Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

PIGO JINGINE KWA CLOUDS MEDIA GROUP, MTANGAZAJI WAKE EPHRAIM KIBONDE AFARIKI DUNIA

0
0

*Alikuwa akitokea Bukoba kwenye maziko ya Ruge Mutahaba

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

PIGO jingine Clouds Media Group! Ndivyo unavyoweza kuzungumzia taarifa za kufariki Dunia kwa Mtangazaji wake maarufu Ephraim Kibonde.

Kwa mujibu wa taarifa za Uongozi wa Clouds Media Group kupitia kwa Sebastian Maganga ambazo wamezitoa mapema hii zinasema Kibonde amefarikia dunia leo asubuhi ya Machi 7,2019. Amesema taarifa nyingine kuhusu kifo cha Kibonde zitaendelea kutolewa ili kuufahamisha umma. 

Awali Mkuu wa Mwanza John Mongela alikuwa wa kwanza kutoa taarifa za kufariki kwa Kibonde ambapo amesema kifo chake kimetokana na kusumbuliwa na shinikizo la damu ambalo lilianza tangu akiwa mkoano Kagera.

"Ephraim Kibonde amefariki akiwa hapa mkoani Mwanza ambako alikuwa anasumbuliwa na presha tangu akiwa kwenye shughuli za mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba," amesema Mongella.

Kibonde alikuwa miongoni kwa wafanyakazi wa Clouds Media walioambatana na waombolezaji wengine kwenda kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele aliyekuwa Mkurugezi wa Vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba ambaye alifariki Dunia Februari 26 mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Michuzi Media Group, ambayo ilipata kufanya mahojiano ya mwisho na marehemu Kibonde wakati wa msiba wa Ruge kupitia Michuzi TV,  inaungana na Watanzania wengine kutoa pole kwa familia ya marehemu Ephraim Kibonde,wafanyakazi wa Clouds Media Group,ndugu,jamaa na marafiki.
Bwana Ametoa,
 na Bwana Ametwaa.
Jina lake na lihimidiwe
AMINA

WACHIMBAJI WA MADINI WATENGEWA MAENEO MAALUM YA KUUZIA MADINI MKOANI RUVUMA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameawaagiza wachimbaji wa madini kutouza madini holela na badala yake wauze katika vituo usika. Mndeme ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini eneo la MASUGURU Kijiji cha MKEKE kata ya AMANI MAKORO Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA AFUNGUA MKUTANO WA WANAWAKE, KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

0
0
Spika Mstaafu Mh. Mama Anne Makinda akizungumza na wanawake katika mkutano wa majadiliano kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayofanyika Machi 8 Kila mwaka, Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha Wanawake Wanasheria TAWLA na Shirika la OXFARM unafayika kwenye hoteli ya Protea Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la OXFARM Bw. Odokorach Francis akizungumza katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Protea Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake Wanasheria TAWLA Bi. Tike Mwambipile akikmaribisha mgeni rasmi ili kuzungumza na wanachama na waalikwa wa mkutano huo na kufungua mkutano huo.
Mary Matui Mwebdeshaji wa mkutakuhusu matukio mbalimbali yatakayofanyika kwenye mkutano huo.no huo akizungumza jambo 
Kulia ni Mkuu wa Mipango Chama cha Wanasheria Wanawake Mary Richard kulia na Mkamiti Mgawe Ofisa Ubia wa Miradi Oxfarm wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waalikwa wakiwa katika mkutano huo
Katikati ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akiwa katika mkutano huo kulia ni Mbunge wa jimbo la Hanang Dk. Mary Nagu na kushoto ni Mkutugenzi Mtendaji wa TAWLA Bi Tike Mwambipile.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akiimba wimbo maalum wa kuwahamasisha wanawake pamoja na Mbunge wa jimbo la Hanang Dk. Mary Nagu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akisalimiana na mmoja wa wanachama wa TAWLA wakati alipowasili katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawasheria Wanawake Bi. Tike Mwambipile akimuongoza Spika Mstaafu wa Bunge Mama Anne Makinda wakati akiingia kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA akiwaongoza wanawake kuimba wimbo maalum wa kuwahamasisha wanawake katika mkutano huo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akizungumza na Mbunge wa Hanang Dk. Mary Nagu kushoto ni Mama Kijo Bisimba mwanaharakati.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akizungumzana baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA wa kwanza kulia ni Mbunge wa viti maalum Chadema Bi. Suzan Lyimo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mara baada ya kufungua rasmi.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR,CCBRT YAWAFANYIA UCHUNGUZI WA MACHO WATOTO 165.

0
0
Wizara ya Afya Zanzibar kwa kushirikiana na Hospitali ya CCBRT ya Dar esd salaam wamewafanyia uchunguzi wa macho Watoto 165 katika kambi ya Macho Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.

Kati ya Watoto hao wawili wameonekana kuwa na Kensa ya Jicho na wanatarajiwa kusafirishwa kwenda Tanzania bara kwa ajili ya kufanyiwa matibabu

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed ametembelea kambi hiyo na amesema lengo kuu la ziara hio ni kuangalia namna ya zoezi la Uchunguzi linavyofanyika .

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara hiyo, Waziri wa Afya amesema wizara yake itatoa ushirikiano ili kuhakikisha watoto wote watakaogundulikana kuwa matatizo ya macho wanapata matibabu mapema ili kuwanusu na kupata upofu watakapo kuwa watu wazima.

Alisema hadi sasa maradhi ya macho yaliyogundulika kuwasumbua watoto waliofanyiwa uchunguzi kuwa ni Mtoto wa Jicho, Uvimbe katika macho, Presha ya macho na Uoni hafifu.



Kambi hiyo ya macho kwa watoto itadumu kwa wiki moja na Waziri Hamad Rashid amewaomba wazazi na walezi ambao watoto wao wanamatatizo ya macho kuwapeleka Hospitali kuu ya Mnazimmoja Kitengo cha macho ili kufanyiwa uchunguzi.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Muandishi wa Habari kuhusiana na ziara alioifanya katika kambi ya Macho kwa Watoto,katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja kwa kushirikiana na Hospitali ya CCBRT ya Tanzania Bara.

Uzinduzi wa jukwaa la NAWEZA wafana Jijini Mwanza

0
0
Kaimu Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Esther Mariki akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa jukwaa la mawasiliano ya afya kwa watu wazima liitwalo NAWEZA lililo chini ya mradi wa USAID TULONGE AFYA. Uzinduzi huo ulifanyika jana Machi 06, 2019 Jijini Mwanza, lengo likiwa ni kuhamasisha utekelezaji wa afya mbalimbali ili kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto chini ya miaka mitano. BMG Habari
Kaimu Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Esther Mariki akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa jukwaa la Naweza.
Kaimu Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Esther Mariki akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Emily Kasagara akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Ukumbusho wa picha na viongozi mbalimbali.
Tazama BMG Online TV hapa chini

Taxify kuanza kufahamika kwa jina la ‘Bolt’

0
0
KAMPUNI inayotoa huduma za usafirishaji Barani Afrika na Ulaya Taxify imebadilisha nembo na jina lake kuwa ‘Bolt’. 

