Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110087 articles
Browse latest View live

Dodoma Kupambana na Vifo vya Akina Mama na Watoto Wachanga

$
0
0
Na Adelina Johnbosco, MAELEZO- Dodoma 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge amezindua rasmi kampeni ya ‘JIONGEZE! TUWAVUSHE SALAMA’ jijini Dodoma, kampeni ambayo imelenga kumsaidia mama mjamzito kujifungua salama.Katika hotuba yake Mhe.Mahenge, amewataka viongozi wote kuwa washiriki na watendaji wa kampeni hii, ili kuhakikisha mama anakuwa salama kwa kutoa elimu ya uzazi popote kwa wananchi. 

Aidha, amesema lengo la tamko hili ni kuongeza kasi ya uwajibikaji katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga nchi nzima. 

‘’Tumeamua kuchukua kuchukua hatua hii muhimu kwa sababu, kifo cha mama mjamzito au anayejifungua au aliyejifungua na kifo cha mtoto mchanga aliyezaliwa havikubaliki,’’ alisema Dkt. Mahenge. 

Hata hivyo, amezitaja sababu kuu zinazosababisha vifo hivi kwa kina mama kuwa ni pamoja na kutokwa na damu nyingi kabla na baada ya kujifungua, kifafa cha mimba, kuchanika kizazi, upungufu mkubwa wa damu, kondo la nyuma kushindwa kutoka, matatizo yatokanayo na ugonjwa wa UKIMWI, uchungu pingamizi, matumizi ya dawa za miti shamba zinazoaminika kuongeza uchungu wa kujifungua na matatizo yatokanayo na kuharibika kwa mimba kwa njia yoyote ile. 

Dkt. Mahenge amesema kuwa sababu za vifo vya watoto wachanga ni pamoja na kushindwa kupumua kwa mtoto akiwa tumboni na mara baada ya mama kujifungua, matatizo yatokanayo na kuzaliwa njiti na matatizo ya ulemavu wa kuzaliwa nao (Congenital abnormalities). 

Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa Tanzania kwa mwaka 2017, vifo vya wanawake wajawazito 556 kwa kila vizazi hai 100,000 vilitokea, na lengo la Serikali ni kupunguza vifo hivi hadi kufikia 292 kwa vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2020. 

Ameongeza kuwa kwa mwaka 2017, vifo vya watoto wachanga ni 25 kwa kila vizazi hai 1,000 na lengo ni kupunguza hadi kufikia vifo 16 kwa kila vizazi hai 1,000 ifikapo mwaka 2020. 

“Kwa Mkoa wetu wa Dodoma, takwimu za miaka mitano mfululizo zinaonesha bado tunayo kazi kubwa ya kufanya ili kukabiliana na matatizo yanayojitokeza wakati wa ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua hasa unapoangalia namba halisi ya kinamama na watoto wanaofariki. Jumla ya wajawazito 309 walifariki, ambao ni sawa na mabasi 5 ya abairia 62 au waumini wa kanisa/msikiti mzima,’’ amebainisha Dkt. Mahenge 

Katika kuhakikisha huduma inaimarika, amesema tayari serikali imejenga na kukarabati kwa awamu miundombinu ya afya katika jumla ya vituo vya afya 22, kufadhili ujenzi wa hospitali tatu za wilaya katika Halmashauri ya Chemba, Chamwino na Bahi ambazo hazikuwa na Hospitali za Wilaya. 

Pia Serikali imeongeza bajeti ya dawa ambapo katika mkoa wa Dodoma bajeti ya dawa imeongezeka kutoka shilingi milioni 900 mwaka 2015/16 hadi shilingi bilioni 4.3 mwaka 2018/19. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamis Mkunda, amesema amepokea kwa furaha kampeni hii na yuko tayari kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wananchi katika kuhakikisha elimu inamfikia kila mmoja ili tahadhari ichukuliwe kwa kipindi cha ujauzito. 

Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. James Charles Kiologwe amesisitiza akina baba kuwa na ushirikiano na wake zao kipindi cha ujauzito, ikiwemo kuhudhuria kliniki, na kuwa waangalizi wao muda wote ili kuwasaidia inapotokea hali ya tofauti kiafya. 

Vile vile, ametoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Dodoma kutoa ushirikiano wa kuyachunguza magari ya kubebea wagonjwa na kuhakikisha yanafanya kazi inayopaswa, hii itasaidia wagonjwa ikiwemo kina mama kufikishwa hospitalini mapema. 

Dkt. Kiologwe amewataka wataalamu wa afya kufanya uchunguzi yakinifu ili kubaini mapema dalili zozote za hatari na kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za chanjo, ubora wa matibabu ya utotoni, ushauri kuhusu lishe bora, ikiwemo kutoa lugha nzuri kwa akinamama. 

Huu ni mwendelezo wa mapambano dhidi vifo vinavyotokea kwa akina mama wakati na baada ya kujifungua, pamoja na watoto wao, kwani serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa Afya ya Uzazi na Mtoto, ilizindua kampeni hii mnamo tarehe 06 Novemba, 2018 hapa Jijini Dodoma, ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Mikoa kusaini tamko la ahadi mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge


Usajili na Utambuzi wa Wanchi ni Bure

$
0
0


Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwakumbusha wananchi wote kuwa Huduma ya Usajili na Utambuzi wa Watu kwa ajili ya kupatiwa Kitam- bulisho cha Taifa inatolewa BURE. Mwananchi anatakiwa kufika katika ofisi za NIDA akiwa na nakala (Photocopies) za viambatisho vyake muhimu.

