Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Je, Unamjua DJ Emperor??

$
0
0
DJ Emperor akiwajibika ghorofa ya Saba New Africa hotel enzi hizo
Haya DJs walikuwa, na bado ni watu muhimu katika shughuli za muziki Tanzania. Labda nikupe maelezo mafupi. Baada ya Biribi Discotheque kupumzika, akazuka kijana huyu, kwanza kwenye parties maeneo ya Upanga, na baadaye kuwa DJ maarufu aliyejulikana kama Dj Emperor, akiburudisha sana pale Motel Agip na kisha kuhamia ghorofa ya saba New Africa Hotel. Alifanya mambo makubwa Arusha pia. Wapenzi wa disco mnamkumbuka? na je, disko lake liliitwaje? 
Hivi sasa je...?

TAARIFA KWA UMMA: UHAKIKI WA WASTAAFU WA MFUKO WA PSSSF

Taarifa kamili kutoka kwa familia Bukoba atakapozikwa Ruge Mutahaba

Hali ya usalama Bukoba atakapozikwa Ruge Mutahaba ni shwari

BREAKING NEWZZZZ: RUFAA DHIDI YA FREEMAN MBOWE NA ESTER MATIKO YARUDISHWA MAHAKAMA KUU

$
0
0
MAHAKAMA ya Rufani imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko.

Hata hivyo, mahakama hiyo imeelekeza jalada la kesi hiyo kurudishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikiliza rufaa ya Mbowe kuhusu kufutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Novemba 23, 2018.

TAMASHA LA KIBIASHARA LA KIMATAIFA LAFANYIKA GÖTEBORG SWEDEN 2019

$
0
0
TAMASHA  la Siku ya biashara la kimataifa limefanyika katika mji wa Goteborg Sweden magharibi ikiwa ni katika kuendelea kuwasaidia washiriki na wamiliki wa kampuni kufahamu mwenendo wa biashara na mkakati wa mauzo ndani na nje ya Sweden pamoja na Ulaya.

Mambo muhimu  yaliyojadiliwa katika mkutano huo  ni pamoja na changamoto Katika ulimwengu wa biashara katika dunia ya leo na kimataifa.

Mkutano huo ulikua ni wakati muafaka wa kukutana na wamiliki na viongozi mbali mbali wa makampuni kutoka pembe mbali mbali za dunia na makampuni mengine ya kuuza nje na maslahi Sawa kwa wote. Zaidi ya kampuni 190 zimehudhuria kutoka kila nyanja ya biashara halikadharika benki kubwa zikiwemo Swedbank na Nordea waliovutiwa sana na taswira ya Tanzania kwasasa.

 Balozi Dr Willibrod Peter Slaa akiwa na mkalimani nguli mswedishi Denis Nystrom aka Juma alieishi Tanzania kwa miaka 17 alimsaidia Mh balozi kutafsiri toka lugha ya kiswedishi kwenda kiswahili fasaha
 Balozi Slaa akizungumza na Mr Livio Benedetto afisa uhusiano mambo ya nje toka mji wa Trollhattan aliesimama Katika na kulia ni mkuu wa mambo ya nje kutoka Export center west of Sweden region Mr Olle Jonäng.
Team Tanzania waliwakilisha vyema chini ya uongozi wa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Willibrod Slaa , kutoka kushoto ni Chef Issa, Afisa ubalozi Mr Juma Ndwatta, Mh balozi Slaa, mjasilia Mali Ms Nimco Kapande, Mkalimani Mr Denis Nystrom aka Juma, afisa ubalozi Bi Joyce Malipula na afisa ubalozi Ms Agnes Mwaiselage.
 Mjalisimali Katika idara ya chakula na lishe Chef Issa pia alishiriki kuwakilisha upande wa wafanyabiashara upande wa Tanzania
 Maafisa wa ubalozi waliohudhulia kutoka kulia kwenda kushoto ni afisa Juma Ndwatta, Joyce Malipula na Agnes Mwaiselage na wa mwisho ni Chef Issa.
 Panel discussion ikiendelea na hayo hapo juu ndio majina ya watoa Mada

Balozi Slaa alihudhuria pia seminar maalumu kwajili ya Norway 🇳🇴 wa kumzungumzia fursa na changamoto za Uwekezaji.

