Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109974 articles
Browse latest View live

MICHEZO YA MAJESHI KUANZA KUTIMUA VUMBI JUMAMOSI HII

$
0
0
*Wananchi waombwa kujitokeza kwa wingi kujipatia burudani kutoka kwa vyombo vyao vya ulinzi

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
VYOMBO vya ulinzi na usalama kupitia Baraza la Michezo ya Majeshi ya Tanzania (BAMMATA) wameandaa michezo ya majeshi yenye kauli mbiu ya “ Michezo ni Kazi na Mshikamano” yatakayofanyika jijini Dar es salaam katika viwanja vya Uhuru kuanzia Jumamosi ya tarehe 23 na kuhitimishwa Machi 9 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) Brigedia Jenerali Suleiman Mzee amesema kuwa lengo la kufanya mashindano hayo ni kuendeleza uhusiano, urafiki na undugu baina ya majeshi ya ulinzi, usalama na idara maalumu za Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na wananchi, kuibua na kuinua vipaji, kuendeleza na kudumisha sera ya taifa  ya michezo katika majeshi ya ulinzi na usalama na kuendeleza elimu ya viungo na utimamu wa mwili katika majeshi.

Brigedia Jenerali Mzee amesema kuwa mashindano hayo yatafunguliwa  rasmi siku ya jumamosi na Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kufungwa rasmi Machi 9 mwaka huu na Waziri mwenye dhamana ya Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi na baadaye kufuatiwa na hafla ya chakula cha jioni ambapo Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Akieleza washiriki wa mashindano hayo Brigedia Jenerali Mzee amesema kuwa timu zitakazoshiriki ni kutoka Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania, vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Jeshi la Polisi, Jeshi la kujenga taifa, Idara ya uhamiaji, Magereza na zima moto huku michezo inayotarajiwa kushindaniwa ni pamoja na mpira wa pete(kwa wanawake,) mpira wa miguu (kwa wanaume,) mpira wa mikono (kwa wanawake na wanaume,) mpira wa wavu (kwa wanawake na wanaume,) mpira wa kikapu(kwa wanawake na wanaume,) ndondi kwa wanaume, kulenga shabaha (kwa wanawake na wanaume) na riadha kwa wanawake na wanaume.

Pia amewaalika wakazi wa jiji la Dar es salaam na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya michezo hiyo ili kuweza kujipatia burudani safi kutoka kwenye vyombo vyao vya ulinzi na usalama pamoja na kujipatia fursa ya kuimarisha uelewano, urafiki na ushirikiano baina yao na vyombo vinavyowalinda.

Michezo hii ilianza rasmi mwaka 1997 ikihusisha  Brigedia na vikosi vya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania pekee na mwaka 1984 kwa mara ya kwanza michezo hiyo ilianza kuwashirikisha washiriki wengine nje ya JWTZ waliojulikana kama kanda.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) Brigedia Jenerali Suleiman Mzee akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na michezo itakayoshirikisha vyombo vya ulinzi na usalama, mashindano yanayotarajiwa kuanza kutimia vumbi jumamosi hii katika viwanja vya uhuru, jijini Dar es salaam.

WAFANYABIASHARA 7000 MBAGALA KUNUFAIKA NA MRADI WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA SOKONI

$
0
0
Naibu Balozi wa Uholanzi hapa nchini, Lianne Houben, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia katika Soko la Mbagala Rangi Tatu na Kampochea yaliyopo wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam jana. Mradi huo ambao unaendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG), unajulikana kama Mpe Riziki si Matusi.
Wasanii wa Kikundi cha Nimujo wakiigiza igizo la kupinga ukatili wa kijinsia sokoni.
Mfanyabiashara Mariam Rashid akitoa ushuhuda jinsi alivyopambana na ukatili wa kijinsia.
Katubu wa Soko la Gezaulole lililopo Manispaa ya Ilala, Salum Yusuph Salum akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Wanawake wafanyabiashara katika masoko hayo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mtaalamu Mshauri wa Miradi wa EfG, Glory Blasio, akiwajibika.
Mwezeshaji wa kisheria sokoni, Consolater Cleophas, akitoa ushuhuda kwenye hafla hiyo.
Uzinduzi ukiendelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita, akihutubia kwenye uzinduzi huo.
Viongozi wa masoko wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Soko la Kampochea, Hemed Njiwa, Mwenyekiti wa Soko la Mbagala Rangi Tatu, Mrisho Juma Mlyomi na Hanzuluni Kwemeye kutoka soko la Kampochea.
Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita akiserebuka sanjari na Naibu Balozi wa Uholanzi hapa nchini, Lianne Houben wakati wa uzinduzi huo.
Hapa ni kuserebuka kwa kwenda mbele wakati wimbo wa wanawake na maendeleo ukipigwa.
Wafanyakazi wa EfG waliojumuika kwenye uzinduzi huo.
Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, Shaban Othman, akizungumza kwa niaba ya Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu.
Mwenyekiti wa Soko la Mbagala Rangi Tatu, Mrisho Juma Mlyomi, akizungumza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EfG, Penina Reveta akizungumza.
Picha ya pamoja

Na Dotto Mwaibale

WAFANYABIASHARA 7000 katika Soko la Mbagala Rangitatu na Kampochea yaliyopo wilayani Temeke jijini Dar es Salaam kunufaika na mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia katika masoko hayo ujulikanao kama Mpe Riziki si Matusi.

Mradi huo unaendeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Equality for Growth (EfG) kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uholanzi hapa nchini ambao wametoa shilingi milioni 34 ukiwa na lengo la kuhakikisha wafanyabiashara hao wanajua haki zao na kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao pasipo kuwepo na vitendo vyovyote vya ukatili wa kijinsia.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua mradi huo jijini Dar es Salaam juzi, Naibu Balozi wa Uholanzi hapa nchini, Lianne Houben alisema nchi yake itaendelea kufadhili miradi ya namna hiyo ili kuhakikisha wafanyabiashara wanafanya biashara zao kwenye mazingira rafiki.

"Tunaunga mkono juhudi zinazofanywa na EfG za kuwawekewa mazingira bora ya kufanyia biashara wafanyabiashara masokoni" alisema Houben.

Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, Shaban Othman, akizungumza kwa niaba ya Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu alisema Serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yamekuwa yakiisaidia katika shughuli mbalimbali kama linavyofanya shirika hilo la EfG.

