Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 07.03.2019


Total Tanzania Yamwaga Mamilioni Kwa Washindi wa Shindano la Ujasiliamali, Serikali Yawapongeza

0
0
.Kampuni ya Mafuta ya Total, Imetoa zawadi za Milioni 65 za Tanzania, kwa Washindi Watatu wa Shindano la Total Staterupper of Year Total Challenge ambapo erikali Yaipongeza Kampuni ya Total Tanzania kwa misaada mbalimbali wanayoitoa kusaidia maendeleo ya jamii ya Tanzania, ikiwemo uwezeshaji wajasiliamali wadogo na wakati, kwa kuwapatia mitaji na mafunzo ya kitaalamu ya ujasiliamali.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Kazi na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, wakati wa hafla ya kuwatangaza washindi wa shindano la Total Starupper of Year, kwa mwaka huu, ambapo washindi watatu wa mwanzo, walipatiwa tuzo na fedha taslim, jumla ya Shilingi milioni 75 za Kitanzania.

Naibu Waziri  Mavunde amesema, anaipongeza sana kampuni ya Total kwa kusaidia vijana wenye mawazo mazuri ya kibiashara, na kuzitaka kampuni nyingine ziige mfano wa Total kwa kujenga uwezo kwa Watanzania, kwa sababu serikali pekee haiwezi kufanya kila kitu peke yake, hivyo kunahitajika juhudi za pamoja kwa kushirikiana na sekta binafsi, katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, tTarik Moufaddal, amesema, tuzo hizo, ni uthibitisho wa nia ya dhati ya Total, kuwa ni mshirika wa maendeleo wa Tanzania, na kusisitiza kuwa bado kuna mambo mengine mengi makubwa Total imepanga kuwafanyia Watanzania katika kuchangia maendeleo.

Washindi hao nao kwa upande wao, wameishukuru kampuni ya Total kwa kutambua vipaji vyao, na hivyo kuwapatia zawadi watakazozitumia kuboresha miradi yao.

Mshindi wa kwanza ni Doreen Peter Noni, amepata tuzo na zawadi ya fedha taslim Shilingi Milioni 30 za Tanzania kwa wazo la uanzishaji kipindi cha TV kinachoitwa Peter’s Daughter Show Project, kwa lengo la kusaidia vijana kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo, ikiwemo tatizo kubwa la msongo wa mawazo, kwa vijana walioshindwa kufanikiwa.

Mshindi wa pili ni Michael Sayi, aliyepata tuzo na fedha taslimu Shilingi milioni 20, kwa mradi wa Kasome International Project, unaowasaidia wanafunzi wa sekondari Tanzania, kujipatia vitabu na masomo ya ziada kupitia mtandao, hivyo kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi kutoka familia masikini, kupata mafunzo bora kwa gharama ndogo.

Mshindi wa Tatu ni  Prince Tillya aliyepata Tuzo na fedha taslim Shingi milioni 15 kwa mradi wake wa FixChap Project, unaounganisha mafundi bora wa huduma mbalimbali za majumbani kwa gharama nafuu. 

Shindano la « Startupper of the year by Total » ni juhudi za Kampuni ya Total ya kimataifa kuhamasisha  maendeleo yakiuchumi na kijamii ili  kusaidia nchi zote  duniani ambako kampuni ya Total ipo. Shindano hili ni hatua madhubuti sanayenye lengo la kusisimua ubunifu wa  miradi ya maendelea yenye lengo la kuchangia uanzishwaji wa viwanda vidogo vitakavyotoa ajira na kuchangia maendeleo ya jamii na ya nchi za bara la Afrika kwa ujumla. Shindano hii linalenga kuibuka kwa miradi mipya, iliyotokana na wananchi wenyewe ambayo inaendena na malengo ya jumla ya uwepo wa kampuni yaTotal 

 Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za  kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total Katika kujitanua kibiashara kuelekea kwenye matumizi ya nishati mbadala, kampuni ya Total Tanzania Limited kupitia mradi wake wa Total Access to Solar (TATS) project, inasambaza taa za nishati jua zinazoitwa  AWANGO kwa jamii ya Watanzania. end.
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde (Mb), (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, Tarik Moufaddal (Kushoto) wakikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”Doreen Peter Noni aliyejinyakuwa Milioni 30,  katika hafla fupi iliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde (Mb), (Kulia) akikabidhi cheti kwamshindi wa kwanza wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge” Doreen Peter Noni aliyejinyakuwa Milioni 30,  katika hafla fupi iliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde (Mb), (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, Tarik Moufaddal (Kushoto) wakikabidhi zawadi ya hundi ya Shilingi Milioni 15, kwa Mshindi wa Tatu wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”  Prince Tillya wakati wa hafla fupi iliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde (Mb), (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, Tarik Moufaddal (Kushoto) wakikabidhi zawadi ya hundi ya Shilingi Milioni 20, kwa Mshindi wa Pili wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”  Michael Sayi wakati wa hafla fupi iliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam.
Washindi watatu wa shindano la wajasiriamali kwa vijana la Total, “Startupper of The Year by Total Challenge”  katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi zao katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam juzi. Mshindi wa Kwanza, Doreen Peter Noni (katikati) aliyenyakuwa Milioni 30, Kulia kwake ni Mshindi wa Tatu Prince Tillya alipata Milioni 15 na Kushoto ni Mshindi wa Pili, Michael Sayi aliyepata Milioni 20.
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde (Mb), Kushoto,  akimpongezazawadi ya hundi ya Shilingi Milioni 20, kwa Mshindi wa Kwanza wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”  Doreen Peter Noni (katikati) aliyeshinda Milioni 30. wakati wa hafla fupi iliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam. Kulia ni  Mshindi wa Tatu Prince Tillya aliyepata Milioni 15.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania,  Tarik Moufaddal (Kushoto) akihutubia katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”  katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam jana. Kutoka Kushoto ni mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Mh. Anthony Mavunde (Mb), Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mshindi wa Kwanza, Doreen Peter Noni aliyenyakuwa Milioni 30, Mshindi wa Tatu Prince Tillya alipata Milioni 15 na Mshindi wa Pili, Michael Sayi aliyepata Milioni 20.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, Tarik Moufaddal (Kushoto), Mh. Anthony Mavunde (Mb), Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mshindi wa Kwanza, Doreen Peter Noni aliyenyakuwa Milioni 30, Mshindi wa Tatu Prince Tillya alipata Milioni 15 na Mshindi wa Pili, Michael Sayi aliyepata Milioni 20, wakinyanyua glasi kutakiana heri, katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la wajasiriamali kwa vijana “Startupper of The Year by Total Challenge”  katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam jana

WAZIRI NDALICHAKO ASEMA SAYANSI NA TEKNOLOJIA NI MUHIMU KATIKA UKUAJI WA UCHUMI

0
0

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ilboru Maximillian Masesa akitoa maelezo kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako juu ya kifaa cha kubaini wanafunzi ambao wanatumia simu shuleni alichobuni.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiangalia ubunifu wa injini ya Ndege uliofanywa na Emmanuel Chibula kutoka Musoma, Mkoani Mara wakati wa kilele cha mashindano ya kitaifa ya sayansi, teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Wanafunzi mbalimbali wa shule za msingi na baadhi ya wananchi wakifuatilia mashindano ya kitaifa ya Sayansi,Teknlojia na Ubunifu yaliyofanyika katika viwanja vya mwalimu Nyerere jijini Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na washiriki mbalimbali hawapo pichani wakati wa kufunga mashindano ya kitaifa ya kitaifa ya sayansi, teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Wanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji nchini NIT wabuni gari lisilotumia injini, na badala yake linatumia umeme kuendesha mifumo yake. Pichani Waziri akiwa kwenye gari hilo akipewa maelezo ya namna gari hilo linavyofanya kazi.

