Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WATUHUMIWA WA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI

$
0
0

Jeshi la Polisi Makao Makuu  Kitengo Maalum cha Kupambana na uhalifu kikiongozwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas (pichani), kwa kushirikiana na Jeshi  la  Polisi Mkoa wa Njombe leo tarehe 12/02/2019 limefanikiwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa watatu wa mauaji ya watoto Mkoa wa Njombe.


Kati ya hao watuhumiwa ni pamoja na mhusika wa mauaji ya watoto wa familia moja  anayetambulika kwa jina la  Joel Joseph Nziku mwenye umri wa miaka 35 na mkazi wa Magegere,  Makambako


 Inadaiwa Joel Joseph Nziku  alihusika na mauaji ya watoto hao siku ya jumamosi tarehe 19.01.2019 majira ya saa moja jioni, watoto hao ni Godliver Nziku miaka 12, Gasper Nziku miaka 7 na Giliad miaka 5 wote  wakiwa wa familia moja ambao baba yao alifahamika kwa jina la Danford  Nziku miaka 52 mkazi wa kijiji IKando wilaya ya Makambako mkoani Njombe


Aidha Naibu kamishna Sabas amesema kwa sasa  Mkoa wa Njombe na nchi kwa ujumla ni salama na amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano baina yao na Vyombo vya Ulinzi na  Usalama



WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA MKOANI ARUSHA KESHO, KUFUATILIA MAAGIZO YAKE, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Arusha. 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewasili jijini Arusha leo, kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi ya siku kumi kwa kutembelea Wilaya zote za Mkoa huo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake. 
Waziri Lugola anatarajia kuanza ziara hiyo rasmi kesho Februari 13, 2019 jijini humo kwa kukutana na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na kupokea taarifa ya Kamati hiyo, kabla ya kuanza kuzungumza na Wakuu wa vyombo vyake na baadaye atakutana na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa, na kumaliza kwa kuzungumza na Baraza la Askari na Watumishi wote wa Wizara hiyo waliopo jijini humo. 

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, leo, Lugola amesema baada ya kuzungumza na Askari na Watumishi wa Wizara yake pamoja na kupokea changamoto zao, atafanya mkutano mkubwa wa hadhara wa wananchi utakaofanyika katikati ya Jiji hilo ili wananchi wengi waweze kufika kwa wingi na aweze kusikiliza kero zao na Waziri huyo kuweza kuzitatua. 

“Nitafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika jiji la Arusha, ambapo utaanza saa 10:00 hadi 12:00 jioni, hivyo nawaomba wananchi wa Jiji hili wajitokeze kwa wingi kunisikiliza kile ambacho nimepanga kuwaambia na pia nitawapa nafasi wananchi waulize maswali bila woga, waniambie kero zao nami nitazitatua katika mkutano huo,” alisema Lugola. 

Pia Lugola alisema lengo la ziara hiyo ni kufuatilia maagizo yake mbalimbali ambayo aliyatoa mwaka jana 2018 katika mikutano yake kama yalifanyiwa kazi na viongozi wa Taasisi anazoziongoza au yalipuuzwa, yakiwemo ya dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe. 

Lugola alisema katika ziara yake aliyoifanya mwaka jana Mkoani Kigoma na mwezi Januari Mwaka huu Mkoa wa Kagera, aligundua wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo hawezi kulala akiwa ofisini, lazima afanye ziara nchi nzima kuwasaidia wananchi kutatua kero zao ambapo wengi wao wakiwalalamikia Polisi wakiwaonea. 

Waziri Lugola ameongeza kuwa, kupitia mikutano yake ya wananchi mkoani Kigoma na Kagera ndipo ameamua kufanya ziara ya tatu kwa kuutembelea Mkoa wa Arusha ambao changamoto zake zinafanana kwa sehemu kubwa kwa kuwa mikoa hiyo ni ya mipakani na changamoto kubwa ni uwepo wa wahamiaji haramu pamoja na matukio kadhaa ya ujambazi ambayo kwa kiasi kikubwa Serikali inaendelea kuyadhibiti. 

“Wananchi wanapojitokeza kwa wingi inasaidia kusikiliza matatizo yao yanayowakabili, ndio mana nimepanga kufanya ziara kama hizi nchi nzima, hii inasaidia sana kujua matatizo mbalimbali ya wananchi pamoja na kuangalia utendaji kazi wa Taasisi zangu zilizopo ndani ya Wizara hii, na hakika Serikali ya Rais Dokta John Magufuli inawajali wananchi wake ndio mana inawafuata mahali walipo, ili wazungumze na Serikali yao uso kwa uso,” Alisema Lugola. 

Waziri Lugola baada ya kumaliza ziara yake Jijini Arusha, ataenda Wilaya ya Arusha ambayo itakua Februari 14, Meru Februari 15, Arumeru, baadaye Longido, Monduli, Karatu na ataimaliza ziara yake akiwa Wilaya ya Loliondo mkoani humo. 

Katika Wilaya zote atakazozitembelea pia atazungumza na wananchi pamoja na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni ambayo jukumu lake kuu ni kupunguza msongamano gerezani na kusimamia wafungwa waliopewa adhabu mbadala na Mahakama au wafungwa waliopata msamaha kupitia sheria ya huduma kwa jamii na kutumikia kifungo chao nje ya Gereza.

Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii. 

JUMLA  ya Mashahidi 54 na vielelezo 218 vinatarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi, katika kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA), Harry Kitillya na wenzake wanne kwa ajili ya kwenda kuanza kusikilizwa.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni  Maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, Kamishna wa Sera ya uchambuzi wa Madeni kutoka Wizara Fedha na Mipango, Bedason Shallanda na msaidizi wake Alfred Misana ambapo wote wanakabiliwa na mashtaka 58 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Hatua hiyo imekuja huku tayari Kitilya na wenzake wawili Shoe na Sioi wakiwa wamekaa gerezani kwa takribani miaka mitatu ambapo walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Aprili 16, 2016. Kesi hiyo imehamishiwa Katika mahakama ya mafisadi leo Februari 12, 2019 mara baada ya washtakiwa kusomewa upya mashtaka yao na kutajiwa Idadi ya mashahidi na vielelezo vitakavyowasilishwa wakati wa ushahidi. 

Baada ya kusomewa maelezo hayo,  Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi aliwauliza washtakiwa kama walikuwa na lolote la kuongeza ambapo wote walidai kuwa hawana cha kuongeza. Kufuatia hayo,  mahakama hiyo imetoa amri ya kuhamishia shauri hilo Mahakama Kuu Kitengo cha mafisadi.

Wakati watuhumiwa wakisomewa maelezo hayo ya mashahidi (Commital) upande wa mashtaka uliwasilishwa na jopo la mawakili watatu, walii wakiongozwa na Wakili Mkuu wa serikali,  Fredrick Manyanda,  wakili wa serikali Mkuu Tumaini Kweka na wakili wa serikali George Barasa.
Aidha upande wa utetezi uliwasilishwa na jopo la mawakili  watatu wakiongozwa na Cuthbert Tenga akisaidiana na Alex Mgongolwa pamoja na Majura Magafu. Miongoni mwa mashahidi wanaotarajiwa kuitwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, aliyekuwa mwanasheria Mkuu Wa Serikali, Fredrick Welema.

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kughushi, moja la kuongoza uhalifu,  49 utakatishaji fedha, mawili ya kutoa nyaraka za uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanyanyifu moja na shtaka moja la kutoa nyaraka kwa nia ya kumdanganya kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango. 

Wanadaiwa  kati ya Machi 15, 2013 na Januari 10, 2014 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kudanyanya washtakiwa wote walijipatia Dola za Kimarekani Milioni sita wakionesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji wa upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd. 

