Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Masauni aokoa Milioni Mia Mbili za Rais Magufuli

$
0
0
Jeshi la Polisi nchini limeelekezwa kutumia wafungwa ili kuweza kuokoa kiasi cha Shilingi Milioni Mia Mbili  kati ya Milioni Mia Saba zilizotolewa na Rais Dk. John Magufuli   katika Mradi wa Ujenzi wa Mabweni na Madarasa ya  Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo  Kurasini jijini Dar es Salaam.

Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipotembelea majengo chakavu ya chuo hicho baada ya kupokea kiasi cha Shilingi Milioni Mia Saba alizoahidi Rais Dkt. John Magufuli akihutubia katika mahafali ya kuhitimisha Mafunzo ya Kozi za Uofisa na Ukaguzi Msaidizi  chuoni hapo mwishoni mwa mwaka jana

“Wizara ina taasisi ya magereza ambayo ina nguvu kazi ya kutosha, na Rais alishaagiza wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji, sioni sababu ya kutumia kiasi hicho cha pesa kuwalipa vibarua wa nje, naagiza muwasiliane na Jeshi la Magereza pamoja na kikosi cha ufundi kilichopo ndani ya Jeshi la Polisi ili muweze kuona ni vipi mnaokoa kiasi hicho”alisema Masauni

Akitoa taarifa ya awali ya ujenzi huo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi, Naibu Kamishna Anthony Rutashuburugukwa alitaja  majengo yatakayojengwa kuwa ni ghala la chuo, madarasa matatu,bweni moja la askari wa kiume na bweni lingine la askari wa kike.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina wanafunzi wa chuo hicho walimshukuru Rais Dkt. Johh  Magufuli kwa kiasi cha fedha alichotoa ili kuweza kujenga sehemu mbalimbali za chuo hicho ikiwemo mabweni ambayo wamekiri ni chakavu na si rafiki kwa matumizi ya binadamu.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza  na  Askari  Polisi  ambao  ni  wanafunzi  katika  Chuo cha Taaluma ya  Jeshi  la  Polisi, wakati  alipotembelea  chuoni  hapo  kufuatilia maandalizi  ya awali  baada  ya  jeshi  hilo  kupokea kiasi cha Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho.Ziara hiyo imefanyika  leo jijini Dar es Salaam. Picha  na  Wizara  ya Mambo ya Ndani  ya Nchi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitembelea maeneo ya Chuo cha Taaluma ya Polisi  ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo hicho, kulia ni Mkuu wa Chuo, Naibu  Kamishna, Anthony  Rutashuburugukwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akitembelea maeneo ya Chuo cha Taaluma ya Polisi  ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli  kwa  ajili  ya  ujenzi  wa majengo ya chuo hicho,Wengine  ni  viongozi wa chuo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi wakati wa ziara katika  Chuo  cha Taaluma  ya  Polisi, jijini Dar es Salaam  ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi  Milioni  Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa  majengo  ya  chuo hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MWENYEKITI WA UWT TAIFA AFANYA ZIARA KUSINI UNGUJA

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
UMOJA wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), umewataka Akina Mama wa Mkoa Kusini Unguja kutobweteka na hali ya kisiasa Mkoani humo na badala yake waandae mbinu imara za kulinda ustawi wa CCM.

Wito huo ameutoa Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka katika mwendelezo wa ziara yake katika Mkoa huo alipokuwa akizungumza kwa wakati tofauti na wanawake wa UWT wa Wilaya mbili za Mkoa, huo ambazo ni Wilaya ya Kati na Wilaya ya Kusini Unguja.

Alisema licha ya Mkoa huo kusifika kwa kuwa ngome ya CCM Visiwani Zanzibar bado hakina Mama wana jukumu la kulinda heshima hiyo ili isichafuliwe na Vyama vya upinzani nchini.

Aliwasihi wanawake hao kuungana na kuhakikisha wanafanya kazi kwa pamoja katika kukiletea ushindi Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu ujao. Alisema mafanikio yaliyofikiwa katika Chama Cha Mapinduzi yametokana na juhudi kubwa za wanawake wa UWT wanaopigania maslahi ya taasisi hiyo usiku na mchana ili isonge mbele kimaendeleo.

Katika maelezo yake Mwenyekiti huyo Bi.Gaudensia alikemea vitendo vya udhalilishaji wa watoto katika Mkoa huo na kuiagiza taasisi za kisheria kuchukua hatua kwa watu wanaofanya uhalifu huo kwani unaharibu ndoto na malengo ya watoto ambao ndio taifa la leo na kesho.

Pamoja na hayo aliwakumbusha wanawake wa Mkoa huo kuhakikisha wanakuwa wanachama hai wa CCM kwa kulipia ada ili pindi pakitokea nafasi yoyote ya kuwania uongoi wake na vigezo sahihi vya kuingia katika ushindani wa nafasi hizo. Alisisitiza umuhimu wa UWT na CCM, kufanya uhakiki wa mara kwa mara wa wanachama ili kujiridhisha na kutambua takwimu sahihi za wanachama.

Awali aliwapongeza Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wakiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa utendaji wao ulioiletea heshima kubwa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.

Alieleza kuwa Zanzibar imekuwa ni nchi yenye maendeleo endelevu kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa kutoa huduma muhimu katika nyanja za kijamii,kiuchumi na kisiasa. "Wananchi nyote ni mashahidi juu ya mambo ya maendeleo yaliyotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi wa Dk.Shein.

Hatuna cha kuwalipa viongozi wetu kwa utendaji wao kwani nchi zetu zimepiga hatua kubwa za maendeleo,wananchi wameondoka katika wimbi la umaskini uliokithiri na kuwa na kipato cha kati kinachowawezesha kujikimu kimaisha.",alisema Mwenyekiti huyo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwaiba Kisasi, alimwakikishia Mwenyekiti huyo kuwa Mkoa huo una historia ya kudumu ya wanachama wake kuwa wanachama wazalendo wenye misimamo imara isiyoyumba.

Akizungumza Katibu Mkuu wa Umoja huo Taifa, Mwl.Queen Mlozi alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM sambamba na maandalizi ya kongamano la kumpongeza Rais wa Zanzibar, na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa utekelezaju wake wa Ilani kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo alisema Akina Mama wa UWT wanajengewa uwezo juu ya masuala mbali mbali ya kimaendeleo ikiwemo ujasiriamali wajiajiri wenyewe.

Naye Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kusini Unguja,Ndugu Shemsa Abdallah Ali alisema kuwa CCM imeendelea kuimarika kisiasa,kijamii na kisiasa. Alisema kuwa katika kupambana na Changamoto ya kujikwamua kiuchumi Akina Mama wamekuwa wakijiajiri wenyewe kupitia miradi mbali mbali ya vikundi vya ujasiriamali katika Mkoa huo.

Aidha Mwenyekiti huyo wa Umoja huo Taifa Bi.Gaudensia amewakabidhi wanachama wapya 338 kadi za UWT ,ambapo Wilaya ya Kati ni wanachama 188 na Wilaya ya Kusini wanachama 150. Sambamba na hayo Wilaya zote mbili pamoja na CCM Mkoa huo wamekabidhi Taarifa za Utekelezaji kwa Mwenyekiti huyo.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti huyo amekabidhi Mifuko 100 ya saruji kwa Hospitali ya Wilaya ya Makunduchi iliyotolewa na Wabunge na Wawakilishi wa Viti Maalum wa Mkoa huo. Sambamba na hayo Mbunge wa Jimbo la Paje Mhe.Jaffar Sanya Jussa amekabidhi shilingi milioni tano kwa Vikundi Vitano vya ushirika vya Jimbo hilo. 
  MWENYEKITI wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka akizungumza na Akina Mama Wajasiriamali wa Jimbo la Peje katika ziara yake Wilaya ya Kusini Unguja.
 MWENYEKITI wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka(kulia), akimkabidhi fedha shilingi milioni tano za vikundi vitano vya Jimbo la Paje zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Katibu wa CCM Wilaya ya Kusini Ndugu Hafidh Hassan Mkadam.
MWENYEKITI wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka akikabidhi Saruji mifuko 100 iliyotolewa na Wabunge, na Wawakilishi wa Viti Maalum wa Mkoa huo kwa uongozi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Makunduchi Unguja.


