Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

MAMIA YAJITOKEZA KUMWAGA RUGE MUTAHABA, DIAMOND AIBUKA MSIBANI

0
0
 MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.  Kutoa salamu kwa Ruge Mtahaba aliyegusa nyoyo za wengi ziliongozwa na Rais Dkt.John Magufuli, Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete aliyeambatana na mkewe pamoja na Waziri mkuu Kassimu Majaliwa na mkewe bi. Mary Majaliwa.  Wakati huo huo msanii Naseeb Abul maarufu kama Diamond Platnumz pia amewasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kutoa salamu za mwisho.( Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)


  














Uzalishaji Sekta ya Kilimo na Ufugaji Kuongezeka Chamwino

0
0
Frank  Mvungi - MAELEZO, Dodoma
Urasimishaji ardhi Wilayani Chamwino mkoani Dodoma umetajwa kuwa kichocheo cha kukuza uzalishaji katika sekta ya kilimo na ufugaji baada ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wilayani humo.
Akizungumza katika mahojiano maalum Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Bw. Antony Temu amesema kuwa wakulima wamejengewa uwezo kupitia mafunzo yaliyoratibiwa na mpango huo baada ya urasimishaji wa mashamba ya wakulima hao.
“ Wakulima hawa wataweza kuzalisha kwa tija na kuongeza uzalishaji kutoka magunia 4 kwa sasa hadi kufikia magunia 10 kwa ekari moja na pia wataweza kutekeleza dhana ya ufugaji bora wa kuku na mifugo mingine ili kuendana na fursa zilizopo kutokana na Serikali kuhamia Dodoma,”alisisitiza Temu.
Akifafanua, Bw. Temu amesema kuwa wakulima zaidi ya 100 wamenufaika na mafunzo ya kuwajengea uwezo ambapo wakulima kutoka kijiji  cha Membe wameonesha mwitikio mkubwa katika mafunzo hayo hali inayoonesha kuwa mafunzo yataleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa wakulima wilayani humo.
Aliongeza kuwa wakulima hao sasa wametambua mbegu bora za mazao wanayozalisha ikiwemo alizeti hali itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa kijiji cha Membe akiwemo Bi. Pelestatili Msilili amesema kuwa urasimishaji ardhi utawasidia kutatua changamoto zilizopo katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo na hivyo kujikwamua kiuchumi.
“Tutaweza kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha hivyo tunawashukuru MKURABITA kwa kuja na mpango huu wa kutujengea uwezo ambao ni ukombozi wa kweli,”alisisitiza  Bi Msilili
Naye Bi Suzana Kuanikwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Membe amebainisha kuwa anaishukuru Serikali kwa namna inavyowajali wananchi wake kupia uwezesjhaji  huu unaotuwezesha kuwa na matumizi bora ya ardhi katika kijiji chetu.
Aidha, Bi Kuanikwa amebainisha kuwa kwa sasa wakulima wa kijiji hicho watapata mwamko mpya katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo na mifugo.
MKURABITA imekuwa  ikiendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima baada ya kurasimisha mashamba yao katika halmashauri mbalimbali hapa nchini, kwa ujumla halmashauri 24 zimeshafikiwa na Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania.
 Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bw. Antony Temu akisisitiza kuhusu  faida watakazopata wananchi baada ya za kutumia fursa zinazotokana na mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wa kijijin cha Membe wilayani Chamwino hivyo  kuchangia katika kukuza uchumi na ustawi wa wananchi hao .
Sehemu ya wakulima zaidi ya 100 wa Kijiji cha Membe Wilayani Chamwino wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoratibiwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).
(Picha zote na Frank  Mvungi- MAELEZO, Dodoma)

Mkuu wa mkoa Chalamila atembelea viwanda vya Mbeya

KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIA TGNP MTANDAO YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO

0
0
* Wajadili changamoto na mikakati ya kuimarisha ukombozi wa mwanamke, waiomba Serikali kuendelea kushirikiana nao

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
KATIKA kuelekea siku ya wanawake duniani mtandao wa jinsia nchini (TGNP) kwa kushirikiana na SIDA pamoja na mashirika yanayotetea haki za wanawake umewakutanisha wadau mbalimbali katika kutathimini miaka 25 ya mkutano wa Beijing.

Mkutano huo wa Beijing uliofanyika mwaka 1995 ulilenga kuwashirikisha na kuwawezesha wanawake katika maendeleo ili kuimarisha mapambano dhidi ya umaskini na hiyo yote ni kwa wanawake kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.

Akizungumza katika mkutano huo uliolenga kujadili mafanikio ya miaka 25 ya mkutano wa Beijing Mkurugenzi mtendaji wa TGNP Lilian Liundi amesema kuwa ushirikishwaji wa wanawake katika shughuli za kimaendeleo bado unahitaji msukumo zaidi ili kuwajenga wanawake katika kujikomboa zaidi.

Akizungumzia kuhusu changamoto Lilian amesema kuwa, vikwazo vimepungua na masuala kama unyanyasaji wa kijinsia, umiliki mali na ushiriki wa wanawake katika shughuli za kimaendeleo unahitaji msukumo zaidi kwa wanawake.

Lilian amesema kuwa ili waweze kufikia malengo hayo ya milenia ni  kuendelea kuwainua wanawake  katika masuala ya kiuchumi, kifikra na kielimu sambamba na kutoa mawazo na maamuzi katika masuala mbalimbali. Amesema kuwa kupitia mkutano huo wamejadili masuala mbalimbali ya kuweka usawa na kuondoa zile dhana potofu kuhusiana na haki za mwanamke.

Mwanzilishi wa mfuko wa wanawake nchini Mary Lusimbi amesema kuwa mkutano wa Beijing umewafungua wanawake  hasa katika kujua haki zao na kutafuta fursa na ameiomba serikali kwenda nao pamoja ili kupata matokeo chanya. Amesema kuwa  miongoni mwa mambo waliyojadili na yamefanyiwa kazi kwenye bajeti ni pamoja na suala la usawa wa 50 kwa 50.

Mtandao wa jinsia TGNP umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha haki za wanawake na watoto zinaimarika hasa kupitia kampeni mbalimbali ambazo zinapinga ukatili wa ngono na kudumisha haki za watoto.
 Mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa jinsia nchini TGNP Lilian Liundi akizungumza katika warsha hiyo ambapo amesema kuwa mkutano wa Beijing ulifanyika nchini 1995 ni nguvu na thamani ya mwanamke.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mjadala huo kuelekea siku ya wanawake duniani hapo Machi 8.
Mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa jinsia nchini TGNP Lilian Liundi akizungumza katika warsha hiyo ambapo amesema kuwa mkutano wa Beijing ulifanyika nchini 1995 ni nguvu na thamani ya mwanamke.

Waziri Kakunda auomba Ubalozi wa Japan kuendelea kufadhili mfumo wa Kaizen

0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara, George Kakunda ameuomba Ubalozi wa Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo kuendelea kufadhili mfumo wa Kaizen ili kuongeza chachu ya maendeleo ya uchumi.

Pia amesema ni lazima taasisi zote za serikali na viwanda kutumia mfumo huo ili kuleta mabadiliko ya tabia kwa wafanyakazi na kuongeza uzalishaji.

