Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

SEKTA ZA AFYA NCHINI ZA SHAURIWA KUITEKELEZA AFYA MOJA

0
0
Na OWM DODOMA.
Afya Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo.

Kwa kutambua  umuhimu wa  Afya moja nchini, sekta za Afya zenye kujumuisha wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wametakiwa kuanza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia dhana hiyo ili uimarishaji wa Afya ya binadamu uwe wa Ufanisi na matokeo bora.

Akiongea wakati wa warsha ya  maafisa viungo wa Afya moja kutoka Wizara, Idara, Taasisi,  Mashirika ya serikali na ya Kimataifa, mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019, Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Matamwe Jimmy, amefafanua kuwa tayari wataalamu hao wanao Mkakati wa kuzileta pamoja  Sekta za Afya kwa ajili ya kuzuia, kukinga na kuthibiti madhara na magonjwa yanayoikumba nchi yetu, yaani magonjwa ambukizi kati ya wanyama na binadamu pamoja na usugu wa vimelea vya magonjwa hivyo ni wakati wa kutekeleza mkakati huo kwa  kuitumia dhana ya Afya moja.

“Ninaamini kwamba, wote mnafahamu kuhusu tishio kubwa la magonjwa kama vile homa ya bonde la ufa, kwenye nchi za Afrika Mashariki , virusi vya Ebola Afrika Magharibi, kusambaa kwa kiasi kikubwa cha ugonjwa wa mafua ndege, (HPAI), matatizo ya kupumua yanayosababishwa na virusi vya Corona, mlipuko wa homa ya Lassa huko Africa Magharibi na homa ya Zika huko Amerika ya Kusini, kwa hiyo mifano michache magonjwa hayo yamekuwa tishio kubwa kwa afya ya binadamu na wanyama duniani kote.” Amesisitiza Kanali Matamwe.

Wakiongea wakati wa warsha hiyo wataalamu wa sekta za Afya hizo wamebainisha kuwa tayari wamekubaliana mfumo wa kutoa taarifa na kuhuisha utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana na USAID na   Chemonics International wameandaa mkutano wataalam hao.
 Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akieleza  jambo wakati  wa warsha ya  maafisa viungo wa Afya moja mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019.
 Mtaalamu wa Afya moja toka sekta ya Afya ya Mifugo, Dkt. Joseph Masambu akichangia juu ya  umuhimu wa dhana ya Afya moja nchini wakati  wa warsha ya  maafisa viungo wa Afya moja mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019.
 Baadhi ya Wataalamu wa sekta za Afya , sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira  wakifuatilia  warsha ya  maafisa viungo wa Afya moja mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019.
 Mtaalamu wa Afya moja toka sekta ya Afya ya Binadamu, Profesa. Japhet kilewo akichangia juu ya  umuhimu wa dhana ya Afya moja nchini wakati  wa warsha ya  maafisa viungo wa Afya moja mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019.
Maafisa viungo wa Afya moja kutoka Wizara, Idara, Taasisi,  Mashirika ya serikali na ya Kimataifa, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa warsha ya Uongozi wa  maafisa viungo wa Afya moja mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019.

Buhari apata ushindi wa kwanza Nigeria

0
0
Waangalizi wa uchaguzi wanakosoa kuchelewesha ufunguaji wa vituo katika maeneo mengi nchini Nigeria, wakisema uchelewashaji huo na kuahirishwa kwa uchaguzi huo kwa wiki nzima viliwakatisha tamaa watu wengi kupiga kura.

Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afrika umesema katika ripoti yake kuwa uchaguzi ulipita kwa amani kwa sehemu kubwa licha ya matukio kadhaa wa kadhaa ya vurugu na udanganyifu.

Kundi la Situation Room, ambalo ni muungano wa mashirika ya kiraia yaliosimamia uchaguzi huo kw apamoja, limesema watu wasiopungua 39 waliuawa nchini Nigeria kote kwenye siku ya uchaguzi.

Kundi la waangalizi wa Jumuiya ya Madola limezitaja vurugu zilizoukumba uchaguzi huo kuwa suala linalohuzunisha na mwenyekit wake, rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema Nigeria ingeweza kufanya vizuri zaidi.

"Kumekuwa na ugumu wa kimandalizi, kilojistiki na kiufundi katika uchaguzi huu ambavyo tunajua na kuamini kuwa INEC na wadau wote nchini Nigeria watahitaji kuvishughulikia.

Jambo la pili, vurugu zinazohusiana na uchaguzi na upotevu wa maisha vilivyotokea katika maeneo kadhaa vinasikitisha. Naamini Nigeria inaweza kufanya vizuri zaidi. Vurugu hazina nafasi katika demokrasia ya kisasa."

Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya Maria Arena amesema kura hiyo ilitatizwa na kosoro za kiutendaji zilizosababisha ugumu kwa wapigakura.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na makamu wake Yemi Osibanjo.

WATANO KIZIMBANI KWA KUINGIZA KEMIKALI NCHINI

0
0
 WAFANYABIASHARA watano wa jijini Dar ea Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka manne ya kuingiza kemikali bila kuwa na kibali cha Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA).

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali, Wankyo Simon amewataja wfanyabiashara hao kuwa ni Jumanne Mazunde, Godfrey Kiwelu, Nsia Mbonika, Chanikan Mhina na Joseph Omoll.
Wakisomewa mashtaka yao leo Februari 26.2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, imedaiwa,  Septemba 13, 2017 huko katika maeneo ya Ubungo Maziwa Dar es Salaam, mshtakiwa Mazunde aliingiza kemikali mbalimbali zenye uzito wa kilogramu 1,514.5 kutoka Nairobi nchini Kenya bila kibali cha mkemia.

Pia mashitakiwa, Godfrey na Mbonika wanadaiwa Septemba 13, 2017 maeneo ya Ubungo Dar es Salaam, waliingiza kemikali zenye uzito wa kilogramu 87,  zilizoingizwa kutoka Nairobi nchini Kenya bila kibali cha mkemia. Imeendela kudaiwa kuwa, siku na mahali hapo mshtakiwa, Mhina aliingiza kemikali zenye uzito wa kilogramu 100 bila kuwa na kibali cha mkemia.

Katika shitaka la nne, Septemba 13, 2017 maeneo ya Ubungo washtakiwa wote waliingiza kemikali bila kuwa na kibali. Hata hivyo, washitakiwa  wamekana mashitaka hayo na kwa mujibu wa upande wa mashitaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Akiwasomea msharti ya dhamana, Hakimu Shaidi amewataka washitakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka serikalini na vitambulisho watakaosaini kulipa Sh milioni 10. Hata hivyo, washitakiwa watatu walipata dhamana huku wawili walirudishwa rumande kwa kukosa dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 12 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa

WAZIRI WA KILIMO AZINDUA MATREKTA MAPYA YA SONALIKA JIJINI DAR

0
0
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi moja kati ya Matrekta mapya ya ya Sonalika, yanayosambazwa na Kampuni ya Rellance, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, leojana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kulia) ni Meneja Masoko, Sajal Bagga na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Stephen Mloshi. Picha na Mafoto Media.
Furaha baada ya uzinduzi huo....
WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Stephen Mloshi, akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo.




