Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 278 | 279 | (Page 280) | 281 | 282 | .... | 3272 | newer

  0 0

  DUNIA MZOBORA
  Aliyekuwa Mhariri  Mwandamizi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Marehemu Dunia Mzobora, ambaye amefariki dunia jana, anatarajiwa kuzikwa leo saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
           Habari zimesema Mzobora (49), ambaye alifariki dunia ghafla jana saa 12 asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alikokuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi, akitokea Hospitali ya Aga Khan pia ya Dar es Salaam.

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akisistiza jambo kwa watangazaji wa vipindi vya redio mbalimbali (hawapo pichani) kuhusu vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel ya "Mimi ni bingwa" itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kushinda tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku.Kulia kwake ni ofisa wa matangazo wa Airtel Bw. Abdallah Gunda.
  Toka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airte Tanzania Bw Jackson Mmbando akibadilishana mawazo na watangazaji wa kipindi cha jahazi bw Musa Huseni (kati) na Ephraem Kibonde mara baada ya mkutano maalum na watayarishaji na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio kwa lengo la kuwaeleza vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel Mimi ni bingwa" inayowawezesha wateja wa Airtel kushinda tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku

  0 0

  Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini, Suleiman Nyambui (Kulia),  akimkabidhi fomu ya ushiriki wa mbio za kilomita 3 za Uhuru Marathon, mwanamichezo Imani Madega (Kushoto), huku mratibu wa mbio hizo, Innocent Melleck akishuhudia wakati wa tukio la kuonyesha njia mbio hizo zitakazoshirikisha watu wa rika tofauti na viongozi mbalimbali zitakavyokuwa kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo ambazo lengo lake ni kuhamasisha umuhimu wa uwepo wa amani nchini zitafanyika Desemba 9 mwaka huu.

  KUMEKUCHA! Mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, sasa zimefikia patamu baada ya waandaaji jana kutangaza njia itakayotumika kwa ajili ya mbio hizo.
   Mbio za Uhuru Marathon zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu na zitaanzia viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni na kumalizikia hapo.
   Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Selemani Nyambui alisema, njia hizo zimepimwa kwa kuzingatia taratibu zote za mbio za kimataifa.
   Nyambui alisema, upimaji ulifanyika kwa umakini mkubwa kwa kuhakikisha wale watakaokimbia mbio za kilomita 42, kilomita 21 na kilomita 5 wanakimbia kwa kiwango sahihi zaidi.
   Nyambui alitaja njia zitakazotumika kwa wanariadha wa kilomita 42 kuwa, wataanzia Viwanja vya Leaders na kupitia Barabara ya Alli Hassan Mwinyi kuelekea Morocco, watapitia Old Bagamoyo kuelekea Kawe na kufuata barabara ya Tegeta.
   Wanariadha hao watapita pia Mwenge hadi Makumbusho ambapo watafika eneo la Morocco na kuchukua Barabara ya Kawawa hadi katika taa za Chang’ombe, ambapo wataelekea Tazara na wakifika hapo watafuata Barabara ya Mandela hadi Uwanja wa Taifa.
   Wakifika hapo watapita Barabara ya Taifa na kutokea Chang’ombe na kwenda hadi Kinondoni kwa Manyanya watakapochukua barabara ya kuelekea makaburini (Kinondoni Road) na kutoka Barabara ya Alli Hassan Mwinyi na hatimaye kuingia Viwanja vya Leaders.
   Nyambui alisema, mbio za kilomita 21 zitatumia njia hizo lakini lakini hazitafika eneo la Chang’ombe kama ilivyo kwa zile za kilomita tano.
   “Naamini kwa dhati kabisa mbio hizi zitafanikiwa kwa kiasi kikubwa na mpaka sasa wanariadha wengi wamejitokeza kushiriki,” alisema.
   Naye Katibu wa Kamati ya mbio hizo, Innocent Melleck alisema, wanaamini kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa haswa kwa mipango waliyoiweka.
   Melleck alisema, mpaka sasa usajili unaendelea ambapo kwa wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.  0 0

   Clara Noor baada ya kuibuka mshindi wa kwanza taji la ufukwe 
   Clara Noor na washindi wengine

