Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109935 articles
Browse latest View live

MABALOZI WATAKIWA KUDUMISHA AMANI.

$
0
0
Na Frankius Cleophace Tarime.

Mabalozi wametakiwa kuendelea kudumisha suala la Amani kuanzia ngazi za chini mpaka ngazi za Juu kwa lengo la kuendelea Amani Upendo na Mshikamano wa Nchi ya Tanzania.

Hayo yamebainishwa na Nancy Msafiri ambaye ni katibu Mwenezi Chama cha Mapinduzi Mkoani Mara katika uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho kwa mabalozi wanatokana na chama cha Mapinduzi Wilayani Tarimre.

Nancy alisema kuwa mabalozi wanapaswa kulinda Usalama wa watanzania kwa sababu ndiyo wanaoishi nao kuanzia ngazi za chini hivyo wakidumisha na kulinda Amani itakuwa faidaka Nchi.

“Sisi Viongozi wa Mkoa hadi Taifa hatuna watu wakiwemo wananchama lakini nyie mabalozi mnaishi na watu mnawajua hivyo mkidumisha Amani Askari hawana kazi pamoja na vyombo vyote vya ulinzi na usalama” alisema Nancy.

Akiongea na Mabalozi hao Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa chama cha Mapinduzi Taifa Gerald Martine ambaye amejitoa kutengeneza vitambulisho hivyo alisema endapo vitakamilika vitaghalimu kiasi cha Shilingi Mill11.7.

Gerald aliongeza kuwa ataendelea kusemea chama cha mapinduzi ikiwa ni pamoja na kuyasema yale yaliyofanywa na chama hicho kutokana na ilani ya chama katika sekta ya Afya, Elimu, Maji na Miundombinu ya Barabara.

Pia Martine aliwataka mabalozi hao kujitokeza kwa wingi na kutoa ushirikiano katika chaguzi za serikali za mitaa ili kuweza kushinda na kurudisha viti vyote ambavyo vipo upinzani.

Aidha katibu wa CCM Wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka Kura alisema kuwa wanaendelea na mchakato wa kutengeneza vitambulisho kwa ajili ya mabalozi hao wote wilaya ya Tarime ili wawezekutambulika na serikali ili wafanye majukumu yao bila kubugudhiwa.

Picha ya Nancy Msafiri ambaye ni katibu mwenezi CCM Mkoa wa Mara ambaye alikuwa Mgeni rasmi akikabidhi vitambulisho hivyo kwa mabalozi kutoka wilay ya Tarime katikati ni katibu wa chama hicho wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka Kura.


MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 5,2019

Wajasiliamali Wilayani Nkasi Watakiwa kuwa Wabahili ili kufanikiwa

$
0
0
Wawakilishi wa vikundi vya Wanawake, vijana na walemavu wakipokea hundi ya mfano yenye thamani ya shilingi milioni 53 kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo (kaunda nyeusi) katika hafla fupi ya kukabidhi mikopo hiyo kwa vijana.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akikabidhi mkopo kwa mmoja wa wanakikundi cha Mshikamano kutoka kijiji cha Chala katika hafla fupi ya utoaji mikopo katika Halmshauri ya Wilaya ya Nkasi ambapo vikundi 15 vilipatiwa mikopo ya jumla ya Shilingi milioni 53.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda akitoa nasaha zake kwa wanavikundi wajasiliamali waliopewa mikopo (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kutoa mikopo hiyo. 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa nasaha zake kwa wanavikundi wajasiliamali waliopewa mikopo (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kutoa mikopo hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wajasiliamali wa Wilaya ya Nkasi kuhakikisha fedha ya mkopo waliyopewa na halmashauri hawazitumii katika matumizi binafsi bali wazielekeze katika biashara ili ziweze kuwapatia faida na kuwainua kiuchumi na hatimae kupata fedha za kujikimu kimaisha.

“Kwenye vikundi vyenu mna malengo mahususi na ili haya malengo mahususi yaweze kutimia kwenye biashara hakuna kingine zaidi ya kuwa bahili lazima muwe mabahili, lazima muwe watu ambao hamkubali kutoa fedha hovyo hovyo, uskibali kutoa fedha ambayo haina mpango, leo unaambiwa kuna msiba pale wewe unachukua fedha ya mkopo unapeleka, huu sio ubahili, weka fedha yako vizuri, kama kuna shida tafuta hela nyingine,na ukichukua fedha inayotokana na hapo labda ni faida,” Alisema.

Ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 53 ikiwa ni asilimia 10 ya fedha za mapato ya ndani ya halmashauri kwa vikundi 15 vya halmashauri ya wilaya ya Nkasi ikiwa ni utekelezaji wa kisheria chini ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lililoanzishwa Mwaka 2005 chini ya sheria na 16 ya mwaka 2004 yenye adhima ya kuwainua wananchi kiuchumi ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Katika kulisisitiza hilo Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini Mh. Ally Kessy alisema kuwa pesa hizo ni kodi za wananchi ambazo halmashauri inapita kuzikusanya nahatimae asilimia 10 ya mapato hayo kuyagawa kama mikopo kwa wajasiliamali wanawake, vijana na walemavu na kusisitiza kuwa fedha hiyo irudishwa kadiri inavyotakiwa.

“Fedha hii ni mkopo na sio sadaka, isiwe kukopa harusi na kulipa matanga, kulipa ni wajibu, hizi pesa sio sadaka ni kodi ya wananchi na kodi ya wanachi haiendi bure, mnakopeshwa mkafanye maendeleo sio muanze kununua magauni au kwenda harusini hakuna ni kufanyia mtradi, kama unaona kikundi chako hakina uwezo na kulipa msichukue ili wapewe wengine,” Alisisitiza.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emanuel Sekwao wakati akiseoma taarifa alisema kuwa Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Jumla ya vikundi 15 viliomba mikopo ya Tshs. 68,292,000.00. lakini baada ya Kamati ya Mikopo kukaa na kupitia maombi ya mikopo jumla ya kiasi cha Tshs 53,000,000 kiliidhishwa.

“Vikundi vitakavyokopeshwa ni 15 ambapo Vikundi vya Vijana vitatu Jumla ya fedha Tshs 12,687,000 Kikundi cha Walemavu kimoja, Jumla ya fedha Tshs 2,000,000 na Vikundi vya Wanawake kumi na moja, jumla ya fedha Tshs 38,313,000. Vikundi hivyo vimetoka katika kata za Mashete, Kipundu, Majengo, Sintali, Namanyere, Chala, Kipande, Kabwe, Kate, Kirando na Kala.”

Nae mkuu wa wilaya hiyo Mh. Said Mtanda alimuhakikishia mkuu wa mkoa kuwa watajitahidi kuhakikisha wanakusanya mapato ya halmashauri kwa asilimia 100 na kutoa mikopo hiyo kwa vijana na kuwapa fursa ya kujiajiri lakini pia kuongeza viwanda vidogovidogo kutokana na shughuli mbalimbali za uzalishaji wanazojihusisha nazo wajasiliamali hao.

