Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI KAHAMA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi. (Picha na Ofisi ya Makamu Rais)
 Matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka kwa gharama ya shilingi blioni 24.72. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa Kagongwa, wilayani Kahama waliojitokeza kwa wingi kumsalimu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa Kagongwa, wilayani Kahama waliojitokeza kwa wingi kumsalimu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna mazingira yatakavyoachwa mara baada ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kufungwa kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Ufungaji Mgodi Bi. Rebecca Stephen.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari wakicheza ngoma wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye aliweka jiwe la msingi la ufunguzi wa madarasa la mradi wa TEA na P4R. Mkamu wa Rais yupo wilayani Kahama kwa ziara yenye lengo la kuhamasisha na kukagua shughuli za maendeleo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Bodi ya Wadhamini ya Taasisi JKCI yaridhishwa na huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo

$
0
0
Kuongezeka wa idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa vipimo na uzibuaji wa mishipa ya damu ya moyo ambayo imeziba kupitia  mtambo wa Cathlab ni ishara kuwa watu wengi wanahitaji kupata huduma hiyo.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akisoma ripoti ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya Oktoba hadi Desemba kwa bodi ya Wadhamini.

Prof. Janabi alisema tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo mwaka 2016 hadi 2018 katika mtambo wa Cathlab wameona zaidi  ya wagonjwa 2389 ambao waliwafanyiwa vipimo na kuwazibua  mishipa ya damu ya moyo iliyokuwa  imeziba.

“Kupitia mtambo huu tunafanya upasuaji wa moyo wa  bila kufungua kifua kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja.  Kwa mwaka jana pekee tulifanya upasuaji kwa wagonjwa 1056 na kuvunja rekodi katika nchi za Afrika Mashariki na Kati”, alisema Prof. Janabi.

Alisema hivi sasa madaktari wa magonjwa ya moyo kwa watoto kupitia mtambo huo wa Cathlab  wameanza  kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu iliyoziba.

“Kipindi cha nyuma watoto walikuwa wanafanyiwa upasuaji huu na madaktari wageni hii ilitokana na kutokuwa na daktari wa kutoa huduma hiyo katika Taasisi yetu. Mwaka jana daktari wetu mmoja aliyekuwa anasoma Afrika ya Kusini amerudi baada ya kumaliza masomo yake na anafanya upasuaji siku ya Jumatano”,.

“Tumetenga siku moja kwa wiki ambayo ni jumatano watoto wanafanyiwa upasuaji wa kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu iliyoziba, uhitaji ni mkubwa na mtambo uliopo ni mmoja. Kuna haja ya kuwa na mtambo mwingine wa Cathlab ili wagonjwa wengi wenye uhitaji wa huduma hii waweze kuipata”, alisema Prof. Janabi.

Katika hatua nyingine Prof. Janabi alisema mwezi wa sita mwaka huu Madaktari Afrika kutoka nchini Marekani watakuja nchini kupanda  mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangia fedha za matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Prof. William Mahalu aliipongeza menejimenti na wafanyakazi wote wa Taasisi hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma ya matibabu ya magonjwa ya moyo.

Prof. Mahalu ambaye pia ni daktari bingwa wa upasuaji wa  moyo na mishipa ya damu alisema kufanya vizuri kwa mtambo wa Cathlab kunaonesha kuwa watu wengi  wanahitaji huduma hiyo na wao  kama bodi wameona  kunahaja ya kuongeza mtambo wa pili wa Cathlab ili wagonjwa wengi wapate huduma hiyo.

“Mmetuambia hivi karibuni mmesaini mkataba wa makubaliano ya  kuletwa kwa wagonjwa kutoka nchi ya Malawi na Visiwa vya Zanzibar kwa ajili ya matibabu, hongereni sana. Endeleeni kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili watu wengi zaidi wafaidike na huduma mnayoitoa”, alisema Prof. Mahalu.

Alisema miaka minne au mitano ijayo wataalamu kutoka nje ya nchi  wanaokuja  kufanya kambi maalum za matibabu ya moyo watakuja nchini kujifunza  kutoka kwa watanzania  baada ya wao kuja kutoa msaada.

Prof. Mahalu alimalizia kwa kuwataka wataalamu wa magonjwa ya moyo kufuatilia maendeleo ya  wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo pindi wanaporuhusiwa kurudi nyumbani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu akizungumza jambo na wafanyakazi wa maabara alipotembelea maabara hiyo kwa ajili ya kuangalia mashine mpya za uchunguzi wa vipimo vya magonjwa ya moyo zilizofungwa. Watatu kulia kutoka kwa Prof. Mahalu ni mjumbe wa bodi Dkt. Donan Mbando.
Watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa wanacheza gemu kama walivyokutwa  na mpiga picha wetu. Watoto wawili kati yao wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua  na wawili wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu na mjumbe wa bodi hiyo Dkt. Donan Mbando wakitoka kuangalia wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo ambayo imejengwa na kufanyiwa ukarabati.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu na mjumbe wa bodi hiyo Dkt. Donan Mbando wakiangalia chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) kilichopo katika wodi  mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo ambayo imejengwa na kufanyiwa ukarabati. Chumba hicho kikianza kufanya kazi kitakuwa na vitanda nane na kuweza kurahisisha kutoa huduma kwa watoto wanaohitaji matibabu  ya dharula.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu akiangalia (medical gas bed head panel) mahali pa kuchomeka mashine ya kutolewa hewa ya matibabu  kwenda kwa mgonjwa  katika wodi mpya ya kulipia ya watoto wenye magonjwa ya moyo ambayo imejengwa na kufanyiwa ukarabati. 
Picha na JKCI

MASHINDANO YA BAMMATA SOKA JKT WAAGA KWA KISHINDO

$
0
0

Nahodha wa Kanda ya Magereza Sajini Tausi Abdul akipambana na Private Ester Lisu wa Ngome wakati wa Mchezo wao katika Michauano ya BAMMATA kuwania nafasi ya pili katika Mchezo huo Ngome ilishinda Magereza vikapu 68 kwa 60 . Picha na Luteni Selemani Semunyu.

