Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

FURSA ZAIDI ZATANGAZWA SEKTA YA KILIMO NA UWEKEZAJI

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu ametangaza fursa za kiuchumi ndani ya Tarafa ya Mihambwe kwenye sekta ya kilimo na uwekezaji.

Gavana Shilatu aliyasema hayo kwenye kikao kilichohusisha Madiwani, Watendaji kata, Watendaji Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji, Wazee maarufu, Maafisa na wadau wa maendeleo kilichofanyika Leo Jumatatu Machi 4, 2019 katika ofisi ya Mtendaji kata Mihambwe ambapo amewakaribisha Wadau wa maendeleo kutumia vyema fursa za kiuchumi zilizopo ndani ya Tarafa ya Mihambwe.

Gavana Shilatu amezitaja fursa hizo kwenye sekta ya kilimo ardhi ya Mihambwe inafaa kwa kilimo cha Korosho, Mahindi, Mihogo, Alizeti, Mbaazi na Njugu. 

Pia Gavana Shilatu amekaribisha wawekezaji wa viwanda vya kubangua Korosho waje wawekeze ndani ya Tarafa ya Mihambwe inayozalisha kwa wingi zao la Korosho.

Kama ambavyo Rais Dkt. John Pombe Magufuli anavyosisitiza Kauli mbiu ya "Hapa kazi Tu", Gavana Shilatu amewakaribisha Wadau wa maendeleo kuja kutumia vyema fursa zilizopo ndani ya Tarafa ya Mihambwe kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.


Tamasha la Utamaduni Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyika Tanzania.

$
0
0
Na Chalila Kibuda , Blog ya Jiamii


Watanzania wametakiwa kudumisha tamaduni zao ili zilete mvuto kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kukuza sekta ya utalii nchini kwa kuwa na tija ya maendeleo ya Taifa. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Maandalizi ya Tamasha la Nne la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Michezo, Utamaduni na Sanaa, Susan Mlawi amesemakuwa Tamasha limeandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (SADC) kwa lengo la kukuza sekta ya utalii nchini lakini pia kukuza lugha ya kiswahili katika nchi mbalimbali duniani.

Aidha Tamasha hilo litatoa fursa mbalimbali kwa wafanya biashara kuonyesha bidhaa zao ili kukuza uchumi wao.Tamasha litatoa hamasa kwa watanzania kuweka kipaombele katika utamaduni wao pasipo kuendeleza tamaduni za kigeni ambazo kwa sehemu zinaathiri tamaduni za kiafrika.

AmesemaTamasha litahusisha zaidi ya nchi sita(6) za Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda,Rwanda, Burundi na Sudani ya Kusini.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Taifa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Joyce Fisoo amesema kwenye Tamasha hilo kutakuwepo na maonyesho mbalimbali ikiwemo mafunzo kwa wadau mbalimbali, Ngoma za asili, Sanaa na michezo na filamu mbalimbali.Hivyo amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujionea fursa mbalimbali za kiuchumi na utajiri uliopo Afrika.

Fisoo amesema kuwa katika nchi wanaoshiriki wametakiwa kukata mshiki mmoja atakayepanda mlima Kilimanjaro.Kwa upande Kamishina Msaidizi wa Utamaduni wa Wizara ya Jinsia, Kazi na Maendeleo ya Jamii wa Uganda EuniceTumwebaze amesema kuwa amejifunza mengi katika tamasha lilifanyika nchini mwao lilipofungua fursa kwa vijana wa Uganda wasanii.

Amesema Tanzania nao waonyeshe umahiri katika tamaduni zao ikiwa ni pamoja na kutangaza utalii.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Tamasha la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fisoo akitoa maelezo kuhusiana walipofikia katika maandalizi ya tamasha la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Mchezo na Sanaa Susan Mlawi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na serikali ilivyojipanga katika kufanikisha Tamasha la Utamaduni litalonyika Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kamishina Msaidizi wa Wizara ya Jinsia, Kazi na Maendeleo ya Jamii nchini Uganda EuniceTumwebaze akizungumza kuhusiana na uzoefu wa tamasha lililopita nchini Uganda katika kuzunguka fursa kwa watu wa nchi hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Mchezo na Sanaa Susan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Tamasha la Nne la Utamaduni litalonyika nchini Septemba mwaka huu.

Serikali yawekeza nguvu miradi ya maji -Profesa Mbarawa

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

SERIKALI imesema kuwa hali ya upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 66 hivyo nguvu zaidi inatumika katika kuhakikisha inafikia asilimia 90 wakati mkoa wa Dar es Salaam ukiwa na asilimia 85 ya upatikanaji wa maji.

Hayo ameyasema Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakati akitangaza maadhimisho ya wiki ya maji ambayo hufanyika Machi 22 ya kila mwaka,amesema kuwa serikali imewekeza katika miradi ya maji katika kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Profesa Mbarawa amesema azimio la Umoja wa Mataifa ulizitaka nchi wanachama kuanzia mwaka 1993 kutenga siku hii kuwa siku maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma kuhusu sekta ya maji kwa njia mbalimbali, kama vile machapisho, mikutano, semina na maonesho. Lengo la maadhimisho haya ni kukuza uelewa kwa umma kuhusu umuhimu wa maji katika shughuli za uchumi, kijamii na maisha kwa ujumla.

Amesema maadhimisho hayo yamekuwa yakiadhimishwa siku ya maji duniani kwa kuandaa shughuli mbalimbali zinazochochea ushiriki wa umma katika kulinda na kuendeleza rasilimali za maji na Shughuli mbalimbali zikiwemo kwa njia ya mikutano, semina, warsha na maonesho. 

Mbarawa amesema maadhimisho ya siku ya maji yataanza Machi 16 na kuhitimishwa Machi 22 kwa Shughuli mbalimbali zikiwemo mikutano, warsha, semina, maonesho, pamoja na ukaguzi na uzinduzi wa miradi ya maji. 

Amesema katika siku ya maadhimisho ya wiki ya maji kutambua umuhimu wa kufikia malengo yaliyowekwa ya kupanua huduma ya maji ifikapo mwaka 2020, kauli mbiu ya siku ya maji ya mwaka 2019 imepangwa kuwa: “Hakuna Atakayeachwa: Kuongeza Kasi ya Upatikanaji wa Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa Wote katika dunia inayobadilika kitabia nchi. 

Aidha amesema pamoja na shughuli mbalimbali zitakazofanyika nchi nzima, ikiwemo ukaguzi na uzinduzi wa Mkutano wa kitaifa wa mwaka wa maji utakaoshirikisha wadau na wataalamu wa maji utakaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya St. Gaspar Jijini Dodoma.

Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Mafuta EWURA itazindua na kuwasilisha Ripoti ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini ya mwaka 2017/18; na kuwashirikisha wadau kuhusu shughuli za udhibiti katika Sekta ya Maji .

Katika kilele cha maadhimisho hayo kutakuw na Mkutano wa Mapitio ya Sekta ya Maji ni maalumu kwa wadau kutathmini utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) nchini.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Wiki ya Maji itakyofanyika kuanzia Machi 16 hadi 22.

Benki ya UBA yazindua shughuli Uingereza.

$
0
0
LONDON, UINGEREZA

WIKI tatu tu baada ya Kundi la Himaya ya Kibenki la United Bank of Africa (UBA Group) kuzindua shughuli zake nchini Mali, limefanya hivyo pia katika jiji la London, Uingereza.

Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa hafla maalumu Alhamisi iliyopita wakati jiji hili la kibiashara lilipokuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa kibiashara na sekta ya umma.

