Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAKABIDHI ENEO LA MRADI WA UMEME WA MAJI MTO RUFIJI KWA MKANDARASI TAYARI KWA KAZI KUANZA

$
0
0


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
SERIKALI imekabidhi rasmi eneo la mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (RHPP), leo Februari 14, 2019 kwa mkandarasi Kampuni ya Arab Contractors kwa pamoja na ile ya Elsewedy  Electric zote kutoka nchini Misri.
 Hatua hiyo sasa inaashiria kuanza kwa kazi ya ujenzi wa mradi huo wa umeme ambao utazalisha Megawati 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye dridi ya Taifa na kuifanya Tanzania kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.
 Akizungumza  wakati wa kukabidhi mradi huo kwa mkandarasi katika hafla iliyofanyika ndani ya Pori la Akiba la Selous, Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, amesema kuwa hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli kwa kusimamia uamuzi wa ujenzi wa mradi huo mkubwa.
 Alisema mradi huo ulibuniwa kwa muda mrefu tangu mwaka 1970 ambapo kazi ya uchambuzi ilifanyika lakini haukutekelezwa kwa sababu ya gharama zake kuwa kibwa.
 "Wakati ule (1970), mahitaji ya umeme yalikuwa megawati 100. Lakini leo mahitaji ya umeme ni makubwa sana. Na ilipangwa kwa wakati ule kutekelezwa kwa awamu ambapo ungeanza na megawati 400, awamu ya pili 800 na baadaye megawati 900. Hatua tuliyofikia leo ndiko serikali ya awamu ya tano inataka ya Tanzania ya viwanda
 "Huu ni mradi wa manufaa miji yote iliyozunguka mradi huu itakuwa kwa kasi sambamba na uzalishaji wa umeme," alisema
 Waziri huyo wa Nishati, alisema kuwa mkandarasi Arab Contractors, atafanyakazi ya kujenga bwawa la umeme ikiwamo kingo za kuta pamoja na kujenga vituo  ya kuzalisha umeme.
 "Ninapenda mtekeleze mradi huu kwa wakati na kwa ufanisi ili kuondoa mashaka kwa watu ambao wenye shaka. Leo mnakabidhiwa eneo la kazi ni matumaini yetu itaifanyakazi hii kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na umeme.

"Na kuanzia leo (jana) wakandarasi msiondoke site nyumba zipo, miundombinu ipo iwe jua, mvua jengeni mradi wakati wote na msiondoke hapa," alisema

Alisema pia kitajengwa kituo cha kupoza na kukuza umeme cha kV 400  na njia za kusafirisha umeme kwa msongo wa kV 400 kutoka eneo la mradi hadi Chalinze kwenda Dodoma na Dar es Salaam na utakamilika mwaka 2022.
MANUFAA YA MRADI
 Dk. Kalemani, alitaja manufaa ya mradi huo ikiwamo kuifanya nchi kuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha utakaosaidia maendeleo ya uchumi wa viwanda na maendeleo endelevu ya wananchi.
 Mbali na hiyo pia nchi itakuwa na maji ya uhakika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao na ufugaji kwenye eneo lililo chini ya eneo la mradi wa maporomoko ya Mto Rufiji.
 "Kuboresha shughuli za utalii katika Pori la Akiba la Selous kwa kuwapo mazingira mazuri ya ustawi wa wanyama pori kutokana na uhakika wa maji wakati wote ya bwawa litakalotokana na ujenzi wa mradi.
 "Kuongeza mapato ya nchi kutokana na kustawi kwa shughuli za kitalii katika eneo la mradi. Kuvutia uwekezaji katika sekta ya viwanda na sekta mbalimbali za uchumi kutokana na kuwepo kwa umeme wa uhakika na wa bei nafuu hivyo kupunguza tatizo la ajira.
 "Kupunguza athari za mafuriko ya Mto Rufiji kwa wakazi waliopo maeneo ya Rufiji chini hadi delta ya Mto Rufiji na kuongeza pato la Taifa na lishe kutokana na mazao ya uvuvi," alisema Dk. Kalemani. 
MAKAMU WA RAIS ARAB
 Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya Arab Contractors,  Wael Hamdy, alisema umuhimu wa mradi huo si kwa Tanzania tu bali ni kwa Afrika kwa ujumla.
 Alisema kwa niaba ya Serikali ya Misri, watahakikisha wanatekeleza mradi huo kwa si mara ya kwanza kupingwa kwani hata walipoteleleza ujenzi wa Bwawa la Azuan, walipingwa na mataifa mengine lakini Tanzania kupitia Mwalimu Julius Nyerere, aliwaunga mkono Misri.
 "Hata kazi ya kupata zabuni ya mradi huu haikuwa kazi nyepesi lakini tunaamini kwa usimamizi wa Rais Dk. John Magufuli, tunaiona Tanzania ikiwa kwenye mwekeo sahihi. Na katika hili linadhirisha hata mwaka jana nilipofika hapa Tanzania na Rais Abdufatah Al-sis, ninaiona Tanzania leo ikiwa imepiga hatua kubwa hapa ni kazi tu," alisema Hamdy

WIZARA YA FEDHA
Akitoa salamu za Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Ashatu Kijaji, alisema kuwa wao kama wizara ambao ni wadau muhimu kwenye utekelezaji watatoa ushirikiano wa kila aina unaohitajika ili kazi ikamilike kwa wakati.

"Haya matunda ya Serikali ya awamu ya tano sote tunajua wapi tulipotoka, tulipo na tunapokwenda. Na tunajua sasa tupo kwenye utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa Awamu ya pili ambao hadi kufikia mwaka 2025 tunataka kuwa Tanzania inayotekegea uchumi wa kati na wa viwanda. Na utekelezaji wa mradi huu tunaambiwa hakuna viwanda bila umeme na mradi huu sasa unakwenda kulifanya Taifa kuwa na umeme mwingi na wa uhakika zaidi," alisema Dk. Kijaji

