Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 275 | 276 | (Page 277) | 278 | 279 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Mwishoni wa wiki, Uwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa mataifa, ulitembelewa na wanafunzi wanajeshi wanane wanaoshiriki katika mafunzo ya miezi kumi, kupitia International Fellows Program yanayotolewa United States Army War war College and Carlisle Barrace. 
  Chuo hicho ambacho kipo nchini Marekani, kila mwaka huanda mafunzo hayo katika ngazi ya maafisa kutoka mataifa mbalimbali marafiki. 
   Kwa mwaka huu, mafunzo hayo yanawanafunzi 367 kati yao 300 ni wamarekani na waliobaki 67 wanatoka katika mataifa mbalimbali ikiwamo Tanzania. 
  Wanafunzi hao walifika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kama sehemu ya ziara ya mafunzo ambapo pamoja na masuala mengine, walitaka kufahamu vipaumbele vya Tanzania katika masuala muhimu yanayoikabili dunia hivi sasa ikiwani ni pamoja na matatizo yanayotokana na Mabadiliko ya Tabia nchi na matatizo ya maji kwa Afrika na namna gani Tanzania kama sehemu ya Afrika imejipanga kukabiliana nayo.
  Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza na sehemu ya wanafunzi wanajeshi wanaohudhuria  mafunzo ya miezi kumi katika  Chuo cha Kijeshi cha Marekani kupitia International Fellows Program, wanafunzi hao akiwamo Luteni Kanal Francis Ronald Mbindi kutoka Jeshi la  Wananchi wa Tanzania  (JWTZ) walifika  katik Uwakilishi wa Kudumu ikiwa ni sehemu ya  zaira ya mafunzo ili kujifunza  masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo ni vipaumbele vya Tanzania. Kushoto kwa Balozi Manongi, ni  Naibu Muwakilishi wa Kudumu, Balozi Ramadhan Mwinyi.
  Muwakilishi wa Kudumu Balozi  Manongi akisisitiza kwamba  mabadiliko  ya  Tabia nchi ( Climate Change) si suala la nadharia kwa sababu yapo matukio mengi yanayoendelea hivi sasa duniani kote ambayo ni dhahiri yanatokana na  mabadiliko hayo. akatolea mfano wa Tanzania ambako kumekuwapo na  migogoro na hata mapigano ya mara kwa mara  kati ya wakulima na wafugaji wakigombea  ardhi,   maji na malisho. Akasema migogoro kama hiyo ambayo inaathari kubwa kwa jamii za wafugaji na wakulima lakini pia hata kwa serikali kuu.  Na kwamba  inaweza kuonekana kama ni tatizo la eneo fulani au nchi fulani lakini   kama likiangaliwa katika mapana yake   dhahiri  nyuma yake ni matokeo ya   mabadiliko ya tabia nchi.  Hata hivyo akasema serikali ya Tanzania inajitahidi sana katika kujaribu kutafuta suluhu  kuhusiana na tatizo hilo ambalo anaamini linatokea pia katika nchi nyingine hususani  Afrika
  Luten Kanali,  Francis Ronald Mbindi kutoka  JWTZ akitoa neno la shukrani kwa niaba ya  wenzake baada ya mazungumzo yao na  Uongozi wa  Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
  4.IMG-4708. Luteni Kanal  Francis Mbindi  akimkabidhi  kwa niaba   ya wenzake, Balozi Tuvako Manongi,  sehemu ya  hotuba maarufu ya Rais Abraham Lincolin aliyoitoa  Novemba, 19, 1863 katika maadhimisho ya miaka 150 ya GettysBury  (  The turning   Point :the 150th Anniversary of the Gettysbury address) hotuba hiyo ya   Rais Lincolin inayohesabika kama hotuba muhimu sana  kuwahi kutolewa na  Rais Lincolin  ilikuwa ikielezea kuhusu vita vya wenyewe kwa  wenyewe ( CIVIL War).  vita hivyo vilivyotokea katika eneo hilo la GettysBury  vinaelezewa kama vita vilivyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu, ambapo inasadikiwa zaidi  ya wanajeshi 50,000 waliathirika ama kwa kupoteza maisha,  kuchukuliwa mateka,  kujeruhiwa au hawakujulikana waliko
  Luten Kanali,  Francis Ronald Mbindi kutoka  JWTZ akitoa neno la shukrani kwa niaba ya  wenzake baada ya mazungumzo yao na  Uongozi wa  Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
  4.IMG-4708. Luteni Kanal  Francis Mbindi  akimkabidhi  kwa niaba   ya wenzake, Balozi Tuvako Manongi,  sehemu ya  hotuba maarufu ya Rais Abraham Lincolin aliyoitoa  Novemba, 19, 1863 katika maadhimisho ya miaka 150 ya GettysBury  (  The turning   Point :the 150th Anniversary of the Gettysbury address) hotuba hiyo ya   Rais Lincolin inayohesabika kama hotuba muhimu sana  kuwahi kutolewa na  Rais Lincolin  ilikuwa ikielezea kuhusu vita vya wenyewe kwa  wenyewe ( CIVIL War).  vita hivyo vilivyotokea katika eneo hilo la GettysBury  vinaelezewa kama vita vilivyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu, ambapo inasadikiwa zaidi  ya wanajeshi 50,000 waliathirika ama kwa kupoteza maisha,  kuchukuliwa mateka,  kujeruhiwa au hawakujulikana waliko
  Wageni wetu  wakipeana   na kusaini  kitabu cha wageni, hawa wote ni wanajeshi katika ngazi ya maafisa , hawakuhitaji kukaa mezani ili kusaini kitabu
  Balozi Tuvako Manongi akiendelea kubadilishana  mawazo na wageni wake,  nyuma anayeonekana kwa mbali ni Balozi  Ramadhan Mwinyi. HABARI NA PICHA NA MDAU MAURA MWINGIRA  WA UWAKILISHI WA KUDUMU WA TANZANIA  UMOJA WA MATAIFA

