Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

DC NJOMBE AWAAGIZA WATENDAJI WA WILAYA KUBANDUA MABANGO YA WAGANGA WA KIENYEJI MITAANI

$
0
0


Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Mkoa Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto wakati wa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika mjini Njombe.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Bumi Mwamasage akieleza lengo la Kamati ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto kukutana wakati wa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika mjini Njombe.
Kiongozi wa Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Hanifa Selengu akieleza lengo la timu hiyo kwenda mkoani Njombe wakati wa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika mjini Njombe.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bw. Denis Bashaka akileza namna Sheri ya uchawi sura ya 18 ya Mwaka 2002 inavyozuia vitendo vya upigaji ramli na kazi za uganga wa kienyeji wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto kilichokutana Mjini Njombe

Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Mwanaisha Moyo akielezea umuhimu wa Kamati hiyo kutoa huduma kwa wahanga wa vitendo vya ukatili kwa haraka wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto kilichokutana Mjini Njombe.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Mkoa wa Njombe ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto wakiongozwwa na Mkuu waWilaya ya Njombe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Ruth Msafiri (wa pili kulia) wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika mjini Njombe.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

………………………..

Na Mwandishi Wetu Njombe

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amemuagiza Katibu Tawala wa Wilaya hiyo na watendaji wote kuzunguka katika mitaa kubandua mabango yote yanayotangaza huduma za waganga wa kienyeji ambao wanafanya kazi kinyume cha Sheria.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Kamati ya Mkoa wa Njombe Ulinzi wa Mwanamke na Mtoto kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa na kusisitiza kuwa hatovumilia vitendo vya ukiukwaji Sheria ya Uchawi Sura ya 18 ya mwaka 2002 inayokataka upigaji ramli na kujihusisha na masuala ya kishirikina.

Ameongeza kuwa Serikali haitovumilia vitendo vyovyote vinavyojihusisha na masuala ya kishirikina kufanyika katika Wilaya ya Njombe kwani vimekuwa vikisababisha mifarakano na taharuki kubwa na kupelekea kutokea kwa utekaji na mauaji katika jamii.

Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa baadhi ya watendaji wa Serikali za Mitaa na vijiji wamekuwa wakishiriana na waganga wa kienyeji kutekeleza masuala yanayohusishwa na imani za kishirikina.

“Nimemuagiza Katibu Tawala wa Wilaya kushusha agizo hili kwa watendaji wa vijiji na mitaa na sitaki kuyaona mabango hayo na nikiyaona tena nitachukua hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kuyaweka” alisema

“Niseme tu sitosita kuwachukulia hatua watendaji watakaoendelea kushirikiana na waganga wa kienyeji na kuwakaribisha katika vijiji na mitaa yao na kuwasaidia kufanikisha kazi zao ambazo ziko kinyume cha Sheria” alisema

Mkuu huyo wa Wilaya ameomba ushirikiano kutoka kwa Kamati za Ulinzi wa Mwanamke na Mtoto kuanzia ngazi ya mkoa na Halmashauri ili kusaidiana katika mapambano ya kutokomeza vitendo vya ukatili kwa watoto.

Akizungumza katika kikao hicho kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Bumi Mwamasage amesema kuwa Kamati hiyo inatakiwa kuwajibika katika jamii kwa kutoa elimu na ishuke kwa jamii ili kuwawezesha wanajamii hao kuunga mkono mapambano ya vitendo vya kikatili dhidi ya Mwanamke na Mtoto.

Kwa upande wake Kiongozi wa Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Hanifa Selengu amesema kuwa Wizara imeamua kushirikiana na Mkoa wa Njombe kwa kuitisha Kamati ya Ulinzi wa Mwananmke na Mtoto ili kujadili kwa pamoja na kupata namna bora ya kupambana na kutokomeza vitendo vya kikatili kwa mwamake na Mtoto.

“Tumekuja kuongeza nguvu katika masuala haya yaliyojitokeza Mkoani hapa kwani wote tunadhamana ya kumlinda Mtoto dhidi ya vitendo vya kikatili” alisema. Naye Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Mwanaisha Moyo amesema kuna umuhimu wa Kamati hiyo kutoa huduma kwa wahanga wa vitendo vya ukatili kwa haraka na kwa wakati.

Aidha Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bw. Denis Bashaka namna Sheria ya Uchawi Sura ya 18 ya Mwaka 2002 inavyozuia vitendo vya upigaji ramli na kazi za uganga wa kienyeji ambavyo vinahusishwa na mauaji yaliyojitokeza mkoani Njombe.

Kamati ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto ya Mkoa wa Njombe imekutana Mjini Njombe kujadiliana na kupata namna bora ya kuondokana na vitendo vya kikatili hasa vitendo vya utekaji na mauaji ya watoto mkoani humo.

MABANGO YA WAGANGA WA KIENYEJI MITAANI YABANDULIWE-DC NJOMBE

BREAKING NEWZZZ:MSANII MAARUFU WA BONGOFLEVA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Hivi punde chumba cha habari Globu ya Jamii imepokea taarifa za kusikitisha/huzunisha  zinazohusu aliyekuwa Msanii mahiri katika miondoko ya kughani a.ka Rap almaarufu kwa jina la Godzilla amefariki Dunia.

Taarifa zinaeleza kuwa Msanii huyo maye kwa jina halisi anaitwa Golden Mbunda,aliyekuwa akitikisa anga ya bongofleva katika miondoko ya hip hop nchini ,amefariki Dunia ghafla  usiku wa kuamkia leo Jumatano Februari 13,2019 akiwa nyumbani kwao maeneo ya Salasala,jijini Dar.

Mwili wake umepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Lugalo,Mwenge.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi-AMIN.

TUTAENDELEA KUWAJUZA HABARI ZAIDI KADIRI ZITAKAVYOKUWA ZIKIINGIA.

WAKAZI WA HALMASHAURI YA CHALINZE WATAKIWA KUWA NA VYOO BORA

$
0
0
Wakazi wa vijiji vya kisanga,kata ya talawanda katika halmashauri ya chalinze mkoani pwani wametakiwa kujenga utamaduni wa kuwa na vyoo bora .
Mtendeji wa kijiji cha kisanga Exaud Edward mhelela akitoa ufafanuzi wa jinsi ya kuwa na vyoo bora



NA FREDY MGUNDA, PWANI

WAKAZI wa vijiji vya kisanga,kata ya talawanda katika halmashauri ya chalinze mkoani pwani wametakiwa kujenga utamaduni wa kuwa na vyoo bora ilikuepukana na magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na kula kinyesi cha binadamu.

Akizungumza na wakazi wa vijiji hivyo wakatika wa kampeni ya uhamasishaji wa ujenzi wa vyoo bora,mtendeji wa kijiji cha kisanga Exaud Edward mhelela,alisema ni muhimu kwa kila kaya kuhakikisha inakuwa na chuo safi na bora watakachotumia kwa ajili ya kujisitili.

Amesema kila kaya inatakiwa kuwa na chuo bora na safi kwa ajiri ya familia yake,kwani magonjwa mengi ya mlipuko husababishwa na watu kula kinyesi cha binadamu na endapo kutakuwa na magonjwa ya mlipuko ya mara kwa mara,basi yatasababisha kupunguza nguvu kazi ya taifa na maendeleo kurudi nyuma.

