Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAZIPIGA JEKI HALMASHAURI 12 KUTEKELEZA MIRADI YA KIMKAKATI YA SHILINGI BILIONI 137

$
0
0
Na  Saidina Msangi, WFM, Dodoma
Serikali, kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, imezipatia Halmashauri 12 nchini ruzuku ya shilingi bilioni 137 kwa ajili ya kutekeleza Miradi 15 ya kimkakati, yenye lengo kuhakikisha Halmashauri zinaongeza mapato ya ndani  na kupunguza utegemezi wa kibajeti kutoka Serikali Kuu.

Hafla ya uwekaji wa saini mikataba ya ruzuku hiyo umefanyika Jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Doto James na wakurugenzi wa Halmashauri huku ikishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Doroth Gwajina na baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa ambao Halmashauri zao zimepata ruzuku hiyo.

Katibu Mkuu Bw. Doto James amezitaka Halmashauri  zilizopata fedha hizo kutumia fedha kwa malengo yaliyokusudiwa na kuonya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watendaji watakao kiuka makubaliano yaliyomo kwenye Mkataba wa makubaliano.

"Maafisa Masuuli mhakikishe mnafuata na kuzingatia Sheria ya Bajeti Namba 11 ya Mwaka 2015 na Kanuni zake, ambayo pamoja na mambo mengine inasisitiza juu ya matumizi bora ya fedha kwa shughuli zilizoidhinishwa" alisisitiza Bw. James. 

Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, ilipoanzisha utaratibu huu haikuwa inatania wala kufanya mazingaombwe, inayo dhamira ya dhati ya kuzijengea uwezo halmashauri zijitegemee kiuchumi na kutoa huduma bora kwa wananchi badala ya kutegemea ruzuku ya Serikali Kuu na kuwahakikishia wadau kuwa fedha hizo zipo na kuzitaka Halmashauri zichangamkie fursa hiyo kikamilifu

Miradi inayotarajiwa kutekelezwa  inahusisha masoko ya kisasa, kiwanda cha kusindika korosho, uendelezaji wa fukwe ya Oysterbay pamoja na maegesho ya malori, iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Kigamboni, Tanga, Kibaha, Bagamoyo, Mwanza, Tarime, Hanang, Iringa na Biharamulo.

Kwa upande wake Kamishina wa Bajeti wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga amesema Awamu ya Pili ya Miradi ya Kimkakati kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa miradi iliyokidhi vigezo ni  15 yenye thamani ya Sh. Bilioni 137.38.

Amesema kuwa katika Awamu ya Kwanza ya Mpango huo wa Serikali wa kuzijengea uwezo Halmashauri kutekeleza miradi ya kimkakati kwa Mwaka wa Fedha 2018/2018, Halmashauri 17 zenye miradi 22 zilifuzu vigezo na kupatiwa ruzuku ya shilingi bilioni 131 hivyo kufanya miradi yote mpaka sasa kufikia 37 ikiwa na thamani ya shilingi bilioni 268.38

Naye Naibu Katibu Mkuu, kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Dkt. Doroth Gwajima, ameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha ambazo zitachochea miradi ya maendeleo katika Halmashauri nchini.

Dkt. Gwajima, amezitaka Halmashauri zilizofanikiwa kusaini mikataba hiyo, kuhakikisha kuwa zinazingatia lengo la mkataba huo na kutekeleza miradi kwa muda mwafaka na viwango vilivyoainishwaa na kwamba ufuatiliaji wa miradi hiyo utakuwa ni wa kiwango cha juu.

Pia amekiagiza Chuo cha Serikali za Mitaa – Hombolo, kuandaa mafunzo ya kuzijengea uwezo Halmashauri nchini ambazo hazikufanikiwa katika uandikaji wa miradi ili ziweze kufanikiwa kwa awamu ijayo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia), akikabidhi Hati ya makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa kimkakati katika Mkoa wa Pwani, wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi. Theresia Mmbando, wakati wa hafla ya utiaji saini wa miradi hiyo iliyofanika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, akisaini mikataba ya miradi 15 ya Kimkakati ya awamu ya pili kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa,  hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, akieleza kuhusu Halmashauri zilizokidhi vigezo vya kupewa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati yenye thamani ya Sh. bilioni 137.38, kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo kwa lengo lililokusudiwa, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Wakuu wa Idara na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakishuhudia uwekaji saini wa miradi ya kimkakati ya awamu ya pili kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa, iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Uwekaji saini wa mikataba ya miradi 15 ya Kimkakati ya Awamu ya Pili kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa ukiwemo mkoa wa Iringa uliofanyika, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Makatibu Tawala Kutoka Mikoa ya Tanga, Pwani na Iringa Bi. Zena Said, Bi Theresia Mmbando na Bi Happiness Seneda, wakizungumza jambo katika hafla ya uwekeji saini wa miradi ya kimkakati ya Awamu ya Pili kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyofanika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Mhasibu Mkuu wa  Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 21, Bw. Sayi Nsungi (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Mifumo ya Kifedha Bw. Hamza Rashid, wakifurahia jambo wakati wa hafla ya uwekeji saini mikataba ya miradi ya kimkakati ya Awamu ya Pili kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyofanika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Wadau mbalimbali wa miradi ya Kimkakati ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa wakiwa katika hafla ya uwekeji saini wa Mikataba ya miradi hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dkt. Doroth Gwajima, akitoa maelekezo mbalimbali kwa Halmashauri zilizopata ruzuku kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, kuhusu namna bora ya kutekeleza miradi hiyo kwa viwango na ubora wa hali ya juu, Jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)

TANESCO,ABB WAENDELEA KUFUNGA TRANSFOMA YA MEGAWATI 240 KITUO KIKUU CHA UBUNGO

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

TIMU ya wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kwa kushirikiana na Mkandarasi ABB wa nchini Switzerland, wameendelea na kazi ya kufunga transfoma yenye uwezo wa Megawati 240 katika Kituo Kikuu cha Kupoza na Kusambaza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya TANESCO iliyoitoa leo imesema transfoma hiyo iliingia hapa nchini Januari 28, 2019 na lengo ni kuendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuleta ufanisi katika usambazaji wa umeme katika jiji la Dar es Salaam na Pwani.