Katika hafla maalumu ya mkutano huo, UBA UK ilitambulishwa rasmi kwa viongozi wa kibiashara kutoka Ulaya na Afrika ikiwa na dhamira na utayari wa kuchochea biashara baina ya mabara hayo.

Kwa uzinduzi huo, UBA Group inazidi kujipanua katika sekta ya kibenki ikiwa kama taasisi ya kwanza na pekee ya kifedha kusini mwa jangwa la Sahara Afrika inayoendesha shughuli nchini Uingereza na Marekani.

Hilo linaifanya kuzidi kuitambulisha hadhi yake kama benki ya kidunia kutoka Afrika inayowezesha biashara na mtiririko wa mitaji baina ya Afrika na Dunia.

Akizungumza katika tukio hilo, Mwenyekiti wa UBA Group, Tony Elumelu alisema benki imefurahishwa na mamlaka za Uingereza kuiruhusu kuimarisha na kupanua operesheni zake na hivyo kutimiza dhamira yake ya kupanua biashara na uwekezaji baina ya Afrika na Ulaya.

Elumelu pia alieleza furaha yake kuona UBA kama benki kutoka Afrika inavyoweza kuchomoza na kusaidia wawekezaji katika miji muhimu ya kifedha duniani.

Akizungumza katika tukio hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa UBA Group, Kennedy Uzoka, alisema; “Wakati huo huo tunahudumia mahitaji ya kibiashara na mitaji kwa wateja wetu wa Afrika, ambao wanatafuta masoko Ulaya.

“Kwa kuzindua UBA UK Limited, tunafurahi kupanua huduma hizo kwa wateja wa sasa, wakati huo huo tukikaribisha wapya waweze kikamilifu kutimiza ndoto zao za kifedha kupitia mtandao wetu wa kibenki.”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Uingereza, Patrick Gutmann, Mkurugenzi Mtendaji, UBA Plc, Kennedy Uzoka, Rais Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote, Mwenyekiti wa UBA Group, Tony Elumelu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wakati wa uzinduzi wa UBA London nchini Uingereza.

WASHIRIKI KILI MARATHON TAKRIBANI 4, 000 WATIBIWA BURE

$
0
0
Kampuni ya huduma za afya nchini, AAR Healthcare imepongezwa kwa kuwahudumia bure washiriki takribani 4,000 wa Kili Marathon iliyofanyika Jumapili iliyopita wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

AAR Healthcare ilitoa huduma za uchunguzi wa afya za washiriki, huduma ya kwanza pamoja na huduma ya gari la wagonjwa (standby ambulance service).

Meneja wa Kampuni hiyo Mkoani Arusha, Dkt. Aggrey Mapunda aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutokana na uzoefu wao katika ushiriki wa Kili Marathon, wamebaini kuwepo changamoto ya washiriki kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa kufanya uchunguzi wa afya zao kabla ya kushiriki, suala ambalo alilielezea kuwa wamelifanyia kazi katika tukio la mwaka huu ili washiriki wawe na uhakika wa afya zao na hivyo kuepuka madhara hasi.

“Kitaalam, washiriki wote wa mbio wanapaswa kuchunguzwa afya zao, na sisi kama kampuni inayotoa huduma bora za afya tunaamini ni jukumu letu kutoa elimu inayohitajika pamoja na kuwapa huduma hiyo bure ili kuwahamasisha kuwa na utamaduni huo katika maisha yao ya kawaida,” alisema Dkt. Mapunda.

“Tunafahamu kuwa ajali na dharura za aina mbalimbali hutokea katika kipindi kama hiki, na hii ndio sababu imetufanya kutoa huduma ya gari la wagonjwa ambalo liko tayari muda wote kutoa huduma hapa, nalo pia tumelitoa bure,” aliongeza.

Aidha, Lydia Nasimiyu, mshiriki wa Kili Marathon kutoka Kenya ambaye ni mmoja kati ya waliofaidika na huduma ya afya bila malipo ya AAR aliizungumzia huduma hiyo na kuwapongeza kwa hatua waliyoichukua.

“Ningependa kuwashukuru AAR Healthcare kwa msaada wao wa huduma ya afya walionipa. Kweli nilipata huduma kwa muda. Ninashukuru wamekuwa hapa kuhakikisha washiriki tunapata huduma hii muhimu,” alisema Nasimiyu na kuongeza, “ningependa pia kuwapongeza kwa hiki walichokianzisha ili wengine pia waige kwa mafufaa ya wote na ninaamini huduma ya matibabu ni muhimu sana kwenye kila mashindano ya mbio (Marathon).

Mbali na huduma hiyo, AAR Healthcare pia ni moja kati ya wadhamini wakuu wa Kili Marathon, na mwaka huu umekuwa mwaka wa pili kwao kudhamini tukio hilo.

“Tumekuwa tukifanya kazi na Kili-Marathon tangu mwaka jana kwa lengo la kufikisha kwa usahihi huduma bora za afya kwa watu. Na kwakuwa sisi ni wadau muhimu kwenye sekta ya afya na michezo, tunaamini kula vizuri na kwa usahihi pamoja na kufanya mazoezi ni kitu bora kwa afya ya kila mmoja wetu. Hivyo, tutaendelea kutoa mchango wetu na kuunga mkono kwa vitendo Kili Marathon kwa ajili ya kuhuisha afya bora,” alisema Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa AAR Heathcare, Doscar Massaba.

Takribani watu 9,000 kutoka nchi mbalimbali walijiandikisha kushiriki kwenye Kili Marathn 2019, kwa mujibu wa tovuti ya waratibu wa mashindano hayo.

Kili Marathon imekuwa huhudhuriwa na watu wa nchi takribani 45 duniani kote na imekuwa chachu ya kuibua vipaji, kuchangia huduma za kijamii, kuongeza pato la nchi, kutangaza utalii na kuhamasisha mazoezi kwa afya bora ya jamii.

RC Dkt Kebwe:Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa.

$
0
0
Andrew Chimesela - Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Mkoa na Wilaya ya Kilosa kuwakamata wale wote wanaotuhumiwa kuwavamia wananchi wanaolima  katika mashamba yaliyofutiwa umiliki wake na Mhe. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dkt. Kebwe ametoa kauli hiyo Machi, 3 Mwaka huu alipofanya ziara Wilayani Kilosa iliyolenga kujiridhisha utekelezaji wa mashamba yaliyofutwa mwaka 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na kuagiza mashamba hayo kupangiwa matumizi mengine ikiwa ni pamoja na kuyagawa kwa wananchi wa maeneo jirani na mashamba hayo.
Akiwa Wilayani Kilosa, Dkt. Kebwe aliongea na wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe ambavyo viko jirani na shamba hayo matano kati ya 11 yaliyofutiwa umiliki Wilayani humo huku wananchi waliopewa kuyatumia kwa muda wakilalamika kupewa vitisho na baadhi ya watu kutojihusisha kulima mashamba hayo kwa madai kuwa ni mali yao.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro baada ya kupokea malalamiko hayo anaagiza Jeshi la polisi kuwakamata wale wote wanaowatishia wakulima hao. “Na hili naelekeza  Vyombo vya Ulinzi na Usalama, muanze kupekua kuanzia sasa, kama kuna kikundi cha watu kuna watu au hata mtu binafsi kafanya hivyo chukua hatua, kwa sababu sheria zipo” alisema  Dkt. Kebwe. 
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa aliwahakikishia wananchi wa vijiji hivyo kuwa kila mtu ambaye hana eneo la kulima atapatiwa kupitia mashamba hayo yaliyofutwa na Mhe. Rais ili kila mwananchi aweze kuzalisha na kujikimu kimaisha huku akionya kutoingiza itikadi ya aina yoyote kwenye mashamba hayo yaliyofutwa na Mhe. Rais.