“ndugu zangu maendeleo yoyote hayawezi kuja katika kijiji chetu cha kisanga bila kuwa na maji safi,mazingira na rafiki ikiwemo (vyoo),hivyo ni muhimu tutahidi katika uhamasishaji wa kuwa na vyoo safi na bora kwa kila kata” alisema.

Kwa upande afisa mradi wa WARIDI,Samson Mbwasi alisema hali ya usafi na mazingira katika vijiji vya kisanga na Msigi ilikuwa sio nzuri kwa sababu kaya nyingi zilikuwa hazina vyoo bora.

Alisema mara baada ya kuingia kwa mradi huo wa PDF/WARIDI Chalinze na kuwapatia mafunzo watendaji wote wa vijiji,walikusanya taarifa za usafi wa mazingira na imesaidia wananchi wengi kujenga vyoo bora.

Alisema uongozi wa kijiji ukiongozwa na mtendaji wa kijiji,waliwahimiza wananchi na kwapamoja walikubariana kuboresha hali zao za usafi hususani kwenye ujenzi na matumizi sahihi ya vyoo.

Alisema katika vijiji vyote viwili vya kisanga na msigi,wamefanikiwa kuhamasisha ujenzi wa vyoo katika kaya hamsini na nane (58) kati ya mia moja tisini na saba (197) sawa na asilimia 29.9. 

PBPA yatakiwa kuhakikisha kuwa Bandari zote zinatumika kupokea\kushusha mafuta

$
0
0
Na Teresia Mhagama,
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameitaka Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kuhakikisha kuwa bandari zote nchini zinatumika katika shughuli za kupokea na kushusha mafuta ili kuongeza wigo wa upatikanaji  mafuta katika sehemu mbalimbali nchini.

Aliyasema  hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na Wajumbe wa Bodi ya Wakala huo  ambapo kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua, Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Mwanamani Kidaya na watendaji wengine wa Wizara.

Dkt. Kalemani aliyasema hayo baada ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PBPA, Erasto Simon, kumueleza kuwa, mpaka sasa mafuta yanapokelewa katika Bandari Tatu tu ambazo ni Dar es Salaam, Mtwara na Tanga.

“Tunataka kila Bandari ifanye kazi ya kupitisha mafuta mfano ni  Bandari ya Bukoba ambapo mafuta yakipokelewa pale yanaweza pia kusafirishwa kwenda nchini jirani badala ya kusafirishwa kwa njia ya barabara kutoka jijini Dar es Salaam,” alisema Dkt Kalemani.

Aidha, Dkt Kalemani aliagiza kuwa, Bandari zote zinazotumika sasa zipokee pia mafuta ya taa kwani wananchi bado wanatumia mafuta hayo kwa shughuli mbalimbali kwa kuwa usambazaji wa nishati ya umeme bado haujafikia asilimia 100.

Pia, Dkt Kalemani aliiagiza Bodi ya PBPA kuhakikisha kuwa ushiriki wa wazawa katika shughuli za uingizaji mafuta nchini  unaongezeka kwa kuwajengea uwezo wa aina mbalimbali ikiwemo kuwapa elimu kuhusu shughuli hizo.

Kwa ujumla, Dkt Kalemani aliitaka Bodi hiyo kuwa na mikakati mbalimbali itakayopelekea kampuni nyingi zaidi kushiriki katika kazi ya uingizaji wa mafuta nchini tofauti na ilivyo sasa ambapo kati ya kampuni 25 zilizosajiliwa, kampuni zisizozidi Saba ndizo zinashiriki katika uletaji wa mafuta nchini.

Vilevile aliiagiza Bodi hiyo kuhakikisha kuwa, inasimamia masuala mbalimbali ikiwemo  suala la nchi kupata mafuta kwa wakati huku yakiwa salama, kutokuwepo migogoro katika shughuli za uingizaji mafuta nchini, kutokuwepo kwa upotevu wa mafuta, mafuta kushushwa ndani ya muda mfupi  mara yanapowasili na kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na  mafuta ya ziada katika muda wote.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alitoa angalizo kwa Bodi hiyo kuhakikisha kuwa, kampuni zinazopewa kazi za uingizaji mafuta nchini zinakuwa na uzalendo na hivyo kuepusha hujuma zozote zinazoweza kutokea na kusababisha nchi kuwa na upungufu wa nishati hiyo au kupata mafuta yasiyo salama.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Dkt Lutengano Mwakahesya, akizungumza katika kikao cha Bodi hiyo na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Sita kushoto), Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa nne kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua  (wa Tatu kulia) na watendaji wengine wa Wizara.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa tano kushoto) akizungumza  katika kikao chake na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa nne kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua  (wa Tatu kulia) na watendaji wengine wa Wizara.
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) (kushoto) na Watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati (kulia), wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani wakati wa kikao chake cha Bodi ya PBPA kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Dkt. Kalemani ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAAHIDI KUENDELEZA TAFITI ZA TIBA ASILIA

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo                          
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja Dk. Ali Salum Ali amesema Wizara ya Afya itaendelea kufanya utafiti aina mbali mbali za mimea iliyopo Zanzibar ili kuzalisha dawa mpya za Tiba Asilia kwa ajilia ya kutibu maradhi mbali mbali.

Akizungumza katika mkutano wa Tafiti wa Tiba asilia ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) na kuwashirikisha wadau wa tiba hiyo na ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Tianjin cha China, Dk. Ali alisema dawa nyingi zinazotumika Hospitali zinatokana na mimea baada ya kufanyika tafiti mbali mbali za kisayansi.

Alisema kutokana na kutambua umuhimu wa mimea kwa ajili ya Tiba asilia, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na watibabu wa tiba hiyo ambao wanatumia mizizi, majani na magome ya mimea.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja aliweka wazi kuwa Zanzibar imepiga hatua katika matibabu ya Tiba asilia na sehemu nyingi watibabu wa tiba hiyo wanapatikana hivyo kitu muhimu ni kuongeza wigo wa kufanya Tafiti.

Alisema kutokana na umuhimu wa Tafiti kwa maendeleo ya Taifa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha vitengo vya utafiti kwa kila Wizara na kuanzisha Taasisi maalumu ya masuala ya afya ili kuona kazi hiyo inafanyika kwa ufanisi mkubwa.

Mkurugenzi wa Taasisi ya ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) Dk. Mayasa Salum Ali alisema Watibabu wa Tiba asilia wanatoa mchango mkubwa kusaidia jamii katika matatizo mbali mbali ya kiafya yanayowakabilili na kuyapatia ufumbuzi.

Alisema iwapo wananchi wote wanaopata matatizo ya afya wangeenda Hospitali na vituo vya afya kutafuta matibabu visingeweza kukidhi mahitaji lakini mchango wa Watibabu wa Tiba asilia ni mkubwa na unathaminiwa.

Aliahdi kuwa ZAHRI itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali wa Tiba asila na wananchi wa mijini na vijijini kuhakikisha lengo la kuundwa kwa Taasisi hiyo linafanikiwa.

Mhadhiri wa Kitivo cha Afya kutoka Chuo Kikuu cha Tianjin cha China Prof. Yuhong Bian alisema WHO  imeweka mipango endelevu ya Kidunia na Kikanda katika kukuza na kuendeleza Tiba asilia kutokana na kutambua mchango wake kwa wananchi.

