Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

GAVANA SHILATU ASHIRIKI UJENZI ZAHANATI ‘NI ULE ALIOAGIZA UENDELEZWE’

$
0
0

Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Afisa Tarafa Mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu ameshiriki ujenzi wa Zahanati ya Ngongo iliyopo Kijiji Cha Ngongo kilichopo kata ya Michenjele.
Gavana Shilatu alienda kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake ya ujenzi wa mradi huo wa Zahanati alioagiza ndani ya siku mbili uanze kutokana na kutelekezwa tangu Mwaka jana. 

Gavana Shilatu alifurahishwa kukuta nyasi zimefyekwa na Mafundi wapo kazini Kama alivyoagiza na kuwasisitiza watangulize mbele uzalendo kwa kuhakikisha mradi unajengwa kwa kuzingatia ubora na viwango vinavyolingana na thamani ya pesa. 

Katika ushiriki wa ujenzi huo Gavana Shilatu aliambatana na Serikali ya Kijiji pamoja na kamati ya ujenzi.


UZINDUZI WA JUKWAA LA NAWEZA WAFANA MWANZA

$
0
0
SERIKALI ili kupunguza vifo vya uzazi Mama na Mtoto ikishirikiana na Mradi wa USAID Tulonge Afya fhi 360 imezindua Jukwaa la mawasiliano ya afya kwa watu wazima (NAWEZA) ili kufikisha elimu sahihi itakayoijengea jamii ya Watanzania uwezo na kubadilisha mitizamo na tabia zao za kiafya na kuleta matokeo chanya.

Pia jukwaa hilo unganishi litatoa huduma jumuishi za afya katika maeneo matano ya afya kuiwezesha serikali kufanikisha mikakati na vipaumbele vyake vya kupunguza maambukizi ya Ukimwi (VVU), vifo vya  akina mama vitokanavyo na uzazi,vifo vya watoto wachanga, malaria na kifua kikuu (TB).
Akizungumza kwenye uzinduzi huo jana Mratibu wa Afya ya Uzazi Wizara ya Afya, Martha Shakinyau alisema NAWEZA itaunganisha jitihada za wadau wa miradi ya mawasiliano ya kuhamasisha na kutoa elimu na maarifa sahihi kwa jamii,  familia, makundi rika ili kubadilisha tabia kulingana na mahitaji na vipaumbele vya maisha yao wakati wa ujauzito au wa malezi ya watoto chini ya umri wa miaka mitano , kuwapa ari ya kuboresha afya zao na kuishi maisha bora.

“Serikali imejitahidi kuboresha huduma kwa kujenga vituo vya afya,upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na vitedanishi ili  kupunguza vifo vya Mama vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga chini ya miaka mitano lakini vifo hivyo vimeendelea kutokea kutokana na changamoto mbalimbali,” 
“NAWEZA inalenga maeneo matano muhimu ya vipaumbele vya serikali vya kupunguza maambukizi ya VVU, malaria, afya ya uzazi kabla na baada ya kujifungua,afya ya mama na mtoto  na TB.Tunaamini Watanzania wote wakiguswa kwenye eneo moja la kiafya kati ya yaliyoanishwa afya za wengi zitaboreka,”alisema Shakinyau.

Hivyo, NAWEZA itawafikia wananchi tofauti tofauti itachangia kuboresha afya na ustawi wa Watanania wengi, itakuwa ikibadilika badilika ili kukidhi mahitaji ya maeneo mengine ya kiafya muhimu kwa walengwa hao ama makundi mengine.
Kwa mujibu wa Shakinyau changamoto ya umbali wa vituo, umaskini, ukosefu wa elimu ya uzazi salama kwa jamii, huduma za afya zisizokidhi, mila na desturi potofu, uhaba wa dawa, huduma hafifu za rufaa,watoa huduma wa kada zisizo rasmi wasio na weledi, ushirikishaji mdogo wa wanaume na jamii, viongozi wa dini, wanasiasa na serikali.

“Asilimia kubwa ya vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga vinazuilika endapo wadau wa maendeleo, serikali na jamii itawekeza kwa pamoja katika ubunifu na kudhibiti vifo,kuongeza kasi ya uwajibikaji kwenye ngazi zote za utoaji huduma.Pia, ili kufikia Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati, kila mmoja ana jukumu la kuikumbusha jamii kuweza kupunguza vifo hivyo. 
“Rais  John Magufuli anataka kuipeleka Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ili kufikia huko, kipimo ni kupungua kwa vifo vinavyotokana na uzazi usio salama na watoto wachanga.Tunatamani  kuvipunguza vifo vya akina mama kutoka 556  hadi 292 kati ya vizazi hai 100,000 na watoto kutoka vifo 25 hadi 16 kati ya 1,000 kwa mwaka ifikapo 2020,”alisema Shakinyau.

Aidha kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Esther Mariki akizindua jukwaa hilo alisema Kanda ya Ziwa ina changamoto nyingi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya vifo vya wajawazito na watoto wachanga huku maambukizi ya VVU yakiwa juu.
Hivyo serikali kuwekeza kwenye sekta ya afya ina imani NAWEZA katika kuboresha na kuhamasisha jamii na wajawazito kuhudhuria kliniki na vituo vya kutolea huduma baada ya kupata ujauzito kutapunguza vifo na pia  kutaibua wateja wapya wa maambuki ya VVU.