Mchezaji wa Kanda ya Magereza Sajini Mary Kimiti akipambana na Private Ester Lisu wa Ngome wakati wa Mchezo wao katika Michauano ya BAMMATA kuwania nafasi ya pili katika Mchezo huo Ngome ilishinda Magereza vikapu 68 kwa 60 . Picha na Luteni Selemani Semunyu.

Wachezaji wa Mpira wa Wavu kutoka Magereza na JKT wakichuana wakatika wa Michuano ya Majeshi BAMMATA katika Mchezo huo Magereza walishinda Seti tatu kwa moja Picha na Luteni Selemani Sem unyu.

Na Luteni Selemani Semunyu

Mashindano ya Majeshi Tanzania BAMMATA yameendelea kushika kasi huku timu ya Soka ya JKT ikiaga mashindano hayo kwa mwaka 2019 kwa kishindo baada ya kuifunga Zimamoto magoli 10 kwa Moja.

Matokeo hayo yamejitokeza katika mchezo wa kufunga Dimba uliochezwa katika Dimba la Uhuru licha ya Timu hizo zote hazikuwa na nafasi ya kuingia katika Hatua ya Nusu Fainali.

Katika Soka sasa Mchezo kati ya Ngome na Magereza unaotarajiwa kuchezwa kesho katika Dimba la Uhuru utaamua nani wa kucheza na Polisi na nani kucheza na SMZ katika hatua ya Nusu Fainali.

Katika Ridha atika mchezo mwingine Mpira wa Kikapu Wanawake mchezo uliokuwa ukiamua mcshindi wa Pili Ngome wameibuka na Ushindi kwa Vikapu 68 kwa 60. Katika Mpira wa Wavu wanawake Magereza wameifunga JKT kwa seti tatu kwa Moja huku kwa Upande wa Wanaume Ngome wameifunga Polisi Seti tatu bila.

Katika Shabaha pistor wanawake mshindi wa Kwanza Pc Pili Mkama wa pili PC Salvina Mhiche na PC Bertha Jonathan wote wa Polisi.

Kwa Upande wa Wanaume Sajini Kenya Kiula wa Polisi wa pili ni Sajini Jumanne Wambura wa Ngome na watatu ni PC Joseph Mwenda Polisi.

Kwa Upande wa Rifle Wanawake ni Private Elizabeth Kibondo Ngome wa pili ni Mteule Daraja la Pili Sophia Ramadhani wa Ngome na PC Sharifa Kibwana Ally wa Polisi huku kwenye Riadha relay wanaume Mita 400 Timu ya Ngome imeibuka na Ushindi.

HATIMAYE EDWARD LOWASSA ARUDI CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM,Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Mh.Edward Lowassa mara baada ya kutangaza kurejea CCM leo kwenye ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijin Dar.

*Mwenyewe asema ametafakari na kuamua kurudi nyumbani

*Rais Dk. Magufuli atoa neno, CCM wachekelea kila kona

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZIRI Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Edward Lowassa ametangaza rasmi kurudi Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuanzia leo Machi 1,2019.

Lowassa aliondoka CCM na kwenda upinzani katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wakati wa mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.Aliondoka CCM na kwenda upinzani baada ya jina lake kukatwa katika kugombea urais kupitia Chama hicho.

Hivyo  alipata ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais kupitia Chadema waliokuwa wameunganisha nguvu na vyama vingine vinne vya siasa vilivyokuwa vimeunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Akiwa upinzani Lowassa aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema lakini kuna kipindi aliamua kwenda Ikulu kufanya mazungumzo na Rais Dk.Magufuli ambapo baada ya kukutana na Rais alisema amevutiwa na utendaji kazi wake na anampongeza.

Akizungumza leo katika Ofisi za ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam,Lowassa hakuwa na maneno mengi ya kueleza zaidi ya kuwaambia Watanzania kuwa ameamua kurudi nyumbani (CCM).

"Nimetafakari na sasa nimeamua kurudi nyumbani CCM ambako sehemu kubwa ya maisha yangu nimekuwa huko,"amesema Lowassa huku mamia ya wananchi wakiwamo wanachama na wapenzi wa CCM walikuwa wanamshangilia.

Wakati Lowassa anatangaza kurejea CCM alikuwa amesikindikizwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga ambaye pia aliwahi kuwa Mtunza wa fedha wa CCM Rostam Aziz.

Akizungumza baada ya Lowassa kurudi CCM, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli amesema wamempokea Lowassa na katika kuthibitisha hilo waliona ni vema uamuzi wake akautangazia Ofisi za CCM Lumumba kama sehemu ya uthibitisho.

"Kama ambavyo amezungumza kwa kifupi mwenye Mzee Lowassa kwamba amerudi nyumbani ambako ni huku CCM, tumempokea.Amekuja kutangazia hapa Lumumba kama sehemu ya kutoa shuhuda.

"Kwa upande wetu tumekaa, tumefakari na kujiridhisha Lowassa amekaa kwenye Chama kwa muda mrefu na kwa bahati mbaya zilizojotokeza aliamua kwenda upinanzani.Tumemsikiliza mawazo yake kwamba amekaaa kwenye Chama Cha Mapinduzi sehemu kubwa ya maisha yake na kwamba kutokana na sababu ambazo amezieleza aliamua kwenda upinzani na leo hii amerudi nyumbani,"amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo kabla ya Rais Magufuli kuzungumza aliamua kuwatania watu waliokuwa wamejitokeza Lumumba na kuwaambia imekuaje wako hapo au wanamaono na hivyo walijua kitakachotokea.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Ally amesema Lowassa amefikia uamuzi wa busara kwa kurudi nyumbani kwa ajili ya kushirikiana katika kuleta maendeleo ya wananchi wote.

