Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 273 | 274 | (Page 275) | 276 | 277 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Paul Okoye wa kwanza kulia, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu tamasha watakalolifanya kesho Jumamosi. Novemba 23 katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P Square, wakiwa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa ambao ni wadhamini wa wasanii hao pamoja na Lady Jay Dee mmoja wa wasanii watakaowasindikiza jukwaani wasanii hao.
    Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akipeana mkono na wasanii, Peter na Paul Okoye, maarufu kama P Square wakati walipowasili kwenda kutoa msaada katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa usonji “Autism” (utindio wa ubongo) cha Msimbazi Mseto, jijini Dar es Salaam.
   .Msanii Peter Okoye akimuweka vizuri katika bembea  mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu wa usonji katika shule ya Msimbazi Mseto jijini Dar es Salaam. Wa kwa nza kutoka kushoto ni mwalimu Mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi  na Mjumbe wa bodi ya shule hiyo Mtumwa Nindi, na wa kwanza kulia ni mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Precious Hughes ambao ni wadhamini waliofanikisha wasanii hao kutua nchini.
   Wasanii wa kundi la P Square (Peter na Paul Okoye) katikati wakimsikiliza Mtoto mwenye ulemavu wa Usonji,  Erick wa shule ya msimbazi Mseto walipokwenda kushiriki kutoa msaada kwa kituo cha watoto hao. Wa kwanza kushoto ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi na kulia ni Mkuu  wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.
   Wasanii wa kundi la P Square wakikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu wa usonji  wa kituo cha Msimbazi Mseto cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akishuhudia makabidhiano hayo, na katikati ni walimu wa shule hiyo wakipokea kwa pamoja misaada hiyo.
  Wasanii Peter na Paul Okoye Maarufu kama P square wakiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma za jamii Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule wakicheza pamoja na watoto wenye ulemavu wa usonji  wa shule ya msingi ya Msimbazi mseto, wakati waliposhiriki kutoa msaada katika shule hicho kwa watoto hao wenye mahitaji maalum.

  ·        Waviomba kuwapa ushirikiano wasanii wa muziki nchini
  ·        kufanya onesho kwa masaa mawili mfululizo
  ·        Washiriki katika shughuli za kijamii
  Baada ya kuwasili nchini usiku wa jana wanamuziki mapacha Peter na Paul Okoye maarufu kama “P – Square” wametoa wito kwa  vyombo vya habari nchini kuwasaidia wasanii wandani na kuwa chachu ya mafanikio ya muziki kama vilivyo vyombo vya nchi nyingine, huku wakiahidi kufanya makubwa katika Shoo yao ya siku ya leo kwa mashabiki wao watakaojitokeza katika Viwanja vya Leaders Club.
  Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hotel ya Hyatt jijini Dar wasanii hao wamesema wamefurahishwa na mapokezi waliyoyapata kutoka kwa jamii ya Watanzania na waandaaji wa Tamasha hilo na kuahidi burudani ya kipekee kwa Watanzania.
  Peter Okoye ambaye ni mdogo wake na Paul alisema, vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuwajenga wasanii huku akitoa wito kwa vyombo hivyo kuwa kichocheo cha kuwajenga wasanii na sio kuwabomoa.
  “Vyombo vya nchini kwetu vimetufikisha hapa tulipo wamejitahidi kutujenga na kutusaidia kusikika Afrika nzima., Tutaona fahari kama vyombo vya hapa nchini pia vitajenga uwezo wa kuwasaidia wasanii wa ndani nao waweze kufika au hata kuzidi hapa tulipo, Tutafurahi siku tukiwaona wasanii kama kina Jay dee na Ben Pol wakija Nigeria kama sisi tulivyokuja nchini kwao, alisema Paul.
  Paul Okoye ambaye ni kaka kwa Peter  amesema “Tumefurahishwa sana na mapokezi tuliyoyapata tangu jana usiku hadi kufikia sasa, tumejisikia faraja kuwa katika nchi hii ya Tanzania watu wake ni wakarimu sana sifa hizi tumezisikia kwa watu mbalimbali na tumeshuhudia wenyewe tunawaahidi Mashabiki wetu kufanya Shoo ya uhakika., alisema Paul Okoye.
  Kwa upande wa wadhamini wakuu wa Tamasha hilo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa,alisema wamejisikia faraja kwa pamoja kufanikiwa kuwaleta wasanii hao ili watoe burudani kwa Watanzania na kuweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kutoa msada wa vyakula katika shule ya Msingi Msimbazi Mseto kwa kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom” Vodacom Foundation”.
   “Kwa upande wetu sisi kama waandaaji kila kitu kimekamilika kuanzia, masuala ya usalama na jukwaa vyote vimekamilika, Pamoja na mambo mengine tunatoa wito kwa Watanzania kuwai kufika maana onyesho litaanza saa 1 na kuwa sihii kuwa wastaarabu wakati wote wa Shoo hiyo na kujiepusha na vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
  Wasanii kutoka Bongo watakao toa burudani katika Tamasha hilo ni pamoja na wakongwe, Prof. Jay, Lady Jaydee, Jo Makini”mwamba wa kaskazini”pamoja na Ben Pol.

