Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110035 articles
Browse latest View live

BREAKING NYUZZZZZ....: NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINE YAANGUKA IKIWA SAFARINI KULEKEA NAIROBI

$
0
0
Serikali ya Ethiopia imetoa taarifa ya vifo vya abiria 157 ambao walikuwa wamepanda ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege la Ethiopia iliyokuwa ikisafiri kutoka Ethiopia kuelekea Nairobi, Kenya baada ya ndege hiyo kupata hitilafu na kuanguka. Ni moja kati ya ndege  mpya zilizonunuliwa na shirika hilo miezi minne iliyopita.

Halmashauri ya Kilolo yakopesha wanawake navijana Tsh milioni 110

$
0
0
NA  FRANCIS GODWIN,IRINGA 

KATIKA utekelezaji wa agizo la  serikali la  kila Halmashauri  nchini  kutenga kiasi cha fedha asilimia 10 ya makusanyo yake ya ndani kwa ajili ya  kuyawezesha makundi ya  vijana ,walemavu na wanawake ,Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa   imetumia sherehe  za siku ya  wanawake duniani kwa kutoa  mikopo kiasi cha shilingi milioni 110 kwa vikundi  mbali mbali  vikiwemo  vikundi vya wanawake katika wilaya  hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi  wa Halmashauri ya Kilolo Aloyce Kwezi mwakilishi  wake katika sherehe hizo juzi  Dr John Mwingira alisema  kuwa  kwa kutambua  umuhimu wavikundi vya wanawake  wajasiliamali ndani ya  wilaya ya  Kilolo Halmashauri  iliona ni vizuri  kuweza kutumia  siku hiyo ya wanawake duniani inayoadhimishwa Machi 8 kote  duniani kwa ajili ya  kuwawezesha  wanawake hao kiuchumi.

Kuwa  mikopo hiyo ambayo imetolewa kwa wanawake ni mikopo isiyo na riba na  wakopaji watatakiwa kurejesha  mikopo  hiyo kwa muda uliopangwa bila ya kutozwa  riba yoyote na  kuwa pindi mikopo hiyo inaporejeshwa kwawakati vikundi vingine vya  wanawake huendelea  kukopeshwa zaidi  .

" Halmashauri  kupitia makusanyo ya mapato ya  ndani  imeendelea kutekeleza agizpo la  serikali lililotolewa na Rais Dkt John Magufuli kwa Halmashauri zote nchini kupitia makusanyo  yake ya ndani kutenga asilimia 10 kwa  ajili ya  kuwakopesha vikundi vya wanawake ,walemavu na vijana na  halmashauri yetu  imekuwa ikitekeleza kwavitendo na kwa  wakati agizo hilo " alisema 

 Kuwakiasi hicho cha  shilingi milioni 110 kimetumika kukopesha wanawake ,vijana na walemavu ambao kwa  umoja  wao  walikabidhiwa  fedha hizo kupitia sherehe hizo za siku ya wanawake duniani na kuwa azma ya  Halmashauri kuendelea kuwasaidia mikopo vijana ,wanawake na  walemavu ambao  wamejiunga katika vikundi .

Alisema kuwa kupitia  sherehe hizo vikundi vya  wanawake 59 kutoka kata mbali mbali za  wilaya ya Kilolo walikopeshwa  kiasi cha  shilingi milioni 66 wakati  vikundi vya  vijana  vilivyopewa mkopo ni vikundi  24 ambavyo vilikopeshwa  shilingi milioni 43 na kikundi kimoja  cha  walemavu kilichokopeshwa  kiasi cha  shilingi milioni 1.

Akikabidhi   mfano wa hundi ya  mikopo kwa vikundi hivyo   mwenyekiti wa Halmashauri ya  Kilolo  Vallence Kihwaga  alisema  kuwa  fedha  hizo za mikopo  walizokopeshwa na sehemu  tu ya bajeti  ya Halmashauri  iliyotengwa kwa mwaka 2019 na kuwa kwa sasa  wameanza kutekeleza  matumizi ya  bajreti hiyo kwa kuanza kutoa mikopo kwamakundi mbali mbali  na  wataendelea  kutoa  mikopo  na kuwataka  walengwa  kuendelea kujiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiliamali .

" Tutaendelea  kutoa mikopo  hii  mara kwa mara kama ambavyo bajeti yetu ilivyopangwa  kwa mwaka huu  na  tunauhakika kuwa baada ya leo kutoa  mikopo hii muda si mrefu  tutatoa mikopo tena kwa makundi ya  wanawake ,vijana na walemavu  hivyo  endeleeni  kuunda vikundi vyenye  tija  vya ujasiliamali nacha kujivunia ni tayari Rais wetu mpendwa Dkt  John Magufuli kwa  kuwajali  wajasilimali amekwisha  toa  vitambulisho kwa kila halmashauri kwa ajili yenu  wajasiliamali kazikwenu  kuchangamkia vitambulisho  hivyo ili msinyanyasike mnapofanya shughuli zenu" alisema Kihwaga.

Aidha  alisema wakopaji ambao watachelewesha  kurejesha mikopo ama  kushindwa kurejesha kabisa  watakuwa  wamejiondoa katika orodha ya  watakaoendelea  kukopeshwa mikopo hiyo na wale  watakaoonyesha uaminifu wataendelea  kunufaika na mikopo hiyo inayotengwa na Halmashauri ikiwa ni asilimia 4 vijana  na asilimia 2 walemavu huku wanawake wakipata nao asilimia 4  katika asilimia 10 ya mikopo itokanayo ya makusanyo ya ndani ya Halmashauri .

Kihwaga  alisema kuwa  sifa kuu ya vikundi  hivyo kukopeshwa ni kuwa kuwa na akaunti bank ambayo ni hai na sio akaunti iliyosinzia ambayo haionyeshi kama inatumika kuweka na kuchukua  fedha .

Kwa upande wake wake  wanawake    wanufaika na  mikopo  hiyo Amina Sanga akizungumzia mikopo hiyo alisema  kuwa  imekuwa ni  mkombozi mkubwa kwao kwani  itawawezesha kuongeza uzalishaji katika  kikundi na  kuwa pale  wanawake  wanapokuwa na kipato  kizuri ndani ya familia hata ndoa zao zimekuwa zisimama pasipo  kuyumba  kwani mama anakuwa na sauti  kama baba ndani ya nyumba.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya  wilaya ya Kilolo mkoani IringaVallence Kihwaga (mwenye koti jeusi kushoto) na mwakilishi wamkurugenzi wa Halmashauriya Kilolo Dr John Mwingira ( wapili kulia)  wakiwakabidhi  mfano wahundi ya shilingi milioni 110  wanawake wa vikundi 59 vya wajasiliamali wilaya ya Kilolo kwa  niaba ya vikundi vya walamavu na vijana  juzi  wakati wa sherehe za  wanawake wilaya ya Kilolo (picha na Francis Godwin). 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Vallence Kihwaga (kushoto) akimkabidhi mmoja kati ya wazee wanaotoka katika familia masikini ndani ya mji wa Ilula kwa niaba ya wazee wengine ,msaada wa sabuni na vitu mbali mbalivilivyotolewa na wanawake wa wilaya ya Kilolo kwa wazee hao kwa ajili ya kusherekea siku ya wanmawake duniani juzi Machi 8 mwaka huu (Picha na Francis Godwin).