RAIS DKT. SHEIN AFANYA ZIARA WILAYA YA MJINI NA KUWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MNARA WA TANGI LA MAJI KILIMANI

$
0
0
MNARA wa Tanki la Maji Safi na Salama linalojengwa katika eneo la Mnara wa Mbao Kilimani Zanzibar, likiendelea na ujenzi wake, lililowelkwa jiwe la Msini leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara yake Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi ya Maendeleo ya Wilaya hiyo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wajenzi wa Kampuni ya Stecol kutoka China wanaojenga Mnara huo wa Tangi la Maji katika eneo la Mnara wa Mbao Kilimani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Mradi ya Ujenzi wa Tanki Jipya la Maji linalojengwa Mnara wa Mbao Kilimani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mnara wa Tanki la Maji Safi na Salama katika eneo la Kilimani Mnara wa Mbao Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Waziri wa Ardhi.Maji Nishati na Makaazi Zanzibar Mhe. Salama About Talib, wakati akiwasili katika viwanja vya Ujenzi wa Mradi wa Mnara wa Tanki la Maji kilimani Mnara wa mbao Zanzibar, akiwa katika ziara yake Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Ndg.Mussa Ramadhan Haji, akitowa maelezo ya ujenzi wa Mradi Mnara wa Tanki la Maji katika eneo la Mnara wa Mbao Kilimani akiwa katika ziara yake Wilaya ya Mjini Unguja,kushoto kwa Rais Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kulia Waziri wa Ardhi.Maji Nishati na Makaazi Zanzibar. Mhe. Salama Aboud Talib.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kulia Waziri wa Ardhi Maji Nishati na Makaazi Mhe. Salama Aboud Talib, wakiimba wimbo wa Sisi Sote Tumegomboka, wakati  ziara yake katika Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)
/MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud. Akizungumza wakati wa Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Mnara wa Tangi  jipya la maji katika eneo la mnara wa mbao kilimani Zanzibar.(Picha na Ikulu)





Serikali yaimarisha Mazingira ya Uwekezaji-Kairuki

$
0
0
Na Grace Semfuko-MAELEZO 

Serikali imeweka mpango wa kuboresha mazingira ya Biashara na uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi mpango unaolenga kurahisisha vibali na upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa Viwanda na maeneo ya Kilimo. 

Hayo yamebainishwa Jijini Dar Es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye makao makuu ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC, baada ya kupokea ujumbe wa raia saba wa Hongkong China waliowasili Nchini wakiwawakilisha wafanyabiashara wa nchi hiyo waliokuja kufanya utafiti wa maeneo ya kuwekeza. 

Waziri Kairuki alisema hivi sasa Wizara yake iliyopo Chini ya Waziri Mkuu imeanza kuufanyia kazi mpango huo ambapo pamoja na kuimarisha uchumi wa Nchi kwa kuingiza fedha za kigeni pia utaongeza ajira kwa watanzania. 

“Sisi kama Serikali lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunaimarisha uwekezaji, mpango huo ambao ulifanyika mwezi Mei mwaka jana unalenga kuondokana na vikwazo vya kibiashara na kuharakisha vibali na kutoa ardhi kwa ajili ya uwekezaji, tunayafanya haya ili kuongeza ufanisi katika sekta ya uwekezaji, tunataka Watanzania wanufaike” alisema Angellah Kairuki. 

Alisema mwaka 2018 mwezi Mei Serikali iliweka mkazo katika andiko la mpango wa kuboresha biashara na uwekezaji pamoja na mpango mkakati wa kuhakikisha kuondoa vikwazo vya biashara mpango ambao unafanikiwa kwa kiwango kikubwa. 

Nae Jessica So ambaye ni Mwakilishi wa Balozi wa Heshima wa Tanzania Hongkong alisema lengo la ujio wao ni kufanya utafiti wa maeneo ya uwekezaji na kibiashara ambapo wanaanza kwa kuangazia maeneo manne yaliwepo ya Sekta ya Dawa, Kilimo cha Ufuta na Korosho pamoja na Sekyta ya Utalii. 

“Sisi ni ujumbe wa watu saba kutoka Hongkong China, tumekuja hapa kuangalia ni kwa namna gani tutashirikiana na Tanzania katika kuwekeza kwenye maeneo manne ya Dawa, Ufuta,Korosho na Utalii, tunawawakilisha wafanyabiashara wengine na tutawapelekea ujumbe wa tutakayoyaona hapa Tanzania” alisema Mwakilishi wa Wajumbe hao Jessica So Raia wa HongKong China. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Geoffrey Mwambe alisema tayari walishafanya mazungumzo na Mamlaka ya maendeleo ya biashara Hongkong ambayo inashughulikia biashara na uwekezaji kusaini makubaliano ya kuhakikisha wafanyabiashara wengi wanatumia fursa zilizopo Hongkong na Tanzania. 

Ujio wa Wajumbe saba kutoka Hongkong Nchini China ni sehemu ya wafanyabiashara wengi kutoka Jijini humo wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania hatua ambayo imekuja kufuatia kuwepo kwa hamasa ya uwekezaji na kuimarishwa kwa mazingira hayo nchini.

TANESCO Imetekeleza Mikakati ya Kumaliza Tatizo la Umeme Dar es Salaam, Pwani.

$
0
0
Na. MSAFIRI ULIMALI- MAELEZO.

Utekelezaji wa miradi ambayo itaisaidia Tanzania kufikia “Tanzania ya Viwanda” unazidi kutoa nuru, ambapo Serikali imejikita zaidi katika kutengeneza miundombinu rafiki ya kuzalisha umeme wa uhakika, Juhudi hizi za Serikali zilijikita zaidi vijijini; mradi wa umeme vijijini, sasa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kadhia ya umeme kwa wakazi na viwanda vya jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani inakwisha. 

Kazi ya ujenzi wa miundombinu ya kuweza kusimika Transfoma yenye uwezo wa MVA 300 sawa na Megawati 240, Ubungo, jijini Dar es Salaam, imepamba moto chini ya Mkandarasi wa ABB kutoka Switzerland, huku TANESCO ikisema ufungwaji wa Tranforma utaanza februari, 22 na wanatarajiwa kukamilisha rasmi mwezi Mei mwaka huu. 

Chombo hicho kitaongeza nguvu katika kituo cha umeme cha Ubungo kutoka MVA 300 hadi 600, sawa na MW 480, hapana shaka ni taarifa njema katika miji hii miwili kwani sasa wataondoka katika umeme wa mashaka na kuwa katika mwanga tosha na mahitaji ya viwandani kwa maendeleo ya jamii; majumbani na maofisini, pia ukuzaji wa uchumi wa viwanda na biashara. 

Afisa Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji anaeleza, “kuongezeka mahitaji ya umeme katika Mkoa wa Dar e salaam na Pwan, Serikali ya Awamu ya Tano, imeona kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza nguvu ya umeme katika Mkoa wa Dar es salaam Pwani.” 

Idadi ya watu, hususani kwa Mkoa wa Dar es Salaam inachangia kama sababu kubwa ya hitaji hilo la nishati ya umeme, inaelezwa kuwa Mkoa wa Dar es salaam pekee una jumla ya wakazi wapatao 5,465,420 huku Mkoa wa Pwani ukiwa na jumla ya 1,098,668; hawa wote wanahitaji nishati hiyo.

Msemaji huyo wa Tanesco alieleza kuwa hapo awali kituo cha umeme cha Ubungo kilikuwa na transfoma mbili ambazo kila moja ilikuwa na uwezo wa kutoa umeme wa MVA 150, na kuwa ongezeko la transfoma mpya itafikisha MVA 600, “kihesabu unaweza kusema ni ndogo, kifizikia ni nguvu kubwa itakayotoka hapo.” Alisema Leila

Ongezeko la idadi ya viwanda katika Mkoa wa Pwani ni moja ya sababu ya ujio wa Transfoma hiyo, kwa sasa Pwani inaonekana kama ndio Mkoa wenye viwanda vingi na vikubwa ukianzia Mkuranga, Kisarawe, Kibaha Mjini, Rufiji ,Mafia, Kibiti, Bagamoyo mpaka Chalinze, maendeleo haya makubwa ya uanzishwaji wa viwanda unachochea ongezeko la uhitaji wa nishati ya umeme. 

