Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapindunzi  ya Zanzibar, Balozi Seif Iddi kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Machi 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Iddi, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Machi 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS KAGAME WA RWANDA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Rwanda Paul Kagame akifurahia zawadi ya Kinyago aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Rwanda Paul Kagame akifurahia zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro mara baada ya kupewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya picha kutoka kwa  Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

UTENDAJI KAZI TBS WAMKOSHA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameridhishwa na utendaji kazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Waziri Mkuu Majaliwa alifanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo jijini Dar es Salaam akiwa ameongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji),  Angella Kairuki.

Pia alikuwepo Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya pamoja na maofisa wengine wa ngazi mbalimbali serikalini.

Akizungumza baada ya kujionea shughuli za Shirika hilo, Waziri Mkuu ametoa pongezi kwa kazi nzuri inayofanywa na Shirika la Viwango 

Tanzania na kwamba ameridhishwa na utendaji wa kazi pamoja na kuwepo kwa vifaa vya kisasa na wataalam wazuri katika maabara zake.

"Nimefurahishwa na utendaji kazi wenu pamoja kuwepo kwa vifaa vya kisasa vya maabara pamoja na wataalamu," alisema.

Waziri Mkuu Majaliwa ameielekeza TBS kufanya kazi kwa weledi kwa kuhakikisha inakuwa na maofisa kila Mkoa na Wilaya ili kuweza kusogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi.

Ametoa mwito kwa wafanyakazi wa TBS kuendelea kufanya kazi kwa weledi na juhudi na kuhakikisha umma wanaelimishwa zaidi kuhusiana na shughuli zinazofanywa na shirika hilo hapa nchini.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka  Mawaziri wa Kilimo, Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mifugo na Uvuvi na Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto wakutane na wafanye mapitio ya taasisi zao na kuangalia maeneo yanayogongana kiutendaji ili kila mmoja abaki na jukumu lake.

Aliagiza apelekewe taarifa za mapendekezo hayo  ifikapo Machi 30,2019. Amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamedai kuwepo kwa muingiliano wa majukumu ya kiutendaji wa taasis hizo.

“Kutaneni na kisha pitieni maelekezo ya Serikali yanayoelekeza namna ya kuzifanya taasisi  hizi na zingine zinazofanya shughuli zinazofanana zilizo katika wizara zenu bila  kusahau Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (blue print). Ifikapo Machi 30,2019,  niwe  nimepata mapendekezo yenu,” amesisitiza.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Cunbert Kapilima wa Shirika la Viwango Tanzania  -TBS (kushoto) kuhusu upimaji wa ubora maguani unaofanywa na TBS wakati alipotembelea ofisi za TBS, Ubungo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu upimaji wa betri kutoka kwa Mhandisi  Anectus Nduguru wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati alipotembelea Ofisi za TBS, Ubungo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu upimaji wa vifaa vya umeme kutoka kwa Mhandisi  Anectus Nduguru wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati alipotembelea Ofisi za TBS, Ubungo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati alipotembelea ofisi za  TBS,  Ubungo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, wa tatu kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa nne kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI KIGWANGALA ATOA MSIMAMO VITA DHIDI YA UJANGILI, ASEMA ASKARI WANAOLINDA HIFADHI WANAFUATA SHERIA.

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dkt. Hamisi Kigwangala amewataka Watanzania kuondokana na dhana iliyojengeka miongoni mwao kuwa watumishi wa Wizara hiyo hususan  wahifadhi wa  wanyamapori na Misitu  ni watu katili  wanaowatesa Wananchi.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akifungua mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi jijini Mwanza.

Amesema watumishi hao ni watu wenye utu na weledi wa hali ya juu na wanaozingatia  sheria katika kutimiza majukumu yao na hulazimika kutumia nguvu wakati wakipambana na majangili wanaokutwa katika maeneo ya hifadhi wakifanya vitendo vya ujangili.