Katika kutoa shukrani mmoja wa vijana wa kikundi cha Panda Miti Rukwa (PAMIRU) Uswege Mwasomola alisema kuwa lengo lao ni kuwa na shamba la miti la kikundi ili kusaidia kutunza mazingira na kuongeza kuwa kutokana na mkopo huo walioupata wataweza kutatua changamoto walizokuwa nazo kwa asilimia 100.

“Mkuu wa Mkoa pamoja na viongozi wote nadhani mwaka ujao hatutakuja kukimbizana kufuatilia mikopo zaidi tutakwenda kifua mbele kwa kuhakikisha tunairudisha kwa muda muafaka ili tutoe fursa kwa vijana wengine,” alisema.

Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi katika mwaka wa fedha 2018/2019 inatarajia kukusanya jumla ya Tshs 2,304,000,000/= kupitia vyanzo vyake vya ndani. Katika kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi Februari 2019 jumla ya Tshs 1, 511,915,838.67 ilikusanywa ambapo sawa na asilimia 65.62 ya bajeti ya mwaka wa fecha 2018/2019.

SERIKALI KUENDELEA KUDHIBITI MATUMIZI YA KEMIKALI NCHINI

$
0
0


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisema jambo na wadau wa biashara ya kemikali (hawapo pichani) kwenye mkutano na wafanya biashara za kemikali nchini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Prof Esther Hellen Jason akisema jambo na wadau wanaojihusiha na biashara ya kemikali (hawapo pichani) katika mkutano na wadau wanaojihusisha na biashara ya kemikali.

Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akisema jambo kwa wadau wa biashara ya kemikali nchini (hawapo pichani) katika mkutano na wadau wanaojihusisha na biashara ya kemikali nchini.

Mdau wa bishara ya kemikalina Katibu Mkuu wa Mawakala wa Forodha Tanzania Mhandisi Anthony Swai akiwa amebeba sampuli ya kemikali mapema leo kwenye kikao cha wadau wanaojihusisha na bishara ya kemikali nchini.

Wadau wanaojihusisha na biashara ya kemikali wakiwa kwenye mkutano uliotishwa na Ofisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kujadili namna bora ya kuboresha biashara ya kemikali nchini.



Serikali itaendelea kusimamia na kudhibiti matumizi ya kemikali ili kuhakikisha hazileti madhara kwa afya za wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo alipokuwa kwenye mkutano na wadau wa kemikali kujadili namna ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara ya kemikali nchini.

“Kemikali zisipodhibitiwa vizuri zinaweza kuleta madhara katika afya, mazingira pamoja na kuhatarisha usalama wa nchini, ipo haja ya kuweka mazingira mazuri ya kusimamia na kudhibiti uingizaji na matumizi ya kemikali nchini ili zisilete madhara” amesema Waziri Ummy.

Hata hivyo takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2014 zinaonyesha vifo milioni 12.6 vilitokana na mazingira duni ya kuishi, mojawapo ya kichocheo ni athari za kemikali ambazo zimekuwa zikisababisha magonjwa na vifo.

Waziri Ummy amesema kuwa kemikali zimekuwa na athari kubwa kwa binadamu kwa kusababisha magonjwa zaidi ya 100 huku akiyataja magonjwa ya moyo, saratani, ngozi, athari katika mifumo ya fahamu, upumaji pamoja na chakula kuathiri zaidi wananchi wengi.

“Tukubali kuwa kemikali zina madhara kwa wananchi lakini sasa tuwe na mazingira mazuri ya kuzidhibiti” amesema Waziri Ummy na kuendelea kusema kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira mazuri kwa wafanya biashara ya kemikali nchini.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amezitaka Taasisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) kuangalia upya tozo wanazotoza kwa wafanyabiashara za kemikali nchini pamoja na kupunguza urasimu usiokuwa na ulazima ili kuwawekea mazingira rafiki wafanya biashara za kemikali.

“Msiwe ni kikwazo kwa uwekezaji na biashara, kikwazo cha kushamiri na kukua kwa uwekezaji nchini, nataka muwe mawakala wa kukuza biashara na uchumi nchini” amesema Waziri Ummy.Awali akisoma taarifa yake Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amesema Sheria ya Kemikali ya mwaka 2003 imekuwa na mchango mkubwa katika udhibiti wa matumizi ya kemikali nchini.

“Kabla ya kutungwa kwa sheria hii, kemikali zilikuwa zikiingizwa nchini kiholela na kutumika bila ya kuwa na ufatiliaji au udhibiti wowote” alisema Dkt. Mafumiko.Dkt. Mafumiko amesema Sheria ya kemikali imewawezesha kudhibiti usafirishaji, utumiaji pamoja uteketezaji wa taka zinazotokana na kemikali.

“Ofisi ya Mkemia inasimamia kwa ukaribu matumizi ya kemikali zote zinazoingizwa nchini kuanzia zinapoingia, mahali zinapokwenda pamoja na matumizi yaliyokusudiwa” alisema Dkt. Mafumiko.Naye Katibu Mkuu wa Mawakala wa Forodha Tanzania Mhandisi Anthony Swai amesema tozo zimekuwa nyingi kiasi cha kuwaumiza wafanyabiashara wa kemikali huku urasimu pia ukisababisha wafanyabiashara kutumia muda mwingi kufuatilia vibali vya uingiza wa kemikali nchini.

Aidha Mhandisi Swai ameiomba Serikali kuainisha mipaka ya taasisi za umma pamoja na tozo wanatostahili kulipa kwani kumekuwa na mwingiliano wa majumuku baina ya taasisi za Serikali ambazo amezijata kuwa ni GCLA, TDFA na TBS (Shirika la Viwango Tanzania

RC Wangabo Aagiza Ushirikiano kwa Ma-DC kutekeleza Miradi ya Serikali

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda (aliyeshika tofali) akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo wakati wa ziara fupi ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya hiyo ulioanza mapema mwaka huu na kutakiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (rainboot za kijani) akiangalia uimara wa matofali yaliyojengewa msingi katika moja ya majengo saba ya hospitali ya wilauya ya Sumbawanga inayojengwa katika bonde la ziwa Rukwa, kata ya Mtowisa. (mwenye shati ya kitenge) Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule.


………………………….

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakuu wa Wilaya za Mkoani Rukwa kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa pamoja katika kutembeleana na kuelezana changamoto na mafanikio katika maeneo ya mradi wa ujenzi wa hospitali za wilaya ili kujenga hospitali hizo katika hadhi sawa na hatimae kupeana ujuzi wa utekelezaji wa mradi huo.

Amepongeza ushirikiano unaoonyeshwa na uongozi wa wilaya ya Nkasi unaoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo mh. Said Mtanda pamoja na wabunge, madiwani na mkurugenzi na kusifu mafunzo waliyoyapata na kuyarekebisha wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa vituo vitatu vya afya katika wilaya hiyo na kuonyesha dalili za kutojirudia kwa makosa waliyoyafanya wakati wakitekeleza ujenzi wa vituo hivyo.

