Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live

BENKI YA CRDB TAWI LA QUALITY CENTER LILIVYOSHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NA WATEJA WAKE

0
0

Meneja Mikopo kwa Wajasiriamali Wanawake wa Benki ya CRDB, Rehema Shambwe, akitoa mada katika kongamano la wanawake jijini Dar es Salaam, kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo ‘Malkia Account’ wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Kongamano hilo limefanyika chini ya uratibu wa Chama cha Wahandisi Wanawake. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akipata maelezo alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika kongamano la wanawake jijini Dar es Salaam, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akipata maelezo alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika kongamano la wanawake jijini Dar es Salaam, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akiagana na Meneja Mikopo kwa Wajasiriamali Wanawake wa Benki ya CRDB, Rehema Shambwe.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akiagana na Ofisa wa Benki ya CRDB anayehudumia wateja Wadogo na wa Kati katika tawi la Pugu Road, Amir Konji.
Ofisa wa Benki ya CRDB anayehudumia wateja wadogo na wa Kati, Amir Konji (kushoto), akitoa maelezo kwa mmjoa wa wateja waliofika katika banda lao.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja.
Meneja Maendeleo ya Biashara Benki ya CRDB tawi la Pugu Road, Rehema Njavike, akitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda lao.
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB tawi la Pugu Road, Neema Daniel, akimkabidhi kadi mteja.
Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika kongamano la wanawake.
Wafanyakazi wakilishwa keki.
Mmoja wa wateja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Farida Nassoro, akilishwa keki na Meneja wa tawi hilo, Clementina Kinabo. 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo, akimlisha keki mmoja wa wateja wa benki hiyo, Leticia Mbunda, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika tawi hilo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Mmoja wa wateja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center Farida Nassoro akikata keki wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo benki hiyo ilisherehekea na wateja wake. 
Mteja wa Benki ya CRDB ambaye ni mmiliki wa Farida Hardware, Farida Nassoro, akijiandaa kukata keki. 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo, akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika tawi hilo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center wakiwa katika picha pamoja. Katikati ni Meneja wa tawi hjilo, Clementina Kinabo. 

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center wakiwa katika picha ya pamoja. 

MAMA ASAHAU KICHANGA CHAKE UWANJA WA NDEGE, AKIKUMBUKA AKIWA HEWANI, RUBANI AGEUZA KUKIRUDIA

0
0
Na Sultani Kipingo
Aghalabu ndege inapopata dharura angani, waongoza ndege waliopo ardhini hawasiti kuiruhusu kurudi uwanjani, wakati mwingine kutokana na kusahaulika kitu. Majuzi kati katika uwanja wa Mflamu Abdulazizi wa Saudi Arabia mama mmoja alisahau motto wake mchanga hapo uwanjani.


Yaani huyo mama, aliyekuwa anasafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Saudi Arabia, alisahau kichanga chake kwenye eneo la kusubiria la wanaoondoka. Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News, japokuwa yeye ni mzazi, mama huyo alipanda hiyo ndege akiwa hana shaka na jambo lolote.


Ni wakati ndege ikiwa imeshapaa angani ndipo akakumbuka kwamba kaacha kichanga uwanjani! Na mara tu baada ya kugundua hilo, akawaarifu wahudumu wa ndege kwamba kasahau motto mchanga uwanjani, na kumfanya rubani wa Ndege namba SV832 kutoka mji mkuu wa Saudi Arabi, Jeddah, ikielekea Kuala Lumpur, Malaysia, irudi uwanjani.


Tukio hilo lilishangaza kila mtu wakiwemo wahudumu wa ndege, abiria wenzake na hata waongoza ndege uwanjani Jeddah. Video inayoonesha rubani wa ndege hiyo akiomba ruhusa kurudi uwanjani kumchukua motto mchanga aliyesahaulika imeshika kazi mitandaoni huku wengi wakijiuliza mtu unasahau vipi motto wako?


“Ndege hii inaomba ruhusa kurudi…kuna abiria kasahau kichanga chake uwanjani, maskini”, rubani anasikika katika video hiyo.


Waongoza ndege walichukua dakika kadhaa kufikiria itifaki ipi itumike katika kuruhusu ndege kurejea uwanjani kwa sababu kama hiyo.

“Haya rudi tena getini. Hili ni jambo jipya kwetu!” anasema mmoja wa waongoza ndege. Hata hivyo ndege ikatua na mama akaungana na kichanga chake na kuendelea na safari baadaye.


 The ATC executives spent several minutes figuring out the protocol to be observed during such incidents. “Ok, head back to the gate. This is totally a new one for us!” says one of the ATC operator. The woman was finally reunited with her baby at the airport. 





Meya Mwita. Jiji la Dar kuomba zabuni ya kutoa huduma ya usafiri Gerezani, Mbagala

0
0
HALMASHAURI ya jiji la Dar es salaam imesema kuwa imepanga kuomba zabuni ya utoaji huduma ya usafirishaji abiria kupitia mabasi yaendayo haraka kutoka Kariakoo Gerezani hadi Mbagala.

Kauli hiyo imetolewa jijini hapa leo na Mstahiki Meya Isaya Mwita mara baada ya kumalizika kwa kikoa cha baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee.

Meya Mwita amesema kuwa tayari Wakala wa mabasi yaendayo haraka wameshatangaza zabuni ya ujenzi wa awamu ya pili ya miundombinu ya mabasi itakayoanzia Kegerezani hadi Mbagala hivyo kama jiji limeona kunahaja ya kuomba zabuni hiyo ilikutoa huduma hiyo ya usafiri.

Amefafanua kuwa jiji linania ya kuomba zabuni hiyo kutokana na kuwa wanaweza kutoa huduma hiyo ili kusaidia adha ya foleni iliyopo kwa sasa katika maeneo ya Mbagala.

“ Tunatarajia kuomba zabuni ya kutoa huduma ya kusafirisha abiria hapa jijini ,iwapo tutakubaliwa basi kama jiji nalo litakuwa miongoni mwa watoa huduma hiyo” amesema Meya Mwita.

Tunajua kwamba pesa tunazo, nauwezo wakutoa huduma hiyo tunao,kwahiyo wakazi wa jijini hapa wafahamu kuwa kama tutakubaliwa tutatoa huduma hiyo, ndio mana leo nimewaeleza madiwani kwamba uliangalie jambo hili kwa umuhimu wake ilitujiandae” ameongeza.

Katika hatua nyingine baraza hilo limepitisha kwa kauli moja taarifa mbalimbali za utendaji na miradi mbalimbali zilizotolewa na wenyeviti wa kamati mbalimbalimbali za jiji.

Imetolewa leo Machi 12 na Christina Mwagala .Afisa habari ofisi ya meya wa jiji.

RC MWANRY AZINDUA JUKWAA LA NAWEZA MKOANI TABORA

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry(kushoto) akizindua jukwaa la “NAWEZA” litakalolenga kutoa elima ya Afya kwa wananchi hususani watu wazima.Uzinduzi huo umefanyika leo mjini Tabora.Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa, Roberth Makungu na Mkuu wa Wilaya Igunga, John Mwaipopo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry(kulia) akikata utepe kuashilia uzinduzi wa jukwaa la “NAWEZA” litakalolenga kutoa elima ya Afya kwa wananchi hususani watu wazima.Uzinduzi huo umefanyika leo mjini Tabora.Kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa, Honoratha Rutatinisibwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akizindua jukwaa la “NAWEZA” litakalolenga kutoa elima ya Afya kwa wananchi hususani watu wazima.Uzinduzi huo umefanyika leo mjini Tabora.

