Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

NAIBU KATIBU MKUU UWT ZANZIBAR AZUNGUMZIA MIAKA 42 YA KUZALIWA KWA CCM

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR

NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Zanzibar Bi.Tunu Juma Kondo amesema katika kipindi cha miaka 42 ya Chama Cha Mapinduzi Wanawake wamekwea kilele cha mlima wa mafanikio kwa kunufaika na fursa za elimu,uongozi na kusogezewa karibu huduma za msingi za kijamii.

Kauli hiyo ameitoa leo katika mahojiano maalum ya miaka 42 ya CCM katika Kituo cha Redio ya Coconut FM kisiwani Unguja, amesema kundi la wanawake limekuwa mfano wa kuigwa katika jamii kutokana na mafanikio wanayoyapata katika awamu mbali mbali za uongozi wa Dola.

Amesema wanawake wanatakiwa kuchangamkia fursa za elimu,uongozi na ujasiriamali ili wafikie kiwango cha kujitegemea wenyewe bila kusubiri utegemezi kutoka kwa kundi la wanaume.

Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo wa UWT, amesema kundi la wanawake limetoa mchango wake katika harakati za kuasisiwa kwa CCM mnamo mwaka 1977,ambapo wanawake mbali mbali walijitokeza kuunga mkono juhudi za taasisi hiyo.

Akizungumzia baadhi ya maendeleo yaliyopatikana katika miaka 42 ya CCM,Ndugu Tunu ametaja utekelezaji wa Ilani za Uchaguzi za CCM katika vipindi tofauti vya uongozi wa dola chini ya uongozi wa ASP hadi CCM.

Amebainisha kwamba wanawake wanawake wengi wamepata nafasi za uongozi, utendaji katika taasisi mbali mbali za binafsi,Serikalini na katika Chama,sambamba na ongezeko la wanawake wengi wasomi tofauti na ilivyokuwa wakati wa enzi za ukoloni na usultani.

Akifafanua historia fupi ya CCM Naibu Katibu huyo,ameeleza kuwa baada ya kupatika kwa uhuru wa Tanganyika tarehe 9 disemba ,1961 na ule wa Zanzibar kupitia Mapindizi ya Zanzibar ya Januari 12,1964 ,kulifanya TANU na ASP viwe vimekamilisha jukumu la ukombozi wa nchi hizi kutoka katika makucha ya kisultan na ukoloni.

Anaeleza kwamba wakati huo mataifa machanga yaliishi katika hali ya ungonge lakini viongozi wake walitawaliwa na fikra za ukombozi wakipanga mikakati yao kwa siri,ili kujinasua katika utawala wa wageni, jambo lililochangia Zanzibar na Tanganyika kuungana mnamo April 26,1964.

Anasema baada ya muungano huo ikazaliwa Tanzania iliyokuwa na Vyama viwili vya ASP na TANU katika mazingira ya Chama kimoja cha siasa huku vikitambua kuwa kuna umuhimu wa kuwa na chombo madhubuti cha uongozi katika utekelezaji wa majukumu yake.

Amesema baada ya viongozi wakuu wa vyama hivyo kwa wakati huo kujitathimini na kutafakari kwa kina wakaamua kuviunganisha ASP na TANU na ikazaliwa rasmi CCM.

Pamoja na hayo ameongeza kwa kueleza kuwa UWT inalaani vikali vitendo vya udhalilishaji wa Kijinsia kwa wanawake na watoto vinavyofanyika kwa baadhi ya maeneo nchini.

Amevishauri vyombo vya kisheria vinavyohusika na udhibiti wa vitendo hivyo hasa vinavyohusika na utoaji wa hukumu kwa wahalifu wa kesi za udhalilishaji kutenda haki katika utoaji wa hukumu hizo ili kutoa fundisho kwa watu wenye tabia hizo.

Naye Afisa Habari wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Ndugu Is-haka Omar Rweyemamu, amesema taasisi hiyo ya kisiasa inajivunia kuwa karibu na Vyombo vya Habari nchini,ambao ni wadau wakubwa wa kufikisha taarifa na matukio ya CCM na Jumuiya zake kwa jamii.

Ametoa wito kwa viongozi wa Chama na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza utamaduni wa kushirikiana vya Vyombo vya habari ili wananchi wajue namna Serikali inavyotekeleza Ilani ya CCM kupitia miradi mbali mbali ya maendeleo.

UMOJA WA WABUNGE WANAWAKE TANZANIA (TWPG) WAJADILIANA KUHUSU UJENZI WA VITUO KWA AJILI YA WANAWAKE WANAOHASIRIKA KINJISIA

$
0
0
 Mwenyekiti Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Margaret Sitta (katikati)akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa umoja huo (hawapo kwenye picha) wakati wa semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Mhe. Susan Lyimo na Katibu Mhe. Lolensia Bukwimba

Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia, Bajeti kwa Mtazamo wa kijinsia na Haki za Binadamu, Ndg. Gemma Akilimali akizungumza na wajumbe wa Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) katika semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Muwezeshaji kutoka TGNP, Ndg. Zainab Mmary akizungumza na Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) wakati wa semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Mjumbe Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Zainab katimba akizungumza na wajumbe wa umoja huo pamoja na wawezeshaji kutoka TGNP wakati wa semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Viongozi kutoka Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) wakiwa katika semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Mwenyekiti Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Margaret Sitta, wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Mhe. Susan Lyimo, Katibu Mhe. Lolensia Bukwimba (kulia) na Mratibu, Ndg. Angelina Sanga.
  Wajumbe Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) wakiwa katika semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

TRC YAWAPA SHAVU WASANII KUTEMBELEA MRADI WA RELI YA KISASA YA STARDARD GAUGE

$
0
0
*Wasanii wapewa fursa adhim kutembelea mradi wa standard garge

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.
Shirika la reli nchini (TRC) limetoa nafasi kwa wasanii kutembelea mradi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge ili kujionea unavyoendelea. Mradi huo wa reli ya Kisasa ya Standard Gauge umeanzia jijini Dar es Salaam na kuelekea Morogoro utarahishisha usafiri wa abiria na mizigo, pia inatarajia kukuza biashara kati ya Tanzania na nchi Jirani kama vile Burundi, Rwanda na DRC kwa kuwa baadaye itaendelezwa kwenda hadi nchi zote zilizoko mpakani mwa Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mtendaji Mkuu wa shirika la reli nchini (TRC) Jamila Mbarouk amesema ni fursa adhimu kwa wasanii pamoja na waandishi wa habari kwa pamoja kupanda treni hiyo kwa lengo la kuangalia mradi huo uliweza kujengwa kwa awamu mbali mbali.

