Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUBORESHA COCO BEACH,YATOA BILIONI 28 KWA WILAYA YA KINONDONI KUENDELEZA

$
0
0
Na Grace Semfuko-MAELEZO 

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imetoa jumla ya shilingi Bilioni 28 kwa Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuendeleza miradi miwili ikiwepo ujenzi wa soko la Tandale na uboreshaji kwa kuendeleza ufukwe wa Osterbay, maarufu Coco Beach, lengo likiwa ni kulipa thamani eneo hilo na kuongeza watalii wa ndani nan je. 

Utiaji saini kwa ajili ya mkataba wa ujenzi huo ulifanywa February 4 mwaka huu, kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dotto James na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagulumjuli, ambapo kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 14 zitaendeleza Ufukwe wa Osterbay, eneo la Coco Beach na zingine Bilioni 14 zitajenga Soko la Tandale. 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mazingira ya “Mchanga Pekee” iliyo na lengo la kubadilisha mazingira ya fukwe za bahari ya Hindi, jijini Dar Es salaam, iliyofanyika leo asubuhi kwenye ufukwe wa Coco, zoezi lililoambatana na usafi wa mazingira kwenye eneo hilo. 

“Wilaya yangu ya Kinondoni tumekuja na mpango maalum wa kuimarisha mazingira ya Bahari, tunazo Bilioni 28 kwa ajili ya miradi miwili ya kuimarisha mazingira; zikiwemo fukwe za Osterbay zinazojumuisha eneo hili la Coco pamoja na kuimarisha mazingira ya soko la Tandale” Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Chogolo Wanavikoba wa Buguruni na taasisi mbalimbali zilizofika kushiriki. 

Akisikilizwa na karibu mamia ya watu, wengi wao wakiwa akina mama wa vikoba, Bw. Chongolo alisema zoezi lililopo sasa ni hatua ya kutangaza mzabuni kwa ajili ya ujenzi huo ambapo katika kipindi cha miaka miwili ijayo shughuli hiyo itaanza. 

Mbali na fedha hizo za miradi miwili, Serikali mwaka jana ilitoa zaidi ya shilingi Bilioni 9 kwa ajili ya ukarabati wa soko la Magomeni, Jijini Dar Es Salaam zoezi ambalo linaendeleo mpaka sasa, aidha Chongolo alitoa wito kwa jamii kuhusu kuendeleza na kuzitunza fukwe za bahari ili kutengeneza mazingira mazuri ya wananchi kupumzika pia kubarizi 

Naye Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania – TTB, Geofrey Tengeneza alisema fukwe za Bahari ni maeneo muhimu kwani watalii wengi wa ndani na nje ya nchi hutembelea maeneo hayo na hivyo yanahitaji kutunzwa katika hali ya usafi. 

“Fukwe hizi ni muhimu sana kwa utalii katika nchi yetu, hivyo tunahitaji kuzitunza na tusichafue mazingira ya fukwe zetu” alisema Tengeneza na kusisitiza kuwa ufukwe wa Coco ni maarufu kwa watu wote na serikali inatambua hilo na kwamba utaendelea kutumiwa na watu wote kwa ajili ya kupumzika na burudani. 

Kampeni ya “Mchanga pekee” imeanzishwa na Kampuni ya Cocacola kwanza na inalenga kuboresha mazingira ya fukwe za Bahari na kuwa safi na Cocacola inashirikisha Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na mashirika na taasisi mbalimbali nchini. 

Kampeni hiyo imekuja kufuatia ripoti ya Shirika la “International Council of Beverages Associations (ICBA)” iliyotolewa mwishoni mwa mwaka 2018 ikionesha uchafuzi mkubwa wa fukwe za bahari duniani kufikia wastani wa vipande vya plastiki kilomita elfu 13 na kubainika kuwepo kwa tani milioni 150 za plastiki kwenye fukwe hizo mpaka leo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Cocacola, Bazil Gadzios leo alisisitiza kuwa kampeni hiyo inalenga kufanya usafi kwenye fukwe wa Coco Beach, kukusanya chupa za plasitiki elfu kumi kila mwezi, kutoa elimu kwa jamii kuhusu kuhifadhi mazingira ya fukwe za bahari, kupunguza chupa hizo pamoja na kuhifadhi ekolojia ya viumbe vya Baharini na nchi kavu. 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AIHIRISHA BUNGE

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba  ya kuahirisha Bunge jijini Dodoma, Februari  9.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akijadili jambo na Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki, bungeni jijini Dodoma, Februari 9.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

USIYOFAHAMU KUHUSU AJALI YA HIACE NA CANTER BUKOBA

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus – Kagera

Ni Tarehe 08, Februari, 2019 usiku vilio, simanzi na hofu vinatawala katika mtaa wa Hamugembe, Nyangoye Manispaa ya Bukoba Eneo maarufu sana kwa matukio ya ajali mbalimbali zilizogharimu maisha ya watu na wengine kufariki kabisa.

Usiku huu tena ikiwa yapata majira ya saa tatu usiku, unasikika mshindo mkubwa wa Ajali ukihusisha Magari mawili yaliyogongana uso kwa uso, magari hayo ni Roli dogo aina ya Canter,yenye namba za usajili T223 ATK mali ya Bwana Jibril, pamoja na Gari dogo la Abiria Daladala yenye namba za usajili T 869 CHT, inayofanya safari zake Kutoka Bukoba kwenda Mutukula. 

Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo Bwana Abdul Itembwe anaeleza kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea katikati ya mteremko wa Nyangoye, ambapo daladala ilikuwa ikipanda na Canter ikiteremka, hivyo gari hiyo aina ya canter kupata itilafu upande wa breki, na kupelekea kuigonga daladala na kuserereka nayo hadi kandoni mwa barabara yapata mita 150 kutoka barabani katikati. 

Hali hiyo ikamkumba na mwendesha pikipiki aliyefahamika kwa jina moja tu Bonge mkazi wa Nyakanyasi, ambae bado haijafahamika alikuwa katika mwelekeo gani. Kufuatia magari hiyo kugongana mara baada ya kuwa tayari yamesimama, zilianza kuibuka cheche ndogo ndogo upande wa daladala wakati jitihada za uokoaji zikiendelea kujaribu kuwanasua marehemu wa ajali hiyo.

Shuhuda huyo anaongeza kuwa ghafla moto mkubwa ulilipuka na kuanza kuunguza gari hilo huku ndani wakionekana watu watatu ndani ya Daladala, ambao walionekana kupoteza fahamu kama sio kufariki kabisa. Wakati hayo yakiendelea tayari upande wa gari aina ya Roli ambalo lilikuwa na abiria wawili pamoja na dereva, abiria hao walifanikiwa kunusurika na kutoka kupitia dirisha la mlango wa abiria kabla gari halijashika moto .

Wakati jitihada za uokoaji zikiendelea inadaiwa kuwa dereva wa Roli Marehemu Dickson Ndyetabula (25) alijitahidi kujinasua lakini haikuwa rahisi huku akipiga ukulele mkubwa wa kuomba msaaada, licha ya wasamaria mwema kufika eneo hilo na kuanza kumvuta, lakini alionekana kukwama na hivyo hadi mauti yanamkuta alisikika akisema “…Asanteni kwa msaada wenu mimi nakufa..” hadi Jeshi la Polisi na lile Uokoaji (zimamoto) wanafika eneo la tukio tayari moto ulishawazidia wananchi ambao awali walionyesha juhudi za kuuzima kwa maji na mchanga ikiashindikana.

Usiyoyafahamu kuhusu Madereva wote wawili: marehemu Nelsoni Nestory Gerevazi (Miaka 32), Dereva wa Daladala iliyoungua iliyokuwa ikifanya safari za Bukoba – Mutukula, ameacha Mjane na watoto Watatu, ambapo kwa mujibu wa mke wake Bi. Adelina Marchol (34), anasema kuwa mumewe kabla ya mauti kumkuta aliondoka asubuhi kuelekea kazini mara baada ya kupigiwa simu na Tajiri wake (mmiliki wa Hiace) akimtaka aende na Leseni yake, baada ya kupakia na kuondoka kuelekea Mutukula, wakiwa njiani wakirejea walipofika Rwamisheneye ambapo ndipo makazi yao marehemu alimpigia simu Bi. Adelina akimfahamisha kuwa amerejea salama na mizigo alokuja nayo ataileta ngoja kwanza akashushe abiria stendi kuu ya mabasi. 

