Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KINANA AANZA ZIARA WILAYA YA NYASA MKOA WA RUVUMA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Kingerikiti wilaya ya Nyasa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Luhangarasi  wilaya mpya ya Nyasa.
 Katibu wa NEC  Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia  wananchi wa kijiji cha Luhangarasi wilaya mpya ya Nyasa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba  matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Kata ya Luhangarasi.
 Wanachama  wa shina namba 1 kwa Balozi Joseph Nduguru tawi la Luhangarasi wilaya ya Nyasa wakicheza kwa furaha wakati wa kumaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ofisi ya CCM  wilaya ya Nyasa kulia ni Mbunge wa Mbinga Kapteni Jonh Komba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Kilosa wakati wa  ukaguzi,timu ya Kilosa ilicheza mechi ya kujipima nguvu na timu ya Mbamba Bay.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga mpira kama ishara ya ufunguzi wa mechi kati ya timu za mpira za wanawake Kilosa na Mbamba bay
Mbunge wa Mbinga Magharibi Ndugu Kapteni John Komba akihutubia wananchi kwenye viwanja vya michezo Mbamba bay.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Rudisha baada ya kumsimamisha na kumtaka asalimiane wananchi .
 Ujumbe unaomtaka Katibu Mkuu wa CCM Ndugu asimame kwenye kijiji cha Maganagana japo wamsalimi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na wananchi wa kijiji cha Makatani wakati akielekea wilaya mpya ya Nyasa.

BODI YA NBC YAFANYA MAZUNGUMZO NA WATEJA WAO JIJINI DAR

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) William Erio katika hafla iliyoandaliwa na bodi kwa wateja wa makampuni kubadilishana mawazo na kuwajulisha mipango na maendeleo ya benki hiyo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sekta za Umma na Huduma za Kibenki kwa Taasisi wa benki hiyo, William Makoresho na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Hazina, Burton Hamisi.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC, Dk. Mussa Assad (kulia) akisalimiana na mmoja wa wateja wa makampuni ya benki hiyo, Ankush Shah katika hafla hiyo. Katikati ni Mujumbe wa Bodi ya NBC, Daniel Btits.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi. Mizinga Melu (kulia), Mjumbe wa Bodi, Dk. Hussein Kassim (kushoto), wakifurahi pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla hiyo ambayo NMBC imesema huo ni mwanzo wa matukio ya kila mara ambapo viongozi watakuwa watakutana na wateja ili kujua mahitaji yao na kubadilishana mawazo.  Wa pili kushoto ni Rishad Karimjee na Farishta Kohli wote kutoka Toyota.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Akiba wa Mashirika ya Umma (PPF), William Erio (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha Benki ya NBC Tanzania, Andre Potgieter katika hafla. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa NBC, Minnie Adolf Kibuta.
Baadhi ya wateja wakibadilishana mawazo na maofisa wa NBC katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam.

MAPACHA WATATU KUADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA LEO

$
0
0
Meneja wa bendi ya Mapacha Watatu, Khamis Dakota akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho yao ya miaka minne tokea bendi yao imeanzishwa. Pembeni yake wanamuziki wajasiriamali, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Joseph Michael Mponezya ‘Jose Mara’. 
Waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano huo ndani ya kiota cha Etasi (zamani Business Park) uliopo Victoria jijini Dar.
---
 BENDI ya Mapacha Watatu inayoongozwa na wanamuziki wajasiriamali, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Joseph Michael Mponezya ‘Jose Mara’ leo Ijumaa Nov 22 katika ukumbi wa letasi (zamani Bussines Park) uliopo Victoria jijini Dar inatarajia kuzindua albam yake ya pili waliyoipa jina la Yarabi Nafsi.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari meneja wa bendi hiyo Khamis Dakota alisema kuwa baada ya miaka mine yenye changamoto nyingi wameamua kusherehekea pamoja na wanamuziki wakongwe kutoka bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

Bendi ya Mapacha Watatu ina albamu mbili ambazo ni Shika Ushikacho na Yarabi nafsi.

Dakota akizitaja nyimbo zilizomo katika albamu yao ya pili Yarabi Nafsi ni pamoja na Yarabi Nafsi uliobeba jina la albamu, Ujasiriamali, Naonewa, Chanzo Wanaume, Sumu Ya Mapenzi Remix, Usia wa Babu, Mpenzi Nenda na Wivu.