Ameyasema hayo jana Machi 1, 2019 wakati akitoa tuzo kwa kampuni zilizoongoza katika matumizi ya Kaizen.
Kakunda amesema ili kufikia Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 ya kuwa na uchumi wa kati, ni lazima kupunguza vizuizi ikiwemo kodi nyingi zinazotozwa na mamlaka mbalimbali ambazo haziwezi kusaidia kufikia uchumi husika.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, George Kakunda akizungumza wakati wa kutoa tuzo kwa kampuni zilizoongoza katika matumizi ya Kaizen katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, George Kakunda akimkabidhi tuzo kwa kampuni zilizoongoza katika matumizi ya Kaizen katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, George Kakunda akiangalia bidhaa za baadhi ya wajasiriamali mara baada ya kutembelea mabanda wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa kampuni zilizoongoza katika matumizi ya Kaizen katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Picha ya pamoja

BODI YA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR YAANGAMIZA TANI 520 ZA SUKARI ILIYOKOSA KIWANGO

0
0
Na Maryam Kidiko  - Maelezo.                                   
Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Hassan  Khamis Hafidh amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itachukuwa hatuwa kali kwa Mfanyabiashara yoyote atakaeingiza bidhaa isiyokuwa na kiwango kwa ajili ya matumizi ya wananchi.
 Aliyasema hayo Bandari ya Malindi Zanzibar alipofika kuangalia zoezi la kuhamisha tani 520 za sukari kwenda kuangamizwa kwenye mashimo ya mchango katika kijiji cha Zingwezingwe baada ya kugundulika kukosa kiwango kwa matumizi ya binaadamu.
Alisema kuwa Serikali ipo makini kulinda afya za Wananchi wake hivyo haitakubali kuingizwa bidhaa yoyote isiyofaa kwa matumizi ya wananchi  ili kuwaepusha na maradhi.
Aidha alisema ulinzi mkali wa vikosi vya ulinzi na usalama umeandaliwa kwa ajili ya kusimamia sukari hiyo ili kuhakikisha hakuna mtu atakaefanya mbinu ya kuipata mpaka zoezi zima la kuiangamiza limalizike.
Aliwataka Wafanyabiashara kuendesha biashara zao kwa njia za halali na kuacha tabia ya kununua bidhaa za gharama nafuu bila ya kuangali ubora wake kwa lengo la kutafuta faida kubwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Chakula na Dawa Dk. Khamis Ali Omar alisema Makontena 20 ya sukari isiyo na kiwango yenye uzito wa Tani 520 ya Kampuni ya Rashid Ali Trader yaliingizwa Zanzibar mwaka uliopita kwa awamu mbili na alipewa tahadhari kuhusu tatizo la sukari hiyo alipoingiza kwa mara ya kwanza lakini aliendelea kuiingiza.
Alisema baada ya sukari hiyo kufanyiwa uchunguzi ilionekana haina kiwango na kuchukuwa hatua za kisheria ili isiweze kufika kwa wananchi kwa matumizi mbali mbali.Alisema baada ya kugundulika kasoro hiyo, mmilikiwa huyo Rashid Ali  alishauriwa kuirejesha ilikonunua ama kuiingamiza lakini mashauri yote mawili aliyakataa.
Katika siku ya kwanza ya zoezi la kuangamiza sukari hiyo katika mashimo ya mchanga ya Zingwezingwe makontena matatu kati ya 20 yaliharibiwa chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya ulinzi na usalama
Kwa Upande wake Mrakibu Muandamizi wa Jeshi la Polisi Khamis Ramadhan alisema zoezi la kusafirisha sukari hiyo kutoka Bandari ya Malindi na kufika katika sehemu ya kuangamizwa limeenda vizuri na hakuna tatizo lolote lililojitokeza hadi lilipomalizika kwa siku ya kwanza.
Alisema zoezi hilo lililoongozwa na maafisa wa Bodi ya Chakula na Dawa Zanzibar limeshirikisha Vikosi vya Ulinzi na Usalama na wafanyakazi wa kitengo cha Mazingira Zanzibar.
 Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula na Dawa wakimwaga sukari katika mashimo ya mchanga ya Zingwezingwe Wilaya ya Kaskazini B wakiwa katika zoezi la kuiangamiza sukari   tani 520 baada ya kugundulika kukosa kiwango kwa matumizi ya binaadamu.     iliyokosa kiwango kwa matumizi ya binadamu. 
 Gari aina ya kijiko ikiangamiza sukari katika mashimo ya mchanga ya Zingwezingwe Wilaya Kaskazini B baada ya kugundulika kukosa kiwango kwa matumizi ya wananchi.
 Gari zikiwa zimepakia sehemu ya tani 520 za sukari bandarini Malindi zikisubiri kupelekwa mashimo ya mchanga Zingwezingwe, Wilaya Kaskazini B, kwa ajili ya kuangamizwa baada ya kugundulika kukosa kiwango kwa matumizi ya wananchi.
 Shehena ya sukari ikiwa imemwagwa katika mashimo ya mchanga ya Zingwezingwe Wilaya Kaskazini B ikisubiri kuangamizwa baada ya kukosa kiwango kwa matumizi ya wananchi.
 Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Chakula na Dawa Zanzibar Dk. Khamis Ali akizungumza na waandishi wa habari kwenye mashimo ya mchanga Zingwezingwe wakati wa kuangamiza sehemu ya tani 520 za sukari iliyoingizwa nchini ikiwa haina kiwango kwa matumizi ya wananchi.PICHA NA RAMADHANI ALI MAELEZO ZANZIBAR.

RC MTAKA ATOA WITO KWA WANAWAKE KUHIMIZA JAMII KUSOMESHA WATOTO ILI KUONDOKANA NA MILA POTOFU

0
0
 Askofu Jimbo Katoliki la Musoma Mhashamu Michael Msongazila (kulia) akimweleza jambo Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika Machi Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake WaKatoliki Tanzania(WAWATA)  .
 Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiimba pamoja na Kwaya ya Upendo kutoka Kanisa la Anglikana Musoma katika Siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika Machi Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake WaKatoliki Tanzania(WAWATA)  . 
 Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na Askofu Jimbo Katoliki la Musoma Mhashamu Michael Msongazila wakifurahia jambo katika Siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake WaKatoliki Tanzania(WAWATA)  , Machi Mosi, 2019.
 Kwaya kutoka Kanisa Katoliki Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma ikiimba katika ibada ya siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA)  , Machi Mosi, 2019.
 Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa pili kushoto), viongozi wa Kanisa na baadhi ya viongozi wa wanawake wakiwa  ibada ya siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika Machi Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma na  kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) .


 Baadhi ya wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA)wakiwa katika ibada ya siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika Machi Mosi katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma.

Na Stella Kalinga, Mara.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wanawake, kuwa mstari wa mbele kuhimiza jamii juu ya umuhimu wa kuwasomesha watoto, ili kuondokana mila potofu  zilizopitwa na wakati, ukiwemo ubaguzi wa kijinsia na mfumo dume.

Mtaka ametoa wito huo, wakati wa siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika Nyamiongo  Manispaa ya Musoma Mkoani Mara ambako alikuwa mgeni rasmi, ambayo yaliwahusisha wanawake kutoka katika madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA).