Tutatumia uzoefu wa wastaafu wetu- AG

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi akimkabidhi zawadi ya kitabu Mwandishi Mkuu wa Sheria Bibi Sarah Kinyamfula Barahomoka katika hafla ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi Saba wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao wamestaafu na wanastaafu Utumishi wa Umma. Bibi Sarah Barahomoka ambaye anastaafu rasmi mwezi Julai Mwaka huu ni Mwanamke wa Kwanza kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria ( Chief Parliamentary Draftsman) amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 33.
Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao wanastaafu utumishi wa Umma.Halfa ya kuwapongeza na kuwaaga ilifanyika mwisho mwa wiki. miongoni mwa zawadi walizopewa ni pamoja na Kitabu 'Retiring Gloriuosly'. Kutoka kushoto na miaka yao ya utumishi kwenye mabano ni Bw. Hussein Shabani Kaweto (37), Bibi Esther James Manyesha (35), Bibi Sarah Kinyamfula Barahomoka (33), Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Evaristo Longopa, Bibi Mary Mahingu Maganga(30), Bibi Benadetha Cosmas Karadisy (36) na Bw. Cosmasi Bayi Machupa (16).


Na Mwandishi Maalum, Dodoma 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi amesema, Ofisi yake itaandaa utaratibu wa kuwatumia watumishi wake waliostaafu katika maeneo mbalimbali yakimamo ya kufundisha na ushauri. 

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki,( Ijumaa) wakati wa hafla ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi saba ambao wamestaafu na wanastaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria. Hafla hiyo na ambayo pia ilihudhuriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Evaristo Longopa ilifanyika katika ukumbi wa Veta Jijini Dodoma 

Miongoni mwa watumishi hao wanaostaafu ni pamoja na Mwandishi Mkuu wa Sheria Bibi Sarah Kinyamfula Barahomoka , Mwanamke wa Kwanza kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria tangu Tanzania ipate uhuru na amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 33. Miaka hiyo yote amefanya kazi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

“Watumishi wenzangu mnaostaafu. Mnastaafu bado mkiwa na akili timamu na afya njema, mnastaafu utumishi wa Umma kwa Heshima kubwa hongereni sana. Uzoefu mnaoondoka nao hamkuupata kwa mwaka mmoja au mwili, ni uzoefu ambao umejijengea katika kipindi chote cha utumishi wetu” akasema Mwanasheria Mkuu . 

Na kuongeza “ Ofisi yangu tutaandaa utaratibu wa kuangaliana namna ya kuutumia uzoefu wenu huu, iwe kwa kutoa ushauri au kwa kuja kufundisha. Na kwa hiyo msishangae mkiona hata katika ustaafu wenu tunawaomba mje mtusaidie katika kutuongezea nguvu katika maeneo fulanifulani mkiwa kama washauri au wakufunzi.Na ninaomba sana tutakapowaomba na kuwahitaji mtukubalie” akasisitiza na kushangiliwa na watumishi. 

Profesa Kilangi amewataka wastaafu hao kwenda na kuutumia uzoefu wao waliojijengea katika utumishi wa umma kwa maendeleo na manufaa yao wenyewe na familia zao lakini pia kwa manufaa na maslani pamana ya Serikali na Nchi kwa Ujumla. 

Kuhusu watumishi wate wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Kilangi amewashukuru na kuwapongeza kwa namna ambavyo wameupokea na kuanza kuutekeleza Muundo Mpya wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufuatia mabadiliko yaliyofanya na Mhe Rais John Magufuli mwaka jana. 

“Niwashukuruni sana kwa namna mnavyotekeleza majukumu yenu, wengi wetu tumeyapokea vema mabadiliko ya Muundo wa Ofisi aliyoyafanya Mhe Rais mwaka jana na mmeelewa lengo na nia yake ambayo ni kuboresha huduma zinazotolewa na Ofis ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na nipende kusema mbele yenu kwamba sasa ukizungumza na wadau wetu wengi huko nje wanafurahi sana, wanaridhika sana na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali” akasema . 

Pamoja na pongezi hizo, amewataka watumishi wote wa Ofisi yake ni vema wakafahamu ulimwengu wa sasa unahitani watu au watumishi wasomi na wenye uwezo wa juu wa kuelewa mambo na kutatua matatizo na katika muktadha huo ametoa wito wa watumishi wote kila mmoja kwa mujibu wa kada yake kujiendeleza ili Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikawe kioo na kielelezo bora katika Taifa letu. 

“Natoa wito mjiendeleze kwa kulingana na kada zanu mwenye certificate basi apate diploma, mwenye diploma apate degree ya kwanza na mwenye degree ya kwanza apate ya pili na na mwenye ya pili alenge kupata udaktari na hatimaye uprofesa hakuta kuwa na shinda kama ofisi hii itajaa madokta” akasisitiza kwa mkazo. 

Pia amewataka watumishi wote kujiandaa kifikra kwa mapokeo ya matumizi ya tehama katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku pamoja na kutumia vema muda wa kazi na kutumia vema raslimali na vitendea kazi vilivyovopo ili kutekeleza vema na kwa tija kauli mbiu ya ‘hapa Kazi tu’ 

Aidha amesema anaridhiswa na kufurahishwa na idadi kubwa ya watumishi wanawake ambao wameshika nafasi na Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Vitengo utaratibu ambao amesema ameukuta hataka kabla yake. 

Akitoa salamu za Shukrani kwa niaba ya wastaafu wenzie Mwandishi Mkuu wa Sheria Bibi Saraha Barahamoka amemshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuwaandalia hafla ya kuwapongeza na kuwaaga ikiwa ni pamoja na kuwapatia vyeti vya utumishi. 

Akasema yeye binafsi na wenzake wamefurahishwa sana na namna Ofisi ilivyotambua na kuthamini mchango wa utumishi wao katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Serikali na Nchi kwa Ujumla. 

Aidha akasema, katika kipindi chote cha utumishi wao katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamepata ushirikiano mzuri kutoka kwa viongozi wa juu na watumishi wenzao na kwamba wanaomba ushirikiano na moyo huo wa kusaidiana unaendelezwa baina ya viongozi wa wajuu na watumishi wote. 

Watumishi wengine waliostaafu ni Bibi Ester James Manyesha ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Uandishi wa Sheria na amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 35, Bibi Grace Mlondezi Mfinaga, Mwandishi wa Sheria Mkuu Daraja la kwanza na amekuwa katika utumishi wa umma kwa Miaka 36 na Bw. Hussein Shabani Kaweto Msaidizi Kumbukumbu Daraja la kwanza ambaye amedumu katika utumishi wa Umma kwa Miaka 37. 

Wengine ni Bibi. Benadetha Cosman Karadisy ambaye ni Msaidizi wa Mtendaji Mkuu Daraja la Pili na amedumu katika utumishi wa Umma kwa miaka 36, Bw. Cosmasi Bayi Machupa ambaye ni Dereva daraja la Kwanza yeye amedumu katika utumishi wa Umma wa miaka 16 na Bibi Mary Mahigu Maganga ambaye ni Msaidizi wa Ofisi Mkuu yeye amedumu katika utumishi wa Umma kwa miaka 30 

Imetolewa na Kitengo 
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali 
Dodoma

BINTI HUYU ANAOMBA MSAADA WA HALI NA MALI

$
0
0
Binti wa miaka 24, RADHIA SOLOMONI Mkazi wa Mtaa wa chemuchemu, magomeni mapipa Jijini Dar es salaam ambae amejifungua Watoto wanne, anaomba msaada kutoka kwa wadau mbalimbali kumsaidia mahitaji muhimu ya watoto kutokana na hali yake ya maisha kuwa ngumu na kushindwa kumudu mahitaji ya watoto hao, atakaeguswa awasiliane nae kwa namba 0682604202.