…………………………

Serikali imewataka wabunifu nchini kujikita katika kuangalia shughuli za ambazo zinafanyika katika mazingira yao na wabuni jinsi ya kuzirahisisha kwa kutumia Sayansi na kiteknolojia ili kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako katika kilele cha Mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu mjini Dodoma. Waziri Ndalichako pia aliongeza kuwa eneo la Sayansi na Teknolojia ni muhimu kwa taifa na likitumika vyema litasaidia kuongeza uzalishaji na Kurahisisha utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

“Kwa muda mrefu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa ikisimamia zaidi Elimu kuliko masuala ya Sayansi na ubunifu hivyo ni vyema wabunifu waendelee kujitokeza zaidi na wajikitike katika ikubuni mbinu za kurahisisha mifumo ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo Kilimo, ufugaji na njia bora za upatikanaji wa maji”, alisema Waziri Ndalichako.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Profesa James Mdoe amesema lengo la Mashindano hayo yaliyohusisha wabunifu kutoka ngazi mbali za Elimu ni kuibua ubunifu, umahiri, kuchochea ugunduzi kwa lengo la kukuza matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika maendeleo.

Mashindano hayo yalifunguliwa rasmi na Naibu Waziri Mhe. William Ole Nasha Machi 5, 2019 na leo yamefikia kilele ambapo washindi mbalimbali walipata zawadi za fedha na kutunukiwa vyeti.

Kauli mbiu ya mashindano hayo kwa mwaka huu ni ” kukuza ujuzi na ubunifu kwa uchumi wa viwanda”.

MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

0
0

Mimi ninajua, Wewe unafahamu na Tanzania inaelewa juu ya Safari Huru aliyoifunga dada yetu @mwasitij kuelekea Mafanikio kupitia Talanta ya muziki aliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu.

Katika Safari yake amekutana na Changamoto zilizomtoa machozi na kumkwamisha, ila kutokana na Juhudi, Maarifa na Ubunifu alipambana nazo na hatimae alijongea mbele na kutimiza Ndoto zake hatimae kuwa Shujaa.

Kesho ataungana na Wazungumzaji Mahili akiwa ni Mgeni wa Heshima katika tukio la #BintiShujaa ambalo litafanyika katika Ukumbi wa Anatoglo uliopo Mnazi Mmoja.

Kwa taarifa zaidi tembelea kurasa yetu Instagram @safarihuru au tupigie kwa namba 0715171587.

@tanisah_mansour @kijanapositive
#SafariHuru #Womensday #KijanaPositive #BintiPositive #ActivatedBillionaire

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI:WAZIRI BITEKO ATOA UJUMBE KWA WANAWAKE WIZARA YA MADINI

WAZIRI NDALICHAKO KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA KIMATAIFA WA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA SHIRIKA LA NGUVU ZA ATOMIKI DUNIANI

0
0
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojiaa Profesa Joyce Ndalichako anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kimataifa wa waratibu wa kitaifa wa miradi inayotekelezwa na Shirika la nguvu za Atomiki duniani kwa nchi 46 kanda ya Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 15 mezi Machi jijini Arusha wenye lengo la kujadiliana na masuala mbali. 

Mkutano huo utashirikisha washiriki 60 kutoka nchini 46 duniani kutoka baara la AFRIKA ambao ni wanachama wa Shirika la nguvu za Atomiki duniani ambao wataweza kujadiliana masuala mbali mbali . 

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ,Profesa Lazaro Busagala amaesema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na kwamba wana imani mkutano huo utaweza kusaidia nchi washiriki kuweza kusonga mbele katika namna ya uboreshaji wa sekta mbali mbali kutokana na miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani(IAEA). 

Amesema katika mkutano huo ,washiriki watapata nafasi ya kujadiliana kwa mapana juu ya namna ya. 

Pia Profesa Busagala ameongeza kuwa mkutano huo pia utahudhuriwa na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki kanda ya AFrika Bwana Shaukat Abdrazak ambaye baada ya mkutano huo ataweza kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali na uongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Wizara nne ambazo zimekuwa zikihusika katika miradi mbali mbali ya kitaifa inayotekelezwa na Shirika la Nguvu za Atomiki duninia(IAEA) . 

Amesemsa kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,Mkurugenzi Shaukat atakutana na Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi . Kwa upande wa Tanzania Bara Shaukat atafanya mazungumzo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Waziri wa Maji . 

Pia ataweza kufanya ziara katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Seliani,Taasisi ya Chakula na Lishe na Taasisi ya Saratani Ocean Road. Profesa Busagala amesema kuwa mazungumo hayo yataweza kusaidia nchi kwenye uboreshaji wa miradi mbali mbali inayofanyika hapa nchini hasa katika sekta ya Afya,Kilimo,maji. 

Ameeeleza kuwa Tanzania ni moja ya nchi iiliyoweza kufadika kwa kiasi kikubwa kwa miradi katika ya udhibiti na kuhamasisha matumizi salama ya tekenolojia ya nyuklia inayotekelezwa na Shirika la Nguvu za Atomiki duniani .

MAGAZETI YA LEO IJUMAA,MACHI 8,2019

RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”

0
0


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyevaa Kapelo) akiongoza ukaguzi wa ujenzi wa madarasa manane yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi na michango ya wadau katika shule ya Msingi Msia, kata ya Milepa Wilayani Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akipewa maelezo juu ya marekebisho yanayoendelea katika ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Msia na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mh. Kalolo Ntila (kaunda suti nyeusi) wakati wa kuyakagua madarasa hayo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea.

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akikabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa niaba ya umoja wa waalimu wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Kipeta kwaajili ya wanafunzi ambao vitabu vyao vilirowa na mvua kutokana na mabweni kuezuliwa.

………………………………………………………..

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameliagiza jeshi la polisi Mkoani Humo kuhakikisha wanamsaka na kumkamata mganga wa jadi anayesadikiwa kuwaibua na kuwaadhiri wachawi katika bonde la ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga.

Agizo hilo limekuja baada ya kufanya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali katika bonde hilo pamoja na kujionea maendeleo na changamoto za shule ya sekondari Kipeta iliyoezuliwa paa pamoja na shule ya msingi Msia iliyobomoka madarasa manne kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyosababisha madhara hayo mwezi Disemba mwaka 2018.