Prof. Kabudi na Dkt. Mahiga wakabidhiana ofisi

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye awali alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akikabidhi Taarifa ya Makabidhiano ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ambaye awali alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dodoma tarehe 12 Machi 2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) akimkabidhi Taarifa ya Makabidhiano ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiweka saini Kitabu cha mahudhurio mara baada ya kukabidhiwa ofisi jijini Dodoma. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi mara baada ya makabidhiano ya ofisi. 
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakishuhudia makabidhiano ya ofisi kati ya Waziri wa Katiba na Sheria na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa ofisi na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga. 
Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hayupo pichani). 
Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi Savera Kazaura akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Katiba na Sheria kabla zoezi la makabidhiano kuanza. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana na baadhi ya watumishi mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Anayemkaribisha ni mmoja wa watumishi hao, Bw. Shaban Mtambo. 
Bi. Chiku Kiguhe akisalimiana na Mhe. Prof. Kabudi. 
Bw. Habibu Ibrahim akisalimiana na Mhe. Waziri. 
Bw. Maulidi Mkenda akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongea na baadhi ya watumishi waliojitokeza kumpokea mara alipowasili kwa mara ya kwanza katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje jijini Dodoma. 
Bw. Caesar Waitara akisalimiana na Mhe. Prof. Kabudi 

KAZI NA DAWA

$
0
0
 Dereva wa daladala akipata chakula cha mchana huku akiendelea kusuburi abiria wajae  katika  kituo cha mabasi makumbusho kilichopo wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

Mpiga debe akipata chakula cha mchana  huku akiendelea na kazi kama alivyo naswa na kamera yetu katika  kituo cha mabasi leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

SUKARI ISIYO NA UBORA, MAFUTA YANASWA MBWENI

$
0
0
*Ni baada ya Polisi, DC Kinondoni kufanya msako usiku wa manane
*Ng'ombe waliopewa mafunzo maalumu watumika kubeba magendo 
*Waliohusika wakimbia nyumba...sasa msako wa nyumba kwa nyumba kufanyika

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

SUKARI bandia kilo 350 na mafuta ya kupikia madumu 25 ambayo hayana ubora yamekamatwa katika eneo la Mbweni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Sukari na mafuta hayo ya kupikia yamekamatwa usiku wa kuamkia leo, Machi 12.2019 eneo la Mbweni ambako kumebainika kuwepo kwa bandari bubu ambayo watu wasiowaaminifu wanatumia bandari hiyo kuingiza bidhaa za magendo na kibaya zaidi zisizokuwa na ubora.

Msako mkali uliofanyika usiku wa kuamkia leo, kupitia Jeshi la Polisi Kituo cha Polisi Mbweni kilichopo katika Wilaya ya Konondoni pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo wamefanikiwa kukamata bidhaa hizo za magendo.

Kwa mujibu wa Polisi Mbweni ni kwamba wanaopitisha bidhaa hizo za magendo wamekuwa wakitumia ufukwe wa Bahari ya Hindi katika eneo hilo na kisha baada ya kuingiza bidhaa hizo nchi kavu wanatumia ng'ombe ambao wamepata mafunzo maalumu kwa ajili ya kubeba mizigo hiyo na kukimbia nayo kwa ajili ya kufichwa.

Akizungumza akiwa katika Kituo cha Polisi Mbweni ambako ndiko bidhaa hizo za magendo zimehifadhiwa, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amesema, kutokana na msako mkali ambao umefanywa na Polisi wamekamata bidhaa hizo ambapo kimsingi ni hujuma kubwa kwa Serikali kwani wanaopitisha wanakwepa kodi na kibaya zaidi wanahatarisha maisha ya wananchi.

"Baada ya kufanyika kwa msako huu usiku kucha tumekamata mifuko 70 ya sukari na kila mfuko una kilo 50, hivyo kwa ujumla tumekamata kilo za sukari 350 pamoja na mafuta madumu 25.Haifahamiki hii sukari na haya mafuta yanatoka nchi gani lakini wanaofaya biashara hii haramu wakifika nchi kavu wanachukua hiyo sukari na kisha kuijaza kwenye mifuko ya sukari ambayo inazalishwa nchini na kisha kwenda kuuza.

Hata hivyo amesema kuwa jahazi au boti ambayo imetumika kuleta sukari hiyo baada ya kuona Polisi wamefika eneo la tukio wahusika waliirudisha kwenye maji na hivyo haikufanikiwa kupatikana kwani iliondolewa.

Chongolo amesema Serikali haiko tayari kuona zinaingizwa bidhaa ambazo ziko chini ya ubora na wanaofanya hivyo watambue mwisho wao umefika na wote ambao wamehusika watachukuliwa hatua kwani majina yao yamefahamika.

Amefafanua kuwa kwa sasa sukari kutoka nje hairuhusiwi kuingizwa nchini kwani viwanda vilivyopo vinazalisha sukari ya kutosha huku akifafanua sukari ambayo wameikamata haijathibitishwa ubora wake wala inakotoka.

"Hatuwezi kukubali kuona wananchi wanadhuruka.Huu msako ambao tumeuanzisha ni endelevu na utaendelea kila siku, wale ambao wamezoea kufanya biashara kiujanja ujanja ikiwa pamoja na kukwepa kodi watambue mwisho wao umefika.

Amesema kitendo cha kuingiza sukari ambayo haina ubora inaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo kupata saratani ya tumbo au vidonda vya tumbo."Hii sukari ambayo tumeikamata haijulikani ni ya viwandani ama wapi? Wanaohusika na michezo hii wajue hatutawaacha."

Kwa upande wake Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Polisi Kawe Dk. Ezekiel Kyogo amesema bidhaa hizo zinapitishwa kupitia bandari bubu na matokeo yake kuikosesha Serikali mapato yatokanayo na kodi.Amefafanua baada ya kufanya uchunguzi wao wamebaini nyumba zinazotumika kuficha bidhaa za magendo pamoja na majina ya wahusika ambao wengine wamekimbia nyumba zao baada ya kufanyika msako.

Amesema kuwa watu wanne wanashikiliwa na Polisi kutokana na kutuhumiwa kuhusika kwenye kuingiza bidhaa hizo za magendo na sheria itachukua mkondo wake."Tutafanya msako nyumba hadi nyumba kuhakikisha wote ambao wamehusika wanachukuliwa hatua".

Kuhusu jahazi ambalo limetumika kuleta bidhaa hizo za magendo, Dk.Kyogo amesema wameshindwa kulipata kwani walikimbia eneo la tukio.
Mkuu wa Wilaya ya KInondoni Mh Daniel Chongolo akioneshwa bidhaa hizo za Magendo zilizokamatwa leo katika Bandari Bubu,Mbweni jijini Dar
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya  Kipolisi Kawe ,Dkt Ezekiel Kyogo  akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Daniel Chongolo (kulia) mashine iliyokuwa ikitumika  kwenye boti za kubebea mizingo ya magendo kutoka baharini katika Bandari Bubu ya Mbweni jijini Dar es Salaam.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kukamatwa kwa bidhaa mbalimbali za magendo katika Bandari Bubu ya Mbweni,leo jijini Dar.
 Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya  Kipolisi Kawe ,Dkt Ezekiel Kyogo akitoa ufafanuzi namna bidhaa hizo za magendo zilivyokamatwa katika bandari bubu,Mbweni jijini Dar. 
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya  Kipolisi Kawe ,Dkt Ezekiel Kyogo  akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Daniel Chongolo (kulia) Ng'ombe wanaobeba mizingo ya magendo kutoka baharini katika  Bandari Bubu ya Mbweni jijini Dar es Salaam.
Bidhaa mbalimbali za magendo zilizokamatwa katika bandari Bubu ya Mbweni jijini Dar es Salaam .
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo akipewa maelezo na
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kipolisi Kawe ,Dkt Ezekiel Kyogo mara baada ya kukamatwa bidhaa za magendo katika ufukwe wa Mbweni (bandari Bubu),leo jijini Dar

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh DaniellChongolo akizungumza jambo na vijana wanaodaiwa kutumika kubeba mizigo hiyo ya magendo inapofikishwa nchi kavi,Mbweni jijini Dar

SHUKURANI

$
0
0
Ndugu zetu Wapendwa,

Familia ya Kileo & Kimei Tunawashukuru Sana kwa upendo mliotupa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mama yetu Mpendwa Mh. Mrs. Venus B. Kimei-Kileo. Mmetufariji, mmetujali, mmetuongoza, mmetupa moyo kwa ujumla tumeuona Upendo wa kweli na tumepata faraja sana. Tunamshukuru sana Mungu kwa ajili yenu.

Tunaomba muendelee kuwa nasi tunapoenda kutoa sadaka ya shukrani Jumapili 17 Machi, 2019 saa 4:00 asubuhi katika kanisa la KKKT Msasani. Mara baada ya Ibada tutashiriki Chakula cha Mchana saa 7 mchana Nyumbani Mikocheni B.