"Serikali imekuwa ikikaribisha wahisani na mashirika yasiyo ya kiserikali yenye nia njema ili kufanya kazi na serikali kwa lengo la kupunguza pengo lililopo serikalini na kusogeza huduma za msaada wa kisheria kwa waanchi wa Tanzania" alisema Othman.

Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita alisema utafiti uliofanywa na shirika hilo katika masoko hayo ulionesha kuwepo kwa vitendo vya ukatili kwa asilimia 78 na pia asilimia 100 hakuna msaada wa kisheria unaotolewa kwenye masoko hayo na kuwa asilimia 85 hawa ripoti vitendo vya ukatili pindi vinapotokea sokoni kwao.

RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN AMALIZA ZIARA YAKE WILAYA YA KUSINI UNGUJA

$
0
0
 Baadhi ya Viongozi wa CCM wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika ukumbi wa Hoteli ya Residence Kimzimkazi Wilaya ya Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)
 Baadhi ya Mawaziri na Viongozi wa CCM wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Hoteli ya Residence Kizimkazi wakiimba wimbo wa 'Sisi Sote Tumegomboka' wakati wa mkutano wa Majumuisho ya Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika Wilaya ya Kusini Unguja leo20-2-2019.(Picha na Ikulu) 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa Siasa na Serikali wakiwa wamesimama wakati wakiimba wimbo wa 'Sisi Sote Tumegombaka' wakati wa hafla ya Mkutano wa Majumuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Kusuini Unguja leo, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Residence Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja Mkoa wa Kusini. (Picha na Ikulu)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisoma Ripoti ya Utekelezaji ya CCM Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa mkutano wake wa Majumuisho ya ziara yake katikia Wilaya hiyo. (Picha na Ikulu)
 Katibu wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Ndg. Hafidh Hamad Mkadam, akiwakilisha Ripoti ya Utekeleza ya Kazi za CCM za Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Mkutano wa Majumuisho ya ziara yake katika Wilaya hiyo.  (Picha na Ikulu)

 Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Ndg. Idirisa Kitwana, akiwasilisha Ripoti ya Utekelezaji ya Kazi za Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa Mkutano wa Majumuisho ya Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa mkutano wake huo baada ya kumaliza ziara yake katika Wilaya hiyo.  (Picha na Ikulu)
 Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Ndg. Idrisa Kitwana akikabidhi Ripoti ya Utekelezaji wa Kazi za Wilaya ya Kusini kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa mkutano wa Majumuisho ya ziara yake uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Residence Kizimkazi Unguja leo.(Picha na Ikulu)
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar(ZAWA) Ndg. Mussa Ramadhan Haji akitowa maelezo ya uimarishaji wa huduma ya Maji Safi na Salama katika Miradi ya Usambazaji wa Maji katika Wilaya ya Kusini Unguja unavyotekelezwa na ZAWA kwa Wananchi wa Wilaya hiyo, wakati wa majumuisho ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Residence Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo, wakati kuhitimisha ziara hiyo katika Wilaya ya Kati Unguja. (Picha na Ikulu)

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdallah Juma Mabodi akizungumza wakati wa Mkutano wa Majumuisho ya Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Wilaya ya Kusini Unguja uliofanyika katiuka ukumbi wa hoteli ya Residence Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika mkutano wa Majumuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja leo,20-2-2019, katika ukumbi wa Hoteli ya Residence Kizimkazi.(Picha na Ikulu)

WANYAMA HIFADHI YA RUAHA WAFA KWA KUKOSA MAJI

$
0
0
Na Francis Godwin, Iringa.

IMEELEZWA  kuwa  shughuli  za  kibinadamu  zikiwemo  za  kilimo  zinazofanywa  kando kando  ya  mto  Ruaha  mkuu  na  vyanzo  vya maji    katika mikoa ya Njombe ,Mbeya na  Iringa ambavyo  vinaelekeza maji yake  katika  mto  Ruaha  mkuu  ni  chanzo  cha mto  Ruaha  kuendelea  kukauka na  kusababisha  baadhi ya  wanyama  wanaotegemea  maji  kuanza kufa.

Akizungumza na  wanahabari  waliotembelea  hifadhi hiyo ya  Ruaha kwa ajili ya  kuhamasisha  jamii  ya  kitanzania   kujenga utamaduni wa  kufanya  utalii wa ndani katika hifadhi  hiyo ya Ruaha na vivutio  vingine  vya  utalii mikoa ya  nyanda  za  juu  kusini , mhifadhi  mkuu wa  hifadhi ya Ruaha Iringa Izumbe  Msindai alisema  kuwa  mbali ya  vifo  vya  wanyama  kuendelea  kuongezeka  ila magonjwa ya  mlipuko kwa wanyama  yamekuwa  yakiibuka mara kwa mara.

Msindai  alisema  kuwa  hali ya  kina cha maji  katika  mto   Ruaha  mkuu kimezidi  kupungua na  kwa  sasa maji yaliyopo  ni machache  sana  na   hivyo  kupelekea  baadhi ya wanyama  kuanza  kufa kwa  kukosa maji na wengine  kumbumbwana  mlipuko kwa magonjwa mbali mbali .

 Alisema  miaka ya  nyuma   kipindi kama   hiki mto Ruaha mkuu ulikuwa  unatiririsha  maji kwa kipindi cha mwaka mzima pasipo maji  kupunguka  ila kwa  miaka ya   hivi karibuni  hadi mwaka huu maji yamekuwa yakikata mapema  zaidi na  kupelekea  wanyama  kufa kwa  kukosa maji .

"  Zimekuwepo  jitihada mbali mbali za  serikali katika  kukabiliana na uharibifu wa vyanzo  vya maji  vinavyoelekeza maji yake katika mto Ruaha na  jitihada  hizo zimeendelea  kuzaa matunda  ila bado jamii inapaswa  kuelimishwa  zaidi juu ya matumizi   sahihi ya maji " alisema 

Kwa  upande  wao kama hifadhi  ya Rauha  wamepata  kutembelea  vyanzo mbali mbali  vya maji kama kile cha Kimani wilayani Makete mkoani Njombe na kuona maji yakiendelea  kutiririka kwa  wingi ila  sababu ya  maji kutofika katika mto Ruaha  inawezekana  maji hayo yanaishia  njiani .

katika hatua nyingine  Msindai  aliwataka  wanahabari  nchini  kuwa kielelezo  chema katika Taifa kwa kuendelea  kuhamasisha  jamii  kuepuka uharibifu  wa mazingira  pamoja na  kuwahamasisha watanzania  kutembelea   hifadhi  hiyo ya  Ruaha  kujifunza utali  wa ndani  badala ya  kuwaachia  wageni  kutoka nje .