Alisema China ni moja ya nchi zinazothamini na kuendeleza matibabu ya Tiba asilia kwa miaka mingi na ziko Hospitali na Taasisi kubwa zinazotoa matibabu hayo na wananchi wanaziamini na wanaendelea kuzitumia kwa matatizo mbali mbali ya afya zao.
 Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Ali Salim akifungua Mkutano wa siku moja wa utafiti wa maswala ya Tiba asilia uliofanyika ukumbi wa Mikutano Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
 Mrajis wa Tiba asilia Zanzibar Haji Juma Haji akitoa mada yake ya uchambuzi wa dawa za jadi ulivyo Zanzibar katika mkutano wa utafiti wa maswala ya Afya kupitia Tiba asili.
Picha No.03- Mshiriki wa Mkutano wa utafiti wa Afya, Tiba asilia, Dkt. Mahamed Said Ali wa Hospitali inayotibu kwa kutumia miti shamba iliyopo Bububu Kijichi, akichangia katika Mkutano wa utafiti wa Tiba asilia.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar Dkt. Mayassa Salum ally akimpa maelezo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tianjin cha China Prof. Bian Yuhong katika Mkutano wa siku moja wa utafiti wa Tiba asilia.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tianjin cha China Prof. Bian Yuhong akitoa mada kuhusu matibabu ya Tiba asilia nchini China
Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya dawa Zanziba Zahran Ali Hamad akitoa neno la shukrani na kufunga Mkutano wa siku moja wa utafiti wa Tiba asili.
Picha na Makame Mshenga.

Prof Kikula akagua Shughuli za uchimbaji wa Madini na Kuhamasisha ulipaji wa Kodi

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya madini Nchini Prof Idris Kikula akifanya ukaguzi wa ulipaji wa Maduhuli wa kampuni ya Uchimbaji wa Kokoto ya Nyanza Road works alipokuwa akikagua machimbo na mitambo ya uzalishaji wa kokoto eneo la Chigongwe Jijini Dodoma.Katikati ni kamishna wa Tume ya Madini Dkt.Athanas Macheyeki na Afisa Madini wa Mkoa Jonas Mwano.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge(kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya madini nchini Prof Idris Kikula alipomtembelea kumweleze juu ya ziara yake ya kukagua Shughuli za uchimbaji wa Madini na Kuhamasisha ulipaji wa Kodi na Ufahamu wa Sheria ya Madini katika Mkoa wa Dodoma.
 :Makamishna wa Tume ya Madini nchini Prof Abdulkarim Mruma na Dkt.Athanas Macheyeki wakifuatilia jambo wakati walipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Tume ya madini Nchini Prof Idris Kikula na Kamishna wa Tume ya Madini nchini Prof Abdulkarim Mruma wakifuatilia hatua mbalimbali za  uchenjuaji wa dhahabu leo Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Nchini Prof Idris Kikula(mwenye kofia na miwani)  akiangalia moja ya sehemu ya machimbo ya mawe leo Jijini Dodoma.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.

RAIS DKT.SHEIN AFANYA MAJUMUISHO YA ZIARA YAKE WILAYA YA MJINI UNGUJA

$
0
0
 MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Mjini Unguja Kichama Ndg. Juma Faki, akizungumza wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa majumuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Mjini Unguja kutembelea Miradi ya Maendeleo ilioko katika Wilaya hiyo majumuisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 MKUU wa Wilaya  ya Mjini Unguja Bi. Marinev Joe Thomas, akisoma taarifa ya utekelezaji ya Wilaya ya Mjini wakati wa Mkutano wa Majumuisho ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, yaliofanyika katika ukumbi wa kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisoma Taarifa ya Utekelezaji ya Wilaya ya Mjini Unguja baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Bi. Marine Joe Thomas, wakati wa mkutano wa majumbuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Mjini Unguja .
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala zac Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ. Haji Omar Kheri, akizungumza wakati wa mkutano wa Majumuisho ya Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, yaliofanyika katika ukumbi wa kiwanja cha Watoto kariakoo Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Majumuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Mjini Unguja katika ukumbi wa Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar, baada ya kumaliza ziara yake katika Wilaya hiyo.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa mkutano wake wa majumuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Mjini Unguja, uliofanyika katika ukumbi wa Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.
 BAADHI ya Makamanda wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Wilaya ya Mjini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa majumuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Mjini yaliofanyika katika ukumbi wa kiwanja cha watoto kariakoo Zanzibar.
 BAADHI ya Masheha wa Wilaya ya Mjini Unguja wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamedv Shein,wakati wa mkutano wake wa Majumuisho uliofanyika katika ukumbi wa kariakoo baada ya kumaliza ziara yake katika Wiala ya Mjini Unguja.
MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza na kutowa neno la shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa mkutano wa majumuishoi ya ziara yake katika Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)  