“Wakuu wa Wilaya waweke program ya kutembeleana kwa pamoja ili kujifunza, wanakuja kwa mfano (wilaya ya) Nkasi, wanakwenda wilaya ya Sumbawanga, Wanakwenda wilaya ya Kalambo halafu watakaa chini wafanye tafakari ili waone ni namna gani wanweza wakasimamia vizuri hizo hospitali zetu za wilaya kwasababu tunapaswa tuwe na kitu bora, hospitali zote tatu ziwe bora ndani ya mkoa wetu,” Alisisitiza.

Alisema kuwa halitakuwa jambo jema kwa wilaya moja kuwa na ufanisi sana ilihali wilaya nyingine inakuwa na changamoto na hivyo vyema wakaungana kama timu na kutembelea miradi hiyo ya ujenzi wa hospitali za wilaya ili kila mmoja aweze kujifunza kutoka kwa mwenzie.

Ameyasema hayo baada ya ziara yake ya kutembelea ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi pamoja na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga ili kujionea changamoto mbalimbali zinazoukabili mradi huo ambao unatakiwa kuisha mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu.

BASHUNGWA NA AWESSO WAMUELEZEA MAREHEMU RUGE KAMA LULU YA TAIFA

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus – Kagera.

Mwili wa marehemu Rugemalila Gerazi Mutahaba umepumzishwa jana katika Nyumba yake ya Milele , Nyumbani kwao Kable Bukoba Mkoani Kagera, huku mazishi hayo yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Naibu Waziri, Wabunge, na Viongozi wa Siasa, Wakuu wa Mikoa wasanii na watu mashuhuri.

Wakiongea mara baada ya shughuli hiyo ya mazishi baadhi ya Viongozi hao wamezidi kumzungumzia Marehemu Ruge kama lulu ya Taifa kwa yale yote aloyafundisha na kuelekeza njia kuwa yafaa kuigwa na kuenziwa kwa namna moja ama nyingine.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa kilimo na Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mh. Innocent Bashungwa akiongea na Michuzi Tv amemuelezea Ruge kuwa, Alikuwa kijana tofauti mwenye maono ya mbali, na ameweza kuyaishi na kutuonyesha kwamba na sisi kama vijana wakati wa ujana tutumie ujana wetu kuhakikisha tunaacha alama hapa Duniani. Pia ameongeza kuwa, kama vijana wa Kitanzania tumeachiwa changamoto kwamba hata kama muda wa kuishi ni mfupi, tukitumia vizuri muda wetu tutaweza kulisaidia Taifa letu la Tanzania.

Nae Naibu Waziri wa Maji Jumaa Awesso amesema Marehemu RUGE kwake ni kama Daktari wa fikra kwani ameweza kubadiri fikra hasi kuwa fikra chanya, na ameweza kuwasaidia Vijana, na akitusisitiza tusiwe vijana Kaa badala yake tusaidiane, kuhakikisha taaluma na Vipaji tulivyonavyo tuinuane katika mambo mbalimbali na kuweza kulisaidia Taifa letu, hivyo katika kumuenzi tunatakiwa kuwa na upendo, ushirikiano na ubunifu kwamba changamoto zipo lakini tunaweza kuzigeuza kuwa fursa, hivyo na sisi kama Vijana tutahakikisha hatuwi Vijana Kaa ili tuweze kusaidiana na kulisaidia Taifa letu.

Katika Upande Mwingine Mh. Deodatus Kinawiro Mkuu wa Wilaya ya Bukoba alipozikwa Ruge amesema Marehemu Ruge amekuwa mhamasishaji mkubwa katika kutumia fursa zilizopo nchini kwa ajili ya kujipatia kipato, kujenga Uchumi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla, kupitia fikra alizokuwa nazo na ndoto kubwa za kuinua vijana wenzake, hivyo mchango ake katika Taifa hili utazidi kuwa mkubwa kupitia kuyaenzi matendo yake.

Nae Mh. Murshidi Ngeze Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba anasema Ruge amekuwa mpambanaji ambae ametuachia somo kubwa kwetu, na alama yake haiwezi kufutika ambapo ni kazi yetu kuzingatia yale yote aliyotufundisha na kuyaenzi, hivyo kama Halmashauri wananafikiria kuiomba familia Watengeze Foundation ambayo itayaishi yale yote alokuwa akiyafanya, huku akiongeza kuwa kazi kubwa sasa imebaki kwa Pacha wake Marehemu Ruge, Bwana Joseph Kusaga kuhakikisha anandelea kijenga familia ya Clouds kuwa pamoja na wasione kama Ruge amewatoka kimoyo bali kisura hivyo ni Jukuma la Clouds kama Taasisi kuendelea kuimarika na kusonga mbele.
 Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akiwa ameketi pembeni yake ni Mh. Ridhiwani Kikwete (MB), Mh. Angella Kairuki _ Waziri wa Uwekezaji Mh. Dotto Biteko Waziri wa Madini na Na Mh. Innocent Bashungwa Naibu Waziri wa Kilimo, wakifuatilia Shughuli ya Kuaaga Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba katika Viwanja vya Gymkhana Bukoba.
 Mh. Innocent Bashungwa Naibu Waziri wa Kilimo akiweka maua katika kaburi la Marehemu Ruge kama Ishara ya Kuzika.
  Mh. Deodatus Kinawiro Mkuu wa Wilaya Bukoba akiweka maua katika kaburi la Marehemu Ruge kama Ishara ya Kuzika.
  Mwenyekiti Halmashauri ya  Wilaya Bukoba,Murshidi Ngeze akiweka maua katika kaburi la Marehemu Ruge kama Ishara ya Kuzika.
Wakuu wa Mikoa ya Kagera na Dar es salaam Mh. Gaguti na Mh. Makonda wakiweka shada  la maua katika kaburi la Marehemu Ruge kwa Niaba ya Wananchi wa Mikoa yao.

Mabadiliko ya kanuni za mpira kwa msimu ujao 2019/2020 .

$
0
0
The International Football Association Board (The IFAB) , imebadilisha baadhi ya kanuni za mchezo wa soka kwenye kikao kilichofanyika wiki iliyopita nchini Scotland . Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:-

1. KUTAKUWA HAKUNA MREJESHO KUTOKANA NA PIGO LA PENATI

Mchezo utasimama kwa kuanzishwa kama penati imeokolewa au imegonga mwamba , hii ina maana hakuna tena nafasi ya kufuata mpira na kufunga ( Rebound ) kwa maana hiyo wachezaji hawatokuwa na uhitaji wa kujipanga nje ya 18.

2.MPIRA KUCHEZWA NA MKONO.

Kuanzia Juni mosi goli litakalofungwa ambalo limegusa mkono wa mchezaji kwa maksudi au bahati mbaya ( Mfungaji ) halitakubaliwa.

3.MABADILIKO YA MCHEZAJI 

Mchezaji ambaye atakuwa anafanyiwa mabadiliko ataruhusiwa kutoka kupitia upande wowote ule wa uwanja 

4. GOAL KICK 

Mchezaji ataruhusiwa kugusa mpira hata ndani ya eneo la 18 kutoka kwa kipa , ambapo sasa hivi ni mpaka mpira utoke kwenye 18 ndio unaruhusiwa kuugusa.

5. KADI KWA MAKOCHA.

Makocha sasa nao watakuwa wanaoneshwa kadi ya njano na nyekundu tofauti na sasa hivi wanaambiwa tu toka kwenye eneo la benchi la ufundi.