Alisema kuwekuwa na tofauti kubwa ya gharama za kiingilio  katika  hifadhi  kati ya  watalii wa ndani na watalii wa  kigeni na  kuwa serikali  kupitia   wizara  husika  imefanya  hivyo  ili  kila mtanzania kuweza  kutembelea  hifadhi  bila kikwazo chochote na kuwa  serikali imeendelea  kuboresha  miundo mbinu ya  kufika  hifadhini hapo kirahisi zaidi .

Mhadhiri  wa  chuo  kikuu cha Iringa   Jimson Sanga ambe ni mratibu wa  mradi wa  kuendeleza  utamaduni na utalii nyanda za juu  kusini alipongeza  jitihada za  hifadhi ya  Ruaha  Iringa kwa  kuendelea  kutumia  mbinu mbali mbali  za kuitangaza hifadhi  hiyo  kwani  alisema   pamoja na kuwa  hifadhi ya  Ruaha  ni kubwa  kuliko  zote Afrika ila kwa Tanzania nguvu za utalii  zilielekezwa  hifadhi  za kaskazini ila  sasa  serikali imepania  kuelekeza   nguvu zake katika hifadhi za  kusini ikiwemo ya Ruaha Iringa .

Sanga alisema  iwapo  vyombo  vya habari vitaendelea na kasi ya  kueleza uzuri wa  hifadhi za kusini ni  wazi Taifa linaweza kuongeza mapato  yake  kutokana na sekta hiyo ya utalii  pekee .

 Tembo  wa  hifadhi ya  Ruaha  mkoani Iringa wakihangaika kutafuta  maji katika  vidimbwi  kufuatia kukauka kwa mto Ruaha mkuu  kutokana na uendeshaji  wa shughuli za kibinadamu kando kando ya mto Ruaha kwa mikoa ya Iringa , Mbeya na Njombe (PICHA NA  FRANCIS GODWIN).
Baadhi ya wanahabari kutoka mkoa wa Iringa na Morogoro wakiwapiga picha wanyama aina ya Pundamilia waliokuwa wakijipatia malisho yao ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa ,waandishi hao walikuwa katika ziara ya utalii wa ndani kama sehemu ya kuhamasisha watanzania kutembelea hifadhi ya Ruaha Iringa juzi (picha na Francis Godwin)




Wachimbaji wadogo wilayani Mbogwe wafurahia ahadi ya kupata umeme ndani ya Siku Kumi.

$
0
0
Na Teresia Mhagama,

Wachimbaji wadogo katika machimbo ya Nyakafuru yaliyo katika Kijiji cha Nyakafuru wilayani Mbogwe wameonesha kufurahishwa na ahadi ya Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ya kufikisha umeme katika machimbo hayo ndani ya siku kumi.

Ahadi hiyo aliitoa jana mara baada ya kufanya ziara ya kikazi wilayani Mbogwe mkoani Geita ambapo akiwa katika machimbo hayo, wachimbaji hao walilalamika kuhusu gharama kubwa wanazotumia katika kununua mafuta ya kuendesha mitambo mbalimbali ikiwemo ya kuchenjulia ya madini.

Kwa nyakati tofauti walieleza kuwa, mchimbaji mmoja anaweza kutumia zaidi ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya mafuta ya kuendeshea mitambo suala ambalo linawafanya kutopata faida inayostahiki katika shughuli zao.

Kutokana na hilo, Dkt Kalemani alisema kuwa, “kutoka umeme unapoishia hadi hapa ni kilometa 1.5 tu, na hapa kuna wachimbaji wadogo zaidi ya Elfu Nne na mashine za kuchenjulia madini zaidi ya 200, hivyo nakuagiza Meneja wa TANESCO kuleta umeme hapa ndani ya siku Kumi na pia muwafungie transfoma itakayohudumia eneo hili,”.

Waziri wa Nishati pia alitembelea mitambo ya kisasa ya kuchenjulia madini tani 10 kwa saa ambayo ipo katika Kijiji cha Shenda wilayani Mbogwe ambayo nayo uendeshaji wake unatumia mafuta badala ya umeme.

Baada ya kukagua mitambo hiyo, Dkt. Kalemani alimwagiza Meneja wa TANESCO wilayani Mbogwe kuhakikisha kuwa, ifikapo tarehe 25 mwezi huu awe ameshafikisha umeme katika eneo hilo.

Akiwa wilayani Mbogwe, Dkt Kalemani pia alikagua kazi ya usambazaji umeme katika Kijiji cha Bulugala na kukuta nguzo zimesimikwa huku nyaya zikiwa bado hazijavutwa hivyo alimuagiza mkandarasi wa umeme (kampuni ya WhitecityGuangdong JV) kuwasha umeme katika Kijiji hicho kabla ya tarehe 5 mwezi ujao.

Katika ziara yake wilayani Mbogwe pia aliwasha umeme katika Kijiji cha Kasosobe, Kitongoji cha Mkolani ambapo awali alielezwa kuwa umeme huo bado haujafika katika maeneo muhimu ya kijamii kama Shule na Nyumba za ibada pamoja na vitongoji vingine vya Kijiji hicho.

Dkt Kalemani alimuagiza mkandarasi wa umeme kufikisha umeme katika vitongoji vyote vya Kijiji hicho ikiwemo ikiwemo Shule, na Nyumba za Ibada ndani ya siku 14.

Vilevile Dkt.Kalemani alifanya ziara katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo aliwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Ryobaika, kilicho katika Kata ya Uyovu na kutoa wasaa kwa wananchi kulipia huduma ya umeme mapema na wataalam wa TANESCO pamoja na mkandarasi kutokataa malipo ya wananchi kwa kisingizio chochote kile.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa umeme katika Kijiji chaKasosobe, Kitongoji cha Mkolani wilayani Mbogwe. Wa Tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tatu kutoka kulia) akiwa katika machimbo ya Nyakafuru yaliyo katika Kijiji cha Nyakafuru wilayani Mbogwe ambapo aliwaahidi wachimbaji wadogo wa eneo hilo kupata umeme ndani ya siku Kumi.
Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nishati aliyokuwa akiitoa katika Kijiji cha Ryobaila wilayanu Bukombe ambacho kimepata huduma ya umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) akikagua mitambo ya kisasa ya kuchenjulia madini tani 10 kwa saa ambayo ipo katika Kijiji cha Shenda wilayani Mbogwe na kuahidi kupeleka umeme hivi karibuni.

