Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109935 articles
Browse latest View live

THT waomboleza msiba wa Ruge Mutahaba kwa kumuimbia


Benki ya Exim yazidi kujiimarisha, yainunua benki ya UBTL

$
0
0
 Benki ya Exim Tanzania imezidi kujitanua na kujiimalisha zaidi  hapa nchini baada ya kuonesha nia na utayari wa kuinunua  rasmi kuwa  benki ya UBL Tanzania Limited (UBTL) kwa asilimia 100. Hii ikiwa ni baada ya kusainishana barua ya kuonesha nia (Letter of Intent)
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  leo jijini Dar es Salaam na  Naibu Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim Bw Jaffari Matundu, inasema  ununuzi huo  unaohusisha mali na madeni unazidi kuifanya benki hiyo ambayo kwasasa ni miongoni mwa benki tano kwa ukubwa hapa nchini kuzidi kujitanua zaidi ndani na nje ya nchi.
“Kwetu ni furaha kubwa kuona kwamba familia yetu inazidi kuongezeka  kwa kuwa tayari tunaungana na wanafamilia kutoka benki ya UBTL . Zaidi ya yote tunaamini pia kuwa wafanyakazi  wa benki ya UBTL wataongeza nguvu ambayo kwa pamoja tutaweza kutoa huduma bora zaidi za kibenki kwa wateja wa UBTL,’’ alisema bw Matundu.
Alisema kuwa benki ya Exim inatarajia kukaribisha wateja wa benki ya UBTL katika mtandao mpana wa matawi ya benki ya Exim huku akiongeza kuwa hatua ya ununuzi huo ni upanuzi wa asili na uimarishaji wa uwepo wa benki hiyo katika soko la ndani ya nchi.
Benki ya Exim ilianzishwa mwaka 1997 na ndio benki ya kwanza hapa nchini kuvuka mipaka na kujiimarisha nje ya nchi ambapo kwasasa imefanikiwa kuwa na matawi yake katika nchi za Uganda, Comoro and Djibouti.
Tangu kuanzishwa kwake benki hiyo imekuwa ikijipambanua kwa ubora wa huduma ikilenga kujenga thamani ya uwekezaji kwa wadau wake  na kufikia ukuaji wake kwa kutoa huduma kwa upekee na iliyoboreshwa.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa UBTL Bw Gasper Njuu alisema benki hiyo pamoja na wanahisa wake wamekuwa na mtazamo chanya juu ya fursa za ukuaji nchini Tanzania na kwasasa hilo linakwenda kufanikiwa kupitia benki ya Exim.
“Wakati tukiwa kwenye mkakati wa mabadiliko ya kibiashara kupitia uwekezaji zaidi kwenye huduma za kidigitali ndipo tulipokea ombi kutoka benki ya Exim wakiomba kununua benki ya UBTL na baada ya kufikiria kwa kina  pande zote wakiwemo wanahisa wetu walikubaliana na ombi hilo hasa kwa kuzingatia ubora, weledi na sifa za benki ya Exim kwa hapa nchini ambao kimsingi unaleta tija kubwa kwa wadau na wateja wetu,’’ alibainisha  bw Njuu
Benki ya UBTL ilianzishwa mwaka 2013, kama benki tanzu inayomilikiwa na  Benki ya United Bank Limited (UBL) ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini Pakistan na imetoa huduma za benki za rejareja na za jumla kwa wateja mbalimbali.
Alisema hatua ya ununuzi inahusisha taratibu kadhaa za kisheria zikihusisha  nchi za Tanzania na Pakistan na zinatarajiwa kukamilika katikati ya  mwaka 2019.

Kufuatia hatua hiyo  pande zote yaani Benki ya Exim na UBTL wameahidi kushirikiana vyema na Benki Kuu ya Tanzania  ndani ya wiki zijazo kuhakikisha kwamba mabadiliko hayo yanafanyika kwa urahisi na kwa kuzingatia taratibu zote za kisheria.
Naibu Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim Bw Jaffari Matundu

UN-MICT President Hon Justice Carmel Agius visits African Court in Arusha

$
0
0
The newly elected President of the UN International Residual Mechanism for Criminal Tribunals Hon Justice Carmel Agius (first pix left) today, Wednesday 6th March 2019, paid a courtesy call on his counterpart at the African Court Hon Justice Sylvain Oré in Arusha, Tanzania. The two exchanged views on judicial matters and how to strengthen the existing co-operation. In the picture, President Agius admires  the just-launched 2nd Volume of the African Human Rights Yearbook.

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI KATIKA IBADA YA JUMATANO YA MAJIVU KANISA KUU LA MTAKATIFU JOSEPH JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipakwa majivu na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Joseph Mosha wakati wa Ibada ya Jumatano ya Majivu kanisani hapo leo Machi 6, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Mkate wa Sakramenti Takatifu kutoka kwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Joseph Mosha wakati wa Ibada ya Jumatano ya Majivu kanisani hapo leo Machi 6, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa ameongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli, akila Mkate wa Sakramenti aliopokea toka kwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Joseph Mosha wakati wa Ibada ya Jumatano ya Majivu kanisani hapo leo Machi 6, 2019
Sehemu ya waumini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam wakiwa katika Ibada ya Jumatano ya Majivu kanisani hapo leo Machi 6, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa ameongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli, akiaga waumini wenzie katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Joseph Mosha baada ya kuhudhuria Ibada ya Jumatano ya Majivu kanisani hapo leo Machi 6, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa ameongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli, akiagana na Padri Joseph Matumaini nje ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Joseph Mosha baada ya kuhudhuria Ibada ya Jumatano ya Majivu kanisani hapo leo Machi 6, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Ibada ya Jumatano ya Majivu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2019

PICHA NA IKULU

LUGOLA KUANZA ZIARA MKOANI MOROGORO KESHO, KUFUATILIA MAAGIZO YAKE, KUZUNGUMZA NA WANANCHI WILAYA ZOTE MKOANI HUMO

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MOHA-Morogoro.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewasili mjini Morogoro leo, kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi kwa kutembelea Wilaya zote za Mkoa huo, akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake.

Waziri Lugola anatarajia kuanza ziara hiyo rasmi kesho Machi 7, 2019 mjini Morogoro kwa kukutana na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na kupokea taarifa ya Kamati hiyo, pia atakutana na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa na Wilaya, na baadaye atazungumza na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vya Wizara yake, na baada ya hapo atafanya kikao na Baraza la Askari na Watumishi raia wote wa Wizara hiyo waliopo mjini humo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, leo, Lugola amesema atafanya mkutano mkubwa wa hadhara wa wananchi utakaofanyika mjini humo ili aweze kusikiliza na kuzitatua kero mbalimbali zitakazosemwa na wananchi katika mkutano huo.

“Nawaomba wananchi wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Wilaya zake, wahakikishe wanakuja kwa wingi katika mikutano yangu kuanzia mkoani hapa na Wilaya zote nitakazozitembelea, ili tuweze kubadilishana mawazo, kusikiliza kero zao na pia kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya, wananchi nileteeni kero zenu ili tuzitatue na tuijenge nchi yetu,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, mkutano huo utafanyika saa 10:00 hadi 12:00 jioni utaanza mjini humo na pia atatoa muda wa wananchi kujitokeza mbele kuja kuuliza maswali na yeye aweze kuyajibu.

Waziri Lugola ambaye alisema atafanya mikutano katika Wilaya zote atakazozitembelea pamoja na kufuatilia maagizo yake mbalimbali ambayo aliyatoa mwaka jana 2018 katika mikutano yake, kama yalifanyiwa kazi na viongozi wa Taasisi anazoziongoza au yalipuuzwa.

