Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

RC GAGUTI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUUPOKEA MWILI WA RUGE - BUKOBA.

$
0
0
Anaandika Abdullatif. Yunus. 

Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E.  Gaguti ameongoza mamia ya wakazi wa Mkoa Kagera Kuupokea na kuusindikiza Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba mpaka Nyumbani kwao Kabale.

Awali imewasili Ndege ya Abiria ikiwa na Wanahabari, watu mashuhuri na wasanii kabla ya kuwasili Ndege ya Serikali iliyobeba Mwili wa Marehemu pamoja na Waombolezaji mbalimbali  wakiwemo wafiwa.

Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Bukoba, na kupokelewa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo Sheikh wa Mkoa Kagera Haruna Kichwabuta, Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatusi Kinawiro, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba atakapozikwa Ruge, Viongozi Mbalimbali pamoja na Wanachama wa CCM Mkoa wa Kagera, Msafara huo ulianza safari ya Kuelekea Kijijini Kiziru - Kabale kwa kupitia Barabara Kashai, Uganda, Kibeta, Magoti, Hadi Nyumbani Kabale. Tayari Mwili huo umewasili salama Na umepumzishwa Nyumbani huku Kwaya zikiendelea kutumbuiza na watu mbalimbali wanafika kusaini katika kitabu cha Waombilezaji.

Kesho Mwili wa Marehemu Ruge unatarajiwa kutolewa Nyumbani hapo kwa Msafara kuelekea Viwanja vya Gymkhana ampapo shughuli nyingine zitaendelea huko ikiwemo kuaga, na Ibada kabla ya Kurejeshwa tena Kiziru kwa Msafara kwa ajili ya Mazishi.


Mwili Wa marehemu Ruge Mutahaba tayari umekwisha wasili nyumbani kwao kijijini Kiziru Bukoba mkoani Kagera leo,ambapo watu mbalimbali wamejitokeza kumpokea,huku msafara huo ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti .

Sanduku lenye mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba ukipokelewa uwanja wa ndege wa Bukoba 'Bukoba Airport',na kupokelewa na watu mbalimbali huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiongoza mapokezi hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Brigedia Jenerali Marco Gaguti  amefika uwanja wa ndege kuongoza mapokezi ya mpendwa wetu Ruge Mutahaba. Kabla Brigedia Jenerali Marco Gaguti kufika hapa Kagera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kipindi kile alikuwa ni Kanali kabla ya kupanda cheo amefanya kazi za kizalendo bega kwa bega na Ruge Mutahaba mojawapo ikiwa ni Fursa na Ile ya Umoja wa Mataifa Kigoma Programu ya pamoja.
Wazazi wa Marehemu Ruge,Prof Mutahaba na Mkewa akiwasili uwanja wa ndege wa Bukoba.
Mtoto wa kwanza wa Marehemu akifarijiwa baada ya kuwasili Bukoba.
Sanduku lenye mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba likipokelewa uwanja wa ndege wa Bukoba 'Bukoba Airport',na kupokelewa na watu mbalimbali huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiongoza mapokezi hayo.



BONANZA LA KUPINGA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI LAFANA KIGOMA

$
0
0
WAZIRI wa elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amefungua na kushuhudia bonanza la mpira wa miguu kwa watoto kike wa shule za msingi, Sekondari na vyuo lililofanyika katika Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma huku likiwa limemebea ujumbe wa Mimba na ndoa utotoni basi, Elimu ni haki yangu.

Akizungumza katika bonanza hilo Prof. Ndalichako amesema kuwa masuala ya mimba na ndoa utotoni zisiwe sababu za watoto kukatisha masomo yao, na ameitaka jamii kuhakikisha tamaduni hizo zinakufa mara moja na kila mmoja awe na wajibu wa kuhakikisha watoto wa kike wanatimiza malengo yao kielimu.

Amesema kuwa mpango wa Serikali kutoa elimu bure kwa wote umelenga watoto wote wanufaike na mpango huo  na kueleza kuwa Serikali haitawafumbia macho wale wote wanaokatisha masomo kwa watoto wa kike kwa namna yoyote ile.

Katika mashindano hayo zawadi mbalimbali zilitolewa kwa washiriki zikiwemo fedha taslimu pamoja na vyeti, washindi walioibuka katika bonanza hilo ni pamoja na Chuo cha Ualimu Kabanga, chuo cha F.D.C, Kinkati sekondari na chuo T.T.C Kasulu.

Pia timu zote zilizoshiriki mashindano hayo zilipata jezi, mipira, vifaa ya shule,taulo za kike huku wanafunzi wa chuo cha uwalimu Kasulu wakiondoka na kombe baada ya kuongoza katika mashindano hayo, wakifuatiwa na Murusi, Kinkati, Murubona sekondari, Muka sekondari, Kasulu F.D.C, Bogwe Sekondari na Kabanga TC.

Bonanza hilo liliandaliwa na mwakilishi wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) Mariam Ntakisivya na mashindano hayo kuitwa (Mariam Cup) kwa UWT Mkoa wa Kigoma.
 Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kufungua bonanza la mpira wa miguu kwa watoto kike wa shule za msingi, Sekondari na vyuo lililofanyika katika Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma huku likiwa limemebea ujumbe wa Mimba na ndoa utotoni basi, Elimu ni haki yangu. Kushoto ni Mwakilishi wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) Mariam Ntakisivya mwanzilishi wa bonanza hilo.
Mwakilishi wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) na muandaaji wa Bonanza hilo Mariam Ntakisivya  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  bonanza la mpira wa miguu kwa watoto kike wa shule za msingi, Sekondari na vyuo lililofanyika katika Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma huku likiwa limemebea ujumbe wa Mimba na ndoa utotoni basi, Elimu ni haki yangu.
Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipiga mpira kuashiria ufunguzi rasmi wa bonanza la mpira wa miguu kwa watoto kike wa shule za msingi, Sekondari na vyuo lililofanyika katika Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma huku likiwa limemebea ujumbe wa Mimba na ndoa utotoni basi, Elimu ni haki yangu.
Baadhi ya timu za watoto wa kike wa shule za msingi, Sekondari na vyuo  wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho ya bonanza hilo.

DK. MABODI : KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE NA WAWAKILISHI KUTOPITA MAJIMBONI MWAO HAKIKUBALIKI

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Zanzibar Dk. Juma Abdullah Saadala { Mabodi } ameonya kwamba kitendo cha baadhi ya Wabunge  na  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wenye kushindwa kupita Majimboni ni kitendo cha kidhalimu kisichokubalika na wapiga kura wao pamoja na Chama cha Mapinduzi.

Dk. Mabodi Ametoa onyo hilo wakati akiufungua Mkutano Mkuu wa CCM wa Jimbo la Mahonda ulioelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo hilo katika kipindi cha Mwaka 2015 /2019 uliofanyika  kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM Mkoa uliopo Mahonda.

Dk. Abdullah Mabodi amesema kwamba tabia hiyo ya  utoro Majimboni kwa baadhi ya Wabunge na Wawakilishi ambayo kwa kiasi kikubwa hubebwa na mizozano inayosababishwa na Makundi ya Wabunge na Wawakilishi hao haitavumiliwa tena na Chama chenyewe.

Akiwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM  katika Jimbo la Mahonda kuanzia Mwaka 2016/2019 Mwakilishi wa Jimbo hilo Balozi Seif  Ali Iddi amesema amekuwa Mtu mwenye furaha kutokana na ushirikiano anaoendelea kuupata katika kuwatumikia Wananchi kwa kasi kubwa. 

Balozi Seif amesema  Jumla ya Shilingi Milioni Mia 433,237,700/- zimetumika katika kuendeleza Miradi mbali mbali  katika kipindi cha Miaka Mitatu ambayo imeleta faraja kwa Wananchi walio wengi ndani ya Jimbo hilo hasa ile Miradi ya Huduma za Maji, Elimu, Afya pamoja na Bara bara.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mahonda Mheshimiwa Bahati Abeid  Nassir  akiwasilisha Utekelezaji wa Ilani kwa Mwaka 2016 /2019 amesema tatizo la huduma za Maji safi na salama lilikuwa sugu, lakini kutokana na jitihada kubwa zilizochukuliwa na Uongozi kwa kushirikiana na Wananchi changamoto hiyo imepunguwa kwa asilimia kubwa.