Pia malezi ya watoto chini ya miaka mitano yanayozingatia maadili pamoja na mila na desturi yataleta mabadiliko chanya kwenye jamii na katika kuhakikisha kunakuwa na ujauzito salama na wanajifungua salama akinamama wahudhurie kliniki kabla ya ujauzito kutimiza wiki 12 na wakamilishe mahudhurio manane kliniki wakati wa ujauzito.

Aidha, kaimu mganga mkuu huyo alihimiza watumie IPTP ili kumkinga mtoto na madhara yanatokanayo na malaria, kumkinga kwa chandarua chenye dawa, kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya,kunyonyesha ndani ya saa moja baada ya kujifungua, kuzungumza na mtoa huduma na kupeleka watoto kliniki baada ya kutimiza wiki nne hadi sita kwenda kituo cha kutoa huduma wanapoona dalili za hatari.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Esther Mariki(kulia) akizindua Jukwaa la NAWEZA litakalolenga mawasiliano ya Afya kwa Watu Wazima na Watoto lililozinduliwa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Mratibu wa Afya ya Uzazi Wizara ya Afya, Martha Shakinyau, Mkurugenzi wa Mawasiliano USAID Tulonge Afya, Prisca Rwezahura na Dokta Jaiws Hiliza.
 Mratibu wa Afya ya Uzazi Wizara ya Afya, Martha Shakinyau, akiwasilisha maada wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la NAWEZA lenye malengo ya mawasiliano ya Kiafra kwa Watu Wazima na Watoto lililozinduliwa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa USAID Tulonge Afya, Prisca Rwezahura akizungumza jambo wakati  wa uzinduzi wa Jukwaa la NAWEZA lenye malengo ya mawasiliano ya Kiafra kwa Watu Wazima na Watoto lililozinduliwa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wadau wa Afya kutoka sehemu mbalimbali jijini Mwanza wakifuatili kwa makini utambulisho wa Jukwaa la NAWEZA LENYE Malengo ya mawasiliano ya Afya kwa watu wazima na watoto. 

MSAFARA WA JAFO WAZUILIWA NA WAFANYABIASHARA MLANDIZI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, MLANDIZI.

MSAFARA wa Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo umezuiliwa na watumiaji wa Stendi ,wafanyabishara wa soko na wauza mitumba (WARUMBA) eneo la Mtongani Mlandizi ,wilayani Kibaha kupinga kuhamia kwenye eneo jipya la Mama Salmini ambako wanadai hakuna maslahi kwao. 

Kufuatia hali hiyo ametoa maelekezo kuwa kutokana na soko hilo kutokuwa mali ya serikali ni ya mtu binafsi kwa maslahi mapana ya wananchi soko la mama salmini wawe huru na wale wanaotegemea Mlandizi waendelee huku wakisubiri ukamilishaji wa soko jipya. 

Kuhusu stendi ,Jafo amesema medereva daladala wanapata shida na stendi wawe na uhuru chini ya usimamizi wa wilaya waendelee kutumia stendi ya mlandizi hadi hapo stendi itakapokmilika. 

Akizingumza na wafanyabiashara hao, alieleza wafanyabiashara hao waachiwe wafenye biashara kwa utaratibu na kufuata sheria bila kubughudhiwa. 

"Nimeangalia idadi ya watu na eneo hilo la mama Salmini wenye hiari ya kufanya biashara wafanye biashara kwenye eneo hilo,lakini na wanaotegemea biashara Mlandizi waendelee "alisisitiza Jafo. 
"Mnajengewa soko la kisasa na serikali ipo kwenye mchakato wa kujengwa stendi mpya,hivyo taratibu nyingine zitafuata. "

Hata hivyo, Jafo alifafanua, Watu wadogo wasinyanyasike ofisi ya mkuu wa wilaya na halmashauri iangalie utaratibu wa kuwasogeza kwenye eneo lisilo hatarishi na wafanya biashara wafuate utaratibu, sheria na utaratibu hadi hapo soko maalum litakapokamilika. 

"Wafanyabiashara toeni ushirikiano na serikali ya chama cha mapinduzi kwa maslahi ya wilaya na mkoa. "alisema Jafo. Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa,aliwataka wawe watulivu na kutoa ushirikiano kwa serikali. Kwa upande wake mwenyekiti wa Warumba ,Nasoro Soma alisema kuwa wao hawako tayari kwenda kufanyabiashara kwenye soko jipya kutokana na mazingira yake hayako vizuri kibiashara .

Alieleza, eneo wanalopelekwa ni dogo na siyo rafiki kufanyia biashara na Halmashauri ikisema sehemu wanayofanyia si sahihi kwani ni barabarani.

Alisema zaidi ya wafanyabiashara 200 wamepata vitambulisho vya ujasiriamali ili kuweza kutambulika.
 Waziri Jafo akizungumza na Wananchi

BAADA YA KUREJEA CCM MGEJA AENDA MBUGA ZA WANYAMA KUONDOA 'STRESS'

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii 

SIKU chache baada ya kurejea Chama Cha Mapinduzi(CCM) Hamisi Mgeja amesema ameamua kwenda kuondoa 'Stress' katika mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti.

 Mgeja aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga amerejea Chama hicho mwanzoni mwa wiki iliyopita akitokea Chadema ambapo alijiunga na chama hicho wakati wa mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

 Akizungumza leo kwa njia ya simu Mgeja ameiambia Michuzi Blog kuwa kwa sasa wameamua kwenda kujipumzisha mbuga za wayama baada ya kurejea CCM na hiyo inatoa nafasi kwake na wenzake kutafakari maisha mapya ndani ya CCM baada ya kurejea tena.

