Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110087 articles
Browse latest View live

TAFF YATOA OMBI KWA SERIKALI KUISAIDIA TIMU YA TAIFA YA WALEMAVU

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

SERIKALI imeombwa kuisaidia Timu  ya Taifa mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu ili wafanye vizuri katika mashindano ya kombe la mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

akitoa ombi hilo leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF), Riziki Lulida ambapo amesema ni vema Serikali ikatoa kutoa kipaumbele katika kuisaida timu hiyo ili iibuke na ushindi katika mashindano hayo ya Afrika Mashariki na Kati.

Amefafanua ni imani yao heshima ya nchi inaweza kutengenezwa kupitia timu yoyote hivyo hakuna sababu ya kuzibagua timu kwa kuangalia maumbile yao."Tunatoa ombi kwa Serikali kuisaidia timu hii ili nayo iweze kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ikiwemo hiyo ya Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Mwenyekiti huyo TAFF ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum(CUF), amesema atawashirikisha wabunge wenzake hasa wenye ulemavu ili waweze kusaidia timu hiyo ya taifa kwani ikisaidiwa itafanya vema katika michuano mbalimbali.

Kuhusu mashindano ya Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Katibu wa TAFF Moses Mabula amesema yataanza kuanzia Juni 22 mwaka huu na yatashirikisha nchi 11 za Ukanda wa Afrika Mashariki.

Amezitaja baadhi ya nchi ambazo zitashiriki kwenye mashindano hayo ni mwenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Sudan Kusini na Sudan huku akifafanua licha ya auhitaji wa misaada mbalimbali hitaji lao kubwa ni kuona Watanzania wengi wanajitokeza katika viwanja wakati wa mashindano hayo.

"Matarajio yao ni kubakiza kombe la mashindano hayo hapa nyumbani Tanzania.Hii ni mara ya kwanza sisi kushiriki mashindano hayo lakini tunaamini tukiiungwa mkono tutafanya vizuri na kuitangaza nchi kimataifa,"amesema.

Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo Juma Kidevu amesema maandalizi yanaendelea vizuri na kuahidi kuibuka kidedea katika mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika nchini na kwamba changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni uhaba wa vifaa kama fimbo za kutembelea, jezi na mipira hivyo wanaomba wadau kujitokeza kuwasaidia.

 Wachezaji wa timu ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya maandalizi ya mshindano ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati yanayotarajiwa kufanyika Juni 22 mwaka  huu hapa nchini Tanzania. 
 Wachezaji wa timu ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya maandalizi ya mshindano ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati yanayotarajiwa kufanyika Juni 22 mwaka  huu hapa nchini Tanzania. 
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya maandalizi ya mshindano ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati yanayotarajiwa kufanyika Juni 22 mwaka  huu hapa nchini Tanzania. 

HAKI ARDHI YAENDESHA MAFUNZO KWA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA HAKI ZA ARDHI NA MABADILIKO YA TABIANCHI,BAGAMOYO

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi (Haki Ardhi) Bw. Cathbert Tomitho akielezea kwa kina juu ya mfumo wa utatuzi wa migogoro ya ardhi.
Ofisa Programu wa Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi (Haki Ardhi) Bw. Joseph Chiombola akitoa mada juu ya Sheria za ardhi kwa wanawake.
Bw. Nuhu Kitaluka akitoa mada juu ya mabadiliko ya Tabianchi, athari zake kwa wazilishaji wadogo wadogo katika kilimo,ufugaji na afya pia alitoa mifano kutoka wilaya za Morogoro na Mufindi
Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa wahariri na waandishi wa Habari juu ya haki za ardhi na mabadiliko ya Tabianchi
Bw. Samson Mollel akielezea mbinu shirikishi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi vijijini
Picha ya pamoja.

MKURUGENZI WA LEBO YA CHANEL NA FENDI AFARIKI DUNIA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MBUNIFU maarufu duniani na Mkurugenzi wa kampuni za Chanel na Fendi Karl Lagerfeld (85) amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Vyombo vya habari nchini ufarasa vimeeleza kuwa Karl hajaonekana katika matukio makubwa ya mitindo  tangu mwezi uliopita likiwemo lile la Channel na alilazwa katika hospitali ya Paris na kuruhusiwa na umauti kumkuta jana kabla ya kulazwa huku chanzo cha kifo chake hakijathibitishwa.

Wanamitindo wakubwa wakiwemo Kim Kardashian, Victoria Beckham na  Donatella Versace wametoa salamu za rambirambi kutokana na kifo cha mbunifu mkongwe ambaye alifahamika zaidi kwa kuvaa miwani nyeusi na mtindo wa ubanaji wa nywele.

Wengi wa watu maarufu wamemuelezea Karl kama mtu mcheshi na mkarimu kuwahi kutokea, na tasnia ya mitindo na ubunifu imepata pengo kubwa sana.

Lebo ya Fendi imekuwa maarufu zaidi duniani kote ikiwemo nchini huku nchini China ikishika kasi tangu mwaka 2007.

