Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

TUNDURU WAFANIKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOKUWEPO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WILAYA ya Tunduru imefanikiwa kumaliza changamoto mbalimbali kwa baadhi ya shule za sekondari wilayani humo ikiwemo ya ukosefu wa vitanda katika Shule ya Sekondari Namasakata .

Kutatuliwa kwa changamoto hiyo kunatokana na jitihada mbalimbali ambazo zimewekwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera kwa kushirikiana na timu ya wataalam wa Wilaya na wananchi.

Akizungumza na Michuzi Blog jana Machi 10,2019 ,Mkuu wa Wilaya hiyo Homera amesema kuwa katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo wametumia fursa ya uwepo wa mfuko wa elimu kutokana na mazao mbalimbali yanayolimwa wilayani hapo.

Amefafanua kuwa wadau wa zao la ufuta waliridhia kukatwa mkulima sh.30 kwa kila kilo na kufanikiwa kukusanya zaidi ya Sh.milioni 27 ambazo zimetumika kutengeneza miundombinu kama vile kujenga vyoo vya walimu Namwinyu sekondari, na kutengeneza vitanda 58 (double deka).

Pia ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari Namasakata na kufanikiwa kuwapatia vitanda wanafunzi 116 kwa wakati mmoja. Aidha Homera amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Tunduru Gasper Balyomi kwa usimamizi thabiti wa fedha zinazochangwa na wananchi kupitia mazao yao na harambee mbalimbali.

Hata hivyo Homera na timu yake wamefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh. milion 60 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari ambazo na Serikali kuu kuunga mkono nguvu za wananchi kwa kuiletea Sh.milion 137.5 ili kukamilisha madarasa hayo na samani zake.

"Tunawashukuru wadau wa maendeleo,wananchi wa Tunduru kutokana na kila aina ya ushirikiano ambao wanautoa kuhakikisha tunaondoa changamoto katika sekta ya elimu. Meza na viti).#Tukutane site ,Tukutane Kazini#," amesema Homera. 
 Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera akizungumza jambo kwenye moja ya kikao cha kuhakikisha kinafanikiwa kumaliza changamoto mbalimbali kwa baadhi ya shule za sekondari wilayani humo ikiwemo ya ukosefu wa vitanda katika Shule ya Sekondari Namasakata .
 


TCAA YATOA SALAMU ZA POLE KUFUATIA AJALI YA NDEGE YA ETHIOPIA

SPIKA WA BUNGE LA EAC AKUTANA NA TAASISI YA DORIS MOLLEL KUZUNGUMZIA WATOTO NJITI

0
0
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Martin Ngoga (katikati) akipokea picha maalum yenye kuonyesha uhalisia wa Mtoto Njiti, kutoka kwa Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (kulia) mara baada ya kukutana na kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu hali ya Watoto Njiti kwa ukanda wa Afrika Mashariki, katika kikao kilichofantika kwenye ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe aliyeambatana na Taasisi hiyo.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Martin Ngoga (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na Taasisi ya Doris Mollel kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu hali ya Watoto Njiti kwa ukanda wa Afrika Mashariki, katika kikao kilichofantika kwenye ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel na kulia ni Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe aliyeambatana na Taasisi hiyo.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel akizungumza jambo wakati wa kikao na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Martin Ngoga, kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu hali ya Watoto Njiti kwa ukanda wa Afrika Mashariki, katika kikao kilichofantika kwenye ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar mwishoni mwa wiki.
Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe akizungumza wakati akitolea ufafanuzi hali ya Watoto Njiti katika kikao cha pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.




KAMPUNI YA BIMA YA UAP OLD MATUAL YATOA MSAADA WA MABEGI 400 KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU

0
0
Meneja Uendelezaji Biashara na Masoko wa Kampuni ya bima ya UAP Old Mutual Tanzania Jabir Kigoda ( wa tatu kulia) akikabidhi sehemu ya mabegi 400 ya shule kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk. Ave Maria Semakafu ( wa nne kushoto) , iliyotolewa na UAP kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu katika hafla iliyofanyika Muheza mkoani Tanga. Anayeonekana nyuma ya Naibu Katibu Mkuu ( mwenye hijab) ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo.

Na Ripota Wetu, Globu  ya jamii

KAMPUNI ya Bima ya UAP Old Mutual Insurance Tanzania imetoa msaada wa mabegi 400 ya shule ya kuwekea vitabu na madaftari kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanaosoma katika shule zilizopo wilayani Muheza mkoani Tanga.

Akizungumzia msaada huo, Meneja Uendelezaji Biashara na Masoko wa UAP Jabri Kigoda amesema lengo la msaada huo ni kunyanyua ushiriki wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum nchini.

Msaada huo umekabidhiwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu . "Kampuni ya UAP tunaamini elimu si tu ni nguzo ya mafanilkio ya binadamu, bali pia ni haki ya msingi ya mtoto, wakiwemo wenye mahitaji maalum kama hawa,"amesema Kigoda.

Pia Kigoda amewaomba wadau wa maendeleo nchini kuwa mstari wa mbele kutoa misaada yenye lengo la kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu walioko shuleni."Tunakila sababu kusaidia sekta ya elimu hasa kwa kutambua Serikali imebeba jukumu la kutoa elimu bure.

" Amefafanua kampuni ya UAP yenye matawi maeneo mbalimbali nchini ikiwamo Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Kahama, Zanzibar, Morogoro na Mtwara ni moja kati ya kampuni iliyoweka kipaumbele kuwekeza kwenye misaada ya kuchangia maendeleo ya jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo akizungumza katika hafla hiyo ya makabdhiano.Kulia kwake ni Meneja wa Uendelezaji Biashara na Masoko wa UAP Jabir Kigoda, na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr. Ave Maria Semakafu.
Meneja Uendelezaji Biashara na Masoko wa Kampuni ya bima ya UAP Old Mutual Tanzania , Jabir Kigoda ( wa tatu kulia) akikabidhi sehemu ya mifuko 400 ya shule kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk. Ave Maria Semakafu ( wa tatu kushoto) , iliyotolewa na UAP kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu katika hafla iliyofanyika Muheza, Tanga. Anayeonekana nyuma ya Naibu Katibu Mkuu ( mwenye hijab) ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo.
Watoto wenye mahitaji maalum wakiwa kwenye picha ya pamoja na naibu katibu mkuu, mkuu wa wilaya na viongozi wa UAP baada ya kupokea msaada.

VIJANA WA ARUSHA WASHIRIKI KUKUZA MBINU ZA UJASIRIAMALI

0
0
Na Ahmed Mahmoud, Arusha.

Majukwaa ya Vijana yaliyoko katika kata mbalimbali za Wilaya ya Arusha yameshiriki katika maonyesho ya Ujasirimali yaliyoandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la Infoy ambapo vijana hao wameonyesha shughuli za ufugaji wa samaki na bidhaa za usindikaji.

Mratibu wa Shirika lisilokua la kiserikali la INFOY, Laurent Sabuni alisema kuwa Maonyesho hayo yanalenga kuhimiza ushiriki wa vijana katiika uchumi wa viwanda na kuongeza kuwa kutokana na vijana kuchangamkia fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo suala la vifungashio linapaswa kutiliwa mkazo ili kuinua ari ya uzalishaji .

Sabuni alisema kuwa Majukwaa ya vijana ni moja ya njia muhimu ya kuwakusanya vijana na kuwaweka pamoja ili waweze kupata mafunzo ya ujasiriamali pamoja kuwafikia vijana wengi ambao wana nia ya kusonga mbele kiuchumi.