  Nyota ya mrembo wa Tanzania anayewania taji la Miss Earth, Clara Noor imeanza kung’ara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika taji la fukwe ya Pagudpud iliyopo nchini Phillipines.
  Mbali ya kutwaa taji hilo, Clara pia ameibuka mshindi wa tatu katika taji la vazi la Taifa na kuzipiku nchi nyingine nyingi na kuzawadiwa medali ya shaba.
  Katika mashindano ya tuzo maalum, jumla ya tuzo 11 zilikuwa zinagombaniwa na warembo 88 walikuwa wanawania mataji hayo ambayo zawadi zake zilitolewa na wadhamini hao.
  Clara alionyesha uwezo mkubwa katika taji hilo na kuwa mwafrika wa kwanza kushinda katika historia.  Katika vazi la Taifa, Clara aliwavutia wengi na kupata ushindani mkubwa kutoka kwa mrembo wa warembo kutoka Afrika Kusini, Ashanti Mbanga na kutoka Nigeria, Marie Miller ambao walishika nafasi ya kwanza nay a pili.
  Muandaaji wa Miss Earth Tanzania, Maria sarungi Tsehai alisema kuwa ni faraja kubwa kwa Clara kuitangaza Tanzania kwa kupitia mataji hayo mawili kwani mbali ya jina lake, kinachotangazwa pia ni nchi.
  “Amefanya vyema mpaka sasa, tunatarajia kuona anaendelea kufanya vizuri na kutuletea sifa, mpaka sasa anastahili pongezi,” alisema Maria ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications.
  Alisema kuwa fainali ya mashindano hayo yatafanyika Desemba 7 kwenye ukumbi wa Versailles Palace, Alabang, Muntinlupa City na kurushwa live na vituo vya televisheni vya STAR World, ABS-CBN, Velvet, The Filipino Channel, Ustream na Venevisión.

  0 0

  Ujumbe wa benki ya dunia (WB) kutoka ofisi ya kanda ya Afrika Mashariki ukiongozwa na Mkuu wa miradi ya sekta ya usafirishaji Eng. Solomon Waithaka wa pili kulia leo umetembelea TPA kukagua miradi inayofadhiliwa na benki hiyo. Wengine kwenye picha ni Eng. A. Matei Naibu Mkurugenzi Mkuu - TPA katikati na kulia kwake ni Ndg. Phares Magesa Mkurugenzi wa ICT - TPA na Kiongozi Msimamizi wa miradi ya WB, na wa kwanza kulia ni Ndg. Suluo Mratibu wa miradi hiyo kwa sekta ya usafirishaji na wengine ni wakuu mbali mbali wa vitengo TPA.
  Kwa ujumla benki imeridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo.
  Miradi inayofadhiliwa na WB na wadau wake katika Mamlaka ya Bandari ni:
  I. Integrated security system( ISS)
  II.electronic Single Window System(eSWS)
  Iii.Port security Training (ISPS )
  Iv. Mradi wa Patrol boats

  0 0

  MO SFW Banner

  Or by TextingSWFA SMP O3TO15678

  0 0

  Marehemu Askofu John Simalenga

  0 0

  Princess Haifa Bin AbdulAzizi Mogrin of Saudi Arabia looks at a bust of Mwalimu Nyerere when she visited the Tanzania National Parks Headquarters in Arusha and held talks with the Management of TANAPA regarding the forthcoming youth forum on Biodiversity Conservation
  scheduled for January next year in Arusha.
  Princess Haifa Bin AbdulAzizi Mogrin of Saudi Arabia signs the guest book when she visited the Tanzania National Parks Headquarters in Arusha 
  Princess Haifa Bin AbdulAzizi Mogrin of Saudi Arabia talks with the Director General of 
  TANAPA Mr Allen Kijazi regarding the forthcoming youth forum on Biodiversity Conservation
  scheduled for January next year in Arusha.

  0 0

   - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hituba yake ya uzinduzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Miaka 10 ya Mapinduzi katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania, yaliyozinduliwa rasmi leo katika Ukumbi wa Mliman City,jijini Dar es Salaam
    Wadau wakisikiliza hotuba ya ufunguzi
   Wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi
   Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.

