Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 27,2019


CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHATOA SALAMU ZA POLE NA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA RUGE MUTAHABA

New-Bagamoyo road widening construction gets Japanese Contractor

$
0
0

                                                            27thFebruary, 2019



Contract agreement for the construction and widening of New-Bagamoyo road (Morocco-Mwenge section, total 4.3 km) is scheduled to be signed between Tanzania National Roads Agency (TANROADS) and the Nippo-Dai Nippon Joint Venture on 28th February, 2019 (Thursday). The project is funded by the Government of Japan through Japan International Cooperation Agency (JICA) as a Japanese Grant.

The project will repave the current road, install new streetlights, service roads and footpaths for pedestrians. It will create a model of high-quality road infrastructure, which is resilient against floods and provide enough space for both motorists’ and pedestrians’ safety.

As we see in the Mfugale Flyover which was opened to the public in September 2018, High-quality infrastructure” is not just a building or a civil structure, but it also has features such as the finest finishing, safety both during and after construction, and lower operation and maintenance expenditure. Following the Mfugale Flyover, the New-Bagamoyo widening project will be the next model of “High-quality infrastructure” in Tanzania.

In response to increasing demand, the city of Dar es Salaam is developing remarkably.  JICA continues to support Tanzania for the comprehensive development of infrastructure of Dar es Salaam.

Date:

28th February, 2019

Time:

10:00am -

Venue:

Tanzania Ports Authority Building (34th Floor)

Sokoine Drive, Dar es Salaam

Guests of Honour

·       Minister of Works, Transport and Communication

·       Regional Commissioner (RC) of Dar es Salaam

·       CEO of TANROARDS

·       Japanese Ambassador to the United Republic of Tanzania

·       Executive Senior Vice President of JICA



RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AFUNGUA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LEO UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikagua gwaride maalum llililoandaliwa kwa ajili ya Ufunguzi wa Bunge la Afrika Mashariki katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga, alipowasili katika viwa vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.(Picha na IKULU)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga wakiingia katrika ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya Ufunguzi.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Afrika Mashariki lililofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)

Baadhi ya wabunge wa bunge la Afrika Mashariki wakisikiliza hotuba  ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  amesema kuwa suala la kupambana na rushwa lina umuhimu mkubwa katika maendeleo ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa ikizingatiwa kwamba vitendo hivyo vinazorotesha uchumi na maendeleo.

Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Chukwani mjini Zanzibar wakati akizindua Mkutano wa Nne wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambapo kwa mwaka huu unafanyika hapa Zanzibar.

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alieleza kuwa kuwepo kwa Mswada wa rushwa katika mkutano wa Bunge hilo mwaka huu kuna umuhimu mkubwa kwani utasaidia katika kupambana na vitendo vya rushwa ambavyo vimekuwa vikiathiri sana uchumi na maendeleo ya nchi na wananchi wake.

Amesema kuwa Mkutano huo ambao katika Miswada yake ambapo miongoni mwao kutakuwepo Mswada huo ambao utajadiliwa unakwenda sambamba na juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na nchi wanachama katika kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa na uhujumu wa uchumi.

Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika jitihada zake za kukomesha vitendo vya rushwa imeunda Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kwa lengo la kushughulikia suala zima la kupambana na rushwa.

Alisema kuwa juhudi hizo zinaendelea kwa mashirikiano ya pamoja na wananchi hatua ambayo imepelekea Mamlaka hiyo kuweza kupiga hatua kubwa.

Aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli imeongeza juhudi zaidi katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa kwa kuweka mikakati mbali mbali.

Alisema kuwa Serikali zote mbili ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeimarisha usimamizi wa sheria na kuongeza Bajeti katika sekta ya sheria sambamba na kuongeza wataalamu ili kusimamia kesi zinazohusiana na rushwa.

Hivyo, Rais Dk. Shein alisema kuwa juhudi hizo zitasaidia sana pamoja na zile sheria zitakazotungwa na Bunge hilo ambazo zote kwa pamoja zinaweza kufikia lengo lililokusudiwa.

Aidha, Rais Dk. Shein alisisitiza suala zima la kuzingatia umhimu wa maadili na tabia njema katika kutekeleza majukumu ya viongozi hao hasa katika wakati huu ambao teknolojia na mifumo ya maisha imebadilika na baadhi ya wakati hupelekea Wabunge kufanya vitendo ambavyo vinahitaji umakini na maamuzi ya busara ili waweze kulinda hadhi yao.

Alisema kwamba inatia moyo kuona kwamba Ukanda wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa Kanda zinazoongoza katika ukuaji mzuri wa uchumi duniani ambapo katika mwaka wa 2017 uchumi ulikuwa kwa asilimia 4.6 ikilinganishwa na mwaka 2016 ambapo uchumi ulikuwa asilimia 4.4.

Alieleza kuwa hayo ni mafanikio makubwa ambayo yanapaswa kuendelezwa  huku akisisitiza kuwa kutokana na Afrika ya Mashariki kuwa na zaidi ya watu milioni 162 hali hiyo inapelekea kuwepo kwa soko kubwa la bidha mbali mbali pamoja na huduma muhimu.

Pia, alieleza kuwa Afrika Mashariki ina ardhi kubwa yenye kilomita za mraba 1.82 milioni ambayo ni vyema rasilimali hiyo ikatumika vizuri ili iweze kuleta tija kwa nchi wanachama.

Vile vile, Rais Dk. Shein alipongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na nchi wanachama katika kuhakikisha kwamba Jumuiya hiyo inafikia malengo yake hasa katika suala zima la kukuza uchumi, uimarishaji wa utawala Bora, uismarishaji wa sheria pamoja na uimarishaji wa amani na utulivu.

Rais Dk. Shein ameeleza kutiwa moyo sana na juhudi za Umoja huo za kuimarisha lugha ya Kiswahili ambayo hivi sasa imekuwa ni lugha inayounanisha wanachama katika shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii.

Alieleza kuwa Zanzibar inathamini sana fursa iliyopewa ya kuwa Makamo Makuu ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki na kuahidi kuwa fursa hiyo itaitumia vizuri ili kuhakikisha malengo yaliokusudiwa yanafikiwa.

Dk. Shein alimuhakikishia Spika wa Bunge hilo Martin Ngonga kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza na kuitangaza lugha ya Kiswahili na kufahamisha kwamba kupitia Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) imekuwa ikiandaa makongamano mbali mbali ya Kiwahili ambayo yanajumuisha wataalamu kutoka sehemu mbali mbali duniani.

