Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

WAZIRI SHONZA ASHIRIKI MAONESHO YA WADAU WA SHEREHE NA HARUSI YA ADORABLE WEDDING TRADE FAIR JIJINI DAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akipata maelekezo kuhusu bidhaa za wajasiriamali wa Sherehe na Harusi kutoka kwa Mkurugenzi wa Adorable Wedding Trade Fair Bi. Anna Lema wakati wa maonesho ya wadau wa Sherehe na Harusi ya Adorable Wedding Trade Fair yaliyofanyika jana jijini Dar Es Salaam.

Rwanda yawasihi wananchi wake kusitisha ziara na biashara nchini Uganda

$
0
0
Serikali ya Rwanda imewasihi wananchi wake kusitisha ziara zao nchini Uganda baada ya kuishtumu nchi hiyo kuwanyanyasa raia wake wanaoishi ama kutembelea nchini humo.

Uganda imeishutumu Rwanda kufunga mipaka baina ya nchi mbili,lakini Rwanda imekanusha na kusema mipaka iko wazi.

Alhamisi iliyopita mamlaka ya mapato ya Rwanda iliamrisha maroli ya mizigo kutotumia tena mpaka wa Gatuna kwa madai ya shughuli za ujenzi wa kituo kimoja cha mpakani 'one stop border' baina yake na Uganda.

Kwa mjibu wa mamlaka ya mapato ya Rwanda malori yaliombwa kutumia mpaka wa pili wa Kagitumba kaskazini mwa Rwanda.Hata hivyo watumiaji wa mipaka hiyo miwili hupendelea njia ya mpaka wa Gatuna kuwa rahisi na fupi kuliko ya mpaka wa Kagitumba.

Rwanda inaishutumu Uganda kunyanyasa wanyarwanda wanaoishi ama kufanyia biashara nchini Uganda na pia kuunga mkono makundi ya waasi hususani kundi la Rwanda National Congres linaloongozwa na mkuu wa zamani wa majeshi Jenerali Kayumba Nyamwasa aliyeko uhamishoni nchini Afrika kusini.

Kwa upande mwingine, Uganda inashutumu Rwanda kwa vitendo vya kijasusi kwenye ardhi yake huku ikiwashuku baadhi ya raia wa Rwanda kuhusika na vitendo hivyo.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI WAWILI, BALOZI MMOJA PAMOJA NA KUSHUHUDIA UAPISHWAJI WA MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Dkt. Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Yahya Simba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha Mawaziri wawili, Balozi mmoja na kushuhudia uapishwaji wa Maofisa watano wa Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna Benedict Michael Wakulyamba mara baada ya hafla ya uapisho kukamilika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na Makamishna watano kutoka jeshi la Polisi, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi, pamoja na Balozi Yahya Simba mara baada ya hafla ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Dini mara baada ya hafla ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na Maofisa Mbalimbali wa Jeshi kutoka Jeshi la Polisi mara baada ya hafla ya Uapisho wa viongozi mbalimbali  Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustine Mahiga akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma   na  Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na Makamishna watano kutoka Jeshi la Polisi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimvalisha cheo kipya cha Kamishna Liberatus Sabas ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimuapisha Kamishna Liberatus Sabas ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimvalisha cheo kipya cha Kamishna Leonard Paul Lwabuzala ambaye ameteuliwa kuwa kamishna wa kamisheni ya polisi Fedha na Lojistiki, Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU 

RAIS DK. MAGUFULI ASHANGAZWA NA UKIMYA WA POLISI SAKATA KUTEKWA MO

$
0
0
 *Asema Watanzania wanajiuliza maswali mengi
 *Akumbuka mtekwaji alivyokunywa chai na Mambosasa

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amesema anashangazwa na ukimya wa Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya waliohusika na utekaji wa mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewj 'MO'.

Hayo ameyasema leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuapishwa kwa mawaziri wawili baada ya kufanya mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri ambapo Profesa Paramagamba Kabudi aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria , amemteua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wakati Dk.Agustino Mahiga aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa amemteua kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Rais Magufuli akiwa anazungumzia utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini  ametumia nafasi hiyo kutolea mfano tukio la kutekwa kwa MO ambaye baada ya kutekwa kuna mambo mengi yamezungumzwa.

"Baada ya tukio la kutekwa kwa Mohamed stori zilikuwa nyingi sana, tukaambiwa kuwa kuna wazungu wamehusika.Tukaambiwa ameonekana Gymkhana , watu wanajiuliza aliendaje pale?Aliyeteka akaacha na bunduki , watu wanajiuliza alivyoacha bundiki eneo la tukio je angekutana na wanaomtafuta(Polisi).


"Pia tukaambiwa mtekaji alijaribu kuchoma gari.Baadae tunaona mtekwaji anakunywa chai na Mambosasa.  Lazima hili jambo lifike mwisho,watanzania walitarajia mmiliki wa nyumba anakamatwa na Polisi ili ajibu watu waliingiaje nyumbani kwake na wakaa siku zote hizo?

"Watanzania hata kama watakuwa kimya katika jambo hili lakini moyoni wana vingongo sana. Watanzania sio wajinga kwani wanajua kuchambua mambo,"amesema Rais Magufuli.