MAJOHE KWANGOSOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA KITUO CHA POLISI KUDHIBITI MATUKIO YA UHALIFU

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAKAZI wa Kata ya Majohe kwa Ngosoma iliyopo Ukonga Gongo la mboto jijini Dar es Salaam wameiomba Serikali kusaidia ujenzi wa Kituo cha Polisi kwenye kata hiyo ili kudhibiti matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara kiasi cha kusababisha hofu. Wakizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam jana na leo kwa nyakati tofauti wananchi wa kata hiyo wamesema matukio ya uhalifu yamekuwa yakitokea mara kwa mara , hivyo wanaamini kikijengwa kituo cha polisi itaisaidia kupunguza matukio ya uhalifu.

Wamesema Kata ya Majohe kwa Ngosoma inalo eneo kubwa na hivyo kuna idadi kubwa ya wakazi lakini cha kusikitisha hakuna kituo cha polisi licha ya jitihada mbalimbali kufanywa na Serikali za mitaa. "Kumekuwa na matukio ya uhalifu huku kwetu na sasa tumechoka kuendelea kushuhudia yakiendelea kutokea. 

Tunaomba Serikali itusaidie kujenga kituo cha Polisi hasa kwa kuzingatia tayari eneo lilishatengwa na baadhi ya hatua za awali ziliasha. Tukiwa na kituo cha Polisi itasaidia kudhibiti uhalifu na wananchi tutakuwa na sehemu ya kukimbilia kutoa taarifa na kupata msaada wa Polisi,"amesema Shaban Said anayeishi mtaa wa Kichangani.

Ameongeza wiki mbili zilizopita saa mbili usiku , kuna watu wanaosadikiwa ni majambazi walivamia maduka yaliyopo eneo la Kona na kabla ya kupora fedha walijeruhi baadhi ya waliokuwamo kwenye maduka hayo na kisha kukimbia eneo la tukio hilo.

 "Tukio ambalo nimelizungumzia ni moja tu lakini kuna matukio ya aina hiyo yamekuwa yakitokea huku kwetu, hivyo kilio chetu wananchi wa Majohe Kwasoma tunaomba tujengewe kituo cha Polisi, tuko tayari kuchanga na nakumbuka kuna kikao kiliitishwa na wananchi wote tukakubaliana kuchanga fedha ili kituo cha Polisi kijengwe,"amesema Jumanne Joseph anayeishi Majohe Kona.

Kwa upande wa baadhi ya viongozi wa Kata ya Majohe kwangosoma wameiambia Michuzi Blog kuwa , kuna hatua mbalimbali ambazo znaendelea kuhakikisha kituo cha polisi kinajengwa hasa kwa kuzingatia eneo lipo na wananchi wanafahamu.

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAWASHIKILIA RAIA 10 WA ETHIOPIA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI

$
0
0
*Wengine  washikiliwa kwa tuhuma za ubakaji na kupatikana na mali za wizi

JESHI la polisi Mkoani Mbeya linawashikilia raia 10 wa Ethipia kwa tuhuma za kuingia nchini bila kuwa na kibali maalumu na hiyo ni baada ya msako uliofanywa na jeshi la polisi tarehe 19 mwezi huu  katika kijiji cha Lugelele Wilaya ya Mbarali katika barabara ya itokeayo Njombe kuelekea Mbeya wakiwa wanatembea kwa miguu pasipokuwa na vibali maalumu vya kuishi nchini.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi Mkoani humo Charles Kakola (30) mkazi wa Iwindi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka mitatu ambapo imeelezwa kuwa mtuhumiwa akitekeleza hayo mara baada ya kulewa na mtuhumiwa  amekiri kosa hilo na uchunguzi unaendelea.

Pia katika tukio jingine la ubakaji Samwel Msukila (22) mkazi wa Kilasiro anatuhumiwa kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka tisa na hadi sasa mama wa mtuhumiwa huyo amekamatwa huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Katika tukio jingine la ubakaji lililotokea Mbeya vijijini  Alinani Mwakifuna (59) ambaye pia ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwaselela anashikiliwa na jeshi lapolisi kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 15 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni tama za kingono, imeelezwa kuwa mtuhumiwa alimrubuni binti kabla ya kumwingilia kimwili.
 Pia jeshi la polisi Mkoani humo Mkoani humo linawashilia watuhumiwa kadhaa kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo, kukutwa na mali zinazosadikika kuwa za wizi, kukutwa na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini pamoja na makosa ya kuingiza bidhaa nchini  bila kuwa na kibali na watuhumiwa wanashikiliwa na jeshi la polisi huku uchunguzi ukiendelea.