Karibuni mshiriki nasi, 

E.S Kileo - Mwenyekiti 
Asanteni Sana

THE SUSTAINABLE DEVELOPMENT GOALS (SDGs) ROAD SHOW, VOLUNTARY NATIONAL REVIEW (VNR) BUSINESS AND CSO CONSULTATIONS STACK-HOLDERS MEET IN DAR ES SALAAM

$
0
0

GEITA Gold Mine Tanzania, Vice-President Simon Shayo gives his remarks during the opening of  VNR Businesses and CSO Business Consultative meeting in Dar es Salaam March 11 2019. 
(Photos by Robert Okanda)


A SECTION of participants follow the proceeding of the VNR Businesses and CSO Business Consultative meeting in Dar es Salaam.




TANZANIA Private Sector Foundation (TPSF), Executive director Godffrey Simbeye gives his remarks during the opening of  VNR Businesses and CSO Business Consultative meeting in Dar es Salaam.   

A SECTION of participants follow the proceeding of the VNR Businesses and CSO Business Consultative meeting in Dar es Salaam March 11 2019.

A SECTION of participants follow the proceeding of the VNR Businesses and CSO Business Consultative meeting in Dar es Salaam.   

UNGCNT National Coordinator, Emmanuel Nnko presents an issue on during the meeting. 


UNDP Economic Advisor, Fistum Abraha  gives an overviews of the SGD's and the NFYDP.

TRANS-FORMATIVE Development Capacities (PTY) Ltd, Executive director Jacob Gyamdi-Aidoo presents his paper on business opportunity during the opening meeting. 


PARTICIPANTS pose for a souvenir photo.   


WELCOME REMARKS BY MR. GODFREY SIMBEYE, TPSF EXECUTIVE DIRECTOR, AT THE SUSTAINABLE DEVELOPMENT GOALS (SDGs) ROAD SHOW, VOLUNTARY NATIONAL REVIEW (VNR) BUSINESS AND CSO CONSULTATIONS
ON 11TH MARCH 2019, DAR ES SALAAM

I am privileged to welcome you this morning to the peer-to-peer dialogue platform, this being one of the significant events of our countries’ private sector.

On behalf of the Tanzania Private Sector Foundation and on my own behalf, allow me to extend a warm welcome to you to this forum.

At the same time, I would like to express my gratitude to ATE, CTI, TAHA, TATO who are all members of TPSF and lastly but not the least, the UN Global Compact Network Tanzania for organizing this seminar. I am sure that your support and enthusiasm has contributed to the success of this seminar immensely. Through these initiatives, we are enabling the private sector in Tanzania to continue to play its role as an engine of economic growth and employment creation.

TPSF draws its mandate and influence from a network of over 4.7 million businesses (formal and informal) who are direct members in more than 200 business associations registered in TPSF membership book.  According to the TPSF constitution, the ''Private Sector'' is that part of the National Economy, which is made up of private enterprise, - individuals, groups, and corporate bodies not owned or operated by the State and which are for profit both formal and informal. It includes groups such as farmers and artisanal miners.  It is recognized as a key partner of the Government towards the achievement of the National Development Vision 2025 and universally adopted Sustainable Development Goals (SDGs). It plays an important role as an engine of growth and job creation. It provides goods and services, generates tax revenues to finance essential social and economic infrastructure, it develops new and innovative solutions to tackle development challenges. 

Ladies and Gentlemen,
Where do we stand? Are we on track? What are the inspiring breakthroughs and success stories that are showing results and impacts? What are the good practices that can be replicated and scaled up? What are the gaps and constraints and how should we address them? Looking ahead, what steps should we take to accelerate progress? 

How can we ensure that business’ involvement in the SDGs on the ground becomes an integral part of the follow-up and review mechanism? a key question is how we can best tell our stories of SDG impact, both individually and collectively?.

Answers to these questions shall be addressed collectively through the SDGs Road Show and Voluntary National Review (VNR) as a regular and inclusive reviews of progress at the national and sub-national levels, which are country-led and country-driven. As you may all be aware, in July 2019, the United Republic of Tanzania will submit its first Voluntary National Review (VNR) on Tanzania’s progress in implementing the Sustainable Development Goals (SDGs) i.e. SDG 4, SDG8, SDG10, SDG13,SDG16 & SDG17  to the UN’s High-Level Political Forum in New York. The VNR provides an opportunity to highlight Tanzanians achievements, priorities and challenges both domestically and internationally in advancing the 2030 Agenda. This Roadshow therefore, has come at an opportune time.

This is the opportunity for businesses to tell your story, creating a common language and shared tools to drive future action and positive impact. It is also a platform to mobilise opportunities. It is estimated that globally participation will drive USD 12 Trillion in market opportunities, let Tanzania make its share

Distinguished Guests, Ladies and Gentlemen 
The former Prime Minister of Britain, Sir Winston Churchill was one of very staunch proponents of the private sector. He said, and I quote, “Some people regard private enterprise as a predatory tiger to be shot. Others look on it as a cow they can milk. Not enough people see it as a sturdy horse, pulling a heavy wagon”. Our government agrees with Churchill that the private sector is a healthy horse which pulls a heavy object (development of our economy), and that is why we recognise our responsibility of supporting the sector and other agencies so that they can invest in productive businesses. 

Ladies and Gentlemen; 
Tanzania is the fastest growing economies in Sub-Saharan Africa with 7.2% growth rate respectively recorded in 2017. Our country is richly endowed with natural resources and connected to the sea, which makes their position strategic as the gateway to the EAC and Central Africa region. 

We still need Government support to the private sector through formulation of appropriate policies, creation a conducive environment for doing business and investment, and by helping to bring about institutional changes, which will help build investors’ confidence. 

Tanzania has successfully implemented sweeping reforms geared to creating conducive business environment and attractive investment climate. 

Distinguished Guests, Ladies and Gentlemen; 
 We all know very well that the Government opened up the economy, introduced appropriate policies, laws and regulations, and continues to take various measures to promote the private sector in the country. Through such efforts, Tanzania is now among the countries with a vibrant and liberalized economy making it one of the most preferred destinations to invest in Africa. 

Distinguished Guests, Ladies and Gentlemen 
The industrial, trade and marketing sector will not grow without deliberate steps to develop it. Such development will be possible if challenges related to production costs are addressed. This will be achieved through ensuring adequate energy support, business registration, legal and regulatory support, reducing bureaucracy; and providing better fiscal and monetary regimes. What is basic, however, is to do away with the mistrust between the public and private sectors. 

There is a mistaken notion by the public sector that the private sector carries out its business unscrupulously; while the private sector considers the public sector to think of nothing but slashing its profit margins through unfriendly tax regime and a host of other rates. This is a challenge we have to all face and solve without fear. 

Distinguished Guests, Ladies and Gentlemen 
The government plays a critical role in coordinating and providing guidance to private sector development and investments. The government’s core functions include preparing policy, legal framework and strategies for private sector as well as development and investment to monitor their implementation. 

Distinguished Guests, Ladies and Gentlemen 
Let me end my welcome address with a call for a united private sector in so that it can foster sustained growth fed by integrity, hard work, dedication and innovation. 

I would nevertheless wish to my fellow private sector stakeholders in Tanzania to come out in an aggressive way so that you demonstrate thinking big, and take bold strides that reflect our ability to take daring decisions as serious entrepreneurs. When you think big and take daring decisions there will be an impact on the economy of the country as well. This is what I look forward to – an aggressive private sector and a robust economy for our countries.

My belief is that our countries stand to benefit from the SDG Road Show and the VNR in July, hence cohesive and increased bilateral trade opportunities and we should therefore, not lose track of this opportunity.

May I also take this opportunity to wish you all very fruitful deliberations which will lead to creation of a national stakeholder’s forum later this month during which we will all take stock of what worked and what didn’t work, and why.  

