Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109935 articles
Browse latest View live

Mahakama yawaamuru wadhamini wa Mbunge Tundu Lissu kufika mahakamani Februari 25

$
0
0
Na Karama Kenyunko globu ya Jamii 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru wadhamini wa Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chama cha Chadema, Tundu Lissu kufika Mahakamani hapo Februari 25, 2019 kueleza maendeleo ya afya yake.

Amri hiyo,  imetolewa  leo Februari 4, 2019 baada ya Wakili wa serikali Mwandamizi Patrick Mwita kudai mahakamani hapo,  Mbele ya  Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa na kwamba hadi sasa hawajajua hali ya mshtakiwa wa nne, ambae ni Lisu inaendeleaje. 

"Mheshimiwa, Kesi hii leo imekuja kwaajili ya kuendelea kusikilizwa lakini hadi sasa hatuna taarifa ya hali ya mshtakiwa wa nne,tunaamini hata Mahakama hii haina rekodi ya Maendeleo yake" amedai  Wakili Mwita

Hakimu Simba amesema, kwa kuwa mahakama hiyo haina rekodi ya taarifa ya hali ya Lisu hivyo Februari 25 wadhamini wafike Mahakamani ili kueleza maendeleo ya afya yake.

Kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa mashtaka, inamkabili Lissu na wenzake Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Kwa pamoja, wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Inadaiwa, Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifaza uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13 ,2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ATEMBELEWA NA WADAU WA MAENDELEO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na marafiki zake ambao ni wadau wa Maendeleo kutoka Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya tukio lililofanyika leo tarehe 4 februari, 2019 nje ya viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na marafiki zake ambao ni wadau wa Maendeleo kutoka Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya tukio lililofanyika leo tarehe 4 februari, 2019 nje ya viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na marafiki zake ambao ni wadau wa Maendeleo kutoka Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya tukio lililofanyika leo tarehe 4 februari, 2019 nje ya viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kushoto kwa Naibu Spika, Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga na kulia kwa Naibu Spika ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa

Serikali Yanunua Tani 214,269.7 za Korosho Ghafi Kufikia Januari 30

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Hadi kufikia Januari 30 mwaka huu Serikali imenunua tani 214,269.7 za korosho ghafi zenye thamani ya shilingi 707,089,957,200.00 sawa na asilimia 89.3 ya lengo la uzalishaji wa msimu wa korosho wa mwaka 2018/2019.

Hayo yameelezwa leo Bungeni, Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Omari Mgumba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kawe, Mhe. Halima Mdee kuhusu tani ngapi zimenunuliwa na Serikali mpaka sasa na wakulima wangapi na vyama vingapi vya msingi vimelipwa na vingapi bado havijalipwa.

"Ununuzi wa korosho unafanywa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ambapo malipo yaliyolipwa na kuingizwa kwenye akaunti za wakulima hadi tarehe 30 Januari, 2019 ni kiasi cha shilingi 424,849,405,110 zilizotokana na korosho za wakulima kiasi cha tani 134,535.9," alisema Mhe. Mgumba.

Ameendelea kusema, jumla ya wakulima 390,466 wamelipwa hadi kufikia tarehe 30 Januari, 2019. Aidha vyama vya msingi 603 vimelipwa kati ya vyama vya msingi 605 vilivyohakikiwa.Aidha amesema, zoezi la operesheni korosho linaenda vizuri na linatarajia kukamilika ifikapo tarehe 15 Februari mwaka huu.

Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ni taasisi ya kibiashara yenye lengo la kupata faida na mtaji wake unatokana na ruzuku kutoka Serikalini na mikopo kutoka taasisi za Fedha kama Benki ya Maendeleo ya Kilimo - TADB, NMB na CRDB.

Mnamo Novemba, 2018 Serikali iliungana na msimamo wa wakuliwa wa kukataa bei zilizotolewa na kampuni za ununuzi wa korosho, ambapo zilitangaza kununua korosho kwa bei ya kati ya shilingi 2,717 na shilingi 1,900 kwa kilo ikiwa imeshuka kutoka zaidi ya shilingi 3,600 ya msimu uliopita.

Aidha, Mhe. Rais Dkt. Magufuli alitangaza Serikali kununua korosho hizo kwa shilingi 3,300 badala ya shilingi 3,000.

Wavuvi wanne Kizimbani kwa uvuvi haramu

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii. 

WAVUVI wanne wakazi wa jijini Dar es Salaam,  leo Februari 4.2019 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za  kukutwa wakitumia vifaa vya kuvulia ambavyo vimekatazwa kinyume cha sheria namba 66(2)(q) na (4) ya sheria ya Uvuvi ya mwaka 2009.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi Maria Kasonde Wakili wa Serikali Sada Mohamed  amewataja washtakiwa hao kuwa ni Athumani Fakih (42), Mbwana Fakih (61), Mohamed Ushanga (38) na Khalifa Abdallah wote wakazi wa Kigamboni.
Wakili Saada amedai,katika shtaka la kwanza, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa,  Novemba 3, mwaka jana,  wakiwa katika bahari ya Hindi eneo la Fungu Baraka lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam walikutwa wakivua kwa kutumia nyavu ambazo zilikuwa chini ya kiwango au zimekatazwa. 

Katika shtaka la pili, imedaiwa,  siku hiyo hiyo washtakiwa wakiwa katika bahari ya Hindi eneo la Fungu Baraka Kigamboni jijini Dar es Salaam walikutwa wakitumia vifaa vya kuvulia vilivyokatazwa ambavyo ni mitungi ya gesi 28, leguleta sita, pea tatu za viatu vya kuvulia samaki pamoja vifaa 13 vya kuvulia samaki (mask to capture fish). 

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama.  Ambapo wametakiwa kila mmoja kuwa mdhamini mmoja wenye barua ya utambulisho ya serikali za mitaa,  vitambulisho na Pia wametakiwa kusaini bondi ya Sh. Milioni 10 kila mmoja.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi Februari 18, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. 

RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE ATEMBELEA KIWANDA KINACHOSHONA MASHATI YAKE

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii 

Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania.

Akizungumza na Michuzi TV, Dkt. Kiwete amesema kuwa Binti Afrika imemshonea nguo muda mrefu kwa ubunifu wa hali juu, amepongeza kwa kuwa nguo hizo za aina ya Batiki zina viwango vya ubora zinazoweza kuuzika kokote duniani.