Wakati anafafanua zaidi kuhusu sakata hilo la MO, Rais Magufuli amesema Watanzania walitarajia kuoana wanaotuhumiwa siku inayofuata wanafikishwa Mahakamani lakini tangu tukio hilo litokee ni miezi sita sasa, hakuna chochote ambacho kimeendelea.

"Watanzania walitarajia kesho yake watuhumiwa wapelekwe mahakamani,basi hata mwenye nyumba alitakiwa kuuliza waliokuwa ndani ya nyumba ni akina nani? Lazima tujenge taswira nzuri ya Jeshi la Polisi kama lilivyoanzishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,"amesema Rais Magufuli.

Akizungumzia zaidi utendaji kazi wa Jeshi la Polisi ,Rais Magufuli amesema wachache ambao wanalichafua Jeshi la Polisi lazima wachukuliwe hatua."IGP wale ambao watashindwa kutekeleza majukumu yako wasiwe wanapelekwa makao makuu bali wawe chini ya Ma-RPC wengine.
"IGP usiogope kuleta majina ya watakaoshindwa kufanya vizuri.Lete tuwatoe nyota zao.Najua wapo ambao wameshindwa kufanya vizuri, ndio maana yule wa Shinyanga tulimtoa kwani katika lile sakata la sukari tunajua nini ambacho kilikifanyika,"amesema Rais Magufuli.

Pia amesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu naye hakufanya  vizuri, aliyekuwa ana Kaimu Mkoa wa Arusha naye hakuwa anafanya vizuri huku akieleza kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ameponea chupuchupu.

"Amesalimika kwasababu tunajua uwezo wake wa kufanya kazi ni mzuri ndio maana tukaamua kumuangalia na kisha tumempeleka  Arusha.Wakati wa tukio la kuibwa kwa Almasi yeye alikwenda kujificha Ukerewe,"amesema Rais Magufuli.

BALOZI KAMALA AISHUKURU TAASISI YA WORLD VISION KWA KAZI NZURI YA KUHUDUMIA WANANCHI WA MISSENYI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala  katikati, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa World Vision Tanzania Mhe. Gilbert Kamanga wa kwanza kulia na Mkurugenzi wa Miradi wa World Vision Tanzania  Dr Yosh Kasilima kushoto mara  baada ya kikao cha pamoja kilichofanyika Makao Makuu ya World Vision Arusha leo  hii. Balozi Kamala amefika World Vision kuwashukuru  kwa kazi nzuri wanayofanya Missenyi  kuhudumia Wananchi katika sekta za maji, elimu, na kupambana na umaskini.

wajasiliamali maeneo ya Goba ,Ubungo jijini Dar

$
0
0
Wafanyabiashara ndogondogo wa kituo cha mabasi Goba wilaya ya Ubungo  jijini Dar es Salaam wakipanga biashara zao tayari kuwa kusubiri wateja.
Wafanyabiashara ndogondogo wa kituo cha mabasi Goba wilaya ya Ubungo  jijini Dar es Salaam   wakisubiri  wateja wanaotoka maeneo mbalimbali ya jijini ili kununua mahitaji yao.
Wafanyabiashara wakendelea na biashara zao katika kituo cha mabasi Goba wilaya ya Ubungo  jijini Dar es Salaam .  (Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)

MKAZI WA KIMARA AIBUKA NA MILIONI TANO ZA BIKO

$
0
0
Mshindi wa sh milioni tano, ambaye mkazi wa Kimara King'ongo, jijini Dar es Salaam, Jafari Juma Said anayejihusisha na ufundi wa magari, amekabidhiwa fedha zake za ushindi huo kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam. Picha zote na Mpigapicha Wetu.

DC PANGANI AWAFUNDA VIJANA

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Zainabu Abdallah akizungumza wakati akifungua warsha ya vijana juu ya kutambua malengo 17 ya maendeleo endelevu ya Dunia yaliyoendeshwa na serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) yakishirikisha vijana 100 wa kike na kiume kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Alvaro Rodrigues kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange 
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Alvaro Rodrigues akizungumza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia ni Mwenzeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Didi Nafisa ambaye pia ni Afisa Habari wa Shirika hilo 
Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange akizungumza 
Mwenzeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Didi Nafisa ambaye pia ni Afisa Habari wa Shirika hilo akizungumza 
Sehemu ya Vijana kutoka maeneo mbalimbali wilayani Pangani wakifuatilia warsha hiyo kwa umakini 



MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Zainabu Abdallah amesema umaskini hauwezi kuondoka ikiwa vijana bado watakuwa mawazo ya potofu kuhusiana na umaskini huku wakitakiwa kuuchukia. 

Zainabu aliyasema hayo mjini Pangani wakati akifungua warsha ya vijana juu ya kutambua malengo 17 ya maendeleo endelevu ya Dunia yaliyoendeshwa na serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) yakishirikisha vijana 100 wa kike na kiume. Alisema lazima vijana watambua upo umuhimu wa kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao badala ya kukaa na kuacha kufikiria kukaa vijiweni na kujiingia kwenye makundi yasiyokuwa na tija kwa maendeleo. 

“Matatizo ya vijana wanayafahamu vijana hivyo serikali ipo tayari kuwaunga mkono kwa juhudi zozote mnatakazo anzisha …lakini pia mwaka huu kuna chaguzi za serikali za mita hivyo tunataka viongozi vijana tutakaoweza kuzungumza nao lugha moja na kusimamia maendeleo endelevu ya dunia”Alisema. 