Akielezea uwezo wa Transfoma hiyo, Mkuu wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme Ubungo, Mhandisi Joseph Msumali amesema transfoma hiyo yenye uwezo wa kusukuma takribani Megawati 240 kutoka kwenye msongo wa kilovoti 220 kuelekea Msongo wa kilovoti 132 kwa ajili ya usambazaji na matumizi ya nishati ya umeme katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
 Ufungaji wa Transfoma ukiendelea

 

JOSE MOURINHO AHUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA AU FAINI EURO 182,500 NCHINI HISPANIA

$
0
0

Kocha wa zamani wa Mancester United Jose Mourinho amekubali adhabu ya kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la ukwepaji kodi nchini Uhispania.

Uhispania hata hivyo huwa haiwafungi jela wahalifu ambao wamehukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili na wale ambao hawajatumia mabavu kwenye kutenda uhalifu wao. 

Mourinho ambaye amekiri makosa yake, anatarajiwa kulipa faini ya Euro 182,500 (£160,160) ili kujihakikishia kuwa hatupwi jela. 

Kwa ujumla Mourinho ametozwa faini ya Euro milioni 2 kama adhabu ya kukwepa kodi. Wendesha mashtaka walimtuhumu kocha huyo kukwepa kodi ya Euro milioni 3.3m (£2.9m) katika kipindi ambacho alikinoa kikosi cha Real Madrid Real Madrid kati ya 2011-2012. Mourinho anatuhumiwa kuanzisha makampuni kadhaa visiwani British Virgin Islands ili kusimamia mapato yake yatokanayo na picha. 

Waendesha mashtaka wanadai kuwa makampuni hayo yaliundwa ili kuficha mapato halisi ya mkufunzi huyo na kuathiri kiasi cha kodi alichotakiwa kulipa. Makubaliano ya adhabu hiyo yalifikiwa na Mourinho na maafisa kodi hapo awali, na leo walienda mahakamani ili kuyapa uhalali wa kisheria. 

Kocha huyo ni nyota mpya wa mchezo wa soka kufikia makubaliano na 
Mwezi Januari Cristiano Ronaldo alikubali kulipa faini ya Euro milioni 18 kuepuka kifungo cha miezi 23 , katika kesi ya mapato ya picha pia.

Ronaldo alitenda makosa hayo mwaka 2012 mpaka 2014 kipindi ambacho Mourinho alikuwa akikinoa kikosi hicho. Mchezaji mwenza wa zamani wa Ronaldo kikosini Madrid Xabi Alonso, pia anakabiliwa na mashtaka ya ukwepaji kodi wa kiasi cha Euro milioni 2, lakini anakanusha mashtaka hayo. 

Marcelo Vieira amekubali kifungo cha nje cha miezi minne kwa kutumia makampuni ya ughaibuni kushughulikia mapato yake ya Euro nusu milioni. 
Wachezaji wa Barcelona Lionel Messi na Neymar (sasa yupo PSG) pia wameshawahi kujikuta matatani na mamlaka za kodi za Uhispania hapo awali.

CHANZO BBC.

WAFANYABIASHARA, WAGANGA WA JADI WAKAMATWA NJOMBE MAUAJI YA WATOTO

$
0
0

Baadhi ya waganga wa kienyeji wa Njombe walikutana wa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni wiki iliyopita.

Wafanyabiashara 10 mashuhuri ni miongoni mwa washukiwa 28 waliyokamatwa kuhusiana na mauaji ya kikatili ya watoto katika eneo la Njombe Tanzania. 

Mbunge wa Mkambako Deo Sanga, ameliambia bunge kuwa hali ya taharuki imetanda katika eneo hilo kiasi cha kuwa wageni wanachukuliwa kama washukiwa au washirika wa karibu wa wauaji. 

''Karibu wafanyibiashara 10 ambao wamewaajiri watu 200 wamekamatwa siku nne zilizopita na hatujui kinachoendelea kufikia sasa'' alisema Mbunge Deo Sanga kama alivyonukuliwa na Gazeti la kingereza la The Citizen la Tanzania akiongezea kuwa shughuli za kiuchumi katika eneo hilo zimekwama. 

Bw. Sanga alikua akichangia hoja iliyotolewa na mbunge mwenzake wa Lupembe Joram Hongole aliye muomba spika Job Ndugai kuahirisha shughuli za siku ilikujadili suala la mauaji ya watoto mkoani Njombe. 

Mamlaka za eneo hilo zinasema kuwa takribani watoto 10 wameuawa Njombe katika kipindi cha mwezi mmoja na kwamba wauaji wamekuwa wakiwakata wathiriwa viungo vya mwili kama macho, meno na kunyofoa sehemu zao za siri. 

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mauaji ya watoto hao sita wilayani humo yalichochewa na imani za kishirikina.Waganga wa tiba za jadi wilayani Njombe hata hivyo wamejitenga na tuhuma kuwa wanachochea mauaji ya watoto wilayani humo.

Akithibitisha kukamatwa kwa washukiwa 28,kamanda wa polisi katika eneo la Njombe Bi Renata Mzinga ameongeza kuwa shughuli ya kuwasaka washukiwa zaidi wa mauaji hayo inaendelea.''Tumevumbua mtandao wa watu waliyohusika na mauaji hayo.Tunashirikiana na kitengo maalum cha polisi kutoka makao makuu ya polisi mjini Dar es Salaam kuhakikisaha wote waliyohusika na ukatili huo wanatiwa nguvuni'' alisema Bi Renata.

Spika wa bunge Job Ndugai ameipatia serikali hadi Ijumaa ya Februari 8 kutoa taarifa kamili kuhusiana na matukio mkoani Njombe.

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI ATEMBELEA KITUO CHA CHANNEL TEN NA RADIO MAGIC FM

$
0
0

 Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Mkurugenzi mtendaji African Media Group (AMG) Jaffari Haniu wakimsikiliza mtangazaji wa kituo cha Channel Ten Hanifa Roy alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
 Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth wakimsikiliza mtayarishaji vipindi wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten Issa Didi alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam Febuari 5, 2019.
 Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mtayarishaji vipindi wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten Abdalaah Lugisha alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam Febuari 5, 2019. 
  Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth wakiwa katika chumba cha kusomea Habari cha kituo cha Televisheni cha Channel Ten alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam Febuari 5, 2019.
  Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji African Media Group (AMG) Jaffari Haniu akisoma habari, alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam Febuari 5, 2019.
  Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth katika chumba cha kurushia matangazo cha Rdio Magic Fm alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam Febuari 5, 2019.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji African Media Group (AMG) Jaffari Haniu alipotembelea ili kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam Febuari 5, 2019. 
 Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Ufundi wa Channel Ten Agustino Mganga alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
 Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mmoja wa Wafanyakazi na Mtangazaji wa Radio Magic Fm Orest Kawawo alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam. Febuari 5,2019.




 Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumzana Wafanyakazi na Watangazaji wa Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Bi. Diana Mwakatundu ambaye ni Mlemavu aliwapokuwa akizungumza na Wananchi mbalimbali waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam. Febuari 5, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mbalimbali waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam. Febuari 5, 2019.
 Wananchi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliwapokuwa akizungumza nao Wananchi hao waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam. Febuari 5, 2019.
Mama Janeth Magufuli Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimu Wananchi mbalimbali waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm,  walipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam. Febuari 5, 2019
PICHA NA IKULU


MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AMEKAGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA CCM SUKITA LUMUMBA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole wakimsikiliza Msimamizi wa Ujenzi  wa ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega wa Kitega Uchumi la Ccm  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya  Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
 Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole akitoa maelekezo kwa  Msimamizi wa Ujenzi  wa ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya  Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza Wajasiliamali wadogo Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu pamoja Dunia Seleman Simba Mjasiliamali wa Miwa mara baada ya kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya  Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam Febuari 5, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlipa  pesa Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu mara baada kununua Madafu yake, alipotembelea ili kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya  Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam Febuari 5, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na Katibu Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole  kunywa Dafu alilonunua kwa mjasiliamali Paschal Sabas mara baada a kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya  Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam Febuari 5, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akinywa Dafu alilonunua kwa mjasiliamali Paschal Sabas mara baada a kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya  Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam Febuari 5,2019.
PICHA NA IKULU

SPIKA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAFADHILI WA MRADI WA KULIJENGEA BUNGE UWEZO

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wa pili kutoka mwisho upande wa Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na wakwanza ni Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson (kulia) akifafanua jambo wakati wa Kikao kati ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai na Wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo.
Mtaalam Mwadamizi wa masuala ya Jinsia na Utawala katika Ubalozi Ireland nchini Bi. Aran Corrigan (wakwanza kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao kati ya Spika wa Bunge na Wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (watatu kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dodoma. Kushoto kwa Spika ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.

PICHA NA BUNGE

WAZIRI UMMY AONGOZA WATUMISHI WIZARA YA AFYA KUMUAGA ALIYEKUWA KATIBU MKUU DKT MPOKI

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amewaongoza watumishi wa wizara hiyo katika hafla fupi ya kumuaga rasmi aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Mpoki Ulisubisya ambae ameteuliwa kuwa Balozi.

Wakati huo huo aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Wizara ya Afya, ambaye amekuwa Naibu Katibu Mkuu Idara ya Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Idara ya Afya TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Afya na aliyekuwa Mganga Mkuu wa Dar es salaam ambaye kwa sasa ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe

Katika hafla hiyo Waziri Ummy amewashukuru watumishi wote wakiongozwa na Dkt Mpoki Ulisubisya kwa ushirikiano waliouonesha katika kipindi chote walichofanya kazi Wizara ya Afya na kuwasihi kuendeleza uchapaji kazi ili kusukuma gurudumu la Maendeleo hususani maendeleo ya Sekta ya Afya.

Aidha, Waziri Ummy amewakaribisha Watumishi wote walioamia katika Wizara ya Afya, Waziri Ummy amesema kwamba licha ya mafanikio makubwa ambayo Sekta ya Afya imepiga, bado kuna changamoto nyingi ambazo zinapaswa kutatuliwa ikiwemo suala la uhaba wa watumishi, na upatikanaji wa Dawa na vifaa tiba.

Naye Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Fustine Ndugulile amewakumbusha Watumishi wa Sekta ya Afya juu ya uwajibikaji na kuwatoa hofu kuwa, kama Serikali milango yao ipo wazi muda wote, hivyo kwa yoyote mwenye wazo zuri la kujenga na kuipeleka mbele Sekta ya Afya asisite kuwaona.

Kwa upande wake, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amewashukuru Watumishi wote wa Sekta ya Afya wakiongozwa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu kwa ushirikiano waliomuonesha katika kipindi chote alichohudumu katika Wizara ya Afya, kisha kuahidi kuwa Balozi Mzuri huko atakoenda ili kuikuza Sekta ya Afya.

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula amewakumbusha Watumishi wa Sekta ya Afya juu ya umoja na ushirikiano baina yao, huku akisisitiza kila mmoja ni lazima ahakikishe anatimiza wajibu wake ili kusukuma mbele Maendeleo ya Sekta ya Afya.

Kwa upande wake, aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Wizara ya Afya ambae sasa ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Idara ya Afya Dkt Dorothy Gwajima ameahidi kuwa daraja zuri na imara baina ya Wizara ya Afya na TAMISEMI kutokana na kuzijua Wizara zote mbili kiundani na kuahidi kuendeleza mazuri yote yalioachwa na Dkt. Zainab Chaula.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy Mwalimu akimkabidhi Zawadi Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa Hafla ndogo ya kumuaga yeye na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla ya kuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisaini Biblia Takatifu aliyopewa kama zawadi Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Baozi Dkt Mpoki Ulisubisya Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula, hafla ilofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Wakwanza kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifuatilia alichakuwa akiongea Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Balozi Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula (Wakatikati) na (Wakwanza kishoto) ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Idara ya Afya Dkt Dorothy Gwajima.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (kushoto) akiwa na Naibu wake Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) wakifuatilia alichakuwa akiongea Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakar Kambi (hayupo pichani) wakati wa hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Balozi Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Balozi Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.
 
