Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI NYASA,AKWEA MV SONGEA KUELEKEA KYELA MKOANI MBEYA KUENDELEA NA ZIARA YAKE.

$
0
0


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana, asubuhi hii amemaliza ziara yake katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na kuanza safari ya kwenda Kyela mkoani Mbeya, ambako ataanza ziara rasmi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzipatia ufumbuzi.Pichani, Kinana na wajumbe wake wa sekretarieti ya CCM, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Dk. Asha-Rose Migiro (Siasa na Uhusiano wa Kimataifa), wakiwapungia mikono wananchi wa Nyasa, baada ya kupanda Mv Songea, kuanza safari ya kwenda Kyela. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ernest Kahindi
Kwaherini wakazi wa wilaya ya Nyasa,sasa tunaelekea wilaya ya kyela mkoani Mbeya.

Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM wakiwa na shamra shamra wakati wakiusindiza ujumbe wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana walipokuwa wakielekea Kyela mkoani Mbeya mapema leo asubuhi kuendelea na ziara yake.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania afanya mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Emmanuel Nchimbi aliwasili nchini Zambia tarehe 22 Novemba 2013 na kuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia, Dkt. Edgar Lungu siku hiyo hiyo. 

Mazungumzo baina ya Mawaziri Hawa yaljikita katika kuendeleza ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali yanayohusu Wizara zao. Aidha wamekubaliana kuagiza mapema iwezekanavyo wataalam wa Wizara zao wakutane kwa majadiliano ya kuweka misingi ya ushirikiano huo.
Waziri Mambo ya Ndani wa Tanzania, Mhe Dkt. Nchimbi (kushoto) na Mhe. Edgar Lungu (kulia) kwenye Ofisi za Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia.

SID LAUNCHES STATE OF EAST AFRICA REPORT 2013

$
0
0
The Speaker of EALA, Rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa is calling on the region to seek solutions to the existing inequalities as a pre-cursor to progress and the achievement of the Millennium Development Goals (MDGs).

Speaking at the launch of the Society for International Development (SID) State of East Africa Report 2013 today, Rt. Hon Zziwa said the EAC needed a stronger social economic fiber.

“7 out of the 10 persons you see walking out there in the streets are jobless, while another 6 out of 10 live in informal settlements. The largest population, the youth, constitute about 8 out of 10 persons and their age range is below 30 years. Many are jobless and live below a dollar a day. This is a trend that needs to change” she maintained.

The EALA Speaker called on stakeholders to join in the task of securing an economic future of East Africa.  She hailed the recent unveiling of the UWEZO fund in Kenya and said it would incubate enterprise and creation of jobs.   Such initiatives should be replicated in the region as a way of take-off of the industrial revolution,” Speaker Zziwa remarked.

The report published by the Society for International Development (SID) anticipates improvement of quality of life of East Africans through attainment of sustainable growth and development by promotion of a balanced and harmonious development. It suggests equal distribution of benefits and commitment to people centred and market driven competition as envisaged by Article 7 of the EAC Treaty.  The report is themed: One People, One Destiny: the future of inequality in East Africa.

The SID publication reports of trends in the last two decades pointing to reducing inequalities in the republics of Rwanda and Burundi.  The gap between the rich and poor is expanding in Kenya and Tanzania while Uganda has kept stable.

On malnutrition, 42% of the region’s 24 million children under five were stunted in 2010. The Report however states that the region achieved the global target of 100% gross enrolment at primary school level.  The reports paints a fairly good picture of the East African Community’s economy, stating that it recorded an impressive growth rate trend of 6% in 2011 and a GDP of $83 billion.

However corruption, the report maintains, continues to blight the landscaper of East Africa;s important institutions including institutions responsible for security and justice.

In attendance at the launch today was the Cabinet Secretary for EAC, Hon Phyllis C. Kandie, EALA Members, the Regional Director of SID, Ali Hersi and representatives from the Civil Society and Private Sector.