Mabadiliko hayo ya alama ya utambulisho wa kampuni yamelenga kuenda sawia na malengo ya kampuni katika huduma za usafirishaji ambapo mpaka sasa tayari imepanua huduma za safari zake kwenye magari na pikipiki. 

Akizungumza na na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu mabadiliko hayo Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi mwenza wa Bolt, Markus Villig, alisema jina hilo jipya la Bolt litaanza kufahamika hatua kwa hatua katika masoko ya kimataifa katika wiki zijazo. 

Alisema Taxify ilizinduliwa miaka mitano iliyopita kwa malengo ya kutoa huduma za usafiri mijini kwa njia rahisi na bei nafuu. 

“Kampuni hiyo ya kiteknolojia kutoka Estonia imefanikiwa kukua na kuvuka mipaka tangu kuanzishwa kwake ambapo sasa imewafikia wateja milioni 25 katika nchi zaidi ya 30 duniani, na kuifanya kuwa kampuni inayoongoza barani Ulaya na Afrika. 

“Ilikuwa pia kampuni ya kwanza ya kurahisisha huduma za usafiri na kwa sasa inafanya kazi katika kupanua huduma ya usafiri wa pikpiki kwenye miji kadhaa ya Ulaya,” alisema. 

Aidha, Meneja Mkazi nchini Tanzania kutoka Bolt, Remmy Aseka alisema bidhaa ya kwanza ya kampuni hiyo ya usafirishaji ilikuwa ni kutoa suluhisho la kurahisisha upatikanaji wa huduma za teksi kwa wateja wake. 

"Tumefanikiwa kuongeza uboreshaji katika malengo yetu, tumeanza pia kukuza jina la kampuni yetu katika maeneo mbalimbali. Lengo letu ni kutatua matatizo ya usafiri kwa kiwango kikubwa zaidi, tunataka jina la kampuni liendane na mambo yajayo ya kampuni na sio yaliyopita. Jina jipya la 'Bolt' linamaanisha kufanya jitihada bila kutumia nguvu, hasa uzoefu wa kuzunguka katika mji kwa gari, pikipiki au usafiri wa umma. 

“Pia inaendana na matarajio yetu kuwa baadaye huduma za usafirishaji zitakuwa kwa njia ya umeme. Pia watumiaji wa Bolt hawatahitaji kufanya mabadiliko yoyote kwenye program zao kwa kuwa Bolt itajibadilisha moja kwa moja kwenye program hizo,” alisema.

Fundi Magari Mkazi wa Kimara King'ongo akabidhiwa fedha zake za Biko.

MKONGWE WA MUZIKI BOZI BOZIANA ‘MZEE BENZI' BADO YUMO

0
0
Na: Moshy Kiyungi
Machi 07, 2019. 

 Licha ya umri wake wa miaka wa miaka 67 hivi sasa, Bozi Boziana bado anao uwezo mkubwa wa kutunga na kuimba nyimbo za muziki wa dansi. Alijipatia umaarufu wakati akisikika akirap maneno ya “Nzawisaa, Nzawisaaa maama Nzawisaaa..Yelooh!!!..” kwenye nyimbo za bendi yake. 

 Majina yake halisi anaitwa Mbenzu Ngamboni Boskill, aliyezaliwa mwaka 1952 huko Jamhuri ya Kidemkokrasia ya Kongo. 

 Katika hatua za kutafuta mafanikio, Boziana alipitia katika bendi nyingi kubwa na ndogo nchini mwake zikiwa ni pamoja na Bamboula de Papa Noel, Minzoto Sangela, Zaiko Langa Langa, Isifi Lokole, Yoka Lokole, Langa Langa Stars na Choc Stars. 
 Baadhi ya wapenzi wakampachika jina bandia la ‘Mzee Benzi’ ambalo limekuwa maarufu. Katika kutafuta njia ya kujikwamua kimaisha, Bozi Boziana aliamua kuunda bendi yake ya Orchestra Anti-Choc, ambayo anaiongoza hadi sasa. 
 Licha ya utunzi na uimbaji, pia ni mkung’utaji mzuri wa gitaa na kulishambulia jukwaa akishirikiana na akina dada wawili Betty na Scolla Miell. Mzee Benzi alianzia muziki wa Afro-Pop katika bendi ya Air Marine. Lakini alianza kuyaona mafanikio ya kazi zake ilipotimu mwaka 1974 alipojiunga na bendi ya Zaiko Langa Langa, hivi sasa bendi hiyo inaongozwa na Nyoka Longo. 

 Zaiko LangaLanga ilikuwa na waimbaji mashuhuri wakati huo wakiongozwa na mkongwe Papa Wemba na mwezake Evoloko Jocker. Lakini haikuzidi mwaka, Papa Wemba na Evoloko waliondoka bendi hiyo baadae hata Bozi Boziana aliwafuata kwenda kuanzisha bendi mpya ikaitwa Isifi Lokole.


 “ Fahari wawili hawakai zizi moja” usemi huo ulijidhirisha baada ya wanamuziki hao kushindwa kukubaliana katika maswala mbalimbali ya msingi yaliyopelekea wanamuziki wake akina Papa Wemba, Boziana, Mavuela Somo na wengine kuondoka bendi ya Isifi Lokole. Walienda kuunda bendi yao mpya iliyopewa jina la Yoka Lokole. Bendi ya Yoka Lokole ilipata mafanikio makubwa mwaka 1976, japokuwa ilipotimu mwinshoni mwa mwaka huo, Papa Wemba aliiacha bendi hiyo, akaenda kuanzisha bendi ya Viva la Musica. 


 Bozi Boziana mwaka 1977 naye aliicha bendi hiyo ya Yoka Lokole, licha ya bendi hiyo kuwa maarufu kwa kipindi kifupi. Kwa miezi michache Boziana alishirikiana na mwanamuziki Efonge Gina, ambaye naye alikuwa katika bendi ya Zaiko Langa Langa. Walirekodi nyimbo kadhaa kama vile Selemani iliyotungwa na Bozi Boziana na Libanko Ya Ngai utunzi wake Gina. Mwanamuziki aliyekuwa na uwezo mkubwa wa fedha Kiamuangana Mateta ‘Verkies’ mwaka 1981, aliibadilisha bendi ya Soukous SuperGgroup na kuita Langa Langa Stars. 

Bendi hiyo ilikuwa imesheheni vipaji vya wanamuziki kaiwemo Evoloko Jocker, Dindo Yogo na wnengine wengi. Bozi Biziana aliakwa kujiunga vijana hao naye akaubali na kuicha Zaiko Langa kwa mara ya pili. Langa Langa Stars ilidumu kwa miaka michache iliyofuatia kabla na Boziana naye akaondoka kwenda kujiunga na bendi kubwa nchini humo ya Choc Stars, aliyokuwa chini Ben Nyamabo ambako alipiga hadi mwezi Novemba 1985. Akiwa na bendi hiyo ya Choc Stars, Boziana alirekodi baadhi ya nyimbo ambazo zilikuja kuwa maarufu za Sandu Kotti, Alena, Mbuta-Mutu na Retrouvailles a Paris. 