Mhe. Bahati amesema ahadi alizozitoa wakati wa Kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 anatarajia kuzitekeleza kwa nguvu zake zote ndani ya kipindi cha Miaka Mitano huku akiamini kwamba wasaidizi wake wataendelea kumpa ushirikiano.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Machi 03, 2019








Waziri Ummy aipongeza Mloganzila, awaagiza wataalam kuandaa takwimu za kitaifa

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amewaagiza watalaam wa wizara ya afya kuhakikisha kunakuwa na takwimu za kitaifa kuhusu hali ya usikivu nchini ili kubaini ukubwa wa tatizo hilo.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam alipokua akizungumza katika maadhimisho ya siku ya usikivu duniani ambapo katika kuadhimisha siku hiyo Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imetoa huduma ya upimaji wa usikivu bure kuanzia Machi 02 hadi Machi 03, 2019.

Amesisitiza kuwa takwimu hizo zigawanywe kwa watu wazima na watoto wenye umri wa kwenda shule ili kuisaidia Serikali kuweka afua na kuona ni jinsi gani itawawezesha watoto hao kufanya vizuri katika masomo yao.

Amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 5 ya watu duniani ambayo ni sawa na watu milioni 466 wana ukosefu wa usikivu, miongoni mwa watu hao milioni 432 ni watu wazima na milioni 34 ni watoto. Pia, inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 zaidi ya watu milioni 900 watakuwa na tatizo la usikivu.

Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wagonjwa waliohudumiwa katika Idara ya Masikio, Pua na Koo kati ya Novemba 2018 na Januari 2019 ni 5,959, kati yao 454 sawa na asilimia 8 walikuwa na tatizo la usikivu.

Amesema azma ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaendelea kuboresha upatikanaji huduma za kibingwa nchini hivyo amewataka wananchi kutoiogopa Hospitali ya Mloganzila kwa kuwa gharama za matibabu za hospitali hiyo ni sawa na za Muhimbili-Upanga.

Waziri Ummy ametumia fursa hiyo kupongeza uongozi wa Hospitali ya Mloganzila kwa kutoa huduma bora za fya na kueleza kuwa hivi sasa malalamiko yamepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokua awali.

“Niwapongeze sana kwa kazi kubwa na nzuri ya utoaji wa huduma mnayofanya, hivi sasa malalamiko ya wananchi dhidi ya Mloganzila yamepungua, nilikua napata meseji nyingi, lakini sasa hawalalamiki tena,’’amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bw. Makwaia Makani amesema MNH imekua ikifanya jitihada mbalimbali katika eneo la usikivu ikiwemo kuanzisha huduma ya upandikizaji wa vifaa vya kusaidia kusikia kwa watoto wenye matatizo ya usikivu ambapo tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo Juni 2017, watoto 21 tayari wamepandikizwa vifaa hivyo.

Akielezea kuhusu huduma ya upimaji wa usikivu Bw. Makani amesema mpaka jana wananchi 264 wamepatiwa huduma hiyo ambapo 64 sawa na asilimia 24 wamekutwa na tatizo la usikivu na kupatiwa rufaa.

Kauli mbiu ya siku ya usikivu duniani mwaka huu ni “Chunguza Usikivu wako”

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi waliojitokeza leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila kwa ajili ya kupima kiwango cha usikivu ikiwa ni kuadhimisha siku ya usikivu duniani ambayo hufanyika Machi 3 kila mwaka.
 Pichani ni wananchi waliojitokeza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kupima kiwango cha usikivu. Baadhi ya wananchi waliofika katika hospitali hiyo wametoka mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma, Morogoro na Mwanza. 
 Waziri wa Afya, Mhe. Mwalimu akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika kupima kiwango cha usikivu katika hospitali hiyo kutoka kwa wataalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makwaia Makani akizungumza katika maadhimisho hayo kabla ya kumkaribisha Waziri wa Afya, Mhe. Mwalimu kuzungumza na wananchi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Sufiani Baruani, na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Mloganzila, Dkt. Mohamed Mohamed, Dkt. Edwin Liyombo wa Muhimbili. 
 Viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wakifuatilia maadhimisho hayo leo.
 Mtaalam wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo wa Hospitali ya Mloganzila, Dkt. Godlove Mfuko akimpima masikio Mhe. Ummy Mwalimu leo katika hospitali hiyo.
  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua, na Koo wa Mloganzila, Dkt. Ashfag Abdulshakoor akijibu maswali ya wananchi waliofika Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila kupima kiwango cha usikivu.
Baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wakimuaga Mhe. Mwalimu leo.

dc newala akimbizwa muhimbili baada ya kupata ajali

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara Aziza Mangosongo akisaidiwa kupandishwa katika gari la wagonjwa baada ya kupata Rufaa toka hospital ya sokoine kwenda muhimbili..
 Mkuu wa mkoa wa lindi akiwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda(kulia ) wakimsindikiza mkuu wa wilaya ya Newala Aziza Mangosongo aliepata ajali jana usiku katika kijiji cha mandawa wilayani kilwa mkoani lindi na kukimbizwa katika hospital ya sokoine akiwa na majreuhi wengine watatu
 kuu wa wilaya ya Newala Aziza mangosongo akiwa tayari katika gari la wagonjwa kuanza safari ya matibabu Zaidi katika hospital ya Muhimbili
 Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi,akimsalimia mkuu wa wilaya ya newala Aziza Mangosongo kabla ya kupewa rufaa mchana leo

 Mkuu wa mkoa wa lindi,Godfrey zambi akibadilishana mawazo na mkuu wa mkoa wa mtwara,Gelasius Byakanwa mara baada ya kumtakia hali mkuu wa wilaya ya Newala Aliepata ajali jana na kulazwa katika hospital ya sokoine Mjini Lindi
 Mkuu wa mkoa wa lindi,Godfrey zambi akiwa na mkuu wa mkoa wa mtwara Gelasius Byakanwa ,pamoja wakuu wa wilaya waliofika kumtakia heri Mkuu wa wilaya newala katika hospital ya sokoine

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MTAMBO WA KUTEKETEZA TAKA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya Dkt. Paul Lawala mara baada ya Mhe. Sima kutembelea Hospitali hiyo kukagua namna taka ngumu na hata hatarishi zinavyo teketezwa. 
Shimo ambalo linatumika kwa sasa kuteketeza taka za Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, mara baada ya mtambo maalumu wa kutetekeza taka hizo kuwa katika hatua za ukarabati. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Paul Lawala kuja na Mkakati wa haraka wa kupata mtambo mpya (Incinerator) ya kuteketeza taka hatarishi. 
Mtambo wa kuteketeza taka wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kama unavyoonekana ukiwa katika hali chakavu na ukifanyiwa ukarabati. Katika ziara ya kikazi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima ameagiza kukarabatiwa kwa mtambo huo mapema iwezekanavyo kama hatua za haraka na kutafuta kiteketezi taka ambacho kitakidhi mahitaji ya Hospitali ya Rufaa.



Frank Mvungi – MAELEZO, Dodoma

Urasimishaji ardhi Wilayani Chamwino mkoani Dodoma umetajwa kuwa kichocheo cha kukuza uzalishaji katika sekta ya kilimo na ufugaji baada ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wilayani humo.


Akizungumza katika mahojiano maalum Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Bw. Antony Temu amesema kuwa wakulima wamejengewa uwezo kupitia mafunzo yaliyoratibiwa na mpango huo baada ya urasimishaji wa mashamba ya wakulima hao.


“ Wakulima hawa wataweza kuzalisha kwa tija na kuongeza uzalishaji kutoka magunia 4 kwa sasa hadi kufikia magunia 10 kwa ekari moja na pia wataweza kutekeleza dhana ya ufugaji bora wa kuku na mifugo mingine ili kuendana na fursa zilizopo kutokana na Serikali kuhamia Dodoma,”alisisitiza Temu.

Akifafanua, Bw. Temu amesema kuwa wakulima zaidi ya 100 wamenufaika na mafunzo ya kuwajengea uwezo ambapo wakulima kutoka kijiji cha Membe wameonesha mwitikio mkubwa katika mafunzo hayo hali inayoonesha kuwa mafunzo yataleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa wakulima wilayani humo.