6.  KWENYE UKUTA WA KUZUIA MIPIRA ILIYOKUFA

Wachezaji wa upande ambao wanapiga mipira iliyokufa ( freekick ) hawatoruhusiwa kwenda kujumuika kwenye ukuta wa timu ambayo inazuia mipira hiyo , tofauti na sasa huwa wanachanganyika kama kuwatoa mchezoni.

7. PENATI .

Magolikipa wataruhusiwa kuweka mguu mmoja tu kwenye mstari na huo mwingine wataamua wao wenyewe waweke wapi , tofauti na sasa kwamba miguu yote lazima iwe kwenye mstari wakati anapigiwa penati.

TRA YATOA MSAADA WA BIDHAA ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILL 14.3 KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU

$
0
0
Na Franlkius Cleophace Tarime.

Mamlaka ya Mapato Nchini TRA MkoanI Mara imetoa msaada wa bidhaa mbalimbali kwenye taasisi za serikali na zisizokuwa za serikali ili kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo watoto na wazee.

Akikabidhi bidhaa hizo Meneja TRA Mkoa wa Mara Wallace Mnkande alisema kuwa wameamua kugawa bidhaa hizo ambazo baadhi yao zilikamatwa sababuya wafanyabiashara kukiuka tararibu za Kiforodha na muda wake wa kukaa pale kuisha nakuamua kuzigawa kwa taasisi zenye mahitaji.

“Bidhaa hizi baadhi yao zilikuwa zikielekwa nje ya Nchi na nyingine kuingia ndani ya Nchi yetu na baadhi kufuata taratibu zote lakini wanapopatiwa jumla ya tozo wanashindwa kulipia na kupewa muda lakini sasa muda wake umeisha na kuamua kutaifisha nakuzigawa ili jamii inufaike” alisema Meneja TRA Mara.

Mnkande aliwataka wafanyabaishara wote kufuata taratibu na kutimia njia rasmi katika kuingiza na kutoa bidhaa mbalimbali nje ya Nchi huku wananchi wakidai sitakabadhi pale wanaponunua bidhaa.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa TRA Mkoa wa Mara Wallace Mnkande kipindi akikabidhi Msaada wa bidhaa mbalimbali kwa Tasisi zikiwemo za serikali ili kuwasaidia watu wenye mahitaji wakiwemo watoto yatima, Wazee pamoja watu wasiojiweza.

Pia Wallace aliwataja bidhaa hizo zilizogawiwa katika taasisi hizo kuwa zinajumla ya shilingi Millioni 14.3.

Aidha wanufaika wa bidhaa hizo wametoa shukrani kwa mamlaka ya mapato Nchini TRA Mkoa wa Mara kwa kuwapatia bidhaa hizo kwa ajili ya Vituo vye Mahitaji wakiwemo Wazee na Watoto yatima.
Meneja TRA Mkoa wa Mara Wallace Mnkande aliyevaa miwani kutoka kushoto na koti jeusi akikabihi bidhaa hizo kwa taasisi mbalimbaloi zilizokuja kupokea msaada huo.



IGP SIRRO AONGOZA MAAFISA, ASKARI NA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DCP MATANGA MBUSHI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Simon Sirro akiweka sahihi kwenye kitabu cha waombolezaji baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi DCP Renatus Matanga Mbushi, aliyefariki dunia tarehe 03/03 mwaka huu huko Mkoani Mbeya alipokuwa kwenye ziara ya kikazi na mwili wake kusafirishwa kuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu za mazishi.(Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Simon Sirro, akiteta jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu IGP Said Mwema wakati walipokutana nyumbani kwa Marehemu Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi DCP Renatus Matanga Mbushi, katika kambi ya Maafisa wa Polisi Oysterbay, Kinondoni jijini Dar es salaam, msiba huo ulitokea tarehe 03/03 mwaka huu huko Mkoani Mbeya alipokuwa kwenye ziara ya kikazi na mwili wake kusafirishwa kuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu za mazishi.(Picha na Jeshi la Polisi).
Maofisa wa Jeshi la Polisi wakiingiza mwili wa Marehemu Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi DCP Renatus Matanga Mbushi katika Kanisa la Parokia ya Mt. Petro lililopo Oysterbay  jijini Dar es salaam kwa ajili ya  misa ya kuuaga, msiba huo ulitokea tarehe 03/03 mwaka huu huko Mkoani Mbeya alipokuwa kwenye ziara ya kikazi na mwili wake kusafirishwa kuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu za mazishi.(Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Simon Sirro akiaga mwili wa marehemu Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi DCP Renatus Matanga Mbushi, katika Kanisa la Parokia ya Mt. Petro Oysterbay jijini Dar es salaam msiba huo ulitokea tarehe 03/03 mwaka huu huko Mkoani Mbeya alipokuwa kwenye ziara ya kikazi na mwili wake kusafirishwa kuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu za mazishi.(Picha na Jeshi la Polisi).

Balozi Seif akabidhi setu tani za Jezi kwa klabu ya Ujamaa

$
0
0
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Soka ya Ujamaa yenye mastakimu yake Mtaa wa Rahaleo Mjini Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameukumbusha Uongozi wa Klabu hiyo kuendelea na jukumu lake la kuwafinyanga vyema vijana wao ili wafikile lengo walilokusudia.

Alisema hatua hiyo mbali ya  kuirejeshea hadhi yake Klabu hiyo iliyokuwa nayo katika nyanja ya soka Visiwani  Zanzibar lakini pia itatoa nafasi kubwa zaidi ya kuwajengea njia ya maisha bora Vijana wao katika fursa za ajira kupitia Sekta hiyo ya Michezo.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mlinda Mlango mahiri ya Ujamaa Spots Club zamani maarufu ikijuilikana kwa jina la Worlves alitoa kumbusho hilo wakati akiukabidhi Uongozi wa Timu hiyo Seti Tano za Jezi hapo Ofisini kwake Mtaa wa Vuga akitekeleza ahadi aliyoitoa kwa Timu hiyo wakati alipoitembelea Mwaka jana.

Mchezaji huyo wa zamani wa Ujamaa Sports Club ambae aliahidi pia kutoa Seti nyengine Tano kwa Timu hiyo kabla ya kumalilika kwa Mwaka 2020 alisema Mchezo wa soka hivi sasa ni ajira inayowajengea mazingira bora ya kimaisha wachezaji ambao wamejikubalisha kujifunza kwa kina mchezo huo maarufu Duniani.

Alishauri kwamba  Uongozi huo wa Ujamaa lazima uhakikishe kwamba Vijana wao wote waliokubali kujisajili na Timu hiyo wanaendeleza nidhamu mchezoni kwa kufanya mazoezi kwa juhudi ili iwawezeshe kupata  mafanikio makubwa.

Balozi Seif  pia alitumia nafasi hiyo kuupa pole Uongozi, Wachezaji pamoja na Jamaa wa Familia ya Mchezaji wa Zamani wa Timu hiyo Marehemu Nassor Mashoto aliyefariki Dunia Tarehe 24 Januari Mwaka huu wa 2019.