Mbarouk amesema Safari hiyo itasaidia kutangaza utalii uliopo ndani hasa kuwepo kwa treni hiyo ya umeme ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo ya tani elfu 10 huku iikiwa na spidi ya kilomita 160 kwa saa. "Shirika la reli (TRC) limewapa kipaumbele wasanii, wachoraji, wacheza mpira, Washehereshaji (MC), Waimbaji watakuwa mabalozi wazuri katika kuutangazia umma treni hiyo kukagua Standard Garge mpya itakayotoka Dar es salaam hadi Morogoro" alisema Mbarouk.

Aidha ameeleza treni hiyo imeitengeneza kwa pesa za watanzania kutokana na kodi zilizokusanywa. Mbarouk ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi ili iweze kusaidia uchumi wa Tanzania maana bila kodi hakuna maendeleo. Kwa upande wake Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere amepongeza uongozi wa Shirika la Reli (TRC) kwa kuwapa fursa wasanii na kutambua mchango wao katika jamii.

"Mkuu wa mkoa Paul Makonda anakaribisha kwa wote wanaohitaji mikopo aliyohaidi wakati wa Mkutano wa wasanii wote nchini kuweza kupata mkopo huo utakaowezesha kufanya kazi kwa weledi mzuri ili kukuza tasnia zote nchini." alisema Nyerere. Ameongeza kuwa ni vyema wasanii kuendelea kutangaza mema yote yanayofanywa na rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo Watanzania kwa kuwa wao ni vioo vya jamii na wananguvu kweli kuleta mabadiriko.
  Kiongozi wa Wasanii, Steve Nyerere akuongea na wanahabari kuwaelezea madhumuni ya Safari ya wasanii wote katika wote Februari 7, 2019 kutembelea mradi wa Reli ya Kisasa ya reli ya Kisasa ya Standard Gauge inayoanzia Dar es Salaam na kuelekea Morogoro. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.   Kaimu Mtendaji Mkuu wa shirika la reli nchini (TRC) Jamila Mbarouk (kulia) akiongea na wanahabari jinsi walivyoweza kudhamini wasanii hao kutembelea Mradi wa mradi wa Reli ya Kisasa ya reli ya kisasa ya Standard Gauge inayoanzia Dar es Salaam na kuelekea Morogoro ambapo amesema kuwa wametoa nafasi hiyo ili wasanii wakienda, warudi na watoe ushuhuda wa kweli kwa wananchi maana wao ni kioo cha jamii.
Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka ambaye ni mwakilishi wa wamiliki na wasanii wa bendi za muziki wa Dance akitoa machache mbele ya wanahabari.
Msanii wa Muziki wa Taarabu Khadija Kopa akitoa msisitizo wa wasanii kuendelea kumuunga mkono rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutangaza yale mazuri ambayo amekuwa akiyafanya katika kusukuma kurudumu la maendeleo Tanzania.

Diwani atimiza ahadi yake kwa kukarabati ofisi

$
0
0
Ofisi ya CCM Upanga Magharibi baada ya kufanyiwa ukarabati na Diwani wa Kata hiyo. 


DIWANI wa Kata ya Upanga Magharibi (CCM), Adnan Kondo ametimiza ahadi yake ya ujenzi wa ofisi za Serikali ya Mtaa na Kata ya Upanga Magharibi kama alivyoahidi kipindi cha kampeni aliyotoa mwaka 2015.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kondo alisema ujenzi huo umekamilika hivi karibuni ambako amefanikisha hatua hiyo ya maendeleo kwa asilimia 98 huku asilimia iliyobaki imetokana na marafiki zake.

Kondo alisema gharama za ujenzi huo ni zaidi ya shilingi milioni 20 ambako alitoa wito kwa viongozi wenzake wa chama waliopata dhamana ya kuongoza kukijenga chama kwa hali na mali.

Alisema awali kabla ya kufanikisha ujenzi huo, miaka iliyopita katika ofisi hiyo lilikuwa banda ambalo lilikuwa halina hadhi ya CCM ndipo alipotekeleza ilani ya chama kwa vitendo.

"Nawaomba viongozi wenzangu tuliopata dhamana ya kuongoza tutekeleze kwa vitendo ili kukijenga chama kwa sababu asilimia kubwa ya wananchi wana imani kubwa na chama chao," alisema Kondo.

Aidha aliwataka wanachama wa Kata yake kuitumia vilivyo ofisi hiyo kwa shughuli za kimaendeleo kwani CCM ndio baba wa nchi hii.

RC NDIKILO ATOA AGIZO WATOTO WA WAFUGAJI WASIOPELEKWA SHULE WASAKWE

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 


MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo, ametoa agizo kwa wakuu wa wilaya, maafisa tarafa na watendaji wa kata kuwasaka baadhi ya watoto wa wafugaji wenye umri wa kwenda shule za msingi na sekondari ambao hawajapelekwa shule hadi sasa na badala yake wakishinda kuchunga mifugo .

Aidha amewataka wakuu wa wilaya , wakurugenzi kwa kushirikiana na halmashauri kuhakikisha wanajenga madarasa 119 ili kuwawezesha wanafunzi 4,713 waliofaulu kidato cha kwanza mwaka jana na kukosa kuendelea na masomo kutokana na upungufu wa mdarasa hayo waweze kuanza masomo .

Akitoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa ambayo aliyoianza mkoani Pwani, akiwa Bagamoyo mkuu huyo wa mkoa aliwaasa ,wazazi wao waache tabia ya kuwatumikisha watoto hao katika ufugaji na kuwasababishia kukosa elimu haki yao ya kielimu .

Alieleza, endapo watoto hao wakisakwa na kupelekwa shule itasaidia kupata elimu kwani ndio msingi wa maisha yao. 

Akielezea suala la ujenzi wa miundombinu ya madarasa, Ndikilo alisema hadi kufikia January 31 mwaka huu wanafunzi walifaulu na kuripoti mashuleni ni 11,822 awamu ya kwanza ambapo wanafunzi 4,713 wameshindwa kutokana na ukosefu wa madarasa. 

"Hadi sasa mkoa umepokea bilioni 12.9 kwa ajili ya elimu bila malipo, pamoja na bilioni 3.245 ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa, kwa hivyo serikali wakati inafanya jitihada hizo na jamii tushirikiane kutatua kero zilizopo "alisisitiza Ndikilo. 

Nae mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa alisema kuwa, Bagamoyo ina uhaba wa madarasa 22 hadi sasa baada ya ujenzi wa madarasa nne kuendelea kujengwa shule ya Mapinga sekondari .

Awali diwani wa Mapinga ,Ibrahim Mbonde alisema ,ujenzi wa madarasa manne shule ya sekondari ya kata Mapinga hadi sasa upo hatua ya gebo, umegharimu milioni 33,na hadi kukamilika utahitajika milioni 100.

Alisema kukamilika kwa ujenzi huo kutawezesha kupunguza msongamano shule ya sekondari Kerege ambayo inahemewa na wanafunzi ambao wengine wanatokea kata ya Mapinga. 