Ameonya kuwa hataki yaliyotokea mkoa wa Njombe yajirejee katika Mkoa wa Rukwa ikiwa bado watu hawajasahau machungu waliyoyapata kutokana na matukio hayo, na kuongeza kuwa mganga huyo wa kienyeji analindwa na kiongozi wa chama cha kisiasa na hivyo kumtaka mkuu wa kituo cha Kijiji cha Kilyamatundu kuhakikisha anamkamta kiongozi huyo hata kama ni wa Chama cha Mapinduzi.

“OCS na vyombo vyako vile fanya upepelezi wa kina na ukamate yeyote yule ambae ametoka nje ya mkoa huu, nje ya Kilyamatundu anayefanya shughuli hizi, kamata weka ndani fanya mahojiano ya kina, na wengine nimeambiwa hap ani viongozi wa vyama vya kisiasa, usijali huyu ni chama tawala, huyu ni nani, kama ukijua kwa uhakika kamata mhoji mpaka kieleweke, sisi hatutaki kuletewa Lambalamba hapa,” Alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Mh. Wangabo aliwapongeza waalimu, Uongozi wa vijiji husika pamoja na wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha katika kuhakikisha majengo yaliyobomoka na kuezuliwa katika shule hizo yanarudi katika hali yake ya kawaida na hatimae wanafunzi kuendela na masomo.

Pamoja na michango ya wadau mbalimbali iliyohamasishwa na Mh. Wangabo ambayo imesaidia kurudishisa mapaa ya majengo ya utawala, mabweni mawili, nyumba sita za waalimu na vyoo vya wasichana na wavulana kwa shule ya sekondari Kipeta na kujenga madarasa manane kwa shule shule ya Msingi Msia, Wizara ya Elimu pamoja kwa ushirikiano na Wizara ya TAMISEMI imetoa shilingi Milinoni 75.2 kwaajili ya kuongezea ujenzi wa madarasa na vyoo kwa shule hizo.

Naye Diwani wa kata ya Milepa Mh. Apolinari Macheta alipongeza juhudi za Mkuu wa Mkoa kwa kuhakikisha shule hizo zinakuwa bora zaidi ya zilivyokuwa na kumuahidi kuwa Shilingi Milioni 48.6 walizopatiwa kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili na vyoo matundu sita kwa shule ya msingi Msia atahakikisha kwa ushirikiano wa wananchi watapata darasa jingine kwa fedha hizo.

Watanzania waombwa kujitokeza kwenye kongamano na maonesho ya Afya sayansi jumuiya ya Afrika Mashariki

0
0
KATIBU Mtemdaji wa Tume ya Utafiti katika Afya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Profesa Gibson Kibiti Amesema kuwa Utafiti unachangia katika kuimarisha ushirikiano katika kanda kwenye sekta ya Afya kwa mujibu wa ibara ya 118 ya mkataba.

Amesema mkataba wa kubuniwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na vipengele vingine vya itifaki ya soko la pamoja ,tume hiyo pia hukuza dhamira kuu ya Jumuiya ambayo ni uhamiaji huru wa watu pamoja na uhamiaji wa huduma na bidhaa.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam ,kuhusu kongamano na maonyesho ya awamu ya Saba ya Afya ,sayansi,na biashara Jumuiya ya Afrika Mashariki .

Kibiti amesema Baraza la Mawaziri wa Jumuiya liliidhinisha kufanyika kwa kongamano na maonyesho kila mwaka na kila nchi ikiwa ni Mwenyeji kwa mzunguko kwa ushirikiano wa karibu na mashirika ya kimataifa ya kanda yanayoshughilika katika masuala ya Afya,asasi,za kuraia,watu binafsi na wadau wengine.

Akizungumzia maonyesho hayo na kongamano Kibiti amesema kongamano na maonyesho ya awamu ya Saba ya Afya ,sayansi,na biashara Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na maonyesho ya kimataifa vimepangwa kufanyika kuazia Machi 23,hadi 29 mwaka 2019 jijini Dar Es Salaam.

Kauli mbiu ya mwaka huu'' Tecknolojia kwa ajili ya kubadili mifumo ya Afya ili kutimiza malengo endelevu ya maendeleo ya umoja wa mataifa" .alisema Kibiti

Kwaupande wake Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi akizungumzia kuhusu Tehama alisema dunia ya sasa Tehama katika sekta ya afya haiepukiki kwani hata Serikali imejipanga kuhakikisha eneo la afya linaleta tija.

Amesema ili serikali kuweza kupata mapato ,makusanyo yake yanafanyika kwa njia ya tehema huku akitolea mfano kwamba ndio maana hivi sasa hata mitandao ya Simu inatumika kwa ajili ya miamala ya fedha nakusisitiza hiyo yote ni maendeleo ya Tecknolojia ya Tehama.

"Nivema watanzania wakajiitokeza katika kongamano na maonyesho hayo ambayo yatafanyika kwa zaidi ya Siku moja kwani kutakuwa na mada 200 zitawasilishwa siku hiyo." Alisema Profesa kambi.
Mganga Mkuu wa Serikali,Profesa Mohamed Bakari akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewaomba watanzania kujitokeza katika kongamano na maonyesho ya saba ya Sayansi na Biashara ya jumuiya ya Afrika Mashariki Machi 27-29 mwaka huu,katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa NIMR Prof. Yunus D Mgaya akisisitiza jambo katika mkutano ulio fanyika leo jijini Dar es Salaa.(katika) Katibu Mtemdaji wa Tume ya Utafiti katika Afya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Profesa Gibson Kibiti (kulia) Mganga Mkuu wa Serikali,Profesa Mohamed Bakari.
Mwenyekiti wa kongamano la saba la Sayansi jumuiya ya Afrika Mashariki,Profesa Eligius Lyamuya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano na maonyesho ya awamu ya saba ya Afya sayansi jumuiya ya Afrika Mashariki Machi 27-29 mwaka huu,katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.(katika) Katibu Mtemdaji wa Tume ya Utafiti katika Afya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Profesa Gibson Kibiti. (kulia) Mganga Mkuu wa Serikali,Profesa Mohamed Bakari.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

KASONGO WA KANEMA ALIYETISHA KWENYE ‘GEMU’ LA MUZIKI

0
0
Na Moshy Kiyungi.

Mnamo miaka ya 1970 hadi 1980, sauti ya mwanamuziki Kasongo wa Kanema ilikuwa ikisikika kwenye redio nyingi Afrika ya Mashariki.

Sauti yake ilitawala hususan kwenye wimbo wa Kakolele Viva Krismasi, wakati akiwa katika bendi ya Baba Gaston.Kasongo wa Kanema alianza shughuli za muziki akiwa na umri mdogo wa miaka kumi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Nguli huyo alikuwa akichukua muda mwingi akisikiliza nyimbo za wanamiziki mahiri katika uimbaji akina Tabu Ley naLuambo Makiadi Lokanga la dju Pene Francois ‘Franco’ambaye pia alijulikana kwa majina maarufu ya Franco Yogo au Le Grand Mitre.