  0 0

  Kikosi cha Kilimanjaro Stars kinaagwa kesho (Novemba 25 mwaka huu) tayari kwa safari ya Nairobi, Kenya kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza kutimua vumbi Novemba 27 mwaka huu.

  Hafla ya kuiaga timu hiyo itafanyika saa 5 asubuhi kambini kwao katika hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Msafara wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager utaongozwa na Ahmed Idd Mgoyi.

  Wachezaji waliomo katika msafara huo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).

  Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).

  Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

  Hata hivyo, washambuliaji Samata na Ulimwengu watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba Mosi mwaka huu wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

  Benchi la Ufundi la timu hiyo linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu), Frank Mhonda (mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).

  Kilimanjaro Stars ambayo ipo kundi B katika michuano hiyo itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.

  0 0

   New Life Band ya Arusha
  Lilian Kabaganza wa Rwanda

  KUNDI la Muziki wa Injili la New Life Band la jijini Arusha limethibitisha kushiriki Tamasha la Krismas linalotarajia kuanza Desemba 25 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na mikoa mingine minne hapa nchini.  
  Bendi hiyo ni muendelezo wa waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo la Kimataifa lenye kauli Mbiu ya kuimalisha amani hapa nchini.
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alisema kuendelea kujitokeza kwa waimbaji hao kunatokana na kufanyika kwa taratibu stahili ambazo zitafanikisha tamasha hilo.
  “Bado tunaendelea kufanya mazungumzo na waimbaji wengine kutoka nchi mbalimbali ambazo ni majirani zetu, lengo ni kuimarisha uhusiano mwema na maendeleo mengine kwa ujumla,” alisema Msama.
  Aidha Msama alisema mbali ya bendi hiyo ya New Life Band, mwimbaji mwingine kutoka Rwanda ni Lilian Kabaganza.
  Msama aliwataja wengine waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, kundi la The Voice (Tanzania), Solomon Mukubwa (Kenya).