Waombaji wote wa Vitambulisho vya Taifa mnakumbushwa kuwa “Rushwa ni Adui wa Haki. Usikubali kudai, kutoa wala kupokea Rushwa.” Kitambulisho cha Taifa ni haki yako ya msingi na hakiuzwi.

Hakikisha unahudumiwa katika Ofisi au Vituo rasmi vya Usajili vya NIDA na Afisa wa NIDA na sio Vishoka wanaojipenyeza kwenye zoezi.

Ukiombwa Rushwa Toa Taarifa kwa Mawasiliano :-

Simu: 0800758888 au 0673 333 444 au 0759102010 au 0765201020, Barua: S.L.P 12324 Dar es Salaam, Barua pepe (email): nida.tanzania@nida.go.tz. Tembelea tovuti yetu: www.nida.go.tz, Facebook nidatanzania, twitter @nidaTanzania au twitter.com/nidatanzania

Imetolewa na:- Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Viongozi Mloganzila Watakiwa Kujituma

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru (katikati) akifungua mafunzo ya mfumo wa tathimini na upimaji wa wazi wa utendaji kazi (OPRAS) kwa viongozi wa Hospitali ya Mloganzila.
Baadhi ya viongozi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji alipokua akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika Februari 19 na Februari 20, 2019 hospitalini hapo.
Mtaalam kutoka Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Renatus Mgusi akiwasilisha mada mbalimbali kuhusu mfumo wa OPRAS.
Dkt. Catherine Shari kutoka Idara ya Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila akichangia hoja katika mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo hayo.


………………………………………


Viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili na Miongozo ya Utumishi wa Umma ili kutimiza dira na malengo ya Hospitali.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru wakati akifungua mafunzo ya mfumo wa tathimini na upimaji wa wazi wa utendaji kazi (OPRAS) kwa viongozi wa Hospitali ya Mloganzila yaliyofanyika hospitalini hapo.

Akizungumza katika mafunzo hayo Prof. Museru amesema nidhamu na kujituma kwa viongozi kutawawezesha watumishi wa ngazi zote kutimiza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

“Huwezi kufikia malengo yoyote kama hujitumi na kujitoa katika kazi, kiongozi bora ni lazima awe mfano wa kuigwa katika utendaji wake hatua itakayowawezesha watumishi wa chini na wao kufanya kazi kwa bidii”. Amesema Prof. Museru.

Akitoa mada katika mafunzo hayo, mtaalam kutoka Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Renatus Mgusi amesema OPRAS ni nyenzo kuu inayotumika katika kutathimini utendaji kazi wa mtumishi hivyo hauna budi kutekelezwa kwa ufanisi.

Mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija na yatawezesha kujiwekea malengo mahususi yanayopimika na yenye uhalisia na ambayo yanawekewa muda maalum wa utekelezaji.

DC MSHAMA AWAASA WAZAZI WENYE WATOTO WALIO NA ULEMAVU KUWAFICHUA NA KUWAPELEKA KUANZA SHULE

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

WAZAZI na walezi walio na watoto wenye ulemavu ,wameaswa kuwafichua watoto wao walio na sifa ya kuanza elimu ya awali badala ya kuwaficha na kusababisha kukosa haki ya kupata elimu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kujifunzia, kusomea na vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu katika shule za awali mkoani Pwani ,vilivyogharimu milioni 48.5 kutoka shirika la kimataifa la ADD, mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama, aliomba jamii ihamasike na kuibua watoto hao.

Alieleza ,endapo tabia ya kuficha watoto wenye ulemavu itaachwa itasaidia kupunguza idadi kubwa ya watoto walio na ulemavu mbalimbali ambao hawajaandikishwa shule.

“Watoto wenye ulemavu wapelekwe shule kama wasio na ulemavu kwani wote wana haki ya msingi kupata elimu kuanzia awali hadi chuo kikuu “alisisitiza Assumpter. 

Aidha Assumpter aliitaka jamii, kufuatilia na kuwakemea watoto wanapokosea ama kugundua wanajiingiza kwenye makundi yasiyo na maadili, ikiwezekana wachapwe viboko ilihali kuondokana na wimbi la watoto Dotcom

Awali ofisa program uhamasishaji wa shirika la kimataifa linalotetea na kuhudumia watu wenye ulemavu nchini (ADD)Isack Idama alisema, wametoa vifaa hivyo vilivyogharimu milioni 48.5 ambapo vitagawiwa katika shule tano kwenye kila halmashauri mkoani hapo. 

Alifafanua kwamba, mgao huo ni awamu ya kwanza hivyo wanatarajia kutoa vifaa vingine hivi karibuni katika shule nyingine ishirini .

Alieleza, wanatekeleza miradi ya elimu jumuishi kwa kufanyakazi na wizara ya elimu na TAMISEMI kuboresha elimu na mradi unatekelezwa hadi mwaka-2021,ambapo hadi sass watoto 395 wameandikishwa shule za awali tangu mradi uanze.