Makamu wa Rais afanya ziara wilayani Iramba mkoani Singida

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha kusindika alizeti cha Yaza katika kijiji cha Ndago, wilayani Iramba mkoa wa Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mhe. Mwigulu Nchemba (kushoto) mara baada ya kutembelea kiwanda cha kusindika alizeti cha Yaza katika kijiji cha Ndago, wilayani Iramba mkoa wa Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kutembelea kiwanda cha kusindika alizeti cha Yaza katika kijiji cha Ndago, wilayani Iramba mkoa wa Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Bw. Maulid Njau (kushoto) juu ya maboresho na ukarabati wa chuo cha ualimu Kinampanda, wilayani Iramba mkoa wa Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Naibu Waziri Nditiye afanya ziara Vodacom

$
0
0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi (kushoto), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom, Rosalynn Mworia akizungumza juu ya utendaji kazi wa kidijitali wa kampuni hiyo  mapema leo kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Mhandisi Peter Ulanga.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akisikiliza kuhusu utendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Hisham Hendi (wa pili kulia) alipotembelea makao makuu ya kampuni ya Vodacom mapema leo na kujionea namna ambavyo kampuni hiyo inafanya kazi zake kidijitali. Kushoto ni Naibu Katibu mkuu wa Wizara hiyo, Dr Jim Yonaz na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Mhandisi Peter Ulanga.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (Katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (wa kwanza kushoto) wakisikiliza shughuli zinazofanywa na kitengo cha Ufanisi wa mtandao kutoka kwa Mhandisi Pendo Boshe wa kitengo hicho wakati wa ziara ya naibu waziri katika ofisi za Vodacom Tanzania mapema leo, ambapo naibu waziri alijionea namna ambavyo kampuni hiyo inafanya kazi zake kidijitali.

WAHAMIAJI HARAMU 22 MIKONONI MWA POLISI MKOANI TABORA

$
0
0
Na Amisa Mussa
Jeshi La Polisi Mkoani Tabora Kwa kushirikiana na raia wema limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu  ishirini na wawili ambao walikua wakisafiri kutoka Burundi kupitia Kigoma, Tabora kuelekea nchini Zambia wakiwa kwenye usafiri wa basi  la An.

Miongoni mwa raia hao wa Burundi  waliokamatwa tisa ni watoto wadogo ,ambao walikua pamoja na wazazi wao katika safari yao, raia hao wamekamatwa wakiwa wanaingia kwenye  kituo kikuu cha mabasi Mjini Tabora ndani ya basi  la An ambalo linafanya  safari zake  katika Mikoa ya Tabora na Kigoma

Kamanda wa Polisi Wilaya  ya Tabora Mjini John Mfinanga, ambaye aliongoza  kikosi kazi cha askari Polisi wasaidizi  amesema wamefanikiwa kuwakamata raia hao wa Burundi baada ya kupata taarifa za siri juu ya  ujio wao  ambao walikua wakipita hapa Mkoani  Tabora wakielekea nchini Zambia.

baadhi ya wananchi wameviomba vyombo vya dola kuwachukulia hatua kali za kisheria mawakala ambao wanawasafirisha  wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.

Wananchi waaswa kutoa taarifa Polisi wanapopata ujumbe wa matapeli-TCRA

$
0
0
 Wananchi wameshauriwa kutokukaa kimya  pindi wanapopokea ujumbe wa matapeli bali waripoti Polisi  namba iliyokutuma ujumbe huo ili jeshi hilo  ilifanyie kazi.

Ushauri huo umetolewa na mkuu wa kitengo cha makosa ya kimtandao mkoa wa Arusha Inspekta Aman Ngaleni alipokuwa akitoa elimu kwa wananchi waliohudhuria  Kampeni ya Mnada Kwa Mnada, karibu Tukuhudumie inayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya Mawasiliano TCRA, Jeshi la Polisi kitengo cha uhalifu mitandaoni, makampuni ya siku ya Vodacom, Tigo, Airtel, Halotel, Zantel na TTCL.

Kampeni hiyo imefanyika Februari 20, 2019 katika viwanja vya stendi ya Kilombero, jijini Arusha.
 Wananchi  wakipata huduma katika kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Stendi ya Kilombelo Jijini Arusha ikiwa kampeni ya TCRA kuelimisha wananchi kuhusiana na huduma za mawasiliano zinazotolewa na wadau mbalimbali.
 Wadau wakijadiliana masuala ya Mawasiliano katika kampeni ya Mnada kwa Mnada katika stendi ya Kilombelo Jijini Arusha.
Mwananchi akisoma jarida la Kituo cha Daladala cha Kilombelo Jijini Arusha katika  Kampeni  ya Mnada kwa Mnada  inayoendeshwa na Mamlaka ya Makatika St kuelimisha mawasiliano (TCRA).

MWILI WA MENEJA HABARI, MAWASILIANO TFS KUAGWA KESHO DAR

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MWILI wa marehemu Glory Mziray ambaye enzi za uhai wake alikuwa Meneja Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) unatarajiwa kuagwa kesho Alhamisi katika Kanisa la KKKT Tanki Bovu jijini Dar es Salaam kuanzia saa sita mchana.

Glory alifikwa na umauti jana saa saba mchana akiwa anazungumza na waandishi wa vyombo mbambali vya habari nchini katika Ofisi za Jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii ambalo linajulikana zaidi kwa jina la Mpingo House jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo, TFS inaeleza kuwa mwili wa marehemu Glory leo utapelekwa na kulala nyumbani kwake Goba-Kinzudi na kesho Alhamisi utaagwa katika Kanisa la KKKT Tanki Bovu jijini Dar es Salaam na baada ya hapo atasafirishwa kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Ijumaa baada ya chakula cha mchana.