Amesema suluhisho la mila potofu zilizopitwa na wakati kama mfumo dume, ubaguzi wa kijinsia na kuona watoto wa kiume ni bora kuliko wa kike ni kuwasomesha watoto wote pasipo kujali kuwa ni wa kike au wa kiume.
“Ukisomesha watoto wako vizuri wakafanikiwa kwenye hiyo nyumba hakuna atakayesema yeye ni bora zaidi ya mwenziye, hakuna atakayesema mimi ndiye mwanaume kwenye hii nyumba na huyu ni  mwanamke, somesheni watoto hayo mambo yote yaliyopitwa na wakati yataisha” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amewaomba wanawake na waumini wote wa ujumla kuendelea kuliombea Taifa, Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine, ili nchi iendelee kuwa na amani na viongozi waweze kufanya mazuri yaliyokusudiwa kwa ajili ya Watanzania wote.
Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa madhehebu ya dini pamoja na kusimamia kiroho wawe msaada kwa makundi mbalimbali yaliyomo makanisani hususani vijana na wanawake, ili yaweze kuendesha miradi ya maendeleo itakayowasaidia kubadilisha maisha yao kiuchumi.
Baadhi ya wanawake walioshiriki katika Maombi ya dunia baada ya kusikia hotuba ya Mkuu  wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alikuwa mgeni rasmi wamesema watahakikisha wanasimamia vema malezi ya watoto wao na kuhakikisha wanasoma huku wakiunga mkono wazo la vikundi kuwa na miradi ya maendeleo.
“ Kama mama nimejifunza mengi; moja ni kuwa tukiwasomesha watoto wetu hakutakuwa na unyanyasaji, mfano kama kuna watu wanafanya ukeketaji kwa watoto wa kike, jamii ikielimika haya hayatakuwepo na tutahakikisha wanasoma mpaka vyuo vikuu; ujasiriamali nao tutafanya ili tujikwamue kwenye umaskini” Devotha Charles mshiriki kutoka Mwisenge
“Baadhi ya wanawake katika makanisa yetu tulikuwa hatua miradi na wengine waliokuwa nayo  ilikuwa  inaenda kwa kusuasua, lakini baada ya ujumbe tulioupokea leo nina hakika utaleta mwamko kwa wanawake wengi kuanzisha miradi ya kuwasaidia kupata kipato” Jackline Cheche mshiriki kutoka Parokia ya Nyamiongo Musoma.
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma Mhashamu Michael Msongazila amesema maombezi kwa ulimwengu yaendelee kufanyika ili watu waweze kuheshimu uhai wa mwanadamu.
“Ombeeni ulimwengu uheshimu uhai wa mwanadamu tumeumbwa katika sura na mfano wa Mungu, tumekabidhiwa dhamana hiyo ya uumbaji, uhai huu tuulinde tuutetee na tuukuze kwa ajili ya kujenga ulimwengu, maisha yetu yana nafasi ya pekee yanapokuwa na Mungu” alisema Askofu Mlonganzila.
Maombi ya Dunia kwa wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) hufanyika kila mwaka Machi Mosi yakiwa na lengo la kuombea familia, Taifa na Dunia kwa ujumla juu ya amani na mahitaji mengine.

Tigo yamzawadia mkimbiaji shupavu mwenye miaka 93 nyumba

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania Simon Karikari (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria kumkabidhi rasmi nyumba mzee Joram Mollel (93) ambaye amekuwa akishiriki mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka minne mfululizo. Kulia kwake ni mzee Mollell akifautiwa na mwanaye Elibarik Mollel pamoja na Afisa Biashara Mkuu wa Tigo Tarik Boudiaf. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha. Kulia ni kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba

 Babu Joram Molle (93)  akitoa neno la shukrani muda mfupi baada ya kukabidhiwa nyumba na Kampuni ya Tigo kutokana na ushiriki wake wa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka minne mfululizo. Wanaomsikiliza kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari akifuatiwa na Afisa Biashara Mkuu Tarik Boudiaf, na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania Simon Karikari, akimkabidhi fungua za nyumba mzee Joram Mollel ikiwa ni kama zawadi na kukubali mchango wake kwa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka minne mfululizo pamoja na umri mkubwa. Anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja muda mfupi baada ya Kampuni hiyo kumzawadia nyumba mzee Joram Mollel mkazi wa Jijini Arusha ikiwa ni kutambua mchango wake katika mbio za Tigo Kili Half Marathon ambazo mzuee huyo ameshiriki kwa miaka minne mfululizo. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tigo Simon Karikari akizungumza na wahabari hawapo pichani wakati wa hafla ya kumkabidhi nyumba Mzee Joram Mollel (93), aliyekuwa akikimbia mbio za Tigo Kili Half Marathoni kwa miaka minne mfululizo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha.





KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo imemkabidhi nyumba ya vyumba 17 ikiwa na samani zote za ndani Babu Joram Mollel (93), kutokana na ushiriki wake wenye mafanikio katika mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka mine mfululizo.

Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika eneo la Mushono nje kidogo ya Jiji la Arusha, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari pamona na Afisa Biashara mkuu Tarik Boudiaf 

Akizungumza kwenye hafla hiyo Karikari alisema, nyumba hiyo ilinunuliwa na kukarabatiwa kisha kumkabidhi Babu Mollel kama ishara ya shukrani kwa kujituma na umahiri wake katika riadha.

'Babu Mollel amekuwa akishiriki mashindano ya Tigo Kili Half Marathoni kwa miaka mingi sasa. Tulipoona hali ya makazi yake si nzuri Tigo tuliona njia sahihi ni kuwezesha apate nyumba yake mwenyewe,"alisema Karikari.

“Katika nyumba yake hii ya hapa Mushono, Babu atakuwa anakaa katika nyumba ya kisasa, iliyo tayari na samani pamoja na vyombo vyote muhimu vya ndani. Nyumba hii pia imeunganishwa na umeme na maji. Hati ya nyumba pia ipo kwa jina lake, hivyo yeye ndiye mmiliki halali wa nyumba hii,” aliongeza Karikari. 

Aidan Komba, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini alisema kwamba nyumba imegawanyika sehemu tatu na kuongeza kuwa Babu Mollel atakaa katika nyumba moja na mbili zilizobaki ataweza kuzipangisha na kujipatia kipato cha kuendeshea maisha yake ya kila siku. 

“Napenda kuwashukuru sana Tigo kwa zawadi hii ya kipekee. Maneno yangu hayawezi kuelezea furaha niliyonayo. Ktendo hiki kina maana kubwa sana kwangu. Maana hivi sasa ninaweza nikasema sasa nina mahali pakuita kwangu,” alisema Babu Mollel. 

Ushiriki wa Babu Mollel katika mashindano ya Kilimarathon ni wa zaidi ya miaka 15, ambapo amekuwa akiwavutia watu wengi kumshangilia wakati akishiriki mbio za marathon, pamoja na uzee wake. Katika miaka minne mfululizo iliyopita, Tigo imekuwa mlezi na mdhamini mkuu wa mbio za kilometa 21 zinayojulikana kama ‘Tigo Kili Half-Marathon’, ambayo ni nusu ya mbio kamili ya kilometa 42 za marathon ambayo hufanyika katika vilima vya Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kuliko wote barani Afrika. 

“Babu Mollel ni taswira halisi ya uanamichezo, ujasiri na jitihada. Yeye ni mfano aliye hai kwamba kama binadamu tunaweza tukafanikiwa katika lolote lile ambacho tukiamua kukifanya kwa dhati, na kuondoa dhana nzima kwamba umri au changamoto zingine zozote zinaweza zikawa sababu ya kutokufanikiwa kwetu. Leo, tunamsheherekea yeye,” alieleza Karikari kuhusu mzee huyo wa miaka 93.

Mwaka jana, Tigo ilishirikiana na Babu Mollel katika kampeni maalum ya Tigo Kili Half-Marathon iliyoitwa ‘Tisha kama Babu’. Kampeni hiyo ilikuwa na lengo kubwa la kuhamasisha Watanzania kuweza kuishi maisha ya kujali afya zao. Wakati huo huo, Tigo pia ilisitisha rasmi namba ya mbio aliyokuwa akiitumia Babu Mollel ‘1040’ na alitambuliwa rasmi kama mwanamichezo wa heshima ‘Hall of Fame’.. 


KARIBU RUGE UNASUBIRIWA NYUMBANI UPUMZIKE .

0
0
Anaandika Abdullatif. Yunus

Siku ya Jumamosi Bado Masaa machache kabla ya kumpokea Mpambanaji, Shujaa, Muongoza njia Marehemu Ruge Mutahaba Nyumbani kwao Kiziru, Kabale - Bukoba. Hali ni shwari nyonyo za waombolezaji zikiwa zimejaa simanzi na masikitiko kwa kuondokewa na kipenzi chao Ruge, Kamati ya Maandalizi chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inazidi kujipanga kuupokea ugeni Mkubwa uliobeba zawadi ya Mpendwa wao, kiu ikiwa kubwa zaidi kwa ndugu jamaa na marafiki kutaka kushuhudia kwani wengi hawajaamini kile wanachokiona na kukisikia Dar es salaam. 