Alisema Marehemu Nassor  mbali ya kuiletea sifa Timu yake ya Ujamaa lakini pia aliacha athari kubwa kwa wapenda soka wakati akiichezea Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar katika kipindi cha umahiri wake alipokuwa dimbani.

Balozi Seif  alisema msiba huo haukuwa wa Uongozi wa Timu, Wachezaji pamoja na Familia bali uliwagusa wanasoka wote wa Visiwa vya Zanzibar, Tanzania, Afrika ya Mashariki na hasa katika Mji wa Mombasa Nchini Kenya.

Akitoa shukrani wakati akipokea msaada huo wa seti Tano za Jezi kwa niaba ya Uongozi na Timu  ya Soka ya Ujamaa Mwenyekiti wa Timu hiyo Mohamed Makame Machano alisema Vijana wa Timu hiyo hivi sasa wanaendelea vyema katika mashindano yao ya Daraja la Pili.

Mohamed alimueleza Balozi Seif  kwamba Uongozi wa Klabu hiyo umepata faraja kubwa kutokana na Vijana wao kufanya vyema ndani ya msimu huu unawajengea mazingira ya kusonga mbele kutokana na nafasi waliyonayo katika muendelezo wa mashindano yao.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa Klabu ya Ujamaa iliyopo Mtaa wa Rahaleo alimuomba Mchezaji huyo wa zamani wa Klabu hiyo kufikiria wazo la kuwapatia Viatu wachezaji wao ili kuwajengea hadhi bora zaidi hasa wakati wanapokuwa kwenye mashindano.

Ujamaa ni miongoni mwa Timu kongwe za Soka Visiwani Zanzibar iliyojipatia umaarufu mkubwa kutokana na Historia yake za kusakata kabumbu lililopelekea kutoa wachezaji kadhaa wa Timu ya Taifa ya Zanzibar kwenye Mashindano ya Challenge kwa wakati huo yakiitwa Gorsage.
 Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Soka ya Ujamaa  Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Seti Tano za Jezi Mwenyekiti wa Klabu hiyo Mohamed Makame Machano kutekeleza ahadi aliyoitoa alipoitembelea Klabu hiyo Mwaka 2018. Anayeshuhudia  tukio hilo wa kwanza kushoto ni Mzee wa Klabu ya Ujamaa Mzee Ameir Makungu.
Balozi Seif  wa Pili kutoka Kulia akiukumbusha Uongozi wa Klabu ya Ujamaa kuhakikisha kwamba Vijana wao wanazingatia nidhamu katika mazoezi yao ili kuijengea sifa Klabu hiyo. Picha na – OMPR – ZNZ.

SERENGETI BOYS WAJIFUA NCHINI UTURUKI KUJIANDAA NA FAINALI ZA AFRIKA ZA VIJANA U-17

$
0
0
 Taswira za Timu ya Taifa ya Vijana U17 “Serengeti Boys” Leo wamefanya   mazoezi mepesi ya kutembea na kukimbia barabarani,pamoja na kucheza mpira kwenye Uwanja wa Tennis,Serengeti Boys wapo nchini Uturuki kwenye mashindano ya Kimataifa ya UEFA ASSIST kujiandaa na Fainali za Afrika za Vijana U17 zitakazofanyika Tanzania mwezi April mwaka huu.






MAHAKAMA YAAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUWASILISHA TAARIFA ZA KESI YA MKURUGENZI WA NIDA NA WENZAKE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeutaka upande wa mashitaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa zamani  (NIDA), Dickson Maimu na wenzake, kuharakisha mchakato wa kuwasilisha taarifa Mahakama Kuu kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Salim Ally ameyasema hayo leo Machi 5, 2019 baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kudai kuwa wapo katika kukamilisha taratibu za mwisho kuwasilisha nyaraka Mahakama ya Kuu, na kwamba wataitaarifu mahakama hiyo hatua walizofikia.

Hata hivyo, wakili wa utetezi, Joseph Ndunguru amedai upande wa mashitaka unatakiwa kusema ni taratibu zipi zinazokwamisha mpaka sasa ili mahakama itoe msaada maana tangu Januari 29, mwaka huu upande huo wa mashitaka wamekuwa wakidai upelelezi umekamilika na kuomba mahakama ipange kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa maelezo ya mashahidi.

Akijibu hoja hiyo, Wakili Simon amedai maandalizi wanayofanya ni ya nyaraka mbalimbali hivyo wanaomba wavumilie na kwamba hawataomba msaada kwao kwa sababu hatua hiyo ikikamilika watawapatia nyaraka.

Hatahivyo, Hakimu Ally alisema bado kuna mchakato wa kuwasilisha taarifa mahakama Kuu licha ya kwamba upelelezi umekamilika, ameongeza  upande wa mashitaka wafanye mchakato na wasichukue muda mrefu bali muongeze spidi ili shauri liendelee.

Maimu na wenzake  wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 7/2019 na kuisabishia serikali hasara ya Sh bilioni 1.16.

kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 19, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Maimu washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni Kayombo Xavery,  Meneja Biashara wa (NIDA), Aveln Momburi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers,  Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond.

Awali washitakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 26 likiwemo la uhujumu uchumi,  ila Januari 28,2019 waliachiwa huru na mahakama hiyo baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) kusema hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi yao.

Hata hivyo baada ya washitakiwa kuondolewa mashtaka hayo na kuachiwa huru walikamatwa tena na walifikishwa katika mahakama hiyo kisha kusomewa mashtaka mapya 100 yakiwemo 25 ya utakatishaji fedha. 

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 22 ya kughushi, mashtaka 43 ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri, mashtaka mawili ya kula njama, mashtaka 25 ya kutakatisha fedha na mashtaka matano ya kuisababishia hasara NIDA.

Pia washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la matumizi mabaya ya madara lipo moja ambalo linamkabili  Maimu na Sabina.

TANZANIA YAPATA MKOPO WA MASHARTI NAFUU SHILINGI BILIONI 589.26 KUTOKA AFDB KWA UJENZI WA BARABARA YA KABINGO (KAKONKO)-KASULU-MANYOVU KM 260 KWA KIWANGO CHA LAMI

$
0
0
 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James kulia akisaini mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu wenye thamani ya Shilingi bilioni 589.26 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB iliyowakilishwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo hapa nchini Dkt. Alex Mubiru (kushoto akisaini) katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. Fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akibadilishana mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) hapa nchini Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kutiliana saini mikataba miwili ya  mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Shilingi bilioni 589.26 itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akionesha mkataba wa mkopo wa masharti nafuu pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kusaini katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo kuhusiana na ramani ya ujenzi wa barabara ya kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 zitakazojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Kigoma.

 . Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya (Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo na wanahabari kuhusiana na mkopo huo wa masharti nafuu ambao utatumika katika ujenzi wa barabara mkoani Kigoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya (Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kusaini mikataba hiyo ya mkopo wenye masharti nafuu katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. 
Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii


EAC SPEAKERS LAUNCH REGIONAL PARLIAMENTARY INSTITUTE

$
0
0
cid:image001.png@01D4CAAF.6A5FD560
EAST AFRICAN LEGISLATIVE ASSEMBLY 
East African Legislative Assembly, Nairobi, Kenya: 4th March, 2019: Regional Speakers have launched the East African Parliamentary Institute (EAPI) in Nairobi, with the training outfit expected to harness capacities and narrow the skills gap of Parliamentarians and staff in the quest to further strengthen the integration process.