Tanzania na Umoja wa Ulaya waazimia kuimarisha Uhusiano

$
0
0
Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kuimarisha uhusiano na ushirikiano kwa kufanya majadiliano ya mara kwa mara yatakayojengwa katika misingi ya kuaminiana, usawa, uwazi na kuheshimiana ili kujenga uelewa wa pamoja katika maeneo mbali mbali yenye changamoto kwa manufaa mapana ya watu wa pande zote mbili.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) na Mkurugenzi wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki, Huduma za Nje katika Umoja wa Ulaya, Bw. Patrick Simonnet wakati wa ziara yake iliyofanyika nchini kuanzia tarehe 17 hadi 20 Februari 2019.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri aliushukuru Umoja wa Ulaya kwa misaada ambayo umekuwa ukiipatia Tanzania kwa ajili ya utekelezji wa miradi mbalimbali ya maendelea katika sekta za kilimo, nishati na ujenzi wa miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege. “Umoja wa Ulaya ni mbia muhimu wa Tanzania katika shuguli za maendeleo tokea mahusiano rasmi ya kidiplomasia yalipoanzishwa mwaka 1975; baada ya kusainiwa kwa mkataba wa kwanza wa Rome baina ya kundi la nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (ACP) na nchi wanachaama wa Umoja wa Ulaya”; alisema Mhe. Mahiga.

Viongozi hao walihitimisha mazungumzo yao kwa kuazimia kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya pande mbili hizi katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, ushirikiano wa maendeleo na usalama wa majini, hususan katika pwani ya Bahari ya Hindi.

Aidha, walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kimataiafa ikiwa ni pamoja na kusaidia juhudi za kudumisha na kuimarisha hali ya amani, usalama na utulivu katika eneo la Maziwa Makuu.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
21 Februari 2019

AQRB Yaendesha Mafunzo Maalumu kwa Wanafunzi Wanaosoma Masomo ya Sayansi

$
0
0

Na Philemon Solomon

BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) imeendesha mafunzo maalumu kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kwa shule za sekondari ili waweze kuzitofautisha taaluma hizo na ile ya wahandisi.

Akizungumza na wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi shule ya Azania Jijini Dar es Salaam February 21, 2019 Ofisa Mafunzo wa AQRB Matondo Daniel aliwataka wanafunzi kuutambua umhimu wa taaluma hizi katika mustakabli wa maendeleo ya taifa.

"Taaluma ya wataalamu wa Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi ni muhimu kwa taifa kutokana na uhaba wa wataalamu wa fani hiyo kwa sasa,"alisema Matondo na kuongeza kuwahamasisha wanafunzi wa sayansi kusoma taaluma hiyo ili kulipunguzia taifa changamoto ya wataalamu hao.
Alisema tathimini zinaonesha kuwa wataalamu wa fani hiyo ni wachache na kwamba mpaka sasa kuna Wabunifu Majengo 474 na Wakadiriaji Majenzi 427 nchi nzima hao ni wale ambao wanatambuliwa na Bodi.

Pia alisema kutokana na idadi hiyo ipo haja kwa taifa kuwa na idadi kubwa zaidi ili hapo baadaye taifa liwe na wataalamu wa kutosha katika taaluma hiyo ambao wataweza kusimamia nchi kuwa na makazi na majengo bora.

Akizungumzia upande wa sheria ya majengo alisema mpaka sasa bado haijawa tayari na kwamba serikali ipo mbioni kuikamilisha ili iweze kusimamia vyema majenzi na kuwabana wote ambao watakwenda kiyume cha taratibu kwa kuwapeleka kwenye vyombo husika ili sheria ifuate mkondo wake.

Kwa upande wao wanafunzi wa sayansi shuleni hapo wamefurahia sana kupata elimu juu ya utoafuti baina ya wahandisi na wajkadiriaji majenzi na kuiomba bodi kuendelea kuisambaza elimu hiyo kwa wanafunzi wengi zaidi ili aweze kuhamasika na kuzisomea taaluma hizo mara watakapomaliza masomo yao ya sekondari.

Godlove Kapufi mwanafunzi wa shule hiyo anayechukua PCM aliema kuwa anashukuru kupata elimu hiyo na atajitahidi kuwashawishi na wenzake kuisoma kwani anaamini iko katika soko.

"Sikuwa nafahamu kabisa taaluma hiyo, nashukuru sana AQRB kwa kutuelewesha naamini kufanya hivi kutatuwezesha kufanya uchaguzi mzri wa fani hapo mbele na kuweza kupunguza mzigo kwa serikali kwa kutokuwa na wataalamu wa kutosha wa taaluma hio,"alisema Kapufi.

Naye Mohamed Ally mwanafunzi mwingine wa kidato cha tano shuleni hapoa nayesoma PCM aliiomba bodi iishie hapo badala yake iendelee kuisambaza elimu hiyo nchi nzima ili vijana ambao ni wanafunzi wa sayansi waweze kuzitambua fursa zilizopo katika maomo hayo.

Alisema hapo awali wengi wao walikuwa wakijua mwanafunzi anayesoma sayansi anaweza kuwa daktari, mhandisi na zingine lakini walikuwa hawajui kama kuna taaluma ya wabuinifu majengo na wakairiaji majenzi.
 Ofisa Mafunzo kutoka Bodi  ya Usajili wa Wabunifu  Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Matondo Daniel akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule ya sekandari ya Azania jijini Dar es Salaam  juu ya umuhimu wa kusoma masomo ya  Sayansi.( PICHA NA PHILEMON SOLOMON).

Dodoma Yajipanga Kuokoa Maisha ya Wajawazito, Mama na Mtoto


TANGAZO: AMEPOTEA ANATAFUTWA

$
0
0
NDUGU JOHN STEPHEN MAKINDA (KABAKULI) MKAZI WA IGUNGA-TABORA ,AMEPOTEA TAREHE 16.02.2019 YEYOTE ATAKAYEMWONA APIGE SIMU NAMBA 0784485104 AU 0768959660

Mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Kuutangaza Utalii wa Tanzania nje ya Nchi

$
0
0
Na Grace Semfuko-MAELEZO 

Bodi ya Utalii Tanzania TTB kwa kushirikiana na Magnet Youth Sports Organization ya Tanzania February 15 hadi 19 mwaka huu walishirikiana katika kuandaa safari ya kitalii ya kocha andreas Pach na Martin Hammel wa Ujerumani ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kutembelea vivutio vya Utalii lengo likiwa ni kuutangaza Utalii wa Tanzania. 