Sehemu ya washiriki katika hafla ya uzinduzi huo.

Wawakilishi wa benki ya CRDB waliohudhuria hafla hiyo wakitambulishwa.

Waziri akimpongeza mmoja wa wakulima walionufaika na Matrekta hayo.... kutoka Mbinga
Waziri akionyesha zawadi aliyokabidhiwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo (kushoto).
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi


Waziri katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

WATUMISHI WA UMMA NCHINI MARUFUKU KUTUMIKA KISIASA

0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi wa umma nchini kutotumika kisiasa kwani uwepo wao una lengo mahususi la kuboresha utoaji huduma wenye viwango stahiki ikiwa ni pamoja na kuijenga Serikali ili iweze kuleta maendeleo kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri huyo wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla ya kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Kisarawe ili  kujiridhisha na utekelezaji wa mpango huo. 
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, serikali inahitaji utaalam wa watumishi wa umma katika kujenga utumishi wa umma imara uliotukuka, utumishi ambao utaziwezesha taasisi za umma zote nchini kutoa huduma stahiki kwa wananchi. 
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, hategemei kumuona mtumishi wa umma yeyote akijihusisha na siasa zinazosababisha kukwamisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa kuwasimamia kikamilifu Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri ili kujenga ushirikiano wa kiutendaji kati ya Makatibu Tawala wa Wilaya  na Wakuu wa Wilaya kwa lengo la kuboresha utoaji huduma bora kwa umma. 
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amehimiza ushirikiano wa watendaji hao ili kurahisisha utendaji kazi wa shughuli za serikali kwa ujumla, na kuongeza kuwa, serikali iliyopo madarakani ni moja tu inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, hivyo anashangaa inakuwaje Makatibu Tawala wa Wilaya wasiarifiwe masuala yanayoendelea katika halmashauri.

“Kuanzia sasa barua yoyote ya kiutendaji itakayotoka mkoani kuelekezwa kwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, ni lazima nakala ya barua hiyo ielekezwe pia kwa Makatibu Tawala wa Wilaya ili wafahamu kinachoendelea na kumuarifu Mkuu wa Wilaya kufanya ufuatiliaji wa utendaji kazi’, amesisitiza Dkt. Mwanjelwa.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameyasisitiza yote hayo wilayani Kisarawe ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma Mkoani Pwani ambapo mpaka hivi sasa ameshakutana na watumishi katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. 
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kabla ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Kisarawe. 
 Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye  lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla ya Naibu Waziri huyo  kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Kisarawe. 
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji. 
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wananchi na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wanufaika wa TASAF katika kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. Aliyeambatana naye ni  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo.

NIKIKABIDHIWA TIMU 'AZAM' HUWA SITAKI MASIKHARA- IDD CHECHE

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KOCHA wa muda wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amefunguka kuwa jambo kubwa linalombeba kila akikabidhiwa timu hiyo, ni kutokana na kuifahamu vema na kutopenda masikhara.

Cheche anayesaidiana na Meja Mstaafu, Abdul Mingange, wote wakiwa makocha wa timu za vijana za Azam FC, wameshika nafasi hizo kwa muda baada ya kusitishiwa mikataba kwa Hans Van Der Pluijm na Msaidizi wake, Juma Mwambusi.

Wawili hao waliiongoza Azam FC jana usiku kuichapa Rhino Rangers mabao 3-0 na kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), mabao yakiwekwa kimiani na kiungo mshambuliaji Tafadzwa Kutinyu, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na mshambuliaji Obrey Chirwa.

Cheche amesema  kuwa kwa sasa walichofanikiwa ni kunyanyua ari za wachezaji na kuwajenga kisaikolojia jambo ambalo limepelekea ushindi huo mnono.

“Mimi huwa ni mshindani, napenda kushindana, sipendi kupoteza, ninapopata nafasi ya kuishika timu huwa sipendi masikhara, kingine naifahamu vizuri Azam FC wachezaji wengi nawajua, nawapongeza vijana kwa kazi nzuri na kubwa waliyofanya na kupata ushindi huu muhimu,” alisema.

Kocha huyo mwenye ushawishi mkubwa ndani ya viunga vya Azam Complex, aliwaomba mashabiki wa timu hiyo kuwapa ushirikiano kwa kipindi hiki kifupi walichokuwa na timu hiyo.

“Nawaahidi mambo mazuri yanakuja kama walivyonizoea, cha muhimu ni mashabiki kutupa ushirikiano kwa kujaa kwa wingi uwanjani na kuisapoti timu pia, hata pale atakapokuwa amepatikana kocha mpya,” alisema.

Mara baada ya mchezo huo, Azam FC inaelekeza nguvu zake zote kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya African Lyon, utakaofanyika Ijumaa hii.

Mabingwa hao, sasa wamerejea kwenye mwendo wa ushindi ambapo kwa kutoa dozi hiyo kunawafanya kupata ushindi wa kwanza tokea kuanza kwa mwezi huu Februari katika mechi sita ilizocheza.

MAFUNZO YA KUNDI LA NNE YA MWANAMKE WA WAKATI UJAO YAZINDULIWA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
CHAMA cha waajiri Tanzania (ATE) wamezindua mafunzo ya kundi la nne  kwa wafanyakazi wa kike ikiwa ni programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) kwa ajili ya kuboresha ufanisi kwa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi nchini Tanzania.

Mafunzo hayo yataendeshwa kwa muda wa miezi 9 na yatakuwa wanakutana mara 14 ikiwemo na kufanya mtihani na lengo kuu itakuwa ni kulenga zaidi katika kuwapa mwongozo bora wafanyakazi wa kike ili waweze kumudu nafasi zao za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.



Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka amesema kuwa wameshasajili wafanyakazi wa kike 31  kutoka makampuni tofauti ambapo wapo waliolipiwa na kampuni zao na wale waliojilipia wenyewe.

Dkt Mlimuka amesema mafunzo haya yatachochea mazingira bora ya kujifunza na kuendeleza viongozi kwa maendeleo ya kampuni na yatawapa ujasiri wanawake kuomba nafasi za uongozi sehemu mbalmbali ikiwemo bodi ya wakurugenzi..

Amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa juu ya uongozi, ufanisi katika bodi, ufanisi katika mawasiliano, kuomba nafasi za juu za uongozi  na katika maisha yao kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) kwa muda wa siku 14 muda wa darasani kwa kozi zote  ndani ya miezi tisa na yatafanyika kwa mfumo wa kuunganishwa na shughuli za kila za muhusika mahali pake pa kazi.



" Tumewasajili wahitimu wote kama wafanisi wa bodi za wakurugenzi na uongozi, ujuzi huu utaendelezwa katika kizazi cha baadae lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na mazingira bora ya kazi," amesema.

Amesema kuwa, makampuni mengi yanayoonozwa na wanawake yamekuwa na ufanisi mkubwa sana kwenye maendeleo na yamekuwa na tija na mchango mkubwa na kwa mafunzo haya ya nne kumekuwa na muitikio mkubwa sana.

Dkt Mlimuka aliongeza kuwa ATE inatambua ushiriki kutoka makampuni hayo kama chachu ya kuendeleza mipango mikakati katika usawa, elimu bora na mazingira bora ya kazi katika kuinua uchumi wa nchi.