Kufuatia Msiba huo tayari Sheikh wa Mkoa Kagera Alhaj Haruna Kichwabuta amefika msibani kutoa pole kwa wafiwa, Mara baada ya kurejea akitokea Zanzibar akiwa ameambatana na Sheikh wa Mkoa wa madhehebu ya Ijumaa na Adhuhuri Alhaji Kamugunda.

Kutokana na Shughuli za siku ya Jumatatu (siku ya mazishi) kuhamishiwa Viwanja vya Gymkhana Kamati ipo katika mipango ya kuratibu eneo kwa ajili ya mpangilio wa majukwaa, maegesho na huduma nyingine, pia katika kuheshimu ukubwa wa Msiba huu tayari barabara ya kuelekea Kijijini Kiziru Kabale Nyumbani kwao Marehemu imeanza kukarabatiwa ili kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa upande wa usafirishaji wa watu watakaokwenda msibani.

Hali ilivyo sasa Nyumbani tayari kaburi limekamilika likingoja kwa heshima Mwili wa Shujaa, upande mwingine maandalizi yanaendelea baada ya kufungwa Turubai (tents) waombolezaji sasa wanaendelea kufika hapa kwa ajili ya kutoa pole.
Kaburi likiwa limefunikwa vizuri likingoja Kumsitiri  mpendwa wetu,Shujaa
Sheikh wa Mkoa Kagera (BAKWATA) Haruna Kichwabuta alievaa Koti, pamoja na Sheikh wa Mkoa madhehebu ya Ijumaa na Adhuhuri Alhaji Kamugunda wakiwa Nyumbani kwa Profesa Mutahaba Kiziru Kabale.
Sheikh Haruna Kichwabuta akiwa na Mzee Revelian Rwabyo mmoja wa waasisi wa Familia ya Mzee Mutahaba, Mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao Marehemu Ruge Kutoa pole.
Pichani ni marekebisho na ukarabati unaoendelea katika barabara ya kuelekea kijijini Kiziru Kabale Bukoba, katika kusawazisha mashimo na baadhi ya maeneo korofi ili ipitike kiurahisi.
Pichani Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akijadiliana jambo na Katibu wake Ndg. Salala Katika viwanja vya Gymkhana wakati Kamati hiyo ilipofika viwanjani hapo kuendelea kuratibu shughuli ya kuupokea ugeni wa Msibani wa Ruge.
Pichani ni Askofu TZA wa Clouds (mwenye kofia) akitoa ufafanuzi kuhusu jukwaa litakalofungwa eneo hilo kwa ajili ya shughuli ya kuaga.
Pichani ni viwanja vya Gymkhana ambapo shughuli nzima ya Ibada na Kuaga itakapofanyika, kama unavyoona Kamati chini ya Mkuu wa Mkoa Kagera Tayari imefika Kuendelea kuratibu tukio.

PICHA HII INANITOA MACHOZI,niifute ama niiache kama kumbukizi? Nishaurini.

0
0
Picha hii Ilipigwa 15/August/2018, ni dhahiri ni picha ya Mwisho Ruge kuonekana Public,alikua na nafuu,alikuja ofisini, juzi yake nilikua nimepokea ujumbe kuachana na Clouds kuuanza Utumishi wa Umma na mtu wa kwanza kumpigia kabla hata ya baba yangu mzazi alikua ni Ruge si kwa nia mbaya ila nilitaka mwongozo wa Haraka.

Alifurahia na hapo hapo Aliwapigia simu viongozi mbalimbali kwa wito wangu na direct hasa Katibu mkuu Utumishi Dk.Ndumbaro akimuomba anipokee kijana wake serikalini na akimsisitiza kua “ni kijana niliemlea kwa nguvu sana na nimewekeza sana kwake, mtumie vizuri, nimeumia kumpoteza ila ni kazi yangu kuandaa vijana wakaitumikie nchi yao,alimwambia huyu ni azina kwa taifa hili na atawasaidia”,aliyasema haya akiwa kitandani anaumwa.

Baada ya kuripoti siku hii pichani alipata nafu akaenda ofisini akanisihi nije Dar niondoke Dodoma haraka anataka anipe baraka zake na kunikutanisha na Mwalim wangu wa Sayansi ya Siasa Ndugu Bashiru Katibu Mkuu wa CCM Taifa ofisini kwa Clouds ambae pia alifanya kipindi Clouds360 siku hiyo, alimwambia Katibu “kijana wangu huyu Serikali imeninyang’anya anaenda Pangani kuitumikia nchi,ni kijana ninaemuamini sana na ana uwezo mkubwa sana” baada ya hapo tuliongea mengi na baadae kumsindikiza katibu mkuu chama na kupiga picha ya ukumbusho na kumbe ni picha ya mwisho na akaniita tena ofisini na kunambia “nenda usiniangushe na usiisahau Clouds na THT ,utafika mbali”.

Ulilalamika kuwa naondoka huku unaniitaji sana na umeniandaa ili nije kuuinua Clouds Media mimi na vijana wengine unaowatengeneza maana unataka kupumzika mambo ya Clouds hivo utatuachia sisi sikuelewa kupumzika kwa maana gani?

Picha hii imenikumbusha mafundisho ulionipa mara zote, ni kila wakati naada ya kazi ungenpigia kila mmoja aliefanikisha kumwambia “Im proud of you” ,ulikua mtu wa kutoa moyo sana na kushukuru kila jambo, lililofanikiwa kwenye project zako

Ruge nadhani tunapaswa kuandika KITABU juu yako na natoa rai tuungane kufanya hili..!tukisema mengi tutawachanganya watu, wengine hawaelewi wanahisi tunaongeza chumvi ila ni wazi kwetu ulikuna kama NABII..!
Sisi nasi tuna mioyo ya namba gani tusikulilie kwa kilio cha uchungu na machozi ya damu.?
#shujaamwogozanjia


Na Gibson George Bayona Ruge.
 

BIMA YA AFYA NDIYO SULUHISHO LA UHAKIKA WA MATIBABU-WAZIRI UMMY MWALIMU

0
0
aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (kushoto) akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Dkt Halima Mangiri. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisema jambo wakati wa kikao na watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa (hawapo pichani) 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu ( kulia) akiwasalimia mama na mtoto katika wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisoma nyaraka za dawa katika chumba cha dawa cha Hospitali ya Wilaya ya Kilosa. 
 

Na WAMJW – Kilosa, MOROGORO.

Wananchi wametakiwa kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo alipokuwa ziarani Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro akikagua hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa. “Ni muhimu kwa wananchi kuwa na bima ya afya ili waweze kuwa na uhakika wa kupata matibabu ikiwemo dawa bila ya kikwazo cha fedha” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa matarajio ya wananchi mara baada ya kujiunga na bima ya afya ni kupata huduma bora za afya bila usumbufu huku wakiwa na uhakika wa kupata dawa kwa makundi yote ikihusishwa wale wa Bima ya Afya pamoja na Mfuko wa Bima ya Afya Ngazi ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa.

“Mwananchi yeyote ambaye amekuja na bima ya afya, CHF iliyoboreshwa wanapaswa kupata huduma zote, kumwona daktari bure, vipimo bure, na dawa bure” amesema Waziri Ummy na kuongezea “Bila ya kufanya hivyo hakuna umuhimu wa kuwaambia wananchi kukata bima za afya.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amewataka watoa huduma za afya nchini kutoa huduma bora kwa kuzingatia Mwogozo wa Taifa wa Matibabu na orodha ya dawa muhimu huku akiwataka kutoa huduma bora za matibabu kwa kutoa dawa kulingana na mwogonzo unavyobainisha. “Badala ya kumwandikia unayoitaka wewe au mgonjwa, tumeweka utaratibu weka dawa ambayo ipo kwa mujibu wa mwongozo” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wananchi wanapata dawa katika vituo vya kutolea huduma kwani kumekuwa na malalamiko hapo zamani wagonjwa wakisema madaktari walikuwa waki waambia dawa hakuna huku ili hali dawa zipo.