  0 0

  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Mh. Sadifa Juma Khamis akitoa Taarifa fupi kwenye Mkutano wa kutambulishana baadhi ya wajumbe wa Kamati ndogo ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Jengo Jipya la Ofisi Kuu ya UVCCM Zanzibar. 
  Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Jengo Jipya la Ofisi Kuu ya UVCCM Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, kulia yake Makamu Mwenyekiti wa Kamati Hiyo waziri Mkuu Mstaafu wa  Mh. Edward Lowasa pamoja na wajumbe wengine wakiwa katika mkutano wa mwanzo wa Kamati hiyo.
  --------------------------------------
  Wananchi wa Majimbo ya Donge, Kitope na Bumbwini yaliyomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B” wameombwa kuitumia fursa na bahati waliyoipata ya uwepo wa kiwanda cha Sukari Mahonda ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa nafasi za ajira wakati kitakapoanza rasmi kazi zake za uzalishaji wa sukari. 
  Ombi hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa salamu maalum kwenye Mkutano wa hadhara wa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika katika uwanja wa michezo wa Mkaratini ndani ya Jimbo lake la Kitope. 
  Balozi Seif alisema tabia ya baadhi ya watu kujaribu kufanya hujuma kwa kuchoma moto mashamba yaliyooteshwa miwa ya kiwanda hicho inaweza kuwafukuzisha wawekezaji ambao tayari wameshaonyesha nia ya kutaka kuwekeza vitega uchumi vyao hapa Nchini. 
  Alieleza kwamba wananchi wa Majimbo hayo wanapaswa kuwa makini pamoja na kukemea vitendo hivyo viovu ambavyo endapo vitaachiliwa kuendelea kufanyika katika maeneo hayo vitachangia kurejesha nyuma juhudi za Serikali kuu za kukaribisha wawekezaji wanaopewa nafasi ya kuwekeza ili kusaidia uchumi wa taifa pamoja na ustawi wa jamii. 
  “ Vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya wenzetu tunapaswa kuelewa kwamba hatuwatendei haki wawekezaji wetu waliojitolea kuweka vitega uchumi vyao hapa Nchini “. Alifafanua Balozi Seif.
  Alisema inasikitisha kuona kuwa zaidi ya ekari kumi na nane zilizooteshwa miwa kwa ajili ya usagaji wa sukari wakati utakapoanza uzalishaji tunaarifiwa kwamba zimeteketea kwa moto unaosadikiwa kuwa ni hujuma za makusudi “. Alionyesha Masikitiko yake Balozi Seif. 
  Aliwashauri wananchi hao kuwa walinzi wa miradi ya uwekezaji ambayo mingi kati yao huwanufaisha wananchi walioziunguukwa na miradi hiyo. Akizungumzia suala la siasa Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mbunge wa Kitope aliwatahadharisha wana CCM na wanachi wote Nchini kutokubali kudanganywa na baadhi ya wanasiasa wenye sera zisizotekelezeka. 
  Alisema wanachokihitaji wananchi walio wengi nchini ni sera pamoja na kile wanachokihitaji kitekelezwe na Viongozi waliowachagua katika maeneo yao na si vyenginevyo. Alifahamisha kwamba baadhi ya wanasiasa hivi sasa wamekuwa kero mitaani kwa tabia yao ya kuendeleza matusi na lawama kiasi kwamba zinakwenda kinyume na mfumo wa vyama vingi vya siasa lakini hata na maadili ya dini. 
  Aliwataka wananchi kuendelea kuiamini Serikali yao yenye lengo la kuwaletea maendeleo kwa kujenga miundo mbinu itayotoa fursa ya kutanuka kwa huduma za Kiuchumi samba mba na kupunguza umaskini. “ Tunapaswa tuangalie kwa makini tokea mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hadi leo Bara bara ngapi zilizojengwa katika maeneo yetu. Sasa lazima tuelewe kwamba Zanzibar ni ya Wazanzibari wenyewe na wao ndio watakaohusika katika kuijenga “. Alisisitiza Balozi Seif. 
  Aidha Balozi Seif alieleza kwamba lengo la Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha Muungao kwa faida ya watu wake wote. Alifahamisha kwamba cheche ya ubaguzi inayoendelezwa na baadhi ya watu kwa kutaka kuvunja muungano haiwatendei haki Wazanzibari walio wengi wanaoishi upande wa Bara wa Muungano. Alisema choko choko hizo zinaendelea kuchochewa wakati tayari wazanzibari hao wameshawekeza miradi kadhaa ya kiuchumi inayoweza kusambaratika kama fitina hiyo ikiachiliwa kuchomoza zaidi. Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi alisisitiza na kuweka wazi kwamba msimamo wa Chama cha Mapinduzi uko wazi wa mfumo wa Serikali mbili ambazo ndio muhimili wa kuendelea kuwepo kwa Muungano uliopo hivi sasa. Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 23/11/2013.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu kwenye mkutano wa hadhara wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika kwenye kiwanja cha michezo cha Mkaratini kilichopo ndani ya Jimbo lake la Kitope.
   Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia matukio yaliyokuwepo kwenye Mkutano wa Hadhara wa Wana CCM wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Hapo Kitope ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Haji Juma Haji.
  Wana CCM walijikuta wakinengua wakati Kikundi cha burudani cha CCM Big Star kikifanya vitu vyake kwenye mkutano wa hadhara wa CCM mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika kwenye kiwanja cha michezo cha Mkaratini kilichopo ndani ya Jimbo lake la Kitope. Picha na Hassan Issa wa OMPR