“Vijana wakiwa katika vikundi ni rahisi kusaidika tofauti na kuwafikia kijana mmoja mmoja inakua ngumu hivyo ni vyema vijana wakajiunga kwenye vikundi” Alieleza Sabuni

Mjasiriamali Goodness Shayo Alisema kuwa maonyesho hayo yatasaidia kuinua ari ya vijana kujikita katika shughuli za uzalishaji badala ya kuwa walalamikaji na pia kuondokana na kasumba ya kuchagua kazi.

Alisema kuwa mkoa wa Arusha vijana wamekua wakizalisha bidhaa mbali mbali licha ya uhaba wa viwanda vya kutengeneza vifungashio vya bidhaa suala linalowazimu kuagiza kutoka mikoa mingine hivyo kuongeza gharama za usafirishaji na kuathiri bei ya bidhaa zao katika soko.

Goodness ameiomba serikali na taasisi binafsi kuungana kutatua changamoto hiyo kwa kuanzisha viwanda vya kutengeza vifungashio kutokana na mwamko wa vijana wa kuchangamkia fursa za uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya usindakaji wa nafaka.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabiel Daqqaro akipata Maelezo juu ya bidhaa zinazozalishwa na vijana kutoka Majukwaa ya Vijana Wilaya ya Arusha yaliyoandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la INFOY. Picha na ahmed mahmoud Arusha

CHECHE ATAMBA USHINDI WA AZAM NI KUCHEZA NA AKILI ZA WACHEZAJI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KOCHA wa muda wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amesema kuwa timu hiyo ina matokeo mazuri hivi sasa kutokana na kufanikiwa kucheza na akili za wachezaji.

Azam wamefaniiwa kupata ushindi wa goli 6-1  dhidi ya  JKT Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.


Ameyasema hayo baada ya kufanikiwa kuondoka na ushindi mnono wa pili wa mabao zaidi ya mabao matano kuwahi kuupata kwenye ligi hiyo, awali iliwahi kuipiga Villa Squad mabao 6-2 msimu wa 2008/2009.


Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Cheche anayesaidiana na Meja Mstaafu, Abdul Mingange, ameuambia mtandao rasmi wa klabA alisema kama ukishindwa kucheza na akili za wachezaji basi unaweza kuwa na wachezaji wazuri lakini ukashindwa kuwatumia.

“Unaweza ukaja na mazoezi mengi lakini ukaja na vitu vingi lakini bila kucheza na akili zao mafanikio yanakuwa ni magumu,” alisema

Akizungumzia ushindi huo mnono, licha ya ubora wa timu ya JKT Tanzania, ikiwa ngumu kufungika, Cheche alisema kuwa: “Mimi nasema kwenye mpira linawezekana, kama Brazil waliweza kufungwa goli saba kwao, kwanini JKT wasifungwe goli sita?,” alihoji Cheche.

Huo ni ushindi wa tatu mfululizo kwa kikosi hicho kikiwa chini ya makocha hao wa muda, awali ilitangulia kuzichapa Rhino Rangers (3-0) kwenye kombe la FA na kutinga hatua ya robo fainali kabla ya kuinyuka African Lyon 3-1 kwenye mchezo wa ligi.

Mara baada ya mchezo huo kikosi cha Azam FC, kinatarajia kurejea mazoezini leo Jumatatu, kuanza maandalizi ya kuikabili Singida United, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Machi 16  huu saa 1.00 usiku. 

Mabao ya Azam  yamewekwa kimiani na mshambuliaji Donald Ngoma, aliyetupia mawili, nahodha Agrey Moris, Obrey Chirwa, Mudathir Yahya na Danny Lyanga.

MAHAKAMA YAWATAKA WADHAMINI WA MSHTAKIWA ZITTO KABWE KUFIKA MAHAKAMANI APRILI 9

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaamuru wadhamini wa Zitto Kabwe pamoja na yeye mwenyewe kufika mahakamani hapo Aprili 9, 2019 na kujieleza kwa nini mshtakiwa Zitto leo hajafika mahakamani.

Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakamani hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Mapema, Wakili wa serikali Wankyo Simon alidai kuwa kesi dhidi ya Zitto leo Machi 11, 2019 imekuja kwa ajili ya kutajwa, na wana dhahidi mmoja ambaye yuko tayari kutoa ushahidi wake lakini mshtakiwa Zitto hayupo.

Hata hivyo, Wakili anayemtetea Zitto, Steven Mwakibolwa amedai kuwa amepata taarifa kutoka kwa ndugu yake Zitto, Vincent Kasafa kuwa Zitto ni mgonjwa, ambapo alipotakiwa na mahakama kueleza, mtoa taarifa hiyo, amedai kuwa yeye ni shemeji yake na Zitto, mke wake Zitto alimpigia simu na kumtaarifu kuwa Zitto anaumwa lakini yeye hajui yuko wapi.

Baada ya taarifa hiyo, Hakimu Shahidi amemwambia, "umepewa taarifa huna hakika, tusitafutane maneno, wadhamini siku ya kesi wafike mahakamani na waeleze kwa nini leo hawajafika", pia hakimu Shaidi amemuonya Shahidi ASP Shamira Nkoma kufika Aprili 9,2019 mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi.

Zitto ambaye yupo nje kwa dhamana, katika kesi hiyo, anadaiwa Oktoba 28, mwaka jana, Zitto akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliyofanyika katika Makao Mkuu ya ofisi ya Chama cha ACT_Wazalendo alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Wanahabari Mwanza wapigwa Msasa

0
0
WIZARA ya afya kwa kushilikiana na ​Mradi wa USAID Tulonge Afya​ fhi 360 ​ wametoa mafunzo kwa wanahabari jijini Mwanza juu ya utoaji habari wakati wa maandalizi ya uzinduzi wa Majukwaa mawili ya mawasiliano ya afya kwa watu wazima litakaloitwa “NAWEZA” na kwa vijana “SITETELEKI” ili kufikisha elimu sahihi itakayoijengea jamii ya Watanzania uwezo na kubadilisha mitizamo na tabia zao za kiafya na kuleta matokeo chanya.

Mafunzo hayo yalifanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki katika Hotel ya Gold Crest ambapo yalipata mwitikio mkubwa na ulewa mzuri kwa wanahabari waishio jijini Mwanza. Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu mambo ya Afya kutoka Wizara ya Afya na USAID Tulonge Afya fhi 360.

NAWEZA ni jukwaa litakalolenga kuwafikia wananchi tofauti tofauti itachangia kuboresha afya na ustawi wa Watanania wengi, itakuwa ikibadilika badilika ili kukidhi mahitaji ya maeneo mengine ya kiafya muhimu kwa walengwa hao ama makundi mengine hususani watu wazima. SITETELEKI ni jukwaa litakalolenga zaidi kuwafikia Vijana wenye umri kati ya 15 – 24, wanaokabiliwa na changamoto nyingi za malengo ya maisha. 
 Mratibu wa Afya ya Uzazi Wizara ya Afya, Martha Shakinyau(kushoto) akizungumza na Wanahabari jijini Mwanza wakati wa mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya amajukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI.Kulia ni baadhi ya Wanahabari wa jijini Mwanza wakimsikiliza Mratibu huyo.Mafunzo hayo yalifanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa USAID Tulonge Afya, Prisca Rwezahura(kushoto) akizungumza na Wanahabari jijini Mwanza wakati wa mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI.Kulia ni baadhi ya Wanahabari wa jijini Mwanza wakimsikiliza Mratibu huyo.Mafunzo hayo yalifanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza.
Wanahabari wa Jijini Mwanza wakifuatili kwa makini mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI..Mafunzo hayo yalifanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

TUNDURU WAANZA MKAKATI WA KUMALIZA UGONJWA WA TB

0
0
HOSPITALI ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,imeanza zoezi la upimaji wa viashiria vya ugonjwa wa kifua kikuu(TB) kwa wanafunzi wa Bweni katika shule za Sekondari  kama mkakati wa kumaliza na kuzuia maambukizi kwa ugonjwa huo hasa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi.