Naye Khalid Chuma Chokoraa alisema kwamba anawaalika mashabiki wa bendi hiyo waje kwa wingi leo kwani kutakuwa na burudani ya aina yake ambapo wakishuka FM Academia wakiingia Mapacha Watatu kazi itakuwa bubwa.

Akizuungumzia safari ya muziki ya bendi hiyo Meneja Dakota amesema kwamba wamepitia misukosuko mingi, kiingilio ni sh. 10,000.

haya tena... mambo ya warsaw, poland, hayo...

MKEKA WA NGUVU KUTOKA WILAYA YA NAMTUMBO KUELEKEA WILAYANI MBIGA MKOA WA RUVUMA

MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA AMTEMBELEA BALOZI EDUARDO MEDINA ICAZA WA MEXICO WASHINGTON DC

$
0
0
Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika mazungungumzo na Mhe. Balozi Eduardo Medina-Mora Icaza Ofisini kwa Balozi huyo Washington DC pamoja na taswira mbali akiwa na Balozi huyo.
Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico jana alimtembelea Mhe. Eduardo Medina-Mora Icaza, Balozi wa Mexico nchini Marekani. Balozi Mulamula alimtembelea Balozi Eduardo ili kujitambulisha na kufahamiana nae. Katika mazungumzo yao,Balozi Mulamula alimweleza Balozi huyo wa Mexico historia ya uhusiano wa Tanzania na Mexico tangu Enzi ya Mwalimu Julius Nyerere kupitia Taasisi ya South South Commission. Aidha, alimkumbusha uhusiano wa karibu na wa siku nyingi baina ya chama cha Kimapinduzi cha Mexico(PRI) na Chama cha Mapinduzi (CCM) cha Tanzania ambapo wakati wa kuapishwa Rais mpya wa Mexico Mhe. Enrique Nieto mwezi Desemba 2012, Mhe. Dr. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais alimwakilisha Mhe.Rais Jakaya Kikwete,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla hiyo. Sambamba, Mhe. Balozi Mulamula alipata wasaa pia wa kupata taarifa za muda ambao atawasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa nchi hiyo mapema mwakani.

Precision Air Hosts its 2nd Shareholders’ Annual General Meeting predicting brighter future ahead with five-year strategic plan

$
0
0
The Precision Air Managing Director and CEO Sauda Rajab briefs the company’s shareholders during the company’s Annual General Meeting held in Dar es Salaam yesterday. Photo by Staff Photographer.

The Precision Air Board Chairman Michael Shirima briefs the company’s shareholders during the company’s Annual General Meeting held in Dar es Salaam yesterday. Photo by Staff Photographer.

The Precision Air Managing Director and CEO Sauda Rajab (centre) briefs the company’s shareholders during an Annual General Meeting held in Dar es Salaam yesterday. Looking on at the left is the company’s board member Vincent Shirima and the Precision Air Group Secretary Elias Mwashiuya. Photo by Staff Photographer.

RAIS KIKWETE KUWA MIONGONI MWA VIONGOZI MBALIMBALI WATAKAOPEWA TUZO ZA KUTAMBUA MCHANGO WAO KATIKA KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO

$
0
0
mchango wao katika kuboresha afya ya mama na mtoto. Tuzo hizo zimeandaliwa na Taasisi ya Madaktari Waliosoma Vyuo Vikuu nchini (THPI), na miongoni watakaopewa tuzo ni Rais Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mke wa Rais, Salma Kikwete na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi NOVEMBA 23, mwaka huu, viongozi mbalimbai watapewa tuzo za kutambua

Kuhusu THPI, ilianzishwa mwezi Machi, 2009 na madaktari 12, na Mkurugenzi  wa taasisi hiyo, Dk. Telesphory Kyaruzi, anasema wanaamini wakiwa wengi, watahudumia watu wengi na jamii kubwa zaidi. Anasema, hadi sasa taasisi ina madaktari  wanachama zaidi ya 120 ambao wamesambaa nchi nzima. "Lengo kuu la taasisi yetu ni kushiriki katika kuhamasisha uboreshaji huduma za afya nchini na kushiriki kikamilifu katika kutoa huduma bora za afya kwa watanzania,"anaongeza. Madaktari hao ni wale walioamua kubaki nchini badalayakukimbilia nje
ya nchi kufanya kazi...kwa kifupi ni madaktari wazalendo.