Alisema kuwa hatua hiyo ina lengo la kukiimarisha na kukuza matumizi sahihi ya Kiswahili fasaha kwa kuangalia kwamba Zanzibar ndio chimbuko la Kswahili sanifu.
Rais Dk. Shein alisema anaamini kwamba Jumuiya hiyo inaweza kuwa eneo muhimu la kiuchumi duniani, hivyo jitihada zaidi zinahitajika katika utekelezaji wa malengo makuu yaliopangwa na Jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kushajiisha uekezaji, kuendeleza sekta ya utalii, viwanda, elimu na kutilia mkazo  suala zima la kuongeza ajira na kuimarisha miundombinu.

Pamoja na hayo, Rais Dk. Shein aliitaka Jumuiya ya Afrika Masharik kupitia Bunge lake hilo kuchukua jitihada katika kupambana na vitendo mbali mbali vyenye kuathiri uchumi ikiwemo suala zima la utakasishaji wa fedha.

Vile vile, Rais Dk. Shein alieleza haja ya kuendeleza teknolojia ya Habari na Mawasiliano huku akiwasisitiza Wabunge wa Bunge hilo kufanya kazi kwa mashirikiano mazuri na Mabunge mwengine ya nchi wanachama ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mzuri zaidi.

Aidha, Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kulipongeza Bunge hilo kwa kufanya mkutano wake huo hapa Zanzibar na yeye kupata fursa kwa mara ya pili kuufungua mkutano huo na kutoa shukurani zake kwa kuweza kukaa pamoja na chombo hicho muhimu cha kutunga Sheria.

Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumpongeza Spika wa Bunge hilo kwa  kuchaguliwa kuwa Spika wa tano na kuweza kukiongoza chombo hicho huku akiwapongeza Wajumbe wote wa Bunge hilo kwa kuchaguliwa kukiongoza chombo hicho muhimu katika Afrika Mashariki.

Pamoja na hayo, alisifu utaratibu wa Bunge wa kufanya mikutano katika miji ya nchi wanachama jambo ambalo linapelekea wananch kufahamu majukumu ya chombo hicho ambapo alisema utaratibu huo unaenda sambamba na falsafa ya kuweka umoja na mshikamano kwa watu wa Afrika Mashariki.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein ameleza kufurahishwa kwake na moja ya Miswada ambayo itajadiliwa katika Bunge hilo ambayo ni pamoja na Mswada wa vita dhidi ya rushwa, masuala ya kijinsia,ulemavu pamoja na mada nyengine zitakazojadili vitendo vya ugaidi vilivyojitokeza nchini Kenya.

Nao Wabunge hao walitoa shukurani kwa Rais Dk. Shein kwa heshima kuwa aaliyowapa ya kwenda kuzindua mkutano wao huo na kueleza kufurahishwa kwa kiasi kikubwa na hotua aliyoitoa ambayo imewapa matumaini makubwa.

Nae Spika wa Bunge hilo Martin Ngoga alitoa shukurani kwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na uongozi wake chini ya Spika wa Baraza hilo Zubeir Ali Maulid kwa mashirikiano mazuri wanayoyapata ambayo ni chachu katika utekelezaji wao wa kazi.

Aidha, Spika huyo alieleza umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika Umoja huo pamoja na Wajumbe wa Bunge hilo na kueleza mikakati waliyoiweka katika kuhakikisha lugha hiyo inatumika vyema ndani ya Bunge hilo pamja na nchi zote za Jumuiya hiyo.

Nae Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid alieleza mashirikiano mazuri yaliopo kati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Bunge hilo Afrika Mashariki na kueleza mafanikio makubwa yaliopatikana katika mashirikiano hayo.
Katika uzinduzi huo wa Mkutano wa (EALA) ambao unatarajiwa kuwa wa siku 10 moja, viongozi mbali mbali walihudhuria akiemo Spika wa Bunge hilo Martin Ngoga, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Wenyeviti na Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid, Spika Mstaafu Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wajumbe wa Bunge hilo la Afrika Mashariki.

WATUMISHI WA UMMA NCHINI MARUFUKU KUTUMIKA KISIASA - DKT MWANJELWA

$
0
0



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi wa umma nchini kutotumika kisiasa kwani uwepo wao una lengo mahususi la kuboresha utoaji huduma wenye viwango stahiki ikiwa ni pamoja na kuijenga Serikali ili iweze kuleta maendeleo kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri huyo wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla ya kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Kisarawe ili  kujiridhisha na utekelezaji wa mpango huo. 
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, serikali inahitaji utaalam wa watumishi wa umma katika kujenga utumishi wa umma imara uliotukuka, utumishi ambao utaziwezesha taasisi za umma zote nchini kutoa huduma stahiki kwa wananchi. 
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, hategemei kumuona mtumishi wa umma yeyote akijihusisha na siasa zinazosababisha kukwamisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa kuwasimamia kikamilifu Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri ili kujenga ushirikiano wa kiutendaji kati ya Makatibu Tawala wa Wilaya  na Wakuu wa Wilaya kwa lengo la kuboresha utoaji huduma bora kwa umma. 
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amehimiza ushirikiano wa watendaji hao ili kurahisisha utendaji kazi wa shughuli za serikali kwa ujumla, na kuongeza kuwa, serikali iliyopo madarakani ni moja tu inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, hivyo anashangaa inakuwaje Makatibu Tawala wa Wilaya wasiarifiwe masuala yanayoendelea katika halmashauri.

“Kuanzia sasa barua yoyote ya kiutendaji itakayotoka mkoani kuelekezwa kwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, ni lazima nakala ya barua hiyo ielekezwe pia kwa Makatibu Tawala wa Wilaya ili wafahamu kinachoendelea na kumuarifu Mkuu wa Wilaya kufanya ufuatiliaji wa utendaji kazi’, amesisitiza Dkt. Mwanjelwa.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameyasisitiza yote hayo wilayani Kisarawe ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma Mkoani Pwani ambapo mpaka hivi sasa ameshakutana na watumishi katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. 
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kabla ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Kisarawe. 
 Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye  lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla ya Naibu Waziri huyo  kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Kisarawe. 
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji. 
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wananchi na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wanufaika wa TASAF katika kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. Aliyeambatana naye ni  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo.

Dkt. Amani Abeid Karume ahutubia mkutano wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul, Korea

$
0
0
  Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume akihutubia katika mkutano wa  amani uitwao Global Peace Convention jijini Seoul.
Mkutano huu unaofanyika  kila baada ya miaka 2, umekuwa ukizunguka nchi mbalimbali duniani. Mwaka huu mkutano huo umefanyika nchini Korea ili kuhamasisha Korea Kusini na Korea Kaskazini waondoe tofauti zao na kuwa wamoja (OneKorea).

