Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 277 | 278 | (Page 279) | 280 | 281 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la 
  Michezo Wizarani Bw.Moshi Makuka 

  Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo la Wizarani (SHIMIWI) Bw. Moshi Makuka amesema shirikisho hilo linatarajia kufanya mkutano wa tathmini wa mashindano ya SHIMIWI ya mwaka huu mjini Morogoro tarehe 13 na 14 Desemba, 2013.

  Akiongea ofisini kwake Bw.Makuka alisema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kujadili changamoto zilzojitokeza kwenye mashindano ya mwaka huu.

  “Lengo ni kujadili changamoto zilizojitokeza katika mashindano ya SHIMIWI ya mwaka huu na kuzipatia ufumbuzi kwa ajili ya kuboresha michezo ya mwaka ujao” alisema Bw.Makuka.

  Aidha,Bw Makuka aliwataka Wenyeviti wa vilabu,Makatibu wa Vilabu na Maafisa Michezo kufika bila kukosa ili kukuza michezo serikalini.

  “Wenyeviti,Makatibu na Maafisa Michezo wa vilabu wahudhurie kwa wingi ili waje kutoa changamoto zao walizokutana nazo katika michezo ya mwaka huu” alifafanua Bw.Makuka.

  Shirikisho la Michezo Wizarani (SHIMIWI) kila mwaka huandaa michezo inayowakutanisha watumishi wa serikali kutoka katika Wizara,Idara zinazojitegemea,Wakala wa serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa ambapo kwa mwaka huu yalifanyika mjini Dodoma kuanzia tarehe Septemba 21 hadi Oktoba 5.


  Wajumbe wanaotakiwa kuhudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti, Katibu na maafisa michezo wote kutoka vilabu vya SHIMIWI. Hadi sasa mikoa ya Dodoma na Kilimanjaro imeshatuma maombi ya kushiriki, na mikoa mingine inahimizwa kufanya hivyo mapema iwezekanavyo>

  0 0
 • 11/26/13--23:19: Nemc lawamani KILWA
 • Na Abdulaziz Video, Lindi
  Wananchi wa wa vijiji vya Singino wilayani Kilwa mkoani Lindi wamelalamikia Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC )kwa kitendo cha kutokusimamia vyema kazi iliyopewa na Bodi ya Korosho Tanzania katika zoezi la uteketezaji kemikali zilizotelekezwa kwa zaidi ya miaka 20 zinazosadikika kuwa sumu inayoweza kuathiri afya ya binadamu, mifugo na mimea. 
  Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao Diwani wa kata ya Kivinje, Bw. Jafari Arobaini na Mwenyekiti wa kijiji cha Singino Maulidi Mbulula walisema kitendo cha mkandarasi kumwaga ovyo dawa hizo kunaweza kusababisha madhara makubwa kwa wananchi,mifugo na mimea na kuathiri kukua kwa mji huo. 
  Pamoja na zoezi hilo kusimamiwa na watu wa mazingira lakini bado zoezi linaonyesha kutotekelezwa kama lilivyopangwa katika makubaliano ya pamoja kati ya serikali ya kijiji, halmashauri, na NEMC baada ya kukutwa kemikali hizo zikiwa zimemwagika njiani 
   Bw. Bakari Mussa Mkazi wa kilwa Masoko ambae alipata kazi katika ghala hilo alieleza athari alizoziona na kuacha kazi hiyo kulinda afya yake huku Abdu Saidi mjumbe wa Singino ameomba uongozi wa wilaya kusimamisha zoezi ili kunusuru maisha ya wananchi wa eneo hilo kutokana na ukiukwaji unaoonekana sasa kazi inavyoendelea. 
   Kwa upande wake Afisa msimamizi mazingira NEMC Jorome Kayombo alisema kuwa awali NEMC ilimwagiza mkandarasi kuchimba shimo futi tano na kutandika kapeti chini, pembeni na juu ili kuzuia mwingiliano wa kemikali hizo na udongo huku akikataa kupigwa picha na kutoa ufafunuzi zaidi wa kemikali hizo kwa madai si msemaji wa NEMC 
  Katika hali isiyo ya kawaida Uongozi wa ghala hilo ulimwamuru mlinzi kutoruhusu waandishi kuingia kuangalia hali ya utoaji wa madawa hayo ghalani kufuatia malalamiko ya vibarua wanaofanya kazi hiyo hatarishi
  Eneo la uteketezaji kemikali hizo
  Mkaazi wa maeneo ya Singino wilayani Kilwa mkoani Lindi akionesha hali ilivyo
  Mmoja wa mifuko ukiwa umeanguka chini