Katika hatua nyingine Dkt. Kebwe amewataka wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe, kufuata utaratibu uliotolewa na Serikali wa kuyatumia mashamba hayo kwa muda wakisubiri mpango rasmi unaoendelea kuandaliwa na Serikali huku akiwaonya wanaotaka kuanzisha mipango mingine ya matumizi ya Ardhi hiyo  kinyume na mipango ya Serikali kusitisha mara moja mipango hiyo.
“Vyombo vyangu vinaniambia wale walikwenda wakavamia maeneo hayo walitaka waanzishe  mpango mwingine mpya, yaani juhudi zote hizi ambazo Serikali imefanya kwake yeye  si kitu. sasa hao mtusaidie tuwafahamu ni akina nani na tuwachukulie hatua, sio kuwafahamu tu” aliongeza Dkt. Kebwe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amewataka wananchi wa vijiji vya Mvumi na Gongwe kukomesha tabia ya ubishi na ugomvi baina yao, badala yake watekeleze maagizo ya Serikali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na kuwatahadhalisha kuwa atakayekwenda kinyume na maagizo hayo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za sheria.
Awali Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Kati, Hezekiely Kitilya aliewaeleza wananchi wa vijiji vya Mvumi na Gongwe kuwa Ardhi ya mashamba hayo matano kwa sasa bado ni ya Mhe. Rais na iko chini Kamishna wa Ardhi na wananchi wamepewa kuitumia kwa muda, hivyo ni vema wananchi wakawa watulivu na kuacha ugomvi baina yao.
Sambamba na hilo Bw. Kitilya aliwakumbusha wananchi maelekezo yaliyotolewa na ya Mhe. Rais mara baada ya kuyafuta, ambapo alisema kipaumbele cha kwanza kinawalenga  wananchi wanaozunguka mashamba hayo, cha pili ni kutenga Ardhi hiyo kwa ajili ya Uwekezaji wenye tija wa ndani na nje ya nchi na kuwa na hazina ya Ardhi kwa ajili matumizi mengine ya baadae.
Kwa mujibu wa Afisa Ardhi Wilaya ya Kilosa Bw. Ibrahim Ndembo, alisema Mashamba hayo matano Na. 32 hadi 36 yenye jumla ya Ekari 2,685, baada ya Mhe. Rais kuyafuta, Wilaya ilipeleka maombi Serikalini ili kupewa idhini ya kutumia mashamba hayo kwa muda ombi ambalo lilikubaliwa.
Baada ya kukubaliwana Wilaya iliunda Kamati za ugawaji maeneo ya mashamba hayo na kuyagawa katika sehemu mbili, Ekari 1000 kwa ajili ya wananchi wa Kijiji cha Mvumi na Ekari 1000 nyingine kwa ajili ya kijiji cha Gongwe. Hii inatokana na asili ya vijiji hivyo ambavyo awali kilikuwa ni kijiji kimoja na mwaka 2014 kiligawanyika na kuwa vijiji viwili, Mvumi na Gongwe.
Kwa upande wao Wananchi wa vijiji hivyo akiwemo Bi. Lakero Mkandawile wa kijiji cha Gongwe na Bi. Sara Seleman wa Kijiji cha Mvumi pamoja na Adhi Valaluke wa Kijiji cha Gongwe walimweleza  Mkuu wa Mkoa kero zao kuhusu mashamba hayo ikiwa ni pamoja na kupewa maeneo ya kulima kwenye mashamba ambayo tayari yana watu, kunyang’anywa mashamba waliokwisha pewa na kutishiwa kukatwa na mapanga tuhuma ambazo zilimhusisha pia Mwenyekiti wa Kijiji cha Mvumi Bw. Abdul Tumbo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiongea na wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe Wilayani Kilosa Mkoani humo kuhusu matumizi ya mashamba matano yaliyofutiwa Umiliki na Dkt. John Pombe Magufuli.
Umati wa Wananchi kutoka Vijiji vya Mvumi na Gongwe waliofika kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuhusu matumizi ya Ardhi ya mashamba matano yaliyofutiwa Umiliki na Dkt. John Pombe Magufuli .
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adamu Mgoyi (anayeongea na kipaza sauti) akiwaonya wananchi kufuata maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa kuhusu utaratibu wa kuyatumia mashamba yaliyofutiwa umiliki wake.

NEC, VIONGOZI VYAMA VYA SIASA WAKUTANA KUJADILI MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2020

$
0
0

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage akifungua mkutano kati ya tume hiyo na viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 unaofanyika kwenye ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchuguzi (NEC), Athuman Kihamia akitoa utangulizi wa majadiliano katika mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchuguzi (NEC), Athuman Kihamia kutoka kulia wakiwa pamoja na viongozi wengine wa tume ya uchaguzi katika kutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam.
Picha zikionyesha wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya siasa wakiwa katika mkutano huo leo.
 

*Mwenyekiti NEC aelezea mwenendo wa maandalizi,vituo vya kupiga kura vyaongezeka

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imekutana na viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 huku ikielezwa kuwa vituo vya kupigia kura vimeongezeka ikilinganishwa na vituo vilivyotumika mwaka 2015.

NEC na viongozi hao wa vyama vya siasa wamekutana leo Machi 5,2019 jijini Dar es Salaam ambapo kwa sehemu kubwa watatumia mkutano huo kujadili namna ya kuboresha  Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, pia mchakato wa uchaguzi mkuu ili kuhakikisha unakuwa huru na haki.

Akizungumza mbele ya viongozi wa vyama vya siasa , Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Semistocles Kaijage amesema wadau na watanzania wanafahamu kuwa nchi yetu ipo katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 .

Amesema NEC imeanza maandalizi ya  mchakato wa kuboresha  Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwa ni mkakati wa kujiandaa na Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwaka 2020.

"Katika maandalizi hayo ,Tume chini ya Ibara ya 74(6) ya Katiba ya nchi yetu ya mwaka 1977 imepewa mamlaka ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya msingi ikiwa ni pamoja na jukumu la kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge pamoja na uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara," amesema.

Amefafanua kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ,sura ya 324 na ya kifungu cha 21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa sura ya 292 ,Tume inapaswa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mara mbili katika Uchaguzi Mkuu mmoja na uchaguzi mwingine unaofuata.

"Napenda kuwataarifu ,Tume inaendelea na maandalizi ya kuboresha Daftari ambapo mpaka sasa tayari imekamilisha baadhi ya michakato kama vile uhakiki wa vituo vya kujiandikisha ,maandalizi ya vifaa vya uboreshaji daftari na mkakati wa elimu ya mpiga kura," amesema Jaji Kaijage.

Ameongeza mchakato wa uhakiki wa vituo lililenga kuona kama kuna haja ya kuongeza vituo katika baadhi ya maeneo, vituo vilivyopo kama bado vinakidhi matakwa ya kisheria na kufanya marekebisho mengine kama kubadilisha majina ya vituo au kurekebisha majina ya vituo yaliyokosekana.


Jaji Kaijage amesema matokeo ya uhakiki huo kwa Tanzania Bara yanaonesha kuwa vituo vya kuandikisha wapiga kura vimeongezeka kutoka vituo 36,549 vilivyotumika kuandikisha wapiga kura mwaka 2015 hadi vituo 37,407.Vituo 6,208 vimebadilishwa majina na vituo 817 vimehamishwa kutoka Kijiji/ Kata mmoja kwenda kata nyingine.