Choc ilikuwa na wanamuziki wengi wenye vipaji lukuki wakiwemo akina Fifi Mofude, Djo Nolo, Koffi Alibaba, Wally Ngonda, Rigo Star, Ngouma Lokito, Deesse Mukangi, Marthe Lamugenia, Ngimbi Yespe na Maoussi Solange. Mpiga gita wa kwanza katika bendi hiyo alikuwa Matou Samuel ambaye kwa sasa anaimba muziki wa Injili na nafasi yake ilishikwa na Dodoly ambaye kabla ya kujiunga humo alitokea katika bendi ya mwanamuziki Lita Bembo ya Orchestre Stukas. Dodoly alipachikwa jina bandia la ‘The sewing machine’ kwa umahiri wake wa kutumia vidole vyake kucharaza nyuzi kwa kasi kubwa. 

 Tokea miaka ya 1980 Boziana aliendelea katika bendi yake ya Anti-Choc ikiwa ni pamoja na kurekodi nyimbo akishirikiana na wanamuziki wengine mahiri. Boziana aliwahi kushinda zawadi ya Kora All-African kwa album yake kuwa bora toka nchi za Afrika ya Kati. Wapenzi wa muziki hapa nchini watamkumbuka Bozi jinsi alivyoziteka nyioyo za wapenzi katika maonesho kadhaa aliyoyafanya hapa nchini. 

 Alifanya maonesho kadhaa akishirikiana na wasanii wake wa kike Deesse Mukangi na Joly Detta walivyokuwa wakiimba na kulishambulia jukwaa kwa mtindo wao wa ‘Nzawisa’ katika nyimbo za Tembe na Tembe, Palpitation na zingine nyingi zilifanya watu kuviacha viti vyao kwenda kuwatuza. Bozi Boziana mwenye sauti nzuri yakupendeza, kuna kipindi alibadili dini yake na kuwa muislamu, akapewa jina la Abubakar. 

 Baadhi ya nyimbo alizowahi kufyatua ni pamoja na Masumu Akey, Ba Bokilo, Fiko Fikolo, Chama Chiko, Mya , Ka Munu Ve’ , Mifune, Popy Bopase ya mwaka 1998 na Tembe na Tembe. Zingine ni Bana DRC, Riana, Anytha, Sonto ya 1989, Makambo Evelyne ya mwaka 1989, Pot Pourri , Mfumu na Alena. 

Bozi alachia vibao vingine vya Sisina, Doukoure, Switzerland, Wakamba, Mansanga na Betlem. Bozi alifyatua vibao vingi vilivyompa sifa nyingi ukiwemo wa La reine de Sabah, Lelo Makambo Lobi na Fleur de Lys ambazo alimshirikisha mwimbaji wa kike Joly Delta. 

 Watanzania watamkumbuka alivyofanya mambo makubwa katika muziki kwa mara ya mwisho alipokuja humu nchini kwa mwaliko wa Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) iliyo chini ya uongozi wa Mkurugenzi Asha Baraka. 



 Mwandishi wa makala hii anapatikana 
kwa namba: 0784331200, 0713331200 na 0767331200

Uunganishwaji Mamlaka Ndogo za Maji Kupunguza Changamoto za Utendaji Kazi

0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Uunganishwaji wa Mamlaka ndogo za maji zilizopo katika miji midogo nchini kwa nia ya kuhudumiwa na Mamlaka za Maji za Mikoa husika unategemewa kupunguza changamoto za utendaji kazi zinazotokea katika maeneo hayo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa wakati akifungua mkutano wa Wadau wa Maji nchini unaolenga kuwaelimisha wadau hao kuhusu uanzishwaji wa Wakala wa Maji Vijijini. 
Prof. Mbarawa amesema kuwa katika Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira kuna kitu kinaitwa ‘Cluster’ ambapo Mamlaka za Maji za Mikoa zitasimamia Mamlaka ndogo ndogo zilizopo chini ya mkoa husika hali itakayosaidia upatikanaji wa huduma za maji Mijini na Vijijini kuwa sawa.
“Kwa vile sheria imeruhusu uunganishwaji huo, Mamlaka za Maji zinaweza kujitanua, kufanya biashara nzuri, kuongeza kipato na kupunguza changamoto za utendaji kwa sababu baadhi ya maeneo yamewekwa mitambo mikubwa lakini Mamlaka husika ni ndogo haziwezi kuendesha kazi hizo,” alisema Prof. Mbarawa.
Vile vile ametoa rai kwa mamlaka hizo kutojiweka mijini pekee na badala yake zijikite zaidi katika kuongeza kasi ya utoaji huduma za maji hata nje ya miji husika.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema kuwa pamoja na jitihada kubwa za kuanzisha Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) utendaji kazi wake ni kitu kingine hivyo, watendaji wanatakiwa kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa ya kupeleka huduma za maji vijijini yanatekelezeka.
“Ili kuhakikisha huduma za maji zinafika katika maeneo husika, wataalam wa sekta ya maji lazima tubadilike kuhusu suala la kuandaa miradi kwani Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuhakikisha wananchi hasa wa vijijini wanapata maji lakini miradi inamalizika na maji hayatoki, hilo sio jambo zuri na sio mpango wa Serikali,” alisema Aweso.
Aidha, Aweso ametoa rai kwa wadau wa sekta hiyo kuchagua wakandarasi wenye uwezo wa kutekeleza miradi na kuikamilisha kama ilivyopangwa ili kuhakikisha fedha za Serikali zinatumika ipasavyo na wananchi wanapata huduma iliyokusudiwa.
Mkutano huo umehusisha wadau wa sekta ya maji wakiwemo watumishi kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), Mabonde ya Maji, Wakala wa Uchimbaji Visima, Mfuko wa Maji pamoja na Chuo cha Maji.
  Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa akizungumza leo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa Wadau wa Maji nchini unaolenga kuwaelimisha wadau hao kuhusu uanzishwaji wa Wakala wa Maji Vijijini. 
 Baadhi ya Wadau wa Maji wakimsikiliza Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati akifungua kikao hicho.
 Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa na baadhi ya Wenyeviti wa Bodi za Mamlaka za Maji wakisainishana mkataba wa utendaji kazi utakaosaidia kuimarisha usimamizi wa sekta ya maji katika ngazi mbalimbali nchini mara baada ya kufungua kikao hicho. Mikataba hiyo itakua ikipimwa na Wizara husika kila mwaka.
Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya maji mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa Maji nchini unaolenga kuwaelimisha wadau hao kuhusu uanzishwaji wa Wakala wa Maji Vijijini. 