NIC Bank Tanzania yaadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutoa msaada katika taasisi ya saratani ocean road

0
0

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania, Margaret Karume, akihojiwa na waandishi wa habari.

Afisa Ustawi wa ORCI , Malkiory Niniko akipokea msaada kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania, Margaret Karume.
Afisa Ustawi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Malkiory Niniko akitoa shukrani.

wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja.



Benki ya NIC Tanzania yatoa msaada katika Taasisi ya Saratini ya Ocean Road(ORCI)

Dar es Salaam, 8th Machi,2019, Benki ya NIC Tanzania leo imeadhimisha siku ya wanawake duniani inayosherehekewa kote duniani tarehe 8 Machi kwa kutembelea na kutoa msaada katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road(ORCI).

Akiongea katika tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania, Margaret Karume alisema, “Siku ya wanawake duniani ni siku kubwa katika kalenda ya wafanyakazi wa benki hii, kwa ajili ya kusaidia na kuyainua maisha ya wanawake wasiojiweza katika jamii iliyotuzunguka. Saratani ni ugonjwa ambao umeathiri na unaendelea kuathiri watanzania wengi sana, Zaidi kama haijagundulika mapema”.

Aliongeza kwa kusema, kila mmoja wetu ananafasi ya kucheza katika jamii, ambapo dunia inahitaji usawa. Katika uamuzi wetu wa kutoa msaada kwa wagonjwa wa saratani, tujenga usawa kwa ajili yakuwa na dunia iliyobora.

“Kama Benki, tumejikita kuhakikisha tunatoa mchango chanya, kwa jamii tunazo endesha shughli zetu. Ndio sababu kusaidia Taasisi kama hizi ipo katika mkakati maalum wa kusaidia jamii,” alisema Karume.

Akiongea katika hafla hiyo Afisa Ustaei wa Taasisi hiyo Malkiory Niniko alisema, “Tunaipongeza Benki ya NIC Tanzania, kwa kutoa msaada huu, na tunawaomba wadau mbalimbali waige mfano huu adhimu, na Taasisi inakaribisha usaidizi kutoka idara mbalimbali kwa sababu haiwezi kufanikisha malengo yake yote kwa mkupuo”

WANANCHI WAJITOLEA KUWEKA ALAMA ZA BARABARANI

0
0
Na Ahmed Mahmoud,Arusha.

Wananchi wa kata ya Lemara eneo la Nanenane jijini Arusha wameamua kujitolea kwa hali na mali kuweka alama za vivuko viwili vya waenda kwa miguu katika barabara inayoingia katikati ya jiji kwenye eneo linalodaiwa kutokea ajali za mara kwa mara na kusababisha watu wasiyo na hatia kupoteza maisha .

Wanahabari walifika kwenye eneo la nanenane na kushuhudia wakazi wa eneo hilo wakichangishana fedha kwa ajili na kuweka alama hizo huku mafundi wakiendelea na kazi ya kuweka alama hizo ambazo zinatajwa kua ni suluhisho la kuzuia ajali kutokea katika eneo hilo.

Wakazi wa kata hiyo wakizungumzia hatua waliochukua ya kujitolea kwa michango yao wakishirikiana na diwani wao nibaada ya eneo hilo kukidhiri ajali za mara kwa mara ambazo wakati mwingine zinaepukika.

Alfredy Maulid na Pascal Silvery ni wakazi wa kata ya lemara walisema upatikanaji wa kivuko hicho ni mkombozi mkubwa hasa watoto wa shule kuvuka kwa amani kwakua kipindi cha nyuma hali ilikua mbaya ya watu kupoteza maisha kwa kugongwa na magari.

Pascal alisema kuwa wanaamini kuwepo kwa alama hizo kutasaidia wanaovuka waweze kuvuka salama hususan wanafunzi ambao hupata adha kubwa wanapotaka kuvuka barabara.

Diwani wa kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha alisema kuwa ameungana na wananchi kutokana na umuhimu wa eneo hilo hawezi kuvumilia kuona watu wakiumia wakati wananchi wanaweza kujitoa na kufanikisha jambo hilo .

“Ushirikiano kati ya Wananchi na Viongozi wao umeweza kufanikisha jambo hili muhimu ,tayari tulishatoa taarifa uongozi wa Jiji umetoa ridhaa kwa wananchi kufanya jambo hili hivyo lina Baraka zote za jiji” Alisema Profesa Mosha

Dereva wa magari Johnson Mlay alisema hatua iliyofanywa na wananchi itawasaidia kufuata sheria ili kuepusha ajali zisizo za lazima.
Mafundi wakiweka alama za vivuko barabarani katika eneo la Nane nane jijini Arusha baada ya Wananchi kata ya Lemara kuchangia zoezi hilo ambalo limefanyika kwa kushirikiana na Wataalamu kutoka Jiji la Arusha ili kuzuia ajali za barabarani hususan kwa wanaopita kwa miguu. Picha na Mahmoud Ahmad Arusha

WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI

0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer ambaye amemweleza Waziri Biteko kuhusu ujio wa kampuni zipatazo 3 kutoka mataifa mbalimbali zenye nia ya kuwekeza katika sekta ya madini.

Dkt. Gollmer amesema kampuni hizo zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini hususan katika masuala ya utafiti na uchimbaji wa madini kutokana na ushawishi unaofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi  ambaye amekuwa akihamasisha watu wa mataifa mbalimbali nchini humo kuwekeza nchini.

Pia, ameeleza kwamba, kampuni hizo hazina shaka ya kuwekeza Tanzania kutokana na mazingira tulivu ya kisisasa yaliyopo nchini pamoja na utajiri wa rasilimali madini ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko amemweleza Dkt. Gollmer kuwa kikao hicho ni muhimu na kwamba milango kwa ajili ya wawekezaji wenye dhamira ya dhati ya kuwekeza nchini iko wazi na kuongeza kuwa, kama wizara inaratajia kukutana na kampuni hizo.

Wengine walioshiriki kikao hicho ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mkurugeni wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal na Katibu wa Waziri Kungulu Kasongi.
 Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer.
Kamishna wa Madini David Mulabwa akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Waziri wa Madini Doto Biteko na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Anayefuatilia ni Mkurugenzi wa Ssera na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal.
Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Kulia wanaofuatilia ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na Katibu wa Waziri, Kungulu Kasongi.

MKUTANO WA IAEA WAANZA JIJINI ARUSHA

0
0
Naibu waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia William Olenasha akizungumza na waandishi wa habari leo alipohudhuria mkutano wa waratibu Kimataifa NGO'Swa nchi mbalimbali zinazotekeleza miradi kwa ushirikiano wa IAEC. Picha zote na Vero Ignatus

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki nchi profesa Lazaro Busagala akizungumza  na waandishi wa habari katika mkutano wa waratibu wa nchi mbalimbali zinazotekeleza miradi kwa ishirikiano wa IAEC

Mkurugenzi  wa Afrika katika Shirika la International Atomic Agency Profesa Shaukat Abdulrazak akizungumza na waandishi wa habari
Naibu Waziri Elimu Sayansi na Teknolojia Willium Olenasha akizungumza katika mkutano wa waratibu wa nchi mbalimbali zinazotekeleza miradi kwa ishirikiano wa IAEC

Washiriki wa mkutano wa waratibu wa nchi mbalimbali zinazotekeleza miradi kwa ishirikiano wa kama wanavyoonekana pichani
Washiriki wa mkutano huo kutoka Nigeria, Namibia, Morocco
Washiriki kutoka Libya, Kenya 
Washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Central African Republic, Congo
Picha ya pamoja ya mkutano wa waratibu wa nchi mbalimbali zinazotekeleza miradi kwa ishirikiano wa IAEC


Na. Vero Ignatus, Arusha.