  0 0

  Na Mohamded Mhina wa
   Jeshi la Polisi, Zanzibar
  Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 55, mkazi wa Kijiji cha Kidutani Gando mkoa wa Kaskazini Pemba ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 12 na baadaye kujitosa bahari kukwepa mkono wa dola.
  Mzee huyo Muslih Mserembe, alikamatwa na wananchi waliokuwa wamekizingira kibanda chake kilichojengwa kwa miti, kuezekwa kwa makuti na kukandikwa kwa udongo wakati akimbaka binti huyo bila ya huruma. (Jina la binti huyo linahifadhiwa kwa usalama).
  Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12.00 alfajiri wakati binti huyo akiwafuatilia wenzake kwenda shambani kuokota maembe na ndipo mzee huyo alipomuona na kumuita.
  Amesema baada ya binti huyo kumsogelea mzee huyo, alimwambia waingie ndani ya nyumba yake akidai kuwa angempatia maembe badala ya kuwafuata wenzake na ndipo alipombaka na binti kupiga kelele za kuomba msaada.
  Kamishna Mussa alisema baada ya kelel hizo wananchi walikwenda nyumbani kwa mzee huyo na wakati wakiizingira nyumba yake, mzee huyo alitoka na kutimua mbio na kwenda kujitosa baharini lakini wananchi nao walijitosa humo na kumvua kama samaki.
  Amesema baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo, wananchi hao walimpeleka katika kambi moja ya KMKM na ndipo Polisi walipofika na kumchukua kwa hatua zaidi.
  Kamishna huyo wa Polisi Zanzibar amesema kuwa binti aliyebakwa alikimbizwa katika Hospitali ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba kwa matibabu zaidi na hali yake imeelezwa kuendelea vizuri.
  Kamishna Mussa ambaye amelaani vikali kitendo hicho, lakini amepongeza hatua za wananchi za kumkamata mtuhumiwa bila ya kumzuru na kumfikisha kwenye vyombo vya dola akiwa salama.
  Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu shitaka lake.

  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pindaakitoa heshima za mwisho kwa Askofu John Andrew Simalenga katika mazishi ya Askofu huyo wa Dayosisi ya South West Tanganyika ya Kanisa la Anglican lyaliyofanyika Njombe  Novemba 28, 2013.  Kushoto ni Askofu Mkuu wa kanisa la Anglican nchini, Dr. Jacob  Chimeledya
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Anne Makinda wakishiriki katika Ibada ya mazishi ya Askofu wa Kanisa la Anglican Dayosisi ya South West Tanganyika yaliyofanyika Njombe 
   Mwili wa Askofu wa Kanisa la Anlican Dayosisi  ya Southa  west, John Andrew Simalenga ukitelemshwa kaburini kwenye mazishi yaliyofanyika kwenye kanisa kuu la  Dayosisi hiyo mjini Njombe 
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka mchanga katika kaburi la Askofu wa Dayosisi ya  South West Tanganyika ya Kanisa la Anglican, John Andrew Simalenga yaliyofanyika  mjini Njombe.