Kitongoji cha Kamleshe chasababisha RC Wangabo Kuacha Gari yake

$
0
0
*Atumia Siku mbili kukifikia
*Msafara wake watembea saa 1:30 kukifikia kijiji.
*Walikuwepo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na wataalamu kutoka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 
Gari waliopanda wataalamu kutoka Ofisi ya mkoa wa Rukwa likiwa limekwama huku wataalamu hao kwa ushirikiano na wajumbe wa Kamati ya ulinzi ya Mkoa wakijaribu kulikwamua kutoka kwenye tope zito wakati wakitokea kijiji cha Jengeni Kata ya Kitete, Wilayani Kalambo. 
Gari la Mkuu wa Wilaya ya Kalambo likiwa limekwama na kujaribu kukwamuliwa kutoka kwenye tope zito liliosababishwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha hali ya barabara kuwa mbaya. 
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura akivuka daraja la miti kuelekea katika kijiji cha Jengeni, Kata ya Kitete, Wilayani Kalambo. daraja hilo ndilo wanalotumia wananchi katika shughuli zao za kila siku hasa wakati wa masika. Chini ya daraja hilo unapita mto China. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele) akivuka daraja la miti lililojengwa juu ya mto Kalambo kuelekea katika kitongoji cha Kamleshe ambacho kipo karibu na Kijiji cha Jengeni alipokwama kuendelea na safari kwa siku ya kwanza.  
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura akivushwa katika daraja la miti na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nondo Robert Sikombe kuelekea katika kitongoji cha Kamleshe ili kukutana na wananchi hao na kufahamu changamoto mbalimbali wanazokumbana nanzo. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akivuka daraja la miti katika mto china ili kufika katika kijiji cha Jengeni na kuelekea katika kitongoni cha Kamleshe kijiji cha Nondo, Kata ya Mpombwe Wilaya ya Kalambo. 
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura akivuka daraja la miti kuelekea katika kijiji cha Jengeni, Kata ya Kitete, Wilayani Kalambo. daraja hilo ndilo wanalotumia wananchi katika shughuli zao za kila siku hasa wakati wa masika. Chini ya daraja hilo unapita mto China.
Kaimu RAS - Kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya akivuka daraja la miti kuelekea katika kijiji cha Jengeni. kuonana na wananchi kisha kuelekea katika kitongoji cha Kamleshe kilichopo kijiji cha Nondo, Kata ya Mpombwe, Wilayani Kalambo.

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA KISHAPU

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia wananchi waliokuja kumlaki wakati akiwasili kwenye mgodi wa Almasi Mwadui mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Meneja wa Huduma za Kiufundi wa Mgodi wa Williamson Diamond Richard Jumanne akimuonyesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan eneo ambalo uchimbaji wa almasi unafanyika katika mgodi huo uliopo Mwadui, Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi wa ujenzi wa maabara ya shule ya Sekondari  Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia wanafunzi waliokuja kumlaki wakati akiwasili kwenye mgodi wa Almasi Mwadui mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Shinyanga wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye yup kwenye ziara ya kikazi mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiangalia shughuli ya uchambuaji  wa almasi klatika mgodi wa Wiliamson Diamond Ltd, wengine pichani ni Naibu Waziri Madini Mhe. Stanslaus Nyongo (kushoto) na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelline Mabula pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara (kulia). Makamu wa Rais yupo mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa Makamu wa Rais Mhunze, Kishapu mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kusema ameridhishwa hatua iliyofikiwa.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka. Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Alhamisi, Februari 28, 2019) amesema amefurahi kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi.

Kufuatia kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha  taratibu za kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika. Kadhalika, Waziri Mkuu ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa sababu jengo ni zuri na linavutia. Pia amewapongeza Watanzania wanaofanya kazi kwenye mradi huo.