Baada ya hapo simu aliyoipata nyingine ilikuwa ya Dereva rafiki wa marehemu akimtaarifu habari za ajali na msiba. Kinachoumiza zaidi ni kuwa marehemu Nelsoni katika watoto wake watatu mmoja wa mwisho IVAN NELSON nae ni siku chache zimepita kapata ajali ya Kuungua kwa maji moto wakati akicheza na motto wa jirani na yupo anaugulia nyumbani huku msaada pekee ulikuwa ni baba yake mzazi.

Marehemu Dickson Ndyetabura Jackson (25), yeye ameanza kuendesha magari akitokea katika kazi ya ufundi magari maeneo ya Rwamishenye akiajiriwa na tajili wa kwanza na kuendesha fuso ambalo pia aliliterekeza polini maeneo ya Geita baada ya kuharibika kwa kipindi kirefu, Gari alilopata ajali nalo usiku ni gari amabayo ameanza kuiendesha kwa kipindi cha wiki moja na usiku wa ajali alikuwa akitokea Wilayani Missenyi kuchukua mzigo wa Matikiti maji.

Tayari jeshi la polisi Mkoani Kagera wamethibitisha vifo vya marehemu hao pamoja na marehemu wengine ambao ni pamoja na Peter Ifunya motto wa mwenye Daladala, na Bonge.
Mke  wa Marehemu Bi. Adelina Marchol (34), aliyefariki kwenye ajali hiyo

 Msiba ukiendelea nyumbani kwa marehemu

TAMASHA LA PASAKA KURINDIMA VIWANJA VYA POSTA, KIJITONYAMA JIJINI DAR

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Tamasha kubwa la Pasaka linalosubiriwa kwa hamu linatarajiwa kuanza kuwasha moto kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, April 21, 2019.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema tamasha hilo litakuwa la kihistoria kutokana na kuzunguka mikoa isiyopungua 10, amesema Mikoa hiyo itaongezwa kwa ajili yakutoa fursa kwa wengine kushuhudia burudani hiyo.

Msama amesema Mikoa ambayo imethibitishwa mpaka sasa kwa Wananchi kukaa mkao wa burudani ni Simiyu, Mwanza na Iringa ambayo imepitishwa na Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo.

‘’Wakazi wa Dar es Salaam na Mikoani mjiandae na Tamasha hili la Kihistoria, kuna Msanii mkubwa anatarajiwa kuhudhuria tamasha hili, si lakukosa’’, amesema Msama

Pia Msama amesema kuwa lengo kubwa kufanya Tamasha hilo ni kuombea Amani Taifa pamoja na Viongozi wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amefanya kazi kubwa na nzuri katika kipindi cha uongozi wake ndani ya miaka mitatu.

Kaulimbiu ya Tamasha hilo ni: Umoja na Upendo, hudumisha amani katika nchi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari maandalizi ya tamasha la Pasaka linalosubiriwa kwa hamu,ambalo linatarajiwa kuanza kuwasha moto kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, April 21, 2019. Msama amesema kuwa tamasha hilo litakuwa la kihistoria kutokana na kuzunguka mikoa isiyopungua 10, amesema Mikoa hiyo itaongezwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa wengine kushuhudia burudani hiyo.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Msama Promotions, Alex Msama alipokuwa akizungumza nao leo jijini Dar kuhusu muendelezo wa maandalizi ya tamasha la pasaka.

TANZIA: MKURUGENZI MKUU TPA ANATANGAZA KIFO CHA BABA YAKE MZAZI MZEE CONATUS VITALIS KAKOKO

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit C.V Kakoko anasikitika kutangaza kifo cha Baba yake mzazi, Mzee Conatus Vitalis Kakoko (81) kilichotokea juzi katika Hospitali ya Agakhan alipokuwa amelazwa kwa takribani wiki moja akisumbuliwa na maradhi ya Ini na Figo.

Hadi umauti unamkuta, Mzee Conatus Vitalis Kakoko ameacha watoto wanne (4) na wajukuu kumi na tano (15).

Misa ya kumuaga marehemu Mzee Conatus Vitalis Kakoko itafanyika katika kanisa la MT. Petrol lililopo Oysterbay siku ya Jumatatu, tarehe 11/2/2019 saa tatu asubuhi.

Mara baada ya misa hiyo, mwili wa marehemu Mzee Conatus Vitalis Kakoko utasafirishwa siku ya Jumatato tarehe 13/02/2019 kweda kijijini kwake, Munjebwe, Rulenge mkoani Kagera kwa mazishi.



Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa. Jina lake litukuzwe.

Wananchi watakiwa kushiriki katika kufanikisha elimu kwa wasichana

$
0
0
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dr. AveMaria Semakafa ameitaka jamii kuzingatia utoaji na upatikanaji wa elimu kwa kuhakikisha kwamba wanaboresha mazingira yake.
Akizungumza katika kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, alisema maelekezo mpya kuhusu elimu yanahitaji ushirikishaji wazazi katika kila jambo kwa lengo la kuwezesha utekelezaji wa sera ya elimu.
Mpango huo unaotekelezwa kwa majaribio katika wilaya za Ngorongoro, Sengerema, Kasulu na Mkoani kisiwa cha Pemba.
Alisema kwa sasa kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo wakaguzi wamepewa namna mpya ya ukaguzi wa maendeleo ya shule ikiwa ni pamoja na kuangalia majirani na wazazi.
Alisema ingawa kwa sasa wavulana ndio wanaocha shule kwa wingi kuliko wasichana, serikali imekazania wasichana kwa sababu mara zote msichana anapokwama kuendelea na shule huwa ndio mwisho wa ndoto zake.
“Watoto wa kiume wanaacha sana shule kuliko wasichana, lakini hawa huacha na kujitumbukiza katika fursa mbalimbali za kiuchumi, lakini wasichana wakikwama inakuwa ndio mwisho wao” alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.
Hata hivyo katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano kazi huo alisema kwamba tatizo la utamaduni linafanya maamuzi mengi katika namna ya kuokoa mtoto wa kike hapa nchini kuwa na sababu za kutofautiana.
Alisema wasichana wengine wanaacha shule si kwa sababu ya mimba, lakini ni kutokana na umbali wa shule na mazingira magumu ya kupata elimu hiyo; pia kuwapo kwa mabadiliko ya kimwili kwa kuzingatia asili ambayo humkatisha mwanamke siku 4 au sita kuhudhuria masomo kila mwezi.
Aidha alisema tatizo jingine ni saikolojia iliyoambatana na utamaduni ambapo wasichana wengi hushawishiwa na wazazi wao kutofanya vyema ili wasiendelee na shule.
Alisema kutokana na ukweli huo serikali imeanzisha kampeni ya kujenga hosteli na madomitori kwa ajili ya wasichana ili kuwapunguzia adha ya usafiri kwa kuangalia mazingira yao.
Alisema ingawa serikali inafahamu shida iliyopo kwa watoto wa kiume, kwa sasa mkazo uko kwa mabinti na baadae ndio wanaume.
Alisema hata hivyo kwamba serikali ya Tanzania inajikita zaidi katika kuhakikisha kwamba inatoa elimu ya msingi yenye ubora kwa wananchi kwa mujibu wa sera ya mwaka 2014 na kuwashukuru wadau kwa kuchangia katika kuimarisha elimu hiyo.
Alisema mipango mingi ya wadau ikiwemo ya kusoma kwa njia ya mtandao, mpango ulioanzishwa Ngorongoro sasa unafaa kusambazwa maeneo mengine yenye ugumu kama wilaya ya Igunga ambapo baadhi ya wanafunzi hulazimika kutembea kilomita 15 kufuata shule.
Pia alisema mradi kama huo wa kuwezesha mabinti unatia shime katika juhudi za serikali kuwakomboa wanawake na kwamba kazi inayofanywa na wadau ni ya kufanikisha sana.
Mradi huo unashirikisha mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNESCO, UNFPA, UN Women umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Korea (KOICA).
Katika mkutano huo kulijadiliwa ripoti za utekelezaji wa mradi kwa mwaka jana, matokeo yake na kupanga kazi za mwaka huu.
 Mwenyekiti wa semina ya kuwawezasha wasichana na wanawake katika elimu Tanzani, Dr. Ave Maria Semakafu (kushoto) ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi akifungua kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos.
 Naibu Mkurugenzi wa KOICA Tanzania, Inae Kim akifuatilia taarifa ya kamati ya kuwawezesha wasichana na wanawake katika elimu Tanzania wakati wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dkt. Edicome Shirima (wa pili kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos (wa pili kushoto) akichangia mada wakati wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa semina ya kuwawezasha wasichana na wanawake katika elimu Tanzani, Dr. Ave Maria Semakafu ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
 Msimamizi wa mradi wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA, Bi. Viola Kuhaisa akiwasilisha taarifa kwa washiriki wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu kilichofanyika katika Hotel ya Courtyard jijini Dar es Salaam
Washiriki wakisikiliza taarifa iliyowasilishwa na UNESCO wakati wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Picha ya pamoja ya wadau na waandaaji wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa semina ya kuwawezasha wasichana na wanawake katika elimu Tanzani, Dr Ave Maria Semakafu ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi katika picha na bango la mradi huo.