Mkuu wa mkoa wa Pwani, ameanza ziara hiyo wilaya ya Bagamoyo kwa kukagua mradi wa ujenzi wa madarasa hayo manne, mradi wa kituo cha afya Matimbwa na mradi wa mfereji wa maji mtaa wa benki. 
 MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo, akitoa agizo kwa wakuu wa wilaya, maafisa tarafa na watendaji wa kata kuwasaka baadhi ya watoto wa wafugaji wenye umri wa kwenda shule za msingi na sekondari ambao hawajapelekwa shule hadi sasa na badala yake wakishinda kuchunga mifugo .



Ni Mkeka na Mvinyo Maadhimisho ya Valentine Dar

$
0
0
   Wadau mbalimbali wa uzalishaji wa mvinyo hapa nchini pamoja na watumiaji wa kinywaji hicho wanatarajia kufurahia pamoja Siku ya wapendanao yaani Valentine Day katika hafla ya maalum inayofahamika kama ‘Mkeka na Mvinyo’ itakayofanyika usiku wa Februari 14 katika hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa hafla hiyo kutoka kampuni ya Real PR Solutions (RPR), Bi Calorine Kirwanda amesema mbali na kuwakutanisha wadau muhimu wa kinywaji hicho, hafla hiyo inalenga kutoa fursa kwa watumiaji wa mvinyo hapa nchini kufurahia vinywaji tofauti vya aina hiyo vinavyozalishwa hapa nchini huku wakiwa wamekaa kwenye mikeka.

“Pamoja na kutoa fursa kwa watumiaji wa mvinyo siku hiyo kufurahia pamoja na wapendwa wao, usiku wa Mkeka na Mvinyo unalenga kuunga mkono jitihada za serikali katika kutangaza utalii na kukuza viwanda vya ndani kupitia uhamasishaji wa matumizi ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo aina tofauti ya mvinyo bora kabisa unaozalishwa hapa nchini,’’

“Upekee wa hafla hii unaanzia kwenye jina lake ‘ Mkeka na Mvinyo’. Hivyo basi itahusisha matumizi ya mikeka ambapo wageni wetu watapata fursa ya kuketi kwenye mikeka huku wakifurahi mvinyo bora unaozalishwa hapa nchini pamoja na nyama choma kadili ya matakwa yao,’’ alisema.

Aliwataja baadhi ya wadau muhimu katika kufanikisha hafla hiyo kuwa ni pamoja na Hoteli ya Whitesands, Bodi ya Utalii Tanzania, (TTB), GS 1, pamoja na kampuni ya magazeti ya TSN wazalishaji wa magazeti ya Daily News pamoja na Habari Leo.

Bi Kirwanda aliongeza kuwa hafla hiyo ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo utakaozinduliwa hivi karibuni unaolenga kutangaza utalii wa ndani pamoja kuvumbua fursa mbalimbali za kibiashara ndani ya nchini kwa lengo la kukuza uchumi unaofahamika kwa jina la ‘Domestic Tourism Promotion Initiative’ (DTPI).

“Tunahitaji kuhamasisha zaidi matumizi ya bidhaa za ndani ili kukuza uchumi wetu kama taifa,’’ aliongeza bi Kirwanda huku akitaja baadhi ya maeneo ambayo tiketi za hafla hiyo zinapatikana kuwa ni pamoja na Hoteli ya Whitesands na Shamo Tower Mbezi Beach.

Alisema, tofauti na mtu mmoja mmoja au kwa wale ambao watakuwa na wapendwa wao, Mkeka na Mvinyo inatoa fursa kwa mashirika na taasisi mbalimbali kufurahia pamoja katika dhana nzima ya kuonesha upendo, shukrani na pongezi baina yao na wadau wao katika shughuli zao za kila siku huku wakifurahia mvinyo na chakula kizuri katika viunga vya hoteli ya Whitesands.

“Ifahamike kwamba siku ya wapendanao sio kwa ajili ya wale wenye mahusiano ya kimapenzi tu bali pia inaweza kutumiwa na mashirika au taasisi mbalimbali lengo likiwa ni kuonesha upendo, shukrani na pongezi kwa wafanyakazi, na wadau mbalimbali wanaoshirikiana nao katika shughuli zao za kila siku,’’ alifafanua.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya magazeti ya TSN, Januarius Maganga alisema kampuni hiyo imeaamua kuunga mkono mpango huo kutokana na kuguswa kwake na namna unavyolenga kuchochea harakati za masoko kwa bidhaa za ndani sambamba na kuunga mkono agenda ya serikali ya uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw Geofrey Tengeneza alisema kupitia mpango huo mbali na kutangaza utalii wa fukwe pia utatangaza utalii wa asili kwa kuwa utahusisha mvinyo unaozalishwa hapa nchini huku watumiaji wakiwa wameketi kwenye mikeka ya asili.


Afisa Uhusiano wa kampuni ya GS 1, Bi Clementine Kahamba (kushoto) akizungumza kuhusiana na hafla hiyo. akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hafla hiyo itakayohusisha adau mbalimbali wa uzalishaji wa mvinyo hapa nchini pamoja na watumiaji wa kinywaji hicho itakayofanyika siku ya wapendanao yaani Valentine Day Februari 14 katika hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mratibu wa hafla hiyo kutoka kampuni ya Real PR Solutions (RPR), Bi Calorine Kirwanda (wa pili kushoto), Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya magazeti ya TSN, Januarius Maganga (wa pili kulia), pamoja na Meneja Uendeshaji wa Hotel ya Whitesands Bw Ali Hilika.
Mratibu wa hafla ya ‘Mkeka na Mvinyo’ kutoka kampuni ya Real PR Solutions (RPR), Bi Calorine Kirwanda (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hafla hiyo itakayohusisha adau mbalimbali wa uzalishaji wa mvinyo hapa nchini pamoja na watumiaji wa kinywaji hicho itakayofanyika siku ya wapendanao yaani Valentine Day Februari 14 katika hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya magazeti ya TSN, Januarius Maganga (wa pili kulia), Afisa Uhusiano wa kampuni ya GS 1, Bi Clementine Kahamba (kushoto) pamoja na Meneja Uendeshaji wa Hotel ya Whitesands Bw Ali Hilika. 

SPIKA WA BUNGE AKIZUNGUMZA NA WAZIRI MKUU OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akiteta jambo na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) mapema leo  Jijini Dodoma.
PICHA NA BUNGE.