Katika kipindi cha mwaka 2018 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeweza kupata, mafanikio makubwa katika uboreshaji wa miondombinu ya usamabazaji wa umeme katika pande zote nchini kutokana na miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikiendelea.Kazi hiyo kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inaonyesha dhahiri dhamira ya kuondoa tatizo la umeme nchini ili kuondoa kadhia ya upatikanaji wa umeme kwa wananchi

Akifafanua kuhusu uwezo wa Transfoma hiyo, Mkuu wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme Ubungo, Mhandisi Joseph Msumali amesema uwezo wa kusukuma takribani Megawati 240 kutoka kwenye msongo wa Kilovoti 220 kuelekea Msongo wa Kilovoti 132 kwa ajili ya usambazaji na matumizi ya nishati ya umeme katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Hata hivyo ilikuwa ni kawaida kuona matangazo kwenye vyombo vya habari TANESCO ikiomba radhi kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo ya Pwani na Dar es Salaam, kwa kuhakikisha huduma zinapatikana, Shirika la Umeme Tanesco limeweza kuanza na mradi mpya ujulikanao Mradi wa kuimarisha Mifumo ya usambazaji umeme (TEDAP).

“huenda ikawa ni mara ya kwanza kusikia, hawa TEDAP wanajishughulisha na uondoaji wa mifumo yote ya zamani na kufanya ukarabati,” Afisa Mahusiano, TANESCO alifafanua. 

Mifumo mingi ya usambazaji ya umeme imekuwa chakavu jambo ambalo TEDAP imekuja na utaratibu wa kuhakikisha wanarekebisha kabla ya kutokea tatizo kubwa, na kwa sasa wameweza kufanikisha ukarabati sehemu mbalimbali ndani ya Mkoa wa Dar es salaam kwa asilimia 98, katika maeneo kama Mbagala, Gongo la Mboto, Kurasini pamoja na Kipawa, na mradi TEPAD uko kwenye hatua za mwisho.

Pamoja na jitihada za kukarabati, Tanzania imebarikiwa kuwa na nishati ya gesi ambapo miradi mingi mikubwa inatekelezwa kwa kasi ili nchi ifanikiwe kuwa na umeme wa kutosheleza hasa kwenye miradi mipya ya viwanda na reli ya kisasa (SGR),Pia na mahitaji ya jamii kwa ujumla.

Kwa sasa miradi mingi imekamilika kwa asilimia kubwa kama vile Mradi wa Kinyerezi 1 na Kinyerezi 2, huku kinyerezi 1 wenye jumla ya MW 150 ukipanuliwa ili kuongeza MW 180, zingine ambapo jumla ya MW 340 zitazalishwa, ikumbukwe kuwa nishati ya umeme wa gesi ni teknolojia mpya nchini itakayoweza kuzalisha umeme na kupunguza gharama za umeme nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanesco Dkt. Tito Mwinuka katika mkutano wake na wahariri Mkoani Arusha alionesha maono yake ya kuliona Shirika hilo likijiendesha kifaida zaidi, huku akionesha baadhi ya kazi ambazo zimeshaanza kufanyika na nyingine kukamilika. 

“Huwa nasema mbele ya wafanyakazi wenzangu, kwamba ningependa kuona TANESCO ambayo inafanya kazi kwa ufanisi na ndiko tunakokwenda, ndoto yangu ni kuona TANESCO inajiendesha kwa faida", Dkt. Mwinuka.
Mbali na maono hayo, Dkt. Mwinuka amehakikisha upatikanaji wa umeme katika maeneo muhimu ili kuhakikisha uendeshaji usiodorora katika viwanda ili bidhaa za viwanda vyetu ziweze kushindana katika soko la kimataifa.

“Katika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya umeme kama nguzo muhimu ya ujenzi wa Tanzania yenye viwanda, Serikali kupitia TANESCO hivi sasa inatekeelza miradi mikubwa ya umeme 22 kwa wakati mmoja na kwa fedha za Serikali.”Dkt. Mwinuka- Mkurugenzi Mtendaji TANESCO.

Tanesco imeendelea na utekelezaji wa miradi ya umeme ukiwemo ujenzi wa mradi wa Kinyerezi 1 extension MW 185, ufungaji wa mitambo na kukamilisha ujenzi wa kituo cha kupoza umeme ambapo shilingi bilioni164 fedha za ndani zimetengwa.Huku miradi mengine ianyoendelea kutekelezwa ni Mradi wa kuzalisha umeme Rusumo wa MW 80, Mtwara Power Project MW 300, Somanga Fungu MW 330 pamoja na Mradi wa Kakono MW 87.

RAIS WA ZANZIBAR NA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA WANACHAMA CCM WILAYA YA MJINI UKUMBI WA AMANI MKOA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, na kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Talib Ali TRalib, wakiwa wamesimama wakipiga makofi baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani , kuzungumza na Wana CCM wa Wilaya ya Mjini akiwa katika ziara yake leo.(Picha na Ikulu)

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na WanaCCM wa Mkoa wa Mjini waki wa ziara yake, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi na kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Ndg. Talib Ali Talib.(Picha na Ikulu)
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi akizungumza wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika Wilaya ya Mjini kabla ya kumkaribisha kuzungumza na Wana CCM wa Mkoa wa Mjini katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekitiu wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi, wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wa Afisi Kuu ya Mkoa wa Mjini Amani wakati wa mkutano wake na Wanachama wa CCM Mkoa wa Mjini, akiwa katika ziara yale leo(Picha na Ikulu)
 KATIBU Mkuu wa CCM Mkoa wa Mjini Ndg Mohammed Omar Nyawanga, akitowa Taarifa ya utekelezaji ya CCM Mkoa wa Mjini wakati wa Mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara yake Wilaya ya Mjini leo.(Picha na Ikulu)


 MBUNGE wa Jimbo la Amani Zanzibar Mhe. Mwalim Mussa Hassan Mussa akizungumza na kutowa neno la shukrani kwa niaba ya Wanachama wa CCM Mkoa wa Mjini, wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein. uliofanyika ukumbi wa mkutano wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar.(Picha na Ikulu)

 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa katika ukumbi wa mkutano Afisi  ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi na kushoto Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Bi. Leila Burhan Ngozi.(Picha na Ikulu)

CANADA KWA USHIRIKIANO NA SERIKALI YA TANZANIA YAENDESHA MAFUNZO YA MRADI WA KUKUZA AJIRA KWENYE SEKTA YA UFUNDI STADI NCHINI

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Serikali za Canada na Tanzania zinaendesha mradi wa miaka mitano wenye lengo la kusaidia vijana kuweza kuwa na umahiri wa kujiajiri na kujifunza kwa kutenda.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa vyuo vya ufundi nchini Dkt.Noel Mbonde wakati akifungua semina ya mradi huo inayoendelea jiji Arusha na kubainisha kuwa mradi huo utafikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa Kati wa viwanda.

Amesema kuwa mradi huo ulionza mwaka 2014 unatarajiwa kufika tamati Machi mwakani utasaidia Sana vijana kwani unalenga kumuwezesha kijana na mwalimu kuwa karibu na umeleta mabadiliko chanya nchini.

"Serikali imejipanga kuhakikisha mradi huu unakuwa endelevu baada ya kumalizika kwani tuna miradi mingi inaendeshwa nchini yenye lengo la kuongeza weledi kwa vijana wetu kuweza kufikia adhma ya serikali ya uchumi wa Kati wa viwanda"alisema Dkt.Mbonde.

Kwa upande wake mwakilishi wa Balozi wa Kanada nchini Tanzania bi Nathalie Garon amesema kuwa serikali ya nchi yake itaendeleza ushirikiano wa dhati kuhakikisha vijana wa kitanzania wanafikia malengo endelevu na nchi inapiga hatua.