Aidha alisema kupitia mafunzo hayo yatasaidia kuongeza wigo mpana wa fursa kwa vijana wilayani humo ambao watakwenda kuibadilisha wilaya hiyo na kuwataka wazazi kuhakikisha wanawapatia elimu bora watoto waop badala ya kujiingiza kwenye shughuli za uvuvi. Mkuu huyo wa wilaya aliwataka vijana wa Pangani kuchangmkia fursa hiyo ili iweze kuwasaidia ikiwemo kujitambua kwamba wana nafasi gani kwa Taifa na wilaya kwa kujiletea maendeleo kwani wao ndio chachu ya mafanikio kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kiuchumi, kisiasa na kujamii. 

Awali akizungumza wakati wa warsha hiyo Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Alvaro Rodrigues alisema uwepo wao ni kwa ajili ya kutekeleza malengo endelevu ambayo ndio malengo ya dunia 2016 hadi 2030 kwa kuwapatia elimu vijana ili wawezi kujitambua na kuona namna ya kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao. 

Alisema pia kwenye mafunzo hayo wanajikita kuwasaidia wanawake kutokana na kwamba asilimia 50 ya watu duniani ni wanawake hivyo wakiachwa nyuma dunia inaweza kudhoofisha maendeleo. 
“Nusu ya idadi ya watu dunia ni wanawake hivyo ikiwa wataachwa nyuma kwenye Nyanja zote za kimaendeleo maanake tutakuwa tumerudisha nyuma ukuaji wa uchumi kwa wananchi”Alisema .

Hata hivyo alisema ifikapo 2030 wawe na ulimwengu bora kwa kuzingatia malengo ya milenia katika kuhakikisha vijana wanazingatia malengo ya maendeleo endelevu ambayo ni watu, sayari, ustawi, amani na ushirikiano. 

Kwa upande wake Mwenzeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Didi Nafisa aliwataka vijana walioshiriki kwenye warsha hiyo kuzingatia mafunzo hayo ili yaweze kuwa na tija ikiwemo kubadilisha maisha yao. 

Nafisa ambaye pia ni Afisa Habari wa Shirika hilo alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwakwamua vijana na tatizo la ukosefu wa ajira ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa nchi nyingi dunia. 
“Tatizo la ukosefu wa kazi dunia linaongezeka kutoka watu milioni 170 kwa mwaka 2007 hadi kufikia milioni 202 mwaka 2012 hapo utaona sasa watu milioni 75 kati ya hao ni vijana wa kike na kiume”Alisema.

RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN AWAAPISHA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Sheria Ndg Goerg Joseph Kazi, hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, wakihudhuria hafla ya kuapishwa Mawaziri na Makatibu Wakuu walioteuliwa hivi karibuni,hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar leo,(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi, anayeshuhulikia Masuala ua Uvuvi na Mifugo Dr.Omar Ali Amir.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Dkt. Ali Mohamed Shein,akisaini Hati ya Kiapo ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar anayeshughulikia Masuala ya Mifugo na Uvuvi Dr.Omar Ali Amir.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Ndg Seif Shaban Mwinyi, hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba, Maji na Nishati. Ndg. Salhina Ameir Mwita, hafla hiyi imefanyika leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Bi.Mansura Misi Kassim, hafla hiyo imefanyika Ikulu leo Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa Serikali  Said Hassan Said na kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh, Omar Saleh Kabi,waliosimama nyumba ni Mawaziri aliowaapisha leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)   
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa Serikali  Said Hassan Said na kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh, Omar Saleh Kabi,waliosimama nyumba ni Makatibu Wakuu na Manaibu aliowaapisha leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)     
 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, wakihudhuria hafla ya kuapishwa Mawaziri na Makatibu Wakuu walioteuliwa hivi karibuni,hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar leo,(Picha na Ikulu)

TRA IGUNGA YAFANYA OPERESHENI YA KUKAGUA MATUMIZI YA MASHINE ZA EFD

$
0
0
Na Amisa Mussa
Mamalaka ya  Mapato ( TRA ) Wilaya   ya  Igunga  Mkoani Tabora imeendesha  Operasheni maalumu ya  kukagua  na kutoa Elimu ya matumizi ya mashine za Kielektroniki ( Efd ) kwa Wafanyabiashara wilayani humo,na kubaini kuwepo kwa baadhi ya Wafanyabiashara ambao Bado  wanafanya biashara bila kutoa risiti za Manunuzi kwa Wateja wao,jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya mapato.
Oparesheni hiyo ambayo  imeongozwa na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato  (TRA)  Wilaya ya Igunga,John Mgeni amesema  Mamlaka hiyo licha ya kuwaelimisha Wafanyabiashara  na Wananchi Wilayani humo kuhusu Matumizi Sahihi  ya mashine za Kielektroniki  (Efd), Lakini bado amebaini kuna tatizo,hivyo amebainisha kuwa hatua kali  zitakazochukuliwa dhidi ya Wafanyabiashara na Wateja watakao shindwa Kuzingatia  Utaratibu huo na kusababisha kurudisha nyuma Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali.
Kaimu Meneja Wa Mamlaka Ya Mapato (TRA) Wilaya Ya Igunga, John Mgeni akikagua mashine ya EFD
Kaimu Meneja Wa Mamlaka Ya Mapato (TRA) Wilaya Ya Igunga, John Mgeni akikagua mashine ya EFD kwenye moja ya duka.