  Wakati huo huo wasanii hao na kitengo cha huduma za jamii cha Vodacom Foundation wameshiriki katika kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa  watoto wenye ulemavu wa akili cha Msimbazi Mseto kilichopo jijini Dar es Salaam. Huku wakitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuwasaidia watu wote wasio na uwezo ili kujenga jamii yenye maisha sawa kwa wote.


  0 0


  Picha ya pili, Abeid Semira wa kutoka Mwanza anapokea zawadi yake kutoka kwa Bi, Hytham Ahmed wa Masoko Ltd. kupitia promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Colgate Palmolive.  
  Valarie Urio wa Dar es Salaam, anapokea jiko la Gesi cooker kutoka kwa Bi, Hytham Ahmed wa masoko Ltd kupitia promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Colgate Palmolive. 
  =======   =======  =======
  Wakazi wa jijini Dar es salaam na mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya waliokuwa wakinunua bidhaa za  Sta- Soft  na Axion (sabuni ya kuoshea vyombo) zinazosambazwa na Colgate Pamolive wamekabidhiwa zawadi zao kupitia promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Colgate Palmolive.

  Kampuni ya Colgate Pamolive imekuwa ikiendesha promosheni  maalum ya CLEAN HOUSE kwa muda wa miezi miwili iliyokuwa na lengo la kuwafahamisha watanzania jinsi bidhaa zao za Sta- soft ambazo ni maalum kwa kufulia nguo na Axion maalum kwa usafi wa vyombo vya nyumbani. Bidhaa hizi ni maalum  kwa kufanya usafi kwa ufanisi mkubwa.

  Akieezea bidhaa hizo Afisa Masoko wa Colgate Pamolive  Bw, Meshack Mdingi alisema “ Lengo la promosheni  hii ni kuwajulisha wateja wetu jinsi wanavyoweza kuepuka magonjwa ya ngozi kwa kufua nguo zao na Sta- soft inayotunza nguo zako na kuziweka laini  wakati wote na harufu nzuri na  kusafisha vyombo vya ndani.  Wateja wetu tunawashauri watumie  bidhaa yetu ya Axion inayofanya vyombo vibaki na mng’ao wake mzuri siku zote”

  Walioibuka washindi kwenye promosheni ya Clean House ni wale wote walionunua bidhaa hizi kati ya September na Oktoba ambapo walichaguliwa kupitia droo maalum iliyofanyika wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar Es Salaam.

  Baadhi ya walioibuka washindi  kupitia promosheni hiyo ni  Valeria Urio mkazi wa Dar Es Salaam, aliyejishindia Jiko la Gas cooker,  Abeid Semira mkaazi wa Mwanza aliyejishidia Jagi la Kuchemsha maji, Hassan Ibraim mkaazi wa Tanga kati ya wengine 50.

  Bw, Mdingi alisema hadi kufikia mwisho wa promosheni  wameweza kuwaelimisha watu wengi kuhusiana na Usafi wa jamii, pia kurudisha faida wanazopata kwa jamii kwa kutoa zawadi ambapo jumla ya Majiko ya Gesi 3,Seti za Masufuria 8,  Seti za jagi za maji 8, pamoja na  mashine za umeme za kukausha mkate (Toaster) 8 za  kisasa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na zawadi nyengine ndogo ndogo.

  Kupitia bidhaa zetu bado tutaendelea kuwafikia wateja wengi kwa kufanya promosheni kama hizi huku tukitoa elimu kuhusiana na usafi kwa jamii na kutoa zawadi tofauti tofauti ili kuwafaidisha wale wote wanatumia bidhaa zetu za Colgate Pamolive, alimazia Bw, Mdingi