NGOs zitakazokiuka Sheria kukiona

$
0
0
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nchini kutoka Wizara ya Afya, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii  Neema Mwanga ametoa onya kuwa atachukua hatua kali dhidi ya Shirika lolote Lisilo la Kiserikali litalokiuka kufanya kazi kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya NGOs ya Mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005.
Akiwa katika ziara ya kutembelea mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyoko katika Mkoa wa Kilimanjaro Msajili Mwanga amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanawajibu wa kuzingatia kanuni mpya za Sheria ya NGOs zinazoelekeza Mashirika hayo kufanya kazi kwa kuzingatia Misingi ya uwazi na uwajibikaji maana miradi hiyo imeanzishwa kwa lengo la kuwanufaisha wananchi ambao ndio walengwa wakuu.
Msajili Mwanga aliwaambia viongozi wa Mashirika manne aliyoyatembelea leo hii ikiwemo TAWREF, White Orange, Elimu Mwangaza na Tusonge Community Organisation kwamba Misingi ya uwazi na uwajibikaji kama inavyobainishwa katika Sheria hiyo inasisitizwa kwa lengo la kukuza ushiriki wa wanufaika katika kutambua vyanzo vya mapato ya NGOs, kiasi cha fedha zinazopolkelewa na mashirika na kutoa taarifa za miradi yao inayotekelezwa kwenye ngazi ya jamii ili kufuata matakwa ya kisheria na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Kufuatia azma ya Serikali ya kuacha kufanya shughuli za NGO kwa mazoea, Msajili Mwanga ameonya kuwa NGO yoyote itakayobainika kufanya kazi bila kusajiliwa au kupata hati ya ukubalifu itakosa sifa na kupelekea kupata zuio la usajili kwa mujibu wa kanuni ya sheria ya NGO ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005.
‘’Naelekeza NGO zote kubainisha kazi zinazotekelezwa, kwa sasa tuko kwenye hatua ya kuwajengea wadau wote wa NGOs uelewa ili kuwezesha kila mmoja kuzingatia sheria na mashirika amabyo yatashindwa kuzingatia sheia, taratibu na kanuni za utekelezaji wa miradi yao zitashurutishwa kusitisha miradi yao maana hazitakuwa na sifa stahiki”. Alisema Msajili  N. Mwanga.
Katika ziara hiyo ya kikazi Msajili wa NGOs amepongeza kazi inayofanywa na Mashirika ya TAWREF, White Orange, Elimu Mwangaza na Tusonge Community Organisation na kuwataka Wakurugenzi wa taasisi hizo kwa kuzingatia vipaumbele vya Mikoa, Halmashauri, na changamoto zinazowakabili wananachi katika Mkoa wa Kilimanjaro na nje ya Mkoa huo. Ameongeza kuwa utendaji wa Taasisi hizo umeonesha kuzingatia yale yaliyobainishwa katika kanuni za sheria ya NGOs na kuwataka kuwasiliana na Ofisi ya Msajili ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri katika kuendelea kuboresha mazingira ya kazi zao kama kutakuwa na suala lenye kuwatatiza katika utendaji wa akzi zao. 
Aidha Msajili Mwanga amewataarifu wadau wa NGOs kuwa katika kuhakikisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanatatuliwa chanagmoto zinazowakabili, Serikali Inaendelea kukamilisha mfumo wa usajili na utoaji wa taarifa kwa njia ya mtandao (online). Mfumo huu utatumiwa na wadau, wasajili wasaidizi ngazi ya mikoa na Halmashauri pamoja na Ofisi ya Msajili ya taifa. Juhudi hizi zitasaidia Taifa kukuza mchango wa Mashirika katika uchumu wa Taifa na kukuza uwajibikaji.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nchini Neema Mwanga amebainisha kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya Idara kuu ya Maendeleo ya Jmaii Jinsia wazee na watoto inakamilisha kanzidata ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali hapa Nchini ili kuwa na nyenzo ya kufuatilia mchango wa mashirika hayo katika pato la Taifa. Wakti huo huo Ofisi ya Msajili wa NGOs inaandaa mfumo wa Ufuatiliaji na tathmini ili kufanikiha kazi ya uratibu kwa kuonesha wadau kutambua maungufu yao na kuyafanyia maboresho katika muda stahiki. Juhudi hizi zitasaidia mfumo wa uratibu katika ngazi mablimbali kuwa na uelewa wa pamoja na kuchukua hatua dhidi ya Taasisi ambayo itaonekana kutozingatia sheria.
Wakiongea kwa muda tofauti wakati wa ziara hiyo Bw. Michael Reuben ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ‘Elimu Mwangaza’ amepongeza juhudi za Wizara katika kutatua chanagmto zinazokwamisha ufanisi katika utendaji wa NGOs Nchini. Moja ya hatua iliyofurahiwa na wadau wengi ni uandaaji wa mfumo wa usajili kwa njia ya matandao ili kupunguza gharama za safari wakati wa kufuata huduma hiyo.
Vilevile mmoja wa viongozi wa NGOs moja kutoka Manispaa ya Moshi(jina limehifadhiwa) ameeleza ziara ya Msajili amabye amefika katika Ofisi ya Shirika hilo imekuwa na manufaa makubwa maana imemjengea ari na uelewa wa kukamilisha taratibu za uasajili ili atambuliwe na hivyo kuendesha kazi zake kwa mujibu wa matakwa ya kisheria. 
Mwisho Neema amepongeza Maafisa Wasaidizi wa Mkao wa Kilimanjaro kwa namana wanavyotekelezakazi yao ya kusimamia na kuratibu kazi za NGos kwa weledi katika uzingatiaji wa kanuni za sheria ya NGOs ya Mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005. Watendaji hao wa ngazi ya Mkoa na Halmashauri wamekumbushwa wajibu wao wa kuyasimamia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa  kufuata katiba, Sera za kitaifa, kanuni za maadili, vipaumbele vya kijamii, vibali vya kazi kwa watendaji wasio raia wa Tanzania pamoja na umuhimu wa uwasilishaji wa mikataba ya miradi ya kazi zilizopata ufadhili kwa ajili ya utekelezaji.
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanadhamana ya kutoa mchango katika jamii masikini na isiyo na uwezo ili kuwezeshwa katika kuboresha ustawi na maendeleo ya maisha ya wananchi wenye uhitaji. 
Katikati Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha S. Amour na Katibu Tawala wa Msaidizi Utawala Bwai Biseko wakifuatilia kwa makini maelezo ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nchini wa (pili kulia) Neema Mwanga na ujumbe wake kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa ziara ya kufuatilia uratibu na usajili wa NGOs katika mkoa huo.
Kulia, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Moshi Bw. Michael Mwandezi akiongea na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati  Neema Mwanga  kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa ziara ya kufuatilia uratibu na usajili wa NGOs katika mkoa wa Kilimanjaro.
Msajili wa Mashirika Yasiyo Yakiserikali Neema Mwanga(kulia) kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akipokea maelezo ya shughuli za Mradi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Lisilo la Kiserikali la ElIMU MWANGAZA Bw. Michael Reuben liloko Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara ya kufuatilia uratibu na usajili wa NGOs katika mkoa huo .
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TAWREF, Dafrosa Itemba (kushoto)akitoa ufafanuzi wa mafanikio ya Shirika hilo kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Neema Mwanga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Msajili huyo kufuatilia uratibu na usajili wa NGOs katika mkoa wa Kilimanjaro mapema wiki hii.
Msajili wa Mashirika Yasiyo Yakiserikali Bi. Neema Mwanga (Katikati) kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akisisitiza hoja ya kisheria ya uwazi na uwajibikaji kwa uongozi wa Shirika Lisilo la Kiserikali la TAWREF (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kufuatilia uratibu na usajili wa NGOs katika Mkoa wa Kilimanjaro mapema wiki hii. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Changamoto za hali ya hewa nchini chanzo cha kuongezeka kwa joto: TMA

$
0
0
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imesema changamoto mbalimbali za hali ya hewa zinazojitokeza hapa nchini zimesababisha kuongezeka kwa kasi joto nyakati ya usiku ikilinganishwa na mchana.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Utabiri wa TMA, Dk Radslaus Chang'a ameyasema hayo leo Februari 13, wakati katika warsha ya siku moja na waandishi wa habari wakati wakijadili mwelekeo wa msimu wa mvua za masika kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei mwaka huu. Alisema hivi karibuni kumekuwa na changamoto ya hali ya hewa ambayo imekuwa ikijitokeza kwa athari mbaya ya hewa.

Dk.  Chang'a alisema athari mbalimbali zimekuwa zikijitokeza kama kuwepo kwa upepo mkali,mvua kubwa zilizosababisha wananchi kukosa makazi na  kutokea kwa joto kali. "Ingawa majanga ya asili hayawezi kuepukika lakini taarifa zikiwafikia walengwa mapema kabla ya janga kutokea zitasaidia jamii husika, "alisema

"TMA imekuwa ikitoa utabiri wake wa kila siku kwa njia ya televisheni kwa kutumia programu mpya ya teknolojia ya kidigitali ya kisasa,” amesema.
Dk. Chang’a amewaomba wananchi waendelee kufuatilia taarifa za hali ya hewa ili waweze kuchukua hatua stahiki mapema.


Amesema leo watajadili aina mpya ya utabiri wa kila siku kwa watumiaji wa radio lengo lao kusambaza taarifa ili ziweze kuwafikia kwa wakati. Aidha, amezitaka taasisi za maafa pamoja na Serikali kujiweka tayari kukabiliana na madhara yanayoweza kutokea, TMA haina budi kutoa taarifa zake mapema na kwa wakati ili ziwafikie wananchi na sekta husika mapema.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladslaus Chang'a akifungua warsha kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM). 
Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri - TMA, Bw. Samwel Mbuya akiwasilisha mada katika warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Law School of Tanzania Mawasiliano jijini Dar es Salaam. 
Mtaalamu (Utabiri) wa Hali ya Hewa, Elias Lipiki akiwasilisha mada kwa wanahabari katika warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Law School of Tanzania Mawasiliano jijini Dar es Salaam. 
Mwanahabari Faustin Shija kutoka Nipashe, akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA. 
Jerome Mshanga wa Clouds Media akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA kwenye warsha hiyo. 
Mwanahabari na Bloga, John Bukuku akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladslaus Chang'a akifafanua jambo kwenye warsha kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM).