Dkt. Karume, ambaye ni moja wa wazungumzaji wakuu katika kujadili maswala ya violent extremism and radicalisation (misimamo mikali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, ameeleza matumaini yake kwamba iko siku kutakuwa na Taifa la Korea Moja.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Tanzania Bi. Martha Nghambu, Watanzania mbalimbali wanashiriki kwenye mkutano huo akiwema mke wa Dkt. Karume, Mama Shadya Karume, ambaye ameongozana naye. 
Bi. Nghambu amesema Mkutanio huu unatarajiwa kufungwa Februari 1, mwaka huu.

 Mama Shadya Karume akiwa na washiriki wengine kwenye mkutano huo
 Sehemu ya wshiriki wa mkutano wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
 Sehemu ya wshiriki wa mkutano wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
 Sehemu ya wshiriki wa mkutano wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
 Sehemu ya wshiriki wa mkutano wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Tanzania Bi. Martha Nghambu akiwa katika mkutano huo wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
 akiwa katika mkutano huo wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
Bi Shamira Mshangama  akiwa katika mkutano huo wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
Bi Emma Kawawa akiwa katika mkutano huo wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.

Serikali Kusimamia Maadili ya Askari Polisi

$
0
0
Serikali imesema haitakua tayari kuona Jeshi la Polisi linachafuliwa na baadhi ya Askari Polisi wasiofuta maadili huku ikisisitiza haitosita kumchukulia hatua askari atakaebanika kukiuka maadili

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akifunga mafunzo kwa Vikundi vya Ulinzi Shirikishi Visiwani Zanzibar ambapo jumla wa walinzi 681 walihitimu mafunzo hayo

Akizungumza na wahitimu pamoja na askari katika hafla hiyo Naibu Waziri Masauni alisema Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na askari polisi waadilifu huku akiweka wazi kuwepo kwa askari wasio waadilifu

“Jeshi letu la Polisi lina miiko yake katika utendaji wa kazi zake,lakini wapo askari wachache wanaovujisha taarifa kwa wahalifu, wanasaidia wahalifu kutenda makosa sambamba na kupokea rushwa,hali hiyo haikubaliki na atakebainika hatutosita kumchukukia hatua kwa mujibu wa taratibu za jeshi,” alisema Masauni

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Saleh Mohamed Saleh, aliwataka wananchi kufichua wahalifu wanaowafahamu katika makazi yao ili matendo ya uhalifu yaweze kupungua

“Polisi Jamii ni dhana pana,tunawategemea wananchi mtusaidie kufichua wahalifu katika maeneo mnayoishi maana uhalifu ukifanyika nyie ndio mnaathirika hivyo basi ni bora mkawa mabalozi wazuri katika maeneo yenu kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi,” alisema Kamishna Saleh

Katika mafunzo hayo jumla ya Walinzi Shirikishi 681 walihitimu ambapo walipitishwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo ukamataji salama,namna ya kuendesha doria,jinsi ya kumfikisha mtuhumiwa kituo cha polisi na elimu jinsi ya kujikinga na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wahitimu wa Mafunzo ya Ulinzi Shirikishi (hawapo pichani), wakati wa Kufunga mafunzo hayo katika Mkoa wa Kusini Unguja.Lengo la mafunzo hayo ni kudhibiti uhalifu Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Saleh Mohamed Saleh, akizungumza na wahitimu wa Mafunzo ya Ulinzi Shirikishi (hawapo pichani), wakati wa Kufunga mafunzo hayo katika Mkoa wa Kusini Unguja.Lengo la mafunzo hayo ni kudhibiti uhalifu Visiwani Zanzibar.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Wahitimu wa Mafunzo ya Ulinzi Shirikishi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati akizungumza na kufunga mafunzo ya Ulinzi Shirikishi Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea salamu baada ya kuwasili katika Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Ulinzi Shirikishi yaliyofanyika Visiwani Zanzibar. Lengo la mafunzo hayo ni kudhibiti uhalifu Visiwani humo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KATIBU MKUU UJENZI ATEMBELEA TEMESA NA KUKAGUA VIFAA VIPYA VYA KARAKANA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga wa kwanza kushoto akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe kuhusu vifaa vipya vya karakana vilivyonunuliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kusambazwa kwenye karakana zake mikoani, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe kulia akimpa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga katikati kuhusu mashine mpya za karakana zilizonunuliwa na Wakala huo kwa ajili ya kusambazwa kwenye karakana zake mikoani. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga wa tatu kulia akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Sylvester Simfukwe kushoto kuhusu mashine mpya ya kukagua gari na kupima uwiano wa matairi ya magari (3D Wheel Allignment) iliyonunuliwa na kufungwa katika karakana ya Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle na Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga wa nne kulia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Sylvester Simfukwe kushoto kuhusu mashine ya kukagua gari na kupima uwiano wa matairi ya magari (3D Wheel Allignment) iliyonunuliwa na kufungwa katika karakana ya Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam, wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle na Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga wa pili kulia akifurahia jambo na mafundi wa karakana ya Mt. Depot mara baada ya kumaliza kukagua karakana hiyo, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO - (TEMESA)


WAZIRI KANYASU AWAHAKIKISHIA WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU KUONGEZEWA MIKATABA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii. Mhe. Constantine Kanyasu amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya misitu Tanzania kuwa atashughulikia ombi lao la kutaka kuongezewa muda wa mikataba yao kutoka  miaka miwili hadi  mitano ya kupewa mgao wa vitalu vya miti

Pia ameahidi kuyafanyia kazi malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa ofisini kwake na wamiliki hao yakiwemo ya gharama za tozo ya ushuru wa mazao ya misitu  (Cess) inayotozwa na Halmashauri za wilaya ya Mufindi ambayo licha  Serikali kutoa maagizo ya kuzuia tozo hiyo bado wadau hao wanaendelea kutozwa.

 Mhe. Kanyasu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Rais wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu Tanzania (SHIVIMITA) na Wanachama wa Shirikisho hilo  waliomtembelea ofisini kwake  jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo,  Rais wa SHIVIMITA, Ben Sulus amemuomba Naibu Waziri  aangalie  namna ya kuwasaidia wadau hao waongezewe muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi mitano ya kupewa mgao wa vitalu vya misitu ili waweze kupata mikopo kutoka kwenye Taasisi za Kifedha kwa ajili ya kuendeshea viwanda vyao

Rais huyo ameeleza kuwa Taasisi za Kifedha  zimekuwa zikiwanyima  mikopo kwa kuhofia fedha zao kupotea kutokana na wadau hao kutokuwa na uhakika wa kuongezewa mikataba mara baada ya mikataba yao ya kuvuna magogo ya miaka miwili waliyopewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).