Mkurugenzi wa MSD ambae pia ni mwakilishi wa Wakurugenzi wa Taasisi zote za Wizara ya Afya Laurean Bwanakunu akitoa salamu za taasisi zote za Afya wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula, hafla hiyo imefanyika katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Waziri Ummy wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Waziri Ummy wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Idara ya Afya Dkt Dorothy Gwajima.
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula, hafla ilofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TAHARUKI ILIYOTOKEA MAPEMA LEO BUNGENI

Rais Dkt Magufuli Aipa Heshima Tanzania Kimataifa

SERIKALI YAMWAGA NEEMA KWA WAVUVI KUPITIA SHERIA MPYA ZA UVUVI

$
0
0
Waziri waMifugonaUvuvi, LuhagaMpina(mwenyekotijeusina tai nyekundu) akionyesha rasimu ya awali ya sheria mpya ya uvuvi inayofanyiwa marekebisho kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya uvuvi jijini Mwanza hivi karibuni.Kushoto nimwakilishiwaMkuuwaMkoawa Mwanza ambaye pia niMkuuwa Wilayaya SengeremaEmanuel enocckkipole kulia ni mfugajiwasamaki Meck Sadick, anayefuataniDkt Rashid TamatamaKatibuMkuu Uvuvi
Sehemu yaumati wa wadau waliohudhuria katika mkutano wakanda ya ziwawakuchangiamarekebishoyasheriajijini Mwanza hivikaribuni.
 Picha ya pamoja baina ya Waziri waMifugonaUvuvi, LuhagaMpina (mwenyekoti jeusina tai nyekundu) akiwa ameketi na viongozi wa Wizara,Bunge na Mikoa inayopakana na ukanda wa pwani. Waliosimama nyuma ni viongozi jumuiya ya elimu ya juu(TAHLISO)walioongozwa na rais wajumuiya hiyoPeter Niboye(wanne kutoka kulia mwenye suti nyeusi)



Na JOHN MAPEPELE 

SERIKALI imeamua kuifumua Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 ili kuondoa vikwazo vya kibiashara na uwekezaji katika sekta ya uvuvi ili kwenda na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya awamu ya tano inayolenga kujenga Tanzania ya viwanda na kuwatetea, kuwalinda wanyonge. 

Akizungumza katika uzinduzi zoezi la ukusanyaji maoni ya wadau kuhusu rasimu ya Sheria ya Uvuvi na Sheria ya Ukuzaji viumbe kwenye maji katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam jana Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametaja sababu nyingine zilizosababisha kuwepo mabadiliko hayo. 

Ni pamoja na kutoa ulinzi madhubuti wa rasilimali za uvuvi, kuongeza uzalishaji na kuwa na masoko ya uhakika sambamba na kudhibiti utoroshwaji na uingizaji holela wa mazao ya uvuvi nchini. 

Aidha Waziri Mpina alisema sheria hiyo mpya inatakiwa iendane pia na mabadiliko na matumizi ya sayansi na teknolojia katika uvuvi na ukuzaji viumbe kwenye maji ili kwenda sambamba na mahitaji pamoja na kuwepo mwamko mkubwa wa ufugaji wa samaki kwenye maji uliojitokeza miongoni mwa wananchi. 

Alisema pamoja na rasimu ya sheria hizo mbili pia Serikali iko kwenye hatua za mwisho za kufazifanyia marekebisho Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Namba 29 ya mwaka 1994 na Kanuni zake za mwaka 2009 na Sheria ya Bahari Kuu Cap 388 na Kanuni zake za mwaka 2007 na 2016. 

Hivyo Waziri Mpina aliwasihi wananchi kutoa maoni yasiyofungamana na upande wowote na kuacha tabia ya kila mmoja kuvutia upande wake ili kuwezesha kutunga sheria madhubuti. 

Aidha Waziri Mpina alieleza utajiri wa kipekee wa rasilimali za uvuvi hapa nchini ikiwemo kuwa na eneo kubwa la maji lenye kilomita za mraba 346,337 sawa na asilimia 36.7 ya eneo lote la nchi yetu, fukwe ndefu na za kuvutia, kuwepo kwa samaki na viumbe vingine ambavyo vimetoweka na vingine vikiwa kwenye tishio la kutoweka duniani. 

Pia kuwepo kwa mito, mabwawa na maziwa yenye sifa za kipekee ikiwemo Ziwa Victoria ambalo ni la pili kwa ukubwa duniani na Ziwa Tanganyika ambalo ni la pili kwa kina duniani na la kwanza kwa ujazo wa maji duniani. 
Hivyo alisisitiza kuwa wakati nchi inakwenda kutunga sheria hiyo mpya ya uvuvi ni muhimu kama Taifa kujiuliza maswali kadhaa ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali hizo. 

“lazima tujiulize tunapata wapi uhalali wa kuagiza samaki kutoka nje ya nchi?, tujulieze kwa nini tumeshindwa kulihudumia soko la ndani na la nchi jirani, Afrika na dunia?, kwa nini tuzidiwe uzalishaji na mauzo na nchi ambazo tunazizidi kwa mbali kwa rasilimali?”alihoji Mpina, 

“Vilevile Kwanini tuwe na wavuvi masikini tena ambao hawana zana bora za uvuvi, kwanini biashara, uwekezaji na ujenzi wa viwanda ni wa kusuasua ? haya ndio maswali tunayopaswa kujiuza kama Taifa”alihoji Mpina. 

Hivyo Waziri Mpina alisema kutokana na ugumu wa maswali hayo ndio maana wizara yake ikaamua ni bora kuifumua Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 ili kusaidia kupata majawabu ya namna gani kama taifa litatoka kwenye mkwamo huo. 

Wakichangia rasimu hiyo iliyowahusisha wavuvi, wachakataji wa samaki, wauza zana za uvuvi, wafugaji wa samaki kwenye maji, wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halamshauri, wawakilishi wa vyuo vikuu na viongozi wa dini. 

Wakizungumzia mapungufu ya sheria hiyo baadhi ya wadau wa wavuvi walisema sheria imekataza matumizi ya taa za sola, jenereta pamoja na utitiri wa leseni hali iliyochangia wavuvi wengi kushindwa kutekeleza kikamilifu majukumu yao. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa aliipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kubuni wazo hilo na kusisitiza kuwa wao kama Bunge wako tayari kushirikiana na Serikali katika kubadilisha sheria zote zinazokwamisha juhudi za kujenga Tanzania ya viwanda huku akisitiza wadau kutumia vizuri fursa hiyo na kwamba wasijitoe katika uandaaji wa sheria hizo mpya. 

Katibu Mkuu Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatama alisema atasimamia kikamilifu uratibu wa zoezi zima la ukusanyaji maoni ya wadau na kwamba timu ya wataalamu wa wizara hiyo itaenda kila mahali walipo wadau. 