Kwa upande wa Naibu Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB Ester Kitoka amesema kuwa wameamua kudhamini kozi ya nne ya mwanamke wa wakati ujao kwani yamekuwa na umuhimu mkubwa sana katika jamii.

Amesema tafiti zinaonesha kuwa mwanamke ana mchango mkubwa sana katika makampuni na wamekuwa na tija na hicho kimeweza kuwapelekea na kuwaleta wafanyakazi wao wa CRDB kuja kupata mafunzo hayo uweze kuwasaidia katika nafasi nyeti za juu.

Moja ya washiriki wa mafunzo hayo, Mkuu wa Idara wa Rasilimali watu wa Benki ya I & M, Martha Kimweri  amesema, mafunzo haya yanawaleta wanawake pamoja na kubadilishana mawazo, kujifunzam na kuweza kutatua changamoto wanazokutana nazo katika majukumu ya kila siku.

Programu huu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) ilizinduliwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu mwaka 2016 ambapo ililenga zaidi kuongeza ufanisi kwa waajiri wa kike mahali pa kazi pamoja na mambo mengine ilibanishiwa kuwa wahusika wataunda mtandao wa kubadilishana uzoefu katika fani mbalimbali.
Mkurugenzi wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka  akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua mafunzo ya awamu ya nne ya wafanyakazi wa kike ikiwa ni programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) kwa ajili ya kuboresha ufanisi kwa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi nchini Tanzania.

Naibu Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB Ester Kitoka akielezea mada katika ufunguzi wa mafunzo ya awamu ya nne  ya wafanyakazi wa kike ikiwa ni programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) kwa ajili ya kuboresha ufanisi kwa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi nchini Tanzania. Picha ya chini washiriki wakiwa wanasikiliza makini.

TFF IFIKAPO MACHI 5 TUTANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA

0
0
Na Agness  Francis, Blogu ya Jamii
KAMATI ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania  (TFF)  imefunguka rasmi kuwa itatangaza tarehe ya uchaguzi wa klabu ya Yanga  ifikapo machi 5 mwaka huu. Hiyo ni  baada ya  kamati hiyo kukaa kimya kwa muda mrefu na kuleta sintofahamu kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo iliyokita maskani yake Jangwani maeneo ya Kariakoo Jijini Dar Da Salaam.

Amesema hayo mwenyekiti wa kamati  ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania  (TFF)  Ally Mchunguhela  kuwa tayari ameshakutana na viongozi wa klabu ya Yanga  na kukubaliana  kuwa sasa  kinachosuburiwa ni kutangazwa kwa tarehe rasmi ya uchaguzi huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa klabu hiyo.

Mchungahela amesema kuwa uchaguzi huo ulipaswa kufanyika januari 13 mwaka huu  lakini kutokana na  baadhi ya wanachama wa Yanga kufungua  kesi mahakamani kusimamisha mchakato huo  na kupelekea zoezi zima  la uchaguzi  kusimama.

"Uchaguzi wa Yanga  utafanyika na hakutakuwa tena na mchakato mwingine  mpya  bali utaendelea palepale  ulipokuwa umefikia ,na  ifikapo Tarehe 5 Machi tutatangaza rasmi tarehe  mpya ya uchaguzi wa  Yanga na naamini utafanyika",amesema mchungahela.

Aidha Mchungahela amesema kuwa  mpaka kufikia tarehe itakayotangazwa rasmi ya uchaguzi  huo kila kitu kitakwenda sawa na hakutakuwa tena na kizuizi kingine ambacho kitafanya mchakato mzima kusimama.

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AFUNGUA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LEO UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  amesema kuwa suala la kupambana na rushwa lina umuhimu mkubwa katika maendeleo ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa ikizingatiwa kwamba vitendo hivyo vinazorotesha uchumi na maendeleo.

Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Chukwani mjini Zanzibar wakati akizindua Mkutano wa Nne wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambapo kwa mwaka huu unafanyika hapa Zanzibar.

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alieleza kuwa kuwepo kwa Mswada wa rushwa katika mkutano wa Bunge hilo mwaka huu kuna umuhimu mkubwa kwani utasaidia katika kupambana na vitendo vya rushwa ambavyo vimekuwa vikiathiri sana uchumi na maendeleo ya nchi na wananchi wake.

Amesema kuwa Mkutano huo ambao katika Miswada yake ambapo miongoni mwao kutakuwepo Mswada huo ambao utajadiliwa unakwenda sambamba na juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na nchi wanachama katika kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa na uhujumu wa uchumi.

Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika jitihada zake za kukomesha vitendo vya rushwa imeunda Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kwa lengo la kushughulikia suala zima la kupambana na rushwa.

Alisema kuwa juhudi hizo zinaendelea kwa mashirikiano ya pamoja na wananchi hatua ambayo imepelekea Mamlaka hiyo kuweza kupiga hatua kubwa.

Aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli imeongeza juhudi zaidi katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa kwa kuweka mikakati mbali mbali.

Alisema kuwa Serikali zote mbili ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeimarisha usimamizi wa sheria na kuongeza Bajeti katika sekta ya sheria sambamba na kuongeza wataalamu ili kusimamia kesi zinazohusiana na rushwa.

Hivyo, Rais Dk. Shein alisema kuwa juhudi hizo zitasaidia sana pamoja na zile sheria zitakazotungwa na Bunge hilo ambazo zote kwa pamoja zinaweza kufikia lengo lililokusudiwa.

Aidha, Rais Dk. Shein alisisitiza suala zima la kuzingatia umhimu wa maadili na tabia njema katika kutekeleza majukumu ya viongozi hao hasa katika wakati huu ambao teknolojia na mifumo ya maisha imebadilika na baadhi ya wakati hupelekea Wabunge kufanya vitendo ambavyo vinahitaji umakini na maamuzi ya busara ili waweze kulinda hadhi yao.

Alisema kwamba inatia moyo kuona kwamba Ukanda wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa Kanda zinazoongoza katika ukuaji mzuri wa uchumi duniani ambapo katika mwaka wa 2017 uchumi ulikuwa kwa asilimia 4.6 ikilinganishwa na mwaka 2016 ambapo uchumi ulikuwa asilimia 4.4.

Alieleza kuwa hayo ni mafanikio makubwa ambayo yanapaswa kuendelezwa  huku akisisitiza kuwa kutokana na Afrika ya Mashariki kuwa na zaidi ya watu milioni 162 hali hiyo inapelekea kuwepo kwa soko kubwa la bidha mbali mbali pamoja na huduma muhimu.

Pia, alieleza kuwa Afrika Mashariki ina ardhi kubwa yenye kilomita za mraba 1.82 milioni ambayo ni vyema rasilimali hiyo ikatumika vizuri ili iweze kuleta tija kwa nchi wanachama.

Vile vile, Rais Dk. Shein alipongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na nchi wanachama katika kuhakikisha kwamba Jumuiya hiyo inafikia malengo yake hasa katika suala zima la kukuza uchumi, uimarishaji wa utawala Bora, uismarishaji wa sheria pamoja na uimarishaji wa amani na utulivu.