Aliongeza kuwa wakulima hao sasa wametambua mbegu bora za mazao wanayozalisha ikiwemo alizeti hali itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa kijiji cha Membe akiwemo Bi. Pelestatili Msilili amesema kuwa urasimishaji ardhi utawasidia kutatua changamoto zilizopo katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo na hivyo kujikwamua kiuchumi.

“Tutaweza kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha hivyo tunawashukuru MKURABITA kwa kuja na mpango huu wa kutujengea uwezo ambao ni ukombozi wa kweli,”alisisitiza Bi Msilili.Naye Bi Suzana Kuanikwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Membe amebainisha kuwa anaishukuru Serikali kwa namna inavyowajali wananchi wake kupia uwezesjhaji huu unaotuwezesha kuwa na matumizi bora ya ardhi katika kijiji chetu.

Aidha, Bi Kuanikwa amebainisha kuwa kwa sasa wakulima wa kijiji hicho watapata mwamko mpya katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo na mifugo.

MKURABITA imekuwa ikiendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima baada ya kurasimisha mashamba yao katika halmashauri mbalimbali hapa nchini, kwa ujumla halmashauri 24 zimeshafikiwa na Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania.

SPIKA ZA MASIKIONI CHANZO CHA MATATIZO YA USIKIVU

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akifanyiwa uchunguzi wa sikio na Daktari bingwa wa masikio Dkt. Godlove Mfuko
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza maelekezo ya namna bora ya kutunza sikio kutoka kwa Daktari Bingwa wa Masikio Dkt. Godlove Mfuko kutoka Hospitali ya Taifa muhimbili - Mloganzila.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(kulia) akisalimiana na watoto waliofika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya usikivu.



Na WAMJW - Dar Es Salaam 

Spika za masikioni maarufu kwa jina la “Headphones” zimetajwa kuwa chanzo kinachopeleka tatizo la usikivu hafifu kwa watu. 

Hayo yamesemwa leo na Waziri mwenye dhamana ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na wananchi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Jijini Dar Es Salaam katika kuadhimisha siku ya usikivu duniani. 

Waziri Ummy amesema kuwa matumizi ya simu za kisasa yameongeza kasi ya watu kutumia spika za masikioni jambo ambalo linahatarisha kuwa na watu wengi wenye matatizo ya usikivu. 

“Unakuta kijana kuanzia asubuhi mpaka jioni ameweka spika za masikioni anasikiliza muziki hawajui wanajiweka katika hatari ya kupata tatizo la usikivu” amesema Waziri Ummy na kuendelea kusema kuwa kundi la vijana liko hatariki kupata matatizo ya usikivu. 

Waziri Ummy ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kupunguza matumizi ya spika za masikioni ili kuweza kujikinga na matatizo ya usikivu. 

“Nitoe rai kwa vijana wapunguze matumizi ya spika za masikioni kwa muda mrefu, tusipo kuwa makini tunaweza kujikuta tuna taifa lenye watu wengi wenye matatizo ya kutosikia vizuri” amesema Waziri Ummy. 

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa tatizo la usikivu hutokea pia kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa kuzaliwa na tatizo hilo au kulipata ukubwani kutokana na sababu nyinginezo ambazo zinaambata kwa kukaa kwa muda mrefu kwenye sehemu zenye kelele nyingi pamoja matatizo yanayoambata na afya ya sikio. 

Waziri Ummy amesema kuwa ni jambo jema kuona sasa matibabu ya matatizo ya usikivu hafifu yanapatikana hapa hapa nchini huku akiwataka wananchi kukata bima za afya ili kuweza kupata matibabu kwa uhakika. 

“Serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha tatizo hili linazuiliwa kabla ya kutokea lakini pia kuhakikisha matibabu yanapatikana yakiwemo kutumia mashine ya mawimbi ya sauti, upasuaji wa kuziba tundu la ngoma ya sikio pamoja na kupandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia” amesema Waziri Ummy. 

Hata hivyo alisema takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2018 Hospitali ya Muhimbili imefanikwa kuwapatia wagonjwa 116 vifaa vya mawimbi ya sauti, wagonwja 43 walifanyiwa upasuaji wa kuziba tundu la ngoma ya sikio. 

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali itaendelea kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa na kuhakikisha matibabu yanapatikana hapa hapa nchini. 

Awali akitoa taarifa yake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bw. Makwaiya Makani amesema kuwa wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali katika eneo la usikivu ikiwemo kutoa huduma ya upandikizaji vifaa vya usikivu kwa Watoto wenye matatizo ya hayo. 

“Tangu mwezi Juni mwaka 2017 tayari watoto 21 wamepandikizwa vifaa vya usikivu kitaalam kwa jina la 'cochlear implants” amesema Bw. Makani 

Bw. Makani amesema kuwa wameendesha kliniki ya siku mbili katika Hospitali ya Mloganzila kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya matatizo ya usikuvu ambapo watu 264 wamejitokeza kati yao watu 172 walihitaji uchunguzi zaidi wa usikivu, watu 64 wamekutwa na matatizo ya usikivu na tayari wamepatiwa rufaa kwa ajili ya matibabu zaidi na watu 31 wamekutwa na nta za masikioni,pia watu 26 wamekutwa na maambukizi kwenye masikio ambao wamepatiwa rufaa ya matibabu zaidi. 

Tatizo la usikivu linazidi kuongezeka siku hadi siku. Inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 5 ya watu duniani wana tatizo la usikivu. Tatizo hili litaongezeka maradufu ifikapo mwaka. Kila mmoja wetu achukue hatua kujikinga na tatizo hili ikiwemo kuepuka sehemu zenye kelele na pia kusikiliza mziki kwa sauti kubwa na kwa muda mrefu na kwa kutumia spika za masikioni. 

ACACIA KULIPA FIDIA WANANCHIZAIDI YA 200 BILL3.8

$
0
0
Na Frankius Cleophace Tarime.

Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA North Mara Uliopo Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara unatarajia kuanza kulipa malipo yafidia ya ardhi kiasi ch Shilingi Billioni 3.8 ambapo zaidi ya Wananchi 200 kutoka vijiji Vilivyofanyiwa tathimini Mwaka 2011-2012 pamoja na awamu za 35, 41,na 42 katika vijiji vya Nyabichune, Mjini kati, Nyangoto, na Nyakunguru watalipwa fedha hizo.

Akiongea na Waandishi wa habari Richard Ojendo ambaye ni Menejani wa idara ya Jamii Endelevu Mgodi wa Dhahabu wa North Mara alisema kuwa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unakusudiua kuanza zoezi la malipo ya fidia ya ardhi kwa wananchi waliopo kwenye vijiji Vinne katika eneo la Nyamongo.

Ojendo aliongeza kuwa vijiji hivyo vilifanyiwa tathimini katika awamu ya 20 ya mwaka 2011-2012 pamoja na awamu za 35,41,na 42 vitalipwa kuanzia kesho.

Pia aliongeza kuwa wananchi wa kijiji cha Nyabichune waliofanyiwa tathimini eneo la Makerero awamu ya 47 kwa waende kuechukua malipo yao ya fidia ifikapo 04 Machi Mwaka huu.

“Zoezi hili ni kwa wananchi halisi wa maeneo na awamua ambazo zimetajwa ambao taarifa zao zilichukuliwa na mgodi kwa ajili ya malipo ya fidia na orodha kamili wananchi watakaolipwa tayari tumekabidhi viuongozi wa vijiji na vitongoji huska” alisema Ojendo.

Aidha Richard aliongeza kuwa malipo kwa awamu nyingine yataendelea kulipwa na wahuska watajulishwa pale muda utakapofika na kuomba wananchi kuendelea kutoa ushirkiano mkubwa dhidi yao na Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA North Mara.

Picha ya Richard Ojendo ambaye ni Menejani wa idara ya Jamii Endelevu Mgodi wa Dhahabu wa North Mara akiongea na Waandishi wa habari juu ya zoezi zima la malipo ya fidia kwa vijiji zaidi ya 200.
Richard Ojendo ambaye ni Menejani wa idara ya Jamii Endelevu Mgodi wa Dhahabu wa North Mara


BENKI YA NMB YACHANGIA VITANDA VYA KUJIFUNGULIA NA VIFAA TIBA KITUO CHA AFYA MIRERANI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Jenesta Mhagama (kulia) akiangalia sehemu ya vifaa vya afya vilivyotolewa na Benki ya NMB.



Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Filbert Mponzi akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Jenesta Mhagama (kulia) baadhi ya vifaa tiba vilivyotolewa na NMB kwenye Kituo cha Afya Mirerani. Vifaa vilivyotolewa ni vitanda vitatu maalum kwa kujifungulia, vitanda 6 vya kulalia wagonjwa na magodoro yake, mashuka 70 na vifaa vya kupima kasi ya moyo, vyote vikiwa na thamani ya Sh Milioni 10. 
Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Filbert Mponzi akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Jenesta Mhagama (kulia) baadhi ya vifaa tiba vyenye thamani ya Sh Milioni 10 vilivyotolewa katika Kituo cha Afya Mirerani.

Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Filbert Mponzi akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Jenesta Mhagama (kulia) juu ya vifaa tiba vilivyotolewa katika Kituo cha Afya Mirerani. Vifaa vilivyotolewa ni vitanda vitatu maalum kwa kujifungulia, vitanda 6 vya kulalia wagonjwa na magodoro yake, mashuka 70 na vifaa vya kupima kasi ya moyo, vyote vikiwa na thamani ya Sh Milioni 10.



NA MWANDISHI WETU, SIMANJIRO

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vitanda vya kujifungulia pamoja na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh Milioni 10 katika Kituo cha Afya Mirerani kilichopo mkoani Manyara. Vifaa hivyo vimekabidhiwa wakati wa ufunguzi wa Kituo cha kutolea huduma za tiba na matunzo kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU), Mirerani, kituo kilichojengwa na Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF).

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Filbert Mponzi alivitaja vifaa hivyo kuwa ni vitanda vitatu maalum kwa kujifungulia, vitanda 6 vya kulalia wagonjwa na magodoro yake, mashuka 70 na vifaa vya kupima kasi ya moyo, huku vyote vikiwa na thamani ya Sh Milioni 10.

"Napongeza Serikali kwa juhudi za kuboresha huduma za afya, NMB tunajua ni muhimu wadau binafsi kuunga mkono juhudi za Serikali na ndiyo maana huwa tunatenga asilimia moja baada ya kodi kusaidia sekta ya elimu na afya," alisema Mponzi.

Awali akizindua Kituo hicho, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Jenesta Mhagama, amewataka viongozi, wananchi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika eneo la Mji Mdogo wa Mirerani, Mkoani Manyara, ambalo lina asilimia 16 ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Amesema jitihada za wadau zinahitajika ili kupunguza maambukizi mapya katika eneo hilo kwani Mamlaka ya mji mdogo ina maambukizi makubwa ikilinganishwa na maambukizi ya Mkoa mzima wa Manyara ambayo ni asilimia 2.3, huku akikemea vitendo vya unyanyapaa kwa walio na maambukizi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, amesema bado kuna tatizo kubwa nchini la watu wengi kutokujitokeza kupima Ukimwi na ndiyo maana wamelazimika kusogeza huduma ya Kituo hicho katika eneo la Mirerani hususani kwa ajili ya wachimbaji.

Amesema kuwa licha ya Kituo hicho kulenga wananchi wote,kitasaidia wachimbaji wengi kuhamasika kupima ili wajue afya zao na kuiomba Serikali na wadau kwa ujumla kufanya survey katika migodi yote nchini ili kujua hali ya maambukizi.


RUGE MUTAHABA KUZIKWA LEO KIJIJINI KWAO KIZIRU-BUKOBA MKOANI KAGERA,VIONGOZI WA SERIKALI WAMIMINIKA

$
0
0

 Sanduku lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Marehemu Ruge Mutahaba ukiwa tayari umewekwa katika uwanja wa Gymkana,Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya kuagwa,Ibada  na baadae kurejeshwa tena Kiziru kwa ajili ya Mazishi.Katika sughuli hiyo viongozi mbalimbali wa Serikali,ndugu jamaa na marafiki wamefika uwanjani hapo kumpa heshima ya mwisho mpendwa wao.V
  Sanduku lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Marehemu Ruge Mutahaba ukiwa tayari umewasili katika uwanja wa Gymkana,Bukoba mkoani Kagera tayari kwa kupewa heshima ya mwisho.













 



Familia ya Khakoo yatoa mito ya kulalia 100 kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea  kutoka kwa  Ain Shariff  mto mmoja wa kulali kati ya mito 100 iliyotolewa  na familia ya Khakoo kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika Taasisi hiyo. Licha ya kutoa mito hiyo ya kulalia familia hiyo pia ilitoa mchango wa milango mikubwa miwili ya vioo na milango mikubwa miwili ya mbao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Khalil Khakoo wakati wa tukio la kukabadhiwa mito ya kulalia 100 iliyotolewa  na familia ya Khakoo kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika Taasisi hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa shukrani kwa familia ya Khakoo mara baada ya kukabidhiwa mito ya kulalia 100 iliyotolewa  na familia hiyo  kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika Taasisi hiyo.Picha na JKCI.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishuhudia tukio la kukabidhiwa kwa mito ya kulalia 100 iliyotolewa  na familia ya Khakoo kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika Taasisi hiyo. Licha ya kutoa mito hiyo ya kulalia familia hiyo pia ilitoa mchango wa milango mikubwa miwili ya vioo na milango mikubwa miwili ya mbao.

HALI YA UJANGILI YAPUNGUA NCHINI, JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZAPONGEZA

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii 

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA) imesema kiwango cha Ujangili kimeshuka hadi kupelekea kupata maoni mbalimbali ya Wadau kutoka Jumuiya za Kimataifa, kutokana nakufanyika kazi kubwa ya kuzuia ujangili huo. 

Takwimu zinaonyesha kuwa Ujangili umeshuka ukilinganisha na miaka ya nyuma. Ujangili wa Wanyamapori unafanywa kwa Wanyama wanaowindwa zaidi, Mfano Tembo, katika Hifadhi ya Selous inayoongoza kuwa na Tembo wengi zaidi inaonyesha mwaka 2014/2015 waliuawa Tembo 18, 2015/2016 Tembo 16, 2016/2017 Tembo 7 na 2017/2018 hakuna idadi yoyote ya Tembo aliyeuawa. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Siku ya Wanyamapori Duniani,  Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Dkt. James Wakibara amesema Serikali imeweka nguvu kubwa kupiga vita Ujangili nchini ikiwa sambamba nakuanzishwa kwa 'Wildlife Crime Task Force' itakayokuwa inatafuta Wahalifu wanaojiusisha na Ujangili sehemu yoyote hapa nchini. 

"Kwa sasa suala la Ujangili tunapumua, sio kama miaka ya nyuma, Ujangili wa Watu kukimbiza Wanyama kwa ajili ya kula, huu hauathiri sana tafauti na Ujangili wa kuuwa Wanyama kwa ajili ya Biashara ndio changamoto hapa nchini", amesema Dkt. Wakibara.

Dkt. Wakibara amesema Wanyamapori wachululiwe kama rafiki wa mazingira, rafiki wa Uchumi kwa nchi, rafiki wa Uchumi wa maisha yao.

Amesema mwaka 1982, Hifadhi ya Selous iliingizwa kwenye Urithi wa Dunia kwa kuwa Tembo 106, 000, idadi hiyo imefanya kuingizwa kwenye Urithi huo, wakati Miaka minne iliyopita Tembo hao walishuka hadi 13, 500 sawa na 87%.

Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Utalii na Huduma za Biashara - TAWA, Imani Nkuwi amesema maeneo madogo yanayofahamika kama Vitaru vya Uwindaji, kwa sasa yameanza kugaiwa kwa utaratibu mpya kwa Mfumo wa Kieletroniki kwa njia ya mnada, amesema wakati wowote Vitaru 81 vitaanza kugaiwa baada ya Kamati kuidhinisha Utaratibu huo, kunadi Vitaru hivyo kwa utaribu wa Kieletroniki.