Aidha Dk Tamatamata alisema zoezi hilo kwa ukanda wa Ziwa Victoria lilizinduliwa na Waziri Mpina Januari 28 mwaka huu ambapo wadau walijitokeza kutoa maoni yao na kwamba zoezi hilo litaendelea hadi Februari 28 mwaka huu huku akisisitiza maoni yanakaribishwa kwa maandishi kupitia barua pepe ya maoni@uvuvi.go.tz

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI, MEJA JENERALI JACOB KINGU AKAGUA UJENZI NYUMBA ZA MAKAZI YA MAAFISA MAGEREZA

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (vazi la kiraia) akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza alipowasili Gereza Kuu Ukonga leo februari 5, 2019 katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la ukaguzi wa ujenzi wa makazi ya Maafisa Magereza unaotekelezwa chini ya Wakala wa Majengo Tanzania – TBA katika eneo la Gereza Kuu Ukonga jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (wa tatu toka kulia) akitoa maagizo kwa Mratibu wa Mradi wa ujenzi wa Makazi ya Maafisa Magereza Ukonga, Mhandisi Khadija Salum(wa tatu toka kushoto) alipotembelea mradi huo leo februari 5, 2019. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.
Moja ya majengo ya ghorofa yanayojengwa chini ya Wakala wa Majengo Tanzania – TBA.
Mkuu wa Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, ACP. John Itambu akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (vazi la kiraia) sehemu mbalimbali za Kiwanda hicho ikiwemo sehemu ya Useremala pamoja na sehemu ya Ushonaji wa nguo za aina mbalimbali katika Kiwanda hicho(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (vazi la kiraia) akiangalia baadhi ya samani za Ofisi zinazotengenezwa katika Kiwanda hicho.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Phaustine Kasike akimwelezea jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (vazi la kiraia) alipote,mblea Kiwanda cha Useremala cha Gereza Kuu Ukonga.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (vazi la kiraia) akiagana na Mkuu wa Gereza Kuu Ukonga, ACP. Widson Mwanangwa baada ya kutembelea Kiwanda cha Magereza, Ukonga leo Februari 5, 2019(Picha na Jeshi la Magereza).

Rais Magufuli Ang’ara Afrika Kiuchumi, Utawala Bora

$
0
0



Mkurugenzi wa Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma. Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na waandishi wa habari ni wa kwanza kwa mwaka huu ambao ameutumia kuwaelezea wananchi juhudi mbalimbali za kimageuzi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.


Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kung’ara kimataifa katika mapambano dhidi ya rushwa na utawala bora.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi leo Jijini Dodoma, wakati akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Serikali.

“Kutokana na utendaji wa kimageuzi wa Rais Magufuli, licha ya juhudi za watu wachache kuhaha kutaka kuichafua nchi yetu kimataifa, Tanzania imeendelea kuwa na taswira nzuri na heshima kubwa na ikiendelea kukubalika sana miongoni mwa Mataifa mbalimbali” amesema Dkt. Abbas

Dkt. Abbasi amefafanua kuwa, kimataifa Rais Magufuli amekuwa akiipatia heshima kubwa nchi ya Tanzania kwa mapambano yasiyokoma dhidi ya rushwa hivyo taasisi za kimataifa ikiwemo TRANSPARENCY INTERNATIONAL zimeonesha Tanzania inaendelea kufanya vizuri katika miaka hii mitatu ikitoka nafasi ya 117 hadi 99.

Aidha, Dkt. Abbasi ameongeza kuwa, Novemba, 2018 Serikali ya Nigeria ilitoa Tuzo ya Uongozi Bora kwa viongozi mbalimbali duniani akiwemo Rais Magufuli, mara baada ya Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa na Ufundi yaliyofanyika nchini humo.

“Jumla ya washiriki 123,446 walipiga kura kwenye tovuti ya Jarida la ALM kutoka Afrika na sehemu mbalimbali duniani, huku wengine 33,000 wakitumia mitandao ya kijamii na 3,400 wakituma maoni yao kupitia baruapepe na majukwaa mengine hivyo ili kupata ushindi huo. Rais Magufuli aliwashinda viongozi wengine mashuhuri wa Afrika ambao ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha APC, Nigeria, Chifu Bola Ahmed Tinubu, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana”ameeleza Dkt. Abbasi.

Akizunguza kuhusu hali ya uchumi nchini Dkt. Abbasi ameeleza kuwa, Serikali inaamini Mwaka huu 2019 ukuaji wa uchumi nchini utafika asilimia 7.2 na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa katika mataifa matano Afrika kwa uchumi unaokua kwa kasi na kuendelea kuwemo katika 10 ya dunia.

“Tanzania imekuwa nchi ya tano barani Afrika katika ukuaji wa uchumi na hii inatokana na utekelezaji wa miradi na huduma mbalimbali za kiuchumi zinazoendelea” amesema Dkt. Abassi.

Mbali na hayo Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza kwa kasi wajibu wake kwa umma ikiwemo kuhakikisha hali ya amani, utulivu, kusimamia utawala bora na utawala wa sheria.

Wananchi wajitokeza kwa wingi kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Yeyeye akimpima msukumo wa damu mwilini (BP) mwananchi aliyetembelea katika banda la Taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uuguzi sasa iliyozinduliwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mahawa Asenga akimuonesha Mwananchi kifaa kinachotumia kupasua kifua wakati wa upasuaji wa moyo katika uzinduzi wa kampeni ya uuguzi sasa ambayo ilizinduliwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mariselina Granima akiwaeleza wananchi kuhusu huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uuguzi sasa iliyozinduliwa jana katika uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma

Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakitoa elimu ya magonjwa ya moyo pamoja na huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uuguzi sasa iliyozinduliwa jana katika uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rydness Mulashani akimwelekeza mwananchi jinsi kifaa kinachousaidia moyo kufanya kazi (Pacemaker) kinavyowekwa kwa mgonjwa ambaye moyo wake haufanyi kazi vizuri wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uuguzi sasa iliyozinduliwa jana katika uwanja vya Jamhuri mkoani Dodoma.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aisha Omary akimpima urefu mwananchi aliyetembelea katika banda la Taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uuguzi sasa iliyozinduliwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelezo ya jinsi mgonjwa aliyeko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) anavyohudumiwa mara baada ya kutoka katika chumba cha upasuaji wa moyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uuguzi sasa iliyozinduliwa jana katika uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.
Picha na Englibert Kayombo – WAMJW 

UJENZI WA SGR-LA MGAMBO LIMELIA,WASANII ZAIDI YA 300 KUTEMBELEA MRADI WA SGR DAR-MORO.