RAIS MAGUFULI ATEUA MKEMIA MKUU,MKURUGENZI NA MWENYEKITI

WAZIRI KAIRUKI AITAKA TIC KUIMARISHA HUDUMA ZA MAHALA PAMOJA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angella Kairuki akipata ufafanuzi kuhusu huduma za mahala pamoja kwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wawekezaji Bi Anna Lyimo, Waziri Kairuki alifanya ziara kwenye ofizi za TIC leo February 20, 2019
Mkurugenzi Mtendahi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Geoffrey Mwambe akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angela Kairuki alipotembelea kwenye ofisi hizo leo February 20, 2019
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angella Kairuki akitoa ufafanuzi wa jambo alipotembelea kwenye ofisi za kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Mapema February 20, 2019 ili kujionea baadhi ya kazi zinazofanywa na kituo hicho sehemu ya huduma za mahala pamoja
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angella Kairuki akipata ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Geoffrey Mwambe kuhusu huduma za mahala pamoja


Na Grace Semfuko-MAELEZO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji ) Angela Kairuki amekitaka Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kupitia mfumo wa huduma za mfumo wa mahala pamoja kuboresha utoaji wa huduma kwa wawekezaji kupitia mfumo wa kielektroniki na kuwaagiza kuunganisha mfumo wa dirisha la uchakataji miradi (TIW) kwenye Kanda zote saba za kituo hicho Nchini ili kurahisisha mwenendo wa upatikanaji wa huduma kwa wawekezaji.

Kairuki alisema mfumo huo unasaidia kuondokana na urasimu,ucheleweshwaji na unarahisisha upatikanaji wa leseni,cheti na vibali ambao utasaidia kuongeza wawekezaji nchini ambapo kati ya kanda saba za TIC ni kanda moja tu ya Kaskazini ndio iliyoingizwa kwenye mfumo na kuagizwa kanda zingine ziharakishe mfumo huo ndani ya mwezi mmoja.

Waziri Kairuki aliyasema hayo February 20, 2019, baada ya kuzungumza na maafisa wanaotoa huduma ndani ya mfumo wa mahala pamoja na kufanya nao majadiliano juu ya namna ya kuboresha huduma hizo ambazo zinatolewa na taasisi 11 ndani ya jengo la TIC.

“Mfumo wa huduma za mahala pamoja ni mzuri sana, lakini tuhahitaji kuyafanyia kazi masuala kadhaa kwenye kila taasisi 11 zilizopo kwenye huduma za mahala pamoja ili kuondokana na changamoto ambazo zinachelewesha upatikanaji wa huduma za uwekezaji” alisema Kairuki.

Aidha aliwataka watendaji wa ardhi ndani ya kituo hicho kuweka vizuri takwimu za ardhi ya uwekezaji na kushughulikia changamoto za upatikanaji wa ardhi kwa wawekezaji ambao unasimamiwa na TIC.

Akiwa katika sehemu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Waziri Kairuki aliagiza watendaji hao kuuona umuhimu wa utoaji wa cheti cha utambulisho wa namba ya mlipakodi TIN kwenye Kituo hicho ili kurahisisha huduma kwa wawekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Bw. Geoffrey Mwambe alisema iwapo Serikali itawezesha taasisi zote zinazohusika na huduma za mahala pamoja kutoa huduma zake stahiki zinazohusu uwekezaji ndani ya ofisi za TIC itakuwa ni hatua kubwa katika uwekezaji.

“Taasisi zilizopo ndani ya mfumo wa mahala pamoja zinafanya kazi kubwa, tunachoomba sisi kama TIC ni kwamba huduma za taasisi hizo kwa wawekezaji zikamilike ndani ya TIC badala ya kwenda kwenye makao makuu ya ofisi hizo kufuata idhini ya vibali,leseni na vyeti husika kwa wawekezaji” alisema Mwambe.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya huduma kwa wawekezaji Anna Lyimo alisema kwa sasa huduma za mahala pamoja zimekuwa na manufaa makubwa kwa wawekezaji kutokana na kuwapo kwa taasisi zote muhimu Kituoni na kwamba marekebisho yaliyotajwa na Waziri yatafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo.

“Tumeyapokea maagizo ya Waziri na tutayafanyia kazi, ni maagizo yenye tija kwa kituo” alisema Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Mahala Pamaoja wa TIC Anna Lyimo.

Huduma za mahala pamoja kwenye kituo cha uwekezaji Tanzania TIC zinajumuisha taasisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Baraza la Taifa la usimamizi na uhifadhi wa Mazingira (NEMC), Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA), Shirika la viwango Tanzania (TBS), Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na wenye ulemavu, Wizara ya Ardhi, Idara ya Uhamiaji,Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA),

WATOA HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI WAHAMASISHWA KUONGEZA NGUVU KUTAFUTA WALIOACHA KUTUMIA DAWA ZA ARVs

$
0
0


Watoa Huduma za VVU na UKIMWI mkoani Shinyanga wametakiwa kuongeza juhudi za kuwatafuta,kuwarudisha na kuhakikisha Watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI waliopotea katika huduma wanaendelea kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU.

Wito huo umetolewa Februari 19,2019 na Mratibu wa Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi mkoa wa Shinyanga, Dkt. Peter Mlacha wakati akifunga warsha ya Watoa Huduma za VVU na UKIMWI mkoani Shinyanga.

Warsha hiyo iliyodumu kwa muda wa siku tatu iliyoandaliwa na Asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) ilijikita zaidi katika kujadili na kupanga mikakati namna ya kukabiliana na changamoto ya wateja kupotea katika huduma.

Dkt. Macha alisema ili kuondokana na changamoto ya wateja kupotea katika huduma,watoa huduma za VVU na UKIMWI wanayo nafasi kubwa ya kuwarudisha kwenye huduma wateja hao.“Ili Mteja azingatie dawa zake vizuri ni lazima awe na elimu ya kutosha kuhusu dawa,VVU na UKIMWI kwa ujumla, hakikisheni mnawapa elimu kwani takwimu zinaonesha kuwa wateja wengi wamekuwa wakipotea katika huduma kwenye hatua za mwanzo kabisa hasa wakati wa usajili”,alifafanua.