"Baada ya kumaliza kazi ya kumsindikiza Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa  nyumbani Monduli na kupokelewa na maelfu ya Wananchi wa Mkoa wa Arusha na Wana-CCM katika tukio la kurejea kwake rasmi na kupewa kadi mpya.

"Tumeamua kuja mbuga za wanyama kupumzika kidogo, ni wakati sahihi kwetu kuondoa 'Stress' za Chadema wakati tunafakari namna ya kushirikiana na Mwenyekiti wetu wa Chama Rais Dk.John Magufuli katika kuleta maendeleo ya Taifa letu,"amesema Mgeja.

Amesisitiza kuwa baada ya kurejea CCM kwa sasa moyo wake umejaa amani tele na kueleza anajihisi mwenye furaha na ameutua mzigo uliokuwa kichwani hasa kutokana na aina ya maisha aliyokuwa anaishi Chadema.

 "Nimekaa Chadema , kuna mambo nimejifunza nikiwa huko.Ndio maana wakati narejea CCM niliamua kuwapa ushauri iwapo  wanataka kuwa Chama cha siasa lazima wabadilike tofauti na hapo watabaki kama walivyo,"amesema Mgeja.

Akizungumzia mwenendo wa siasa nchini Mgeja amesema anampongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo."Hakika Rais wetu mpendwa anafanya kazi kubwa sana ya kuleta maendeleo, ni jukumu letu kumuunga mkono kwa kila hatua."amesema Mgeja.
 Hamisi Mgeja (Katikati) akifafanua jambo wakati anazungumza na makada wenzake wa CCM ambao wameamua kwenda kujipumzisha mbuga ya  wanyama Ngorongoro baada ya kurejea katika Chama hicho akitokea Chadema
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Hamisi Mgeja ambaye aliamua kuhamia Chadema na sasa amerejea tena CCM akiwa katika moja ya jengo lililopo katika mbuga ya wanyama Ngorongoro ambako amekwenda kupumzika.
Hamisi Mgeja wa pili kushoto akiwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa(mwenye nywele nyeupe) pamoja na baadhi ya Wana-CCM wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili mkoani Arusha

UNESCO watembelea Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro

$
0
0
Na Ripota wetu ,Arusha

Timu ya Wataalamu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), imetembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA.

Wataalamu hao walitembelea eneo hilo la urithi wa dunia mchanganyiko kutokana na Tanzania kujiunga na kuwa mwanachama wa UNESCO tangu mwaka 1962.

Katika ziara yao timu hiyo ilifanikiwa kutembelea maeneo ya mradi wa ujenzi wa barabara unaotarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni na NCAA kwa kiwango cha tabaka gumu zege ili kurahisha shughuli za utalii, na masuala mengine ndani ya eneo hilo.

Ujio wa timu hiyo umetajwa kuwa ni utaratibu wa kawaida ambapo hutembelea maeneo ya urithi wa dunia kuangalia changamoto za uhifadhi na kutoa ushauri au mapendekezo.

Mkuu wa timu ya wataalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa inaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamduni (UNESCO), Edmound Moukala (katikati), akimsikiliza Kaimu Meneja Idara ya Urithi wa Utamaduni na Mratibu wa UNESCO eneo la NCCA Selestine Ummanuel.

Meneja wa Idara ya Utafiti na Ufuatliaji Mamlaka ya Hifadhi ya gorongoro(NCAA), Julius Kibebe akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi NCAA Dk. Fredy Manongi kwenye majumuisho ya ziara ya wataalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamduni (UNESCO), waliopo kushoto kwake.

Mkuu wa timu ya wataalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamduni (UNESCO), Edmound Moukala akisisitiza jambo kwenye kikao cha majumuisho baada ya kutembelea baadhi ya maeneo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorogoro.

Pix6. Mwakili wa Baraza la Wafugaji Tarafa ya Ngorongoro akichangia wakati wa majumuisho ya timu ya wataalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamduni (UNESCO), waliotembelea maeneo tofauti ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA. 

HUWEZI KUBADILI HATI MILIKI KAMA UMEANDIKIA MKATABA SERIKALI ZA MITAA.

$
0
0

Na Bashir Yakub. 

Hapo awali niliandika namna sheria isivyowaruhusu viongozi wa serikali za mitaa (watendaji kata, wenyeviti wa mitaa,wajumbe, na ule uongozi wote wa huko chini) kuandaa na kusimamia mauzo na manunuzi ya nyumba au viwanja, kwa ujumla ardhi. Nikasema kuwa kitu hicho hakiruhusiwi katika sheria na wanaofanya hivyo wako katika makosa makubwa. 

Nikasema zaidi kuwa, na asilimia kumi wanayowatoza ni makosa na ndio maana hailipwi kwenye akaunti ya serikali bali mkononi au utapewa risiti za kuchana kwenye daftari badala ya EFD, wizi mtupu. 

Leo tena tutizame kama unaweza kuruhusiwa kubadili jina la ardhi kutoka kwa aliyekuuzia kwenda kwenye jina lako mnunuzi ikiwa ulisimamiwa na serikali za mitaa katika manunuzi hasa ardhi iliyopimwa. 

Sheria Namba 4 ya 1999, Sheria ya Ardhi kifungu cha 62( 1) kinasema kuwa kila nyaraka(document) yoyote ya ardhi iliyosajliwa ambayo itatumika katika mauzo,rehani,zawadi,kurithi, au pango ni lazima iwe katika mfumo wa fomu maalum. Kifungu hiki kinaturejesha katika kanuni za ardhi za mwaka 2001 ili kuziona fomu zinazohusika katika manunuzi ya ardhi na mahitaji yake. 