HON. CHIKAWE’S INTERVENTION AT THE 12TH ASSEMBLY OF STATE PARTIES TO THE ROME STATUTE ON SPECIAL SEGMENT REQUESTED BY THE AU ON ICC, THE HAGUE

$
0
0
Hon. Mathias Chikawe (Second from Right) who is heading the Tanzania Delegation seated with Mr. Anselm Mwampoma (Assistant Director from Attorney General Chambers), Hon. Wilson Masilingi (Ambassador of United Republic of Tanzania to the Nethrelands), Ms Tully Mwipopo (First Secretary at the Permanent Mission of the United Republic of Tanzania to the UN) and Mr. Abdallah Mtibora (Second Secretary, Ministry of Foreign Affairs and International Relations) during the discussions of the special segment.

Following the request by the African Union, the Assembly of State Parties to the Rome Statute of the International Criminal Court that is currently taking place in The Hague, Netherlands organized a special segment on “Indictment of sitting Heads of State and Governments and its consequences on Peace and Stability and Reconciliation”.

During the discussions on the special segment, Hon. Mathias Chikawe, Minister for Constitution and Legal Affairs of the United Republic of Tanzania intervened and commended the Assembly of State Parties for according Africa an opportunity to present insights on the Challenges that Africa is facing in indictment of its sitting Heads of States and Government and its impact on peace, stability and reconciliation.

Hon. Chikawe told the ASP that, Africa is living in a world where some countries are still developing institutions which highly depend on strong leadership, thus indicting sitting Head of State or Government is more likely to fuel chaos and instability.

He further proposed to the Assembly of State Parties to come up with recommendations on addressing the concerns raised by African States for the Court to be effective.


He reiterated Tanzania’s firm commitment to support the work of the ICC and the efforts by all State Parties to the Rome Statute to end impunity in the world. 

Rais Kikwete arejea nchini leo alitokea Poland

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakilakiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik(kushoto) muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaaam. leo jioni.Rais Kikwete amerejea nchini akitokea Warsaw Poland ambapo alihudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi Duniani na awali wiki iliyopita alikuwa nchini Srilanka kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola.(picha na Freddy Maro)

Mdau Fredrick Juventine Dotto alamba nondozz yake ya Uzamili katika Uhusiano wa Kimataifa,Chuo Kikuu cha Dodoma leo

$
0
0
Mdau Fredrick Juventine Dotto akiwa nje ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jioni ya leo mara baada ya kulamba Nondozz yake ya Uzamili katika Uhusiano wa Kimataifa (Masters of International Relations) katika Chuo Kikuu hicho.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

Balozi Sefue akutana na Mkuu wa Taasisi ya Uongozi ya China

$
0
0
Makamu wa Rais wa Taasisi ya Uongozi ya Jamhuri ya Watu wa China Mh.Hong Yi akimkabidhi nakala ya kitabu chenye nasaha za watu mashuhuri kutoka jamhuri ya watu wa China Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Tanzania Profesa Joseph Semboja.

 Awali viongozi hao wawili walifanya mazungumzo yenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Taasisi ya Uongozi ya China na ile ya Tanzania.Taassisi hizo mbili zinatarajia kutia saini mkataba wa ushirikiano wiki hii. Taasisi ya Uongozi Tanzania(Uongozi Institute pamoja na Taasisi ya Uongozi ya China(Chinese Academy of Governance) zinatarajiwa kusaini Mkataba wakukuza ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili Jumanne wiki ijayo jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Institute Profesa Joseph Semboja ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo baada ya Ujumbe kutoka Taasisi ya Uongozi wa China( Chinese Academy of governance) kumtembelea Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ikulu jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo kutoka Jamhuri ya Watu wa China unaongozwa na makamu wa Rais wa Taasisi hiyo Bwana Hong Yi na ziara hiyo inafuatilia ziara ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambayo pamoja na mambo mengine uhusino kati ya taasisi hizo mbili ulitiliwa mkazo. 

Profesa Semboja aliongeza kusema kuwa mkataba wa mahusiano kati ya taasis hizo utawezesha ubadilishanaji wa teknolojia na utaalamu na hivyo kuboresha mafunzo yanayotolew na taasisi ya Uongozi Tanzania. Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alimshukuru Bwana Hong Yi kwa nia yake njema ya kushirikiana na Taasisi ya Uongozi Tanzania na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya China na Tanzania ni wakihistoria na wenye manufaa makubwa kwa wananchi wa nchi hizo mbili.
Katibu Mkuu balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Uongozi ya China Mh.Hong Yi ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)

TAMKO LA KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA) WA CHADEMA

$
0
0
Said A. Arfi (MB)
Salaam,
Napenda kuwasilisha kwako (Mwenyekiti Taifa CHADEMA) taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki. 


Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu. Pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki  wa kupindukia.



Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi.
Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu



Nawasilisha.
Said A. Arfi (MB)

JK AKIONGEA NA WATANZANIA WAISHIO POLAND JUU YA WANA DIASPORA

IOM yawakwamua wahamiaji wasio na nyaraka toka Tanzania walio mipakani huko Maziwa makuu

$
0
0
Taarifa zinasema maelfu ya wahamiaji kutoka Tanzania wamekwama mipakani huku hali ya wasiwasi juu ya majaliwa yao ikiibuka. Hii inafuatia zoezi la serikali ya Tanzania kuwaondoa wahamiaji hao katika zoezi lililotangazwa na kutekelezwa na serikali hiyo. Hivi karibuni.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limejikita kuwasaidia wakimbizi hao kama msemaji wa shirika la uhamiaji IOM Jumbe Omari Jumbe aanavyofafanua alipohojiwa na Joseph Msami wa idhaa hii. Kusikiliza bonyeza hapa.http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/2013/11/iom-yawakwamua-wahamiaji-wasio-na-nyaraka-mipakani-huko-maziwa-makuu/

MAHAFALI YA NNE YA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) YAFANA LEO KATIKA VIWANJA VYA CHIMWAGA

$
0
0
 Bendi ya Jeshi la Wananchi likiongoza masafara wa elimu kuelekea katika viwanja vya Chimwaga kwaajili ya Mahafali ya Nne ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyohitimishwa leo kwa Wahitimu Mbalimbali kutunukiwa Shahada mbalimbali na Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Benjamin Mkapa.
 Msafara wa Elimu ukienda kwenye Viwanja Vya mahafali leo, mahafali ya Nne ya Chuo Kikuu Cha Dodoma yaliyohitimishwa leo katika Viwanja vya Chimwaga Chuoni hapo
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idrisa Kikula (Mbele) akiongozana na Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Benjamin Mkapa (katikati) na Mkuu wa Baraza la Bodi ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Balozi Juma Mwapachu (kulia) leo katika mahafali ya Nne ya Chuo Kikuu Cha Dodoma yaliyohitimishwa katika Viwanja vya Chimwaga Chuoni hapo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Dkt Nchimbi akutana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia, Lusaka

$
0
0
Waziri Mambo ya Ndani wa Tanzania, Mhe Dkt. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na  Mhe. Edgar Lungu (kulia) kwenye Ofisi za Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia.  Dkt Emmanuel Nchimbi aliwasili nchini Zambia tarehe 22 Novemba 2013 na kuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia, Dkt. Edgar Lungu siku hiyo hiyo. Mazungumzo baina ya Mawaziri Hawa yaljikita katika kuendeleza ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali yanayohusu Wizara zao. Aidha, wamekubaliana kuagiza mapema iwezekanavyo wataalam wa Wizara zao wakutane kwa majadiliano ya kuweka misingi ya ushirikiano huo.

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI TUZO KWA WATANZANIA WALIO MSTARI WA MBELE KATIKA KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO, JIJINI DAR LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa hafl ya kutoa Tuzo kwa Watanzania walio mstari wa mbele katika kuboresha Afya ya Mama na Mtoto, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akimkabidhi Tuzo, Mwnyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi, wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo kwa Watanzania walio mstari wa mbele katika kuboresha Afya ya Mama na Mtoto, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam,leo. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mery Nagu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akimkabidhi Tuzo,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mery Nagu, aliyepokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo kwa Watanzania walio mstari wa mbele katika kuboresha Afya ya Mama na Mtoto, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam,leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Ghari Bilal, akimkabidhi Tuzo, Dkt. Faraji Mkwakwacha, wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo kwa Watanzania walio mstari wa mbele katika kuboresha Afya ya Mama na Mtoto, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam,leo. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mery Nagu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akimkabidhi Tuzo, Nesi Yasinta Baruti, kutoka Mkoa wa Katavi, wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo kwa Watanzania walio mstari wa mbele katika kuboresha Afya ya Mama na Mtoto, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam,leo. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mery Nagu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akimkabidhi Tuzo, Elia Elikana, kutoka mkoa wa Singida ambaye ni mwanaume aliyepata tuzo hiyo kwa kumsindikiza mkewe Kliniki mara nyingi, wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo kwa Watanzania walio mstari wa mbele katika kuboresha Afya ya Mama na Mtoto, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam,leo. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mery Nagu.
Picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi ya Madaktari wahitimu Tanzania na waliopata Tuzo.
Picha ya pamoja na wanamuziki wa Sikinde, waliokuwa wakitoa burudani katika hafla hiyo.Picha na OMR.