Amesema MAFUNZO hayo ni moja ya ushirikiano Kati ya nchi yake na serikali ya Tanzania kuonyesha jinsi wanavyothamini vijana katika suala zima la KUKUZA maendeleo ya bara la Afrika.
Mwakilishi wa balozi wa Canada nchini bi Nathalie Garon ambaye pia ni karibu wa Kwanza wa maendeleo na kiongozi wa ukiaji endelevu wa uchumi wa ubalozi huo akifungua semina ya mradi wa kusaidia vyuo vya ufundi nchini unaondelea. Kwenye chuo cha Veta njiro jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Mkurugenzi wa elimu ya ufundi wizara ya elimu na ufundi Dkt.Noel Mbonde akizungumza kwenye semina ya mradi wa kusaidia vyuo vya ufundi nchini iliyofanyika kwenye chuo cha Veta Njiro jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha 

Tom Tunney meneja mradi wa ushirikiano na serikali za Canada na Tanzania kuhusu mafunzo ya kukuza maarifa kwenye sekta ya ajira rasmi na isiyo rasmi akitoa mada kwenye semina ya mafunzo yaliowakutanisha wakuu wa vyuo vya ufundi (veta) inayofanyika jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.



SERIKALI KUPITIA UPYA MKATABA WA UJENZI KITUO CHA FORODHA HOROHORO- TANGA

$
0
0
Na Peter Haule, WFM, Tanga
Serikali imetoa agizo kwa watendaji wa Kituo cha pamoja cha Forodha Mpakani- Horohoro, kuwasilisha nyaraka za ujenzi wa Kituo hicho ukiwemo mkataba kwa kuwa miundombinu iliyopo haijakidhi viwango jambo lililosababisha kutofunguliwa rasmi kwa kituo hicho tangu mwaka 2015.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro walipofanya ziara ya kutembelea na kukagua Kituo hicho ambapo hawakuridhishwa na miundombinu yake.

Dkt. Kijaji, alisema kuwa Kituo hicho hakina mawasiliano kati ya upande wa Tanzania na Kenya hivyo kutokidhi vigezo vya kuwa Kituo cha pamoja cha Forodha kati ya nchi hizo mbili.

Alisema kuwa ukosefu wa mawasiliano unasababisha urasimu katika kuwahudumia wananchi jambo linalosababisha wateja katika mpaka huo kutafuta njia nyingine ambazo sio rasmi katika usafirishaji bidhaa jambo ambalo linaathari kubwa katika ukusanyaji wa mapato.

Miongoni mwa kasoro zilizobainika wazi ni kamera maalum za usalama zinazotakiwa kufanyakazi ni zaidi ya 14 lakini zinazofanyakazi mpaka sasa ni 4 pekee jambo linalotiashaka kuhusu usalama wa Kituo hicho

Dkt. Kijaji, alisema pia, utaratibu wa wakazi wa Horohoro kwenda kupata huduma za TRA katika Wilayani Muheza usitishwe na badala yake watumishi wa Mamlaka hiyo waende kuwahudumia wananchi katika Wilaya ya Mkinga ili kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara wanapotaka kulipa kodi au kutafuta huduma za masuala ya forodha.

Aidha, Manaibu Waziri hao wameiagiza Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Tanga kuhakikisha Jenereta la Kituo hicho cha Pamoja cha Forodha linafanyakazi ndani ya saa 24 ili kukabiliana na upotevu wa mapato katika eneo hilo kinyume na hapo hatua zingine zitachukuliwa.

Manaibu Waziri hao wametoa maagizo hayo baada ya kuelezwa kuwa jenereta halifanyikazi baada ya kuharibika kwa takribani siku 14 na kusababisha Seikali ikose mapato na kuleta usumbufu kwa watumiaji wa Kituo hicho kwani hulazimika kukaa muda mrefu kusubiri umeme urejee baada ya kukatika.

“Kutofanya kazi kwa Jenereta katika Kituo cha Forodha- Horohoro kumechangia kukosekana kwa kumbukumbu sahihi ya magari yanayopitisha bidhaa katika mpaka huo hivyo kuwa na athari katika takwimu za mapato ya eneo hilo lakini pia usalama wa Taifa”. Alisema Dkt. Kijaji

Viongozi hao wameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA kutengeneza skana ya kuchunguza usalama wa mizigo na wateja wanaoingia kwenye Kituo hicho ambayo imeharibika muda mrefu hali inayohatarisha usalama wan chi, raia na mali zao

Kwa upande wake Dkt. Ndumbaro, ameagiza kuchimbwa kwa kisima cha maji eneo hilo kwa kuwa kiasi cha Sh. milioni sita kinachotumika kuagiza maji kila mwezi kinaweza kutumika kujenga kisima cha kudumu na kuokoa fedha nyingi zisipotee.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Damas Ndumbaro wapo katika ziara mkoani Tanga na maeneo mengine katika kutatua changamoto za ukusanyaji wa mapato na suala la usalama katika mpaka wa Tanzania na Kenya.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro na  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakikagua Scana katika Kituo cha pamoja cha Forodha katika eneo la Horohoro Mkoani Tanga ambayo ilikuwa haifanyi kazi kwa kukosa umeme jambo lilololeta shaka kwa usalama bidhaa zinazoingia na kutoka nje ya nchi.
 Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Bi. Specioza Owure, akifafanua jambo wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Damas Ndumbaro na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), walipotembelea na kukagua Kituo cha pamoja cha Forodha katika eneo la Horohoro Mkoani Tanga.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Bw. Yona Mark, akieleza Changamoto za Kituo cha pamoja cha Forodha katika eneo la Horohoro ambazo ni pamoja na  kuwepo kwa njia nyingi zisizo rasmi za upitishaji wa bidhaa kutoka Tanzania na Kenya, jambo ambalo linaikosesha nchi Mapato. 
 Afisa Mfawidhi wa  wa Mamlaka ya Mpato Tanzania Kituo cha pamoja cha Forodha katika eneo la Horohoro mkoani Tanga, Bw. Bakari Athuman, akitoa ufafanuzi wa changamoto za ukusanyaji mapato katika Kituo hicho wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) Kituoni hapo.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Damas Ndumbaro (kulia), wakihoji namna ambavyo Kituo cha pamoja cha Forodha - Horohoro  kinavyotunza kumbukumbu za vyombo vya moto vinavyoingia na kutoka, kwa kuwa hawakulidhika na idadi ya magari ambayo yalipita kwa siku mbili, jambo lililotia shaka ukusanyaji wa mapato Kituoni hapo. Katikati ni Afisa Mfawidhi wa Uhamiaji  Kituo cha pamoja cha Forodha - Horohoro Bw. Antony Kasitu.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Dkt. Damas Ndumbaro, wakikagua nmyaraka mbalimbali na kutoa agizo la kuboresha kumbukumbu ili kulisaidia Taifa katika suala la ukusanyaji wa mapato na usalama.
Mhandisi wa Mifumo ya Tehama wa Kituo cha pamoja cha Forodha – Horohoro, Mossy Mundonko,  akieleza changamoto ya kutokuwepo kwa mawasiliano kati ya upande wa Tanzania na Kenya jambo linalosababisha kushuka kwa ufanisi wa Kiutendaji wa Kituo hicho, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro wakatoa maagizo ya kupelekwa makataba wa ujenzi wa Kituo hicho kabla ya hatua zingine kuchukuliwa.
 (Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango)

WANAFUNZI MANYARA NA SINGIDA WANUFAIKA NA SWASH

$
0
0
WANAFUNZI wa vilabu 1,700 vya afya na usafi mashuleni kwenye wilaya za Mbulu, Hanang Mkoani Manyara na Mkalama Mkoani Singida, wamenufaika na elimu ya afya waliyopatiwa kupitia kituo cha pembe nne za utamaduni Haydom (4CCP). 

Ofisa miradi wa kituo cha pembe nne za utamaduni Haydom (4CCP) Nelson Faustine aliyasema hayo wakati wa kongamano la wanachama wa klabu za afya na usafi mashuleni lililohusisha walimu na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. 