Maagizo hayo ni dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote nchini zilizopo vituoni ziondolewe ambazo hazina kesi mahakamani.

Lugola alisema katika ziara yake aliyoifanya mwaka jana Mkoani Kigoma, na mwaka huu Mkoa wa Kagera na Arusha, aligundua wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo hawezi kukaa ofisini, lazima afanye ziara nchi nzima kuwasaidia wananchi kutatua kero zao ambapo baadhi yao wakiwalalamikia Polisi wakiwaonea.

“Wananchi wanapojitokeza kwa wingi inasaidia kusikiliza matatizo yao yanayowakabili, ndio mana nimepanga kufanya ziara kama hizi nchi nzima, hii inasaidia sana kujua matatizo mbalimbali ya wananchi pamoja na kuangalia utendaji kazi wa Taasisi zangu zilizopo ndani ya Wizara hii, na hakika Serikali ya Dokta Magufuli inawajali wananchi wake ndio mana inawafuata mahali walipo, ili wazungumze na Serikali yao uso kwa uso,” Alisema Lugola.

Lugola alisema Taasisi zilizopo ndani ya Wizara yake ambazo ni Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Idara ya Probesheni na Huduma kwa Jamii, wajipange ili waweze kumpa taarifa za utendaji kazi wao kuanzia ofisi za Mkoa hadi Wilaya zilizopo mkoani humo.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola

TAWA yasitisha kibali cha kuwinda kampuni ya Green Miles Safaris Ltd.

$
0
0
Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori nchini(TAWA),imejipanga kuendelea kuboresha sekta ya uwindaji wa kitalii na imesitisha kibali cha uwindaji wa kitalii cha kampuni ya Green Miles Safaris Ltd, kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya umiliki wa vitalu vya uwindaji.

Naibu Kamishna wa Utalii na Biashara wa TAWA, Imani Nkuwi alisema kampuni hiyo, imeshindwa kulipa ada za kutotumia zaidi ya asilimia 40 ya mgao wa kuwinda katika vitalu.

"kampuni hii tumeinyia huduma za kuwinda katika vitalu vyake vyote wakati suala lao likifanyiwa kazi"alisema.Kampuni hiyo, inamiliki vitalu wilayani Longido na katika pori la akiba la Selous na katika siku za karibuni, imekuwa na migogoro na vijiji ilipowekeza wilayani Longido.

Hata hivyo, Nkuwi alisema bado wamiliki wengi wa vitalu wanazingatia sheria na taratibu zilizowekwa na serikali, ikiwepo kutunza vitalu vyao, kuzuia matukio ya ujangili na kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe ametoa agizo , kukamatwa mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Green Miles Salim Abdalah Awadhi, kutokana na kushindwa kulipa deni hilo la vijiji na halmashauri ya Longido mkoa wa Arusha.

Mwaisumbe alisema vijiji 23 vya wilaya hiyo, vinaidai kampuni hiyo, kiasi cha sh 329 milioni kutokana na makubaliano walioingia tangu mwaka 2017/18 na jitihada za malipo zimekwama kwa njia ya mazungumzo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Longido, Wakili Jumaa Mhina, alisema ofisini yake imekuwa ikiitaka kampuni hiyo kuwa na mahusiano na vijiji na kulipa fedha za vijiji na halmashauri bila ya mafanikio.

Hata hivyo,Mkurugenzi wa Green Miles Safari Ltd, Salim Abdalah Awadhi ambaye yupo nje ya nchi , amekuwa akikanusha tuhuma mbali mbali dhidi ya kampuni yake,ikiwepo kudaiwa na vijiji fedha .

BREAKING NEWZZZ: Mwalimu aliyempiga mwananfunzi mpaka kumuua ahukumiwa kunyongwa hadi kufa.

$
0
0
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba imemhukumu Mwl. Respicius Mutazangira Kunyongwa hadi kufa baada ya Kupatikana na hatia ya Kumpiga mpaka kusababisha kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius, wa darasa la tano, Shule ya Msingi Kibeta.

 Aidha mahakama hiyo, imemuachia huru Mwalimu   Elieth Gerald baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Washtakiwa hao wote walikuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia Namba 56 ya 2018.

 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba imemhukumu Mwl. Respicius Mutazangira Adhabu  (pichani kwenye kizimba) ya Kunyongwa hadi kufa baada ya Kumkuta na hatia ya Kumpiga na Kumuua mwanafunzi Sperius Eradius Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kibeta, Huku Mwl.   Elieth Akiachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia dhidi ya kesi yao Namba 56 ya 2018 
 Mwl.   Elieth akitafakari jambo kabla ya kuachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia dhidi ya kesi yao Namba 56 ya 2018. 
Wakili mkuu wa Serikali Hashimu Ngole akifafanua jambo mbele ya wanahabari mara baada ya Mahakama kuu kanda ya Bukoba kutoka hukumu kwa Mwl. Respicius Mutazangira Kunyongwa hadi kufa baada ya Kupatikana na hatia ya Kumpiga mpaka kusababisha kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius, wa darasa la tano, Shule ya Msingi Kibeta.