ZITTO KABWE NA DKT KITILA MKUMBO KUKUTANA NA WANAHABARI LEO

$
0
0

Taarifa inatolewa kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe pamoja na Dk Kitila Mkumbo watakutana na wahariri na waandishi wa habari leo Jumapili tarehe 24 Novemba 2013. 

Watatumia nafasi hii kutoa maoni na msimamo wao kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA ya hivi karibuni. 
Mkutano huu na waandishi wa habari utafanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5.00 asubuhi.



Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe, 
Dar es Salaam.
Jumamosi, 23 Novemba 2013. 
Dar es Salaam. 




KINANA NA UJUMBE WAKE WAWASILI WILAYANI KYELA MKOANI MBEYA LEO KWA ZIARA YA SIKU 11.

$
0
0
Sekretarieti kuu ya CCM,ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (pichani kati),Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro (kulia) pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakiwapungia wakazi mbalimbali waliofika kuwalaki mapema leo walipokuwa wakiwasili kwenye Bandari mpya ya Kiwila Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli. 
 Pichani shoto ni Nahodha Mkuu wa Meli ya Mv Songea akitoa maelezo mafupi namna ya moja ya chombo cha meli kinavyofanya wakati ikisafiri majini, kwa Sekretarieti kuu ya CCM,ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC,siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye mapema leo walipokuwa wakienda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli.Pichani kulia ni Nahodha msaidizi wa Meli ya Mv Songea.Conrad Shauritanga akiongoza meli hiyo.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro akiuliza jambo kwa Manahodha wa meli hiyo wakati ikiwa safarini kuelekea Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli.
 Mbunge wa jimbo la Kyela na Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe akimlaki kwa furaha kubwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake walipowasili mapema leo  kwenye Bandari mpya ya Kiwila, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli. 
Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.David Mwakyusa akimlaki  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake waliowasilia mapema leo  kwenye Bandari mpya ya Kiwila Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli. Pichani kati ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya (CCM),Dkt Mary Mwanjelwa akishuhudia tukia hilo
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipokelewa na Mwenyekiti Mkoa wa Mbeya,Bwa. Godfrey Zambi wakati wakishuka ndani ya meli ya Mv Songea mapema leo  kwenye Bandari mpya ya Kiwila, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na baadhi ya wanachama wa CCM waliofika kumlaki na ujumbe wake mara baada ya kupokelewa vyema katika  kwenye Bandari mpya ya Kiwila, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma. 
  Mbunge wa jimbo la Kyela na Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe akitoa ufafanuzi  kwa Katibu Mkuu wa  CCM,Ndugu Kinana kuhusiana na kivuko cha Tungi ambacho kwa sasa hakifanyi kazi .Kinana na ujumbe wake tayari amewasili leo kwa meli ya Mv.Songea Wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Wilayani Nyasa mkoani Ruvuma 
 Sehemu ya kivuko cha Tungi ambachao hakitumiki kwa sasa mara baada ya kujaa mchanga,kwa sasa hakitumiki tena kama kionekanavyo pichani mapema leo.
"UMOJA NI USHINDI".! Mbunge wa jimbo la Songwe Mh.Phillip Mulugo, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya (CCM),Dkt Mary Mwanjelwa Mbunge wa jimbo la Kyela na Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe wakiwa wameshikana mikono kwa pamoja mara baada ya kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake

MISS ILALA 2013 DORICE MOLLEL HANDS OVER 132 STORY BOOKS WORTH 200,000 TO UKONGA PRIMARY SCHOOL

$
0
0
download(3)
Mkuki wa Nyota Editor Godance Mkuki(right) hands over 132 story books to Miss Ilala 2013 Doris Mollel at the Ukonga primary school premises in Dar es Salaam during the climax celebration of the International Children’s day.
In an efforts to promote a reading culture in the country Mkuki wa Nyota publishers recent during the international children day decided to give 132 story books worth 200,000 to Miss Ilala 2013 Doris Mollel who hands over to Ukonga Primary school.
download(4)download(13)
Miss Ilala 2013 Doris Mollel finally hands over story books worth Tsh 200,000 to academic teacher of Ukonga Primary school during the International Children day in Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI WA MAJI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MIRADI SINGIDA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge ameridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Singida. Dk. Mahenge amesema hayo akiwa anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Singida kukagua miradi ya maji katika Halmashauri za Wilaya ya mkoa huo.