Katika zoezi hilo, Hospitali kupitia kitengo cha kifua kikuu na ukoma,inawashirikisha baadhi ya waganga wa jadi na tiba asilia pamoja na watu waliougua kifua kikuu na kupoma kukusanya makohozi kutoka kwa watu na kupeleka hospitalini kwa ajili ya vipimo.

Mratibu wa Kifua kikuu wa Hospitali ya wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema, zoezi la kukusanya makohozi kwa wanafunzi wa shule za sekondari hasa zile za Bweni ni mpango wa Serikali kwa kushirikiana na mfadhili MDH na GLOBAL FUND ambao unakusudia kumaliza ugonjwa huo unaotajwa kuwa ni kati ya magonjwa yanayoongoza kuuwa watu wengi hapa nchini.

Alisema, katika zoezi hilo kwa kuwatumia waganga wa jadi na tiba asili ambao wanakusanya makohozi hasa katika maeneo ya vijijini na kupeleka Hospitali kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kupunguza ukubwa wa tatizo na kuokoa Maisha ya wananchi ambaao wanaumwa Tb ambapo wale wanaogundulika kupata ugonjwa huo wanaanzishiwa dawa mara moja.

Alisema, kuanzia mwezi Januari hadi Februari mwaka huu tayari wamefanikiwa kutembelea shule nne za sekondari ambazo ni Tunduru Sekondari,Muhesi,Ligoma na Nandembo ambapo wale waliobainika kuwa na viashiria vya ugonjwa huo wanashauriwa kuanza dawa.

Dkt Kihongole alisema, wameamua kufanya zoezi la upimaji wa Tb kwa wanafunzi wa shule za Bweni kwa kuwa ni rahisi sana kuambukizana kutokana na kukaa pamoja  kwa muda mrefu.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nandembo Salma Ali na Gramaki Abdala , wameishukuru Hospitali ya wilaya ya Tunduru kwa kuendesha zoezi hilo ambalo litasaidia sana kupunguza uwezekano wa kuambukizana TB n ahata wale waliopata kuanza Dawa.

Salma Ali alisema,elimu inayotolewa inayokwenda sambamba na zoezi la upimaji wa kifua kikuu kwa  wanafunzi wa shule za Bweni  ni muhimu kutokana na muingiliano uliopo na kushauri elimu  na upimaji ufanyike kila mwezi au kila mwanzo wa muhula hasa pale shule zinapofunguiwa kwani kuna wanafunzi ambao wanatoka moja kwa moja nyumbani ambao wanakwenda kuishi na wenzao bwenini.

Mmoja wa wahamishaji na mkusanyaji makohozi katika Kijiji cha Nandembo Joseph Hyera alitaja dalili za ugonjwa huo ni kutokwa na jasho,kupungua uzito na kutokwa na Damu wakati wa kukojoa.

Alisema, ili kuzuia kuenea na kuambukizwa ni vema kuepuka msongamano,kutotema mate ovyo, kuishi kwenye mazingira safi, na kupata chanjo maalum kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Alisema, dalili za TB kwa kawaida zinaanza kujitokeza kuanzia siku 30 hadi 90 kutegemea na kinga ya mwili ya Binadamu, hata hivyo njia pekee ni watu kwenda kupima Afya zao mara kwa mara na kumaliza dozi wanazopewa badala ya kuamini ugonjwa huo na Imani za kishirikina.

Hyera alisema, madhara ya ugonjwa huo ni makubwa kuliko ukimwi kwani  ni ugonjwa ambao unaambukiza kirahisi sana watu na yule asiyetumia dawa anaweza kupoteza Maisha katika kpindi cha miaka miwili.
 Mmoja wa wahamishaji makohozi wanaofanya kazi ya kukusanya makohozi kwa ajili ya vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu wilaya ya Tunduru akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Nandembo kabla ya zoezi la upimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
 Mhamishaji makohozi kutoka katika kijiji cha Nandembo Joseph Hyera akitoa elimu ya madhara ya ugonjwa wa kifua kikuu  kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Nandembo jana.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nandembo wakijaza fomu kabla ya kuanza kwa zoezi la upimaji makohozi ili kubaini waliopata ugonjwa wa Kifua Kikuu na kuanza kupatiwa Dawa zoezi linalofanywa na Idara ya kifua kikuu na ukoma katika Hospitali ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

WASTAAFU ENDELEENI KULIUNGA MKONO JESHI LA POLISI - RPC SHANA

0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Askari pamoja na watumishi raia waliolitumikia Jeshi la Polisi mpaka kufikia kustaafu wametakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kutoa taarifa mbalimbali zitakazosaidia kupambana na uhalifu.

Wito huo umetolewa na Kamanda mpya wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana jana usiku, katika sherehe ya kuwaaga wastaafu hao ambao ni Mkaguzi mmoja, askari wa vyeo mbalimbali 10 pamoja na watumishi raia wawili iliyofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi uliopo jijini hapa. 

“Ninyi ndugu zetu tunaomba muendelee kutusaidia katika azma yetu ya kupambana dhidi ya uhalifu na wakati wowote mlango ya ofisi yangu upo wazi kwa ajili ya kuwasikiliza”. Alisema Kamanda Shana ambaye aliwasili mkoani hapa juzi usiku akitokea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Aidha kamanda Shana aliahidi kuwaunga mkono TPF NET mkoani hapa na kuwataka wanawake wasikubali kunyanyaswa na kujiona wanyonge bali wanatakiwa kusonga mbele kwa ajili ya maendeleo ya familia zao huku akitoa mifano ya baadhi ya nafasi za juu za wanawake ambao wapo katika idara na taasisi mbalimbali na wameonekana wakifanya vizuri zaidi kiutendaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF NET) mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi Namsemba Mwakatobe alisema kwamba, wameamua kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuunganisha sherehe ya kuwaaga wanawake wenzao pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali.

Alisema baadhi ya wastaafu hao katika kipindi chao cha utumishi walikuwa walimu wa askari na watumishi raia waliopo hivi sasa hali ambayo imesaidia kuendelea kupata kizazi kingine kinachofanya kazi kwa ufanisi na uweledi wa hali ya juu.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja wa wastaafu Bi. Azama Libundilo ambaye alikuwa na cheo cha Staff Sajenti alisema kwamba kitendo kilichofanywa na wanamtandao huo pamoja na viongozi wa Polisi mkoa,cha kuwathamini wastaafu kinapaswa kuigwa na ofisi zote ambazo hazina utamaduni huo kwani kinawatia moyo nakujiona kwamba bado ni familia ya jeshi hilo.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana akimkabidhi zawadi Sajenti mstaafu wa Polisi Rukia Msofe wakati wa sherehe ya kuwaaga wastaafu iliyoandaliwa na TPF NET Arusha na kufanyika bwalo la Maofisa wa Polisi lililopo jijini hapa (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)
   Mary Simbano  ambaye alikuwa Mhasibu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Arusha, akipewa zawadi binafsi na wanachama wa TPF NET Arusha wakati wa sherehe za kuwaaga wastaafu ambao ni  askari na watumishi raia waliokuwa wanafanya kazi mkoani hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)
 Baadhi ya Polisi wanawake ambao ni wanachama wa TPF NET Arusha wakifungua Champaign wakati wa sherehe ya kuwaaga wastaafu waliotumikia Jeshi hilo iliyofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi. (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)
 Baadhi ya wageni waalikwa wakihudumiwa chakula wakati wa sherehe ya kuwaaga wastaafu ambao ni askari na watumishi raia iliyoandaliwa na TPF NET Arusha (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha). 