Faustine alisema wametoa mafunzo ya matumizi sahihi ya vyoo, vibuyu chirizi, kichanja, shimo la taka, usafi binafsi na namna ya kutibu maji. "Tumepanga kuongeza vifaa vya usafi, kuandaa majarida yanayohusiana na afya na kuhamasisha matumizi ya muongozo wa kitaifa wa maji, elimu ya afya na usafi wa mazingira mashuleni," alisema. 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Horace Kolimba alisema aliagiza shule zote za halmashauri hiyo kuanzisha klabu za afya na usafi mashuleni. Kolimba alisema wametoa maagizo kwa watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha hadi Februari 28 shule zote ziwe na vyoo ili wanafunzi wavitumie wakiwa wanasoma. 

Ofisa miradi wa shirika la Norwegian Church Aid, Zachayo Makobero alisema mpango huo umekuwa na manufaa makubwa kwa wanafunzi wa klabu za afya na usafi mashuleni. Mwalimu wa shule ya msingi Mwengeza wilayani Mkalama mkoani Singida, Julieth Gara alisema elimu hiyo imewasaidia mno wanafunzi kutokana na kufanya usafi wa mazingira. 

Mwalimu Gara alisema awali kabla ya elimu hiyo wanafunzi walikuwa wanaugua magonjwa ya tumbo na kuharisha ila sasa hivi hawana tatizo hilo tena. Mwanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari Dokta Olsen ya Haydom, Aisha Monyo alisema kupitia klabu za afya na usafi mashuleni, wamepata elimu ya usafi na mazingira mashuleni. 

Monyo alisema wanafunzi wamepokea elimu hiyo kwa kusafisha mazingira ya shule na vyoo pamoja na kunawa mikono pindi wanapotoka vyooni tofauti kabla ya kupata elimu hiyo. Ofisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Omary Mtamike alisema awali walikuwa na shule moja ya klabu ya afya na usafi mashuleni ila hivi sasa zipo shule 28.

Mtamike alisema kutokana na manufaa ya mradi huo wa Swash, wao kama halmashauri wamejipanga kuhakikisha wanaboresha zaidi kwa kuongeza shule nyingine za msingi na sekondari. 
 Ofisa miradi wa kituo cha pembe nne za utamaduni Haydom (4CCP) Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Nelson Faustine akizungumza kwenye kongamano la klabu za afya na usafi mashuleni. 
 Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Wilaya za Mbulu na Hanang' Mkoani Manyara na Mkalama Mkoani Singida wakiwa kwenye kongamano la klabu za afya na usafi mashuleni kwenye Mji mdogo wa Haydom Wilayani Mbulu. 
 Baadhi ya wadau wa elimu  wa Wilaya za Mbulu na Hanang' Mkoani Manyara wakiwa kwenye kongamano la klabu za afya na usafi mashuleni lililoandaliwa na kituo cha pembe nne za utamaduni Haydom, (4CCP). 
Mshauri mkuu wa miradi ya maji na afya kwa Norwegian Church Aid (NCA) Manfred Arlt akizungumza na wadau wa elimu kwenye kongamano la klabu za afya na usafi mashuleni lililoandaliwa na kituo cha pembe nne za utamaduni Haydom (4CCP).  

Serikali yaahidi kuendelea kushirikiana na Halotel

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng; Atashasta Nditiye akiongea na waandishi wa habari kuhusu dhima ya ziara aliyoifanya kwa ofisi za Makao Makuu ya Halotel jijini Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Nguyen Van Son. 
Makamu wa Kitengo cha Idara ya Umeme wa kampuni ya Halotel, akitoa maelezo jinsi mfumo wa Umeme unavyofanya kazi kwenye kituo cha data kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng; Atashasta Nditiye (Kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Nguyen Van Son wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu waziri huyo katika ofisi za makao makuu za Halotel jijini Dar es Salaam. 
Pichani kati ni  Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye  akimsikiliza  Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Nguyen Van Son alipokuwa akifafanua jambo wakati wa kikao chao cha pamoja mara baada ya kufanya ziara ya kuitembelea kampuni hiyo ili kujua shughuli wanazozifanya katika kuwahudumia wateja pamoja na changamoto wanazokumbana nazo kila siku.
Kikao cha pamoja kikiendelea


 
· Yaipongeza kutimiza ahadi ilizozitoa kwa serikali.

Kwa kutambua umuhimu na ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchini Tanzania, serikali imeiahidi kampuni ya mawasiliano ya Halotel kuendelea kushirikiana nayo katika kutatua changamoto wanazozikabili kwa pamoja.

Hayo yalisemwa wakati wa ziara maalum ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye wakati alipoitembelea kampuni hiyo ili kujua shughuli wanazozifanya katika kuwahudumia wateja pamoja na changamoto wanazokumbana nazo kila siku.

“Lengo la ziara hii ni kuja kuwasikiliza, kujua shughuli mnazozifanya pamoja na changamoto mnazokumbana nazo. Serikali inatambua ukuaji na umuhimu wa sekta ya mawasiliano katika kuchangia uchumi. Na wadau wakubwa katika sekta hii ni makampuni ya simu kama Halotel. Hivyo hatuna budi kuyatembelea, kuongea nayo, kuyasikiliza na kushirikiana nao wapi tufanye kipi kama serikali katika sekta nzima ya mawasiliano. Ningependa kuwatoa hofu kwamba kama serikali tuko pamoja nao,” alisema Mhandisi Nditiye.

“Serikali inatambua sana mchango wa makampuni ya simu na ndiyo maana tumeamua kuwatembelea ili kujua shughuli wanazozifanya. Kwa mfano, mbali na kuzungumza na kusikiliza changamoto zao lakini nimepata fursa ya kutembelea kitengo chao wanacho hudumia wateja, mitambo na kitengo chao wanakitumia kufanyia huduma za kifedha. Nimezisikiliza changamoto zao na ninaahidi kwenda kuzifanyia kazi,” alihitimisha Mhandisi Nditiye.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halotel Nguyen Van Son, aliezea mafanikio ambayo kampuni yake imeyafikia mojawapo ikiwa ni ahadi ilizozitoa kwa serikali katika utoaji wa huduma nchini.

“Katika utoaji wa huduma za mawasiliano Tanzania tulitoa ahadi kadhaa kwa serikali na ningependa kuchukua fursa hii kuifahamisha serikali kuwa tumetekeleza kwa kiasi kikubwa. Tuliahidi kutoa huduma za mtandao wa intaneti katika shule 450 na tumevuka lengo kwa 455. Tuliahidi kutandaza kebo za huduma ya intaneti katika ofisi za mabaraza ya wilaya 150 na tumefanikiwa kwa kufikia ofisi 147. Pia kusambaza miundombinu ya mawasiliano ya fibre katika hospitali za wilaya 150 na tumefanikiwa zote 150. Tuliahidi kusambaza miundombuni ya mawasiliano ya fibre kwa vituo vya polisi vya wilaya 150 na tumefanikiwa 121. Lakini pia, tuliahidi kusambaza miundombinu ya mawasiliano ya fibre katika vituo vya ofisi za posta za wilaya 65 na tumevuka kwa kufunga 66,” alisema na kuongezea Son.

Licha ya mafanikio hayo ambayo Halotel imeyafanikisha kwa kutimiza ahadi ambazo iliipatia serikali, kampuni hiyo ilielezea changamoto kadhaa inazokumbana nazo.

“Ili kutimiza dhima yetu ya kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma za mawasiliano kwa bei nafuu lakini pia tunakumbwa na changamoto kadhaa. Mojawapo ni pamoja na kuharibiwa kwa mifumo yetu ya miundombinu ya mawasiliano na baadhi ya wananchi ambao sio waaminifu katika baadhi ya mikoa. Vitendo hivi si tu vinakwamisha juhudi zetu za kufikisha mawasiliano katika kila pembe ya nchi lakini pia inawazuia wananchi kufikiwa na huduma zetu hivyo kukwamisha shughuli za mawasiliano na uchumi. Tungeomba katika hili serikali kushirikiana nasi ili kuzuia vitendo hivi vya kihalifu na kujenga hamasa juu ya umuhimu wa mitambo hii,” aliongezea Son.