  0 0

  Mamiss Tanzania USA Pageant wakimsikiliza Lady Kate mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant alipokuwa akiwaasa jinsi ya ushiriki wao kwenye Miss Tanzania USA Pageant itakayofanyika siku ya Jumamosi Novemba 30, 2013 Hollywood Ballroom iliyopo 2126 Industrial Pkwy, Silver Spring, MD 20904
  Lady Kate, Pamela, Ma Winny na Asha katika picha ya pamoja na Mamiss Tanzania USA. kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema kuanzia mwaka wa masomo 2014/15 vyuo vyote vya ufundi nchini vinaendesha mafunzo ya kozi zenye ithibati tu ili kuondoa usumbufu kwa wahitimu. 
   Aidha ametangaza rasmi kuanza kwa mtaala wa Stashahada ya Elimu ya Msingi ambao utaanza kutekelezwa kwa vyuo vilivyo na sifa kuanzia mwaka wa masomo wa 2014/15. 
   Akifungua mkutano wa kitaifa wa wakuu wa vyuo vya ufundi nchini ulioandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na kufanyika jijini hapa, atalazimika kutumia polisi kukagua na kuvifunga vyuo ambavyo wamiliki wake wanashindwa kutekeleza masharti ya vyuo vyao kupata ithibati. 
   “Siku hizi kumeibuka wimbi kubwa la vyuo holela vinavyoendeshwa pasipokuzingatia vigezo vilivyowekwa na NACTE. 
   “Jamii yetu imeendelea kuhujumiwa na watu wanaojitafutia fedha kwa njia za mkato na hasa wanaojitangaza kutoa Elimu ya Ufundi tena kwa ada ndogo,” alisema. 
   Aliwaasa wazazi na walezi kabla ya kuwapeleka watoto wao kujiunga na vyuo vya ufundi wahoji mambo muhimu ikiwa ni pamoja na usajili wa vyuo hivyo, taaluma za wakufunzi wake ili wawe na uhakika na taalum inayotolewa kwa watoto wao. Aliliagiza Baraza hilo, “ikiwa katika kutekeleza agizo langu mtakutana na kikwazo cho chote basi ofisi yangu ambayo ni mamlaka ya rufaa kwa mujibu wa sheria yenu itatoa ushirikiano kuhakikisha tatizo la kozi zisizotambuliwa linadhibitiwa kwa nguvu zote.” 
   Alisema kabla ya kuanzishwa NACTE, serikali haikuwa na chombo mahsusi cha kuratibu elimu na mafunzo ya ufundi hali ambayo ilisababisha kila mwenye chuo kujiwekea vigezo na viwango vyake vya taaluma na hivyo kusababisha nchi kuwa na vyuo ambavyo vinatoa tuzo ambazo vigezo vyake havilingani. 
   “Kila mwenye chuo alikuwa akitayarisha mtaala wake wa mafunzo kama alivyoona inafaa, na hivyo, kusababisha utofauti wa viwango vya tuzo zinazotolewa baina ya chuo kimoja na kingine,” alisema. 
   Alisema katika mfumo wa soko huria na kutokana na kiu ya Watanzania kupata elimu ya ufundi, ilikuwa ni rahisi kudanganywa na kupewa elimu duni na pia ilikuwa vigumu kwa serikali kuweka mikakati ya kuendeleza Elimu ya Ufundi ili kukidhi mahitaji ya maendeleo ya nchi na watu wake. Katibu Mtendaji wa NACTE, Dk. Primus Nkwera, alivitaka vyuo na taasisi za elimu za ufundi nchini zinazotoa mafunzo bila kusajiliwa pamoja na wale wote wenye nia ya kuanzisha vyuo vipya kuhakikisha vyuo vyao vinapata usajili kutoka Baraza hilo kwa mujibu wa sheria. “Baraza linapenda kuwasisitizia wadau wote ikiwemo wazazi, wanafunzi na umma kwa uiumla kujiunga na vyuo vilivyosajiliwa na Baraza na si vinginevyo,” alisema. 
   Alisema matarajio ya soko la ajira ni kuona vyuo vinatoa wahitimu wenye ujuzi na maarifa yanayokidhi viwangao vya utendaji kazi katika taaluma husika. 
   Mwenyekiti wa NACTE Mhandisi Steven Malote, alisema baraza hilo limeweka mfumo wa tuzo za kitaifa za Elimu ya Ufundi ambazo zimeunganishwa na Tuzo za Kitaifa za Ufundi Stadi (NVA), ili kuwa na ngazi kumi za Mfumo wa Kitaifa wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi (TVET). 
   Pia alisema imewaka kanuni za usajili na ithibati pamoja na masharti ya vyuo/taasisi kuanzisha kozi za shahada.
    Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw.Philipo Mulugo(katikati)akimkabidhi tuzo  Mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Ufundi(NACTE)Prof.B.L.M.Mwamila na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)Dkt.Primus Nkwera(kulia)mara baada ya kumkabidhi cheti pamoja na Tuzo,kwenye mkutano wa kwanza Kitaifa wa wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi  kwa utendaji bora kwa miaka mitatu mfululizo,Mkutano huo wa siku tatu unafanyika  katika ukumbi wa mikutano wa Arusha( AICC) jijini Arusha.
  .Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw.Philipo Mulugo(katikati)akifurahia pamoja na  Mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Ufundi(NACTE)Prof.B.L.M.Mwamila na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)Dkt.Primus Nkwera(kulia)mara baada ya kumkabidhi cheti pamoja na Tuzo,kwenye mkutano wa kwanza Kitaifa wa wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi  kwa utendaji bora kwa miaka mitatu mfululizo,Mkutano huo wa siku tatu unafanyika  katika ukumbi wa mikutano wa Arusha( AICC) jijini Arusha.
   Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw.Philipo Mulugo,akiongea na wadau wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi,alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano  wa kwanza Kitaifa wa siku tatu unafanyika  katika ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha wenye lengo la kujadili ubora wa mafunzo ya ufundi nchini.

  Washiriki katika mkutano wa kwanza Kitaifa wa wakuu wa vyuo vya ufundi,Serikali na wadau wengine wa elimu ya ufundi,wakijadiliana jambo baada ya Naibu Waziri Philipo Mulugo kuzindua rasmi mkutano huo wa kwanza Kitaifa wa siku tatu unafanyika  katika ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha.