Dkt. Kikwete amepongeza Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Johari Sadiq licha ya mchango kutoka kwa Mama yake mzazi, kwa kujituma na ubunifu huo ambapo unaweza kutengeza mazingira yoyote kujipatia kipato. "Watu wakumbuke Wabunifu wapo hapa nchini, wasifikirie vitu vya nje peke yake hapa ndani (Tanzania) wanaweza kupata vitu vyenye ubora wa hali ya juu",amesema Dkt. Kikwete.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji Nguo, Johari Sadiq amesema wamepata heshima kubwa kupata ugeni wa Dkt. Kikwete katika Kiwanda hiko amesema hatua hiyo imetokana na ubora na ubunifu walionao hivyo imepelekea kuwa mteja wao muda mrefu. 


"Dkt. Kikwete amekuwa mteja wetu toka alipokuwa Rais wa nchi hii, tumeanza kuvalisha nguo zetu toka mwaka 2013, alinikuta kwenye Maonyesho nikiwa na bidhaa zangu akazipenda ubora wake, akajaribu kwa kuagiza Shati mbili", amesema Johari


Johari amesema kuwa amekuwa akijifunza muda mrefu kwa watu wengine ambapo wamefanya kazi hiyo ya ubunifu kwa muda mrefu.Ametoa wito kwa Wabunifu kutofautisha ubunifu wa majukwaani na uzalishaji nguo kuweka msingi wa uzalishaji wakuvaa nguo za kila siku, ametoa wito kwa Wabunifu kujikita zaidi kwenye uzalishaji zaidi wa nguo. Amesema miaka mitano anataka kuwa na 'Brand' ambayo itatambulika zaidi nchini kwa kuvalisha viongozi na watu wakawaida. 

 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya  kutembelea Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania, leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia nguo zinazo tengenezwa na  Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania. kulia ni MKurungezi wa kiwanda hicho, Johari Amour Sadiq.
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia mashine mbalimbali  katika Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa ambacho kimemshonea Nguo zake tangu alipokuwa Rais wa Tanzania, leo jijini Dar es Salaam.
Mafundi wa  Kiwanda cha Ubunifu wa Nguo cha Binti Africa wakiendelea na kazi.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa kiwanda  cha nguo cha Binti Africa leo jijini Dar es Salaam.

WABUNGE WA EALA WATOA ELIMU YA MTANGAMANO WA EAC

$
0
0
Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuwaeleza zoezi walilopanga la kuelimisha wadau kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya AAfrika Mashariki.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Abdallah Makame na Katibu wake, Mhe. Josephene Sabastian wakiwa katika kikao na Wbunge wenzzao wa Tanzania, maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bunge la EALA na Trade Mark East Africa katika Hoteli ya Serena. Mkutano huo ni maandalizi ya zoezi la siku nne la kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu fursa za Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuanzaia tarehe 04 hadi 07 Februari 2019 jijini Dar Es Salaam. 
Mhe. Habib Mnyaa, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Marym Ussi wakishiriki kikoa cha maandalizi ya zoezi la kutoa elimu kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Mhe. Pamela Maasay (kulia) na Mhe. Happiness Legiko wakifjiandaa kukutana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu ya Mtangamano. 
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao Wizara yao ndio mratibu w mauala ya Mtangamano wakiwa katika kikao cha maandalizi cha kutoa elimu ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Maafisa kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika kikao cha maandalizi ya zoezi la kutoa elimu kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Mhe. Dkt. Abdallah Makame akitoa maelekezo kwa Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa dawati la Bunge. 
Kikao kinaendelea Mkutano wa Waandishi wa Habari 
Waandishi wamefurika kusikiliza Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu zoezi la kuelimisha wadau kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Waheshimiw wabunge (kushoto) na wandihi w habari wkiendelea na mkutano wao. 
Bandari ya Dar Es Salam 
Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar Es Salaam akiwakaribisha Wabunge wa EALA katika Bandari ya Dar Es Salaam. Waheshimiwa Wabunge walienda Bandari ya Dar Es Salaam kuona maboresho yanayofanywa na bandari hiyo pamoja na kusikiliza wadau wanotumia bandari hiyo changamoto wanaokutana nazo. 
Waheshimiwa Wabunge walienda kutembelea gati namba moja ambalo ni moja ya mageti ynayofnyiwa maboresho makubwa. 
Mheshimiwa Maryam akisherehekea Siku yake ya kuzaliwa tarehe 04 Februari kwa kuwalisha keki Wabunge wenzake. 
Happy Birthday kwa Mhe. Maryam Ussi kutoka kwa Mhe. Fancy Nkuhi. 

ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI

$
0
0
Serikali imetoa kiasi cha shilingi 5,558,604,325.95 kwa ajili ya kugharamia elimu bila malipo kwa Wilaya ya Hai kuanzia Desemba 2015 ambapo kati ya fedha hizo shilingi 1,633,980,574.16zimetumika kugharamia elimu bila malipo kwa shule za msingi na 3,924,623,751.79 kwa ajili ya kugharamia elimu bila malipo kwa kidato cha kwanza hadi cha nne.

Hali hiyo imesababisha ongezeko la uandikishaji wanafunzi ngazi ya awali kutoka 3,843 mwaka 2015 hadi kufikia 4,127 mwaka 2018 na msingi kutoka 4,201 mwaka 2015hadi kufikia 4,758 mwaka 2018.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa miaka mitatu katika wilaya ya Hai, Mkuu wa Wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya amesema sera ya elimu bila malipo kwa watoto wenye umri kwenda shule imefanya watoto wengi kutoka kwenye familia duni kupata fursa hiyo muhimu kwa ajili ya maendelo ya taifa.

Alisema serikali imeendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ufuatiliaji wa shule ambapo kwa mwaka 2018 Wilaya ilikabidhiwa pikipiki 17 kwa ajili wa waratibu elimu kata ikiwa ni sambamba na uboreshaji wa miundo mbinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba 35madarasa ya elimu msingi, matundu 120 ya vyoo.

Aliongeza kuwa Wilaya imepokea walimu 22 wa masomo ya sayansi na kuongeza idadi ya walimu kutoka 118 hadi walimu 140 katika juhudi za kuimarisha masomo ya sayansi shuleni.

“Kutokana na juhudi za serikali kuboresha sekta ya elimu pamoja na usimamizi na ufuatiliaji unaofanywa na viongozi wa ngazi zote, Wilaya ya Hai ilishika nafasi ya pili kimkoa na nafasi ya nane kitaifa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana” Alisisitiza Sabaya.

Mbali na elimu; Sabaya alisema pia serikali imeendela kutoa fedha kupitia mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) katika mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo hadi Desemba 2018 jumla ya shilingi 3,049,467,299.98 zimetolewa kwa kaya 3,890 walizotumia kuanzisha miradi midogomidogo inayowapatia kipato ikiwemo kufuga kuku, kilimo cha bustani za mbogamboga na biashara mbalimbali.

Akizungumzia sekta ya Afya; Dc Sabaya alisema kiasi cha shilingi 1,496,355,495.00 zimetumika kununua dawa na kufanya kiwango cha upatikanaji wa dawa kufikia asilimia 90.57 ukilinganisha na asilimia 73.59 ya mwaka 2014.