Andreas Pach na Mwenzake Martin Hammel ni Makocha ambao wapo nchini Tanzania wakitokea kwenye mradi wa ITK Pathfinder 2019 uliopo chini ya Chuo Kikuu cha Leipzig cha nchini Ujerumani mradi ambao unalenga kuwafundisha Makocha na Vijana kwenye mchezo wa Soka na kumtangaza Mchezaji nyota mwenye asili ya Tanzania anaechezea Ligi daraja la kwanza nchini Ujerumani Yusuph Poulsen. 

Wakiwa Nchini Tanzania Makocha hao walipata nafasi ya kutoa mafunzo ya michezo kwa makocha 25 na Vijana 120 wa Kitanzania lengo likiwa ni kukuza Vipaji vya michezo nchini. 

Ujio wa makocha hao ni mwaliko wa Magnet Youth Sports Organization chini ya Mkurugenzi mwendeshaji wake Tuntufye Mwambusi ambapo bodi ya utalii kupitia ujio huo wameamua kushirikiana katika kuutangaza utalii wa ndani ikiwepo Mlima Kilimanjaro 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alisema bodi hiyo imeanza mazungumzo ya wali na mchezaji huyo nyota Yusuph Poulsen ambaye anachezea ligi daraja la kwanza nchini Ujerumani ili kuutangaza Utalii wa ndani. 

“kwetu sisi TTB tunachukulia ujio huu wa makocha hawa na mashirikiano yaliyopo kati ya ITK na Tanzania, na tumeanza mazungumzo na Mchezaji mwenye asili ya Tanzania Bw. Yusuph Poulsen ikiwa ni mkakati wetu wa kutumia watu maarufu katika kuutangaza utalii wa ndani na tunataka kumfanya kuwa Balozi wa hiyari wa utalii wa Nchi yetu” alisema Jaji Mstaafu Thomas Mihayo. 

Nae mmoja kati ya makocha hao wawili wa kutoka Nchini Ujerumani Bw.Andreas Pach alisema Tanzania kuna Vipaji vingi vya Michezo na hivyo ni muhimu kuviendeleza. 

“tumefurahishwa kuona Watanzania ni watu wakarimu, Tanzania kuna Vijapi vingi vya Michezo na vipaji hivi vikiendelezwa tutakuwa mbali kimichezo, Poulsen anafanya Vizuri sana kule Ujerumani” alisema Andreas Pach 

Kwa upande wake Mkurugenzi mwendeshaji wa Magnet Youth Sports Organization Bw. Tuntufye Mwambusi alisema wataendelea kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania na wanamichezo katika kukuza Utalii wa Tanzania.

Airtel yazindua Dabo Data na SMATIKA

$
0
0
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isaac Nchunda, akionyesha bango la promosheni ya ‘Dabo Data na Smatika’ wakatin wa uzindulzi wa promosheni hiyo Dar es Salaam jan, Dabo Data na SMATIKA itamwezesha mteja wa Airtel Money kupata mara mbili ya bando kwa bei ile ile y ash 2000. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isaac Nchunda, akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya ‘Dabo Data na Smatika’ itakayomwezesha mteja wa Airtel Money kupata mara mbili ya bando kwa gharama ileile ya sh 2000, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando.


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza kuzindua ofa mpya kwa wateja wake inayojulikana kama Dabo Data na SMATIKA ambapo inawawezesha wateja wake wanaotumia huduma ya Airtel Money kupata mara mbili zaidi kila wanaponunua bando kupitia Airtel Money kuanzia leo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza uzindua huo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isaac Nchunda alisema kuwa “Promosheni ya Dabo Data na SMATIKA itawafaidisha wateja wetu wanaonunua vifurushi kujipatia bando mara mbili yaani 2GB kwa bei ileile ya Sh 2,000 badala ya ilivyokuwa awali 1GB, vilevile mteja ataweza kudumu na bando hilo la 2GB kwa muda wa siku tatu, Nchunda aliongeza kuwa “kulingana na ripoti ya TCRA ya hivi karibuni inaonyesha kuwa wateja wanaoutumia huduma ya kifedha ya simu za mkononi imeongezeka kutoka 21 milioni Disemba 2017 mpaka kufikia 23 milioni kwa sasa na hii ndio inayotupa msukumo sisi Airtel kuenedelea kuleta huduma za kibunifu kama hizi ili kuwarahisishia wateja wetu kila mahali.”

“Airtel Tanzania bado tunaendelea kuleta huduma na bidhaa ambazo ni nafuu na zenye ubunifu zaidi ili kuendelea kukidhi matakwa ya wateja wetu, aliongeza Nchunda.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Airtel Jackson Mmbando alisema kuwa kuzinduliwa kwa huduma hii ya Dabo Data na SMATIKA ni hatua nyingine muhimu ya kuendelea kubadilisha maisha ya wateja wetu. ‘Tunaona wateja wengi wanaongezeka na kutumia huduma ya Airtel Money. Kuanzia leo, mteja yeyote wa Airtel Money anaweza akanunua bando ya Dabo Data na SMATIKA kwa kupitia menu ya Yatosha *149*99# kisha changua 1 na kuchagua Dabo Data na SMATIKA. Vile vile, mteja anaweza kupiga menu ya Airtel Money moja kwa moja *150*60# kisha akachangua 2, aliongeza Mmbando.

Airtel tunaamini kwa kuwapatia wateja wetu uhuru wakuchagua huduma watakayo kama hivi, inaokoa muda wa mteja kupata huduma haraka na hiyo kuongezea faida kwa mteja kuona thamani ya matumizi ya fedha yake kutokana na unafuu. Kwa sasa mteja atapata mara mbili kwa kutumia Dabo Data na SMATIKA na atalipa kwa Airtel Money yake kuendelea kufurahia huduma zingine za Airtel Money.