Mkutano wa wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za atomu International Atomic Energy Agency IAEA kanda ya Afrika  umeanza rasmi Mkoani Arusha.



Taarifa inasema kuwa lengo la Mkutano huo ni kujadili namna ya kuboresha ushirikiano katika kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Matumizi salama ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia katika nchi wanachama.



Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolijia William Ole Nasha amesema Tanzania imekuwa ikishiriki katika Miradi ya kudhibiti na kuhamasisha Matumizi Salama ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia zinazofadhiliwa na Shirika hilo la IAEA.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Atomu Tanzania Profesa Lazaro Busagala amesema Tanzania imendelea  kunufaika na Miradi mbalimbali ambayo imesaidia  kuboresha  sekta ya Kilimo,Afya, Mifugo, Maji, Rasilimali watu  nishati na Viwanda kutoka Shirika hilo.

Aidha amesema kuwa Miradi hiyo inayo tekelezwa sasa iko Saba na inathamani ya zidi ya bilioni 9.


Mkurugenzi huyo amesema kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 Shirika la IAEA liliisaidia Tanzania kwa kuipatia vifaa vya uchunguzi na Tiba ya Maradhi ya Saratani.



Amesema vifaa hivyo  vimefungwa  katika hospital ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, na Hospital ya Ocen Road pamoja na vifaa vya Maabara vilivyo gharimu billion 6.2.



Hata hivyi Mkutano umehudhuliwa  na washiriki 46 Kutoka nchi 46 ambao ni wanachama wa Shirika la kimataifa la Nguvu za Atom na unatarijia kuisha tarehe 15 mwezi huu wa Tatu.

HOTEL YA ILBORU SAFARI YATEKETEA KWA MOTO

0
0
Na Ahmed Mahmoud,Arusha
Hoteli ya Kitalii ya Ilboru Safari Lodge inayomilikiwa na kanali Mstaafu wa Jwtz Mika Metil iliyopo Ilboru wilaya ya Arumeru, Mkoani hapa imeteketea kwa Moto uliozuka Mapema Leo na kuteketeza vitu vyote vilivyokuwemo ndani ikiwemo kisanduku(Selfu) cha kuhifadhia fedha kinachodaiwa kuhifadhi mamilioni ya fedha.

Tukio hilo limetokea majira ya Saa 20.30 asubuhi huku chanzo cha Moto huo kikiwa bado hakijajulikana na taarifa za awali zinadai ni kutokana na hitilafu ya umeme. Moto huo pia umetetekeza Nyumba mbili za kulala wageni ikiwemo ofisi ya Mkurugenzi wa hotel hiyo ambaye ni Raia wa Kigeni.

Akizungumzia tukio hilo ,Kanali Metil pamoja na  kusikitishwa na tukio hilo Alisema kwa sasa hamiliki hotel hiyo kwani ameikodisha miaka 10 iliyopita kwa mwekezaji ambaye ni raia wa Kigeni.

Kwa upande wake meneja wa hotel hiyo,Eddy Jack amesema kuwa moto huo ulizuka leo majira ya asubuhi ambapo waliwasiliana na jeshi la zima moto na wokozi ambao walifika eneo la tukio na kukuta sehemu kubwa ya mali zimeteketea kiasi cha kutookoa chochote.

Hata hivyo alieleza kuwa jeshi la zima moto na uokozi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na kampuni binafsi ya ulinzi walifanikiwa kuimarisha ulinzi na kufanikiwa kuzima moto huo ingawa ulishateketeza sehemu kubwa samani za ndani na majengo.

Hata hivyo utata umeibuka katika tukio hilo la kuungua kwa hotel mara baada ya kuibuka taarifa zinazodai kufanyika hujuma juu ya tukio hilo. Tukio hilo limeibua utata mkubwa Mara baada ya Mamilioni ya Fedha zikiwemo za kigeni zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye kisanduku  'Selfu'kutoonekana.

Licha ya kisanduki hicho kuungua na Moto lakini ilipofunguliwa haikukutwa na kiasi chochote cha fedha huku raia huyo wa Kigeni Anneliese Metil ambaye anayeendesha hotel hiyo kwa sasa, akiangua kilio akidai kuhujumiwa na ataeleza kila kitu kilichofanyika Mara atakapokuwa sawa kiakili.

Ameeleza kuwa wao kama wafanyakazi hawana mamlaka ya kuingia ndani hivyo kutoweza kusema chochote kama kiasi kilichopotea au thamani ya Mali Zaidi kueleza tukio na uongozi utatoa taarifa kwenu baada ya kutoa tathmini ya Mali na majengo vilivyoteketea.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha,Jonathan Shanna alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa thamani halisi ya Mali zilizoteketea hakijajulikana na Polisi wanaendelea na uchunguzi.

Alifafanua kuwa katika tukio hilo nyumba mbili za kuishi zimeteketea kabisa huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa bado hakijulikani na kwamba uchunguzi unaendelea na hakuna aliyejeruhiwa na wala hakuna anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
 Sehemu ya vyumba vya kulala wageni kwenye hotel ya Iboru Safari lodge baada ya kuzimwa Moto vikiwa vimeteketea. Picha zote na Mahmoud Ahmad Arusha. 
 Jengo la hotel ya Iboru Safari lodge likiwa limeteketa baada ya kuzuka Kwa Moto majira ya saa mbili na nusu asubuhi leo wilayani Arumeru .
 Sehemu ya mabaki ya Kishubaka cha kuhifadhia fedha selfu kikiwa kitupu mara baada ya kufunguliwa na kuzua taharuki Kwa mmiliki wa hotel hiyo Raia wa kigeni Anneslies Metil.

BALOZI WA JAPANI NCHINI TANZANIA ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof. Audax Mabula akimweleza jambo Balozi wa Japani Nchini Tanzania, Shinichi Goto aliye mbele yake alipotembelea Makumbusho ya Taifa (leo asubuhi) Mtaa wa Shabani Robert, jijini Dar es Salaam, wengine ni wasaidizi wa Balozi wa Japani. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Bi Flower Manase (wa kwanza kushoto) akimweleza Balozi wa Japani Nchini Tanzania, Goto jambo alipotembelea ofisini kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa leo. Kulia kwa Balozi ni Msaidizi wake Bi Brayan Nassoro Salle.
 Balozi wa Japani nchini Tanzania Shinichi Goto (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof. Audax Mabula na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Bi Flower Manase wakifurahia kalanda ya mwaka 2019 iliyotolewa kama zawadi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho na Balozi wa Japani.
  Balozi wa Japani nchini Tanzania Shinichi Goto  akiangalia kompyuta za watoto alipotembelea maktaba ya watoto, iliyopo Makumbusho ya Taifa. Kushoto kwake ni Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa Anamery Bagenyi.
  Balozi wa Japani nchini Shinichi Goto akisiliza maelezo kuhusu maktaba ya watoto kutoka kwa Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa, Anamary Bagenyi alipotembelea Makumbusho ya Taifa (leo asubuhi).
 Balozi wa Japani nchini, Shinichi Goto akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Amandus Kweka kuhusiania na chimbuko la mwanadamu katika ukumbi wa maonesho wa Chimbuko la Mwanadamu, Makumbusho ya Taifa.
Picha na Maelezo na Joyce Mkinga wa Makumbusho ya Taifa

BEYONCE ALETA GUMZO DUNIAN

0
0

Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam


Msanii maarufu wa muziki wa R&B wa nchini Marekani Beyonce, ametikisa ulimwengu baada ya kuanzisha dini yake iitwayo Beyism.