Fomu ya kwanza ni fomu namba 38 ambayo ni sawa na mkataba wa mauzo(contract for disposition). Fomu hii inalazimisha kuwa ni lazima iwe imegongwa muhuri wa Wakili au kushudiwa na wakili. 

Fomu ya pili ni namba 35 ambayo kisheria ni nyaraka ya kuhamisha umiliki(transfer of right of occupancy).Fomu hii nayo inatoa ulazima wa kuwa imeshuhudiwa na kugongwa muhuri wa Wakili pande mbili, yaani upande wa mhamisha umiliki/muuzaji, na upande wa mpokea umiliki/mnunuzi.

                  KUSOMA  ZAIDI sheriayakub.blogspot.com


Mobile technology, an enabler of inclusive development and women empowerment.

$
0
0
The 21st century has been characterized by rapid technological advancement giving rise to breakthroughs that will affect our politics, economies, improve medicine and influence our culture. Technology has transformed social and economic activities, increased connectivity and created a global village. However, there has been an uneven distribution in mobile technology access and usage between men and women. 

 According to a GSMA report, 14% of women are less likely to own a phone, this equates to 200 million fewer women than men engaging in mobile technology. Sub-Saharan Africa is identified as the second leading region with the gender gap in mobile ownership and internet usage after South Asia. In Tanzania, various interventions in education, health and agriculture sectors such as CodeLikeAGirl, Wazazi Nipendeni and Women Farmer Network respectively, seek to address the gender imbalance in uptake of mobile technology. 

Social and economic factors contribute significantly to gender discrepancy in low and middle – income countries. Social norms and inequality between men and women in education have predominantly contributed to the gender gap in the tech space. The financial cost of possessing a phone coupled with not being tech savvy featured as a deterrent. Women also cited security and harassment in their respective communities as a hindrance to ownership of a mobile phone. 

In Tanzania, the government and various stakeholders in the public and private sector have incorporated mobile technology that will improve service delivery in key areas such as maternal health and education. 

The aspirations highlighted in the Second Five Year Development Plan (FYDPII), are expected to see a reduction in maternal mortality by 50%. Through the ‘Wazazi Nipendeni’ initiative, the Ministry of Health in partnership with public and private sector actors delivers a solution that dispenses pre and post-natal information. 

 Commenting on Vodacom Foundation’s commitment to improve maternal health, Rosalynn Mworia, Director Corporate Affairs and Vodacom Foundation said, “This program has reached nearly 40,000 women and significantly reduced maternal mortality rate in the lake zone as a result of mobile technology.” ‘At a minimum, women should be equipped with information that will allow them to deliver their babies safely. Mobile technology allows us to reach women in remote areas by sending informative text messages on their progress, providing them with peace of mind throughout their pregnancy.’

Removing impediments to learning include identifying and addressing factors such as that affect school attendance. UNESCO estimates that young girls miss 20% of school per year and according to a 2015 report issued by Tanzania Water and Sanitation Network (TAWASANET), about 75% of schoolgirls acknowledge that menstruation impacts their performance in school. By utilizing mobile technology to advice on menstrual hygiene management and sexual reproductive health education the ‘Hakuna Wasichoweza Project’ empowers girls with education on hygiene and selfcare. Additionally, the collaboration between T-MARC and Vodacom Foundation has equipped more than 10,000 schoolgirls in Mtwara and Lindi with sanitary pads that has resulted in an increase in school attendance. 

As the leading economic contributor in Tanzania, agriculture employs over 70% of the population and according to the Ministry of Health, women make up 52% of the labor force in the sector. Vodacom’s Women Farmer Networks has empowered women in the agriculture sector through skills development programs and providing access to capital and markets using mobile technology. 

The network reaches women’s cooperatives in nearly 300 projects in the Northern zone and have recorded remarkable success such as financial independence, awareness of best practices and unlocked opportunities to other economic activities such as livestock keeping and significantly triggered financial inclusion of women. 

Mobile technology has the muscle to substantially bring about the socio-economic transformation of communities. However, it is important for women to be included from the inception phase of these technologies and provide solutions that cater to their needs

WANAHABARI TABORA WAPIGWA MSASA ELIMU YA AFYA UZAZI, MAMA NA MTOTO

$
0
0
WIZARA ya Afya kwa kushirikiana na Mradi wa USAID Tulonge Afya fhi 360 wametoa mafunzo kwa wanahabari mkoani Tabora juu ya utoaji habari baada ya uzinduzi wa majukwaa mawili ya mawasiliano ya afya kwa watu wazima ‘NAWEZA’ na vijana ‘SITETELEKI’ yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Majukwaa hayo yanalenga kufikisha elimu sahihi itakayoijengea jamii ya Watanzania uwezo ili kubadilisha mitizamo na tabia zao za kiafya na kuleta matokeo chanya.

Mafunzo hayo yamendeshwa na wataalamu wa masuala ya afya kutoka Wizara ya Afya na USAID Tulonge Afya fhi 360 yalifanyika leo katika Hotel ya Rastalemi mjini Tabora na kupata mwitikio mkubwa na uelewa mzuri kwa wanahabari wa mkoani humu yakiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa majukwaa hayo ya NAWEZA na SITETEREKI mkoani humo.