Bonanza la Muhimbili lafana, timu zagawana makombe

$
0
0
Bonanza la michezo lililoandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) limefana na kuleta ushindani mkubwa kwa timu shiriki za mpira wa pete na miguu za hospitali hiyo na hivyo timu hizo kugawana makombe.

Bonanza hilo limehusisha timu za Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Upanga pamoja na Hospitali Taifa Muhimbili-Mloganzila ambapo katika mchezo wa mpira wa Pete Muhimbili-Upanga imeichapa Muhimbili-Mloganzila magoli 17 kwa 1. Katika mchezo huo timu ya Mloganzila ilionekana kuelemewa kwani walipokua wakifika langoni mwa timu pinzani walishindwa kufunga na hivyo kuwapa uhakika wa kushinda mabao mengi.

Kwa upande wa mpira wa miguu katika kipindi cha kwanza dakika ya 14 timu ya  Muhimbili Mloganzila imeichabanga bao 1 kwa 0 timu ya Muhimbili Upanga bao lililofungwa na mshambuliaji machachari  Edger  Mtitu. Katika kipindi hicho  cha kwanza timu ya Muhimbili Mloganzila ilitawala mpira na kusababisha Muhimbili Upanga kushindwa kufurukuta uwanjani.

Baada ya kumalizika kwa mchuano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof. Lawrence Museru alizungumzia umuhimu wa kuendeleza michezo mahala pa kazi ili kudumisha amani, umoja na upendo na pia watumishi kuwa na afya bora hatua ambayo italeta tija katika maeneo ya kazi.

“Nitaendelea kuunga mkono suala la michezo na kusapoti kadiri inavyowezekana maana michezo ni afya, hivyo nawasihi watumishi wa Hospitali ya Muhimbili Upanga na Mloganzila kuendeleza michezo na mjitokeze kwa wingi kushiriki katika michezo mbalimbali,"amesema Prof. Museru.

Kwa upande wao washiriki wa Bonanza hilo wameushukuru uongozi wa hospitali kwa kufanikisha shughuli hiyo ambayo imewaweka karibu watumishi wote wa MNH Upanga na Mloganzila. Bonanza la michezo la Hospitali ya Taifa Muhimbili, Upanga na Mloganzila limefanyika katika viwanja vya michezo vya Jakaya Kikwete Youth Park Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akishangilia ushindi wa timu ya mpira wa pete baada ya timu hiyo kuifunga timu ya pete ya Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila magoli 17-1 katika mchezo wa Bonanza uliofanyika katika  Viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu) jijini Dar es Salaam.  Wengine katika picha ni  wakurugenzi na watumishi wa hospitali hizo wakishangilia pamoja.
 Kepteni wa timu ya mpira wa miguu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila akishangilia baada ya kuifunga timu ya Muhimbili ,Upanga bao moja kwa sifuri. Muhimbili Mloganzila 1-0 Muhimbili Upanga. Wengine katika picha hii ni Wakurugenzi wa Muhimbili Upanga na Muhimbili Mloganzila.
 Mashabiki wa timu ya mpira wa miguu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wakishangilia pamoja baada ya timu yao kuifunga timu ya Muhimbili Upanga bao 1-0.
 Mashabiki wa mpira wa miguu wakifuatilia mechi kati ya timu ya Muhimbili Upanga na Muhimbili-Mloganzila.
 Mechi ikiendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu) leo.
 Wachezaji wa mpira wa pete wa Muhimbili Upanga wakiifungia timu yao bao la sita katika mchezo uliofanyika Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu).  Muhimbili Upanga 17- 1 Muhimbili-Mloganzila.
 Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mpira wa pete uliofanyika leo kwenye viwanya vya  Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu).  
 Baadhi ya watumishi wa Muhimbili wakifanya mazoezi ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wa mpira wa pete na mpira wa miguu.
 Watumishi wa hospitali hizo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Bonanza hilo.
Wachezaji wa Muhimbili Upanga na Muhimbili-Mloganzila wakiwa katika picha ya pamoja.

Dkt. Gwajima Awashukia TAMISEMI, Awaonya Ubinafsi

$
0
0
Na. Atley Kuni- Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya Afya Dkt. Dorothy Gwajima, amewaonya na kuwatahadharisha watendaji katika ofisi hiyo kuepuka ubinafsi na kuwahimiza kufanya kazi kwa pamoja. Dkt.Gwajima ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, wakati wa kikao kazi kilicho wakutanisha Wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi na Maafisa wa Wizara hiyo kutoka Idara za TEHAMA pamoja na Afya, wkati wa wasilisho la mfumo wa uendeshaji wa shughuli za Serikali (GoTHOMIS).

 Alisema,iliwaweze kufanikiwa lazima wafanye kazi kama timu moja bila kubaguana na kuonya, tabia ya ubinafsi sio nzuri na kama wanataka kukwama katika mipango yao watangulize ubinafsi mbele badala ya maslahi ya nchi kwanza. “Mimi sipo tayari kuona tunakwama wakati nilikula kiapo mbele ya Mhe. Rais, ni bora mniondoe lakini nitasimama katika kweli .“alisema Gwajima.

 Dkt.Gwajima alisema anashangazwa na mataifa ya Ulaya kuendelea kupiga hatua kwenye maendeleo huku Watanzania tukibaki nyuma. “Lakini kikubwa ninacho kiona ni hali ya uratibu (Cordination) ndio changamoto kubwa katika utendaji wetu wa kila siku.” alibainisha Dkt.Gwajima.

Naibu Katibu Mkuu huyo, amezitaka Idara hizo kushirikiana kwa karibu hasa ikizingatiwa mabadiliko ya sasa ya sayansi na teknolojia yanahitaji uwajibikaji wa pamoja. “Natambua tunafanya kazi nzuri sana, lakini bila kuishirikisha kwa karibu idara ya TEHAMA, hatutaweza kufika tunapotaka kwenda” alisema Gwajima.

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi kutoka Idara ya Afya wizarani hapo, Dkt. Anastazia Nswila, aliwataka wajumbe kuwa na msimamo  mmoja katika maamuzi, kuacha kutegemea na kupangiwa misaada mbalimbali kutoka kwa wadau . “Wadau wana pesa nyingi, isiwe sababu yakutupangia nini watatuletea, ni vizuri mahitaji yatoke kwetu sisi, kama ni Laptop tuwaambie ni aina gani tunataka, kama ni vifaa tiba huko kwenye kwenye vituo sisi ndio wakuamua aina gani ya vifaa vinafaa kulinga na mazingira yetu” alisisitiza Dkt. Nswila.

Kikao hicho kilichodumu kwa takribani saa 3 kimetoka na maazimio matano ikiwepo, kuandaliwa mafunzo maalumu kwaajili yakuwawezesha idara mama ya masuala ya afya kuutambua mfumo, kuandaa andiko la jinsi gani Wizara hiyo inavyofanya katika mfumo huo, kila Wizara ifanye maamuzi ya kisekta ya ndani kabla yakukutana TAMISEMI na Wizara ya Afya, na mwisho kuwa na kikao cha wadau ili kuwapa muelekeo na msimamo wa Serikali.
 Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI (Afya), Dkt. Dorothy Gwajima alipokuwa akiongea na watendaji hao wa Wizara wakati wa kikao cha kupitia mifumo ya Afya kwenye ukumbi wa Reform mkoani Dodoma.
 Moja ya Wakurugenzi, Dkt. Anna Nswila, akichangia mada wakati wa kikao cha kupitia mifumo ya Afya kwenye ukumbi wa Reform mkoani Dodoma.
Mmoja ya maafisa wa Wizara hiyo, aliposimama kushauri jambo wakati wa kikao cha kupitia mifumo ya Afya kwenye ukumbi wa Reform mkoani Dodoma.
 Baadhi ya wakurugenzi, Wakurugenzi wasaidizi na maofisa wengine wa Wizara hiyo, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Dkr. Dorothy Gwajima wakati wa kikao cha kupitia mifumo ya Afya kwenye ukumbi wa Reform mkoani Dodoma.
  Naibu katibu Mkuu na Timu ya (RHMT) ya Mkoa wa Dodoma alipofanya ziara yake ya kwanza na kuhimiza uwajibikaji na uratibu wa kazi kwa pamoja wakati wa ziara yake ya kwanza toka aingia katika Wizara hiyo aliyoifanya kwenye Sekretarieti ya mkoa wa Dodoma. (Picha na habari na Atley Kuni-OR-TAMISEMI)


Benki ya Standard Chartered yazindua programu ya “Goal” in Tanzania

$
0
0
BENKI ya Standard Chartered imetangaza uzinduzi wa program ya Goal ikishirikiana na taasisi ya BRAC Tanzania.Programu hiyo imelenga kuwawezesha wasichana kupitia michezo na taaluma za maisha. Programu hiyo imeingia katika awamu yake ya pili. Kwa mujibu wa Benki ya Standard Chartered program hiyo inawezesha wasichana kujifunza mambo ambayo yatawafanya kuwa viongozi wa kiuchumi katika familia zao, jamii na taifa.