SERIKALI YAAGIZA KUHAMISHWA KWA DAMPO LA KIHESA KILOLO

0
0
Na Lulu Mussa, Iringa
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima ameagiza kuhamishwa kwa dampo la Kihesa Kilolo lililopo katika Kata ya Kihesa Manispaa ya Iringa kutokana na kuwepo katika mazingira yasiyo rasmi. 
Agizo hilo limetolewa hii leo Mkoani Iringa mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kukagua namna bora ya kuteketeza taka bila kuathiri mazingira  na kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesela kusimamia maelekezo hayo mapema iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na kuteketeza taka zilizozagaa katika eneo hilo na kuweka katazo la watu kuingia katika dampo kwa lengo la kuokota chupa za plastiki kwa ajili ya kuziuza. 
Akiwa katika eneo hilo la dampo la Kihesa Kilolo Naibu Waziri Sima ameshuhudia maji machafu yakitiririka kutoka katika dampo hilo na kwenda kwenye makazi ya watu jambo ambalo linahatarisha afya za wakazi wa maeneo ya jirani pamoja na tishio la mlipuko wa magonjwa.
Akitoa msimamo wa Serikali Naibu Waziri Mussa Sima ameagiza kwa hatua za haraka kuwekwa utaratibu wa  kudhibiti maji yanayotiririka kutoka katika dampo kwa kujenga mifereji ili kunusuru ikolojia ya vyanzo vya maji katika maeneo hayo.
“Ndugu zangu hali ni mbaya sana katika dampo hili, simamieni uteketezaji wa taka mapema iwezekanavyo, Serikali haiwezi kuvumilia vitendo vya namna hii, wananchi wanalipia gharama za ubebaji wa taka, zinaletwa dampo kisha mnaruhusu tena wananchi kuingia dampo, kwa maana nyingine tunakusanya taka katika mitaa na kuzirudisha tena katika mitaa, hii haikubakiki ” Sima alisisitiza.
Naibu Waziri Sima pia ameagiza eneo lililotengwa na Manispaa kwa matumizi ya dampo lililopo katika Kijiji cha Mkoga, Kata ya Isakalilo lenye ukubwa wa ekari Ishirini na tano kufanyiwa Tathmini ya Athari kwa mazingira kabla ya kuanza kutumiwa, sambamba na kulipa fidia wakazi wa maeneo hayo
Wakati huo huo, Naibu Waziri Sima pia amemuagiza Mratibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kanda za Nyanda za juu kusini Bw. Godlove Mwamsojo kuhakikisha anafuatilia utekelezaji wa agizo hilo na endapo Halmashauri haitatekeleza kwa kipindi walichokubaliana hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao . 
Nae Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Mazingira ya Uteketezaji wa taka gumu Bw. Christian Ndenga amekiri kuwa kwa takribani mwezi mmoja taka katika dampo hilo hazijateketezwa kutokana na sababu za kuharibika kwa ‘kijiko – Wheel loader’.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesela amesema kuwa takriban tani 108 huzalishwa kwa siku katika Manispaa ya Iringa, na kuahidi kusimamia zoezi la kuteketeza taka zilizopo na kuhamisha dampo ndani ya wiki mbili ikiwa ni utekelezaji wa maagizo.
Naibu Waziri Mussa Sima yuko katika ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yenye changamoto za kimazingira hususan katika sekta ya afya na udhibiti wa taka ngumu pamoja ikolojia ya vyanzo vya maji vinavyo changia maji katika bonde la Rufiji.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (katikati) akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesela (Kulia) na Bi. Ritha Kabati Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Iringa mara baada ya kutembelea dampo la Kihesa Kilolo lilipo katika Kata ya Kihesa Manispaa ya Iringa
Sehemu ya dampo la Kihesa Kilolo kama linavyoonekana pichani, taka hazijateketezwa kwa kipindi kirefu na halina uzio wowote. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mussa Sima ametoa muda wa wiki mbili kuhakikisha eneo lote linasafishwa ili kuepuka mlipuko wa magonjwa na kulinda ikolojia ya vyanzo vya maji.

TUSIMSAHAU DR. REMY ONGALA

0
0
Kama kuna mwanamuziki ambaye hawezi kusahaulika katika kumbukumbu za wapenda muziki, ni Dk. Remmy Ongalla.

Desemba 13, 2018 alitimiza miaka minane tangu aiage dunia, baada ya kufariki dunia usiku wa kuamkia Jumatatu Desemba 13, 2010 nyumbani kwake Sinza, jijini Dar es Salaam.

Ilikuwa ni siku ya majonzi kwa wapenzi wa muziki wa dansi hapa Tanzania, Afrika ya Mashariki na Ulimwenguni kwa ujumla baada ya kusikika kwa kifo chake.

Kifo cha Dk. Remmy kiliwaacha wapenzi wake na wananchi kwa ujumla katika dimbwi la majonzi yasiyosahaulika kufuatia tungo za nyimbo zake zenye maudhui maridhawa, ambazo hadi leo zinarindima katika vituo vingi vya redio hapa nchini hata nje ya mipaka yetu.

Yapo mambo kadhaa aliyoyafanya ambayo yanasababisha watu wengi kutokumsahau nguli huyu.

Dk. Remmy alikuwa wa kwanza kupata ujasiri wa kukemea ngono zembe, akatunga wimbo ‘Mambo kwa soksi’ Lakini jamii ikambeza kwamba wimbo huo haukuwa na maadili mema. Baadaye  viongozi wa serikali, vyama na dini na wengine kwa ujumla walielewa nini alichokuwa akisema Dk. Remmy, wakaanza kuhubiri majukwaani tahadhari hiyo.

Alijipatia umaarufu katika jiji la Dar es Salaam hususan maeneo ya Sinza, kufuatia gari lake dogo ‘soloon’ ambalo popote lipitapo watu walilishangaa. Lilikiwa na maandishi nyuma ya gari hilo yakisema ‘ Baba yako analo’?

Historia ya maisha ya Dk.Remmy Ongala yaelezwa kwamba mara alipozaliwa, wazazi  wake walimuita Ramadhani Mtoro Ongala. Majina yake kamili alikuwa akiitwa Ramadhan Mtoro Ongala. Alizaliwa mwaka 1947 katika mkoa wa Kivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Familia yake iliishi katika eneo lililoitwa Kindu eneo ambalo halikuwa mbali sana kutoka mpakani na Tanzania.

Baba yake alikuwa ni mwanamuziki mashuhuri pia alikuwa mpiga ngoma kwa kutumia mkono na pia mbira. Baada ya kuzaliwa kwake haikuchukua muda mrefu familia yake ilihamia katika mji wa Kisangani huko DRC.

Ipo habari kwamba kabla ya kuzaliwa kwake, mama yake alipata ujauzito mara mbili lakini kwa bahati mbaya kila alipojifungua, mtoto alifariki. Alipopata ujauzito mara ya tatu alienda kwa mganga wa kienyeji kumuomba ushauri afanye nini ili mtoto atakayezaliwa asiiage dunia pia.