MAGAZETI YA LEO JUMATANO,FEBRUARI 6,2019

KAMPUNI YA UTURUKI YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA ZA UCHUKUZI, UTALII, NISHATI, USAFIRI WA ANGA NA UJENZI.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe, wakiwa katika kikao na wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies wakati walipofanya kikao juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akimkabidhi Kitabu chenye Fursa na Miradi yenye Uhitaji Mitaji ya Uwekezaji nchini , Mwekezaji toka nchini Uturuki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya MNG Group of Companies mara baada ya kufanya kikao juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.


Wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies wakifuatilia kikao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki (hayupo pichani), wakati walipofanya kikao juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini, tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akiongea na wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies, wakati walipofanya kikao ofisini kwake juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akiwasikiliza wataalamu wa masuala ya uwekezaji wa Ofisi ya waziri Mkuu wakati wa kikao na wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies (hawapo pichani), wakati walipofanya kikao ofisini kwake juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.


Na. OWM, DODOMA.

Kampuni ya MNG Group of Companies ya nchini Uturuki imeonesha nia ya kufanya uwekezaji mkubwa nchini katika sekta mbalimbali; zikiwemo sekta za Uchukuzi, Utalii, Nishati na Usafiri wa Anga.

Uwekezaji huo umebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya MNG Group of Companies, Mehmet Gunal, wakati alipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki (Mb), jijini Dodoma, tarehe 5 Januari 2019.

Waziri Kairuki amebainisha kuwa nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha uwekezaji wenye tija nchini, na kwa kutumia mfumo wa sera ya Ushirikiano baina ya sekta Binafsi na Umma inahakikisha inavutia wawekezaji zaidi nchini.

“Tunazo fursa na miradi inayohitaji mitaji ya uwekezaji hapa nchini, jukumu letu ni kuhakikisha wawekezaji mnapata mazingira wezeshi katika fursa na miradi mnayotaka kuwekeza ili nchi iweze kupata tija kutokana uwekezaji huo” Amesisitiza Mhe. Kairuki.

Akiongea katika kikao hicho mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya MNG Group of Companies, Mehmet Gunal, amefafanua kuwa , Kampuni hiyo iko tayari kuwekeza nchini katika Sekta mbalimbali, kwa kuwa wamevutiwa na mazingira ya uwekezaji ya hapa nchini.

Aidha, Gunal alifafanua kuwa wamejipanga kutumia fursa na miradi yenye kuhitaji uwekezaji nchini ili kuweza kufanya uwekezaji mkubwa , pia alisema kampuni yake ipo tayari kuwekeza hata kwa mfumo wa sera ya ushirikiano baina ya Sekta ya Binafsi na Umma au kuwekeza wao wenyewe.

Kampuni ya MNG Group of Companies inao uzoefu katika masuala ya uwekezaji kwa miaka 42 katika mabara matatu Duniani, ikiwa imejikita katika uwekezaji kwenye sekta sita na tayari hadi hivi sasa imetekeleza miradi zaidi ya mia mbili katika mabara hayo.

Baadhi ya Miradi ambayo imetekelezwa na Kampuni hiyo ni pamoja na , Bwawa la kufua Umeme la Chief Dam la nchini Algeria, Ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa KOTOKA (terminal III), wa nchini Ghana, Ujenzi wa makao makuu ya na Benki ya Halk nchini Uturuki.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe, Wataalamu wa masuala ya Uwekezaji na maendeleo ya Sekta Binafsi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, pamoja na wataalam kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini.

Jafo alaaani vitendo vya watumishi kutumia nguvu dhidi ya wananchi

$
0
0

Nteghenjwa Hosseah, Itigi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amelaani vikali vitendo cha watumishi wa umma kutumia nguvu nyingi dhidi ya wananchi hali inayopelekea kuletea machafu kwenye jamii na hata kupelekea mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia.

Jafo amelaani vitendo hivyo wakati wa mazishi ya marehemu Isaka Petro aliyefariki jumamosi katika vurugu zilizotokea katika kanisa la Waadiventisti Wasabato Itigi kundi Namba Two na kuzikwa nyumbani kwao kijiji cha kazikazi kata ya Kitaraka; Mazishi hayo pia yamehudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Singida pamoja na Wilaya ya Manyoni.

Jafo amesema tukio hilo lilitokea sio agizo la Serikali na waliotekeleza wamefanya kwa utashi na akili zao binafsi na hawakuagizwa na mtu yeyote na zaidi wametenda kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.

“Hakuna namna tunaweza kusema vinginenevyo kuhusu tukio hili zaidi ya kuwa tukio baya na la kusikitisha sana kuwahi kutokea kwa wananchi wetu, tena likiwa limetekelezwa na watumishi wa Serikali inasikitisha sana nawasihi watumishi wa umma tutangulize utu mbele katika kila kazi tunazozifanya”

Aliongeza kuwa watumishi wa umma haijalishi unafanya kazi gani katika mazingira gani lakini hakikisha unatanguliza ubinadamu kwanza ili tulinde maisha yetu na ya wale tunaowahudumia haipendezi wewe ukawa chanzo cha mtafaruku katika jamii tusaidie kuwaunganisha wananchi na kuwafanya kuwa kitu kimoja na sio kuwa chanzo cha ugomvi na mafarakano.

Kwa taarifa nilizopewa na nimezithibitisha ni kuwa wote waliohusika na tukio hili wameshakamatwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama bado vinaendelea na taratibu zao alisema Jafo.

Katika msiba huo Waziri Jafo akiwa na viongozi wa Mkoa wa Singida alitoa pole kwa familia ya marehemu sambamba na rambirambi pia alishirikiana na ndugu, jamaa na marafiki katika shughuli zote za mazishi ya marehemu Isaka Petro nyumbani kwao kazikazi.

Akizungumza katika mazishi hayo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema kuwa msimba huo ni pigo kwa Serikali pamoja na wananchi wote wa kijiji cha kazikazi.

“Serikali inawahudumia wananchi walio hai na sio wafu sasa mwananchi wetu anapotutoka tena kwa kifo cha kwa namna hii na sisi tunapata pigo kwa sababu dhamira yetu ya kufikisha huduma bora kwake haitafikiwa”

Sisi kama Serikali tuna wajibu wa kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya wananchi wetu kufanya shughuli zao kwa usalama wa hali ya juu sasa wajibu huu unapotekelezwa kinyume na taratibu zetu ni makosa ninatoa na kila mtu atawajibika kwa kadiri ya kosa lake alisema Dkt. Nchimbi.