  0 0

  DSC_0170
  The Charge d’ Affaires from the Embassy of the Federal Republic of Germany, Hans Koeppel speaks to invited guests and reporters (not in picture) during the official handing over ceremony of the New Model Volkswagen Touareg held at Umoja House premises in Dar.
  All photos by Zainul Mzige

  Germany Embassy in Dar has chosen 
  TOUAREG as it’s official car
  By Damas Makangale, MOblog
  THE Embassy of the Federal Republic of Germany has launch the new model of the Volkswagen TOUAREG sport utility vehicles as part of the Embassy’s mobility fleet. It has been established.
  Speaking to invited dignitaries during the official handover ceremony at Umoja House in Dar es Salaam, the Charge d’ Affaires from the Embassy of the Federal Republic of Germany, Hans Koeppel said that Volkswagen is one of the largest automobile company in the world, in Tanzania and underlined that German products are known worldwide for high class technology and innovative engineering.
  “The embassy of Germany is promising to provide high quality products into Tanzanian market and while assuring Tanzanians to see the new model of Volkswagen in the street,”
  DSC_0183
  The Managing Director of Alliance Autos Wayne McIntosh pointed out to the newly Volkswagen Touareg during the official launching and handing over ceremony to the Embassy of the Federal Republic of Germany in Dar.
  “The Touareg redefines the Sports Utility Vehicle (SUV) featuring extraordinary luxury, exceptional versatility and technological advances that are simply ahead of their time,” he said.
  Koeppel further said that the innovating of another model of Volkswagen is a clear picture of the spirit of cooperation between Tanzania and Germany and mutual respect between the two countries.
  On his part the Managing Director of Alliance Auto, Wayne McLntosh felt honored that the TOUAREG was chosen as the official Embassy car while introducing the product to Tanzanian market.
  “It provides a unique combination of four-wheel drive, off road capabilities, sustainable energy efficiency and high driving performance,”
  “Not only winning prizes as “Best Luxury SUV” and “Sport/Utility of the year, the TOUAREG also introduces success and experience of Rally Dakar-winners onto the road,” He underscored.
  He said that in the coming months, the stylish, sophisticated and refined second generation of the TOUAREG will conquer the streets of Dar es Salaam.
  McLntosh explained further that Volkswagen has opened its showroom in Tanzania in collaboration with Alliance Auto in March 2013 and is aiming to provide Tanzanians with high quality engineering “Made in Germany’ offering the TOUAREG Amarok pick-up and Tiguan.
  DSC_0189
  The Managing Director of Alliance Autos, Wayne McIntosh together with the Charge d’ Affaires from the Embassy of the Federal Republic of Germany, Hans Koeppel showing invited guests and reporters the newly Germany Auto mobile product Volkswagen TOUAREG during the official launching held in Dar at Umoja House.
  DSC_0196
  Congratulating each other.
  DSC_0202
  The Managing Director of Alliance Autos, Wayne McIntosh hands over a key to the Charge d’ Affaires from the Embassy of the Federal Republic of Germany, Hans Koeppel.
  DSC_0216
  Volkswagen TOUAREG at the back

  0 0
 • 11/28/13--05:26: Treni ya mwakyembe...

 • 0 0

  Mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda na wafanyabiashara, viwanda na kilimo Tanzania mkoa wa Iringa TCCI , Lucas Mwakabungu (katikati),akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya utafiti  uliofanywa na Institute of Business Environment Strengtheniing for Tanzania (IMED) kwa kushirikiana na Tanzania Chamber of Commerce,Industries and Agriculture (TCCIA) Mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa mwanzoni mwa wiki.(Picha na Denis Mlowe)
  ========  =======  =========
  Na Denis Mlowe,Iringa.

  UTAFITI uliofanywa na Institute of Business Environment Strengtheniing for Tanzania (IMED) kwa kushirikiana na Tanzania Chamber of Commerce,Industries and Agriculture (TCCIA) Mkoa wa Iringa umebaini Tanzania inapoteza mapato zaidi ya shilingi bilioni 174  kwa mwaka kutokana na wakulima kutotumia mizani katika upimaji wa mazao ya mahindi na mpunga.
   Mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda na wafanyabiashara, viwanda na kilimo Tanzania mkoa wa Iringa TCCI , Lucas Mwakabungu amebainisha hayo wakati akzungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa kuwa utafiti huo kuhusu sheria ya vipimo na mizani wa mwaka  1982 unavyosimamiwa na kutekelezwa na kurudiwa Julai na Septemba mwaka 2013.