DK. MWINUKA
 Awali akitoa maelezo kuhusu mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk. Tito Mwinuka, alisema kuwa ujenzi huo utajumuisha bwawa kuu aina ya Rollar Compacted lenye uwezo wa kutunza maji takribani mita za ujazo bilioni 34, kituo cha kufua umeme zenye uwezo wa MW 2,115. 
"Aidha patajengwa majengo ya ofisi, karakana, makazi, stoo na huduma za jamii kwa ajili ya uendeshaji wa kituo," alisema
Alisema zabuni ya kumpata mkandarasi wa ujenzi ilipelekea kuipata Kampuni ya ubia ya Arab Contractors ambayo inaundwa na kampuni za Osman A. Osman & Co na Elsewedy Electric zote kutoka nchini Misri.
Mkurugenzi huyo Mtendaji alisema katika kutekeleza mradi huo kutakuwa na mtaalamu mshauri wa mradi kwa ajili ya kuangalia ubora wa utendaji kazi wa mkandarasi kwa kushirikiana na timu ya timu ya wazalendo kwa niaba ya mwenye mradi.
 Alisema baada ya kusainiwa kwa mradi huo kuna mambo ambayo mkandarasi alitakiwa kuyafanya na amekamilisha kwa mujibu wa masharti ya mkataba.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akibadilishana mawazo na naibu waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu, (wapili kulia) Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, (watatu kulia) na Mkurugenzi Mtedaji wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka muda mfupi baada ya hafla hiyo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (katikati) akisindikizwa na manaibu waziri na wakandarasi, akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi mradi wa ujenzi wa kuzalisha umeme wa bonde la Mto Rufiji leo Februari 14, 2019.
Mratibu wa Mradi wa umeme wa Rufiji Mhandisi Justus Mtolela (waliokaa kulia) na mwakilishi wa mkandarasi  Mhandisi Ahmed Ouda wakisaini mkataba wa makabidhiano ya eneo la mradi tayari kuanza kazi. Hafla hiyo iliyoshuhudiwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani manaibu waziri na viongozi mbalimbali wa serikali ilifanyika eneo la mradi wilayani Rufiji leo Februari 14, 2019.


Mratibu wa Mradi wa umeme wa Rufiji Mhandisi Justus Mtolela(kulia) na Mhandisi Ahmed Ouda, wakionyesha hati hizo baada ya ksuaini.
 Makamu wa Rais wa kampuni ya Elsewedy Electric ya Misri, Mhandisi Wael Hmdy, akitoa hotuba yake
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa hotuba yake kwa niaba ya Serikali.
Mbunge wa Rufiji Mhe.Mohammed Mchengerwa, akitoa hotuba.
 Dkt. Kalemani akisalimiana na Naibu waziri wake, Mhe. Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, na Naibu Waziri wa Maliasili Costantine Kanyasu, mara baada ya hafla hiyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akijadiliana jambo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo anayeshughulikia uwekezaji, Mhandisi Khalid James, mara baada ya hafla hiyo.

REMEMBERING OPP IN SWAHILI BY TANZANIAN SALEH JABIR

Muhimbili, MOI, JKCI na Mloganzila wakutana kuboresha huduma kwa wagonjwa

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kuhusu madaktari kuimarisha mawasiliano na wagonjwa ili kuwapa fursa ya kujua mwendendo wa matibabu yao.
Baadhi ya wakurugenzi wa Muhimbili na JKCI wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru leo kuhusu uboreshaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaotibwa katika taasisi hizo.
Baadhi ya wakurugenzi wa Muhimbili, MOI na Muhimbili-Mloganzila wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi akichangia mada kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea leo katika ukumbi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. 



Viongozi wa taasisi nne; Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila zimekutana leo kujadiliana jinsi ya kuboresha huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hizo.

Katika mkutano huo, wakurugenzi na wakuu wa idara wamekubaliana kuimarisha mawasiliano katika taasisi hizo ili kuhakikisha wagonjwa wanaendelea kuonwa na wataalam kwa wakati.

Akizungumza na viongozi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru ambaye amekuwa Mwenyekiti wa mkutano huo, amewaomba wakurugenzi wenzake kuendelea kuimarisha ushirikiano na kuandaa mikutano ya mara kwa mara baina ya taasisi hizo.

“Sisi kama wakurugenzi tuendelee kuwahimiza madaktari na watalaamu wengine kuimarisha mawasiliano yao na wagonjwa ili kuwapa fursa ya kujua mwendendo wa matibabu yao,” alisisitiza Prof. Museru.

Alisema uwepo wa mawasiliano mazuri baina ya watoa huduma na wananchi wanaohudumiwa utapunguza malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara kuhusu mwenendo wa matibabu kwa wagonjwa.

Pia, katika mkutano huo, taasisi hizo zimekubaliana kutumia miundombinu iliyopo kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa endapo taasisi moja itakua imeelemewa.

“Kwa mfano, MOI au Muhimbili inaweza kulaza wagonjwa wa ICU wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa muda kama ICU yao imejaa huku wakisubiri kupata nafasi ya kitanda katika taasisi hiyo ya Moyo,” amesema Mkurugenzi huyo.

Taasisi hizo zitakuwa zikikutana mara kwa mara ili kujadiliana changamoto mbalimbali zinazojitokeza, huku lengo kubwa likiwa ni kuboresha huduma za matibabu zinazotolewa MNH, MOI, JKCI na Muhimbili- Mloganzila.

WADAU WA MADINI KUANDAMANA MANYARA KUMPONGEZA JPM

$
0
0
WACHIMBAJI na wadau wa madini wa Mkoa wa Manyara, wanatarajia kuandamana kesho jumamosi kwa lengo la kumshukuru Rais John Magufuli kwa kukubali kusaini muswaada wa dharura wa marekebisho ya sheria za fedha, kupunguza na kufuta kodi zilizolalamikiwa. 

Maandamano hayo ya kilomita tatu yataanzia kwenye lango la Magufuli la kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite hadi kwenye uwanja wa Barafu wa CCM mji mdogo wa Mirerani. 

Kaimu Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara (Marema) Tawi la Mirerani, Shwaibu Mushi (Bahati) alisema maandalizi ya maandamano hayo yatakayopokelewa na mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti yanaendelea vizuri. 

Mushi alisema Maandamano hayo yatawahusisha wachimbaji wote wa madini wa mkoa wa Manyara, kutoka wilaya zote za Simanjiro, Kiteto, Babati, Hanang' na Mbulu. Alisema wanampongeza Rais Magufuli kwa kuwakubalia ombi hadi wabunge wakapitisha sheria hiyo baada ya mkutano wa kisekta wa wadau wa madini uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam. 

Alisema kauli mbiu ya maandamano hayo ni 'Rais wetu, madini yetu, uchumi wetu' ambapo wadau mbalimbali wa madini wakiwemo wachimbaji, wamiliki wa migodi na wazamiaji (WanaApolo) watashiriki. "Pia wadau wengine wanaonufaika na madini wakiwemo wafanyabiashara, madalali na wanunuzi wa madini mbalimbali watashiriki maandamano hayo ya kumpongeza Rais Magufuli," alisema Mushi. 

Alisema wanaandamana kumpongeza Rais Magufuli baada ya kupita siku 17 tangu mkutano wake na wadau wa madini kufanyika na kisha kupitishwa kuwa sheria na bunge. Alisema wao wenyewe kama wadau wa madini hawana cha kumpa Rais Magufuli hivyo wanatumia maandamano hayo kwa lengo la kumuunga mkono na kuonyesha kuwa wapo naye pamoja katika uongozi wake. 

"Maandamano hayo yanatarajia kuanzia saa mbili asubuhi na kumalizika saa nne asubuhi ambapo itasomwa risala ya kumpongeza Rais Magufuli kudhibiti utoroshwaji madini, ulipaji kodi na kumuunga mkono," alisema Mushi. Hata hivyo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara Agostino Senga alisema maandamano kama hayo huwa yanaruhusiwa kufanyika mradi wahusika wawe na kibali kutoka kwa mkuu wa polisi wa wilaya husika. 