Rais Dk. Shein ameeleza kutiwa moyo sana na juhudi za Umoja huo za kuimarisha lugha ya Kiswahili ambayo hivi sasa imekuwa ni lugha inayounanisha wanachama katika shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii.

Alieleza kuwa Zanzibar inathamini sana fursa iliyopewa ya kuwa Makamo Makuu ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki na kuahidi kuwa fursa hiyo itaitumia vizuri ili kuhakikisha malengo yaliokusudiwa yanafikiwa.

Dk. Shein alimuhakikishia Spika wa Bunge hilo Martin Ngonga kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza na kuitangaza lugha ya Kiswahili na kufahamisha kwamba kupitia Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) imekuwa ikiandaa makongamano mbali mbali ya Kiwahili ambayo yanajumuisha wataalamu kutoka sehemu mbali mbali duniani.

Alisema kuwa hatua hiyo ina lengo la kukiimarisha na kukuza matumizi sahihi ya Kiswahili fasaha kwa kuangalia kwamba Zanzibar ndio chimbuko la Kswahili sanifu.
Rais Dk. Shein alisema anaamini kwamba Jumuiya hiyo inaweza kuwa eneo muhimu la kiuchumi duniani, hivyo jitihada zaidi zinahitajika katika utekelezaji wa malengo makuu yaliopangwa na Jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kushajiisha uekezaji, kuendeleza sekta ya utalii, viwanda, elimu na kutilia mkazo  suala zima la kuongeza ajira na kuimarisha miundombinu.

Pamoja na hayo, Rais Dk. Shein aliitaka Jumuiya ya Afrika Masharik kupitia Bunge lake hilo kuchukua jitihada katika kupambana na vitendo mbali mbali vyenye kuathiri uchumi ikiwemo suala zima la utakasishaji wa fedha.

Vile vile, Rais Dk. Shein alieleza haja ya kuendeleza teknolojia ya Habari na Mawasiliano huku akiwasisitiza Wabunge wa Bunge hilo kufanya kazi kwa mashirikiano mazuri na Mabunge mwengine ya nchi wanachama ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mzuri zaidi.

Aidha, Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kulipongeza Bunge hilo kwa kufanya mkutano wake huo hapa Zanzibar na yeye kupata fursa kwa mara ya pili kuufungua mkutano huo na kutoa shukurani zake kwa kuweza kukaa pamoja na chombo hicho muhimu cha kutunga Sheria.

Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumpongeza Spika wa Bunge hilo kwa  kuchaguliwa kuwa Spika wa tano na kuweza kukiongoza chombo hicho huku akiwapongeza Wajumbe wote wa Bunge hilo kwa kuchaguliwa kukiongoza chombo hicho muhimu katika Afrika Mashariki.

Pamoja na hayo, alisifu utaratibu wa Bunge wa kufanya mikutano katika miji ya nchi wanachama jambo ambalo linapelekea wananch kufahamu majukumu ya chombo hicho ambapo alisema utaratibu huo unaenda sambamba na falsafa ya kuweka umoja na mshikamano kwa watu wa Afrika Mashariki.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein ameleza kufurahishwa kwake na moja ya Miswada ambayo itajadiliwa katika Bunge hilo ambayo ni pamoja na Mswada wa vita dhidi ya rushwa, masuala ya kijinsia,ulemavu pamoja na mada nyengine zitakazojadili vitendo vya ugaidi vilivyojitokeza nchini Kenya.

Nao Wabunge hao walitoa shukurani kwa Rais Dk. Shein kwa heshima kuwa aaliyowapa ya kwenda kuzindua mkutano wao huo na kueleza kufurahishwa kwa kiasi kikubwa na hotua aliyoitoa ambayo imewapa matumaini makubwa.

Nae Spika wa Bunge hilo Martin Ngoga alitoa shukurani kwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na uongozi wake chini ya Spika wa Baraza hilo Zubeir Ali Maulid kwa mashirikiano mazuri wanayoyapata ambayo ni chachu katika utekelezaji wao wa kazi.

Aidha, Spika huyo alieleza umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika Umoja huo pamoja na Wajumbe wa Bunge hilo na kueleza mikakati waliyoiweka katika kuhakikisha lugha hiyo inatumika vyema ndani ya Bunge hilo pamja na nchi zote za Jumuiya hiyo.

Nae Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid alieleza mashirikiano mazuri yaliopo kati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Bunge hilo Afrika Mashariki na kueleza mafanikio makubwa yaliopatikana katika mashirikiano hayo.
Katika uzinduzi huo wa Mkutano wa (EALA) ambao unatarajiwa kuwa wa siku 10 moja, viongozi mbali mbali walihudhuria akiemo Spika wa Bunge hilo Martin Ngoga, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Wenyeviti na Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid, Spika Mstaafu Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wajumbe wa Bunge hilo la Afrika Mashariki.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikagua gwaride maalum llililoandaliwa kwa ajili ya Ufunguzi wa Bunge la Afrika Mashariki katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga, alipowasili katika viwa vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.(Picha na IKULU)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga wakiingia katrika ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya Ufunguzi.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Afrika Mashariki lililofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)

Baadhi ya wabunge wa bunge la Afrika Mashariki wakisikiliza hotuba  ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)

SIMBA YAPELEKA SALAMU YA KAMWENE KWA LIPULI, YASHINDA BAO 3-1

0
0
Na Agness Francis, blogu ya jamii. 

KAMWENE Lipuli!Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara Simba SC kufanikiwa kuuvunja mwiko kwa kuwatandika Wanapaluhengo Lipuli FC mabao 3-1 katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili msimu huu 2018-19.

Mchezo huo wa Simba na Lipuli umefanyika leo Februari 26, 2019 katika dimba CCM Samora lililopo mkoani Iringa .Mchezo ulikuwa ni wa vuta ni kuvute kwa timu zote mbili. Simba walionekana kuwa na morali zaidi ya kutafuta ushindi wa alama tatu ili kujiweka mahali pazuri katika msimamo wa Ligi Kuu.Katika mchezo huo wa leo, kipindi cha kwanza dakika ya tano Simba waliandika bao la kwanza kupitia mchezaji wake mahiri Cloutus Chota Chama a.k.a Triple C.Mchezaji wa Lipuli Paul Nonga aliisawazishia timu yake dakika ya 19 .

Kabumbu liliendelea kuchezwa ambapo kila timu walikuwa wakionesha umakini na kushambuliana kwa zamu.Dakika ya 43 yule yule Cloutus Chama aliifungia tena timu yake goli la pili la kuongoza kupitia mkwaju wa penalti, mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika wachezaji wanakwenda mapumzikoni Simba walikuwa wanaongoza bao 2-1 dhidi ya Lipuli. 

Kipindi cha pili cha mchezo huo kilianza kwa timu ya Simba wakiwa na kasi zaidi huku Lipuli wao walionekana kupotea mchezoni ambapo waliwapa fursa nyingine wachezaji wa Simba kuongeza goli la tatu katika dakika ya 57 ambapo mshambuliaji aliye kwenye ubora wake Medie Kagere a.k.a Mzee wa Jicho Moja kufunga. 