  0 0

  Bingwa wa dunia wa mbio za marathon, Edna Ngeringwony Kiplagat wa Kenya (pichani) amejitokeza kushiriki  katika mbio zaUhuru Marathon zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar ers Salaam Desemba 8, mwaka huu.
   Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, wamefarijika kwa kiasi kikubwa kwa Edna mwenye sifa lukuki katika mbio za marathon kujitokeza kushiriki. 
  “Kwetu tumefarijika mno kutokana na ushiriki wa Edna, kwani ni mwanariadha wa kimataifa mwenye rekodi nyingi za kuvutia na hasa hii ya ubingwa wa dunia kwa upande wa wanawake,” alisema. 
  Edna,34, alitwaa ubingwa wa dunia kwa upande wa marathon mwaka 2011 katika mashindano yaliyofanyika Daegu, Korea Kusini na akafanya hivyo tena mwaka huu katika mashindano ya dunia yaliyofanyika Moscow, Urusi. 
  Pia alishinda katika mbio za Los Angeles Marathon na New York Marathon zilizofanyika mwaka 2010 na muda bora zaidi kupata kuuweka katika mbio hizo ni wa saa 2:19:50 katika mbio za London Marathon mwaka jana.
  Pia ametwaa medali mbalimbali katika mashindano ya vijana wakati anaanza kukimbia mwaka 1996, pale alipoonyesha uwezo wake katika mashindano ya dunia kwa vijana. 
  Melleck alisema, umuhimu wa mbio hizo unaonekana zaidi kwani watu wengi wanazidi kujitokeza kushiriki nab ado fomu za usajili zinaendelea kutolewa. 
  Alisema, katika usajili huo, mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.
   “Pia tunapenda kuchukua fursa hii kuziomba kampuni au taasisi mbalimbali zinazotaka kudhamini mbio hizo zijitokeze na kufanya hivyo, kwani nafasi bado ipo na tukumbuke bila amani hakuna chochote kinachoweza kuendelea, hivyo hata wao pia wanatakiwa kuipigania amani kwa nguvu zote.” 
  Mbio hizo zinatarajiwa kuanza na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders, vilivyopo Kinondoni.

  0 0

  We have just received news that Dr. Malick A. Juma who is the Executive Director at the Ministry of Health in Zanzibar has gone missing. 
  Dr. Malick was in Nairobi attending a meeting and was supposed to be back in the country today. Efforts have been made to reach our Embassy in Nairobi to assist in knowing the whereabout of Dr. Malick. 
  On that same note the Management at the Hotel where he was staying do not have any solid leads of his whereabouts and now there are  searching his room to see if he left behind any of his belongings... 