Mtaalamu wa mambo ya Afya kutoka Wizara ya Afya, Oscar Kapera alisema NAWEZA ni jukwaa linalolenga kuwafikia wananchi tofauti tofauti na itachangia kuboresha afya na ustawi wa Watanzania wengi, itakuwa ikibadilika badilika ili kukidhi mahitaji ya maeneo mengine ya kiafya muhimu kwa walengwa hao ama makundi mengine hususani watu wazima.
 Meneja wa Fhi Tulonge Afya Kanda Kaskazini na Kati, Dkt. Benedict Kafumu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA ITETELEKI. Mafunzo hayo yamefanyika leo katika Hoteli ya Ristalemi mjini Tabora.
 Afisa wa Afya kutoka Wizara ya Afya, Oscar Kapera akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ​mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI.Mafunzo hayo yalifanyika leo katika Hoteli ya Ristalemi mjini Tabora.
Mtaalamu Mkongwe wa Ushauri wa mambo ya Afya kutoka Fhi Tulonge Afya, John Bosco Basso akizungumza jambo wakati wa ​mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI.  


Tanzania Day 2019

MIRIAM ODEMBA NDANI YA TANZANITE WOMEN FORUM & LUNCH

$
0
0
Mwanamitindo wa Kimataifa, Miriam Odemba akiwa katika Mavazi ya Wabunifu wa mitindo mbalimbali wa Tanzania akiwemo Khadija Mwanamboka, Irada style na Katty Collection


Kuna msemo unasema “Asiyemshukuru Binadamu mwenzie kamwe hawezi kumshukuru Mwenye Mungu”. JUKWAA LA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI MKOA WA DAR ES SALAAM (JUWADA), kwa kushirikiana na Mbunifu wa Mavazi maarufu BI.KHADIJA MWANAMBOKA kwa pamoja tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote walioshirikiana nasi kwa hali na mali kuhakikisha tunafanikisha tafrija yetu ya “Tanzanite Women Forum & Lunch 2019”.

Kwa hakika kungekuwa na maneno zaidi ya kusema ‘Asanteni Sana’ basi tungeyatumia hayo kuonyesha ni jinsi gani tunathamini na kutambua msaada wenu katika kufanikisha shughuli yetu ambayo ilikuwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kufungua sehemu ya kuwapatia ujuzi tofauti wanawake wa Jukwaa. Kwa kupitia programme ya Bi Khadija Mwanamboka “Ujuzi Initiative”wanawake hawa watapatiwa Ujuzi mbalimbali wa mikono. Kipekee kabisa JUWADA tunamshukuru sana Bi Khadija Mwanamboka kwa kukubali kushirikiana nasi na zaidi kazi kubwa aliyoifanya kufanikisha “Tanzanite Women Forum & Lunch 2019”.

Kwa umuhimu wa pekee tunaomba kutoa shukrani zetu kwa kila mmoja wenu . Tunaomba kuanza kwa kuwashukuru wadhamini wetu wakuu walioweza kufanikisha shughuli yetu ambao ni ANUFLO INDUSTRIES LTD kupitia product ya “HEDHI MENSTRUAL CUP”. Tunawashukuru sana SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha eneo la kusomea wanawake hao.

Lakini pia tunaomba kuwashukuru wadhamini wengine wote ambao waliweza kwa namna moja ama nyingine kufanikisha shughuli yetu WAKIWEMO I4ID INCLUSIVE DEVELOPMENT, DARLING HAIR TANZANIA, COOL BLUE PURE DRINKING WATER. Tunaomba kuwashukuru kipekee wanawake waliojitolea thamani zao kwa ajili ya kufanya mnada akiwemo LEY JEWELLERS asante sana kwa seti ya Tanzanite. JACQUELINE MASSAWE JEWELLERS tunakushukuru sana kwa kututengenezea “Uhuru Wings” ambayo ni mkufu wa kipekee, NYUMBANI DADAZ NA ROSE VALENTINE asante sana kwa Maasai jewellery nzuri. Grano Foods Ltd na Rona products tunawashukuru mno kwa kutoa zawadi kwa wanawake.

Kipekee tuwashukuru wabunifu wa mavazi ambao mlifanya kazi kubwa sana kufanikisha show yetu akiwemo IRADA STYLE, MALIKA DESIGNER, ASYA KHAMSIN, KATTY COLLECTION, MUSTAFA HASSANALI, MGESE CICI DESIGNS NA ZAMDA GEORGE asanteni sana. Marafiki zetu na wadau wa maendeleo mliojitolea muda wenu mwingi kuhakikisha shughuli yetu inafana akiwemo Shamim Mwasha wa 8020Fashions na Mbunifu wa mavazi Martin Kadinda. Wanamuziki chipukizi Abby Sollo na Mwalimu Habiba Lyengite. Hatuna cha kuwalipa zaidi ya Shukrani. WASAFITV, Tanzanite Women Forum ya mwaka huu ndio ilikuwa ya kwanza kufanyika nanyi mkatupa heshma kubwa isyo kifani ya kuturusha LIVE kwa muda wote wa shughuli, ASANTENI SANA. MIRIAM ODEMBA kwako hatuna la kusema zaidi ya shukrani nyingi mno. Umekuja kutoka Paris kwa ajili ya “Tanzanite Women Forum & Lunch 2019”, na haukutaka chochote kutoka kwetu. Ubarikiwe kwa moyo wako wa kujitolea kwa ajili ya wanawake wenzio. Mwenyezi Mungu akuzidishie kila lenye kheri nawe. Kwa Wanawake wa Dar Es Salaam hususan wale wote mlioweza kujitokeza na kuja kutuunga mkono. Tunaomba mtambue shughuli isingefana bila ya uwepo wenu, hivyo tunawathamini na Kuwapenda sana. Asanteni sana kwa kuja. Tunatambua kwamba katika shughuli hakuwezi kila kitu kwenda sawa, hivyo kama kwa aina yeyote ile tuliwakwaza basi tunaomba Samahani kwani sisi ni binadamu na hakuna aliekamilika kati yetu.
Miriam Odemba akiwa katika mkufu wa kipekee "UHURU WINGS" uliotengenezwa na mbunifu wa madini Jacqueline Masssawe Jewelrs






TANZANIA NA BRAZIL ZAINGIA MAKUBALIANO YA KUINUA ZAO LA PAMBA NCHINI .