WAKENYA WAFURAHIA DAWASA ILIVYOJIPANGA KUWAPA HUDUMA WANANCHI

$
0
0
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Mhandisi Aron Joseph akifunga warsha kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Miradi ya MajiTaka kwa wageni waliofika katika warsha ya siku moja ya kujengeana uwezo baina ya TANZANIA NA KENYA juu ya mafanikio na changamoto zinazowakabili. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutoka Kampuni ya Majisafi na Majitaka Nairobi (NCWSC) na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundi vya jamii ambao walikuja nchini Tanzania kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwatambulisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Miradi ya MajiTaka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) katika warsha ya siku moja ya kujengeana uwezo baina ya TANZANIA NA KENYA juu ya mafanikio na changamoto zinazowakabili. 
Wageni na wenyeji wakifuatilia mkutano huo.
Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam katika mradi wa vyoo vya kisasa kwa wananchi.
Mmoja ya maofisa wa Serikali ya Kenya waliofika Tanzania Bw. Patrick Njoroge wa Akiba Mashirani Trust akielezea hali halisi ya jimbo jipya la Mukuru, Nairobi- Kenya ambalo mipango mji wake haujapangika. 
Bi. Kellen Muchira kutoka Shirika la Caritas Switzerland akizungumza machache. 
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Mhandisi Charles Makoye akiwaelezea juu ya miradi wa kuchakata MajiTaka inayosimamiwa na kuendeshwa na DAWASA kwa wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI.
Mmoja ya wageni kutoka nchini Kenya Nancy akitia shukrani zake za peke kwa DAWASA na CCI kwa kuweza kuwapokea na kuwatembeza kujionea miradi mbali mbali ya MajiTaka jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti Rahimu Seif Gassi akitoa shukrani kwa wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) mara baada ya kumaliza mkutano. 

Picha ya pamoja. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

WAKENYA wamefurahishwa na jinsi Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka ilivyojipanga katika kusaidia wananchi ili kuwaondolea kero ya MajiTaka kupitia miradi yake. Miradi ya MajiTaka iliyowavutia ni ule wa Kigamboni na Vingunguti jijini Dar es Salaam ya kuwa jengea vyoo wananchi ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu juu ya kusimamia kutipia wadau wao Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI Tanzania).

 Akizungumza mmoja ya maofisa wa Serikali ya Kenya waliofika Tanzania Bw. Patrick Njoroge wa Akiba Mashirani Trust amesema binafsi amefurahishwa kwanza na ujio wao umekuja kujifunza masuala ya MajiTaka kwa vile nchini Naironi kuna eneo la Mukuru limetangazwa kuwa jimbo jipya hivyo wao wamepewa kazi ya kupanga mfumo mzima wa majisafi na Majitaka. 

 "Binafsi niwavutiwa sana na jinsi DAWASA mlivyoweza kuzuia milipuko ya magonjwa kwa kuwawekea wananchi wenu mifumo mizuri ya majitaka kwa kuwajengea vyoo kupitia wadau wenu CCI, hatuna budi tukirudi kule tutatoa mapendekezo mazuri na ikiwezekana mradi huu utaanza na kwetu," amesem Njoroge. Njoroge ameongeza kuwa jimbo jipya la Mukuru lililopo Nairobi linafanana kabisa na Mazingira mabovu yasipo rasmi kama ya Vingunguti, na wananchi wake wengine wanaishi katika vijumba vya mabati na wengine wamechukua mantanki makubwa na kufanya nyumba hivyo teknolojia waliyotumia CCI Tanzania itafaa hata huko kwao. 

Upande wake Bi. Kellen Muchira kutoka Shirika la Caritas Switzerland lililpo Kenya amesema kazi waliyopewa na serikali yao ya Kenya inafikia mwisho kwa kupitia maeneo yote ambayo wanao kwao itakuwa ni rasmi kusoma mazingira na kwenda kutoa mrejesho ili mambo yasonge mbele. 

"Kazi yetu tuliyopewa imefika mwisho hivyo hatuna budi kwenda kutoa mapendekezo yatakayoweza kufanya jimbo la Mukuru kuwa la mfano kwa kuweza kuwepa mipango iliyobora kuwasaidia wananchi. Awali akifungua warsha hiyo Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Mhandisi Aron Joseph ambaye akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu amewakaribisha wageni na kuwaambia wamefikia mikono salama na kuwa DAWASA imejipanga zaidi kuwatatulia wananchi matatizo ya Majisafi na Majitaka kwa kumaliza miradi ya majisafi ya Kimbiji na Mpela na miradi yote ikiwemo lile tanki la Kibamba na Kisarawe. 

Upande wa MajiTaka amesema kwa sasa wanayo miradi mbali mbali ikiwemo huo wa kuwajengea vyoo salama wakazi wa Vingunguti kupitia CCI, Toangoma ambao wakazi wa Kigamboni hawapati shida sehemu ya kupeleka majitaka kwa vile unaweza kupokea lita 10,000 kwa siku huku akiongezea miradi ya Mlalakuwa, Mburahati na Temeke Wires. 

"Tumejipanga kutoa huduma bora kwa wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kwa kiwango cha juu kabisa, tunangoja kufungua milango mwezi ujao kwa kuweza kupata fedha zaidi ili kuendeleza miradi mingi zaidi, niwaombe mkienda huko kwenu mje tena muone tulivyosomba mbele," amesema Mhandisi Aron Joseph.

RAIS MAGUFULI ATOA MILIONI 200 KWAJILI YA UNUNUZI WA VIFAA VYA KISASA KITUO CHA CHANEL 10 NA AFRICAN MEDIA GROUP

$
0
0
 Rais Dkt Magufuli.
 
Na. Vero Ignatus

Katika kushehereke miaka 42 ya kuzaliwa chama cha mapinduzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametembelea kituo cha Luninga cha Chanel ten sambamba African group na kuzungumza na wafanyakazi na kusikiliza changamoto zao

Katika ziara hiyo Rais ameahidi shilingi milioni 200 kwaajili ya kununua vifaa vipya kwaajili ya kurushia matangazo ambapo amesema kupitia chombo hicho Watanzania watanufaika kwa kupata taarifa na watajifunza mambo mengi ,

Rais Magufuli amezungumzia pia kuhusu Uhuru wa vyombo vya habari ambapo amesema kuwa kila mtanzania anayohaki ya kuzungumza, kupata habari na kuelewa mambo yanayoendelea katika nchi yake

Ametoa angalizo kwa wanahabari kuwa wazingatie Maadili pale wanapotoa habari katika vyombo vyao na wahakikishe kuwa habari hizo zinaukweli ndani yake.'' Wanahabari mnatakiwa mzingatie maadili wakati mnatoa habari zenu, unaweza kutoa habari amabayo haina uhakika ukahatibu maisha ya mtu kabisa, kisha baadae unakuja kugundua siyo jambo la ukweli italeta picha mbaya kayika jamii''Amesisitiza Rais Magufuli

Rais amesisitiza kuwa Vyombo vya habari vinatakiwa vizungumze kwani vinaibua mambo mengi ambayo ni msaada kwa viongozi na watanzania kwa ujumla hivyo mnahitaji vinahitajika umakini mkubwa.