"Amerudi nyumbani, kwa hiyo tunaanza kazi ya kujenga Taifa letu na kujenga utu wetu, Lowassa ni kiongozi ambaye ametoa mchango mkubwa katika nchi yetu.Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama chetu tumepanga kumpokea na yupo tayari kushirikiana nasi kuwatumikia wananchi,"amesema Dk.Bashiru.

Hata hivyo uamuzi  huo wa Lowassa umeonekana kuwakosha wana-CCM kwani baadhi yao wameonesha kufurahia uamuzi huo.

Waziri Mwakyembe afanya mazungumzo na Amnesty International kuhusu Sekta ya Habari

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (Kushoto ) akizungumza  leo ofisini kwake Jijini Dodoma na Mwakilishi na Mchambuzi wa Sera kutoka Amnesty International Bibi Joan Nyanyuki  kuhusu Sekta ya Habari hususani Wajibu wa vyombo vya Habari nchini kuandika na kusambaza habari zenye ukweli.
 Mwakilishi na Mchambuzi wa Sera  kutoka Amnesty International Bibi Joan  Nyanyuki (Kulia) akizungumza leo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe ofisini kwa Mhe.Waziri Jijini Dodoma  kuhusu Sekta ya Habari hususan Wajibu wa vyombo vya Habari nchini kuandika na kusambaza habari zenye ukweli.
Mchambuzi wa Sera kutoka Amnesty International  Bw.Roland Ebole (Kulia) akizungumza leo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati)  kuhusu Sekta ya Habari hususan Wajibu wa vyombo vya Habari nchini kuandika na kusambaza habari zenye ukweli ofisini kwa Mhe.Waziri Jijini Dodoma.  Kulia ni Mwakilishi na Mchambuzi wa Sera kutoka Amnesty International Bibi Joan Nyanyuki

MKUTANO WA 11 WAKUTATHMINI SEKTA YA AFYA WAFUNGWA ZANZIBAR

$
0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ zitaendelea kujenga Nyumba za kuishi Wahudumu wa afya katika kila eneo lenye Kituo cha Afya ili kuhakikisha wahudumu hao wanapatikana muda wote hasa maeneo ya Vijijini.

Kwa kufanya hivyo kutapunguza kasi ya wahudumu hao kukimbilia kufanyakazi Mijini na kuviacha vituo vya Afya vya Vijijini bila wahudumu. Hayo yameelezwa katika Mkutano wa 11 wa kutathmini maendeleo ya sekta ya Afya kwa mwaka 2017/2018 ikiwa ni mapendekezo yaliyotolewa na washiriki wa mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa Hotel ya VERDE, nje kidogo ya mjini Zanzibar.

Katibu wa Wizara ya Afya Asha Ali Abdulla amesema mkutano huo umekuwa wa mafanikio makubwa kutokana na kujadili mambo muhimu na mapendekezo ya kuimarisha huduma ya afya kwa mwaka 2019/2020. Amesema katika kukabiliana na changamoto ya maradhi yasiyoambukiza ikiwemo Maradhi ya Miguu, Mgongo ambayo yamekuwa yakiwasumbua wananchi wengi wa Zanzibar Katibu huo amesema mkutano umependekeza kufanya tafiti mbali mbali kubaini chanzo cha maradhi hayo.

Hata hivyo amesisitiza kutolewa kwa elimu ya afya kuhusu maradhi mbali mbali kama vile Shinikizo la Damu, Kisukari na Saratani ili wananchi waweze kubadili mifumo yao ya maisha ambayo huchangia ongezeko la maradhi hayo. Amesema njia muhimu ni kuhakikisha wananchi wanakula vyakula salama na kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuiepusha miili yao na kitisho cha maradhi hayo.

Kwa upande wake Atie Juma Shaame Mkurugenzi wa Mipango sera na utafiti Wizara ya Afya amesema licha ya huduma kutolewa bure Serikali itaendelea kuimarisha huduma hiyo kwa kiwango cha juu kabisa. Amesema kwa upande wa Serikali kupitia Wizara ya Fedha imeahidia kushirikiana na Wizara hiyo pamoja na washirika wa maendeleo ili kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi Zanzibar Amina Abdulqadir amesema mkutano huo umekuwa na mafanikio makubwa hasa kutokana na kushirikisha wadau wote kutoka Serikalini na Taasisi binafsi ambao michango yao ilikuwa muhimu.

Amesema Sera ya ugatuzi itasaidia kwa kiasi kikubwa kupatikana wauguzi watakaokidhi haja ya kila eneo na kusisitiza serikali kutoa elimu kwa wananchi kufahamu maana halisi ya ugatuzi.

"Ugatuzi kwa kweli umesaidia sana kupeleka madaraka mikoani kubwa linalohitajika ni kuhakikisha kuwa Wananchi wanapatiwa elimu wajue hasa maana ya Ugatuzi ili waweze kutoa ushirikiano ipasavyo" alisema Mwenyekiti Amina

Amesema akiwa Mwenyekiti wa Wauguzi jukumu lake ni pamoja na kuwakumbusha wenzake kutumia lugha nzuri wakati wanapowahudumia wagonjwa.