  0 0
 • 11/24/13--08:57: neshno ya warsaw, Poland

 • 0 0

  The EAC Deputy Secretary General in charge of Planning and Infrastructure Dr. Enos Bukuku (pictured) has affirmed that the 15th Meeting of the EAC Sectoral Council on Legal and Judicial Affairs met on 15 November, 2013 in Arusha, Tanzania and cleared the legal content of the draft Protocol for the Establishment of the East African Monetary Union (EAMU) paving the way for its signing by the EAC Heads of State Summit on 30 November 2013.
   The Sectoral Council recommended the draft Protocol for adoption since it met the requirements of the Treaty for the Establishment of the East African Community and recommended to the Council of Ministers to recommend to the Summit to approve and sign the Protocol on 30 November 2013. 
  The Attorneys General, Solicitors General as well as Ministers responsible for Justice and Constitutional Affairs who constitute the Sectoral Council on Legal and Judicial Affairs among others directed the Secretariat to make a compilation of all documentation used in the negotiations of the draft Protocol to be used as working documents in drafting the legal instrument establishing the institutions to support the Monetary Union.
   Reacting to media reports alleging that some Partner States were differing over Articles in the draft Protocol ahead of its signing, the Deputy Secretary General said there were no disagreement to warrant postponement or any delay in the signing of the Protocol.
   He said the Sectoral Council decided that the various Articles that were operational in nature be used in the enabling laws that will establish the various institutions that will guide the Monetary Union such as the East African Central Bank (EACB).
   “This guidance is consistent with established practice and has always been followed in other EAC Protocols. After signature of the EAMU Protocol by the EAC Heads of State, the next two years will see passage of Bills to establish the four institutions to support Monetary Union” noted Dr. Bukuku. 
  “As the public may wish to recall, the procedure for concluding legal texts in the EAC among others includes adoption of the policy document by the Council of Ministers which refers it to the Sectoral Council on Legal and Judicial affairs for legal input.  This is in line with the practice in the Partner States, whereby policy documents are considered by the Attorneys General for legal input,” affirmed the EAC official.
   By way of improving the text of the draft Protocol, the Sectoral Council, has re-arranged the logical flow of the draft EAMU Protocol and eliminated repetitions in order to have a more concise legal text.  “This is probably where some observers not very well versed in drafting end up wondering as to how come 77 Articles were collapsed into 32 Articles in the draft EAMU Protocol okayed by the Sectoral Council on Legal and Judicial Affairs.
   Introduction of single currency has been made clearer in the final version and now spells out how Partner States will join the last stage of the EAMU which is the single currency and that the East African currency will be the legal tender in the single currency area.
  “This means that national currencies will not be used alongside the East African currency in the single currency area. Indeed, there cannot be two legal tenders in one single currency area. The provisions on how the single currency shall start have not been changed from what was contained in the policy document as it had been stated in the policy, that the Summit of the EAC Heads of State would announce the dates for the start of the single currency” Dr. Bukuku concluded.


  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji RUBADA Bw. Aloyce Masanja, (kulia) akiteta na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, Bi. Azimina Mbilinyi wakati wa semina ya kuwajengea uwezo watendaji wa ngazi mbalimbali wa Halmashauri hiyo juu ya mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) pamoja na mpango wa uendelezaji wa kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), Bw. Aloyce Masanja, (kushoto) akizungumza na Meneja wa shamba la kampuni ya Kilombero Plantation Ltd (KPL), Bw. Mare Dempsey (katikati) alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya shamba hilo.  Kulia ni Meneja rasililimali watu wa kampuni hiyo, Bw. David Lukindo.

  --------------------------------------------------------------
  Zaidi ya wakazi wapatao 1000 wamefaidika na ajira za kudumu na za muda kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni ya kilimo ya Kilombero Plantation Ltd (KPL) katika kata ya Mngeta Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), Bw. Aloyce Masanja wawekezaji hao mbali na kutoa ajira, wanatoa ruzuku ya Tshs milioni 50 kwa mwaka kwa vijiji vitatu vya wilaya hiyo.

  “Kuna watu wanasema uwekezaji hauna faida katika nchi hii, mimi nataka kuwaambia waache kupotosha…leo hii tunazungumzia ajira elfu moja katika eneo la Mngeta ambapo kiwanda hiki kipo, bila uwekezaji ajira zingetoka wapi,” alihoji Masanja.

  Alisema kwa sasa RUBADA inafanya mikakati ya kuhakikisha inatenga maeneo mengine kwa ajili ya uwekezaji mkubwa ili vijana na watanzania wengine waweze kufaidika na uwekezaji huo.

  “Kinachofanyika sasa ni kutenga maeneo mengi iwezekanavyo, tayari kuna eneo la Lingamila katika wilaya ya kilombero, ardhi ile inafaa kwa kilimo cha miwa hivyo ni jukumu la RUBADA kusimamia zoezi hilo kwa ajili ya kuleta muwekezaji ili aanze kazi,” alisisitiza.