MKURABITA Yatajwa Kuchochea Maendeleo Endelevu

$
0
0
Na Frank Mvungi- Dodoma
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) umetajwa kuchochea ustawi wa wananchi na kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwakwamua wananchi kiuchumi baada ya kurasimisha mashamba yao ili kufikia maendeleo endelevu.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100  wa Kijiji cha Mahama Wilayani Chamwino mbunge wa jimbo la Chilonwa Mhe. Joel Mwaka amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wakulima waliorasimisha mashamba yao na kupata hati za hakimiliki za kimila kutumia fursa zitokanazo za urasimishaji huo .
“ Mpango wa matumizi bora ya Kijiji cha Mahama umewezesha mashamba 1000 yamepimwa na hatimiliki 500 zimeweza kuandaliwa ili ziweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi kwa kuongeza tija katika uzalishaji” Alisisitiza Mhe. Mwaka
Akifafanua amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imewekeza fedha nyingi katika uwezeshaji wananchi kiuchumi katika Wilaya hiyo kupitia kuwajengea uwezo wakulima hao, miradi ya maji, elimu na afya, lengo likiwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na maisha bora.
Pia aliwaasa wananchi hao kutumia mafunzo hayo vizuri na kutumia ujuzi watakaoupata kuleta mageuzi ya kweli yakiuchumi kupitia sekta ya kilimo, ufugaji na nyinginezo zilizopo katika Wilaya hiyo.
Kwa upande wake mratibu wa MKURABITA Dkt. Seraphia Mgembe  amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kupitia mpango huo ni kuhakikisha kuwa inawawezesha wananchi kushiriki katika kujenga uchumi na kuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali zilizopo katika maeneo yao.
“ Serikali inatambua umuhimu wa kuwezesha wananchi wake ndio maana imekuja kuwajengea uwezo ili mtumie hatimilki za kimila za kumiliki ardhi kujikwamua kiuchumi kwa kuchukua mikopo katika taasisi za fedha ili muweze kuboresha kilimo cha mazao ya biashara hasa alizeti.” Alisisitiza Dkt. Mgembe
Akifafanua Dkt. Mghembe  amesema kuwa wananchi wanapaswa kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali kupitia mpango huo  ili kujenga msingi  wa maendeleo endelevu yanayoendana na uchumi wa viwanda.
Naye Meneja Urasimishaji wa MKURABITA Bw. Antony Temu amesema kuwa wakulima hao watafundishwa kilimo bora cha alizeti na mahindi, utafutaji wa fursa na kuzitumia, ufugaji wa kuku wa kienyeji, utunzaji wa kumbukumbu, huduma zitolewazo na mabenki hususani kufungua akaunti za kuweka akiba na upatikanaji wa mikopo.
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupunguza tatizo la kuwepo kwa rasilimali vijijini zinazomilikiwa na katika mfumo usio rasmi ikiwemo ardhi.
 Mbunge wa jimbo la Chilonwa Wilayani Chamwino Mhe. Joel Mwaka akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia hatimilki za kimila za kimili ardhi kujikwamua kiuchumi baada ya kurasimisha mashamba yao katika Kijiji cha Mahama Wilayani humo leo.
 Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Dkt. Seraphia  Mgembe akisisitiza kuhusu dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwalwawezesha wananchi,  Ameyasema hayo  wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 wa kijiji cha Mahama jimbo la Chilonwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma mapema leo, mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wakulima hao ili watumie hatimilki za kimila za kumiliki ardhi kujikwamua kiuchumi.
 Meneja Urasimishaji  Ardhi Vjijini kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bw. Antony Temu akieleza manufaa  ya mafunzo yakuwajengea uwezo wakulima wa kijiji cha Mahama Wilayani Chamwino.
 Mbunge wa jimbo la Chilonwa Mhe. Joel Mwaka akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wananchi waliopatiwa hatimilki za kimila za kumiliki ardhi leo jimboni humo.
   Kwaya ya kijiji cha Mahama  ikitumbuiza wakati wa hafla ya Ufunguzi wa mafunzo yakuwajengea uwezo wakulima zaidi ya 100 ili waweze kutumia hati milki za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Mahama  Wilayani Chamwino mkoani Dodoma Bi. Grace Mfereji akipoa hatimilki ya kimila kutoka kwa Mbunge wa jimbo la Chilonwa Mhe. Joel Mwaka leo wakati wa hafla ya kufungua mafunzo yakuwajengea uwezo wakulima zaidi ya 100 wa kijiji hicho, mafunzo hayo yameratibiwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmashuri ya Wilaya hiyo. (Picha zote na Frank Mvungi- Dodoma)

Kamati ya Bunge ya Bajeti yafanya ziara katika kiwanda cha Transfoma na kupongeza uzalishaji

$
0
0
Na Teresia Mhagama
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, George Simbachawene wametembelea kiwanda cha kuzalisha transfoma cha TANELEC kilichoko jijini Arusha ili kukagua masuala mbalimbali ikiwemo uwezo wake katika uzalishaji wa transfoma lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na vifaa vya umeme vya kutosha.

Katika ziara hiyo waliambatana na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Baada ya kukagua shughuli za uzalishaji wa transfoma katika Kiwanda hicho, Wajumbe hao kwa nyakati tofauti waliwapongeza watendaji wa Kiwanda hicho kwa kuzalisha transfoma nyingi ambazo ni 14,000  kwa mwaka huku mahitaji ya transfoma nchini kwa mwaka yakiwa ni 10,000.

Aidha Wajumbe hao walipongeza uamuzi wa Serikali wa mwaka 2017 ambao ulielekeza kuwa miradi yote ya umeme nchini itumie vifaa vya umeme vinavyopatikana nchini hali inayopelekea miradi hiyo kutekelezwa kwa kasi. Wajumbe hao pia walimtaka Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo kuongeza uzalishaji na kuwa mbunifu kwa kuangalia pia masoko mengine ya transfoma na si kulenga miradi ya umeme ya ndani ya nchi pekee.

Awali, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani alisema kuwa, Serikali ilichukua uamuzi wa kusitisha kuagiza nje vifaa vya umeme vinavyopatikana nchini ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya umeme. Alitoa mfano kuwa upatikanaji wa transfoma nje ya nchi unaweza kuchukua hadi miezi 12  hali wakati transfoma zinazozalishwa ndani ya nchi zinachukua muda mfupi kufika katika eneo zinapohitajika.

Aidha Waziri wa Nishati alisema kuwa, uagizaji wa transfoma nje ya nchi ni gharama kubwa kwani transfoma moja kutoka nje ya nchi inauzwa kwa takriban shilingi milioni Tisa wakati zinazozalishwa nchini ni takriban shilingi milioni 6.5. Akitoa taarifa ya kiwanda hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TANELEC, Zahir Saleh alisema kuwa kiwanda hicho kilichoanzishwa mwaka 1981 kwa sasa kinazalisha transfoma kiasi cha 14,000 kwa mwaka.

Alisema kuwa,  kiwanda kinazalisha transfoma za uwezo wa kvA 50 hadi kVA 5000 na kufanya matengenezo ya transfoma kutoka nchi mbalimbali za Afrika kama Rwanda, Burundi na Kenya. Aliongeza kuwa, uamuzi wa Serikali kuzuia kuagiza vifaa nje ya nchi umekinufaisha kiwanda hicho kwani kabla ya uamuzi walikuwa wakizalisha transfoma 7000 kwa mwaka lakini sasa wanazalisha transfoma 14,000.

Kuhusu ajira alisema kuwa, awali waliajiri wafanyakazi 30 lakini kwa sasa wafanyakazi walioajiriwa ni 70 na kwa mwaka huu wataajiri wafanyakazi wengine 40. Vilevile alisema kuwa, kutokana na uamuzi huo wa Serikali, Kiwanda kinafanya kazi kwa faida na wameanza kupeleka gawio serikalini la takribani shilingi milioni 500 kwa mwaka 2018 na wanategemea kuongeza kiasi cha gawio hilo kwa miaka inayokuja.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene (wa kwanza kushoto) wakiongoza Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti katika kukagua kazi zinazofanywa na kiwanda cha transfoma cha TANELEC kilichoko jijini Arusha.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika kiwanda cha kuzalisha transfoma cha TANELEC kilichopo jijini Arusha. Wa Pili kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha transfoma cha TANELEC, Zahir Saleh ( wa nne kulia) akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati walipotembelea kiwanda hicho kilichopo jijini Arusha. Wa Tatu kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ambaye aliambatana na Wajumbe hao na wa Tano kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, George Simbachawene.

EAC SECRETARIAT ALERTS PARTNER STATES ABOUT AN INCREASED RISK FOR DISEASE OUTBREAKS DUE TO ABOVE NORMAL RAINFALLS

$
0
0
cid:image001.png@01D4CAAF.6A5FD560EAC Secretariat
  East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, 5th March, 2019: Above normal rainfall is expected in the East African region over the next few months, a scenario that could expose the region to increased risks of disease outbreaks.

This forecast is based on the regional climate outlook for the March to May 2019 long rainfall season provided by the Greater Horn of Africa Climate Outlook Forum held in Entebbe, Uganda.

Mr. James Kivuva, the Senior Meteorologist, who represented the East African Community Secretariat at Forum warned that the higher than normal rainfall would increase the risk for outbreaks of infectious diseases. Mr. Kivuva urged EAC Partner States to be on the alert, inform the public, and put preparedness and mitigation measures in place while closely monitoring the rainfalls.

Between October and December 2018 parts of the region experienced a late start and early end of rains. However, above to near normal rainfalls were experienced in parts of Tanzania and in the Western parts of the region. Burundi, Rwanda and Uganda even reported flooding with landslides that impacted on some communities in the Eastern region where some lives were lost.  

