni ya mauzo ya moja kwa moja, huwa yanafanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali duniani kote ikiwa na lengo la kuonyesha bidhaa zake na huduma kwenye masoko mapya. Onyesho hilo pia linakuwa kama jukwaa kwa wateja na wadau wengine wanaotaka kufahamu kuhusu QNET na mtindo wake wa biashara. 

Nadharia ya Absolute Living (Kuishi Kikamilifu) inaakisi juhudi za QNET za kukuza mwenendo wa kujali afya, mtindo wa maisha wenye uwiano sahihi, ikiwa inatilia mkazo katika Afya, Ustawi na Elimu. 

Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari Meneja Mkuu wa Kanda wa QNET kwa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika, Biram Fall alisema kwamba, "Tunatoa aina mbalimbali za bidhaa za kiwango cha juu na huduma kwa wateja wetu kuwasaidia waweze kuishi maisha yenye uwiano sahihi, na pia kutatua tatizo la msingi kama vile elimu, ufahamu, na maendeleo binafsi kupitia program za mafunzo yetu, ambayo yanawasaidia katika safari yao ya kujiajiri mwenyewe. 

 Kutoka katika kozi za elimu kwa njia ya mtandao kama vile SELI/qLearn, mpaka katika vifurushi vya sikukuu kama vile Tripsavr, mpaka bidhaa za kuongeza nguvu kama vile Bio Disc3, virutubisho kama EDGE, na saa za mkononi kama Bernhard H. Mayer, QNET ina aina mbalimbali za kukidhi mahitaji mbalimbali ya watu. Katika kitovu cha yote haya, ni hamu yetu ya kutoa fursa ya Kuishi Kikamilifu "Absolute Living” 

Zaidi ya watu elfu mbili wanatarajiwa kuhudhuria maonyesho ya siku 2 ambayo yatakuwa na bidhaa za mfano katika onyesho, na kuonyesha namna ya matumizi ya bidhaa na faida zake kwa wateja na watumizji wa mwisho. Kwa kuongezea, wataalamu wa bidhaa na biashara watakuwepo kwa ajili ya kujibu swali lolote kutoka kwa wageni ili kuelewa vizuri ulimwengu wa QNET. 

QNET inaalika watu wote kuhudhuria onyesho hili jijini Dar es salaam na kujifunza kwanza kuhusu bidhaa, huduma na fursa za biashara. 

Maonyesho ya Dar es salaam yanafuata mfululizo wa maonyesho kama hayo yaliyofanikiwa nchini Togo, Guinea, Ivory Coast, Senegali, Burkina Faso na Cameroon mwaka jana. 

Msafara wa maonyesho utasisimama katika mji wa Kumasi, Ghana, baada ya Dar es salaam kuanzia tarehe 23 mpaka 24 Machi mwaka 2019. 

MAJARIBIO YA MITAMBO YA LIVE YA MICHUZI TV

Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images