  0 0
 • 11/26/13--23:32: Article 20


 • 0 0

  Katika kuelekea Fainali ya EBSS 2013 kesho kutakuwa na Press Conference pale katika ufukwe wa ESCAPE ONE  Saa Tano Asubuhi, ambapo utawaona washiriki wote walioingia Fainali kwa pamoja kabla ya siku yenyewe ya Jumamosi tarehe 30 ambapo wote kwa pamoja tutashuhudia Yule Mshindi wa Milioni 50.

  Waliofanikiwa kuingia fainali ni Amina Chibaba (MBEYA), Melisa John (DSM), Elizabeth Mwakijambile (DSM), Emannuel Msuya (MWANZA) na Maina Thadei (DSM)

  Pia siku ya Fainali kutakuwa na Burudani kutoka kwa Snura, Barnaba, Young Killer, Shaa, Walter Chilambo, Peter Msechu  na Makomandoo

  Kiingilio katika Fainali hizo kitakuwa : VIP TSH 50,000/= KAWAIDA  : TSH 20,000/=

  Tiketi  za siku ya Fainali zinapatikana sehemu zifuatazo :
  -          Shear illusion
  -          Biggy Respect (Kariakoo)
  -          Steers Mjini
  -          Zizzoue Fashion (Victoria na Sinza)
  -          Photo Point (Mayfair)
  -          Robby One Fashion (Kinondoni)
  -          Best Bite
  -          Engen Mbezi
  -          Escape One (Mikocheni)
  -          Benchmark Office Mikocheni
  -          American Nails (Kinondoni)

  0 0

  Tarehe 24 Nov 2013 Swahili Fashion Week walifanya mchujo wa kutafuta wanamitindo mbalimbali ambao wataonesha mavazi ya wabunifu katika wiki ya maonesho ya mavaz ya swahili kuanzia tarehe 5 dec hadi tarehe 8 dec 2013, wanamitindo mbalimbali walijitokeza kwa wingi kutaka kushiriki kwa namna moja na nyingine katika maonesho hayo.
  Mgeni rasmi alikuwa Herrieth Paul ambaye ni mwanamitindi maarufu Mtanzania mwenye makazi yake nchini Canada, waliohudhuria maonesho hayo pia alikuwapo Jamillah Vera Swai,(Mbunifu wa Mavazi), Gabriel Mollel (Mbunifu wa mavazi), Pedaiah John (Mbunifu wa Mavazi), Honest Arroyal (Mratibu wa mitindo na ubunifu SFW), Mustafa Hassanali (Mwanzilishi wa Swahili Fashion Week) na Esi Mgimba (Afisa Habari na Mahusiano SFW)
  Wanamitindo wa kike katika mchuzjo wa pili
  wanamitindo wa kike wakijiandaa kuonesha uwezo wao wa kutembea
   jukwaani katika mchujo wa pili
  wanamitindo wa kiume wakionesha mbwembwe zao za kutembea 
  jukwaani katika mchujo wa pili.

  wanamitindo wa kiume wakiwa katika mchujo wa tatu
  wanamitindo wakimsikiliza mwanamitindo maarufu duniani ... 
  H. Paul ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchujo huo
  jopo la majaji wakijadiliana jambo kuhusiana na wanamitindo 
  waliopita katika mchujo

  0 0

  Kapteni wa timu ya mpira wa miguu ya NMB tawi la Kilombero,Taiti Kamba akipokea kombe la ushindi kwa niaba ya timu yake, kutoka kwa Meneja wa NMB kanda ya Mashariki Bw. Nazareth Lebbi (tatu kushoto) baada ya kuibuka washindi katika bonanza la Ujirani Mwema kwa taasisi zilizopo Kidati-Kilombero lililoshirikisha timu 12. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Ofisa wa Ilovo Romanus Mwaipinga, Mkurugenzi Rasiliamali watu-Ilovo Bw. Beda Marwa, Meneja wa tawi la Kilombero, Bw.Henry Shadolo pamoja na Maofisa kutoka NMB.