Wakulima Ruvuma Wanufaika na Uwekezaji wa Viwanda

WASOMI NCHINI WATAKIWA KUWEKEZA KATIKA TAFITI

$
0
0
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Wasomi Vyuo Vikuu na vyuo vya elimu ya juu nchini wametakiwa kuwekeza katika tafiti mbalimbali ili kuisadia Jamii ya kitanzania katika harakati za kufikia uchumi wa kati.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo alipokuwa kifungua kongamano la siku tatu la kimataifa la lenye kauli mbiu ya ‘State Building in Africa: Prospects and Challenges’ lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam.

“Tafiti zinatija kubwa katika maendeleo ya jamii kwa sababu wasomi hutambua majibu sahihi ambayo hutoa dira ya kuisaidia jamii. Vyuo vinamajukumu matatu, kufundisha , kutafiti na kuhudumia jamii, kwa hiyo elimu inayotolewa na vyuo inatakiwa kurudisha huduma kwa jamii kwa kuwa na majibu sahihi ya kusaidia maendeleo ya watu,” anasema Akwilapo.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Profesa. Shadrack Mwakalila alisema kongamano hilo la Kimataifa limewakutanisha wanazuoni kutoka mataifa mbalimbali.

Anasema kusudio la kongamano hilo ni wanazuoni kuchakata mawazo kwa kuchambua tafiti mbalimbali kwa lengo la kujenga nchi za Kiafrika.

“ Kongamano hili la Kimataifa ni la kwanza kufanyika hapa Chuoni. Ila Chuo kina utamaduni wa kufanya makongamano mara kwa mara kwa lengo la kukutanisha wasomi na wadau wa elimu na maendeleo kujadili mambo mengi yanayotokana na tafiti walizozifanya ikiwa ni pamoja na Kukumbuka Waasisi wa Taifa letu.” anasema Profesa Mwakalila.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Utafiti wa Chuo cha Sayansi ya Jamii kwa Afrika kutoka Urusi, Dk. Dmitri M. Bondarenko alisema Chuo chao kimejikita katika tafiti za kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikabiri jamii.

“Kujenga Taifa baada ya uhuru ilikuwa rahisi lakini changamoto za sasa kutokana na utandawazi zinachochea kupoteza uzalendo hatua ambayo imesababisha changamoto kubwa kwa nchi nyingi kupiga hatua za kimaendeleo,” anasema Dk. Bondarenko.

Awali akitoa salam za ukaribisho, Naibu Mkuu wa Chuo – Taaluma Prof. Richard Kangalawe amesema Kongamanao hilo limeandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na Chuo cha Sayansi ya Jamii kwa Afrika kutoka Urusi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la Kimataifa la kwanza katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Profesa. Shadrack Mwakalila akitoa neno kwa wana taaluma waliohudhulia katika Kongamano la Kimataifa 
Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Richard Kangalawe akitoa Salamu za Ukaribisho kwa Wanataaluma waliohudhuria katika Kongamano la kwanza la kimataifa 
Naibu Mkuu wa Chuo - Utawala Dk. Godwin Kaganda akitoa neno la shukrani kwa wana Taaluma waliofika katika kongamano hilo.
Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mh Yuri Popov akisalimia Washiriki waliofika katika Kongamano la Kimataifa lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na Chuo cha Sayansi ya Jamii kwa Afrika kutoka Urusi. 
Baadhi ya wageni walioshiriki kwenye kongamano hilo lenye kauli mbiu ya 'State Building in Africa: Prospects and Challenges’ 
Baadhi ya wageni walioshiriki kwenye kongamano hilo lenye kauli mbiu ya 'State Building in Africa: Prospects and Challenges’. Zaidi ya nchi saba zimeshiriki katika Kongamano hilo.
Baadhi ya wageni walioshiriki kwenye kongamano hilo lenye kauli mbiu ya 'State Building in Africa: Prospects and Challenges’ 
Viongozi wa Meza Kuu wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya Wadau na wana taaluma kutoka Mataifa mbalimbali walioshiriki Kongamano la Kimataifa katika Chuo cha Kumbukumbu ya MwalimuNyerere Kampasi ya Kivukoni

MKURUGENZI KAMPUNI YA UWINDAJI YA OBC APANDISHWA KIZIMBANI

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uwindaji ya Otterlo Business Corporation (OBC) inayofanya shughuli zake katika Mji wa Loliondo wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha Isack Mollel{59} amepandishwa kizimbani kujibu mashitaka kumi ikiwemo uhujumu uchumi,utakatishaji fedha haramu,kugushi na kutoa maelezo ya uongo ya kukwepa kodi ya mabilioni ya pesa.

Akisomewa mashitaka na Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Serikali,Osward Tibabyekomya akisaidiwa na Materius Marandu na Dismas Mwigunyiza mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha ilidaiwa kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo kati ya mwaka 2011 hadi 2018 kinyume cha sheria ya makosa ya jinai vifungu namba 333,335 na 337 vya kanuni ya adhabu na kufanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Tibabyekomya alidai kuwa shitaka la kwanza linalomkabili Mollel ni kosa la kugushi nyaraka kwani kati ya septemba 15 mwaka 2017 na aprill 7 mwaka jana ndani ya Jiji la Arusha Mollel aligushi ivoince namba 9091 ya septemba 15 mwaka 2017 ikieleza kuwa kampuni ya OBC  ilinunuwa gari la kifahari lenye namba za Chassis WDB62433615367735 kutoka kampuni ya magari ya Evarest Motors(FZD) ya Dubai kwa gharama ya dola za kimarekani 12,800 .