Amesema  endapo watapewa mikataba  ya miaka mitano watakuwa na uhakika wa kuweza kuendeleza viwanda vyao kwa vile Taasisi hizo za Kifedha zitaweza kuwapa mikopo watakayoomba na  zitakuwa na uhakika wa kurudishiwa  fedha hizo.

Katika hatua nyingine, Wadau hao wamemuomba awe mlezi wao katika jitihada wanazozichukua za kuhakikisha wanakuwa wazalishaji wa bidhaa za mwisho kama vile milango pamoja na meza   zitokanazo na mbao badala ya kujikita kuuza mbao tu.
 .Rais wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu Tanzania ( SHIVIMITA)  Ben Sulus akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu kuhusu kuongezewa muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi miaka mitano ya kupewa vitalu vya miti katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo mkoani Iringa wakati Washirika hao walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisalimia na baadhi yaWanachama wa Shirikisho la Viwanda vya misitu Tanzania mara baada ya kufanya mazungumzo nao kuhusu ombi la  kuongezewa muda wa mikataba kutoka miaka miwili hadi miaka mitano ya kupewa vitalu vya miti katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo mkoani Iringa wakati Washirika hao walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma

MGALU AWATAKA WAKANDARASI UMEME VIJIJINI KUWA NA MAGENGE KILA WILAYA

$
0
0
Na Veronica Simba – Ruangwa
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kuweka magenge yenye vifaa vya kazi katika kila wilaya nchi nzima ili kuboresha utendaji kazi wao. Alitoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti jana, Februari 26, 2019 akiwa katika ziara ya kazi katika vijiji kadhaa vya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa kuwaunganishia umeme wananchi wengi wa vijijini, Naibu Waziri alisema ni lazima wakandarasi husika wahakikishe wanakuwa na genge lenye vitendea kazi katika kila wilaya ili kusiwepo na sababu au kisingizio cha kuchelewa kuunganisha umeme katika maeneo yao.

Akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Lindi, Mgalu aliviwashia umeme vijiji vya Chimbila B, Mtakuja na Nandanga vilivyoko wilayani Ruangwa, ambapo pia alisisitiza kuwa taasisi za umma zipewe kipaumbele katika kuunganishiwa umeme kwa manufaa ya wananchi.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri aliwataka wakandarasi kuwapa kipaumbele wenye ulemavu pamoja na wazee katika zoezi la kuunganishiwa umeme kwa kutumia vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) ambavyo serikali imetoa 250 bure kwa kila eneo.

Aidha, aliwaagiza wasimamizi wa miradi ya umeme vijijini kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa agizo hilo.

Vilevile, alihamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kulipia gharama za kuunganishiwa umeme ambazo ni shilingi 27,000 tu kupitia mradi wa umeme vijijini ili waweze kupatiwa nishati hiyo na waitumie kwa shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato hivyo kuboresha maisha yao.

Alisisitiza kuwa, serikali imepitisha azimio la kuwaunganishia umeme wananchi wote walioko vijijini kwa gharama ya shilingi 27,000 tu pasipo kujali aina ya mradi unaohusika.

“Mwananchi yeyote wa kijijini ataunganishiwa umeme kwa shilingi 27,000 tu. Uwe ni umeme wa REA au TANESCO au wowote ule, gharama ni hiyo. Mkitozwa gharama tofauti, toeni taarifa kwa mamlaka husika zichukue hatua mara moja.”

Pia, aliwaelekeza Wakuu wa Wilaya katika maeneo yote nchini kuwasimamia wakandarasi hao wa miradi ya umeme vijijini na kuchukua hatua stahiki pindi wanapoona hawatekelezi kazi zao kama wanavyotakiwa.

Naibu Waziri yuko katika ziara ya kazi ya siku nne mkoani Lindi ambayo anatarajia kuhitimisha Februari 27, mwaka huu.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mtakuja, Kata ya Nandanga wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi, kabla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo, alipokuwa katika ziara ya kazi Februari 26, mwaka huu.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa umeme katika Zahanati ya Nandanga, wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi, Februari 26, mwaka huu.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha rasmi  umeme katika Zahanati ya Nandanga, wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi, Februari 26, mwaka huu.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akikabidhi Jenereta katika Kituo cha Afya Nkowe, Kata ya Nkowe, wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi akiwa katika ziara ya kazi, Februari 26, mwaka huu.

 Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mtakuja na Nandanga, wilayani Ruangwa, Februari 26, mwaka huu.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba) akizungumza na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakati akikagua utekelezaji wa miradi ya umeme Manispaa ya Lindi, Februari 26, 2019.
 Sehemu ya umati wa wananchi wa kijiji cha Chimbila B, Kata ya Mnacho, wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipofanya ziara eneo hilo na kuwasha rasmi umeme Februari 26, 2019.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnacho, Kata ya Mnacho wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipofanya ziara eneo hilo na kuwasha rasmi umeme Februari 26, 2019.

KUMBUKIZI: BAADHI YA MAMBO MAKUBWA ALIYOYAFANYA RUGE MUTAHABA ENZI ZA UHAI WAKE

$
0
0


JUMAPILI AGOSTI 5, 2017

Makonda, Ruge na Tanzania All Stars walinogesha sherehe za uwekaji jiwe la msingi la mradi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga kijijini Chongolieni. Ruge ndiye alikuwa anawezesha wasanii  nyota karibu wote wa nchi hii kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kitaifa na kijamii.

 Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya wanaounda kundi la Tanzania All Stars wakijiandaa kupanda jukwaani kutumbuiza kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Wasanii nyota wa filamu wa Bongo Movie wakiwa  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wamalize tofauti zao na kuweka maslahi ya nchi mbele wakati alipohutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Baada ya kupatanishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba walishuka jukwaani bega kwa bega huku wakitabasamu.
 Kisha wakaelekea kwenye jukwaa la wasanii wa Tanzania All Stars
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella  akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Naibu Waziri Mkuu wa Uganda Dkt Ali Kirunda Kivenjija akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.  Ashatu Kijaji wakiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakisubiri  kuwapa mikono wasanii wa Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016










































Onesheni uzalendo kwa kurejesha mikopo ya HESLB – RC Gambo

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kuonesha uzalendo kwa kujitokeza na kuanza kurejesha ili watanzania wengine wanufaike.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo leo (Jumatano, Feb. 27, 2019) jijini Arusha katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo za utambuzi kwa waajiri 12 kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambao wanatekeleza vizuri sheria ya Bodi ya Mikopo.

Taasisi hizo kutoka mkoani Arusha ni World Vision Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Kampuni ya Off-Grid Electric, Vision Fund Tanzania, Shule ya Mtakatifu Jude na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha ambazo kwa jumla zina wanufaika 410 wanaorejesha Tshs 74.08 milioni kwa mwezi.