Taarifa ya TFS imefafanua zaidi kuhusu ratiba hiyo kwa leo inaonesha kwamba waombolezaji wameanza kuwasili nyumbani kwa marehemu Kinzudi saa tatu asubuhi na itakapofika saa 09:30 alasili mwili utawasili nyumbani hapo na kisha kufuatiwa na ibada itakayoanza saa 11 jioni.

Pia kwa kesho Alhamisi ratiba inaonesha waombolezaji wataanza kuwasili saa mbili asubuhi na itakapofika saa nne asubuhi chakula na saa sita ibada ya kuaga(KKKT Tanki Bovu) ikifuatiwa na kutoa heshima za mwisho saa 7:15 mchana.Kwa mujibu wa ratiba hiyo safari ya kuelekea Morogoro itaanza saa 8:00 mchana.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa Ijumaa ya Februari 22, 2019 , inaonesha 02:30 itakuwa ni kifungua kinywa, saa sita chakula cha mchana na saa nane mchana itafanyika ibada ya mazishi ikifuatiwa na kuweka mashada na salamu za makundi maalum.

NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
Kwa mujibu wa TFS ni kwamba kwa waombolezaji wanaotaka kufika, Kinzudi ipo katikati ya Salasala na Goba.Njia zipo mbili moja ingia Mmbuyuni elekea njia ya Kinzudi, pia kuna mabasi unashuka Kinzudi Stand kisha unachukua bajaji au bodaboda ambaye itakupeleka Mendeleo street.

Pia unaweza kuingia njia ya Masana halafu unashuka kituo kinaitwa njia panda ya Kata, baada ya hapo chukua bodaboda ikupeleke Maendeleo street ndipo msiba ulipo.Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu ya mkononi katika namba 

0786670454(baba June Amini) au Dk.Martin 0620488216, 0714529562.

WATUMISHI WA SERIKALI WANAODAIWA KODI YA ARDHI KUSHTAKIWA

$
0
0
Na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Dkt. Angeline Mabula ameagiza kuanza mchakato wa kuwaorodhesha watumishi wa umma ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi hadi sasa ili wafikishwe katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba.

Dkt. Mabula ameyasema hayo alipofanya ziara katika Wilaya ya Bunda na Serengeti mkoani Mara na wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza wakati wa ziara yake inayoendelea ya kuhamasisha malipo ya kodi ya pango la ardhi  katika kanda ya ziwa.

“Nyinyi watumishi wa Serikali mnatakiwa kuwa wa mfano katika kulipa kodi za serikali kwa sababu hatuwezi kwenda kudai wengine wakati sisi wenyewe hatujalipa kodi ya pango la ardhi, na kokote ntakapopita nataka majina ya watumishi ambao hawajalipa ili wafikishwe katika mabaraza” alisisitiza Dkt. Mabula.

“Mheshimiwa Rais anasimamia miradi mikubwa hapa nchini kama ule wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa Mto Rufiji, Stiegler's Gorge na uimarishaji wa Shirika la Ndege la Tanzania ambayo miradi hii yote inategemea kodi na mapato ya ndani, hivyo ni lazima tumuunge mkono katika kulipa kodi hizi” aliongeza Dkt. Mabula.

Wakati akiwa Wilayani Ukerewe alipokea taarifa ya afisa ardhi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Tewe Shaban kuwa hadi sasa halmashauri yake imeshakusanya jumla ya Tsh 41,288,175 wakati lengo ni 100,000,000 kwa mwaka wa fedha 2018/2019, ambayo ni sawa na 41.2% iliyokusanywa.

Afisa huyo alimueleza Dkt. Mabula kuwa hadi sasa jumla ya ilani 131 zenye thamani ya Tshs 54,446,550 za madai ya kodi ya ardhi zimesambazwa kwa wadaiwa kodi ya ardhi ambao wameanza kupunguza madeni yao na mpaka sasa wameshalipa Tshs. 3,100,700 na kubaki Tshs. 51,345,850.

Baada ya kupokea taarifa hiyo Dkt. Mabula alishangazwa na ukusanyaji huo hafifu wa maduhuli ya Serikali na alimuagiza Afisa huyo kuwafikisha mahakamani wadaiwa sugu wa kodi ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo, na aanze na watumishi wote wa Serikali katika halmashauri ya wilaya ya Ukerewe.

Katika kuhakikisha linatekelezwa hilo Dkt. Mabula akaagiza kuwepo kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi atakayesimamia kesi hizo na kuzitolea hukumu kwa wadaiwa sugu waweze kulipa kwa wakati na kama hawatotekeleza basi milki zao zitauzwa ili kulipwa deni hilo.

Akiwa wilayani Bunda Dkt. Mabula alimuagiza afisa ardhi mteule kumfikishia majina ya maafisa wa halmashauri ya wilaya ya Bunda ambao wanadaiwa kodi ya pango la ardhi na hawajalipa hadi sasa wakati muda wa kulipa kwa hiari ushaisha tangu tarehe 31 januari 2018.