Speaking at the official launch  on Friday last week, EALA Speaker, Rt Hon Ngoga K Martin, underscored the importance of the institute’s presence in the region, to catapult the integration process and provide a valuable link between people within the EAC and beyond.  He remarked that EAPI would provide an adequate base of knowledge on legislative matters to Members of Parliament and staff who at times come from different background when they join Parliaments.

Rt Hon Ngoga lauded the regional speakers for their contribution to the process.  “The launch of the EAPI is definitely an indication of the total commitment accrued to the integration dispensation by Parliaments and by yourselves.    It is only befitting to recognize each and every one of you for the support you have personally and/or collectively accorded and extended to the EAPI”, Rt Hon Ngoga said.

The launch of EAPI follows the enactment of the East African Parliamentary Institute Bill, 2011, which anchors and provides for the legal framework of its establishment. The EAPI Act inter alia establishes a mechanism for capacity and skills development to promote professionalism through establishment of the institute thus giving effect to article 5 (1) of the Treaty.  The Speaker lauded the EAC Heads of State for assent to the Bill, whose operationalization, now sets basis for motion of the objectives of the Institute.

According to the Act, the regional Speakers form the Board of Trustees of the new Institution which shall be chaired by the EALA Speaker while the Clerk of the regional assembly shall oversee the activities of its Governing Council.  At the recent 38th Meeting of the Council of Ministers, the matter of an institutional structure was discussed and according to Rt Hon Ngoga, the Board of Trustees shall promptly propel forward the administrative framework to make EAPI fully operational.

Present at the occasion were Speaker of the Kenya National Assembly, Rt Hon Justin Muturi, Rt Hon Kenneth Lusaka, Speaker of the Senate of Kenya, the Vice President of the Senate of Rwanda, Hon Gakuba Jean d’ Arc and the Chair of the EAC Committee in Parliament of Uganda, Hon Ouma George Abbott, who represented the Speaker. The Speaker Emeritus of EALA, Rt Hon Abdirahin H. Abdi, was also in attendance.

In his remarks, Speaker of Senate of Kenya, Rt Hon Kenneth Lusaka, rallied for capacity development of legislators saying in remained critical in ensuring effective service delivery to the Parliamentary leadership, legislators and the electorate. The Speaker called for collective effort on the part of parliaments and all other stakeholders towards offering sustained commitment and unity of purpose.

On his part, Speaker of the Kenya National Assembly, Rt Hon Justin Muturi, affirmed that EAPI would be a catalyst in guiding legislators to embrace evidence-based legislation which would play a key part in ensuring quality of legislation is improved.  The Vice President of the Senate of Rwanda, Hon Gakuba Jean d’ Arc hailed the inception of the Institute as visionary and said the Parliament of Rwanda was committed to ensuring it is fully in operations.  Hon George Ouma Abbot of Parliament of Uganda reiterated the need for strong institutions in the integration dispensation. 

EAPI was initially mooted in 2001 as a joint venture between the State University of New York (SUNY), the National Assemblies of the Partner States and EALA as well as the United States International University (USIU). At that point, the FORD Foundation offered the initial seed fund.  

A key conference, bringing together senior parliamentary staff from the region took place 3 years later (in 2004) and the occasion served as an avenue to share experiences with regards to implementing change and embracing modernization in the respective legislatures. Under the new arrangement, Parliaments of the region are to largely fund the institution, a move hailed as key in its long-term sustainability.

 Earlier on, the regional Speakers and Clerks of the respective Assemblies met prior to the launch of the EAPI.
 The EALA Speaker, Rt Hon Ngoga Martin officiates at the launch of the East African Parliamentary Institute EAPI.  The Centre of the Parliamentary Studies and Training (CPST) is to house EAPI.
 Speaker of the Senate of Kenya, Rt Hon Kenneth Lusaka (left) is received by the Executive Director of the Centre for Parliamentary Studies and Training, Prof Nyokabi Kamau.
Earlier on, the regional Speakers and Clerks of the respective Assemblies met prior to the launch of the EAPI.
OFICIALLY UNVEILED: EALA Speaker, Rt Hon Ngoga K Martin unveils the plaque at the launch of the EAPI as other guests look on 

Wanaofanya vurugu mashamba ya Kilosa Kukamatwa, aonya RC Kebwe

$
0
0

Andrew Chimesela - Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Mkoa na Wilaya ya Kilosa kuwakamata wale wote wanaotuhumiwa kuwavamia wananchi wanaolima  katika mashamba yaliyofutiwa umiliki wake na Mhe. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dkt. Kebwe ametoa kauli hiyo Machi, 3 Mwaka huu alipofanya ziara Wilayani Kilosa iliyolenga kujiridhisha utekelezaji wa mashamba yaliyofutwa mwaka 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na kuagiza mashamba hayo kupangiwa matumizi mengine ikiwa ni pamoja na kuyagawa kwa wananchi wa maeneo jirani na mashamba hayo.
Akiwa Wilayani Kilosa, Dkt. Kebwe aliongea na wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe ambavyo viko jirani na shamba hayo matano kati ya 11 yaliyofutiwa umiliki Wilayani humo huku wananchi waliopewa kuyatumia kwa muda wakilalamika kupewa vitisho na baadhi ya watu kutojihusisha kulima mashamba hayo kwa madai kuwa ni mali yao.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro baada ya kupokea malalamiko hayo anaagiza Jeshi la polisi kuwakamata wale wote wanaowatishia wakulima hao. “Na hili naelekeza  Vyombo vya Ulinzi na Usalama, muanze kupekua kuanzia sasa, kama kuna kikundi cha watu kuna watu au hata mtu binafsi kafanya hivyo chukua hatua, kwa sababu sheria zipo” alisema  Dkt. Kebwe. 
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa aliwahakikishia wananchi wa vijiji hivyo kuwa kila mtu ambaye hana eneo la kulima atapatiwa kupitia mashamba hayo yaliyofutwa na Mhe. Rais ili kila mwananchi aweze kuzalisha na kujikimu kimaisha huku akionya kutoingiza itikadi ya aina yoyote kwenye mashamba hayo yaliyofutwa na Mhe. Rais.