Serikali ya awamu ya tano haichukii wawekezaji - Rais Dkt. Magufuli

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amesema Serikali ya awamu ya tano anayoiongoza inathamini wawekezaji, tofauti na dhana ya baadhi ya watu kuwa wawekezaji katika awamu ya tano wanaonekana kuwa ni maadui.

Mhe. Rais Magufuli alisema hayo wakati wa sherehe ya kufungua mwaka 2019 ya wanadiplomasia (sherry party) iliyofanyika Ikulu jijini Dar Es Salaam tarehe 08 Machi 2019, na kuhudhuriwa na Mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yaliyopo hapa nchini.

Mhe. Rais Magufuli alisema uamuzi aliochukua hivi karibuni wa kuunda Wizara maalum ya uwekezaji ni ishara ya wazi kuwa Serikali ya awamu ya tano inathamini wawekezaji, na kuwasihi wanadiplomasia kuitumia wizara hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambayo ameifanyia mabadiliko.

Rais Magufuli alisema, Serikali yake imeshaanza mpango kabambe wa kuboresha mazingira ya uwekezaji na kutoa wito kwa wale wenye dhamira ya dhati ya kuwekeza nchini, waende mamlaka husika ili wahudumiwe.  “Mwenye dhamira ya dhati ya kuwekeza nchini, aende Wizara ya Uwekezaji au Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akikwamishwa huko aje kwangu ili nimkwamue huyo aliyekwamisha”, Rais Magufuli alisema.

Wanadiplomasia walioshiriki hafla hiyo, walisisitizwa kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo, mifugo, uvuvi, utalii, madini na viwanda vya nguo. “Serikali inahimiza uwekezaji katika sekta zinazotumia malighafi zinazopatikana nchini na zitakazotoa ajira za kutosha kwa vijana wa kitanzania kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa nchi”.  Rais Magufuli alisema.

Kuhusu utalii, Rais Magufuli alieleza kuwa, Tanzania ina vivutio vingi vya utalii, zikiwemo fukwe, uoto wa asili, malikale, mbuga za Wanyama na kwamba Serikali imejipanga kutangaza vivutio hivyo, hususan, vile vinavyopatikana kanda ya kusini. Mhe.  Rais aliitumia fursa hiyo kulipongeza Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa uamuzi wake wa kuanzisha channel maalum ya kutangaza vivutio vya utalii.

Kwa upande wa sekta ya madini, Serikali imejipanga kudhibiti wizi, biashara ya magendo, kuanzisha masoko ya kuuza madini na kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya kuchakata madini, ili sekta hiyo iwe na mchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi.

Aidha, Rais Magufuli alitumia hafla hiyo kuwaeleza wanadiplomasia, mafanikio ya Serikali ya mwaka 2018, mafanikio hayo ni Pamoja na Serikali kuendelea kulinda na kudumisha amani ya nchi; kukuza uchumi wa nchi ambapo katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018, Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi tano barani Afrika, uchumi wake umekua kwa kasi ikizidiwa na Ethiopia pekee.

Tanzania pia iliweza kudhibiti mfumuko wa bei na iliongoza katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji wa Dola za Marekani bilioni 1.18.

Mafanikio mengine ni Pamoja na ujenzi wa Miundombinu ikiwemo: ujenzi unaondelea wa reli ya kiwango cha Kimataifa kutoka Dar Es Salaam hadi Dodoma; ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme wa Mega Watts 2100 katika Mto Rufiji; ujenzi na upanuzi wa barabara mbalimbali nchini; ujenzi wa meli mpya katika Ziwa Victoria; upanuzi wa bandari za Dar Es Salaam, Mtwara na Tanga na kuboresha viwanja vya ndege mbalimbali nchini ikiwemo ujenzi wa Terminal 3 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Serikali pia imepiga hatua katika kuboresha utoaji wa huduma za kijamii katika sekta ya afya, elimu na maji. Kwa upande wa afya, bajeti ya sekta hiyo imeongezeka kutoka bilioni 31 hadi kufikia bilioni 270 ambapo ujenzi wa vituo vya afya 305 umekamilika na ujenzi wa hospitali 67 za Wilaya unaendelea, ukilenga kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Kuhusu elimu, Serikali imeendelea na mpango wake wa kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari na kuongeza bajeti ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Aidha, Miundombinu ya maji imeimarishwa ambapo upatikanaji wa maji kwa maeneo ya mijini umefikia asilimia 80 na asilimia 65 kwa maneo ya vijijini.
Rais Magufuli alieleza kuwa mafanikio ambayo Serikali ya awamu ya tano inaendelea kuyapata yanatokana na Ushirikiano na mchango mkubwa kutoka kwa wanadiplomasia, na kuahidi kuwa Serikali yake itaendelea kudumisha Ushirikiano huo.

Alihitimisha hotuba yake kwa kueleza kuwa, watumishi wengi wa Serikali walishahamia Makao Makuu ya Serikali jijini Dodoma na kuelezea matumaini yake kuwa, baadhi ya Balozi zitakuwa zimeshaanza mchakato wa kuhamia Dodoma, ukizingatia kuwa Serikali imetoa viwanja bure kwa ofisi zote za balozi.  
  
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar Es Salaam, Tanzania

09 Machi 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yaliyopo nchini katika Sherehe za kufungua Mwaka 2019 (sherry party) zilizofanyika Ikulu, Dar Es Salaam jana. Sherehe hizo zimehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuzungumza wakati wa sherehe hizo.
Mabalozi wakimpongeza Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli 
Rais Magufuli akiendelea kuzungumza na wanadiplomasia

Kiongozi wa Mabalozi ambaye ni Balozi wa Comoro nchini, Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed naye akizungumza kwa niaba ya Jumuiya ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa.
Sehemu ya Mabalozi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (kulia)
Mshereheshaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Bertha Makilagi akisherehesha kwenye Shughuli hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana na Balozi wa Namibia, Mhe.Theresa Samaria mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana na Balozi wa Oman hapa nchini, Mhe. Ali A. Al Mahruqi mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Sarah Cooke mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sandeep Arya mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akisalimiana na Balozi wa Ufaranza nchini, Mhe. Frederic Clavier mara baada ya kumalizika kwa sherehe za mwaka 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Utawala wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wakazi wanaoziwakilisha taasisi mbalimbali za kimataifa hapa nchini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wadogo wanaoziwakilisha nchni zao hapa nchini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoziwakilisha nchni zao hapa nchini

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumapili Machi 10, 2019. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto kwake ni Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa. Picha na Ikulu

KABAKA ATUA UNGUJA KUENDELEA NA ZIARA YAKE.

$
0
0


MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka akipokelewa na Viongozi mbali mbali wa CCM na Jumuiya zake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Unguja akitokea Pemba.

Viongozi mbali mbali wa UWT Taifa wakiwa katika Chumba cha Wageni Mashuhuri(V.I.P),mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Unguja wakitokea Pemba.

WANACHAMA wa CCM na Jumuiya zake wakicheza kwa furaha katika mapokezi ya viongozi mbali mbali wa UWT Taifa kisiwani Unguja.
……………………………………………………………………….
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

MWENYEKITI WA Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Tanzania Ndugu Gaudensia Kabaka leo amewasili Unguja kwa lengo la kuendelea na ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 katika Wilaya mbali mbali za Unguja.