Bila kusita mganga wa kienyeji akampa ushauri wake. Akamwambia kwanza safari hii asiende kujifungulia hospitali bali akajifungulie maporini. Pia alipewa ushauri kwamba mtoto akishazaliwa asije akamkata nywele zake. Yote hayo yalitendeka.

Ramadhan Mtoro Ongalla akazaliwa akiwa na meno mawili ya mbele kinywani mwake  na akaonekana kana kwamba ni  mtoto wa ajabu.

Pia inasemekana Remmy alizaliwa akiwa tayari na meno mawili ya mbele, akaonekana kama mtoto wa ajabu.

Kuzaliwa akiwa hivyo ikachukuliwa kama ishara ya baadaye kuja kuwa mganga wa kienyeji .

Ili kutimiza maelekezo ya mganga, Dk. Remmy hakuwahi kunyolewa nywele zake kwa miaka yote hadi alipokuja kuokoka akiwa hapa nchini Tanzania.

Mwenyewe aliwahi kusema kwamba mwanzoni alikuwa anajisikia aibu sana kwa kuwa na nywele ndefu namna ile. Lakini baadaye jina na taswira ya mfalme wa reggae ulimwenguni, hayati Bob Marley lilipopata umaarufu nchini Kongo, ndipo alipoipenda staili ile ya nywele kwani hata watu wengine pia walianza kuikubali na kuionea fahari.

Ingawa utabiri huo haukutimia, inasemekana huo ndio mwanzo wa yeye kujulikana hapo baadaye kama Doctor Remmy Ongalla.

Baba yake ndiye aliyeanza kumfunza mambo ya muziki tangia akiwa mdogo kabisa. Jambo lililomfanya aamini kabisa kwamba kama jinsi ambavyo watu wengine wamezaliwa kuwa madaktari, wanasheria, waalimu, wakulima nk, yeye alizaliwa ili awe mwanamuziki.
Kwa bahati mbaya baba yake huyo alifariki dunia mwaka 1963, akamuacha Remmy akiwa na miaka sita.

Baadaye alianza shule ya msingi, lakini kutokana na ukosefu wa fedha na kwa sababu mama yake hakuweza kuendelea kumlipia karo za shule, Remmy ilibidi aache masomo shuleni hapo.

Ilipofika miaka ya 1960, Remmy tayari alikuwa ameshafuzu kupiga gitaa.

Mwaka mmoja baada ya kifo cha Baba yake mzazi, mwaka uliofuatia wa 1964 ulikuwa si mzuri tena kwa Remmy. Alkipata pigo la kufiwa na mama yake mzazi jambo ambalo lilimuacha Remmy na mzigo wa kuwalea wadogo zake kwani yeye sasa ndio alikuwa mkubwa katika familia licha ya umri wake mdogo.

Bila elimu na ujuzi mwingine wowote, alilazimika kuanza rasmi kujitafutia riziki kupitia muziki. Ujuzi wake wa kupiga gitaa uliongezeka kwa kasi ya ajabu kitu ambacho kilimuwezesha kutumbuiza kwa kupiga ngoma na gitaa katika hoteli na sehemu mbalimbali nchini ya Kongo akiwa na kundi lake likiwa limesheheni vijana wenzake lililoitwa ‘Bantu Success’.

Kwa miongo kadhaa iliyofuatia Dk. Remmy Ongala alizunguka katika sehemu mbalimbali za Kongo akiambatana na bendi kadhaa maarufu za wakati huo nchini Kongo zikiwemo Success Muachana na ile ya Grand Mickey Jazz nchini Uganda.

Japokuwa kwa ujumla Dk. Remmy alijifunza mwenyewe kupiga gitaa, lakini aliwahi kukiri kwamba muziki wa kutoka nchini Cuba ambao wakati huo ulikuwa unaanza kujipatia umaarufu barani Afrika, ulimsaidia katika kupata staili ya pekee katika upigaji gitaa.
Kwa upande wa uimbaji anasema uimbaji wa Joseph Kabasele ‘Grand Kale’ na ule  wa Franco Lwambo Makiadi ulimsaidia kupata staili yake ya uimbaji kama tulivyoizoea kusikia enzi za uhai wake.

Mwaka 1978 Remmy aliingia jijini Dar es Salaam baada ya kuitwa na mjomba wake mzee Kitenzogu Makassy  ili aje ajiunge na bendi maarufu ya wakati huo ya Orchestra Makassy, iliyokuwa chini ya uongozi wa mjomba wake huyo.

Huo ukawa ndiyo mwanzo wa maisha ya Dk. Remmy nchini Tanzania. Akiwa na bendi ya Orchestra Makassy, alitunga wimbo wake wa kwanza uliojulikana kama ‘Siku ya Kufa’, wimbo ambao aliuandika kumkumbuka rafiki yake aliyefariki. Wimbo huo ulianza kumpatia umaarufu mkubwa na kujulikana kwa haraka hapa nchini.

Hata hivyo mzee Makassy  aliamua kuihamishia bendi yake keipeleka nchini Kenya, kitendo hicho cha mjomba wake kilichomfanya Dk. Remmy  kujiunga na bendi ya Matimila baada ya kudumu kwa katika bendi ya Orchestra Makassy kwa takriban miaka mitatu hivi.

Jina la bendi hiyo ya  Matimila lilitokana na jina la kijiji kimoja kilichoko kusini mwa Tanzania. Kujiunga kwa Remmy katika  bendi ya Matimila, alijiongezea umaarufu katika anga za muziki nchini Tanzania wakati huo.

Chini ya uongozi wake Dk. Remmy aliisuka upya bendi hiyo na kuibadilisha  jina ikaitwa Orchestra  Super Matimila.

Miaka iliyofuatia Watanzania tulishuhudia umaarufu wa Remmy ukiongezeka hususan kutokana na mashairi ya nyimbo zake ambayo yaliegemea katika kuzungumzia mambo halisi ya kijamii kama vile umasikini, afya, siasa , majanga ya Ukimwi nk.

Mafanikio ya Remmy na kundi lake zima la Orchestra Super Matimila hayakuishia nchini Tanzania kwani katika miaka ya mwishoni ya 1980 walianza kujipatia umaarufu nje ya mipaka ya Tanzania na Afrika.

Dk.Remmy Ongala aliwahi kusema kwamba kupata mialiko ya nje lilikuja kama mchezo tu. Kasseti yenye nyimbo zao rafiki yake mmoja mzungu aliyekuwa akiondoka nchini Tanzania kurejea kwao Uingereza.