‘’ Ulinzi wa Rasilimali za nchi ni jukumu letu sote, wizara imepewa dhamana ya kusimamia na kuongoza kwa niaba ya watanzania, kama kuna watumishi wa Wizara hii wanaowanyanyasa wananchi naomba walete ushahidi kwetu ili tuwachukulie hatua’’ amesema Dkt. Kigwangala.

Waziri Kigwangala amesikitishwa na idadi ya watumishi walipoteza maisha kwa ajali na wengine kuuwawa na majangili wakati wakipambana nao katika maeneo yote ya hifadhi  nchini na kutoa wito kwa wananchi wote wenye taarifa au ushahidi juu ya vitendo vyovyote vya kihalifu kuziwasilisha katika mamlaka zinazohusika.

Amesema kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na vitendo vya ujangili na uhalifu katika maeneo ya hifadhi na wale wote wanaoshirikiana na makundi ya watu wenye nia ovu ya kukwamisha juhudi za uhifadhi wa rasilimali za Taifa.

Ametoa wito kwa wananchi kuheshimu sheria za uhifadhi na kuepuka kuvamia maeneo ya hifadhi kwa shughuli za kijamii na ufugaji akitoa wito kwa viongozi mbalimbali wa Siasa kuunga mkono juhudi za wizara za ulinzi wa maeneo ya hifadhi kwa kuwaelimisha wananchi wanaowaongoza kujiepusha na vitendo vya uvamizi wa maeneo ya hifadhi badala ya kuwatetea.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof.Adolf Mkenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho amesema kuwa jumla ya watumishi 23 walifariki dunia  wakati wakitekeleza majukumu ya uhifadhi   na   5 walijeruhiwa na majangili wakiwa kazini.

Prof. Mkenda amesema kuwa waliofanya vitendo hivyo  hawaitakii mema Tanzania na ni maadui wa shughuli za uhifadhi nchini akiongeza kuwa Serikali itaendelea kusimama na kuwatetea watumishi na askari wa wanyamapori wanaotimiza majukumu yao kwa kuzingatia sheria.
 Katibu Mkuu wa  Maliasili na Utalii Prof, Adolf Mkenda akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo (hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi wa baraza la 26 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo liliofanyika  leo Jijini Mwanza.

 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala akisisitiza jambo  wakati akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo kuhusu umuhimu wa kutekeleza maagizo kwa wakati yanayotolewa na Viongozi wa Wizara hiyo katika kikao cha Baraza la 26 la  Wafanyakazi wa Wizara hiyo  kilichofanyika leo Jijini Mwanza.
 Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii Mhe,Constantine Kanyasu akizungumza na Watumishj wa Wizara  hiyo katika kikao cha Baraza la 26 la  Wafanyakazi kilichofanyika leo Jijini Mwanza.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri  wa Wizara, Mhe, Constantine Kanyasu wakiwa wameshikana na watumishi wengine  hukuwakiimba wimbo wa mshikamano Daima katika Kikao cha Baraza la 26 la Wafanyakazi kilichofanyika leo jijini Mwanza.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Constantine Kanyasu wakati akikagua gwaride la Jeshi Usu katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Pasiansi.
Wafanya kazi wa  Maliasili na Utalii wakiimba wimbo wa mshikamano Daima katika Kikao cha Baraza la 26 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo jijini Mwanza.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WALIVYOSHIRIKI KILI MARATHON 2019

$
0
0
 Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushiriki mashindano ya mbio za Kili Marathon 2019, zilizofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro. Jumla ya wafanyakazi 208 wakiwemo Mameneja walishiriki mashindano hayo kutoka matawi yetu ya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro pamoja na wale wa Makao Makuu.