  0 0

  Urais Tanzania 2015.jpg The next Tanzania's General Elections are almost two years away. To be exact, Tanzanians [registered voters of course] will be on hopeful long ques in October 2015 to elect the next President of The United Republic and Members Of Parliament.In a country where almost everything is attached to politics, that is an important month and year. 
   While two years seems to be such a long stretch, in politics days are counted differently. 365 days could as well mean 65. 
  They say politics is a sneaky game. You need to be prepared, you need to know yourself and your potential opponents way ahead. That, of course, makes politics take the title of a dirty game as well. Before you realize, the streets knows you as Mr. Inappropriate. 
  Your lights are punched out and all you can see is darkness. You are no longer in control. The scene of dirty games and dirty wars I am trying to explain above is already on. If you are not aware please raise your hands up and better be in a don't shoot pose because I know you are not telling me the truth. 
  I believe you have heard how some politicians are already exchanging words[ in a war-like styles] whenever they get a chance or whenever they see cameras flashing and microphones are set. They aren't telling jokes. They mean it. Holly! They love the attention. 
   Now,we live in a different era. Nowadays, you can easily tell what is in someone's mind just from their status posted on their pages over social network platforms. You can see excitement, anger, frustrations, jealousy, hopelessness, craziness from those lines. You just gotta master the art of reading between the lines. 
  Few people and certainly few politicians are going to survive against the power of social networks. You gotta be a social lion to survive or completely avoid to expose your true feelings and arguably your "agenda". 
  The ugly part is; if you are a politician and you are not on social networks, your chances are cut in half or unless if the office you are aiming is just Mjumbe wa Nyumba Kumi Kumi. In that case, all you need is ability to walk and drink evening tea with watu wako wa kitaa. 
   Given some of the factors I am talking about above [political jabs, war of words, social networks expose etc] it has become a bit easier [ I said a bit easier because please never underestimate a Politician] to do some guess work on our politicians' [they want to be called Waheshimiwa] next move or the office and position they are aiming for. 
  I could be wrong and I could be damn right! Long story short, the men and women[ sorry a woman] whose photos appear above, are mentioned [and some have openly mentioned themselves] to be potential Presidential Candidates for Tanzania's next General Elections come October 2015. And honestly speaking, given their credentials and experiences [good and bad] and the nature of our politics or political system, anyone can the next man/woman who keeps you in "foleni" for hours because he/she is going "out".[You know] 
   The list above is not final. It can change anytime. Politicians are known to attract scandals too. So we may wake up the day after tomorrow and hear some rape charges or sale of national treasure and boom,some dreams are shattered. 
  Who do you think we missed in the list?[that's why we left rooms] And most important question; Who would you vote for if elections were held today? 
  Your opinion matters.Speak! 
   Jeff Msangi is a Writer/Blogger and Owner of www.bongocelebrity.com. You can reach him at bongocelebrity@gmail.com

  0 0

  Picture: Jerry Isaac Mruma
  The late Jerry Isaac Mruma

  From Mrs. Ritah Asunda, 
  Deputy Vice Chancellor 
  Student Affairs & Enrollment Management
  United States International University
  Nairobi, Kenya

  "Dear USIU Community,
  It is with deep sorrow that we regret to announce the death of Jerry Isaac Mruma, who until his death was an MBA major, the SAC Representative for Graduate students and a member of various committees in the university. 
  Jerry's body was found yesterday after a frantic search undertaken by the USIU Acting Head of Security, the Police and other members of the USIU Community.

  The search began soon after he was reported missing to the Dean of Students. His death comes even before we as a community have come to terms with the death of Brian Frisby who passed on in a fatal car accident. The deaths of the two students come as a big blow to the USIU community and we pass our sincere condolences to their families and friends.

  May God rest their souls in eternal peace."

  -------------------------------------------
  BELOW IS THE MESSAGE SENT EARLIER 

  Jerry Isaac Mruma is a Tanzanian USIU-Africa Student (in Nairobi, Kenya) who went missing on Saturday night. (You may click here to watch him in this video)
  Jerry had left the Tanzania Night at Pan Afrique Hotel and spoke to his friend Ogwellah at around 11:40PM

  Another friend tells that Jerry had called her to inform her that he was on his way home. Unfortunately, he never got there. She has not heard nor seen Jerry since Saturday and calls to his phone aren't going through. She has filed a report with the Police for missing persons.


  ---------------------------------------------------


  0 0

   Rais Kikwete akiongea na Watanzania waishi nchini Poland katika hoteli ya Bristol jijini Warsaw usiku wa kuamkia leo. 

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Fatma Fereji wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nchi katika Makamu wa Rais Dkt Tereiya Huvisa wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Katibu Mkuu  katika Ofisi ya Makamu wa  Rais  Mhe Sazi Salula  wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono Mwandishi wa Uhuru na Mzalendo Bw. Ramadhani Mkoma wakati akaiaga na kuondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika. Kushoto ni mwandishi wa ITV Bw. Emmanuel Buhohela, akifuatiwa na Naibu Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi na Msaidizi wa Waziri Huvisa
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Terezya Huvisa na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Fatma Fereji wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika.Picha Zote na IKULU