Amewataka wanahabari kufanya kazi huku wakitanguliza Uzalendo wa Taifa la Tanzania mbele kwani watakapo kwenda kinyume wataharibu Amani iliyopo na mataifa jirani wataitazama nchi kwa mtazamo mwingine

'' Hakuna mtu mwingine atakayetoka nje ya nchi kuja kutusaidia kujenga nchi ni sisi wenyewe tutangulize maslahi ya Taifa zungumzeni mambo mema kwaajili ya nchi yenu'' Alisema Rais. Amesema katika nchi ya Tanzania vyombo vya habari vilivyopo vinatakiwa kuizungumzia nchi vyema hivyo wanahabari wote
Wanao wajibu wa kuzungumza mambo chanya bila kupindisha ukweli wala kumuonea mtu yeyote.

Pia amewataka Watanzania kila mmojawapo anapoingia ofisini kwake afanye kazi kwa ajili yake na kwa maslahi ya Taifa lake akitanguliza uzalendo ,'' Miaka ijayo tunataka kuwa na mabilionea, wanyabiashara wakubwa, wakulima na wafugaji katika nchi yetu wanaofanya kazi na kulipa kodi ya serikali watakaotambuliwa kimataifa kwamba wanatoka Tanzania'' Amesema Magufuli.


Kituo cha Luninga cha Chanel ten na African Media group, vya Jijini Dar es salaam, vyote hivyo vinamilikiwa na Chama cha Mapinduzi(CCM) nchini 

SIJAWAHI KUONA RATIBA YA LIGI KUU KAMA HII- MWINYI ZAHERA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KOCHA Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amelalamikia ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuwa haiwapi nafasi wachezaji muda wa kupumzika.

Ameyasema hayo baada ya kuwasili Mkoani Singida jana usiku ikiwa ni safari ya masaa 15 kutoka  Tanga walipokwenda kucheza na Coastal Union.

Zahera amesema, wachezaji wake wamemaliza kucheza mechi siku ya Jumapili jioni na jana Jumatatu wametoka Tanga na kuanza safari majira ya saa 1 asubuhi na kufika Singida sa 3 usiku ikiwa ni masaa 15 ya safari.

Amesema, katika ratiba ya kawaida wachezaji wake watapata muda mchache sana wa kupumzika na kesho watatakiwa wacheze na Singida United.

"Ratiba ya Ligi sijawahi kuona katika maisha yangu, huwezi kucheza mechi ukasafiri siku masaa 15 kuja Singida ucheze mechi halafu urudi tena masaa 15 Tanga kucheza mechi nyingine," amesema Zahera.

Zahera amesema ratiba imekuwa inamnyima fursa ya kuandaa programu kwa wachezaji wake hususani baada ya kumaliza mechi na pia timu nyingi zimekuwa zikichoka sana kutokana na ratiba kuwa ngumu kwa sababu ya miundo mbinu na jiografia ya nchi.

 Yanga inashuka dimbani siku ya Jumatano kucheza na Singida United katika muendelezo wa Ligi kuu Tanzania Bara na kisha itarejea tena Tanga kucheza na JKT Tanzania Februari 9 mwaka huu.

Yanga inaongoza ligi kwa alama 54 akifuatiwa na Azam mwenye alama 47 huku nafasi ya tatu ikiwa ni kwa KMC mwenye alama 35.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akizungumza mara baada ya Bunge kurejea Jijini Dodoma. Spika ametoa Taarifa fupi kuhusu Kingora cha hatari kilicholia kuashiria hali ya hatari  Bungeni  kuwa hakukuwa na hatari yeyote.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson akiuliza swali leo Bungeni Jijini Dodoma.

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe.Musa Sima akijibu maswali mbalimbali ya wabunge Bungeni leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof . Palamagamba Kabudi akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge Mhe.Stephen Kagaigai akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira  na Wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama,Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi na Mbunge wa Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema wakati Bunge lilipositishwa kwa muda baada ya King’ora cha kuahsiria hatari  kulia leo Bungeni JIjini  Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki wakijadili jambo na Mbunge wa Ubungo Mhe.Said Kubenea na Mbunge wa Kigoma kaskazini Mhe.Zitto Kabwe leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Wageni mbalimbali wakifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge leo Jijini Dodoma.

 Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa  akifurahia jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Wenye Ulemavu Mheshimiwa Stella Ikupa nje ya Ukumbi wa Bunge.Dodoma leo Februari 5/2019
 Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya Wabunge na Wananchi mbalimbali katika Viwanja vya Bunge, Jijini Dodoma. leo Februari 5/2019
Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa  akiwa katika maongezi na , Kaimu Askofu Mkuu wa Kanisa la Assemblies of God Tanzania(TAG). Dkt. Magnus Mhiche wakati alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Februari 5/2019

IGP SIMON SIRRO AMEFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA

WAZIRI WA KILIMO AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga, Naibu Mawaziri wa kilimo Mhe Innocent Bashungwa na Mhe Omary Mgumba, pamoja na wataalamu wa wizara ya kilimo wakizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019.
Pichani ni Naibu mawaziri wa kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Kulia) na Mhe Omary Mgumba, wakifatilia kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga wakizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akimsikiliza mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke akizungumza kwenye kikao kazi wakati alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. SARAH COOKE, jana tarehe 4 Januari 2019 amemtembelea Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Uingereza katika sekta ya kilimo.


Katika mazungumzo hao, Mhe Hasunga na Bi. COOKE wamekubaliana kuongeza kasi ya Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, makubaliano ambayo yatasaidia uwezekano wa kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo kwa nchi zote mbili.

Katika kikao kazi hicho Waziri Hasunga amemueleza Balozi huyo kuwa serikali ya Tanzania imeanza zoezi la utambuzi wa wakulima nchini kwa kuwaandikisha ambapo mpaka sasa wakulima wa zao la Tumbaku wamekwisha andikishwa.


Hasunga alisema kuwa lengo la zoezi hilo la uandikishaji ni kuimarisha utambuzi wa wakulima ili serikali iweze kuwahudumia kwa weledi wakulima kote nchini kupitia pembejeo mbalimbali za kilimo ili kuondokana na wakulima hewa ambao wanatumia mwanya huo kuiibia serikali.


Vilevile amemueleza Balozi huyo kuwa serikali imejipanga kuimarisha sekta ya utafiti wa kilimo nchini jambo litakaloongeza tija na manufaa makubwa kwa wakulima nchini.

Katika mazungumzo hayo, Mhe Hasunga amemueleza Bi COOKE namna ambavyo serikali ya Tanzania imejipanga kuimarisha masoko ya ndani na nje ya nchi kwa wakulima.