For March to May the climate predictions indicate an increased likelihood of above to near normal rainfalls over much of the equatorial sector.“Most parts of the region are likely to have an earlier seasonal rain onset, but the rains will also end earlier than usual,” said Mr. Kivuva. 

“There is an increased chance for flash and riverine flooding mainly in the flood prone areas of the EAC Partner States, which might trigger landslides, mudslides and enhance the risk for outbreaks of infectious diseases with consequences for sectors such as health and agriculture including livestock,” he added.

The officer warned that flooding was likely to cause mass mosquito breeding that can transmit Malaria in humans and Rift Valley Fever (RFV) in animals and humans. “Already, the first cases of RVF in animals and humans have been reported from Kenya. Flooding increases the risk for diarrheal diseases, like cholera, especially in low laying areas,” said Mr. Kivuva.

On a positive note, the rain falls are good for the crop, if they are not excessive, and also for the pastoralist’s prospects. There is also a likelihood of a reduction in fall army worm infestation, as high rains are unfavorable for their multiplication.

“This would increase food security. The expected enhanced rains would also bring some relief, especially in areas that suffered from low rain falls and even droughts in the past season.” 

In an effort to prevent and mitigate disease outbreaks in the region, Mr. Kivuva urged Partner States to undertake with the following precautionary measures:

The animal and human health disease surveillance units should actively monitor the disease trends in the affected areas;
  • Citizens should protect themselves and especially children against mosquito bites. Adequate measures are the use of impregnated mosquito nets, personal insect repellents, if available light coloured clothing (long-sleeved shirts and trousers) and avoiding outdoor activities at peak biting times of mosquitos.
  • Livestock farmers should contact the veterinary services for early information on vaccinating their animals against RVF.
  • People in contact with ruminants should practice hand hygiene, wear gloves and other appropriate individual protective equipment when handling sick animals or their tissues or when slaughtering animals;
  • In case of an RVF outbreak, people should avoid consuming fresh blood, raw milk or animal tissue and products without thoroughly roasting them;
  • The Ministries of Health should intensify social mobilisation and health promotion efforts with preventive messages that enable the public to manage the risks at hand.
  • The Meteorology departments should continue to monitor and analyse the weather patterns and share information with other departments to plan and prepare for outbreaks of infectious diseases of public health concern.

The Climate Outlook Forum meets on a quarterly basis to formulate mitigation strategies for key socioeconomic sectors in this region, such as agriculture, health and infrastructure. The meetings provide a regional platform for decision makers, climate scientists, research scientists as well as users of climate information.

Tanzania Kinara tena tuzo za ‘DStv Eutelsat Star Awards’

$
0
0
      Priscilla Marealle awaburuza maelfu kutoka kote barani Africa
         Ni mara ya tatu mfululizo Tanzania kuonyesha cheche zake
        Majaji washangazwa na uwezo mkubwa wa mwanafunzi huyo Mtanzania
   Wazazi, Waalimu na Marafiki wasema alistahili tuzo hiyo

 Kwa mara nyingine tena Tanzania imeibuka kinara  katika tuzo za kimataifa za wanafunzi zijulikanazo kama DStv Eutelsat Star Awards ambapo mwanafunzi Priscilla Marealle kutoka shule ya sekondari ya St. Mary Goreti mkoani Kilimanjaro ameweza kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa kunyakua nafasi ya kwanza katika kipengele cha uchoraji bango  ikiwa ni baada ya mchuano mkali baina ya mamia ya wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. 

Kwa upande wa uandishi wa insha kijana Tanaka Chonyera kutoka  nchini Botswana aliweza kujinyakulia ushindi wa kwanza.

Tuzo hizi ambazo huhusisha uandishi wa insha maalum au kuandaa bango yenye ujumbe kuhusiana na elimu ya anga hususan Setelait ni za wazi kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wenye umri kati ya miaka 14 – 19 kote barani Afrika ambapo kampuni ya MultiChoice inaendesha shughuli zake.

Katika msimu huu wa nane, washindani walitakiwa kuandika insha au kubuni bango litakaloelezea licha ya Satelait kutumika katika shughuli mbalimbali, ni namna gani zitaweza kutumika zaidi ili kuleta maendeleo chanya ulimwenguni.

Priscilla ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha sita wa mchepuo wa Sayansi katika shule ya Mtakatifu Maria Goreti alitangazwa rasmi kuwa mshindi mjini Accra nchini Ghana ambapo ndipo jopo la watahini liliongozwa na Paolo Nespoli, mwanaanga nguli kutoka European Space Agency (ESA) lilikaa kupitia kazi kutoka kwa wanafunzi walioshinda katika nchi mbalimbali. 

Akiongea baada ya kukabidhiwa cheti cha uthibitisho wa ushindi wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya shule ya Mtakatifu Mary Goreti iliyopo Moshi Kilimanjaro, Priscilla amesema amefurahi sana kwa ushindi huo mkubwa ambao umemletea yeye, shule yake na taifa zima kwa ujumla sifa kubwa. “Nimefurahi sana kupokea taarifa hizi nzuri. Naamini ushindi wangu utakuwa ni chachu kubwa kwa wanafunzi wenzangu kote nchini kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika tuzo kama hizi na mashindano mengine ya kitaaluma ya ndani na nje ya nchi, na kusisitiza  kuwa Ndoto huanza kufanya kazi pale unapojiamini” alisema Priscilla.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo ya Mtakatifu Maria Goreti Sister Lucresia Njau alisema kuwa anaishukuru sana kampuni ya MultiChoice Tanzania kwa kuwapatia nafasi ya kushiriki katika Mashindano hayo na hatimaye kuweza kunyakua tuzo hiyo kupitia mwanafunzi wao Priscilla.

“Huyu kijana ana jitahidi sana katika chochote kile anachokifanya, iwe ni darasani au hata katika majukumu mengine nje ya darasani. Ni msikivu mtiifu lakini zaidi ya yote ni mbunifu sana. Naamini haya ndiyo yaliyomfanya aweze kushinda tuzo hizi” alisema Sr. Lucrecia Njau.

Naye, Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania Johnson Mshana alisema,” Huu ni msimu wa tatu mfululizo kwa Tanzania kuendelea kung’ara katika tuzo hizi za DStv Star Awards. Tulianza kupeperusha bendera yetu na kijana Davids Bwana msimu wa sita baada ya kushika nafasi ya pili Afrika katika kipengele cha uandishi wa insha, kisha tukaibuka kidedea baada ya kupokea taarifa za ushindi wa kwanza wa kijana Taheer Rashid katika msimu wa saba mwaka jana na leo hii tunayofuraha kubwa kuona kuwa tumeendeleza wimbi la ushindi.”

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya Pricilla kutangazwa kuwa mshindi, walimu na wazazi wa mwanafunzi huyo wa kidato cha sita mwenye umri wa miaka 19, wamesema kuwa wanamfahamu vyoma Pricilla kuwa ni kijana mwenye kupenda kujibidisha sana katika masuala ya kitaaluma na kijamii hivyo ushindi wake ni kitu kilichotarajiwa na kwamba wanaamini kuwa anastahili ushindi huo.