Dini hiyo ni ya kuabudu iliyoanzishwa rasmi mwaka 2014, alishirikiana na marafiki zake mjini Atlanta, Georgia nchini humo, akaanzisha kanisa lake liitwalo The National Church of Bey.

Kwa mujibu wa kiongozi muanzilishi wa dini hiyo, Pauline John Andrews, alianza kwa kufungua tovuti ya kuwaita watu kujiunga nao ambapo alifanikiwa kupata wafuasi 12, ndani ya kipindi kifupi wakajitokeza wafuasi wengine 200 kanisani hapo.

“Ni dini halisi inayoongea, yeye Beyonce kuwa ni mungu anayepumua, anayeonekana kila siku” alitamka Pauline.

Baada ya kuanzishwa mjini Antlanta, Dini hiyo ya Beyism imeendelea kutawanyika hadi katika jiji la San Francisco, California, nchini Marekani ambapo katika Kanisa la Grace wanayo misa maalumu ya Beyonce.

Katika kanisa hilo linaloongozwa na mchungaji Yolanda Norton, ambaye anatumia biblia iitwayo Beyble katika mafundisho pamoja na nyimbo zake.

Tayari makanisa yanayomuabudu Beyonce, yanatumia Biblia hizo maalum ziitwazo Beyble.

Yaelezwa kwamba utaratibu unaandalia wa kuchapishwa kwa biblia hizo nyingi zitakazoanza kupatikana bure duniani kote.

Mbali na Beyble, makanisa yanayomuabadu Beyonce hutumia nyimbo zake kama sehemu ya kwaya na kila wimbo na maana yake.

Umetolewa mfano wa nyimbo za Pretty Hurt, ambao ni wa kiroho, Drunk in Love ni wa Uhusiano na Upendo, Heaven ni wa kifo, Blue ni wa wa Watoto, Grown Women ni wa Nguvu na Uhuru, Superpower ni wa Upendo, Mine ni wa Uhusiano na Upendo, Blown ni wa Uhusiano pamoja na No Angel nao ni wa Upendo na Mapenzi.

Beyonce hivi karibuni ameongeza wigo wa dini yake kwa kununua kanisa mjini New Orleans nchini Marekani, lenye thamani ya dola za Kimarekani zipatazo 850,000 (zaidi ya shilingi za Kitanzania Biion 1.7)

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, kanisa hilo lilijengwa mwanzoni wa miaka ya 1990, ambapo linasemekana kuwa na umri wa zaidi ya miaka 100. Kanisa hilo limekuwa halitumiki kwa muda mrefu baada ya waumini wengi kufariki dunia. Kanisa hilo lina ukubwa wa mita za mraba wa 7,500 linasemekana haliko mbali sana na anapoishi dada wa Beyonce, Solange.

Adha Beyonce tayari amekwisha nunua mjengo wa kuishi karibu na kanisa lake.

Dini hiyo ya Beyble, imechota waumini maelfu ambapo inaonesha baadhi ya wafuasi watu maarufu kama akina Kanye West, Mariah Carey, Rihanna Nicki Minaj na wengine wengi.

Wasifu wa Beyoncé unaeleza kuwa alizaliwa Septemba 04, 1981 ni mwimbaji wa muziki wa R & B, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji na mwanamitindo kutoka Marekani.

Alizaliwa na kukulia Houston, Texas na alihudhuria shule mbalimbali zinazofunza sanaa. Beyonce pia alianza kushiriki katika mashindano ya kuimba na kucheza ngoma akiwa mtoto.

Akiwa na umri wa miaka tisa, alijiunga kwa mara ya kwanza katika shule ya Parker Elementary huko Hounston, Marekani.

Alikuja kujulikana mwishoni wa miaka ya 1990 kama mwimbaji kiongozi wa kikundi cha wasichana cha R & B, Destiny's Child. Kulingana na Sony, mauzo ya rekodi za Beyonce Knowles, yakiunganishwa na yale ya kikundi cha Destiny's Child, yamezidi milioni 100.

Wakati wa kuvunjika kwa kikundi cha Destiny's Child, Beyonce Knowles alitoa albamu yake ya kwanza, Dangerously in Love mwaka 2003, ambayo ilikuwa mojawapo ya albamu za mwaka zilizokuwa na mafanikio zaidi.

Jambo hilo liliashiria uwezo wake wa kufaulu kama msanii kivyake. Albamu hiyo ilikuwa na mafanikio muhimu ya kibiashara, huku ikitoa nyimbo mashuhuri kama "Crazy in Love", "Baby Boy", zilizopelekea kujishindia tuzo tano za Grammy mwaka 2004.

Kutawanyika kwa kikundi cha Destiny's Child mwaka 2005, kuliendeleza mafanikio yake: Albamu yake ya pili, B'Day, iliyotolewa mwaka 2006, ilikuwa namba moja kwenye chati za Bango, na ilikuwa na nyimbo kama "Déjà Vu", "Irreplaceable", na "Beautiful Liar".

Albamu yake ya tatu, I Am... Sasha Fierce, ilitolewa Novemba 2008, ilikuwa na nyimbo kama "If I Were a Boy", "Single Ladies (Put a Ring on It)", "Halo" na "Sweet Dreams".

Beyonce amefikisha idadi ya nyimbo tano zinazopendwa sana miongoni mwa orodha ya nyimbo 100, hivyo kuwa mmoja kati ya wasanii wawili wa kike walio na idadi kubwa ya nyimbo zilizochukua nafasi ya kwanza katika miaka ya 2000.

Mafanikio ya albamu alizoimba akiwa peke yake yamemfanya Knowles kuwa mmoja wa wasanii wanaosifika sana katika tasnia ya muziki.
Msanii huyo amepanua kazi yake kwa kujihusisha na uigizaji na kuidhinisha bidhaa.Beyonce alianza kazi yake ya uigizaji mwaka 2001, aliposhiriki katika filamu ya kimuziki.

Mwaka wa 2006, alishiriki kama mmoja wa wahusika wakuu katika filamu ya malinganisho ya 1981 ya Broadway musical Dreamgirls, ambayo ilimfanya kuteuliwa mara mbili katika Golden Globe Nominations.

Knowles alizindua shirika la familia yake la mitindo,House of Deréon, mwaka 2004, na limekuwa likihusika na kuidhinisha bidhaa kama Pepsi, Tommy Hilfiger, Armani na L'Oréal.