“Dhamira ya Airtel ni kuendelea kuwekeza kwenye huduma zetu zote kama ilivyo kwa Airtel Money ambapo hadi sasa Airtel tayari imefikisha huduma za Airtel Money kila kona kwa kusambaza Airtel Money Branch zaidi ya 500 nchini kote, Lengo letu kwa kupeleka maduka haya karibu na wateja zaidi ni kudhihirisha mkakati wetu wa kuwa kampuni ya simu za mkononi ambayo inatoa suluhisho kwenye huduma za kifedha hapa nchini. Nia yetu ni kuendelea kujenga mtandao imara na kutengemea huduma rafiki kama Airtel Money aliongeza Mmbando.

KISARAWE YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 30 KWA MWAKA 2019 /2020

$
0
0
VICTOR MASANGU, KISARAWE

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoa wa Pwani imeazimia kwa pamoja kupitisha makadirio ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2019 /2020 kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na matumizi mengine.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la kupitisha bajeti ya mwaka 2019 /2020 amewataka watendaji wote kuachana kabisa na tabia ya uzembe na badala yake wahakikishe wanajikita zaidi katika kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na kuongeza kasi katika suala zima la ukusanyaji wa mapato kwa maslahi ya wananchi.

“Kwanza kabisa nipende kuwashukuru madiwani na watendaji wote ambao kwa namna moja au nyingine mmeweza kushirikiana kwa pamoja hadi kuweza kufanikisha mpango huu wa bajeti kwa hiyo kikubwa mimi ninachowaomba tuongeze kasi zaidi katika kukusanya mapato ya ndani ili tuweze kufikia malengo ambayo tumejiwekea,”alisema Dikupatile.

Aidha alisema kwamba lengo kubwa la halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ni kuweka mikakati madhubuti katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ya nadani pamoja na kuibua miradi mingine mbali mbali ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kukubwa katika suala zima la kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wake Diwani wa wa kata ya Kibuta Mhandisi Mohamed Kilumbi akizungumza kwa niaba ya wenzake amebainisha kuwa bajeti ambayo wameipitisha itaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo ikiwemo kumuunga Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kutekeleza azma ya ujenzi wa viwanda.

Naye Mkurugenzi mteandaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama amesema kwamba atahakikisha kwamba anaimarisha mifumo yote kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato ya nadani sambamba na kuongeza uzalishaji katika kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa lengo la kuondokana na wimbi la umasikini.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe Halfan Sika amempongeza Rais wa awamu ya tano Dk John Pombe Magufuli katika suala zima la upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa wananchi na kuwaasa wakandarasi kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwemo kumaliza tenda wanazopatiwa kwa wakati na ziwe katika ubora unaotakiwa.
 Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza na wajumbe wa kikao cha baraza la madiwani mara baada ya kupitisha makadirio ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa 2019 /2020 kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi mengine.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Baadhi ya viongozi wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, kulia ni Mbunge wa viti maalumu Zainabu Vulu,kati kati ni  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Mussa Gama na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Hamisi Dikupatile.
 Mbunge wa viti maalumu kupitia Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu akichangia jambo katika kikao hicho cha baraza la madiwani halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kupitisha mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2019 /2020
Baadhi ya madiwani wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.

Waziri Kalemani Amkabidhi Kifaa Cha Umeme tayari (UMETA) Mkazi Wa Kijiji Cha Ryobaika Bukombe.

Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kuharakisha utolewaji wa matibabu yao

$
0
0
Na Mwandishi maalum

21/02/2019 Kuwepo kwa chumba cha watoto wenye matatizo ya moyo walioko katika uangalizi maalum (ICU) katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuharakisha utolewaji wa matibabu yao.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Idara ya watoto wenye magonjwa ya moyo Dkt. Sulende Kubhoja wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi.

Dkt. Kubhoja alisema chumba hicho chenye vitanda nane kipo katika wodi mpya ya watoto ambayo imejengwa na kufanyiwa ukarabati imeanza kutumika mwanzoni mwa wiki hii.

“Mwanzo ilikuwa ni changamoto pale ambapo mtoto alitakiwa kupata huduma ya dharula na kulazwa katika chumba cha uangalizi maalum lakini kuwepo kwa ICU yao kutaharakisha upatikanaji wa huduma hiyo”.

“Kabla ya kuanza kutumika kwa jengo hili watoto walikuwa wanatibiwa katika jengo ambalo watu wazima walikuwa wanatibiwa na hivyo kutokuwa na nafasi ya kutosha. Hivi sasa watoto wana jengo lao ambalo lina nafasi kubwa na kuwafanya wapate nafasi ya kucheza tofauti na ilivyokuwa awali”, alisema Dkt. Kubhoja.

Alisema kutokuwachanganya watoto na watu wazima kutaboresha huduma kwani dawa na vifaa tiba zitakuwa kwa ajili ya watoto na mazingira ya cliniki na wodini yatakuwa rafiki kwao tofauti na ilivyokuwa awali.

Kwa upande wake Afisa Muuguzi ambaye ni msimamizi wa wodi ya watoto Husna Mzungu alisema kukamilka kwa ukarabati wa jengo hilo ni jambo jema na la furaha kwani kumebadilisha muonekano wa wodi ya watoto ukilinganisha na ilivyokuwa awali.

Husna alisema katika jengo hilo jipya kuna vitanda vya kutosha ambavyo vinasaidia kuwaweka watoto katika mazingira ya nafasi na kuweza kulala mmoja mmoja ukilinganiha na wodi ya zamani ambako kulikuwa na vitanda vichache vya watoto, hivyo kukiwa na wagonjwa wengi walikuwa wanapata tabu.

Jengo hilo lina ofisi nane, vyumba vya madaktari vinne, wodi yenye vitanda 41 kati ya hivyo 23 viko katika wodi ya kawaida, nane chumba cha uangalizi maalum (ICU) na 10 wodi ya kulipia.Gharama za ujenzi na ukarabati wa jengo hilo ni shilling bilioni 1.3 ambapo asilimia 60 ya fedha hizo zimetolewa na Serikali na asilimia 40 zimetolewa na Jumuia ya Kihundu nchini (BAPS Charity).
Wazazi wakiwa katika jengo jipya la watoto la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuwapeleka watoto wao kwa madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kupata matibabu.Picha na JKCI 
Picha ya Jengo jipya la watoto la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambalo lina ofisi nane, vyumba vya madaktari vinne, wodi yenye vitanda 41 kati ya hivyo 23 viko katika wodi ya kawaida, nane chumba cha uangalizi maalum (ICU) na 10 wodi ya kulipia. Kuwepo kwa jengo hilo kutaboresha huduma za matibabu ya moyo kwa watoto.