Pamoja na kupata cheti maalum cha ushindi, Pricilla atapata fursa (Yeye na Mzazi au mlezi) ya kutembelea kitua cha Anga cha Afrika Kusini na pia kutembelea makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg kama mgeni maalum wa DStv  huku shule aliyotoka ikipata zawadi ya cheti pamoja na kufungiwa huduma ya DStv.
  Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana akimkabidhi mshindi wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle cheti cha ushindi wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika shule ya St Mary Goretti hivi karibuni. Kulia ni Afisa Uhusiano  wa MultiChoice Tanzania. Grace Mgaya. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg.
 Mkuu wa shule ya  St Mary Goretti Sr. Lucrecia Njau akifurahi baada ya kupokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana mara baada ya shule hiyo kufanikiwa kutoa mshindi wa jumla wa wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg
 Mshindi wa Jumla wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle akikabidhiwa kikombe cha ushindi na Mkuu wa shule ya St Mary Goretti Sr. Lucrecia Njau baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa jumla wa wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg.
Mshindi wa Jumla wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle akifurahi na wazazi wake Calvin Marealle  na Jamila Marealle mara baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg. 
Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (Kulia) na Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Grace Mgaya (kushoto) wakikabidhi seti ya DStv kwa mkuu wa shule ya sekondari St Mary Goretti Sr. Lucrecia Njau na mshindi wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika shule ya St Mary Goretti hivi karibuni. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg wakati shule yake imepata cheti na zawadi ya kufungiwa huduma ya DStv. 

siku ya madaktari nchini yaadhimishwa Dar es salaam

$
0
0
 Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Bakari akizungumza kwenye mkutano wa kuadhimisha siku ya madaktari nchini ambayo hufanyika Machi 4 kila mwaka. Katika mkutano huo, Prof. Kambi amewataka madaktari kuzingatia weledi na maadili wakati wa kutoa huduma katika sehemu zao za kazi. Prof. Kambi alimwakilisha Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu. Katika mkutano huo, Prof. Kambi aliwataka madaktari nchini kuzingatia weledi na maadali katika kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi. Pia, amewataka madaktari nchini kuiunga mkono Serikali katika mipango yake ya kuboresha huduma za afya nchini ikiwamo huduma za ubingwa na ubingwa wa juu. Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).
 Baadhi ya madaktari wakimsikiliza Prof. Kambi wakati akizungumza nao kwenye mkutano ambao umefanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
 Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Elisha Osati akieleza historia fupi ya  maadhimisho ya siku ya madaktari duniani.
  Madaktari wakifuatilia mkutano huo ambao umewakutanisha madaktari mbalimbali.
 Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bw. Makwaia Makani akizungumza kwenye mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Prof. Kambi kuzungumza na madaktari hao.  
  Baadhi ya madaktari vijana wakisikiliza nasaha kutoka kwa Bw. Makani ambaye pia aliwasisitiza kuzingatia weledi wakati wa kuwahudumia wagonjwa ili kutoa huduma bora za matibabu.
 Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed akimkabidhi tuzo Prof. Philimon Sarungi kwa kuthamini mchango wake alioutoa katika Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT).
Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Bakari akimkabidhi tuzo Prof. Yadon Mtarima Kohi ikiwa moja ya njia ya kutambua mchango wake alioutoa katika chama hicho.
  Prof. Bakari akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari wakongwe wakiwamo waliokabidhiwa tuzo.
Picha ya pamoja katika mkutano wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT)

WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA MZUMBE MKOANI MOROGORO WAADHIMISHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI

$
0
0

Umoja wa wanawake wa chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro wamedhamiria kuwakomboa wanafunzi wa kike wanao soma shule za sekondari zinazozunguka chuo hicho kwa kuwajengea mabweni ili kukuza kiwango cha elimu.

Wanawake hao wametoa ahadi hiyo wakati wakisherehekea siku ya wanawake duniani ambapo wameeleza kuwa sababu ya kuchukua uamuzi huo ni kutokana na changamoto nyingi zinazo wakabili wasichana na ikiwemo vishawishi vinavyosababisha mimba za utotoni jambo linalipelekea wanafunzi wengi kukatisha masomo yao.

Miongozni mwa shule ambazo zinazunguka chuo hicho cha Mzumbe ambacho ndio kinaongoza kwa ubora nchini ni pamoja na shule ya sekondari mongola, Adrian Mkoba, na kipela pamoja na shule ya msingi Mzumbe.

Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila terehe nane ya mwezi wa tatu kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Fikiri sawa, jenga uwezo na kuleta maendeleo endelevu.
Mgeni resmi katika mahadhimisho hayo, Bi Enedy Mwanokwate ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akiangalia maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiliamali wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha mzumbe.
Mgeni resmi katika mahadhimisho hayo Bi Enedy Mwanokwate ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akiangalia maonyesho ya bidhaa ya vitenge vya batiki vinazozalishwa na wajasiliamali wanawake wa kata ya bibwa manispaa ya morogoro.
Prof Aurelia kamuzola akitoa mada ya kuwahamasisha wanawake kujitambua na kuwa na hamasa ya kufikia malengo katika hafla ya kushrehekea maadhimisho ya siki ya wanawake duniani yaliyofanyika katika chuo kikuu cha mzombe mkoani morogoro.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe za siku wa wanawake duniani ambaye pia ni kuu wa kitengo cha maendeleo ya jinsia chuo kikuu cha mzumbe Dr Elizabeth Genda akitoa ahadi ya kujenga mabweni ya wasichana wa shule za sekondari zinazo zunguka chuo hicho.
Mwakilishi wa mgeni rasmi Bi Enedy Mwanokwate akipokea picha cha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina chonjo iliyochorwa na mmoja ya wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha mzumbe katika hafla ya kusherehekea siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika chuo hicho.

MVUA KUBWA KUNYESHA DAR, RC MAKONDA ATOA RAI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
BAADA ya Mamlaka ya hali ya hewa nchini kutoa tahadhari juu ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda amewataka wananchi kuanza kuchukuwa tahadhari  mapema katika kukabiliana na majanga ya mafuriko huku akiwataka wakazi wa mabondeni na walioko pembezoni mwa mito kuhama katika maeneo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Makonda amesema kuwa ujenzi holela na tabia ya watu kutupa taka kwenye mifereji inayopitisha maji ya mvua  na mito ndio  chanzo kikubwa cha mafuriko hivyo amewahimiza wananchi kuacha mara moja tabia hiyo huku akiwataka wananchi kumripoti kwa wenyeviti wa mtaa kwa yeyote atakayekaidi hilo.

Aidha  Makonda ametoa siku saba kwa wakala wa barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha wanaziba viraka katika barabara kwakuwa vimekuwa usumbufu na kero kwa watumiaji wa barabara huku akiwaagiza TANROAD kusafisha miundombinu ya Mito,mitaro na madaraja yaliyoziba kwa usalama zaidi.

FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY YAZINDUA NEMBO MPYA

$
0
0
Baada ya uzinduzi huu ndio muonekano wa Nembo mpya ya Foundation for Civil Society (FCS).

BAADA  ya zaidi ya muongo mmoja na nusu kufikia Azaki nchi nzima,  Foundation for Civil Society (FCS) inajikita katika kuongeza ufanisi na juhudi za kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wote katika kuleta maendeleo nchini.
Hayo yameelezwa mapema leo  jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS  Francis Kiwanga wakati wa uzinduzi nembo mpya ya shirika hilo ambayo itaendana na mabadiliko na mfumo wake wa utendaji.

Amesema kuwa nembo hiyo  itahusisha kushirikiana na taasisi zote za Serikali, Bunge, Sekta binafsi, Asasi za kiraia (AZAKI) ili kufikia Maendeleo endelevu ya dunia pamoja na mpango wa Maendeleo wa Taifa wa kuboresha maisha ya watanzania ifikapo 2025.