Mafunzo hayo yamelenga kuwajenga wasichana hao katika ngazi za kujiamini, elimu na ujuzi mahsusi wa kuwafanya kuwa viongozi. Programu hiyo awali ilizinduliwa nchini Tanzania mwaka 2013 na kulenga kuwafikia wasichana na wavulana 15,000 katika kipindi cha miaka miwili ikiwapatia uwezo wa taaluma za maisha. Mkuu wa Masuala ya Kisheria, Masoko na Bidhaa wa benki hiyo, Juanita Mramba amesema benki hiyo imefurahishwa na mafanikio katika awamu ya kwanza hasa kutokana na jamii kuwa na msisimuko mkubwa wa program hiyo na hasa wasichana walivyowezeshwa kubadilisha maisha.

Awamu mpya ya programu ya GOAL imelenga kuwapatia taaluma za ujasiriamali na hali ya kuajirika kwa kuzingatia ajenda za kitaifa ya kuelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sanjay Rughani alisema ni matarajio yake kwamba wasichana watapatiwa ujuzi unaohitajika ili kuwawezesha kuanzisha na kuendesha biashara zao kuajiri wengine na hata wao kuajiriwa.

Kwa mujibu Juanita, programu hiyo itaambatana na mafunzo ya michezo na elimu. Alisema wale ambao wataonesha uwezo mkubwa wa uongozi wataingizwa kuwa machampioni wa Goal.
Ili kuifanikisha programu kuwa endelevu Goal inaendeshwa kwa mtindo wa kufunza walimu.
Programu hiyo inaendeshwa kwa pamoja kati ya benki hiyo na BRAC Tanzania ambayo ina sifa ya kuwawezesha watu waliokosa nafasi kupata elimu.

BRAC Tanzania pia imejijengea uwezo mkubwa kuwawezesha wasichana kupata taaluma wanazohitaji katika maisha na kuwapatia nafasi ya kupata mikopo midogo na uanzishaji wa viwanda na biashara ndogo. Chini ya program ya GOAL, BRAC Tanzania itasaidia wasichana kati ya miaka 13-24 kufikia kiwango cha juu cha kiuchumi kwa kuwawezesha mafunzo na kuwapatia usimamizi.
Programu hiyo itahakikisha inawapatia uwezo wa kuanzisha biashara katika Nyanja kama ya ushoni, ususi na kilimo. Programu hiyo pia itawawezesha wasichana kupata kazi kokote. Rughani amesema kwamba awamu mpya ya GOAL itsaidia kukuza ujasiriamali na utengenezaji wa nafasi za ajira.
 Mgeni rasmi  Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ally Msaki (kulia) akitoa hotuba kabla ya kuzindua Programu ya Goal inayowalenga wasichana wenye umri wa miaka 16-18 inayofadhiliwa na benki ya Standard Chartered uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mchumi Mkuu wa benki ya Standard Chartered kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati, Radhia Khan akihutubia wasichana katika uzinduzi wa Programu ya Goal inayoendeshwa na benki hiyo katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Rayson Foya akieleza malengo ya Programu ya Goal inayowalenga wasichana wenye umri wa miaka 16-18 inayofadhiliwa na benki hiyo katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam
 Wasichana walengwa wa Programu ya Goal wakimsikiliza mgeni rasmi wakati akisoma hotuba yake katika hafla fupi ya uzinduzi wa programu hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mchumi Mkuu wa benki ya Standard Chartered kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati, Radhia Khan akipiga mpira ishara ya kuzindua Programu ya Goal wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Programu ya Goal  inayowalenga wasichana wenye umri wa miaka 16-18 inayofadhiliwa na benki ya Standard Chartered katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi rasmi  Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ally Msaki katika picha ya pamoja na meza kuu mara baada ya kuzindua Programu ya Goal  inayowalenga wasichana wenye umri wa miaka 16-18 inayofadhiliwa na benki ya Standard Chartered katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi rasmi  Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ally Msaki katika picha ya pamoja na wanufaikaji wa Programu ya Goal mara baada ya kuzindua Programu hiyo inayowalenga wasichana wenye umri wa miaka 16-18 inayofadhiliwa na benki ya Standard Chartered katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Rayson Foya akitambulishwa kwa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou (wa pili kulia) aliyeambatana na Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa (wa pili kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ally Msaki (kulia) akiwasili kwenye eneo la tukio akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Rayson Foya (katikati) pamoja na Mchumi Mkuu wa benki ya Standard Chartered kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati, Radhia Khan wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Programu ya Goal inayowalenga wasichana wenye umri wa miaka 16-18 inayofadhiliwa na benki ya Standard Chartered jijini Dar es Salaam.

WAZIRI UMMY AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI - MTUMBA DODOMA

$
0
0
Na WAMJW - DOM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amewaongoza Watumishi wa Wizara ya Afya katika zoezi la upandaji miti katika mji mpya wa Serikali ulio katika kata ya  Mtumba, tarafa ya Kikombo Jijini Dodoma.
Katika zoezi hilo Waziri Ummy ameagiza Watumishi wote waliohusika katika upandaji wa miti hiyo kuhakikisha wanaitunza vizuri isitawi, na ameagiza kila mtu kuchukua jukumu hilo. "Hii miti ambayo tumeipanda sio tu miti ya kivuli na mapambo tu, bali imejumuisha miti ya matunda. Miti hii ambayo tunaipanda ili ikue na kustawi, lazima kila mtu, ambae amepanda mti wake kuhakikisha kwamba haufi" Alisema Waziri Ummy.
Mbali na hayo, Waziri Ummy amemwagiza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Cheula kutenga maeneo kwa ajili ya Watumishi kufanya mazoezi ikiwa ni mpango wa Serikali ya awamu ya Tano kupambana na Magonjwa yasiyo yakuambukiza. "Mazingira ya hapa ni mazuri kweli kutembea, ukizunguka huu mji hukosi Kilomita 5, nitamwandikia Waziri  Jenister atusaidie kuwa na mabafu kwa ajili ya watu wanaofanya mazoezi kubadilisha nguo jioni, ni lazima sehemu za kazi ziwe rafiki kwa watu kufanya mazoezi" alisema Waziri Ummy.
Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amempongeza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula na kikundi chake kwa kuja na wazo la upandaji wa miti katika mji huo, na kuwa mfano wa kuigwa na Wizara nyingine. Katika zoezi hilo lililojumuisha viongozi mbalimbali wa wizara, jumla ya miti 470 imepandwa katika awamu ya kwanza, lengo ikiwa ni kupanda miti 525. Miti 320 iliyopandwa ni ya matunda, na mingine ni kwa ajili ya mapambo na kivuli.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akijiandaa kupanda mti, wakati  wa zoezi la upandaji miti katika Mazingira ya jengo la Wizara ya Afya lililo katika mji wa Serikali katika kata ya Mtumba jijini Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimwagilia maji mti wake aliopanda, wakati  wa zoezi la upandaji miti lililo fanywa na Watumishi wa Wizara ya Afya katika mji wa Serikali ulio kata ya Mtumba jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akimwagilia maji mti alioupanda katika Mazingira ya Wizara ya Afya, yaliyo katika Mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba jijini Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akiweka mbolea katika mti wake, katika Mazingira ya jengo la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililo katika mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula (Wakatikati) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku  (Wakulia) na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi (Wakwanza kushoto)
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifanya ukaguzi wa jengo la Wizara ya Afya lililo katika hatua ya mwisho, leo wakati wa zoezi la upandaji miti katika Mazingira ya jengo la Wizara ya Afya lililo katika mji wa Serikali katika kata ya Mtumba jijini Dodoma.