  0 0

  Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dr. Syrivia Mamkwe akizungumza katika mkutano wa uanzisshwaji wa mpango wa Tiba kwa Kadi (TIKA) katika Manispaa hiyo. Mpango huo unasimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
  Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Betha Minga akifungua mkutano huo.
  Ofisa Sheria wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Matilda Kagombora akitoa salaam za wizara kwa wadau wa TIKA.
  Wadau wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo.


  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka maafisa mipango miji nchini kurekebisha utendaji wao wa kazi ili waweze kubadili taswira mbaya iliyojengeka miongoni mwa jamii dhidi yao.

  Ametoa kauli hiyo huo leo mchana (Alhamisi, Novemba 27, 2013) wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Wataalam wa Mipangomiji waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji ulioanza leo jijini Dar es Salaam.

  “Taswira ya utendaji kazi katika taaluma ya mipangomiji na katika  sekta  ya  ardhi  kwa  ujumla miongoni mwa wananchi na Serikali siyo nzuri sana. Watafiti wanatueleza kuwa kati ya asilimia 60 na 80 ya makazi kwenye miji  yetu hapa nchini yamejengwa kiholela. Na kwa kiwango hicho hicho wakazi wa mijini wako kwenye makazi hayo na wanaishi kiholela,” alisema.

  “Wako wanaosema ninyi ndiyo chanzo cha hiyo migogoro, wako wanaosema ninyi kwa rushwa ndiyo wenyewe, mimi sishangai madai haya ila ninawasihi muwe na roho ngumu katika kushinda vishawishi hivi,” alisisitiza.


  0 0

   Miongoni mwa vitendo vinavyoshamiri Makete vya watoto kujihusisha na biashara ya kuuza mkaa
   Mkaa ukisubiri wateja.
  -------
  Na Edwin Moshi,Makete.

  Mafunzo ya ulinzi na usalama wa mtoto dhidi ya ukatili na unyanyasaji yaliyoanza jana wilayani Makete mkoani Njombe yanaendelea katika ukumbi wa Sumasesu Tandala

  Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Makete Bw. Leonce Panga yameshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, dawati la jinsia kutoka kituo cha polisi Makete, maafisa elimu, mwanasheria, magereza, wauguzi, madaktari pamoja na hakimu mfawidhi wa wilaya ya Makete

  Katika mafunzo hayo yanayowezeshwa na Bi Asha Mbaruku pamoja na Ramadhani Yahaya kutoka  ustawi wa jamii makao makuu jijini Dar es Salaam wamesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wadau hao namna ya kuwahudumia watoto wanaokuwa wamefika kwenye ofisi zao kupata msaada endapo anakuwa amepata tatizo akitolea mfano kufukuzwa shule kwa kukosa ada

  Wamesema washiriki hao wanapaswa kuwa timu ya ulinzi na usalama wa mtoto ili waweze kumsaidia mtoto, huku Bi Asha akisisitiza kuwa kuna huduma ya msaada kwa watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili iliyoanzishwa wizarani inayoitwa huduma mtandao (Child helpline) inayohusu mtoto kupiga simu moja kwa moja na kueleza shida yake na kupatiwa suluhu

  Washiriki pia wamefundishwa njia mbalimbali za ufundishaji wa masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto kwa ngazi ya chini ya serikali

  Kwa upande wao washiriki wametoa visa mbalimbali vinavyoendelea katika jamii ya Makete ikiwemo kata ya Mbalatse ambayo watoto wa kike wanafanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa siri kubwa

  Mafunzo hayo yameweka wazi hatua zinazochukuliwa na serikali kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo kutunga na kusimamia sheria mbalimbali zinazomlinda mtoto


  Mafunzo hayo ya siku 5 yaliyoanza jana yameandaliwa na ustawi wa jamii makao makuu jijini Dar es Salaam na yanatarajiwa kuhitimishwa Jumamosi wiki hii

  0 0

  DSC_0063Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark Ltd. Chedi Ngulu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Bodi ya ushauri wa Umoja wa Afrika ya kupambana na Rushwa yaani African Union Advisory Board on Corruption (AUABC) na Tamasha la wasanii lenye lengo la kufikisha ujumbe juu ya Madhara ya Rushwa kwenye Jamii, Kati kati ni Emmanuel Atenga toka (AUABC) na Stephane Ndilimbaye toka AUABC.