Katika msimamo wa Ligi Kuu, Simba ikiwa nafasi ile ile ya 3 akiwa na alama 48 na michezo 19,Yanga wao wakiwa vinara wa ligi hiyo wakiwa na alama 61 michezo 25,wakifuatiwa na Azam kwenye alama 50 akiwa ameshacheza michezo 25 pia.
 Simba SC
Lipuli FC

BREAKING NEWZZZ: MKURUGENZI WA CLOUDS FM RUGE MUTAHABA AFARIKI DUNIA

0
0
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba amefariki dunia leo nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu. Kufuatia msiba huo Rais Dkt John Pombe Magufuli ametoa pole kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI

AMIN.


RC KAGERA AMALIZA MGOGORO WA WAFUGAJI NA WAKULIMA ULIODUMU ZAIDI YA MIAKA KUMI,ATOA WIKI MOJA WAVAMIZI KUONDOKA

0
0
Na Sylvester Raphael
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amemaliza mgogoro wa wakulima na wafugaji uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi na moja katika Kijiji cha Kahundwe kata Chanika Tarafa Kituntu Wilayani Karagwe,baada ya kukutana nwa wananchi wa kijiji hicho na kutoa msimao wa Serikali na kuonya juu ya uvunjifu wa amani uliowahi kutokana na mgogoro huo mwaka 2008.
Awali kabla ya kwenda Kijijini Kahundwe Februari 26, 2019 kuwasikiliza wananchi hao wakulima (wavamizi) na Wafugaji na kumaliza mgogoro huo Mkuu wa Mkoa Gaguti aliunda timu ya wataalam kupitia nyaraka mbalimbali kuhusu kijiji hicho na kuwasikiliza wananchi pande zote mbili ili kubaini ukweli na chanzo cha mgogoro ambapo timu hiyo ilifanya kazi yake na kuwasilisha majibu kwake.
Mkuu wa Mkoa Gaguti baada ya kupitia taarifa ya timu aliyoiunda na kuwasili Kijijini Kahundwe na kusikiliza pande zote mbili za Wakulima (Wavamizi) na wafugaji aliwaeleza wananchi hao kuwa tayari Serikali ilishabaini ukweli wa ni nani mmiliki halali wa eneo hilo la Kijiji cha Kahundwe kati ya Wakulima na Wafugaji.
“Mwaka 1987 mamlaka za vijiji vinne zilikaa na kukubaliana kutenga eneo la kufugia  mifugo yao na lilitengwa eneo la Kijiji Kahundwe kuwa eneo la wafugaji na kusajiliwa kisheria, lakini kuanzia mwaka 2008 hadi 2015 baadhi ya wananchi kutoka maeneno mengine walivamia eneo hilo na wavamizi sita walikamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na kupatikana na hatia na kufungwa jera miezi sita kila mmoja.” Alieleze Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Mkuu wa Mkoa Gaguti aliendelea kuwaeleza wananchi kuwa tangu wakati huo kumekuwa na uvamizi wa wakulima kutoka nje ya Kijiji hicho na kuleta mgogogro mkubwa kati yao na wafugaji. Aidha, alisema kuwa Serikali tayari imebaini ukweli wa uhalali wa nani anatakiwa kuwa katika eneo hilo na itasimamia ukweli huo wa mwaka 1987  na kama kutakuwa kuna wananchi wanataka mabadiliko wafuate sheria kama wenzao walivyofanya katika kutenga eneo hilo kuwa la wafugaji.
“Hapa hakuna mgogoro wa ardhi bali ni uvunjifu wa sheria tu, nitahakikisha namaliza uvunjifu huu kuanzia sasa na sitaki kusikia jambo hili linaendelea. Lengo la kuja hapa ni kusimsmia msimamo wa Serikali kwa njia ya amani na utulivu. Natambua kuwa kuna wakazi au wafugaji 200 lakini 43 kati ya hao ni wavamizi si wenyeji nataka jambo hilo liishe mara moja.” Alitoa msimamo wa Serikali Mkuu wa Mkoa Gaguti.
MAAGIZO
Mkuu wa Mkoa Gaguti alimwagiza na kumpa wiki moja  Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka kuanzia tarehe 27/02/2019  kufanya uhakiki na utambuzi wa wafugaji wadogo ambao walisajiliwa katika Kijiji hicho cha Kahundwe na kuwaondoa wavamizi ambao ni wakulima na wafugaji wakubwa waliotoka maeneo mengine.
Pili Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka na timu yake wafanye uhakiki wa mifugo ili kubaini wafugaji ambao kwanza si raia wa Tanzania na pili kubaini wingi wa mifugo kusudi kama kuna wafugaji wakubwa wenye mifugo mingi waondolewe ili wafuate sheria za kuomba vitalu vya kufugia kama wafugaji wakubwa au wawekezaji katika vitalu.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kahundwe walimweleza Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuwa mgogoro huo unachochewa na Diwani wa Kata ya Chanika kwasababu wakati wa Kampeini ya mwaka 2015 aliwahidi baadhi ya wananchi hao wavamizi kuwa akipata madaraka atahakikisha wanalichukua eneo la Kijiji cha Kahundwe kama eneo lao la kilimo.

Naye Bw. Bernard Sau Afisa Ardhi Wilaya ya Karagwe akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa kijiji cha Kahundwe kilisajiliwa mwaka 1987 kwa GN namba 620 kama Kijiji cha wafugaji na wakati huo ilikuwa Wilaya moja ya Karagwe kabla ya kutengwa Wilaya mbili za (Karagwe na Kyerwa) na baada ya kutenga Wilaya mbili kijiji cha Kaundwe kilibaki Wilaya ya Karagwe na kijiji hicho kina jumla ya Hekta 20,000 za kufugia. 

IBADA YA HIJJA YAIBUA FURSA ZA KIBIASHARA

0
0


Mgeni rasmi wa uzinduzi wa Usajili wa vyeti vya Ndoa na safari za Ibada ya Hijja Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela wa pili kutoka kushoto, kaimu sheikhe wa Mkoa huo alhaji sheikhe Hasan Kabeke wakiomba dua iliyoongozwa na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Ali Hamis Ngeruko (kulia) baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kuzindua mkakati huo juzi

………………….

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

IBADA ya Hijja nchini Saudi Arabia imeibua fursa za kibiashara kwa Watanzania hivyo wanatakiwa kuchangamkia ili wanufaike kiuchumi.

Hayo yalielezwa juzi jijini Mwanza na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Ali Hamis Ngeruko wakati wa uzinduzi wa elimu ya Hijja na Usajili wa Vyeti vya Ndoa kwa waumini wa dini ya kiislamu uliofanyika kitaifa jijini humu.

Alisema Ibada hiyo ya Hijja ni jambo linalohitaji elimu kwa kuwa giza haliwezi kuongoza jambo, hivyo ufinyu wa elimu husababisha watu wengi kuharibu mengi ukiwemo uhusiano wao kwa ujinga na wengine huendelea kuharibu.

Alieleza kuwa soko hilo lililopo Mina huko Makka kuna fursa ya soko la kimataifa la mifugo, vyakula, mikeka na tasbihia lakini bado Watanzania hawajalitambua wala kufikiria kutumia fursa hizo kibiashara zilizopo kwenye mji huo Mtakatifu wakati wa Ibada ya Hijja na kunufaika kiuchumi.