Nkuwi amesema Mapato ya Serikali yalishuka kutokana na Vitaru hivyo kuwa wazi, mapato yalishuka kwa 10% kwa sababu yakurudishwa kwa Vitaru hivyo. 
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Dkt. James Wakibara akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Dunia yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

ZOEZI LA UTOAJI ELIMU UNAENDELEA KWA WASAFIRISHAJI MKOANI MBEYA

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Julius Chambo, akitoa elimu kwa madereva wa malori kuhusu utekelezaji wa Sheria mpya ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, mjini Tunduma, mkoani Mbeya. Sheria hiyo imeshaanza kutumika tarehe 1 Machi, 2019.
 Dereva wa malori ya mizigo Bw. Juma Nachikolo, akiuliza swali kwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Julius Chambo (hayupo pichani), mara baada ya kupewa elimu ya Sheria mpya ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoanza kutumika tarehe 1 Machi, 2019, mjini Tunduma, mkoani Mbeya.
Baadhi ya madereva wa malori wakisikiliza elimu inayotolewa juu ya utumikaji wa  Sheria mpya ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoanza kutumika tarehe 1 Machi, 2019.

NAIBU WAZIRI KANYASU AWANYOSHEA KIDOLE WATOA HUDUMA ZA UTALII HOTELINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amewanyoshea kidole baadhi ya wahitimu wa masomo ya utalii wanaoajiriwa katika maeneo mbalimbali nchini wanaoshindwa kutafsiri vyeti na elimu waliyoipata vyuoni kwa kutoa huduma bora kwa watalii nchini.

 Amesema bado kuna tatizo la watoa huduma wengi katika maeneo ya hoteli ambao ni wavivu, wasiojituma,wenye kukosa ubunifu na wasiotumia lugha nzuri kwa watalii.
Akizungumza wakati wa mahafali ya 38 kwa  wahitimu 21 wa kozi ya ukarimu yanayotolewa bure kupitia mradi wa Trade Aid, kwenye mji mkongwe wa kihistoria wa Mikindani uliopo  katika Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara, Kanyasu amewataka wahitimu hao pindi  watakapoajiriwa waoneshe utofauti na kuwa mfano bora  kwa kuchochea utalii katika mikoa ya Kusini.

 Amesema mradi huo wa Trade Aid umekuwa ukitoa mafunzo hayo  kwa muda wa miezi sita kwa  wanafunzi wenye elimu mchanganyiko kuanzia  darasa la saba na kuendelea lengo likiwa kuisaidia jamii ya Mikindani kuchangamkia fursa za utalii.

 Aidha, wanafunzi wanaohitimu mafunzo hayo kila mwaka huajiriwa moja kwa moja kwenye sekta ya hoteli nchini kutokana na ubora wao. Amesema watalii wengi wanaokuja nchini ni matokeo ya huduma bora na pale inapotokea wamehudumiwa vibaya hawawezi tena kurudi.

Hata hivyo, Kanyasu amesema licha ya kuwa kuna vyuo vingi vinavyotoa mafunzo hayo kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada, bado watoa huduma walio wengi wamekuwa na uwezo mdogo wa kuwahudumia watalii kwa viwango vya juu ikilinganishwa na elimu waliyonayo.

Amesema licha ya   wafanyabiashara  kujenga Hoteli za kitalii katika maeneo mbalimbali nchini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kuwapata watoa huduma wenye uwezo wa kutoa huduma bora za kumfanya mtalii aongoze siku za kukaa nchini kutokana na huduma alizopata.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Mikindani, Elias Mwanjise akizungumza wakati wa mahafali hayo ametoa wito kwa wahitimu hao pindi  watakapojiriwa wafanye kazi kwa bidii na maarifa ya hali ya juu hali itakayopelekea watalii wengi kuja nchini.

Pia amewataka  wazazi wasiwaozeshe binti zao wanaomaliza darasa LA saba na badala yake wachangamkie fursa hiyo ambayo ni nadra kupatikana katika maeneo mengine. Naye Meneja wa Mradi wa Trade Aid nchini Tanzania,Barnabas Mwambe  amemweleza Naibu Waziri Kanyasu kuwa wahitimu wanaomaliza katika Chuo hicho karibu wote wamekuwa wakiajiriwa  kutokana na ubora wao na jinsi walivyoandaliwa.

Amebainisha kuwa mkazo waliouweka Chuo hapo ni mafunzo kwa vitendo kuliko nadharia ili kuwajengea uwezo wahitimu kutoa huduma bora. Mbali ya kutoa mafunzo hayo bure,  Meneja Mradi huo amesema kuwa wamekuwa  wakiwafungulia akaunti za benki pamoja na kuwawekea kiasi cha shilingi 150,000 kwa ajili ya nauli wakati wakitafuta kazi pamoja na kupewa  kadi ya mafao uzeeni
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo Husna Ally akizungumza wakati wa mahafali hayo amesema baada ya kuhitimu mafunzo ameanza kuona mwanga wa maisha kutokana na elimu ya darasa la saba aliyokuwa nayo.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza  na  wahitimu 21 wa kozi ya ukalimu yanayotolewa bure kupitia mradi wa Trade Aid katika mji mkongwe wa kihistoria wa Mikindani uliopo  katika Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara ambapo Kanyasu amewataka wahitimu hao mara watakapoajiriwa waende wakaoneshe utofauti wakawe  mfano bora  kwa kuchochea utalii katika mikoa ya Kusini.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliohitimu mafunzo ya ukarimu kwa msaada wa Shirika la Trade Aid la Marekani katika Mji wa Kihistoria wa Mikindani mkoani Mtwara.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akimsikiliza   Salum Kidume alimpotembelea nyumbani kwake Mikindani mkoani Mtwara  akimuelezea kuhusu  alimvyompokea Hayati Mwl. Julius Nyerere mnamo mwaka 1950 wakati wa  harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. 
 Baadhi ya wanafunzi wakiimba kwa furaha mbele ya Naibu Waziri wa Maliasilia na Utalii, Constantine Kanyasu wakati wa mahafali yao mkoani Mtwara.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akikabidhi cheti cha kuhitimu kwa Jum Abdallah ambaye ni mhitimu wa kozi ya ukalimu katika chuo cha Old Boma Mikindani mkoani Mtwara
Baadhi ya wazazi pamoja na wananchi walioshiriki katika mahafali ya 38 yaliyofanyika katika jengo la kihistoria la Olda Boma wakati wahitimu 21 walipohitimu kozi ya Ukarimu yaliyofanyika  mkoani Mtwara. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)

WAFANYAKAZI WAKALA WA UCHIMBAJI VISIMA NA UJENZI WA MABWAWA(DDCA) WAHAKIKISHIWA AJIRA ZAO ZIKO SALAMA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amewataka wafanyakazi wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA)kuendelea na majukumu yao kama kawaida na wasiwe na wasiwasi na ajira zao kwani wako salama.

Profesa Mkumbo ametoa kauli hiyo katika Ofisi za DDCA jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na wafanyakazi kuhusu mabadiliko makubwa ya kiuundo ambayo yamefanyika ndani ya Wizara yao na sekta ya maji kwa ujumla.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea uwepo wa Sheria Mpya ya Huduma za Maji ambayo imepitishwa siku za karibuni ambapo kupitia sheria hiyo imeundwa rasmi Wakala wa Maji Vijijini(RUWASA), hivyo DDCA imekufa kifo cha kawaida huku akiwahakikishia wafanyakazi kuwa ajira zao ziko salama waendelee kuchapa kazi.

Akifafanua zaidi kuhusu mabadiliko ndani ya Wizara ya Maji, Profesa Mkumbo amesema "Kuna mabadiliko makubwa sana yanaendelea katika sekta ya maji. Ni vema Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa mkafahamu nafasi yenu kutokana na mabadiliko haya.

"Kuna mabadiliko yamefanyika wizarani lakini ninyi Wakala wa visima hayajawawagusa.Kuna sheria mpya ya maji ambayo imekuja na Wakala wa Maji Vijijini ambayo hiyo sasa ndio inachukua jukumu la halmashauri katika utoaji wa huduma za maji.