Kamanda Senga alisema hivi karibuni yalifanyika maandamano kama hayo ya wafugaji na wakulima kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwatetea hivyo hata hayo ya wadau wa madini watayaruhusu wakiomba kibali. 
 Kaimu Mwenyekiti wa Marema Tawi la Mirerani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Shwaibu Mushi (Bahati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kesho jumamosi. 
 Wazamiaji wa migodi ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara (WanaApolo) wakipanga viroba vilivyotolewa mgodini, ambapo kesho jumamosi wanaandamana kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kuwajali na kuwatetea. 
Baadhi ya wanaApolo wa mgodi wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakisomoa viroba mgodini, huku wakijiandaa kwa ajili ya kuandamana kesho jumamosi ili kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kuwajali wachimbaji madini. 

JUMUIYA AFRIKA MASHARIKI YAFANYA SEMINA KUTENGENEZA MWONGOZO WA PAMOJA KUTATHIMINI MATUMIZI YA DAWA ZANZIBAR

$
0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 

Wananchi wametakiwa kuzitumia Dawa vizuri kwa kufuata kikamilifu miongozo wanayopatiwa na Wataalam wa Afya ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokea kupitia Dawa hizo.

Aidha wameombwa pale yatakapotokea madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kuripoti haraka kwa Wataalam wa Afya ili hatua za matibabu ziweze kuchukuliwa.

Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad ameyasema hayo alipokuwa akifungua Semina ya siku mbili ya kutengeneza Mwongozo wa pamoja wa kutathimini matumizi ya Dawa kwa nchi wanachama wa Afrika Mashariki katika Hoteli ya Marumaru mjini Zanzibar.

Amesema matumizi ya Dawa yanahitaji umakini mkubwa ili kuepuka madhara zaidi kwa wagonjwa wanaotumia Dawa.Amesema kutokana na hali hiyo Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika imeona ipo haja ya kuwa na mwongozo mmoja ambao utahakikisha Wananchi wanakuwa salama dhidi ya matumizi ya Dawa.

“Dawa si chakula, Dawa ni Sumu, ukiitumia vyema kwa kufuata miongozo yake itakutibu lakini kama utaitumia vibaya kinyume na inavyotakiwa basi itakuletea madhara” alitahadharisha Zahran.Amefahamisha kuwa watu wanaweza kupata matatizo mbali mbali pale wanapotumia Dawa bila kufuata mwongozo sahihi kama vile kupata muwasho na baadhi ya wakati hata kusababisha madhara ndani ya mwili hivyo umakini unahitajika.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Uwiano wa Dawa wa nchi za Afrika Mashariki Hidaya Juma, amesema kupitia Mradi huo wameweza kutengeneza miongozo tofauti ikiwemo ya usajili wa Dawa, kupima ubora wa dawa zenyewe na kuvifanyia ukaguzi Viwanda vya Dawa vya Afrika Mashariki.

Bi Hidaya ameongeza kuwa malengo ya Mkutano huo ni kuhakikisha Dawa zote zinazoingia nchi wanachama wa Afrika ya Mashariki ziwe katika kiwango kimoja cha ubora.Amesema mara baada ya kukalmilika Mradi huo wataweza kuweka hali ya Dawa kuwa na usalama Afrika Mashariki

Hivyo amesisitiza Wananchi pale wanapopata tatizo linalotokana na matumizi ya Dawa walizozitumia kuliripoti tatizo hilo kwa wahusika.Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa Semina hiyo Mohamed Omar Simba amesema Mwongozo huo baada ya kukamilika utawasaidia kuwapa uelewa mpana wa kujua namna ya kuzitumia vyema Dawa hizo kwa matumizi.

Amesema Wataalam wamegundua kwamba baadhi ya Wagonjwa wanaoletwa Hospitalini kwa matibabu magonjwa yao hutokana na matumizi mabaya ya dawa.Afisa mwandamizi wa Afya kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki Jane Mashingia amesema wamekuja kuchukua maoni ya Wadawau wanaofanya kazi za kutoa Dawa kutoka taasisi tofauti ikiwemo Wasambazaji wa Dawa, Watengenezaji wa Dawa na Mamlaka ya kudhibiti ubora wa Dawa Zanzibar ZFDA.

Ameongeza kuwa zoezi la kukusanya maoni ili kutengeneza mwongozo huo limeanza nchi tofauti kama vile Kenya, Uganda, Tanzania Bara ambapo kwa sasa wapo Zanzibar kabla ya kuhitimishwa katika nchi zilizobaki za Burudi, Rwanda na Sudan Kusini.

BREAKING: Airbus to scrap A380 superjumbo production

PPRA Yapongezwa Uanzishaji wa Mfumo wa Manunuzi wa Kielekroniki

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) jijini Dodoma.
 Mwakilishi wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Nimrod Mahozi wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) jijini Dodoma.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Mhandisi Leornard Kapongo akitoa neno la shukrani wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Usimamizi wa Manunuzi wa Umma (PPRA) jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu(wapili kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi  wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) jijini Dodoma.Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Nimrod Mahozi, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leornard Kapongo, Katibu wa Baraza la PPRA, Martine Sapanjo na Katibu Msaidizi wa Baraza hilo Bi. Maria Mng’ong’o.
 Baadhi ya Menejimenti na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la PPRA wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akionyesha  vitendea kazi vya Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) mara baada ya kuzindua rasmi baraza hilo jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Bodi ya Udhamini ya PPRA, Nimrod Mahozi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Mhandisi Leornard Kapongo, Katibu wa Baraza la PPRA, Martine Sapanjo na Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Bi.Maria  Mng’ong’o.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Mhandisi Leornard Kapongo akiwakabidhi vitendea kazi Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa PPRA, Martine Sapanjo na Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Bi.Maria  Mng’ong’o  wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Usimamizi wa Manunuzi wa Umma (PPRA) jijini Dodoma.
 Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Martine Sapanjo(wapili kushoto) na Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Bi.Maria  Mng’ong’o  wakionyesha dhana zao za kazi mara baada ya kukabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leornard Kapongo (katikati) wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) jijini Dodoma.Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu(wapili kulia) na Mwakilishi wa Bodi ya PPRA, Nimrod Mahozi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu(katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa PPRA wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) jijini Dodoma. (Picha na Frank Shija – MAELEZO)

MAOFISA WATANO WA JESHI LA POLISI NCHINI KENYA WAPATIKANA NA HATIA YA MAUAJI YA BABY PENDO

$
0
0
MAOFISA watano wa Jeshi la Polisi walioongoza operesheni ya 2017 ambapo mtoto kwa jina baby Pendo aliuawa katika Mji wa Nyalenda kaunti ya Kisumu wamepatikana na hatia ya kifo chake. Uchunguzi ulioongozwa na hakimu mwandamizi Beryl Omollo ulitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi mjini Kisumu.Makamanda hao ni Linah Kosgei, Benjamin Koima, Christopehr Mutune Maweu, Titus Yoma na John Thiringi.