“BAKWATA Taifa imeona izindue elimu ya Ibada ya Hijja Mwanza na kila mkoa utafanya kazi hiyo , utasimamia na kuelimisha waumini.Pia Uhusiano na ushirikiano wa Serikali na BAKWATA upo kwenye mambo mbalimbali japo baadhi ya watu wanaweza kuona uzinduzi wa elimu ya Hijja una uhusiano gani au hauna uhusiano,” alisema.

Nguruko alieleza zaidi kuwa Tanzania imejaaliwa madini na vito yanayotumika kutegeneza tasbihi, wana mifugo na nguo (vitenge) hivyo Watanzania wakiitumia fursa hiyo wataingiza fedha nyingi za kigeni kutokana na kuuza bidhaa za aina hiyo Makka lakini wamelalia soko hilo.

“Watanzania tutanufaika na mengi kwani Makka si ibada tu, kuna biashara inafanyika pia na kwa kuwa tunayo mikeka, vitenge, madini na mifugo na mchele bado soko hilo hatujaliona na haliwezi kutambuliwa bila kutambulishwa.Hivyo watu wawe na maarifa na hijja yao pamoja na neema watumie fursa zilizopo Makka,”alisema mjumbe huyo wa baraza la Ulamaa.

Kwa mujibu wa Nguruko waumini wanaokwenda kuhiji wanatakiwa kuchangamkia fursa za soko la Makka ambalo raia wengi wa nchi za Afrika Magharibi (Nigeria, Cameroon na Senegal) ndio pekee wamelitumia kwa uchumi wa nchi zao na mtu mmoja mmoja kunufanika nalo kwa kupeleka na kuuza bidhaa zao huko.

Kwamba tasbihi , mikufu, mikeka na vitenge ni ubunifu wa watu wa mataifa hayo ambao umewanaingizia vipato vizuri kupitia Makka huku biashara ya mifugo na mchele ikifanywa na raia wa kutoka Thailand na Australia na kuhoji “ sidhani kama Watanzania tunalitambua soko hilo , tumelala na mifugo yetu na mchele.”a

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela ambaye mgeni rasmi alisema hakuwahi kufikiria fursa za kiuchumi kwenye Hijja hivyo Watanzania wazione, wajue watanufaika nazo vipi iwe kwa Waislamu na wasio Waislamu.

Alisema jambo hilo serikali italibeba na BAKWATA taifa kwa upande wao walichukue na kuwataka waumini wa dini ya kiislamu waliowekeza nchini waone watakavyoshiriki kwenye fursa hizo ingawa kinachoangaliwa zaidi ni ubora wa bidhaa na mifugo.

Mongela alipongeza utaratibu huo unaofanywa ndani ya BAKWATA kuwa ni mapinduzi na migogoro iliyokuwepo wakati Hijja itakwisha na kuifanya serikali itapate ahuweni kwa kuwa nchi yetu haina dini ila wananchi wake wana dini.

Naye kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Hasan Kabeke alisema BAKWATA kutoa elimu hiyo ya safari ya Ibada ya Hijja inalenga kuwazindua Waislamu ikiwa ni pamoja na kutumiza majukumu yake kwa mujibu wa katiba ya baraza hilo.

Alifafanua kuwa Tanzania imetengewa nafasi za mahujaji 23,000 lakini wanaojaaliwa kwenda ni 2,500 hadi 3,000 kulinganisha na Kenya inayopeleka mahujaji 4,500 hivyo Waislamu wanayo fursa bado ya kwenda kuhiji kwa gharama ya sh. 10,105,000 sawa na Dola 4300 za Marekani

MRADI WA SOKO LA KISASA MANISPAA YA MOROGORO WAMKUNA DOKTA KIJAJI

0
0
Na Peter Haule, WFM, Morogoro
Halmashauri zote nchini zimetakiwa kujifunza kutekeleza miradi ya Kimakakati inayopatiwa ruzuku na Serikali, katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kuwa thamani halisi ya mradi wa Soko la kisasa utakaogharimu Sh. bilioni 17 hadi kukamilika kwake inaonekana.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua mradi wa kimkakati wa ujenzi wa Soko la Kisasa katika Manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro wenye lengo la kuzifanya Mamlaka za Serikali za Mitaa ziweze kujitegemea kimapato.
Dkt. Kijaji alisema kuwa Kama ipo halmashauri iliyopewa fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati kwa kuwekeana mkataba na Serikali na bado inashindwa kufuata makubaliano ya mkataba ijifunze kutoka Manispaa ya Morogoro.
“Ukilinganisha na miradi mingine ya kimkakati niliyoikagua katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, huu ni wa mfano, zipo halmashauri ambazo zimepewa fedha halafu zinarudi tena kuangalia upya mikataba ambayo waliwekeana saini na Serikali jambo ambalo linatia mashaka, tuje tujifunze kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa nini ameweza kwenda na wakati ulio katika mkataba”alisema Dkt. Kijaji.
Alipongeza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo ambao umefikia asilimia 30 japo walitakiwa kufikia asilimia 40 katika kipindi hiki kutokana na changamoto ya kujaa maji na kuutaka uongozi wa Manispaa hiyo kukamilisha ujenzi ndani ya kipindi cha miezi mitano ili wafanyabiashara waanze kulitumia soko hilo.
"Mapato ya Soko hili yataongezeka kutoka Shilingi bilioni moja, kwa mwaka hadi Sh. bilioni 4 kwa kuwa idadi ya wafanyabiashara itaongezeka kutoka 400 kwa sasa hadi 900 na huduma zingine zitatolewa kama Benki" alieleza Dkt. Kijaji.
Dkt. Kijaji alisema kuwa dhamira ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ya kuanzisha miradi ya kimkakati kwa manufaa ya watanzania itatimia kupitia mradi wa Soko la Kisasa la Manispaa ya Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo, ameishukuru Serikali kwa kupeleka mradi huo Wilayani kwake, kwa kuwa soko lililokuwepo lilijengwa mwaka 1953 hivyo kuwa na miundombinu mibovu iliyosababisha wananchi kuwa na magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipindupindu, hivyo mradi huo si tu utaongeza mapato na kuweka mandhari nzuri, lakini pia utaimarisha afya za wananchi.
Naye Meya ya Manispaa ya Morogoro  Bw. Pascal Kihanga, alisema kuwa waliwaahidi wananachi kusimamia ujenzi wa Soko hilo jambo ambalo linatekelezwa kwa juhudi kubwa, hivyo kufikia mwezi Septemba mwaka huu mradi utakabidhiwa kwa Serikali na wafanyabiashara wote walioondolewa kupisha mradi na  wengine watarudi.
Mhandisi wa Mradi huo Antonio Mkinga, amesema kuwa mradi huo utakamilika katika muda uliopangwa, kwa kuwa mpaka sasa hakuna vikwazo ambavyo vinaweza kuzuia utekelezaji wake.
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ni miongoni mwa Halmashauri 17 zilizokidhi vigezo vya kutekeleza jumla ya miradi 22 ya kimkakati nchini kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kwa gharama ya shilingi bilioni 147 ambapo Manispaa hiyo ilipata mradi huo wa soko la kisasa litakalogharimu shilingi bilioni 17.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo, wakati akikagua ujenzi wa Soko la Kisasa la Kimkakati la Manispaa ya Morogoro, ambalo ndilo la mfano katika miradi ya kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kujitegemea kimapato. 
 Muonekano wa Soko la Kisasa la Kimkakati la Manispaa ya Morogoro, ambalo limekamilika kwa asilimia 30 na linatarajiwa kukabidhiwa kwa Serikali Septemba mwaka huu na kuhudumia wafanyabiashara zaidi ya 900.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa nne kushoto) akietendelea na ukaguzi wa ujenzi wa Soko la Kisasa la Kimkakati la Manispaa ya Morogoro  Mkoani Morogoro .(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