  0 0
 • 11/22/13--15:27: TUKIO LA MAUAJI ILALA
 •  Christina Newa akisimulia mkasa mzima wa tukio la mauaji hayo yalitokea Novemba 19 Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam baada ya mpenzi wake Gabriel Munisi kuwashambulia kwa risasi ndugu wa familia moja na kuwaua watu wawili na kisha yeye mwenyewe kujiua. (Picha na Francis Dande)
  Christina Newa.
   Dada wa Christina Newa, Carolyne Newa ambaye alimpoteza mume wake Capt. Francis Shumila katika tukio hilo, akisimulia maisha ya Christina Newa na mpenzi wake, Gabriel Munisi.
   Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani Ilala Bungoni.
    Mama mzazi wa Christina Newa ambaye alijeruhiwa na risasi begani akisaidiwa na mtoto wake, Carolyne Newa alipokuwa akirudi nyumbani baada ya kuruhusiwa na madaktari kutoka hospitali ya taifa Muhimbili alipokuwa akipata matibabu.
   Pole mama....
   Waombolezaji msibani.
   Christina Newa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la mauaji lililofanywa na Gabriel Munisi kuwashambulia ndugu wa familia moja na kuwaua watu wawili kisha mwenyewe kujiua, katika eneo la Bungoni jijini Dar es Salaam.
  Marehemu Captain Francis Shumila enzi za uhai wake.

  MLENGWA wa shambulizi la mauaji lililotokea Novemba 19, mwaka huu  Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam, Bi. Christina Newa, ameibuka na kuwalaumu polisi kwa kushindwa kuzuia mauaji yaliyosababishwa na mpenzi wake, Gabriel Munisi.
  Katika tukio hilo Gabriel Munisi aliwashambulia ndugu wa familia moja na kuwaua watu wawili, Alpha Newa 'Nando' na shemeji yake Capt. Francis Shumila kabla ya yeye mwenyewe kujiua.
  Christina alifafanua kuwa licha ya kutoa taarifa za kutishiwa maisha katika kituo cha Polisi Kirumba jijini Mwanza na Pangani jijini Dar es Salaam, polisi walipuuza tishio hilo huku wakiwadhalilisha kwa kauli za kebehi.
  Alisema uhusiano wake na Munisi haukuwa wa muda mrefu na kwamba baada ya kubaini kuwa kijana huyo ana tabia ya ukatili alifanya kila njia kuachana naye ikiwa ni pamoja na kwenda nchini Cyprus kwa ajili ya masomo.
  Aliongeza kuwa akiwa nchini Cyprus Munisi alimpigia simu na kumuomba atakaporejea kwa likizo asiijulishe familia yake ili apate nafasi ya kumpokea akiwa peke yake.
  “Ni kweli niliporudi likizo Munisi alinipokea na alionekana kuwa mtu aliyebadilika kitabia na hata tukapanga safari ya kwenda Mwanza tuliongozana katika gari dogo lakini tukiwa sehemu moja ya Singida alinishusha na kunitolea bastola huku akiniambia nimueleze sababu ya kwenda kusoma nje bila kumtaarifu,” alisema Christina.

  Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo alimuomba msamaha na hali ikawa ya utulivu mpaka walipofika Mwanza huku Munisi akiwa amezuia kila kitu alichotoka nacho Cyprus ikiwemo Laptop.
  Christina alisema kuwa hata hivyo hakuwa na wasiwasi na Munisi baada ya kuona amebadilika na kwamba katika hali hiyo alimuomba ruhusa ya kurejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya mambo  kabla ya kurejea jijini Mwanza.
  Alisema akiwa jijini Dar es Salaam, Munisi alipeleka Laptop kwa mafundi kwa ajili ya kuondoa namba za siri na akaweza kuona picha zinazomuonyesha Christina akiwa ufukweni na wanafunzi wenzake jambo aliloeleza kuwa lilimkera na kuwa mwanzo wa mgogoro.
  Huku akiushika mguu wake uliojeruhiwa kwa risasi Chrstina alisema, baada ya hali hiyo Munisi alianza kumpiga kila wakati huku akimfungia mlango asitoke nje mpaka atakaporudi  na kwamba hali hiyo ilidumu kwa muda mrefu mpaka alipopata msaada wa majirani walioweza kuwataarifu polisi na kumuokoa
  Baba wa Munisi awatimua
   Chrstina alisema baada ya kipigo cha mara kwa mara alilazimika kufikisha malalamiko yake kwa mzazi wa Munisi ambaye hakutaka kuwasikiliza na kumtaka aondoke nyumbani kwake.
  Alisema kutokana na hali hiyo hakuwa na jinsi zaidi ya kurudi kwa Munisi na kuendelea kupokea manyanayaso mpaka siku alipopata msaada kutoka kwa mpita njia aliyewasiliana kupitia dirisha la nyumba yao.

   Christina alisema alimpa namba za mama yake mpita njia huyo ambaye aliwasiliana na mama wa Christina ambao walifika jijini Mwanza na kufanya mawasilino na Polisi wa Mwanza na kufanikiwa kumuokoa.