Muonekano wa jengo la Wazara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililo katika mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba jijini Dodoma,  jengo hilo liko katika hatua ya mwisho ya ujenzi

WAZIRI MKUU ATOA SIKU 21 KWA VIWANDA VYA VILEO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 21 kwa viwanda vyote vinavyozalisha vileo nchini viwe vimefunga mfumo ukusanyaji kodi kwa kutumia stempu za kielektroniki. Pia ameziagiza Wizara na Taasisi zote za Umma ziwe zimejiunga na Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji na usimamizi wa maduhuli (GePG) kabla ya Juni mwaka huu.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumamosi, Februari 9, 2019) , wakati akiahirisha mkutano wa kumi na nne wa Bunge la kumi na moja, Bungeni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) isimamie uwekaji wa mifumo hiyo na ifikapo februari 28, 2019 kila kiwanda kiwe kimefunga mfumo huo.

 “Naielekeza TRA kusimamia uwekaji wa mifumo ya kukusanya kodi za vileo kwa kutumia stempu za kielektroniki kwa viwanda vyote vinavyozalisha vinywaji hivyo.” Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuongeza mapato na kuimarisha usimamizi wa matumizi ya fedha na rasilimali za umma ili kufikia malengo.

Miongoni mwa mikakati hiyo ni kutumia mfumo wa kielektroniki wa stempu za kodi kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa na zile zinazoingizwa nchini. Waziri Mkuu amesema mfumo huo utasaidia Serikali katika kupata taarifa sahihi za uzalishaji na kupunguza uvujaji wa mapato ya Serikali.

 Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. John Magufuli aliyoyatoa Januari 22, 2019, alipokutana na wadau wa sekta ya madini. AmesemaSerikali imefutaKodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Zuio ya asilimia  tano ya mwisho inayotozwa kwenye bei ya kuuzia madini ya aina zote kwa wachimbaji hao. 

 Waziri Mkuu amesema hatua hiyo inatarajiwa kupunguza utoroshwaji wa madini; kuwatambua wachimbaji wadogo kupitia masoko ya madini yatakayoanzishwa. Pia itasaidia kuwapunguzia gharama wachimbaji wadogo na hivyo kuendesha shughuli zao kwa ufanisi pamoja na kuongeza wigo wa mapato kwa kuwa madini yatauzwa ndani ya nchi. 

“Nitoe rai kwa wachimbaji wote wadogo kushirikiana na Mamlaka mbalimbali za Serikali kutekeleza maazimio yaliyofikiwa katika kikao na Mheshimiwa Rais.” Amesema siku zote Watanzania wanamuenzi Rais Dkt. John Magufuli, kwa hatua za makusudi anazochukua katika kuhakikisha anaimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato. Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli anafanya hayo yote kwa lengo la kuona Tanzania inapunguza utegemezi wa misaada kutoka katika mataifa mengine.

“Mifano maelekezo aliyoyatoa kwa Mawaziri, Wakuu wa Mikoa wawasilishe mapendekezo kuhusu namna bora ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani katika maeneo yao.” Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imeshapokea mapendekezo hayo na imetoa maagizo mahsusi kwa TRA na TAMISEMI zishirikiane katika ukusanyaji wa kodi za majengo.

Akizungumzia kuhusu hali ya uchumi, Waziri Mkuu amesema imeendelea kuimarika, ambapo kati ya Januari hadi Septemba 2018, pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 6.2 katika kipindi kama hicho mwaka 2017. AmesemaOngezeko hilo la ukuaji wa uchumi limechochewa zaidi na uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu hususan ujenzi wa barabara, reli na viwanja vya ndege.

 Waziri Mkuu amesema masuala mengine yaliyochangia ukuaji mzuri wa uchumi ni kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati na hali nzuri ya hewa kwa upande wa kilimo. “Shughuli za kiuchumi zilizoendelea kutoa mchango mkubwa katika pato la Taifa kwa kipindi hicho ni kilimo (asilimia 33.4), ujenzi (asilimia 15.7) na biashara (asilimia 10.2).”

Amesema kutokana na umuhimu wa sekta ya kilimo, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, kuhakikisha pembejeo za kilimo zinapatikana kwa wakati. Pia kuhakikisha huduma za ugani zinaimarishwa katika maeneo yote nchini pamoja na  kuboresha upatikanaji wa miundombinu ya hifadhi na masoko. Lengo la Serikali ni kuongeza tija kwenye uzalishaji wa mazao ya kilimo na hivyo kumwongezea kipato mkulima kitakachomwezesha kujikimu na kujikwamua na umaskini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba  ya kuahirisha Bunge jijini Dodoma, Februari  9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

STEVE NYERERE AMUOMBA RADHI OMMY DIMPOZ,AMWAMBIA KAULI YAKE HAIKUWA NA NIA MBAYA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Glob ya Jamii 

MUIGIZAJI maarufu nchini Steven  Mengere almaarufu Steve Nyerere amemuomba radhi msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpozy.

Kwa kukumbusha Steve Nyerere alitoa kauli ya kwamba Ommy Dimpoz hawezi tena kutoa nyimbo yeyote kutokana na maradhi yanayomsumbua.

Hata hivyo msanii Ommy Dimpoz ameipua wimbo wake kabisa unaokwenda kwa jina la Ni wewe.Steve Nyerere baada ya Kutoka kwa wimbo huo amekuwa akishambuliwa na makundi ya watu mbalimbali mitandaoni .

Kupitia ukurasa wake wa Istagramu Steven Nyerere leo februari 9,2019 ameandika hivi ." kwanza nichukuwe fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu ,lakini pili nichukuwe fursa hii kumuomba radhi ndugu yangu Dimpoz kwa namna alivyopokea kauli yangu niliyoitoa dhidi yake na zaidi niwaombe radhi watanzania wote na wapenzi wa Sanaa .Binadamu unapoona hapa umekosea busara inatutaka kukiri kukosea nami nikiri kukosea kutokana na ile kauli yangu kwa Dimpoz.

" Lakini ifahamike kwamba kauli ile haikuwa kwamba namtakia mabaya Dimpoz hapana ila kwa tulivyokuwa tunapata taarifa kwakweli zilikuwa zinatukatisha tamaa," amesema Steve Nyerere.

Ameongeza kuwa mengi yameongelewa lakini ifahamike kwamba hakuwa na nia mbaya wala hakuwa na ugomvi na Dimpoz bali kama Binadamu hutokea kuteleza kwenye kuzungumza na hivyo asichukuliwe kwaniambaya .

"Lakini tunafahamu kwamba Mwenyezi Mungu hufanya miujiza yake kutokana na sababu furani hivyo miujiza ya kumuinua ndugu yetu na kurudi kwenye kazi zake imetokana na imani aliyonayo Dimpoz kwa muumba wake.

" Najua mie niliteleza kwa kusema kwamba Dimpoz hatoimba tena lakini sikuwa na nia hiyo ,kwangu natamani Dimpoz asiimbe tena Hapana kutokana na vichekesho mbalimbali vinavyotolewa juu yangu lakini vinanifurahisha kwani vinazidi kuupaisha wimbo mpya wa Ni wewe. 

"Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba watanzania na wapenzi wa
Muziki kuzidi kumsapoti ndugu yetu pamoja na Kumuombea dua kwa Mwenyezi Mungu ili azidi kuimarika kiafya."amesema Steven Nyerere.
Ikumbukwe kuwa Ommy Dimpoz kwa muda mrefu amekuwa kimya katika muziki kutokana na kusumbuliwa na tatizo la koo ambapo alilazimika kwenda nje ya nchi kwa matibabu .

Hata hivyo kwasasa afya yake imeimarika na tayari ametoa wimbo mpya wa Ni wewe ambao umeaza kukubalika na kupendwa na wapenzi wa muziki.

WE WILL NEVER ALLOW YOU TO FLOOD THE BOAT FOR ALL OF US

$
0
0
  I don’t doubt many politicians have done things worthy of regret, but it is becoming difficult to keep up with the sorry spectacle. I would like to share with you this story, please take some few minutes to read it.