kila inapofika kipindi cha uandaaji wa Bajeti mpya Wizara ya Afya huwaita wadau wake wote kujadili namna ya kuimarisha sketa hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Kwa takriban miaka 15 sasa Wizara ya afya imekuwa ikifanya mikutano ya kutathmini matokeo ya utekelezaji wa kipindi cha mwaka mmoja ambapo mwaka huu mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na washiriki zaidi ya 120 kutoka sekta binafsi, Washirika wa maendeleo wakiwemo WHO, UNICEF, UNFPA, UNDP, ujumbe wa mwaka huu ‘‘Kuimarisha ushikiriano kwa lengo la kuinua huduma za Afya bora kwa wote ’’
 Mkuu wa Idara ya Maradhi ya Kina mama na Uzazi Hospitali ya Mnazi Mmoja Dkt,Ummulkulthum Omar akiwasilisha mada kuhusu Uzazi katika ufungaji wa  Mkutano wa 11 wakutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
 Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Afya waliohudhuria katika ufungaji wa  Mkutano wa 11 wakutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
 Mkurugenzi Utawala na Uwendeshaji Hospitali ya Mnazi Mmoja Abubakar Khamis Hamad akiuliza maswali katika mkutano wa 11 wakutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
 Daktari Bingwa wa maradhi ya akina mama Hospitali ya Mnazi mmoja Hamed Mahfudh akifafanua baadhi ya maswali yalioulizwa katika ufungaji wa  Mkutano wa 11 wakutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdulla akitoa hotuba ya ufungaji wa Mkutano wa 11 wakutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

HIVI NDIVYO RUGE MUTAHABA ALIVYOPOKELEWA LEO JIJINI DAR,SIMANZI ZATAWALA KILA KONA

MAELFU YA WANANCHI DAR WAJIPANGA BARABARANI KUTOA HESHIMA KWA RUGE

$
0
0
*Wapo waliamua kushika gari iliyobeba mwili wake

*...Kwe heri Ruge...nenda kaka,...mbela yako, nyuma yetu

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAELFU ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kushuhudia mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Ukweli ni kwamba mwili wa Ruge kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameupokea kwa heshima kubwa na hiyo inaonesha namna alivyokuwa kwenye mioyo ya watu.

Mwili wa Ruge uliwasili nchini saa tisa Alasiri ukitokea Afrika Kusini ambako kabla ya kuanza safari ukiwa uwanjani hapo uliwekwa kwenye gari ndogo yenye rangi nyeusi.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa jijini Dar es Salaam mamia ya wananchi walianza kujipanga kuanzia uwanjani hapo.Aliyeongoza mapokezi ya mwili wa Ruge ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu ya Rais-Muungano na Mazingira.

Mwili wa marehemu Ruge baada ya kutoka Uwanja wa Ndege ulipita Barabara ya Uhuru, Karume ,Magomeni ,Morocco Hotel,Sinza Kijiweni. Bagama, ITV, Clouds ,Kawe na kisha Lugalo.

Michuzi Blog na Michuzi TV waliokuwa kwenye msafara huo walishuhudia mamia ya watu wakiwa barabarani wakisuburi kuona jeneza lililobeba mwili wa Ruge.

Baadhi ya watu walishindwa kujizuia kiasi cha baadhi yao kuamua kwenda kushika gari iliyobeba mwili wa marehemu Ruge ambaye hakika amethibitisha kuwa alikuwa yupo kwenye mioyo ya Watanzania.

 Kutokana na idadi kubwa ya watu iliyojitokeza barabarani, ilisababisha msafara huo kusimama mara kwa mara.Waendesha bodaboda nao walioekana kutokuwa nyuma kwani nao waliamua kuungana na magari yaliyokuwa kwenye msafara huo.

Wakati mwili wa Ruge unapita katika baadhi ya barabara wapo wananchi ambao walikuwa wakisikika wakisema hivi "Nenda Ruge...nenda kaka,...hakika sote ni wa mwenyezi Mungu... nenda Ruge mbele yako , nyuma yetu.

Ukweli ni kwamba kadri msafara wa Ruge ulivyokuwa unaendelea kwenda ndivyo ambavyo idadi ya watu ambavyo ilikuwa inaongeza, kiasi cha cha kufanya gari ambayo imebeba msafara huo kupunguza mwendo na kwenda taratibu.

 Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliamua kutoa maelekezo ya kuhakikisha wananchi waliokuwa barabarani wanapata nafasi ya kuona vizuri jeneza ambalo lilikuwa limebeba mwili huo.

Hata hivyo, aliamua kutoa maagizo ya kuwataka waendesha bodaboda kukaa nyuma ya gari iliyobeba mwili kwani kabla ya kutoa maelekezo hayo , waendesha bodaboda walikuwa wametangalia mbele na kufanya msafara kushindwa kwenda kwa utaratibu mzuri na kutoa nafasi ya wengine kuuona.

Hata hivyo wakati wananchi wengi wakiwa barabarani, kuna wengine ambao wao waliamua kwenda kuusubiri mwili wa Ruge katika Kituo cha Redio cha Clouds.Kwa mujibu wa ratiba mwili wa Ruge kabla ya kwenda Lugalo ulipitishwa katika eneo hilo ambalo ni ofisi zake alizokuwa anafanya kazi enzi za uhai wake.

Sababu za kuupeleka mwili huo Clouds ilikuwa ni kutoa nafasi kwa wafanyakazi wenzake kupata nafasi ya kuona jeneza lililobeba mwili wake.

Mwisho

Hata hivyo msafara wa mwili wa Ruge bado unaendelea na Michuzi Blog itaendelea kukufahamisha hatua kwa hatua.

TASWIRA ZA EDWARD LOWASSA ALIPOREJEA CHAMA CHA MAPINDUZI

$
0
0

*Mwenyewe asema ametafakari na kuamua kurudi nyumbani

*Rais Dk. Magufuli atoa neno, CCM wachekelea kila kona

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

WAZIRI Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Edward Lowassa ametangaza rasmi kurudi Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuanzia leo Machi 1,2019. 
Lowassa aliondoka CCM na kwenda upinzani katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wakati wa mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.Aliondoka CCM na kwenda upinzani baada ya jina lake kukatwa katika kugombea urais kupitia Chama hicho.