Vivyohivyo Dkt. Mabula akiwa katika Halmashauri ya wilaya ya Serengeti amamuagiza Afisa Ardhi Mteule kukabidhi majina ya watumishi wa umma ambao wadaiwa wa kodi ya ardhi kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo ili waweze kufikishwa katika baraza ardhi iwapo watakuwa hawajalipa.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Dkt. Angeline Mabula akimuagiza Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ukerewe Tewe Shaban kuwa na usimamizi mzuri wa makusanyo ya Kodi ya pango la ardhi na kuwa mfumo mzuri wa uhifadhi wa nyaraka za ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Dkt. Angeline Mabula akiongea na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Dkt. Angeline Mabula wakati alipofanya ziara katika wilaya hiyo. Picha zote Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Dkt. Angeline Mabula akimuagiza Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ukerewe Tewe Shaban kuwa na usimamizi mzuri wa makusanyo ya Kodi ya pango la ardhi na kuwa mfumo mzuri wa uhifadhi wa nyaraka za ardhi. Picha zote na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.

SINGIDA UNITED KUTUMIA UWANJA WA AZAM COMPLEX DHIDI YA COASTAL UNION

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mchezo wa Kombe la Shirikisho Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Singida United na Coastal Union sasa kufanyika Jijini Dar es Salaam. Singida United wameuomba uongozi wa TFF kuuruhusu mchezo huo kuchezwa Jijini Dar badala ya Singida kutokana na ugumu wa ratiba ya ligi na FA.

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United United Festo Sanga amesema kuwa Kutokana na Ugumu wa ratiba yetu ya Ligi na kombe la FA, Mchezo wao dhidi ya Costal Union wa kombe la FA sasa utachezwa Dar es Salaaam tar 23/02/2019 badala ya Namfua Singida  ulivyopangwa awali.

Amesema kuwa,  leo Jumatano wanacheza na Ndanda Fc huko Mtwara, hivyo kesho  timu inatakiwa iondoke Mtwara kurejea Singida ambapo kwa umbali wa Mtwara hadi Singida ni safari ya Siku mbili, hivyo timu ingefika Singida tarehe Februari 22.

Sanga ameeleza kuwa mechi yao dhidi ya Coastal itachezwa Feb  23 wakiwa nyumbani Namfua na wameona kuwa  Jambo hilo tumeona sio salama kwa Afya ya wachezaji na mchezo husika.

Ameeleza kuwa kwa pamoja  viongozi wa Singida United wameuomba uongozi wa TFF ambao wao ndiyo wanaosimamia kombe la Azam Sports Federation Cup (FA) watubadilishie Uwanja ili kuendana na muda, angalau timu ipumzike na iweze kucheza Feb 23.

Sanga amewashukuru  TFF kwa kukubali ombi lao na wamewapatia Uwanja wa Azam Complex  na mechi itachezwa saa 1:00 usiku.

Uongozi wa Singida United umewaomba radhi kwa mashabiki na wanasingida, kwakuwa wameamua kubadili uwanja na wamefanya hivi kwa afya ya wachezaji wao na mchezo wenyewe.

MUSEVENI APITISHWA TENA NA CHAMA CHAKE KUGOMBEA URAIS KWA MUHULA WA SITA

$
0
0
CHAMA tawala nchini Uganda kimemteua Rais Yoweri Kaguta Museveni kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2021. Hiyo inamaana ya kuwa, kiongozi huyo mwenye miaka 74, na aliyeingia madarakani  mwaka 1986, atagombea urais kwa muhula wa sita.

Taarifa ya Chama cha National Resistance Movement (NRM) kimesema katika kikao kilichoongozwa na Museveni kimesema Rais huyo aendelee kuongoza harakati za taifa kwa kugombea tena urais kwa mwaka 2021 na kuendelea ili kuondosha vikwazo vya mabadiliko na maendeleo.

Kwa mujibu wa taarifa hii iliyoandikwa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC)linasema miaka ya nyuma Museveni aliwahi kueleza kuwa viongozi "wanaodumu" madarakani ndio chanzo cha matatizo barani Afrika.

Hata hivyo,wakati akigombea muhula wa tano wa madaraka mwaka 2016, Rais Museveni aliwahi kueleza  kuwa huo haukuwa muda muafaka kwake kuondoka madarakani kwani bado alikuwa na kazi ya kufanya. CHANZO BBC.

RAIS WA UFARANSA AZURU ENEO LA MAKABURI YA WAYAHUDI

$
0
0
RAIS wa Ufaransa Emmanuel Macron ameyatembelea maziara ya Wayahudi baada ya makaburi 80 ya Wayahudi kuharibiwa kwa makusudi ambapo wanasiasa wa pande zote wanalaani vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi.

Imeelezwa kuwa Rais Macron jana Jumanne alikwenda kwenye jimbo la Alsace mashariki mwa Ufaransa ambapo makaburi 80 ya Wayahudi yaliharibiwa kwa makusudi na kukashifishiwa kwa kaulimbiu za kifashisti.

Rais Macron alikutana na viongozi wa Wayahudi wa sehemu hiyo na kusisitiza dhamira ya kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi katika kila namna itakayojitokeza na kwamba vitendo 541 vya chuki dhidi ya Wayahudi viliripotiwa mwaka jana nchini Ufaransa. Takwimu hizo zinawakilisha ongezeka la aslimia 74, kulinganisha na mwaka 2017.