Katika mwaka wa 2009, jarida la Forbes lilimworodhesha Knowles namba nne katika orodha yake ya watu mashuhuri walio na nguvu na ushawishi mkubwa katika dunia, wa tatu katika orodha ya wanamuziki wa hadhi ya juu, na namba moja katika orodha ya juu ya watu mashuhuri wanaolipwa malipo bora zaidi chini ya miaka 30, akiwa na zaidi ya mapato ya dola milioni 87, kati ya 2008 na 2009.

Wasifu wa Beyonce ambaye ni msanii wa muziki wa R&B, unaonesha kuwa mwaka 1990, akiwa na umri wa miaka tisa, alijiunga kwa mara ya kwanza katika shule ya Parker Elementary huko Hounston, Marekani.

Akiwa shuleni hapo ambapo pia hufundisha muziki, Beyonce alikuwa mmoja wa waimba kwaya wazuri.Miaka minne baadae, Beyonce aliteuliwa kuwa kiongozi wa kwaya katika kanisa walilokuwa wakisali wazazi wake la St. John’s United Methodist.

Katika hali ya kuonesha kuwa muziki umo ndani ya damu yake, katika kipindi hicho Beyonce alikutana na rafiki yake, La Tavia Roberson. Wakaamua kutengeneza kikundi cha kuimba na kucheza dansi kiitwacho Girls Tyme, hapo ndipo kukaibuka wasanii sita akiwemo Kelly Rowland.

Baada ya kupitia matamasha mengi, Girls Tyme waliamua kubadili majina na kujiita Destiny’s Child ambapo walibaikiwa kuwa wasanii watatu ambao ni Beyonce Knowles, Kelly Rowlands na Michelle Williams.

Kama Waswahili wasemavyo kuwa “Ivumayo haidumu” badaye kundi hilo liligawanyika kila mmoja akifanya maisha yake.Ni kipindi kirefu sasa Beyonce amefanikiwa kuiteka dunia katika burudani kupitia nyimbo zake , tangu alipoibuka na albamu yake ya kwanza ya Dangerously in Love mwaka 2003.

Beyonce ambaye hivi sasa ni mama wa watoto watatu aliwazaa na rapa mashuhuri Shawn Carter ‘J Z’.


Makala hii imepatikana toka mitandao mbalimbali.Muandaaji anapatikana kwa namba: 0784331200, 0767331200 na 0713331200. 
BEYONCE AKIFURAHIA JAMBO WALIPOKUWA NA MUMEWE JZ

VISA, MABENKI 15 WAZINDUA HUDUMA YA VISA KWENYE SIMU YA MKONONI JIJINI DAR

0
0

Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Kampuni ya VISA kwa Sab-Sahara Afrika Aida Diara akizungumza katika katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amesema lengo la kuzinduwa huduma hiyo ni kuhamasisha uboreshaji huduma na kupunguza makato kwa wateja, wafanyabiashara na sekta ya huduma ya fedha kwa ujumla.



Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Mauzo ya Biashara Kennedy Luhombo akitoa ufafanuzi juu ya huduma ya VISA inavyofanya kazi katika simu za mkononi katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.



*BoT yasema Tanzania imepiga hatua kuongeza malipo ya kieletroniki *Yaelezwa Watanzania milioni 20 wana usajili au akaunti za fedha kwenye simu Na Said Mwishehe, Globu ya jamii. VISA na benki 15 nchini Tanzania wamezindua huduma ya kwanza ya malipo ya simu bure ambapo sasa wateja wanaofanya miamala watakuwa na uwezo wa kutuma au kupokea fedha ndani na nje ya nchi bila makato yoyote.
 
 Akizungumza leo Machi 12, 2019 jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Bernad Kibese amesema uzinduzi huo wa VISA kwenye simu ya mkononi ni hatua nzuri na Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuongeza malipo ya kieletroniki na kukuza ushirikishwaji wa fedha. "Uzinduzi wa Visa kwa njia ya simu ya mkononi unaonesha hatua muhimu katika kuongeza kasi ya uhamaji kutoka fedha taslimu kwenda mfumo wa uchumi wa kidigitali Tanzania ambao ni mzuri kwa jamii zetu,"amesema Dk. Kibese. 
 
Kwa upande wake Rais wa Kampuni ya VISA kwa Sab-Sahara Afrika Aida Diara amesema lengo la kuzinduliwa kwa huduma hiyo ni kuhamasisha uboreshaji huduma na kupunguza makato kwa wateja, wafanyabiashara na sekta ya huduma ya fedha kwa ujumla. Amesema ili kutumia huduma hiyo , Diara amesema mteja wa benki anatakiwa kupakua programu ya simu ya benki husika, kisha atatafuta Visa kwenye programu na lipia bidhaa na huduma ama kwa kupiga picha alama ya QR au kwa kutumia USSD (Unstructed Supplimentary Service Data)katika sehemu ya biashara ulipo.
 
Huduma hiyo ni ya Visa na inapatikana bure na salama. "Matumizi ya malipo ya kieletroniki yanaongeza usalama na urahisi barani Afrika huku ikipunguza gharama na kuongeza uwazi katika shughuli za kifedha.Sehemu kubwa ya uchumi wa Afrika na usio rasmi, malipo hufanyika kwa kubadilishana fedha taslimu kwa zaidi ya asilimia 90.
 
 "Inatia moyo kuona Watanzania tayari wanafuata na kukubali teknolojia ya simu ikiwa na usajili wa watu zaidi ya milioni 41 na zaidi ya asilimia 80 ya waliosajiliwa hutumia mtandao kwa kutumia simu za mkononi.Ni ukweli unaofahamika kuwa zaidi ya Watanzania milioni 20 wana usajili au akaunti za fedha kwenye simu.Hizi zote ni ishara za matumaini kwa VISA,"amesema. 
 
Diara amesisitiza lengo la uzinduzi wa Visa kwa njia ya simu nchini Tanzania, lina msingi imara na kwamba wafanyabiashara watafurahia na kuthamini utamaduni huo mpya kabisa wa malipo ya fedha taslimu wa kulipa au kulipwa. Ameongeza kuwa uhamaji wa kutoa fedha taslimu kwenda kidigitali unapanua wigo wa juu na chini wa thamani .
 
Kwa mteja huduma za fedha za simu zinaleta usalama,urahisi, mazingira mazuri ya malipo kuliko fedha taslimu na inaokoa muda na gharama za safari. Kuhusu malengo yao kwa upande wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Diara amesema wameendelea kukuza mipango yao, biashara na teknolojia katika ukanda huo kwa kufungua mtandao wao kuunga mkono mahitaji ya taasisi za fedha, wauzaji , waendelezaji na washirika wa FinTech ili kujenga mazingira jumuishi ya kimazingira. 
 
Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley amesema kulingana na jarida la TanzaniaInvest , eneo la biashara ya simu nchini Tanzania inashuhudia ukuaji wa haraka unaofikia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 1.6 zilizofanyika kila mwezi mwaka 2018. Amezitaja baadhi ya benki ambazo zimeshirikiana na VISA kutoa huduma hiyo ni CRDB, NMB, NBC, benki ya Azania, TIB , benki ya Posta, DCB, benki ya Mkombozi, Mufindi Community Bank Limited, Benki ya Watu wa Zanzibar , Benki ya Uchumi,Benki ya Mwalimu,Benki ya Maendeleo na Yetu Microfinance Bank.

MARIAH CAREY ALIYEBAGULIWA KWA URAIA WAKE.

0
0
Na Moshy Kiyungi,Tabora.