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Walaka wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo hilo limekamilika kwa asilimia 95.
Mhandisi huyo alisema tayari wamefanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa mbalimbali na kwamba mkandarasi anatarajia kukabidhi mradi huo Mei 31 mwaka huu. Jengo hilo linauwezo kubeba abiria milioni sita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Teminal Three  jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiaga wakati alipoondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Terminal Three, jijini Dar es salaam baada ya kukagua ujenzi wa uwanja huo ambao umekamilika kwa asilimin 95 na unarajiwa kukamilika Mei mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NENDA SALAMA RUGWE: THT NA MRISHO MPOTO

NEWZ ALERT: RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA AMEFANYA UTEUZI NA KUWAPANDISHA VYEO BAADHI YA MAOFISA WA POLISI KUWA MAKAMISHNA WA POLISI NA KUWAHAMISHA WENGINE WAWILI

$
0
0


1.              NAIBU KAMISHNA WA POLISI (DCP) CHARLES MKUMBO AMETEULIWA NA KUPANDISHWA CHEO NA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA KAMISHNA WA POLISI, ATAKAYEONGOZA KAMISHENI YA POLISI INTELIJENSIA YA JINAI              (CP INTEL)


2.              NAIBU KAMISHNA WA POLISI (DCP) LIBERATUS MATERU SABAS AMETEULIWA NA KUPANDISHWA CHEO NA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA KAMISHNA WA POLISI, ATAKAYEONGOZA KAMISHENI YA POLISI OPERESHENI NA MAFUNZO (CPO&T)


3.              NAIBU KAMISHNA WA POLISI (DCP) SHABAN MLAI HIKI AMETEULIWA NA KUPANDISHWA CHEO NA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA KAMISHNA WA POLISI, ATAKAYEONGOZA KAMISHENI YA POLISI MAABARA YA UCHUNGUZI WA KISAYANSI (CP F&B)


4.              NAIBU KAMISHNA WA POLISI (DCP) LEONARD PAUL LWABUZALA, AMETEULIWA NA KUPANDISHWA CHEO NA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA KAMISHNA WA POLISI, ATAKAYONGOZA KAMISHENI YA POLISI FEDHA NA LOJISTIKI (CPF&L)

5.              KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI SACP BENEDICT MICHAEL WAKULYAMBA, AMETEULIWA NA KUPANDISHWA CHEO NA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA KAMISHNA WA POLISI, ATAKAYEONGOZA KAMISHENI YA POLISI UTAWALA NA MENEJIMENTI YA UTUMISHI (CPA&HRM)

 


WALIOHAMISHWA KWENDA  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI NI WAFUATAO:

                                                                                                                          

  1. KAMISHNA ALBERT MATHIAS NYAMHANGA, KUTOKA KAMISHNA WA POLISI UTAWALA NA MENEJIMENT YA UTUMISHI KWENDA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI IDARA YA WAKIMBIZI.

  2. KAMISHNA NSATO MSSANZYA MARIJANI, KUTOKA KAMISHNA WA POLISI OPERESHENI NA MAFUNZO KWENDA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI IDARA YA WAKIMBIZI.

WAKATI HUO HUO, INSPEKTA JENERALI WA POLISI AMEFANYA UHAMISHO WA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA, KAMA IFUATAVYO:


  1. KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI GEMINI S. MUSHI, ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA RUVUMA KWENDA KUWA MKUFUNZI MKUU CHUO CHA POLISI (CCP) MOSHI

  2. KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI (SACP) RENATA M. MZINGA, ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA NJOMBE ANAKWENDA MAKAO MAKUU YA POLISI DSM

  3. KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) SIMON SILVERIUS HAULE, ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA  SHINYANGA ANAKWENDA MAKAO MAKUU POLISI DSM

  4. KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) JONATHAN SHANA, ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA ARUSHA

  5. KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP)  AMON DAUD KAKWALE, ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA KIPOLISI TEMEKE

  6. KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) SIMON MARWA MAIGWA, ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA RPC RUVUMA


  1. KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) SALUM  RASHID HAMDUNI, ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA NJOMBE


  1. KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) RICHARD GEORGE ABWAO ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA  SHINYANGA


  1. KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) ZUBER SEIF CHEMBERA ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI  MKOA WA KIPOLISI ILALA.