Shirika la Habari la Uingereza limesema leo kuwa wakati wa operesheni hiyo iliokumbwa na utata Bwana Yoma alikuwa Kamanda wa polisi wa kaunti ya Kisumu, Bwana Maweu alikuwa OSPD wa Kisumu Mashariki, bwana Thiringi alikuwa OSC wa kisumu ya kati huku Koima akisimamia Kisumu magharibi huku naye bi Kosgei akiongoza kituo ha polisi cha Nyalenda. Mtoto huyo aliyekuwa na miezi sita aliuawa ndani ya nyumba ya babake na maafisa wa polisi wa kitengo cha kukabiliana na ghasia ambao walikuwa wakijaribu kuzima maandamno yalioanza kufuatia matokeo ya uchaguzi wa 2017.

Katika uamuzi wake , hakimu huyo pia alimuagiza Mkurugenzi wa mashtaka Noordin Haji kuwachunguza maofisa 31 wa kikosi cha GSU ambao aliwataja kuwa 'washukiwa muhimu'. Pia maofisa wengine 20 wa polisi ambao walikuwa chini ya usimamizi wa Kosgei mjini Nyalenda pia watachunguzwa mahakama hiyo iliamuru. Wakati huo huo wazazi wake Bwana Joseph Abanja na mkewe Lencer Achieng, walisema kuwa walikuwa wakiomba maajabu ya Valentines na ni hicho walichopata na wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo maofisa hao(Makamanda hao walilaumiana huku hakuna hata mmoja akitaka kuchukuwa lawama.

Imeelezwa kuwa Baby pendo alifariki Agosti 2017, baada ya kudaiwa kupigwa katika kichwa na maofisa wa polisi kutokana na ghasia zilizokumba kaunti ya Kisumu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais. Maofisa wa Polisi walishutumiwa kwa kuvunja na kuingia katika nyumba ya Bw. Abinja katika mtaa wa mabanda wa Nyalenda.Mtoto huyo alifairiki siku tatu baadaye wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan.CHANZO BBC.

IAAF YAKANA KUIAMBIA MAHAKAMA KUWA WANARIADHAA KAMA CASTER SEMENYA WATAZAMWE KAMA WANAUME

$
0
0
SHIRIKISHO la Riadhaa Duniani (IAAF) limekana kwamba litaiambia Mahakama kuwa wanariadha wote wanawake wenye viwango vikubwa vya homoni za kiume mwilini, yaani testosterone kama vile Caster Semenya wanapaswa kutambuliwa kama wanaume. Bingwa wa dunia na Olimpiki katika mbio za mita 800 anapinga sheria iliyopendekezwa na IAAF inayonuiwa kudhibiti viwango vya homoni hiyo kwa wanariadha wanawake. Kesi hiyo itasikilizwa katika mahakama ya malalamiko katika michezo (Cas) wiki ijayo.

Gazeti la the Times limeripoti kuwa mawakili wa IAAF watasema kuwa Semenya "kibayolojia ni mwanamume" pamoja na kwamba anatambuliwa kuwa mwanamke. Shirikisho hilo la riadha linasema "halitambui" mwanariadha yoyote mwenye "tofuati za kukuwa kijinsia" (DSD) ambapo raia wa Afrika kusini, Semenya ndiye anayeonekana zaidi kuwa mwanamume .

 "Kinyume na hicho, tunakubali jinsia zao kisheria pasi na shaka, na tunawaruhusu washiriki katika kitengo cha wanawake," lilisema siku ya Jumatano. "Hata hivyo, iwapo mwanariadha aliye na hali hiyo ya DSD, atakuwa na sehemu nyeti za kiume, na viwango vya kiume vya homoni hiyo ya testosterone, wanapata ongezeko la mifupa na uzito wa misuli na nguvu na huongeza damu mwilini ambayo mwanamume hupata wanapo baleghe, ndicho kinachowapatia wanaume nguvu zaidi ya wanawake katika mashindano.

"Kwahivyo, ili kuwa na ushindani wa sawa katika kitengo cha wanawake, ni muhimu kuwataka wanariadha walio na hali ya DSD kuzipunguza homoni kusalia kuwa kama za wanawake kabla hawajaruhusiwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa" IAAF ilinuia kuuidhinihsa sheria mpya Novemba 1, 2018 lakini ikaahirisha hadi Machi 26 kusubiri matokeo ya kesi aliowasilisha Semenya na Shirikisho la Riadha Afrika Kusini. 

 Kuahirishwa huko kunamaanisha kuwa wanariadha wenye hali hiyo ya DSD hawatoruhusiwa kushiriki katika mashindano kwa miezi 6 kutoka tarehe ambayo mabadiliko ya sheria yataidhinishwa ambayo, huenda ikamfanya Semenya akakosa kushiriki baadhi ya mashindano ya msimu wa nje 2019.

Hata hivyo wakati Semenya, alipotangaza kwamba atapambana na sheria hizo mwaka jana Afrika kusini alisema: "Si haki. Nataka nikimbie kama kawaida, namna nilivyozaliwa. Mimi ni Mokgadi Caster Semenya. Mimi ni mwanamke na nina kasi." Wakati huohuo Mtafiti Mkuu Mwenza katika Chuo Kikuu cha Yale na Mtaalamu Mkuu wa masuala ya homoni hiyo ya testosterone Katrina Karkazis ni miongoni mwa walioshutumu shirikisho hilo la riadha duniani kuhusu msimamo wake. 

 Amesema IAAF "inatafasiri vibaya sayansi ya bayolojia ya jinsia" na inatafuta "kuunda ufafanuzi wake binafsi wa jinsia kutokana na imani zenye makosa kuhusu bayolojia na jinsia," na kuongeza hilo halina msingi na linaweza kuwa na madhara zaidi kwa kuidhinihsa ukosefu wa uelewa na kuchangia unyanyasaji zaidi.

DJINNIT AHIMIZA WANAWAKE WAPEWE NAFASI ZA UONGOZI AFRIKA

$
0
0
NCHI zinazokabiliwa na misukosuko na mapigano katika ukanda wa Maziwa Makuu zahimizwa kutoa nafasi zaidi kwa wanawake katika nyadhifa za uongozi ili kuwashirikisha katika mchakato wa kuleta amani. Akizungumza leo Februari 14,2019 Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Maziwa Makuu Said Djinnit amezitaka nchi za ukanda huo zinazokabiliwa na misukosuko na mapigano ya mara kwa mara kutoa nafasi zaidi kwa wanawake katika nyadhifa za uongozi ili kuwashirikisha katika mchakato wa kuleta amani ya kudumu kwenye eneo hilo.