Ndugu Gaudensia mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, aliwapongeza Wanachama wa CCM na Jumuiya zake kwa mapokezi na maandalizi mazuri ya Kongamano la kupongeza Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka mitatu ya Dk.Shein pamoja na ziara yake kisiwani Pemba.

Alisema kupitia ziara hiyo amejiridhisha kuwa Chama Cha Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar kina mtaji na azna kubwa ya wanachama hai wenye uwezo,uzalendo na uthubuti wa kusimamia maslahi ya taasisi hiyo bila kuyumba na kwa mafanikio makubwa.

Alieleza kuwa CCM inaisimamia Serikali zote mbili ya Zanzibar na Tanzania bara ziendelee kuwatumikia wananchi wa makundi yote bila ya ubaguzi kwa kuwasogezea huduma muhimu za kijamii, kiuchumi,kisiasa na kimaendeleo.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo, alipongeza Mwenyekiti huyo na Ujumbe aliofuatana nao kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kukagua miradi mbali mbali ya CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kisiwani Pemba.

Alieleza kuwa ziara hiyo imeleta mafanikio makubwa ya kisiasa kwani wanachama wengi hasa wanawake, wamehasasika na kutambua kuwa viongozi wa ngazi za Taifa wanawathamini na kuwajali.

Pamoja na hayo Naibu Katibu Mkuu huyo Ndugu Tunu, alisema Wanawake mbali mbali hasa Wajasiriamali wamejenga matumaini makubwa kwa kuungwa mkono juu ya kazi wanazozifanya za kuwaingizia kipato chao cha kila siku.

Awali Naibu huyo Tunu, alifafanua ratiba ya ziara ya Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia, kuwa Machi 11, mwaka 2019 kuanzia saa 2:00 asubuhi atawasili katika Ofisi ya UWT Mkoa wa Magharibi na kuzungumza na Viongozi mbali mbali katika Wilaya ya Dimani kichama,ambapo saa 9:00 ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Mfenesini kichama kwa kutembelea miradi mbali mbali na kuzungumza na Wana CCM.

Machi 12,mwaka huu Mwenyekiti wa UWT Taifa ataendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja kwa kukagua Utekelezaji wa Ilani katika Wilaya mbili za Mkoa huo.

Aidha ziara ya Mwenyekiti huyo itaendelea Machi 13, mwaka huu katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM sambamba na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Wilaya mbili za Mkoa huo.

Sambamba na hayo ziara hiyo itahitimishwa katika Mkoa wa Mjini Machi 14,mwaka huu ambapo Mwenyekiti huyo atatembelea miradi mbali mbali katika Wilaya mbili za Mkoa huo pamoja na kushiriki shughuli mbali mbali za Ujenzi wa Taifa.

Mwenyekiti huyo ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwaiba Kisasi, Katibu Mkuu wa UWT Mwl.Queen Mlozi pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania Bara Ndugu Jesca Mbogo na kupokelewa na Viongozi mbali mbali wa Chama na Jumuiya zote Tatu za UWT,uvccm pamoja na Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania

WAZIRI LUGOLA AAGIZA POLISI KUWAKAMATA WAPINZANI WANAOMTUKANA RAIS KUPITIA MIKUTANO YA NDANI, ASISITIZA MIKUTANO YA SIASA YA HADHARA MARUFUKU

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kilosa, Mkoani Morogoro, jana, ambapo amewaagiza Makamanda wa Polisi nchini kuwachunguza na kuwakamata wapinzani wanaomtukana Rais pamoja na Serikali kwa ujumla kupitia vikao vyao vya ndani vya siasa, nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kilosa, Amer Mbaraka, wakati alipokuwa anawasili katika Mkutano wa hadhara, mjini humo, Mkoani Morogoro, jana, kwa ajili ya kuzungumza na wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya Wizara yake. Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Adam Mgoyi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimfafanulia jambo Mkazi wa Mji wa Kimamba, Wilayani Kilosa, Aris Diamond, wakati alipokuja kutoa kero yake, katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini humo, jana. Lugola aliwataka Polisi Mkoani Morogoro kufuata sheria na utaratibu uliopangwa na Jeshi la Polisi bila kuwanyanyasa wananchi wakati taarifa za malalamiko ya ardhi yanaporipotiwa vituoni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkazi wa Mji wa Kilosa, Mkoani Morogoro, Juma Haruni akitoa malalamiko yake ya ardhi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani), wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Waziri huyo, na kufanyika katika uwanja wa Kilosa Town, Mkoani Morogoro, jana. Lugola aliwataka Polisi Mkoani Morogoro kufuata sheria na utaratibu uliopangwa na Jeshi la Polisi bila kuwanyanyasa wananchi wakati taarifa za malalamiko ya ardhi yanaporipotiwa vituoni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

UMMY MWALIMU AKEMEA WAAJIRI SEKTA BINAFSI KUFUKUZA KAZI WANAWAKE WAJAWAZITO

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu ( wa pili kulia) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na wanawake wa Mkoa Mwanza katika moja ya banda lililokuwepo katika viwanja vya Kisesa Bujora wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani humo kulia ni Mwalikishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake UN Women Bi. Hodan Addou na wa tatu kulia ni Balozi wa Sweden Bw. Anders.

……………………………………………………………………………..

Na Mwandishi Wetu Mwanza

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametaka kupewa taarifa za waajiri wote hasa Sekta Binafsi waliowafukuza wanawake kazi au kuwashusha vyeo kwa sababu wamepata ujauzito wakiwa kazini.

Ameyasema hayo mkoani Mwanza alipokuwa akizungumza na Wanawake na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Aidha ameitaka Jamii katika maeneo ya kazi kuondokana na rushwa za ngono jambo ambalo ni tatizo katika upatikanaji wa haki za wanawake na waajiri wa Sekta za Binafsi kuzingatia utu na haki za wanawake wafanyakazi.

“Mwanamke kupata mimba ni haki yake ya asili kutokana na uumbaji wa Mungu na hivyo ni marufuku kuwafukuza kazi Wanawake wafanyakazi hasa Sekta Binafsi kisa kuwa na ujauzito” alisema.

Ameongeza kuwa suala la usawa wa kijinsia ni muhimu kwa wanaume kushiriki kwani wao ni pia ni wahusika wakuu wa kuwepo kwa vitendo vya Ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Waziri Ummy amesema yeye kama Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Wanawake atahakikisha wanapata fursa sawa katika masuala muhimu kwa manufaa ya haki na ustawi wao.

Ameagiza kutekelezwa kwa haki ya Mwanamke kunyonyesha mara baada ya kumaliza likizo zao za uzazi kwani ni suala la muhimu sana kwa Mtoto kupata maziwa ya mama katika ukuaji wa Mtoto katika umri wa miezi ya awali.

Aidha Waziri Ummy amekemea vitendo vya rushwa ya nono na kuipongeza Taasisi ya kuoambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU
kwa kukiona suala hilo ni moja kti ya vitendo vya kikatili afanyiwavyo mwanamke na kumyima haki yake.

Akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Philis Nyimbi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana amesema mkoa unatekeleza mikakati mbalimbali katika kumuwezesha Mwanamke na Mtoto wa kike kwa kumuweka mbali na Vitendo vya Ukatili dhidi yao ili kuwawezesha kupata fursa zitakazowezesha kufikia usawa wa kijinsia.

Naye Mwakilishi Mkazi Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez amesema kuwa Umoja wa Mataifa unataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia na kuondoa vikwazo vyote vinavyosababisha kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia kama vile mimba na ndoa za utotoni ambazo zimekuwa zikiwanyima fursa watoto wa kike kutimiza ndoto zao.