Hivyo  alipata ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais kupitia Chadema waliokuwa wameunganisha nguvu na vyama vingine vinne vya siasa vilivyokuwa vimeunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Akiwa upinzani Lowassa aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema lakini kuna kipindi aliamua kwenda Ikulu kufanya mazungumzo na Rais Dk.Magufuli ambapo baada ya kukutana na Rais alisema amevutiwa na utendaji kazi wake na anampongeza.

Akizungumza leo katika Ofisi za ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam,Lowassa hakuwa na maneno mengi ya kueleza zaidi ya kuwaambia Watanzania kuwa ameamua kurudi nyumbani (CCM).

"Nimetafakari na sasa nimeamua kurudi nyumbani CCM ambako sehemu kubwa ya maisha yangu nimekuwa huko,"amesema Lowassa huku mamia ya wananchi wakiwamo wanachama na wapenzi wa CCM walikuwa wanamshangilia.

Wakati Lowassa anatangaza kurejea CCM alikuwa amesikindikizwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga ambaye pia aliwahi kuwa Mtunza wa fedha wa CCM Rostam Aziz.

Akizungumza baada ya Lowassa kurudi CCM, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli amesema wamempokea Lowassa na katika kuthibitisha hilo waliona ni vema uamuzi wake akautangazia Ofisi za CCM Lumumba kama sehemu ya uthibitisho.

"Kama ambavyo amezungumza kwa kifupi mwenye Mzee Lowassa kwamba amerudi nyumbani ambako ni huku CCM, tumempokea.Amekuja kutangazia hapa Lumumba kama sehemu ya kutoa shuhuda.

"Kwa upande wetu tumekaa, tumefakari na kujiridhisha Lowassa amekaa kwenye Chama kwa muda mrefu na kwa bahati mbaya zilizojotokeza aliamua kwenda upinanzani.Tumemsikiliza mawazo yake kwamba amekaaa kwenye Chama Cha Mapinduzi sehemu kubwa ya maisha yake na kwamba kutokana na sababu ambazo amezieleza aliamua kwenda upinzani na leo hii amerudi nyumbani,"amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo kabla ya Rais Magufuli kuzungumza aliamua kuwatania watu waliokuwa wamejitokeza Lumumba na kuwaambia imekuaje wako hapo au wanamaono na hivyo walijua kitakachotokea.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Ally amesema Lowassa amefikia uamuzi wa busara kwa kurudi nyumbani kwa ajili ya kushirikiana katika kuleta maendeleo ya wananchi wote.

"Amerudi nyumbani, kwa hiyo tunaanza kazi ya kujenga Taifa letu na kujenga utu wetu, Lowassa ni kiongozi ambaye ametoa mchango mkubwa katika nchi yetu.Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama chetu tumepanga kumpokea na yupo tayari kushirikiana nasi kuwatumikia wananchi,"amesema Dk.Bashiru.
Hata hivyo uamuzi  huo wa Lowassa umeonekana kuwakosha wana-CCM kwani baadhi yao wameonesha kufurahia uamuzi huo.

WAZIRI Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa akiwasili Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019 
Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally akimpokea Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa aliyeongozana na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho walipowasili Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli  na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally wakimwangalia Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa akiweka sahihi kweny kitabu cha wageni akiwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho walipowasili Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli  akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally wakiongea na Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa  na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho walipowasili Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019 

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli  akimpeleka ofisini kwake Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa  alipowasili  Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli  akifurahia wakati Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa  na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz wakisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika  Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli  akifurahia jambo wakati wa maongezi na Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa  na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika  Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli  akiongea  jambo  na Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa  wakati wakitoka nje wakuwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika  Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli  akimsikiliza Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa  wakati akitangazia umma rasmi kwamba anarudi nyumbani  akiwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika  Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019 

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli  akiongea baada ya Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa  kuutangazia umma rasmi kwamba anarudi nyumbani  akiwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika  Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli  akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa  baada ya kuutangazia umma rasmi kwamba anarudi nyumbani  akiwa na aliyekuwa Mbunge wa Igunga na mweka hazina wa cha hicho Ndg. Rostam Aziz, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika  Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019 

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli  akiagana na Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Edward Lowassa  baada ya kuutangazia umma rasmi kwamba anarudi nyumbani  akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika  Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Ijumaa March 1, 2019. 

WATOTO WASIORIPOTI SHULE NA WAZAZI WAO KUFIKISHWA MAHAKAMANI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera akizungumza katika kikao cha tathimini ya elimu ambapo ameagiza kufikishwa mahakamani kwa watoto wasioripoti shule na wazazi wenye watoto ambao hadi sasa bado wako majumbani.
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera wa pili kulia,akiongoza kuimba wimba wa Taifa kabla ya kuanza kwa kikoa cha tahimini hya elimu katika wilaya hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Klasta mjini Tunduru kulia ni mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Gaspar Balyomi.

 Baadhi ya wadau wa elimu wa wilaya ya Tunduru wakimsikiliza mkuu wa wilaya hiyo Juma Homera wakati wa kikao cha tathimini ya elimu ambapo hadi kufikia tarehe 28 Februari jumla ya watoto 1239 kati ya 4195 waliochaguliwa kuanza masomo kwa mwaka 2019 hawajaripoti shule.
 Afisa elimu ya msingi wa wilaya ya Tunduru Anderson Mwalongo akitoa taarifa ya hali ya elimu katika kikao cha tathimini ya elimu katika wilaya hiyo katika ukumbi wa Klasta mjini Tunduru.