"Matokeo ya uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura kwa Tanzania Zanzibar yanaonesha kuwa vituo vimeongezeka kutoka 380 hadi vituo 407 na kwamba wadau watapewa orodha ya vituo vya kuandikisha wapiga kura kabla kuanza kwa mchakato wa daftari la kudumu la wapiga kura," amesema.

Kuhusu vifaa kwa ajili ya uboreshaji wa daftari hilo ,Jaji Kaijage amesema mchakato wa kupata vifaa vya kukarabati mashine za BVR umekamilika na kinachosubiriwa ni kufanyia majaribio ya uandikishaji katika kata mbili za Kihonda iliyopo Manispaa ya Morogoro na Kata ya Kibuta iliyopo wilayani Kisarawe.

Amefafanua ni kawaida kabla ya kuanza kwa mchakato wa uandikishaji ,hufanyika majaribio ili kuona namna na jinsi vifaa vya uandikishaji vinavyofanya kazi katika mazingira tofauti ,lengo likiwa ni kupata na kuwa na namna  bora ya kufanikisha mchakato huo.

 Ameongeza maandalizi mengine ambayo tayari yamefanyika ni uchapishaji wa miongozo mbalimbali kwa wadau ikiwemo ya kutoa elimu kwa mpiga kura na maelekezo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ,kwa watendaji na wadau wa uchaguzi vikiwemo vyama vya siasa.

Pamoja na mambo mengine Jaji Kaijage amesema Tume imejiwekea utaratibu wa kuwashirikisha wadau katika hatua mbalimbali za uchaguzi ,kwa lengo la kuhakikisha inajenga na kutekeleza misingi ya kidemokrasia katika kusimamia ,kuratibu na kuendesha chaguzi zilizo huru ,wazi ,za haki na kuaminika.

"Madhumuni ya kukutana kwetu leo ni kuwafahamisha kuwa Tume imekamilisha jukumu lake la kuhuisha na kuboresha kanuni ambazo ziliandaliwa chini ya sharia hizo mbili mwaka 2008.

" Tume imeona ni vema ikawapitisha katika kanuni hizo kwa kuangalia Yale maeneo ambayo yamefanyiwa marekebisho ama kwa kuondoa au kuongeza vifungu lakini kwa kueleza sababu za marakebisho hayo,"amesema Jaji Kaijage.
 

340 Wakutwa na Maambukizi ya VVU Magerezani

$
0
0
Jumla ya wafungwa na mahabusu 15,250 nchini wamepima Virusi vya Ukimwi huku 340 wakikutwa na maambukizi baada ya Jeshi la Magereza wakishikiana na Wizara ya  Afya  kutoa elimu ya Upimaji katika Magereza mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akiwasilisha Taarifa Kuhusu Hali ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Upatikanaji wa Tiba ya Magonjwa Nyemelezi na Udhibiti wa Biashara na Matumizi ya Dawa za Kulevya Magerezani kwa mwaka ulioisha.

Akisoma taarifa  hiyo  mbele  ya  Kamati  ya  Kudumu  ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI iliyofika katika Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira mkoani Morogoro, Naibu Waziri Masauni alisema kati ya mahabusu na wafungwa waliopima wanaume waliokutwa na maambukizi ni 292 na wanawake ni 48

“Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Wizara ya Afya wanahakikisha huduma za afya zinaboreka magerezani ikiwemo lishe nzuri kwa  wanaothibitika wana maambukizi huku jumla ya wafungwa na mahabusu wanaotumia dawa za kufubaza  makali wakiwa 1,496” alisema Naibu Waziri Masauni

“.. elimu ya kifua kikuu na upimaji inatolewa kila siku Magerezani kwa wafungwa na mahabusu, kwa mwaka jana jumla ya waliopima ni 12,870 huku waliobainika na maambukizi ni 167 na tunashirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) kwa kuandaa Mpango Mkakati wa UKIMWI na kifua Kikuu kwa miaka mitano.” Aliongeza Masauni

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kuwatembelea wafungwa katika Gereza la Kingolwira  Wajumbe wa  Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI , walilipongeza Jeshi la Magereza kwa kuwahudumia mahabusu na wafungwa wanaoishi na maambukizi magerezani huku wakitoa wito kwa wafungwa walioathirika kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao kuhusiana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Akizungumza mbele ya kamati hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Afya na Lishe wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Dkt.Hassan Mkwiche alisema magereza yana utaratibu wa kupima afya za mahabusu au wafungwa siku ya kwanza tu anayoingia gerezani  ikiwemo ujauzito, Ukimwi, kifua kikuu na magonjwa mengine ili waweze kuhudumia kila mfungwa na mahitaji yake.

“Mfungwa anapoingia humu anaenda kukutana na kazi mbalimbali kwahiyo ni muhimu kujua afya ya kila mmoja tangu siku ya kwanza anaingia ili kuweza kumpangia majukumu kulingana na afya yake lakini pia aina ya mlo anaotakiwa ale akiwa kifungoni” alisema Dkt. Mkwiche.

Juhudi mbalimbali za kuboresha afya za wafungwa magerezani  zinaendelea huku Wizara ikiendelea  kuboresha vituo vya kutoa huduma za afya ambapo mwaka 2018 zahanati ya Gereza Mahabusu mkoani Morogoro ilikamilika na imeshaanza kufanya kazi huku gharama za ujenzi zikiwa ni fedha za ndani za serikali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiwaongoza Wajumbe wa  Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi,walipowasili katika Gereza la Wanawake Kingolwira Mkoani Morogoro kuzungumza na wafungwa ikiwa ni ziara ya kufuatilia utekelezaji wa serikali.Picha na  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WAZIRI LUGOLA AONGOZA KIKAO CHA TUME YA JESHI LA POLISI, MAGEREZA NA UHAMIAJI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (meza kuu katikati) akiongoza kikao cha Tume ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Kiutumishi na Kiutendaji wa Askari katika Majeshi hayo, katika  Ukumbi wa Ofisi ndoo ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto Meza Kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimuapisha Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Hilda Tegwa kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa Askari wa Majeshi hayo, katika Ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (meza kuu katikati) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu (kulia), alipokuwa anamfafanulia jambo katika kikao cha Tume ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Kiutumishi na Kiutendaji wa Askari katika Majeshi hayo. Kikao hicho kilifanyika, ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto Meza Kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

BRELLA KUSAINI MOU NA TAMISEMI KWA AJILI KUSOGEZA HUDUMA ZA USAJILI KARIBU NA WANANCHI

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
WAKALA  wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELLA) inatarajia kuingia makubaliano na Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kwa ajili ya kuona jinsi ya kuwatumia Maafisa Biashara wa Halmashauri ili kusogeza karibu huduma za usajili wa majina na nembo za biashara kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa BRELLA Bakari Mketo wakati wa semina ya siku moja iliyowahusiasha Maafisa Biashara, Maendeleo ya Jamii, Wanasheria, , SIDO na TCCIA mkoani Tabora. Alisema lengo la BRELLA ni kumuondolea usumbufu mwananchi anayetaka kusajili jina la biashara na nembo ya biashara yake katika mazingira yaliyo karibu yake badala ya kusafiri kwenda Dar es salaam na wakati mwingine kukutana na vishoka ambapo wanamuibia fedha zake.

Mketo alisema wameamua kuangalia uwezekano wa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kuwa ziko karibu na wananchi wengi na baadhi ya shughuli za kila siku za Maafisa biashara ni pamoja na kukutana na wafanyabaishara. Alisema baadhi ya wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa wamekuwa hawanufaiki na kazi zao kwa sababu ya kushindwa kusajili na kuwa na nembo ya biashara zao.