Ameongeza kuwa mapambano wa usawa wa kijinsia yatafanikiwa pale yatakaposhirikisha wanaume na wavulana katika kuhakikisha wasichana na Wanawake wanapata fursa sawa katika kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake UN Women Bi. Hodan Addou amesema kuwa Shirika hilo linashirikiana na Serikali na Mashirika ya kitaifa kuhakikisha elimu inatolewa na usawa wa kijinsia inakuwa suala la kipaumbele katika Jamii zetu.

SERIKALI YAHAKIKISHA VYANZO VYA MAJI VINALINDWA KUFANIKISHA MRADI WA RUFIJI HYDRO POWER PROJECT

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (kushoto) akipata maelezo ya kitaalamu juu ya hali ya mazingira katika eneo la mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Rufiji Hydro Power Project kutoka kwa Dkt. Samuel Gwamaka Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Naibu Waziri amefanya ziara ya kikazi kutembelea eneo hilo mwishoni mwa wiki.
 
Na Lulu Mussa,Morogoro

Serikali imesema itahakikisha kuwa vyanzo vya maji vinavyopeleka maji Mto Rufiji havivamiwi kwa shughuli za kilimo na kibinadamu ili Mradi Mkubwa wa kufua umeme katika bonde la Mto Rufiji uweze kutekelezeka.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima mara baada ya kukamilisha ziara yake katika Mikoa sita hapa nchini kwa lengo la kukagua maeneo yenye changamoto za kimazingira pamoja na kutafuta ufumbuzi kwenye ikolojia ya vyanzo vya maji vinavyo changia maji katika bonde la Rufiji.

Akiwa katika eneo la mradi litakapojengwa bwawa la kufua umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji Naibu Waziri Sima amesema amefanya ziara ya kukagua vyanzo vya maji vya Bonde la Rufiji ambavyo vinahusisha matawi matatu ya mito ambayo ni Mto Ruaha Mkuu, Kilombero, Luegu, na kutoa wito kwa wananchi kutoharibu vyanzo hivyo ili kuwa na maji ya kutosha kutekeleza mradi huo mkubwa.

“Ziara yangu imeanzia Lindi, Ruvuma, Njombe, Mbeya, Iringa na Kilombero kote huko nimelenga kujione vyanzo hivi vikuu. Mito hii ya Ruaha Mkuu, Kilombero na Luegu inapoungana ndio inatengeneza Mto Rufiji ambako ndiko kuna maporomoko ya “Stiglers Gorge”. Na nimeridhishwa na hatua za watendaji katika ngazi zote za Serikali kwa kuwa mstari wa mbele kukahikisha kuwa vyanzo vya maji vinalindwa na kuhifadhiwa.” Sima alisisitiza.

Katika ziara yake Naibu Waziri Sima ameweza kutoa miongozo muhimu yenye kukuza, kulinda na kusimamia mazingira kwa namna endelevu husunan Ikolojia ya Vyanzo vya maji katika Mikoa aliyopita. Naibu Waziri Sima amesema Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa kufua umeme wa Maji wa Rufiji Hydro Power Project ambapo zaidi ya MW 2100 za umeme zitazalishwa, hivyo kulingana na ukubwa wa mradi huu ni wazi uhifadhi wa Mazingira katika vyanzo hivyo ni muhimu ukatiliwa mkazo.

“Uhifadhi wa Mazingira katika Bonde la Rufiji ni wafaida kwa pande zote hasa ustawi wa wananchi. Wananchi ndio walinzi na wahifadhi wa kwanza katika kutunza Mazingira, aidha Sheria ya Mazingira, 2004 kifungu cha 6 kimetamka wajibu wa kila mwananchi kutunza Mazingira kwamba; Mtu yeyote anayeishi Tanzania atakuwa mdau na atawajibika kutunza na kuendeleza Mazingira na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu shughuli au jambo lolote ambalo kwa kiasi kikubwa linaweza kuathiri mazingira. Hivyo kupitia sheria hii si jukumu la Serikali pekee kusimamia uhifadhi wa Mazingira, wananchi nao wana wajibu wa moja kwa moja wa kutunza Mazingira”. Sima alisisitiza.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini Dkt. Samuel Gwamaka alieambatana na Naibu Waziri Sima katika ziara hiyo amesema kuwa Baraza limedhamiria kufungua Ofisi katika eneo hilo la mradi ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya kila siku za Baraza.

Bonde la Rufiji lina ukubwa wa KM2 177,420 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya Tanzania na linapita katika mikoa 11 ya Tanzania na Wilaya 32 za Tanzania, Bonde hili ni Mashuhuri kwa Kilimo, ufungaji, uvuvi na uzalishaji wa umeme katika vituo vya Mtera na Kihansi.

KANYASU ASISITIZA MAHUSIANAO MEMA KATI YA WANANCHI NA ASKARI WANYAMAPORI

$
0
0


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akifunga Mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Canisius Kalamaga (kulia) mara baada ya Naibu Waziri huyo kufunga Baraza la 26 la Wafanyakazi wa Wizara lililofanyika jijini Mwanza kwa muda wa siku mbili. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Dkt. James Wakibala.
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda akizngumza kabla ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kufunga Mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara akizungumza na watumishi kabla ya Mhe. Constantine Kanyasu kufunga Mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Mwanza.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Adolf Mkenda akiwa ameshikana mikono na baadhi ya watumishi wakiimb wimbo wa mshikamano wakati wa Baraza la 26 la Wafanyakazi jijini Mwanza.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa wameshikana mikono wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa Baraza la 26 la Wafanyakazi jijini Mwanza.

……………………………….

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amewataka wananchi kuwachukulia askari wa Wanyamapori na Misitu kama rafiki wa umma na watendaji waliotumwa na Serikali kulinda rasilimali hizo kwa niaba yao.

Akifunga kikao cha 26 cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Mwanza, Mhe. Kanyasu amesema Askari hao waliopewa dhamana ya kulinda maeneo ya hifadhi nchini wanafanya kazi nzuri ya kuifanya Tanzania iendelee kuwa na maeneo mazuri yaliyohifadhiwa.

Amesema Askari hao wameajiriwa kwa mujibu wa sheria hivyo hutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kazi zao na pale wanapokiuka sheria mamlaka zinazohusika huwachukulia hatua.

“Sisi kama Wizara tunaamini kwamba askari wetu na wahifadhi wetu wanafanya kazi nzuri, pale ambapo wamekuwa wakilaumiwa kwa kuwapiga na kuwanyanyasa watu kwa namna yoyote ile tumetuma Tume maalum kuchunguza na kuchukua hatua” Amesema

Mhe, Kanyasu amesema uchunguzi unapofanyika na ikathibitika kuwa tukio lililofanyika halikuongozwa na matumizi ya sheria na kuwepo kwa haki wizara imekua ikichukua hatua.

Ameeeleza kuwa askari wanaolinda Hifadhi nchini wanategemewa na bila wao hakuna uhifadhi unaoweza kuendelea nchini akibainisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakipinga juhudi za uhifadhi kwa kuwatetea watu wanaovunja sheria.

“Watu hawafahamu tu, tukiwaondoa askari wetu wote katika maeneo ya hifadhi na tukawaondoa Maafisa ukaguzi wa mazao ya Misitu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) barabarani, katika kipindi cha miezi 6 nchi hii itageuka kuwa jangwa” Amesisitiza Mhe. Kanyasu.