Aliwataka watu wanaoishi na maambukizi ya VVU watumie dawa kwa usahihi na kufuata miongozo wanayopewa na wataalamu wa afya.“Dhumuni la Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ni kutoa huduma nzuri kwa wananchi wake,tunaishukuru AGPAHI kwa kuendelea kushirikiana nasi katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI,tunahitaji Shinyanga isiyo na maambukizi mapya ya VVU”,alisema Dkt. Mlacha.

Kwa upande wao,Washiriki wa warsha hiyo waliahidi kutoa elimu zaidi kwa wateja kuhusu VVU na UKIMWI sambamba na kuwatafuta na kuwarudisha kwenye huduma wateja waliopotea.

Mratibu wa Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi mkoa wa Shinyanga, Dkt. Peter Mlacha wakati akifunga warsha ya Watoa Huduma za VVU na UKIMWI mkoani Shinyanga katika ukumbi wa Virgimark Hotel Mjini Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Mratibu wa Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi mkoa wa Shinyanga, Dkt. Peter Mlacha akiwaomba watoa Huduma za VVU na UKIMWI kuongeza juhudi katika kufuatilia wateja waliopotea katika huduma.

Mratibu wa Huduma za VVU na UKIMWI katika jamii mkoa wa Shinyanga, Edwiga Zumba akizungumza wakati wa warsha hiyo.

Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga Nastervella Rweyemamu akizungumza wakati wa warsha hiyo.

Washiriki wa warsha hiyo wakijaza fomu ya ufuatiliaji wa wateja kwenye vituo vya tiba na matunzo (CTC).

Watoa huduma za VVU na UKIMWI wakiendelea kujaza fomu.

Watoa huduma za VVU na UKIMWI wakisoma maelekezo kwenye fomu za ufuatiliaji.


Wawezeshaji wakati wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.Kushoto ni Mwezeshaji wa Huduma za VVU na UKIMWI katika jamii Manispaa ya Shinyanga, Mwita Thomas na Mratibu wa Huduma za VVU na UKIMWI katika jamii mkoa wa Shinyanga, Edwiga Zumba.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

ASSEMBLY COMMENCES PLENARY SITTING IN ZANZIBAR

$
0
0
cid:image001.png@01D4BE42.6CDFEB00
EAST AFRICAN LEGISLATIVE ASSEMBLY


East African Legislative Assembly, Arusha, February 19, 2018The Isles of Zanzibar hosts the East African Legislative Assembly (EALA). The Assembly convenes for the 4th Meeting of its 2nd Session which runs from February 18th, 2019 to March 8th, 2019.

The President of Zanzibar and the Chairman of the Revolutionary Council, H.E. Dr Ali Mohammed Shein is expected to officiate at a special Sitting on February 26th, 2019. Key items at the Sitting include debate on the East African Supplementary Appropriation Bill, 2019 and the consideration of various key Committee reports.

The Assembly is further expected to receive a briefing by the EAC Secretary General on the status of EAC projects. The Sitting is also to be interspersed in Week 1 by rigorous Committee work with all 6 Committees reviewing pertinent issues that precede debate next week.  The six Committees are:
·         the Committee on Accounts,
·         the Committtee on Agriculture, Tourism and Natural Resources
·         the Committee on General Purpose
·         the Committee on Regional Affairs and Conflict Resolution
·         the Committee on Communication, Trade and Investment, and
·         the Committee on Legal Rules and Privileges.  

The whole House will also meet with a number of key EAC and other institutions. Two EAC Institutions, the EAC Kiswahili Commission and the Inter-University Council of East Africa (IUCEA) are on the cards.  In addition, the executives of the African Palliative Care Association and the with Doris Mollel Foundation will also touch base with the Assembly to discuss matters pertinent to integration.  As part of its outreach programmes, the Assembly similarly has a date with stakeholders from the Zanzibar Business Board (ZBB) and the University of Zanzibar.

The Assembly which holds six Plenary Sessions in the region every financial year, embraces the principle of rotation in a bid to create awareness of its work. Zanzibar last hosted EALA (Second Meeting of the Fifth 

ABOUT EALA

The East African Legislative Assembly is the Legislative Organ of the East African Community. Its Membership consists of a total of 62, of whom 54 are elected Members (9 from each Partner State) and eight ex-officio members (the Ministers responsible for EAC Affairs from the Partner States, the Secretary General of the Community and the Counsel to the Community).

The East African Legislative Assembly has legislative functions as well as oversight of all East African Community matters.  The enactment of legislation of the Community is put in effect by means of Bills passed by the Assembly and assented to by the Heads of State, and every Bill that has been duly passed and assented to become an Act of the Community and takes precedent over similar legislations in the Partner States.  EALA has to date passed 80 pieces of legislation.

EAC, GERMANY SIGN USD 35 MILLION AGREEMENT

$
0
0
cid:image001.png@01D4BE42.6CDFEB00                           
   
 East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, 19th February, 2019: The Government of the Federal Republic of Germany committed a grant of over USD 35 million (EUR 31,5 million) to the East African Community (EAC) to further support the regional organisation in the areas of health, regional economic integration and education.

The EAC Secretary General, Amb. Libérat Mfumukeko, and the German Ambassador to the EAC, Dr. Detlef Wächter, jointly signed the  Agreements in Arusha today.

Germany’s commitment includes USD 14.5 million (EUR 13 million) for the continuation of the joint financial cooperation programme under the Regional Network of Reference Laboratories for Communicable Diseases” and EUR 3 million for the technical cooperation programme “Pandemic preparedness in the EAC Region”, thereby supporting the EAC’s efforts in  fighting communicable diseases and strengthening the EAC’s capacities in dealing with pandemics.