Mketo alisema wanapotekea wajanja wachache wanatumia nembo zao ambao hazijasajiliwa kwenda kusajili na kisha waanzirishi kubaki maskini na kushindwa kisheria kwa sababu walichelewa kujisajili. Aidha alisema BRELLA pia imeanzisha mfumo mpya wa kusajili biashara na nembo za wafanyabiashara kupitia Mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao(ORS) ambapo mtu aweza kujisajili sehemu yoyote ambapo simu yake ina huduma ya  tovuti.

Alisema wameamua kutumia njia hiyo ili kupunguza urasimu kwa wananchi wa kuwataka kwenda Dar es salaam ndio wasajili nembo za biashara zao. Naye Afisa kutoka BRELLA Suzan Senso alisema ili mtu asajili nembo ya biashara yake atapaswa kuwa na kitambulisho cha Taifa.

Kwa upande wa Mfanyabisahara kutoka Sikonge Faibeti Michael alisema elimu waliyopatiwa itawasidia kulinda haki za nembo za biashara zao na pindi akitaka kuitumia itabidi alipwe na hivyo kunufaika. BRELLA watembelea maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuwaelimisha mfumo mpya wa usajili wa biashara na nembo.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Wakala  wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELLA)  Bakari Mketo akitoa elimu leo kwa Maafisa Biashara, Maendeleo ya Jamii, Wanasheria, , SIDO na TCCIA mkoani Tabora juu ya umuhimu wa kusajili majina ya biashara na nembo za biashara.

Serikali Yajipanga Kuziwekea Mikataba Taasisi Zake

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Serikali kupitia wizara ya maji imejipanga kuleta utaratibu wa kuziwekea mikataba ya utendaji kazi taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo ili kuimarisha usimamizi wa sekta ya maji katika ngazi mbalimbali nchini.

Hayo yamezungumzwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa wakati alipokuwa akifungua mkutano uliowahusisha  Makatibu Tawala wa Mikoa nchini kwa ajili ya kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu uendeshaji mpya wa sekta ya maji kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Sheria Namba 5 ya mwaka 2019.

Prof. Mbarawa amesema kuwa wizara imeamua kuja na mikataba hiyo itakayokuwa na malengo maalum ya kuzipima taasisi kwa kila mwaka mmoja ambapo nia ya serikali sio kumkomoa mtendaji bali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyokusudiwa.

“Mamlaka hizi zikisimamiwa kwa malengo zitafanya kazi vizuri zaidi na zitakuwa na uwezo mkubwa wa kujiendesha pia kupimana utendaji kazi ni jambo zuri kwa sababu tukifanya kazi kimazoea mamlaka na taasisi zetu hazitoweza kufanya kazi vizuri wala kuimarisha utoaji wa huduma za maji safi na salama kwa wananchi wetu,” amesema  Prof. Mbarawa.

Ameendelea kusema kuwa, mkutano huo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Magufuli alilolitoa mwezi Mei, 2018 kuhusu mfumo wa uendeshaji wa sekta ya maji ambapo aliagiza sekta ya maji isimamiwe na wizara moja ili kurahisisha usimamizi na uwajibikaji wa watendaji.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Kitila Mkumbo amefafanua kuwa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Namba 12 ya mwaka 2009 imepitiwa na kutungwa upya na kwa sasa inajulikana kama Sheria ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019 ambapo kikubwa katika sheria hiyo ni kuanzishwa kwa Wakala wa Maji Vijijini.

“Haitawezekana kukamilisha mipango ya sekta ya maji bila ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo kupitia mkutano huu Makatibu Tawala watapata nafasi ya kupitia na kuielewa sheria mpya kwa kina na kubaini nafasi zao katika usimamizi na uendeshaji wa sekta ya maji kwenye sheria hii," amesema Prof. Mkumbo.

Kuanza kutumika kwa sheria hiyo mpya kutaimarisha mfumo wa utoaji huduma za maji na usafi wa mazingira nchini, kutaongeza ufanisi na uwajibikaji katika kutoa huduma za maji, kutaimarisha ujenzi na usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji, kutachochea utendaji katika sekta  nyingine na kuongeza mchango wa sekta ya maji katika uchumi wa nchi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa nchini (hawapo pichani) walioshiriki katika mkutano wa kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu uendeshaji upya wa sekta ya maji kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Sheria Namba 5 ya mwaka 2019. Ufunguzi huo umefanyika leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akizungumza wakati akifungua mkutano uliowahusisha Makatibu Tawala wa Mikoa nchini kwa ajili ya kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu uendeshaji upya wa sekta ya maji kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Sheria Namba 5 ya mwaka 2019. Ufunguzi huo umefanyika leo Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Makatibu Tawala wa Mikoa nchini, Mama Rehema Madenge akitoa neno la shukrani baada ya Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa kufungua mkutano huo.
 Baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa nchini na wafanyakazi wa Wizara ya Maji waliohudhuria katika mkutano huo.

MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO YAJIPANGA KUJENGA BARABARA YA KILOMETA 88

$
0
0
 Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Dk. Fredy Manongi akitoa maelekezo kwa wasaidizi wake alipokuwa akizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara ya Kilometa 88 zitakazojengwa kwa kiwango cha tabaka gumu la Zege kuanzia geti la kuu la Lodware hadi goloni ulipo mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
 Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Dk. Fredy Manongi akizungumza na wahabari kuhusu kuendelea kwa mchakato wa ujenzi wa barabara ya kilometa 88 kwa kiwango cha tabaka gumu la Zege kuanzia geti la kuu la Lodware hadi goloni ulipo mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


Sehemu ya barabara inayotelemka Kreta ta Ngorongoro yanayoendelea kufanyiwa matengenezo ikiwamo maandalizi ya kuwekewa mawe ili kurahisisha usafiri kwa magari na watalii wanaotelemka kuangalia vivutio mbalimbali vya utalii  

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAZUNGUMZIA MVUA ZA MASIKA

$
0
0
Na Karama Kenyuko, Globu ya jamii 

MAMLAKA ya Utabiri wa Hali ya Hewa(TMA) imetoa utabiri wa mvua za masika ambazo tayari zimeanza kwa baadhi ya mikoa na zitaendelea kunyesha hadi mwaka huu. 

Taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyoitoa leo jijini Dar es Salaam imesema utabiri wa mvua za masika (MAM) 2019 ni kwamba kuanzia wiki ya nne ya Februari katika mikoa ya Kagera mvua itanyesha na kusambaa katika mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga,Simiyu,Kigoma Kaskazini na Mara wiki ya pili ya Machi 2019. 

Mvua hizo kwa baadhi ya meeneo zitakuwa juu ya wastani hadi wastani na kwamba mvua za msimu 2018,2019 zinaendelea hadi Aprili mwaka huu.Kwa mujibu wa TMA ni kwamba mvua zitaisha wiki ya kwanza ya Mei mwaka huu. 

Pia kuanzia kati ya wiki ya nne ya Februari na wiki ya kwanza ya Machi 2019 mvua itanyesha katika maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani ,Visiwa vya Unguja na Pemba na kusambaa maeneo ya mikoa ya Tanga na Morogoro Kaskazini ifikapo wiki ya kwanza ya Machi 2019 na itaisha wiki ya nne ya Aprili 2019.

Serikali Yajipanga Kuziwekea Mikataba Taasisi Zake

SWAHIBA WA LOWASSA, KHAMISI MGEJA KESHO KUZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MUSTAKABALI WA NCHI, DEMOKRASIA

$
0
0
*Ni yule aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga aliyeondoka na Lowassa kwenda upinzani

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWANASIASA Mkongwe na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja baada ya ukimya wa muda mrefu amesema kesho Jumatano ya Machi 6, 2019 atazungumzia mustakabali wa nchi na mwenendo wa demokrasia nchini Tanzania.