Katika hatua nyingine Dkt. Kebwe amewataka wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe, kufuata utaratibu uliotolewa na Serikali wa kuyatumia mashamba hayo kwa muda wakisubiri mpango rasmi unaoendelea kuandaliwa na Serikali huku akiwaonya wanaotaka kuanzisha mipango mingine ya matumizi ya Ardhi hiyo  kinyume na mipango ya Serikali kusitisha mara moja mipango hiyo.
“Vyombo vyangu vinaniambia wale walikwenda wakavamia maeneo hayo walitaka waanzishe  mpango mwingine mpya, yaani juhudi zote hizi ambazo Serikali imefanya kwake yeye  si kitu. sasa hao mtusaidie tuwafahamu ni akina nani na tuwachukulie hatua, sio kuwafahamu tu” aliongeza Dkt. Kebwe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amewataka wananchi wa vijiji vya Mvumi na Gongwe kukomesha tabia ya ubishi na ugomvi baina yao, badala yake watekeleze maagizo ya Serikali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na kuwatahadhalisha kuwa atakayekwenda kinyume na maagizo hayo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za sheria.
Awali Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Kati, Hezekiely Kitilya aliewaeleza wananchi wa vijiji vya Mvumi na Gongwe kuwa Ardhi ya mashamba hayo matano kwa sasa bado ni ya Mhe. Rais na iko chini Kamishna wa Ardhi na wananchi wamepewa kuitumia kwa muda, hivyo ni vema wananchi wakawa watulivu na kuacha ugomvi baina yao.
Sambamba na hilo Bw. Kitilya aliwakumbusha wananchi maelekezo yaliyotolewa na ya Mhe. Rais mara baada ya kuyafuta, ambapo alisema kipaumbele cha kwanza kinawalenga  wananchi wanaozunguka mashamba hayo, cha pili ni kutenga Ardhi hiyo kwa ajili ya Uwekezaji wenye tija wa ndani na nje ya nchi na kuwa na hazina ya Ardhi kwa ajili matumizi mengine ya baadae.
Kwa mujibu wa Afisa Ardhi Wilaya ya Kilosa Bw. Ibrahim Ndembo, alisema Mashamba hayo matano Na. 32 hadi 36 yenye jumla ya Ekari 2,685, baada ya Mhe. Rais kuyafuta, Wilaya ilipeleka maombi Serikalini ili kupewa idhini ya kutumia mashamba hayo kwa muda ombi ambalo lilikubaliwa.
Baada ya kukubaliwana Wilaya iliunda Kamati za ugawaji maeneo ya mashamba hayo na kuyagawa katika sehemu mbili, Ekari 1000 kwa ajili ya wananchi wa Kijiji cha Mvumi na Ekari 1000 nyingine kwa ajili ya kijiji cha Gongwe. Hii inatokana na asili ya vijiji hivyo ambavyo awali kilikuwa ni kijiji kimoja na mwaka 2014 kiligawanyika na kuwa vijiji viwili, Mvumi na Gongwe.
Kwa upande wao Wananchi wa vijiji hivyo akiwemo Bi. Lakero Mkandawile wa kijiji cha Gongwe na Bi. Sara Seleman wa Kijiji cha Mvumi pamoja na Adhi Valaluke wa Kijiji cha Gongwe walimweleza  Mkuu wa Mkoa kero zao kuhusu mashamba hayo ikiwa ni pamoja na kupewa maeneo ya kulima kwenye mashamba ambayo tayari yana watu, kunyang’anywa mashamba waliokwisha pewa na kutishiwa kukatwa na mapanga tuhuma ambazo zilimhusisha pia Mwenyekiti wa Kijiji cha Mvumi Bw. Abdul Tumbo.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiongea na wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe Wilayani Kilosa Mkoani humo kuhusu matumizi ya mashamba matano yaliyofutiwa Umiliki na Dkt. John Pombe Magufuli.
 Umati wa Wananchi kutoka Vijiji vya Mvumi na Gongwe waliofika kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuhusu matumizi ya Ardhi ya mashamba matano yaliyofutiwa Umiliki na Dkt. John Pombe Magufuli .
    Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adamu Mgoyi (anayeongea na kipaza sauti) akiwaonya wananchi kufuata maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa kuhusu utaratibu wa kuyatumia mashamba yaliyofutiwa umiliki wake.

Germany Tuebingen festival and GAIEXPO 2019

$
0
0
The biggest global platform for Africa, Africans, fans and Africa interested in Germany is now open for registrations. To all Diaspora organizations, companies, Associations, groups and private Initiatives in Africa, Europe, Britain, USA, China etc...Register and participate. Dateline for Registration is June 30th. For all inquiries call, Email or Whatsapp us. 



RC Mghwira awataka wafanyabiashara wa Kilimanjaro kuchangamkia fursa za Benki ya CRDB

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amewataka wafanyabishara wa mkoa huo kuchangamkia fursa za kibiashara zinazopatikana ndani ya Benki ya CRDB ili kuboresha tija na ufanisi wa biashara zao na kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika dhana yake ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Mama Mghwira aliyasema hayo alipokuwa akifungua rasmi semina ya wafanyabishara wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi. Semina hiyo ilijumuisha wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, ili kuwaonyesha fursa mbalimbali zilizomo ndani ya Benki ya CRDB zitakazowawezesha kuongeza mitaji, kupata mikopo pamoja na ushauri wa kitaalamu ili kuongeza ufanisi wa biashara zao.

Alisema kuwa pamoja na lengo la kubwa la Benki ya CRDB kuandaa semina hiyo ya wafanyabiashara na wajasiliamali ili waweze kukua na Kukopesheka na kuboresha biashara zao, bado jukumu la kutumia fursa hizo linabaki mikononi mwa wafanyabishara hao.

Alisema kuwa Serikali kushirikiana na wadau kama Benki ya CRDB wana nia thabiti ya kujenga mazingira ya kuwawezesha wafanyabishara kupata mitaji ili kuongeza ukuzaji wa uchumi. Alisema kuwa kwa ubunifu ulionyeshwa na benki ya CRDB katika kuwainua wafanyabishara unaonyesha ni kwa kiasi gani Benki ya CRDB inasapoti kwa vitendo juhudi za serikali katika kujenga uchumi endelevu na wenye kugusa sekta zote za uzalishaji.

Kwa upande wa wafanyabishara wadogo maarufu kama wamachinga, Mheshimiwa Mghwira aliitaka Benki ya CRDB kuendelea kuwa wabunifu na kuleta bidhaa kwa ajili ya kundi la wateja wadogo yaani wamachinga ambao wana mchango mkubwa katika uchumi wa taifa. “Serikali imeanza kwa kutoa vitambulisho kwa wajasiliamari ili kuwarasimisha, hivyo Benki zina kujukumu la kwenda mbele zaidi kwa kuwapatia mikopo nafuu ili waweze kukuza baishara zao” alisema mheshimiwa Mughwila.

Akizungumza katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela, alisema “Hakuna biashara inayofanikiwa bila kuongeza mitaji na kuzikabili changamoto zake. Lengo kuu la Benki ya CRDB ni kuwafungulia fursa nyingi zinazoweza kuendeleza biashara zao.

Mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina hii, wafanyabiashara pia watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao na hivyo kuongeza ujuzi wa kibiashara na kupanua wigo na masoko ya biashara zao” alisema.

 Nsekela alisema kuwa Benki ya CRDB inatambua umuhimu wa wafanyabiashara katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanyabiashara hao hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.

“Nichukue fursa hii kuwahakikishia wafanyabishara wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa Benki ya CRDB imejipanga vyema katika kufikia matarajio yao yote ya kibenki.