ZOEZI LA UPIMAJI WA MARADHI YA MOYO LAANZA MKOANI ARUSHA

0
0
Na Vero Ignatus, Arusha
Imeelezwa kuwa 75%ya vifo vinavyotokea katika mataifa yanayoendelea ukanda wa Afrika ikiwemo Tanzania vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukizwa kwa utafiti uliofanywa 2012 na shirika WHO.
Hayo yamesemwa na Dkt Bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya inayojihusisha na magonjwa ya moyo ya JKCIA Dkt Samwel Rweyemamu katika Uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maradhi ya moyo mkoani Arusha.

Amesema kuwa kutokana na takwimu zilizofanywa 2016 wilayani simanjiro mkoa wa Manyara zinaonyesha kuwa 30%ya wanaume wote waligundulika kuwa na shinikizo la damu, hiyo ikiwa ni data zinazofanana za watu wanaoishi mjini.
 
'' Data zinaonyesha tukiweza kupambana shinikizo la damu, uzito uliokithiri, kuangalia sukari kwenye miili yetu na kupima mafuta kwenye mwili tutapunguza vifo kwa 80% '' alisema Dkt Rweyemamu

Kwa upande wa mwenyekiti wa Bodi Balozi Dkt. Ladis Komba amesema kuwa azma la AICC katika eneo la Afya lina shabiana na azma ya serikali katika kusogeza huduma bora kwa wananchi wengi zaidi

Amesema AICC itaendelea kuwa mstari wa mbele kwenye kutoa huduma za Afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na huduma ya upimaji ili kufanikisha malengo ya hospitahi hiyo na kwa Taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa AICC Elishilia Kaaya amesema kuwa kwa mujibu wa wataalam wa Afya magonjwa haya yanatokana na kubadilika kwa mtindo wa maisha ambapo watu wengi hawapati muda wa kufanya mazoezi kutokana na kuelemewa na ratiba za kazi za ofisini na kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya magonjwa haya.
 
''Magonjwa haya kwa bahati mbaya hayaonyeshi dalili za wazi na hivyo ni vigumu kwa mtu anayeugua maradhi haya kujitambua mapema hivyo kuchelewa kupata matibabu, na mara nyingi imepelekea watu wengi kupoteza maisha ghafla na wengine kupata ulemavu wa kudumu''alisema

Zoezi hilo la upimaji wa Afya ya moyo linatarajia kuchukua wiki moja kuanzia tarehe 11-18 marchi, hivyo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupima afya ya moyo pamoja na shinikizo la damu.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Samwel Rweyemam kutoka JKCI akimpima Mwenyekiti wa Bodi AICC Dkt. Ladis Komba leo Jijini Arusha katika uzinduzi wa upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Samwel Rweyemam kutoka JKCI akimpima Kaimu mkurugenzi wa AICC Mkunde Senyagwa Mushi leo Jijini Arusha katika uzinduzi wa upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuja kupima afya zao leo katika uzinduzi wa upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus

ABDALLA SHAIBU 'NINJA', TINOCO WASIMAMISHWA MECHI TATU

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
SHIRIISHO la mpira wa miguu nchini (TFF) kupitia Kamati ya Nidhamu ya TFF imetoa hukumu baada ya kuwatia hatiani wachezaji wa Abdallah Shaibu na Benedict Tinoco kwa kuwakuta na hatia ya kutenda makosa ya utovu wa nidhamu.

Kamati ya nidhamu imemkuta na hatia Ninja kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa timu ya Coastal Union kwenye mchezo wa ligi kuu (TPL) na Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF.

Katika maamuzi mengine Kamati ya nidhamu ya Nidhamu ya TFF, imemtia hatiani Mchezaji wa Mtibwa Sugar Benedict Mlekwa Tinoco kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa timu Biashara United Fc aliyekuwa ameanguka baada ya kuchezewa rafu, Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF.

Mbali na hilo, Kamati pia imetoa maamuzi kwenye mashauri mengine kwa Simba na Yanga wote wakipigwa faini kwa makosa waliyoyafanya katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, uliowakutanisha Februari 16 mwaka huu.

Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema kuwa kulikuwa na vitendo vya ajabu katika mchezo huo kitu ambacho kilipelekea kamati ya masaa 72 kukaa na kutoa maamuzi juu ya Vilabu hivyo.

Kwa upande wa Klabu ya Yanga imepigwa faini ya milioni 6 kwa kosa la kuingia Uwanjani kwa mlango usio rasmi pia kutoingia vyumbani na kusababisha wachezaji kukaguliwa wakiwa koridoni.

Klabu ya Simba pia imepigwa faini ya milioni 3 kwa kuingia Uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.

Mauzo ya moja kwa moja yanazidi kuongezeka Afrika Mashariki

0
0

Mauzo ya moja kwa moja yanazidi kuongezeka Afrika Mashariki wakati vijana wenye ujuzi wa teknolojia wakitafuta fursa mpya za ujasiriamali. 

· QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inaimarisha soko la kanda kwa kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na kukuza ari mpya ya ujasiriamali. 

Mauzo ya moja kwa moja (maafuru kama network marketing) yanakuwa kwa kasi katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara ya Afrika na hasa Afrika Mashariki, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limesababishwa na ongezeko la idadi ya watu katika kanda hii pamoja na vijana mahiri ambao kwa mujibu wa taarifa ya Uchambuzi wa Ongezeko la Vijana ya Taasisi ya Maendeleo ya Afrika - sasa Afrika Mashariki ina zaidi ya 45% ya vijana kati ya watu milioni 150 walioko Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda. Wengi wa vijana hawa wana elimu, kwa ujumla wana ufahamu wa teknolojia, wepesi kufuata mienendo mipya, wana hamasa ya kuweka juhudi na fikra za ujasiriamali - jambo ambalo ndio sifa ya awali ya mafanikio endelevu katika biashara ya uuzaji wa moja kwa moja. 

Kwa wanaoanza, mauzo ya moja kwa moja ni wazo la biashara ya kimataifa na linaelezewa kama 'uuzaji wa bidhaa za matumizi au huduma, kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mtu mwingine, mbali na maeneo ya maduka ya kawaida'. Mtindo huu wa mauzo una zaidi ya miaka 100 na mwanzoni kabisa ulianzia huko USA. Leo, sasa karibu takribani watu milioni 117 wanajihusisha nayo. Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2018 ya Shirikisho la Chama cha Wauzaji wa moja kwa moja Ulimwenguni.(World Federation of Direct Selling Association (WFDSA), mauzo ya moja kwa moja yalizalisha $190 bilioni na karibu nusu ya mauzo yote yametoka katika masoko yanayochipukia: 


Inatosheleza kusema, Afrika ina chukua chini ya 1% ya jumla ya mauzo ya WFDSA lakini wataalamu wanakadiria kwamba soko la Afrika Mashariki linatoa fursa ya kukua kwa wajasiriamali wanaochipukia na hata kwa wale walioajiriwa na wana kiu ya kujipatia kipato cha nyongeza kupitia mauzo ya moja kwa moja. 