MTANZANIA ASHIKWA NA KILO ZA DAWA ZA KULEVYA ALIZOMEZA NCHINI INDONESIA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MTANZANIA  Nabbed Abdul Rahman Asman (42) amekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bali nchini Indonesia baada ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya Methamphetamine ambazo alizimeza na kukutwa ndani ya tumbo lake. 

Jarida la Citizen limeeleza kuwa mamlaka ya usalama nchini Indonesia imeeleza hayo mapema jumanne, na hiyo ni baada ya mamlaka ya uhamiaji kitengo cha kuzuia dawa za kulevya kueleza kuwa walimkatama Nabbed Abdul Rahman Asman akiwa na dawa hizo uwanjani hapo mapema Januari 30 mwaka huu.

Imeelezwa kuwa zaidi ya kilo moja za  Methamphetamine zilizokuwa zimemezwa na Asman ziligundulika  kupitia mashine za x-Ray na Ct scan, Mamlaka hiyo imeeleza kuwa takriban vifuko 99 vilivyowekwa unga mweupe vilifika zaidi ya kilo moja.

Asman (42) anashikiliwa na vyombo vya dola nchini humo na bado haijafahamika kama atahukumiwa kifo na hiyo ni baada ya nchi hiyo (Indonesia) kuwa moja ya nchi ambazo zina msimamo na sheria kali dhidi ya dawa ya kulevya diniani.

Matukio mengine ya kukamatwa madawa ya kulevya nchini humo ni pamoja na lile la Husein Ashad Bhari (60) kukamatwa na kilogram 45 za Marijuana  na akahukumiwa miaka 15 jela, na wengine kadhaa waliokamatwa na dawa hizo kuhukumiwa kifo.

Upelelezi kesi ya Wema umekamilika

$
0
0

Na Karama Kenyunko
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesema Februari 21, mwaka huu itamsomea  maelezo ya awali (PH) msanii wa Filamu nchini,  Wema Sepetu anayekabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mitandaoni ya kijamii.

Hatua hiyo imefikiwa leo Februari 13, 2019 baada ya Wakili wa Serikali, Glori Mwenda kuieleza mahakama kuwa, upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuimba mahakama kupanga tarehe ya kumsomea mshtakiwa huyo PH.
Kufuatia taarifa hiyo Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, ameiahirisha kesi hiyo mpaka Februari 21, mwaka huu.

Wema ambaye alikuwa Miss Tanzania mwaka 2006,
anatetewa na Wakili, Ruben Simwanza, alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Novemba Mosi, 2018, kujibu shtaka hilo.

DKT. KIJAJI: FEDHA ZA MABORESHO YA SHULE KONGWE ZITUMIKE KWA LENGO LILILOKUSUDIWA NA KWA UBORA

$
0
0
Na Peter Haule, WFM, Korogwe
Serikali imewataka watendaji katika maeneo yote ambayo fedha zimetolewa zikiwemo sh. bilioni 18 za kuboresha shule kongwe nchini, kusimamia matumizi yake ipasavyo ili kufikia lengo lililokusudiwa na kwa ubora unaotakiwa.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, alipotembelea na kukagua maboresho ya Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Korogwe, Mkoani Tanga, ambayo hivi sasa imekuwa ya kisasa na mwonekano mzuri.

Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali imeamua kutekeleza kazi zake nyingi kwa mfumo ujulikanao kama Force Account, ambao unatoa fursa kwa Wakandarasi wazawa kushiriki kikamilifu kwa lengo la kufanikisha maendeleo kwa gharama nafuu na kwa ubora unaotakiwa.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe, Bi. Annisia Mauka, katika taarifa ya utekelezaji wa maboresho ya shule hiyo, alisema,   Serikali, kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) iliwapatia kiasi cha  Sh. bilioni1.3 kwa ajili ya kujenga miundombinu 27 ya Shule, ikiwemo umeme, majisafi na taka na pia Mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

“Tumefanikiwa kukarabati majengo 26 ambayo ni pamoja na  vyumba vya madarasa 23,  maabara, maktaba, jengo la utawala, mabweni, bwalo la chakula, vyoo vyenye matundu 116, jengo la Zahanati, Mfumo wa Maji taka na safi na pia mfumo wa kupikia kwa njia ya nishati ya gesi” alifafanua Bi. Mauka.

Alisema kuwa hadi sasa fedha zilizotumika kununulia vifaa ni takribani Sh. bilioni 1.05 huku gharama za ufundi zikiwa Sh. milioni 315.9 hivyo kusalia na zaidi ya Sh. milioni 2.09.

Bi. Mauka, ameiomba Serikali kufanikisha ujenzi wa Bweni jipya linalogharimu zaidi ya Sh. milioni 109.6 kwa kuwa Bweni hilo lilishindikana kufanyiwa maboresho kwa kuwa uharibifu wake ulikua mkubwa baada ya kufanyiwa tathmini ya kina, pia aliiomba Serikali kufanikisha ujenzi wa ukuta wa Shule hiyo kwa kuwa kukosekana kwa ukuta huo kunahatarisha usalama wa wanafunzi na watumishi wengine.

Naibu Waziri Dkt. Kijaji, ameahidi kufanyia kazi maombi hayo kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mhe. Mary Chatanda, na kutoa agizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, kufanya tathmini ya gharama ya ukuta huo ili kujua gharama halisi  kwa lengo la kupata fedha za ujenzi ili kulinda usalama wa Wanafunzi.

Dkt. Kijaji, aliupongeza Uongozi wa Shule na Wadau wengine kwa kuwezesha ukarabati Mkubwa wa Shule hiyo hivyo kurudisha hadhi yake na kuwa sehemu bora ya wanafunzi kupata taaluma kwa viwango vya juu.

Akizungumza na wanafunzi wa Shule hiyo Dkt. Kijaji aliwataka kusoma kwa bidii ili kuweza kufaulu masomo yao na kuwa chachu ya maendeleo ya Taifa na pia kuwa viongozi imara wa baadae.

Jumla ya Sh. bilioni 18 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya ukarabati wa Shule Kongwe za Sekondari 17 kuanzia mwaka wa Fedha 2016-217.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe Annisia Mauka, akisoma taarifa ya utekerezaji wa maboresho ya Shule hiyo yaliyogharimu takribani Sh. bilioni 1.374, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), Wilayani Korogwe MkoaniI Tanga.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe katika moja ya Jiko la Gesi la Shule hiyo, kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Zena Said.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia) akiongozwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe Bi. Annisia Mauka (katikati) kukagua maboresho ya Shule hiyo iliyogharimu takribani Sh. bilioni 1.3. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bi Kissa Gwasongwa.
 Muonekano wa baadhi ya majengo ya Sekondari ya Wasichana Korogwe yaliyokarabatiwa.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wanne kulia) akifurahia jambo na wanafunzi wa kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maboresho ya shule hiyo uliogharimu takribani Sh. bilioni 1.374, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bi Kissa Gwasongwa na wapili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Zena Said.
 Mwanafunzi wa kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe, Mesi Swai, akimuahidi  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) kwa niaba ya wenzake kusoma kwa bidii ili wafaulu vizuri na kuweza kuchangia katika maendeleo ya nchi.
 Wanafunzi wa kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe wakifanya Jaribio la Somo la Uraia, wakati wa ziara ya Kikazi ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) Shuleni hapo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na Marietha Yohana na wanafunzi wengine wa kidato cha kwanza ambao ni walemavu, katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe ambapo alisema wana nafasi ya kufanya vizuri katika masomo yao na kuwa msaada mkubwa kwa Taifa siku za usoni.
(Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango)