“Tunaendelea kuboresha sekta hii muhimu na tumejenga duka la dawa linalotoa huduma kwa gharama nafuu saa 24 kwa wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali nadni na nje ya wilaya” alisema.

“Tumekamilisha wodi ya wanawake katika hospitali ya wilaya, kukamilika kwa miundo mbinu hii muhimu kumewapunguzia wananchi adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma na kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wanalazimika kwenda Hospitali ya Mkoa Mawenzi’alisisitiza Sabaya.

Katika kuboresha sekta ya umwagiliaji; serikali kwa kipindi hicho imetoa shilingi 844,000,000 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa mifereji 3 ya umwagiliaji ili kuongeza eneo la umwagiliaji kwa lengo la kuimarisha uzalishaji.

Aidha wilaya ya Hai imeanzisha kilimo cha mazao mawili ya biashara ambayo ni Korosho na vanilla kwa lengo la kuinua uchumi wa mkulima.

Akizungumia huduma ya maji Sabaya alisema serikali imetoa kiasi cha shilingi 4,062,951,699.35 kuimarisha usambazaji wa maji ambazo zimetumika kufanya ujenzi na upanuzi wa mradi wa maji wa Losaa-Kia, kujenga vituo 58 vya kutolea huduma kwenye vijiji 10 vya Mkalama, Mijongweni, Ngosero, Mbatakero, Mungushi, Kimashuku, Sanya Station, Tindigani, Mtakuja na Chemka.

Naye mgeni wa heshima Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndugu Kheri James alipongeza ushirikiano ulipo kati ya viongozi wa Wilaya ya Hai na kutaka hali hiyo iendelezwe.
Kheri alisema kuwa juhudi zilizoonyeshwa na waatalamu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya na Kamati ya ulinzi na usalama imeifanya Wilaya kuwa ya kwanza Kimkoa na ya kumi kitaifa katika ukusanyaji wa mapato na kwamba hali hiyo itaboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,  Ndugu Kheri James  akinyoosha juu ngao aliyokabidhiwa na wananchi wa Wilaya ya Hai kumpelekea Mhe. RAis wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya .

 Aliyekuwa mhandisi wa Ujenzi, Msangi akibadhiwa zawadi kutokana na usimamizi bora ya miradi ya ujenzi

 Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa mgeni wa heshma kutokana na usimamizi na ufuatiliaji bora uliofanya wilaya kushika nafasi ya kumi kitaifa.
  Viongozi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,  Ndugu Kheri James  (hayupo pichani). Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Kumotola Kumotola; Mbunge wa Jimbo la Siha Mhe. Godwin Mollel; Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mhe. Lengai Ole Sabaya  na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hai Mhe. Wang’uba Maganda.

CCM PWANI YAPOKEA WANACHAMA WAPYA 250 MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 42

$
0
0
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) MKOA WA Pwani Kimepokea Wanachama 250 kutoka vyama vya upinzani katika maadhimisho ya sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga.

 Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo pamoja na kuwapokea wanachama hao wapya Mwenyekiti wa CCM MKOA Wa Pwani Ramadhani Maneno amewapongeza na kuwakaribisha wanachama hao wapya kuwa CCM ni chama bora nchini hivyo hawakukosea kufanya maamuzi ya kujiunga na chama hicho.

Waziri wa Tamisemi na Mbunge wa Kisarawe,Mh.Suleiman Jafo akizungumza na wananchi wa mkoa wa Pwani kuhusu changamoto zote zinazohusiana na wizara yake yeye akishirikiana na Naibu Waziri Wake Mwita Waitara watahakikisha wanatatua matatizo yote na kuwaomba watanzania wawaombee wao na Rais Magufuli Wawe na Afya njema watekeleze majukumu yao kwa asilimia 100%. 

"Ndugu zangu wanaccm wapya nawapongeza kwa kujiunga na chama dume chama tawala cha CCM na tena msijutie kujiunga na chama hiki kwa kuwa tunaye Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa na Rais wa Jamburi ya Muungano wa Tanzania,Cde Dk.John Magufuli ambaye tangu aliposhika hatamu mambo mengi mazuri ameyafanya tena yanaonekana hivyo karibuni tuijenge Pwani yetu" Alisema Mwenyekiti Maneno.

 Pia Mwenyekiti Maneno Amewataka Wanachama wote wa chama hicho kuacha tabia ya kujipitisha pitisha kutaka nafasi ya udiwani na ubunge na kuwataka mara moja kuacha tabia hiyo mara moja na kuwasisistiza muda wa wao kutembea kwa wanananchi na wanachama kujinadi bado akasema kwa mwanachama yeyote wa CCM anayejipitisha na kujinadi kutaka nafasi yeyote kati ya hizo alizozisema anafanya makosa na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake.

 Naye Naibu Waziri wa Nishati Subirá Mgalu amesema kuwa Serikali ya Dk. John Magufuli kupitia wizara yake inahakikisha inasambaza umeme nchi nzima katika mkoa wa Pwani mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme stigle gorge umezinduliwa utakapokamilika pale Rufiji utafanikisha maeneo mengi nchini kuwa na umeme wa uhakika. 

Hata Hivyo Waziri wa Tamisemi na Mbunge wa Kisarawe,Mh.Suleiman Jafo amewahakikishia wanapwani na nchi kwa ujumla kuhusu changamoto zote zinazohusiana na wizara yake yeye akishirikiana na Naibu Waziri Wake Mwita Waitara watahakikisha wanatatua matatizo yote na kuwaomba watanzania wawaombee wao na Rais Magufuli Wawe na Afya njema watekeleze majukumu yao kwa asilimia 100%. 

Akizungumza wakati akisoma risala ya wilaya ya Mkuranga Katibu wa CCM wilaya hiyo,Hakimu Jackson alisema kuwa kutokana na utaratibu wa kila wilaya,kata na matawi kuwa na vitega uchumi ili chama kiondokane na mfumo wa kuombaomba amemshukuru mbunge wa jimbo lá Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega na família yake kwa kuisaidia chama wilaya kwa kujenga vibanda vya fremu 11,ukuta na ukumbi wa kisasa ambao utaiwezesha chama kuongeza mapato yake. 

"Ndugu Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno vibanda hivi vyote,fremu 11 na uzio hivi vyote kwa pamoja vimejengwa kwa thamani ya Sh. Milioni 34,686,500 kwa fedha yake Mwenyewe mh.Mbunge Ulega bila kusaidiwa na mtu yeyote" Alisema Katibu Jackson Aidha Katibu Jackson aliongeza kwa kusema kuwa pamoja na kujenga ukuta na vibanda vya fremu pia mh.Ulega anaendelea na ujenzi wa ujenzi wa ofisi za kata 19 Kátia ya kata 25 ambapo ametumia Sh.Milioni 20,930,000 ukijumlisha fedha alizotoa kata na wilaya jumla ni Sh.Milioni 55,616,500 kitendo hiki anachokifanya mbunge ulega kinapaswa kuigwa na wabunge wengine wa CCM nchi nzima.