“A group of people were travelling in a boat. One of them took a drill and began to drill a hole beneath himself. His colleagues said to him: “Why are you doing this?” The man replied: “Why are you concerned about it? Am I not drilling under my own place?” They said to him: “But you will flood the boat for all of us!” 

Imagine being a passenger on this boat, and one person, without concern for you or others, endangers  your safety and security. The person drilling a hole on the boat may have valid reasons for doing so. Perhaps they want to drop a fishing line because they are hungry. Maybe they want to use the water to cool their feet or wash. Maybe the boat is on a lake and they want water to drink. But no matter how rational the reason, drilling a hole in a boat to fulfill the desires of just one individual jeopardizes everyone’s safety. 

This story warns us of the destructive power of letting our selfish desires overtake all other considerations. It’s not about whatever floats your boat.”



It is true that patriotism has lost feeling for most of politicians, the hierarchy of importance has been Self, family, friends and finally Country. Self interests has driven politicians to the extent of setting their peaceful Countries to war, for example in 1992 Angola ,more than 300,000 people died, in 1994 more than 800,000 died in Rwanda. I believe under President Magufuli’s administration this will not happen, he promised to protect Tanzanian and he is walking the talk.

Tindu Lissu may have valid reasons for what he is currently doing , touring abroad and tarnishing our Country’s image, he might be revenging against the so called “unknown people” thinking that the government is behind them for the tragedy incident which happened to him in Dodoma. He may also have hidden intentions such as trying to win a Presidential nomination from his political party and therefore gaining popularity through western media. However no matter how rational the reason may seem to him, spoiling your Country’s reputation globally has absolutely no excuse, and therefore he needs to apologize to Tanzanians for what he has done to our beloved Tanzania.


For a mature politician who was born and raised up in Tanzania, studied in Tanzania where education by the time was free, and he was paid by the Government at University level, cannot be pushed this far by circumstantial evidence of the tragic incident that happened to him. The wise thing is to cooperate with the police and other security organs to allow intensive investigation of the incident and send the suspects to the court of law.

Moreover, you seem to be in a fit state to come back home and continue with your responsibility of representing your constituency, bearing in mind in several occasions people have believed in you and voted for you to represent them in Parliament, it is not that you are very special among other people in your constituency, but the person your people used to see inside you before becoming greedy and start drilling the boat Tanzania to fulfill your desires. The cost of doing what you’re doing in western media will be reflected in vote ballot in 2020! be careful for the citizens of Tanzania love President Magufuli because he is working for them.

Another important advice, please learn to appreciate, too much demanding is not going to help you, there are so many good things the people and Government of Tanzania has done to you, the Government has paid for your medical expenses with taxpayers money when you were in Nairobi, more than Tsh 246.7 million has been paid in Belgium.

Now letting you destroy the plate in which more than 50 million Tanzanians are served including yourself by spreading malicious lies against Tanzanians and the Government is unacceptable. Who doesn’t know what the current Administration has done, in three years time? We have corruption in the Country going down and public embezzlement diminishing faster than ever. 


President Magufuli has revived the public airline which had only one plane with six brand new airplanes which has facilitated local and international trade, major projects with significant impact to ordinary people’s income are underway like Stigler’s Gauge, SGR project, Port expansions and road networks to name a few. 

My fellow Tanzanian Mr.Lissu, as you may be aware in fighting corruption and bringing about real economic transformation for a developing country like Tanzania there are serious challenges, this shift will never bring smile to those who are greedy and those who want to see us as a receiving Country other than a donor Country. 

Those who believe that this positive transformation Tanzania is going through is a threat to their interests will never stop fighting to undermine the efforts of our beloved President Dr John Magufuli. It is true that corruption in most of African countries have benefited a few people, record shows how much politicians like you have benefited from minerals contracts,and other contracts when working in different parliamentary committees as well as the foreign countries.

I would therefore advice my fellow Tanzanian Mr Lissu, that it seems he is one of the very few people in Tanzania who have a notion that, Tanzania is still under colonialism and not a free country. It is high time you realize that Tanzania is a free Country and can choose between what is democracy and what is violence, what is free speech and what is hate speech, as well as crime. We are governed by a Constitution and the rule of Law.

Most of our people and good friends of Tanzanian appreciates what Dr Magufuli is doing, the benefits of trade can be enjoyed in a peaceful and democratic state, and democracy can be exercised in a peaceful environment. One cannot exercise true democracy where there is no peace.We are sailing in this boat together , therefore we will never allow you to drill a hole and flood our Boat Mr.Tundu Lissu.


Eng Abdalah Kileo 



Bonanza la Muhimbili lafana, timu zagawana makombe

$
0
0



 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akishangilia ushindi wa timu ya mpira wa pete baada ya timu hiyo kuifunga timu ya pete ya Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila magoli 17-1 katika mchezo wa Bonanza uliofanyika katika  Viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu) jijini Dar es Salaam.  Wengine katika picha ni  wakurugenzi na watumishi wa hospitali hizo wakishangilia pamoja.
????????????????????????????????????
Kepteni wa timu ya mpira wa miguu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila akishangilia baada ya kuifunga timu ya Muhimbili ,Upanga bao moja kwa sifuri. Muhimbili Mloganzila 1-0 Muhimbili Upanga. Wengine katika picha hii ni Wakurugenzi wa Muhimbili Upanga na Muhimbili Mloganzila.
????????????????????????????????????
Mashabiki wa timu ya mpira wa miguu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wakishangilia pamoja baada ya timu yao kuifunga timu ya Muhimbili Upanga bao 1-0.
????????????????????????????????????
Mashabiki wa mpira wa miguu wakifuatilia mechi kati ya timu ya Muhimbili Upanga na Muhimbili-Mloganzila. 
005
Mechi ikiendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu) leo.
????????????????????????????????????
Wachezaji wa mpira wa pete wa Muhimbili Upanga wakiifungia timu yao bao la sita katika mchezo uliofanyika Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu).  Muhimbili Upanga 17- 1 Muhimbili-Mloganzila.
????????????????????????????????????
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mpira wa pete uliofanyika leo kwenye viwanya vya  Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu).
008
Baadhi ya watumishi wa Muhimbili wakifanya mazoezi ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wa mpira wa pete na mpira wa miguu.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Wachezaji wa Muhimbili Upanga na Muhimbili-Mloganzila wakiwa katika picha ya pamoja.
…………………………………………………………………………
Bonanza la michezo lililoandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) limefana na kuleta ushindani mkubwa kwa timu shiriki za mpira wa pete na miguu za hospitali hiyo na hivyo timu hizo kugawana makombe.
Bonanza hilo limehusisha timu za Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Upanga pamoja na Hospitali Taifa Muhimbili-Mloganzila ambapo katika mchezo wa mpira wa Pete Muhimbili-Upanga imeichapa Muhimbili-Mloganzila magoli 17 kwa 1.
Katika mchezo huo timu ya Mloganzila ilionekana kuelemewa kwani walipokua wakifika langoni mwa timu pinzani walishindwa kufunga na hivyo kuwapa uhakika wa kushinda mabao mengi.
Kwa upande wa mpira wa miguu katika kipindi cha kwanza dakika ya 14 timu ya  Muhimbili Mloganzila imeichabanga bao 1 kwa 0 timu ya Muhimbili Upanga bao lililofungwa na mshambuliaji machachari  Edger  Mtitu. Katika kipindi hicho  cha kwanza timu ya Muhimbili Mloganzila ilitawala mpira na kusababisha Muhimbili Upanga kushindwa kufurukuta uwanjani.
Baada ya kumalizika kwa mchuano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof. Lawrence Museru alizungumzia umuhimu wa kuendeleza michezo mahala pa kazi ili kudumisha amani, umoja na upendo na pia watumishi kuwa na afya bora hatua ambayo italeta tija katika maeneo ya kazi.
“Nitaendelea kuunga mkono suala la michezo na kusapoti kadiri inavyowezekana maana michezo ni afya, hivyo nawasihi watumishi wa Hospitali ya Muhimbili Upanga na Mloganzila kuendeleza michezo na mjitokeze kwa wingi kushiriki katika michezo mbalimbali,”amesema Prof. Museru.
Kwa upande wao washiriki wa Bonanza hilo wameushukuru uongozi wa hospitali kwa kufanikisha shughuli hiyo ambayo imewaweka karibu watumishi wote wa MNH Upanga na Mloganzila.
Bonanza la michezo la Hospitali ya Taifa Muhimbili, Upanga na Mloganzila limefanyika katika viwanja vya michezo vya Jakaya Kikwete Youth Park Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam.