  0 0

  Hon. Bernard K. Membe (MP), Tanzania Minister for Foreign Affairs and International Co-operation and Hon. Ephraim Chiume, Malawi Minister for Foreign Affairs and International Co-operation today handed over the written submission of the issues raised by the Mediation Forum of the Africa former Heads of State and Government of the Southern African Development Community (SADC) in Maputo, Mozambique. The meeting took place at the office of the former Mozambique President Joachim Chissano in Maputo. (All Photos by Tagie Daisy Mwakawago, Maputo - Mozambique).

  0 0

  Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama, akimtangaza mwimbaji kinara wa Tamasha la Krismasi 2013 kutoka Afrika Kusini, Pastor Solly Mahlangu “Obrigado” ambaye ataimba na kundi lake uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Desemba 25.
  =====  =====  ====
  WAKATI Tamasha la Krismas likikaribia, muimbaji nguli wa muziki wa Injili wa Afrika Kusini, Solly Mahlangu ‘Obrigado’ni mmoja wa waimbaji ambaye anatarajia kuimba kwenye tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama mwimbaji huyo ataimba live siku hiyo pamoja na waimbaji wake wengine 14.Msama alisema mwimbaji huyo anatarajia kushiriki katika tamasha hilo jijini Dar es Salaam, tamasha ambalo litafanyika pia katika mikoa ya Morogoro (26), Tanga (28), Arush(29) na Dodoma (1). 

  Aidha Msama alisema bado wanaendelea kufanya mazungumzo na waimbaji wengine yameshakamilika kwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja, Solomon Mukubwa (Kenya), Ephraim Sekeleti (Zambia), Liliane Kabaganza (Rwanda). Waimbaji wa Tanzania ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, New Life Band na John Lissu.


  0 0

  Marehemu Jerry Mruma alikuwa mwanafunzi wa uzamili katika chuo kikuu cha kimataifa cha USIU Nairobi alikutwa alhamisi iliyopita katika chumba cha maiti mjini Nairobi baada ya kuripotiwa kupotea tangu Jumamosi iliyopita.
  Jerry alikuwa mmiliki wa kampuni ya Kilimo yetu akiuza hisa za Kilimo kijana huyu mtanashati na mwenye akili ya biashara alikuwa akisoma wakati huo huo akifanya biashara hii iliyopata umaarufu sana huko nchini Kenya. 
  Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi na kamera za CCTV ni kwamba Jerry alionekana hai mara ya mwisho saa tano na dakika tisa usiku alipokuwa akitoka kwenye hafla ya usiku wa Mtanzania aliyokuwa ameandaa katika hoteli ya Sarova. 
   Aliondoka hotelini hapo kwa miguu akiwa peke yake na kwa mujibu wa Chuo hicho alituma ujumbe wa mwisho kwa rafiki yake wa kike mnamo saa 5 na dakika 38 za usiku akimwambia ametoka kwenye hafla hiyo na anaelekea nyumbani kwake. 
  Jerry aliwahi kufanya mazungumzo na Sauti ya Amerika juu ya kampuni yake Kilimo yetu nchini humo. Jerry amezikwa Jumanne katika makaburi ya Kinondoni mjini Daressalaam. Chuo cha USIU kimeamua kuanzisha mfuko wa kusomesha wanafunzi kwa jina lake. 
   Uchunguzi wa awali unaeleza kuwa kijana huyu alipata majeraha ya kichwa na mpaka sasa Polisi wa Kenya wanasema bado wanafanya uchunguzi. 
   Wanafunzi na wakazi wengi wa jiji la Daressalaam na Nairobi walijitokeza kumzika mwenzao, msiba ambao umeacha majonzi makubwa na simanzi katika familia na kuangalia mazungumzo yake huko Nairobi na GBSTV bofya hapa.