USD 10.7 million (EUR 9.5 million) were committed to the continuation of the technical cooperation programme “Support to the EAC Integration Process” which supports the EAC in increasing intra-regional trade through value addition in productive sectors, better market access, improved customs processes and harmonized standards. USD 1.1 million (EUR 1 million) were committed for the ongoing programme “Strengthening of a Regional Quality Infrastructure” that focusses on reliable quality control mechanisms and services for products in selected sectors that are traded in the EAC region and exported abroad.

USD 5.5 million (EUR 5 million) are dedicated for the continuation of the “EAC Scholarship Programme” which supports East African Master students and is implemented in cooperation with the Inter-University Council of East Africa (IUCEA).

The German Ambassador underlined: "Germany remains a strong supporter of the EAC and the organisations’ efforts to enhance regional integration in its different facets. Strengthening economic integration, supporting the EAC in addressing key health and education challenges are at the core of our joint cooperation. Regarding our health cooperation, we believe it is vital to support the secretariat and the EAC Partner States to be better positioned when it comes to epidemics and pandemics.

The current Ebola crisis in the neighbouring Democratic Republic of Congo highlights the necessity for regional cooperation dramatically.” On Germany’s commitment in the education sector, the Ambassador went on saying: “We know from our experience in Europe that regional integration is futile if we leave the youth and young generation behind.

The East African students that will benefit from this scholarship programme will not only have improved job perspectives through this programme but they themselves will become ambassadors for the East African Community. We need this young generation to carry the EAC’s vision forward. “added,German Ambassador

On his part, the EAC Secretary General, Amb  Libérat Mfumukeko said that the Federal Republic of Germany and the EAC have historically had strong and cordial relations since the founding of the EAC almost 20 years ago. For the last 20 years, German development cooperation has supported the EAC to the tune of USD 350including  the new commitments signed today.

It is my sincere hope and trust that the EAC cooperation with Germany will grow stronger based on the already existing robust foundation of our common goals.’’

Millard Ayo Voted 2018 Most Influential Young Tanzanian

$
0
0

Hello,

Kindly find attached the press details for winners of the 2018 Most Influential Young Tanzania ranking.

Would appreciate your support again in sharing on your platforms

You can reach out to me via +233242307379 if you need more details.

For more press details you can also visit tz.avancemedia.org or www.avancemedia.org/blog

Regards

Prince Akpah

Blogger & On Air Personality, Millard Ayo has been voted the 2018 Most Influential Young Tanzanian in the 2nd edition of the annual ranking poll by international rating firm, Avance Media.
Millard Ayo was nominated in the Media category whiles he amassed the endorsement from voters who participated in the 2018 polls of the 50 Most Influential Young Tanzanians.
Millard Ayo is the founder of AYO TV and Millardayo.com, Tanzania’s most recognized, trusted and reliable digital media company with the biggest social media following and the largest online audience in Tanzania. Millard also works with Clouds FM Tanzania as on air personality.
The ranking which was launched in 2017 by Avance Media had footballer, Mbwana Samatta being voted the 2017 Most Influential Young Tanzanian.

Following keenly in the 2018 ranking are: last year’s winner, Mbwana Samatta (Footballer), Jokate Mwegelo (District Commissioner), Faraja Nyalandu (Shule Direct) and Diamond Platnumz (Musician) who were voted among the top 5 most influential young Tanzanians.
District Commissioner for Kisarawe, Jokate Mwegelo who was nominated in the Law & Governance category also got the nod as the leading woman on the list crowning her feat as the 2017 Most Influential Young Tanzanian woman.
Sharing insights about the 2018 year’s polls, Prince Akpah, MD of Avance Media mentioned; the ranking was instituted to highlight the works of young Tanzanians who are contributing in diverse ways towards the advancement of development in Tanzania and across Africa.
Avance Media also runs same initiative in Kenya, South Africa, Nigeria, DR Congo, Ghana & Cameroon in partnership with various organisations and is expected to release a global ranking in 2019.
Below are winners in the various categories:
  1. Business - William Mshery  - Vijana Think Tank
  2. Entertainment - Diamond Platnumz - Musician
  3. Law & Governance - Jokate Mwegelo - District Commissioner, Kisarawe
  4. Leadership & Civil Society - Doris Mollel - Doris Mollel Foundation
  5. Lifestyle - DJ Ommy Crazy
  6. Media  - Millard Ayo - Blogger & On Air Personality
  7. Personal Development & Academia - Badru Juma Rajabu - Youth of United Nations Association of Tanzania
  8. Science & Technology - Jumanne Mtambalike - Sahara Ventures
  9. Social Entreprise & Philanthropy - Faraja Nyalandu - Shule Direct
  10. Sports - Mbwana Samatta