   “Siku Polisi walipokuja nyumbani, Munisi hakuamini kama wanamfuata kwa heri akanilazimisha tutoke pamoja nilikuwa na kanga tu mwilini na hapo ndipo tulipoanza safari ya kituoni kwa ajili ya kuandikisha taarifa,” alisema Christina.
  Aliongeza kuwa wakiwa njiani kuelekea kituoni Munisi alipigia simu kwa ndugu wa Christina na kumtaka awaambie Polisi kwamba hakuna tatizo, jambo alilosema alilitekeleza kutokana na hofu aliyokuwa nayo.

  Chrstina aliongeza kuwa baada ya kufikishwa kituoni alikataa kurudi kwa Munisi na ndipo akarejea jijini Dar es Salaam baada ya kutumiwa tiketi na ndugu zake.
  Munisi amuwinda Dar
  Alisema baada ya kurejea jijini Dar es Salaam, Munisi alianza harakati za kutaka kupata msaada wa Polisi kutokana na vitisho vya Munisi ambapo alifika katika kituo cha Polisi Pangani na kutoa taarifa pasipo kupewa msaada wowote.
  “Pale Pangani tulimkuta mpelelezi mmoja, huyu bwana alitusaidia mwanzo mpaka ndugu yetu aliporudi lakini kuhusu vitisho vya bastola, alisema hayo ni mambo ya mapenzi na hayawahusu,”.
  Chrstina anasema baada ya kauli hiyo ya Polisi hawakuwa na njia ya kufanya na kuamua kutulia nyumbani kabla ya kubaini uwepo wa Munisi katika jiji la Dar es Salaam, aliyekuwa akifuatilia nyendo ya familia yao kila siku.
  Alisema mara kwa mara Munisi alikuwa akimtumia ujumbe wa simu na wakati mwingine kwenda kugonga katika nyumba yao na kumueleza kuwa hawezi kumuacha na kwamba ikitokea amemuacha atafanya mauaji katika nyumba zote tatu za familia hiyo

  Siku moja kabla ya Mauaji.
  Christina alisema siku moja kabla ya mauaji kutokea alipokea ujumbe wa simu kutoka kwa Munisi ukimsifia kuwa amependeza hali iliyozidi kumtia hofu na kuamua kumueleza shemeji yake Kapten Francis Shumila ambaye aliahidi kumlinda.
  “Nilimwambia Shemeji juu ya ujumbe wa Munisi naye akaniambia atanilinda na kama kufa ataanza yeye kabla ya kifo changu kumbe ndivyo alivyomaanisha,”alisema Chrstina kwa hisia kali.


  Wakati wa Mauaji

  Akisimulia hali ilivyokuwa muda mfupi kabla ya mauaji Christina alisema wakiwa wanatoka getini walimuona Munisi akiwafuata kwa kasi na kisha kutoa bastola hali iliyomfanya shemeji yake Kapten Shumila ashuke katika gari kwa ajili ya kutaka kumtuliza.
  Alisema wakati Shumila akishuka katika gari Munisi alimfyatulia risasi ya kichwa na kisha risasi zingine akizielekeza katika gari na kumuua Dada wa Chrstina aitwae Alpha pamoja na kumjeruhi mama yao mzazi sehemu ya begani.
  “Alikuwa kama Mnyama na katika hali hiyo niliweza kumsukumiza mama chini kwa ajili ya kumuokoa huku tukiwa tayari tumejeruhiwa na wengine wameshauawa Munisi kuona wote tumelala chini ndipo akajimaliza na bastola akidhani kwamba wote alishatumaliza,”alisema Chrstina.