RAIS DKT. SHEIN AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYA YA MAGHARIBI A UNGUJA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Kinga Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed, baada ya kuweka jiwe la Msingi Kituo hicho cha Afya kilichojengwa na Mradi wa Tasaf na Nguvu za Wananchi wa Shehia ya Kianga,wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Magharibi A Unguja leo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Kinga Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed, (katikati) anayefuata ni Daktari Dhamana Wilaya ya Magharibi A Unguja. Dkt.Amina Hussein, na wa mwisho Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Haji Omar Kheri.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akipanda mti wa muembe katika eneo la Kituo cha Afya Kianga Wilaya ya Magharibi A Unguja baada ya kuweka jiwe la msingi leo, akiwa katika ziara yake katika Wilaya hiyo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Kituo cha Afya Kianga, Wilaya ya Magharibi A Unguja, akiendelea na ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo.
 MKURUGENZI Mkuu wa TASAF Tanzania Ndg. Ladislous Mwamanga, akizungumza na kutoa salamu za Tasaf wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Kituo cha Afya katika Kijiji cha Kianga kilichojengwa na Mradi wa TASAF, na nguvu za Wananchi wa Kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi A Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Ndg. Abdallah Hassan Mitawi akitowa maelezo ya Kitaalam ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Kianga wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi leo, wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, katika Wilaya hiyo, Kituo hicho kimejengwa kupitia Mradi wa TASAF.
 JENGO Jipya la Kituo Cha Afya Kijiji cha Kianga lilijengwa na Tasaf na Nguvu za Wananchi kilichowekwa jiwe la Msingi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, leo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Magharibiu A Unguja,leo.(Picha na Ikulu)

Europa League: Arsenal ugenini kwa watengeneza magari BATE Borisov

$
0
0
Pengine ulikuwa hujui jina BATE ni kifupisho cha Borisov Automobiles and Tractor Electronics, ndio! Nimetaja trekta, FC BATE inamilikiwa na kiwanda cha magari huko nchini Belarus. FC BATE wameshinda taji la Ubingwa wa ligi kuu ya Belarus mara 13 mfululizo, hawa ndio watawakaribisha Arsenal katika uwanja wa Borisov Arena Alhamisi hii majira ya saa 2:55 Usiku.

Mchezo wa Arsenal ni moja kati ya 16 itakayochezwa Usiku wa Alhamisi hii katika hatua ya 32 bora. Michezo ambayo kwa hapa Tanzania itarushwa na kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee kupitia chaneli zao za michezo.

Kwa upande wao Arsenal huenda wakaendelea kumkosa mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Americk Aubameyang ambaye ni mgonjwa. Hata hivyo Arsenal watajipa matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo baada ya kushinda mchezo wa ugenini dhidi ya Huddersfield 2-1 katika ligi kuu ya Uingereza. Itakumbukwa pia msimu uliopita Arsenal waliichapa BATE 4-2 ugenini na kisha 6-0 katika dimba la Emirates, hivyo wataingia uwanjani historia ikiwabeba.

Kwa upande wa Chelsea wao watahitaji kuwa na utimamu wa kimchezo baada ya kufungwa ugenini kwa Manchester City kwa magoli 6-0 Jumapili iliyopita. Chelsea pia watakuwa ugenini nchini Sweden kucheza dhidi ya Malmo FF. Malmo imewahi kushinda mara moja tu dhidi ya timu za Uingereza. Mechi hii itaruka LIVE majira ya saa 5:00 Usiku kupitia ST World Football pekee.

Michezo mingine itayakayochezwa Alhamisi Usiku Saa 2:55 ni SS Lazio vs Sevilla (Sports Premium), Krasnodar vs Leverkusen (Sports Arena) na ile ya Saa 5:00 Usiku ni Sporting CP vs Villarreal (Sports Focus), Celtic FC vs Valencia CF (Sports Arena), FC Zurich vs Napoli SSC (Sports Premium) na nyingine zote kupitia chaneli za michezo sa StarTimes.

Michezo yote ya Europa league inaonekana kupitia StarTimes ambapo mteja anatakiwa kulipia kifurushi cha kati, kwa upande wa Antenna ni MAMBO Tsh 14,000 pekee na kwa upande wa dish ni SMART kwa Tsh 21,000 pekee. Pia mechi za Arsenal na Chelsea zina uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili.


Wadau wakutana kujadili mfumo wa kwenda katika Bima ya afya kwa Wote

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Wadau mbalimbali wamekutana kujadili namna ya kwenda katika Bima ya afya ya wote ili kusaidia wananchi kuwa na uhakika wa matibabu.  Wakizungumza katika na waandishi habari jijini Dar es Salaam wamesema kuwa kuwa katika huduma za Afya zinazotolewa na mfuko wa bima ya afya ya Jamii (CHF) umefanikiwa  na sasa kwenda na Bima ya afya kwa kutokana kwa kuandaliwa kwa mswada wa sheria wa bima ya afya kwa wote.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto  na Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Subi amesema kuwa Tanzania imefanya vizuri katika mfuko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa Afrika Mashariki na kufanya watu wengine kuja kujifunza hivyo sasa ni kwenda katika Bima ya afya kwa wote kufikia 2030. Amesema serikali  imewekeza nguvu kubwa katika sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya ikiwemo  na kuja na Bima ya afya kwa wote.

Dkt.Subi amesema kuwa watu wanaopata huduma za bima ya afya ni asilimia 33 hivyo kwa asilimia 67 iliyobaki itafikiwa katika na Bima ya Afya kwa wote. Amesema vituo vya afya 300 vimejengwa huku vingine vikiwa vimeboreshwa katika kipindi kifupi huku upatikanaji wa dawa muhimu ni asilimia 90 na Hospitali 67 zimeboreshwa. Nae Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma Afya Ofisi ya Rais-Tamisemi  Anna Nswila  amesema kuwa mkutano huo utakuja namna ya kufikia utoaji wa bima ya afya kwa wote na serikali imewekeza katika sekta ya afya katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na uhakika wa matibabu.

Amesema kuwa uchumi wa viwanda unategemea na wananchi kupata matibabu bima ya afya katika kufanya wananchi washiriki katika fursa za uchumi mbalimbali. Kiongozi wa mradi wa Tanzania Health  Promotion (TPH)  Profesa Manoris Meshack amesema kuwa mradi wa CHF umefanikiwa katika mikoa 17 na unaendelea na kwenda hivyo bima ya afya kwa wote utakuwa umejibu changamoto mbalimbali za upatikanaji wa matibabu kwa wananchi.