Hamis Mgeja ni mmoja wa marafiki wakubwa wa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambapo wakati alipoamua kwenda upinzani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Mgeja naye aliamua kumfuata na aliacha nafasi zake zote ndani ya CCM na kisha kuungana na  Lowassa upinzani.

Taarifa yake iliyotolewa katika  vyombo vya habari  jijini Dar es Salaam Mgeja amesema kuwa amekuwa nje ya ulingo wa siasa kwa muda mrefu na katika kipindi chote alijikita kwenye shughuli za kilimo lakini kesho (Jumatano) amejipanga kuzungumza na  Watanzania kupitia vyombo vya habari kuhusu mustakabali wa nchi katika nyanja mbalimbali pamoja na demokrasia.

"Mimi Khamisi Mgeja kesho Jumatano ya Machi 6 , 2019 , kuanzia saa 4:30 asubuhi nitaongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam. Nataka kuzungumza hali ya nchi yetu katika nyanja mbalimbali ikiwemo eneo la demokrasia nchini kwetu,"amesema Mgeja na kutoa mwito kwa waandishi wa habari kujitokeza kwa wingi ili kupata nafasi ya kumsikiliza na kisha kumuuliza maswali.

Hata hivyo haifahamiki iwapo Mgeja naye atatangaza kurudi CCM au laa hasa kwa kuzingatia kuwa Lowassa ambaye ni rafiki yake mkubwa tayari amerejea nyumbani (CCM),  mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu leo , Mgeja amesema hiyo kesho ndio itakuwa siku ya pekee kwake kutoa ya moyoni , hivyo  Waanzania watapata nafasi ya kumsikia kile ambacho amepanga kukizungumza.

Alipoulizwa iwapo naye atarejea CCM, Mgeja amejibu "Hiyo kesho nitakuwa na nafasi ya kutosha kuhusu mambo mbalimbali, hivyo hilo swali lako nitalijibu kesho ambayo nimepanga kuzungumzia mustakabali wa nchi yetu."

KAMATI YA BAJETI YA BUNGE YATEMBELEA KIWANDA CHA TANELEC ARUSHA, WAPOKELEWA NA WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI

$
0
0
 Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene wakimsikiliza Mkurugenzi mkuu wa TANELEC Zahir Saleh akiwaeleza kuhusiana na utendaji, uzalishaji katika kiwanda hicho
 Mkurugenzi wa TANELEC akiendelea kuelezea utendaji wa kazi katika kiwanda hicho
Kutoka kulia ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Mwenyekiti wa kamati ya bajeti ya Bunge George Simbachawene, Mkurugenzi mkuu wa TANELEC  Zahir Saleh wakibadilishana mawazo na baaadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge
 Mmoja wa wafanyakazi wa TANELEC akionyesha vikombe vya kupitishia nyaya na kupunguzia umeme mara unapopita
Mmoja wa wafanyakazi katika Kiwanda cha TANELEC akisuka Transfoma kama inavyoonekana katika picha. 
 Mkurugenzi mkuu wa TANELEC Zahir Saleh ufafanuzi mbele ya waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani pamoja na Kamati ya bajeti ya bunge kama wanavyoonekana pichani
 Mwanamama huyu akiwa anapanga sumaku zinazokaa ndani ya transfoma kama anavyoonekana ambapo kwa siku huwa anapanga mbili ila inategemea size
 Wafafanyakazi wakiwa katika hatia za awali wa kusuka transfoma kama wanavyoonekana katika picha 
 Taransfoma ikiwa katika hatua ya kukamilishwa kama inavyoonekana katika picha
 Transfoma ikiwa imeshakamilika na ipo kwa ukaguzi wa mwisho kupitishwa ili iingie sokoni
Transfoma zikiwa zimekamilika zikiwa tayari kuingia sokoni kwa matumizi. Picha zote na Vero Ignatus. 


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha kutengeneza Transfoma cha TANELEC kilichopo Njiro Jijini Arusha 


Na. Vero Ignatus, ARUSHA




Kamati ya kudumu ya  bajeti  Bunge  imetembelea kiwanda cha kutengeneza  Transfoma cha Tanelec ikiwa  na lengo la kuona utendaji, uzalishaji, pamoja maendeleo ya kiwanda hicho




Ugeni huo umepokelewa na Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani,ambapo amesema  lengo la serikali ni kuhakikisha inawezesha viwanda vya ndani ili viweze kupiga hatua na katika kufanikisha kufikia uchumi wa kati.




Dkt. Kaleman amesema  kiwanda hicho kwa kushirikiana na serikali kimefanya jitihada za kukifufua na kufanikisha uongezaji wa uzalishaji  unapanda toka mwaka  2016 walipokuwa wakizalisha Transfoma 7,000, mwaka 2017 Taransfoma 10,000  na sasa 14,000.




Ongezeko hilo la Transfoma ni kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza uchumi wa nchi kufikia wakati kupitia sekta viwanda ambavyo vingi vinatumia umeme.




Hata hivyo serikali imekipongeza kiwanda cha kuzalisha Transfoma cha Tanelec kilichopo Jijini hapa kwa kuongeza uzalishaji wa Transfoma kutoka 7,000 hadi 14,000 kwa kipindi cha mwaka jana.




Akitoa pongezi hizo leo mbele ya kamati ya Bunge ya Bajeti,Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani, alisema uzalishaji huo unawezesha uanzishwaji wa viwanda na kuchangia kukuza ajira.




Aidha alisema kuimarika kwa kiwanda hicho na msimamo wa Rais John Magufuli wa kutaka watanzania kujenga utamaduni wa kupenda vitu vinavyozalishwa nchini kumesaidia kuepuka gharama iliyokuwa ikitokana na uagizaji Taransfoma nje ya nchi.




"Kupitia kiwanda chetu gharama za usafirishaji,muda wa kutumia kusubiri kuletwa na bado zikija sio bora kama zetu tumeachana nazo,"alisema




Aidha alisema kufikia kwa hatua hiyo kumeleta maumivu makubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao walikuwa wakinufaika na uagizaji Tarnsfoma hizo nje ya nchi.




Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene aliahidi kumpa ushirikiano Waziri katika kulisimamia hilo ili kukipa nguvu zaidi kiwanda hicho na vingine nchini.




"Nikupongeze Waziri kwa kusimamia wazabuni katika sekta ya nishati kutumia bidhaa za ndani,natambua siasa za wafanyabiashara kuna wakati zilikupa wakati mgumu ukabaki peke yako endelea kusimamia uamuzi huu sisi tupo nyuma yako kukulinda,"alisema




Akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa mjumbe wa kamati ya Bunge kuhusiana na umeme kupanda na kushuka Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka amesema inaweza kuwa ni matatizo ya kiufundi katika mifumo ya umeme wala haihusiani na Transifoma




Amesema yapo maeneo mengi ambayo TANESCO wanahitaji AVR ili umeme uweze kwenda kwa wateja ukiwa mzuri




Kuhusu ombi la Mkurugenzi wa kiwanda cha Tanelec  Zahir Saleh la kutaka Transfoma zinazoingia nchini kutozwa asilimia 40 atalisemea bungeni.




Mkurugenzi wa kiwanda cha Tanelec,Zahir Salehe ameomba bunge na serikali kutoza bidhaa za nje zinazoingizwa nchini hususanibTaransfoma ili kulinda bidhaa za ndani.