  Akizungumzia uwekezaji  mkubwa uliopo katika shamba la Mngeta Wilayani Kilombero Bw. Masanja alisema mbali na ajira zilizopo pia wapo wakulima wadogowadogo katika eneo hilo ambao wanashirikiana kwa karibu na muwekezaji huyo kutoka nchini Uingereza.

  “Kuna wakulima wadogo ambao wanazalisha mpunga katika eneo la Mngeta na soko lao kubwa ni katika kiwanda hicho kutokana na ukaribu na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya wakulima hap na muwekezaji huyo,” aliongeza Mkurugenzi huyo.

  Bw. Masanja alielezea shughuli nyingine za kijamii ambazo zinatekelezwa na muwekezaji kuwa pamoja na shule moja pamoja na hospitali kwa ajili ya wananchi wa eneo la Mngeta na vijiji vya jirani.

  Alisema shamba hilo ambalo lina ukubwa wa hekta 5800 ni mkombozi kwa wakazi wa eneo hilo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitegemea kilimo cha mkono kuzalisha mpunga lakini kwa sasa wamepata faida kutokana na zana bora ambazo wanazipata kupitia muwekezaji huyo.

  Alifafanua kwamba hivi sasa kuna mashine za kisasa kwa ajili ya umwagiliaji, matreka pamoja na mbolea ya kutosha, hivyo ni jukumu la wananchi kuwaunga mkono wawekezaji hao ili pia nao waendelee kufaidika.

  “Sioni sababu ya kuwachukia wawekezaji, kama mtu anafanya kazi na inaonekana kwanini umchukie…wawekezaji ambao ni wababaishaji, huwa tunawashughulikia na tunawapokonya na kuwapa watu wanaoweza kufanya kazi,” alisema Masanja.

  Aliwataka watendaji wa kata, vijiji pamoja na vitongoji mbalimbali vilivyopo katika wilaya ya kilombero kutoa ushirikiano kwa RUBADA pamoja na wawekezaji wanaokuja kuwekeza katika wilaya hiyo ili uchumi wa eneo hilo uweze kukua na kuondoa umasikini uliopo.

  “Viongozi waone kuwa hii ni fursa muhimu kwao, hakuna sababu ya kulumbana,” alisisitiza Mkurugenzi huyo.  0 0
 • 11/24/13--10:16: Article 3


 • 0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi na Mkurugenzi wa utafiti Dkt. Ladislaus Chang’a walishiriki katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo kati ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Serikali ya Norway yaliyofanyika mjini Warsaw Nyumbani kwa Balozi wa Norway nchini Poland tarehe 21 Novemba,2013.

   Kutoka kushoto ni Katibu mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Bw.Michel Jarraud, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe; Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Msaidizi wa Katibu mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Bi. Elena Manaenkova na kulia kabisa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi katika mkutano wa COP 19 huko Warsaw Poland.

  Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani alipomtembelea Mheshimiwa Rais katika hoteli ya Bristol tarehe 20 Novemba 2013, alimjulisha kuhusu msaada huo na kwamba Tanzania imechaguliwa kuwa nchi ya awali katika kutekeleza mpango huo kwa imani kwamba TMA itasimamia vyema utekelezaji wake na kupata matokeo mazuri yatakayosaidia kupanuliwa kwa mpango huo katika nchi zingine za Afrika. Kwa upande wake Mheshimiwa Rais alimshukuru Bw. Jarraud kwa misaada ambayo WMO inaisaidia Tanzania na aliahidi kwamba serikali itaendelea kuisaidia Mamlaka ya Hali ya Hewa ili iweze kutekeleza majukumu yake na kushiriki vyema katika program za WMO.


  0 0


  0 0   Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo,wakati akitoa taarifa yake ya kuhusu kuvuliwa nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na aliekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Kitika Mkumbo (kushoto),kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
  Aliekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Kitika Mkumbo akizungumza.
  Waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo

  Na Ripota wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam.

  MBUNGE wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe amesema hawezi kufanya maamuzi magumu ya kutaka kujitoa ndani ya chama hicho kwa kile kilichotokea ndani ya chama hicho hivi karibuni. Amesema yeye atakuwa wa mwisho kutoka Chadema na si vinginevyo,kama wanavyofikiria watu wengine.

  Zitto ameyatoa maneno hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,wakati alikizungumzia maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema ya kumvua nafasi zake zote za uongozi yeye pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Dk. Kitilla Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa  Arusha,Samson Mwigamba.