Bi. COOKE, kwa upande  wake amefurahishwa na jinsi ambavyo Waziri wa Kilimo pamoja na wasaidizi wake wanapambana kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika kuimarisha sekta ya kilimo sambamba na kuboresha masoko ya wakulima nchini.


Balozi huyo amemueleza waziri wa kilimo kuwa Uingereza itaendeleza maradufu ushirikiano na Tanzania kwani ni nchi yenye Amani na utulivu mwingi kwa wananchi wake.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA KUTOKA UTURUKI OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wafanyabishara kutoka Kampuni ya MNG ya nchini Uturuki walipomtembelea mapema leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Rais  wa  Kampuni ya MNG ya nchini Uturuki Bw. Mehment Nazif Gunal akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai wakati walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.
  Spika wa Bunge (kulia) katika picha ya pamoja na Rais  wa  Kampuni ya MNG ya nchini Uturuki Bw. Mehment Nazif Gunal mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai katika picha ya pamoja na Wafanyabishara kutoka Kampuni ya MNG ya nchini Uturuki mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dodoma.

PICHA NA BUNGE

MADIWANI MOSHI KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UBADHILIFU WA FEDHA KITUO CHA AFYA PASUA

$
0
0
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi,RAymond Mboya akiwa aameongozana na Madiwani wa Halmashauri hiyo kukagua shughuli za ukarabati unaoendelea katika kituo cha Afya cha Pasua mjini Moshi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya akijaribu kuzungusha moja ya vitanda vilivyowekwa katika wodi ya wazazi katika kituo hicho. 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akizungumza mara baada ya kutembelea kituo cha Afya cha Pasua kujionea shughuli za ukarabati wa kituo hicho zinavyoendelea. 
Baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wakiwa katika kituo hicho kuunga mkono shughuli za maendeleo . 
Diwani wa kata ya Bomambuzi ,Juma Raibu kilipo kituo hicho cha Afya akizungumza mara baada ya ukaguzi . 
Moja ya jengo la kituo hicho likiwa katika hatua za mwisho kukamilika. 
Shughuli za upakaji rangi ikiendelea kwa baadhi ya majengo katika kituo hicho. 
Baadhi ya majengo mapya yaliyoongezwa katika kituo hicho cha Afya Pasua .


Na Dixon Busagaga,wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.


BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi limeeleza kufanyia kazi tuhuma za ukiukwaji wa taratibu katika mradi wa ukarabati wa Kituo cha Afya cha Pasua unaotajwa kupelekea upotevu wa fedha .

Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya wakati wa ziara ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi walipotembelea kituo cha Afya cha Pasua kujionea ukarabati unavyoendelea.

“Kuna matatizo na hayo matatizo nimesema nije kwanza kuangalia ,kwa kuwa bado hili swala liko kwenye vikao vya ndani tutatoa taarifa yakikamilika kwenye vikao kwanza, ni kwamba kuna taratibu hazijakaa vizuri kwenye mchakato mzima wa ukarabati wa kituo cha afya.”alisema Mstahiki Mboya .

Alisema fedha zilizotumika katika ukarabati wa kituo hicho ni fedha za serikali zinazotokana na kodi inayokusanywa kutoka kwa wananchi na kwamba zinapotumika ni lazima baraza la Madiwani kufuatilia na kujiridhisha kama zimetumika kwa utaratibu uliokusudiwa.

“Hizi fedha ni kodi zetu ,ambazo wakati mwingine zinaitwa fedha za serikali sasa zinapotumika hapa ni lazima tuhakikishe zinatumika kwa utaratibu uliokusudiwa na kwa utaratbu ambao hauta leta mashaka wala tatizo kwa hiyo tusubiri mchakato na taratibu za vikao zitakapo kamilika tutawajulisheni”alisema Mboya 

Akizungumzia kuhusu ukarabati wa Kituo hicho ,Mstahiki Mboya alisema hakuna mradi unaofanyika mahala popote bila ya kupitishwa katika vikao halali vya baraza la Madiwani na kwamba hadi kuanza kwa ukarabati kwa kituo hicho taratibu zilifuatwa.

“Tangu mwaka 2013 tulikuwa tunatenga fedha kwenye Bajeti ya ujenzi wa vituo vya Afya kikiwemo kituo cha Afya cha Pasua ,na ilikua ni sehemu ya upasuaji ,wodi ya kujifungulia kina mama,chumba cha mionzi ya X-ray na chumba cha kuhifadhi maiti”alisema Mboya .

“Tumekuwa tukitenga na kwa kuwa ukarabati ulitakiwa uwe mkubwa ,tumeendelea kutenga miaka yote na ilivyoingia serikali ya awamu ya tano ikaingia na mkakati wa kuboresha vituo vya Afya na manispaa ya Moshi tulifanikiwa kwa sababu ilikuwa kwenye mpango”alisema Mboya.

Alisema katika ukarabati huo serikali imetoa kiasi cha Sh Mil 400 ikiwa ni mchango wake huku fedha nyingine zikitakiwa kutolewa na Halmashauri hali iliyowalazimu kubadilisha matumizi ya fedha kwa baadhi ya vifungu ili zikamalizie maeneo ambayo bado hayajakamilika katika kituo hicho.

“Kukamilika kwa kituo hichi kutawezesha wananchi wa maeneo ya kata ya Bomambuzi ,Pasua ,Matindigani na Kaloleni waweze kupata huduma ambayo ni ya kiwango na hasa tuilenga kwe nye eneo la wodi ya wazazi.”alisema Mboya .

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Pasua ,Juma Raibu alisema ukarabati wa vituo vya Afya ni mpngo mkakati wa taifa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi na kupunguza changamoto zilizokuwa zikiikabili sekta ya Afya nchini.

“Mimi kama Diwani nilipewa maelekezo kwa barua kwamba niunde kamati mbalimbali za kuweza kusaidia ukarabati wa kituo hiki uweze kuendelea ,kamati ya kwanza niliambiwa niunde ya manunuzi,kamati ya mapokezi na kamati ya ujenzi ili wazawa wa eneo hili wawe ni sehemu ya wasiamamizi wa mradi huu”alisema Raibu.

Katika ziara hiyo Globu ya Jamii ilishuhudia wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwa wamoja katika kukagua maeneo mbalimbali ya kituo hicho .

Mstahiki Meya ,Raymond Mboya(Chadema) akazungumzia hali hiyo na kuungwa mkono na Diwani wa kata ya Kilimanjaro ,Priscus Tarimo wakieleza kuwa linapofika suala la maendeleo itikadi za kisiasa huwekwa pembeni.

“Hii inaashiria Moshi tumekomaa ,nah ii inaashiria kwamba kwa nini inaitwa Moshi ,kwamba baada ya uchaguzi kauli yetu ni maendeleo ,anayeleta siasa huwa hatumpia nafasi ,na ndio maana mimi kama Meya kwenye baraza nawaambia tunaongea lugha ya maendeleo”alisema Mboya.