"Tuliamua kubaki nchini badala ya kwenda nchi za nje kutafuta maslahi mazuri    zaidi kwa sababu ya uzalendo juu ya nchi yetu. "Dira ya taasisi yetu, tunaona watanzania wenye afya bora, huduma bora , na miundombinu bora katika kutoa huduma za afya nchini . Katika taasis yetu  nguvu yetu ni umoja;  wote ni sawa, kila mtu ni muhimu na kila mtu ni kiongozi.  Nguvu yetu ni matumaini,"anaongeza.

Naibu Spika aongoza vikao vya ACP/EU jijini Addis Ababa,Ethiopia

$
0
0
Mhe Naibu Spika Job Ndugai akiongoza kikao cha Kamati ya Masuala ya Jamii na Mazingira cha Umoja wa Mabunge ya Africa,Carribean na Pacific ambacho kinafanyika jijini Addis Ababa kama utangulizi wa Mkutano wa Mabunge ya nchi za ACP na Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Ulaya.Mhe Ndugai ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa mwaka wa pili sasa.Wengine pichani ni maafisa wa Sekretarieti ya Umoja huo.
Washiriki toka Tanzania wakimpongeza Mhe Naibu Spika Ndugai kwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kumalizika kwa kikao.Pichani kulia ni Mhe Mussa Zungu,Mbunge wa Ilala na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge na kulia ni Katibu wa Msafara huo Nd.Aggrey Nzowa ambae pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Maktaba Bungeni.Picha na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI DODOMA KATIKA DARAJA LA RELI LA BAHI-KINTINKU

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa tatu kutoka kulia), akiongea na fundi ambaye anafanya shughuli za ujenzi katika Daraja la Reli la Bahi-Kintinku. Dk. Charles Tizeba amefanya ziara kwenye daraja hilo na kupata taaarifa kuwa limekamilika kwa asilimia 98. Aidha daraja hilo limegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 3.5.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa pili kutoka mbele), akishuka chini ya daraja la bahi-kintinku kuangalia maendeleo ya ujenzi wake. Daraja hilo linajengwa na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation(CCECC). Kukamilika kwa daraja hilo kutasababisha Treni za abiria na mizigo kupita kwa uhakika majira yote ya mwaka.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkazi wa mradi kutoka kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation(CCECC), Bw. Wang Chao(aliyevaa fulana ya rangi ya karoti), wakati alipotembelea mradi huo mapema wiki hii. Ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 98 na litakabidhiwa kwa Serikali mapema tarehe 28 Novemba 2013.
Mafundi wakiendelea na ukamlilishaji wa daraja la Reli la Bahi-kintinku kama walivyokutwa mapema wiki hii katika eneo la bahi mkoani Dodoma. Daraja hilo ambalo lina tani 32 litawezesha treni la Abiria na mizigo kupita kwa majira yote kwa uhakika.
Muonekano wa daraja la reli linalojengwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation(CCECC) katika eneo la Bahi mkoani Dodoma. Kukamilika kwa daraja hilo kutawezesha treni ya reli ya kati kupita kwa majira yote ya Mwaka. Aidha daraja hilo limekamilika kwa asilimia 98.

Kiota kipya chafunguliwa jijini Dar

$
0
0
Kiota Kipya cha SHADE Lounge and Grill ambachi ni cha kisasa na muonekano wa kivingine kabisha ukilinganisha na Viota vingi,Kiota hiki kipo Masaki,Barabara ya Kahama jijini Dar es Salaam.Pichani ni sehemu moja wapo ya Kiota hicho ambayo unakutana nayo pindi uingiapo tu. 
Mmiliki wa Kiota hicho,Dada Devolta (kati) akiwa na wadau waliotembelea kiota hicho wakati wa Ufunguzi wake.Kushoto ni Mbunifu wa Mitindo,Ally Remtullah
Taswira Mwanana kabisa ndani ya Kiota hicho.
Kunapendeza sana kwa kweli.