Amesema kwa upande wao wameweza kutoa gawio kwa serikali  Sh. Milioni 500 kwa mwaka jana.

RC SHINYANGA ATAMBULISHA MRADI WA 'BADILISHA TABIA TOKOMEZA MALARIA'

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack ametambulisha rasmi mradi wa 'Badilisha Tabia Tokomeza Malaria' unaotekelezwa na asasi ya T- MARC Tanzania kwa ajili ya kazi za uhamasishaji jamii kupambana na ugonjwa wa malaria katika halmashauri za wilaya za Ushetu,Msalala na Kishapu mkoani Shinyanga.

Mradi huo umetambulishwa leo Jumanne Machi 5,2019 katika ukumbi wa Submarine Hoteli Mjini Kahama wakati wa mkutano wa utambulisho wa mradi huo uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa kutokomeza Malaria.

Lengo la mradi huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili ni uhamasishaji wa kuzuia ugonjwa wa malaria ambapo walengwa ni akina mama wajawazito,wanaonyonyesha,walezi wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na watoa huduma kwenye kliniki za akina mama na watoto.Akitambulisha mradi huo,Telack alisema ripoti ya Viashiria vya maambukizi ya Malaria ngazi ya jamii ya mwaka 2017/2018 inaonesha kuwa maambukizi ya ugonjwa wa malaria yamefikia asilimia 6 kutoka asilimia 17 kwa mwaka 2015/2016.

“Pamoja na kupungua kwa maambukizi kulikochangiwa na juhudi za serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa mikakati ya udhibiti wa malaria iliyopo inatakelezwa kwa ufanisi,hivyo bado juhudi zinatakiwa kufanyika ili kupunguza kiwango hiki kufikia asilimia 1 na hatimaye kutokomeza kabisa Malaria katika mkoa wetu”,alieleza.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kupitia Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015-2020) wa Kudhibiti Malaria ulioandaliwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, kumekuwepo mafanikio mkoani Shinyanga ikiwemo kuongezeka kwa uwepo wa vyandarua vyenye dawa kwa jamii. 

Aidha alisema kutokana na kuwepo kwa mwitikio mdogo wa wanajamii kushiriki katika mikakati ya kupambana na malaria ni imani yake kwamba kupitia mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria utatumika kuhamasisha jamii kushiriki kwenye mikakati ya kudhibiti malaria kwa vitendo. 

Telack aliwataka viongozi na wataalamu wa ngazi ya mkoa,wilaya na halmashauri kushirikiana na T- MARC kutekeleza mradi huo vizuri ili kutokomeza Malaria huku akiitaka T-MARC kujipanga kutekeleza mradi huo kwenye mkoa mzima. “Malaria inazuilika na inatibika,tiba ya mapema baada tu ya dalili za homa kuanza ni muhimu kuzuia vifo hususani kwa watoto na akina mama wajawazito”,aliongeza Telack. 

Awali Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC, Hamid Al- Alawy alisema kupitia mradi watahamasisha wanawake wajawazito,wanaonyonyesha na watoto kutumia vyandarua vyenye dawa kuzuia ugonjwa wa malaria lakini pia jamii kupima afya badala ya kuanza kutumia dawa kwani siyo kila homa ni malaria. 

Naye Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Teresia Shirima aliwataka wananchi kuondokana na dhana potofu kuwa vyandarua vinapunguza nguvu za kiume huku akiwahamasisha kutumia vyandarua kwa matumizi yaliyokusudiwa. Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria' unatekelezwa na asasi ya T- MARC Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais -TAMISEMI na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ili kutekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti Malaria. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria unaotekelezwa na asasi ya T- MARC kwa ajili ya kuhamasisha jamii kupambana na ugonjwa wa malaria katika halmashauri za wilaya za Ushetu,Msalala na Kishapu mkoani Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack, akiwasihi viongozi na wataalamu kushirikiana na asasi ya T- Marc kutekeleza mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria.Wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akifuatiwa na Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Teresia Shirima. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC, Hamid Al- Alawy akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha. 
Kushoto ni Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- Marc, Hamid Al- Alawy akifuatiwa na Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka T- MARC, Levina Thobias na Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Teresia Shirima (kulia). 
Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Teresia Shirima akielezea kuhusu Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015-2020) wa kudhibiti Malaria ulioandaliwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto. 
Wadau wakiwa ukumbini. 
Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- Marc, Hamid Al- Alawy akielezea kuhusu mradi huo na shughuli mbalimbali zinazofanywa na T-MARC katika kuwahudumia wananchi. 
Wadau wa kupambana na ugonjwa wa malaria wakiandika dondoo muhimu. 
Wadau wa kuzuia ugonjwa wa malaria wakiwa ukumbini. 
Wadau wakiwa ukumbini. 
Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka T- MARC, Levina Thobias akiwasilisha mada kuhusu tafiti mbalimbali zilizofanywa na T-Marc ambapo walibaini kuwa bado jamii ina imani potofu kuwa utumiaji wa vyandarua unapunguza nguvu za kiume lakini pia kuleta kunguni. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akiwataka wadau wanaotekeleza miradi mbalimbali wilayani Kahama kuhakikisha wanatumia lugha ya Kiswahili badala ya Kiingereza akibainisha kuwa baadhi ya wadau wamekuwa wakisambaza vipeperushi vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza wakati wananchi wanaelewa vizuri zaidi Kiswahili. 
Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC, Hamid Al- Alawy akiagana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack. 
Picha ya pamoja. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WAZIRI MKUU AONGOZA MAZISHI YA IMAMU WA MSIKITI WA MTORO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Machi 5, 2019) amewaongoza wakazi wa jijini la Dar es Salaam katika mazishi ya Imamu wa Msikiti wa Mtoro Sheikh Zubeir Yahya Mussa yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu.

Sheikh Zubeir ambaye ni miongoni mwa masheikh maarufu jijini Dar es salaam alifahamika sana kutokana na kuwa Imamu wa msikiti huo, ambao ni miongoni mwa misikiti mikubwa na maarufu zaidi hapa nchini, alifariki dunia jana usiku.

Pamoja na Uimamu wake, Sheikh Zubeir aliwavutia watu wengi sana kutokana na darasa zake alizokuwa akiziendesha kwa ufundi mkubwa katika msikiti huo wa Mtoro na maeneo mengine.

Sheikh Zubeir alikuwa miongoni mwa masheikh waliojiweka karibu sana na jamii na kuwa na uhusiano mzuri na masheikh wenzake kutoka taasisi mbalimbali.

Sheikh Zubeir alipata elimu yake ya juu katika chuo kikuu cha Madina, (Ummul- Quraa) akiwa pamoja na Sheikh Juma Omar Poli, Sheikh Muharram Juma Doga, Sheikh Abdallah Ahmad Bawazir na wengineo.

 Baadhi ya viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba.

Wengine ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, Mbunge wa Kibaha Vijijini, Abuu Jumaa, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MACHI 5, 2019.

UVCCM SHINYANGA, FRIENDS OF TULIA WAENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

$
0
0
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) mkoani Shinyanga (UVCCM) kwa kushirikiana na Marafiki wa Taasisi ya Dkt. Tulia Ackson 'Friends of Tulia' wameendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake lengo likiwa ni kutoa fursa kwao ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mafunzo hayo yanayotolewa pia na wakufunzi kutoka taasisi ya Mjasiriamali Kwanza Enterprises yamezinduliwa leo Machi 5,2019 kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ushetu wilayani Kahama. 