UJENZI JENGO LA TATU LA ABIRIA JNIA WAFIKIA ASILIMIA 95

WIZARA YAKUTANA NA MSANII SHETTA KUJADILI ANDIKO LA KAMPENI YA KIKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

Bodi ya Wadhamini ya Taasisi JKCI yaridhishwa na huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu akizungumza jambo na wafanyakazi wa maabara alipotembelea maabara hiyo kwa ajili ya kuangalia mashine mpya za uchunguzi wa vipimo vya magonjwa ya moyo zilizofungwa. Watatu kulia kutoka kwa Prof. Mahalu ni mjumbe wa bodi Dkt. Donan Mbando.
Watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa wanacheza gemu kama walivyokutwa  na mpiga picha wetu. Watoto wawili kati yao wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua  na wawili wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu na mjumbe wa bodi hiyo Dkt. Donan Mbando wakitoka kuangalia wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo ambayo imejengwa na kufanyiwa ukarabati.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu na mjumbe wa bodi hiyo Dkt. Donan Mbando wakiangalia chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) kilichopo katika wodi  mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo ambayo imejengwa na kufanyiwa ukarabati. Chumba hicho kikianza kufanya kazi kitakuwa na vitanda nane na kuweza kurahisisha kutoa huduma kwa watoto wanaohitaji matibabu  ya dharula.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu akiangalia (medical gas bed head panel) mahali pa kuchomeka mashine ya kutolewa hewa ya matibabu  kwenda kwa mgonjwa  katika wodi mpya ya kulipia ya watoto wenye magonjwa ya moyo ambayo imejengwa na kufanyiwa ukarabati. 
Picha na JKCI
Kuongezeka wa idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa vipimo na uzibuaji wa mishipa ya damu ya moyo ambayo imeziba kupitia  mtambo wa Cathlab ni ishara kuwa watu wengi wanahitaji kupata huduma hiyo.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akisoma ripoti ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya Oktoba hadi Desemba kwa bodi ya Wadhamini.

Prof. Janabi alisema tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo mwaka 2016 hadi 2018 katika mtambo wa Cathlab wameona zaidi  ya wagonjwa 2389 ambao waliwafanyiwa vipimo na kuwazibua  mishipa ya damu ya moyo iliyokuwa  imeziba.

“Kupitia mtambo huu tunafanya upasuaji wa moyo wa  bila kufungua kifua kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja.  Kwa mwaka jana pekee tulifanya upasuaji kwa wagonjwa 1056 na kuvunja rekodi katika nchi za Afrika Mashariki na Kati”, alisema Prof. Janabi.

Alisema hivi sasa madaktari wa magonjwa ya moyo kwa watoto kupitia mtambo huo wa Cathlab  wameanza  kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu iliyoziba.

“Kipindi cha nyuma watoto walikuwa wanafanyiwa upasuaji huu na madaktari wageni hii ilitokana na kutokuwa na daktari wa kutoa huduma hiyo katika Taasisi yetu. Mwaka jana daktari wetu mmoja aliyekuwa anasoma Afrika ya Kusini amerudi baada ya kumaliza masomo yake na anafanya upasuaji siku ya Jumatano”,.

“Tumetenga siku moja kwa wiki ambayo ni jumatano watoto wanafanyiwa upasuaji wa kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu iliyoziba, uhitaji ni mkubwa na mtambo uliopo ni mmoja. Kuna haja ya kuwa na mtambo mwingine wa Cathlab ili wagonjwa wengi wenye uhitaji wa huduma hii waweze kuipata”, alisema Prof. Janabi.

Katika hatua nyingine Prof. Janabi alisema mwezi wa sita mwaka huu Madaktari Afrika kutoka nchini Marekani watakuja nchini kupanda  mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangia fedha za matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Prof. William Mahalu aliipongeza menejimenti na wafanyakazi wote wa Taasisi hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma ya matibabu ya magonjwa ya moyo.

Prof. Mahalu ambaye pia ni daktari bingwa wa upasuaji wa  moyo na mishipa ya damu alisema kufanya vizuri kwa mtambo wa Cathlab kunaonesha kuwa watu wengi  wanahitaji huduma hiyo na wao  kama bodi wameona  kunahaja ya kuongeza mtambo wa pili wa Cathlab ili wagonjwa wengi wapate huduma hiyo.

“Mmetuambia hivi karibuni mmesaini mkataba wa makubaliano ya  kuletwa kwa wagonjwa kutoka nchi ya Malawi na Visiwa vya Zanzibar kwa ajili ya matibabu, hongereni sana. Endeleeni kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili watu wengi zaidi wafaidike na huduma mnayoitoa”, alisema Prof. Mahalu.

Alisema miaka minne au mitano ijayo wataalamu kutoka nje ya nchi  wanaokuja  kufanya kambi maalum za matibabu ya moyo watakuja nchini kujifunza  kutoka kwa watanzania  baada ya wao kuja kutoa msaada.

Prof. Mahalu alimalizia kwa kuwataka wataalamu wa magonjwa ya moyo kufuatilia maendeleo ya  wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo pindi wanaporuhusiwa kurudi nyumbani.

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI KAHAMA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi. (Picha na Ofisi ya Makamu Rais)
 Matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka kwa gharama ya shilingi blioni 24.72. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa Kagongwa, wilayani Kahama waliojitokeza kwa wingi kumsalimu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa Kagongwa, wilayani Kahama waliojitokeza kwa wingi kumsalimu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna mazingira yatakavyoachwa mara baada ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kufungwa kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Ufungaji Mgodi Bi. Rebecca Stephen.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari wakicheza ngoma wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye aliweka jiwe la msingi la ufunguzi wa madarasa la mradi wa TEA na P4R. Mkamu wa Rais yupo wilayani Kahama kwa ziara yenye lengo la kuhamasisha na kukagua shughuli za maendeleo.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

UGANDA HANDS OVER CHAIRMANSHIP OF THE JOINT REGIONAL POLICY STEERING COMMITTEE MEETINGS FOR LAKE VICTORIA BASIN TO RWANDA

$
0
0

LAKE VICTORIA BASIC COMMISSION

Lake Victoria Basin Commission Secretariat, Kisumu, Kenya,1 March, 2019: The Republic of Uganda, which has been chairing the Joint Regional Policy Steering Committee Meetings (JRPSC) for Lake Victoria Basin, has handed over the chairmanship to the Republic of Rwanda on February, 28th 2019 in Kisumu, Kenya.