Familia ya Kasongo haikuwa nyuma kumpa moyo kwa kiasi kikubwa wa kufanya muziki. Kipaji chake kilionekana pale alipoungana na wenzake kuunda bendi ya Super Mazembe. Baadhi ya wanamuziki hao walikuwa akina Atia Joe, Lovi Longomba, Bukalos Kayembe Rapok, Songole, lobe Mapako, Talos, Longwa Didos na Fataki Lokasa ‘Masumbuko ya dunia’.

Kwa mapenzi ya mungu, baadhi yao wameshatangulia mbele za haki.

Walio hai ni yeye Kasongo wa kanema na Dodo Dorris, ambaye hivi sasa anaishi nchini Afrika ya Kusini. Akiwa katika bendi ya Baba Gaston iliyokuwa ikiongozwa na Baba Nationale Omar Ilunga wa Ilunga, Kasongo wa Kanema alijijengea umaarufu zaidi alipoimba wimbo kwa umahiri mkubwa wimbo wa Kakolele Viva Krismas.

Wimbo huo kila ikaribiapo nyakati za sikukuu ya Krismasi, hurindima takriban katika vituo vingi vya redio.Baadaye Kasongo akatoka kwa Baba Gaston akaenda kujiunga katika bendi ya Super Mazembe.

Alishiriki vilivyo kuimba nyimbo nyingi katika bendi hiyo ya Super Mazembe akisaidiana na watunzi na waimbaji wengine akina Lovy Longomba na Fataki Lokassa ‘Masumbuko ya duniya’.

Walishirikiana vilivyo kutunga na kuimba nyimbo kama Bambina, Shauri yako, Likasi, Bamama, Mukala, Loboko na nyingine nyingi.Aidha Kasongo wa aliwahi kupigia katika bendi ya Shika Shika, ambako nako aliimba kwa umahiri mkubwa katika nyimbo za Maya na Nyako Ber.

Akiwa na bendi hiyo ya Shika Shika alikutana na mwimbaji Fumimoto Jimmy Moni Mambo, kwa pamoja waliweza kuchanganya sauti zao na kuifanya bendi hiyo kuwa tishio katika jiji la Nairobi miaka hiyo.

Kanema baadae akaamua kuunda bendi yake ikiwa na baadhi ya wanamuziki mahiri akiwemo yeye kama mwimbaji kiongozi na kiongozi wa bendi, mwanaye aitwaye Kasongo jnr. ambaye alikuwa akiimba na kubofya kinanda.

Wengine ni Ale Maindu ambaye alikuwa akicharaza gitaa la solo, Lei Mkonkole, akichangaya drums na Longwa Disco, aliyekuwa mwimbaji. Gitaa la kati rhythm na solo yalikung’utwa na Alpha Nyuki.
Kasongo wa Kanema amefaya makazi yake katika jiji la Nairobi nchini Kenya. Ni baba wa familia yenye mke aiitwaye Achieng na watoto kadhaa.
PICHA YA KASONGO WA KANEMA (KULIA), AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI MJINI NAIROBI.


Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba: 0713331200, 0767331200 au 0784331200.

MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA

0
0

MWENYEKITI wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka, Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Thuwayba Kisasi, Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Bi.Tunu Juma Kondo wakipewa maelezo na Mhandisi Abubakar Khamis Mati juu ya maendeleo ya ujenzi wa shule ya Kisasa ya Sekondari ya Wara iliyojengwa na SMZ kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
MWENYEKITI wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akishiriki shughuli za ujenzi wa Tawi la CCM Kangani ambalo ni Tawi la asili la harakati za ASP linalojengwa upya ili liendane na hadhi ya CCM.
MWENYEKITI wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akishiriki shughuli za ujenzi wa Tawi la CCM Kangani ambalo ni Tawi la asili la harakati za ASP linalojengwa upya ili liendane na hadhi ya CCM.

……………………………………………………………………..

NA IS-HAKA OMAR,PEMBA.

WANAWAKE wa Chama Cha Mapinduzi kisiwani Pemba wametakiwa kufanya Mapinduzi ya kisiasa kwa kuhakikisha CCM inavunja na kusambaratisha ngome ya CUF na hatimaye kushinda majimbo yote ya Uchaguzi ya mwaka 2020.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka katika mwendelezo wa ziara yake huko Shule ya Sekondari ya Mohamed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, alisema ni wakati wa wanawake kuonyesha uwezo wao na kutekeleza kwa vitendo falsafa ya ‘Wanawake ni jeshi la ukombozi la CCM’.

Alisema hakuna chama cha siasa, wala taasisi yoyote itakayoweza kuzuia ushindi wa CCM mwaka 2020 kisiwani Pemba endapo wanawake wataamua kuungana kwa pamoja ili kufanikisha ushindi wa CCM.

Katika maelezo yake Ndugu Gaudensia alisema Jeshi la UWT la Chama Cha Mapinduzi litakuwa mstari wa mbele kupambana vita ya kisiasa kwa mbinu zote ili kuandika historia mpya katika uwanja wa siasa za ushindani Tanzania kwa kuhakikisha CCM inashinda kwa kiwango kikubwa Zanzibar na Tanzania bara.

“Wanawake tuna nguvu, uwezo, ujasiri, mikakati,nyenzo na mbinu za medali za kisiasa hivyo hatuna sababu ya kuyaachia majimbo ya Pemba yaendelee kubaki kwa wapinzani bali yatarudi mikononi mwa CCM.”,alisema Bi.Gaudensia.

Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia, alipongeza hatua za kimaendeleo zilizofikiwa katika Sekta ya Elimu Pemba hasa katika suala zima la miundombinu ya Majengo ya Kisasa ya kiwango cha Ghorofa.

Aidha aliyataja mageuzi makubwa katika miundombinu ya Barabara za kisasa mijini na Vijiji kuwa ni ya kiwango bora cha kuridhisha hatua ambayo wananchi wa kisiwa cha Pemba wanastahiki kuithamini Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo mema yaliyotekelezwa.

Pamoja na hayo aliwasisitiza hakina Mama Visiwani Pemba bila kujali tofauti zao za kisiasa kushiriki katika kongamano la Kitaifa litakalofanyika Machi 9 mwaka 2019, katika Kiwanja cha Tibirinzi Wilaya ya Chake Chake Pemba.

Alieleza kuwa Kongamano hilo lililoandaliwa na UWT ni la kupongeza utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 pamoja na masuala mbali mbali ya kimaendeleo yaliyoasisiwa na Serikali za CCM kwa awamu tofauti za Uongozi.

Pamoja na hayo aliwapongeza Wabunge na Wawakilishi wa Viti Maalum Pemba kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Naye Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mwl.Queen Mlozi alikemea vitendo vya udhalilishaji wa Kijinsia kwa Watoto wa Kike vinavyochangia kukwamisha maendeleo ya wanawake katika kunufaika na fursa za elimu.