Below is the list of Avance Media’s 2018 50 Most Influential Young Tanzanians
  1. Millard Ayo (OAP)
  2. Mbwana Samatta
  3. Jokate Mwegelo (District Commissioner)
  4. Faraja Nyalandu (Shule Direct)
  5. Diamond Platnumz (Musician)
  6. Ali Kiba (Musician)
  7. Jebra kambole (Advocate)
  8. DJ Ommy Crazy (DJ)
  9. Rebeca Gyumi (Msichana Initiative)
  10. Doris Mollel (Doris Mollel Foundation)
  11. Badru Juma Rajabu (Youth of United Nations Association of Tanzania)
  12. William Mshery (Vijana Think Tank)
  13. Jumanne Mtambalike (Sahara Ventures)
  14. Salim Mussa Omar (Green Light Foundation)
  15. Seleman Yusuph Kitenge (African Network of Youth Policy Experts)
  16. Agnes Kahamba (Tupaze Sauti Foundation)
  17. Herieth Paul (Model)
  18. Joseph Sayi (TV1/Kwese)
  19. Idris Sultan (OAP)
  20. Vanessa Mdee (Musician)
  21. Isaya Yunge (Somaapps Technologies)
  22. Diana Mbogo (Millennium Engineers Enterprise)
  23. Evans Makundi (Evmak)
  24. Allen Kimambo (Zaidi General Enterprises Limited)
  25. Lameck Kiula (Jambo Bukoba)
  26. Alqaim Lalani (Tumaini la Maisha)
  27. Petrider Paul (Youth for Change Tanzania)
  28. Jennifer Shigoli (Malkia Investments Company Limited)
  29. Rose Mmbaga (World Merit Tanzania)
  30. Felix Manyogote (Child in Action Foundation)
  31. Wilhelm Oddo (Nlab)
  32. Salha Kibwana (Her Africa)
  33. Fortunatus Francis (Photographer)
  34. Catherine Ruge (Member of Parliament)
  35. Geline Alfred Fuko (Tangible Innitiative for Local Development Tanzania)
  36. Fahad Awadh (YYTZ Agro Processing)
  37. Asia Botea (Botea Designs)
  38. Dina Marios (OAP)
  39. Stephano Temu (Vlogger)
  40. Paul Makonda (Regional Commissioner)
  41. Hashim Thabit Manka
  42. Araika Zawadhafsa Mkulo (Safe Space)
  43. Wema Sepetu (Actress)
  44. Mrisho Ngasa
  45. Zainab Katimba (Member of Parliament)
  46. MC Pilipili (Comedia)
  47. Hamisi Mandi (OAP)
  48. Shomari Kapombe
  49. Alphonce Simbu
  50. Casto Dickson (OAP)

The 2018 50 Most Influential Young Tanzanians ranking was conducted by Avance Media in partnership with Blue Blazer International, VIPI State, Jagari Designs, COSDEF Group, 1000 African Voices, CliqAfrica, WatsUp TV, & MyNaijaNaira.com

HABARI ZA UN: Kutoka Nairobi hadi New York, Gavana Sonko azungumza

VOA SWAHILI: Marekani imetoa wito kwa Nigeria kuhakikisha uchaguzi utafanyika kwa uhuru

UJENZI SGR-Watanzania wajitokeza Vingunguti Kushuhudia Utandikaji Wa Reli mpya ya SGR.WAMPA TANO JPM

INTRODUCING "WEKA" BY FANY & G NAKO

INTRODUCING NYIMBO MPYA KUTOKA KWENYE MIKONO SALAMA(BLESSING HANDS) producer STEVE WHITE


WATOA HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI WAHAMASISHWA KUONGEZA NGUVU KUTAFUTA WALIOACHA KUTUMIA DAWA ZA ARVs

$
0
0

Watoa Huduma za VVU na UKIMWI mkoani Shinyanga wametakiwa kuongeza juhudi za kuwatafuta,kuwarudisha na kuhakikisha Watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI waliopotea katika huduma wanaendelea kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU.

Wito huo umetolewa Februari 19,2019 na Mratibu wa Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi mkoa wa Shinyanga, Dkt. Peter Mlacha wakati akifunga warsha ya Watoa Huduma za VVU na UKIMWI mkoani Shinyanga.
Warsha hiyo iliyodumu kwa muda wa siku tatu iliyoandaliwa na Asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) ilijikita zaidi katika kujadili na kupanga mikakati namna ya kukabiliana na changamoto ya wateja kupotea katika huduma. 
Dkt. Mlacha alisema ili kuondokana na changamoto ya wateja kupotea katika huduma,watoa huduma za VVU na UKIMWI wanayo nafasi kubwa ya kuwarudisha kwenye huduma wateja hao.
“Ili Mteja azingatie dawa zake vizuri ni lazima awe na elimu ya kutosha kuhusu dawa,VVU na UKIMWI kwa ujumla, hakikisheni mnawapa elimu kwani takwimu zinaonesha kuwa wateja wengi wamekuwa wakipotea katika huduma kwenye hatua za mwanzo kabisa hasa wakati wa usajili”,alifafanua.
Aliwataka watu wanaoishi na maambukizi ya VVU watumie dawa kwa usahihi na kufuata miongozo wanayopewa na wataalamu wa afya.
“Dhumuni la Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ni kutoa huduma nzuri kwa wananchi wake,tunaishukuru AGPAHI kwa kuendelea kushirikiana nasi katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI,tunahitaji Shinyanga isiyo na maambukizi mapya ya VVU”,alisema Dkt. Mlacha.
Kwa upande wao,Washiriki wa warsha hiyo waliahidi kutoa elimu zaidi kwa wateja kuhusu VVU na UKIMWI sambamba na kuwatafuta na kuwarudisha kwenye huduma wateja waliopotea.
Mratibu wa Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi mkoa wa Shinyanga, Dkt. Peter Mlacha wakati akifunga warsha ya Watoa Huduma za VVU na UKIMWI mkoani Shinyanga katika ukumbi wa Virgimark Hotel Mjini Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mratibu wa Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi mkoa wa Shinyanga, Dkt. Peter Mlacha akiwaomba watoa Huduma za VVU na UKIMWI kuongeza juhudi katika kufuatilia wateja waliopotea katika huduma.
Mratibu wa Huduma za VVU na UKIMWI katika jamii mkoa wa Shinyanga, Edwiga Zumba akizungumza wakati wa warsha hiyo.

Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa  Shinyanga Nastervella Rweyemamu akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Afisa Mawasiliano na Uraghbishi wa AGPAHI, Glory Macha akitoa neno la shukrani kwa washiriki wa warsha hiyo na kuwasisitiza kufanyia kazi mambo yote waliyojifunza kwa muda wa siku tatu kwenye warsha.