UTENDAJI KAZI TBS WAMKOSHA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu upimaji wa betri kutoka kwa Mhandisi Anectus Nduguru wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati alipotembelea Ofisi za TBS, Ubungo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu upimaji wa betri kutoka kwa Mhandisi Anectus Nduguru wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati alipotembelea Ofisi za TBS, Ubungo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu upimaji wa vifaa vya umeme kutoka kwa Mhandisi Anectus Nduguru wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati alipotembelea Ofisi za TBS, Ubungo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati alipotembelea ofisi za TBS, Ubungo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, wa tatu kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa nne kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Na Mwandishi Wetu, Globu ya jamii 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameridhishwa na utendaji kazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Waziri Mkuu Majaliwa alifanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo jijini Dar es Salaam akiwa ameongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angella Kairuki. 

Pia alikuwepo Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya pamoja na maofisa wengine wa ngazi mbalimbali serikalini.

Akizungumza baada ya kujionea shughuli za Shirika hilo, Waziri Mkuu ametoa pongezi kwa kazi nzuri inayofanywa na Shirika la Viwango .Tanzania na kwamba ameridhishwa na utendaji wa kazi pamoja na kuwepo kwa vifaa vya kisasa na wataalam wazuri katika maabara zake.

"Nimefurahishwa na utendaji kazi wenu pamoja kuwepo kwa vifaa vya kisasa vya maabara pamoja na wataalamu," alisema.Waziri Mkuu Majaliwa ameielekeza TBS kufanya kazi kwa weledi kwa kuhakikisha inakuwa na maofisa kila Mkoa na Wilaya ili kuweza kusogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi.

Ametoa mwito kwa wafanyakazi wa TBS kuendelea kufanya kazi kwa weledi na juhudi na kuhakikisha umma wanaelimishwa zaidi kuhusiana na shughuli zinazofanywa na shirika hilo hapa nchini.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka Mawaziri wa Kilimo, Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mifugo na Uvuvi na Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto wakutane na wafanye mapitio ya taasisi zao na kuangalia maeneo yanayogongana kiutendaji ili kila mmoja abaki na jukumu lake.

Aliagiza apelekewe taarifa za mapendekezo hayo ifikapo Machi 30,2019. Amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamedai kuwepo kwa muingiliano wa majukumu ya kiutendaji wa taasis hizo.

“Kutaneni na kisha pitieni maelekezo ya Serikali yanayoelekeza namna ya kuzifanya taasisi hizi na zingine zinazofanya shughuli zinazofanana zilizo katika wizara zenu bila kusahau Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (blue print). Ifikapo Machi 30,2019, niwe nimepata mapendekezo yenu,” amesisitiza. 

WABUNGE WA CHADEMA SUZAN KIWANGA NA PETER LIJUALIKALI WAENDELEA KUSOTA LUMANDE

$
0
0


Mbunge wa mlimba Susan Kiwanga na mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali wakijadili jambo Fulani katika mahakani ya Mkazi mkoa wa Morogoro kabla ya kesi yao kusomwa.


NA FARIDA SAIDY MOROGORO


WABUNGE wa Chama cha Deomkrasia na Maendeleo (CHADEMA) Peter Lijualikali wa Jimbo la Kilombero na Suzan Kiwanga wa Jimbo la Mrimba na wafuasi saba wa chama hicho wamerudishwa mahabusu leo March 7,2019 baada ya kushindwa kutimza masharti ya dhamana yaliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro baada ya kusota mahabusu kwa siku kumi na saba.

Washitakiwa hao wamepewa masharti ya dhamana na Hakimu Mfawidhi Elizabeth Nyembele ambapo amesema pingamizi lililowekwa kwa upande wa Jamhuri halikuzingatia sheria hivyo kuamua kulitupilia mbali pingamizi hilo.

Katika masharti hayo, washitakiwa wametakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambapo wa kwanza anatakiwa kusaini bondi ya Milioni tano na wapili awe na mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni tatu na nusu na kwamba kesi hiyo itaanza kusikilizwa March 22 mwaka huu.

Hata hivyo kutokana na uamuzi huo wa mahakama wakili wa upande wa utetezi Bw. Hekima Mwasiku amesema kuwa atahakikisha wateja wake wanatimiza masharti ya ya dhamana.