Kauli hiyo ameitoa jijini Nairobi, Kenya alipoongoza mkutano wa kimataifa kuhusu mchango wa wanawake katika suala la kutafuta amani na mapatano katika nchi za ukanda huo. Djinnit amesema uchaguzi wa hivi karibuni uliofanyika katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo unaashiria kuna uwezekano wa kufikia hali ya amani na mapatano katika eneo hilo. Djinnit ameendelea kusema: ''Tunataraji kwamba wakati huu ambapo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imeondokana na mchakato wa zoezi la uchaguzi basi tunatazamia kuwa wanawake watapewa nafasi katika nyadhifa za uongozi katika nchi hiyo''.

Amesema wanawake wana ushawishi mkubwa katika kushinikiza amani na mapatano ukizingatia kwamba akina mama na watoto ndio waathiriwa wakuu katika mataifa yanayokabiliwa na majanga au vita na migogoro ya kisiasa. Aliyekuwa Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza pia alikuwa miongoni mwa washiriki wa mkutano huo wa siku moja uliohudhuriwa pia na viongozi wanawake wa ngazi za juu kutoka nchi za Maziwa Makuu, wanadiplomasia pamoja na wawakilishi kutoka mashirika ya kijamii.

Wasemaji katika mkutano huo wamesisitiza umuhimu wa watu kuheshimu haki za binadamu. Wamekemea vikali vitendo vya dhulma dhidi ya wanawake katika nchi kama vile Sudan Kusini ambapo kumekuwa na ongezeko la visa vya ubakaji wa watoto na unyanyasaji wa kijinsia kwa ujumla. 

 Miongoni mwa nchi zilizowakilishwa kwenye mkutano huo ni pamoja na Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Pia wajumbe kutoka Umoja wa Afrika na wawakilishi kutoka shirika la maendeleo ya Ujerumani GIZ ni miongoni mwa mataifa mengine ya Ulaya.
CHANZO DW.

UTT AMIS YAWANOA WASTAAFU MKOANI MOROGORO

$
0
0
UTT AMIS ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Fedha ambayo inatoa huduma ya Uwekezaji kupitia mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja.

Kwa sasa inaendesha mifuko mitano ambayo ni Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Jikimu na Ukwasi.UTT AMIS hutoa elimu bure kwa makundi mbalimbali ili kuwawezesha kuwa na uelewa mpana juu ya masuala ya uwekezaji kwenye masoko ya fedha na mitaji.

Kwa sasa timu ya maafisa wa UTT AMIS walishiriki katika mafunzo ya wastaafu yaliyoandaliwa na Kampuni ya Taifa ya Tija ya (NIP) ili kuwajengea wastaafu watarajiwa uelewa mpana juu ya mpango wa uwekezaji kwenye mifuko inayoendeshwa na UTT.
Baadhi ya washiriki wa semina ya wastaafu iliyoandaliwa na Shirika la Tija la Taifa 'National Institute of Productivity' wakisikiliza mada juu ya uwekezaji wa pamoja pindi watakapostaafu.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga, akitoa mada katika semina iliyoandaliwa kwa ajili ya wastaafu mkoani Morogoro iliyoandaliwa na Shirika la Tija la Taifa 'National Institute of Productivity'. 
Ofisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS, Martha Mashiku, akisikiliza maswali kutoka kwa washiriki wa semina.


DKT. MWANJELWA AWAPA WIKI MOJA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA MKINGA

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wilayani Mkinga, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 
Baadhi ya watumishi wa umma wilayani Mkinga wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiteta jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said, kabla ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 
Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Baraka N. Nangosongo akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa watumishi wa umma wilayani Mkinga wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said kuhakikisha watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga wanaoishi nje ya vituo vya kazi kuhamia wilayani Mkinga ndani ya siku saba ili kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa wakati. 

Agizo hilo amelitoa wilayani Mkinga wakati wa kikao kazi na watumishi wa halmashauri hiyo, alipowatembelea kuhimiza uwajibikaji kabla ya kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo kwa lengo la kukagua na kujiridhisha kuhusu utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga wanaoishi nje ya vituo vya kazi na kutumia rasilimali za serikali, ni dhahiri kuwa wanatumia vibaya rasilimali za umma hivyo wanafanya kosa kwa mujibu wa Kanuni, Sheria na Taratibu za Utumishi wa Umma. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, ni marufuku kwa mtumishi wa umma yeyote nchini kuishi nje ya kituo cha kazi, kwani kitendo hicho kinawanyima haki ya msingi wananchi wanaohitaji huduma katika Taasisi za Umma kutokana na watumishi wengi kuchelewa kufika kazini kwasababu ya kuishi nje ya vituo vyao vya kazi. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amehoji uwepo wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga na wakuu wake wa Idara kushindwa kushughulikia tatizo hilo la watumishi kuishi nje ya vituo vya kazi, na kumtaka Mkurugenzi huyo kuhakikisha anashirikiana na menejimenti yake kushughulikia suala hilo kwa wakati na kuongeza kuwa, iwapo tatizo hilo litaendelea kuwepo wilayani humo, itakuwa ni ishara tosha kwamba, wamedhihirisha kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa umma wilayani humo kuzingatia nidhamu ya kazi na kutochezea fursa waliyonayo ya kuutumikia umma na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwa na utumishi wa umma wenye viwango na unaomjali mwananchi pindi anapofuata huduma katika taasisi za umma. 

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Tanga na Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kushughulikia ubadhirifu wa fedha uliopo katika Kituo cha Afya cha Kiwegu na kutaka apatiwe mrejesho mapema iwezekanavyo. 

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga na Maafisa Utumishi kuhakikisha ifikapo Februari 21 mwaka huu, watumishi wote wanaoishi nje ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga wawe wameshahamia wilayani Mkinga. 

Bi. Said amemshukuru Dkt. Mwanjelwa kwa kuwahimiza watumishi wilayani Mkinga kuvaa mavazi yenye staha na kumtaka kila mtumishi wa umma wilayani humo kuzingatia Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007. 

Kuhusiana na ubadhirifu wa fedha katika Kituo cha Afya cha Kiwegu, Bi. Said amemuahidi Dkt. Mwanjelwa kutekeleza maelekezo aliyoyatoa kwa wakati kwa kufanya ufuatiliaji ili kutatua tatizo hilo. 

Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Tanga yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi kwa umma, ikiwa ni pamoja na kukagua na kujiridhisha na utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na TASAF mkoani humo. Mpaka sasa ameshatembelea Halmashauri ya Mji wa Tanga, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga. 

ZAIDI YA BIL. 16.324.9 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI PWANI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, RUFIJI 


JUMLA ya kilo 5,623,277 za korosho zenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 16.324.9 tayari zimelipwa kwa wakulima mkoani Pwani. 

Aidha wakulima wa korosho 24,543 ,wenye kilo 14,370, 844 kati ya kilo 21,130,598 zilizopo kwenye maghala makuu wameshakikiwa, sawa na asilimia 68 . 

Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Ndikilo alitoa taarifa hiyo wakati alipokuwa akizungumza kwenye ziara yake wilaya ya Mkuranga na Rufiji.