Aidha Dr Nchimbi aliwaeleza wananchi wa kazikazi pamoja na Kitaraka kuwa wale wote wanaolima katika Shamba la Kitaraka waendelee na shughuli zao kama kawaida na wasilipe ushuru wa shilingi elfu ishirini kama ilivyokuwa hapo awali mpaka hapo yatakapokuja maelekezo mengine.

“Watumishi wa halmashauri mupeleke ujuzi na pembejeo kwa wakulima wadogo wa shamba la Kitaraka na sio kwenda kuwabugudhi kwa kuwadai ushuru nyie endeleeni na wawekezaji wenu wakubwa kwa kadiri ya makubalino mliyoingia lakini hawa wananchi wanaolima ekari moja moja waacheni waendelee na kilimo chao” alisema Dkt. Nchimbi.

Naye Mchungaji wa Kanisa la Waadiventista Wasabato Itigi Kundi Namba Two Manigina F.S Manigina aliwaasa wanakijiji cha kazikazi kutokua na kisasi na kumuomba Mungu ili tukio kama hilo lisitokee tena katika kijiji chao.

“Visasi ni vya Mungu nyinyi msiweke visasi na mtu ila endeleeni na maisha yenu kama kawaida na Mungu atazidi kuwashushia baraka zake katika kazi zenu” alisema Mchungaji Manigina.

Katika vurugu zilizotokea siku ya jumamosi katika kijiji cha kazikazi eneo la Kanisa la Waadiventista Wasabato Kundi Namba Two baina ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi akiwa na askari wa wanyamapori na baadhi wa wananchi wa kijiji hicho zilipelekea kifo cha kijana Isaka Petro mwenye umri wa miaka 28.

Marehemu ameacha mke na watoto watatu. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa Mhe. Selemani Jafo akitoa pole kwenye ibada ya mazishi ya Isaka Petro aliyefariki siku ya jumamosi katika vurugu zilizotokea kijiji cha kazikazi Kata Kitaraka kwenye kanisa la Waadventista Wasabato Kundi Namba Two.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa Mhe. Selemani Jafo(katikati aliyekaa), Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi(kushoto), Katibu Tawala za Mkoa Dkt. Angelina Lutambi(kulia) wakati wa ibada ya mazishi ya Isaka Petro aliyefariki katika vurugu zilizotokea kijiji cha kazikazi Kata Kitaraka kwenye kanisa la Waadventista Wasabato Kundi Namba Two.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (aliyesimama mbele) akitoa pole wakati wa wa ibada ya mazishi ya Isaka Petro aliyefariki katika vurugu zilizotokea kijiji cha kazikazi Kata Kitaraka kwenye kanisa la Waadventista Wasabato Kundi Namba Two.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa Mhe. Selemani Jafo akishiriki kubeba jeneza la marehemu Isaka Petro wakati wa mazishi yake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa Mhe. Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, Katibu Tawala Dkt. Angelina Lutambi wakiondoka baada ya kukamilisha taratibu za mazishi ya Isaka Petro. 

KIBAHA KUJENGEWA HOSPITALI YA KISASA KWA AJILI YA KUBORESHA HUDUMA YA AFYA KWA WANANCHI WAKE

$
0
0

VICTOR MASANGU,KIBAHA

KATIKA kukabiliana na changamoto ya utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi wa Wilayani Kibaha Mkoani Pwani serikali ya awamu ya tano imeamua kujenga hospitali mpya ya kisasa katika eneo la kata ya Picha ya ndege kwa lengo la kuwaondolea kero ya siku nyingi ya kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na ujenzi huo Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Lulanzi inapojengwa hospitali hiyo Thobiasi Shilole alisema kuwa kukamilka kwa mradi huo utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa maeneo mbali mbali ya Kibaha kwani hapo awali walikuwa wanapata usumbufu mkubwa pindi wanapohitaji huduma ya matibabu.

Kwa upande wake Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka ambaye amefanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua na kujionea mwenendo mzima wa eneo hilo la ujenzi na kumpongeza Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuamua kutoa kiasi cha shilingi bilioni 1.5 ya ujenzi huo na kuwataka wakandarasi kuhakikisha wanajenga majengo yenye ubora unaotakiwa na kuachana na tabia ya kufanya kazi ambazo zipo chini ya kiwango.

Koka alibainisha kwamba kujengwa kwa mradi huo wa ujenzi wa hospitali ni kutokana na juhudi ambazo alizifanya kwa kushirikiana na viongozi mbali mbali wa wilaya pamoja na serikali kuu kwa ujumla na kuahidi kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi katika sekta mbali mbali.

“Huu mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya kwa kweli umeletwa kwetu kwa lengo la kuwasaidia wananchi katika suala zima la kuwasogezea huduma ya matibabu, kwa hivyo mimi kama Mbunge ninatoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwaboreshea wananchi huduma ya afya pamoja na mambo mengine,”alisema Koka.

Naye Diwani wa kata ya Picha ya ndege Robert Machumbe akizungumza na wananchi mara baada ya kutembelea eneo hilo la mradi amebainisha kuwa nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuwaletea wananchi mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika nyanja mbali mbali ambapo kwa sasa wameshapata eneo lenye ukumbwa wa Hekari 25 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya Wilaya.

“Kwa kweli tunapenda kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuweza kutuletea mabadiliko chanya ya kimaendeleo ambapo utaona kwa sasa katika kata hii ya picha ya ndege kuna hatua kubwa sana ambayo tumeifanya katika nyanja mbali mbali na sasa tumeshaanza ujenzi wa hospitali yetu ya Wilaya ambayo itajengwa katika mtaa wa Lulanzi kwa hivyo hii ni hatua kubwa sana pamoja na shule ya sekondari ambayo tayari eneo la hekari 11.7 limeshapatikana,”alisema.

KUKAMILIKA kwa ujenzi huo wa hospitali ya Wilaya kwa wananchi wa Kibaha mkoani Pwani na maeneo mengine ya jirani kutaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuondokana na changamoto ya kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kwenda kutafuta huduma ya afya katika maeneo mengine.