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus

Tanzania na Nchi ya Brazil zimeingia makubaliano ya kufufua na kuinua upya Kilimo cha  Pamba Nchini, ili zao hilo liweze kuwa na tija kwa kumnufaisha Mkulima na Taifa kwa ujumla.

Makubaliano hayo baina ya Nchi za Tanzania, Burundi, Kenya na Brazil  yameingiwa mapema Machi 1, 2019 Jijini Mwanza katika Ukumbi wa Belmont Hotel katika Mkutano maalum wa kuinua kilimo cha Pamba "Victoria Cotton Project" ambapo mradi huo utajikita zaidi kuhakikisha wakulima wa zao hili Nchini na Nchi Wadau wanapata pembejeo bora na kwa wakati ,pia uzinduzi wa utafiti unamfikia Mkulima ili aweze kuongeza tija.
 Mh. Innocent Bashungwa Naibu Waziri wa Kilimo, akiwa na baadhi ya wajumbe pamoja na wadau wa zao la Pamba kutoka ndani na nje ya Nchi, wakati walipotembelea moja ya mashamba ya Pamba Jijini Mwanza.
 Pichani ni Balozi wa Brazil Nchini Tanzania Antonio Augusto Martins akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Uzinduzi wa Mradi wa Kuinua Kilimo cha Pamba,(hawapo pichani) uliofanyika Jijini Mwanza, Pembeni ni Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa.
 Sehemu ya Wajumbe wakiohudhuria Uzinduzi wa Mradi wa Kuinua Kilimo cha Pamba "Victoria Cotton Project" wakifuatilia Mkutano huo Jijini Mwanza.
Pichani ni Naibu Waziri wa Kilimo Nchini, Innocent Bashungwa akichangia katika Mkutano maalumu wa Victoria Cotton Project uliozinduliwa Machi 11, 2019. Jijini Mwanza na kuzishirikisha Nchi za Kenya, Burundi na Brazil.

BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA KATIKA WILAYA YA DIMANI UNGUJA.

$
0
0

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania(UWT), Ndugu Gaudensia Kabaka amewataka Akina Mama katika Wilaya ya Dimani kicha Unguja kufanya maandalizi ya kina ya kisiasa yatakayoleta ushindi wa CCM mwaka 2020.

Rai hiyo aliitoa katika ziara yake wakati akiwahutubia Akina Mama wa UWT wa Wilaya hiyo katika Afisi za Umoja huo huko Kiembe Samaki Zanzibar.

Alisema Akina Mama wanatakiwa kujipanga vyema kwa kuhakikisha CCM inashinda na kuendelea kuongoza Dola katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Alieleza kwamba tayari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa asilimia 97 hivyo kazi iliyobaki, kwa akina Mama hao ni kunadi, kutangaza na kueneza Sera za maendelezo zinazotekeleza na Chama pamoja na Serikali.

Alieleza kuwa maendeleo yaliyopatikana kwa CCM yamechangiwa na busara na nguvu za Akina Mama kwani wameanza harakati za kupigania uhuru na maendeleo ya Nchi toka enzi za ASP na TANU toka Uongozi wa Marehemu Mzee Abeid Karume na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Aliwambia kuwa ni lazima wanawake waliende hadhi na heshima zao katika kusimamia ukweli na Falsafa za za Uongozi bora zilizoasisiwa na Akina Mama waasisi wa UWT toka ilivyoanzishwa.

Alisema kuwa pamoja na majukumu waliyokuwa nayo katika Medali za Kisiasa ni lazima waendeleze ubunifu katika kufanikisha kwa vitendo Sera ya Siasa na Uchumi Nchini, kwa kufanya ujasiriamali ili wajiongezee kipato.

Akizungumza na Akina Mama wa Kanisa la Anglicana huko Mbweni aliwapongeza kwa juhudi zao za kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi.

Aliwambia kuwa Chama cha CCM hakina ubaguzi wa kidini kwani kinapokea na kufanya kazi na wanachama wa dini zote, hatua inayokitofautisha na Vyama vingine vinavyoanzishwa kwa misingi ya kidini.

Aliwasihi Akina Mama hao kuendeleza umoja na mshikamano wa kudumu kwa kushirikiana katika masuala mbali mbali ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndungu Thuwaiba Kisasi ameeleza kwamba Akina Mama hao wa kanisa la Anglicana wamekuwa wanachama waaminifu na wachapakazi kwa kipindi chote na wenye msimamo usioyumba.

Naye Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mwl. Queen Mlozi aliwataka wazazi na walezi kusimamia malezi ya Watoto wa Kike ili wapate haki ya Elimu bila vikwazo.

Amesema watoto wa Kike wasiposaidiwa na kulelewa katika mazingira salama hapatopatikana wataalamu na viongozi jasiri na wachapakazi nchini hivyo wanastahiki kulindwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi Ndugu Zainab Ali Maulid, alisema wanawake wa Mkoa huo wamekuwa mabalozi waaminifu wa kulinda na kutetea maslahi ya CCM kwa vitendo.