Honorable Chairman of the Board, Board Members, Private Sector Stakeholders, Invited Guests, Ladies and Gentlemen. Thank you very much

DC KASESELA : MARUFUKU WANAUME KUWAKATAZA WANAWAKE KUMILIKI ARDHI

$
0
0
Na Fredy Mgunda,Iringa. 
 WANAWAKE mkoani Iringa wametakiwa kuanza kumiliki ardhi kwa ajili ya kufanya shughuli za kimaendeleo na badala yake waachane na tamaduni kandamizi za kuwaachia wanaume katika umiliki wa mali. 
 Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Richard Kasesela katika kilele cha maadhimisho ya wanawake yaliyofanyika katika kijiji cha ibangamoyo kata ya ulanda wilaya ya Iringa alisema kuwa wanawake waaze kumiliki ardhi ili kujiinua kiuchumi kwa kuwa wanawake ndio walezi wa familia tofauti na wanaume wanaokuwa na makazi tofauti tofauti. Kasesela aliwataka wanaume kuwapa haki wanawake kumiliki ardhi kwa kuwa wanahaki hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi hivyo mwanaume atakayemkataza mwanamke kumiliki ardhi atachukuliwa hatua za kisheria. 
 “Nasema nileteeni wanaume wote wanaowazuia wanawake kumiliki ardhi tutamtafutia sehemu ya kuishi kwa kuwa atakuwa anakiuka katiba ya nchi yetu hivyo ni lazima sheria ifuate mkondo wake” alisema Akitembelea banda la mradi wa urasilmishaji ardhi vijijini (LTA), Kasesela alisema kuwa mradi huo umekuwa mkombozi kwa wanawake kumiliki ardhi kutokana na kutoa elimu kwa wanaume na kufanikisha wanawake kupatiwa hati miliki za kimila ambazo ndio limekuwa suluhisho la migogoro ya ardhi vijijini. 
 Aidha Mtaalam wa mawasiliano na uenezi wa mradi wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA), Jackline Mhegi alisema kuwa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasisitiza kuwa binadamu wote ni sawa na huzaliwa huru hivyo basi wanatakiwa kupata ulinzi sawa na sheria za nchi ikiwepo kumiliki ardhi. 
 “Kwa mujibu wa ibara ya 24(I) inasema kila mtu anahaki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyokuwanayo kwa mujibu wa sheria,hivyo mwanamke ana haki ya kumiliki ardhi kama mojawapo ya mali na kupata ulinzi wa mali kulingana na katiba ya nchi” alisema Mhegi 

 Mhegi alisema, sera ya taifa ya ardhi ya mwaka 1995 inaeleza kuwa “ni haki ya kila mwanamke kupata,kumiliki,kutumia na kuuza au kugawa ardhi kwa kuwa hata mwanaume ana haki hiyo” Sheria ya ardhi namba 4 na 5 ya mwaka 1999,Kwa mujibu wa kifungu cha 3 (2) cha Sheria ya ardhi Na.5 ya Vijiji ya mwaka 1999 inasema 
“Haki ya kila mwanamke kupata, kumiliki, kutumia na kuuza au kuigawa ardhi ifahamike kuwa ni sawa na haki ya mwanamume yeyote kwa viwango vilevile na masharti yaleyale” “Sheria hizi zimeondoa ubaguzi dhidi ya mwanamke. Mwanamke anaehitaji ardhi atafuata taratibu zinazohusika na hapaswi kunyimwa ardhi kwa sababu tu yeye ni mwanamke, Sheria ya mahakama za utatuzi wa migogoro namba 2 ya mwaka 2002, Sheria ya marekebisho ya utatuzi wa migogoro namba 2 ya mwaka 2004, Sheria ya ndoa ya mwaka 1971”alisema Mhegi 
 Mhegi alimalizia kwa kusema, Wanawake ni watumiaji wakuu wa ardhi hivyo vyombo vinavyohusika na masuala ya usimamizi na utawala wa ardhi vihakikishe kuwa wanawake na wanaume wanashirikishwa ipasavyo katika masuala yahusuyo ardhi ili kuleta usawa wa kijinsia katika usimamizi na umiliki wa ardhi utakao changia maendeleo endelevu kutoka na rasilimali ardhi kiuzalishaji, 
Hivyo wanawake wahakikishe wanatumia nafasi walizonanzo kwa kushiriki na kutoa mawazo yao kwa lengo la kuboresha maslahi ya familia zao na taifa kwa ujumla. Naye Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Stella Mosha, alisema ni wakati sasa kwa wanawake kutambua ya kwamba wana haki ya kumilki ardhi sawa kama wanavyomiliki wanaume kwa njia mbalimbali zikiwemo wao binafsi, wao Pamoja na waume au ndugu zao. 
 “Pia jamii inakumbushwa kuachana na mila na desturi kandamizi katika zinazo wazuia wanawake kuto miliki ardhi kwa sababu wakati umebadilika wanawake na wanaume wanatakiwa kushirikiana ili kuweza kuinua uchumi wa familia na baadae taifa kwa ujumla” alisema mosha Mosha aliesma,Mradi uliweza kutoa elimu ya juu ya haki ya wanawake kupitia mikutano ya hadhara kwa kila kijiji kwa wanawake pekee na baadae kuwaunganisha na wanaume ili kuwa na majadiliano ya pamoja.
 “Mradi ulitoa mafunzo juu ya Sera na Sheria za ardhi zinazoelezea haki ya wanawake kumiliki rasilimali ardhi” alisema mosha Mosha alimalizia kwa kusema,mradi uliwajengea uwezo wanawake kuingia katika vyombo mbalimbali vinavyosimamia masuala ya usimamizi wa ardhi ngazi ya kijiji, kama vile: kamati ya Mpango bora wa Matumizi ya ardhi, Kamati ya Uhakiki wa maslahi ya ardhi, Baraza la utatuzi wa migogoro ya ardhi ya kijiji.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi mbalimbali wakati wa maazimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyikia katika kata ya ulanda mkoani Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi mbalimbali akiwa kwenye banda la mradi wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA) ambao ndio wamesaidia kutoa hati miliki kwa wanawake na kupunguza migogoro wilaya ya Iringa
Baadhi ya wadau wakiwa kwenye banda la mradi wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA)
 Wadu wakiwa kwenye banda la mradi wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA)



MADAKTARI BINGWA WA MOI NA MUHIMBILI WASHIRIKIANA KUFANYA UPASUAHI WA KIHISTORIA

$
0
0
 Jopo la Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo,Mgongo na Mishipa ya Fahamu wa MOI kwa kushirikiana na Madaktari bingwa wa Pua, Koo na Masikio wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifanya upasuaji Mkubwa wa kuondoa uvimbe kwenye Ubongo kwa kupitia kwenye tundu la pua. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)




NA KHAMISI MUSSA

Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya Fahamu wa MOI kwa kushirikiana na Madaktari bingwa wa Pua, Koo na Masikio wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefanya upasuaji mkubwa wa kuondoa uvimbe kwenye Ubongo kwa kupitia kwenye tundu la Pua (Endoscopic Trans nasal transsphenoidal pituitary surgery) ambao ulikua haufanyiki hapa nchini.


Upasuaji huo wa kihistoria umefanywa kwa mafanikio makubwa na jopo la madaktari bingwa wazalendo wanne kwa kutumia muda wa masaa matatu ambapo wamefanikiwa kuondoa uvimbe wote.



Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu MOI, Dkt Lemery Mchome amebainisha kwamba upasuaji huu umefanyika kwa mafanikio makubwa na mgonjwa hatatumia muda mwingi hospitalini na ataruhusiwa kwenda nyumbani ndani ya siku chache.



“Upasuaji huu ni wa kisasa na wenye matokeo chanya kwa mgonjwa kwani tunaondoa uvimbe kwa kupitia puani badala ya kufungua fuvu kama ambavyo imezoeleka ambapo mgonjwa anatumia muda mwingi kurudi kwenye hali ya kawaida, pia kwa njia hii mgonjwa hatahitaji kupumua kwa kutumia mashine baada ya upasuaji na tutamruhusu ndani ya siku chache zijazo” Alisema Dkt Lemery



Dkt Lemery amesema upasuaji huu umewezekana kutokana na uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na Serikali katika miundombinu pamoja na wataalamu hivyo madaktari bingwa Wazalendo wanaweza kufanya upasuaji huo bila ya utegemezi wa wataalamu kutoka mataifa mengine.



Kwaupande wake daktari bingwa wa magonjwa ya Masikio, Pua na Koo Dkt Edwin Liyombo Kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema upasuaji huu wa kuondoa uvimbe kwa kupitia kwenye tundu la pua ni wa kisasa na wenye matokeo bora zaidi ya njia iliyozoeleka ya kufungua fuvu.



“Tumefanya upasuaji huu kwa mafanikio makubwa sana, tunaamini mgonjwa atakuwa salama na atakwenda nyumbani mapema, awali wagonjwa hawa walilazimika kwenda nje ya nchi kwa gharama kubwa, kwakuwa vifaa vipo hapa MOI tumeamua tushirikiane kuwahudumia Watanzania wenzetu hapa nchini na kuipunguzia Serikali mzigo wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa gharama kubwa” alisema Dkt Liyombo.



 Kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli umepelekea huduma nyingi za kibingwa ambazo zilikua hazipatikani hapa nchini kuanzishwa na hivyo kuokoa maisha ya Watanzania wengi.


Wauguzi wasisitizwa kuzingatia maadili ya kazi

$
0
0
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukungu nchini Agnes Mtawa amewataka wauguzi na wakunga kuzingatia maadili ya kazi ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Sista Mtawa amesema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza katika mafunzo ya siku moja ya kuwaongezea ujuzi wauguzi na wakunga   wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila sambamba na kuwakumbusha maadili ya kazi.
“Katika kutoa huduma tuna maadili (Professional Code of Conduct) na miongozo (The Guiding Principle) ambayo kila muuguzi na mkunga anatakiwa afuate hizo taratibu kwakua jamii
inawategemea katika usimamizi na utoaji wa huduma bora” amesema Sista Mtawa.
Pia amesisitiza kwamba kila muuguzi na mkunga anapaswa kuwa na leseni hai inayompa nafasi ya kutoa huduma kwani kutokuwa na leseni hai ni kosa na mtoa huduma anaweza kupoteza kazi. 
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Mlogaznila Sista Redamptha Matindi ameshukuru kutolea kwa mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo wauguzi wa hospitali hiyo.