Washitakiwa hao wanadaiwa kushitakiwa kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali, kula njama kutenda kosa, kufanya maandamano, kufanya uchochezi wa kutenda kosa, kuchoma moto ofisi ya serikali na kuharibu mali kwa makusudi makosa ambayo wanadaiwa kutenda katika marudio ya uchaguzi mdogo kata ya Sofi wilayani Malinyi Novemba 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame Ikulu jijini Dar es Salaam. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame kabla ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

KAMATI YA BAJETI YATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA K VANT NA TBL JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akiwa ameambatana na wajumbe wake wakiwasili katika kiwanda cha Tanzania Breweries Limited (TBL)Arusha kwa ajili ya kuangalia jinsi Mfumo wa Stempu za Kielektroniki (ETS) unavyofanya kazi katika kiwanda hicho
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. George Simbachawene wakiangalia namna ya uazalishaji wa bia wakati walipotembelea katika kiwanda cha Tanzania Breweries Limited (TBL) Arusha kwa ajili ya kuangalia jinsi Mfumo wa Stempu za Kielektroniki (ETS) unavyofanya kazi katika kiwanda hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akiwa ameambatana na wajumbe wake wakionyeshwa namna ambavyo bia zinabandikwa Stempu za kielektroniki na Meneja wa Kiwanda cha Tanzania Breweries Limited (TBL) Ndugu Joseph Mwaikasu.Wajumbe hao walitembelea kiwanda hicho kwa lengo la kuangalia jinsi Mfumo wa Stempu za Kielektroniki (ETS) unavyofanya kazi katika kiwanda hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Mega Breweries Limited Arusha watengenezaji wa kinywaji cha K VANT, Ndugu Francis Kimaro wakati Kamati ilipotembelea Kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia jinsi Mfumo wa Stempu za Kielektroniki (ETS) unavyofanya kazi katika kiwanda hicho, pembeni yake ni Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Ndugu Abdul Zuber.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, wakiongozwa na Mhe. George Simbachawene wakiangalia baadhi ya mitambo inayotumika kutengeneza kinywaji cha K VANT cha Arusha wakati Kamati ilipotembelea Kiwanda cha Mega Breweries Limited Arusha kwa ajili ya kuangalia jinsi Mfumo wa Stempu za Kielektroniki (ETS) unavyofanya kazi katika kiwanda hicho.

TANZIA: TAARIFA YA MSIBA WA MZEE DANIEL SAITORE KAAYA (DSK) JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC Ndugu Elishilia Kaaya anasikitika kutangaza kifo cha Baba yake Mzazi Mzee Daniel Saitore Kaaya DSK kilichotokea  Jumatano Usiku tarehe 06/03/ 2019 katika Hospitali ya AICC Arusha.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika nyumbani kwake  kijijini Nguruma Duluti wilayani Arumeru siku ya jumanne tarehe 12/03/2019.Habari ziwafikie ndugu jamaa na marafiki

Vodacom watoa msaada kwa watoto wenye uhitaji maalumu

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bw. Filberto Sanga akipokea msaada uliotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kutoka kwa Meneja Mawasiliano na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Christina Murimi (kushoto) na Meneja Mahusiano, Alex Bitekeye (kulia), kwa ajili ya kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu wanaoshi katika kituo cha Mwanangu Special kilichopo Vikindu mkoani Pwani. 



Meneja Mawasiliano na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Christina Murimi (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo cha Mwanangu Special, Walter Miya vifaa vya watoto wenye mahitaji maalumu kutoka taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation. Akishuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bw. Filberto Sanga (katikati). Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC kupitia mpango wao wa Pamoja na Vodacom wametoa msaada wenye thamani ya TZS 9.5m kwa watoto hao kwa lengo la kuwawezesha katika maisha yao ya kila siku ili kufikia ndoto na malengo yao. 