Kwaupande wake mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni naibu waziri wa Mifugo na uvuvi Abdalah Ulega ambaye amechangia gharama za ujenzi wa ukuta na fremu katika jengo la ccm amesema ujenzi huo utasaidia kukuinua chama hicho kiuchumi.Ulega amesema jengo hilo lililogharimu zaidi ya milion hamsini,amelijenga kwa mapenzi yake na chama cha Mapinduzi CCM.

Hata hivyo amewashukuru viongozi wote wa wilaya ya Mkuranga akiwemo Mkurungenzi wa halmashauri na diwani wa Mkuranga kwa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha ujenzi huyo.Sherehe za kumbuku za kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi kutimiza miaka 42 kwa mkoa wa Pwani,imebeba kaulimbiu isemayo kazi ni kipimo cha utu, kazi,tulinde uhuru wetu.nae,Ahmed Salum kada wa chama cha Mapinduzi amempongeza mbunge kwa jitihada kubwa anzozifanya za kuendelea ilani ya chama hicho ameahidi kumuunga mukono katika miladi mbalimbali ya unjezi wa ofisi za chama. Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Pwani,Ramadhani Maneno akiwahutubia wakazi wa Pwani na vitongoji vyake ndani ya uwanja wa (CCM) Mkuranga,wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani, ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga. Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi Mbalimbali wa Kitaifa. Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Pwani,Ramadhani Maneno akiwaongoza wakazi wa mkoa Pwani kufyeka majani eneo la Hospital ya wilaya ya Mkuranga wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga. Semu ya viongozi mbalimbai wakiwa meza kuu. Sehemu ya wananchi walio hudhuria wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga. (Picha zote na Emmanuel Massaka,MMG) Naibu Waziri wa Nishati Subirá Mgalu akizungumza na wananchi wa mkoa Pwani kuhusu mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme Stigle Gorge utakapokamilika utanufaisha maeneo mengi nchini kuwa na umeme wa uhakika. Ahmed salum kada wa chama cha Mapinduzi akimpongeza mbunge kwa jitihada kubwa anzozifanya za kuendelezaa Ilani ya chama hicho,aidha ameahidi kumuunga mkono katika miradi mbalimbali ya ujezi wa ofisi za chama. Maandamano yakiendelea sambamba na ubebaji wa mabango yenye Ujumbe wa mbalimbali.(Picha zote na Emmanuel Massaka,MMG)Sehemu ya wananchi walio hudhuria wakati wa sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Kwa Mkoa wa Pwani ambapo shughuli hiyo kimkoa imefanyika wilayani Mkuranga. Semu ya viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu.


CHANJO YA MLANGO WA KIZAZI HAIHUSIANI NA UZAZI WA MPANGO

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika siku ya Saratani Duniani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma, 
Mkurugenzi wa Ubora ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Mohammed akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe leo katika tamko la siku ya Saratani Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Ubora kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Mohammed ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya. 
Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati akitoa tamko la siku ya Saratani Duniani, leo jijini Dodoma 
Mkurugenzi wa Ubora kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Mohammed. ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya leo katika tamko la siku ya Saratani Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………………. 

Na WAMJW – DOM 

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amewatoa hofu Wananchi kwa kusisitiza kuwa chanjo ya kuwakinga wasichana na Saratani ya Mlango wa kizazi haihusiani na uzazi wa mpango wala kumzuia msichana kuja kupata uja uzito baadae. 

Ameyasema hayo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika siku ya Saratani Duniani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “NITAFANYA JITIHADA ZOTE KUPUNGUZA JANGA LA SARATANI DUNIANI”. 

Waziri Ummy amesema kuwa Chanjo ya Mlango wa kizazi ni salama na imethibitishwa na Shirima la Afya Duniani kwaajili yakuwakinga Wasichana dhidi ya maambulizi ya Saratani ya Mlango wa kizazi. 

” Chanjo ya kuwakinga wasichana na saratani ya mlango wa kizazi haihusiani na uzazi wa mpango, ni chanjo ambayo imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani kwaajili yakuwakinga wasichana dhidi ya maambukizi ya Saratani ya mlango wa Kizazi” Alisema Waziri Ummy 

Waziri Ummy amesema kuwa katika kila wagonjwa wa Saratani 100, takribani wagonjwa 31 ni wanawake wa Saratani ya Mlango wa kizazi, hivyo amewahasa wazazi na walezi nchini kuhakikisha wasichana wanaostahili kupata chanjo hii, wanaipata bila vikwazo vyovyote ili kutokomeza kabisa Saratani hii nchini. 

“Katika kila wagonjwa wa Saratani 100, Wagonjwa takribani 31 ni wanawake wa Saratani hii ya Mlango wa kizazi, kwahiyo hatuna haja ya kuiogopa chanjo hii kwasababu ndio itayowakinga watoto wetu na maambukizi ya Saratani ya mlango wa kizazi” alisema Waziri Ummy. 

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Tafiti za Saratani (IARC), zinaonyesha kwamba kwa Tanzania kunatokea mgonjwa 1 wa Saratani kwa kila watu 1000, hivyo Tanzania inakua na wagonjwa wapya wa Saratani 55,000 kwa mwaka na takribani wagonjwa 28,610 hufariki kwa mwaka, ambapo ni vifo asilimia 52 ya wagonjwa wapya. 

Aliendelea kusema kuwa Taarifa kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonesha kwamba kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa Saratani mwaka hadi mwaka, huku akisema kuwa Mwaka 2015 wagonjwa wapya 5,764, huku mwaka 2016 wagonjwa wapya 6,338, na mwaka 2017 wagonjwa wapya 7,091, pia mwaka 2018 wagonjwa wapya 7,649. 

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amedai kuwa Serikali imeanzisha huduma kwenye vituo 624 vilivyopo katika Halmashauri mbalimbali nchini ambapo jumla ya wanawake 375,522 walifanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti mnamo mwaka 2017, ukilinganisha na wanawake 416,841 waliofanyiwa uchunguzi huo mwaka 2018. Kati ya hao, wanawake 16,147 waligundulika kuwa na mabadiliko ya awali mwaka 2017, na wanawake 18,341 mwaka 2018.