"Tunakumbuka ilitolewa sera, hivyo Januari 31,2019 wabunge walipitisha sheria ya huduma za maji na mazingira ambayo kwa sasa inasubiriwa kusainiwa na Rais ili ianze kutumika. Hivyo DDCA inaondoka maana tayari kuna wakala wa maji vijijini ambayo itameza taasisi nyingine, ikiwemo hii ya kwenu ambayo inakufa kifo cha kawaida,"amesema Profesa Mkumbo.

Hata hivyo amesema hakuna ambaye ataondolewa kazini kwasababu ya kuwepo kwa mabadiliko hayo kwani wamezingatia ajira ya kila mmoja.
"Baada ya kupita sheria hii utaratibu ni kwamba iwapo kuna wakurugenzi wawili mmoja ilikuwa lazima aondoke.Lakini hapa DDCA Mkurugenzi wenu alikuwa anakaimu, hivyo hakuna wakurugenzi wawili.

"Kwa lugha rahisi Mkurugenzi wenu alikuwa ana -Act na kiswahili ni kuigiza, hivyo akiwambia acha kuigiza kuna tatizo gani?Ujio wa sheria ya Huduma za Maji kinachobadilika hapa kwenu ni jina tu.Hivyo DDCA itakuwa ndani ya RUWASA na kikubwa ambacho tunasisitiza ni kushirikiana kikamilifu ili kufikia lengo la Serikali kupitia sheria ya Maji,"amefafanua.

Kutokana na mabadiliko hayo wamesimamisha mchakato wa kupata wajumbe wa bodi, na hilo si tatizo kwani Serikali inayo mfumo na muundo mzuri wa kufanya kazi zake hata kama bodi itakuwa bado haijapatikana.
Profesa Mkumbo amewahakikishia wafanyakazi wa DDCA kuwa mabadiliko hayo yanatoa fursa nyingi zikiwemo za nafasi za ajira ambazo zitatangazwa kwa ajili ya RUWASA na watakaopewa kipaumbele ni wale walipo ndani ya Wakala hiyo.

"Kuna fursa nyingi zimefunguliwa, kuna nafasi zinatajiwa kujazwa na ni nyinyi, huu ndio wakati wenu kuzichangamkia.Mtakaoomba tutawashindanisha na kisha tutawapata wenye sifa zinazohitajika.
Amesema wafanyakazi wa DDCA ndio wababe katika uchimbaji visima na mabwawa vijijini. "Katika uchimbaji visima na mabwawa ninyi ndio washauri wakuu wa Serikali lakini bado hawajatumika vizuri na sasa ndio wakati wake".

Amewashauri DDCA kupanga malengo sahihi na mkakati wa Serikali ni kuona wakala hao wanajitegemea kwa asilimia 100 na hatimaye kuwa na Kampuni inayojiendesha kwa faida inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100.

"Tunataka kuona mnajiendesha kwa fedha zenu wenyewe, hivyo hata Mkurugenzi wa RUWASA atapewa malengo ya kuwahakikisha anawalea maana tunajua uwezo wenu katika kuchimba visima na ujenzi wa mabwawa.Akitoa Mkurugenzi mjinga wa RUWASA ataona kama vile huu Wakala ni mshindani wake wakati si kweli.Mkurugenzi wa RUWASA atakayekuja lazima ailee,"amesisitiza.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na viongozi pamoja na wafanyakazi wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa(DDCA),jijini Dar es Salaam  kuhusu mabadiliko mbalimbali yanayoendelea ndani ya Wizara na sekta ya maji kwa ujumla nchini
 Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) wakimsililiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Process Kitila Mkumbo baada ya kukutana nao kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya Maji
 Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa Domina Msonge(katikati).
 Wafanyakazi wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa wakifuatilia mkutano ambao mgeni rasmi ambaye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prodesa Kitila Mkumbo
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo ( aliyevaa shati nyeupe) akizungumza na viongozi pamoja na Wafanyakazi was Wakaja wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa

LIVE: KINACHOENDELEA MAZISHI YA RUGE MUTAHABA UWANJA WA “GYMKHANA” BUKOBA MKOANI KAGERA

MAFUNZO YA SAIKOLOJIA KWA WADAU WA MAPAMBANO DHIDI YA UDALILISHAJI WANAWAKE NA WATOTO YAFUNGULIWA ZANZIBAR

$
0
0
Na Ramadhani  Ali - Maelezo                
Vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto bado vinaendelea kuongezeka Zanzibar licha ya juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Serikali, Taasisi za kiraia na Mashirika wahisani ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa watoa huduma wa waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinisi, mtoa huduma kutoka Kitengo cha Mkono kwa mkono Hospitali kuu ya Mnazimmoja Bi. Fatma Ali Haji alisema udhalilishaji wa kijinsia ni masuala yote ambayo hayapaswi kufanyiwa binadamu ikiwemo kuingiliwa kwa nguvu, kupigwa na kunyanyaswa.

Hata hivyo alisema hivi sasa jamii imekuwa na mwamko mzuri wa kutoa taarifa katika sehemu husika inapotokea vitendo vya udhalilishaji kinyume na ilivyokuwa zamani ambapo vitendo hivyo vilikuwa vikipatiwa suluhisho kwa njia za siri mitaani ili kuepuka aibu kwa muhusika.

Alisema hivi sasa kumefunguliwa vituo saba vya mkono kwa mkono viliopo katika hospitali za Zanzibar na vimekuwa vikitoa huduma nzuri kwa waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na wamejenga imani kutokana na msaada mkubwa wanaopata wanapofikwa na matatizo hayo.

Alisema mafunzo ya siku tano yaliyoandaliwa kwa ushirikiano na Shirika linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) na Wizara ya Afya yanalengo la kuwajengea uwezo wahudumu wa vituo hivyo waweze kutoa huduma bora zaidi kwa waathirika.

Alisema mtoto anapobakwa pamoja na wazazi huwa wanachanganyikiwa na kupata msongo wa mawazo hivyo huhitaji msaada mkubwa kutoka kwa wahudumu wa vituo vya mkono kwa mkono ili waweze kurejea katika hali ya kawaida.

Aliwashauri wazazi na walezi wanapopata matatizo ya udhalilishaji wa kijinsia watoe taarifa katika vituo vya mkono kwa mkono ambavyo vinawatendaji kutoka taasisi mbali mbali ili kurahisisha utoji wa huduma .

Akifungua mafunzo hayo, Naibu Waziri wa Afya Bi. Harusi Said Suleiman aliwataka washiriki wa mafunzo hayo ambao ni watoa hudumu wa watu walioathirika kutumia lugha nzuri na kuwapa upendo kwani kufanya hivyo ni kuwapunguzia maumivu waliyopata.

Alisema kuanzishwa kwa vituo vya mkono kwa mkono katika Hospitali za Zanzibar kunatoa nafasi ya kuimarisha huduma kwa wahanga wa matendo ya udhalilishaji na kuona huduma zinazotolewa katika vituo hivyo vinafikia vigenzo vya kimataifa vinavyokubaliwa na Shirika la Afya ulimwenguni WHO.
 Baadhi ya Wadau wa Mapambano dhidi ya Udhalilishaji waliohudhuria katika Mafunzo ya siku Tano ya Saikolojia yaliofanyika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Kidongo chekundu mjini Unguja.
 Msaidizi Meneja Kitengo Shirikishi Afya ya Mama na Mtoto Dk Mtumwa Ibrahim akitoa hotuba ya kumkaribisha Mgeni Rasmi ili kuyafungua  Mafunzo ya siku Tano ya Saikolojia kwa Wadau wa Mapambano dhidi ya udhalilishaji  yaliofanyika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Kidongo chekundu mjini Unguja.
 Naibu Waziri wa Afya Harusu Saidi Suleiman akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mafunzo ya siku Tano ya Saikolojia kwa Wadau wa Mapambano dhidi ya udhalilishaji  yaliofanyika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Kidongo chekundu mjini Unguja.
 Mwezeshaji wa Mafunzo Edwick Mapalala akitoa mafunzo ya Saikolojia kwa Wadau wa Mapambano dhidi ya udhalilishaji  yaliofanyika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Kidongo chekundu mjini Unguja.
Mtoa huduma wa kitengo cha Mkono kwa Mkono Dk,Fatma Ali Haji akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Udhalilishaji katika ufunguzi wa Mafunzo ya siku Tano ya Saikolojia kwa Wadau wa Mapambano dhidi ya udhalilishaji  yaliofanyika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Kidongo chekundu mjini Unguja. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

MKUU WA MKOA WA PWANI AZIKARIBISHA KAMPUNI 13 ZINAZOTAKA KUJENGA VIWANDA MBALIMBALI

$
0
0
*Ni zile ambazo zimepelekwa na Kiluwa,Mkurugenzi Mtendaji TIC atoa neno
*Kiluwa asema ni jukumu la kila Mtanzania kufanikisha uwekezaji nchini

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SERIKALI ya Mkoa wa Pwani,kupitia Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo amesema hawako tayari kuzikosa kampuni 13 ambazo zimepelekwa mkoani kwake kutokana na jitihada za Mkurugenzi wa Makampuni ya Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa.