Alisema, zoezi la uhakiki lilikuwa mwisho february 15 lakini mkoa huo unaomba kuongezewa muda hadi february 28 mwaka huu, kwakuwa umechelewa kuanza zoezi hilo na bei ya daraja la pili ilichelewa kutoka ambayo itakuwa sh. 2,640 kwa kilo .

Ndikilo alieleza, hadi tarehe 12 februari, mwaka huu jumla ya kilo 23,066,238 za korosho zimekusanywa, ambapo kilo 21,130,598, sawa na asilimia 91.6 zipo kwenye maghala makuu.

"Ghala kuu la Mwanambaya zipo kilo 6,549,204, Kibiti kilo 2,650,529, TANITA kilo 1,705,621, Kurasini PISAH kilo 3,727,669, Kurasini SCALABLE kilo 6,325,237 ,Kiegeani- Mafia kilo 213,593 na kilo 6,488,690 zipo kwenye maghala madogo ya AMCOS"alibainisha Ndikilo. 

Nae katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji, Shangwe Twamala alisema mkoa wa Pwani ulichelewa kuanza ukusanyaji wa korosho tarehe 30 Oktoba, 2018 tofauti na mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma, ambayo ilianza mapema.

"Baadhi ya korosho kuendelea kuwepo kwenye maghala ya AMCOS, Ili kutatua changamoto hii, tunashauri malipo kwa wasafirishaji yafanyike kwa wakati ili waweze kufanya kazi hii"

"Kama itawezeakana tutumie magari ya jeshi kuhamisha korosho kutoka kwenye AMCOS kwenda maghala ya Kurasini"alieleza Twamala. Kwa upande wao mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga alisema, tani zaidi ya 4,000 za korosho kati ya 6,000 walizokusanya zipo chini ya sakafu ambapo wamezitandikia maturubai lakini wanahofia unyevunyevu zisije kuharibika. 

Mkuu wa wilaya ya Rufiji Juma Njwayo alisema, wakulima wilayani hapo wamelipwa korosho sh. bilioni 3.7 ,kwa wakulima 2,665.#

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA PROFESA BIANG YOHONG IKULU ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mtaalam wa Dawa za Asili kutoka Nchini China Profesa Yuhong Biang, alipofika Ikulu Zanzibar kushoto Mtafiti wa Dawa Asili kutoka Kenya Ndg. Siambi Kikete na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Afya Zanzibar Dr. Mayassa .S.Ally, wakifuatilia mazungumzo hayo.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Wataalam wa Utafiti wa Dawa za Asili ukiongozwa na Profesa Yuhong Biang kutoka Nchini China,Mtafiti kutoka Kenya, Siambi Kikete na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya ya Afya Zanzibar. Dr. Mayassa.S.Ally. (Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akiongozana na mgeni wake Profesa Yuhong Biang, wakitoka katika ukumbi baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Profesa Yuhong Biang,Mtaalam wa Utafiti wa Dawa za Asili kutoka China.(Picha na Ikulu) 

PICHA MBALIMBALI ZA SOKO LA SAMAKI LA KIBIRIZI KATIKA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI

$
0
0
  Wafanyabiashara wa samaki katika soko la Kibirizi kwenye Manispaa ya Kigoma Ujiji, Amina Sadiki (kushoto) na Halima Ramadhani (kulia) wakipaa samaki sokoni hapo, Februari 15, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Wachuuzi wa dagaa katika soko la samaki la Kibirizi kwenye  Manispaa ya Kigoma Ujiji, Odes Aloys  (kulia) na Rashidi Haji (kushoto) wakianika dagaa sokoni hapo Februari 15, 2019. 
 Muuzaji wa mafuta ya mawese yanayotokana na michikichi, Mwajuma Khamis   akitamka bei za mafuta hayo aliyokuwa akiyauza  kati ya Shillings 1,000 hadi 10,000 katika soko la samaki la Kibirizi kwenye Manispaa ya Kigoma Ujiji, Februari 15, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


MABULA AKABIDHI HATI ZA ARDHI NA KUIPA TANO HALMASHAURI YA BUCHOSA

$
0
0
Na Munir Shemweta,  BUCHOSA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula  ametoa hati za ardhi kwa wananchi kumi na tisa wa halmashauri ya Buchosa wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza na kuifagilia halmashauri hiyo kwa  kuwa na mfumo mzuri wa kutunza kumbukumbu za majalada ya ardhi.

Dkt Mabula alitoa pongezi hizo leo tarehe 15 Februari 2019 alipozungumza na wananchi wa Buchosa wakati wa kukabidhi hati za ardhi  akiwa katika ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli yaserikali kupitia kodi ya ardhi.

Alisema,kwa mara ya kwanza katika ziara zake kwenye halmashauri mbalimbali  ameikuta halmashauri ya Buchosa ikiwa inatunza kumbukumbu za majalada ya ardhi kwa mujibu wa sheria sambamba kuwepo mawasiliano kati ya afisa mmoja kwenda kwa mwingine wakati wa kushughulikia majalada na kuongeza kuwa migogoro mingi ya ardhi inayojitokeza inasababishwa na utunzaji mbaya wa majalada ya ardhi.

"Taratibu za utunzaji majalada ya ardhi pamoja na mawasiliano baina ya ofisa mmoja na mwingine zimekaa vizuri ni tofauti kabisa na niliyoyaona katika halmashauri nyingine,  Buchosa mko vizuri" alisema Dkt Mabula.

Alizungumzia utoaji hati kwa wananchi wa Buchosa,  Dkt Mabula aliwapongeza wananchi hao kwa kupatiwa hati na kueleza kuwa wananchi hao wanaelewa kuwa ardhi ni mali na hati walizokabidhiwa zitawawezesha kukuwa kiuchumi.

Alisema, mambo makubwa yanayofanyika nchini kama ununuzi wa ndege,  mradi wa treni ya mwendokasi, mradi wa kufufua umeme wa  Stiglers George ni jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuwahudumia wananchi na hayo yote yatafanikiwa kwa wananchi kutekeleza jukumu la kulipa kodi ikiwemo ile ya ardhi.

Aliongeza kwa kusema  wananchi 19 waliopewa hati watafungua milango kwa wananchi wa Buchosa na wengine kuchangamkia kupata hati ambapo pengine walikuwa hawajui kama hati inaweza kupatikana Buchosa na kuongeza kuwa wale wananchi walio katika urasimishaji  nao wachangamkie kupata hati. 

Hata hivyo, Dkt Mabula pamoja na kuipongeza halmahauri ya Buchosa lakini ameilaumu kwa kushindwa kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji na kuiagiza halmashauri hiyo kuanza kupanga na kupima pamoja na kuanisha maeneo ya huduma.