WAZIRI JAFO AWAONYA WANAOTUPA TAKATAKA KATIKA MITARO YA BARABARA, ATOA MAAGIZO

0
0

*Asema Serikali inatumia fedha nyingi kujenga miundombinu
*Awataka wananchi kulinda barabara zinazojengwa nchini

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WANANCHI wenye tabia ya kutupa takataka katika mitaro iliyopo pembezoni mwa barabara na kusababisha kuziba na kujaa taka imeonekana kumkera Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa(TAMISEMI)Selemani Jafo kutoa onyo kali.

Jafo ametoa onyo hilo leo Februari 26 ,mwaka 2019 wakati ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo akiwa
katika barabara ya Kijichi Toangoma ameshuhudia baadhi mitaro ya barabara hiyo ikiwa imeanza kujaa taka.

"Serikali inatumia fedha nyingi kutengeneza miundombinu ya barabara ,hivyo lazima wananchi nao waitunze ili iwe salama.Wenye tabia ya kutupa taka waache na hii tabia hatuwezi kuacha iendelee,viongozi wa wilaya hakikisheni usafi wa mitaro unapewa kipaumbele," amesema Waziri Jafo.

Wakati huo huo amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Felix Lianiva kuanzisha kampeni ya usafi katika maeneo yote ya miundombonu ya barabara ili ibaki salama."Nitoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya ukiwemo Mkuu wa wilaya ya Temeke kuanzisha kampeni ya usafi.Nataka mitaro yote iwe
safi,"amefafanua.

Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya DMDP ,Waziri Jafo amesema jumla ya Sh.Bilioni 660 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo na kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kwa sasa kuna mabadiliko makubwa ambayo yametokana na kukamilika kwa miradi na maeneo mengine bado inaendelea na ipo hatua mbalimbali za utekelezaji.

Waziri Jafo amepata nafasi ya kutembelea ujenzi wa kituo cha afya Buza ambacho
kinajengwa kisasa na lengo ni kuondoa adha ambayo wananchi wa Buza na maeneo jirani wamekuwa wakiipata.Amefafanua kuwa ujenzi huo wa kituo cha afya unafanyika chini ya ufadhili wa fedha za miradi ya DMDP na kwamba kabla ya kuanza ujenzi huo ilikuwa ni zahanati lakini kwa namna ambavyo kitakuwa kitakapokamilika kitakuwa kituo cha afya.

"Serikali ya Awamu ya tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.John Magufuli kuna mambo makubwa yanaendelea kufanyika nchini ya kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo sekta ya afya.Wananchi wa Buza ni mashahidi kupitia ujenzi huu wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi," amesema Waziri Jafo.

Amewahakikishia wananchi wa Buza kuwa baada ya ujenzi kukamilika Serikali itapeleka vifaa tiba vyote ambavyo vinahitajika kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa bora.Pia amesem Serikali itapeleka Gari mpya ya kubeba wagonjwa( Ambulance).

"Tutaleta Ambulance mpya kabisa kwa ajili ya kituo cha afya Buza,lengo ni kuhakikisha mnakuwa mnakuwa na kila kitu ambacho kinahitajika hapa.Hii yote inatokana na dhamira njema ya Rais wetu ya kupeleka huduma muhimu kwa
wananchi wote," amesema Waziri Jafo.

Waziri Jafo ameendelea kutoa shukrani kwa Benki ya Dunia kutokana na misaada ya fedha ambayo wanaitoa kwa Serikali ya Tanzania na kufafanua kupitia fedha hizo katika Majiji,Manispaa na Halmashauri kote nchini miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa na mingine imekamilika.

"Kuna zaidi ya Sh.Trilioni mbili ambazo zinatumika kuboresha miji yote nchini.Na
kwa Dar es Salaam zimetengwa fedha hizo Sh.Bilioni 660 kuendeleza Jiji na ukweli kuna mabadiliko makubwa hata maeneo ambayo yalikuwa hayapitiki, hivi sasa
yanapitika vizuri," amesisitiza Waziri Jafo.

Tangulia Ruge Mutahaba !

0
0
Ni siku ya Jumanne ya Februari 26, majira ya saa mbili na robo nikiwa naendesha gari kurudi nyumbani Madale! Kupitia mitandao ya kijamii naona uzi kwamba ndugu yangu Ruge ametangulia mbele ya haki! Moyo wa binadamu umeumbwa kwa kuogopa taarifa mbaya hasa za kifo tena cha mtu mnayefahamiana.

Nikiwa kwenye mshtuko na mtanziko huo, ghafla kwenye simu yangu unaigia ujumbe wa Mfalme! Ujumbe ambao unathibitisha kifo, safari hii si kupitia taarifa za Gerson Msigwa isipokuwa kupitia kwenye ukurasa wa twitter ya Mheshimiwa Rais, Dk John Magufuli. Kwa kweli umemwelezea Ruge vizuri zaidi! 

Ujumbe huo ukanikumbusha thamani ya kila mwanadamu awapo duniani na baada ya kuondoka, utakumbukwa kwa jambo gani? baya ama zuri? Nikakumbuka tena kwamba Ruge hajafa isipokuwa amelala tu! Maana ameacha icon na benchmark nyingi ambazo kupitia hizo namwona akiendelea kuishi. 

Jina Ruge katika tasnia ya burudani pamoja na mambo mengine ya kijamii ni sawa na maji! Usipoyanywa basi utayaoga, kama ikishindikana kuyaoga basi hata chooni utachambia. Ruge ulikuwa zawadi kwa familia na ukoo wa Mutahaba, kwa tasnia ya habari ulikuwa nguzo na katika tasnia ya burudani, ulikuwa funguo!

Tazama zawadi imepotea na nguzo imeanguka, lakini funguo imebaki! Kupitia kwako Ruge umewafungulia vijana wengi dunia kuwa wanachotaka! Bila ufunguo wako pengine leo vijana wengi wangekuwa kama kipofu asiyekuwa na fimbo nyeupe! Changamoto zingekuwa nyingi zaidi, lakini tazama leo umelala usingizi mzito lakini ufunguo umetuachia vijana, kikubwa ni kuutumia vizuri ili isije kutulazimu kubadili kitasa. 