Aidha amesema  kuwa kwa sasa FCS itatoa ruzuku kwa wastani wa Asasi 150 kwa pande zote mbili za muungano yaani Tanzania Bara na Visiwani kila mwaka, ambapo hapo awali ilikuwa ikitoa kwa Azaki zaidi ya 5500 zilizokuwa zikihudumia wananchi wa mikoa yote hapa nchini.

Ameeleza kuwa kuwa kiasi cha ruzuku kitaongezeka na kwa sasa taasisi hiyo itatoa ruzuku zenye thamani ya billion 11  kwa mwaka na muda wa mkataba pia utakuwa mrefu hadi kufikia miaka miwili ili kupata matokeo mazuri kwa miradi itakayofadhiliwa na FCS.

Akieleza sababu ya kufanya hivyo amesema kuwa wamejikita katika eneo la utawala bora na maendeleo hivyo siyo rahisi kuboresha maeneo hayo kwa mkataba wa mwaka mmoja au miezi sita tu, Hivyo wameona kuna haja ya kuongeza mkataba na kiwango cha ruzuku katika kufanikisha hilo.

Na mwisho alisisitiza watu kupenda kufahamu  kuwa FCS ipo kwa ajili ya watanzania hivyo waondoe mila potofu ya kuwa ni chombo ambacho hakina ubia na serikali na kwa sasa watafanya mambo mengi mazuri kwa kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society  Francis kiwanga akifafanua kuhusiana na nembo mpya iliyozinduliwa na kusema kuwa wamejizatiti kuwafikia wananchi wengi zaidi katika kuleta maendeleo, leo jijini Dar es Salaam.
Zoezi la uzinduzi wa nembo mpya ya Foundation for Civil Society likifanyika, ambapo taasisi ya FCS imehaidi kushirikiana na serikali katika kuhakikisha ufadhili wao kwa Asasi za kiraia unazaa matunda, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka AZAKI mbalimbali hapa nchini wakifuatilia matukio yanayoendelea katika Tafrija hiyo ya Uzinduzi wa nembo mpya ya FCS.
Baada ya Uzinduzi wa nembo mpya ya FCS kulifuatiwa na tukio lingine la uzinduzi wa tovuti mpya (Website) mpya ya shirika hilo kama inavyoonekana pichani.
Washiriki wa semina wakiendelea kusherehekea tafrija.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa shirika la Foundation For Civil Society. 
Wafanyakazi wa Foundation for Civil Society wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Tafrija hiyo, Ambao pia ni wana AZAKI wanaofanyanao kazi kupitia miadi mbalimbali wanayoiendesha, leo jijini Dar es Salaam.

MGEJA AITOSA CHADEMA ARUDI CCM KWA KISHINDO

$
0
0
*Awapa CHADEMA ushauri mzito, ampongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kuleta maendeleo kwa watanzania

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

ALIYEKUWA mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga na baadaye kuhamia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Khamis Mgeja amerudi kwenye chama chake cha awali huku akiwaasa watanzania kutohadaika na propaganda za kuchafua taifa kwenye mataifa ya nje.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mgeja amesema kuwa alipumzika kwa muda katika masuala ya siasa na sio kustaafu kama inavyoelezwa na katika mapumziko hayo alipata wakati mzuri wa kutafakari mustakabali wa nchi kisiasa na kiuchumi na hasa kutafakari mwenendo wake wa kisiasa katika chama alichohamia akitokea CCM, na kugundua kuwa sababu zilizomfanya ahamie CHADEMA hazipo tena.

Amesema kuwa kwa muda aliokuwa CHADEMA walishauri kuhusu masuala ya kujenga nchi ikiwemo kuwa na sera mbadala, kuchangia bungeni, kuachana na mkakati wa kuichafua nchi nje ya nchi na kuacha siasa za kejeli na matusi lakini hawakusikilizwa.

Akieleza sababu zilizomfanya kuhamia CHADEMA Mgeja amesema kuwa walilenga mabadiliko ambayo yalilenga kuondoa kero kwa wananchi hasa kuboresha ustawi wao katika njanja zote muhimu lakini mambo yote hayo hayapo tena upinzani ila yanafanyika vizuri sana na kwa kasi ya ajabu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, na amesema kuwa walitumia muda wao mwingi kushauri chama hicho kuwa cha kisiasa na sio cha kiharakati lakini hawakusikilizwa na kueleza kuwa chama hicho kimegubikwa na ubinafsi na hakuna uwazi kabisa.

Aidha Mgeja ameomba radhi kwa mwenyekiti wa CCM taifa, wanachama, watanzania na familia yake huku akieleza sababu za kuamua kurudi nyumbani ikiwa ni pamoja na kazi nzuri za Rais Dkt. John Magufuli hasa mpango wa kuhamia Dodoma mpango uliokuwa tangu enzi za mwalimu Julius Nyerere pamoja na kuboresha sekta muhimu zikiwemo elimu, afya, barabara, reli,ununuzi wa ndege, miradi mikubwa ya umeme, kukemea vitendo vya rushwa pamoja na kutetea vitendo vya rushwa.

Vilevile Mgeja ametoa ujumbe wa CHADEMA kwa kuwahusia kuchukua maamuzi na kufanya harakati za kidemokrasia na kujenga hoja mbadala lasivyo wajiandae kisaikolojia kwa anguko kubwa litakalowakumba.

Waziri Mkuu aipongeza TFDA katika udhibiti

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) inafanya kazi zake vizuri na kuifanya Tanzania kwa nchi Kwanza katika udhibiti wa ubora wa dawa, vifaa, Tiba, vipodozi pamoja na vitendanishi.

Waziri Mkuu Majaliwa aliyasema hayo wakati alipokwenda ziara ya kikazi katika Mamlaka hiyo amesema kuwa katika kufanya udhibiti huo waongeze kituo vya ukaguzi katika mikoa hasa katika mikoa inayopakana na nchi jirani ikiwa kwa ajili ya kulinda afya za watanzania kutokana na mwiingiliano wa dawa na vyakula nchi zilizo jirani kwa kuweza akiingia bila ukaguzi.
Amesema kuwa katika kufanya kazi za kisayansi wafanyakazi waongozwe na weledi pasipo na mwanya wa kuwepo kwa rushwa katika ukaguzi wa bidhaa mbalimbali.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa changamoto rasilimali watu atatue Waziri mwenye dhamana kwa kuomba kibali serikalini katika kuongeza utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja wawekezaji wakati serikali ikiwa katika kipindi cha kuimarisha uchumi. Aidha amesema katika mnyororo wa upimaji wa bidhaa mbalimbali kusiwepo kwa Mahusiano na wataalam na mwenye bidhaa kinachotakiwa kufanyika kwa mfanyabiashara kuacha bidhaa ya kufanyiwa uchunguzi katika mapokezi na iondolewe jina la kampuni.

Amesema katika kufanya uchunguzi watalaam lazima wajiridhishe kutokana na bidhaa hizo zinaingia kwa walaji ambao lazima afya zao zilindwe. Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa TFDA inambeba katika majukwaa ya kimataifa katika umahiri wa mfumo wa udhibiti.