Shitaka la pili ni kugushi nyaraka tarehe hiyo hiyo mwaka 2017 na mwaka jana aligushi invoice namba 9092 ikionyesha kuwa OBC ilinunuwa gari aina ya Man Truck yenye chassis namba WMA 5500231W007547 kutoka kampuni ya magari ya Evarest Motors ya Dubai kwa thamani ya dola za kimarekani 12,000.

Tibabyekomya alisoma shitaka la tatu linamkabili Mollel kama Mkurugenzi Mtendaji wa OBC ni pamoja na kutoa taarifa za uongo march 7 mwaka jana kuwa akiwa Holili Mkoani Kilimanjaro mpakani mwa Tanzania na nchi jirani ya Kenya mtuhumiwa anatuhumiwa kutoa taarifa za uongo kwa Mamlaka ya Mapato Nchini{TRA} idara ya ushuru wa forodha yenye lengo la kukwepa kulipa kodi ya serikali.

Ilidaiwa kuwa Kampuni ya OBC ilikwepa kulipa kodi sahihi na kuamuwa kuidanganya serikali na kuingizia hasara ya mamilioni ya fedha kwa kuingiza nchini magari matatu ya kifahari Man Truck chassis WMA5500231W007547, Mercedes Benz chassis namba UWDB62433615367735 na Mercedes   Benz Chassis namba UWDB62430415145210 kutoka kampuni ya magari ya Dubai.

Shitaka la nne linalomkabili Mollel pamoja na kampuni ya OBC akiwa kama Mkurugenzi wa kampuni ilidaiwa kuwa julai 2011 na julai 2015 kwa pamoja katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro waliingiza nchini magari 31 ya utalii na uwindaji na kukwepa kulipa kodi ya serikali zaidi ya shilingi bilioni 2.2.

Mwendesha mashitaka alisoma shitaka la tano linalomkabili Mollel ni kutoa taarifa za uongo kwa TRA mei 25 mwaka 2013 na februali 4 mwaka 2015 na kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya shilingi milioni 299 na kuingiza nchini magari sita bila ya kulipa ushuru wa serikali kutoka kampuni ya magari ya Evarest Motor iliyopo nchini Dubai,

Tibabyekomya alidai kuwa shitaka la sita ni Mollel kutuhumiwa kutoa taarifa za uongo na kukwepa kulipa kodi ya serikali zaidi ya shilingi milioni 111 na kuingiza nchini magari mawili ya kifahari Land Cruisser  Pick Up chassis namba JTELB71J707112476 na Ford Ranger Chassis MNCLS329558W735840 yaliyonunuliwa kutoka kampuni hiyo ya Dubai.

Alisoma shitaka la saba ni Februali 18 mwaka 2017 Jijini Dar es salaam Mollel anatuhumiwa kukwepa kulipa kodi ya serikali ya zaidi ya shilingi milioni 199 kwa kuingiza magari mawili ya kifahari ya Nissan Patroll chassis namba JN8FY1NY3EX002626 na Mercedes Benz chassis namba WDCYR48F78X173956.

Mwendesha mashitaka wa serikali alisoma shitaka la nane la utakatishaji fedha haramu ilidaiwa kuwa aprill 3 mwaka jana Holili Mkoani Kilimanjaro Mollel alificha umiliki na mali kwa kutumia jina la kampuni ya OBC kwani aliandikisha jina la gari aina ya Man Truck chassis WMA5500231W007547 yenye namba za usajili T141DNM iliyosajiliwa kwa jina la kampuni wakati gari hilo ni mali yake.

Tibabyemkomya alisoma shitaka la tisa la utakatishaji fedha haramu kwani inadaiw akuwa Mollel na OBC waliidanganya serikali kwa kuingiza magari na kubadilisha umiliki kutoka kampuni hadi umiliki wake wakati akijuwa wazi kufanya hivyo ni kosa kisheria na kuisababishia serikali hasara.

Shitaka la kumi ni uhujumu uchumi kwani ilielezwa mahakamani hapo kuwa januari 2010 hadi 2018 Mkoani Arusha na Kilimanjaro ,Mollel na kampuni ya OBC waliingizia hasara serikali ya zaidi ya shilingi bilioni 2.8 kwa kutoa maelezo ya uongo TRA juu ya uingizwaji wa magari 31 hapa nchini.

Hakimu Mwakatobe alimweleza mtuhumiwa kuwa hakutakiwa kujibu chochote juu ya mashitaka hayo kwani mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kesi hiyo ilihairishwa hadi marc 18 mwaka huu. Mollel anatetewa na mawakili watatu maarufu Jijini Arusha wakiongozwa na Method Kimomogolo akisaidiwa na Daud Haraka na Godluck Peter.

Wakati huo huo Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa Mkoani Arusha{TAKUKURU} imewapandisha kizimbani Wahasibu wakuu wawili wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro{NCAA},David Shauri na Joseph Msafiri kwa mashitaka mawili ya uhujumu uchumi na kuitia hasara mamlaka hiyo ya zaidi ya dola za kimarekani 82,850.