Shabiki wa Simba atajirika na M-Bet

$
0
0
 Shabiki wa Simba, Arsenal na Real Madrid, Simon Eusebi Muray (32) ameshinda kitita cha Sh 81,097, 540. Baada ya kutabiri kwa baada ya kubashiri kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake jana, Muray ambaye ni mkazi wa Katesh, Hanang, mkoa wa Manyara amesema kuwa atatumia fedha hizo kuongeza mashamba ya vitunguu, kuboresha nyumba yake na kupanua duka la bidhaa za rejareja kuwa la jumla.

Muray alisema kuwa mbali ya kujiendeleza katika masuala ya kilimo, pia atafungua ofisi ili kufanya shughuli zake za kilimo na biashara kisasa zaidi.

“Nina mashamba ya vitunguu eneo la Mkalama, mkoa wa Singida ambayo kutokana na mtaji huu, nitaongeza wigo wa kilimo na vile vile kuboresha nyumba yangu. Nataka kuwa mkulima wa kisasa na mwenye malengo ya kufanya vyema katika sekta hiyo huku nikifanya biashara zangu,” alisema Muray.

Alisema kuwa alipokea taarifa za ushindi kwa furaha sana kwani katika maisha yake, hakutarajia kupata kiasi hicho cha fedha.

“Pia nitamwamisha mtoto wangu wa kutoka shule ya kawaida na kwenda ya kimataifa. Huu ni ushindi wa maana sana kwangu kwani kwa kutumia sh1,000 kushinda kiasi hiki kikubwa cha fedha, ni faraja kubwa sana kwangu, nilianza kucheza muda mrefu na nilibishana na afisa wa M-Bet kwani niliamini kuwa ni matapeli,” alisema.

Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi kuwa Murray anakuwa anakuwa mshindi wa pili wa mwaka huu ikiwa mshindi wa pili kushinda kiasi kikubwa cha fedha tokea kuanza mwaka huu.

“M-Bet ni nyumba ya mabingwa na Murray amejiunga tena na nyumba ya mabingwa kwa kushinda kiasi kikubwa cha fedha ambacho kitabili maisha yake, tunawaomba Watanzania kucheza michezo ya M-Bet ili kuweza kushinda kiasi kikubwa cha fedha na kuanza maisha mapya,” alisema Mushi. 

Naye, Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala alimpongeza Muray kwa ushindi na pia kuipongeza kampuni ya M-Bet kwa kuwa walipa kodi wazuri kwa serikali.
 
 Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi  (Kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa droo ya Perfect 12, Simon Murray (Katikati)  kutoka Manyara aliyejishindia  Sh 81.1milllioni baada ya kubashiri matokeo ya mechi 12 kwa usahihi. Kushoto ni Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala.
 

Wadau wa Mradi wa Utambuzi Wasanii wa Sanaa za Ufundi Nchini Wamtembelea Waziri Mwakyembe.

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wadau wa Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi Tanzania (TACIP) wakati walipomtembelea ofisi ndogo za Dar es Salaam kwa lengo la kutoa tathmini ya maendeleo ya mradi huo
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wadau wa Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi Tanzania (TACIP) wakati walipomtembelea ofisi ndogo za Dar es Salaam kwa lengo la kutoa tathmini ya maendeleo ya mradi huo
 Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) Bw. Adrian Nyangamalle (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati walipomtembelea ofisi ndogo za Dar es Salaam kwa lengo la kutoa tathmini ya maendeleo ya Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi Tanzania (TACIP).

 Mkurugenzi wa Biashara na Uhusiano toka DataVision International, Bi. Teddy Qirtu (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) wakati walipomtembelea ofisi ndogo za Dar es Salaam kwa lengo la kutoa tathmini ya maendeleo ya Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi Tanzania (TACIP), katikati ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) Bw. Adrian Nyangamalle.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia kadi ya utambuzi wa wasanii wa sanaa za ufundi wakati alipotembelewa na wadau wa Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi Tanzania (TACIP) katika ofisi ndogo za Dar es Salaam kwa lengo la kutoa tathmini ya maendeleo ya mradi huo.

 Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasilano (TEHAMA) toka DataVision International, Dkt. Dkt. Shaban Kiwanga ( kulia) akifafanua jambo kwa  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) wakati walipomtembelea ofisi ndogo za Dar es Salaam kwa lengo la kutoa tathmini ya maendeleo ya Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi Tanzania (TACIP),  wa pili toka kushoto ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Biashara na Uhusiano toka DataVision International, Bi. Teddy Qirtu.


Kaimu Katibu Mtendaji toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Onesmo Kayanda (kushoto)  akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wadau wa Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi Tanzania (TACIP) walipomtembelea Waziri Mwakyembe katika ofisi ndogo za Dar es Salaam kwa lengo la kutoa tathmini ya maendeleo ya mradi huo.

Picha na WHUSM – Dar es Salaam.


Serengeti Boys yajifua vilivyo jijini Arusha.

$
0
0
Maandalizi ya timu ya Serengeti Boys wakiwa Kambini Arusha,wakifanya Mazoezi leo asubuhi na jioni katika  Uwanja wa Aghakhan 



MAMIA YA WAOMBOLEZAJI WAAGA MWILI WA MENEJA MAWASILIANO WA TFS GROLY MZIRAY,KUZIKWA KESHO MORO

$
0
0

Mume wa Marehemu Glory Mziray aliyekuwa Meneja wa Uhusiano Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Akiwa na Watoto wake wakitoa Heshima ya Mwisho kwenye ibada ya kuaga Marehemu huyo katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam, ambapo Marehemu amaeagwa hapo na wakazi wa Dar es Salaam kisha kusafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao Mikese Morogoro.
 Wahubiri wakitoa Baraka na Heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Glory Mziray ambae alikuwa Meneja Mahusiano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).
 Watoto wa Marehemu Glory Mziray wakiongoza mbele na Msalaba wakati wakiondoka Katika Kanisa la KKT Usharika wa Mbezi Beacha Kuelekea Mjini Morogoro.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Dk Mary Mwanjelwa akitoa Salamu Kabla ya kuaga Mwili wa Marehemu Glory Mziray aliyekuwa Meneja Mahusiano wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) ,Dk.Mwanjelwa amezungumzia jinsi alivyo mfahamu Mziray tangu alipokuwa nae katika Chuo kikuu cha Mtakatifu agustino na kutaja umhiri wake katika kutimiza wajibu na majukumu anayopewa.
 Mkurugenzi wa Huduma za Misitu ,Emmanuel Willfred, akizungumza na kutoa wasifu wa Marehemu Glory Mziray enzi za uhai wake katika eneo lake la kazi kama Meneja wa Mahusiano.
 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Tume kudhibiti Ukimwi  Tanzania(TACAID'S),Fatuma Mrisho akizungumza juu ya uzoefu wake katika kazi na Marehemu Glory Mziray.