Amesema maagizo ya Waziri Mkuu watayasimamia katika utekelezaji ikiwa ni kuboresha huduma katika Mamlaka hiyo na kuleta matokeo katika uchumi wa viwanda. Kwa upande Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji 

Angela Kairuki amesema kuwa TFDA katika uwekezaji ni daraja na kutaka watu wenye maamuzi katika kituo vya uwekezaji ili kurahisisha huduma kwa wawekezaji wanaopita (TIC).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maabara ya chakula ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakati alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo, Mabibo jijini Dar es salam, Machi 6, 2019. Kulia ni  Meneja wa Maabara wa TFDA, Danstan Hipolite. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika  dawa ya malaria aina ya DUO -COTECXIN,  halisi kulia na bandia kushoto zilizopimwa na kugundulika hivyo  katika  Maabara ya Mamlaka ya Chakula  na Dawa (TFDA)  wakati alipotembelea ofisi za  TFDA , Mabibo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019.   Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki na wa tatu kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu., kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TFDA, Candita Shirima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu upimaji wa dawa na vyakula kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa  Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Justin Mkisi (kulia) wakati alipotembela ofisi za Mamlaka hiyo, Mabibo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki, wa nne kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa tano kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Candita Shirima.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sampuli ya mafuta ya kula yanayosubiri kupimwa wakati alipotembelea ofisi za Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mabibo jijini Dar es salaam,  Machi 6, 2019.  Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA, Justin  Mkisi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) eneo la Mabibo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Candita Shirima.(Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye viwanja vya Ofisi za TFDA, Mabibo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019.  Wa pili kulia ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki na wa tatu kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WANAWAKE WAFANYAKAZI WAKUTANA DODOMA KUJADILI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI DUNIA IKIHADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Tanzania inaungana na Nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku Wanawake Duniani kwa lengo la kutafakari mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto lakini pia kuwakomboa kifikra, kiutamaduni, kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongomano la wanawake wafanyakazi kuhadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike alisema wanawake na wasichana wafanyakazi ni kundi kubwa na muhimu katika jamii linalohitaji kulindwa.

Bw. Golwike alitoa Rai kwa wanawake hao kuwa Haki inakwenda pamoja na Uwajibikaji lakini pia Usawa unakwenda pamoja na kukidhi vigezo, ambavyo ni sifa za kielimu, kitaaluma na uzoefu wa kazi.

Ameongeza kuwa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 8, kwa mwaka huu hapa Tanzania yanafanyika ngazi ya Mkoa, ambapo kila Mkoa umeadhimisha sikukuu hii kulingana na mazingira yake na rasilimali zilizopo kwa kuzingatia Kaulimbiu ya mwaka husika ambayo ni “Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu”.

Aidha Bw. Golwike aliyataja Madhumuni ya Maadhimisho haya kuwa ni kutoa fursa kwa Serikali, Wananchi, Wadau, Wanawake na Jamii yote kubadili fikra na mtizamo ili kuleta Usawa wa Jinsia na kuonesha nia ya kuhamasisha jamii, juu ya umuhimu wa kutambua uwezo wa wanawake katika kuchangia na kuleta Maendeleo Endelevu lakini pia  Kuwezesha ushiriki na kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake kufikia maendeleo jumuishi.

Wakati huo huo Msimamizi wa Maadhimisho hayo kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Silivia Siriwa alitaja mafanikio yaliyopatikana kutokana na juhudi za Wizara kuwa  ni pamoja kutoa elimu kwa jamii kuhusu utatuzi wa changamoto zinazowakabili wanawake ikiwemo Madhara ya Mila na Desturi potofu ambazo zinaelekeza aina ya kazi na nafasi za uongozi za kushikwa na wanawake ambazo ni za kutoa huduma zaidi.

Aliyataja mengineyo ni kuhamasisha jamii kuhusu kuondoa madhara ya ndoa na mimba za utotoni, ambazo zinafifisha ndoto na matarajio ya mtoto wa kike, hamasa na ushiriki  wa wafanyakazi katika  majukwaa ya uwezeshaji wanawake ambayo yanatumika kwa ajili ya kuelimishana, kubadilishana uzoefu na kujiunga katika mtandao wa mashirikiano.

Bi. Siriwa pia alizitaja baadhi ya changamoto zinazojitokeza kwa wanawake mahali pa kazi ni pamoja na kukosa taarifa za mabadiliko ya Sheria na Kanuni za utumishi, Matumizi ya lugha ya kiingereza katika matumizi ya vifungu vya kisheria inawanyima baadhi ya wafanyakazi, haki ya kuzifahamu sheria.

Aidha Wingi wa shughuli na majukumu ya kifamilia, kikazi na kijamii ni hali inayopunguza ufanisi wao, kipato kidogo cha kumudu mahitaji ya familia na ongezeko la wahitaji kutoka katika makundi maalum ya jamii ambayo wanawake wafanyakazi wanayabeba.

Chimbuko la Siku ya Wanawake lilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kufuatia maandamano ya wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani kupinga mazingira duni ya kazi.

Waandamaji hao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira ikiwemo wanawake kulipwa mshahara mdogo kwa kazi sawa na wanaume.
 Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akifungua Kongamano la wafanyakazi Wanawake jiijini Dodoma liliofanyika kwa lengo la kuwakutanisha wafanyakazi hao kujadiliana na kupata namna bora za kuweza kumuwezesha kiuchumi  mwanamke.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Silvia Siriwa akieleza chimbuko la Siku ya Wanawake Duniani katika Kongamano la wafanyakazi Wanawake jiijini Dodoma liliofanyika kwa lengo la kuwakutanisha wafanyakazi hao kujadiliana na kupata namna bora za kuweza kumuwezesha kiuchumi mwanamke.
  Mkurugenzi Msaidizi Wanawake kutoka  Idara ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza akielezea umuhimu wa Siku ya Wanawake Duniani katika  kiuchumi mwanamke katika kongamano la wafanyakazi wanawake Dodoma.  
 Baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa Mkoa wa Dodoma wakifuatlia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika Kongamano la wafanyakazi Wanawake jiijini Dodoma liliofanyika kwa lengo la kuwakutanisha wafanyakazi hao kujadiliana na kupata namna bora za kuweza kumuwezesha kiuchumi mwanamke.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wanawake waliohudhuria Kongamano la wafanyakazi Wanawake jiijini Dodoma liliofantika kwa lengo la kuwakutanisha wafanyakazi hao kujadiliana na kupata namna bora za kuweza kumuwezesha kiuchumi mwanamke.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

JAFO AAGIZA KASI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA UYUI KUONGEZEKA

$
0
0
Na Tiganya Vincent
UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(UYUI) umeagizwa kuongeza kasi katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ili ifikapo Juni mwishoni mwaka huu majengo yote  waliyopangiwa yamewe yamekamilika.

Agizo hilo limetolewa leo wilayani Uyui na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huo.

Alisema fedha zipo hakuna sababu ya kazi ya ujenzi kwenda pole pole kwa kuwa wananchi wanasubiri huduma hiyo kwa hamu.

Jafo alisema katika Halmashauri nyingine ambapo walipewa fedha pamoja tayari majengo yao yako usawa wa madirisha lakini ya Uyui bado yako katika ngazi za msingi.

Alisema sio vizuri kutumia fundi mmoja kujenga majengo yote ni vema wakatumia mafundi wengi ili kuharakisha kazi ya ujenzi wa Hospitali hiyo.

Aidha Waziri huyo alisema ni jambo la kusikitishwa kuona Halmashauri hiyo imetumia kiasi cha milioni 8 kusafisha eneo badala ya kuwahamisha wananchi kushiriki katika usafishaji wa ili fedha hizo zisaidie ujenzi.