Amesema kuwa mradi ulikuwa umejikita katika mikoa mitatu ya Singida , Morogoro pamoja na Dodoma na matokeo yake yamekuwa na ufanisi. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu atakuwa mgeni rasmi katika ufungaji mkutano huo wa kwenda katika Bima ya afya kwa wote.
 Kiongozi wa mradi wa TPH , Profesa  Manoris Meshack akizungumza namna mradi ulivyofanikiwa na kuamua kukutana kujadili masuala mbalimbali ya kwenda katika Bima ya afya kwa wote.
 Mkurugenzi Msaidizi  wa Huduma za Afya wa Ofisi ya Rais-Tamisemi Anna Nswila akizungumza namna na wakijipanga katika sera ya kwenda utoaji huduma ya bima ya afya kwa wote.
 Baadhi ya wadau katika mkutano wa kujadili kwenda katika Bima ya afya wote.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto na Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara hiyo Dkt Leonard Subi akizungumza na waandishi habari kuhusiana na wadau kujadili bima ya afya kwa wote katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

ZAIDI YA MILIONI 200 ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI ZAWARUDISHA SHULENI WANAFUZI 1701 WA KIDATO CHA KWANZA MKURANGA

$
0
0
 Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega amefanikiwa kumaliza changamoto katika sekta ya elimu iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Wilaya ya mkuranga kwa kipindi kirefu hasa kwa watoto walifaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kushindwa kuripoti kutokana na ukosefu wa madarasa.
Akizungumza na wananchi  wa Mkuranga wakati alipokuwa akikagua  shule 3 za sekondari zilizojengwa kwa nguvu ya wananchi kwa kushirikiana na serikali katika kata za Njia nne, Mwandege na kata ya Tambani, Ulega amesema kuwa serikali ya awamu ya Tano imetoa zaidi ya milioni 200 ili kumalizia shule hizo ili wanafunzi waweze kuanza masomo mara moja.

Amesema kuwa awali palikuwa na changamoto kubwa na hivyo kupelekea wanafunzi waliomaliza darasa la saba mwaka jana kukosa shule ya sekondari huku wakiwa na ufaulu wa hali ya juu, amezitaja shule zilizopata msaada huo kutoka kwa serikali ni pamoja na Mwandege, Njia nne na  shule iliyopewa jina lake la Abdala Ulega sekondari.

“Wazazi wenzangu mnatakiwa kuwasimamia watoto wetu waweze kuwa katika maadili mema ili kuwa mfano wa kuigwa nchini kwani itafikia hatua mimi nitastaafu hivyo lazima tuwe na wasomi wengi katika wilaya yetu ya mkuranga na hiyo yote elimu ndio msingi mkubwa.” amesema Ulega.

Aidha Ulega ametoa mifuko 40 ya saruji,  zaidi ya milioni tatu kwa kila  shule ili kuhakikisha mwezi wa tatu wanafunzi hao wanaanza shule mara moja ili kutowaweka wanafunzi hao katika hatari nya kupata vishawishi vitakavyokatisha ndoto zao hasa mimba.

 Kwa upande wake Afisa elimu wa sekondari wa Wilaya hiyo  Benjamini Majoya amempongeza Naibu waziri  kwa jinsi anavyopambania elimu katika wilaya hiyo ili iweze kukua na hiyo ni kwa namna  anavyojitolea katika kuhakikisha miundombinu inakuwa rafiki kwa wanafunzi.

Akitoa taarifa za elimu wilaya humo Afisa elimu huyo amesema  kuwa mara baada ya Serikali kutoa kiasi cha pesa hicho kupitia kwa Naibu waziri Ulega shule hizo zitakamilika haraka na wanafunzi 1071 ambao bado hawajaanza shule wataanza  mara moja na  kumaliza changamoto kwa wanafunzi hao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Firbeto Sanga amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imekuwa ni serikali ya utekelezaji kwa vitendo kuliko maneno hasa katika kuhakikisha sekta muhimu zinaangaliwa kwa makini Zaidi.

Aidha amempongeza Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega kwa jinsi anavyopambania kuipaisha wilaya hiyo katika masuala ya maendeleo mbalimbali hasa miundombinu ya barabara, shule, hospitali mengine mengi.
 Naibu Waziri Mifugo na Vuvi (MB) wa Mkurangara , Abdallah Ulega akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa katika kata Njianne, Mwandege na Tambani, leo Wilayani Mkuranga.(Picha zote na Emmanuel Massaka,MMG)
 Naibu Waziri Mifugo na Vuvi (MB) wa Mkurangara, Abdallah Ulega akikagua madarasa yaliyojengwa na wananchi pamoja na Serikali huku ikitegemewa Machi mwaka huu yataanza kutumika kwa wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza, leo Wilayani Mkuranga.
Afisa Elimu wa Sekondari wilaya ya Mkuranga,Benjamini Majoya akiwahakikishia wazazi na walezi wa wilezi shule hizo zitafunguliawa mwezi wa tatu mwaka huu,(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Muonekano wa Madarasa ya shule hizo ambazo ni; Shule ya Sekondari iliyopewa jina la mbunge huyo Abdallah Ulega, Tambani na Njia nne.

WIZARA YATOA MASAADA WA KISAIKOLOJIA KWA FAMILIA ZILOATHIRIKA NAMATUKIO YA MAUAJI NJOMBE

$
0
0
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara Ustawi wa Jamii imetembelea kuwapa pole na kutoa msaada wa kisaikoloji na kijamii kwa Familia zilizoathirikana mauaji ya Watoto yalitokea mkoani Njombe.

Timu hiyo imetembelea  Familia ya Bw. Gorden Mfugale inayoishi Mtaa wa Joshoni Kata ya Mji Mwema Halmashauri ya Mji Njombe Wilayani Njombe iliyopoteza Mtoto mmoja wa kiume Gidrack Mfugale (5) aliyepotea tarehe 04/02/2019 na kupatika tarehe 10/02/2019 akiwa amefariki dunia huku kiganja cha mkono kikiwa  na  mwili wake ulikutwa na majeraha kichwani katika  eneo la Shule ya Sekondari Njombe.

Akizungumza katika ziara hiyo Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu amesema kuwa Wizara imeamua kujumuika na wanafamilia hao kwa kuja kuwapa msaada wa kisaikolojia na kijamii ili kuondokana na msongo wa mawazo unaotokana na tukio lililompata Mtoto wao.

"Tumeguswa sana na msiba huu na matukio ya mauaji  yaliyotokea na kwa niaba ya Wizara tunawapa pole kutokana na majanga haya na tuko pamoja kuhakikisha mnapata msaada muhimu ya kisaikoloji na kijamii" alisema

"Na Wizara haitowatembelea ninyi tu bali Timu ya Wataalam wengine wa Wizara na Mkoa wapo katika familia nyingine huko wakifanya haya tunayoyafanya hapa" alisema

Naye Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Rehema Kombe amesema kuwa msaada wa kisaikolojia na kijamii ni muhimu sana kwa familia zilizokumbwa na matatizo hayo ya mauaji ya watoto kwani familia zimekumbwa na taharuki kubwa.

“Suala la hili la msaada wa kisaikolojia na kijamii kwa wanafamili hizi ni muhimu sana kwa watu hao na tutawasaidia sana ili kuondokana na msongo wa mawazo unaotokana na vitendo walivyofanyiwa watoto wao" alisema

Pia Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Njombe Bi. Teresia Yomo amesema kuwa mkoa umejipanga kuendelea kuzitembelea familia zote kwa kushirikiana na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri zote za Wilaya ya Njombe ili kutoa msaada wa kisaikolojia na kijamii kwa familia zote sita zilizopatwa na matukio haya ya mauaji ya watoto wanane mkoani Njombe.