Katika kusherehekea wiki ya wanawake duniani wafanyakazi wa kampuni hiyo kupitia mpango wao wa Pamoja na Vodacom wametoa vifaa vyenye thamani ya TZS 9.5m kwa watoto hao ili kuwezesha maisha yao ya kila siku na kufikia ndoto na malengo yao. Wengine ni Mkurugenzi wa kituo hicho, Walter Miya (kati) na Jennifer Shumbusho (wa pili kulia) mmoja wa wazazi wa watoto hao.

Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani, wafanyazi wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Plc, kupitia mpango wake wa Pamoja na Vodacom ulio chini ya taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation leo wamechangia vifaa mbali mbali vyenye thamani ya shilingi milioni 9.6 kwa kituo cha watoto wenye uhitaji maalum kiitwacho Mwanangu Special kilichopo Mkuranga, mkoani Pwani. Kituo hicho kina jumla ya watoto 40, kati yao 20 ni wale wenye mahitaji maalum kama vile mgongo wazi, vichwa vikubwa na down syndrome.

Wafanyakazi hao wametoa vifaa kama vile; viti maalum, magongo ya kutembelea, magongo ya kusimamia, mashine za uzito, viatu vya ‘Special Orthopedics’, vitanda vya watoto walemavu, mashine za kufulia nk. ambavyo ni mahitaji muhimu kwa watoto hao. Mbali na misaada hiyo, wafanyakazi wa Vodacom pia walijitolea muda wao kucheza na kufurahi pamoja na watoto hao kwa ajili ya kuwapatia faraja.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bw. Filberto Sanga aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa mpango huo akisema “Serikali yetu imedhamiria kuboresha maisha ya kila mtanzania ili kutimiza dira ya maendeleo ya taifa na jitihada kama hizi kutoka kampuni binafsi zinasaidia serikali kutimiza malengo yake”. Bw. Sanga pia aliishukuru kampuni ya Vodacom huku akifafanua namna ambavyo msaada huo utasaidia kuhudumia watoto wenye ulemavu nchini na kuhimiza taasisi zingine kufuata nyayo za Vodacom. 

Mpango wa Pamoja na Vodacom umekuwa ukitumiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ili kurejesha fadhila kwa jamii. Mpango huu umewafanya wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwa mawakala wa mabadiliko kwa kusaidia kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Jacquiline Materu alisema “Wafanyakazi wa Vodacom, tunashauku ya kuisaidia jamii yetu na huu umekuwa ni utaratibu wetu kwa miaka zaidi ya 12 kupitia Vodacom Tanzania Foundation. Katika kusherehekea wiki hii ya wanawake duniani, tumeona ni vyema kusherehekea na wadogo zetu, kuwapatia mahitaji muhimu na pia kuwawezesha kuwa na nyenzo muhimu za kuwasaidia kufikia ndoto zao kwani ulemavu sio kikwazo cha mafanikio”. 

Mzazi XXX ambaye pia ni mfanyakazi wa kituo hicho alieleza furaha yake kupokea vifaa vitakavyosaidia watoto anaowalea “ahsanteni kwa ukarimu wenu na kwa kutukumbuka. Zawadi hizi zitawasaidia watoto hawa katika maisha yao ya kila siku”. Walezi wengine pia walionyesha kufurahishwa na kushukuru kwa zawadi zitakazo wasaidia katika malezi ya watoto hao kwani wengi wao wametoka familia duni.

WAMILIKI VYOMBO VYA USAFIRI JIJINI DODOMA WASHAURIWA KUCHANGAMKIA FURSA

$
0
0

Muonekano wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora linalojengwa katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma
IMG_5308
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwasili katika Mji wa Serikali kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Utumishi katika mji huo Ihumwa, jijini Dodoma. 
IMG_5325
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akitoa maelekezo kwa Mhandisi, Lucas Lipambila (kushoto) wakati wa ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
IMG_5486
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza jambo baada ya kukamilika kwa ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb).
IMG_5563
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
IMG_5591
Afisa Tawala Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Donald Bombo akisisitiza jambo kwa Mhandisi Lucas Lipambila (wa pili kutoka kulia) baada ya kumalizika kwa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma

BEI YA NYAMA MAKUMBUSHO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Bei za Nyama katika bucha  mbalimbali katika soko  la Makumbusho wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,kamazinavyo onekana katika picha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)


Prof. Kabudi akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Dkt. Richard Sezibera. Katika mazungumzo yao, Mhe. Sezibera alimpongeza Mhe. Kabudi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Ernest Mangu na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Wilbroad Kayombo. Mhe. Sezibera yupo nchini kwa ajili ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame. 
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Eugene Kayihura (kulia) na Afisa Ubalozi wa Rwanda wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Prof. Kabudi na Mhe. Dkt. Sezibera (hawapo pichani). 
Mhe. Prof. Kabudi akimwelezea jambo Mhe. Dkt. Sezibera wakati wa mazungumzo hayo.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Ernest Mangu pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Bw. Wilbroad Kayombo wakiwa kwenye Mazungumzo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Dkt. Richard Sezibera (wapili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Ernest Mangu (wa kwanza kulia) na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Eugene Kayihura (wa kwanza kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.




BEI ZA NYAMA SOKO LA MAKUMBUSHO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Bei za Nyama katika bucha  mbalimbali katika soko  la Makumbusho wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,kamazinavyo onekana katika picha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)



Wanawake soko la Feri na maeneo jirani waishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0


Na Mwandishi Maalum

Wanawake wa soko la Feri pamoja na maeneo jirani wameishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kufanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na kutoa elimu ya magonjwa hayo.

Upimaji huo umefanywa leo na wafanyakazi wanawake wa Taasisi hiyo ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kitaifa yatafanyika kesho.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wanawake hao walisema muda mwingi wamekuwa wakiutumia katika biashara na kutunza familia zao na hivyo kukosa nafasi ya kwenda kupima afya zao.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi Ashura Omari ambaye ni mfanyabiashara wa chakula katika soko hilo alisema wamefarijika sana kuona wataalamu wa magonjwa ya moyo wamewafuata katika soko la Feri la kuwapa huduma ya upimaji pamoja na kutoa elimu.

“Tunashukuru sana kwa kupimwa afya zetu, nimepimwa urefu, uzito, wingi wa sukari na msukumo wa damu mwilini (BP). Tunaiomba Taasisi hii na Serikali kwa ujumla waweze kutoa huduma kama hii katika maeneo mengi zaidi”, alisema Ashura.Naye Mariam Mohamed ambaye ni mkazi wa Kinondoni alisema amefika katika soko hilo la feri kupata huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake.

Mariam alisema amepata elimu ya jinsi ya kuandaa chakula bora kwa familia, kutotumia chumvi nyingi na mafuta mengi katika chakula, pia anapoandaa chakula ni ahakikishe familia ile chakula chenye mboga za majani na matunda.

“Pia nimeambiwa unywaji wa pombe uliokithiri pamoja na kutokufanya mazoezi ni vitu ambavyo vinapelekea kupata magonjwa ya moyo nitajitahidi mimi na familia yangu kufuata haya yote niliyofundishwa leo”, alisema Mariam.

Akitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa wanawake waliohudhuria upimaji huo Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hildegard Karau alisema mtindo wa maisha unapelekea watu wengi kupata magonjwa ya moyo ikiwemo shinikizo la damu na kuwataka wanawake hao pamoja na familia zao kufanya mazoezi.

“Wanawake ni watu wa muhimu sana katika familia kama mtazingatia mafunzo mliyopewa leo na kuandaa vyakula bora katika familia zenu itawasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda familia familia zao”, alisema Hildegard.

Wakati huo huo wanaume wa soko la Feri waliiomba Taasisi hiyo wakati mwingine watakapoandaa upimaji kama huo wasiwasahau wanaume kwani nao muda mwingi wanahangaika kutafuta fedha za kutunza familia na kukosa muda wa kwenda kupima afya zao.