Mratibu wa leseni na Maadili Sista Jane Mazigo akitoa mada katika mafunzo ya siku moja ya kuwaongezea ujuzi wauguzi na wakunga wa Hospitali ya Mloganzila. 
Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wakimsikiliza Mratibu wa leseni na maadili Wakati akitoa mada katika mafunzo hayo. 

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini Sista Agnes Mtawa (kushoto) akimkabidhi Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dk. Julieth Magandi kitabu cha maadili na miongozo ya wauguzi na wakunga, leo hospitalini hapo
 Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dk. Julieth Magandi (watatu kutoka kulia aliyevaa koti jeupe) akiwa katika picha ya pamoja na Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukungu nchini Agnes Mtawa (watatu kutoka kushoto aliyevaa gauni la bluu) pamoja na washiriki wengine wa mafunzo hayo.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 12.03.2019

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 13,2019

MKUTANO WA AFRICA NOW WAFUNGULIWA LEO JIJINI KAMPALA

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa Africa Now Summit 2019 ulioanza leo kwenye hoteli ya Commonwealth Resort, Munyonyo jijini Kampala, Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Africa Now Summit 2019 ambapo viongozi wa Afrika wanakutana kujadili masuala mbalimbali ya utengamano katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika ambapo Tanzania imewakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akiwa na mwenyeji wa Mkutano wa Africa Now Summit 2019 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi Mohamed (kulia) wakati wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano katika hoteli ya Commonwealth Resort, Munyonyo jijini Kampala Uganda.

WAZIRI KAIRUKI AMKABIDHI RASMI WIZARA, BITEKO

$
0
0


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki, amemkabidhi rasmi majukumu ya Uwaziri wa Wizara ya Madini, Doto Biteko katika kikao kilichohudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo. 

Waziri Kairuki amemshukuru Waziri Biteko kwa ushirikiano aliompatia kwa kipindi chote alichokuwa Waziri wa wizara hiyo na kueleza kwamba, kabla ya makabidhiano hayo, wamepata wasaa wa kupitia kwa pamoja majukumu na vipaumbele vya wizara ikiwemo maeneo muhimu yanayotakiwa kupewa msukumo. 

Naye, Waziri Biteko akizungumza mara baada ya kukabidhiwa majukumu hayo, amemshukuru Waziri Kairuki na kumwelezea kuwa ni Waziri aliyekuwa Mwalimu mzuri kwake kwa kipindi chote alichokuwa Naibu Waziri. 

Ameongeza, Waziri Kairuki hakuwahi kumnyima nafasi ya kujifunza ikiwemo kumtuma kuteleleza majukumu mbalimbali nafasi ambayo imemkomaza. 

” Waziri hakuwahi kuninyima nafasi ya kujifunza ikiwemo kutekeleza majukumu yangu na nitaendelea kuhitaji ushauri wake,”amesema Biteko. 

Makabidhiano hayo yamefanyika Machi 12, Ofisini kwa Waziri Biteko Jijini Dodoma. 

Waziri Biteko aliteuliwa Januari 8, 2019 kushika wadhifa huo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kufanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. 

Waziri Biteko alichukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Madini Angellah Kairuki ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.

BIKO YANG'ARISHA MAISHA YA MKAZI WA JIJI LA DAR,YAMKABIDHI PIKI PIKI,FEDHA TASLIMU MILIONI MOJA

$
0
0


Mratibu Msaidizi wa Matukio wa Biko, Hassan Ahmed kushoto akimkabidhi kadi ya pikipiki mshindi wao wa bodaboda na sh milioni moja, anayejulikana kama Steven Yohana Mbelwa, mkazi wa Dar es Salaam baada ya kufanikiwa kuibuka mshindi kwenye droo kubwa ya juzi Jumapili, ambapo droo hizo kubwa hufanyika kila Jumatano na Jumapili kwa kupitia wachezaji wanaotumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu 2456. Picha na Mpigapicha wetu.
Mshindi wa pikipiki na sh milioni moja, Steven Yohana Mbelwa, kulia akifurahia na wenzake baada ya kufanikiwa kukabidhiwa zawadi zake kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko aliyoshinda katika droo kubwa iliyochezeshwa juzi Jumapili ambapo droo hizo kubwa hufanyika kila Jumatano na Jumapili kwa kupitia wachezaji wanaotumia namba ya Kampuni ambayo ni 505050 na kumbukumbu ni 2456. Picha na Mpigapicha wetu.


MAAFISA ARDHI HALMASHAURI MULEBA WADAIWA KUMCHOSHA NAIBU WAZIRI MABULA

$
0
0
Na Munir Shemweta, MULEBA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameshangazwa na maafisa ardhi wa halamashauri ya wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera kushindwa kuelewa idadi ya viwanja vilivyopimwa katika halmashauri hiyo na kumuagiza kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Shaban Manyama kufanya mabadiliko katika idara hiyo ili kupata watu sahihi watakaoisaidia idara.

Dkt Mabula alikutana na kadhia hiyo katika wilaya ya Muleba jana akiwa katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya kutembelea wilaya za mkoa wa Kagera kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.

Waziri Mabula alisema haiwezekani watendaji wa sekta ya ardhi kuwa katika idara halafu wanashindwa kujua ni viwanja vingapi vimemilikishwa kwa wananchi wakati agizo lilishatolewa tangu mwaka 2017 kuwa viwanja vyote viingizwe kwenye mfumo ili kuwa na takwimu sahihi

‘’Hapa hakuna idara ya ardhi maana watendaji wake hawajitambui lazima pafanyike mabadiliko na kupata watu watakaoweza kusimamia idara hii maana sekta inadidimia kwa kukosa mtu wa kuisimamia’’. Alisema Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Aidha, Dkt Mabula ametaka afisa ardhi Mteule wa halmashauri hiyo kuwekwa chini ya uangalizi maalum wa miezi sita na kubainisha kuwa serikali haiwezi kuwa na sekta isiyofanya kazi zake kwa ufanisi.

Naibu Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi pia ameshtushwa na halmashauri ya wilaya ya Muleba kuwekewa lengo la kukusanya shilingi milioni mia tatu lakini ikifanikiwa kukusanya milioni 72,870,943 pekee huku ikidai bilioni 3.3 jambo alilolieleza kuwa halikubaliki kwani serikali inakosa mapato mengi.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Muleba Shaban Manyama alimueleza Naibu Waziri Mabula kuwa halmashauri yake imeweza kukusanya shilingi milioni 72.87 kupitia kodi ya ardhi ambazo ni sawa na asilimia 24.3 na kuongeza kuwa katika kipindi cha mwezi februari mosi hadi tarehe 11 Machi jumla ya shilingi 1,802,750 zimekusanywa kama kodi ya ardhi.

Naye Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo alisema halmashauri ya wilaya ya Muleba inahitaji kusaidiwa kutokana na watendaji wake kutokuwa makini katika utendaji kazi na kutolea mfano tofauti ya takwimu za umilikishwaji ardhi katika halmashauri hiyo zinazoelezwa na watendaji wa sekta hiyo ni ishara kuwa idara hiyo inahitaji msaada na kuahidi kupeleka mtu kutoka ofisi ya ardhi Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kuweka mambo sawa.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisalimiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera alipowasili wilayani humo kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi. Wa pili kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo na wa pili kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muleba Benjamin Mwakasege.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia moja ya majalada ya ardhi katika Masijala ya ardhi ya halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoa wa  Kagera akiwa katika ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya Benjamin Mwakasege, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Muleba Shaban Manyama na wa pili kulia ni Afisa Ardhi Simon Mosha.

LOVY ALIFUATA NYAYO ZA BABA YAKE VICKY LONGOMBA.

$
0
0
Na: Moshy Kiyungi

Aliyekuwa mtunzi na mwimbaji maarufu Lovy Longomba, aliweza kuzifuata nyayo za uimbaji wa baba yake Vicky Longomba.

Baba yake huyo alikuwa mtunzi na mwimbaji wa kutegemewa katika bendi ya T.P.OK. Jazz, iliyokuwa ikiongozwa na Luambo Makiadi Lokanga La dju Pene Francois ‘Le Grand Mitre’.

Zipo familia zilizojaaliwa kuwa vipaji vya wacheza mpira wa miguu, nyavu, ngumi, na michezo mingine.