Rafiki yake huyo alipofika huko aliwapatia jamaa wa WOMAD (World of Music, Arts and Dance) shirika linalopandisha chati wanamuziki na wasanii mbalimbali kutoka katika nchi za dunia ya tatu. WOMAD  walivutiwa na nyimbo zao, hivyo kuwapa mwaliko kushiriki katika maonyesho yao barani Ulaya ya mwaka 1988.
Baada ya kurudi kutoka Ulaya bendi ya Super Matimila ilitoa album yenye jina la ‘Nalilia Mwana’ ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo zao zilikuwemo nyimbo zilizopendwa sana kama vile ‘Ndumila Kuwili’ na ‘Mnyonge Hana Haki’

Mwaka 1989 Remmy na Matimila walirudi tena Ulaya kufuatia mwaliko mwingine wa WOMAD. Ni wakati huo huo ambapo walipata nafasi ya kurekodi kwenye studio ya kisasa zaidi ya Stud Real World Studios, ambayo ilikuwa inamilikiwa na mwanamuziki maarufu aitwaye Peter Gabriel.

Dk. Remmy aliwahi kufafanua kuwa wimbo maarufu ya ‘Kipenda roho’ aliuimba mahsusi kwa ajili ya mkewe ambaye ni ‘mzungu’ muingereza ambaye wakati huo tayari walikuwa wameshazaa naye watoto watatu.

Mwaka 1990, Remmy na bendi yake ya Super Matimila walirejea tena katika studio za Real World ambako walirekodi album nyingine yenye nembo ya ‘Mambo’ ambayo ilikuwa na nyimbo kama hiyo ya ‘Mambo’ ambayo aliimba kwa lugha ya kiingereza na kuweza kukidhi kiu ya wapenzi wake wasiojua Kiswahili. Zingine ni pamoja na ‘No money, no life’ na ‘One World’.

Umaarufu wake ulizidi kung’ara mwaka 1990 alipotoa wimbo wa ‘Mambo kwa soksi’ ingawa baadhi ya watu waliupinga kwa kusema kwamba haukuwa na maadili mema kwa jamii, ingawa kimsingi alikuwa anawaasa watu hususani vijana kutumia kondomu ili kuepukana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

Akiwa Super Matimila Dk. Remmy alitoka na nyimbo nyingi zikiwemo za ‘Bibi wa mwenziyo’, ‘Kipenda roho’, ‘Asili ya muziki’ na ‘Ngalula’. Zingine  ni pamoja na ‘Mwanza’, ‘Mama nalia’, ‘Harusi’, ‘Hamisa’, ‘Mnyonge hana haki’, ‘Ndumila kuwili’ na ‘Mataka yote’ ambazo zilimuongezea sifa kubwa Dk. Remmy kufuatia maudhui yaliyokuwa yakikidhi jamii.

Baadaye Dk. Remmy Ongala akaanza kusumbuliwa na maradhi ya kisukari iliyompelekea kuamua kuachana na muziki wa dansi kwa madai ya kwamba umejaa mambo mengi ya kishetani. Remmy akaokoka, akatubudu dhambi zake na akaanza kupiga muziki akimuimbia bwana.

Kabla ya kifo chake Dk. Remmy alitoa albamu yake ya Injili aliyooiita ‘Kwa Yesu kuna furaha’. Remmy alikuwa katika hatua  za mwisho za kukamilisha albamu yake ya pili, lakini mungu akampenda sana usiku wa kuamkia Jumatatu ya Desemba 13, 2010 nyumbani kwake Sinza. Eneo hilo alilokuwa akiishi lilipewa jina la ‘Sinza kwa Remmy’ kufuatia umaarufu wake alipokuwa hai.

Mungu aiweke roho yake pahala pema peponi, Amina.
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba: 0784331200, 0736331200, 0767331200 na 0713331200.

MAJALIWA AKUTANA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapindunzi  ya Zanzibar, Balozi Seif Iddi kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Machi 7, 2019
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapindunzi  ya Zanzibar, Balozi Seif Iddi kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Machi 7, 2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Iddi, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Machi 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BREAKING NEWZZZZ BAADA YA SIKU 96 LUPANGO MBOWE, MATIKO WARUDI URAIANI

0
0
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua maamuzi ya kufutiwa dhamana yaliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuamuru warufani hao Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai  Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini kwa tiketi ya chama hicho Esther Matiko waachiwe huru mara moja.

Aidha imeondoa baadhi ya masharti ya dhamana zao  ikiwemo kuripoti kila wiki kwa Kamishina wa Polisi Mkoa na badala yake wametakiwa kuripoti kila mwisho wa  mwezi Mhakama ya Kisutu.

Pia imewaamuru washitakiwa kutokusafiri nje ya Tanzania bila kibali cha mahakama na kwamba masharti mengine yaliyokuwepo Kisutu yataendelea kubaki kama ilivyo.

AFRICAN WILDLIFE FOUNDATION YASEMA TANZANIA INASHIKA NAMBA MOJA KWA KUWA NA SIMBA WENGI BARANI AFRIKA

0
0
 Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania, wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation Kaddu Sebunya (kushoto).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation Kaddu Sebunya akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa nchi za Afrika kuweka mikakati itakayosaidia kulinda uhifadhi wa mazingira na wanyamapori.





*Yapongeza juhudi za Serikali katika kukomesha ujangili

*Yazishauri nchi za Afrika kulinda na kuhifadhi wanyamapori


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

AFRICAN Wildlife Foundation imesema Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na Simba wengi na kwa upande wa Tembo inashika nafasi ya tatu barani Afrika.

Imesema hiyo inatoka na juhudi ambazo zinafanywa na Serikali ya Tanzania kuhakikisha wanyamapori na uhifadhi wa misitu unapewa kipaumbele.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation Kaddu Sebunya wakati akizungmzia umuhimu wa uhifadhi wa wanyamapori na uhifadhi wa mazingira kwa nchi za Bara la Afrika.

"Serikali ya Tanzania ni mfano wa kuigwa katika eneo hilo la uhifadhi wa misitu na utunzaji wa wanyamapori. Hii imefanya katika nchi za Bara la Afrika ,Tanzania kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa na Simba wengi na na inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na tembo wengi. Nchi inayoongoza kwa kuwa na tembo wengi ni Botswana ikifuatiwa na Zimbabwe,"amesema Sebunya.

Amesisitiza ni muhimu wa kila nchi barani Afrika kuweka mikakati itakayosaidia maliasili zilizopo kutunzwa na kulindwa vema huku akieleza kwa sasa kuna changamoto ya wanyamapori wengi hasa Simba na Tembo kupungua.

"Ukweli Simba na Tembo wameendelea kupungua barani Afrika na sababu yake ni uwepo wa majangiri na uwindaji haramu.Hivyo African Wildlife Foundation tunahamasisha kila nchi kuweka mipango ambayo itasaidia kuwafanya Simba na Tembo waendelee kuwepo,"amesema.

Amesema kila nchi ikiamua hakuna ambacho kitashindikana ambapo ametoa mfano kwa Serikali ya Awamu ya Tano namna ilivyofanikiwa kudhibiti majangiri ukilinganisha na miaka ya nyuma.

"Katika hili la kulinda wanyamapori na uhifadhi kila nchi ikiamua inaweza.Niitolee mfano Tanzania miaka ya nyuma Tembo walikuwa wanauliwa sana lakini leo hii tembo hao hao wako salama kutokana na hatua ambazo Serikali inachukua,"amesisitiza.