Amesema yapo madhara makubwa yanayoweza kutokea kama hakutakuwa na uhifadhi imara ikiwemo maeneo mengi ya nchi kugeuka kuwa jangwa kutokana na uharibifu wa misitu, ukosefu wa mvua, ukosefu wa maji, chakula na ukosefu wa hewa safi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa kumekuwa na tuhuma za vitendo vya ukatili dhidi ya raia vinavyofanywa na baadhi ya askari wa Hifadhi nchini na kutoa wito kwa wananchi wote wenye ushahidi na taarifa juu ya vitendo hivyo kuziwasilisha ili hatua stahiki zichukuliwe.

Amesisitiza kuwa Serikali hairuhusu askari kufanya vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya raia badala yake imekua ikiwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa rasilimali zinazowazunguka.

Amewatahadharisha na kuwataka wananchi wawe makini dhidi ya kampeni zenye nia ovu zinazoendeshwa na baadhi ya watu zenye lengo la kuwavunja moyo askari wanaojitolea maisha yao kulinda rasilimali za taifa akieleza kuwa wapo askari waliopata madhara makubwa na kupoteza maisha kwa kushambuliwa na majangili kwa kuchomwa mishale yenye sumu na kukatwa vidole wakati wakitimiza wajibu wao.

Prof. Mkenda amesema kuwa wizara itaendelea kulinda hadhi ya vijana hao waliojitolea maisha yao kulinda rasilimali za Taifa akibainisha kuwa Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria watakaokiuka kanuni na taratibu za kazi kazi ili iwe fundisho kwa wengine.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo amesema kuwa watumishi 23 wa wanyamapori na misitu wamepoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa katika matukio tofauti yaliyotokea wakati wakipambana na majangili.

Amesema matukio hayo yametokea mwaka 2018/2019 na hifadhi inayoongoza kwa matukio hayo ni Sengereti, Prof. Mkenda amesema kuwa watumishi hao waliofariki na wengine kujeruhiwa walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kazi hivyo Wizara inaangalia namna ya kuwaenzi kutokana na mchango wao.

Diwani KAMALA kumuenzi Ruge kwa Vitendo .

$
0
0
   Katika Kumuenzi Marehemu Ruge Mutahaba kwa Vitendo na maisha alokuwa akiyaishi, yakiwemo kusaidia vijana na kuinua vipaji vya Vijana katika sekta mbalimbali, Diwani wa Kata Ijuganyondo iliyopo Manispaa ya Bukoba Al-Masoud Kamala ametangaza kuanzisha Rasmi ligi ya Mpira wa Miguu itayojulikana kama "Ruge Cup"

Diwani Kamala ameyasema hayo katika fainali ya kombe la Wazee lililoandaliwa na Wazee wa Kata ya Kibeta chini ya Mwenyekiti wao Bwana Sadru Nyangasha, ambapo katika Fainali hizo zilizochezwa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kibeta na kuhudhuriwa na wakazi wa kata hiyo na kata jirani, Timu ya Omkituri Fc imeibuka kidedea kwa Ushindi wa Goli 2 kwa 1 dhidi ya Anyama Fc.

Mh. Kamala amesema ili kumuenzi Ruge kupitia Tasnia ya Michezo hususani mpira wa Miguu anaratibu ligi ya Mpira wa Miguu itayoanza hivi Karibuni itakayoitwa Ruge Cup. Katika mashindano hayo ya Kombe la wazee yaliyoshirikisha jumla ya timu sita, Zawadi kutoka kwa Waandaaji Mshindi wa Kwanza kajipatia Kikombe chenye Thamani ya Shilingi Laki Moja, Mbuzi (mnyama) mwenye thamani ya Shilingi laki moja, mshindi wa pili elfu 30, mshindi wa tatu elfu 20, ukiacha zawadi alizotoa Diwani Kamala Pesa taslimu pamoja na mipira miwili.
 Nahodha wa Timu ya Omkituri Gerevazi Nyomo akiwa amebeba Kombe la Wazee Mara baada ya kumalizika mchezo wa fainali uliowakutanisha na Anyama Fc, na Kuibuka kwa ushindi wa bao 2 kwa 1.
Pichani Diwani Kamala akisaidiana na Mzee Sadru Nyangasha muaandaji wa mashindano ya Kombe la Wazee, kukabidhi zawadi ya Mbuzi kwa Timu ya Omkituri Fc.
 Mbuzi aina ya Beberu mwenye thamani ya Shilingi laki moja aliyetolewa kama zawadi kwa Mshindi wa kwanza katika mashindano ya Kombe la Wazee.
Kombe lenye thamani ya Shilingi laki moja likiwa Mezani kabla ya Kupewa Mshindi wa Mashindano ya Kombe la Wazee timu ya Omkituri Fc.


Dereva apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuendesha gari kizembe

$
0
0
DEREVA, Geofrey Elifuraha mkazi wa jijini Dar es Salaam,  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na  tuhuma za kuendesha gari kizembe. 

Katika kesi hiyo namba 257/2019 mshtakiwa huyo amesomewa Shtaka lake hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Hanifa Mwingira. 

Imedaiwa Kuwa, February 5 mwaka huko Kinondoni Hananasifu Mtaa wa Mkulima,  uliopo Katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Elifuraha alitenda kosa hilo. 

Imedaiwa, siku ya tukio,  mshtakiwa akiwa dereva anayeendesha gari namba T. 859CYT aina ya Toyota Noah, aliendesha gari hilo kwa uzembe na kushindwa kulimudu, hatimae akatoka nje ya barabara kisha kugonga mti na kusababisha uharibifu wa gari hilo.

Hata hivyo mshtakiwa huyo amekiri kutenda kosa hilo na amehukumiwa kulipa faini ya Sh. 30,000 ama kutumikia kifungo cha  miezi sita gerezani.

Aidha Mahakama imechukua leseni ya dereva huyo kwa kipindi cha mwezi mmoja. Hata hivyo dereva Elifuraha alifanikiwa kulipa faini hiyo na kufanikiwa kukwepa kifungo hicho.

Hakuna Mtanzania aliyepoteza maisha kwenye ajali ya ndege iliyotokea Ethiopia

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea kwa masikitiko makubwa, taarifa kuhusu ajali ya ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Ethiopia, iliyotokea tarehe 10 Machi 2019 nchini Ethiopia na kusababisha vifo vya watu wote 157 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

Ndege hiyo ya abiria, aina ya  Boeing 737 yenye namba za usajili ET 302 iliyokuwa inafanya safari zake za kawaida kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, mjini Addis Ababa, Ethiopia kuelekea mjini Nairobi, Kenya, ilikuwa imebeba abiria 149 kutoka mataifa mbalimbali na wafanyakazi wa kwenye ndege wapatao 8.

Kwa mujibu wa taarifa kuhusu ajali hiyo, iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Ethiopia, ikiwemo orodha ya abiria na mataifa wanayotoka, hakuna Mtanzania aliyekuwemo kwenye ndege hiyo.

Orodha ya nchi na idadi ya raia (kwenye mabano) waliokuwa kwenye ndege hiyo  ni kama ifuatavyo: Kenya (32), Canada (18), Ethiopia (9), China (8), Italia (8), Marekani (8), Ufaransa (7), Uingereza (7), Misri (6), Ujerumani (5), India (4), Slovakia (4), Austria (3), Urusi (3), Sweden (3), Hispania (2), Israel (2), Morocco (2) na Poland (2).