 Awali,Afisa Ardhi Mteule Halmashauri ya Buchosa Rafael Kilumanga alisema halmashauri hiyo imepima jumla ya viwanja 886 katika maeneo tofauti ya halmashauri hiyo na viwanja 31 kati ya vilivyopimwa 31 vimemishamilikishwa kwa wananchi  na kutolewa hati.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akimpatia hati ya kumiliki ardhi mkazi wa Buchosa mkoani Mwanza Esta Bukombe wakati wa ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia kodi ya ardhi. (picha na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akikagua mafaili katika  masijala ya ardhi ya Halmashauri ya Buchosa, kushoto ni Afisa Ardhi Mteule Rafael Kilumanga. (picha na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi)

WANANCHI WAPIGA KURA ZA SIRI KUBAINI WATUHUMIWA WA MAUAJI YA WATOTO BUSEGA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Wananchi wa Kata ya Lamadi Wilayani Busega mkoani Simiyu wamepiga kura za siri kwa lengo la kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo. Wakizungumza katika zoezi hilo lililofanyika Februari 14, 2019  katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi wananchi hao wamesema kuwa  wamelipokea vizuri zoezi hilo na kubainisha kuwa kura hizo zitasaidia Vyombo vya Dola katika kufanya uchunguzi na kuwabaini wauaji wa watoto wilayani humo.

“Zoezi hili nimelipokea vizuri na nina imani litatusaidia kuwapata wauaji wa watoto wetu na naishukuru Serikali kuona haja ya kuwashirikisha wananchi maana mauaji haya ya watoto yametusikitisha sana wakazi wa Lamadi” alisema Modesta Andrea mkazi wa Lamadi

“ Tukio hili la kupiga kura za siri mimi naona ni zuri kwa sababu naamini kuna baadhi ya wananchi wanaweza wakawa wanafahamu watu waliofanya mauaji ya watoto na kama ikitokea kuna watu wakaandikwa labda kwa sababu ya fitina tunaamini vyombo vyetu vya dola vitachuja na kuchunguza na mwishowe wauaji watabainika tu; tunaomba wakibainika sheria ifuate mkondo wake” alisema Elisha Daniel mkazi wa Lamadi.

Akizungumza na wananchi wa Lamadi mara baada ya zoezi hilo kukamilika, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema kufanyika kwa zoezi hilo hatua ya kwanza ya uchunguzi wa mauaji ya watoto wilayani humo, huku akiwahakikishia wananchi kuwa kura walizopiga zitahesabiwa kwa haki na vyombo vya dola mkoani humo.

“Kupiga kura za siri si kwamba tumeshindwa kufanya upelelezi, hii ni hatua ya kwanza ya sisi kufanya uchunguzi wetu, kura hizi zitahesabiwa na vyombo vya dola mkoani Simiyu ambavyo ni Usalama wa Taifa, Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Jeshi la Wananchi JWTZ (Mkoa wa Simiyu), Jeshi la Zimamoto, Jeshi la Polisi na TAKUKURU” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema Serikali mkoani humo itaendelea kutimiza wajibu wake wa kwanza wa kulinda watu wake na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani ili waweze kufanya vema shughuli za maendeleo.Sambamba na hilo Mtaka amesema Serikali itahakikisha inayafanyia kazi masuala mbalimbali yaliyosemwa na wananchi katika mkutano huo, ikiwa ni pamoja na malalamiko dhidi ya utendaji wa baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali  na kubainisha kuwa  hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaobainika kwenda kinyume katika kuwatumikia wananchi.

“Niwahakikishie kuwa Serikali itayafanyia kazi yote yaliyosemwa na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika hapa Lamadi, kama kuna wakubadilishwa watabadilishwa, wa kuwajibishwa watawajibishwa, wakuhamishwa watahamishwa naomba mniamini” alisisitiza Mtaka. Kwa upande wake Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni ametoa pole kwa wazazi wote waliopoteza watoto wao katika mauaji ya watoto na kuahidi kutoa rambirambi shilingi 500,000/= kwa kila familia iliyokutwa na msiba huku akilaani vikali vitendo vya mauaji ya kinyama ambayo yamekatisha ndoto za watoto hao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera amewashukuru wananchi wa Lamadi kwa  namna walivyojitokeza katika zoezi la kupiga kura za siri na kwa namna walivyolifanya kwa amani na utulivu.
Modesta Andrea kutoka kijiji cha Itongo Kata ya Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu akipiga  kura ya siri katika zoezi maalum la kupiga kura za siri lililowahusisha  wananchi wa Lamadi  lililofanyika katika Kitongoji cha Kisesa Februari 14, 2019  kwa ajili ya kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo.
 Baadhi ya wananchi wa Lamadi wakiweka karatasi zao za kura za siri zilizopigwa katika zoezi maalum la wananchi wa Lamadi  kupiga kura za siri lililofanyika katika Kitongoji cha Kisesa,   kwa ajili ya kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Lamadi wilayani Busega mara baada ya kukamilika kwa zoaezi la wananchi kupiga kura za siri kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo, ambalo limefanyika katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi Februari 14, 2019.
 Baadhi ya wananchi wa Lamadi wilayani Busega wakiendelea kupiga kura za siri na wengine wakisubiri kauli ya Serikali mara baada ya kupiga kura hizo zilizokuwa na lengo la kubaini watuhumiwa wa maujai ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani Busega, zoezi la kupiga kura limefanyika katika Kitongoji cha Kijiji cha Lamadi Februari 14, 2019.
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani na Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni wakiteta jambo katika mkutano maalum ambao wananchi wa Lamadi wilayani Busega, wamepiga kura za siri kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni, zoezi ambalo limefanyika katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi Februari 14,2019.

Mshindi wa Milioni 188.5 za M-BET kuichangia Yanga

$
0
0
Mkazi wa Njombe, Frank Kayombo (24) ameshinda Sh.188,484,550 kwa kubashiri kiusahihi Mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet. Kayombo ambaye  shabiki wa timu za Yanga na Manchester United ya Uingereza  amekuwa mshindi wa kwanza wa droo ya M-BET kwa mwaka huu, Meneja Masoko wa Kampuni ya M-BET Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa  M-Bet inaendelea kuwa nyumba ya mabingwa kwa kubadilisha maisha mbalimbali ya watanzania.

Mushi alisema kuwa serikali imejipatia Sh38 millioni ikiwa ni kodi ya ushindi asilimia 20 na  kuchangia pato la taifa. Alisema kuwa droo yao ya Perfect 12 inazidi kutoa washindi na kuchangia maisha kwa Watanzania ambao wamekuwa wakijishindia mamilioni ya fedha kila wakati.

“Huu ni mwanzo wa mwaka na tayari M-BET imetoa mshindi wa mamilioni ya fedha ambaye ataweza kujiendeleza kimaisha  na vile vile kuchangia taifa lake. M-Bet tunajivunia kuwa kampuni pekee ambayo mpaka sasa imewafaidisha watu wengi kupitia michezo yake, naomba Watanzania kuendelea kubashiri na kampuni michezo yetu kwa njia ya mitandao, simu ya mkononi na mengineyo,” alisema Mushi.