Mariah Carey alizaliwa toka kwenye familia yenye asili mataifa tofauti, ilibaguliwa na kufanyiwa fujo kila mara.

Familia hiyo ilijikuta ikisulubiwa kwa kuchomewa na kutupiwa vitu nje ya nyumba yao, mbwa wao wakinyweshwa sumu na risasi zikipigwa dirishani kwao.

Mariah Carey ni nani?

Ni mwanamuziki aliyezalizwa Machi 27, 1970 katika kitongoji cha Huntington jijini New York, nchini Marekani.

Baada ya kuzaliwa alipewa majina ya Mariah Angela Carey. Ni mwanamuziki mwenye mafaniko makubwa anayejulikana kila pembe za dunia.

Makuzi ya Mariah ni ya kuhuzunisha kwa jinsi alivyopitia msoto, maisha ya dhiki, msongo wa mawazo na kutengwa na jamii.

Mama yake Mariah ni Patricia Hickey, Mmarekani mwenye asili ya Ireland na baba yake Alfred Roy ni Mmarekani mweusi mwenye asili ya Venezuela,.

Mariah akiwa na umri wa miaka 16, aliingia shule Kati ya Oldfield. Huko ndiko akagundua kuwa nacho kipaji kingine cha kuandika nyimbo zake.

Lakini akaanza kutoroka na kukwepa masomo akibakia ghetto kuandika nyimbo, kwani tayari alishaingiza akilini mwake ndoto za kuwa mwanamuziki maarufu.

Alipoingia Harborfield High School, alianza kusafiri kwenda Manhattan na kurudi ili kusoma muziki na wataalamu waliobobea.

Baadaye Carey ilibidi alale akiwa mchovu sana, kwa kuwa alilazimika kuanza kusaka fedha kuingia studio kwa kufanya kazi za ziada baada ya ya masomo,. Pia alitakiwa kupata fedha za kulipia nyumba ndogo ya kupanga waliokuwa wakiisihi na mama yake.

Carey alilazimika kufanya kazi za kuosha nywele za watu saluni, pia alifanya kazi ya kuhudumia kwenye migahawa ili kupata fedha.

Mwaka 1987, alianza masomo yake Harborfields High School na kwenda Manhatan ambako rasmi alianza kurokodi nyimbo na baada ya mwaka mmoja akaanza kuona matunda ya kazi zake.

Novemba mwaka huohuo, Carey alikutana na kigogo wa muziki Mattola ambaye aliingia naye mkataba wa kurekodi albamu. Hapo ndipo alipotoa albamu yake ya kwanza iitwayo “Mariah Carey” mwaka 1990 wakati huo akiwa na umri wa miaka 20.

Albamu hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa ikiwa na nyimbo zilizokaa kwa muda mrefu No. 1 kwenye chati kwa nyakati tofauti ambazo ni “Vision of Love”, “Someday”, “Love takes Time” na “I Don’t Want to Cry”.

Carey aliyetamba na nyimbo kama Touch my Body, I Still Believe, We Belong Together, My All, Without You na Always Be My Baby. Nyimbo hizo zilimletea sifa kubwa diniani kote.

Ameuza zaidi ya albamu milioni 200 duniani kote . (Piga hesabu, hata kama albamu moja ni shilingi 1,000 maana yake ana bilioni 200).

Pamoja na mauzo hayo, Carey pia ‘alipiga’ pesa nyingi aliposaini mkataba na Virgin Records mwaka 2000 akitokea Columbia Records kwa bosi Motola ambapo alilamba dola milioni 100. (zaidi ya Sh. Bilioni 227 za Kitanzania)

Mariah Carey ana tuzo tano za Grammy, 19 za dunia, 10 za Marekani na 14 za Billboard.Hili ni somo tosha kuwa ukipambana bila kukata tama, mwisho wa siku ni lazima utaona matunda.

Au kwa mneno ya Kiswahili “Mvumilivu hula Mbivu”Hata hivyo kwa upande wa pili wa maisha yake, Carey amebadilisha wanaume wengi sana hadi kufikia umri huu wa miaka 50.

Alianza kutoka kimapenzi na bosi wake Mottola wakati akirekodi albamu ya kwanza, na walioana Juni 2005, 1993 lakini wakatengana Mei 30, 1997.

Tangu 1998 hadi 2001 alikuwa kwenye uhusiano na mwanamuziki Luis Miguel. Alikutana na muigizaji wa Nick Cannon wakati wa kushuti video yao ya wimbo wa “Bye Bye’’. Waakaza mahusiano ya kimapenzi na hatimaye wakaoana Aprili 30, 2008, na Aprili 30, 2011 walifanikiwa kupata watoto wawili mapacha Moroccan na Monroe, Cannon Agosti 2014 alithibitisha kutengana na Carey .

Aidha Carey alikutana na James Parker bilionea wa Australia , wakatangaza kuchumbiana.Hadi kufikia Oktoba walikuwa tayari wamekorofishana na kusitisha uchumba wao.

Carey ni Muanglicana. Mwaka 2006 alitamka kuwa “Naamini nimezaliwa mara ya pili. Nadhani nilichobadilika ni vipaumbele vyangu na uhusiano wangu na Mungu.Najisikia tofauti nisipokuwa na muda binafsi wa kusali. Mimi ni mpambanaji, lakini nimejifunza kuwa na maamuzi ya mwisho .

Chochote Mungu anachotaka kitokee ndicho kinatokea. Ni kwa Neema za Mungu bado nipo”.

Huyu ndiye Mariah Carey mweye Ukwasi lufufu.

WAZIRI JAFO ACHUKIZWA NA WATUMISHI WAZEMBE AMBAO WANASHINDWA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO

0
0
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amechukizwa kuona baadhi ya viongozi na watendaji kutotimiza majukumu yao ipasavyo ikiwemo kufanya mambo kienyeji kwa kupokea miradi ya maendeleo pasipo kufahamu mwenendo mzima wa mkataba ulivyo pamoja na kutojua gharama za  fedha ambazo zinatolewa kwa ajili ya utekelezaji.

Jafo ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kituo cha afya cha mlandizi kilichopo Wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa lengo la kujieneo mwenendo mzima wa ukarabati wa majengo pamoja na kujionea ujenzi wa majengo matatu ambayo yamejengwa kwa kiasi cha shilingi milioni 400 fedha ambazo zimetolewa na serikali kuu.

Pia Jafo alibainisha kuwa hawezi kuwavumilia watumishi ambao ni wazembe na wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo na kuwataka kuachana mara moja na vitendo vya kujihusiha na ubadhilifu wa fedha ambazo zinatolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo.

 “Mimi kama  kiongozi wetu sipendi kuona kabisa mnafanya kazi kienyeji bila ya kuzingatia sheria na taratibu amabzo zimewekwa na nchi, na katika hili siwezi kulifumbia macho maana maeneo mengine nimepita nimekuta miradi mingine bado inasua sua nah ii ni baadhi ya watu kutotimiza majukumu yao ipasavyo ni ninachotaka miradi yote inapokuja lazima wahusika kufahamu mikatab ailivyo pamoja na fedha ambayo inatolewa sio kupokea tu,”alisema Jafo.

Aidha aliseama kwamba serikali ya awamu ya tano kwa sasa imeshatoa fedha katika vituo vya afya  zaidi ya 90 hapa nchini   kwa lengo la kuweza kuongeza majengo mengine pamoja na kufanya ukarabati wa miundombinu ya wodi mbali mbali ikiwemo nyumba za watumishi kwa lengo la kuweza kuboresha sekta ya afya kwa wananchi.