WAZIRI MKUU ATOA SIKU 21 KWA VIWANDA VYA VILEO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 21 kwa viwanda vyote vinavyozalisha vileo nchini viwe vimefunga mfumo ukusanyaji kodi kwa kutumia stempu za kielektroniki.

Pia ameziagiza Wizara na Taasisi zote za Umma ziwe zimejiunga na Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji na usimamizi wa maduhuli (GePG) kabla ya Juni mwaka huu.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumamosi, Februari 9, 2019) , wakati akiahirisha mkutano wa kumi na nne wa Bunge la kumi na moja, Bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) isimamie uwekaji wa mifumo hiyo na ifikapo februari 28, 2019 kila kiwanda kiwe kimefunga mfumo huo.

“Naielekeza TRA kusimamia uwekaji wa mifumo ya kukusanya kodi za vileo kwa kutumia stempu za kielektroniki kwa viwanda vyote vinavyozalisha vinywaji hivyo.”Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuongeza mapato na kuimarisha usimamizi wa matumizi ya fedha na rasilimali za umma ili kufikia malengo.

Miongoni mwa mikakati hiyo ni kutumia mfumo wa kielektroniki wa stempu za kodi kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa na zile zinazoingizwa nchini. Waziri Mkuu amesema mfumo huo utasaidia Serikali katika kupata taarifa sahihi za uzalishaji na kupunguza uvujaji wa mapato ya Serikali.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. John Magufuli aliyoyatoa Januari 22, 2019, alipokutana na wadau wa sekta ya madini. AmesemaSerikali imefutaKodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Zuio ya asilimia tano ya mwisho inayotozwa kwenye bei ya kuuzia madini ya aina zote kwa wachimbaji hao. 
Waziri Mkuu amesema hatua hiyo inatarajiwa kupunguza utoroshwaji wa madini; kuwatambua wachimbaji wadogo kupitia masoko ya madini yatakayoanzishwa.

Pia itasaidia kuwapunguzia gharama wachimbaji wadogo na hivyo kuendesha shughuli zao kwa ufanisi pamoja na kuongeza wigo wa mapato kwa kuwa madini yatauzwa ndani ya nchi. “Nitoe rai kwa wachimbaji wote wadogo kushirikiana na Mamlaka mbalimbali za Serikali kutekeleza maazimio yaliyofikiwa katika kikao na Mheshimiwa Rais.”

Amesema siku zote Watanzania wanamuenzi Rais Dkt. John Magufuli, kwa hatua za makusudi anazochukua katika kuhakikisha anaimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato.Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli anafanya hayo yote kwa lengo la kuona Tanzania inapunguza utegemezi wa misaada kutoka katika mataifa mengine.

“Mifano maelekezo aliyoyatoa kwa Mawaziri, Wakuu wa Mikoa wawasilishe mapendekezo kuhusu namna bora ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani katika maeneo yao.”Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imeshapokea mapendekezo hayo na imetoa maagizo mahsusi kwa TRA na TAMISEMI zishirikiane katika ukusanyaji wa kodi za majengo.

Akizungumzia kuhusu hali ya uchumi, Waziri Mkuu amesema imeendelea kuimarika, ambapo kati ya Januari hadi Septemba 2018, pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 6.2 katika kipindi kama hicho mwaka 2017. 

AmesemaOngezeko hilo la ukuaji wa uchumi limechochewa zaidi na uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu hususan ujenzi wa barabara, reli na viwanja vya ndege.Waziri Mkuu amesema masuala mengine yaliyochangia ukuaji mzuri wa uchumi ni kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati na hali nzuri ya hewa kwa upande wa kilimo.

“Shughuli za kiuchumi zilizoendelea kutoa mchango mkubwa katika pato la Taifa kwa kipindi hicho ni kilimo (asilimia 33.4), ujenzi (asilimia 15.7) na biashara (asilimia 10.2).”

Amesema kutokana na umuhimu wa sekta ya kilimo, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, kuhakikisha pembejeo za kilimo zinapatikana kwa wakati.Pia kuhakikisha huduma za ugani zinaimarishwa katika maeneo yote nchini pamoja na kuboresha upatikanaji wa miundombinu ya hifadhi na masoko. 

Lengo la Serikali ni kuongeza tija kwenye uzalishaji wa mazao ya kilimo na hivyo kumwongezea kipato mkulima kitakachomwezesha kujikimu na kujikwamua na umaskini.

KIKOSI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UHALIFU NCHINI KIMEFANIKIWA KUWAKAMATA WAHUSIKA 30 WA MATUKIO YA MAUAJI MKOANI NJOMBE

$
0
0



 Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas,ameongoza kikosi maalum katika kupambana na uhalifu nchini kilichoungana na vikosi  vya jeshi la Polisi mkoa wa Njombe katika kufanya Operesheni katika mapori ya  Nundu na Tanwat mkoani Njombe kuwasaka watuhumiwa wa Mauaji ya watoto. Picha na jeshi la Polisi     


 Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa Njombe Kamishina Msaidizi Mwandamizi SACP Afande  Renata Mzinga  wameongoza kikosi maalum cha  kupambana na uhalifu nchini kilichoungana na vikosi  vya Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe katika kufanya Operesheni katika mapori ya  Nundu na Tanwat mkoani Njombe.(Picha na jeshi la Polisi) 




Jeshi la Polisi Makao Makuu Kitengo Maalum cha Kupambana na uhalifu kikiongozwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, kimeshirikina na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe kuendesha Operesheni Maalum ya kukabiliana na matukio ya mauaji ya watoto wadogo ambayo yamejitokeza mkoani humo, mpaka sasa watuhumiwa 30 wamekamatwa waliojihusisha na matukio hayo, 

Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, amesema watuhumiwa hao ifikapo Jumatatu watakuwa wamefikishwa Mahakamani kukabiliana na tuhuma za mauaji ya watoto, Aidha Naibu Kamishna Sabas, amewataka watanzania kutoa Taarifa za wahalifu popote walipo na amewahakikishia watanzania kuwa matukio hayo yamekoma sasa 

Aidha Naibu kamishna Sabas amesema Jeshi La Polisi halitamuonea mtu yoyote haya awe Mfanyabishara, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Dini, au Waganga wa Kienyeji watakaojihusisha na matukio ya mauaji kwa njia yoyote ile sheria itachukua mkondo wake huku akiapa kupambana na wahalifu wa mauaji yoyote yale kindakindaki

WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI SASA WAJA NA MBINU YA KUJIGEUZA WANAFUNZI

$
0
0


 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah akitoa maelekezo kwa mkuu wa Polisi wilaya ya Hai,Lwelwe Mpina mara baada ya kufanikiwa kukamata watu tisa wakiwa na Dawa za Kulevya aina ya Mirungi ikiwa ndani ya Mabegi yanayotumiwa na wanafunzi kuhifadhi Daftari.
Askari Polisi wakitoa vifurushi vya Dawa za Kulevya aina ya Mirungi iliyokuwa imehifadhiwa katika mabegi yanayotumiwa na wanafunzi kuhifadhi Daftari.
Sehemu ya Dawa za kulevya aina ay Mirungi iliyokamatwa ikiwa imehifadhiwa kwenye mabegi madogo ikisafirishwa kuelekea mkoani Arusha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi Hamisi Issah akiangalia vifurushi vidogo vya Dawa za kulevya aina ya Mirungi iliyokamatwa Latina eneo la KIA Juction.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Hamisi Issah akionesha sehemu ya Dawa za kulevya aina ya Mirungi iliyokamatwa katika wilaya ya Hai ikisafirishwa kuelekea Arusha .
Baadhi ya watuhumiwa wa usafirishaji wa Dawa za kulevya  wakiwa kaaika gari la Polisi tayari kuelekea Mahakamani kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya kaskazini . 
 
WAFANYABIASHARA na Wasafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi wamekuja na mbinu nyingine mpya ya kujigeuza wanafunzi na kisha kuficha Mirungi katika mabegi madogo yanayotumiwa na wanafunzi kuhifadhi Daftari kwa lengo la kukwepa mkono wa askari Polisi.
 
Mbinu nyingine ambazo jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro imezigundua hivi karibuni ni pamoja na kutumia magari ya Kifahari yakiwemo Toyota Land Cruser ,Toyota Alphasad,Toyota Vanguard huku mbinu nyingine zikiwa ni kufanyia mabadiliko gari aina ya Toyota Noah ili kurahisisha ubebaji wa Mirungi kwa kificho.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah alisema wasafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi wameendelea kubuni mbinu kila kukicha baada ya zile za awali kushtukiwa na Polisi huku akitoa onyo kwa wamiliki wa Magari ya abiria kujiingiza katika mtego wa kusafirisha dawa hizo.
 