Katika kanda ambayo mahitaji ya ajira rasmi yanazidi kuwa na ushindani mkubwa na uhaba wa ajira rasmi, mauzo ya moja kwa moja yanatoa njia mbadala za ajira tofauti na ilivyozoeleka kwa wale wanaohitaji kipato cha ziada au mazingira haya ruhusu ajira. 

Akiongea hivi karibuni wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET kwa kanda ya kusini mwa Jangwa la Sahara alisema "QNET imesaidia kuwawezesha maelfu ya watuAfrika, hasa vijana, katika muongo uliopita. Tunaona ongezeko la kukubalika kwa Mauzo ya Moja kwa Moja, na idadi ya watu zaidi ya milioni 200 katika Afrika Mashariki, Mtindo huu ni mtindo unaobadilisha maisha kwa wengi" 

QNET inatoa aina mbalimbali za bidhaa za afya, ustawi na mitindo ya maisha kupitia mifumo yake ya biashara ya mitandao (e-commerce) kwa mamilioni ya wateja katika zaidi ya nchi 100, ikiwa inasaidia watu kuishi maisha bora, na kutoa njia mbadala ya kujipatia kipato kwa yeyote anayehitaji kutumia fursa hii. Kampuni pia ina ofisi na mawakala washirika katika nchi 25 duniani kote, na zaidi ya stoo 50, shughuli za uendeshaji na maduka na wauzaji katika nchi kadhaa duniani. Sasa kwa uwepo wake imara katika Afrika Mashariki, QNET imejidhatiti katika kuendeleza mtindo wa mauzo wa moja kwa moja katika kanda hii. 

Kwa kuongezea QNET pia inarudisha faida yake kwa jamii. Baadhi ya wanufaikaji wa Majukumu ya Kampuni kwa jamii ni pamoja na kituo cha kulelea yatima cha Maunga, na Kituo cha kulele yatima cha Newlife Orphans Home ambavyo vimepokea msaada wa chakula na michango kwa miaka ya hivi karibuni. 

Kwa mujibu wa Biram Fall Meneja Mkuu wa QNET katika Kanda ya Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara; "QNET ina nia ya kurudisha kwa jamii, Hii ndio sababu kwa nini tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika miradi ya uwajibikaji endelevu ya kampuni kwa jamii katika maeneo mbalimbali ya Afrika kupitia katika mkono wetu wa uwajibikaji kwa jamii” alisema Fall. 

QNET Ghana, kwa kupitia RYTHM Foundation, imetoa vifaa maalumu 50 vya kusomea vitabu vya kielektroniki (Kindle e-readers) ambavyo vina vitabu 100 vinavyoendana na tamaduni zao kila kimoja. kwaajili ya wanafunzi wa Nima, eneo lenye watu wa kipato cha chini zaidi ndani ya jiji wa Accra, Ghana. Ilikuwa ni mradi uliofanyika kwa ushirikiano na Worldreader, NGO ya utoaji wa elimu duniani na Achievers Ghana, taasisi ya elimu kwa jamii. 

QNET pia inafanya vizuri katika udhamini wa michezo duniani. Baadhi ya ushirikiano mkubwa wa hivi karibuni unajumuisha kuwa Wauzaji wa Moja kwa Moja wa Klabu ya Mpira wa miguu ya Manchester City na Klabu ya mpira wa miguu kwa wanawake ya Manchester city na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwaajili ya ligi ya mabingwa ya Total CAF, Kombe la shirikisho la Total CAF na Total CAF Super Cup kwa mwaka 2018 na 2019. Hapo awali washirika wakubwa walikuwa ni pamoja na Formula One, badminton na zaidi, kutokana na imani thabiti ya kampuni kwamba msukumo, shauku na kufanya kazi katika timu iliyopo katika michezo inaendana na ule wa QNET. 



Manufaa 

Imani thabiti ya QNET kwamba hakuna kinachowezesha zaidi kwa mtu binafsi kama uhuru wa kifedha ambao unatolewa na jitihada katika sekta ya mauzo ya moja kwa moja, na inaamini kwamba watu wa Afrika Mashariki, pamoja na shauku yao na fikra za ujasiriamali, watafurahia kiwango bora cha bidhaa zinazotolewa na QNET na fursa za kibiashara kwaajili ya maendeleo binafsi. 

Mauzo ya Moja kwa Moja yanaweza kuwa ni kazi ya kutosheleza kwa wale ambao wanachagua kuchukua fursa hii kama kazi yao kuu au hata kuchukua kama kazi ya ziada kwa sababu inatoa faida za kifedha kutegemeana na muda na juhudi unazoweka katika kukuza biashara yako. Kwa kuongezea, tofauti na biashara zingine za kawaida ambazo zinahitaji mtaji mkubwa, rasilimali na hata uzoefu, biashara ya mauzo ya moja kwa moja inatoa fursa hii ya biashara yenye gharama nafuu kwa kila mmoja anayehitaji kuianzisha, bila kujali kiwango chao cha elimu au uzoefu. Zaidi ya hayo, mafunzo na maelekezo ambayo wafanyabiashara wanaoanza wanapitia (Wawakilishi wa Kujitegemea au IRs kama ilivyo katika QNET) inawapatia ujuzi wa pekee ambao unapelekea kuwa na ujasiri, kujitambua na hatimae ukuaji binafsi ambao unatambua utaalamu wa mtu kama mjasiriamali aliyekamilika. 

Huenda, manufaa makubwa zaidi ya mauzo ya moja kwa moja katika masoko yanayoibukia kama Afrika Mashariki ni kwamba mtindo huu unakuwa na athari zaidi hapa kuliko katika masoko yaliyoendelea kwa sababu ya athari za kifedha inayoweza kuleta katika maisha ya watu - kutoa fursa za ujasiriamali kwa wote, bila kujali ujuzi au uzoefu, hivyo hatimae kuchangia katika kupunguza umasikini katika jamii. 

Katika mizizi ya QNET kuna falsafa ya RYTHM – Raise Yourself To Help Mankind - ambayo inaongoza jitihada zake zote, na kuendesha kampuni sio tu kubadilisha maisha ya watu duniani kote, lakini pia kushirikiana nao katika kupanua athari hizi. 

Kama alivyosema bwana Trevor Kuna, Mkurugenzi Mtendaji wa QNET "Tunaamini kwamba mafanikio ya kifedha peke yake hayatoshelezi" Ili tuweze kuleta athari, tunahitaji kuendeleza watu kuwa binadamu bora ili waweze kutumia mafanikio yao kuchangia katika jamii zao" 


Changamoto 

Kama ilivyo katika biashara nyingine yoyote Sekta ya Mauzo ya Moja kwa moja pia inakabiliana na changamoto. Changamoto ambayo ni kubwa zaidi miongoni mwa hizi ni kuenea kwa mifumo ya pyramid schemes inayoenda kinyume cha sheria ambayo inaonekana kama makampuni halisi ya biashara ya moja kwa moja, ikiwa inaahidi wawekezaji kuwa watajipatia faida nyingi kupita kiasi iwapo wataunganisha watu wengine. Ukweli ni kwamba hawa 'matapeli' wanatengeneza taswira potofu ya Sekta ya Mauzo ya Moja kwa Moja, jambo ambalo linatengeneza kikwazo kwa makampuni halisi kama QNET kusajili washauri wa kibiashara kuendesha biashara zao halisi na halali. Wakati inapokabiliana na hali kama hizo, QNET inasema inatatua tatizo kwa kuelimisha umma kuwa makini na 'matapeli' kama hao na kuwahimiza kuthibitisha uhalali wa kampuni yeyote kufuatana na kutii kwake kwa kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa na bodi zinazosimamia na mamlaka zinazohusika. 