MAKAMISHNA WALIOTEULIWA NA MHE. RAIS WATAAPISHWA NA INSPEKTA JENERALI WA POLISI KWA NIABA YA MHE. RAIS TAREHE ITAKAYOPANGWA, MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI.

Imetolewa na:

     Simon N. Sirro 

     Inspekta Jenerali wa Polisi

     Makao Makuu ya  Polisi.

     S.L.P. 9141,

     DAR ES SALAAM.



www.policeforce.go.tz               www.twitter.com/tanpol          www.facebook.com/tanpol


VITUO VYA TICKET ZA MARRIAGE REVIAL DINNER PARTY 2019.

$
0
0


*Life House Posta, NIC 4 Floor Posta 0756 444 619

*Victoria Petrol Station, Alhasani Mwinyi Road

*Mel K Suit,  Bagcama behind TSN Supermarket 658 445 638

*Reno closet boutique,
Shekilongo road Opposite geti la chuo cha Ustawi 0717 374 113

*Coco Beach, Toure drive 0716787633

Online Ticket- 0784 488 184.
Tuma pesa kisha tuma majina yako utatunziwa ticket yako

Watumishi wa Mambo ya Nje wahimizwa kuzingatia sheria za utumishi wa umma

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza kwenye kikao cha pili na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) Pamoja na mambo mengine amewataka Watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo. Kikao hicho kilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano  wa Wizara uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma hivi karibuni
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bibi Savera Kazaura akizungumza wakati wa kikao hicho
Sehemu ya Watumishi wa Wizara wakiwemo Wakuu wa Idara 
Balozi Mteule, Dkt. Mpoki Ulusubisya akitoa mada kuhusu afya kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) wakati wa kikao kati yao na Katibu Mkuu wa Wizara. Pamoja na mambo mengine aliwashauri Watumishi kuwa na utratibu wa kupima afya zao mara kwa mara.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara wakiwemo Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia mada
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara

Sehemu nyingine ya Wakuu wa Idara na Vitengo

Wakuu wa Vitengo akifuatilia mkutano

Wakurugenzi wakiwa kwenye mkutano

Mkutano ukiendelea

Sehemu ya Watumishi wakifuatilia mkutano

Watumishi wakiwa kwenye mkutano

Mkutano ukiendelea

Sehemu nyingine ya Watumishi wakati wa mkutano

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye mkutano na Katibu Mkuu.

RAIS DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI IKULU ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas D.Ndumbaro, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulia leo, 1/3/2019.(Picha na Ikulu) 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alipofika Ikulu kwa mazungumzo na kujitambulisha, leo, 1/3/2019. Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mhe.Dkt. Damas D.Ndumbaro, wakitoka katika ukumbi wa mkutano baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Zanzibar leo,1/3/2019.(Picha na Ikulu)   

HAKUNA TENA NAFASI YA KUFANYA MAKOSA KATIKA MANUNUZI-DKT JINGU

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewaonya viongozi na baadhi ya watumishi wa Wizara yake kuwa hakuna nafasi tena ya kufanya makosa katika utendaji kazi kwa kuwa tayari wana ufahamu mkubwa wa sheria ya manunuzi.

Alisema hayo wakati hotuba yake kwa watumishi hao wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kuhusu sheria ya manunuzi nakuongeza kuwa wanatakiwa kusoma zaidi sheria hiyo baada ya kuwa wamepata mwanga wa kutosha kutokana na mafunzo hayo.

Aidha Kiongozi huyo aliongeza kuwa kutokana na kukosa ufahamu wa sheria ya manunuzi baadhi ya watumishi walikuwa wanafanya makosa ya kimajukumu kwa kutekeleza majukumu ya watu wengine na kuonya kuwa inabidi wajilizishe na sheria ili kuepuka mwingiliano katika majukumu yao.

‘’Baada ya kupitia mafunzo ya majukumu ya kila mtu kisheria ni matumaini yangu kuwa hakutakuwa nafasi tena ya kufanya makosa kwa kufanya maamuzi yanayokiuka sheria na kujikuta unatekeleza majukumu ya mtu mwingine kama vile kutekeleza majukumu ya Katibu Mkuu wakati wewe huna mamulaka hayo.’’ Aliongeza Dkt. Jingu.