   Alisema utafiti huo unaonyesha kwa kiasi gani wakala wa vipimo na mizani unatekeleza sheria hiyo na wafabyabiashara na wakulima wanaifuata na kuitekeleza iadha madhara na matokeo ya kutoifuata sheria hiyo.
  Mwakabungu alibainisha kuwa mikoa ya Iringa na Njombe pekee inapoteza ushuru wa mazao (crop Cess) ya mahindi na mpunga zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kwa mwaka kutokana na mikoa hiyo kuhusika na kilimo cha mazao hayo. Alisema ushuru wa kodi ya mazao unaopotea kwa mazao ya mahindi na mpunga kwa nchi nzima kwa msimu ni shilingi bilioni 14.8.

   Alisema utafiti uliofanywa na IMED ulichukua sampuli za magunia 43 ya mpunga yaliyopimwa uzito na wakala wa vipimo na mizani (WMA) kati ya magunia 482 yaliyokamatwa na kubainika kuwa uzito halisi wa kila gunia ulikuwa wa wastani wa kilo 42 zaidi ya uzito unaostahili sawa na asilimia 56.

   Aidha alibainisha kuwa uzito wa wastani wa gunia la mahindi lililojazwa kwa ndoo za plastiki lina kilo 36 zaidi ya uzito unaostahili sawa na asilimia 40 kutokana na lumbesa ambayo wakulima wanadidimizwa na wafanyabiashara.
  Alisema wakulima wanatumia ndoo za plastiki na lumbesa kwa kuwa kuna upungufu wa mizani na ushuru wa mazao kulipwa kwa gunia badala ya uzito na kutokuwepo kwa vifungishio vinavyokubalika.

  Mwakabungu alisema utafiti huo ilibainisha kuwa wakala wa vipimo na mizani(WMA) hawana rasimali fedha za kutosha, vifaa vya kutosha na hawana rasimali watu wa kutosha kuwezesha kuitekeleza sheria hiyo kama inavyotakiwa.

  0 0

  Mratibu wa matembezi hayo Bw, Matukio Chuma akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam wakati akizindua Matembezi ya Nchi Yangu Wajibu Wangu, yanayo tarajiwa kuanza, Januari 11-2014 kuanzia jijini Dar es Salaam hadi Mkoani Morogoro.

  Matenzi hayo ya kilomita (200km), ambayo yatachukua siku kumi 10,lengo la matembezi hayo kuhamasisha kila Mtanzania anaamua kuamua kuchukua hatua ya kujikwamua kimaisha.

   Ni changamoto inayotolewa mbele ya Watanzania,kukumbuka maana halisi ya uzalendo kujitoa mhanga kuweza kufanikisha maendeleo yao wenyewe kwa kujishughulisha na kujibidiisha katika Nyanja mbalimbali kwa manufaa ya Taifa,kujitolea kuanzia ngazi ya kaya mpaka taifa,kuacha kulalama tu kuwa serikali haijawafanyia moja ama mbili lakini wao wenyewe kutambua mchango wao kama Watanzania na wajibu wao kama wananchi.

  Kubwa zaidi kujivunia nchi iitwayo Tanzania kwa yale mema na adimu yaliyopo na kurekebisha palipo na kasoro kwa moyo mmoja bila kujali itikadi,imani, asili ama mtizamo miongoni mwetu, Tanzania,kwa nini Dar es Salaam mpaka Morogoro.

  Dar es Salaam imendelea kuwa kituo kikuu cha shughuli nyingi za kiuchumi,kiserikali na vilevile ni mkoa ulio na watu wengi zaidi Tanzania, ta kribani milioni mbili na nusu (2.5mil) kawa mujibu wa sensa ya watu ya mwaka 2002, wakati Morogoro ina watu wasiofika laki tatu tu, na kwa ukuaji wa asilia 4.39,hii inawakilisha tofauti kubwa sio tu kwa idadi lakini ya ukuaji, upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii, ukuaji wa kiuchumi na vilivile hali ya kipato na fursa za iuchumi” alisema Chuma.
  Mratibu wa matembezi hayo Bw, Matukio Chuma akiwaonyesha waandshi wa habari vazi litakalotumika kwenye matembezi hayo (kushoto), Mratibu wa matembezi hayo Carren Mgonja.
  Waandishi wa habari wakishuhudia uzinduzi huo.