“Huduma zetu zinakidhi mahitaji ya makundi yote ya jamii kuanzia watoto, wakubwa, kinamama, wafanyabishara wadogo, wakati na wakubwa. Pia tunafanya biashara za Bima na kukusanya malipo yote ya serikali kuanzia malipo ya ankara, kodi na mengineyo. Pia Benki inawahudumia wateja wadogowadogo kupitia kitengo chake cha wajasiliamari yaani CRDB Bank Microfinace” alisema Nsekela.

Semina ya Benki ya CRDB kwa wafanyabishara wa mkoa wa Kilimanjaro ni sehemu ya mipango mkakati wa Benki hiyo wa kuwafikia wateja wake ilik kuwaainishia huduma mbalimbali zinazopatikana ndani ya benki ya CRDB. Benki pia imeshafanya semina kama hizo kwenye mikoa ya Mwanza, Arusha, Iringa na Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akizungumza wakati alipokuwa akifungua rasmi semina ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyoandaliwa na Benki ya CRDB ambayo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa semina ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyoandaliwa na Benki ya CRDB ambayo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akizungumza wakati wa semina ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyoandaliwa na Benki ya CRDB ambayo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.


















DTB FC kucheza ligi ya mabingwa wa mikoa ya TFF

$
0
0
Mchezaji wa timu ya DTB FC, Godfrey Wambura, akikabiliana na washambuliaji toka timu ya Buyuni FC katika mechi ya mwisho ya hatua ya Sita Bora ya ligi ya Kanda ya Dar es Salaam iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwananyamala B. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya benki ya (DTB FC) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanikiwa kufuzu katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayosimamiwa na Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF).



Timu ya mpira wa miguu ya benki ya (DTB FC) imefanikiwa kufuzu katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayosimamiwa na Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF).

DTB FC imepata nafasi hiyo baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Mbuyuni FC katika mchezo wa mwisho uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwananyamala B katika manispaa ya Kinondoni.

Timu hiyo imemaliza katika nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi tisa (9) baada ya kucheza mechi tano.Ubora wa Timu ya DTB umedhihirika baada ya kushinda michezo miwili (2), kutoka suluhu katika michezo mitatu (3) na kutokupoteza mchezo hata mmoja.

Timu nyingine zilizopata nafasi ya kuiwakilisha mkoa wa Dar es Salaam ni Pan African na Buyuni FC.Mbali ya timu hizo tatu, timu nyingine zilizoshiriki katika hatua ya Sita bora ni Kigamboni FC, Ungindoni FC na Panama.

Meneja wa timu ya DTB FC, Michael Lugalela amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya ligi ya mabingwa wa mikoa na kuwataka wasibweteke.

“Natoa shukrani kwa uongozi wa benki ya DTB kwa kuihudimia timu kuanzia kushiriki katika mashindano mbali mbali na mpaka kushiriki katika ligi ya mkoa na kufuzu kuwania nafasi ya kushiriki ligi daraja la pili ya TFF, tunajivunia na tumedhihirisha kuwa tunaweza,” alisema Michael.

Alisema kuwa bado wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanafanya vyema katika mashindano hayo ambayo ushirikisha timu bingwa kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.

WAZIRI MPANGO NA KAIRUKI WAWASILI WILAYA YA HAI KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WAWEKEZAJI WALIYOWASILISHA KWA RAIS MAGUFULI.

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga.Hai.

WAZIRI wa fedha na Mipango Dkt Philip Mpango akiwa ameongozana na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angela Kairuki wamefika katika wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro kushughulikia kile alichokiita unyanyasaji kwa wawekezaji.

Mawaziri hao wanakutana na Makundi mbalimbali kwa nyakati tofauti kusikiliza malalamiko yao waliyowasilisha kwa Mh Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.


Miongoni mwa Makundi na taasisi zinazoshiriki kikao hicho kinachofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai n pamoja na kundi la wawekezaji, Viongozi wa vyama vya ushirika,Mamlaka ya Mapato (TRA) ,Uhamiaji,TIC na Viongozi was serikali ngazi ya mkoa na wilaya ya Hai na Siha.
Waziri was Fedha na Mpango ,Dkt Philip Mpango (katika) akizungumza wakati wa kikao na wawekezaji wenye malalamiko pamoja na Viongozi wa serikali na baadhi ya taasisi zake.kushoto ni Waziri was nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angela Kairuki na kulia no Mkuu wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango kuhusu unyanyasaji kwa wawekezaji.

WAHUJUMU WA ZAO LA KAHAWA MKOANI KAGERA WATAFUTE BIASHARA NYINGINE - RC GAGUTI

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus - Karagwe

Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti imesema haitafumbia macho wale wote wenye mpango wa kuhujumu zao la Kahawa Mkoani Kagera kwa kununua na kuuza kahawa ya magendo, kahawa changa (butula), na wale wote wenye nia ya kuhujumu Biashara hiyo kwa namna yoyote ile katika msimu unaokwenda kuanza Mapema mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 32 wa Chama Kikuu cha Ushirika Wilayani Karagwe na Kyerwa Karagwe Development Cooperative Union Limited (KDCU LTD) Mkuu wa Mkoa Gaguti katika Ukumbi wa CCM Kayanga Machi 05, 2019, amesema kwa msimu uliopita kuna baadhi ya Viongozi wamehusika katika kuhujumu zao la Kahawa kwa kunufaisha matumbo yao na sasa hatua za haraka zitachukuliwa ili kuhakikisha Mkulima ananufaika na Kahawa yake.

Mh. Gaguti amesema Serikali inatambua changamoto ya Bei ya Zao la Kahawa ni ya wadau wengi, lakini kama Serikali itatimiza wajibu wake wa kuendelea kukutana na kuwashirikisha wadau wote wa kahawa kujadili suala hili, huku na KDCU nao kama chama Kikuu kuweka taratibu zao za uberoshaji wa Zao hilo kuanzia katika Vyama vya msingi, na adhma yake ni kuona zao hilo linauzwa katika mifumo rasmi iliyoratibiwa na chama Kikuu, huku takwimu zikionyesha kwa msimu uliopita Mkoa ulikusanya Kahawa kilo Milioni 58. 9 ambapo KDCU Ltd walikusanya Kilo milioni 39 sawa na 67%.

Awali kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Karagwe Mh. Godfrey Mheluka Amewakumbusha wajumbe wa mkutano Mkuu juu ya mfuko wa Bima ya Afya na Mazao yote ya Ushirika uliozinduliwa Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na hivyo kuwataka wanachama wote wa KDCU kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na yale yote yatokanayo na mfuko huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 32 wa KDCU LTD (hawapo pichani) Mjini Kayanga Wilayani Karagwe.
Mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka akisisitiza jambo wakati akitoa salaamu zake kabla ya Kumkaribisha Mgeni rasmi katika Mkutano wa 32 wa KDCU LTD.
Pichani ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Kagera Ndg Hamim Mahamudu akisisitiza juu ya kuimarisha Ushirika, ili kupitia Ushirika huo Mkulima aweze kupambana na Maadui watatu ambao ni Ujinga, Maradhi na Umasikini.

Pichani ni sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KDCU LTD wakiendelea kufuatilia Mkutano huo katika Ukumbi wa CCM Kayanga Karagwe
Viewing all 109935 articles
Browse latest View live




Latest Images