Mpaka kufikia hapa, maelezo kutoka QNET yanasema: "Kampuni yoyote inayokuahidi njia rahisi ya kuwa tajiri inapaswa kuangaliwa kwa tahadhari. QNET kwa mfano, ina maelezo ya kutosha ya mapato yanayopatikana kwenye tovuti yake na vifaa vya mauzo. Kampuni za Masoko ya mtandao zinatoa bidhaa zenye ubora au huduma tofauti na mifumo ya pyramid schemes ambayo haina bidhaa halali au huduma. Kampuni bora ya Masoko ya mtandao huwa inatenga kiwango kikubwa cha rasilimali kwaajili ya utafiti na uendelezaji, kutengeneza bidhaa zenye ubora ambazo zina matumizi halisi kwa watu wakati mifumo ya pyramids scheme huwa haifanyi hivyo" 

Inaongeza: "Kampuni za masoko ya mtandano yana sera na taratibu sahihi, pamoja na kanuni za maadili za masoko. Kamuni yoyote halisi ya masoko ya mtandao ina lengo la kufikia ukuaji endelevu kwa kukuza utamanuni wa masoko ya kimaadili. QNET inaweka msisitizo mkubwa katika kanuni za maadili za utendaji kwa wawakilishi wake wa kujitegemea (IRs) na kuwapatia miongozo ya kina kuhusu masoko ya kitaalamu pamoja na sera na taratibu". 

Kusisitiza uhalali wa mauzo ya moja kwa moja, utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Taasisi ya Ngazi Mbalimbali za Masoko ya India (India Multi-Level Marketing Institute) ilichunguza uendeshaji wa aina mbalimbali kama vile Avon, Mary Kay, QNET na Tupperware na kubaini kwamba 'sio mifumo ya scheme) ya aina ya piramidi au aina nyingine yoyote. 

Changamoto nyingine inayoikabili sekta ya mauzo ya moja kwa moja ni ujuzi ambao haujaendelezwa hasa kwa wale ambao wamechukua fursa hii hivi karibuni. QNET inasema kwamba inatatua changamoto kwa kuweka msisitizo mkubwa sana katika mafunzo na elimu kwa IRs. Mafunzo hayo sio tu kamba yanaendeleza ujuzi wao wa kitaalamu lakini pia unalenga katika ukuaji na maendeleo binafsi. 

Ni wazi kwamba, kufikisha bidhaa katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mbali ni kikwazo kingine lakini QNET imeweza kutatua hili kwa kuajiri IRs ambao wanatengeneza mtandao ndani ya jamii zao kwaajili ya kurahisisha upatikanaji na pia kuwasaidia kuagiza mzigo mkubwa kwa punguzo kwa lengo la kutoa mzigo, hivyo kuhakikisha usambazaji endelevu wa bidhaa. 

Kuingia kwa QNET katika soko la kanda inaweza pia kukabikiana na ushindani kutoka kwa kampuni ambazo tayari zilishaanzishwa za bidhaa za reja reja na nembo za kimataifa lakini mtindo wake wa pekee wa usambazaji utaiweka QNET tofauti na kutengeneza njia ya mafanikio. 

JAFO AELEKEZA HOSPITALI ZA WILAYA MPYA ZINAZOJENGWA ZIKAMILIKE IFIKAPO JUNE 30

0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
WAZIRI wa TAMISEMI, Selemani Jafo ameziagiza halmashauri zote zilizopatiwa fedha za kujenga hospitali ya wilaya mpya, kuhakikisha wanasimamia majengo hayo yanakamilika ifikapo June 30 mwaka huu. 

Aidha ameelekeza watalaamu wa halmashauri hizo wasimamie ubora wa majengo yanayoboreshwa na kupanua vituo vya afya ili yaweze kudumu kwa kipindi kirefu kijacho .
 Pamoja na hayo Jafo ameridhishwa na utekelezaji wa agizo alilolitoa kwa halmashauri ya Kibaha Vijijini, mkoani Pwani miezi michache iliyopita kuhusu kukarabati chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha afya cha Mlandizi. 

Akitembelea ujenzi wa upanuzi wa kituo cha afya Mlandizi na hospitali ya wilaya inayojengwa Kibaha Vijijini, Jafo alitaka hospital hizo zikamilike kwa muda huo na kwa kiwango chenye ubora kulingana na thamani iliyotolewa. 

Alisema serikali imetoa kiasi cha sh. milioni 400-500 kwa vituo vya afya 97 nchini ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi. 

Jafo pia aliyaasa mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo TACAIDS kukabidhi fedha za miradi wanayotaka kuyajenga ikiwemo maabara katika kituo cha afya Mlandizi kwa halmashauri ya Kibaha Vijijini badala ya kusimamia wenyewe ili kuondoa mkanganyiko. 

"Kwanini mkandarasi wamlete wao, nyie wenyewe mmeweza kujenga kwa umakini na kutumia fedha vizuri kuboresha kituo hiki cha afya, kwanini wao wasitoe hizo milioni 600 kwenu mkasimamia miradi hiyo "

"Msije kuingizwa mkenge simamie na wanapaswa kupitisha fedha hizo kwenu "alifafanua Jafo. 
 Kuhusu chumba cha kuhifadhia maiti amepongeza halmashauri hiyo kwa kutekeleza agizo lake kwa asilimia 100. Nae mbunge wa jimbo hilo, Hamoud Jumaa alimuomba waziri huyo kuwaongezea fedha kwa ajili ya kuboresha zahanati ya Dutumi na Kwala. 

Jafo alisema serikali itaangalia uwezekano wa jambo hilo ukizingatia Kwala kunajengwa bandari kavu hivyo ni bora huduma za kijamii zikaangaliwa. 

Wanawake waaswa kujituma ili kuleta maendeleo

0
0
Wanawake nchi wameaswa kuendelea kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujituma ili kuleta maendeleo kwa ajili ya familia zao na taifa kwa ujumla licha ya changamoto ambazo wanakubana nazo.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Saccos for Women Enterpreneurs (Taswe – SACCOS) Anna Matinde wakati akiongea na wanawake wanafanyi kazi wa Airtel Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo yaliandaliwa na kampuni hiyo.

Imekuwa ni kawaida kwa wanawake kulalamika kwamba hawapewi fursa sawa na wanaume ili kuonyesha uwezo wao. Na hii ni popote unapoenda. Wanawake wanasema wanaume ndio wenye furs azote na wao wamekuwa ni kama kivuli kwao. Mimi nataka kuwaambia huo sio ukweli. Sisi wanawake tunao nguvu na fursa kwa wanaume ya kuweza kufanya hata Zaidi yao. Tunachotakiwa kufanya ni kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ili kujijengea heshima kwenye jamii yetu, alisema Matinde.