Sebunya amesema watu wa Bara la Afrika wana maisha yao na tamaduni zao ambazo kimsingi zilizingatia uhifadhi wa misitu, mapori na wanyama lakini kadri siku zinavyokwenda na kuingia kwa tamaduni za nchi nyingine kumesababisha kuibuka kwa changamoto ambazo iko haja ya kuzikabili.

"Katika nchi nyingi sana barani Afrika nusu ya wanyama walikuwa siku za nyuma leo hawapo.Hivyo tutaendelea kuzihamasisha nchi za Afrika kuweka kipaumbele katika eneo hilo.

"African Wildlife tumekuwa tukifanya jitihada za kuhamasisha wadau kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wanyama.Ndio maana hata kile Chuo cha Mwika ni sehemu ya mchango wetu. Watalaamu wengi uhifadhi wa mazingira , misitu na wanyamapori waliopo barani Afrika wamepikwa katika chuo hicho,"amesema Sebunya.

Wakati huo huo Sebunya amesema kadri nchi zinapofanya maendeleo ni vema pia zikazingatia utunzaji wa mazingira."Nchi za Afrika zinahitaji kuwa na maendeleo na wakati huo huo zinapaswa kulinda mazingira.Ni mambo mawili yanayokwenda kwa pamoja,"amesema Sebunya.

Wananchi Waongezewa Maarifa Matumizi ya Ardhi


KCB BANK TANZANIA YAFANYA KONGAMANO LA KIBIASHARA JIJINI ARUSHA

0
0

Benki ya KCB Tanzania imefanya kongamano la kwanza ya Biashara Club kwa mwaka 2019 jijini Arusha baada ya kuandaa kongamano kama hilo jijini Mwanza mwishoni kwa mwaka 2018. 

Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi, KCB Biashara Club pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao kwa kuwakutanisha na wafanyabiashara wa nje na ndani ya nchi.

Tangu kuzinduliwa kwake, KCB Biashara Club imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara  kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara.

Kongamano hilo lilikuwa na lengo mahususi la kukutanisha wadau mbali mbali katika sekta ya utalii wakiwemo wafanyabiashara na lilifanyika katika sehemu mbili ambapo sehemu yakwanza ilikuwa mahususi kwa wateja wa Benki ya KCB wapatao 250, huku sehemu ya pili ikiwa ni jukwaa la wazi kwa wakazi wengine wa Arusha kupata elimu ya huduma za kibenki kutoka kwa wataalam wa Benki ya KCB.

Akiongea wakati wa kufungua kongamano hilo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Christine Manyenye alisema Benki ya KCB imefanya juhudi za mahususi za kuwaleta wadau kama Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.

 Kwa upande wake Meneja wa Tawi, Benki ya KCB Arusha, Judith Lubuva aliwapongeza wafanya biashara, wadau na wakazi wa Arusha kwa kuhudhuria kongamano. Aliongeza kwamba kongamano hilo limefanyika kwa wakati muafaka ambapo sekta ya utalii inaendelea kuimarika katika kanda ya kaskazini na Tanzania kwa ujumla.

Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabishara Wadogo na wa Kati (SME)  Abdul Juma aligusia fursa tofauti zinazoletwa na Biashara Club zikiwemo kuwakutanisha wafanya biashara mbali mbali wa nje na ndani ya nchi, kupanua wigo wa masoko kupitia safari za pamoja kwenda nchi kama China, Malaysia na Afrika Kusini. 

Juma aliwahakikishia wadau kwamba KCB Bank ina dhamira ya kuinua sekta ya utalii kwa kuitambulisha Tour Operator Account inayowezesha malipo ya kieletroniki pamoja na kuwana faida zingine zikiwemo huduma kwa njia ya mtandao kuwa bure na kutoa pesa bure.

Akiongea katika warsha hiyo, mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA), Ombeni Urio aliyekuwa mshauri wa masuala ya kodi, alisisitiza umuhimu wa wafanya biashara hao kufuata kanuni za kodi. Aliipongeza Benki ya KCB kwa kumualika ili aweze kutoa elimu hiyo ambayo ilikuwa inahitajika kwa sana.

 Mkuu wa Idara ya Masoko na Mahusaino Christine Manyenye akijibu maswali kutoka kwa wafanya biashara wa jijini Arusha katika kongamano lililohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 ikiwajumuisha wadau mbali mbali kutoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
 Afisa Masoko wa TANAPA  Ernest Jackinda akiongea na wageni waalikwa katika warsha ya Biashara Club iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Masuala ya Kibenki Masika Mukule akiongea na wageni waalikwa wakati wa maongezi ya ana kwa ana katika warsha ya Biashara Club iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.

Je, Arsenal na Chelsea wataharibu sherehe ya wahispania kwenye Europa?

0
0
Timu kutoka Uhispania zimepata mafanikio makubwa kwenye ligi ya Europa miaka ya hivi karibuni, lakini msimu huu wanakutana na changamoto kutoka kwa timu za ligi ya Uingereza, Arsenal pamoja na Chelsea ambazo zimefuzu kuingia hatua ya  16 bora. Kwa misimu saba iliyopita, timu za La Liga zimeshinda Kombe hilo mara tano, huku Sevilla wakishinda mara tatu mfululizo (2014, 2015 na 2016), wakati Atletico Madrid walishinda mwaka 2012 na 2018.

Timu pekee ambazo ziliingilia kati katika kipindi hicho ni Chelsea (2013) na Manchester United (2017). Usiku wa leo zitachezwa mechi za kwanza za hatua ya 16 bora ambapo timu za Chelsea na Arsenal zinategemewa kufuzu kwenda hatua inayofata. Chelsea watakuwa nyumbani dhidi ya Dynamo Kyiv, timu ambayo imeshiriki mara kwa muda mrefu sana katika mashindano makubwa ya Ulaya, wameshiriki mfululizo tangu  msimu wa 1989/90.
Mahasimu wa Chelsea, Arsenal wana kocha ambaye anajua nini kinahitajika ili kushinda Kombe hilo. Unai Emery ambaye aliwaongoza Sevilla kushinda mara tatu mfululizo.

‘Washika Bunduki’ watakuwa ugenini kwa Rennes kucheza mchezo wa kwanza – Naye kiungo wa timu hiyo Grani Xhaka alisema wamejipanga kufanya vizuri. “Ukishinda Europa League unaenda moja kwa moja kwenye Champions League. Lakini bado naamini Premier League ni nafasi yetu nzuri kufikia Ligi ya mabingwa.” Sevilla (vs Slavia Prague) na Valencia (vs Krasnodar) wataanza safari ya kuitafuta robo fainali wakiwa nyumbani huku Villarreal watasafiri takriban kilomita 4000 kuwafata Zenit St Petersburg.