 Sehemu ya Wafanyakazi wa TFS wakitoa heshima za Mwisho kwa Marehemu Glory mziray
 Sehemu ya Watu mbalimbali waliojitokeza kuaga Mwili wa Marehemu Glory Mziray katika ibada iliyofanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Beach.


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAMIA ya waombolezaji wamejitokeza kwa wingi katika Kanisa la KKKT lililopo eneo la Tangi Bovu  jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa Meneja Habari na Mawasiloano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) Groly Mziray 

Groly Mziray ameagwa leo Februari 21 ,2019 kanisani hapo kuanzia saa saba mchana baada ya kufanyika ibada maalumu.Marehemu Groly atazikwa kesho Ijumaa huko Mikese mkoani Morogoro. Baada ya mwili wake kuagwa kanisani hapo safari ya kuelekea Mikese ilianza. Glory alizaliwaDesemba 27, 1980 na ameacha mume na watoto wawili.

Wakati wa kumuaga vilio,simanzi na majonzi vilitawala Kanisani hapo kutokana na baadhi ya waombolezaji kushindwa kujizuia maumivu yaliyopo moyoni kutokana kifo cha  ghafla kwa Groly Mziray.

Baadhi ya waombolezaji wameiambia Michuzi Blog kuwa kifo cha Groly ni pigo kubwa kwao na eneo ambalo alikuwa anafanyia kazi na watamkumbuka kwa namna ambavyo aliamini katika kufanya kazi kwa bidii na hakuwa mwenye kukata tamaa.

Akimzungumza mbele ya waombolezaji, Mkurugenzi wa Huduma za Biashara kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Wilfred Emmanuel amesema Groly Mziray alikuwa ni mtumishi aliyekuwa anajitoa kwa dhati kwa ajili ya taasisi hiyo na kubwa zaidi alikuwa na mikakati yenye lengo la kuhakikishia taasisi yao inapiga hatua zaidi katika kutoa huduma.

Amefafanua wiki iliyopita walikuwa naye  Morogoro kwa ajili ya kuandaa bajeti na anakumbuka kwenye kikao hicho Groly alitoa maoni na mipango yenye kuifanya TFS inatekeleza majukumu yake vizuri.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dk.Mary Mwanjelwa ameeleza Groly enzi za uhai wake alikuwa mtu mwenye jitihada na kupenda kujifunza na alipenda kusaidia wengine.

Amesema kuwa yeye alisoma na Glory Shahada ya pili na walipokuwa  darasani alikuwa ni mwenye kujituma."Alipenda sana kujifunza na kushirikiana na wenzi.Ni mtu mwenye kusimamia haki na alikuwa na upendo sana". 

Wakati huo huo Msemaji wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Tabu Shaibu amesema kuwa Groly ni kati ya watu waliokuwa mfano kwani alikuwa mpambanaji na hakuwa mwenye kukubali kushindwa na hasa katika mambo ambayo aliona yana tija.

"Kwangu Groly mbali ya kuwa mtumishi mwenzetu akihudumu TFS lakini alikuwa mdogo wangu.Kwa kweli ameondoka tukiwa bado tunamuhitaji lakini tumshukuru Mungu kwa kutupa Groly ingawa leo hii hatunaye tena hapa duniani.Nenda mdogo wangu ,tutakukumbuka daima," amesema Shaibu.

UPDATES YA MSIBA Mtoto wa Waziri Kigwangalla

$
0
0
#UPDATEMSIBA wa Zulqarinain Mtoto wa Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni  Waziri wa Maliasili na Utalii  Dk.Hamisi Andrea  Kigwangalla upo nyumbani kwake Mikocheni A katika Kota za Mawaziri jirani na Victoria.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Familia Bwana  Lumola anataarifu kuwa mwili utasafirishwa kesho asubuhi kwa  ndege na Mazishi yanatarajiwa kufanyika saa Kumi jioni Nzega Vijijini  Jimboni kwa Waziri Dk Kigwangalla.

Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani Dar es Salaam  na Nzega Vijijini.

Msiba umetokea leo February 21 majira ya Saa nne asubuhi  JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE - MUHIMBILI. Zulqarinain alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo.
#R.I.P. Zul.

Inna lillahi wainna illaihi rajiuun

 Baadhi ya watu wakiwemo mawaziri na Majirani  waliojitokeza kwenye msiba mtoto  wa Dk. Kigwangalla muda huu

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AAZA ZIARA YAKE KISIWANI PEMBA KWA UZINDUZI WA BARABARA YA MKANYAGENI HADI KANGANI WILAYA YA MKOANI PEMBA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi la Barabara ya Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba, akiwa katika ziara yake ilioaza leo.(Picha na Ikulu) 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kulia Mama Mwanamwema Shein na kushoto Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dr.Sira Ubwa Mwamboya, wakisoma jiwe la Msingi la Barabara ya Mkayangeni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani baada ya kuweka jiwe la msingi, akiwa katika ziara yake kisiwani Pemba leo,21-2-2019.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Mkanyageni wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi lac Barabara ya Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba, iliojengwa kwa Kiwango cha lami.kushoto Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dr, Sira Ubwa Mwamboya  na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.(Picha na Ikulu )
 WANANCHI wa Kijiji cha Mkanyageni Kisiwani Pemba wakifuatilia hafla ya Uzinduzi na Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Barabara mpya iliojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Mkanyageni hadi Kangani, iliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba leo.(Picha na Ikulu)
 KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe akitowa maelezo ya Kitaalam ya ujenzi wa Barabara ya Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dr, Sira Ubwa Mwaboya akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi na Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Barabara ya Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba.(Picha na Ikulu)
 MWANANCHI wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba akifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la Barabara ya Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba.(Picha na Ikulu)


Viewing all 109974 articles
Browse latest View live




Latest Images