Mfano ni fimiliya ya wanadada wawili Wamarekani weusi, Serena na Vunus Williams, ambao ni mabingwa Kimataifa katika kucheza mpira wa Tennis.

Hapa nchini familia ya akina Uvuruge ilikuwa na watoto waliokuwa na vipaji vya kutunga nyimbo na kupiga muziki. Ndugu hao Jumanne, Stamili, Huluka na Maneno, walijijengea sifa tele katika muziki hapa nchini.

Familia ya akina Katwila, wapo akina Shabani, Adam na….

Aiha familia ya akina Kihwelu nayo ilikuwa ni ya vipaji vya kucheza mpira wa miguu, ambapo walikuwepo akina Mtwa, Jamhuri ‘Julo’ na ndugu zao wengine.Kwa upande wa ngumi, familia ya Matumla imerithisha kucheza mchezo wa ndondi takribani familiya nzima.

Katika makala hii ambayo inaizungumzia Familia ya Longomba, toka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Vicky Longomba ndiye aliye kuwa baba wa familia ya watoto wengi waliojaaliwa vipaji vingi vya muziki.

Huyo Mzee Vicky Longomba alikuwa mmoja kati ya wanamuziki waliokuwa waanzilishi wa bendi ya T.P.OK. Jazz iliyokuwa ikiongozwa na Franco Luanzo Makiadi.Ikumbukwe kwamba Vicky ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa bendi ya Lovy du Zaire, iliyotamba katika muziki nchini Kongo mwaka 1971.

Kwa kuwa familia hiyo ina wanamuziki wengi leo katika makala hii nitamzungumzia mmoja wa watoto wake Lovy Longomba.Wasifu wa mwanamuziki huyo unaelezea kwamba alianza muziki katika bendi ya Orchestra Macchi mwaka 1976, akiwa na mwimbaji mwenzake Dindo Yogo.

Aidha walikishirikiana na mpiga gitaa Nseka Huit, baadaye waliondoka katika bendi ya Macchi, wakaenda kuunda bendi yao ya Etumba. Baadhi ya wanamuziki waliokuwepo kwenye kundi hilo ni waimbaji akina Lofanga, Gaby Yau-Yau na Mukolo, aliyekuwa akiimba sauti ya kwanza.

Wanamuziki wengine waliokuwepo katika bendi hiyo ni pamoja Ngwaka na Huit Kilos, ambaye baadaye alikwenda kuwa nyota katika bendi ya Afrisa International ya Tabu Ley Rochereau.

Mwanamziki Ricardo aliondoka na kwenda katika bendi ya Lemvo in Makina Loca, iliyo na makao yake huko Los Angeles, nchini Marekani.Yaelezwa kwamba Lovy Longomba alikuwa na vipaji vya utunzi, uiimbaji mahiri pamoja na unenguaji wakti mwingine.

Alikuwa kaka wa wanamuziki machachari Awilo Longomba, ambaye kabla ya kuanza kutunga na kuimba, alikuwa mcharazaji hodari wa drums katika bendi mbalimbali nchini humo.

Lovy naye pia alikuwa baba wa familiya yenye watoto wanamuziki akiwemo binti yake aliyerithi uimbaji, Elly Longomba na mapacha Christian na Lovy ambao wote ni nyota katika muziki wa Hip-hop, wakimiliki Kampuni ya ‘Longambas’ huko Nairobi, nchini Kenya.

Baadaye Agosti 1978, Lovy aliicha bendi ya Orchestra Macchi, na kuamua kuondoka Kinshasa.Alitiga katika jiji la Nairobi nchini Kenya ambako alijiunga katika bendi ya Les Kinois.

Kwa kuwa ‘Kiu’ chake hakichakidhiwa, Lovy alidumu kwa miezi mitatu pekee,akatimkia katika bendi ya Boma Liwanza.Lakini huko nako hakudumu kwa kipindi kirefu kwa kuwa baada ya miezi sita, alitimka na kuiacha Boma Liwanza.

Lovy akaenda kujiunga na bendi ya Super Mazembe iliyokuwa ikiongozwa na Mutonkole Longwa Didos.Akiwa katika bendi hiyo alionesha uhodari wa kutumia sauti yake ilivyokuwa nyembemba na nyororo, ambayo ndiyo iliyopelekea kwa yeye kupachikwa jina bandia la ‘Ya Mama’. Sababu kubwa ni kwamba alikuwa na uwezo wa kuimba sauti ya juu ambayo alipashwa aimbe wanamke.

Katika bendi Super Mazembe alikutana na wanamuziki wenzake mahiri akina Joseph Okello Songa, Kasongo wa Kanema, Musa Olokwiso Mandala na Fataki Lokassa ‘Masumbuko ya duniya’ aliyekuwa ametokea katika bendi ya Les Kinois.

Baadhi ya nyimbo alizoachia katika bendi hiyo ni pamoja na ‘Lovy’, ‘Yo Mabe’, ‘Ndeko’, ‘Nanga’, ‘Mokano’ na ‘Elena’.

Sauti yake nyororo mara nyingi husikika katika baadhi ya nyimbo za bendi hiyo, akibwagiza akitamka “Vuta sigara SM, maana yake Super Mazembe…”

Hata hivyo umahiri wa kutunga na kuimba katika bendi hiyo, ilisababisha kuhitajika takribani na kila bendi.

Kwa mara nyingine tena Lovy aliondoka Super Mazembe mwaka 1981 akaenda kuimba katika bendi ya Shika Shika, iliyokuwa ikiongoza na Jimmy Monimambo, kwa kipindi cha miaka miwili.

Ndoto zake za kumiliki bendi yake zilitimia baada ya yeye na wanamuziki wenzake alipounda bendi yake Super Lovy ikiwa na Nembo ya AIT.

Lakini kwa kile alichokieleza ni kuepuka mkanganyiko na mvutano aliamua kutumia jina Bana Likasi wakati aliporekodi katika Kampuni ya Audio Productions Ltd.

Mnamo mwaka 1988 Lovy aliingia Tanzania katika jiji la Dar es Salaam na akapigia katika bendi Orchestra Afriso Ngoma.

Maisha ya nguli huyo yalikatishwa ghafla katika ajali iliyopelekea kufariki dunia nchini Tanzania mwaka 1996.

Mungu aiweke roho yake pahala pema peponi, amina.

ALPHA NA OMEGA YA DK. REMMY ONGALA

$
0
0
Na Kiyungi Moshy,Dar es Salaam.

Kama kuna mwanamuziki ambaye hawezi kusahaulika katika kumbukumbu za wapenda muziki, ni Dk. Remmy Ongalla.

Desemba 13, 2018 alitimiza miaka minane tangu afariki dunia usiku wa kuamkia Jumatatu Desemba 13, 2010 nyumbani kwake Sinza, jijini Dar es Salaam.

Ilikuwa ni siku ya majonzi kwa wapenzi wa muziki wa dansi hapa nchini, Afrika ya Mashariki na Ulimwenguni kwa ujumla baada ya kusikika kwa kifo chake.

Dk. Remmy aliwaacha wapenzi wake na wananchi kwa ujumla katika dimbwi la majonzi yasiyosahaulika kufuatia tungo za nyimbo zake zenye maudhui maridhawa.Nyimbo hizo hadi leo zinarindima katika vituo vingi vya redio hapa nchini hata nje ya mipaka yetu.

Yapo mambo kadhaa aliyoyafanya ambayo yanasababisha watu wengi kutokumsahau nguli huyu.

Dk. Remmy alikuwa wa kwanza kupata ujasiri wa kukemea ngono zembe, akatunga wimbo ‘Mambo kwa soksi’ Lakini jamii ikambeza kwamba wimbo huo haukuwa na maadili mema. Baadaye viongozi wa serikali, vyama na dini na wengine kwa ujumla walielewa nini alichokuwa akisema Dk. Remmy, wakaanza kuhubiri majukwaani tahadhari hiyo.

Alijipatia umaarufu katika jiji la Dar es Salaam hususan maeneo ya Sinza, kufuatia gari lake dogo ‘soloon’ ambalo popote lipitapo watu walilishangaa. Lilikiwa na maandishi nyuma ya gari hilo yakisema ‘ Baba yako analo’?

Dk. Remmy alizaliwa mwaka 1947 katika mkoa wa Kivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Familia yake iliishi katika eneo lililoitwa Kindu eneo ambalo halikuwa mbali sana kutoka mpakani na Tanzania.
Yaelezwa kwamba mara alipozaliwa, wazazi wake walimuita majina ya Ramadhani Mtoro Ongala.