Aidha amewataka viongozi na watumishi hao kuepuka na makosa ya rushwa akionya kuwa makosa hayo ni makubwa na yanashughulikiwa na vyombo husika akiwataka kujiepusha nayo kwani mtu akibainika atapata misukomisuko mikubwa jambo ambalo linaepukika.

Aidha amechukua fursa hiyo kuwataka wafanyakazi wote kuacha kufanya kwa mazoea na kuwataka kuwa wabunifu katika maweneo yao ya kazi na katika Jamii zinazowazunguka ili jamii husika iweze kufaidika na kuwepo kwa taasisi mahali hapo.

Amewaagiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kuhakikisha  wanakuwa na ubunifu na pia kutumia rasilimali zilizopo katika maeneo yanayozunguka vyuo ili wananchi wanaoishi jilani na vyuo hivyo waweze kunufaika na uwepo wa chuo katika maeneo yao.

‘’Kuweni wabunifu achana na kufanya kazi kwa mazoea ili wanajamii wanao wazunguka waweze kunufaika na uwepo wa chuo katika maeneo yao mfano Chuo cha Rundenga kwasasa kinasindika zao la karoti na bidhaa zitokanazo na uwekezaji huo zinauzwa kwa jamii jambo hili ni zuri sana.’’ Aliongeza Dkt. Jingu. 

Mafunzo hayo kwa viongozi wa Wizara, Viongozi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii pamoja na maafisa wa serikali yanahusu sheria ya Manunuzi ya Serikari ya Mwaka 2011 na mabadiliko ya kanuni zake ya mwaka 2013 kama ilivyorekebishwa mwaka 2016.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiongea na viongozi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii pamoja na Wakurugenzi wa Wizara wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya sheria ya manunuzi.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya manunuzi ya Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akiongea jambo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tatu kwa viongozi wa wizara na Wakuu Vyuo vya Maendeleo ya Jamii jana Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Manunuzi ya Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Martha Chuma akiongea jambo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tatu kwa viongozi wa wizara na Wakuu Vyuo vya Maendeleo ya Jamii jana Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii pamoja na Wakurugenzi wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii wakifuatilia jambo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tatu kwa viongozi wa wizara na Wakuu Vyuo vya Maendeleo ya Jamii jana Jijini Dodoma.