Mwl.Queen aliwasihi Wazazi,Walezi pamoja viongozi wa dini na kisiasa kusimamia ajenda za kulinda na kutetea haki za wanawake hasa vijana na watoto ili wanufaike na fursa mbali mbali ndani ya jamii.

Akizungumzia changamoto za dawa za kulevya kwa vijana, Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania bara Ndugu Jesca Mbogo alisema baadhi ya vijana kisiwani Pemba wameingia katika changamoto za kutumia dawa za kulevya hali ambayo ni hatari katika ustawi wa maendeleo ya nchi.

Mapema Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kusini Pemba, ndugu Bimkubwa Khamis Mohamed alisema hali ya kisiasa ndani ya mkoa huo imeendelea kuimarika na wanawake wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kujiunga na CCM.

Alisema Pemba ya Sasa sio Pemba ya zamani kwani wananchi wengi wameanza kutambua ukweli baada ya kuona kwa vitendo mambo mema yanayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayotokana na Chama Cha Mapinduzi.

LES MANGELEPA ILIVYO ACHA HISTORIA KATIKA MUZIKI

0
0
Na: Moshy Kiyungi

Les Mangelepa ilikuwa ni bensi ya muziki wa dansi iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa dansi maeneo mengi ya Afrika Mashariki na Kati.

Walikuwa wamejikita katika jiji la Nairobi, ambapo waliweza kuwavuta vijana wa wakati huo wakaenda kuserebuka katika kumbi mbalimbali za Nairobi Park, Garden Square, Tents Club na ile ya Park Inn ambako bendi hiyo ilikuwa ikiporomosha burudani.

Baadhi ya vibao murua mbazo zilikuwa mashuhuri na kutamba wakati huo ni pamoja na Embakasi na Nyakokonya.

Les Mangelepa ilikuwa na wanamuziki wengi wakiwa ni raia toka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikiwa na makazi yake katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

Ilivyoanzishwa bendi hiyo ilikuwa ni mithiri ya msemo wa Waswahili usemavyo kuwa “Kuvuja kwa Pakacha, nafuu kwa mchukuzi” ndivyo ilivyokuwa baada ya bendi ya Baba Gaston kugawanyika.

Baadhi ya wanamuziki wake wakaenda kuunda kikosi cha Les Mangelepa wakiongozwa na Bwammy Walumona ‘La Capitale.’Vijana hao walikuwa nguzo kuu katika bendi hiyo ya Baba Gaston, iliyokuwa ikiongozwa na Baba Nationale Ilunga wa Ilunga.

Yaelezwa kwamba baada ya kuondoka katika bendi hiyo, kulisababisha kifo cha bendi.Bendi Les Mangelepa ilijipatia umaarufu mkubwa kati ya miaka ya 1970na 1980 baada ya kufyatua nyimbo zilizowakuna wapenzi wa muziki wa
dansi katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.

Baadhi ya nyimbo hizo zilikuwa ni Embakasi, Maindusa, Walter, Safari
ya Mangelepa, Odesia, Dracula, Saad, Maboko Pamba na nyingine nyingi.
Les Mangelepa ilileta ushindani mkubwa katika jiji hilo la Nairobi, dhidi
ya bendi kubwa zilizokuwemo jijini humo.


Baadhi ya bendi hizo ni pamoja na Les Knoirs, Les Wanyika, Orchestra
Shikashika, Orchestra Virunga, Super Mazembe, Baba Gaston na nyingine nyingi.Baada ya ‘kushiba’ umaarufu, pakaingiliwa na mtafaruku mkubwa wa uongozi.Magelepa ikaamua kubadili uongozi, ambapo Kabila Kabanze Eveny, akawa kiongozi wa bendi.

Bendi hiyo ikarejea kwenye umaarufu wake kwa kupiga muziki waKikongo, kama walivyokuwa Super Mazembe na Baba Gaston.Mwaka 1986, Bammy Walumona aliondoka katika bendi hiyo nakuamua kuokoka, lakini aliiacha Mangelepa ikiwa imesheheniwanamuziki wengi wenye vipaji mbalimbali.

Wanamuziki waliokuwa wakiunda kikosi cha Les Mangelepa kiliwajumuisha kina Bwami Walumona ‘Le Capitale’ ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo.Kabila Kabanze ‘Evani’ aliongoza safu ya waimbaji wakati KalengaNzaazi ‘Vivi’, Lutulu Kaniki ‘Macky’ na Babibanga Watshilumba ‘Kai’ walikuwa waimbaji mashuhuri wakati huo. Kai pia alikuwa ni mpuliza
tarumbeta na trombone.

Kwenye drums na gitaa la besi alipiga Kasongo Fundi Petit Jean, Lukangika Maindusa ‘Moustano’ alikuwa akipiga gitaa la solo na rhythm
wakati Mwepe Mutshi ‘Cavalou’ naye alisimama kwenye upulizaji wa tarumbeta.Mwanamuziki mwingine alikuwa Lumwanga Mayombo ‘Ambassador’
aliyekuwa akiliungurumisha gitaa zito labesi na rhythm.

Drums ziligongwa na Mukala wa Mulumba ‘Bebe’, naye Tabu Ngongo Ildephonce ‘Super Sax’ na Tshimanga Zadios walikuwa wakipuliza
saxophone.Kundi hilo machachari pia lilikuwa na wanamuziki wengine kina Twikalewa Twikale na Kabe Kimambe ‘Elombe’ walikuwa wakibofya kinanda nakupiga gitaa la solo. Kabebe Mukangwa ‘Picolo’ na Tambwe Lokasa
walikuwa akiliungurumisha gitaa zito la besi.

Tumba ziligongwa na Mukala Kanyinda ‘Coco’ ambaye alikuwa na
uwezo wa kupuliza hata saxophone.Mwanamuziki mwingine alikuwani Padd ‘Ma Wauwau’ aliyekuwaakipuliza saxophone.Tungo za nyimbo za Mangelepa zilishika chati katika miji mingi hapanchini hususan kwenye kumbi za burudani na maeneo ya starehe namabaa.Wimbo wa ‘Embakasi’ na ‘Kanemo’ zilitungwa na mwanamuziki


Kalenga Nzaazi ‘Vivi’, hadi leo ukipigwa popote watu wengi hufuatilia
neno kwa neno.Nyimbo za ‘Mimba’ na ‘Nyako Konya’ zilitungwa na mwanamuzikiBadi wa Tshilumba nazo zinaendelea kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki hadi leo.

Wimbo wa ‘Maindusa’ ulioimbwa na kupigwa kwa umahiri mkubwa ni utunzi wake Lukangila Maindusa, wakati wimbo wa ‘Mimba’ na ‘Malawi’ zilitungwa na mwanamuziki Kabila Kabanze ‘Evani’. Wimbo ambao huanza kwa sauti ya juu sana wa ‘Walter’ ni utunzi wake Badi Banga wa Tshilumba. Les Mangelepa baadae wakafyatua albamu nyingine
yenye nembo ya Madima ikiwa imesheheni nyimbo za ‘Madina’,
‘N’kimba’, ‘Lolo Mukena’ na ‘Kawala’.