 Awali akizungumza,Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Barack Shemahonge, alisema katika kuelekea Tanzania ya viwanda ili kufikia uchumi wa kati ni lazima wananchi wajitume kufanya kazi, jambo ambalo limemgusa na kuamua kuendesha mafunzo hayo ili kukuza uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla. 

Alisema moja ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuondoa umaskini kwa wananchi, hivyo kupitia mafunzo hayo ya ujasiriamali ambayo yanatolewa bure, ana imani kuwa maisha ya watu hao ambao wamejitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo yatabadilika na kukuza vipato kwenye kaya zao. “Naomba pia mjiunge kwenye vikundi ili muweze kupata mikopo kwenye halmashauri asilimia 10, ili mpate mitaji na kupanua wigo wa biashara zenu na kuinuka kiuchumi ikiwa fedha ni za makusanyo ya mapato ya ndani na mikopo yake haina riba,”amesema Shemahonge.

 Akizindua mafunzo hayo ya ujasiriamali, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa wabunifu kwenye biashara zao pamoja na kuzingatia ubora wa bidhaa jambo ambalo litawafanya kupata wateja wengi na kukua kiuchumi. Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu (CCM) mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga, aliwataka wajasiriamali hao kutokata tamaa pale wanapokumbana na changamoto katika biashara zao, bali wawe majasiri na kuendelea kupambana, kitendo ambacho kitawakomaza na hatimaye kuja kuwa wafanyabiashara wakubwa. 

Nao baadhi ya wajasiriamali hao akiwemo Custa Mwambuli ambao wanafanya shughuli ya kutengeneza mkaa kwa kutumia karatasi, walipongeza utolewaji wa mafunzo hayo na kubainisha kuwa yatawapatia mbinu mbalimbali namna ya kupanua wigo wa biashara zao na kutambulika kimataifa na hatimaye kukua kiuchumi. 

Miongoni mwa mafunzo yanayotolewa kwenye semina hiyo ya ujasiriamali ni utengenezaji keki za harusi, mikate, sambusa,burger, ubuyu wa rangi, ufugaji wa kuku, nyuki, samaki, kilimo cha uyoga, sabuni za miche, dawa za usafi, mishumaa, karanga za mayai chaki za mashuleni, mafuta ya mgando, ushonaji wa mawigi, pamoja na mapambo ya sherehe. Mafunzo hayo yatadumu kwa siku tatu kuanzia leo Machi 5,2019. Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akizungumza kwenye uzinduzi wa semina ya mafunzo ya ujasiriamali ambayo yatadumu kwa muda wa siku tatu kwa vijana na wanawake kupewa ujuzi na mbinu namna ya kuendesha biashara na kukua kiuchumi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Elias Kwandikwa ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ushetu wilayani Kahama akizindua mafunzo ya ujasiriamali mkoani Shinyanga na kuwataka washiriki wawe wabunifu kwenye biashara zao pamoja na kuzingatia ubora wa bidhaa ili wapate wateja wengi na kukua kiuchumi. Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachambwa akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali na kuwataka wayatumie vizuri katika kubadilisha hali ya maisha yao kiuchumi. Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya Shinyanga Mjini wakiwa kwenye uzinduzi wa mafunzo yao ya kutengeneza bidhaa mbalimbali pamoja na kupewa mbinu za kibiashara ili wapate kukua kiuchumi. Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya Shinyanga mjini wakiendelea kusikiliza nasaha za viongozi mbalimbali juu yao kabla ya kuanza kufundishwa namna ya kutengeneza bidhaa na mbinu za kibiashara. Wajasiriamali wakiendelea kusikiliza nasaha za viongozi kabla ya kuanza kufundishwa namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali. Awali Mwenyekiti wa Taasisi ya Marafiki wa Dkt. Tulia Ackson mkoani Shinyanga Shabani Wisandara akitambulisha marafiki wa taasisi hiyo ambayo imejipanga katika kuhakikisha wanashirikiana na serikali kuhudumia wananchi. Usikilizaji wa nasaha ukiendelea kabla ya kuanza ufundishwaji wa kutengeneza bidhaa mbalimbali. Msemaji wa Taasisi ya Dkt Tulia Ackson nchini Tanzania Matiko Nyaiho akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema wameshirikiana na UVCCM mkoa wa Shinyanga, kuleta mafunzo hayo ya ujasiriamali bure kwa vijana na wanawake ili kuwafundisha namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali na hatimaye kujikwamua kiuchumi. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akimpatia cheti cha pongezi Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kushoto) kwa kuleta mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake mkoani humo, ili kuwakwamua kiuchumi. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akimpatia cheti cha pongezi Mwenyekiti wa taasisi ya Marafiki wa Dkt. Tulia Ackson kwa kushirikiana na UVCCM Mkoa wa Shinyanga kuleta mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake ili kuwa kwamua kiuchumi na katika kuelekea Serikali ya viwanda na kufikia uchumi wa kati. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa naye akionyesha cheti cha Pongezi katika kushirikia kuzindua mafunzo ya ujasiriamali na kutoa mbinu za namna ya kufanikiwa kibiashara. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akikagua baadhi ya bidhaa za wajasiriamali ambao walifika kwenye mafunzo hayo kuongeza mbinu namna ya kupanua wigo wa biashara zao na kukua kiuchumi. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa, akiwasisitiza wajasiriamali kuyatumia vizuri mafunzo hayo kujikwamua kiuchumi. Custa Mwambuli ni mjasiriamali ambaye anafanya shughuli ya kutengeneza mkaa kwa kutumia karatasi, akipongeza utolewaji wa mafunzo hayo kuwa yatawapatia mbinu mbalimbali namna ya kupanua wigo wa biashara zao na kutambulika kimataifa na hatimaye kukua kiuchumi. Awali Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa (kulia) akijiandaa na hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali, katikati ni mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, na kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Dotto Joshua. Mbunge wa Viti Maalumu Lucy Mayenga (kushoto) akiwa na msemaji wa Taasisi ya Friends of Dkt Tulia Ackson, Matiko Nyaiho mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa mafunzo ya ujasiriamali. Awali Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Elias Kwandikwa akiwasili ukumbini kwenda kuzindua mafunzo ya ujasiriamali kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga, akiwa na mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM. Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Madereva magari ya watalii wanaoshuka Kreta Ngorongoro wapewa tahadhari

$
0
0
MADEREVA wa magari ya watalii wanaotembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro(NCAA), hususani wanaotelemka Kreta wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa kutokana na barabara hiyo kufanyiwa matengenezo. 

Akizungumzia matengenezo hayo Kamishna wa Uhifadhi NCAA Dk. Fredy Manongi alisema, barabara inayoshuka Kreata kwa sasa imekwanguliwa ili kuifanyia matengenezo ya muda mfupi na mrefu.

“Ile barabara tumeanza mpango wa kuijenga kama barabara ile ya kupandia kutoka Kreta, kwa sasa imefukuliwa pamoja na kuwapo mashine njiani. 

“Kwa mvua hizi zinaendelea kunyesha tunawaomba madereva wawe waangalifu kwani barabara si imara,” alisema Dk. Manongi. 

Mbali ya barabara hiyo Dk. Manongi alibainisha pia barabara nyingine inayoanzia lango kuu la NCAA mpaka goloni ulipo mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nayo itaanza kujengwa kwa kiwango cha tabaka gulu la Zege. 

“Tupo tayari kuhakikisha tunawaondolea kero watalii, wamiliki wa magari ya watalii lakini pia hata sisi Mamlaka kwani tunatumia fedha nyingi kukarabati barabara ya changarawe kila mwaka,” alisema Kamishna wa Uhifadhi Dk. Manongi.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images