Nchi zingine ni Ubelgiji (1), Djibouti (1), Indonesia (1), Ireland (1), Msumbiji (1), Norway (1), Rwanda (1), Saudi Arabia (1), Sudan (1), Somalia (1), Serbia (1), Togo (1), Uganda (1), Yemen (1), Nepal (1), Nigeria (1) na raia aliyekuwa na hati ya kusafiria ya Umoja wa Mataifa (1).

Mamlaka husika zimeanza uchunguzi ili kujua  chanzo cha ajali hiyo.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaungana na wote walioguswa na msiba huu mzito kutoa pole kwa mataifa yote yaliyopoteza raia wake kwenye ajali hiyo.



Imetolewa na: 
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dodoma.

10 Machi 2019

PRESIDENT MAGUFULI MOURNS VICTIMS OF THE ILL FATED ETHIOPIAN AIRLINES' BOEING 737 MAX 8


NMB yazindua ‘Floti Fasta’ kwa Mawakala wao

$
0
0
VINARA wa huduma za kibenki nchini, Benki ya NMB, wamezindua huduma ya kidijitali ya kuwawezesha Mawakala wa NMB kupata mkopo wa salio la kuhudumia wateja ‘Floti Fasta,’ kupitia NMB Mobile na NMB KLiK pindi wanapoishiwa salio.

Floti Fasta ni huduma ya uwezeshaji, inayolenga kuwapa nguvu ya ziada mawakala wa NMB waliotapakaa kila kona, kupata salio la dharura wanalohitaji kuhudumu nyakati za usiku ama wikiendi, wanapokosa huduma za kuongeza salio katika matawi ya benki hiyo.

Huduma hiyo ya kwanza na ya aina yake nchini, imezinduliwa mwishoni mwa wiki, ikilenga kukuza mitaji ya mawakala, lakini pia kuwasaidia kukuza biashara zao, huku wakitengeneza ajira kwa Watanzania wengi kupitia biashara zao za NMB Wakala.

Kiwango cha chini cha kupata salio kupitia ‘Floti Fasta’ni Sh. 50,000 na kiwango cha juu ni Sh. Milioni 5, huduma ambayo haina riba, bali mwombaji atatozwa asilimia 3 itakayojumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambako tozo litafanyika kabla ya mkopo kutolewa.

Akizungumza wakati wa kuzindua Floti Fasta, Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Akaunti, Michael Mungure, aliscma kuwa huduma hiyo, itawawezesha zaidi ya mawakala 6,800 kukuza biashara zao na kuwapa uwezo wa kuhudumia wateja wao muda wote.

“Kupilia huduma hii ya Floti Fasta, tatizo la kuishiwa salio kwa mawakala wetu limepatiwa ufumbuzi, Mteja anatakiwa kutumia NMB Mobile au NMB KliK kuweza kupopa hususani kwa nyakati ambazo hakuna huduma za kibenki kama usiku ama wikiendi,” alisema Mungure.

Mungure aliongeza kuwa: “Dhamira yetu kila siku imekuwa ni kubuni bidhaa na huduma bora kwa kuangalia changamoto mbalimbali za kifedha nchini na kuzipatia suluhu.

“Imekuwa wazi kuwa kuna changamoto kubwa kwa mawakala ya kuishiwa floti na hivyo kusababisha wateja kutopata huduma stahiki za kutoa na kuweka fedha hususani baada ya matawi ya NMB kufungwa.

“Tulipoliona hili tukaona ni fursa kubwa kutoa suruhisho la kifedha ambalo ni rafiki kwa mawakala kupitia NMB Mobile na NMB KLiK,” alisisitiza Mungure.

Mawakala wa NMB wana mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za kifedha na hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa, ambapo Mungure amebainisha kuwa NMB ikiwa kama benki kubwa hapa nchini, inaona umuhimu wa kuwasaidia mawakala wake ilikukidhi mahitaji ya soko.

“Kwa sasa, wateja wanaopata huduma za kifedha kupitia NMB Wakala wana uhakika wa kupata huduma pasipo hofu ya kukosa floti, kwani kupitia huduma hii, Mawakala wa NMB wanakuwa ndio wa uhakika zaidi katika utoaji huduma za kifedha muda wowote na sehemu yoyote,” alisema.

Mungure alisema kuwa, pamoja na kwamba huduma hiyo imeanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia mawakala wa NMB, faida yake inakwenda mbali zaidi na kumfikia hata asiye mteja wa NMB, ambaye ataweza kulipa Kodi za Serikali na bili kama za Dawasco, LUKU, muda wa maongezi na kulipa ving’amuzi.
 Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, Donatus Richard akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma mpya ya kiditali Floti Fasta. Katikati ni  Mkuu wa malipo na akaunti, Michael Mungure na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha wakala, Ericky Willy.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, Donatus Richard akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma mpya ya kiditali Floti Fasta. Kulia ni Mkuu wa malipo na akaunti, Michael Mungure.
 

Kamati ya kitaifa mradi wa BEAR II yakutana Dar

$
0
0
KAMATI ya kitaifa ya mradi mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) imekutana jijini Dar es salaam kupitia pamoja na mambo mengine ratiba ya utekelezaji wa mradi huo.
Mradi huo ambao unajulikana kama The Better Education for Africa's Rise, (BEAR) unaendeshwa pia katika nchi za Madagascar, Ethiopia, Uganda na Kenya na ni sehemu ya mradi wa kimataifa wa elimu maarufu kama Education 2030 Agenda , moja ya malengo ya maendeleo endelevu ya kimataifa, lengo namba nne, na unafadhiliwa na Korea kusini kwa dola za Marekani milioni 10.
Akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la UNESCO nchini, Faith Shayo alisema kwamba mradi huo unaotarajiwa kukamilika 2021 umelenga kuboresha utaalamu na kuwezesha vijana kuajiriwa au kujiajiri wenyewe kwa kuangalia fursa zilizopo kwa kadri ya mahitaji ya nchi.
Mradi huo ambao sasa unaingia katika awamu ya pili,na hivyo kujulikana kama BEAR ll ulianza mwaka 2017 na unatarajiwa kutekelezwa hadi 2021, kazi kubwa ikiwa ni kuwezesha vijana kupata ajira zenye staha na pia kujenga uwezo wa kujiajiri kwa vijana kwa kuboresha mifumo na ufundishaji wa elimu ya ufundi stadi.
Alisema nchini Ethiopia, mradi huu umejikita zaidi katika sekta ya uchakataji mazao ya kilimo; Kenya ipo uhifadhi wa mazingira, utengenezaji wa nafasi za kazi za kutunza mazingira; Madagascar ipo kwenye viwanda vya nguo; Uganda imejikita katika menejimenti ya mazao baada ya kuvunwa na uchakataji wa bidhaa za chakula zinazotokana na kilimo wakati nchini Tanzania imejikita katika biashara za mazao ya kilimo na ubunifu.
“Tunatarajia baada ya kukamilika kwa mradi huu kutakuwepo na maendeleo makubwa katika mifumo ya elimu na ufundishaji wa elimu ya ufundi stadi nchini Tanzania,” alisema Shayo wakati akiwasilisha mpango kazi unaotakiwa kufuatwa katika kikao hicho cha kitaifa mwishoni mwa wiki.
Alisema kwamba BEAR II inatekelezwa kwa kuzingatia fundisho lililopatikana kwenye awamu ya kwanza iliyoanza 2011-2016 ambayo ilisaidia kunoa mifumo ya ufundi stadi na ufundishaji wake katika nchi 5 za Jumuiya ya Uchumi Kusini mwa Afrika (SADC)  za Botswana, DR Congo, Malawi, Namibia, na Zambia.
BEAR II ambayo inajengwa  kwa kuzingatia vipaumbele vya kila taifa, inaingilia maeneo matatu ili kufanya mafunzo ya ufundi kuwa na maana zaidi kwa kuzingatia mahitaji ya kiuchumi na soko; kuboresha zaidi programu zinazoambatana na elimu hiyo na pia kuboresha uelewa na matamanio ya elimu ya ufundi miongoni mwa vijana.
Mradi wa BEAR kwa kila nchi unafanywa kwa ushirikiano kati ya wadau mbalimbali wa elimu, wizara ya elimu na serikali za nchi husika.
Imeelezwa kuwa kazi kubwa ya UNESCO katika mradi huo ni ya menejimenti, ufuatiliaji na ufanyaji wa tathmini na serikali ya Korea yenyewe itatengeneza mfumo wa ufuatiliaji na kufadhili utekelezaji wake.
 Ofisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Jennifer Kotta akitambulisha meza kuu wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akitoa neno la ukaribisho wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo.
 Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (wa pili kushoto) akibariki kuanza kwa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Balozi wa Ubalozi wa Korea Kusini nchini, Jiin An, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee Abdulla (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kushoto).
 Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la UNESCO nchini, Faith Shayo akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia Dk. Noel Mbonde akiwasilisha mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Naibu Balozi wa Ubalozi wa Korea Kusini nchini, Jiin An akishiriki kwenye majadiliano na makubaliano kuhusu mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee Abdulla
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee Abdulla akiwasilisha maoni kwenye majadiliano na makubaliano kuhusu mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo na kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos.
 Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (katikati) akiendesha majadiliano na makubaliano kuhusu mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee Abdulla na kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos
 Ofisa Mwandamizi Elimu, kitengo cha Elimu ya Ufundi Stadi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Fides Lubuva akiwapitisha wajumbe kwenye bajeti wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Unesco (UNESCO-NATCOM), Francis Msungu akishiriki kwenye majadiliano na makubaliano kuhusu mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wajumbe wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa wajumbe akichangia maoni wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 11,2019