Kaka Ruge umeondoka, mdogo wako umeniachia funzo moja kubwa, roho ya kusamehe. Katika maisha yako hukuruhusu chuki na ugomvi vikutawale, hata pale vilipotokea ulihakikisha vinakwisha na maisha mengine yasonge mbele! Ninakumbuka siku Rais anazindua mradi wa bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Hoima, Uganda. Pale ulitoa funzo kubwa kama lile alilolitoa Yesu Kristu akiwa amewambwa msalabani pamoja na wale wanyang'anyi wawili! 

Rais alitaka Ruge usameheane na Gavana wa Darisalama, bila kinyongo tena kwa sura ya tabasamu ukaonesha kukubali na kuishi kile ulichokiamini. Sitaki kuzungumzia suala la ugomvi uliokuwapo baina yako na Mbunge wa sasa wa Mbeya Mjini, baadaye mkashikana mikono na maisha yakaendelea! Moyo wa aina hiyo unapatikana vifuani mwa wanadamu wachache ambao mmoja wao ni Ruge.

Ninasikitika ninaandika mambo yanayokuhusu wakati hutapata fursa ya kuyasikia, lakini nafarijika kwamba kupitia mafunzo hayo machache kutoka kwako wachache miongoni mwetu tunaweza kujifunza kuwa kama Ruge. 

Pumzika kwa amani emanzi eya' Buhaya ninaendelea kuamini kwamba Mwenyezi Mungu amekuchukua baada ya kumaliza kazi ambayo alikutuma uje kuifanya hapa duniani! Amekuita ukafanye kazi nyingine huko mbinguni.

Omukama akuhumuze ne'milembe Amina.

Imeandikwa na Mkinga Mkinga

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 26.02.2019

BREAKING NEWZZZZ: FIFA yamfungia maisha Mwamuzi wa zamani wa Kimataifa na Katibu wa Chama Cha Waamuzi Tanzania (FRAT) Oden Charles Mbaga

0
0

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) chini ya Mwenyekiti wake Vassilios Skouris imemfungia maisha Mwamuzi wa zamani wa Kimataifa na Katibu wa Chama Cha Waamuzi Tanzania (FRAT) Oden Charles Mbaga (pichani) kwa kujihusisha na masuala ya rushwa ya upangaji matokeo.

Baada ya uchunguzi uliofanyika kuanzia July 11,2018 Mbaga amekutwa na hatia ya kuhusika kwenye upangaji wa matokeo ikiwa ni kinyume na kanuni za Maadili za FIFA.

Mbaga amevunja Ibara ya 11 ya Kanuni ya rushwa ya FIFA ya mwaka 2009.

Anafungiwa maisha kutojihusisha na shughuli zozote za Mpira wa Miguu katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa kwa mujibu wa Ibara ya 7j ya Kanuni za Maadili za FIFA za mwaka 2018 pamoja na Ibara ya 22 ya Kanuni ya Nidhamu ya FIFA.

Aidha Mbaga anatakiwa kulipa faini ya kiasi cha fedha ya Uswis Faranga 200,000 ndani ya siku 30 tokea amepata taarifa hizo na anaweza kulipa kwa fedha ya Swiss au kwa dola za Kimarekani.

Vilevile Mbaga anatakiwa kulipa gharama za shauri hilo kiasi cha Faranga za KiSwiss 1,000 ndani ya siku 30 tokea amepata taarifa.

Anaweza kukata rufaa kwenye mahakama ya kimichezo ya FIFA CAS,rufaa ambayo inawasilishwa moja kwa moja CAS ndani ya siku 21 tokea maamuzi yalipofanyika na ndani ya siku 10 baada ya kumalizika siku 21.

Mbaga ambaye ni Katibu wa Chama cha Waamuzi Tanzania (FRAT) anapoteza sifa ya nafasi hiyo kutokana na adhabu ya kufungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya Mpira wa Miguu.

BEI ZA BIDHAA MBALIMBALI KATIKA SOKO LA MAKUMBUSHO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Bei za bidhaa mbalimbali katika soko  la Makumbusho wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,kamazinavyo onekana katika picha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Bei ya mahindi kilomoja ni shilingi 1000,uliezi 1700.
Wafanya biashara wa ndizi  katika soko la Mbakumbusho wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakisubili wateja wanaotoka sehemu mbalimbali ambapo mkungu wa ndini ni shilingi 15000-25000.

Lango kuu la kuingilia katika  soko la Makumbusho lilipo wilaya ya Kinondoni jijini Da es Salaam.

KUMBUKIZI: MJUE RUGE MUTAHABA KWA UFUPI

0
0
JK akiwa na Ruge Mutahaba wakati wa hafla ya miaka mitatu ya kituo cha kukuza vipaji nchini cha Tanzania House of Talents (THT)  usiku wa Desemba 8, 2009  katika viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Juu Ruge akiwa na nduguze. Chini akiwa na familia nzima ya Profesa na mama Mutahaba. Picha kwa hisani ya Nuru the Light

SWALI: Ruge mutahaba ni nani?

RUGE: Nimezaliwa Brooklyn,  New York,  Marekani,  mwaka 1970.


Primary School nimesoma Arusha School standard 1 hadi 6, kisha nikahamia Mlimani Primary School maeneo ya Chuo Kikuu Dar es Salaam na ndipo nilipomaliza darasa la saba. Kisha nikasoma Forodhani Secondary School form 1 – 4, baadae Pugu High School 5 na 6. baada ya hapo nikarudi Marekani ambako nikaenda kusoma San Jose University California ambako nikachukua BA in Marketing na pia nikawa nakachukua BA in Finance, kozi zote nilisoma ndani ya miaka 5, kind of 2 courses at the same time. Baada ya hapo nikarudi tena Tanzania.

SWALI: Nini kilichotokea hadi ukajikuta uko clouds FM.

RUGE: Wakati nipo Marekani, Joseph Kusaga alikuwa na disco, Clouds Disco, mimi nikawa supplier wake wa vifaa mbalimbali vya music, then hapo tuka-build good friendship. Sasa, niliporudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yangu, Joseph Kusaga akanishawishi sana nibaki kutokana na opportunity zilizokuwepo za kuanzisha Radio na kuipeleka katika level nyingine kabisa, ndipo nilipojikuta nipo Clouds Entertainment.

SWALI: Tuambie kuhusu THT.

RUGE: Kama Clouds Entertainment tuliamua kuanzisha kampuni ya management ya wasanii ambayo tuliita Smooth Vibes ambayo ndiyo kampuni iliyowatoa wanamuziki kama Lady Jay Dee, Ray C na wengineo. Unajua utakuta kati ya wasanii watano, only mmoja au wawili wana-survive na suddenly utakuta msanii alikuwepo then kapotea. Hii inatokana na kutokuwa na foundation nzuri. Hivyo nikaona ni bora nianzishe House of Talents ambayo sasa kupitia hiyo, tukawa tunawafundisha wasanii misingi ya muziki, kumfundisha msanii how to Manage Industry, Vocal Coaching, Music Business, Music Instrumentation, Dance Classes na kadhalika.
Nikagundua kuwa unakuta msanii anaenda kwenye show lakini performance inakuwa mbovu na pia ili msanii aweze ku-last longer kwenye game anatakiwa ajue dancing. Ndio maana THT tukawa na dance classes. THT imewatoa wasanii wengi kama Maunda Zorro, Mwasiti, Marlaw, Barnaba na wengineo. 
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images