Alisema fedha walizozitumia katika usafishaji wa eneo zingeweza kusaidia katika uendeleza wa ujenzi wa majengo hayo kama wananchi wangeshiriki katika usafishaji wa eneo badala ya kukodi Greda na kulipa kiasi hicho cha fedha.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya alimwakikishia Waziri kuwa watajitahidi kukamilisha majengo hayo katika kipindi kilichopangwa na kwa kuzingatia maelekezo ya TAMISEMI ili fedha zitakazobaki zisaidie kujenga kichoma taka.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui Said Ntahondi huku akishuhudiwa na viongozi mbalimbali wakati wa ziara yake kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya ( wa pili kutoka kulia) kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akitoa maagizo kwa viongozi wa Wilaya ya Uyui na wa Hamashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui baada ya  kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (mbele) akiwaongoza viongozi wa Wilaya ya Uyui na wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui  kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo leo. Picha na Tiganya Vincent

HATMA YA DHAMANA YA MBOWE NA MATIKO KUJULIKANA KESHO

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam kesho, Machi 7, 2019 inatarajia kutoa hatma ya ama kuendelea kusota rumande au kurudi uraiani kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni takribani miezi minne tangu viongozi hao  wafutiwe  dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 23, mwaka jana baada ya kukiuka masharti yaliyowekwa na mahakama hiyo

Uamuzi huo unatarajiwa  kutolewa na Jaji Sam Rumanyika, baada ya kusiliza hoja za pande zote, ambapo wakata rufaa, waliwakilishwa na Wakili Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya, huku upande wa ukiwa na jopo la mawakili watano wa Serikali, wakiongozwa na wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi, Paul Kadushi Salim Msemo, Wankyo Simon( mawakili wa Serikali) na Wakili Serikali Mwandamizi, Jakline Nyantori.

Jaji Rumanyika amesema amesikiliza hoja zao na uamuzi atautoa kesho saa saba mchana.

Wakiwasilisha hoja zao, wakili Kibatala amedai,  walikuwa na sababu nne za kukata rufaa, lakini baada ya Mahakama hiyo kuziondoa mbili zimebaki mbili, kwa hiyo watajikita katika hoja hizo na kudai kuwa Mahakama ya Kisutu ilifanya makosa kuwafutia dhamana Mbowe na Matiko wakati siku hiyo ambayo ilikuwa ni Novemba 23, 2018 washtakiwa wote walikuwepo mahakamani.
Amedai washtakiwa hao walifika mahakamani hapo bila hata ya kukamatwa licha ya kwamba kulikuwa na hati ya kukamatwa, waliingia mahakamani na kujieleza kuwa siku ambazo hawakuwepo walikuwa nje ya nchi na kwamba kama wateja wake hawafiki mahakamani basi siku hiyo wadhamini wao wanafika mahakamani hapo na kutoa  sababu, lakini cha kushangaza licha ya wadhamini hao kufika na kujileza bado dhamana ilifutwa.

Ameongeza kudai kuwa, mahakama ilikosea kuwafutia dhamana washtakiwa kwani hakukuwa na mantiki yoyote ya kufanya hivyo na hivyo wameomba Mahakama ilidhie ione hoja zao zina mashiko kisheria.

Pia Kibatala aliendelea kueleza kuwa, wakati Hakimu anatoa uamuzi huo wa kuwafutia dhamana hakukuwa na 'material' yoyote ambayo yaliiegemiza Mahakama kutoa uamuzi huo.

Katika suala la kiapo kilichowaailishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Dkt. Zainabu Mango katika Mahakama ya Kisutu, Kibatala anaeleza kuwa haikuwa sahihi kwa wakili huyo kuapa kiapo hicho  kwa niaba ya Jamhuri wakati na yeye ni mmoja wanaoendesha kesi hiyo, ambapo sheria hairuhusu kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Mtobesya alidai ni maoni yao kwa Mahakama Kuu, ikatengua uamuzi wa Mahakama ya Kisutu ili wateja wao warudi kufarahia haki yao ya msingi ya kuwa nje kwa dhamana, kwa sababu uamuzi wa  kuwafutia dhamana haukuwa sahihi.
Wakijibu hoja hizo, Wakili Nyantori  amedai kuwa hakuna hoja za msingi katika misingi ya kisheria ambazo zimewasilishwa na wakati rufaa ( Mbowe na Matiko), zitasababisha rufaa yao kukubaliwa, sababu ya kwamba washtakiwa walikuwepo siku hiyo ya Novemba 23,2018  ndiyo wasifutiwe dhamana, kutokana na kwamba walipewa haki yao ya msingi ya kujieleza na mahakama ikatoa uamuzi huo.

Nyantori alidai kuwa, Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo, baada ya kuwasikiliza wadhamini na washtakiwa wenyewe, ambapo Mbowe aliwasilisha na hati yake ya kusafiria ambayo  iliyoonesha jinsi alivyosafiri sehemu mbalimbali, kwa hiyo haikukosea katika uamuzi wake.

Aliendelea kudai kuwa mara kadhaa Mbowe na Matiko wamekuwa wakionywa na mahakama kwa kutofika mahakamani bila kutoa sababu za msingi.

Novemba 23, 2018 (Mbowe na Matiko) walifutiwa dhamana Mahakama ya Kisutu na siku iliyofuata wakiongozwa na Kibatala walikata rufaa kupinga maamuzi hayo.

Novemba 27, 2018, Jaji Rumanyika aliona kuwa rufaa hiyo imepelekwa chini ya hati ya dharura hivyo aliagiza mwenendo wa shauri upelekwe mahakamani hapo pamoja na wahusika wapande zote wafike.

Hata hivyo, Novemba 28, upande wa mashitaka na wa utetezi walifika mahakamani hapo na mapingamizi ya pande zote yalisikilizwa ikiwemo sababu nne za Mbowe na Matiko za kupinga uamuzi huo kwamba  mahakama haijawapa nafasi wadhamini ya kujieleza kwa mujibu wa sheria.

Pia walidai mahakama imekosea kuwafutia dhamana kwa sababu Novemba 12, 2018 Mbowe na Matiko walifika mahakamani bila kukamatwa na kuwa chini ya ulinzi.

Alidai masharti ya dhamana waliyopewa washtakiwa ni kinyume na sheria.

Hata hivyo, upande wa mashitaka uliomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa hiyo kwa sababu tatu ikiwemo warufani kushindwa kukata rufaa kupinga dhamana iliyotolewa na mahakama ya Kisutu na kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza rufaa  kwani taarifa ya kusudio la kukata rufaa imekosekana.

Baada ya Jaji Rumanyika kusikiliza mapingamizi hayo alikubaliana na hoja za upande wa serikali za kupewa mwenendo wa shauri hilo wa kesi ya msingi iliyopo Mahakama ya Kisutu uliochapishwa ambao unasomeka vizuri na sio kama ule waliopewa awali.

Pia alikubaliana na hoja ya pingamizi ya upande wa serikali  kuwa sababu mbili za rufaa za kupinga masharti ya dhamana, zinakiuka matakwa ya sheria kwa kuwa zimekatiwa rufaa bila kutoa kwanza taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga masharti hayo ya dhamana yaliyotolewa kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka jana.

Hata hivyo, baada ya mahakama kupanga kuanza kusikiliza rufaa hiyo, upande wa mashitaka alidai kuwa wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga maamuzi ya yaliyotolewa na kuiomba mahakama hiyo kuacha kuendelea kusikiliza rufaa hiyo kwa sababu haina mamlaka.
Viewing all 109935 articles
Browse latest View live




Latest Images