  0 0  0 0


  Naomba niseme kitu kimoja kuhusu hili swala la PAPI KOCHA na BABU SEYA.
  Kwanza kabisa naomba nisieleweke vibaya kwa kuwa ninaamini kwamba Kila tendo ambalo linaenda kinyume na sheria katika jamii ni lazima sheria ichukue mkondo wake, na kwa kuwa mahakama iliamua beyond resonnable doubt kwamba hawa jamaa walithibitika kutenda makosa hayo na walistahili adhabu ambayo wanatumikia. Kwa hili ninaiheshimu mahakama na maamuzi yake. 
  Ila kikubwa ambacho nataka kukiongelelea hapa ni kuhusu wasanii na watu mbalimbali ambao kichinichini wamekuwa wakijifanya kuwaonea huruma na kufikiri kwamba hawakutenda bila kuchukua hatua zozote za kimsingi za kuwasaidia hawa jamaa zaidi ya kupiga kelele za chini ya uvungi zisizosaidia. 
  Kimuziki mimi binafsi nilikuwa na bado ni mshabiki mkubwa sana wa PAPII KOCHA na baba yake, sifurahii kama ni kweli walitenda makosa hayo katika maisha yao binafsi. Lakini hii haijalishi mapenzi yako kwa vipaji vyao. 
  Sasa nakuja kwa Hawa wasanii na watu wengine wenye mapenzi na hawa watu na Hasa wale wanaoamini kwamba jamaa walionewa katika hili huko nyumbani Tanzania. 
  Hivi kweli wameshindwa kuunda umoja wenye sauti na kuandika barua yenye nguvu kwa Rais ya kuwaombea msamaha hawa jamaa? Hivi kweli wasanii wote wa Tanzania wakiungana na kutia sahihi katika barua (Petition) ya kuwaombea msamaha wa Raisi hawa jamaa wether walitenda au hawakutenda kosa.
  Hivi mnafikiri kweli Raisi wetu hatalifikiria hili? kwa mawazo yangu mimi nahisi there is 75% chance ya Rais kufanya kitu kama akiombwa na sauti ya wengi hasa wasanii ambao CCM Inawategemea sana hasa katika nyakati hizi za kuelekea kwenye uchaguzi. 
  Sisemi kwamba watu hawajafanya kitu kuwasaidia hawa jamaa, naamini kuna watu wamekuwa hawalali kuwahangaikia hawa jamaa lakini nguvu yao haijatosha na sauti yao haijasikika. 
  Ila naamini fika kama Wasanii wote wenye mapenzi mema ya vipaji na moyo wa kusaidia na kusamehe wakiungana na kupeleka tamko rasmi la maombi ya kimaandishi yenye sahihi za wote ya kuwaombea msamaha hawa jamaa kwa 
  Muheshimiwa Raisi wetu kipenzi Jakaya Mirisho Kikwete atawafikiria na kidogo au kikubwa kitafanyika. 
  NAOMBA KAMA UMEUPENDA WARAKA HUU U-REPOST, SHARE NA USAMBAZE KWA WAHUSIKA HASA WASANII NA VIONGOZI WA WASANII HUKO NYUMBANI TANZANIA.

  <<FROM DJ KAYCEE, HOUSTON TEXAS, USA.>>

  0 0


  Na Edwin Mushi 
  wa Globu ya Jamii, Makete
  Jitihada za kumuua nyati aliyemjeruhi mkazi mmoja wa kijiji cha Ilevelo wilayani Makete kwa takribani siku tatu mfululizo linaonekana kugonga mwamba baada ya mnyama huyo kutafutwa bila mafanikio.
  Zoezi hilo linaloendeshwa chini ya Idara ya maliasili ya halmashauri ya wilaya ya Makete kwa kushirikiana na askari wanyama pori, limeonesha kutokuzaa matunda kutokana na kumtafuta mnyama huyo bila mafanikio hali inayosababisha kutishia usalama wa wakazi wa kijiji hicho na maeneo ya jirani.
  Akizungumza na mwandishi wetu aliyepo eneo la tukio, Bw. Lulesu kutoka idara ya maliasili wilaya ya Makete amesema juzi walifanikiwa kumuona mnyama huyo na wakati wakifanya jitihada za kumuua aliwatoroka na kumtafuta bila mafanikio hali iliyopelekea zoezi hilo kuahirishwa hadi jana alhamisi ambapo pia walimtafuta bila mafanikio.
  Amesema kwa hivi sasa baada ya leo hii kumtafuta bila mafanikio wanadhani huwenda mnyama huyo amehamia vijiji vya jirani ikiwemo Imehe na Luwumbu na kutoa rai kwa wakazi wa vijiji hivyo kuchukua tahadhari hasa wakati wa kwenda kwenye shughuli za kilimo

  Kutokana na hali hiyo ya sintofahamu kuwagubikwa mashaka makubwa kumepelekea wananchi hao kuishi maisha ya wasiwasi na kuishukuru halmashauri ya wilaya ya Makete na wote waliofika kwa ajili ya zoezi la kumuua nyati huyo, kwani kitendo hicho kimeonesha kuwa serikali yao inawajali.
  Miongoni mwa viongozi waliopongezwa kwa kushinda na wananchi hao kwa siku ya jana ni mkurugenzi mtendaji wa hallmashauri ya wilaya ya Makete Iddi Nganya, ambaye alishinda nao kumtafuta nyati huyo bila mafanikio.
  Uongozi wa timu inayoendesha zoezi hilo umetoa rai kwa wananchi wa Ilevelo na vijiji vya jirani ikiwemo Imehe na Luwumbu kutembea kwa makundi na kuchukua tahadhari kubwa kipindi hiki ambapo nyati huyo ametoweka katika mazingira ya kutatanisha na kudhaniwa huwenda ameelekea kwenye vijiji jirani.
  Wiki iliyopita mkazi wa kijiji cha Ilevelo kata ya Lupalilo wilayani Makete Bw Alfred Sanga alijeruhiwa na mnyama huyo, na kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ikonda Consolatha ambapo hivi sasa afya yake inaendelea vizuri