“Hatutaki kuona wananchi wanalalamika dawa hakuna na kutuona tunadanganya wakati dawa zipo, na mwongozo unasema wazi kama hakuna dawa A mpe dawa B. Alisikika akisema Waziri Ummy. Ka upande mwingine Waziri Ummy ameupongeza Uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa kuhakikisha dawa zinapatikana kwa ufanisi muda wote na kuwataka mafanikio ambayo wameyapata wahakikishe waharudi chini.

“Serikali itaendela kuhakikisha inaboresha Sekta ya afya ili Taifa liweze kuwa na nguvu kazi yenye afya bora kazi yenu nyinyi ni kuhakikisha mnaendelea kutoa huduma bora na kuhakikisha dawa zinapatikana muda wote” amesema Waziri Ummy. Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Dkt. Halima Mangiri ameishukuru Serikali kwa kuuongeza bajeti ya dawa wilayani humo.

Dkt. Mangiri amesema kuwa bajeti ya dawa imekuwa ikiongezeka maradufu mwaka hadi mwaka huku akitolea mfano wa mwaka 2017/18 hali ya upatikanaji wa dawa ilikuwa ni asilimia 86, huku kwa mwaka 2018/19 hali ya upatikanaji dawa ikiongezeka na kufikia asilimia 96.

“Tunaishukuru Serikali, Kwa kweli hali sasa sii kama zamani, tunapata dawa na hali inaridhisha” alisema Dkt Mangiri. 

Wananchi Wamiminika Mloganzila kupima Usikivu

0
0
Daktari Bingwa wa Upasuaji Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo, Dkt. Godlove Mfuko wa Hospitali ya Taifa Muhimbili –Mloganzila akimpima mgonjwa kiwango cha usikivu katika zoezi la upimaji wa usikivu linalofanyika leo hospitalini hapo leo na kesho.
002
Katika picha baadhi ya wananchi waliojitokeza kupima kiwango cha usikivu hospitalini hapo.
003
Wazazi wakiwa na watoto kabla ya kwenda kuwaona wataalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo wa Hospitali ya Muhimbili Upanga na Mloganzila.
004 A004 B
Wananchi wakisubiri kupata huduma ya upimaji ya usikivu katika Hospitali ya Mloganzila.
005
Mtaalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Teddy Uisso akimpima mgonjwa kiwango cha kusikia.

006
Mratibu wa Usikivu kutoka Mfuko wa Usikivu wa Starkey akitoa elimu kwa wananchi wanaosubiri kuwaona wataalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.

………………………..
Wingi wa watu waliojitokeza leo kupima usikivu wao umeonyesha ni jinsi gani wananchi wanajali afya zao, huku wakipewa sababu zinazosababisha baadhi ya watu kupoteza uwezo wa kusikia na jinsi ya kuzuia upotevu wa kusikia.
Upimaji wa usikivu bila malipo umeanza leo Machi 2, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ambapo kauli mbiu ni “Chunguza Usikivu Wako (Check Your Hearing” yenye lengo la kuhamasisha kila mmoja kuchukua hatua ya kufanyiwa uchunguzi wa usikivu wake.

Huduma ambazo zimeanza kutolewa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ni; upimaji wa kuona kiwango cha kusikia na rufaa ya kupata matibabu Muhimbili kwa watakaobainika kuwa na tatizo. Pia elimu ambayo imetolewa ni dalili na vyanzo vya kupoteza usikivu, kutoa takwimu za ongezeko la upotevu wa usikivu duniani na hatua zinazochukuliwa nchini.

Katika shughuli ya upimaji huo, wananchi wameelezwa sababu zinazosababisha mtu au watu kupoteza uwezo wa kusikia. Zifuatazo ni sababu zinazosababisha watoto wachanga kupoteza uwezo wa kusikia. Kwanza familia kuwa na watu wenye matatizo ya kutokusikia, maambukizi ya magonjwa kutoka kwa mama wakati akiwa mjamzito, mtoto kuzaliwa kabla ya wakati, mtoto kukosa hewa wakati wa kuzaliwa na kupata homa ya manjano baada ya kuzaliwa.

Kwa upande wa watoto na watu wazima, sababu zinazosababisha kupoteza uwezo wa kusikia ni; kuugua surua, uti wa mgongo au sikio kupata maambukizi na uchafu kutoka sikioni, matumizi yasiyo sahihi ya dawa mbalimbali, kuumia sikio au kichwa, kukaa sehemu zenye kelele au zenye sauti kubwa sana, kusikiliza sauti kupitia vifaa mbalimbali kabla ya umri unaofaa na nta au kitu kisichokuwa cha kawaida kuziba mfumo wa njia ya sikio.

Wazee nao wamekuwa wakipoteza uwezo wa kusikia kutokana umri wao hivyo uwezo wao wa kusikia hupungua, kukaa sehemu zenye kelele au zenye sauti kubwa sana, kupata shinikizo la damu, kuugua sukari na wengine kutumia dawa mbalimbali.

Wataalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo wanaeleza kuwa njia za kuzuia upotevu wa kusikia kwa mtu mzima ni kuweka kifaa au kitu chochote ndani ya sikio, anashauriwa kutumia pamba laini au kifaa maalumu cha kuziba masikio kwenye sehemu zenye sauti kubwa, endapo ana shida ya sikio au masikio anatakiwa kumuona daktari, anatakiwa kuchunguza dawa anazotumia kama zinaweza kuathiri usikivu wake na pia, anashauriwa kutumia vifaa salama vya masikio kama ulivyoelekezwa na daktari.

Kwa upande wa watoto; mzazi anashauriwa asimweke mtoto kifaa au kitu chochote ndani ya sikio labda kama unamsafisha sikio, watoto wanapaswa kufundishwa kutokuweka kifaa au kitu chochote ndani ya sikio, endapo  sikio la mtoto linauma, limeumia, kukatika au linatoka uchafu  ndani mpeleke kwa daktari, usiwaruhusu watoto kuogelea kwenye maji machafu, mzazi usimpige mtoto sehemu za sikio, mkinge mtoto katika sehemu zenye sauti au kelele kubwa na wafundishe watoto kusikiliza kwa kutumia vifaa salama.

Katika hatua hii, mzazi au mlezi anawezaje kuhisi mtoto wake amepoteza uwezo wa kusikia? Mtoto anaweza kuwa na matatizo ya kutokusikia ikiwa hatojibu jambo kwa sauti, kutokuelewa kitu gani kinazungumzwa au kushindwa kuongea kwa ufasaha, kuchelewa kuongea kwa ufasaha, kutokwa na uchafu sikioni, na kuumwa sikio mara kwa mara au sikio kuziba.

Kwa upande wa mtu mzima atakuwa amepoteza uwezo wa kusikia endapo;  atauliza mara kwa mara watu warudie walichoongea, kuwa na tabia ya kuongeza sauti ya redio na runinga, kukosa baadhi ya maneno katika maongezi, kuwa na kelele katika sikio na wakati mwingine watu wanakwambia unaongea kwa sauti kubwa sana.


Upimaji wa usikivu bila malipo umeanza leo Machi 02,2019 na utamalizika Kesho Machi 03,2019.

Morogoro kutumia Tsh. 355 Bil 2019/2020

0
0


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akifungua kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro
Wajumbe wa Kikao cha RCC wakiwa katika Ukumbi tayari kwa majadiliano.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Clifford Tandari (aliyesimama)akimkaribisha Mwenyekiti wa Kikao cha RCC kufungua kikao hicho kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro
Mbunge wa Jimbo la Malinyi Mkoani Morogoro Mhe. Haji Mponda akichangia hoja wakati wa kikao cha RCC kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro
Wajumbewa Kamati ya RCC wakisikiliza kwa makini mawasilisho ya sekta mbalimbali zilizowasilishwa kwenye kikao hicho kilichofanyika Machi Mosi, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro



…………………..