SERENGETI BOYS YAANZA MICHUANO YA UEFA ASSIST,YAKUNWA GOLI 1-0 DHIDI YA GUINEA.

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KIKOSI cha vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys kimeanza michuano ya UEFA Assist kwa kukubali kufungwa goli 1-0 dhidi ya wapinzani wao Guinea.

Mchezo huo wa kwanza kwa Serengeti Boys ulichezwa kwenye Uwanja wa Emri Complex, huku mvua kubwa ikiwa inanyesha.

Katika mchezo huo, kipindi cha kwanza kilionekana kutawaliwa zaidi na wapinzani wao Guinea na wakatumia udhaifu wa safu ya ulinzi ya Serengeti Boys pamoja na golikipa kupata goli la kuongoza.

Safu ya ushambuliaji ya Serengeti Boys ilishindwa kuwa na maelewano mazuri na kushindwa kuwa na mipango ya kusawazisha goli hilo.Mpaka mpira huo unaenda mapumziko Serengeti Boys walitoka wakiwa nyuma kwa goli moja dhidi ya Guinea.

Kipindi cha pili kilianza na Serengeti Boys wakionekana kupata uhai na kutaka kutafuta goli la kusawazisha ila kujiamini kwa wachezaji wa Guinea kilizidi kuwapa wakati mgumu vijana wa Serengeti na kupoteza nafasi nyingi za kufunga.

Wachezaji wToure Alya na Mohamed Lamine wa Guinea walitawala nafasi ya kiungo na kuipa Serengeti wakati mgumu.Hata hivyo, baada ya Lamine kutolewa katika kipindi cha pili, ilitoa nafasi kwa Serengeti kufanya vema zaidi na kutawala huku ikipoteza nafasi kadhaa za kufunga.

Serengeti Boys itashuka dimbani tena keshokutwa Jumatano kuwavaa Australia katika mechi ya pili ya Kundi Namba Moja itakayopigwa saa 9:30 Alasiri kwa muda wa Afrika Mashariki.

Mechi ya mwisho ya Serengeti Boys itakuwa dhidi ya wenyeji Uturuki. Serengeti wapo katika michuano hiyo ikiwa ni maandalizi ya kujianda na michuano ya mataifa Afrika kwa vijana yanayofanyika hapa nchini mwezi April mwaka huu.
KIKOSI cha vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAFUNGUA VITUO VYA KUBADILISHIA FEDHA ZA KIGENI

$
0
0
Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Meneja Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo na kushoto ni Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Mwanaisha Ali Said.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akizungumza wakati akimkaribisha Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Hassan Mwang'ombe (kulia), kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mkakati wa shirika katika kuimarisha maduka yake ya kubadilishia fedha za kigeni nchini. Katikati ni Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Mwanaisha Said. 
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakimsikiliza Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, wakati akizungumza na waandishi leo jijini.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakijadiliana jambo wakati wa mkutano huo.  
Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (katikati), akuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mkakati huo wa shirika.
Baadhi ya wateja wakipata huduma kwenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ya Shirika la Posta leo, Ofisi ya Posta Kuu jijini Dar es Salaam. 
Wateja wakiwa katika Kituo cha huduma mbalimbali za shirika wakisubiri kupatiwa huduma, Ofisi ya Posta Kuu jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ya Shirika la Posta, jijini Dar es Salaam. 

CHINI ni Taarifa iliyotolewa na Postamasta Mkuu kwa waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGULIWA KWA MADUKA NA VITUO VYA KUBADILISHIA FEDHA ZA KIGENI VYA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA


Tarehe 28 february 2019 Benki kuu ya Tanzania ilitangaza kwamba maduka ya kubadilishia fedha yatabaki kwenye mabenki, taasisi za kifedha pamoja na maduka ya fedha za kigeni za Shirika la Posta Tanzania tu.


Tunapenda kuutarifu umma wa watanzania kuwa Shirika la Posta limejizatiti katika kutoa huduma hiyo kwa umma wa watanzania na tunapenda kuwajulisha kuwa mpaka sasa tunavyo vituo kumi (10) vinavyotoa huduma ya kubadilisha fedha ambapo ni Kariakoo, Posta Mpya, Kijitonyama, Oysterbay, City drive (Sokoine ) , Libya Posta, Uwanja wa ndege, vituo hivi vyote vipo jijni Dar es Salaam na mpaka ifikapo tarehe 15 Marchi 2019 tutakuwa na vituo ishirini(20) vya kubadilishia fedha za kigeni.


Pia tuna mikoa miwili ambayo tayari huduma hii imeanza nayo ni ofisi kuu ya Posta Zanzibar na Arusha, Pia tunatarajia mwishoni mwa mwezi Marchi mikoa 17 yenye ofisi za posta zitaanza kutoa huduma hiyo. Tungependa kuutaarifu Umma ,watembelee katika vituo vyetu vya posta kupata huduma hii ya ubadilishaji fedha za kigeni.