JOINT COMMUNIQUÉ: 20TH ORDINARY SUMMIT OF HEADS OF STATE OF EAC

$
0
0


EAST AFRICAN COMMUNITY




COMMUNIQUÉ OF THE
20TH ORDINARY SUMMIT OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY HEADS OF STATE

 ENHANCING THE ECONOMIC, SOCIAL AND POLITICAL INTEGRATION OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY


ARUSHA INTERNATIONAL CONFERENCE CENTRE (AICC), ARUSHA, TANZANIA

1ST FEBRUARY, 2019




EAC SECRETARIAT
ARUSHA, TANZANIA
FEBRUARY 2019






JOINT COMMUNIQUÉ


  1. THE EAST AFRICAN COMMUNITY HEADS OF STATE, THEIR EXCELLENCIES PRESIDENT YOWERI KAGUTA MUSEVENI OF THE REPUBLIC OF UGANDA; PRESIDENT PAUL KAGAME OF THE REPUBLIC OF RWANDA; PRESIDENT UHURU KENYATTA OF THE REPUBLIC OF KENYA; PRESIDENT DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA; H. E. GASTON SINDIMWO, 1ST VICE PRESIDENT, REPRESENTING PRESIDENT PIERRE NKURUNZIZA OF THE REPUBLIC OF BURUNDI; AND HON. PAUL MOYOM AKEC, MINISTER OF TRADE, INDUSTRY AND EAC AFFAIRS REPRESENTING PRESIDENT SALVA KIIR MAYARDIT OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN; HELD THE 20TH ORDINARY SUMMIT OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY HEADS OF STATE AT THE ARUSHA INTERNATIONAL CONFERENCE CENTRE, IN THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, ON 1ST FEBRUARY, 2019. THE HEADS OF STATE MET IN A WARM AND CORDIAL ATMOSPHERE.

  1. THE SUMMIT RECEIVED THE REPORT OF THE COUNCIL OF MINISTERS COVERING THE PERIOD 23RD FEBRUARY, 2018 TO 31ST JANUARY, 2019 AND COMMENDED THE COUNCIL FOR THE PROGRESS MADE IN THE IMPLEMENTATION OF THE PROGRAMMES AND PROJECTS OF THE COMMUNITY.

  1. THE SUMMIT CONSIDERED A REPORT OF THE COUNCIL ON THE IMPLEMENTATION OF THE PREVIOUS DIRECTIVES AND DECISIONS OF THE SUMMIT AND DIRECTED THE COUNCIL TO IMPLEMENT ALL OUTSTANDING DIRECTIVES AND DECISIONS AND REPORT TO THE 21ST SUMMIT.

  1. THE SUMMIT RECEIVED A REPORT ON THE STATUS OF RATIFICATION OF PROTOCOLS AND DIRECTED PARTNER STATES TO RATIFY ALL OUTSTANDING PROTOCOLS AND THE COUNCIL TO REPORT TO THE 21ST SUMMIT.

  1. THE SUMMIT NOTED THE STATUS OF RESOLUTION OF LONG OUTSTANDING NON-TARIFF BARRIERS AND DIRECTED PARTNER STATES AND THE COUNCIL TO RESOLVE THEM.

  1. THE SUMMIT RECEIVED A REPORT OF THE COUNCIL THAT ALL PARTNER STATES HAD NOMINATED CONSTITUTIONAL EXPERTS TO WORK ON THE CONSTITUTION OF THE POLITICAL CONFEDERATION. THE SUMMIT DIRECTED THE COUNCIL TO CAUSE THE EXPERTS TO PROVIDE A PRELIMINARY REPORT WITHIN SEVEN MONTHS.  THE SUMMIT DECIDED THAT PRESIDENT YOWERI KAGUTA MUSEVENI SHALL PROVIDE POLITICAL GUIDANCE TO THE EXERCISE.

  1. THE SUMMIT RECEIVED A PROGRESS REPORT ON THE REVIEW OF THE EAST AFRICAN DEVELOPMENT BANK (EADB) CHARTER TO STREAMLINE IT INTO THE EAC MAINSTREAM. THE SUMMIT DIRECTED THE COUNCIL OF MINISTERS TO EXPEDITE THE PROCESS.

  1. THE SUMMIT CONSIDERED A REPORT ON THE ROADMAP FOR THE ACCELERATED INTEGRATION OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN INTO THE EAC AND DIRECTED THE COUNCIL TO CONCLUDE THE PROCESS.

  1. THE SUMMIT RECEIVED A PROGRESS REPORT THAT THE VERIFICATION EXERCISE FOR THE ADMISSION OF THE FEDERAL REPUBLIC OF SOMALIA INTO THE EAST AFRICAN COMMUNITY HAD NOT BEEN UNDERTAKEN. THE SUMMIT DIRECTED THE COUNCIL TO FOLLOW UP ON THE MATTER AND REPORT TO THE 21ST SUMMIT.

  1. THE SUMMIT CONSIDERED A REPORT ON THE MODALITIES FOR THE PROMOTION OF MOTOR VEHICLE ASSEMBLY IN THE REGION AIMED AT REDUCING THE IMPORTATION OF USED MOTOR VEHICLES FROM OUTSIDE THE COMMUNITY, AND DIRECTED THE COUNCIL TO FOLLOW UP THE MATTER AND REPORT TO THE 21ST SUMMIT.


  1. THE SUMMIT RECEIVED A REPORT ON THE REVIEW OF THE TEXTILE AND LEATHER SECTOR IN EAST AFRICA WITH A VIEW TO DEVELOPING A STRONG AND COMPETITIVE SECTOR THAT GIVES CONSUMERS BETTER CHOICES THAN IMPORTED TEXTILES AND FOOTWEAR. THE SUMMIT DIRECTED THE COUNCIL TO CONCLUDE THE MATTER AND REPORT TO THE 21ST SUMMIT.

  1. THE SUMMIT RECALLED ITS DIRECTIVE OF HAVING TWO DEPUTY SECRETARIES GENERAL AT THE EAST AFRICAN COMMUNITY RECRUITED COMPETITIVELY ON A ROTATIONAL BASIS AND DECIDED THAT THE DEPUTY SECRETARY GENERAL FROM THE UNITED REPUPLIC OF TANZANIA AND THE DEPUTY SECRETARY GENERAL FROM THE REPUBLIC OF RWANDA SHALL SERVE THEIR RESPECTIVE TWO TERMS IN OFFICE.

  1. THE SUMMIT RECEIVED A PROGRESS REPORT FROM  H.E. PRESIDENT YOWERI KAGUTA MUSEVENI, ON THE EU-EAC ECONOMIC PARTNERSHIP AGREEMENT (EPA) AND DECIDED THAT THE EAC ENGAGES THE EU ON THE MATTER IN THE NEXT FOUR MONTHS TO GET MORE CLARIFICATION ON THE PERTINENT ISSUES OF CONCERN.  THEREAFTER, PARTNER STATES WHO WISH TO, MAY OR MAY NOT SIGN THE EPA.