  0 0

  KANISA la Dar es Salaam Pentecostal Church (DPC), la Kinondoni, limeandaa zawadi ya nzuri ya DVD katika msimu huu wa krismasi kwa watanzania na wapenda muziki wa Injili ya Sifa zivume.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul amesema kuwa DVD ya Sifa Zivume imerekodiwa na kundi la Rivers of Life lenye waimbaji wazoefu wenye vipaji na uwezo wa hali ya juu kimuziki ambao wanafanya kazi chini ya kanisa hilo.
  DVD hiyo imerekodiwa katika ubora wa hali ya juu na katika viwango vya kimataifa ambayo inaurefu wa masaa matatu ambapo imerekodiwa moja kwa moja ‘live’ yenyenyimbo 15 zenyeujumbe wa amani na matumaini kwa watu wote huku zikiwa na mguso wa ainayake wenyekuleta mabadiliko katika maisha.
  Katika msimu huu wa siku kuu tunawaomba watu wote kuhakikisha wanapata DVD hii ya auna yake na pia kupata DVD ya Sifa Zuvume kwa ajili ya ndugu na marafiki kama zawadi ya krismasi.
  Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Dar es Salaam Pentecostal, Abel Majaliwa Thomas (katikati), akiwa na mchungaji Elly Mwende (kushoto) pamoja na Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul baada ya kuzindua DVD ya Sifa Zivume. 
   Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul akionesha DVD ya Sifa Zivume wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Dar es Salaam Pentecostal, Abel Majaliwa Thomas (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa DVD ya Sifa Zivume uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Julius Kenyamanyara, Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul na  mchungaji Elly Mwende.    
   Tunashuhudia uzinduzi.
    Picha ya pamoja.
  Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Dar es Salaam Pentecostal, Abel Majaliwa Thomas akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa DVD ya Sifa Zivume.

  0 0


   Msanii wa kundi la sanaa kutoka Bariadi akicheza na nyoka aina ya Chatu wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi –Lamadi leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa Barabara ya Bariadi Lamadi leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(watatu kushoto),Mbunge wa Bariadi  Mhe. Andrew Chenge(kushoto)pamoja na viongozi wengine w akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi na kuzindua ujenzi wa Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8 huko enelo la Old Maswa mkoa mpya wa Simiyu leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Old Maswa muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya kilometa ya Bariadi-Lamadi 71.8 huko eneo la old Maswa, Mkoani Simiyu.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(pembeni ya Rais kulia) pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Barbara ya Bariadi Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8 huko eneo la Old Maswa leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bwana Saguda Kasili mlemavu ambaye pia ni mtendaji wa kijiji cha Ng’wang’wali leo wakati aliposimama kijijini hapo kuwasalimia wananchi wa eneo hilo
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Umeme katika kijiji cha Nkololo wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu leo.Weninge katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh. Steven Masele, Mbunge wa Bariadi Mhe.Andrew Chenge(wapili kushoto),Paroko wa Nkololo Padri Paulo Fegan(wanne kushoto) na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti.


  0 0

  Upinzani wa dancing uliodumu tangia miaka ya 90 kati ya Athumani Diga Diga vs Bosco Cool J nani zaidi? Ufumbuzi kupatikana jumamosi hii ndani ya isumba lounge jollies club

  0 0


  0 0
 • 11/27/13--12:00: KALI TV THIS WEEK
 • It’s another monthly Diaspora Top Six music show from Kali TV. This month Chardelle Moore speaks with the DJ’s from DMV area. DJ Bimshire from Barbados and the only African female DJ in the area, DJ Akuaa from Ghana. Enjoy the music, enjoy the show, enjoy Diaspora top six and Happy Thanks Giving Day to all Kali TV fans and viewers.

  0 0  0 0

  Mnamo April 18, mwaka huu mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA) ilisaini mkataba wa dola za kimarekani 168 (takriban bilioni 275 za Kitanzania) na kampuni ya BAM International ya Uholanzi kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya kwanza ya Terminal III ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. 
  Ujenzi wa awamu hiyo ya kwanza unaotarajiwa kuanza karibuni ukikamilika terminal hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumua abiria milioni 3.5, ambapo awamu yake ya pili ililamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6, na itakuwa ni kwa huduma ya ndege za kimataifa. Sehemu iliyopo sasa ya uwanja huo, yaani terminal II, itatumika kwa abiruia wa ndani. 

older | 1 | .... | 277 | 278 | (Page 279) | 280 | 281 | .... | 3286 | newer