Shirika la Posta Tanzania linapenda kuujulisha Umma kupokea taarifa hii muhimu kwao na kwa maendelea ya Taifa.


 imetolewa na ;
POSTAMASTA MKUU NA MTENDAJI MKUU

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA


RUVU SHOOTING YATOA ONYO KWA TIMU ZA LIGI KUU

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BAADA ya ushindi wa goli  6-2 dhidi ya wachimba madini Mwadui FC, Ruvu Shooting wametoa onyo kwa timu za ligi  na kuahidi  kuzipapasa timu zote zinazokuja mbele yake

Ruvu shooting wamefanikiwa kuondoka na ushindi huo katika Uwanja wa Mlandizi Mkoani Pwani na uongozi wa timu hiyo ukijitapa na kusema mbinu za mwalimu zimeanza kujibu.

Mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) wa Ruvu Shooting utakuwa ni dhidi ya Singida United na utachezwa  Machi 17 katika dimba la Namfua mkoani Singida.

Akizungumzia mechi hiyo na zinazofuata, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kwa sasa hakuna atakayeweza kuwazuia kwani spidi yao ni kubwa mithili ya gari lililokata breki kwenye mteremko mkali.

"Ushindi huu kwetu ni ishara ya kuwa hakuna wa kutuzuia, Kama ni gari basi kwa sasa tunasema limewaka na linapita kwenye mteremko mkali na kuweza kuzuia spidi yetu sio kazi rahisi, mbinu za mwalimu kujibu ni matokeo ya kupata ushindi kwa wapinzani wetu,” amesema Bwire.

"Wachezaji wanatambua kazi yao na tayari akili zao zimejiweka sawa kwa ajili ya kuwapapasa Singida United na tutakuwa pale Namfua Singida Machi 7, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema Bwire.

Ruvu Shooting wanaweka rekodi mpya mzunguko wa pili baada ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye ligi msimu huu na pia mchezaji wao Fully Maganga aliondoka na Mpira baada ya kupiga hat trick ya kwanza kwa Ruvu.

CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BENCHI la ufundi la muda la Azam FC kwa sasa linafanya kazi kubwa ya kurudisha aina ya mpira uliozoeleka kwenye timu hiyo wa kucheza soka la pasi na kasi uwanjani.

Kwa muda wa wiki moja sasa, kikosi cha timu hiyo kipo chini ya makocha wa muda Meja Mstaafu, Abdul Mingange na Idd Nassor Cheche, wakishika nafasi hizo baada ya kustitishiwa mikataba kwa makocha Hans Van Der Pluijm na Msaidizi wake, Juma Mwambusi.

Wawili hao waneiongoza Azam katika michezo miwili na kuifanikisha timu hiyo kushinda na kuingia hatua ya nane bora Kombe la FA pamoja na ushindi wa goli kuu wa kwanza baada ya muda mrefu.

Katika mchezo wa pili dhidi ya African Lyon uliochezwa mwishoni mwa wiki hii Azam  walifanikiwa kupata ushindi wa goli 3-1 ukiwa ni muendelezo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), awali wakipata ushindi mwingine mnono walipoipiga Rhino Rangers 3-0 na kutinga robo fainali ya Kombe la FA.

Kocha wa muda wa timu hiyo Cheche amesema kwa sasa wanataka kurudisha aina ya soka la timu hiyo ili kuleta ushindani na usumbufu kwa timu pinzani kwenye mechi zinazokuja.

“Kwanza Azam ina aina yake ya mchezo ambayo ilikuwa inacheza tofauti, tunajaribu kurudisha mchezo wenye pasi nyingi na spidi ndio tunajaribu kupambana nao, kurudisha wachezaji warudi katika ile hali kuleta ushindani na usumbufu kwa timu pinzani, ndio kitu tunachokifanya sasa hivi, kunyanyua spidi ya wachezaji ambayo ilikuwa ipo chini,” alisema.

Akizungumzia kwa ufupi mchezo uliopita dhidi ya Lyon, Cheche alisema kiujumla ulikuwa ni mzuri huku akikiri kuwa kuna mambo madogo madogo wamekuwa wakizifanyia kazi ili kuondoa baadhi ya makossa yanayoonekana.

“Mchezo tulianza taratibu lakini kadiri tunavyokwenda tumeenda tikibadilika na kufuata yale maelekezo tuliyowapa na mabadiliko tuliyofanya katika kipindi cha pili yameweza kutusaidia kuleta mabadiliko ambayo yametupa ushindi,” alisema Cheche.

Baada ya kumaliza changamoto ya mchezo huo, Azam FC imerejea tena  t mazoezi leo Jumatatu tayari kuanza maandalizi ya mchezo ujao wa ligi, itakaocheza dhidi ya JKT Tanzania Machi 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex.