  1. THE SUMMIT ASSENTED TO THE EAC OATHS BILL, 2018; THE EAC MONETARY INSTITUTE BILL, 2018; AND THE EAC SUPPLEMENTARY APPROPRIATION BILL, 2018.

  1. THE SUMMIT RECEIVED A REPORT ON THE FINANCIAL STATUS OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY AND DIRECTED PARTNER STATES TO FULFILL THEIR FINANCIAL OBLIGATIONS TO THE COMMUNITY IN A TIMELY MANNER.

  1. THE SUMMIT ENDORSED THE REPUBLIC OF KENYA’S CANDIDATURE FOR THE NON-PERMANENT MEMBERSHIP OF THE UNITED NATIONS SECURITY COUNCIL (UNSC) FOR A TWO-YEAR TERM FOR THE PERIOD 2021-2022.

  1. THE SUMMIT, PURSUANT TO ARTICLE 24 (1) OF THE TREATY FOR THE ESTABLISHMENT OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY, APPOINTED HON. LADY JUSTICE SAUDA MJASIRI AS JUDGE TO THE APPELLATE DIVISION OF THE EAST AFRICAN COURT OF JUSTICE WITH EFFECT FROM 13TH FEBRUARY, 2019. THE HONOURABLE LADY JUSTICE SAUDA MJASIRI REPLACES HON. JUSTICE EDWARD M. K. RUTAKANGWA WHO WILL BE RETIRING ON 12TH FEBRUARY, 2019. THE SUMMIT COMMENDED HON. JUSTICE EDWARD M. K. RUTAKANGWA FOR HIS DEDICATED SERVICE TO THE COMMUNITY.

  1. THE SUMMIT PRESENTED AWARDS TO THE WINNERS OF THE EAC STUDENTS ESSAY WRITING COMPETITION, 2017 AND 2018 EDITIONS RESPECTIVELY.


  1. THE SUMMIT DIRECTED THE COUNCIL WITHIN THREE MONTHS TO REVIEW THE RELEVANT POLICIES AND HARMONISE THE FRAMEWORK FOR IMPORTATION OF GOODS INTO THE EAC WITH A VIEW TO SUPPORTING THE GROWTH OF LOCAL INDUSTRIES.

  1. HIS EXCELLENCY PRESIDENT YOWERI KAGUTA MUSEVENI HANDED OVER THE CHAIRMANSHIP TO HIS EXCELLENCY PRESIDENT PAUL KAGAME.  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA TOOK OVER AS RAPPORTEUR FROM THE REPUBLIC OF RWANDA. THE SUMMIT THANKED HIS EXCELLENCY PRESIDENT YOWERI KAGUTA MUSEVENI FOR ABLY STEERING THE AFFAIRS OF THE COMMUNITY DURING HIS TENURE.

  1. THE SUMMIT RECEIVED A REPORT FROM THE FACILITATOR OF THE INTER-BURUNDI DIALOGUE HIS EXCELLENCY BENJAMIN MKAPA, FORMER PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA.  THE SUMMIT THANKED THE FACILITATOR FOR HIS CONTRIBUTION TO THE DIALOGUE DURING HIS TENURE. THE SUMMIT DECIDED TO CONSULT FURTHER ON THE INTER-BURUNDI DIALOGUE PROCESS.

  1. THEIR EXCELLENCIES PRESIDENT YOWERI KAGUTA MUSEVENI OF THE REPUBLIC OF UGANDA; PRESIDENT PAUL KAGAME OF THE REPUBLIC OF RWANDA, PRESIDENT UHURU KENYATTA OF THE REPUBLIC OF KENYA; H. E. GASTON SINDIMWO 1ST VICE PRESIDENT REPRESENTING PRESIDENT PIERRE NKURUNZIZA OF THE REPUBLIC OF BURUNDI AND; HON. PAUL MOYOM AKEC MINISTER OF TRADE, INDUSTRY AND EAC AFFAIRS REPRESENTING PRESIDENT SALVA KIIR MAYARDIT OF THE REPUBLIC OF SOUTH, THANKED THEIR HOST, PRESIDENT DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, FOR THE WARM HOSPITALITY EXTENDED TO THEM AND THEIR DELEGATIONS DURING THEIR STAY IN ARUSHA.
  2. DONE AT ARUSHA, THIS 1ST DAY OF FEBRUARY, 2019.
 (L-R)AMB. LIBERAT MFUMUKEKO,THE EAC SECRETARY GENERAL HON. PAUL MOYOM AKEC, MINISTER OF TRADE, INDUSTRY AND EAC AFFAIRS REPRESENTING PRESIDENT SALVA KIIR MAYARDIT OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN; PRESIDENT UHURU KENYATTA OF THE REPUBLIC OF KENYA;PRESIDENT YOWERI KAGUTA MUSEVENI OF THE REPUBLIC OF UGANDA; PRESIDENT PAUL KAGAME OF THE REPUBLIC OF RWANDA; PRESIDENT DR. JOHN    POMBE JOSEPH MAGUFULI OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA; GASTON SINDIMWO, 1ST VICE PRESIDENT, REPRESENTING PRESIDENT PIERRE NKURUNZIZA OF THE REPUBLIC OF BURUNDI AND RT HON KIRUNDA KIVEJINJA, CHAIR, EAC COUNCIL OF MINISTERS
  PRESIDENT PAUL KAGAME OF THE REPUBLIC OF RWANDA AND THE NEW CHAIR OF THE EAC SUMMIT MAKES HIS OPENING STATEMENT
 PRESIDENT DR. JOHN    POMBE JOSEPH MAGUFULI OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA (R)CONGRATULATES PRESIDENT PAUL KAGAME OF THE REPUBLIC OF RWANDA BEING A NEW CHAIR OF THE EAC SUMMIT



WAZIRI MKUU AKITETA JAMBO NA SPIKA BUNGENI LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai Katika Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma leo Februari 4, 2019. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU .

VOA SWAHILI: Duniani Leo February 4th, 2019

Habari za UN kutoka New York, Marekani leo Februari 4, 2019

HYATT HOTEL’S LUXURY SKY BAR CELEBRATES AUSTRALIA DAY WITH AUSTRALIA’S FAVOURITE SPREADS

$
0
0
General Manager of Hyatt Regency Dar es Salaam Mr. Garry Friend awarding one of the invited guests on Australian National Day at Hyatt Which also they went to Zanzibar ( Mazizini Orphanage Centre) and helped on fundraising some amount to orphanage.

…………………………………………………………………..

Hyatt Regency Dar es Salaam has today unveiled the national pride of Australia to the Tanzanian community at the hotel’s luxury rooftop.