“Hapa kuna mizigo ambayo imekamatwa na askari wetu wakiwa barabarani ,hii ni mbinu mpya  ya usafirishaji  ,haya mabegi unayoyaoona yote ni mabegi yanayoonesha mbebaji amebeba Madaftari  anaenda shuleni ,lakini haya sio madaftari ni Mirungi ,ni mizigo iliyokamatwa kwenye mabasi tofauti tofauti”alisema Kamanda Issah. 
 
Alisema katika tukio hilo watuhumiwa tisa  wakiwemo wanawake wawili wamekamatwa wakiwa na jumla ya kilogramu 64 baada ya sakari Polisi kupekuwa magari matatu ya Abiria yaliyokuwa yakitokea  yakiendelea na safari kutokea Moshi yakielekea Arusha.
 
“Naona mbinu zinaendelea kubadilika ndani ya wiki mbili ,mbinu tatu tofauti,kwanza ya kujaza kwenye magari,pili ya kutoboa magari kabisa,tatu kama mwanafunzi  nyingine kama mtu anaenda hospitali amejifunga maplasta sasa hizi mbinu zitafika mpaka lini na sisi tunashukuru askari wangu wanafanya kazi vizuri”alisema Kamanda huyo wa  Polisi Kilimanjaro.
 
Kamanda Issah amewataja wanaoshikiliwa hadi sasa kuwa ni pamoja na  Ibrahim Masuli, Godfrey Richard, Chrispin  Baltazar, Fanuel Hamad,na Jackline Mushi huku wengine wakiwa ni Lucy Petro ,Nuru Haruna,Silvesta Fabian naMinyari Miandei.
 
Alisema kwa sasa askari polisi wameamua kupekuwa magari yote yakiwemo ya abiria huku akiwataka abiria kutoa ushirikiano kwa jeshi l a Polisi pindi wanapoona mizigo yenye mashaka ili kuwaondolea adha ya kuchelewa kufika safari zao kutokana na usumbufu watakao pata barabarani.
 
“Tunawasihi abiria maana kuna abiria wengine wakiona askari   wanapekua gari wanakasirika,msikasirike hii ndio kazi ya kupekuwa ,vinginevyo  muwe mnatuambia ndani ya gari amepanda mtu wa ajabu na amebeba madawa ya kulevya  aina ya mirungi  hapo ndio itakuwa ni nanafuu na tutafanya kazi kwa muda mfupi li muendelee  na safari “alisema Issah.
 
Kamanda Issah aliwataka wamiliki wa mabasi ya abiria kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi  ili kuhakikisha biashara hiy inakoma kwa kukataa kubeba abiria wenye mizigo ambayo wanatilia shaka na kwamba kwa kuendelea kuwabeba itapelekea kuwaingiza katika matatizo na vyombo vyao.
 
“Sasa hivi sio imekuwa ni wanafunzi ambao madaftari yao ni mirungi iliyobebwa nyuma ,kwa hali kama hiyo tunawasihi  wale wote wasafirishaji wa abiria kutokea Moshi kwenda Arusha wawe makini  utawachelewesha abiria wako,upekuzi utaendelea  na ninaelekeza askari waendelee usiku iwe mchana”alisema Issah.
 
“Kuna watu wakiona gari inapekuliwa wanatubeza ,sasa hivi tukikuona wewe unatubeza askari watakukamat,a  wanawabeza askari wanaofanya kazi yao  halafu tutakuhoji unatubeza kwa sababu gani,kwa hali kama hiyo tunaagiza askari waendelee kukamata mirungi na wasiiache”aliongeza Kamanda Issah.
 
 Kukamatwa kwa Dawa hizo  zinafanya idadi kamili ya Dawa za kulevya aina ya Mirungi zilizokamatwa katika kipindi cha wiki mbili kufikia kilogramu 564 pamoja na vyombo vya usafiri yakiwemo magari matatu na pikipiki moja.

KIKAO KATI YA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE,WAGANGA WA JADI NA TIBA ASILI WILAYA YA NJOMBE

POLEPOLE AWATAKA WANACHAMA NA WANANCHI KUUNGA MKONO KAZI NZURI YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

$
0
0

Na Ahmed Mahmoud Arusha

KATIBU wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole amewataka wanachama wa chama cha Mapinduzi(CCM) pamoja na wananchi kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais John Magufuli ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha amewataka wananchi kumpuunza mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbles Lema na timu yake ambayo imekuwa ikimkashifu rais na serikali kwenye mitandao ya kijamii na kuacha kutekeleza ahadi alizowaahidi wananchi wa wilaya hiyo.

Polepole alitoa rai hiyo hiyo jana wakati wa siku ya kwanza ya ziara yake ya siki14 mkoani hapa ambapo pia alirudhishwa na utekelezaji wa ilani ya ujenzi wa barabara ya lami ya Arusha by Pass yenye urefu wa km 42.4 kutoka Ngaramtoni mpka Usa River.

"Tuna kila sababu ya kumpongeza rais wetu John Magufuli.Niwaombe wananchi wa wilaya ya Arusha Jiji pamoja tuunge mkono utendaji kazi wa rais Magufuli ambaye amejitoa sadaka kwa ajili ya kuwatumikia watanzania haswa wananchi wanyonge kwa mambo makubwa ya kusukuma maendeleo mbele ya nchi yetu".Alisema azma ya serikali ya awamu ya tano ni kuhangaika na shida za wananchi kwa kuhakikisha wanapata maendeleo lakini pia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa kuwa ndiyo ahadi waliyoaahidi kwenye ilani ya CCM 2015-2020.

Akingumza na wajumbe wa halmashauri kuu za kata mbalimbali Jijini hapa Pole pole alizitaka ziwe zinawaalika maofisa watendaji wa kata pamoja na wataalam wa kata zao ili waweze kuileza ni kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwenye kata zao pamoja na kujibu kero ambazo hazijapata ufumbuzi.

Kuhusu Lema kumbeza rais kwenye mitandao ya kijamii Polepole alisema mbunge huyo ni mbunge wa kwenye mitandao na ndiyo sababu hajaweza kutekeleza ahadi yeyote kwa wananachi wake."Lema ni mbunge wenu lakini pia ni mkazi wa kata ya Engutoto lakini hajawahi hata kufika kwenye hosptali hii ya wilaya ambayo iko kwenye kata anayoishi kwa sababu hana mapenzi mema na ninyi".

"Mpuuzeni mwacheni aendelee kumbeza rais kwenye mitando.Na muangalie kazi nzuri na kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya tano ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili".Akikagua ujenzi wa hosptali ya wilaya ya Jiji la Arusha ambayo ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje umeshakamilika kwa gharama ya sh milioni 535.5 Pole pole alisema hosptali hiyo itakuwa mkombozi wa wanawake na watoto.

Baada ya ukaguzi huo Pole pole alikagua ujenzi wa vyumba vya maabara ya Biolojia na Kemia katika shule mpya ya sekondari ya Arusha Terati ambapo ujenzi wake umegharimu sh milioni 80.Awali mhandisi wa wakala wa barabara mkoa wa Arusha (TANROADS) Mgeni Mwanga alisema barabara hiyo yenye urefu wa km 42.4 inayojengwa na kampuni yaHanil Jiangsu Joint Venture Ltd ya Korea itagharimu sh bilioni 139.Alisema hadi sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia 80 na km 28 zimekamilika kwa kiwango cha lami la km 14.4 zimekamilika kwa lami ya awamu ya kwanza.Mhadisi Mwanga alisema fedha hizo ni mkopo wa riba nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika EAfDB .

Kwa upande wa fidia mhandisi hiyo alisema serikali imelipa fidia ya sh bilioni 24 kwa wananchi ambao maeneo yao yamepitiwa na barabara hiyo.

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA PAMOJA YA SMT NA SMZ KUJADILI MASUALA YA MUUNGANO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (katikati) wakati wa Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano, kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
Kikao hicho kimefanyika jana Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea hati ya umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa hekari 30 kwenye mji wa Serikali Dodoma kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika jana Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma.
akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ali Iddi (kushoto) hati ya umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa hekari 30 kwenye mji wa Serikali Dodoma kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika jana 
 Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakati wa kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika jana Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images