  Zitto amekana kabisa kuhusika na wala kuujua waraka wa siri ambao ndiyo uliosababisha kumvua madaraka baada ya uamuzi wa Kamati Kuu ya chama kuunasa waraka huo.

  "Mimi nimeusikia ule waraka kwa mara ya kwanza kwenye Kamati Kuu na nilisikitika sana kwanini haukunifikia haraka kwani ningeanza kutekeleza mara moja." alisema Zitto akizungumza.

  Zitto aliendelea kusema "Huenda leo watu walitegemea nitafanya maamuzi magumu ya kuondoka kwenye chama; "Mimi bado ni mwanachama wa Chadema na nitakaekuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiyari yangu, nitafanya taratibu zote za chama kuhitimisha jambo hili mimi sitoki ng'o kwenye chama hiki labda wanitoe wao," alisema Zitto.

  Zitto alisema anaumia sana anapotuhumiwa kwa kuwa yeye ni binadamu. "...ninapotuhumiwa naumia ninapoambiwa nahujumu chama hiki naumia kwa kuwa nakipenda chama na nimekitumikia muda mrefu. Aidha aliwataka viongozi wa Chadema kuacha siasa za uzushi ili kujenga chama imara na kuwakomboa Watanzania.

  "...Sisemi kama mimi sina makosa,kwani mimi ni binadamu na nimefanya mambo mengi kwa chama changu, lakini kinachoendelea kwa sasa ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia na ni mapambano ya wanaotaka mabadiliko na wasiopenda mabadiliko ndani ya chama...mapambano ya wawajibikaji na wasiopenda kuwajibika ni mapambano ya wanaopenda demokrasia na wanaokwaza demokrasia." alisema Zitto huku akionesha kusikitishwa.

  ZIFUATAZO NI TAARIFA ZAO

  TAARIFA YA MH. ZITTO KABWE
  TAARIFA YA DKT. KITILA MKUMBO

  0 0

   Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakipita kukagua jengo la Maabara katika shule ya  sekondari ya Mwakaleli,katika halmashauri ya Busokelo,Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.Mradi huo wa ujenzi wa madarasa na maabara ni  mpango serikali  wa kuboresha shule za sekondari zilizopo kwenye kata na Taifa kwa ujumla kwa kushirikiana na benki ya Dunia.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Katende,katika halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe,mkoani Mbeya,Kinana aliwaeleza kuwa CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi na kuongeza kuwa ahadi zilizoahidiwa zitatimizwa. Aidha Kinana alikazia pia kuwa chama cha CCM ni chama imara,hivyo ni lazimaa lazima kiihoji serikali juu ya  pesa za ujenzi maendeleo ya wananchi,kwa nini hazitolewi kwa wakati. Ndugu Kinana yupo mkoani Mbeya kwa zaiara ya siku 11 katika kutekeleza Ilani ya CCM,kukagua miradi mbalimbali ikiwemo na kujua matatizo ama kero za Wanachi.


  0 0


  0 0

  From left to right front row are: Abdulla Mwinyi - Regional Commissioner for Zanzibar Urban West Region (2nd); Jefferson Smith - Zanzibar Affairs Officer (3rd); Nassor Mazrui - Minister of Trade and Industry (and Guest of Honor) (4th); Mussa Ali Mussa - Commissioner of Police Zanzibar (5th), and Sterling Roop - Director of the International Law and Policy Institute (ILPI) (6th). The launch for the Centers for Youth Dialogue program took place in Zanzibar recently and was also attended by youth groups from Stone Town and Kikwajuni in addition to youth from other parts of Zanzibar town, MP Hamad Masauni (Kikwajuni), Zanzibar Representative Ismail Jussa (Stone Town), and regional police commanders. The American people have provided $150,000 to ILPI to run programs at two youth centers in Stone Town and Kikwajuni. The goals of the project include: to build trust between communities, police, and the government, with a focus on youth; to provide training for youth on entrepreneurship and job acquisition; to provide training for youth and police on human rights, social and economic issues, tolerance, duties of citizens and government in a democracy; to strengthen the cooperation of communities in reporting crimes and illicit activities to the police; and to strengthen the capacity of police to receive and act on reports from the community.