Bendi hiyo Les Mangelepa itakumbukwa na wapenzi wa muziki wa nchini Zambiaambako ilifanya ziara na kutoa burudani ikiwa humo. Baada ya kurejeawakatoka na vibao vikali vya ‘Dajala’, ‘Saad’, ‘Tshibola’, ‘Mankwazi’ na‘Safari ya Zambia’ wimbo ambao ulipigwa kwa ala tupu.

Mwaka 1978, Mangelepa ambayo ilikuwa ikitumia mtindo wa ‘Chafua Chafua’, walirekodi nyimbo zilizokuwa na sehemu ya kwanza na ya pili za ‘Pambana pambana’ pamoja na ‘Haleluye’. Nyingine zilikuwa ni ‘Dracula’, ‘Mangelepa Kamili’, ‘Kizunguzungu’, ‘Suzanne’ na ‘Trouble’.

Wanamuziki hao walitunga na kuimba nyimbo nyingi zilizokuwa kivutio
cha mashabiki na wapenzi wa muziki. Bendi hiyo ilikuja onekana kama haina mpinzanimiongoni wa bendi zilizokuwa zikipiga katika jiji hilo.
Mangelepa ilijipatia umaarufu mkubwa kati ya miaka ya 1970/80 baada ya kufyatua nyimbo zilizowakuna wapenzi wa muziki katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.

Nyimbo hizo zilikuwa za ‘Embakasi’, ‘Maindusa’, ‘Walter’, ‘Safari ya Mangelepa’, ‘Odesia’, ‘Dracula’ na ‘Maboko Pamba’.


Mangelepa ikatokea kuwa maarufu kwa miziki wa Lingala kama walivyokuwa Super Mazembe, Baba Gaston na Virunga ya Samba Mapangala.

Mwaka 1986, Bammy Walumona aliondoka katika bendi hiyo, akaamua kuokoka. Licha ya kuondoka kwake bendi hiyo bado ilikuwa imesheheni wanamuziki wengi wenye vipaji mbalimbali.

Waliweza kutunga na kuimba nyimbo nyingi zilizokuwa kivutio cha mashabiki na wapenzi wa muziki Afrika Mashariki na Kenya na kuwa bendi pinzani zilizokuwa zikipiga katika jiji hilo.

Safu ya wanamuziki waliokuwa wakiunda kikosi cha Mangelepa kilikuwa kwa kuanzia upande wa mpigaji wa gitaa lililoongoza la solo, alikuwepo mzee mzima, Bwamy Walumona ‘Le Capitaine’ ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa bendi hiyo.

Kabila Kabanze ‘Evani’ aliongoza safu ya waimbaji wakati Kalenga Nzaazi ‘Vivi,’ Lutulu Kaniki ‘Macky’ na Babibanga Watshilumba ‘Kai’ walikuwa waimbaji mashuhuri wakati huo. Kai pia alikuwa ni mpuliza tarumbeta na turombone.

Kwenye drums na gitaa la besi alipiga Kasongo Fundi ‘Petit Jean’, Lukangika Maindusa ‘Moustano’ alikuwa akipiga gitaa la solo na rhythm wakati Mwepe Mutshi ‘Cavalou’ naye alisimama kwenye tarumbeta.

Mwanamuziki mwingine alikuwa Lumwanga Maoyombo ‘Ambassador’ aliyekuwa akiliungurumisha gitaa zito la besi na rhythm. Drums ziligongwa na Mukala wa Mulumba ‘Bebe’, naye Tabu Ngongo Ildephonce ‘Super Sax’ na Tshimanga Zadios walikuwa wakipuliza saxophone.

Kundi hilo machachari pia lilikuwa na wanamuziki wengine kina Twikale wa Twikale na Kabe Kimambe ‘Elombe’ walikuwa wakibofya kinanda na kupiga gitaa la solo. Kabebe Mukangwa ‘Picolo’ na Tambwe Lokasa walikuwa akiliungurumisha gitaa zito la besi.

Tumba ziligongwa na Mukala Kanyinda ‘Coco’ ambaye alikuwa na uwezo wa kupuliza hata saxophone.

Mwanamuziki mwingine alikuwa Padd ‘Ma Wauwau’ aliyekuwa akipuliza saxophone.

Tungo za nyimbo za Mangelepa zilishika chati katika miji mingi hapa nchini hususan kwenye kumbi za burudani na maeneo ya starehe na kwenye baadhi ya baa.


Bendi hiyo itakumbukwa na wapenzi wa muziki wa nchini Zambia ambako ilifanya ziara ikitoa burudani ikiwa humo na baada ya kurejea wakatoka na vibao vikali vya ‘Dajala’, ‘Tshibola’, ‘Mankwazi’ na ‘Safari ya Zambia’ wimbo ambao ulipigwa kwa ala tupu.

Mwaka 1978, Mangelepa walirekodi nyimbo zilizokuwa na sehemu ya kwanza na ya pili za ‘Walter’, ‘Pambana pambana’, ‘Maboko Pamba’ pamoja na ‘Haleluye’. Nyingine zilikuwa ni ‘Dracula’, ‘Mangelepa Kamili’, ‘Kizunguzungu’, ‘Suzanne’ na ‘Trouble’.

Les Mangelepa haipo tena katika ulimwengu wa muziki na baadhi ya wanamuziki wake wametangulia mbele ya haki, wengine wameokoka na kuacha kabisa kupiga muziki wa kidunia

Mwisho.

Mwandishi wa makala hii aanapatikana kwa namba: 0784331200, 0767331200, 0713331200 na 0736331200.

Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewasisitiza wakati wa Kijiji cha Kilyamatundu, Kata ya Kipeta, Wilayani Sumbawanga kuhakikisha wanaitumia vyema fursa inayoletwa kwa kukamilika kwa ujenzi wa daraja la momba ili kuinuka kiuchumi.

Amesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo ni kufunguka kwa neema ambayo muda mrefu wanacnhi wamekuwa wakiisubiri na kuongeza kuwa kazi ya serikali ni kuhakikisha inaweka miundombinu sahihi ili kuwarahisishia wananchi wake kupata huduma wanazostahili na sio kuwawekea fedha wananchi mifukoni.

“Kwahiyo daraja hili la mto momba, nina hakika litakuza uchumi wa mikoa yetu, ndani ya mkoa wetu wa Rukwa na mikoa ya jirani, kuna Katavi watakuja kutumia lakini kuna jirani zetu wa Songwe na hata Mbeya, iliyopo ni kuongeza juhudi katika kuzalisha na hasa kilimo cha mpunga ambacho ndicho kinakubali huku, tulime zaidi halafu tuchakate, tuweke viwanda, awali nilishasema na nitarudia tena kutoa wito kwa wadau mbalimbali waje kuweka viwanda huku,” Alisisitiza.

Aidha, alisikitishwa na baadhi ya wafanyabiashra wanaotoka nje ya Mkoa wa Rukwa kuchukua mazao ya mkoa huo na kuyapeleka kwao na kisha kuweka kwenye vifungashio na kudai kuwa mazao hayo yanatoka katika mikoa yao.