Mhandisi Ndikilo amebainisha hayo ofisini kwake baada ya majadiliano kati ya wawekezaji kutoka China, viongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na idara nyingine serikalini zinazohusika na uwekezaji.

Ambapo Mhandisi Ndikilo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia juhudi ambazo zinafanywa na Kiluwa za kuleta wawekezaji kuwekeza mkoani humo zikiwemo Kampuni hizo 13 ambazo zimekuja kuwekeza na wamepata baraka za mkoa wake.

Amefafanua baada ya kikao cha majadiliano Mhandisi Ndikilo amesema kazi iliyobaki ni kuangalia namna wawekezaji hao watakavyomalizana na mamlaka nyingine za nchi ili kufuata taratibu zinazotakiwa.

"Hawa watu wamejipanga kuwekeza katika viwanda mbalimbali 13, mtaji wanao wapo tayari kuanza hata kesho. Naagiza kila idara ifanye kazi yake ili hawa wawekezaji tusiwakose," amesema Mhandisi Ndikilo.

Katika maelezo yake kutokana na kutumia muda wa zaidi ya saa sita kujadiliana kuhusu mustakabali wa wawekezaji hao wakiwa na kamati ya ulinzi na usalama na maofisa mbalimbali wakiwemo wa TIC na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Ndikilo alisema:

“Fursa na sifa tulizonazo kama mkoa kunavutia wawekezaji wengi, ila kama tunavyofahamu uwekezaji haufanyiki angani bali kwa kutumia ardhi, kulikuwa na mvutano kuhusu ardhi ndio mana tumetumia muda mwingi kujadiliana.

“Vilevile tumejadili mambo mengi kuhusu aina ya uwekezaji mkubwa unaotaka kufanyika, sote tumeridhia namna walivyojipanga wamekuja na mitaji mikononi na aina ya bidhaa na huduma watakazozalisha, wanataaka kuhamisha teknolojia kutoka China kuja Tanzania. Ndiyo maana nimetoa wiki mbili majibu yapatikane hawa wawekezaji waanze kazi.”

Akizungumzia eneo la uwekezaji la Kiluwa Free Processing Zone, Mhandisi Ndikilo amesema hatakubali kuona wazo hilo la mtanzania mzalendo linapotelea hewani wala kuona wawekezaji wanakwenda nchi jirani kwa kukimbia mizengwe nchini.

“Mkoa wetu una ardhi kubwa ya uwekezaji, Kibaha ina maeneo mengi nay a kutosha hata kule Mlandizi tuna ekari zaidi ya 5,000 hazijaguswa. Hivyo, nataka waelewe Mkoa wetu ni wa amani ndio mana tumeiita na kamati ya ulinzi na usalama ishiriki mkutano huu.

“Serikali inataka kuipeleka nchi katika uchumi wa kati kwa kutegemea viwanda, sasa tukiona watu wenye nia ya kuanzisha viwanda wanasumbuliwa hatuwezi kukaa kimya. Taratibu zote wamefuata lakini ikionekana mkoa wangu ndio kikwazo sitakubali,” amesema Mhandisi Ndikilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geofrey Mwambi alisema kazi ya kuleta wawekezaji ni ya serikali. Hivyo, wanavyoona watu wanaisaidia serikali hawawezi kuwavunja moyo.

"Hawa ni wa mwanzo tu wapo wengi, kati ya hao 13 tayar wawekezaji sita wameshakuja na vifaa vyao wanasubiri kupewa ruhusa waanze kazi. Kuna viwanda vya Battery, bidhaa za ngozi na mabehewa," anasema Mwambi.

Mwakilishi wa kundi la wawekezaji hao ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sinoma East Africa Co. Limited, Lu Xiaoqiang alisema wameichagua Tanzania kwa kuwa wanaamini kuna fursa nyingi za uwekezaji na kwa muda wa miaka 10 waliyofanya kazi nchini wamevutiwa na namna watanzania walivyo wakarimu.

“Tupo tayari kushirikiana na watanzania na kuwafundisha ujuzi wa mambo mbalimbali, tunataka kuanzisha viwanda vya bidhaa za plastiki, chuma, battery na vifaa vingine vya kielektroniki. Tunahamisha utaalamu kutoka China kuja Tanzania,” alisema Xiaoqiang.

Naye Kiluwa amesema TIC inawaelekeza nini cha kufanya hivyo hawawezi kuwaangusha na wataendelea kufanya kazi nao kadiri ya uwezo wao.“TIC kazi yao imeshakamilika, huwa wanatupatia elimu ili kufuata taratibu zinazostahiki kusajili wawekezaji, naishukuru serikali ya Mkoa wa Pwani kwa msaada mkubwa iliyotoa kwetu na kukubali kutusikiliza hadi kuelewa lengo letu katika uwekezaji.

“Kuna zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 100 zinataka kuwekezwa hapa, hiyo ni fursa ya ajira na Mamlaka ya Mapato Tanzania itaongeza mapato. "Hawaii wawekezaji wamejipanga hawana muda wa kupoteza, kati ya viwanda 13 wawekezaji sita tayari wameshaleta hadi vifaa wanasubiri kupewa ruhusa tuwaanze kazi,” alisema Kiluwa.

Amesema ni jukumu la Watanzania kila mmoja kwa nafasi take kuhakikisha maono ya Rais Dk.John Magufuli ya kuhamasisha ujenzi wa viwanda unafanikiwa kwa vitendo,hivyo mkakati wake ni kuendelea kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini.

"Nina ardhi ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji,hivyo wawekezaji ninapowamasisha kuja nchini kuwekeza pia nawaeleza na uwepo wa ardhi na wakija nchini wanakwenda TIC ambako ndiko watapewa utaratibu kwani niliamua hati ya ardhi niliyonayo kwa ajili ya uwekezaji iwe wazi kwa TIC pia," ameongeza.

Amesisitiza katika kufanikisha uwekezaji kwake anaona ni jambo jema kwani kikubwa anachoamini mbali ya watanzania kupata ajira,teknolojia ambayo inaletwa na wawekezaji itabaki nchini kwa maslahi ya Watanzania.",Ninachokifanya ni kama nang'oa teknolojia nje naileta nyumbani."
Mkuu wa MKoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mwishoni mwa wiki ,mara baada ya kumaliza kikao cha pamoja wakati wa majadiliano kati ya wawekezaji kutoka China, viongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na idara nyingine serikalini zinazohusika na uwekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geofrey Mwambe akisalimiana na mmoja wa wekezaji mara baada ya kumaliza kikao chao cha pamoja na Mkuu wa Mkoa
Mhandisi Evarist Ndikilo.
 Mwakilishi wa kundi la wawekezaji hao ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sinoma East Africa Co. Limited, Lu Xiaoqiang akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu kwanini wameichagua Tanzania kuwekeza,ambapo alieleza kuwa wanaamini kuna fursa nyingi za uwekezaji na kwa muda wa miaka 10 waliyofanya kazi nchini wamevutiwa na namna watanzania walivyo wakarimu.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari mwisho mwa wiki Kibaha mkoani Pwani,mara baada ya kumaliza kikao chao cha pamoja.