Na. Andrew Chimesela – Morogoro

Mkoa wa Morogoro umepanga kutumia zaidi ya shilingi 355Bil. katika Bajeti yake ya makadirio ya mwaka wa fedha 2019/2020 ambazo fedha hizo zitatumika katika matumizi mbalimbali ikiwemo mishahara ya watumishi wake, Maendeleo na matumizi mengine.

Hayo yalibainishwa katika kikao cha Ushauri cha Mkoa kilichofanyika Machi Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Mjini Morogoro ambapo wajumbe wake waliridhia makadirio ya Bajeti hiyo Kutumika.

Akiwasilisha Bajeti hiyo, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uratibu na Utawala Bw. Diaz Ndomba kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Clifford Tandari alisema bajeti hiyo imezingatia mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya mwaka 2019/2020 na Ilani ya Uchaguzi ya chama cha Mapinduzi (2015).

Aidha, amesema Bajeti hiyo imezingatia pia Dira ya Maendeleo ya Taifa (2020/2025), malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (2030) pamoja na malengo ya Mpango wa kufanya mageuzi ya kiuchumi wa Viwanda hapa nchini.

“kipaumbele kimeendelea kuwekwa katika kuimarisha mazingira wezeshi ya Ujenzi wa Viwanda vidogo, vya kati na vikubwa” alisisitiza Bw. Ndomba.

Mchanganuo wa bajeti hiyo ambayo ni ongezeko la asilimia 16 ukilinganisha na Bajeti ya mwaka 2018/2019 ni za matumizi ya kawaida ambapo Sh. 267,398,052,000 zitatumika kwa ajili ya mishahara huku matumizi mengineyo zitatumika Sh. 36,075524,000 na kufanya jumla yake kuwa Sh. 303,473,576,000.

Kwa upande wa Matumizi ya miradi ya Maendeleo Mkoa huo umepanga kutumia Sh. 37,817,411,000 ikiwa ni fedha za ndani na Sh. 13,953,937,000 zitakuwa ni fedha za nje na kufanya jumla 51,771,348,000 hivyo jumla kuu kufikia Sh. 355,244,924,000.

Mwisho wa mawasilisho hayo Mkoa ulitoa Ombi kwa Serikali kuu hususan Wizara ya Fedha na Mipango kuendelea kutoa kwa wakati fedha zilizopangwa na kupitishwa kama ilivyoainishwa kwenye mpango kazi wa Mkoa.

Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe aliendelea kuwaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa huo kusimamia rasilimali fedha zinazopatikana ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato ya ndani kwa kutumia mashine za kiilektroniki na kuzipeleka Bank kwa wakati.

Aidha, aliwaonya watumishi wa umma wenye tabia ya kutumia vibaya fedha za Serikali kuacha tabia hiyo mara moja la sheria itawafuata huku akiwataka Wenyeviti wa Halmashauri hizo kuwachukulia hatua kali za kisheria na za kinidhamu watumishi hao watakaokiuka katika kutumia vibaya rasilimali fedha za Serikali.

“Ila tu ukivunja utaratibu ndio mambo mengine yanajitokeza kwa bahati nzuri Wenye viti wa Halmashauri mpo, kama hayo yanatokea msisite kuchukua hatua, kwa sababu miongozo ipo na wataalamu wapo muwape taarifa sahihi kwa ajili ya kuchukua hatua.”alisisitiza Dkt. Kebwe

Katika kipindi cha kujadili yatokanayo suala la Kijiji cha Ngombo kilichopo Wilaya ya Malinyi Mkoani humo liliibuka huku baadhi ya wajumbe wakitaka ufafanuzi zaidi ambapo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omari Mgumba (MB) aliwaka wajumbe pamoja na wananchi wa Kijiji cha Ngombo kuendelea na kazi zao kama kawaida kama Serikali ilivyoagiza lakini bila kufanya uendelezaji mwingine katika maeneo hayo hadi hapo Serikali itakapotoa kauli nyingine.

Aidha, Naibu Waziri huyo wa Kilimo alishauri kuwa ili Mkoa uwe na mipango sahihi juu ya kilimo ni lazima Mkoa kuwa na mpango Mkakati kuhusu kilimo na kusimamia kwa karibu zoezi la kupata takwimu sahihi za wakulima hususan wa mazao ya kimkakati kwa kuwasajili ili kujua idadi yao, mahali walipo, kiasi cha eneo wanalolima, mazao wanayolima pamoja na mahitaji yao ya msingi.

AGAPE YAUNDA MABARAZA YA WATOTO KUPIGA VITA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI SHINYANGA

0
0
Shirika lisilo la Kiserikali la Agape AIDS Control Programme (AACP) la mkoani Shinyanga linalotetea haki za watoto limeunda Mabaraza ya Watoto ngazi ya vijiji katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, kwa lengo la kuwajengea uwezo watoto kupaza sauti dhidi ya vitendo ya vya ukatili ambayo huwa wanafanyiwa, ikiwemo kupewa ujauzito na kuozeshwa ndoa za utotoni.

Zoezi la uundaji wa Mabaraza ya watoto limeendeshwa leo Machi 2, 2019  na Ofisa Maendeleo ya Jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari kwa kushirikiana na Shirika la Agape, ambapo jumla ya mabaraza matano yameundwa katika kijiji cha Chembeli, Mwanono, Didia, Mwamalulu na Bukumbi.Akizungumza wakati wa uundaji wa Mabaraza hayo, Meneja Mradi wa Kuzuia Mimba na Ndoa za Utotoni kutoka Shirika la AGAPE Mustapha Isabuda, amesema Mabaraza hayo ya watoto yatakuwa chachu kubwa ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya watoto. 

Alisema watoto wanapokuwa wanakutana kwa pamoja wao wenyewe kupitia mabaraza hayo, huwa wanakuwa wawazi kuelezea changamoto za matukio ya kikatili ambayo huwa wanatendewa na baada ya hapo viongozi wao huziwasilisha kwenye mamlaka husika akiwemo mtendaji wa kijiji na hatimaye kutatuliwa. 

“Tumeunda Mabaraza haya ya watoto ngazi ya vijiji katika kata ya Didia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wetu wa kupinga mimba na ndoa za utotoni, ambao unafadhiliwa na Shirika la kimataifa la FireLight Foundation kutoka nchini Marekani ambapo kwenye kata hii kuna matukio mengi ya ukatili dhidi ya watoto,”alisema Isabuda. 

Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Shinyanga Aisha Omari alipongeza uundaji wa mabaraza hayo ya watoto na kutoa wito kwa watoto wayatumie vizuri ili kujikomboa na kupata haki zao za msingi, ikiwemo kutobaguliwa, kupewa elimu hasa kwa watoto wa kike na kutoozeshwa wangali watoto.Kwa upande wao watoto hao akiwemo Nyamisi Singu ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la watoto katika kijiji cha Bukumbi alisema mabaraza hayo yatakuwa msaada mkubwa sana kwao kwani  idadi kubwa ya watoto huwa wanaogopa kuelezea changamoto zao kwa watu wakubwa, na mwisho wa siku wanaambulia ujauzito ama kuozeshwa ndoa za utotoni. 