“Pia tunaiomba serikali kushirikiana na Halotel katika kupambana na changamoto ya wizi wa mitandaoni. Kama mnavyojua huduma za mawasiliano hususani huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi yanatumika kwa kiasi kikubwa katika kurahisisha shughuli mbalimbali. Wahalifu wa mitandaoni nao wanaoitumia fursa hii kuwalaghai wateja hivyo kuvunja uaminifu baina yetu. Halotel inapendekeza kuwepo na ushirikiano na serikali katika kulikabili hili na kulitatua kwa pamoja. Tunapendekeza kuwepo kwa vikao, semina au warsha za mara kwa mara ili kupanga mikakati na kumaliza kabisa changamoto hii,” alihitimisha Son.

RC GAMBO AITAKA KAMPUNI YA UWINDAJI YA GREEN MILES SAFARI KURIPOTI MBELE YA KAMATI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza wakati alipoagiza mmiliki wa Kitalu cha Kampuni ya Uwindaji ya Green Miles Safaris Ltd, kuripoti mbele ya kamati aliyoiunda ili kueleza sakata la kuuawa Twiga katika kitalu chake na kushindwa kuvilipa vijiji 23 kiasi cha sh 329 milioni ,wananchi wameipongeza serikali kuingia kati mgogoro huo.
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido wakiwa katika mkutano huo wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe akizungumza na kusema amekuwa akipokea vitisho kutoka sehemu mbalimbali kutokana na kuigusa kampuni hiyo lakini alisisitiza kusimamia sheria pamoja na maagizo aliyopewa na Rais John Magufuli katika kutetea wanyonge na maagizo ya Rc Gambo juu ya kutatua shida za wananchi wake hivyo atasimama kidete kuhakikisha haki inatendeka.


Mwandishi Wetu,Longido.

Wakati Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiagiza mmiliki wa Kitalu cha Kampuni ya Uwindaji ya Green Miles Safaris Ltd, kuripoti mbele ya kamati aliyoiunda ili kueleza sakata la kuuawa Twiga katika kitalu chake na kushindwa kuvilipa vijiji 23 kiasi cha sh 329 milioni ,wananchi wameipongeza serikali kuingia kati mgogoro huo.

Mkuu huyo wa mkoa akizungumza katika wilaya ya Karatu, katika hafla yakabidhi vitambulisho 10,000 kwa wafanyabiashara wadogo, alisema kampuni hiyo imekuwa ikikaidi maagizo ya serikali wilaya ya Longido kulipa madai ya vijiji jambo ambalo halikubaliki.

Gambo aliagiza viongozi wa kampuni hiyo wajitokeze mahali popote walipo ili kwenda katika tume maalum aliyounda inayoongozwa na vyombo vya ulinzi na usalama kubaini kwanini mauaji ya Twiga yameshamiri zaidi katika eneo la kitalu hicho na kwanini hajalipa kodi za vijiji kwaajili ya maendeleo zaidi ya sh, milioni 329.

"Hii kampuni wanamaneno mengi sana nawaambia hivi serikali ya awamu hii haina maneno inasimamia sheria popote walipo wajitokeze katika kamati ili kubaini mambo ambayo tumegundua awali na waache kutisha watu taarifa zao tunazo na nakwambia DC Mwaisumbe nipo nyuma yako katika hili simamia sheria na kanuni zilizopo hakuna mtu yoyote kukatisha kwa jambo lolote lazima tuchukue hatua "

Naye Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe alisema amepata matishio kutoka sehemu mbalimbali kutokana na kuigusa kampuni hiyo lakini alisisitiza kusimamia sheria pamoja na maagizo aliyopewa na Rais John Magufuli katika kutetea wanyonge na maagizo ya Rc Gambo juu ya kutatua shida za wananchi wake hivyo atasimama kidete kuhakikisha haki inatendeka. 

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido, Jumaa Mhina alisisitiza kampuni hiyo kulipa deni wanalodaiwa na vijiji hivyo sambamba na halmashauuri kulipwa malimbikizo ya madeni wanayoidai kampuni hiyo.
"Tumekwisha andika barua Wizara ya Maliasili na Utalii ili tulipwe lakini pia kuhakikisha vijiji vinalipwa" alisema


Wananchi Longido waipongeza Serikali.

Wakizungumzia maamuzi ya mkuu wa mkoa,baadhi ya wakazi wa Longido wamepongeza serikali kwa kuingilia kati mgogoro wao na mwekezaji huyo.
Julius Laizer mkazi wa Kutubeine alisema wanataka mwekezaji ambaye atatatua kero za wananchi katika wilaya hiyo na sio kuwa sehemu ya migogoro.

"Tunataka wanyamapori watusaidie kupata maendeleo hivyo tunaomba serikali kuingilia kati kudhibiti matukio ya ujangili" alisema
Peter Maleko kazi wa Mundarara alisema wanaomba serikali isaidie walipwe haki zao kutoka kwa mwekezaji kampuni ya Green Miles kwani wanadaia zaidi ya sh 11 milioni kila kijiji.


"Tunashukuru mkoa umefanyakazi lakini bado tunaomba tulipwe haki zetu" alisema.Hivi karibuni,Mkuu huyo wa mkoa, aliunda kamati maalum kwaajili ya kuchunguza mauaji ya Twiga katika wilaya ya Longido ambapo alibaini mambo mbalimbali ikiwemo Twiga 35 kuuawa kwakipindi cha mwaka miwili katika matukio mbalimbali ikiwemo Twiga 25 kuuliwa kutokana na ujangili.

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR ATEMBELEA MGODI WA BUZWAGI KAHAMA

$
0
0


Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amefanya ziara katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika Februari 11,2019,Balozi Idd ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga alipongeza viongozi wazawa wanaoendesha mgodi huo kwa kuwekeza miundombinu ya huduma za elimu afya na barabara.

"Zamani nilikuwa nasikia tu Buzwagi Buzwagi nashukuru sana Mkuu wa Mkoa nashukuru sana Meneja Mkuu wa Mgodi kwa fursa hii ya kuja kutembelea katika Mgodi wenu lakini kitu kinachonifurahisha ni huduma kwa jamii ya hapa Kahama mmenionyesha skuli ‘shule’mlizokarabati,barabara,na kadhlika.Pia nimeambiwa kuna hospitali mnajenga hayo yote kwa kweli ni kitu kizuri kwamba rasilimali hii inafaidisha vile vile wanajamii nawapongezeni sana muendelee ili Wana Kahama na sehemu nyingine za Mkoa wa Shinyanga waendelee kunufaika na rasilimali yao",aliongeza.

Akimkaribisha Mgodini hapo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack alisema "Mheshimiwa Makamu wa Rais Zanzibar leo tupo kwenye Mgodi huu wa Buzwagi ambao ni pamoja na mali zilizopo kwenye Mkoa ambao wewe ni mlezi tumesema upite kwenye mgodi huu ili kwa kuwa wewe ni Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga ni muhimu uone na rasilimali zilizomo hivyo pamoja na ujumbe ulioambatana nao mtaangalia pamoja na mambo mengine uzalishaji wa Dhahabu".

Naye Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu alimshukuru Makamu wa Rais kwa kufanya ziara hapo Mgodini."Tumefarijika sana kupata ugeni huu tunashukuru sana, tukipata ugeni kama huu tunafurahi sana karibuni sana na kwa fursa kama hii ambavyo umeambatana na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi tunaona ni vyema tupate nafasi kukuonyesha jinsi mgodi umeshiriki katika maendeleo ya jamii na namna tunavyozalisha dhahabu",alisema Busunzu.