Wakati akisoma taarifa ya mradi huo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani Rukwa Mhandisi Ndelalutse Karoza alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo ni muhimu sana kwa mikoa ya Rukwa na Songwe pamoja na Tanzania kwa ujumla na kubainisha kuwa ukamilifu wa daraja hilo utawainua wananchi kiuchumi na kijamii ikiwemo kupunguza gharama za usafirishaji wa mazao.

“Maendeleo ya kazi hadi kufikia Februari 2019 ni asilimia 95 kwenye daraja na asilimia 97 kwenye barabara za maunganisho, kazi muhimu zimekwisha kamilika na daraja linaweza kutumika, kazi ambazo hazijakamilika ni pamoja na alama za barabarani na kazi ya kuweka taa,” Alimalizia.

Ujenzi wa daraja la mto Momba  linalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe kwa upande wa bonde la ziwa Rukwa umefadhiliwa kwa asilimia 100 na serikali ya Tanzania na litagharimu shilingi bilioni 17.7 hadi kukamilika kwake tarehe 24.5.2019 ambapo mpaka sasa limekamilika kwa asilimia 95 na mkandarasi wa ujenzi huo ni Genjio Engineering Group Cooperation kutoka China.
 Daraja la Momba linalounganisha Mkoa wa Rukwa na Katavi lenye urefu wa mita 84 na kugharimu shilingi bilioni 17.7
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyevaa kapelo) pamoja na wataalamu alioambatana nao wakitembea juu ya daraja hilo ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa daraja hilo lipo tayari kwa matumizi ya kuvuka kutoka mkoa wa Rukwa na kuelekea mkoa wa Songwe.
 Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wakitembea juu ya daraja hilo kuonyesha mwanzno wa matumizi ya daraja hilo muda mfupi baada ya kusikiliza nasaha za Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo. 
 Picha ya pamoja ya wataalamu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani Rukwa pamojana Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (wa nne toka kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyevaa kapelo) 

ACHENI TAMADUNI ZA ZAMANI PELEKENI WATOTO SHULE- KATIBU (CCM) TENGELEA

0
0
 Diwani  wa kata ya Tengelea Shabani Manda wa (pili kushoto) akimkabidhi Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa (CCM) Mkoa wa Pwani,Gama J Gama baiskeli kwa  watu wenye ulemavu wa miguu katika  kongamano la elimu lililofanyika shule ya msingi Hoyoyo wilaya ya mkuranga mkoa wa Pwani.
  Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa (CCM) Mkoa wa Pwani,Gama J Gama akiukabidhi  Slyveter Bedu cheti cha taaluma katika  katika  kongamano la elimu lililofanyika katika shule ya msingi Hoyoyo wilaya ya mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa (CCM) Mkoa wa Pwani,Gama J Gama (kulia) akikabidhi tanki la maji lita 2000 uongozi wa shule ya msingi hoyoyo   iliyopo kata ya Tengelea wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. 
 Diwani  wa kata ya Tengelea Shabani Manda akizungumza na wazani pamoja na wale katika  kongamano la elimu lililofanyika katika shule ya msingi Hoyoyo wilaya ya mkuranga mkoa wa Pwani  Alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wazazi kuwekeza kwenye elimu kwa watoto kwani huo ndiyo urithi wenye thamani katika maisha yao.
 Katibu wa Mbunge,Omar Kisatu  akiwasisitiza  wanafunzi  wa shule ya msingi hoyoyo   iliyopo kata ya Tengelea wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. kusoma kwa bidii ili  malengo yao yatimie.
Katibu wa CCM Kata ya Tengelea Twahiri Koki akizungumza na wazazi na walezi katika kongamano la elimu lililofanyika katika shule ya msingi Hoyoyo wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ambapo aliwaomba waache tamaduni za zamani wapeke watoto shule watawasaidia baadae wazazi hao. 
Picha ya pamoja


RAMANI YA KUFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU EPHRAIM KIBONDE


BEI ZA NYAMA MAKUMBUSHO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Bei za Nyama katika bucha  mbalimbali katika soko  la Makumbusho wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kamazinavyo onekana katika picha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)


RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ameliagiza jeshi la polisi Mkoani Humo kuhakikisha wanamsaka na kumkamata mganga wa jadi anayesadikiwa kuwaibua na kuwaadhiri wachawi katika bonde la ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga.

Agizo hilo limekuja baada ya kufanya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali katika bonde hilo pamoja na kujionea maendeleo na changamoto za shule ya sekondari Kipeta iliyoezuliwa paa pamoja na shule ya msingi Msia iliyobomoka madarasa manne kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyosababisha madhara hayo mwezi Disemba mwaka 2018.

Ameonya kuwa hataki yaliyotokea mkoa wa Njombe yajirejee katika Mkoa wa Rukwa ikiwa bado watu hawajasahau machungu waliyoyapata kutokana na matukio hayo, na kuongeza kuwa mganga huyo wa kienyeji analindwa na kiongozi wa chama cha kisiasa na hivyo kumtaka mkuu wa kituo cha Kijiji cha Kilyamatundu kuhakikisha anamkamta kiongozi huyo hata kama ni wa Chama cha Mapinduzi.

“OCS na vyombo vyako vile fanya upepelezi wa kina na ukamate yeyote yule ambae ametoka nje ya mkoa huu, nje ya Kilyamatundu anayefanya shughuli hizi, kamata weka ndani fanya mahojiano ya kina, na wengine nimeambiwa hap ani viongozi wa vyama vya kisiasa, usijali huyu ni chama tawala, huyu ni nani, kama ukijua kwa uhakika kamata mhoji mpaka kieleweke, sisi hatutaki kuletewa Lambalamba hapa,” Alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Wangabo aliwapongeza waalimu, Uongozi wa vijiji husika pamoja na wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha katika kuhakikisha majengo yaliyobomoka na kuezuliwa katika shule hizo yanarudi katika hali yake ya kawaida na hatimae wanafunzi kuendela na masomo.

Pamoja na michango ya wadau mbalimbali iliyohamasishwa na Wangabo ambayo imesaidia kurudishisa mapaa ya majengo ya utawala, mabweni mawili, nyumba sita za waalimu na vyoo vya wasichana na wavulana kwa shule ya sekondari Kipeta na kujenga madarasa manane kwa shule shule ya Msingi Msia, Wizara ya Elimu pamoja kwa ushirikiano na Wizara ya TAMISEMI imetoa shilingi Milinoni 75.2 kwaajili ya kuongezea ujenzi wa madarasa na vyoo kwa shule hizo.