Wakurugenzi Waagizwa kuwawezesha Maafisa Utamaduni kutekeleza majukumu yao

$
0
0
Na Shamimu Nyaki -WHUSM
Waziri   wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Seleman Jaffo amewaagiza Wakuu wa Mikoa  na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuwawezesha Maafisa Utamaduni kwa kuwaongezea Bajeti itakayowawezesha kutimiza majukumu yao kwa ufasaha.
Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dodoma wakati alipokuwa akifunga Kikao Kazi  cha  11 cha Maafisa Utamaduni kilichofanyika kwa siku mbili ambapo amewaagiza Wakurugenzi kutambua majukumu ya maafisa Utamaduni  ikiwemo kuhifadhi kuendeleza mila na desturi pamoja na kukuza lugha ya kiswahili.
"Sekta hii ni muhimu sana kwakua ina wajibu wa kuelimisha na kuburudisha,hivyo naendelea kuwasitiza Wakurugenzi kuwawezesha Maafisa Utamaduni kushiriki katika kila Mkutano,kongamano,warsha zote zinazohusu sekta hiyo".Alisema Mhe. Jaffo.
Aidha ameongeza kuwa thamani ya maafisa Utamaduni ni lazima ionekane kwakua ndio tasnia inayofundisha na kukuza Uzalendo hasa kujua alama,nyimbo na tunu za Taifa kwa vijana na wanafunzi nchini.
Katika hatua nyingine Mhe.Jaffo amewahakikishia Maafisa Utamaduni kuwa wavumilivu kuhusu muundo wa Kada hiyo ambapo amewaahidi kuwa suala hilo limepokelewa na Serikali itaanza mchakato wake ili kutatua changamoto hiyo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Susan  Mlawi amesema kuwa Kikao Kazi hicho ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 inayoeleza kuwa Wasimamizi na Watendaji wakuu wa shughuli za Utamaduni katika ngazi ya Taifa, Mkoa Wilaya na Taasisi za elimu na mafunzo kupata mafunzo ya uendeshaji ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.
"Kikao Kazi hiki kimepitisha maazimio yatakayokuwa mwongozo katika kuboresha utendaji wa Sekta hii ili kuimarisha utendaji kazi Ki-muundo na kisera baina ya maafisa Utamadduni wote waliopo Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI".Alisema Bibi Susan.
Naye Afisa Utamaduni Wilaya ya Urambo Bw.Tito Lulandala ameeleza kuwa Sekta ya Utamaduni ina fursa nyingi zinazoweza kukuza pato la mwananchi mmoja na Taifa kwa ujumla katika nyanja mbalimbali ikwemo Michezo Sanaa na kukuza Utalii.
Katika kikao kazi hicho mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo Umuhimu wa Ubidhaishaji wa lugha ya kiswahili,Uhuishaji wa Sera ya Utamaduni,Sekta ya Filamu nyenzo muhimu katika kuimarisha Asili na Utamaduni
,Fursa za utalii wa Kiutamaduni na nyinginezo.
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI Mhe.Selemani Jaffo  akizungumza na Maafisa Utamaduni wa mikoa na Halmashauri zote nchini (hawapo katika picha) wakati akifunga Kikao Kazi cha Sekta hiyo kilichofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawi. Akizungumza na Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini (hawapo katika picha) wakati akifunga Kikao Kazi cha Sekta hiyo kilichofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bw.Boniface Kadili akitoa maelezo mafupi kuhusu ya Sekta yake wakati wa ufungaji wa Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kilichofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI Mhe.Selemani Jaffo  (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na  Maafisa Utamaduni wa mikoa na Halmashauri zote nchini baada ya  kufunga Kikao Kazi cha Sekta hiyo kilichofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.

NMB YAWAKABIDHI TIKETI WASHINDI WA ‘MASTABATA’ SAFARI YA DUBAI

$
0
0

Mfamasia wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Enstern Ngao (katikati), akikabidhiwa mfano wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi Dubai baada ya kujishindia bahati nasibu ya Benki ya NMB ya MASTA BATA hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Wanao mkabidhi kulia ni Philbert Casmir na Manfredy Kayala maofisa wa NMB kitengo cha huduma za kadi.
Meneja Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Philbert Casmir (kulia) akikabidhiwa mfano wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi Dubai Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Simon Chacha (kushoto) baada ya kujishindia bahati nasibu ya MASTABATA iliyokuwa inaendeshwa na Benki ya NMB hivi karibuni.
Washindi hao Enstern Ngao (wa pili kushoto), pamoja na Simon Chacha (wa pili kulia) wakikabidhiwa mfano wa tiketi zao za ndege kwenda na kurudi Dubai baada ya kujishindia bahati nasibu ya Benki ya NMB iliyojulikana kama MASTABATA hivi karibuni. Wanao wakabidhi wa kwanza kulia ni Philbert Casmir na Manfredy Kayala (kushoto) maofisa NMB kutoka kitengo cha huduma za kadi.
Meneja Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Manfredy Kayala (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kabla ya kuwakabidhi tiketi hizo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Simon Chacha (kushoto) na Mfamasia wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Enstern Ngao (kulia) baada ya kujishindia bahati nasibu ya MASTABATA iliyokuwa inaendeshwa na Benki ya NMB hivi karibuni.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Simon Chacha (katikati) akifurahia tiketi yake mara baada ya kukabidhiwa.

SERIKALI YATOA SIKU 60 KWA HALMASHAURI KUHAMISHA DAMPO

$
0
0
Na Lulu Mussa, Njombe
Halmashauri ya Mji wa Makambako Wilayani Njombe imeagizwa kusitisha mara moja utupaji wa taka ngumu katika dampo lililopo katika Kata ya Saja, Kijiji cha Itengelo Wilaya ya Wanging’ombe kutokana na kutokidhi matakwa ya Sheria ya Mazingira na malalamiko yaliyotolewa na wananchi katika vijiji vya jirani. 