Kulia ni Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd wakati akifanya ziara katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akimwelezea Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kuhusu shughuli za uzalishaji zinazofanyika mgodini.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiuliza jambo.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akiongoza msafara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kutembelea mgodi wa Buzwagi.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizungumza alipofanya ziara katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akishikana mkono na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akiwakaribisha wageni mbalimbali walioambatana na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kutembelea mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. 
Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Mabala Mlolwa, katikati ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack. 
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ukitoka mgodini
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akipunga mkono kumuaga Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd

T-Pesa kuanzisha mfumo wa malipo kwa kutumia card

$
0
0
Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya PayLink ya Korea, MoonKyu Lee (wa pili kushoto) wakisaini leo jijini Dar es Salaam makubaliano ya mradi wa kutengeneza mfumo wa malipo kwa kutumia kadi (T Card) utakaotumika kulipia huduma mbalimbali nchini Tanzania. Wanaoshuhudia kulia na kushoto ni wanasheria wa pande zote. 
Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya PayLink ya Korea, MoonKyu Lee (wa pili kushoto) wakisaini makubaliano ya mradi wa kutengeneza mfumo wa malipo kwa kutumia kadi (T Card) utakaotumika kulipia huduma mbalimbali nchini Tanzania. Wanaoshuhudia kulia na kushoto ni wanasheria wa pande zote. 
Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya PayLink ya Korea, MoonKyu Lee (wa pili kushoto) wakibadilishana nakala za makubaliano yao mara baada ya kusaini leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kulia na kushoto ni wanasheria wa pande zote. 
Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya PayLink ya Korea, MoonKyu Lee (wa pili kushoto) wakibadilishana nakala za makubaliano yao mara baada ya kusaini leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kulia na kushoto ni wanasheria wa pande zote. 
Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya PayLink ya Korea, MoonKyu Lee (wa pili kushoto) wakionesha nakala za makubaliano ya mradi wa kutengeneza mfumo wa malipo kwa kutumia kadi (T Card) utakaotumika kulipia huduma mbalimbali nchini Tanzania. Wanaoshuhudia kulia na kushoto ni wanasheria wa pande zote. 
Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya PayLink ya Korea, MoonKyu Lee (kushoto) wakifurahiya jambo mara baada ya kusaini leo jijini Dar es Salaam makubaliano ya mradi wa kutengeneza mfumo wa malipo kwa kutumia kadi (T Card) utakaotumika kulipia huduma mbalimbali nchini Tanzania. 
Picha ya pamoja ya viongozi waandamizi wa kampuni zote mara baada ya hafla ya kusaini mkataba huo wa ushirikiano kibiashara. 



SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, kupitia mtandao wake wa huduma za kifedha wa T-PESA pamoja na wadau wa kibiashara, Kampuni tatu kutoka nchini Korea zimesaini mradi wa kutengeneza mfumo wa malipo kwa kutumia kadi (T Card).

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Huduma za T- PESA Ndugu Moses Alponce, alisema mfumo huo unaotumia teknolojia za kisasa ni matokeo ya utafiti uliofanywa na kuonesha mahitaji makubwa ya huduma za malipo yasiyotumia fedha tasilimu. 

Aidha aliongeza kuwa kukamilika kwa mfumo huo kutarahisisha shughuli za kibiashara na kuimarisha uwezo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), katika kukusanya kikamilifu kodi za Serikali kutoka kila miamala itakayofanyika, sambamba na kuongeza ufanisi katika biashara na shughuli nyingine za kiuchumi.

Mfumo huo unaotekelezwa na T-Pesa kwa kushirikiana na wadau wake kibiashara kutoka Jamhuri ya watu wa Korea katika muunganiko wa Kampuni tatu, ambazo ni PayLink Korea, KEH Hana Card pamoja na ATECT & Company unakuwa wa kwanza kuletwa na huduma za fedha kwa kutumia simu za mikononi nchini Tanzania.

"..Kampuni hizi zitashirikiana na T PESA katika zoezi la kuandaa, kupanga na kutengeneza Mfumo wa kadi za NFC na POS Cashless Ecosystem," alisema Alponce.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kampuni ya PayLink ya Korea, MoonKyu Lee akiwakilisha kampuni hizo alisema kuingia kwa ushirikiano katika mfumo huo utaongeza uwazi katika miamala ya kifedha jambo ambalo litaongeza mapato ya kodi kwenye mifumo ya malipo nchini na kuleta maendeleo.

Ikiwa sasa ni takribani miaka miwili tangu kuanzishwa kwake, T PESA imekuwa na mchango mkubwa katika huduma za Fedha mtandao Nchini, ambapo kwa mujibu wa ripoti ya TCRA toleo la mwaka 2019, T PESA ni moja ya huduma zinazokua kwa kasi kubwa ikiwa na Mawakala 10,000, wateja laki 320,000 wanaozungusha miamala ya takribani Tsh Bilioni 4.

Simba yaibuka kidedea, yaitandika Al Ahly ya Misri

$
0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Simba wamefanikiwa kushinda katika mchezo wao Kundi D dhidi ya Al ahly ya Misri. Mchezo huo ulioanza kwa kasi katika dakika 10 za Kipindi Cha kwanza timu hizo ziliweza kusomana na kushambulia kwa kupokezana.

Katika kipindi cha kwanza Simba walishindwa kutumia nafasi walizozipata ingawa walifanikiwa kupata kona kwa wingi. Dakika 45 za Kipindi cha kwanza kilimalizika timu zote zikienda mapumziko wakiwa wako 0-0.

Kipindi cha pili kilianza Al Ahly wakisakama lango la Simba, lakini umakini wa safu ya ulinzi ya Simba ikaa makini kuondoa mipira kwenye lango lao. Dakika ya 65, mchezaji wa Kimataifa kutoka Rwanda Meddie Kagere anaipatia Simba goli la kwanza akipokea pasi ya Zana Coulibaly baada ya kuwahadaa ngome ya ulinzi ya Al ahly.

Mpira uliendelea kwa kasi Simba wakilinda goli lao na kutafuta goli lingine zaidi huku Al ahly wakisaka la kusawazisha. Mpaka mpira unamalizika katika Uwanja wa Taifa Simba wanafanikiwa kuondoka na alama tatu, na kutimiza alama 6 akiwa nyuma ya Al Ahly mwenye alama 7 na nafasi ya tatu akiwa As Vita na alama 4 huku JS Saoura akiwa na alama 2.

Katika mchezo mwingine wa kundi D As Vita anakaribishwa ugnini dhidi JS Saoura mechi itakayochezwa majira ya saa 4 usiku kwa saa zaAfrika Mashariki.




















Prof Kikula aagiza wachimbaji wa madini kupewa elimu ya Sheria ya Madini

DKT. NDUGULILE AKASIRISHWA NA KASI YA UJENZI WA MAABARA YA AFYA YA JAMII

$
0
0
Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongoza katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, leo katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifanya ukaguzi wa chumba kwa chumba ili kujidhisha na maendeleo ya ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, unaojengwa katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.
Muonekano wa jengo la Maabara ngazi ya tatu lenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, jengo hilo lililokamilika kwa 90%, linajengwa katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo, wakati akiongea na Mkandarasi pindi alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, unaojengwa katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baada ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, unaojengwa katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.



Na WAMJW – DSM

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amekasirishwa na kasi ndogo ya ujenzi wa Maabara ya Afya ya Jamii ngazi ya tatu, inayoshughurikia magonjwa hatari ya mlipuko kama vile Ebola, Mabag, Kipindupindu hali inayopelekea kuchelewesha utoaji wa huduma hizo kwa Wananchi.


Hayo yamejiri leo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa jengo hilo lililo eneo la Mabibo jijini Dar es salaam ili kujidhihirishia thamani ya pesa zilizotumika na kiasi cha ujenzi wa jengo hilo ulipofika.Dkt. Ndugulile amesema kuwa haoni sababu ya msingi iliyopelekea kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa Maabara hiyo kwani fedha zote zipo, hivyo kukasirishwa kwa kasi ndogo ya ujenzi wa Maabara hiyo ulioanza tangu mwaka 2016.