  0 0  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi, Alex Msama akifafanua jambo kuhusu maadalizi ya tamasha la Krisimasi ambapo kwa mara ya kwanza litafanyika kwenye uwanja wa Mao Tse Tung  mjini Zanzibar. (Picha na Francis Dande)

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi, Alex Msama akifafanua jambo kuhusu maadalizi ya tamasha la Krisimasi ambapo kwa mara ya kwanza litafanyika kwenye uwanja wa Mao Tse Tung  mjini Zanzibar. 

  Na Francis Dande
  WARATIBU wa Tamasha la Krismasi, Kampuni ya Msama Promotions ya Jijini Dar es Salaam, kwa mara ya kwanza wamesema kuwa watapeleka uhondo wa tamasha hilo katika mji wa Zanzibar.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo linalotarajiwa kutikisa kwa mara ya kwanza katika mji wa Zanzibar, Alex Msama alisema kuwa mbali ya Zanzibar, mkoa mwingine ambao umeongezeka ni Tanga.
  Msama aliwataka wakazi wa Zanzibar na vitongoji vyake kuunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha, hilo litakalofanyika kwenye uwanja wa  Mao Tse Tung, ambapo sehemu ya fedha zitapelekwa katika kusaidia kuwalipia ada watoto yatima wa Tanzania Bara na Zanzibar.
  Hivyo, Msama aliwataka Wazanzibar kufika kwa wingi katika tamasha hilo ili kufanikisha malengo hayo, kama alivosisitiza kwa wakasi wa mikoa yote ambayo tamasha hilo litarindima.
  Katika kufanikisha mpango huo, Msama ambaye ni Mkurugenzi pia wa Msama Promotions, ametoa wito kwa wapenzi, mashabiki, wadau na wapendwa katika Kristo Yesu, wajitahidi kumuunga mkono kwa kufika kwenye Tamasha hilo litakalozinduliwa rasmi Desemba 25 jijini Dar es Salaa, kisha kufanyika katika mikoa saba.
  Alisema baada ya Dar es Salaam, litahamia mkoani Morogoro Desema 26 kabla ya kwenda Moshi, Desemba 28 kisha kuvamia jiji la Arusha  Desemba 29, na mjini Dodoma, mikoa mingine ni Tabora, Tanga, Mbeya na Mwanza.
  Alisema mbali ya malengo mengine, pia tamasha la hilo litakuwa na ujumbe wa kuhimiza amani  nchini chini ya kaulimbiu ya ‘Tuilinde na Kuidumisha Amani Yetu.’
  Kwa upande wa waimbaji watakaopamba tamasha hilo la kimataifa, ni kutoka Afrika Kusini, Nigeria, Zambia, DRC Congo, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na wenyeji Tanzania.
  Msama alisema kuwa maandalizi yote kuhusiana na tamasha hilo yanakwenda vizuri na kuwataka watu wajitoleze kwa wingi kupata ujumbe wa Neno la Mungu kwa njia ya sauti za waimbaji mahiri waliojitoa kumtumikia Mungu kwa njia hiyo. 


  0 0

  Dkt Kesi Mtambo anasikitika kutangaza kifo cha Mjukuuu wake Jeffa Othman Kessi Mtambo kilichotokea usiku huu. 

  Mazishi yatafanyika leo Jumamosi Novemba 23, 2013 saa 7 Adhuhuri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.

  Msiba upo Mtaa wa Nyati nambaa 11 Kariakoo, Fire, hapa Dar es salaam. Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote walipo.

  0 0

  eacj-press-banner.jpg

  East African Court of Justice Arusha, 22 November 2013: The First Instance Division today in its decision emphasized that, it is the role of the Council of Ministers to determine the extension of the jurisdiction of the East African Court of Justice as stipulated in Article 27 (2) of the Treaty.

  However the Court declared that the failure by Council of Ministers/ Sectoral Committee on Legal and Judicial Affairs to implement an earlier judgment which was delivered on 30th June 2011, where the Court had ordered that quick action should be taken by the EAC in order to operationalise the extended jurisdiction of the Court under Article 27of the Treaty for the establishment of the East African Community is an infringement of Article 38 (3) of the Treaty which states that; A Partner State or the Council shall take, without delay, the measures required to implement a judgment of the Court.

  Court also ordered that the Secretary General should take action to expeditiously implement previous judgment mentioned above and to pay US$ 52,534.10 as taxed costs to the Applicant.