  0 0

  Kampuni ya Coca Cola ambao ndio wadhamini wakuu wa Kombe la Dunia,wamefanikiwa kulileta Kombe hilo kwa mara nyingine tena Barani Afrika,ambapo leo hii Kombe hili lipo Jijini Nairobi nchini Kenya na kesho Mapema linatarajiwa kuondoka jijini hapa na kulelekea Jijini Mwanza,nchini Tanzania ambapo litapokelea na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae kuelekea jijini Dar es Salaam.hivyo wakazi wa maeneo mbali mbali ya jijini Dar kaeni mkao wa kula kwa ajili ya kuliona na kupiganalo picha Kombe hilo.
   Wakazi wa Jiji la Nairobi nchini Kenya wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa KICC uliopo katikati ya Mji,wakifatilia Burudani mbali mbali za Muziki kutoka kwa wasanii wengi wa nchini humo pamoja na wale wa kimataifa ambao wapo kwenye ziara ya Kutembea na Kombe la Dunia,kupitia Kinywaji cha Coca Cola.Kombe hilo kwa sasa lipo nchini Kenya ambapo kesho litawasini Jijini Mwanza nchini Tanzania na kupokewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae litaelekea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine.
   Msanii wa Muziki kutoka nchini Brazil,David Correy akirusha Fulana zake kwa Mashabiki wake lukuki waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa KICC,jijini Nairobi nchini Kenya jioni hii wakati wa tamasha la wazi la Ziara ya Kombe la Dunia linadhaminiwa na Kampuni ya Coca cola,ambalo leo lipo nchini Kenya na kesho asubuhi litaelekea Jijini Mwanza,nchini Tanzania ambapo litapokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae litaelekea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine.
   Mkali wa miondoko ya R&B na Raga kutoka nchini Kenya,Kevin Wyre akifanya yake mbele ya mashabiki wake lukuki waliofurika kwenye Uwanja wa kwenye Uwanja wa KICC,jijini Nairobi nchini Kenya jioni hii wakati wa tamasha la wazi la Ziara ya Kombe la Dunia linadhaminiwa na Kampuni ya Coca cola,ambalo leo lipo nchini Kenya na kesho asubuhi litaelekea Jijini Mwanza,nchini Tanzania ambapo litapokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae litaelekea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine.


  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda kesho tarehe 29, Novemba 2013 anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tovuti Kuu ya Serikali katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

  Uzinduzi wa Tovuti Kuu hiyo inayopatikana kwa anuani ya www.tanzania.go.tzutahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,  Wananchi, Wafanyabiashara, Washirika wa Maendeleo, Taasisi zisizo za Serikali na Wawakilishi kutoka vyuo Vikuu. 

  Tovuti Kuu hiyo ni mojawapo  ya juhudi za Serikali  katika kuhakikisha kuwa taarifa na huduma zinazotolewa na Serikali zinapatikana na kuwafikia wananchi kwa urahisi,  wakati wowote na mahali popote ndani na nje ya nchi. Tovuti Kuu hiyo pia  ni moja ya mafanikio makubwa katika kutimiza dira ya muda mrefu ya kuwa na dirisha moja linalotoa taarifa na huduma zinazotolewa na Taasisi  za Serikali kwa urahisi.

  Taarifa na huduma katika Tovuti Kuu hiyozimegawanywa katika maeneo makuu sita ya ambayo ni Serikali, Wananchi, Taifa letu, biashara, Sekta na Mambo ya Nje inalenga kutoa huduma mbalimbali kama upatikanaji wa nyaraka zote za Serikali, huduma zinazotolewa na Serikali kwa njia ya simu na mtandao, Viwango vya fedha, Hali ya Hewa, na Soko la Hisa.

  Huduma nyingine katika Tovuti Kuu hiyo imetengwa katika ukarasa wa Nifanyeje? ambao  unamjengea uwezo mwananchi wa kufahamu taratibu za upatikanaji wa huduma zinazotolewa na taasisi mbali mbali za Serikali kama nifanyeje kupata pasipoti, kibali cha kazi, TIN, Cheti cha kuzaliwa na mikopo ya chuo.

  Aidha tovuti hiyo pia inalenga kuziunganisha Tovuti na mifumo ya Taasisi mbali mbali inayotoa taarifa na huduma kwa wananchi na wafanyabiashara katika dirisha moja.