Across the nation and around the world on Australia day, citizens reflect on what it means to be Australian and recall the birth of a new nation, marked in history with the arrival of the first British ships and the raising of the flag of Great Britain at Sydney Cove.

“We are pleased to fly the national flag in the most prominent place in the city, which offers the best music entertainment, food and drinks for local Tanzanians and the Australian community to enjoy together,” said Mr. Garry Friend, General Manager of Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.

“We are here to create a truly memorable experience, and we plan to hold different events every year to help make a difference in society. Today we will raise some money and offer tickets to Zanzibar as a prize, as a means of helping orphanage centers in Zanzibar.” He added

About Hyatt Regency.

The Hyatt Regency brand prides itself on connecting travellers to who and what matters most to them. More than 160 conveniently located Hyatt Regency urban and resort locations in over 30 countries around the world serve as the go-to gathering space for every occasion – from efficient business meetings to memorable

Family vacations. The brand offers a one-stop experience that puts everything guests need right at their fingertips. Hyatt Regency hotels and resorts offer a full range of services and amenities, including the space to work, engage or relax, notable culinary experiences, technology-enabled ways to collaborate and expert event planners that can take care of every detail.

WATUMISHI 6 WASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA YA UBADHIRIFU WA FEDHA ARUSHA

$
0
0
 
Waziri wa Elimu sayansi mafunzo na ufundi profesa Joyce ndalichako


Na. Vero Ignatus Arusha

Waziri wa Elimu sayansi mafunzo na ufundi profesa Joyce ndalichako amewasimamisha kazi watumishi sita wa chuo cha ualimu Patandi kwa tuhuma ya ubadhirifu wa fedha

Profesa Ndalichako amesema kuwa zaidi ya shilingi milioni 2.5 zilizotengwa na serikali kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya chuo hicho imetumika visivyo.Waliosimamishwa kazi ni pamoja Israel Mayage kutoka chuo kikuu cha sayansi na teknonojia mbeya ambae awali alikuwa msimamizi wa mradi shule hiyo, mhasulibu Rose Kijaka na mwenyekiti wa kamati ya mapokezi Peter Mosha

Wengine ni kaimu chuo cha Patandi Isaac myovela, Ofisa manunuzi na ugavi Charles Njarabi na Hendry Malei ambaye alihamishiwa chuo cha Monduli, pia ameagiza mkuu chuo cha Patandi Janesi Mmbaje abadilishiwe majukumu kwasababu za kiafya

Waziri Ndalichako amechukua hatua hiyo mara baada ya kutembelea shuleni hapo kukagua mradi wa majengo licha ya taarifa kuonyesha umechelewa kukamilika bila Sababu ya msingi huku.thamani ya fedha inapingana na hali halisi na pia ubora wake.Amemuagiza Katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo Kupeleka watendaji wengine wakati uchunguzi ukiendelea kufanyika naendapo ikithibitika sheria itachukua mkondo wake

Mimi ninachotaka kujua hayo malori 170 yalimwagwa wapi na hiyo mifuko ya saruji 6520 ipo wapi na hadi sasa imetumikaje. Aliuliza profesa NdalichakoAmesema katika ziara yake amebaini fedha zilizotumika katika ujenzi huo ni shilingi milioni 990 ambapo amesisitiza kuwa fedha hiyo ni nyingi kuliko hali halisi ya ujenzi

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewataka wale wote waliopo kwenye kamati ya ujenzi ukiondoa wale ambao wameondolewa wanakutana leo kupitia mambo yote yaliyosalia ili waweze kuwapokea wanafunzi tarehe 7 feb 2019 
.
Shule ya sekondari ni Patandi ni ya wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali nchi nzima ikimalizika itachukua watoto 640 na itakuwa na vifaa vya kisasa ambavyo watavitumia kwaajili ya kujifunzia

INTRODUCING: Ommy Dimpoz - Ni Wewe (Official Music Video)

MAGAZETI YA LEO JUMANNE ,FEBRUARI 5 2019.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA GEREZA KUU LA WANAWAKE TANZANIA - KINGOLWIRA, MOROGORO

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania - Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe alipotembelea alipotembelea Gereza hilo jana februari 4, 2019 katika ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro.
. Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe akitoa taarifa fupi ya uendeshaji wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania – Kingolwira kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto meza kuu) jana februari 4, 2019 alipotembelea Gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akikagua maeneo mbalimbali ya Gereza Kuu la Wananwake(kulia) ni Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe. Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Udereva cha Magereza – Kingolwira, ACP. Lazaro Nyanga.
Askari wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira wakiwa timamu kazini wakati Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani) akizungumza na Wafungwa wa Gereza hilo jana februari 4, 2019 alipotembelea Gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akiangalia mradi wa kuku wa mayai katika Gereza Kuu la Wanawake Tanzania – Kingolwira alipotembelea jana februari 4, 2019.
Ujenzi wa nyumba kwa njia ya ubunifu katika Kambi mojawapo ya Gereza Mtego wa Simba, Morogoro ukiendelea katika hatua awali za ujenzi.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiangalia mashine kufunga majani ya malisho ya mifugo katika mradi wa ng’ombe wa maziwa Gereza Mtego wa Simba
Mkuu wa Chuo cha Udereva cha Magereza – Kingolwira, ACP. Lazaro Nyanga akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) kukagua majenego mbalimbali yanayokarabatiwa katika chuo hicho kwa kutumia ubunifu(Picha na Jeshi la Magereza).

MAHAKAMA YAANZISHA MPANGO WA KUWALEA WANAFUNZI KIMAADILI

$
0
0

Wanafunzi wa vyuo na shule za sekondari wakiwa tayari kuzungumza na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Latifa Mansoor leo Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma
Wanafunzi wa vyuo na shule za sekondari wakiwa tayari kuzungumza na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Latifa Mansoor leo Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Latifa Mansoor akizungumza na wanafunzi leo Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma
Mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Kilakala akizungumza. Lydia Churi Ntambi



Na Lydia Churi-Mahakama, Dodoma

Mahakama ya Tanzania imeanzisha mpango wa kushirikiana na vyuo na shule za sekondari katika kuwalea na kuwatambua wanafunzi wenye vipawa, tabia na maadili mema ambapo huwafuatilia na kuwafanyia tathmini ili baadaye waje kufanya kazi na Mahakama pamoja na maeneo mengine katika sekta ya Sheria

Katika wiki ya utoaji wa elimu ya Sheria inayoendele jijini Dodoma, wanafunzi kutoka baadhi ya vyuo vikuu na shule za sekondari nchini wanashiriki kwa kujifunza masuala ya mbambali yanayohusu sheria pamoja na taratibu za kimahakama jijini.