Aidha katika hatua nyingine Jafo ameupongeza uongozi wa halmashauri ya Kibaha vijijini  kwa kutekeleza agizo lake la kukukarabati  chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha afya mlandizi ambapo hapo awali kilikuwa hakifanya kazi kabisa kwani kiligeuzwa kuwa  eneo la stoo na kuhifadhia vyuma chakavu.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kibaha vijijini  Butamo  Nuru alisema  kwamba wametekeleza agizo ambalo walipatiwa na waziri wa Tamisemi la kukarabati miundombinu ya chumba cha kuhifadhia maiti pamoja na kununua majokofu  nane ambayo yamegharimi kiasi cha shilingi milioni 36.

WAZIRI Jafo katika ziara yake ya kikazi kwa  halmashauri ya Kibaha vijijini ameweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa  majengo matatu ya wodi ya upasuaji,wazazi,na wagonjwa wa nje (OPD) sambamba na kutembelea miradi mingine miwili ya ujenzi wa hospotali pamoja na jengo la  ofisi za halmashauri hiyo.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kushoto akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kulia kuhusiana na usimamiza wa fedha zinazotolewa katika miradi mbalimbali ya maendeleo katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Homoud Jumaa mara baada ya kukagua ujenzi wa wodi tatu zilizojengwa katika kituo cha afya mlandizi  pamoja na kujionea ukarabati wa  chumba cha kuhifadhia maiti.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kushoto akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kulia kuhusiana na usimamiza wa fedha zinazotolewa katika miradi mbalimbali ya maendeleo katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Homoud Jumaa mara baada ya kukagua ujenzi wa wodi tatu zilizojengwa katika kituo cha afya mlandizi  pamoja na kujionea ukarabati wa  chumba cha kuhifadhia maiti.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kushoto akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kulia kuhusiana na usimamiza wa fedha zinazotolewa katika miradi mbalimbali ya maendeleo katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Homoud Jumaa mara baada ya kukagua ujenzi wa wodi tatu zilizojengwa katika kituo cha afya mlandizi  pamoja na kujionea ukarabati wa  chumba cha kuhifadhia maiti.

wafanyakazi Vodacom Tanzania watembelea shule ya Sangu, Mbeya na shule ya Arusha Day kuadhimisha siku ya wananwake Duniani,watoa msaada wa vifaa mashuleni.

0
0



 Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (kulia) akimkabidhi zawadi Mkuu wa shule ya sekondari Arusha Day, Joyce Gyunah katika hafla iliyofanyika jijini Arusha jana. Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani, Wafanyakazi wa Vodacom wametembelea shule hiyo ya wasichana na kuwapatia vifaa kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.

Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen akizungumza na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Arusha Day na kuwahimiza kusoma kwa bidii, katika hafla iliyofanyika jijini Arusha jana. Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani, kampuni ya Vodacom imetembelea shule hiyo ya wasichana na kuwapatia vifaa kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.

Meneja Masoko wa kampuni ya Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini, Magreth Lawrence (kushoto) akimkabidhi daftari, Jackline Chaula, mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Sangu jijini Mbeya. Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, wafanyakazi wa kampuni hiyo wametembelea, kuongea na kutoa zawadi na vifaa mbalimbali kwa wasichana ili kuwasaidia mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.
Meneja Masoko wa kampuni ya Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini, Magreth Lawrence, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Sangu juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike. Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wametembelea shule hiyo na kuwapatia vifaa mbalimbali kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.

KILAVE -AWATAKA UWT KIGAMBONI KUJITOEZA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA CHAGUZI ZIJAZO

0
0
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Dorothy Kilave akizungumza na Wanawake wa UWT  Kata ya Kigamboni Katika ziara yake ya kikazi kuinua hari ya chama na kukumbushana mambo ya Msingi ikiwa pamoja na fursa za mikopo zinazopatikana katika Halmashauri zetu kwa Asilimia nne Wanawake,Asilimia Vijana na Mbili kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam(UWT),Grace Haule akiwakumbusha majukumu watendaji wa chama ngazi ya kata mpaka matawi na kuwatka kudumisha umoja hili CCM iweze kuibuka na ushindi Mnono katika uchaguzi wa 2019 na 2020
 Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Umoja wa Wanawake(UWT), Chokole Mohamed, akiwasalimia wakazi wa kata ya Kigamboni Katika Mkutano wa ziara ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa.
 Diwani wa Viti Maalum Kata ya Kigamboni, Amina Yakub akisalimia wakazi wa Kigamboni wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam.
 Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa akiwasalimia Wajumbe wa Mkutano wa UWT Kata ya Kigamboni wakati wa Ziara ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kigamboni, Mwajabu Mbwambo akitoa neno la ukaribisho kwa wageni Waalikwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam.
 Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa UWT Kata ya Kigamboni wakifatilia hotuba kutoka kwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam,Dorothy Kilave.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa UWT Kata ya Kigamboni wakifatilia hotuba kutoka kwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam,Dorothy Kilave

WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA UWASILISHWAJI WA MPANGO NA UKOMO WA BAJETI YA MWAKA 2019/20

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma Machi 12, 2019. Mheshimiwa Majaliwa alikwenda Bungeni kuhudhuria kikao cha Uwasilishwaji wa Mpango na Ukomo wa Bajeti ya Mwaka 2019/2020; na Uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango, Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao cha Uwasilishwaji wa Mpango na Ukomo wa Bajeti ya Mwaka 2019/2020; na Uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango, Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, kwenye ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma Machi 12, 2019, kushoto ni Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai na kulia ni Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Fedha Dkt. Philip Mpango akiwasilisha Mpango na Ukomo wa Bajeti ya Mwaka 2019/2020 na Uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango, Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, kwenye ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma Machi 12, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKURUGENZI SHIRIKA LA KIMATAIFA LA NGUVU ZA ATOMU (IAEA) KANDA YA AFRIKA KUTEMBELEA ZANZIBAR

0
0
Arusha, 12 Machi, 2019 

Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (IAEA) kanda ya Afrika Profesa Shaukat Abdulrazak anatarajia kuonana na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Marchi 13. 

Mkurugenzi huyo ataambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Lazaro Busagara ambao watapata nafasi ya kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali. 

Mkurugenzi huyo aliweza pia kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa waratibu (NLOs) wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia unaowahusisha nchi wanachama 46 wa Shirika la Nguvu za Atomu Duniani uliofunguliwa March 11 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha unaoendelea jijini Arusha. 

Shirika la Nguvu za Atom duniani IAEA linatoa ufadhili kwa serikali ya Tanzania katika miradi mbali mbali inayohusisha sekta za Afya, Kilimo, Maji, Mifugo, Rasilimaliwatu, Nishati na Viwanda ambapo mpaka sasa ni jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 9.5 zimetolewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na gharama za mafunzo kwa wataalamu katika masuala ya afya. 