  Tovuti Kuu hiyo ilianza kutengenezwa mwaka 2009 na kupatikana kwa anuani ya www.egov.go.tz chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Tovuti hiyo iliboreshwa na kuunganishwa na iliyokuwa Tovuti ya Taifa kwa anuani ya www.tanzania.go.tz mwaka 2012 chini ya Wakala ya Serikali Mtandao.
  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa, ujenzi wa barabara hapa nchini umekuwa ni kichocheo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii hasa pale barabara hizo zinapopita katika maeneo ya uzalishaji zikiunganisha na maeneo ya masoko. 
   Akizungumza na Wananchi waliojitokeza katika katika eneo la Old Maswa nje kidogo ya mji wa Bariadi wakati wa uzunduzi wa ujenzi wa barabara ya Bariadi - Lamadi, Rais Kikwete alielezea kuwa kukamilika kwa barabara hiyo pamoja na sehemu iliyobaki inayoanzia Bariadi kupitia Maswa hadi Mwigumbi mkoani Shinyanga kutapunguza kwa kiasi kikubwa umbali wa usafiri kwa kuunganisha miji ya Shinyanga na Musoma. 
  Kwa hivi sasa ili kusafiri kati ya Shinyanga na Musoma msafiri analazimika kuzungukia Mwanza mjini kutokana na hali ya barabara hii ambayo ni ya changarawe kutopitika vizuri hasa nyakati za mvua. Rais Kikwete yuko mkoani Simiyu kukagua shughuli za maendeleo ambapo alianza moja kwa moja kuuzindua mradi wa ujenzi wa barabara ya Bariadi hadi Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8 inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Shilingi bilioni 67.4. 
   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Paschal Mabiti alimshukuru Rais Kikwete kwa kuipa kipaumbele barabara hiyo hadi kufanikisha kuanza kwa ujenzi wake. “Barabara hii mbali ya kuwa kiungo muhimu na mikoa ya jirani ya Mara, Mwanza na Shinyanga lakini pia inapita katika maeneo mengi ya uzalishaji na hivyo kuwa kichecheo muhimu katika ukuaji wa uchumi wa eneo hili” alielezea Mhe. Mabiti. 
   Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumzia maendeleo ya mradi huo alibainisha kuwa, hapo awali Mkandarasi anayetekeleza maradi huo Kampuni ya China Communications Construction Company Ltd kutoka Jamhuri ya Watu wa China, alianza hovyo hovyo na kwa kasi kidogo lakini ameweza kubanwa na hatimaye hivi sasa anaendelea vizuri akiwa tayari mefikia asilimia 51 ya kazi yote ya ujenzi wa barabara hiyo. 
   Waziri Magufuli alielezea kuwa tayari Mkandarasi huyo anakamilisha ujenzi wa madaraja 85 na tayari kiasi cha kilometa 16 za lami zimekwishajengwa. Kwa upande mwingine Waziri Magufuli alieleza kuwa ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huo, Serikali ililazimika kulipa fidia kiasi cha Shilingi milioni 795 kwa wananchi waliofuatwa na barabara hiyo na ambao walikuwa nje ya hifadhi ya barabara. 
  Aidha mkandarasi kwa upande mwingine alilazimika kulipa kiasi cha Shilingi milioni 602.14 kwa ajili ya kupata maeneo ya kuchimba mchangarawe na kokoto pamoja na uhamishaji wa miundombinu ya umeme na simu katika maeneo ambayo barabara hii inapita. Akizungumzia kusuasua kwa utendaji wa baadhi ya Makandarasi wanaotekeleza miradi mikubwa ya barabara hapa nchini, Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alisema kuwa kuchelewa kulipwa kwa madai ya Makandarasi kunasababisha kulipia tozo za ziada na hivyo kuyafanya madeni kuongezeka kadri madai hayo yanavyochelewa kulipwa. 
   Ziara hiyo ya Rais Kikwete katika mkoa wa Simuyu inatarajiwa kuendelea katika wilaya nyingine mkoani humo ambapo anatarajiwa pia kuweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa daraja la Mwanhuzi katika wilaya ya Meatu.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la Msingi kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Bariadi hadi Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyeshika mkasi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya Bariadi hadi Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8. Kushoto kwa Rais ni Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kulia kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Paschal Mabit
   Kutoka kushoto; Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, Mkuuwa Mkoa wa Simiyu Mhe. Paschal Mabiti, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Eng. Patrick Mfugale, wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe za uzinduzi wa barabara ya Bariadi - Lamadi inayojengwa kwa kiwango cha lami.
  Moja ya madaraja yanayojengwa katika barabara ya Bariadi - Lamadi

older | 1 | .... | 278 | 279 | (Page 280) | 281 | 282 | .... | 3272 | newer