Naye Diwani wa kata ya Milepa Apolinari Macheta alipongeza juhudi za Mkuu wa Mkoa kwa kuhakikisha shule hizo zinakuwa bora zaidi ya zilivyokuwa na kumuahidi kuwa Shilingi Milioni 48.6 walizopatiwa kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili na vyoo matundu sita kwa shule ya msingi Msia atahakikisha kwa ushirikiano wa wananchi watapata darasa jingine kwa fedha hizo.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (aliyevaa Kapelo) akiongoza ukaguzi wa ujenzi wa madarasa manane yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi na michango ya wadau katika shule ya Msingi Msia, kata ya Milepa Wilayani Sumbawanga. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (kushoto)  akipewa maelezo juu ya marekebisho yanayoendelea katika ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Msia na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga  Kalolo Ntila (kaunda suti nyeusi) wakati wa kuyakagua madarasa hayo.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea. 
 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akikabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa niaba ya umoja wa waalimu wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Kipeta kwaajili ya wanafunzi ambao vitabu vyao vilirowa na mvua kutokana na mabweni kuezuliwa 

WANAWAKE TPA WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MSAADA MUHIMBILI

0
0
 Mmoja wa wafanyakazi wa TPA, Zahara Malika akikabidhi moja kati ya katoni za Biscuit na misaada mbalimbali walizozitoa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi kwa wazazi wenye watoto wenye Kichwa kikubwa na mgongo wazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kilele chake ni leo. Wengine pichani ni baadhi ya wanawake kutoka TPA waliowatembelea watoto hao hospitalini hapo leo na anayepokea kwa niaba ya wagonjwa wengine ni Nesi wa hospital hiyo, Bi Rehema Ally. 
 Mmoja wa wafanyakazi wa TPA, Hilda Mwakatobe akikabidhi moja kati ya katoni za juisi na misaada mbalimbali walizozitoa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi kwa wazazi wenye watoto wenye Kichwa kikubwa na mgongo wazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kilele chake ni leo. Wengine pichani ni baadhi ya wanawake kutoka TPA waliowatembelea watoto hao hospitalini hapo leo na anayepokea kwa niaba ya wagonjwa wengine ni Bi. Cheusi Selemani.
Baadhi ya wanawake ambao ni wafanyakazi wa TPA wakiwasili katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi kwa wazazi wenye watoto wenye Kichwa kikubwa na mgongo wazi ili kuwatembelea na kuwapa misaada ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kilele chake ni leo.
 Mkurugenzi wa Fedha wa TPA, Bi. Nuru Mhando akimbeba mmoja wa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi waliolazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi ambacho wamelazwa watoto hao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kilele chake ni leo.


Baadhi ya wanawake ambao ni wafanyakazi wa TPA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali na pesa taslimu kwa wazazi wenye watoto wenye Kichwa kikubwa na mgongo waliolazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi. 

JAFO ATAKA KUONDOLEWA KWA VIKWAZO KWA VIJANA WENYE UFAULU WA CHINI KUENDELEA NA MASOMO

0
0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo imezitaka Taasisi zinazosimamia mifumo ya elimu kutoweka vikwazo na masharti magumu kwa vijana wenye ufaulu mdogo kuendelea na kozi mbali mbali.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akizindua Kitaifa Mpango wa Elimu Changamani kwa vijana walio nje ya Mfumo rasmi wa Elimu (IPOSA). Jafo alisema kuwakwamisha vijana wenye ufaulu mdogo kuendelea na kozi mbalimbali kwa vigezo vya kuwa na ufaulu wa chini ni kuwanyima vijana haki ya kupata ujuzi. 

“Tuache kuweka mifumo yenye roho mbaya inayokwamisha  vijana kielimu na ndoto zao za kishiriki uchumi wa viwanda” alisema. Jafo alisema kuwa wapo watalaamu wanakaa Ofisini na kuweka vigezo ambavyo vinalenga kukwamisha vijana kuendelea na mafunzo yakiwemo ya ufundi na kuwafanya kushindwa kushirikia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda

Waziri Jafo aliitaka Taasisi ya Elimu ya watu Wazima kuweka mpango kwa vijana ili waweze kuendelea na vyuo vya juu ili taifa liweze kuwa na wataalam wengi. Kuhusu Mpango wa Elimu Changamani ( IPOSA) alisema umekuja kujibu kauli ya utekelezaji wa uchumi wa viwanda kwani unajengwa na vijana wenye Maarifa.

Waziri  Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa nane na wilaya zake ambako mpango wa IPOSA  unatekelezwa kusimamia ipasavyo na baadae uweze kuenea nchi nzima kama ilivyokusudiwa. Alisema utekelezaji wa Mpango wa IPOSA usiwe wa zimamoto bali uwe endelevu ili vijana wanufaika waweze kushiriki katika ujenzi wa  maendeleo ya Taifa.

Jafo aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kutoa fedha kila mwezi kwa ajili ya kugharamia watoto wa kitanzania kupata elimu bila malipo. Alisema jumla ya shilingi bilioni 23.8 zinatolewa kila mwezi kwa ajili ya kugharamia wanafunzi kusoma bila mzazi kulipa ada na kuwataka watoto kutumia fursa hiyo kusoma kupitia mfumo rasmi.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Tixon Nzunda alisema Mpango wa Elimu Changamani kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi unatekelezwa kwa majaribio mikoa nane hapa nchini. Alitaja mikoa hiyo ni Kigoma, Tabora, Dar es salaam, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe na Dodoma.

Nzunda alisema mpango wa IPOSA awamu ya kwanza  unatarajia kuwanufaisha vijana wapatao 10,000 kati ya vijana milioni 3.5 waliopo nje ya mfumo rasmi wa elimu. Alisema Ofisi ya TAMISEMI kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo kama vile UNICEF walitembelea na kubaini vituo 72 vitakavyotekeleza mradi huo katika mikoa hiyo.

Kwa upande wa Mratibu wa Mpango huo Dkt. Sempheo Siafu alisema kuwa mpango huo utachukua miezi 20 hadi kukamilika huku ufundishaji ukifanyika kwa njia ya nadharia na vitendo ukiwahusisha vijana wenye umri wa miaka 14 hadi 17. Alisema lengo kuu la mpango huu ni kuhakikisha kuwa na vijana walioelimika, wenye maarifa, ujuzi na stadi za kuweza kuchangia kwa haraka maendeleo ya taifa na kuhimili ushindani.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Erick Komanya akitoa salamu za Mkoa wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa Mpango wa Elimu changamani kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu(IPOSA).

  Baadhi ya washiruiki wa uzinduzi wa Kitaifa wa Mpango wa Elimu changamani kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu (IPOSA) leo mjini Tabora.
 Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza la Usimamizi  Taasisi ya Elimu ya Watu Waziri Naomi Katunzi akitoa salamu za Taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya Mfumo rasmi (IPOSA) leo mjini Tabora.
 Mratibu wa Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya Mfumo rasmi wa Elimu (IPOSA) akitoa ufafanuzi jinsi watakavyoendesha mafunzo kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi leo mjini Tabora. 
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tixon Nzunda akitoa  maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi ili azindue Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu(IPOSA) leo mkoani Tabora. 

 Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa Mpango wa Elimu Changamani kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu (IPOSA) leo Tabora. Picha na Tiganya Vincent

SHEIKH ZUBER YAHYA AZIKWA NA MAELFU YA WATU. INNALILLAH WAINNA ILAYHI RAJIUWN

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images