Baba yake alikuwa mwanamuziki mashuhuri pia alikuwa mpiga ngoma kwa kutumia mkono na pia mbira.Remmy akiwa bado mchanga familia ilihamia katika mji wa Kisangani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Zipo habari kwamba kabla ya kuzaliwa kwake, mama yake alipata ujauzito mara mbili lakini kwa bahati mbaya kila alipojifungua, mtoto alifariki. Alipopata ujauzito mara ya tatu alienda kwa mganga wa kienyeji kumuomba ushauri afanye nini ili mtoto atakayezaliwa asiiage dunia pia.
Bila kusita mganga wa kienyeji akampa ushauri wake, akamwambia kwanza safari hii asiende kujifungulia hospitali bali akajifungulie maporini. Pia alipewa ushauri kwamba mtoto akishazaliwa asije akamkata nywele zake. Yote hayo yalitendeka.

Yasemekana Remmy alizaliwa akiwa tayari na meno mawili ya mbele, akaonekana kama mtoto wa ajabu.Kuzaliwa akiwa hivyo ikachukuliwa kama ishara ya baadaye kuja kuwa mganga wa kienyeji .

Ili kutimiza maelekezo ya mganga, Dk. Remmy hakuwahi kunyolewa nywele zake kwa miaka yote hadi alipokuja kuokoka akiwa hapa nchini Tanzania.

Mwenyewe aliwahi kusema kwamba mwanzoni alikuwa anajisikia aibu sana kwa kuwa na nywele ndefu namna ile. Lakini baadaye jina na taswira ya mfalme wa reggae ulimwenguni, hayati Bob Marley lilipopata umaarufu nchini Kongo, ndipo alipoupenda mtindo huo wa nywele kwani hata watu wengine pia walianza kuukubali na kuuonea fahari.

Baba yake ndiye aliyeanza kumfunza mambo ya muziki tangia akiwa mdogo kabisa. Jambo lililomfanya aamini kabisa kwamba kama jinsi ambavyo watu wengine wamezaliwa kuwa madaktari, wanasheria, waalimu, wakulima nk, yeye alizaliwa ili awe mwanamuziki.

Kwa bahati mbaya baba yake huyo alifariki dunia mwaka 1953, akamuacha Remmy akiwa na miaka sita.

Baadaye alianza shule ya msingi, lakini kutokana na ukosefu wa fedha na kwa sababu mama yake hakuweza kuendelea kumlipia karo za shule, Remmy ilibidi aache masomo shuleni hapo.

Ilipofika miaka ya 1960, Remmy tayari alikuwa ameshafuzu kupiga gitaa.

Mwaka mmoja baada ya kifo cha Baba yake mzazi, mwaka uliofuatia wa 1954, ulikuwa si mzuri tena kwa Remmy. Alkipata pigo la kufiwa na mama yake mzazi jambo ambalo lilimuacha na mzigo wa kuwalea wadogo zake kwani yeye sasa ndio alikuwa mkubwa katika familia licha ya umri wake mdogo.

Bila elimu na ujuzi mwingine wowote, alilazimika kuanza rasmi kujitafutia riziki kupitia muziki. Ujuzi wake wa kupiga gitaa uliongezeka kwa kasi ya ajabu kitu ambacho kilimuwezesha kutumbuiza kwa kupiga ngoma na gitaa katika hoteli na sehemu mbalimbali nchini ya Kongo, akiwa na kundi lake lilokuwa limesheheni vijana wenzake lililoitwa ‘Bantu Success’.

Kwa miongo kadhaa iliyofuatia Dk. Remmy Ongala alizunguka katika sehemu mbalimbali za Kongo akiambatana na bendi kadhaa maarufu za wakati huo nchini Kongo zikiwemo Success Muachana na ile ya Grand Mickey Jazz.

Japokuwa kwa ujumla Dk. Remmy alijifunza mwenyewe kupiga gitaa, lakini aliwahi kukiri kwamba muziki wa kutoka nchini Cuba ambao wakati huo ulikuwa unaanza kujipatia umaarufu barani Afrika, ulimsaidia katika kupata mitindo kipekee katika upigaji gitaa.

Kwa upande wa uimbaji anasema uimbaji wa Joseph Kabasele ‘Grand Kale’ na ule wa Franco Lwambo Makiadi ulimsaidia kupata mitindo yake ya uimbaji kama alivyozoeleka kusikia enzi za uhai wake.

Mwaka 1978 Remmy aliingia jijini Dar es Salaam baada ya kuitwa na mjomba wake mzee Kitenzogu Makassy ili aje ajiunge na bendi maarufu ya wakati huo ya Orchestra Makassy, iliyokuwa chini ya uongozi wa mjomba wake huyo.

Huo ukawa ndiyo mwanzo wa maisha ya Dk. Remmy nchini Tanzania. Akiwa na bendi ya Orchestra Makassy, alitunga wimbo wake wa kwanza uliojulikana kama ‘Siku ya Kufa’, wimbo ambao aliuandika kumkumbuka rafiki yake aliyefariki dunia. Wimbo huo pamoja na ule wa Athumani zilianza kumpatia umaarufu mkubwa na kujulikana kwa haraka hapa nchini.

Hata hivyo mzee Makassy baadaye aliamua kuihamishia bendi yake nchini Kenya. Kitendo hicho cha mjomba wake kilichomfanya Dk. Remmy kwenda kujiunga na bendi ya Matimila baada ya kudumu kwa katika bendi ya Orchestra Makassy kwa takriban miaka mitatu hivi.

Kujiunga kwa Remmy katika bendi ya Matimila, kulimuongezea umaarufu zaid katika anga za muziki nchini Tanzania wakati huo. Jina la bendi hiyo ya Matimila lilitokana na jina la kijiji kimoja kilichoko kusini mwa Tanzania.

Chini ya uongozi wake Dk. Remmy aliisuka upya bendi hiyo na kuibadilisha majina ikaitwa Orchestra Super Matimila.

Miaka iliyofuatia Watanzania walishuhudia umaarufu wa Remmy ukiongezeka kutokana na mashairi ya nyimbo zake ambayo yaliegemea katika kuzungumzia mambo halisi ya kijamii kama vile umasikini, afya, siasa , majanga ya Ukimwi nk.

Mafanikio ya Remmy na kundi lake zima la Orchestra Super Matimila hayakuishia nchini Tanzania kwani katika miaka ya mwishoni ya 1980 walianza kujipatia umaarufu nje ya mipaka ya Tanzania na Afrika hadi Ulaya.

Dk.Remmy Ongala aliwahi kusema kwamba kupata mialiko ya nje lilikuja kama mchezo tu. Kasseti yenye nyimbo zao ilichukuliwa na rafiki yake mmoja mzungu aliyekuwa akiondoka nchini Tanzania kurejea kwao Uingereza.

Rafiki yake huyo alipofika huko aliwapatia jamaa wa WOMAD (World of Music, Arts and Dance) Shirika linalopandisha chati wanamuziki na wasanii mbalimbali kutoka katika nchi za dunia ya tatu.

WOMAD walivutiwa na nyimbo zao, hivyo kuwapa mwaliko kushiriki katika maonyesho yao Barani Ulaya ya mwaka 1988.

Baada ya kurudi kutoka Ulaya bendi ya Super Matimila ilitoa album yenye jina la ‘Nalilia Mwana’ ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo zao zilikuwemo nyimbo zilizopendwa sana kama vile ‘Ndumila Kuwili’ na ‘Mnyonge Hana Haki’

Mwaka 1989 Super Matimila walirudi tena Ulaya kufuatia mwaliko mwingine wa WOMAD. Ni wakati huo huo ambapo walipata nafasi ya kurekodi kwenye studio ya kisasa zaidi ya Stud Real World Studios, ambayo ilikuwa inamilikiwa na mwanamuziki maarufu aitwaye Peter Gabriel.

Dk. Remmy aliwahi kufafanua kuwa wimbo maarufu ya ‘Kipenda roho’ aliuimba mahsusi kwa ajili ya mkewe ambaye ni ‘mzungu’ Mwingereza ambaye wakati huo tayari walikuwa wameshazaa naye watoto watatu.

Mwaka 1990, Remmy na bendi yake ya Super Matimila walirejea tena katika studio za Real World ambako walirekodi album nyingine yenye nembo ya ‘Mambo’ .

Albam hiyo ilikuwa na nyimbo kama hiyo ya ‘Mambo’ ambayo aliimba kwa lugha ya kiingereza na kuweza kukidhi kiu ya wapenzi wake wasiojua Kiswahili. Zingine ni pamoja na ‘No money, no life’ na ‘One World’.