“Nimetembelea mikoa karibu yote nchini kukagua miradi ya maji, lakini ni Singida pekee ambako karibu miradi yake yote imetekelezwa kwa asilimia kubwa, ikiwemo mitatu iliyokamilika na mingine ipo katika hatua nzuri kiutekelezaji”, alisema Dk. Mahenge.

“Nawapongeza sana watendaji Singida kwa kazi nzuri na nawashauri wasibweteke, bali wafanye bidii kuhakikisha mpaka mwezi Juni 2014 wawe wametekeleza mpango wa kutekeleza miradi yote na si vinginevyo”, aliongeza Dk. Mahenge.

Dk. Mahenge alifurahia utendaji kazi wa mkandarasi wa mradi wa maji wa kijiji cha Ng’unguli, kwa hatua iliyofikiwa licha ya kuwa na miezi mitatu tu tangu ianze na kuahidiwa kuwa mpaka mwezi ujao utakuwa umekamilika. Huku akisisitiza viongozi waelekeze nguvu katika miradi mingine itekelezwe kwa wakati na maji yapatikane.

Pia, alitembelea mradi wa maji wa Mamlaka ya Singida Mjini unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania, Badea na OFID na kufurahishwa na maendeleo ya mradi huo mkubwa ambao unaendelea kujengwa na baada ya kukamilika utakuwa ni moja ya miradi mikubwa inayotoa huduma ya maji nchini.

Katika ziara hiyo Dk. Mahenge alifanikiwa kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo Singida Mjini, Manyoni, Ikungi, Kiomboi, Puma, Iramba, Unghandi, Ikhanoda, Puma, Itigi, Iguguno, Nguvumali.

Mkoa wa Singida umepokea Sh. Bil 41.5 kwa robo ya kwanza ya mgao wa fedha mwaka 2013/14 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya vijiji 10 na programu ya BRN.

Dk. Mahenge amemaliza ziara yake ya mikoa ya Dodoma na Singida mwishoni mwa wiki, katika kuhakikisha utekelezaji wa awamu ya kwanza ya programu ya wa Big Results Now na miradi yote ya maji inatekelezwa kwa kasi na ufanisi ili kuleta matokeo yaliyopangwa kwa wakati.
Naibu Waziri wa Maji,Mhe. Dk. Binilith Mahenge akipokea taarifa ya hali maji Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Naibu Waziri wa Maji,Mhe. Dk. Binilith Mahenge (katikati) akikagua mradi wa kijiji cha Nguvumali, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Dk. Binilith Mahenge akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Singida (SUWASA) hawapo pichani, kulia ni Meneja wa SUWASA Inj. Isaac Nyakonji.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Dk. Binilith Mahenge, akisoma taarifa ya majumuisho ya ziara yake Mkoani Singida katika mkutano na viongozi na watendaji wa mkoa huo.
Mradi wa maji wa Mamlaka ya Maji Singida Mjini.

kikwangua anga ilala

$
0
0
Ankal salaam. Twaishukuru NSSF kutujengea moja ya vikwangua anga vingi vilivyopangwa kujengwa  hapa Ilala, ambacho hadi sasa zimeshafikia ghorofa zaidi ya 23 na ujenzi unaendelea...
Ni wazi kuwa muda si mrefu tutaona "skyline" ya Ilala ikianza kubadilika kabisa kwani wapo wawekezaji waliokuwa wanasubiri tu kuona nani anaanza kujenga majengo makubwa makubwa Ilala ili nao wawekeze fedha zao katika sekta hii inayobadilisha kabisa sura ya jiji la Dar na viunga vyake. Heko NSSF.
Mdau Ilala Boma

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MAKAMU MKUU WA CHUO CHA ST. JOHNES

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images