Baadhi ya wadau wa maendeleo ya uwekezaji wa Viwanda mkoa wa pwani,kwamati ya Ulinzi na usalama  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa
Mhandisi Evarist Ndikilo,wakati wa majadiliano kati ya wawekezaji kutoka China, viongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na idara nyingine serikalini zinazohusika na uwekezaji.
Picha ya pamoja

Biteko asema ufahari wa kiongozi uwe kwenye kuwatumikia Wananchi

$
0
0
Na Issa Mtuwa – Bukombe

Waziri wa Madini ambae pia ni Mbunge wa Bukombe Mhe. Doto Biteko amesema viongozi wa serikali wajibu wao mkubwa ni kuwatumikia wananchi, dhamana yao ya madaraka kama haina msaada kwa wananchi haina maana, yeye kama waziri na mbunge kama shida na matatizo ya wanchi wa Bukombe na sekta nzima ya madini atashindwa kuzitatua haina maana ya uwepo wake na ndio maana anaumiza kichwa kila siku kuhakiksha sekta ya Madini inaleta tija kwa taifa huku pia wananchi wa Bukombe wanaozungukwa na Madini ya dhahabu pia wananufaika.

Biteko ameyasema hayo leo tarehe 02/03/2019 akihutubia wananchi kwa nyakati tofauti tofauti wilaya ya Bukombe katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu katika mkoa wa geita ambapo pamoja na mambo mengine anasikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi na zinazo husu sekta ya madini.

“ Rais Pombe Joseph Magufuli amekuwa akituambia mara kwa mara nendeni mkawahudumie Watanzania muwaondolee kero, ule mfumo wa watu wakiwa ofisini anakuwa Boss Magufuli hataki mfumo huoo, anataka mabosi wawe wananchii, wananchi wasikilizwe kama wana jambo litatuliwe na kama haliwezekani waambiwe ukweli sio kudanganya” amesema Biteko.

Amesema Bukombe inautajiri wa madini ya dhahabu na endapo kila mmoja atajishugulisha katika kutafuta kwa kutumia fursa zilizopo maisha ya wana Bukombe yataboreka, ametoa wito kwa vijana, akina mama na kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi ajishugulishe.

Aidha, ameongeza kwa kusema wajibu alionao kama Waziri wa Madini ni kuhakikisha kodi na malipo mbalimbali yanayohusiana na madini yanalipwa tena kwa wakati, na jamii zinazo zunguka migodi zinachangia maendeleo ya wananchi hao kama sheria inavyo wataka. 

‘Msiwakamue sana hawa wawekezaji kwa sababu wanatumia fedha nyingi katika kuwekeza, sio kila shida ya kijiji, kata au wilaya mnakimbilia kwa mwekezaji wa mgodi hapaaaaaa! lakini sizui kuwaomba msaada lakini kuwe na kipimo yale ya kisheria waacheni watekeleze ili wasipo timiza mimi nitawabana” aliongeza Biteko.
 Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akiongea kwenye kikao cha ndani na viongozi waandamizi wa Wilaya ya Bukombe katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Mkumba akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Bukombe ambae ameanza ziara ya siku tatu wilayani humo.
 .Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akihutubia wananchi mbalimbali wa kata ya wakiwa kwenye mkutano wa pamoja katika Vijiji wilayani Bukombe. 
 Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko mwenye Tshirt ya Njano akimsikiliza msimamizi wa ujenzi wa Zahanati katika kata ya  Wakati wa ziara yake Wilayani Bukombe ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo.

YALIYOJIRI MKUTANO WA KUJADILI AFYA YA WANYAMA DUNIANI ULIOFANYIKA MJINI HAMMAMET, TUNISIA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Hamis Ulega (MB) amehudhuria Mkutano Mkuu wa 23 wa Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (OIE) Kamisheni ya Afrika, uliofanyika Mjini Hammament nchini Tunisia.

Mkutano huo uliojumuisha nchi zaidi ya 25 za bara la Afrika zikiwemo Zambia, Zimbabwe, Misri, Kenya, Uganda, Tunisia na Chad ulikuwa na malengo ya kuangalia afya ya wanyama, haki za wanyama, uzalishaji wa mifugo na usalama wa chakula kitokanacho na mifugo na kutoa mapendekezo kulingana na kanuni za shirika hilo duniani.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Hamis Ulega (MB) akiambatana na Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa wizara hiyo Dkt. Hezron Nonga amepata fursa ya kufanya kikao cha ana kwa ana na uongozi mkuu wa Shirika hilo la Afya ya Wanyama Duniani (OIE) kwa kuzungumza na rais wa shirika hilo Dkt. Mark Schipp, Mkurugenzi Mkuu Dkt. Monique Eloit na mwakilishi wa shirika hilo kwa Ukanda wa Nchi za Kusini mwa Afrika Dkt. Samuel Wakusama.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Ulega ameshukuru uongozi huo kwa ushirikiano wake na Tanzania kwa kuendelea kuisaidia nchi katika miradi mbalimbali ya kulinda afya za wanyama hapa nchini.

Aidha ameelezea nafasi ya Tanzania katika rasilimali za asili ikiwemo mifugo na uvuvi ambapo kwa upande wa mifugo ametoa takwimu za mifugo iliyopo nchini pamoja na vikwazo ambavyo sekta ya mifugo inakabiliana navyo yakiwemo magonjwa, kasi ndogo ya mifugo kuzaliana (Poor Breeding) na uzalishaji duni (Low Productivity) hali ambayo inasababisha nchi kushindwa kusafirisha mifugo na mazao yatokanayo na mifugo kama vile nyama kwenda katika masoko ya nje ya nchi.

Mhe. Naibu Waziri Ulega ameliomba Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (OIE) kuisaidia nchi ya Tanzania katika kukabiliana na changamoto hizo ili kukuza uchumi na kipato cha wadau wa sekta ya mifugo ambapo kwa pamoja uongozi huo umeahidi kuzifanyia kazi.

Licha ya mazungumzo hayo, Mhe. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Hamis Ulega (MB) kupitia kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Dkt. Hezron Nonga, amewakabidhi andiko linalofafanua kwa kina sekta ya uvuvi nchini, changamoto zake na maeneo yenye uhitaji ili kuuwezesha uongozi huo kuendelea katika hatua ya utekelezaji.

Pamoja na mambo mengine, Mheshimiwa Naibu Waziri Ulega ameueleza uongozi wa OIE kuhusu nia ya Tanzania kuandaa mkutano ujao kwa kuwa ni nchi yenye mifugo na wanyamapori wengi, mazingira mazuri ya uwezekaji na taasisi maalum zinazoshughulikia masuala ya viwango, ubora wa bidhaa na usalama wa chakula.

Katika kutathmini afya za wanyama, wataalamu wamejadili magonjwa mbalimbali ya wanyama yaliyopo katika bara la Afrika hususan kwa nchi wanachama, athari na namna yakuyakabili yakiwemo magonjwa ya miguu na midomo (FMD), Kichaa cha mbwa na homa ya Bonde la Ufa (RVF).

Aidha kikao kimetathmini kwa pamoja miradi mbalimbali yenye lengo la kuimarisha afya za wanyama pamoja na michango ya wahisani ikiwemo Benki ya Dunia, Mchango wa Wataalam wa Kati wa Mifugo (Veterinary Paraprofessionals) na nafasi yao katika kuimarisha huduma za afya ya wanyama katika Bara la Afrika.
 Kikao cha ana kwa ana kati ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Hamis Ulega (MB) (wa pili kutoka kulia) na Uongozi wa Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (OIE). Kutoka kushoto: Mwakilishi wa OIE Kanda ya Kusini mwa Afrika Dkt. Samuel Wakusama, Rais wa OIE na Kamisheni ya Australia Dkt. Mark Schipp na Mkurugenzi Mkuu wa OIE Dkt. Monique Eloit na Mkurugezi wa Huduma za Mifugo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (wa kwanza kulia) Dkt. Hezron Nonga.
Picha ya pamoja mara baada ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Hamis Ulega (MB) (katikati), kukamilisha mazungumzo na uongozi wa juu wa Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (OIE). Kutoka Kulia: Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Hezron Nonga (wa kwanza), Mkurugenzi Mkuu wa OIE Dkt. Monique Eloit (wa pili), Rais wa OIE na Kamisheni ya Australia Dkt. Mark Schipp (wa nne) na Mwakilishi wa OIE Kanda ya Kusini mwa Afrika Dkt. Samuel Wakusama (Wa tano)
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images