Handing the instruments of chairmanship, Alfred Okot Okidi the Permanent Secretary, Ministry of Water and   Environment, Republic of Uganda outlined to participating delegates to JRPSC, the key achievements registered during his chairmanship. These included, but not limited to, successful completion of two mega flagship projects—Lake Victoria Water Sanitation Project phase two (LVWATSAN II) and Lake Victoria Environmental Management Project (LVEMP II).

The two regional projects have been coordinated by Lake Victoria Basin Commission (LVBC) and implemented by five East African Community Partner States. Reports from LVBC indicate that the two projects registered tangible outcomes at community levels through improved livelihoods and environmental conservation in East African Community Partner States. 

Acknowledging challenges still hampering the Lake Victoria Basin, the outgoing chairperson of the JRPSC observed that consensus and moving forward with a purpose would contribute in advancing East Africa Community integration agenda through programmes and projects.

The incoming chairperson, Fatina Mukarubibi, the Permanent Secretary, Ministry of Environment Republic of Rwanda commended the good leadership of the outgoing chairperson and committed to keep the pace set by members of JRPSC and LVBC—the latter is the implementer of the decisions and directives of the former.

Mukarubibi called for adoption of innovation, effective regional coordination and working extra harder by EAC Partner States as a way of unlocking existent development challenges—climate change, water hyacinth, among others.  “On climate change, we need to embrace climate adaptation measures in our long term development plans and work together,” Fatina Mukarubibi, the chairperson of RJPSC said.

 LVBC Executive Secretary, Dr. Ally-Said Matano also applauded the able leadership of the outgoing chairperson and congratulated the in-coming chairperson for assuming new responsibilities of steering the policy-making forum (JRPSC) for programmes and projects in the Lake Victoria.  

Dr. Matano expressed gratitude for the policy and strategic support from Principal and Permanent Secretaries and Ministers of the East Africa Community Partner States to the Lake Victoria Basin Commission. He lauded the ongoing support from development partners, specifically, World Bank, African Development Bank, KfW, EU, and USAID among others.

LVBC Executive Secretary cited Lake Victoria Bill as one of the legal and policy instruments which if enacted into law by the EALA Members of Parliament will reinforce LVBC’s resource mobilization efforts.  

The host of JRPSC, Ali Noor, the Principal Secretary for Environment and Forestry, Republic of Kenya welcomed delegates to one of Kenya’s Lake Cities, Kisumu.

He commended LVBC’s use of common approaches in sustainable management of shared resources in the five EAC Partner States. He urged delegates to generate recommendations aimed at realizing the shared vision of Lake Victoria Basin.

The Kenya’s representative called for delegates to observe one minute of silence in remembrance of marine victims from two sister EAC countries—Republic of Uganda and the United Republic of Tanzania.

The 8th JRPSC considered, among other things, the status of implementation of the recommendations and decisions of the previous JRPSC for Lake Victoria Basin held in April 2018 in Entebbe Uganda and other subsequent policy related meetings.

The JRPSC meeting also considered the progress reports for projects and programmes. Other pertinent issues on agenda included, but are not limited to, LVBC Resource Mobilization Initiatives—Pipeline projects and programmes.

SINA MENGI YA KUSEMA, NIMERUDI NYUMBANI - EDWARD LOWASSA

NENDA SALAMA RUGE: THT NA MRISHO MPOTO

WAZIRI MHAGAMA AHIMIZA JAMII KUPIMA VVU

$
0
0
JAMII imeshauriwa kupima afya zao mara kwa mara ili kubaini kama wana maambukizi ya VVU ili kupata huduma mapema na kuchukua hatua muhimu ya kunendelea kulinda afya za wasio na maambukizi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama alipokuwa akizindua kituo cha kutolea huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara Machi1, 2019. 

Waziri Mhagama aliwahimiza wananchi kupima VVU  ili kufanikisha mpango wa 90 tatu na kutoa hamasa kubwa kwa wanaume kuwa mstari wa mbele katika kupima afya zao,na wakina mama kisiwe kipimo chao. 

“Ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi nchini, asilimia 95 ya watanzania ambao hawana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI inapaswa walindwe ili wasiambukizwe na kundi la wanaume wawe mstari wa mbele kujitokeza kupima afya zao,”alisema Mhagama.

Waziri aliongezea kuwa ni vyema jamii kuendelea kujilinda ili kuepuka maambukizi mapya yanayosababisha takwimu za maambukizi nchini kuongezeka badala ya kupungua.

“Pia asilimia tano ya watanzania ambao wana maambukizi ya virusi vya UKIMWI inapaswa walindwe ili asilimia hizo zisiongezeke kutokana na mpango wa 90 tatu”, alisisitiza Mhagama. 

Alisema pia kwenye asilimia hiyo 90 watakaopima na kukuta wamepata maambukizi wanapaswa kutumia dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ili kuhakikisha maambukizi mapya yanatokomezwa kabisa hapa nchini.

Aliwataka wananchi wa eneo hilo kutumia kituo hicho kwa kutunza afya zao na kuishi kwa furaha kwani kinawahusu wenye maambukizi na wale wanaohitaji kujua afya zao. 

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe.Alexander Mnyeti alisema Mirerani ndiyo sehemu inayoongoza kwenye mkoa huo kwa kuwa na watu wengi wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kulinganisha maeneo mengine katika mkoa huo. 

Alisema maambukizi ya VVU kwa mkoa wa Manyara ni asilimia 2.3 na kwenye mji mdogo wa Mirerani ni asilimia 16 hivyo eneo hilo pekee ndilo linasababisha mkoa huo kuwa na asilimia kubwa za maambukizi na kuwataka wananchi kuchukua hatua za dhati za kupambana kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja kwa kuhamasisha kupima na kutumia dawa endapo unagundulika na maambukizi.