Mzee Husein Mbaraka alisema, “Katika soko hili kuna watu wengi wanaofanya kazi mbalimbali wakiwemo wavuvi ambao muda mwingi wanashinda Baharini , tunaiomba Taasisi hii siku nyingine waje kutupima na sisi magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na kutupa elimu.

VOA Swahili: Duniani Leo March 7th, 2019

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK, MAREKANI

OSHA Yatoa mafunzo kwa Wanawake wanaofanya usafi Barabarani.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 


Wakala wa Usalama na Afya Pahala Pa Kazi (OSHA)imesema kuwa nguvu kazi ya Taifa lazima ilindwe katika afya ili iweze kuzalisha kwa kujenga uchumi wa nchi.

Hayo ameyasema Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda wakati wa mafunzo ya wafanyakazi wanawake wanaofanya usafi katika barabara za Manispaa ya Kinondoni na Ilala amesema kuwa wanawake ndio wazalishaji pamoja na wasimamizi wa familia hivyo serikali inaangalia katika jicho ya kulinda afya zao wasiweze kuteteleka na kushindwa kusimamia familia zao.

Amesema kuwa wanawake hao wanaweza kuwa wanafanya usafi lakini hawafahamu jinsi ya kulinda afya zao ambapo OSHA ndio kazi yao katika kuwajengea uwezo wa kutambua umuhimu wa afya zao katika sehemu za kazi zao.

Mwenda amesema kuwa katika kuelekea siku ya kilele cha maadhimisho ya siku wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya kila mwaka OSHA imeona ni wakati mwafaka kutoa elimu ya wafanyakazi wanawake wa usafi katika baadhi ya barabara katika jiji la Dar es Salaam.

Aidha Mwenda amesema kuwa OSHA itaendelea kutoa elimu katika mahala pa kazi katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unajengwa na nguvu kazi yanye afya imara." Tumedhamiria kutoa elimu pahala pa kazi katika kuimarisha Afya za wafanyakazi ya kutokuwa na madhara ya kazi kwa kuwa wana vifaa vya kuzuia madhara hayo"amesema Mwenda 

Amesema kauli mbiu ya OSHA katika siku ya wanawake ni 'Usalama wa Afya kwa kuzinagatia Usawa wa Kijinsia, Badiri Fikra Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu.Katika mafunzo hayo OSHA imetoa vifaa kinga kwa wanawake hao ili waweza kutekeleza majukumu yao katika kujilinda na afya na usalama sehemu zao za kazi.

Nae Mfanyakazi wa Usafi Barabarani Halima Rajab amesema wanachangamoto kwa madereva ambao huwa wanawafaya kuwa waangalifu na bila kufanya hivyo wanagongwa.

Amesema wanaishukuru OSHA kwa kuwaandalia mafunzo kwani wanaamini serikali imewaona. Maendeleo ya Uchi kuhakikisha
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Pahala Pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda akizungumza wakati akifungua mafunzo ya wanawake wanafanya usafi katika barabara za jiji Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa usafi Barabarani wakiwa katika mafunzo ya OSHA
Baadhi ya wanawake na wamiliki wa kampuni za ukandarasi wa usafi wa barabara katika jiji la Dar es Salaam wakipatiwa mafunzo na OSHA.
Halima Rajab Mfanyakazi wa Usafi wa Barabara akizungumza na waandishi habari kuhusiana na changamoto wanazokutana katika usafi wa barabara wakati wa mafunzo ya OSHA ya wanawake.

ALL IS SET FOR THE 7TH EAST AFRICAN HEALTH AND SCIENTIFIC CONFERENCE & INTERNATIONAL HEALTH EXHIBITION AND TRADE FAIR IN DAR

$
0
0


EAST AFRICAN HEALTH RESEARCH COMMISSION

East African Health Research Commission, 7th March 2019: Dar es Salaam: The Executive Secretary and CEO of the East African Health Research Commission, Prof. Gibson Sammy Kibiki, has disclosed that all is set for the 7thEast African Health and Scientific Conference (EAHSC) due to take place on 27th to 29th March 2019 at the Julius Nyerere International Convention Centre (JNCC) in Dar es Salaam, Tanzania.