Pia Rais Macron amelaani uharibifu uliofanywa kwenye makaburi hayo ya Wayahudi, ambapo amesema  chuki dhidi ya Wayahudi ni kinyume na maadili ya Ufaransa na kwamba taifa lote la Ufaransa, linapaswa kupinga kadhia hizo. 

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelaani vitendo hivyo vya kushtusha vilivyomfanya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Israel atoe mwito kwa Wayahudi wa nchini Ufaransa kurejea nyumbani, Israel. 

Waziri Mkuu Netayahu amesema jambo lililotokea ni la kushtusha nchini Ufaransa.Makaburi 80 ya Wayahudi yameharibiwa na kubandikwa nembo za Manazi na watu wanaowachukua Wayahudi. 

Hata hivyo jamii ya Waislamu nchini Ufaransa wamefanya maandamana kupinga chuki dhidi ya Wayahudi. Wakati huo huo waziri mkuu wa Poland alibatilisha mpango wa nchi yake wa kupeleka ujumbe kwenye mkutano wa mjini Jerusalem baada ya waziri wa mambo ya nje wa Israel, Israel Katz kusema kwamba Poland ilishirikiana na mafashisti na kuongeza kuwa Wapolish walinyonya maziwa ya kuwatia chuki dhidi  ya Wayahudi.

Naye Balozi wa Marekani nchini Poland amemtaka waziri huyo wa Israel aombe radhi. Balozi huyo  Georgette Mosbacher amesema Israel na Poland ni washirika thabiti wa Marekani na kwamba hawapaswi  kujibizana. Balozi huyo wa Marekani nchini Poland amesema ushirika wao ni muhimu na kwamba matatizo  yote yanaweza kutatuliwa baina ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa tahtmini ya msomi Jürgen Ritte, mhadhiri kwenye chuo kikuu cha Sorbonne mjini Paris vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi vimeongezeka nchini Ufaransa. Msomi huyo amesema chuki hiyo  inatoka sehemu mbalimbali. 

Msomi huyo Ritte amesema chuki hiyo inatokana na itikadi kali za kidini na kisiasa. Pia amesema kwamba miongoni mwa wanaharakati wa vizibao vya manjano pia wapo watu  wanaowachukia Wayahudi.CHANZO DW(Mwandishi:Zainab Aziz).

MASHAHIDI KESI YA GUGAI WAENDELEA KUSUBIRI KIBALI

$
0
0
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imekwama kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake, inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru),Godfrey Gugai kutokana na kuchelewa kupatikana kwa kibali cha kuwaita mashahidi kutoka mikoani.

Wakili wa serikali kutoka Takukuru Vitilis Peter ameeleza hayo leo Februari 20.2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, pindi kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Amedai,  waliomba kibali cha kuwaita mashahidi kutoka mikoani lakini wamepata taarifa kuwa kibali hicho kimepatikana leo na kusababisha wao kushindwa kuandaa mashahidi.

Amedai,  ili shahidi aweze kutoa kuleta kutoa ushahidi akiwa anatokea mkoani ni lazima kipatikane kibali kwa sababu atatakiwa kulipwa.

Haya hivyo,  wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa ameuomba upande wa mashitaka kuwataja mashahidi watakaowaleta ili kuweka kumbukumbu ili asipokuja mmoja aletwe shahidi mwengine.

Akijibu hoja hiyo, Wakili Peter amedai hawawezi kutaja majina ya mashahidi hao ila mahakama itambue kuwa mashahidi wawili wanatokea Mwanza na watatu wanatokea Musoma. 

Kufuatia hayo,  Hakimu Simba amewataka upande wa mshitaka kuhakikisha wanaleta mashahidi ili kesi hiyo iweze kuendelea.

Kesi hiyo, imeahirishwa hadi Hakimu hadi Machi 4 na 6, mwaka huu kwaajili ya kuendelea na ushahidi kwa upande wa mashitaka.

Mbali na Gugai, washitakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Gugai na wenzake wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decembea 2015.

Inadaiwa kuwa akiwa Takukuru Dar es Salaam, Gugai alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake huku akishindwa kuzitolea maelezo.

YANGA YAVUNJA MWIKO WA KUFUNGWA CCM KIRUMBA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara ( TPL) Yanga wameendelea kukaa kileleni mwa msimamo baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Mbao. Mchezo huo wa TPL umechezwa leo Jijini Mwanza ukiwa ni wa ushindani kwa pande mbili Yanga wakitaka waondoe uteja wa kufungwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Mtanange huo ulianza kwa kasi kubwa sana, kila mmoja akicheza kwa umakini mkubwa na kutokutaka kuruhusu goli la mapema. Ilichukua dakik 45, kwa Mbao kuweza kuandika goli la kuongoza kupitia kwa mchezaji wake Ndaki Robert akimalizia krosi ya Amos Charles akiwaacha mabeki wakiuangalia mpira tu.

Mpaka mapumziko Mbao ilienda vyumbani wakiwa wapo mbele kwa goli 1-0, Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mashambulizi langoni mwa Mbao na katika dakika ya 50 Mshambuliaji wa Kimataifa wa Kongo Heritier Makambo anaisawazishia Yanga na ubao kusoma 1-1.