Kwa mkoa wa Kilimanjaro, taasisi zilizopokea tuzo ni Mamlaka ya Uendelezaji wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO), Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mwenge, Tanganyika Planting Company, Kampuni ya Vinywaji ya Bonite, Kampuni ya Marenga Investment na Benki ya Biashara ya Uchumi ambazo kwa ujumla zina wanufaika 142 wanaorejesha Tshs 23.8 milioni kwa mwezi.

“Lazima wajiulize, kama Bodi (ya mikopo) isingekuwepo, labda wasingeweza kusoma, na kama wasingesoma, wangekuwa wapi?” aliuliza Mkuu huyo wa mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi na kuongeza:

“Ili kuonesha uzalendo, wanapaswa kuwa ‘honest’ na kuwataarifu waajiri wao kuwa walinufaika na mikopo na kuanza kurejesha,” aliongeza katika hafla iliyohudhuriwa na mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mikopo Dkt. Richard Masika ambaye pia ni Mwenyeki wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na majitaka Arusha.

Gambo aliwakumbusha waajiri waliopokea tuzo kuwa Serikali imekuwa ikiongeza bajeti ya fedha za mikopo ili kusomesha watanzania wengi ambao baada ya kuhitimu masomo huajiriwa na taasisi mbalimbali.

“Tangu kuingia madarakani mwaka 2015, Serikali ya Awamu Tano chini ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, imeongeza bajeti ya fedha za mikopo kutoka TZS 322.4 bilioni mwaka 2014/2015 hadi kufikia TZS 427.5 bilioni mwaka wa masomo 2018/2019,” alisema na kuongeza kuwa idadi ya wanufaika nayo imeongezeka kutoka 100,937 hadi 124,000 katika kipindi hicho.

Awali akiongea katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru alisema katika mwaka wa fedha 2017/2018, Bodi ya Mikopo ilikusanya Tshs 181.4 bilioni, na kati ya hizo, Tshs 17.4 bilioni zilikusanywa kutoka kwa taasisi binafsi na umma kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.  

Aidha, Badru alieleza kuwa sheria ya HESLB imetoa wajibu wa aina nne kwa waajiri.

“Kwanza wanapaswa kuwasilisha kwa HESLB orodha ya waajiriwa wapya ndani ya siku 28 baada ya kuwaajiri. Pili, kukata asilimia 15 kutoka kwenye mshahara ghafi wa mnufaika na kuwasilisha kwa HESLB makato hayo ndani ya wiki mbili baada ya mwisho wa mwezi,” alisema Badru.

Mkurugenzi Mtendaji huyo aliongeza kuwa waajiri pia wanapaswa pia kutoa taarifa pale mnufaika anapoanza kazi, kufukuzwa au kufariki ili kuiwezesha Bodi ya Mikopo kuhuisha taarifa zake.
Kwa mujibu wa Badru, wajibu mwingine wa kisheria ni kutoa ushirikiano kwa maafisa wa Bodi ya Mikopo wanapokuwa katika ziara za kikazi kwa waajiri ikiwemo kufanya kaguzi.

Bodi ya Mikopo ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji wa kitanzania wenye sifa za kujiunga na taasisi za elimu ya juu lakini hawana uwezo wa kiuchumi kumudu gharama hizo. Jukumu jingine ni kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika waliopata mikopo kutoka serikalini tangu mwaka 1994/1995.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA) Dkt. Richard Masika tuzo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kufuatia AUWASA kuwa mmoja wa waajiri wanaotekeleza vizuri Sheria ya HESLB. Hafla hiyo imefanyika jijini Arusha leo (Jumatano, Feb., 27, 2019). (Picha na HESLB) 
 Mwakilishi wa kiwanda cha vinywaji baridi cha Bonite cha mjini Moshi Frank Hamba akipokea tuzo ya utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gamba kufuatia kampuni hiyo kuwa moja ya taasisi zinazotekeleza vizuri sheria ya Bodi ya Mikopo. Hafla hiyo imefanyika jijini Arusha leo  (Jumatano, Feb., 27, 2019). (Picha na HESLB). 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi tuzo ya utambuzi Mwakilishi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) Moreen Mwaimale kufuatia mamlaka hiyo kuwa moja ya taasisi zinazotekeleza vizuri Sheria ya HESLB. Hafla hiyo imefanyika jijini Arusha leo (Jumatano, Feb., 27, 2019). (Picha na HESLB)


SERIKALI YAISHUKURU CHINA KWA KUIPATIA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KOMPYUTA MPAKATO 20

$
0
0

Serikali ya Tanzania imeishukuru China kwa kuipatia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kompyuta mpakato 20 zitakazowasaidia katika shughuli za ufundishaji na kuboresha utendaji kazi kwa watumishi wa chuo hicho.
Akipokea kompyuta hizo kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) amemshukuru Balozi huyo kwa mchango wao katika kuboresha Chuo hicho kwa maendeleo ya taifa.
Mhe. Mkuchika amepongeza ushirikiano ambao China imekuwa nao kwa Chuo cha Utumishi wa Umma katika masuala mbalimbali ya kuboresha utendaji ikiwa ni pamoja na watumishi wa chuo hicho kushiriki semina mbalimbali nchini China ambazo zinawasaidia kuongeza ujuzi.
Ameomba ushirikiano huu uzidi kudumu kwani China imekuwa na mahusiano mazuri na Tanzania kwa muda mrefu sasa tangu Serikali ya awamu ya kwanza mpaka sasa.
Pia, Mhe. Mkuchika amemuomba Balozi huyo kusaidia katika ujenzi wa tawi jipya la chuo hicho linalotarajiwa kujengwa jijini Dodoma baada ya Serikali kuhamishia shughuli zake Makao Makuu ya nchi Dodoma na kuongeza kuwa ujenzi wa chuo hicho utatoa fursa kwa watumishi waliohamia Dodoma na mikoa jirani kuongeza ujuzi katika Chuo hicho.
Akikabidhi kompyuta hizo, Balozi Wang Ke amesema, lengo lao ni kuboresha utendaji kazi wa watumishi katika chuo hicho hususan katika kufundisha.
Balozi Wang Ke amefafanua kuwa, anatamani kukiona Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kikitoa elimu bora zaidi na kikizalisha watumishi wa umma bora nchini.
Aidha, Balozi Wang Ke ameahidi kuendeleza ushirikiano ulioanza kati ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania na vyuo vya mafunzo vilivyoko nchini China ili kukuza ushirikiano zaidi na kuendeleza utamaduni wa kujifunza baina ya Tanzania na China.

Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maafisa kutoka ubalozi wa China nchini Tanzania wakiongozwa na Balozi Wang Ke, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi na baadhi ya watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo akitoa neno la utangulizi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo chake yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza kabla ya kukabidhi kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Charles Msonde.
 Baadhi ya watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) katika hafla fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akimkabidhi zawadi Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke alipowasili Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kukabidhi kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akipokea moja ya kompyuta mpakato kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke katika hafla fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro.

RUGE BADO TULIKUWA TUNAMUHITAJI-DKT HASSAN ABBAS

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya  Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt Hassan Abbas akizungumza na waandishi habari wakati alipokwenda kutoa pole ya Msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi wa Clouds Medio Group,Ruge Mutahaba aliyefariki Jana nchini Afrika Kusini. Dkt Abbas amesema Ruge alikuwa kijana wa pekee aliyetoa mchango wake ambao umeweza kuonekana katika kusaidia vijana wengi nchini.Amesema kuwa vijana waliobaki nao waoneshe njia zilizoachwa na Ruge kwa kuamini katika kusaidia wengine. Amesema Ruge ametutoka lakini tulikuwa na muhitaji lakini kazi ya Mungu haina makosa.

Serikali kuwekeza nguvu kwa vijana katika kilimo Biashara -Hasunga

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Serikali imesema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda kunahitaji kuwekeza nguvu kwa vijana kuingia katika Sekta ya Kilimo na kuacha kuzunguka na bahasha ya kaki ya kuomba ajira sehemu mbalimbali nchini.
Hayo ameyasema Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na Kongamano la vijana  Kimataifa kuhusu Kilimo Biashara litakalofanyika Machi 20 hadi 22 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa asilimia 60 ya wanafunzi wanahitimu vyuo vikuu wanakuwa sio wazalishaji  kutokana na kusubiri ajira hivyo Kilimo Biashara ndio suluhisho la ajira kwa vijana nchini.Hasunga amesema kuwa serikali imedhamiria kuweka mazingira ya Kilimo kwenda kisasa kwa kuhakikisha masoko ndani yanakuwa nafasi na ziada kuuza nje ya nchi.

"Vijana wakiingia katika Kilimo suala la kutembea na bahasha kwa ajili ya kutafuta ajira  litakuwa historia kwa kijana kuendesha Kilimo  hakihitaji watu wa kufanya usaili"amesema Hasunga.

Aidha amesema Kilimo kimekuewa kikilimwa kwa mazoea na kufanya kilimo kuonekana kigumu lakini serikali ya awamu ya tano tunakwenda na Kilimo cha kisasa kwa kuhusianisha masoko pamoja na viwanda kwa kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao.

Hata hivyo amesema kuwa vijana kwa kuwa na mwamko wa elimu huku wengine wakiwa wataalam watafanya chachu ya Kilimo na kufanya vijana  waliokata tamaa kuingia katika sekta ya Kilimo.Hasunga amesema nchi yeyote duniani inategemea vijana katika kupata Maendeleo  hivyo serikali haitaweza kuwaacha nyuma  katika sekta ya Kilimo.

Amesema takwimu zinaonyesha asilimia 53 ndio wanatumia jembe la mkono katika kilimo huku asilimia 27 wanatumia wanyama katika kuendesha takwimu na asilimia 20 wanatumia trekta .Nae Mwenyekiti wa Kongamano la Vijana Kimataifa Kuhusu Kilimo Biashara Majabi Emmanuel amesema kuwa  wanatarajia kuwa na washiriki 1000  kutoka sehemu mbambali wa ndani na nje ya nchi.

Amesema kuwa wameanda Kongamano hilo kutokana na vijana kujitenga katika kilimo wakati ndio chenye fursa ya kujiajiri moja kwa moja.
 Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Kongamano la Kimataifa la Vijana   kuhusu Kilimo Biashara litafanyika Jijini Dar es Salaam.

Vijana wa Kilimo Biashara wakiwa na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga mara ya kuzungumza na waandishi habari kuhusiana na Kongamano la Kilimo Biashara.

Ruge ametimiza yake katika uibuaji wa mawazo-Dkt. Tulia

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amesema aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi Ruge Mutahaba aliyefariki Jana usiku nchini Afrika Kusini ametimiza yake katika uibuaji wa mawazo na kuwa na Matokeo chanya.

Dkt Tulia ameyasema hayo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa marehemu Ruge mikocheni jijini Dar es Salaam.Amesema kuwa ni pigo kuondekewa na Ruge kwa familia pamoja na Taifa katika kutoa mchango wake kwa mawazo.

Aidha amesema kuwa wakati wa uhai wake Ruge akianzisha jambo alikuwa haileweki lakini kadri ya muda kwenda watu wanaanza kujua kuhusiana na kitu alichokianzisha."Kazi ya Mungu haina makosa ila Ruge tutaendelea kumkumbuka daima na Milele kwa mchango wake kwa vijana nchini".Amesema Dkt.Tulia Amesema kuwa msiba wa Ruge sio wa Tanzania bali Dunia nzima kutokana na yeye kufahamika kwa kazi anayoifanya.
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mapema leo nyumbani kwa marehemu Ruge Mutahaba,Mikocheni jijini Dar.

LESENI ZA MIGODI MIKUBWA KUTOLEWA KARIBUNI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao baina yake na Viongozi wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi. Kushoto ni mmoja wa viongozi hao.
Mmoja wa Viongozi wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi akizungumza jambo katika kikao hicho. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Madini, Godfrey Nyamrunda.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof.Simon Msanjila akimsikiliza mmoja wa Viongozi wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila wakijadiliana jambo na baadhi Viongozi wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi.
Mmoja wa viongozi wa jumuiya Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi, Francis Nanai ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, akizungumza jambo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi.



Na Asteria Muhozya, Dodoma 

Serikali kupitia Wizara ya Madini inakamilisha taratibu za utoaji wa Leseni kwa Migodi Mikubwa ambazo hazijawahi kutolewa nchini, huku migodi hiyo ikitarajiwa kuanzishwa hivi karibuni. 

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila alipokutana na viongozi wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi ofisini kwake, jijini Dodoma. 

Viongozi hao walikutana na Prof. Msanjila Februari 26, kwa lengo la kujitambulisha, kuelewa shughuli za serikali upande wa sekta ya madini, kupata uelewa kuhusu mabadiliko ya Sheria ya Madini na namna pande hizo mbili zinavyoweza kushirikiana katika kuendeleza sekta husika. 

Prof. Msanjila aliwakaribisha viongozi hao kwenye sekta ya madini huku akiwataka kuzishawishi kampuni mbalimbali kuwekeza nchini hususani katika shughuli za uongezaji thamani madini na kueleza kuwa, suala hilo ni miongoni mwa maeneo ambayo serikali inayapa kipaumbele ikiwemo ujenzi wa vinu vya kusafisha na kuyeyusha madini. 