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na wananchi wa kata ya picha ya ndege katika mkutano wa hadhara mara baada ya kufanya ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Wilaya ambayo inajengwa katika eneo la mtaa wa Lulanzi
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza jambo la waandishi wa habari hawapo pichani katika eneo ambalo limetengwa maalumu kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa hospitali ya Wilaya ambayo imeanza kujengwa katika eneo la Lulaniz kata ya picha ya ndege(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mwenyekiti wa mtaa wa Lulanzi Thobisi Shilole akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kutembelea eneo la ujenzi ambalo limetengwa kwa ajili ya hospotali ya Wilaya katika eneo la mtaa wa Lulanzi
Diwani wa kata ya picha ya ndege Robert Machumbe akizungumza jambo katika mkutano na wananchi kuhusiana na ujenzi wa hospitali hiyo pamoja na masuala mbali mbali yaliyafanyika katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tani 

SERIKALI YAZIPIGA JEKI HALMASHAURI 12 KUTEKELEZA MIRADI YA KIMKAKATI YA SHILINGI BILIONI 137

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, akisaini mikataba ya miradi 15 ya Kimkakati ya awamu ya pili kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa,  hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, akieleza kuhusu Halmashauri zilizokidhi vigezo vya kupewa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati yenye thamani ya Sh. bilioni 137.38, kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo kwa lengo lililokusudiwa, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia), akikabidhi Hati ya makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa kimkakati katika Mkoa wa Pwani, wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi. Theresia Mmbando, wakati wa hafla ya utiaji saini wa miradi hiyo iliyofanika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Wakuu wa Idara na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakishuhudia uwekaji saini wa miradi ya kimkakati ya awamu ya pili kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa, iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Uwekaji saini wa mikataba ya miradi 15 ya Kimkakati ya Awamu ya Pili kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa ukiwemo mkoa wa Iringa uliofanyika, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Makatibu Tawala Kutoka Mikoa ya Tanga, Pwani na Iringa Bi. Zena Said, Bi Theresia Mmbando na Bi Happiness Seneda, wakizungumza jambo katika hafla ya uwekeji saini wa miradi ya kimkakati ya Awamu ya Pili kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyofanika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Mhasibu Mkuu wa  Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 21, Bw. Sayi Nsungi (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Mifumo ya Kifedha Bw. Hamza Rashid, wakifurahia jambo wakati wa hafla ya uwekeji saini mikataba ya miradi ya kimkakati ya Awamu ya Pili kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyofanika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Wadau mbalimbali wa miradi ya Kimkakati ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa wakiwa katika hafla ya uwekeji saini wa Mikataba ya miradi hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dkt. Doroth Gwajima, akitoa maelekezo mbalimbali kwa Halmashauri zilizopata ruzuku kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, kuhusu namna bora ya kutekeleza miradi hiyo kwa viwango na ubora wa hali ya juu, Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)
Na  Saidina Msangi, WFM, Dodoma
Serikali, kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, imezipatia Halmashauri 12 nchini ruzuku ya shilingi bilioni 137 kwa ajili ya kutekeleza Miradi 15 ya kimkakati, yenye lengo kuhakikisha Halmashauri zinaongeza mapato ya ndani  na kupunguza utegemezi wa kibajeti kutoka Serikali Kuu.

Hafla ya uwekaji wa saini mikataba ya ruzuku hiyo umefanyika Jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Doto James na wakurugenzi wa Halmashauri huku ikishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Doroth Gwajina na baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa ambao Halmashauri zao zimepata ruzuku hiyo.

Katibu Mkuu Bw. Doto James amezitaka Halmashauri  zilizopata fedha hizo kutumia fedha kwa malengo yaliyokusudiwa na kuonya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watendaji watakao kiuka makubaliano yaliyomo kwenye Mkataba wa makubaliano.

"Maafisa Masuuli mhakikishe mnafuata na kuzingatia Sheria ya Bajeti Namba 11 ya Mwaka 2015 na Kanuni zake, ambayo pamoja na mambo mengine inasisitiza juu ya matumizi bora ya fedha kwa shughuli zilizoidhinishwa" alisisitiza Bw. James. 

Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, ilipoanzisha utaratibu huu haikuwa inatania wala kufanya mazingaombwe, inayo dhamira ya dhati ya kuzijengea uwezo halmashauri zijitegemee kiuchumi na kutoa huduma bora kwa wananchi badala ya kutegemea ruzuku ya Serikali Kuu na kuwahakikishia wadau kuwa fedha hizo zipo na kuzitaka Halmashauri zichangamkie fursa hiyo kikamilifu

Miradi inayotarajiwa kutekelezwa  inahusisha masoko ya kisasa, kiwanda cha kusindika korosho, uendelezaji wa fukwe ya Oysterbay pamoja na maegesho ya malori, iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Kigamboni, Tanga, Kibaha, Bagamoyo, Mwanza, Tarime, Hanang, Iringa na Biharamulo.

Kwa upande wake Kamishina wa Bajeti wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga amesema Awamu ya Pili ya Miradi ya Kimkakati kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa miradi iliyokidhi vigezo ni  15 yenye thamani ya Sh. Bilioni 137.38.

Amesema kuwa katika Awamu ya Kwanza ya Mpango huo wa Serikali wa kuzijengea uwezo Halmashauri kutekeleza miradi ya kimkakati kwa Mwaka wa Fedha 2018/2018, Halmashauri 17 zenye miradi 22 zilifuzu vigezo na kupatiwa ruzuku ya shilingi bilioni 131 hivyo kufanya miradi yote mpaka sasa kufikia 37 ikiwa na thamani ya shilingi bilioni 268.38

Naye Naibu Katibu Mkuu, kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Dkt. Doroth Gwajima, ameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha ambazo zitachochea miradi ya maendeleo katika Halmashauri nchini.

Dkt. Gwajima, amezitaka Halmashauri zilizofanikiwa kusaini mikataba hiyo, kuhakikisha kuwa zinazingatia lengo la mkataba huo na kutekeleza miradi kwa muda mwafaka na viwango vilivyoainishwaa na kwamba ufuatiliaji wa miradi hiyo utakuwa ni wa kiwango cha juu.

Pia amekiagiza Chuo cha Serikali za Mitaa – Hombolo, kuandaa mafunzo ya kuzijengea uwezo Halmashauri nchini ambazo hazikufanikiwa katika uandikaji wa miradi ili ziweze kufanikiwa kwa awamu ijayo.
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images