Imetolewa na; 
Kitengo cha Mawasiliano 
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania 

BALOZI MAHIGA AWASILI WIZARANI NA KUKABIDHIWA RASMI OFISI

0
0

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amewasili makao makuu ya Wizara jijini Dodoma na kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi. Kitendo hicho kinafuatia kubadilishana wizara baina ya mawaziri hao kufuatia mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Mhe. Rais DKt. John Pombe Magufuli Machi tatu mwaka huu.
Akikabidhi ofisi Prof. Kabudi amewashukuru watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi alichofanya nao kazi na kuwasihi kuendelea kumpa ushirikiano kama huo Balozi Dkt. Mahiga kwani anaamini yale aliyoyaanzisha yataendelezwa na Waziri huyo kwa nguvu zote.
Prof. Kabudi amesema katika kipindi chake cha uongozi Wizarani  amebadilisha  muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali nakutoa ofisi mpya tatu za Mwanasheria Mkuu wa Serikal, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na ana imani kuwa mabadiliko hayo yatatekelezwa kikamilifu chini ya uongozi wa mjenzi mahiri Dkt. Augustine Mahiga.
“Mlinipa ushirikiano mkubwa katika kipindi change, niwasihi muendelee hivyo kwani kwa kushirikiana nanyi tulifanikiwa kubadilisha  muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na hivyo kutoa ofisi mpya tatu za Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, natumai kuwa utekelezaji wa majukumu yaliyo mbele yao utakuwa kamilifu chini ya Mhe. Balozi Dkt. Mahiga ambaye ni mjenzi Mahiri kama mtashirikiana vyema,” alisema Prof. Kabudi.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Ofisi Mhe. Balozi Dkt. Mahiga amesema amepokea jukumu hilo kwa mikono miwili na amewashukuru watumishi wa Wizara hiyo kwa mapokezi waliompatia na kuahidi kushirikiana na watumishi wote katika kazi zao na hivyo kuendeleza yale yote ambayo Prof. Kabudi ameyaacha kwa ajili ya kuiletea nchi maendeleo kupitia sekta ya Sheria nchini.
“Niwashukuru kwa mapokezi yenu leo hii, nimefarijika kuwa nanyi hapa siku hii kama ambavyo Mhe. Rais alisema siku naapishwa kuwa nisiwe na shaka nimezungukwa na wanasheria mahiri,  niwaahidi kuwa tutashirikiana katika kazi zote ili tuendeleze yale yote ambayo mwanafunzi wangu Prof. Kabudi ameishia,” alisema Balozi Dkt. Mahiga
Awali mawaziri hao walikabidhiana majengo ya ofisi zao yaliyoko katika Mji wa Serikali Mtumba na baadaye kuja zilizoko Ofisi za Wizara zilizoko Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM ambako walikabidhiana taarifa mbalimbali za Wizara na kuzungumza na watumishi.
Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria prof. Sifuni Mchome, Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga na watendaji wengine wa Wizara na taasisi zake waliopo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (watatu kulia) katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (wanne kulia)  baada ya kutembelea jengo la Wizara ya Katiba na Sheria lililoko katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ambako pia alitumia nafasi hiyo kumkabaidhi jengo hilo kama asehemu ya makabidhiano ya Wizara baina ya Mawaziri hao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akitia saini kitabu wa cha wageni baada ya kukagua jengo la Wizara ya Katiba na Sheria na kulikabidhi jengo hilo kwa Waziri wa sasa wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (mwenye tai ya Bluu) anayeongea na Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome. Jengo hilo liko katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Agnela Chang’a baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tangu apishwe kushika nafasi hiyo , huku aliyekuwa Waziri Mhe, Prof. Kabudi  na Katibu Mkuu Prof. Mchome wakiangalia.

 Waziri wa Katiba na Sheria mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiambatana na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  mhe. Prof.Palamagamba Kabudi (nyuma yake) wakisalimiana na watumishi wa Wizara baada ya kuwasili makao makuu ya Wizara UDOM kwa ajili ya kukabidhiana Ofisi baina ya Mawaziri hao kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Mhe. Rais hivi karibuni.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akishikana mkono na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga baada ya kumkabidhi ofisi rasmi baada ya kubadilishana wizara hizo kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa hivi karibuni na Mhe. Rais. Makabidhiano hayo yamefanyika makao maku ya Wizara yaliyo katika Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea nyaraka kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi   wakati alipomkabidhi rasmi ofisi baada ya kubadilishana wizara hizo kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa hivi karibuni na Mhe. Rais. Makabidhiano hayo yamefanyika makao maku ya Wizara yaliyo katika Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM- jijini Dodoma, wakiangalia kushoto kwa prof Kabudi ni Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju na kulia ni Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga na watumishi wengine wa Wizara 

Nigeria and Tanzania take first prize in Huawei's Sub-Saharan Africa ICT Competition

0
0
Students from Nigeria and Tanzania were the overall joint winners of this year’s Sub Saharan regional finals of Huawei's global ICT Competition.

Together with second prize winners, Angola and Kenya, the four teams will travel to China for the finals which will see 40 teams from around the world compete for the championship title.

The competition covered latest ICT technologies such as cloud computing, artificial intelligence, mobile networks and big data. Almost 30 thousand students from over 100 universities in Nigeria, Ghana, Kenya, Uganda, Tanzania, Angola, South Africa, Mozambique, Zambia, Botswana and Mauritius participated

At the finals, held this weekend in Johannesburg, it came down to 42 students in14 teams. They sat for theory and practical examinations at the finals at Huawei’s regional headquarters in Woodmead, Johannesburg.

Speaking at the final award giving presentation,Mr.Xue Man, Vice President of Huawei, said“Huawei understands the value of a good talent ecosystem which is the foundation for a smart future. This ICT Competition is part of ourinnovative initiatives to support that and promote ICT skills. We believe that this event will inspire more students’ interest in ICT learning in Africa; it provides them with a world-class stage to showcase themselves and consolidate the vital ICT needed for Africa's development”

Mr. Alfred Cheruiyot, Principal Secretary,State Department for Post Training and Skills Development from Kenya Ministry of Education praised Huawei’s actions to raise skills and partner with national governments and local tertiary institutions to strengthen the skills pool in ICT.
“We are fully aware how important this is for our students to get good jobs and to become successful entrepreneurs. We are fully aware that this will drive our economy forward for many years to come if we can get it right,” Mr. Cheruiyot told the gathering.

Tanzania ICT student Emanuel Chaula was overjoyed that his team emerged as one of the two winning countries. He said, “We worked hard as a team because we wanted to seize the opportunity to get to travel to China to compete in the global finals. We really want to show Africa and the world that Tanzania is an up and coming ICT player and we want to be a part of that growth in our country. We will study and practice for the finals in China as we are going there to win. “

The Huawei ICT Competition is a global ICT talent competition exchange event, which is aimed at the Huawei Authorized Information and Network Technology College (Huawei ICT Academy) and related universities. Since the first Huawei ICT Contest held in 2015, the number of participants in the competition has grown exponentially and has become one of the largest ICT events in the world. The 2018/19 event has attracted more than 1,000 universities in more than 50 countries around the world under the slogan “Connection, Glory and Future”. The total number of students participating global was 80,000 students, including 28 000 students from Southern Africa.

During the competition, through the road show, training, lectures and other special activities, the students will be able to pass on the latest technology, information and trends of the industry to the students and practitioners, and bring them closer to the theoretical study and practical experiencelevel of students joining the job marketand increase their competitiveness.

According to the schedule, the winners of sub-Saharan Africa will go to China in May to participate in the global finals in Shenzhen, China. By then, they will compete with the 40teams from other parts of the world for the global finals.
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live




Latest Images