Matinde alisema kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani mwaka huu ni #BalanceforBetter’ ikimaanisha kwamba kuwaza kwa mbali na kujiandaa kwa mafanikio. Ni muhimu kutambua kwamba wanawake tunaitaji kujikwamua kiuchumu na kuwa na uhuru wa kifedha. Vile vile tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii, nyumbani na sehemu zetu za kazi. Lakini muhimu tunatakiwa kuwa wajasiriamali. Hatuwezi kuendelea kuishi kwa kutengemea mishahara yetu au waume zetu. Ni muhimu kuangalia namna ya kujibadilisha fikra zetu kwenye ujasiriamali ili kuwa na uhuru wa kiuchumi, alisema Matinde.

Mimi nina uzoefu wa kutosha wa kuajiriwa na pia wa ujasiriamali. Wakati naanza maisha ya ujasiriamali hakuna mtu yeyote aliyekuwa anafikiria kama naweza kuwa hapa nilipo leo. Nawaomba mtumie kila dakika yenu kufanya kitu ambacho kitaweza kuwaingizia kipato cha ziada. Ni lazima muelewe ya kwamba wanawake wanayo nguvu ya kupata chochote unachohitaji kama tu mtakuwa na malengo, kufanya kazi kwa bidii na kuwa na mawazo chanya, aliongeza Matinde.

Akiongea kwenye maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano aliwaaza wanawake kujishusha na kuendeleo kufanya kazi kwa moyo wote na bidii ili kuleta mafanikio.

Natoa wito kwa wanawake wote kutokata tamaa. Tunaweza kupata changamoto za hapa na pale lakini cha muhimu ni kujitambua na kuendelea kung’aa. Ni lazima muwe na mawazo chanya lakini muhimu Zaidi ni kuendelea kumuomba Mungu atuongoze na kila jamba, Singano alisema.

Hii ni siku ya wanawake na kusherekea ni kitu cha muhimu. Lakini ni lazima kutafakari na kujiweka juu zaidi. Sisi ni watu muhimu kwenye jamii na ni vizuri kuelewa tunayo fursa za kimaisha sawa na wanaume. Tufanye kazi kwa bidii, tujiheshimu na tutumie muda wetu vizuri ili tufanikiwe, aliongeza Singano.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasimali Watu Airtel Tanzania Stella Kibacha akitoa mada wakati wa mkutano wa wafanyakazi wa Airtel Tanzania uliandaliwa na kampuni ikiwa na maadhimisho ya kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Wafanyakazi wanawake Airtel Tanzania wakionyesha ujuzi wao wa kucheza muziki wakati wa mkutano wa wafanyakazi wa Airtel Tanzania uliandaliwa na kampuni ikiwa na maadhimisho ya kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Kutoka kulia Mkurugenzi na Mwanzilishi wa taasisi ya Tanzania Saccos for Women Entrepreneurs (Taswe-Saccos) Anna Matinde, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo Adriana Lyamba kwa pamoja wakikata keki wakati wa mkutano wa wafanyakazi wa Airtel Tanzania uliandaliwa na kampuni ikiwa na maadhimisho ya kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

MAKAMU WA RAIS AWASILI NCHINI UGANDA TAYARI KWA KUSHIRIKI MKUTANO WA AFRICA NOW SUMMIT 2019

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Dkt. Aziz P. Mlima (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebe, wengine pichani ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe. Philemon Mateke (kushoto).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dkt. Aziz P. Mlima mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe nchini Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe. Philemon Mateke mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe tayari kwa kushiriki mkutano wa Africa Now Summit 2019 utakaofanyika mjini Kampala tarehe 12 na 13 mwezi Machi, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya ndege ya Air Tanzania aina ya Airbus A220-300 wakati akielekea nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa Africa Now Summit 2019 unaoanza kesho tarehe 12 mjini Kampala Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Uganda na kupokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Philemon Mateke pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Aziz P. Mlima katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebe.

Makamu wa Rais pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaru wamesafiri na ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Tanzania aina ya Airbus A220-300 (Dodoma) kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Entebe kupitia Kilimanjaro.

Kesho Makamu wa Rais atashiriki mkutano wa mwaka 2019 wa “Africa Now Summit 2019” ambao utafunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambapo viongozi mbalimbali wa Afrika wanakutana ili kupata majibu ya changamoto za Afrika katika masuala ya kiuchumi.

Katika mkutano huo wa Viongozi wa Afrika, Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambapo katika mada mbalimbali zitakazojadiliwa Makamu wa Rais atazungumzia suala la Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika. 

Viongozi wengine watakaotoa mada ni Rais wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA) Mhe. Abdel Fattah el Sisi; Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa; Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. William Ruto; na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Ahmed Abiy na Rais Paul Kagame wa Rwanda. Mada zote hizi zitajikita kwenye kuonesha chachu ya Uongozi katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika. 

Mkutano utamalizika tarehe 13 Machi 2019 utaanza na hotuba kutoka kwa Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi na baadae kufungwa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

Makamu wa Rais ataambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. 

SERIKALI YAIMARISHA USIMAMIZI NA UDHIBITI MATUMIZI SALAMA YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA NCHINI.

0
0

Mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Profesa Lazaro Busagala akitoa neon la ukaribisho kwa wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi wanachama 49 wa Shirika la Nguvu za Atomiki la kimataifaIAEA)
Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh William Ole Nasha (Kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Shirika la nguvu za Atomiki duniani Profesa Shaukat Abdulrazak kwenye mkutano wa kimataifa unahusisha nchi 49 za kanda ya AFRIKA.
Naibu waziri Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh William Ole Nasha wakati akifungua mkutano wa kimataifa unaohusisha waratibu wa miradi ya sayansi na teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi za kanda ya AFRIKA

Picha ikimuonyesha Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh William Ole Nasha akiwanna washiriki wa mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia kutoka katika nchi wanachama 49 wa Shirika la Nguvu za Atomiki duniani

………………………………………………………………….

Serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imefanikiwa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya Teknolojia ya Nyuklia nchini. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekenolojia Mheshimiwa William Ole Nasha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi 46 wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki ( IAEA ) unaofanyika jijini Arusha.

Naibu waziri Ole Nasha amesema Shirika hilo linafadhili miradi mingi katika sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo sekta ya afya ambapo imewezesha kupatikana kwa vifaa mbali mbali vya uchunguzi wa tiba na maradhi ya saratani ambavyo vimefungwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando jijini Mwanza na Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.

Pamoja na vifaa vya uchunguzi katika hospitali hizo mbili, pia taasisi nyingine mbalimbali zimepata vifaa vya maabara ambapo kwa ujumla wake vifaa vyote vina thamani ya kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 6.2 na pia kutoa mafunzo kwa wataalamu katika eneo la matumizi ya mionzi na Teknolojia ya Nyuklia mpango ambao uligharimu Shilingi za Tanzania Bilioni 3.3.

Mh Ole Nasha amelishukuru na kulipongeza shirika hilo kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa wanachama hususan kwa utaratibu wake wa kuwa na mikutano inayowezesha kubadilishana uzoefu baina ya wanachama. Amewataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha wanafanya majadiliano yenye tija kwa lengo la kusaidia nchi zao kwenye udhibiti na matumizi salama ya teknolojia ya nyukulia. “ majadiliano yenu yalenge katika kuhakikisha mionzi na teknoljia ya Nyuklia katika Afrika inatumika vizuri kwa maendeleo”.Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA ) Profesa Shaukat Abdulrazak amesema wataendeela kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha matumizi salama ya teknolojia ya Nyukilia kwenye sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya , Kilimo,Mifugo,Maji ,Viwanda na Ujenzi.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Nguzu za Atomiki Tanzania , Profesa Lazaro Busagara amesema taasisis yake imeendelea udhibiti na kuwachukulia hatua za kuwafungia taasisi zinazokiuka taratibu za matumizi salama ya Mionzi na Teknolojia ya Nyuklia hapa nchini ikiwemo kutokuwa na leseni, kutokuwa na wafanyakazi wenye utaalamu wa matumizi ya mionzi na teknolojia ya Nyuklia na Mionzi.