Washiriki wa warsha hiyo wakijaza fomu ya ufuatiliaji wa wateja kwenye vituo vya tiba na matunzo (CTC).
Watoa huduma za VVU na UKIMWI wakiendelea kujaza fomu.
Watoa huduma za VVU na UKIMWI wakisoma maelekezo kwenye fomu za ufuatiliaji.
Wawezeshaji wakati wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.Kushoto ni Mwezeshaji wa Huduma za VVU na UKIMWI katika jamii Manispaa ya Shinyanga, Mwita Thomas na Mratibu wa Huduma za VVU na UKIMWI katika jamii mkoa wa Shinyanga, Edwiga Zumba.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Airtel yazindua Dabo Data na SMATIKA

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza kuzindua ofa mpya kwa wateja wake inayojulikana kama  Dabo Data na SMATIKA ambapo inawawezesha wateja wake wanaotumia huduma ya Airtel Money kupata mara mbili zaidi kila wanaponunua bando kupitia Airtel Money kuanzia leo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza uzindua huo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isaac Nchunda alisema kuwa “Promosheni ya Dabo Data na SMATIKA itawafaidisha  wateja wetu wanaonunua vifurushi kujipatia bando mara mbili yaani 2GB kwa bei ileile ya Sh 2,000 badala ya ilivyokuwa awali 1GB, vilevile mteja ataweza kudumu na bando hilo la 2GB kwa muda wa siku tatu,  Nchunda aliongeza kuwa  “kulingana na ripoti ya TCRA ya hivi karibuni inaonyesha kuwa wateja wanaoutumia huduma ya kifedha ya simu za mkononi imeongezeka kutoka 21 milioni  Disemba 2017 mpaka kufikia  23 milioni kwa sasa na hii ndio inayotupa msukumo sisi Airtel kuenedelea kuleta huduma za kibunifu kama hizi ili kuwarahisishia wateja wetu kila mahali.”

“Airtel Tanzania bado tunaendelea kuleta huduma na bidhaa ambazo ni nafuu na zenye ubunifu zaidi ili kuendelea kukidhi matakwa ya wateja wetu, aliongeza Nchunda.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Airtel Jackson Mmbando alisema kuwa kuzinduliwa kwa huduma hii ya Dabo Data na SMATIKA ni hatua nyingine muhimu ya kuendelea kubadilisha maisha ya wateja wetu. ‘Tunaona wateja wengi wanaongezeka na kutumia huduma ya Airtel Money. Kuanzia leo, mteja yeyote wa Airtel Money anaweza akanunua bando ya Dabo Data na SMATIKA kwa kupitia menu ya Yatosha *149*99# kisha changua 1  na kuchagua Dabo Data na SMATIKA. Vile vile, mteja anaweza kupiga menu ya Airtel Money moja kwa moja *150*60# kisha akachangua 2, aliongeza Mmbando.

Airtel tunaamini kwa kuwapatia  wateja wetu uhuru wakuchagua huduma watakayo kama hivi,  inaokoa muda wa mteja kupata huduma haraka na hiyo kuongezea faida kwa mteja kuona thamani ya matumizi ya fedha yake kutokana na unafuu. Kwa sasa mteja atapata mara mbili kwa kutumia Dabo Data na SMATIKA na atalipa kwa Airtel Money yake kuendelea kufurahia huduma zingine za Airtel Money.

“Dhamira ya Airtel ni kuendelea kuwekeza kwenye huduma zetu zote kama ilivyo kwa Airtel Money ambapo hadi sasa Airtel tayari imefikisha huduma za Airtel Money kila kona kwa kusambaza  Airtel Money Branch zaidi ya 500 nchini kote, Lengo letu kwa kupeleka maduka haya karibu na wateja zaidi ni  kudhihirisha mkakati wetu wa kuwa kampuni ya simu za mkononi ambayo inatoa  suluhisho kwenye huduma za kifedha hapa nchini. Nia yetu ni kuendelea kujenga mtandao imara na kutengemea huduma rafiki kama Airtel Money aliongeza Mmbando.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isaac Nchunda, akizungumza wakati wa  uzinduzi wa promosheni ya  ‘Dabo Data na Smatika’ itakayomwezesha mteja  wa Airtel Money kupata mara mbili ya bando kwa gharama ileile ya sh 2000, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa  kampuni hiyo, Jackson Mmbando. 
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isaac Nchunda, akionyesha bango la promosheni ya  ‘Dabo Data na Smatika’ wakatin wa uzinduzi wa promosheni hiyo Dar es Salaam jana, Dabo Data na SMATIKA itamwezesha mteja  wa Airtel Money kupata mara mbili ya bando kwa bei ile ile y ash 2000. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa  kampuni hiyo, Jackson Mmbando.

MAKAMU WA RAIS AWASILI IGUNGA MKOANI TABORA

$
0
0
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora ambapo atatembelea Wilaya zote saba (7) za  Igunga, Nzega, Uyui, Sikonge, Kaliua, Urambo na Tabora .

Lengo la ziara ni kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ili kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 ya Chama Cha Mapinduzi, kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo na kutoa maelekezo kwa watendaji kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji yatakayobainika katika ziara. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasubi mara baada ya kuwasili Igunga, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na kijana wa skauti mara baada ya kuwasili Igunga mkoani Tabora. (picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MBUNGE KANYASU AOMBA UMEME WA REA GEITA MJINI

$
0
0
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameomba umeme kupitia mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini wa REA katika jimbo la  Geita mjini kwa vile Geita mjini, mjini ni kata mbili tu ikiwemo Kalangalala na Bombambili na maeneo yote yaliyobaki ni vijiji.