Katika risala ya Wilaya hiyo Akina Mama hao wamesema CCM imeendelea kuwa na mvuto na kupendwa na wananchi kutokana na Utekelezaji Mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 inayotekelezwa vyema kwa wananchi wote.
 MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akikagua bidhaa zinazotengenezwa na Akina Mama wa Kanisa la Anglicana huko Mbweni Zanzibar.
 WANAWAKE wa Kanisa la Anglicana wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka aliyefika katika Kanisa hilo kwa ajili ya kuwasalimia Akina Mama hao na kukagua vikundi vya ujasiriamali.
 MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akivishwa sikafu na Vijana wa Kikundi Maalum cha UVCCM Wilaya ya Dimani Kichama Unguja mara baada ya kuwasili katika Afisi za Wilaya hiyo kwa ajili ya ziara.
WANAWAKE wa UWT wakiwa Katika ukumbi wa  Afisi ya UWT  Kiembesamaki wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti  wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka katika Kikao cha ndani.

OHOOOOO... ZIDANE AREJEA REAL MADRID KAMA KOCHA

$
0
0
 Zinedine Zidane amerejea Real Madrid kama kocha mkuu akichukua nafasi ya Santiago Solari. Zidane ambaye aliipa Madrid ubingwa wa Ulaya mara tatu mfululizo amesaini mkataba wa miaka mitatu unaomalizika mwaka 2022. Zidane aliachana na Madrid Mei 31, 2018.

DEATH ANNOUNCEMENT

Ushauri wa Bure: ANGALIA UMRI WAKO, UPO SAHIHI? UMEKOSEA? UNAHITAJI KUJIREKEBISHA?

$
0
0
NA REV KADIVA

*20 - 25* = Kama ni kielimu hujafikia malengo yako, sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya, pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.

*25 - 30* = Hakikisha uwe na angalau KAZI RASMI kama umeajiriwa au umejiajiri au una shughuli yeyote ya kukuingizia kipato.

*30 - 35* = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja, tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa. Ni vema ukiwa na familia, kwa maana ya kuwa na watoto kama Mungu kakuwezesha.

*35 - 40* = Ni wakati kiwanja kiwe kimejengwa na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia. Hapa inabidi upambane sana kuweka misingi.

*40 - 45* = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja, kama hukujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki, ni umri wa masahihisho. Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa watoto wapo kwenye level tofauti za elimu, kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.

*45 - 50* = Kwa yule ambae hakukosea huko nyuma basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako, kama ni shughuli zako ni kuanza kuwahusisha, huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fursa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 - 40.

*50 - 60* = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na kazi zinazotumia nguvu au akili nyingi

*60 - 70* = Kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.

*70 - 80* = Kula matunda

*80* - nk = Umri wa kusubiria mauti

*Yote kwa yote, maisha yetu yapo mikononi mwa  MUNGU, kumbuka kufanya Ibada wakati wote...*

Inafaa kwa vijana hata kwetu pia ila unaweza kujaribu kujifanya kutoelewa

ZIARA YA WAZIR MKUU KASSIM MAJALIWA MKOANI KIGOMA

WAJUMBE WA BODI NA MENEJIMENTI YA BOHARI YA DAWA YA TAIFA UGANDA (NMS) WATEMBELEA MSD

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
WAJUMBE wa Bodi na Menejimenti ya Bohari ya Dawa ya Taifa,nchini Uganda (NMS) wametembelea Bohari ya Dawa (MSD)  kubadilishana uzoefu na kujifunza namna MSD inavyoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF).
Pamoja na mambo mengine Meneja Mkuu wa NMS Bwana Moses Kamabare ameipongeza MSD kwa kuboresha utendaji wake ikiwa ni pamoja na huduma zake kwa wateja na kufanya mabadiliko makubwa katika mnyororo wa ugavi.
Akizungumza na ugeni huo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Dkt. Fatma Mrisho amesema ushirikiano wa taasisi hizi mbili ni muhimu sana,hasa kwenye eneo la kubadilishana uzoefu kiutendaji, kwa nia ya kuboresha huduma.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema MSD imefanya maboresho makubwa kiutendaji,na ni siri kubwa ya mafanikio katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) Dkt. Fatma Mrisho (wa pili kulia), akiwaongoza wajumbe hao kwenda kuangalia Ghala la kuhifadhia dawa na vifaa tiba la MSD Keko jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) Dkt. Fatma Mrisho (katikati) akimkabidhi zawadi  Meneja Mkuu wa NMS,  Bwana Moses Kamabare baada ya kutembelea MSD Dar es Salaam leo. Anayeshuhudia kushoto mwenye suti ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) Dkt. Fatma Mrisho, akizungumza na ujumbe huo.
Ujumbe huo ukiwa katika ghala la kuhifadhia dawa la MSD Keko jijini Dar es Salaam.

WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI TANESCO WATUA RUKWA KUKAGUA MIRADI YA UMEME

$
0
0
 Meneja wa Shirika la umeme, TANESCO mkoa wa Rukwa, Frank Chambua (kushoto), akitoa maelezo kuhusu upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme katika mkoa huo kwa viongozi wa bodi ya Tanesco nchini walioongozwa na makamu mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi Dkt. James Nzagi, (mwenye shati ya mabaka) mara baada ya kutembelea kituo  cha kupooza umeme kilichopo eneo la majengo mjini Sumbawanga. 
Meneja wa Shirika la umeme TANESCO mkoa wa Rukwa, Frank Chambua (kulia), akitoa maelezo kuhusu upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme katika mkoa huo kwa viongozi wa bodi ya Tanesco nchini walioongozwa na makamu mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi James Nzagi, leo mara baada ya kutembelea kituo  cha kupooza umeme kilichopo eneo la majengo mjini Sumbawanga. 
 Mdhibiti mifumo ya umeme wa TANESCO mkoa wa Rukwa, Halfan Seba (kulia), akitoa maelezo  kuhusu uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme katika mkoa huo kwa viongozi wa Bodi ya Tanesco nchini walioongozwa na Makamu mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi James Nzagi, leo mara baada ya kutembelea kituo hicho kilichopo eneo la majengo mjini Sumbawanga.
 Mdhibiti mifumo ya umeme wa TANESCO mkoa wa Rukwa, Halfan Seba (kulia), akitoa maelezo  kuhusu uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme katika mkoa huo kwa viongozi wa Bodi ya Tanesco nchini walioongozwa na Makamu mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi James Nzagi, leo mara baada ya kutembelea kituo hicho kilichopo eneo la majengo mjini Sumbawanga.
 Makamu mwenyekiti wa bodi ya shirika la umeme nchini (TANESCO), Balozi Dkt. James Nzagi  akiambatana na wajumbe wengine wa bodi hiyo kukagua eneo lililotengwa kwa ajili ya  kujengwa kwa kituo cha kupoza umeme wa gridi ya taifa mkondo KV 411 lililopo katika kata ya Malangali mjini Sumbawanga Machi 11, 2019 wakati wa ziara ya viongozi wa bodi hiyo mkoani hapa kukagua miundombinu ya Shirika ikiwa ni pamoja na kuangalia hali ya upatikanaji wa umeme.
 Makamu mwenyekiti wa bodi ya shirika la umeme nchini (Tanesco), Balozi Dkt. James Nzagi (katikati), akitoa maelekezo kwa watendaji wa shirika hilo mkoa wa Rukwa mara baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha na kusambaza umeme cha mjini Sumbawanga wakati wa ziara ya viongozi wa bodi ya shirika hilo.
Makamu mwenyekiti wa bodi ya shirika la umeme nchini (Tanesco), Balozi Dkt. James Nzagi (kulia), akitoa maelekezo kwa watendaji wa shirika hilo mkoa wa Rukwa mara baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha na kusambaza umeme cha mjini Sumbawanga wakati wa ziara ya viongozi wa bodi ya shirika hilo.

NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AGAWA TANI MOJA NA NUSU YA SARUJI KIPAWA

$
0
0
 Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akizungumza na wakazi wa Kipawa na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Kabla ya kugawa Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kipawa ambayo inatraji kufanyiwa ukarabati.
 Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa  akikabidhi mifuko 30 ya Saruji kwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Kipawa kwa ajili ya kukarabati ofisi za Chama hicho.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala(UWT),Amina Dodi akitoa neno kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza.
 Katibu Mkuu wa Umojha wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala,Bora Hassan akitoa utambulisho wa Viongozi wa meza kuu.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Kipawa Adiriano Komba akizungumza na kutoa shukrani kwa niaba ya wakazi wa Kipawa.
Wananchi wa Kipawa waliohudhuria katika Mkutano wa Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa (PICHA ZOTE NA HUMPHREY SHAO)

WAFUNGA NDOA WODINI BAADA YA BWANA HARUSI KUSHAMBULIWA NA MAJAMBAZI JANA YAKE

$
0
0
 Na Sultani Kipingo
Wapenzi wawili mjini Cape Town, Afrika ya Kusini, wamefunga ndoa hospitalini siku moja baada ya bwana harusi kushambuliwa na majambazi nyumbani kwake .

Muneer Hercules na Maryam Kallie walifunga pingu za maisha katika hospitali ya Melomed Gatesville Jumapili Machi 10, 2019, huku bwana harusi akiwa kitandani na Bi harusi pembeni yake.

Kwa mujibu wa ukurasa wa Facebook wa Melomed Gatesville, Hercules alikimbizwa hospitalini hapo baada ya kujeruhiwa na majambazi nyumbani kwake Jumamosi Machi 9.

"Asubuhi hii Muneer Hercules na Maryam Kallies wamefanya Nikkah mbele ya watu wa familia zao hapa  Melomed Gatesville Hospital. Muneer alishambuliwa usiku wa kuammia leo na kukimbizwa hospitali.” Ameandika  Melomed.

Hata hivyo, shambulizi hilo halikuzuia wapenzi hao kuoana kwa taratibu za Kiislamu hapo hospitali, na mapicha kibao yaliyo kwenye ukurasa wa Melomed yanaweza kukufanya utokwe na chozi.

Maryam alikuwa amevaa shela lake nzuri nyeupe huku mkononi kashikilia maua wakati akiingia hospitalini hapo, wakati mumewe mtarajiwa akiwa anasubiri kwa hamu kitandani huku akipigana na maumivu, bila shaka akimshukuru Mola kwa kumjaalia mwenza atayeishi naye kwa shida na raha. 

 Muneer Hercules na Maryam Kallie wakikumbatiana baada ya kufunga za maisha katika hospitali ya Melomed Gatesville Jumapili Machi 10, 2019, 
Muneer Hercules na Maryam Kallie walifunga pingu za maisha katika hospitali ya Melomed Gatesville Jumapili Machi 10, 2019, 
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images