Akizungumzia Sheria Mpya ya Madini ya Mwaka 2017, Prof. Msanjila amesema hakuna tatizo lolote katika utekelezaji wa sheria na kueleza kuwa, serikali kupitia wizara ya madini inapokea wawekezaji wengi wenye utayari na nia ya kuwekeza nchini huku utekelezaji wa sheria hiyo ukiwa si kikwazo na kuongeza kwamba, “hakuna mahali ambapo serikali inatengeneza sheria kwa ajili ya kumkandamiza mfanya biashara”. 

“Hakuna tatizo lolote kwenye sheria ya madini. Hata wageni huwa tunakaa nao tunawaelimisha na wanatuelewa vizuri. Kama kuna dosari ni vitu ambavyo tunaweza kuvirekebisha na tayari tumekwishakufanya hivyo kwa baadhi ya maeneo,” alisema Prof. Msanjila. 

Aidha, katika kikao hicho Prof. Msanjila alitoa ushauri kwa viongozi hao kujitangaza zaidi kuhusu kazi zao huku akiwataka kutafuta wasaa kwa ajili ya pande hizo mbili kukutana ili wizara iweze kutoa elimu zaidi kwa Jumuiya hiyo kuhusu sekta ya madini ikiwemo fursa za uwekezaji zilizopo. 

Pia, Prof. Msanjila alisema kuwa suala la kuaminiana linaweza kujengwa huku akiwataka watanzania kuwa wazalendo na namna wanavyotumia fedha za umma. Prof. Msanjila alizungumzia jambo hilo baada ya mmoja wa viongozi hao kueleza kuwa, bado kuna hali ya kutokuaminiana baina ya serikali na taasisi binafsi. 

Kwa upande wake, mmoja wa viongozi wa jumuiya hiyo, Francis Nanai ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited amemweleza Prof. Msanjila kuwa, kama viongozi wa umoja huo, wamezipokea changamoto zilizotolewa kwao na Prof. Msanjila ikiwemo ushauri wa kukutana na wizara kwa lengo la kupata ufafanuzi na elimu zaidi kuhusu sekta ya madini.

DKT NDUMBARO AONGOZA WAGENI MAADHIMISHO YA SHEREHE YA MIAKA 114 YA VITA VYA MAJIJI

$
0
0
 Balozi wa Ujerumani Tanzania na Mkewe akisaini kitabu ofisini kwa Mbunge wa Songea Mjini, Dkt Damas Ndumbaro
Mbunge wa Songea mjini Na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Damas Daniel Ndumbaro, akiwakutanisha Balozi wa Ujerumani Tanzania, Mh Dkt Deltef na Chifu wa Kingoni, Nkosi Amakhosi Zulu Gama, katika mji wa Songea kwaajili ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 114 ya vita  vya Majimaji. Wengine pichani ni mke wa Balozi, Mtemi wa Wasukuma na Fr. Dkt Kazimoto Komba (ambaye aliambatana na Balozi ) na Mlinzi wa Chifu wa Songea

NDITIYE KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU SHULE ZA SEKONDARI LUDEWA

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa nne kulia) akimkabidhi Mbunge wa Ludewa, Deo Ngalawa kompyuta 25 kwa ajili ya sekondari za Wilaya ya Ludewa, Njombe wakati wa ziara yake Wilayani humo. Anayeshuhudia katikati yao ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard 
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Njombe, Mheshimiwa Andrea Tsere akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia aliyeketi) kwa niaba ya wananchi kwa kuzipatia shule za Wilaya hiyo kompyuta 25 wakati wa ziara yake Wilayani humo
Diwani wa Viti Maalumu, Kata ya Ludewa Mjini, Mary Mapunda akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye kwa kugawa kompyuta 25 kwa shule za Wilaya ya Ludewa, ujenzi wa minara 11 ya mawasiliano, meli ya kubeba abiria Ziwa Nyasa na maendeleo ya ujenzi wa barabara za Wilayani humo. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Andrea Tsere.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kutoka mwisho) akicheza ngoma na kikundi cha burudani Wilayani Ludewa kabla ya kugawa kompyuta 25 kwa shule za wilaya hiyo na kuongea na wananchi kuhusu ujenzi wa minara 11 ya mawasiliano, meli ya kubeba abiria Ziwa Nyasa na maendeleo ya ujenzi wa barabara za Wilayani humo.


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amegawa kompyuta 25 kwa shule za sekondari za Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe zenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi kujifunzia na waalimu kufundishia, kuongeza uelewa na kupata maarifa kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuunganisha kompyuta hizo na mtandao wa intaneti ili kuwawezesha wanafunzi wa Wilaya hiyo kuongeza kiwango cha ufaulu

Nditiye amekabidhi kompyuta hizo kwa Mbunge wa Ludewa, Deo Ngalawa kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Ludewa ili ziweze kutumika kwenye shule mbali mbali zilizopo Wilayani humo

“Nimeleta kompyuta 25 ili zigawiwe kwenye shule mbalimbali ili watoto wajifunze kutumia TEHAMA pamoja na waalimu waliopewa mafunzo ya TEHAMA na taasisi yetu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)”, amesema Nditiye. Kompyuta hizo zimetolewa na UCSAF ambayo inahusika na ufikishaji wa huduma za mawasiliano vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara

Nditiye ameongeza kuwa Wilaya ya Ludewa inafahamika katika kipindi cha miaka ya nyuma kwa kuwa moja ya Wilaya saba nchini ambapo wanafunzi wake wana kipaji cha akili ukilinganisha na Wilaya nyingine zilizopo nchini ambapo ameona ni vema kuwapatia wanafunzi wa shule za Wilaya hiyo kompyuta hizo ili waweze kuongeza ufaulu, kujenga uelewa na kupata maarifa ili waweze kuwa wanafunzi vinara kama iliivyokuwa imezoeleka katika kipindi cha miaka ya nyuma. Pia, amesema kuwa Tanzania inaongoza katika matumizi ya TEHAMA katika Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mara baada ya kupokea kompyuta hizo kwa niaba ya wananchi, Mbunge wa Ludewa, Deo Ngalawa alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere kuwa, kuwe na kituo kimoja cha kutunga mitihani Ludewa ili waalimu watunge mtihani wa aina moja na waweze kumaliza kufundisha masomo ya kiada na ziada kama walivyopanga kwa muhula husika wa masomo ili waweze kuwapima wanafunzi wote kwa pamoja

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Andrea Tsere alimueleza Nditiye kuwa wataweka intaneti kwenye kompyuta hizo ili waalimu na wanafunzi waweze kupata notisi. Pia, amesema kuwa kompyuta hizo zitatumika kuinua kiwango cha elimu na zimefika muda muafaka