Kwa upande wake Bw. Gorden Mfugale aliyepoteza mtoto wake Gidrack Mfugale (5) amewashukuru wataalam hao kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wameona umuhimu wa kuwasaidia ili kuomdokana na msongo wa mawazo unaotokana na vitendo walivyofanyiwa watoto wao.

“Asanteni sana kwa kuja kutuona na kutupa pole na tunashukuru kwa kutuletea masaada wa kisakolojia na kijamii utatusaidia sana kurudi katika hali yetu ya kawaida sio kwangu tu hata kwa familia nyingine zilizokubwa na matatizo kama yetu” alisema.

Wizara ya  Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara Ustawi wa Jamii ipo mkoani Njombe kwa kushirikiana na Wataalam wa Mkoa huo katika jitihada ya kutoa msaada wa Kisaikolojia na kijamii kwa familia zilizoathirika na matukio ya mauaji ya watoto mkoani Njombe.
 Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu(mbele) akiongoza timu hiyo na ya wataalam kutoka Mkoa wa Njombe kuitembelea familia ya Bw. Gordeni Mfugale  iliyopoteza Mtoto mmoja katika mauaji 8 yaliyotokea Mkoani Njombe   wakati Wataalam hao walipoitembelea familia hiyo leo.
 Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu (wa tatu kulia) akizungumza na familia ya Bw. Gordeni Mfugale iliyopoteza Mtoto mmoja katika mauaji 8 yaliyotokea Mkoani Njombe wakati Wataalam hao walipoitembelea familia hiyo leo.
Golden Mfugale(wa pili kushoto) aliyopoteza Mtoto mmoja katika mauaji 8 akizungumza na Timu ya Watalaam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Wataalam kutoka Mkoa wa Njombe wakati Wataalam hao walipoitembelea familia hiyo leo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano W

JKCI watwaa tuzo za wafanyakazi bora

$
0
0
 Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli Rweyumamu (kulia) akipokea tuzo kwa niaba ya daktari bora wa mwaka Tryphone Kagaruki wakati wa hafla fupi ya utoaji wa tuzo kwa wafanyakazi bora wa mwaka iliyotolewa na kampuni ya dawa za binadamu ya Atco/Samiro na kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya huduma ya uuguzi wa JKCI Robert Mallya hivi karibuni katika taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
 Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hilda Karau akipokea cheti cha mfanyakazi bora wa mwaka kilichotolewa na kampuni ya dawa za binadamu ya Atco/Samiro na kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya huduma ya uuguzi wa JKCI Robert Mallya hivi karibuni katika taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete( JKCI) Delila Kimambo pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya huduma ya Uuguzi wa Taasisi hiyo Robert Mallya wakionyesha kipeperushi kinachoitambulisha dawa ya aspirini kama moja ya dawa zinazotumika kwa wagonjwa wa moyo baada ya wasilisho la matumizi ya dawa hiyo hivi karibuni katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Waliosimama nyuma ni baadhi ya madaktari bingwa wa moyo wa taasisi hiyo pamoja na wadau kutoka kampuni ya dawa za binadamu ya Atco/Samiro
Picha na: - JKCI

UNITED BANK FOR AFRIC (UBA) BANK DONATES LITERATURE BOOKS TO SECONDARY SCHOOLS IN KISARAWE DISTRICT

$
0
0
  In efforts to support the government in offering quality education in secondary schools, UBA Tanzania through UBA Foundation donated Literature textbooks worth TZS 6,400,000 to Kimani and Makurunge Secondary Schools of Kisarawe District, Coast Region.

The donation of the books was received by the Makurunge Secondary School Head Teacher Hassan Ruheye and Kimani Secondary School Mika Bareri on behalf of the school management.

Speaking after receiving the books, the Makurunge Secondary School Head Teacher Hassan Ruheye said that it was important to recognize the efforts which are being made by private institutions like UBA Tanzania in supporting education sector in the country. “We all understand that our government agenda is on industrialization, but we cannot have industries without good performance and adequate teaching materials in our schools. These books will increase the ability our students in performing good in literature and also in other subjects and in return will reach the government goal on industrialization”, Ruheye said.

Ruheye added “I call upon UBA Tanzania and other stakeholders to continue supporting us in other areas of our school so that we can create a good environment for our students”.

On his part, UBA Bank Tanzania Chief Operating Officer Flavia Kiyanga said that the bank believes in a society were learners get their education on a good environment and schools with learning equipment’s like textbooks. On that case, it’s good to invest on our children’s education and that has been fulfilled by donating these books to Kimani and Makurunge Secondary Schools.

UBA Tanzania has for a long time been supporting the education sector in our country. For that reason, the Bank was recognized by Tanzania Education Authority in 2018 among others as an institution that supports learning, UBA Foundation through its Read Africa Initiative has invested on the African youth to promote learning and a reading culture by donating various literature books to schools in Africa. To achieve this, we have been working with various institutions and I must thank the government for their support as UBA Foundation has been successful, said Kiyanga.

Kiyanga added that English language has been one of the barriers for students to perform well in their final exams. By donating these literature textbooks, we are creating an environment for our students to develop a culture of reading for themselves. We trust that these books will empower these students to perform well in their subjects and also increase the number of students taking who will be performing well in the final exams, said Kiyanga adding that UBA Tanzania will continue supporting schools in the country in various areas aiming at building students for a bright future.

Speaking on behalf Kimani and Makurunge Secondary Schools, the Kisarawe District Secondary School education officer Patrick Gwivaha said the UBA donation has come at the right time as the schools has been facing shortage of various textbooks something which has been affecting the academic performance. I take this opportunity to promise that we will take proper care of these books for the advantage of us and the coming generation.

He added ‘the shortage of textbooks in our schools has been affecting us very much considering that the geographical location of our district that makes it difficult for well-wishers like UBA to reach us. We really thank UBA Bank Tanzania for their support!
UBA Bank Tanzania Chief Operating Officer Flavia Kiyanga hands over literature textbooks to Kisarawe District Commissioner Jokate Mwegelo over the weekend. The UBA Bank Tanzania through UBA Foundation donated literature textbooks to Kimani and Makurunge Secondary Schools in Kisarawe District, Coast Region aimed at improving the school’s student’s performances.
Kimani Secondary School students take a reading of literature books donated by UBA Bank Tanzania to the school. The UBA Bank Tanzania through UBA Foundation donated literature textbooks to Kimani and Makurunge Secondary Schools in Kisarawe District, Coast Region aimed at improving the school’s student’s performances.

UBA Bank Tanzania Head of Marketing and Corporate Communications Brendansia Kileo distribute literature textbooks to Kimani Secondary School over the weekend. The UBA Bank Tanzania through UBA Foundation donated literature textbooks to Kimani and Makurunge Secondary Schools in Kisarawe District, Coast Region aimed at improving the school’s student’s performances.
UBA Bank Tanzania Chief Operating Officer Flavia Kiyanga speaks to students of Makurunge Secondary before handing over literature textbooks to the school. UBA Bank Tanzania through UBA Foundation donated literature textbooks to Kimani and Makurunge Secondary Schools in Kisarawe District Coast Region aimed improving academic performance to students.

Makurunge Secondary School students display literature textbooks donated by UBA Bank Tanzania. The UBA Bank Tanzania through UBA Foundation donated literature textbooks to Kimani and Makurunge Secondary Schools in Kisarawe District, Coast Region aimed at improving the school’s student’s performances
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images