Agizo hilo limetolewa hii leo Mkoani Njombe na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima mara baada ya kufanya ziara ya kikazi na kumuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Makambako Bw. Rashid Hozi kutafuta eneo maalumu litakalokidhi mahitaji husika ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya athari kwa mazingira

Akiwa katika eneo hilo la dampo la Makambako ambalo kwa hivi sasa liko katika Wilaya ya Wanging’ombe, Mhe Sima ameshuhudia wananchi wakiingia kiholela katika dampo hilo kwa ajili ya kuokota bidhaa mfano chupa za plastiki kwa ajili ya kuziuza. “Serikali inatumia pesa nyingi katika huduma za afya ni wakati sasa tupunguze mzigo huu kwa magonjwa yanayoweza kuepukika kwa kuwa na mazingira safi na salama. Kuanzia sasa ni marufuku wananchi kuingia dampo kuokota chupa za plastiki, hii inahatarisha afya zao wenyewe, hivyo utaratibu wa kutenganisha taka uanzie katika vyanzo vya uzalishaji” Sima alisisitiza.

Awali Mratibu wa Kanda wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira  (NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Godlove Mwamsojo amesema kuwa Baraza limetoa notisi ya siku sitini (60) kuanzia tarehe 01/02/2019 kwa Halmashauri hiyo ya kusitisha utupaji wa taka katika eneo hilo na kuwaagiza kuteketeza taka zote zilizopo katika kipindi kilichotajwa.
Bw. Mwamsojo amesema kuwa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, kifungu cha 119 kinazitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kutafuta namna bora ya kuteketeza taka ngumu katika maeneo yao na kuainisha kuwa dampo hilo kwa sasa liko katika eneo la mwinuko hivyo kipindi cha mvua hutiririsha maji ambayo si salama kwa wakazi wa maeneo ya chini.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Sima pia amemuagiza Mratibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuhakikisha anafuatilia utekelezaji wa agizo hilo na endapo Halmashauri haitatekeleza agizo hilo hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao . 
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Makambako Bw. Rashid Hozi amekiri kupokea barua ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na kuahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa kwa muda muafaka.
Naibu Waziri Mussa Sima, yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Nyanda za juu Kusini kuainisha changamoto za kimazingira katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja na  kukagua mitambo ya kuteketeza taka hatarishi katika Hospitali, kujionea hali ya madampo katika mikoa husika endapo utaratibu wa kutenganisha taka unazingatiwa ili kuzuia wananchi kuzifuata baadhi ya bidhaa zinazo rejerezeka katika maeneo ya dampo kwa lengo la kudhibiti milipuko ya magonjwa.
Katika Mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa Mheshimiwa Sima pia atapata fursa ya kuembelea kwenye ikolojia ya vyanzo vya maji vinavyo changia maji katika bonde la Rufiji.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Mratibu wa Kanda kutoka Baraza la Taifa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Bw. Godlove Mwamsojo mara baada ya kutembelea dampo lililopo katika Kata ya Saja, Kijiji cha Itengelo Wilaya ya Wanging’ombe. Naibu Waziri Sima ameagiza kufungwa kwa dampo hilo na kuteketeza taka zote zilizopo.
Sehemu ya wananchi ambao wamekutwa wakiendelea na shughuli za kutafuta bidhaa kwa ajili ya kurejereza katika dampo lililopo katika Kata ya Saja, Kijiji cha Itengelo Wilaya ya Wanging’ombe bila kujali madhara yao kiafya. Naibu Waziri Sima amepiga marufuku wananchi kuingia kiholela katika dampo hilo na kumwagiza Mkurugenzi wa Mji wa Makambako kufunga dampo hilo na kuteketeza taka zote ndani ya siku sitini.