Kwa upande wake, Kayombo alisema kuwa alitumia Sh 1,000 na kubahatika kushinda droo hiyo ya kwanza ambapo atatumia fedha hizo kwa ajili ya kujiendeleza, kufungua miradi na vile vile kununua nyumba. Kayombo ambaye ni mfanyabiashara ya miamala ya fedha kwa njia ya simu, alisema kuwa ndoto yake kubwa ni kupata maendeleo makubwa katika biashara zake na kuweza kuisaidia familia yake.

“Nina furaha sana kupata kiasi hiki cha fedha ambacho kwa kweli ni kikubwa ukilinganisha na kiasi nilichotumia kubashiri, Naona mwanga wa maisha yangu na familia kwa ujumla. Naishukuru M-BET kwa kuonyesha uaminifu kwangu na kwa washindi wengine,” alisema Kayombo.

Mshindi huyo pia alisema atatumia kiasi cha fedha alizoshinda kuichangia timu yake ya Yanga kupitia namba maalum iliyotangazwa kwenye vyombo vya habari. “Naipenda Yanga na kiasi ambacho nitawapa timu yangu kinabakia kuwa siri,” alisema. Kaimu Msimamizi wa Kitengo cha Michezo ya Kubahatisha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Philipo Haule aliipongeza M-BET kwa kuendelea kuchangia pato la Taifa.
Mshindi wa droo ya kwanza  ya mwaka huu ya Perfect 12 ya kampuni ya M-BET Frank Kayombo (wa pili kushoto) kutoka mkoa wa Njombe  akipokea mfano wa hundi ya Sh milioni 188.5 kutoka kwa meneja Masoko wa M-BET, Allen Mushi (wa pili kulia). Wengine katika picha ni Afisa wa Michezo ya Bodi ya Kubahatisha Catherine Lamwai (wa kwanza kulia) na Philipo Haule afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

MBUNGE WA USHETU AKERWA NA VITENDO VYA UHALIFU JIMBONI KWAKE

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amekemea vitendo vya kiuhalifu vinavyoendelea katika Halmashauri ya Ushetu ambavyo vimepelekea kusababisha majeruhi na vifo Halmashaurini hapo.

Amezungumza hayo katika kata ya Mpunze iliyopo katika Halmashauri hiyo ambapo kabla ya kuzungumza nao Mbunge huyo alipita katika kituo cha afya cha Ukune kwa ajili ya kuitizama na kuipa pole familia moja iliyoivamiwa usiku na kikundi cha watu kisichojulikana ambacho kiliwashambulia familia hiyo kwa kukatwa mapanga na kuwaibia fedha.

Mbunge Kwandikikwa, ameonesha kusikitishwa na matukio yanayoendelea katika kata hizo na kuwaahidi  wananchi wake kulisimamia suala hilo kikamilifu.

"Hatuwezi kukubali hali hii kwasababu wananchi wanaogopa kufanya biashara na wengine wanaogopa kuzalisha hivyo suala la ulinzi lipo mikononi mwetu wenyewe ni lazima jambo hili tuliondoe", amesisitiza Mbunge Kwandikwa.

Ameongeza kuwa atafanya juhudi za kuweka Kituo cha Polisi maeneo jirani ili kuweza kuongeza hali ya usalama kwa wananchi na iwe rahisi kwao kuripoti kituoni hapo matukio yote ya kiuhalifu pindi yanapotokea.

Aidha, Mheshimiwa Kwandikwa, amewataka wananchi kutoa taarifa kwake na kwa vyombo vya usalama kwa yeyote wanayemdhani anajihusisha na vitendo vya kijambazi katika maeneo yao ya wanamoishi.

"Hatutovumilia hali hii naomba viongozi wanaouhusika na ulinzi mjipange kisawasawa kwani hata mimi saa hii niko tayari kazini", amefafanua Mbunge huyo.

Katika hatua nyingine, Mbunge huyo amewaeleza wananchi wake baadhi ya miradi inayoendelea kufanyika katika kata hiyo na kata zingine za Halmashauri ya Ushetu na kusisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu na kujitoa katika shughuli za kimaendeleo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Sabasabini, Bw. Emmanuel Makashi, amemshukuru Mbunge huyo kwa kulisimiamia suala la usalama katika kata za jimbo lake kwani limekuwa kero ambapo naye ni miongoni mwa waathirika wa kuvamiwa.

Mbunge huyo yupo mkoani Shinyanga kukagua hatua zilizofikiwa katika miradi inayoendelea kutekelezwa kama vile ujenzi wa hospitali ya wilaya, jengo la halmshauri, na barabara zinazoendelea kujengwa kwa kiwango cha changarawe ya Nyamilangano-Butibu yenye urefu wa kilomita 12.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mpunze kuhusu kutoa ushirikiano wa namna ya kutokomeza matukio ya kiuhalifu yanayoendelea katika kata za jimbo hilo, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga. 
Mbunge wa Jimbo la Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akisalimia baadhi ya wagonjwa  waliofika katika Kituo cha Afya cha Ukune, wilayani Kahama, ambapo alienda kuwajulia hali wananchi waliovamiwa na majambazi na kukatwa mapanga na kuibiwa fedha, mkoani Shinyanga. 
Mbunge wa Jimbo la Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akimtwisha maji Bi. Monica Joseph, yaliyotokana na ujenzi wa kisima kikubwa katika kijiji cha Kayenze, kata ya Ukune, wilayani Kahama.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu, Dkt. Atanasi Lucas, akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya kwa Mbunge wa Jimbo la Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, wakati alipokagua hatua za maendeleo ya mradi huo, mkoani Shinyanga. Ujenzi wa Hosptali hiyo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu na utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.5.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akisalimiana na mafundi wanaojenga jengo la ofisi za Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama.
Kazi za ujenzi zikiendelea katika jengo la ofisi la Halmashauri ya Ushetu, linalojengwa na mkandarasi wa Shirika la Mzinga kwa gharama ya shilingi zaidi ya  bilioni nne.
Muonekano wa majengo ya chumba cha kinamama wa wajawazito (Matenity), chumba cha upasuaji na mochwari lililokamilika kujengwa katika kijiji cha Ukune, wilayani Kahama. Ujenzi wa majengo hayo pia umehusisha maabara na nyumba ya mganga mkuu kwa gharama ya shilingi milioni 400.

Makamu wa rais akabidhi Tuzo ya Kiswahili ya Mabati

$
0
0
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia akiwasili wakati wa hafla ya utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Mabati –Cornell ya Fasihi ya Afrika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia akihutubia wakati wa hafla ya utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Mabati –Cornell ya Fasihi ya Afrika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia akimkabidhi cheti cha ushindi wa tuzo ya Fasihi Bw. Jacob Ngumbau Julius wakati wa hafla ya utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Mabati –Cornell ya Fasihi ya Afrika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia akimkabidhi   tuzo ya ushindi katika Fasihi Bi. Zainab Alwi Baharoon wakati wa hafla ya utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Mabati –Cornell ya Fasihi ya Afrika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images