CRDB NA KIPINDI MAALUM CHA ULIPO TUPO

Tanzania yashiriki Kwenye Kongano la TEHAMA la Dunia La Shirika la Usimamizi wa Mawasiliano Duniani ITU

$
0
0
unnamed 
Katibu Mkuu wa ITU ambalo ni Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani Dr. Hamadoun Toure akisikiliza Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Makame Mbarawa. Katikati ni Waziri wa ICT wa Thailand.

Na Innocent Mungy – Bangkok Thailand

Tanzania inashiriki katika Kongano la TEHAMA la Dunia linaloandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani (ITU-International Telecommunications Union) linalofanyika katika jiji la Bangkok nchini Thailand.

Kongano hilo lenye Kauli Mbiu ya Kuchochea Mabadiliko Katika Ulimwengu wa TEHAMA, unashirikisha nchi wananchama wa ITU na wasio wanachama, Makampuni ya Mawasiliano Duniani, Taasisi na wasimamizi wa sekta ya Mawasiliano Pamoja na Serekali, wanashiriki Kongano hili katika kipindi ambacho mabadiliko makubwa katika Sekta ya Mawasiliano.

FASHION NIGHT OUT DAR ES SALAAM 2013 YA RIO PAUL KUFANYIKA NOVEMBA 30

$
0
0
USAHILI WA KUTAFUTA WANAMITINDO WATAKAO FANYA FASHION SHOW ILIYOANDALIWA NA INTERNATIONAL TANZANIAN FASHION STYLIST RIO PAUL AMBAYE HIVI KARIBUNI ANATARAJIWA KUZINDUA COLLECTION YAKE YA TATU YA MAVAZI , PAMOJA NA LINE YAKE YA VIATU.

 ATASINDIKIZWA NA WABUNIFU WA NDANI NA NNJE YA NCHI. FASHION NIGHT OUT 2013 DAR ES SALAAM ITAFANYIKA TAREHE 30 MWEZI NOVEMBER NA ITAKUA NI USIKU WA KUSHEREKEA TASNIA YA MITINDO TANZANIA IKILETA KARIBU WADAU MBALIMBALI WA MASUALA YA MITINDO.

USAHILI ULIFANYIKA : TAREHE JUMAMOSI YA TAREHE 16 NOVEMBER KATIKA UKUMBI WA THE TERRACE ,SLIPWAY, NA ULIJUMUISHA ZAIDI YA WANAMITINDO MIA MOJA KATI YA HAO NI KUMI NA SITA TU NDIO WALIPITA.
MAJAJI WAKIWA MAKINI KUHAKIKISHA WANAPATA WANAMITINDO BORA WATAKAOFANYA VIZURI KWENYE MAONYESHO HAYO.MAJAJI KUANZIA UPANDE WA KUSHOTO NI : STELLA ERNST WA IMAGE 360, MBUNIFU WA MAVAZI  LUCKY PETER , MFANYABIASHARA AMIR, CEO WA GONGA ENTERTAINMENT BWANA FRANK MGOYO NA DIRECTOR WA ALLURE INTERNATIONAL BIBI JACQUELINE HAIDER.
WANAMITINDO HAO WAKIENDELEA KUFANYIWA USAILI.
MMOJA WA MAJAJI WA USAILI HUO,FRANK MGOYO AKIWAPA SOMO WANAMITINDO HAO.
MMOJA WA WANAMITINDO AKIONYESHA NAMBA YAKE YA USHIRIKI.
WANAMITINDO WAKIFATILIA USAILI.

CHIKAWE SPEAKS AT THE 12TH SESSION OF THE ASSEMBLY OF STATES PARTIES TO THE ROME STATUTE OF THE INTERNATIONAL CRIMINAL COURT IN THE HAGUE TODAY.