Wenyeviti waliochaguliwa kuongoza wenzao katika Mabaraza ya watoto, ni  Yusuf Sita (kijiji cha Mwanono), Aloyce Masele (Chembeli), Ashraf Salumu (Didia), Paschal Maganga (Mwamalulu) na Nyamisi Singu (Bukumbi).Wengine ni Karoline Issaya ambaye amechaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti baraza la watoto kijiji cha Mwanono ,katibu ni Ramadhani Frank, Chembeli Makamu mwenyekiti ni Milembe Maila ,katibu ni Sofia Sudi, Didia Makamu mwenyekiti ni Mwanne Emmanuel ,katibu Sundy Mayala, Mwamalulu Makamu mwenyekiti ni Scholastika Kidaha, katibu Pendo Hassani, Bukumbi Makamu mwenyekiti ni Elivida Kabuga, katibu akiwa ni Ramadhani Mrisho. Meneja Mradi wa Kuzuia Mimba na Ndoa za utotoni kutoka Shirika la Agape la kutetea haki za watoto mkoani Shhinyanga Mustapha Isabuda ,akizungumza na watoto juu ya umuhimu wa Mabaraza ya watoto namna yatakavyoweza kuwasaidia kutokomeza matukio ya ukatili dhidi yao na kuweza kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu, pia kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Ofisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari akiwataka watoto kuyatumia vizuri Mabaraza ya watoto katika kupaza sauti juu ya matukio ya ukatili dhidi yao ili yapate kufanyiwa kazi kabla ya kuwaletea madhara. Ofisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omari, akiwasisitiza watoto kuacha kuficha matukio ya ukatili wanayofanyiwa bali wayafichue ili wawe salama na kuweza kutimiza ndoto zao. Ofisa Maendeleo ya jamii Kata ya Didia wilaya ya Shinyanga Felista Mell, akielezea hali ya matukio ya ukatili kwenye kata hiyo ikiwemo utekelezaji wa watoto pamoja na kupewa wanafunzi kupewa mimba, ambapo kwa mwaka huu tayari wanafunzi watatu wa shule za msingi wana ujauzito na wameshaachishwa masomo, na kuwataka watoto hao wavunje ukimya watoe taarifa mapema ya matukio ya ukatili.Afisa Mtendaji wa Kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Jackson Majenga, akiwataka watoto hao kupitia viongozi wa mabaraza yao, kumpelekea pia taarifa za matukio ya kikatili ili ayafanyie kazi, ambapo mpaka sasa wameshamkamata mtuhumiwa mmoja wapo ambaye amempachika mimba mwanafunzi huku wengine wawili wakiendelea kutafutwa. Watoto wakiwa kwenye mkutano wa kuunda Mabaraza yao, wakisikiliza nasaha kutoka kwa viongozi wa serikali na Shirika la Agape juu ya kuyatumia mabaraza kupaza sauti na kupata haki zao za msingi.Watoto wakiendelea kusikiliza nasaha za viongozi kabla ya kuanza uchaguzi wa kuunda mabaraza yao ambayo yatakuwa msaada mkubwa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi yao likiwemo na suala la mimba na ndoa za utotoni na hatimaye kutimiza ndoto zao. Watoto wakiendelea kusikiliza kwa makini namna ya kutumia Mabaraza yao kutoa taarifa za matukio ya kikatili dhidi yao, ikiwemo fursa ya kupata elimu hasa kwa watoto wa kike na kutoozeshwa ndoa za utotoni kwa tamaa ya wazazi kutaka mifugo. Viongozi wa Baraza la watoto katika kijiji cha Chembeli ambao wamechaguliwa wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa baraza hilo Aloyce Masele katikati ni Makamu mwenyekiti Milembe Maila, akifuatiwa na katibu Sofia Sudi. Ashraf Salum (kulia) amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la watoto katika kijiji cha Didia akiwa na makamu wake Mwanne Emmanuel. Nyamisi Singu (wa kwanza kulia) amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la watoto katika kijiji cha Bukumbi, katikati ni Makamu wake Elivida Kabuga na wa kwanza  kushoto ni Katibu Ramadhani Mrisho. Watoto wakifurahi pamoja na Ofisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya Aisha Omari, mara baada ya kumaliza kuunda Mabaraza na kuchagua viongozi ambao watakuwa wakiwaongoza katika mikutano ya kujadili changamoto ambazo huwa zinawakabili juu ya matukio ya ukatili dhidi yao ili  yatatuliwe.Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI, MACHI 3,2019


NEWZ ALERT: Rais DKTMagufuli afanya mabadiliko madogo Baraza la Mawaziri

WAZIRI MHAGAMA AFUNGUA WARSHA YA MAFUNZO KWA VIONGOZI NA WADAU WA MKOA WA TANGA KUHUSU MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI

0
0


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akihutubia washiriki wa Warsha ya Mafunzo kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda kuja Tanga yaliyofanyika katika Ukumbi wa Tanga Beach Resort Machi2, 2019.
Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shigela akihutubia wakati wa Warsha hiyo.
Sehemu ya Wajumbe walioshiriki Warsha ya Mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa warsha hiyo.
Sehemu ya Wajumbe walioshiriki Warsha ya Mafunzo hayo wakifuatilia hotuba uya mgeni rasmi wakati wa warsha hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akifuatilia jambo wakati wa warsha ya mafunzo hayo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya watendaji wa Serikali wakati uzinduzi wa warsha hiyo mkoani Tanga.


Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’i Issa akizungumza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Tanga alipokutana nao wakati wa Warsha ya Mafunzo kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Machi 2, 2019.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka Sekta ya Umma wakati wa warsha hiyo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

………………………………………


NA.MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama leo Machi 2, 2019 amefungua warsha ya mafunzo kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda kuja Tanga, Tanzania.

Warsha hiyo iliwakutanisha zaidi ya wadau 70 wakiwemo viongozi Waandamizi na Watendaji Wakuu wa Mkoa wa Tanga, Wafanyabiashara wa mkoa huo pamoja na wanahabari na kufanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort mkoani Tanga.

Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo ambayo itafanyika kwa muda wa siku mbili (Machi 02 na 03, 2019),Mhagama alisema Serikali inaendelea kuhimiza wananchi kutumia fursa ya mradi huo katika kujiletea maendeleo yao nan chi kwa ujumla.

“Mkutano huu wa leo ni matumaini kuwa, utaleta mageuzi makubwa ya mipango mikakati yetu ili kuangalia fursa za ujio wa mradi huu kwa kuzingatia ni moja kati ya mradi unaotarajiwa kuwa na manufaa mengi kwa nchi katika kuzalisha ajira, kuendeleza urithishaji wa ujuzi na teknolojia pamoja na ubia kati ya makapuni ya Tanzania na wageni,”alisema Mhagama

Waziri aliongezea kuwa, inawapasa wananchi kutumia warsha hiyo kujadili na kuweka mikakati bora ya kuzitumia fursa zitakazotokana na mradi kwa kuzingatia malengo mahususi ikiwemo kujadili maendeleo ya mradi na fursa za ushiriki wa Watanzania katika ujio ya mradi pamoja na kuwa na majadiliano kati ya Sekta Bonafsi ya Umma ili kuchochea maendeleo endelevu ya kiuchumi

Aliongezea kuwa, mradi huo utasaidia jamii kushiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo kwa kuzingatia kuwa, ni zaidi ya robo tatu ya Bomba hili litapita Tanzania na kuwanufaisha wananchi wake.

“Matarajio ni makubwa kwa kuzingatia mradi huu unatarajiwa kupita katika mikoa 8 ikiwemo Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga ambapo litapita katika Wilaya 24, Kata 134 na Vijiji zaidi 180 hivyo hatuna budi kuchangamkia fursa kwa kuongeza jitihada za ongezeko la ushiriki wetu,”alisistiza Mhagama

Naye Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shiga aliendelea kuhimiza watendaji wake kushiriki kikamilifu katika hatua zote za maandalizi kama Mkoa ili kuona namna bora za kushiriki katika fursa hiyo kubwa ya kujileea maendeleo yao.

Naye Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa alieleza jitihada za Baraza ikiwemo kuanzishwa kwa kanzi data ya nguvu kazi ambayo inachukua takwimu za wafanyabiashara ili kiuwatambua kwa lengo la kushirikisha katika program na kuona namba bora ya kuwashirikisha katika fursa hizo.