Naye Diwani Tarimo akaeleza juu ya hali hiyo “Mazingira ya ya kisiasa katika mkoa wa Kilimanjaro hasa katika manispaa ya Moshi ni tofauti sana kutokana na uelewa mkubwa wa watu na inawezekana kabisa madiwani wa pande zetu tukakaa pamoja na jambo linalohusu maendeleo tukalisimamia kwa pamoja.

LUGOLA ASEMA TANZANIA IPO SALAMA NA IMARA, AKUTANA NA BALOZI WA SWEDEN NCHINI, JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Sweden na Tanzania. Lugola alimwambia Balozi huyo, nchi ipo salama na imara na ayapuuze maneno ya baadhi ya watu wanaoichafua nchi wakiwa na maslahi yao binafsi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Lugola, jijini Dodoma leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg alipokuwa akimfafanulia jambo wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dodoma, leo. Viongozi hao walijadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Sweden na Tanzania. Pia Waziri Lugola alimwambia Balozi huyo, nchi ipo salama na imara na ayapuuze maneno ya baadhi ya watu wanaoichafua nchi wakiwa na maslahi yao binafsi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Lugola, jijini Dodoma leo. 


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Tanzania ni kisiwa cha amani na pia ipo imara katika Bara la Afrika licha ya uwepo wa baadhi ya watu wachache wanaichafua taswira yake kwa maslahi yao binafsi. 

Lugola ameyasema hayo jijini Dodoma leo, alipokua anazungumza na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg, ofisini kwake alimueleza kuwa, Rais Dk John Magufuli anaendelea kuiongoza nchi vizuri, na mpaka sasa Tanzania ipo imara na itaendelea kuwa imara, na wageni mbalimbali wanakaribishwa kuja nchini kuwekeza, kufanya utalii pamoja na masuala mbalimbali ambayo yatawezesha nchi kupata maendeleo zaidi. 

“Mheshimiwa Balozi nchi yetu ipo salama na tunaendelea kuijenga kwa juhudi zote, Sweden na Tanzania ni marafiki kwa miaka mingi, yangu kipindi cha uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, hivyo tutaendelea kushirikiana nanyi ipasavyo, nakukaribisha sana Dodoma na hapa ndio makao makuu ya nchi,” alisema Lugola. 

Lugola aliongeza kuwa, anaikaribisha Serikali ya Sweden pamoja na wananchi wake wafike nchini kuwekeza katika maeneo mbalimbali yakiwemo utalii, pamoja na masuala ya biashara. 

Waziri na Balozi huyo, pia walijadiliana masuala ya ushirikiano katika kuendelea kuimarisha usalama nchini, huku Lugola akimwambia Balozi huyo mikakati ya nchi katika kuimarisha ulinzi ambapo Serikali inatarajia kufunga kamera usalama (CCTV) katika Jiji la Dar es Salaam, Mwanza na Arusha kwa lengo la kuimarisha ulinzi zaidi. 

Waziri Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini. 

“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola. 

Hata hivyo, Balozi Sjoberg alifurahi kuonana na Waziri huyo pamoja na kufika Makao Makuu ya Serikali jijini Dodoma ikiwa ni mara yake ya pili tangu alipofika nchini kwa ajili ya kuiwakilisha nchi yake, pia alimuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Sweden na Tanzania.

KIGOGO MWINGINE BENKI I&M AUNGANISHWA KESI YA MFANYABIASHARA ALIYETAJWA NA RAIS DKT MAGUFULI

$
0
0
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii.

Meneja wa benki ya I&M tawi la Kariakoo, Sameer Khan, amefikishwa Katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuunganishwa na

mfanyabiashara maarufu aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takribani Sh. Milioni Saba kwa dakika, Mohamed Yusufali na mfanyakazi wake Arital Maliwala ambapo wote wamesomewa mashtaka mapya 506.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mapema Leo asubuhi washtakiwa Yusufali na Maliwata kufutiwa mashtaka yao ya zamani mbele ya Hakimu Mkazi Janet Mtega chini ya kifungu cha sheria cha 91(1) cha Mwenendo wa makosa ya jinai ambapo upande wa mashtaka waliomba kuliondoa shtaka hilo kwa sababu DPP hana nia Ya kuendelea na mashtaka dhidi yao. Haya hivyo Washtakiwa walikamatwa tena.

Awali, Yusufali na Maliwala. Walikuwa wakikabiliwa na jumla ya mashtaka 601 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 14

Akisoma hati ya mashtaka mapya wakili wa serikali Mwandamizi Patrick Mwita, akisaidiana na Ester Martin na Wakili kutoka Takukuru Leornad Swai wamewasomea washtakiwa mashtaka 506, ambapo wanakabiliwa na mashtaka ya 293 Ya kughusi, mashtaka 132 Ya kutoa taarifa za uongo na shtaka moja La kwepa kodi Ya zaidi ya Sh. BIL. 24

Pia mshtakikwa Khan anakabiliwa na mashtaka 12 ya utakatishaji huku Yusufali na Maliwata wakikabiliwa na mashtaka 50 ya utakatishaji. Shtaka jingine dhidi ya washtakiwa wote ni kula njama ya kutenda kosa la kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 24.

Katika shtaka la kuisababishia serikali hasara imedaiwa, katika tarehe tofauti tofauti, kati ya Januari 2008 na Januari 2016 washtakiwa waliwasilisha nyaraka za uongo huko Katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh. 24.303.777.4260.70.

Haya hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi Mahakama Kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wako kwenye hatua za mwisho kufaili kesi Mahakama Kuu Kitengo cha mafisadi.

Kesi hiyo itatajwa tena Mahakamani hapo Februari 18.2019

Meneja wa benki ya I&M tawi la Kariakoo, Sameer Khan akifikishwa katika  mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuunganishwa namfanyabiashara maarufu aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takribani Sh. Milioni Saba kwa dakika, Mohamed Yusufali na mfanyakazi wake Arital Maliwala ambapo wote wamesomewa mashtaka mapya 506.

MTIBWA WAENDELEA KUJINOA KUWASUBIRI AFRICAN LYON IJUMAA HII

$
0
0



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

TIMU ya Mtibwa Sugar kinashuka dimbani siku ya Ijumaa ya tarehe katika mchezo wake wa  ligi kuu bara (TPL) dhidi ya African Lyon.


Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa nyumbani wa Mtibwa Sugar (Manungu) unatarajiwa kuwa wa ushindani kwa pande zote mbili..


Kuelekea mchezo huo Msemaji wa klabu hiyo Thobias Kifaru na kusema kuwa maandalizi kwa kikosi kizima yanaendelea vizuri na wachezaji wana hari ya kuhakikisha wanabakisha alama tatu katika Uwanja wa nyumbani.