Waziri Dkt. Fenella Mukangara azindua Bodi mpya ya BASATA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akihutubia wageni waalikwa hawapo pichani wakati wa hafla ya kuzindua Bodi mpya ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)  jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara wa pili kushoto akipokea zawadi ya picha za Tingatinga kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa Prof. Penina Mlama wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Basata.Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermans Mwansoko na wa mwisho kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata Bwana Gedfrey Mngereza. 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ( waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Basata mara baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa BASATA alipo kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya BASATA  jijini Dar es Salaam.
Mzee Jangala mwenye Kibaraghashia na wadau wengine wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Basata  jijini Dar es Salaam

BTG LLC WORKSHOP IN ARUSHA

WADAU YONA NA VAILETH WAMEREMETA

$
0
0
Ni wakati wa furaha kwa wadau Yona Robert Kibela na Mai waifu wake Vaileth Godfrey baada ya kumeremeta katika Kanisa la Maxmillian Kolbe la Mwenge jijini Dar es salaam na baadaye wakaelekea kwenye mnuso wa nguvu kwenye ukumbi wa Skyline Motel Mbezi Makonde.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

NEWS ALERT: WATUHUMIWA 10 WA MAUAJI YA DK. MVUNGI WAPANDISHWA KIZIMBANI LEO

$
0
0
 Watu 10 wanaotuhumiwa na mauaji ya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Marehemu Dkt. Edmund Sengondo Mvungi (pichani) , leo walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na shitaka moja la mauaji ya mwanasheria huyo mkongwe.

Saa 2:30 asubuhi washtakiwa hao wakiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi walifikishwa katika viunga vya mahakama hiyo kwa ajili ya kusomewa mashitaka yao.
Washtakiwa hao ni,  wafanyabiashara Chibago Magozi maarufu kama Chiligati (32), mkazi wa Vingunguti, John Mayunga ama Ngosha (56), mkazi wa Kiwalani na Juma Kangungu (29), mkazi wa Vingunguti.
Wengine ni mlinzi wa Dk. Mvungi, Longishu Losingo (29), mkazi wa Kariakoo Msimbazi, dereva Masunga Msukuma (40), mkazi wa  Kitunda,Paulo Mdonondo (30), mkazi wa Tabata Darajani na Mianda Mlewa ama White (40), mkazi wa Vingunguti Shule ya
Tapa.
Wengine ni, Zacharia Msese (33), mkazi wa Buguruni Ghana kwa Hawa Masudi, Msigwa Matonya (30), mkazi wa Vingunguti Machinjioni na Ahmad Kitabu (30), mkazi wa Kinondoni Mwananyamala.

Walisomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Sundi Fimbo. Wakili wa Serikali Aida Kisumo alidai kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya makusudi.
Wakili Kisumo alidai kuwa Novemba 3, mwaka huu, eneo la Msakuzi Kiswegere, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, washtakiwa kwa pamoja na kwa makusudi  walimuua Dk. Mvungi.
Hata hivyo, Hakimu Sundi alisema kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi za mauaji, hivyo  washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote hadi pale upepelzi wa kesi yao utakapokamilika,  na kesi hiyo kuhamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Upande wa Jamhuri ulidai  kuwa upelelezi haujakamilika hivyo waliomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo. Hakimu Sundi alisema kesi hiyo itatajwa Desemba 5, mwaka huu, aliamuru washtakiwa wapelekwe mahabusu.

MUHIDIN MAALIM GURUMO AUGUA GHAFLA, ALAZWA MUHIMBILI LEO

$
0
0
GWIJI wa muziki wa dansi mstaafu Muhidin Maalim Gurumo (pichani) ameugua ghafla mapema leo na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Gurumo, Juma Mbizo na Said Mdoe, waliokuwepo Muhimbili, wameiambia Globu ya Jamii kuwa mwimbaji huyo mkongwe alipatwa na tatizo la shinikizo la damu na hali ikawa mbaya kabla ya kukimbizwa hospitalini hapo.

Wamesema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na amelazwa katika wodi ya Mwaisela namba 1.

Wajumbe hao wamesema siku chache zilizopita Gurumo alikuwa kwenye afya njema na hata siku ya Jumanne alihudhuria kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Vijana Social Hall Kinondoni.

Aidha, wajumbe hao wamedai kuwa kwa mujibu wa mke wa Gurumo, Bi Pili, ni kwamba hata jana mwimbaji huyo alikuwa hana tatizo lolote na alifanya mizunguko yake bila ya mikwaruzo yoyote.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Gurumo, Bi Asha Baraka amewataka wapenzi wa muziki kuwa watulivu kwa vile hali ya mwanamuziki huyo aliyeitumikia fani kwa miaka 53, inaendelea vizuri. 

Tamasha la Gurumo limepangwa kufanyika tarehe 14 mwezi ujao katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe. Tumuombee dua mzee wetu Gurumo.



Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images