“Niwaombe watanzania kuendelea kujisajili katika kanzi data ya nguvu kazi ili tuweze kuwatambua, uwezo na changamoto zenu na kuwashirikisha katika miradi mbalimbali ukiwemo huu wa bomba la mafuta pamoja na kutatua changamoto hizo,” alisisitiza Beng’i

AWALI
Warsha ya mafunzo hayo imeratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa ufadhili wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) kupitia BEST Dialogue Tanzania kwa lengo la kuwezesha viongozi na Wafanyabiashara wa Mkoa huo kufahamu maendeleo na fursa zitakazotokana na mradi huo.Bomba hilo la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki lina urefu wa KM 1,443 kati ya hizo KM 296 zipo nchini Uganda na KM 1,147 zipo Tanzania

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MSALALA NA USHETU

0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya Ngaya wilayani Kahama, Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
6-3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wajasiriamali katika eneo la Bukondamoyo wakati akiwa njiani kuelekea Ushetu, Kahama mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
7
8-2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akwahutubia wananchi wa Ushetu katika uwanja wa Mikutano Nyamilongo wilayani Kahama, Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
4-4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Ezekiel Maige mara baada ya kuwasili kwenye kituo cha afya Ngaya wilayani Kahama, Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

Mkandarasi wa REA Mkoani Rukwa kukataliwa kuendelea na mradi.

0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesisitiza kukataliwa kuendelea na utekelezaji Mradi wa Mmeme Vijiji (REA) mkandarasi Nakuroi Investment kwa kushindwa kufikia hata nusu ya utekelezaji wa mradi huo hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu.

Mkandarasi huyo ambaye alitegemewa kutekeleza mradi huo katika vijiji 111 vya mkoa wa Rukwa tangu mwezi Novemba mwaka 2017 aliposaini mkataba na kumalizika mwezi June mwaka 2019 huku akiwa amekamilisha mradi katika vijiji 23 tu hadi kufikia februari mwaka 2019.

“itakapofika mwezi June huenda hata robo tutakuwa hatujafika, kwa hali hii niseme tu wazi huyu Mkandarasi Nakuroi Investment mimi naona uwezo wake ni mdogo lakini pia eneo amepewa ni kubwa sana huyu anashughulikia Mkoa mzima vijiji tulivyonavyo ni 339 mkoani kwetu, hap ani lazima wizara ifanye kitu, mi niseme tu wazi kuwa ikifika mwisho wa mkataba wake hatutamkubali tena kuendelea na mkataba mwingine, watuongezee wakandarasi, tunahitaji kupata umeme katika vijiji vyetu vyote kwa mujibu wa mkataba,” Mh. Wangabo Alisisitiza.

Kauli hiyo imetoka wakati wa majadiliano juu ya kusuasua kwa utekelezaji wa mradi REA katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichowashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa ambapo hoja hiyo iliwasilishwa kutoka katika maazimio ya kikao cha kamati ya ushari ya Wilaya ya Sumbawanga iliyowasilishwa katika kikao hicho.

Kwa upande wake Kaimu meneja wa TANESCO Mkoani Rukwa Gilles Daniel alikiri kusuasua kwa utekelezaji wa mradi huo huku akieleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ili kuhakikisha maagizo ya serikali yanatekelezwa kwa wakati na wananchi wote wanapata umeme ambao serikali imewaahidi.

Alisema kuwa changamoto kubwa imekuwa ni upatikanaji wa vifaa kwaajili ya mradi jambo lililosababishwa na uzalishaji mdogo wa vifaa hivyo kwenye viwanda vya ndani na pia kukosa ubora unaotarajiwa.

“umeme umewashwa katika vijiji 23 tu peke yake, ni kweli kwamba mradi unasuasua hatujaenda kwa kasi ile ambayo inatakiwa kwasababu ya changamoto nyingi ambazo zimetokea zinazosababisha mradi kusuasua lakini ni juzi tu waziri alitoa maagizo ya kuwashwa vijiji vitatu kwa kila Wilaya na utekelezaji umeanza na ndani ya siku mbili umeme utakuwa yumewashwa ndani ya vijiji vitatu kila wilaya,” alisema.

Akitetea hoja hiyo Mbunge wa Sumbawanga Mjini Mh. Aeshi Hilaly amesema kuwa si vyema kuwatwisha mzigo huo Shirika la Umeme na hivyo ni jukumu la waheshimiwa wabunge wa mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano kulichukua hilo na kulifikisha bungeni ili kulipatia ufumbuzi.

Matuta 212 yaliyopo barabara ya Tunduma - Sumbawanga yapatiwa ufumbuzi

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewashauri Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani Rukwa kukutana na madiwani pamoja na wenyeviti wa halmashauri zinazopitiwa na barabara ya Tunduma – Sumbawanga ili kuyabaini matuta yaliyowekwa maeneo ambayo hayana ulazima hivyo kutostahili kuendelea kuwepo kwenye barabara hiyo na hatimae kujiandaa kuyapunguza wakati wakiendelea kusubiri maamuzi ya Wizara.

Amesema kuwa endapo zoezi hilo litakuwa shirikishi halitazua mzozo baina ya TANROADS na wananchi pindi ajali zitakapoongezeka na kuwataka wabunge wa maeneo husika nao kukubaliana na maamuzi yatakayotolewa na wizara husika baada ya utambuzi huo wa matuta kufanyika.

“Kuna ukweli kwamba kuna baadhi ya Matuta hayastahili kuendelea kuwepo, matuta zaidi ya 200 lakini kuna baadhi yao yapo maeneo ambayo hayastahili kuwepo, mi nadhani kungefanyika utambuzi wa matuta ambayo sio ya lazima, halafu ndio hoja inakuwa kwamba kuna matuta Fulani ambayo sio ya lazima yapo katika maeneo Fulani ambayo hata waheshimiwa madiwani wa maeneo yale wameyaafiki kwasababu hii isiwe kazi ya TANROADS peke yao,”Alishauri.

Ameshauri hayo katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichowashirikisha Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Wakurugenzi wa halmashauri pamoja na Wenyeviti wa halmashsuri za Mkoa huo.

Ushauri huo umekuja baada ya mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini Mh. Aeshi Hilary kuilalamikia TANROADS kuhusu wingi wa matuta hayo na matokeo yake kuwakera wasafiri wanaotumia barabara hiyo jambo ambalo limekuwa likiwachosha wasafiri wanaotoka mikoa ya mbali na Mkoa wa Rukwa.

“Utakuta kuna matuta ambayo yanawekwa sehemu ambapo wala hayastahili, barabra hii ya Tunduma – Sumbawanga ina matuta zaidi ya 240 inazidi hata kilometa za barabara yenyewe, kuna tuta lipo katikati ya daraja, kwa mfano kuna Kijiji cha Tamasenga peke yake kina matuta kumi, kuna umuhimu gani wa kuyaweka yote hayo katika Kijiji kimoja, mlisema mtayaondoa lakini hapa kwenye bajeti yenu sioni kama mmelizungumzia,” Aliuliza.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS Mkoani Rukwa Mhandisi Masuka Mkina alibainisha kuwa uwepo wa matuta hayo umepunguza kwa kiasi kikubwa ajali za barabarani na kuongeza kuwa wafadhili waliowezesha ujenzi wa barabara hiyo kauli mbiu yao ilikuwa ni “Usalama Kwanza”.

“Alipokuja hapa Katibu Mkuu Nyamhanga nilizungumza lakini baadae akasema tuyaache kwanza, kwahiyo suala la matuta kwa sasa mimi sina la kuzungumza kwasababu serikali bado wanaendelea kulitafakari kwamba wayatoe au yabaki, kwasababu yamesaidia sana ukiangalia takwimu kwa barabara ya Tunduma - Sumbawanga ajali nikama sifuri,” Alisema.

Barabara ya Tunduma – Sumbawanga yenye kilometa 227 inakadiriwa kuwa na matuta 212 huku madatuta kadhaa yakiwa katikati ya madaraja na Kijiji cha Tamasenga kuwa na matuta 10 imefadhiliwa kwa msaada wa watu wa Marekani imesaidia kurahisisha safari ya Tunduma kwenda Sumbawanga ambapo hapo kabla wasafiri walitumia siku nzima.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo.
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images