‘sisi kama wenyeji kila kitu kinaenda vizuri katika maandalizi ya mchezo huo, kilichobaki ni mchezo wenyewe na tunawaomba wana mtibwa ,wana Morogoro na wapenzi wetru waje kwa wingi watupe support,” Kifaru

Tunaamini African Lyon ni timu nzuri lakini hatutawabeza kabisa na hatutaki kupoteza mchezo huo muhimu kwetu.


Kikosi cha Mtibwa Sugar kitaendelea kukosa huduma ya Kelvin Sabato na Dickson Job ambao wako katika majaribio, Sabato yuko Afrika Kusini katika klabu ya Tshakuma Tsha Madzivhandila na Dickson Job yeye yupo katika majaribio Arsenal Kiev.

Lakini kikosi cha wana tam tam kimezidi kuimarika kutokana na wachezaji waliokosekana katika michezo iliyopita kurejea ambao ni Salum Kihimbwa alikuwa anatumikia kadi nyekundu, Juma Luizio na Jaffari Kibaya pia wamerejea katika kikosi baada ya kuwa wamepewa mapumziko.

SERIKALI YA DRC YATETEA MAWAZIRI KULIPWA MAISHA YAO YOTE

$
0
0
Waziri mkuu anayeondoka Bruno Tshibala alisaini maagizo hayo mnamo Novemba. Haki miliki ya picha GETTY IMAGES

Serikali ya Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo imetetea maagizo yanayoruhusu mawaziri kulipwa mishahara na marupurupu kwa maisha yao yote.


Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, serikali imesema malipo hayo "sio ya kuwatajirisha maafisa".
Maagizo mawili, yanayoruhusu mawaziri kupokea marupurupu ya kiwango cha chini zaidi $2,000 yameshutumiwa pakubwa.

Idadi kubwa ya raia nchini Congo wanaishi katika umaskini.

Serikali inayoondoka ilikuwa inawapatia mawaziri "kiwango cha chini kuwatosheleza mahitaji yao ya kimsingi, kama chakula, makaazi na huduma ya afya".

Malipo hayo "ni ya kuwaepusha kuishia katika umaskini", taarifa inasema.

Maagizo hayo mawili, yaliotiwa saini na waziri mkuu anayeondoka Bruno Tshibala mnamo Novemba, yaliripotiwa pakubwa hivi karibuni tu katika vyombo vya habari.

Agizo la kwanza linawapa mawaziri wakuu mishahara ya kila mwezi yalio sawa na 30% ya mshahara anaopokea sasa waziri mkuu, tiketi ya mara moja ya ndege kwa mwaka na marupurupu ya nyumba yenye thamani ya $5,000, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Agizo la pili linawapa mawaziri mishahara sawa na 30% ya mawaziri wa sasa na $1,000 kila mwezi kulipia makaazi. Watapokea pia tiketi ya mara moja kwa mwaka ya ndege, Reuters linaripoti.Haki miliki ya picha REUTERS

Maagizo hayo yalishutumiwa pakubwa katika nyanja zote kisiasa.
Mshauri wa rais wa zamani Joseph Kabila amesema "hayaendani na mtazamo wetu wa kiuchumi na kijamii".

Patrick Nkanga ameandika kwenye Twitter: "Ni kupita kiasi na ni gharama kubwa zisizohitajika kwa fedha za umma." Lakini serikali imetetea maagizo hayo na kueleza kwamba hayatozingatia mawaziri wa awamu iliopita, badala yake ni kwa walioko kwenye serikali ya sasa na serikali zijazo.

Rais mpya wa Jamhuri ya Kidmeorasi ya Congo, Felix Tshisekedi, aliapishwa madarakani mwezi uliopita. Alipokea wadhifa huo kutoka kwa Kabila katika ukabidhi wa kwanza wa madaraka uliofanyika kwa amani katika nchi hiyo na uliowahi kushuhudiwa katika miaka 60.

Matokeo ya uchaguzi yalishutumiwa pakubwa, huku kukiwa na ripoti za makubaliano kati ya rais Kabila na bwana Tshisekedi -hatahivyo pande zote zilikana tuhuma hizo.

Chanzo BBC

Serikali Yatoa Siku 24 Kuhuisha Machapisho

$
0
0
Mkurugenzi wa Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma. Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na waandishi wa habari ni wa kwanza kwa mwaka huu ambao ameutumia kuwaelezea wananchi juhudi mbalimbali za kimageuzi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.


Na Beatrice Lyimo-MAELEZO 

DODOMA 

Serikali imetoa notisi ya siku 24 kwa wamiliki wa machapisho (magazeti na majarida) ambayo bado hayajahuisha leseni zao kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kuhakikisha wanahuisha leseni hizo hadi ifikapo Machi 21, 2019 vinginevyo hayataruhusiwa kuchapishwa. 

agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi leo Jijini Dodoma wakati akiongea na Wanahabari kuhusu utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Serikali ikiwemo utekelezaji wa Sheria ya Huduma ya Habari. 

"Kwa mujibu wa Sheria mpya ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, wamiliki wote wa magazeti na majarida wanapaswa kuhuisha leseni zao kila mwaka na tulitoa notisi kwa ambao hawajahusiha, wapo walioitikia wito na wapo waliokaidi, orodha kamili imewekwa katika www.maelezo.go.tz" ameeleza Dkt. Abbasi. 

Aidha, Dkt. Abbasi ameongeza kuwa, utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari unaendelea hivyo wakati wowote kuanzia sasa chombo cha kwanza cha kusimamia wanahabari yaani BODI YA ITHIBATI itaundwa ambapo kazi yake kubwa ni kusajili wanahabari, kuwapa vitambulisho vya kitaaluma na kusimamia maadili yao. 

katika kuhakikisha kuwa Waandishi wa Habari wanatekeleza majukumu yao bila vikwazo na pia wananchi wanapata taarifa mbalimbali, Dkt. Abbasi ametoa wito kwa Watendaji mbalimbali wa Serikali katika ngazi zote kutoa habari na kueleza utekelezaji wa ahadi mbalimbali za Serikali kwani ni takwa la Katiba na Sheria. 

"Natumia mkutano huu kuwakumbusha watendaji mbalimbali wa Serikali katika ngazi zote kuwa, isipokuwa kama habari husika imezuiwa kisheria, kwa sasa kutoa habari na kueleza utekelezaji wa ahadi tulizoahidi ni takwa la Katiba na Sheria na si utashi mtu binafsi. Tutaanza kufuatilia watendaji wanaokaidi matakwa haya ya kikatiba" amefafanua Dkt. Abbasi. 

Mbali na hayo Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza kwa kasi wajibu wake kwa umma ikiwemo kuhakikisha hali ya amani, utulivu, kusimamia utawala bora na utawala wa sheria.
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images