Prof. Kibiki, who was addressing a Press Conference on the sidelines of the 2nd Meeting of the Regional Steering Committee of the 7th EAHSC taking place at the Tanzania’s National Institute of Medical Research (NIMR) in Dar es Salaam, confirmed that the Vice President of the United Republic of Tanzania, H.E. Samia Hassan Suluhu has confirmed gracing the official opening of the event.

The theme of the 7th East African Health and Scientific Conference (EAHSC) is Technology for health systems transformation and attainment of the UN-Sustainable Development Goals.  

At the press conference, the Executive Secretary was flanked by Prof. Mohammed Bakari Kambi, the Chief Medical Officer in Tanzania’s Ministry of Health; Prof. Yunus Mgaya, the Director General of NIMR; and Prof. Eligius Lyamuya, the Chair of the 7th East African Health and Scientific Conference (EAHSC).

Prof. Kibiki informed the Journalists that the EAC Council of Ministers approved convening of the biannual event and hosted on a rotational basis by the EAC Partner States through their respective National Ministries responsible for EAC Affairs, Ministries responsible for Health, and other relevant organizations, and in close collaboration with regional and international health-related NGOs, civil society organizations, individuals, and stakeholders.

He noted that the EAHSC contributes towards strengthening regional cooperation in health in line with Article 118 of the Treaty for the Establishment of EAC as well as other relevant provisions of the EAC Common Market Protocol. “It enhances the ideals of the EAC, which is free movement of People, Services, and Goods”.

Prof. Kibiki informed the media that based on the Protocol establishing the East African Health Research Commission (EAHRC); the Commission is tasked with the responsibility of coordinating the East African Health and Scientific Conference & International Health Exhibition and Trade Fair.

The EAHSC will bring together stakeholders of the health sector from EAC (EAC Secretariat, East African Legislative Assembly, East African Court of Justice, members of the EAC Council of Ministers, members of the Summit, and EAC institutions, EAC Partner States that include Ministers of Health, Finance, Higher Education, Science and Technology, Members of Parliament from National Assemblies, government officials, researchers, scientists, practitioners, civil society, media, donors and development partners and the public at large.

As part of the pre-conference meetings, the East African Health Research Commission will organize the 1st East African Government Leaders, Legislators, and Legal Executives’ Forum (EAGLES’ Forum) on 26th March 2019 also in Dar es Salaam.

EAGLES’ Forum was approved by the 15th EAC Sectoral Council of Ministers of Health as one of the pre-conference meetings of the East African Health and Scientific Conference. It is a dialogue between Bureaucrats and Technocrats that brings together EAC government leaders, members of parliament, Officials from the judiciary system, health experts and the EAHRC to discuss health issues.

“Bringing together the three pillars of governance in the EAC and its Partner States, the forum allows for attaining consensus and collective position on pertinent health issues” noted Prof. Kibiki, adding that “the 1st EAGLES’ Forum will focus on the Digital Regional East African Community Health (REACH) Initiative Strategic Plan approved by the 17th Sectoral Council of Ministers”.

The dialogue will center on alignment of Digital REACH Initiative and Digital Health Initiatives in EAC Partner States; and on addressing issues of resources mobilization for the Digital REACH Initiative. Digital REACH Iniitative will be launched during the opening ceremony of the 7th EAHSC.

 Prof. Mohammed Kambi (Red tie), the Chief Medical Officer in Tanzania’s Ministry of Health; Prof. Yunus Mgaya (middle), the Director General of NIMR; and Prof. Eligius Lyamuya (far left), the Chair of the 7thEast African Health and Scientific Conference & International Health Exhibition and Trade Fair (EAHSC) at the Press Briefing.
The Executive Secretary and CEO of the East African Health Research Commission Prof. Gibson Sammy Kibiki briefing the media on the forthcoming 7th East African Health and Scientific Conference & International Health Exhibition and Trade Fair
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images