Mpira uliendelea kwa kasi na katika dakika ya 59, beki wa Yanga Kelvin Yondan akiwa nje ya 18 alipiga krosi iliyoishia mkononi mwa beki wa Mbao na mwamuzi kuweka penati.

Mshambuliaji wa Kimataifa  Burundi Amisi Tambwe anaiandikia Yanga goli la pili kwa mkwaju wa penati na kubadilisha matokeo ya ubao na kuwa 2-1.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga wanavunja mwiko wa kutokuifunga Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba wakiwa tayari wamepoteza mechi 2 za Ligi kuu.


Baada ya ushindi huo, Yanga wanatimiza alama 61 wakiendelea kujikita kwenye kilele cha msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara. Yanga inatarajiwa kurejea Jijini Dar es Salaam na kuunganisha safari ya kuelekea Namungo kwa ajili ya mchezo wa FA  dhidi ya Namungo FC.

Uzinduzi wa kampeni ya naweza na vodacom

$
0
0
 Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Bi. Harriet Lwakatare akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya 'NAWEZA NA VODACOM' inayowaelimisha wateja wake njia mbali mbali za kidijitali za kujihudumia na kutatua matatizo kwa haraka leo makao makuu ya kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi. Rosalynn Mworia.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Bi. Harriet Lwakatare akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya 'NAWEZA NA VODACOM' inayoelimisha wateja njia mbali mbali za kidijitali za kujihudumia na kutatua matatizo kwa haraka iliyofanyika leo makao makuu ya kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi. Rosalynn Mworia na Mkuu wa Idara ya ufanisi kwa Wateja, Bi. Najenjwa Mbagga. 

KIKAO KILICHOKUTANISHA WIZARA NA MASHIRIKA YA C-SEMA NA SOS-CHILDREN VILLAGE TANZANIA JIJINI DODOMA

WAZIRI MKUCHIKA ARIDHISHWA NA MAFANIKIO YA WALENGWA WA TASAF WILAYANI LIWALE.

$
0
0
Na Estom Sanga-Liwale

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mheshimiwa George Mkuchika amesema Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- ni mojawapo ya vielelezo vya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015 inayoelekeza serikali na Wananchi kukabiliana na umaskini.

Waziri Mkuchika ameyasema hayo akiwa katika wilaya ya Liwale Mkoani Lindi ambako pamoja na mambo mengine anakutana na Walengwa wa TASAF ili kujionea namna Walengwa hao wanavyotumia fursa zilizoko kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kujiletea maendeleo na kupunguza athari za umaskini miongoni mwao.

“kote nchini ninakofanya ziara kukagua shughuli za TASAF ninashuhudia mabadiliko makubwa katika maisha ya Walengwa jambo ambalo ni zuri na linapaswa kuendelezwa” amesisitiza Mhe. Mkuchika.

Aidha Waziri huyo ametaka Wataalam wa sekta mbalimbali nchini kote kuwa karibu zaidi na Wananchi na hususani Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili waweze kuboresha zaidi maisha yao na kunufaika na jitihada za serikali.

Akiwa katika kijiji cha Mbonde Katika wilaya ya Liwale Waziri Mkuchicha alitembelea baadhi ya kaya za Walengwa na kujionea namna wanavyotumia ruzuku itolewayo na TASAF katika kuboresha makazi kwa kununua mabati na kuezeka nyumba zao huku wengine wakianzisha shughuli za uzalishaji mali kama ufugaji wa kuku,bata, na kukuza shughuli za kilimo na hivyo kujiongezea kipato.

Kuhusu sekta ya afya,Waziri Mkuchika amekagua jengo la zahanati lililojengwa na TASAF kwa kushirikiana na Wananchi katika kijiji cha Mbonde zahanati ambayo imewaondolea wakazi takribani 400 adha ya kufuata huduma za matibabu mbali ya kijiji chao.Amewaasa Wananchi hao kulitunza jengo hilo ili waendelee kunufaika nalo.

Mapema Waziri Mkuchika akizungumza na Watumishi wa Umma waliopo katika Wilaya ya Liwale,aliwataka watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia msingi ya uadilifu na kujituma ili kuondoa kero za wananchi huku akionya kuwa kamwe serikali haitawavumilia Watumishi wanaokiuka misingi ya utawala bora kwa namna yoyote ile. 
Waziri Mkuchika akipata maelezo ya namna jengo la zahanati lililojengwa na TASAF katika kijiji cha Mbonde, Wilayani Liwale mkoani Lindi linavyowanufaisha wananchi wa eneo hilo na vijiji vya jirani.
Waziri Mkuchika (mwenye shati jeupe)akiwa katika nyumba ya mmoja wa Walengwa (kulia kwake)katika kijiji cha Mbonde ,nyumba ambayo imezekwa kwa mabati baada ya kupata ruzuku kutoa TASAF.
Waziri Mkuchika akizungumza na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia TASAF katika kijiji cha Mbonde (picha ya chini).