HATIMAYE RUGE MUTAHABA AZIKWA KIJIJINI KWAO KIZIRU,BUKOBA MKOANI KAGERA JIONI YA LEO

$
0
0
Mtoto wa marehemu Ruge akiweka ua katika kaburi la marehemu baba yake ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba.HATIMAYE mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba umezikwa kishujaa nyumbani kwao katika kijiji cha Kiziru Kata ya Karabagaine Wilaya ya Bukoba na hakuna mahubiri yaliyotolewa na katibu huyo.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga, aakiweka mashada katika kaburi la marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba,Shughuli za maziko zilianza kwa Ibada ya mazishi ambayo iliongonzwa na Katibu wa Parokia ya Itahwa, Anatory Kyatwa huku nyimbo za kihaya zikipamba tukio la mazishi.
Wazazi, familia, wakiweka shada la maua katika kaburi la mpendwa wao,marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba.Katika shughuli hiyo viongozi mbalimbali wa Serikali wameshiriki,wakiwemo wasanii wa Bongo Muvi,Muziki,marafiki,ndugu na jamaa kutoka sehemu mbalimali walitoa heshima yao ya mwisho kwa mpendwa wao Ruge  katika Viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba kabla ya kuzikwa kijijini kwao.
Mkuu wa MKoa wa Dar Es Salmaa,Paul Makonda akiweka maua katika Kaburi la Ruge.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, January Makamba akiweka shada.
Awali wakati wa tukio la kuaga mwili wake katika viwanja vya Gymkhana, Maaskofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba walimtaja Ruge kama kijana jasiri mzalendo na mfano wa kuigwa.
Askofu Desderius Rwoma ameitaka jamii kuenzi mambo mema aliyoacha huku msaidizi wake, Methodius Kilaini akisema vijana wengi wamepata mafanikio kutokana na udhubutu wake na ujasiri wa kusimamia anayoamini.
Mama wa marehemu Ruge Mutahaba (wa pili kushoto), akifuatiwa na mumewe wakiwa na aliyekuwa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala, dakika chache kabla ya mwili wa mtoto wao marehemu Ruge Mutahaba Kuingizwa kaburini, kijijini Kiziru. Rip Ruge

MTANZANIA ASHINDA MBIO ZA TIGO KILI HALF MARATHON

$
0
0



Mkurugenzi Mtendaji Tigo Simon Karikari (wa kwanza kulia)akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa RT Anthony Mtaka waki mkabadhili mfano wa hundi ya Sh milioni 1, 025,000 Falluna Abdi aliyeshika nafasi ya pili kwa wanawake kwenye mbio za Kilometa 21 maarufu kama Tigo Kili Half Maratahon zilizofanyika mjini Moshi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mataka (wa pili kushoto) akimpongeza mshindi wa kwanza katika mbio za kilomita 21 maarufu kamaTigo Kili Half Marathon Emmanuel Giniki baada ya kuibuka mshindi. Wa kwanza kulia aliyeshikilia mfano wa hundi kwa ajili ya kumkabidhi mshindi huyo ni ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Kamuni ya Tigo Simon Karikari
PIC 02-min
Baadhi ya Wafanyakazi wa Tigo wakiwa na nyuso za furaha huku wakionyesha medali zao baada ya  ‘kufuta vilimia’ na kufanikiwa kumaliza mbio za kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon zilizofanyika mjini Moshi ambazo ziliwashirikisha wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 duniani
PIC 03-min
Mshindi wa mbio za Kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon Emmanuel Giniki akihojiwa baada ya kufanikiwa kuibuka mshindi  wa kwanza katika mbio hizo zilizofanyika mjini Moshi na kuwashirikisha wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 duniani

MTANZANIA Emmanuel Giniki ameibuka mshindi wa mbio za kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon zilizofanyika mjini MoshI.
Giniki amevunja mwiko kwa mbio hizo ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikitawaliwa na raia wa kigeni na husasani Wakenya ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiibuka washindi.
Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni mbili, Giniki alisema anayofuraha kushinda mbio hizo na kuiletea heshima nchi yake jambo ambalo amekuwa akilitamani.
“Pamoja na kwamba mbio hizi zimekuwa zikifanyika hapa nyumbani, tumekuwa tukishindwa kuzitendea haki kwa kuwa wageni ndiyo wamekuwa wakizitawala. Ninayofuraha leo nimeweza kulitoa taifa langu kimasomaso,” alisema.
Akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari alisema kampuni yake inayofuraha kuchangia maendelea ya michezo nchini na hususani riadha ambayo pia huboresha afya
Karikari alisema Tigo imekuwa mdhamini wa mbio za Kili half Marathon kwa kipindi ch miaka minne mfululizo na kuongeza kuwa itaendelea kudhamini pamoja na kuboresha mbio hizo kila mwaka.
Waziri wa Habari, utamaduni vijana na Michezo Dk Harrison Mwakyemba aliishukuru Tigo kwa kudhamini mbio hizo na kuwataka wakazi wa Moshi kutumia fursa zitokanazo na mbio hizo kujijenga kiuchumi.
“Mbio hizi zimeleta wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 hapa mjini Moshi. Idadi hii kubwa ya watu itokanayo na mbio hizi ni fursa nzuri ya kibiashara na ni vyema wakazi wa Moshi wakaichangamkia,” alisema Waziri Mwakyembe.
Mbio za Kilimanjaro Marathon hufanyika mjini Moshi kila mwaka. Idadi ya washiriki wa mbio hizo imekuwa ikiongezeka kwa mujibu wa waandaaji kutoka wakimbiaji 750 wakati za kikianza hadi kufikia washiriki 11,000 kwa sasa.

WAFANYAKAZI BENKI YA NMB WALIVYOSHIRIKI KILIMANJARO MARATHON 2019

$
0
0

Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakikimbia mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon 2019 Kilomita 21, zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanajro.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakikimbia mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon 2019 Kilomita 21, zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanajro.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakifurahia Medali walizokabidhiwa baada ya kushiriki na kumaliza mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanajro.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakifurahia Medali walizokabidhiwa baada ya kushiriki na kumaliza mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon Kilomita 21 zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanajro.
Sehemu ya wanariadha walioshiriki mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanajro wakiwa katika picha ya kumbukumbu.
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images