MAELFU YA WANANCHI DAR WAJIPANGA BARABARANI KUTOA HESHIMA KWA RUGE

$
0
0
*Wapo waliamua kushika gari iliyobeba mwili wake
*...Kwe heri Ruge...nenda kaka,...mbela yako, nyuma yetu

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MAELFU ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kushuhudia mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.
Ukweli ni kwamba mwili wa Ruge kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameupokea kwa heshima kubwa na hiyo inaonesha namna alivyokuwa kwenye mioyo ya watu.
Mwili wa Ruge uliwasili nchini saa tisa Alasiri ukitokea Afrika Kusini ambako kabla ya kuanza safari ukiwa uwanjani hapo uliwekwa kwenye gari ndogo yenye rangi nyeusi.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa jijini Dar es Salaam mamia ya wananchi walianza kujipanga kuanzia uwanjani hapo.Aliyeongoza mapokezi ya mwili wa Ruge ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu ya Rais-Muungano na Mazingira.
Mwili wa marehemu Ruge baada ya kutoka Uwanja wa Ndege ulipita Barabara ya Uhuru, Karume ,Magomeni ,Morocco Hotel,Sinza Kijiweni. Bagama, ITV, Clouds ,Kawe na kisha Lugalo.
 Michuzi Blog na Michuzi TV waliokuwa kwenye msafara huo walishuhudia mamia ya watu wakiwa barabarani wakisuburi kuona jeneza lililobeba mwili wa Ruge.
Baadhi ya watu walishindwa kujizuia kiasi cha baadhi yao kuamua kwenda kushika gari iliyobeba mwili wa marehemu Ruge ambaye hakika amethibitisha kuwa alikuwa yupo kwenye mioyo ya Watanzania.
 Kutokana na idadi kubwa ya watu iliyojitokeza barabarani, ilisababisha msafara huo kusimama mara kwa mara.Waendesha bodaboda nao walioekana kutokuwa nyuma kwani nao waliamua kuungana na magari yaliyokuwa kwenye msafara huo.
Wakati mwili wa Ruge unapita katika baadhi ya barabara wapo wananchi ambao walikuwa wakisikika wakisema hivi "Nenda Ruge...nenda kaka,...hakika sote ni wa mwenyezi Mungu... nenda Ruge mbele yako , nyuma yetu.
Ukweli ni kwamba kadri msafara wa Ruge ulivyokuwa unaendelea kwenda ndivyo ambavyo idadi ya watu ambavyo ilikuwa inaongeza, kiasi cha cha kufanya gari ambayo imebeba msafara huo kupunguza mwendo na kwenda taratibu.
 Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliamua kutoa maelekezo ya kuhakikisha wananchi waliokuwa barabarani wanapata nafasi ya kuona vizuri jeneza ambalo lilikuwa limebeba mwili huo.
Hata hivyo, aliamua kutoa maagizo ya kuwataka waendesha bodaboda kukaa nyuma ya gari iliyobeba mwili kwani kabla ya kutoa maelekezo hayo , waendesha bodaboda walikuwa wametangalia mbele na kufanya msafara kushindwa kwenda kwa utaratibu mzuri na kutoa nafasi ya wengine kuuona.
 Hata hivyo wakati wananchi wengi wakiwa barabarani, kuna wengine ambao wao waliamua kwenda kuusubiri mwili wa Ruge katika Kituo cha Redio cha Clouds.Kwa mujibu wa ratiba mwili wa Ruge kabla ya kwenda Lugalo ulipitishwa katika eneo hilo ambalo ni ofisi zake alizokuwa anafanya kazi enzi za uhai wake.
Sababu za kuupeleka mwili huo Clouds ilikuwa ni kutoa nafasi kwa wafanyakazi wenzake kupata nafasi ya kuona jeneza lililobeba mwili wake.Hata hivyo msafara wa mwili wa Ruge bado unaendelea na Michuzi Blog itaendelea kukufahamisha hatua kwa hatua.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na mazingira @jmakamba ameongoza mapokezi ya mwili wa marehemu aliyekuwa  Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Ruge Mutahaba, akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es aalaam Mh.Paul Makonda pamoja na Mkurugenzi wa  Clouds Media Group Joseph Kusaga.
 Mapokezi ya mwili wa marehemu aliyekuwa  Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Ruge Mutahaba, tayari ukiwa umewasili jioni ya leo. 

MAKAMU WA RAIS AAGIZA TRA NA UHAMIAJI KUFUNGUA OFISI WILAYANI KISHAPU MKOA WA SHINYANGA

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images