Pia, Mhe.Kanyasu amemuomba Waziri wa Nishati, Dkt.Medald Kalemani kuharakisha zoezi la usambazaji wa umeme wa REA katika maeneo ya  yaliyoyopitiwa na umeme huo kwa vile tokea mradi huo ulipozinduliwa mwaka jana, kijiji kimoja  tu katika jimbo hilo ndo kimenufaika na mradi huo.

Akizungumza kabla ya kuzindua umeme wa REA katika kijiji cha Ibanda wilayani Geita, Dkt.Meldard Kalemani ametaja sababu zilizoifanya Geita mjini kuchelewa kupata umeme wa REA kwa vile Geita mjini inahesabika kuwa ni  mjini na mjini hakuna  vijiji bali kuna mitaa.

"Sisi tuliambiwa tupeleke umeme kwenye vijiji na sio kwenye mitaa, Mhe. Kanyasu ndo kapigania kutuambia kuwa hii sio mitaa ni vijiji" Amesisitiza Waziri Kalemani

Hata hivyo, Waziri Kalemani amemhakikishia Mbunge wa Geita mjini kuwa jumla ya vijiji 42 tayari vipo kwenye mpango wa kuunganishwa na mradi wa umeme wa REA.

Katika hatua nyingine, Waziri Kalemani amewaagiza  Wakandarasi na Wataalamu wote kuwa hakuna kuruka nyumba wala kubagua nyumba wahakikishe kila mhitaji anaunganishiwa umeme haraka iwezekanavyo.

Aidha, Waziri Kalemani amepiga marufuku kuwatoza wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme zaidi ya shilingi 27,000/- na kutoa wito kwa mwananchi atayetozwa zaidi ya kiasi hicho atoe taarifa ili hatua kali dhidi ya wahusika ziweze kuchukiwa.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa kwa gharama hizo kwani baada ya hapo itabidi walipie kulingana na taratibu za Shirilka la Ugavi wa umeme Tanzania(TANESCO
 Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi  kabla ya  Waziri wa Nishati, Dkt. Medald Kalemani   kuwasha umeme kupitia mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini wa REA katika kijiji cha Ibanda katika wilaya Geita mkoani Geita.
 Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa kwanza kulia) akimueleza  Waziri wa Nishati, Dkt. Medald Kalemani ( wa kwanza kushoto)  kuhusiana na nguzo ambazo zimerundikwa  katika kijiji cha Ibanda ambazo zimekaa zaidi ya mwaka mmoja bila kutumiwa ilhali kuna maeneo mengine ya wilaya hiyo baadhi ya  wananchi wamekosa kuunganishiwa umeme  kupitia mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini wa REA    kutokana na kukosekana kwa nguzo hizo.Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Geita, Josephat Maganga.
 Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akikabidhiwa kifaa maalum ambacho kinamsaidia mwananchi  anayetaka kuunganishiwa umeme bila kusukiwa vifaa vya umeme katika nyumba yake,  anaweza kukitumia kwa ajili  kuwasha umeme majumbani pamoja na matumizi mengine  ya kila siku katika  kijiji cha Ibanda katika wilaya Geita mkoani Geita.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medald Kalemani ( watatu kushoto) akiwa na   Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa kwanza kulia) wakicheza na kuimba na wananchi kabla ya zoezi la kuwasha umeme katika kijiji cha ibanda
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medald Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ibanda kabla ya zoezi la kuwasha umeme katika kijiji hicho.
 Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Geita, Mhe. Josephat Maganga kabla,Waziri wa Nishati, Dkt. Medald Kalemani kuwasha umeme katika kijiji cha Ibanda.

VIONGOZI WA CCM ZINGATIENI KATIBA YA CHAMA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YENU-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba ya chama ili kuepusha migogoro kwenye maeneo yao.

Amesema chama chochote ambacho viongozi wake hawazingatii katiba lazima kiwe na migogoro kwani uzingatiaji wa katiba ni miongoni mwa mambo yanayokitofautisha Chama Cha Mapinduzi na vyama vingine vya siasa nchini.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Februari 21, 2019) wakati akizungumza na viongozi wa CCM, wabunge pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT.

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM mkoa wa Kagera amesema ni muhimu kwa viongozi hao kusoma na kuizingatia katiba ya chama kwa sababu inaelekeza misingi yote ya utendaji.

Amewasisitiza wanachama na wapenzi wa CCM wasome katiba ya chama na kuzielewa kanuni, taratibu na sera ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Akisisitiza jambo hilo Waziri Mkuu amegawa nakala za katiba ya hiyo kwa viongozi hao na kuwataka wazifikishe hadi kwenye ngazi ya mashina.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa nchi nzima unaendelea vizuri na kuhusu changamoto zilizopo katika baadhi ya maeneo nchini wanaendelea kuzirekebisha.
Amesema lengo lao ni kuhakikisha wanatekeleza ilani kama CCM ilivyoelekeza na ili kujiridhisha kama wanafanya vizuri lazima viongozi wawasimamie watendaji katika maeneo yao na watakapobaini kasoro wasisite kutoa taarifa.

Waziri Mkuu amesema viongozi chama lazima wajiridhishe kama huduma za maji, elimu, miundombinu ya barabara, kilimo pamoja nishati ya umeme zinapatikana kwenye maeneo yao yote na ni kwa kiasi gani.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Kagera kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Februari 21, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Februari, 21, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Viewing all 110087 articles
Browse latest View live




Latest Images