SERIKALI YAZUIA SH. BILIONI 5.5 ZA UJENZI WA MRADI WA SOKO LA KISASA LA MAGOMENI DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akisikiliza maelezo ya Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Justin Lukaza, kuhusu ramani ya Mradi wa Kimkakati wa Soko la Magomeni Jijini Dar es Salaam lenye ghorofa tatu ambalo limepewa kiasi cha Sh. bilioni 3.5, huku utekelezaji wa mradi huo ukiwa unasuasua.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akitoa maelekezo ya Serikali ya kuzuia Sh. bilioni 5.5 zilizosalia kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Kimkakati wa Soko la Magomeni Jijini Dar es Salaam kwa kuwa tangu fedha hizo zilipotolewa Mei, 2018 utekelezaji wake hauridhishi. Kulia ni Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Jastin Lukaza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto), akionesha kushangazwa na kitendo cha Mkandarasi wa Mradi wa Kimkakati wa Soko la Magomeni Jijini Dar es Salaam kutokuwepo eneo la mradi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Daniel Chongolo, wa pili kulia ni Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Jastin Lukaza na watatu kulia ni Mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi Bw. Sospeter Leonidas kutoka Kampuni ya GSI.
Mwenyekiti wa Soko la Magomeni Yusuph Waziri, akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Soko la Kisasa la Magomeni, Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam



Na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam


Serikali imezuia Sh. bilioni 5.5 ambazo zilipaswa kutumika kutekeleza mradi wa Kimkakati wa Soko la Magomeni, liliko wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam kutokana na kucheleweshwa kwa utekelezaji wa mradi huo licha ya kupewa fedha za kutosha kwa awamu ya kwanza.

Hatua hiyo imechukuliwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi huo unaotarajia kugharimu shilingi bilioni 9 na kukuta ujenzi wake unasuasua.

Dkt Kijaji alisema kuwa Serikali, imeipatia Manispaa ya Kinondoni shilingi bilioni 3.5 tangu mwezi Mei, 2018 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ambao ungepaswa ukamilike ndani ya miezi tisa tangu kusainiwa kwa mkataba wa ruzuku hiyo lakini ameshangaa kutomkuta mkandarasi kwenye eneo la ujenzi.

“Serikali inasitisha kutoa kiasi cha Sh. bilioni 5.5 mpaka watakapo dhihirisha wako tayari kuwahudumia wananchi na kutekeleza dhamira njema ya Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ya kuwahudumia wananchi wake”, alieleza Dkt. Kijaji.

“Jana Manispaa ya Ilala wametuangusha kwenye usimamizi wa mradi wa Machinjio ya kisasa ya Vingunguti tumerejesha shilingi bilioni 3 Hazina na leo Manispaa ya Kinondoni nao wametuangusha na tunalazimika kuzizuia fedha hizo sh. bilioni 5.5 mpaka tujiridhishe na maendeleo ya ujenzi” alisisitiza Dkt. Kijaji

Awali, akitoa maelezo ya mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi wa Manispaa hiyo Justin Lukaza, ameeleza kuwa Manispaa hiyo imeingia mkataba wa kujenga soko hilo litakalo kuwa na ghorofa tatu na Kampuni ya Group Six International na kwamba ujenzi ungekamilika katika kipindi cha miezi sita ijayo na kutofautiana maelezo na mwakilishi wa Mkandarasi ambaye alimweleza Dkt. Kijaji kuwa ujenzi huo ungechukua muda wa miezi 12.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Daniel Chongolo, amekiri kuwa kuna uzembe umefanywa na watendaji wa Manispaa ya Kinondoni uliosababisha mradi huo kuchelewa kuanza na kumwomba Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ampe muda mfupi wa kurekebisha kasoro hizo.

Alisema kuwa tayari kuna hatua mbalimbali zilichukuliwa kwa maafisa waliofanya uzembe katika utekelezaji wa mradi hapo awali na hakujua kama bado kulikuwa na uzembe uliokuwa unaendelea baada ya kuchukua hatua hizo kwa sababu aliamini watendaji waliokabidhiwa kusimamia ujenzi wa mradi huo walijifunza kutokana na makosa ya wenzao walioondolewa kusimamia mradi huo

“Mimi nakubaliana na wewe (Naibu Waziri wa Fedha) kwamba kuna uzembe na kazi yetu sisi ni kuhakikisha tunarekebisha haya makosa na nichukue dhamana na tutawajika na watu hawa na nitalazimika kutumia dhana ya punda mwenye mzigo na mwenye punda anaye mchapa bakora ili punda aende” alisisitiza Bw. Chongolo

Baadhi ya wakazi wa Kinondoni, wameipongeza Serikali kwa ufuatiliaji wa miradi ya wananchi na kusikiliza kero zao wakitolea mfano wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, na kwamba hatua hiyo inaleta uwajibikaji wa watendaji ambao walijenga mazoea ya kuzembea kwa makusudi kusimamia miradi ya wananchi na kuahidi kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuliletea Taifa maendeleo

Mradi wa Soko la Kisasa la Magomeni ni miongoni mwa miradi 22 iliyopewa ruzuku na Serikali katika Mpango wa Awamu ya Kwanza wa kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kujitegemea kimapato ambapo zaidi ya shilingi bilioni 147 zilitolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.
Viewing all 110087 articles
Browse latest View live




Latest Images