  On the prayer that the Secretary General should be cited for the contempt of the Court for failure to implement the earlier judgment, Court considered the fact that the Secretary General has not flagrantly disrespected the order since he has made an effort to convince the Council to pay the taxed costs to the Applicant and considering the unique circumstances of the case, Court granted the Respondent the opportunity to purge the contempt with respect to the taxed costs and to pay the same within three (3)months from the date of the Judgment.

  The Secretary General was also ordered to pay costs on the 2nd Reference (determined today) because it was a result of the failure by the Partner States to implement the Court’s orders that the said case was filed.

  The second Reference had been filed by Hon. Sitenda Sebalu, a Member of Parliament in the Republic of Uganda, against the Secretary General (SG) of the East African Community for alleged failure of the Council of Ministers/ Sectoral Council of Legal and Judicial Affairs to implement the judgment delivered by EACJ in a previous case involving the same Parties. The Court had ordered that quick action should be taken by the EAC in order to operationalise the extended jurisdiction of the Court under Article 27of the Treaty for the Establishment of the East African Community.

  Present in Court to receive the Judgment, were Mr. Chris Bakiza and Mr. Justin Semuyaba, lawyers for the Applicant (Hon. Sitenda Sebalu) and Hon. Wilbert Kaahwa, Counsel for the Respondent, the EAC Secretary General.

  On the bench of the Judges were, Hon Justices, Jean Bosco Butasi, Principal Judge, Lady Justice Stella Arach Amoko, Deputy Principal Judge, John Mkwawa, Isaac Lenaola, and Dr. Faustin Ntezilyayo. 

  0 0


  0 0
 • 11/22/13--20:00: Obituary

 • 0 0
 • 11/22/13--20:30: Article 13


 • 0 0

  Taswira za mahafali ya cabin crew ya wafanyakazi wa Air Tanzania iliyofanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee Pension Tower jijini Dar es salaam hivi karibuni.
   Afisa Mtendazi Mkuu wa  Air Tanzania Capt. Lazaro akiongea na wafanyakazi
   Sehemu ya wafanyakazi wa Air Tanzania
   Mkurugenzi wa Operations Capt. Shaidi akiongea machache
   Mmoja wa wahitimu akipatiwa cheti cha kufuzu
  Picha ya pamoja

  0 0

  Mfuko wa pensheni wa LAPF ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania wenye makao makuu yake Mjini Dodoma, umekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni tano (5,000,000/=) kwa Chama cha michezo cha Vyuo Vikuu vya Tanzania TUSA, kwa ajili ya mashindano ya TUSA yatakayofanyika mjini Dodoma kuanzia tarehe 10 - 17 Desemba, 2013. Sherehe fupi ya makabidhiano, imefanyika katika Ofisi za LAPF, zilizoko Millennium Towers  jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa LAPF Kanda ya Dar es Salaa, Bibi Amina Kassim, amesema Mfuko wa Pensheni wa LAPF umekuwa pia ukitoa misaada mbali mbali ya kijamii katika kusaidia sekta mbali mbali kama elimu, hospitali, vituo vya kulea watoto yatima na pia katika sekta ya michezo kusaidia kuinua michezo nchini. 
   Bibi Kassim amesema, hii ni mara ya tatu kwa LAPF kudhamini mashindano kwa mara ya kwanza LAPF ilidhamini mashindano ya mwaka 2011 na 2012, ambapo LAPF imetoa vifaa hivi kwa kutambua umuhimu wa wanafunzi wa taasisis hizo kama wanachama wetu watarajiwa. Amesema kufuatia LAPF kuwa Mfuko bora wa Pensheni kwa kudhihirishwa kwa tuzo iliyotolewa na Msimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii SSRA kuwa LAPF kuwa ni Mfuko wa Pensheni unakua kwa kasi Zaidi nchini. 
  Kitendo cha LAPF kuwa imekuwa ikipata tuzo kutoka kwa bodi ya wahasibu nchini NBAA kwa kuwa Mfuko wenye Hesabu Bora za mwaka kwa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2008, 2009, 2010 na 2011, LAPF sasa imeamua kujikita kudhamini michezi, ili kurudisha kwa jamii, sehemu ya mafanikio hayo. 
   Akishukuru kupata vifaa hivyo, Mwenyekiti wa TUSA Taifa, Asnati Chagu aliishukuru LAPF kwa msaada huo, na kusema umekuja wakati muafaka, ila pia akaomba wafadhili wengine wazidi kujitokeza ili kufanikisha michuona hiyo. 
   Amesema msaada huoiwa jezi ni moja tu ya mahitaji, lakini bado kuna mahitaji mengine yanahitajika vikiwemo vikombe na zawadi kwa washindi mbalimbali.


  0 0older | 1 | .... | 273 | 274 | (Page 275) | 276 | 277 | .... | 3272 | newer