Umaarufu wake ulizidi kung’ara mwaka 1990 alipoachia wimbo wa ‘Mambo kwa soksi’ ingawa baadhi ya watu waliupinga kwa kusema kwamba haukuwa na maadili mema kwa jamii, ingawa kimsingi alikuwa anawaasa watu hususani vijana kutumia kondomu ili kuepukana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

Akiwa Super Matimila Dk. Remmy alitoka na nyimbo nyingi zikiwemo za ‘Bibi wa mwenziyo’, ‘Kipenda roho’, ‘Asili ya muziki’ na ‘Ngalula’. Zingine ni pamoja na ‘Mwanza’, ‘Mama nalia’, ‘Harusi’, ‘Hamisa’, ‘Mnyonge hana haki’, ‘Ndumila kuwili’ na ‘Mataka yote’ ambazo zilimuongezea sifa kubwa Dk. Remmy kufuatia maudhui yaliyokuwa yakikidhi jamii.

Baadaye Dk. Remmy Ongala akaanza kusumbuliwa na maradhi ya Kisukari iliyompelekea kuamua kuachana na muziki wa dansi kwa madai ya kwamba umejaa mambo mengi ya kishetani.

Remmy akaokoka, akatubudu dhambi zake na akaanza kupiga muziki akimuimbia Bwana.Kabla ya kifo chake Dk. Remmy alitoa albamu yake ya Injili aliyooiita ‘Kwa Yesu kuna furaha’.

Kabla ya kifo chake, Remmy alikuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha albamu yake ya pili, lakini mungu akampenda sana usiku wa kuamkia Jumatatu ya Desemba 13, 2010 nyumbani kwake Sinza.

Eneo hilo alilokuwa akiishi lilipewa jina la ‘Sinza kwa Remmy’ kabla ya kifo chake kufuatia umaarufu wake.

Mungu aiweke roho yake pahala pema peponi, Amina.
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba:



0784331200,

WASANII WAUNGANA KUMSAIDIA HAMIS ALIYEVIMBA MIGUU,WAISHUKURU SERIKALI

$
0
0
WASANII wa fani mbalimbali nchini wameamua kumsaidia kijana Hamisi Salum anayesumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu kwa kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili ili apate matibabu kwani wanaamini atapona na kutimiza ndoto zake. 

Akizungumza jana Machi 12, 2019 kwa niaba ya wasanii wenzake, Msanii maarufu nchini Steve Nyerere amesema wanamatumaini makubwa Hamis atapona, kikubwa ni Watanzania kumuombea kwa Mungu. 

Amefafanua Hamis alishapelekwa nchini India kwa matibabu na kisha akarejea nyumbani Tanzania na baadae tena alipelekwa Muhimbili. 

Ameongeza wasanii katika kuhakikisha Hamis anapona na kutimiza ndoto zake wameamua kumfuata tena nyumbani kwao na kisha kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili akatibiwe. 

Steve Nyerere amesema baada ya wao kupaza sauti zao Rais Dk.John Magufuli amesikia na kwa kupitia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wameamua kumsaidia. 

"Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kwa kujali wanyonge, wasanii tumepaza sauti zetu kuhakikisha Hamis anasaidiwa na Rais wetu amesikia na leo amepokelewa Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu.Pia tunamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa jitihada zake za kumsaidia Hamis,"amesema Steve Nyerere. 

Amesisitiza kuna kila sababu ya kumsaidia Hamis kwani bado anayo matumaini na vijana wenzake wakiwamo wao wasanii wamejikusanya kumsaidia. 

Kuhusu gharama ya matibabu,Steve Nyerere amesema bado hajafahamu gharama halisi itakayotumika katika matibabu ya kijana huyo lakini wanachoamini nafasi ya kupona ipo, hivyo kikubwa ni watanzania kumsaidia. 

Ametoa onyo kuwa ugonjwa wa Hamis usitumike vibaya kwani wanaweza kujitokeza watu na wakatoa namba za simu ili wawe wanatumiwa fedha kumbe ni matapeli."Hamis anahitaji kusaidiwa na si kutumika kibiashara." 
Wasanii wakimsaidia kijana Hamis Salumu mwenye matatizo ya kuvimba miguu kumuingiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu baada ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kujitolea kumpatia matibabu kwa kupitia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Wasanii wakiongozwa na Steve Nyerere. 
Wasanii wakiwa nje ya Chumba cha wagonjwa wa dharula katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kushuhudia kijana Hamis Salumu akifikishwa kwa ajili ya matibabu. 
Wasanii wakimsanidia Kijana Hamis Salum kumtoa nyumbani kwao Temeke jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelekea hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar.

MAHAKAMA YA RUFANI TANZANIA YASIKILIZA MASHAURI MANANE YA MAHAKAMA KUU YA MBEYA KUPITIA VIDEO CONFERENCE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

 Mahakama ya Rufani Tanzania,   Machi 12, 2019  imesikiliza mashauri manane ya Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kwa kupitia mfumo wa video conference.

Rufaa hizo zimesikilizwa kwa mara ya kwanza kwa njia hiyo katika Kituo cha Mafunzo kilichopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na Mahakama ya Mbeya.,   

Rufaa zilizosikilizwa ni za mkoa mbeya na Rukwa ambapo miongoni mwa rufaa hizo ni ya Venance Kazuri dhidi ya Eldard Sospeter  pamoja na Agness Sanga dhidi ya Among Halinga na Peter Haonga ambazo zimesikilizwa mbele ya Jaji Jacobs Mwambegele.

Pia rufaa namba 38/2018 ya aliyekuwa Askari polisi namba F 5842 DC, Maduhu dhidi ya jamhuri na  namba 1/2019 ya Charles Kalunga na wenzake dhidi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) mbele ya Jaji Rehema Mkuye.

Rufaa nyingine ni pamoja na rufaa namba 3/2018 ya Festo Sodi dhidi ya Ihombe Village Council na kesi namba 100/2018 ya Osward Mruma dhidi ya Mbeya City na rufaa namba 2/2018 ya Ismail Shaban dhidi ya Jamhuri zilizosikilizwa mbele ya Jaji Sivangirwa Mwangesi.

Pamoja na rufaa ya Faman Investment (T) Ltd dhidi ya Dk Anthony Nsonjo na wenzake iliyosikilizwa mbele ya Jaji Gerald Ndika.

Akizungumza  baada ya  usikilizwaji wa mashauri hayo, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Elizabeth Mkwizu amesema, usikilizwaji was mashauri kwa njia ya video conference inapunguza gharama na kwamba inalenga utoaji wa haki kwa wakati.

Amesema, garama inayotumika kuendesha video conference ni Sh 140,000 kwa siku ambayo ni tofauti na majaji kusafiri na watumishi wao kwenda Mbeya kwa ajili ya kusikiliza mashauri hayo.

Ameongeza kuwa faida kubwa ya mfumo huu husaidia kupunguza gharama kwani ili majaji waweze kwenda Mbeya kusikiliza mashauri inawapasa kulipia gharama kubwa za malazi yao pamoja na watumishi wao wanaoongozana nao lakini mfumo huo unatumia Sh 70,000 kwa Kisutu na 70,000 kwa Mbeya ili kukamilisha usikilizwaji huo.

Mkwizu amesisitiza kuwa mashauri yote ya Mbeya na Sumbawanga walitakiwa wafuatwe lakini kwa mfumo huo wanatimiza malengo ya mahakama ya utoaji wa haji kwa wote na kwa wakati.

Moja ya rufaa iliyosikilizwa ni ya Sanga ambaye yupo Mbeya na hakuwa na Wakili kupitia video conference aliiomba mahakama (Jaji ambaye alikuwa Kisutu) kumuongezea muda wa kufungua ili kukata rufaa dhidi ya Halinga na Haonga ambao wanadaiwa kuuza nyumba ya urithi.

Sanga amedai sababu ya kuongezewa muda ni baada ya Mahakama Kuu Kanda hiyo kumkatalia kuomba kesi kusikilizwa nje ya muda. Amedai, alicheleweshewa kupewa nakala ya hukumu ambayo ilitoka Julai 14, 2017 na kupata nakala hizo Agosti 4, 2017 hivyo alichelewa kufungua kesi.

"Kila mtu anatakiwa aridhike na kile alichokitafuta kwa juhudi zake na isiliwe na mtu mwingine hivyo, naomba nipatiwe haki hiyo," alidai Sanga.

Hata hivyo, wadaiwa hao waliiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo kwa sababu katika hati ya kiapo mdai hakueleza sababu ya kuchelewa kukata rufaa kuwa ni kucheleweshewa hukumu lakini alichoeleza ni kwamba alikuwa mgonjwa.

"Tunaomba mahakama itupilie mbali maombi haya kwa sababu mdai ni muongo kwani alichoeleza kwenye hati ya kiapo ni tofauti na anachoeleza," walidai.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Mwambegele alisema atapitia hoja zote na atatoa uamuzi kuhusu shauri hilo na kwamba watajulishwa  tarehe ya uamuzi.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images