” Nitoe asikitiko yangu kwamba, kazi hii imechukua muda mrefu sana, tangia 2016, wenzetu waliozipata fedha hizi wengi wamekwisha kamilisha kazi zao, sisi Tanzania bado tunasua sua, kibong’oto, Temeke, Mawenzi na hapa, najambo linalonisikitisha sana fedha tunazo” alisema Dkt. Ndugulile.pia, Dkt. Ndugulile amesema kuwa ujenzi wa Maabara hiyo utaisaidia Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho inakipeleka nje ya nchi kwaajili yakupima sampuli za magonjwa hayo, hivyo kukamilika kwa Maabara hiyo kutaifanya Tanzania kuwa moja kati ya nchi chache barani Afrika inayotoa huduma hizo.

Aidha, Dkt Ndugulile ameonekana kutoridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa Maabara hiyo, hivyo kutoa onyo katika matumizi ya fedha za ujenzi wa Maabara hiyo, hii ni kutokana na kufanya marekebisho ya mara kwa mara wakati ramani ya jengo hilo ipo.“Fedha tunazo nyingi kupita maelezo, na ndiomaana mnaishia kuzitumia vibaya, matumizi ya hovyo yanapitishwa kwa haraka sana, lakini matumizi ya msingi yanasuasua, sasa niombe kwa niamba ya Kazi zote, hizi fedha tuliziomba kwa matumizi mahsusi kujenga hizi Maabara na isolation centers, naomba nitakaporudi haya tuliokubaliana mtimize” alisema Dkt Ndugulile

Kwa upande mwingie Dkt. Ndugulile amewata viongozi wa Wizara ya Afya kutokuwa kikwazo katika taratibu za ujenzi wa Maabara hiyo, ili kuepusha lawama kutoka kwa Wakandarasi, jambo litalosaidia katika kasi ya ujenzi wa Maabara hiyo.“Taratibu za ndani, sisi kama Wizara naomba zisiwe kikwazo kwakweli, kwasababu gharama za mradi mnazijua, uendeshaji tunaujua, na tulikuwa tunazifahamu, fedha tunazo zakutosha, mzipitishe katika taratibu zake zote ili hawa Wakandarasi wasije kutulalamikia” Alisema Dkt. Ndugulile

MAGAZETI YA LEO JUMATANO FERBRUARI 13,2019

Wagonjwa 12 wafanyiwa uchunguzi wa mishipa ya moyo kupitia mtambo wa Cathlab uliofungwa Hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma

$
0
0
Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakimfanyia mgonjwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (Coronary Angiogram) kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Jumla ya wagonjwa 12 wamefanyiwa uchunguzi katika mtambo huo ambapo watano kati yao wamekutwa na matatizo mmoja atatumia dawa na wengine wanne watazibuliwa mishipa ya moyo iliyoziba (Percutaneous Coronary Intervention – PCI).

Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakimfanyia mgonjwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (Coronary Angiogram) kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Jumla ya wagonjwa 12 wamefanyiwa uchunguzi katika mtambo huo ambapo watano kati yao wamekutwa na matatizo mmoja atatumia dawa na wengine wanne watazibuliwa mishipa ya moyo iliyoziba (Percutaneous Coronary Intervention – PCI).
Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakimfanyia mgonjwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (Coronary Angiogram) kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Jumla ya wagonjwa 12 wamefanyiwa uchunguzi katika mtambo huo ambapo watano kati yao wamekutwa na matatizo mmoja atatumia dawa na wengine wanne watazibuliwa mishipa ya moyo iliyoziba (Percutaneous Coronary Intervention – PCI).


Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumaliza kumfanyia uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) mgonjwa wa 12 kwa kutumia mtambo wa Cathlab ambao umezinduliwa leo katika Hospitali ya BMH.
Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzinduliwa kwa mtambo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na tiba ya mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram).

………………………………………………………………………………………………………

Na Mwandishi Maalum, Dodoma

Jumla ya wagonjwa 12 wamefanyiwa uchunguzi wa kuangalia jinsi mishipa ya damu ya moyo inavyofanya kazi kupitia mtambo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na tiba ya mishipa ya damu ya moyo.

Uchunguzi huo ambao umefanyika kwa siku mbili umefanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi alisema kati ya wagonjwa 12 waliofanyiwa uchunguzi watano wamekutwa na matatizo ya mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri, wanne wanahitaji matibabu ya kuzibuliwa mishipa ya damu na mmoja atatumia dawa.

“Tumefanya uchunguzi kwa wagonjwa 12 , tisa wanamatatizo madogo ambayo hayahitaji matibabu makubwa na wanne wanahitaji matibabu makubwa ambayo ni kuzibuliwa kwa mishipa ya damu na mmoja atatumia dawa”, alisema Prof. Janabi .

Kwa upande wa wagonjwa waliofanyiwa uchunguzi waliishukuru Serikali kwa kusogeza huduma hiyo katika mkoa wa Dodoma ambapo wagonjwa wenye matatizo kama hayo wataweza kupata huduma hiyo katika Hospitali ya Benjamini Mkapa badala ya kusafiri kwenda mkoani Dar es Salaam kufuata huduma hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mwalimu Mstaafu Simon Mesomapya ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mtanana wilayani Kongwa alisema alianza kusumbuliwa na maradhi ya moyo mwaka 2016 na kutibiwa katika Hospitali mbalimbali ambapo mwaka huu alipewa rufaa ya kutibiwa BMH kwa uchunguzi zaidi.

“Kupatikana kwa huduma hii hapa BMH itapunguza gharama za kusafiri kwenda Dar es Salaam au nje ya nchi pia Dodoma ni kati kati ya nchi ni rahisi kwa wananchi wa mikoa jirani kupata huduma hiyo”, alisema Mwalimu Mesomapya.

Aliiomba Serikali iendelee kuboresha huduma hiyo ili wananchi wenye matatizo ya moyo waweze kufurahia huduma hiyo,

Mtambo huo wa kisasa wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo unauwezo pia wa kuchunguza mishipa ya damu ya mikono, miguu na kichwa.

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

$
0
0


Mnamo tarehe 11.02.2019 majira ya saa 23:45 usiku huko eneo la Soweto, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilikamata gari lenye namba za usajili T.937 CKD aina Toyota Saloon likiwa na vipodozi vya aina mbalimbali vilivyopigwa marufuku nchini. Vipodozi vilivyokamatwa ni:- 
Extra Clair katoni nane [08].
Perfect White katoni mbili [02].
Epiderm Cream dazani arobaini na saba [47]
Diproson dazani ishirini na moja [21]
Coco Pulp katoni mbili [02]
Carolight katoni sita [06]
Citro Light katoni tatu [03]
Teint Clair katoni mbili [02]
Top Lemon katoni nne [04]
Clair Men katoni mbili [02]
Princes Clair katoni nne [04]
Movet boksi mbili [02]
Miki Clair katoni mbili [02]
Top Clair Plus katoni moja [01]
Collagen formula boksi mbili [02]
Mont Clair boksi mbili [02]
Movet tube pcs mbili [02]
Movet boksi mbili [02]
Cocoderm boksi moja [01] 

KUPATIKANA NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NCHINI. 

Mnamo tarehe 12.02.2019 majira ya saa 07:15 asubuhi huko eneo la Check Point Igurusi, Kata ya Igurusi, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali na Mkoa wa Mbeya, Polisi wakiwa doria walimkamata SAID IDDY @ MOHAMED [32] Dereva na Mkazi wa Mbadula Arusha akiendesha gari lenye namba za usajili T.298 DCH aina ya Scania Basi la abiria – HAJI’s akitokea Mbeya kuelekea Arusha akiwa na vipodozi vilivyopigwa marufuku nchini aina mbalimbali. 

Vipodozi vilivyokamatwa ni:- 
Diana Boksi mbili [02].
White Max Boksi tatu [03].
Secret White Location Boksi moja [01] 

Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani. 


KUPATIKANA NA SILAHA [GOBORE] BILA KIBALI. 

Mnamo tarehe 11.02.2019 majira ya saa 14:35 mchana huko eneo la Makasini – Uyole, Kata ya Uyole, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata PAUL ABRICK [66] Mkazi wa Mtaa wa Nyahoro – Uyole akiwa na silaha Gobore aina ya Tower yenye namba 1878 bila kibali. Upelelezi unaendelea.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images