“Mmetusaidia sana, umeingia kwenye akili yangu ya kuinua kiwango cha elimu Ludewa,” amesisitiza Tsere wakati akimshukuru Nditiye kwa kuzipatia shule za Wilaya yake kompyuta 25. Tsere amewataka waalimu wakuu wa shule kuzitunza kompyuta hizo na kuzifanyia matengenezo pindi inapohitajika badala ya kuacha ziharibike na pasipo kuzipanga vizuri kwa sababu ni vifaa vya Serikali badala yake wanapanga lini wavichukue badala ya kuzitunza vizuri ili zisaidie wanafunzi wengi na kwa muda mrefu. Aidha, amesisitiza kwa waalimu hao kuwa kompyuta zikipotea na wao wapotee

Katika hatua nyingine, Nditiye amewaeleza wananchi hao kuwa, Wizara yake ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia UCSAF imetoa ruzuku kwa kampuni ya simu ya Halotel na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ili wajenge minara 11 kwenye maeneo ya mwambao kwa wananchi waishio Wilayani Ludewa kwa kuwa hawana mawasiliano.

“Tunahitaji Ludewa iwasiliane na dunia,” amesisitiza Nditye. Amefafanua kuwa minara tisa imejengwa na kampuni ya Halotel na miwili ni ya TTCL

Vile vile, ameongeza kuwa, ujenzi wa meli ya abiria waishio Ludewa kwa ajili ya usafiri wa Ziwa Nyasa umekamilika ambapo kwa sasa meli hiyo inafanyiwa majaribio kabla ya kuanza safari zake na Serikali inakamilisha ujenzi wa gati za kushusha na kupakia abiria kwenye mwambao wa ziwa hilo kwenye maeneo ya Manda, Lupingu, Nsele, Yiga na Nkanda ambapo meli hiyo inatarajiwa kuanza safari zake za kutoka Ludewa, Njombe hadi Kyela, Mbeya mwezi Aprili mwaka huu

“Tunataka Lupingu hadi Matema watu wapite kwa lami,” amefafanua Nditiye. Ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa Ludewa mjini na kuwaeleza kuwa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa barabara ya Lusitu – Mawengi yenye urefu wa kilomita 50 inajengwa kwa kiwango cha zege kwa gharama ya shilingi bilioni 159 ambapo tayari mkandarasi wa kutoka nchi ya Korea yupo na anaendelea na ujenzi wa barabara hiyo ili iweze kupitisha madini ya Mchuchuma na Liganga 

Ngalawa amewaeleza wananchi kuwa anamshukuru Nditiye kwa kuwa alifanya ziara kutoka Lupingu hadi Manda mwaka jana mwezi wa tatu akiwa na miezi minne tu tangu alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri na kushuhudia ukosefu wa mawasiliano kwa wananchi waishio mwambao na sasa minara 11 imejengwa ambapo tayari minara mitatu ya Nkanda, Mawengi na Mahong’olo imewashawa na meli ya abiria pia itaanza safari zake

Tsere alimshukuru Ngalawa kwa kumleta Nditiye ambapo alisafiri na boti siku nzima Ziwani mwaka jana mwezi wa Machi na kushuhudia ukosefu wa mawasiliano kwa kuwa tangu dunia iumbwe wananchi wa mwambao hawajawahi kupata mawasiliano na sasa wanawasiliana.

KATIBU MKUU OFISI YA RAIS DR. MOSES KUSILUKA AKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO NA UONGOZI WA TASAF.

$
0
0
Na Estom Sanga- DSM 

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Dr. Moses Kusiluka amesema Serikali inatambua Mchango muhimu unaotolewa na nchi wahisani na Wadau wa Maendeleo katika kufanikisha jitihada za Serikali za kukabiliana na umasikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF. 

Dr. Kusiluka amesema jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaondolea wananchi adha ya umaskini zimeendelea kufanikiwa na kupongeza ushirikiano uliopo baina ya Serikali kupitia TASAF na Wadau wa Maendeleo ambao amesema unapaswa kuendelezwa ili kuwanufaisha Wananchi. 

Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Rais ameyasema hayo alipokutana na Menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF na Wadau mbalimbali wa Maendeleo katika ofisi ndogo za Mfuko huo jijini Dar es Salaam katika kikao ambacho hufanyika kila mwezi kujadili utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo. 

Dr. Kusiluka amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuendelea kusimamia na kutekeleza kwa karibu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF ili jitihada hizo na nyingine ambazo zinafanywa na Serikali zinazolenga katika kupunguza umaskini uliokithiri miongoni mwa wananchi ziweze kufanikiwa na kuwa endelevu. 

Amewahakikishia Wadau hao wa Maendeleo kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inatambua Mchango wao katika kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF na kuwa itaendelea kushirikiana nao katika kufanikisha malengo ya Mpango huo ambao kwa kiwango kikubwa unaonyesha mafanikio. 

Akizungumza katika kikao kazi hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga amesema mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini yametokana na ushirikianao wa Serikali na Wadau hao wa Maendeleo ambao Wamewezesha kuzihudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki moja ambayo ni asilimia 70 ya vijiji na shehia nchini kote kwa ufanisi . 

Kwa upande wa Wadau hao wa Maendeleo ,Kiongozi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia hapa nchini Bw.Mohamed Muderis amesema kumekuwa na mwitikio mkubwa wa Wadau wa Maendeleo kuendelea kuchangia utekelezaji wa Shughuli za TASAF kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kuipongeza Serikali kwa usimamizi wa karibu ambao umesaidia kupatikana kwa mafanikio hayo. 

Hata hivyo Bw. Muderis ameishauri serikali kupitia TASAF kuweka mkakati thabiti utakaowezesha sehemu ya pili ya utekelezaji wa Awamu ya tatu unaotarajiwa kuanza hivi karibuni kuwa na mtiririko mzuri wa fedha za kugharamia shughuli za Mpango kutokana na kuwa utatekelezwa katika maeneo makubwa zaidi ya awamu inayomalizika na hivyo kuhudumia Walengwa wengi zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga(kushoto) akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Dr. Moses Kusiluka (kulia) katika ofisi ndogo ya mfuko huo jijini Dar es Salaam ambako amekutana na Wadau wa Maendeleo na Uongozi wa TASAF.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Dr. Moses Kusiluka (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga (kushoto) wakiwa katika kikao kazi cha Wadau wa Maendeleo na Menejimenti ya TASAF katika ofisi ndogo ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam.

 Sehemu ya Wadau wa Maendeleo na Menejimenti ya TASAF wakiwa katika kikao kazi ambacho pia kimehudhuriwa na Katika Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Dr. Moses Kusiluka kujadili utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images