Ligi ya Serie A inawakilishwa na Napoli pamoja na Inter Milan ambao nao wana nafasi ya kufanya vizuri. Napoli wanacheza dhidi ya Red Bull Salzburg huku Inter wakianzia ugenini kwa Frankfurt. Mchezo wa Chelsea dhidi ya Dynamo Kyiv utachezwa saa 5:00 Usiku na ule Arsenal vs Stade de Rennais FC ni saa 2:55 Usiku. Zote mbili zitaonyeshwa Mubashara kupitia chaneli ya ST World Football HD Michezo mingine ya Europa kama Inter vs Frankfurt na Napoli vs RB Salzburg itaonyeshwa kupitia chaneli za michezo za StarTimes, Sports Focus HD, Sports Premium HD, Sports Arena HD na Sport Life HD.

Wamiliki wa vyombo vya usafiri washauriwa kuchangamkia fursa Dodoma

0
0
Wamiliki wa vyombo vya usafiri jijini Dodoma, wameshauriwa kuchangamkia fursa ya kutoa huduma ya usafiri kutoka maeneo  mbalimbali ya jiji hilo kuelekea mji wa serikali ambako ofisi za serikali zinajengwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi na wadau wa serikali.
Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi yake katika mji wa serikali, Ihumwa ambayo iko kwenye hatua za mwisho kukamilika kwa ajili ya kutoa huduma.

Mhe. Mkuchika amesema, ofisi yake itaanza kutoa huduma siku chache zijazo, hivyo uwepo wa huduma ya usafiri ni muhimu sana, kwani itawawezesha wananchi kufika kwa urahisi kupata huduma ikiwa ni pamoja na kuwarahisishia watumishi wa ofisi yake na taasisi nyingine kufika kwa wakati katika maeneo yao ya kazi.

Aidha, Mhe. Mkuchika amezitaka taasisi zote za umma zinazojenga ofisi katika mji wa serikali, kuishirikisha Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) ili kupata ushauri wa kitaalamu wa namna bora ya kujenga miundo mbinu rafiki ya TEHAMA itakoyorahisisha utoaji huduma kwa umma.  “Ni vema, taasisi zinazojenga ofisi katika mji wa serikali kuomba ushauri wa kitaalamu wa usimikaji wa miundombinu ya TEHAMA kabla ya kukamilisha ujenzi ili kuziwezesha taasisi hizo kuwa na mifumo ya TEHAMA ya utoaji huduma ya uhakika,” Mhe. Mkuchika amesisitiza.

Mhe. Mkuchika ameipongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa hatua nzuri ya ujenzi iliyofikiwa na Menejimenti ya ofisi yake kwa usimamizi mzuri.  Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameridhishwa na ujenzi wa ofisi hiyo kwani umezingatia mahitaji muhimu ya kundi maalum kwa kuweka miundombinu rafiki itakayowawezesha wananchi wenye ulemavu wa miguu kupata huduma bila kikwazo.

Pia, Dkt. Mwanjelwa amesema, ofisi yake imedhamiria kuwa ya kwanza kutoa huduma katika mji wa serikali kama ilivyokuwa ya kwanza kuanza ujenzi katika mji huo, hivyo haoni kikwazo chochote cha kutekeleza azma hiyo kutokana na hatua nzuri ya ujenzi iliyofikiwa.

Ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mji wa serikali, Ihumwa ni sehemu ya mwendelezo wa utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhamishia shughuli za serikali jijini Dodoma aliyoyatoa tarehe 25 Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwasili katika Mji wa Serikali kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Utumishi katika mji huo Ihumwa, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akitoa maelekezo kwa Mhandisi, Lucas Lipambila (kushoto) wakati wa ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
Afisa Tawala Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Donald Bombo akisisitiza jambo kwa Mhandisi Lucas Lipambila (wa pili kutoka kulia) baada ya kumalizika kwa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza jambo baada ya kukamilika kwa ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb).

Muonekano wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora linalojengwa katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma

Azam FC kuwania pointi tatu dhidi ya JKT Tanzania

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KLABU ya Azam FC, itaingia vitani kuwania pointi tatu muhimu kwa kuvaana na JKT Tanzania, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex kesho Ijumaa saa 1.00 usiku.

Mchezo huo wa raundi ya 30, unatarajia kuwa mkali na aina yake, kikosi cha Azam FC kikiwa kwenye hali nzuri kabisa hadi sasa kikiwa kimejikusanyia pointi 53 katika nafasi ya pili kikizidiwa pointi na 11 na kinara Yanga aliyekuwa nazo 64.

Wakati Azam FC ikitoka kuichapa African Lyon mabao 3-1 kwenye mchezo uliopita, JKT yenyewe ipo nafasi ya sita kwa pointi 36 baada ya mchezo uliopita kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Lyon, uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Azam FC ikiwa na makocha wake wa muda, Idd Nassor Cheche na Meja Mstaafu, Abdul Mingange, wameendelea kufanya kazi kubwa ya kukisuka kikosi hicho, ambacho kimeonekana kuimarika kadiri siku zinavyosogea.

Akizungumzia mchezo huo, Cheche alisema wachezaji wana ari kubwa na wamekuwa wakifanya vema katika mazoezi jambo ambalo linampa matumaini ya kuendelea kupata matokeo mazuri kwenye mtanange huo.

“Wachezaji wana ari kubwa kuelekea mchezo huo na wamekuwa wakifurahia mazoezi, jambo ambalo linanipa matumaini ya kupata matokeo mazuri zaidi, tunaiheshimu JKT ni timu nzuri ila tumejipanga kupata ushindi kwenye mechi zetu mbili zijazo za ligi kabla ya kucheza mechi ya FA dhidi ya Kagera Sugar,” alisema.

Mabingwa hao wa ligi msimu 2013/2014 bila kupoteza mchezo wowote, wataingia kwenye mchezo huo wakimkosa kiungo wake mshambuliaji, Tafadzwa Kutinyu, ambaye atakuwa akitumikia adhabu ya kukosa mechi moja kufuatia kukusanya kadi tatu za njano.

Katika mchezo wa raundi ya kwanza ya ligi, Azam FC iliichapa JKT bao 1-0 ugenini kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam, bao lililofungwa na aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Yahya Zayd, aliyetimkia Ismaily ya Misri, akimalizia pande safi alilopewa na Donald Ngoma.

Profesa Kabudi akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Dkt. Richard Sezibera. Katika mazungumzo yao,Sezibera alimpongeza  Prof. Kabudi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Ernest Mangu na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Wilbroad Kayombo. Sezibera yupo nchini kwa ajili ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda,  Paul Kagame. 
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,  Eugene Kayihura (kulia) na Afisa Ubalozi wa Rwanda wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Kabudi na  Dkt. Sezibera (hawapo pichani). 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi akimwelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Dkt. Richard Seziberawakati wa mazungumzo hayo.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda,  Ernest Mangu pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Bw. Wilbroad Kayombo wakiwa kwenye Mazungumzo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Prof. Palamagamba Kabudi (katikati) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda,  Dkt. Richard Sezibera (wapili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Ernest Mangu (wa kwanza kulia) na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura (wa kwanza kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images