UNITED BANK FOR AFRICA (UBA) BANK CELEBRATES WOMEN DAY BY DONATING BEDDING MATERIALS TO TEMEKE HOSPITAL

$
0
0

The United Bank for Africa Tanzania (UBA) has celebrated the International Women’s Day by donating 100 bed sheets to Temeke Referral Hospital in Dar es Salaam being one of the banks Corporate Social Responsibility (CSR) initiative in supporting the surrounding community.

The Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki, Temeke Member of Parliament Abdallah Mtolea and the Hospitals Senior Consultant Dr Amaan Malima received the donation of the bed sheets on behalf of the hospital.

Speaking after receiving the donations, the Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki said the International Women’s Day is a special day for women to celebrate the social, economic, cultural and political achievements of women. For that matter, I am very happy to learn that the United Bank for Africa Tanzania women staff have contributed their own funds that they have used to purchase the donations of bed sheets we are receiving today. You could have used the money on your celebrations but they decided to and celebrate with the less privileged and sick in this hospital. That is something that must be emulated by others and to me you have set a very good example and I must congratulate you for that, Minister Kariuki said.

The minister added that women are important pillars for our family and nation. You must always work hard and set goals in order to be successful. In addition, it is good to understand that women have the same talents and ability to work just like your counterpart men but is good to stay focused and set your time properly in order to continue being successful on your careers, said Kariuki. Adding, “I call upon UBA Tanzania and other stakeholders to continue supporting us our communities and especially in health sector so that we grow as one nation.

The Temeke Referral Hospital Hospitals Senior Consultant Dr Amaan Malima appreciated the banks donation saying that the hospital has been experiencing shortage of bed sheets for quite long time. ‘Your donation has come at very right time our hospital has been going a difficult time due to bed sheets. We receive large number of patients and so the number cannot match on the bed sheets we have. We cherish you danations and wish you good luck on your activities and we welcome you again for any other donations in future, Dr Malima said.

On his part, UBA Bank Tanzania Chief Operating Officer Flavia Kiyanga said that giving back to the community has been one of the banks’ long time initiatives. The surrounding society means a lot to us, by extending our hands to less privileged is our concern and this time we have decided to support Temeke Referral Hospital putting in mind that some of the patients admitted at this hospital have no close relatives to support them and therefore donating and visiting them will make them feel just like the others.

Kiyanga said that the donation of the bed sheets has been as result of UBA Tanzania women who have decided to contribute their own funds to come and celebrate the women’s International Day by donating bed sheets to this hospital. We are happy that we have managed to fulfill one of our longest commitments and most important we thank the Temeke Referral Hospital for good treatment they have offered to us, said Kiyanga.

UBA Bank Tanzania Chief Operating Officer Flavia Kiyanga (right) hands bed sheets to The Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki (2nd right). UBA Bank Tanzania donated 100 bed sheets to Temeke Referral Hospital as way of celebrating this year’s Women Day Left is Temeke Member of Parliament Abdallah Mtolea and the Hospitals Senior Consultant Dr. Amaan Malima (2nd left). 

UBA Bank Tanzania Chief Operating Officer Flavia Kiyanga (right) hands bed sheets to Temeke Member of Parliament Abdallah Mtolea (left) in Dar es Salaam over the weekend. UBA Bank Tanzania donated 100 bed sheets to Temeke Referral Hospital as way of celebrating this year’s Women Day. Looking on are The Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki (2nd right) and the Hospitals Senior Consultant Dr. Amaan Malima (2nd left). 


The Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki (2nd right) and Temeke Member of Parliament Abdallah Mtolea (left) keenly examine bed sheets donated by UBA Bank Tanzania to Temeke Referral Hospital. UBA Bank Tanzania donated 100 bed sheets to Temeke Referral Hospital as way of celebrating this year’s Women Day. Right is the Hospitals Senior Consultant Dr. Amaan Malima.
The Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki (2nd right) and Temeke Member of Parliament Abdallah Mtolea (left) display bed sheets donated by UBA Bank Tanzania to Temeke Referral Hospital. UBA Bank Tanzania donated 100 bed sheets to Temeke Referral Hospital as way of celebrating this year’s Women Day. Right is the Hospitals Senior Consultant Dr. Amaan Malima.

MAKAMU WA RAIS KUHUDHURIA MKUTANO WA AFRICA NOW SUMMIT 2019 MJINI KAMPALA - UGANDA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kuelekea Kampala, Uganda kushiriki kwenye Mkutano wa mwaka 2019 wa ‘Africa Now Summit’unaotarajiwa kufanyika tarehe12 na 13 Machi.Mhe. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano huu. Mkutano utakuwa na mada mbalimbali ikiwemo ya Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika, mada hii itatolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi wengine watakaotoa mada ni Rais wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA) Mhe. Abdel Fattah el Sisi; Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa; Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. William Ruto; na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Ahmed Abiy. Mada zote hizi zitajikita kwenye kuonesha chachu ya Uongozi katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika. 
Mkutano utamalizika tarehe 13 Machi 2019 utaanza na hotuba kutoka kwa Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi na baadae kufungwa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.
Makamu wa Rais ataambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. 

Imetolewa na: 
Ofisi ya Makamu wa Rais 
Dar es salaam 
11/03/2019
Viewing all 110035 articles
Browse latest View live




Latest Images