Akitoa mfano wa Hospitali amesema mwaka 2018 walifungia hospitali 112 zilizoshindwa kufuata masharti hayo, katika hizi tayari hospitali 40 zimekidhi na kufunguliwa huku hospitali 72 zikiwa bado zimefungiwa kutumia vifaa vinavyotumia mionzi .
Mkutano huo wa Siku tano utamalizika tarehe 15 , Machi 2019.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC)
11/ 3/2019
Arusha, Tanzania

Wafanyakazi wanawake Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) watakiwa kushirikiana na kutengenezeana Fursa Mbalimbali za Maendeleo

0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akizungumza na wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa JKCI Dkt. Delila Kimambo
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akielezea namna ambavyo wanawake wa taasisi hiyo walivyoanzisha kampeni ya kuwasaidia wanawake na watoto katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya viongozi wanawake kutoka katika taasisi za afya wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi baba wa mtoto mwenye magonjwa ya moyo Richard Zaya kiasi cha shilingi 593,000 kilichotolewa na umoja wa wanawake wa JKCI kusaidia matibabu ya mtoto huyo wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa JKCI machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Baadhi wa wanawake wa Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake hao machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Delila Kimambo akimshukuru mgeni ramsi kushirikiana na wanawake wa JKCI kuadhimisha siku ya wanawake duniani wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku hiyo iliyofanyika machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akicheza mziki na wafanyakazi wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa JKCI machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika picha ya pamoja wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake hao machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

…………………………..

Na Anna Nkinda

Wafanyakazi wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kushirikiana na kutengenezeana fursa mbalimbali za maendeleo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula wakati akiongea na wafanyakazi wanawake wa Taasisi hiyo katika sherehe ya kuadhimisha siku ya mwanamke Duniani.

Dkt. Chaula alisema ni muhimu kwa kila mwanamke akahakikisha anatengeneza fursa ya mafanikio kwa mwenzake jambo la muhimu ni kupendana, kushikana mkono na kuhakikisha hakuna mtu atakayefukuzwa kazi na atakayetamani kustaafu kabla ya wakati.

“Hakikisheni mazingira ya kazi yanakuwa mazuri na salama kwenu ninyi wote, kushirikiana kwenu kutawawezesha kufika mbali zaidi katika utendaji wenu wa kazi kwani katika mafanikio yoyote yale mchango wa mwanamke ni mkubwa zaidi ukilinganisha na wa mwanaume”, alisema Dkt. Chaula.

Aliendelea kusema kuwa katika sehemu ya kazi kila mtu anamchango katika mafanikio ya mwenzake, ukiona umefanikiwa tambua nyuma yako kuna watu wamekufanya ukafika hapo ulipo hivyo basi ni muhimu kwa wafanyakazi hao kuwa karibu zaidi.

Dkt. Chaula alimalizia kwa kuwataka wanawake hao kumtanguliza Mungu katika kazi zao za kila siku kwani kwa kufanya hivyo watakuwa na familia njema zenye hofu ya Mungu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi Dkt. Delila Kimambo alisema katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani wafanyakazi wanawake wa Taasisi hiyo walifanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na kutoa elimu kwa wanawake wa soko kuu la Kimataifa la Samaki la Feri pamoja na maeneo jirani.

Dkt. Delila ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema waliamua kwenda kupima magonjwa ya moyo na kutoa elimu kwa wanawake wa Soko hilo kwa kuwa hawana muda wa kwenda kupima afya zao.

“Tuliwafundisha viashiria vya hatari vya magonjwa ya moyo kwa wanawake na kuwapima afya zao. Tafiti zinaonyesha kuwa ukitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa wanawake kwa asilimia 80 utapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo katika jamii”, alisema Dkt. Delila.

Katika kuadhimisha siku hiyo wafanyakazi hao walichanga kiasi cha shilingi 593,000/= fedha ambazo walimkabidhi baba mzazi wa mtoto Yasinta Zaya (15) ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Akizungumza kabla ya kuzikabidhi fedha hizo Daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Anjela Muhozya alisema waliamua kumsaidia mtoto huyo ambaye alianza kuumwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka sita.

“Mtoto huyu anasubiri kwenda kupatiwa matibabu nchini Israel, hivi sasa afya yake imebadilika amelazwa ICU anatakiwa kufanyiwa vipimo mbalimbali ikiwemo MRI (Magnetic Resonance Imaging – MRI. Tumeona tumsaidie kwani wazazi wake hawana uwezo”, alisema Dkt. Anjela.

Akiongea mara baada ya kupokea fedha hizo Baba mzazi wa mtoto huyo Richard Zaya ambaye ni mkazi wa Kalambo mkoani Rukwa aliwashukuru wafanyakazi hao kwa moyo wa upendo waliouonyesha kwa mtoto wake na kuomba waendee kufanya hivyo kwa watu wengine wenye uhitaji.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Dkt. Chaula alitoa kiasi cha shilingi milioni moja na elfu hamsini kati ya hizo shilingi milioni moja itatumika kwa ajili ya vipimo vya mtoto huyo.

KUIONA SIMBA VS AS VITA BUKU TATU TU

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
UONGOZI wa Klabu ya Simba umetangaza viingilio vya mchezo wao wa mwisho wa kundi D wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika utakaopigwa Mach 16 katika Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo wa mwisho kati ya Simba na As Vita utachezwa kuanzia majira ya saa 1 usiku ambapo mechi zote za kundi hilo zitachezwa ndani ya muda mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Ofisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa mchezo huo utakuwa katika viingilio vitatu na kiingilio cha chini kitauwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko na Orange.

Manara amesema, kwa upande wa VIP B kiingilio kitakuwa ni  10,000 na VIP A ikiwa 20,000 huku Platnums itakuwa ni 100,000.

Amesema kuwa, mechi hiyo itachezwa muda mmoja na Al Ahly dhidi Js Saoura ukiwa ni mchezo wa mwisho wa kundi hilo ili kuweza kupata timu mbili zitakazokwenda hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

"Tiketi ya Platnums itampa usafiri shabiki kwenda Uwanjani akitokea Serena Hotel mpaka Uwanjani na atakaa sehemu ambayo itaambatana na vinywaji huku akipewa na jezi,"amesema Manara.


Manara amewaomba mashabii kujitokeza kwa wingi katia mchezo huo ili kuweza kuujaza Uwanja huo ikiwa ni moja ya hamasa kwa timu wawapo Uwanjani. Ameeleza kuwa timu yao ndiyo namba moja Afrika kwa kuweza kujaza Uwanja unaoingia takribani watu 60,000.

Simba inaingia kwenye mchezo huo wakiwa na  kumbukumbu mbaya ya kufungwa goli 5-0 kwenye mchezo wao wa awali uliofanyika nchini DR Congo na pia kutoka kupoteza  2-0 dhidi ya JS Saoura katika mchezo wa mwisho uliopigwa huko Bechar, Algeria mwishoni mwa wiki hii.


Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wadau wa mpira hapa nchini, itapigwa majira ya saa 1 za usiku katika Uwanja wa Taifa.

Hatimiliki za Kimila Kuwanufaisha Wakulima Chamwino.

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images