  0 0

   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.Mh. Rais ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group kwa ubunifu wao wa Kampeni ya Fusra inayowakutanisha na kuwahamasisha vijana mbali mbali nchini kujituma na kufanya kazi ili kutokomeza swala zima la ukosefu wa ajira,Pia Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia waendeshaji wa Warsha hiyo. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,ili aweze kuzungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Naibu Mkuu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) Dr. Abby Nangawe akiongea muda mfupi kabla ya kuanza kwa mhadhara wa wazi ulioandaliwa na Jumuiya ya Wana-masoko ya wanafunzi wa chuo hicho.Katika ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa ambae ndie aliyekuwa mzungumzaji Mkuu mwalikwa kwenye mhadhara huo na kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa CBE Godian Bwemelo.Mhadhara huo ulifanyika jana chuoni hapo jijini Dra es salaam.
  Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Tiwssa akizungumza na Jumuiya ya wana-masoko ya wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara - CBE (COBEMA) chuoni hapo jana. Twissa alikuwa mgeni mwalikwa kwenye mdahalo wa wazi chuoni hapo kubadilishana uzoefu wake katika sekta ya masoko na wanafunzi wa CBE. Vodacom imekuwa ikitumia wafanyakazi wake waliobebea katika fani mbalimbali kushiriki katika midahalo ya aina hiyo vyuoni kuwapa uzoefu wa kitaaluma wanafunzi.
  Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Tiwssa akionesha kwa vitendo mbinu za kimasoko Wakati alipoalikwa kuzungumza na Jumuiya ya wana-masoko ya wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara - CBE (COBEMA) chuoni hapo jana. Twissa ni mmoja kati ya vijana waliobobea katika Nyanja ya masoko na matangazo nchini na alialikwa chuoni hapo kubadilishana uzoefu wake katika sekta hizo na wanafunzi wa CBE. Vodacom imekuwa ikitumia wafanyakazi wake waliobebea katika fani mbalimbali kushiriki katika midahalo ya aina hiyo vyuoni kuwapa uzoefu wa kitaaluma wanafunzi.
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE)wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa(hayupo pichani) ambae ndie aliyekuwa mzungumzaji Mkuu mwalikwa kwenye mhadhara wa wazi ulioandaliwa na Jumuiya ya Wana-masoko ya wanafunzi wa chuoni hapo.

  0 0  0 0

  Baadhi ya washiriki wa kozi ya Ukocha Ngazi ya Pili (Intermediate) wakimsikiliza mkufunzi wa kozi hiyo, Rogasian Kaijage (hayupo pichani) Juni mwaka huu.Kozi hiyo iliendeshwa na DRFA.

  CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimezitaka timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha makocha wao wanakuwa na taaluma ya ngazi ya pili (Intermediate) na mikataba ya kazi hiyo.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa DRFA Kenny Mwaisabula amesema Dar es Salaam kuwa timu zote zinatakiwa kutekeleza agizo ili kuendana na malengo ya chama hicho katika kukuza na kuendeleza mchezo huo.

  “Tunazitaka timu zote zinazoshiriki Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na makocha wenye taaluma hiyo Ngazi ya Pili (Intermediate), tunafanya hivi ili kuendana na dhamira yetu ya kukuza na kuendeleza mpira wa miguu.

  “Kama mtakumbuka vizuri DRFA iliendesha mafunzo ya ukocha wa Ngazi ya Pili (Intermediate) Juni mwaka huu ikiwa na nia njema ya kuhakikisha mafanikio yanapatikana, tumekuwa mstari wa mbele na mfano wa kuigwa katika kuendeleza mpira wa miguu hasa taaluma ya makocha,” alisema.

  Alisema timu hizo zimepewa mechi tatu kutekeleza agizo hilo na iwapo hawatatekeleza zitachukuliwa hatua. Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam ilianza Novemba 23 ikishirikisha timu 32.

  Kamati ya Mashindano ya DRFA inaongozwa na Mwaisabula, wakati Makamu Mwenyekiti ni Shaaban Mohamed huku wajumbe wakiwa ni Hugo Seseme, Daudi Kanuti, Kassim Mustapha, Abeid Mziba na Bakari Mtumwa.

older | 1 | .... | 275 | 276 | (Page 277) | 278 | 279 | .... | 3286 | newer