"Huu ugonjwa umekaa mahali pabaya mno, ningekuwa na jeshi kama lililojenga ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite ningetumia kuzuia UKIMWI lakini siwezi kufanya hivyo ila niwahimize mjitokeze kwa hiari kuja kupima katika kituo hiki," alisisitiza Mnyeti. 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa kudhibiti UKIMWI, Bw. Godfrey Simbeye alisema kituo hicho kimegharimu jumla ya shilingi Milioni 250 ambapo shilingi Milioni 200 ni kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Kituo na Shilingi Milioni 50, ununuzi wa samani na vifaa tiba na litahudumia watu 49,802.

Simbeye ameiomba serikali isaidie mfuko kuhakikisha kinapatikana chanzo cha uhakika cha upatikanaji wa fedha kwani michango pekee haitoshelezi Mfuko huu .

Aidha amewaomba wadau wengine na wafanyabiashara kujitokeza kuchangia katika mfuko huo kupitia namba ya simu 0684 909090 ili kuendelea kudhibiti VVU na UKIMWI nchini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Dkt. Leonard Maboko alisisitizia umuhimu wa wananchi kushiriki na kutumia kituo hicho kikamilifu kipima afya zao na kuanza dawa kwa kadri watakavyoelekezwa na wahudumu wa afya.

Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mhe. James Ole Millya aliishukuru Serikali kwa kufanikisha ujenzi wa kituo hicho na kuwaasa wananchi kujikinga na maambukizi mapya ya VVU ili kuendelea kuwa na afya njema na kujiletea maendeleo yao.

Mwakilishi wa watu wanaoishi na VVU  Wilayani Simanjiro, Wariandumi Kweka alisema kituo hicho kitawasaidia kwani awali walikuwa wanakwenda umbali mrefu kufuata huduma hiyo na wengi kukatishwa tamaa na hali hiyo na kuendelea kuitaka jamii kubadili mitazamo hasi juu yao na kuwapa ushirikiano na kupinga imani potofu za baadhi ya madhehebu  yanayopinga matumizi ya dawa hizo kwa imani ya  kupona bila kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akifunua kitambaa mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Kituo cha kutolea huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara Machi1, 2019. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akihutubia wananchi wa Mirerani wakati wa warsha ya uzinduzi wa Kituo cha kutolea huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara Machi1, 2019. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Dkt. Leonard Maboko akihutubia wananchi wa Mirerani wakati wa warsha hiyo.
 Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe.Alexander Mnyeti akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.
 Baadhi ya wakazi wa Mirereni wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akimpongeza msanii kutoka Sanaa madini group, Alex alipoimba wimbo wa kuhamasisha jamii kupima VVU wakati uzinduzi wa Kituo cha kutolea huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokea vifaa tiba pamoja na vifaa saidizi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Biashara Banki ya NMB Bw.Filbert Mponzi wakati wa uzinduzi wa Kituo cha kutolea huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akimpongeza Bi.Jenita Vicent mara baada ya kujifungua mtoto wa kike katika kituo hicho.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiangalia mtoto aliyezaliwa katika Kituo hicho Mapema mwishoni mwa wiki hii.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na msimamizi wa Kituo cha Afya cha Mirerani Dkt.Hassan Ishabailu mara baada ya kuwasili na kukagua shughuli za kituo hicho Machi 1, 2019 katika Wilaya Simanjiro Mkoani Manyara.

 (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA MAELFU YA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA MAREHEMU RUGE MUTAHABA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Ruge Mutahaba alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao  za mwisho kwa Marehemu Ruge Mutahaba  kwenye hafla ya kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa ndugu na familia ya Marehemu Ruge Mutahaba alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa baadhi wananchi waliofikika kutoa heshima zao kwa Marehemu Ruge Mutahaba alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019  
: Sehemu ya waombolezaji waliofika kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019 .
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MASHINDANO YA BAMMATA SOKA JKT WAAGA KWA KISHINDO

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu
MASHINDANO ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) yameendelea kushika kasi huku timu ya Soka ya JKT ikimaliza mashindano hayo kwa mwaka 2019 kwa kishindo baada ya kuifunga Zimamoto magoli 10 kwa Moja.

Matokeo hayo yamejitokeza katika mchezo wa kufunga Dimba uliochezwa katika Dimba la Uhuru, licha ya Timu hizo zote hazikuwa na nafasi ya kuingia katika Hatua ya nusu Fainali. Katika Soka  Mchezo kati ya Ngome na Magereza unaotarajiwa kuchezwa kesho katika Dimba la Uhuru utaamua nani wa kucheza na Polisi na nani kucheza na SMZ katika hatua ya Nusu fainali.

Aidha katika riadha na  Mpira wa Kikapu  kwa wanawake mchezo katika mchezo huo Ngome waliibuka mshindi wa pili kwa Vikapu 68. Katika Mpira wa Wavu   wanawake Magereza wameifunga JKT kwa seti tatu kwa moja huku kwa upande wa Wanaume  Ngome wameifunga  Polisi Seti tatu bila.

Katika Shabaha pistor wanawake mshindi wa Kwanza Pc Pili Mkama wa pili PC Salvina Mhiche na PC Bertha Jonathan wote kutoka kikosi cha Polisi. Kwa Upande wa Wanaume Sajini Kenya Kiula wa Polisi aliibuka nafasi ya kwanza huku nafasi ya  pili ikishikwa Sajini Jumanne Wambura wa Ngome na watatu ni PC Joseph Mwenda Polisi.

Kwa Upande wa Rifle  Wanawake nafasi ya kwanza ilichukuliwa na  Private Elizabeth Kibondo kutoka Ngome wa pili ni  Mteule Daraja la Pili Sophia Ramadhani wa Ngome na PC Sharifa Kibwana Ally wa Polisi huku kwenye Riadha relay wanaume Mita 400 Timu ya Ngome imeibuka na Ushindi.

Latest Images