Akizungumza na Wanafunzi, Waalimu na Washauri wa wanafunzi hao, kwa niaba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Latifa Mansoor amesema kupitia Mpango huo wa Mahakama, watumishi watakaoajiriwa na Mahakama ni wale tu wenye tabia na maadili mema na wenye uwezo uliothibitika ili waweze kutoa huduma bora hapo baadaye.

Akizungumzia utekelezaji wa mpango huo, Jaji Mansoor amesema baadhi ya mambo ambayo Mahakama inashirikiana na vyuo na shule hizo ni kuwa na mahusiano ya karibu na kuwa na fomu za ufuatiliaji wa mienendo ya maadili na taaluma za wanafunzi ambazo hujazwa na kutumwa kwa Mahakama ya Tanzania mara mbili kwa mwaka.

Aliyataja mambo mengine ya ushirikiano kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa klabu na utoaji wa elimu ya sheria mashuleni pamoja na mpango wa kuwazawadia fursa za masomo na zawadi nyingine wanafunzi wenye vipaji na maadili mema.

Aidha, Jaji Mansoor pia aliwataka Waalimu na washauri wa shule hizo kuwalea na kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanakuwa na ubora katika taaluma, tabia na maadili. Aliongeza kuwa wanafunzi wa vyuo hufuatiliwa na kumbulkumbu zao huhifadhiwa kwa mahitaji ya baadaye ikiwemo ajira kwa watumishi wa Mahakama na Sekta ya Sheria kwa ujumla.

Aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwa na tabia na maadili mema kwa manufaa yao na ya taifa kwa ujumla.” Tunawaalika katika maadhimisho haya ili kubadilishana uzoefu na pia mjifunze masuala mbalimbali ya sheria ili muwe na ufahamu zaidi”, alisema.

Kufuatia Mpango huu wa ushirikiano, Mahakama ya Tanzania inatarajia kuwa na huduma zilizoimarika, watumishi kufanya kazi kwa ubora wa hali ya juu na kwa kuzingatia utawala wa sheria, na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa maadili kupungua.

Vyuo ambavyo mpaka sasa vimeingia kwenye ushirikiano na Mahakama ya Tanzania ni vyuo vikuu vya Dar es salaam, Mzumbe, Dodoma, Ruaha, Iringa na chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.

Shule za sekondari ni pamoja na Maua Seminari. Kisimiri, Shule ya Wavulana Ilboru, Shule ya sekondari Kilakala, Shule za Sekondari za Wavulana za Feza, Marian na Tabora. Nyingine ni Shule ya sekondari Msalato na Mazinde Juu.

Mawaziri wa Tanzania, Rwanda na Burundi wakagua kazi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Rusumo

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa tatu kushoto) pamoja na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Lt. Col. Michael Mntenjele (wa nne kushoto) wakitoka kukagua eneo kutakapojengwa mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 80 katika eneo la Rusumo mkoani Kagera.
Maporomoko ya maji ya Mto Kagera, yatakayotumika kuzalisha umeme wa megawati 80 kwa ajili ya nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kulia), Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Come Manirakiza (wa kwanza kushoto) na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Claver Gatete (wa Tatu kulia mstari wa pili) wakitoka kukagua eneo kutakapojengwa mitambo itakayozalisha umeme wa megawati 80 katika eneo la Rusumo lililopo mpakani mwa nchi ya Rwanda na Tanzania.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati), Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Come Manirakiza (kushoto kwa Dkt. Kalemani) na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Claver Gatete (kulia kwa Dkt Kalemani) wakiwa katika kikao chao na wataalam mbalimbali wanaosimamia mradi wa umeme wa Rusumo kilichofanyika Rusumo mkoani Kagera.
Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (katikati) akifuatilia kikao cha Mawaziri wa Rwanda, Tanzania na Burundi kilichohusu utekelezaji wa mradi wa umeme wa maji wa Rusumo.


Na Teresia Mhagama,

Mawaziri wanaohusika na utekelezaji wa mradi wa umeme wa maji wa Rusumo (MW 80) kutoka Tanzania, Rwanda na Burundi wamekagua kazi ya ujenzi wa mradi huo wilayani Ngara mkoa wa Kagera na kutoa maelekezo mbalimbali yatakayowezesha kasi ya utekelezaji wa mradi huo kuongezeka.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ndiye aliyewaongoza, Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Come Manirakiza na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Claver Gatete katika kukagua kazi mbalimbali zinazoendelea kufanyika ikiwemo ujenzi wa eneo itakapojengwa mitambo ya kuzalishia umeme na ujenzi nyumba za wafanyakazi.

Baada ya kukagua kazi zinazoendelea kufanyika, Mawaziri hao walifanya kikao chini ya uenyekiti wa Dkt Medard Kalemani na kuiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya mradi huo kusimamia ipasavyo kazi mbalimbali za ujenzi ili mradi huo ukamilike mwaka 2020 kama ilivyo katika makubaliano.

Dkt. Kalemani alisema kuwa, kazi ya ujenzi wa mradi huo ilianza mwezi Februari mwaka 2017 na inapaswa kukamilika ndani ya miezi 36 hivyo Bodi hiyo yenye wajumbe kutoka nchi zote Tatu ihakikishe kuwa mkandarasi anakamilisha kazi kwa wakati.

“ Pia tumeiagiza Bodi na wataalam walioko katika mradi huu, wahakikishe kuwa wanashirikisha Mamlaka na Taasisi mbalimbali zilizopo katika maeneo ya mradi katika nchi zote Tatu hasa katika masuala yanayohusu jamii zinazozunguka mradi na stahili za wafanyakazi ili kutokuwa na vikwazo katika utekelezaji,” alisema Dkt Kalemani.

Kuhusu faida za mradi huo, alisema kuwa, kila nchi itapata megawati 27 na kujenga miundombinu ya usafirishaji umeme wa kV 220 ambapo kwa upande wa Tanzania, itajengwa miundombinu hiyo kutoka Rusumo kwenda Nyakanazi kwa umbali wa kilometa 98.

Aliongeza kuwa, miundombinu hiyo ya usafirishaji umeme, kwa upande wa Tanzania, itaingiza umeme katika gridi ya Taifa kupitia njia ya umeme inayotoka Geita na kwamba, vijiji 13 vinavyopitiwa na mradi wa Rusumo vitasambaziwa nishati hiyo.

Kuhusu gharama za mradi, alisema kuwa, kila nchi imegharamia mradi huo kupitia wadau wa maendeleo ambao ni Benki ya Maendeleo Afrika (AfdB) na Benki ya Dunia (WB) ambapo kwa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kila nchi imechangia takribani Dola za Marekani milioni 113.

Kwa upande wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme, alisema kuwa kila nchi imechangia kiasi cha Dola za Marekani milioni 36.7.

Kwa ujumla, alisema kuwa, Mawaziri wa nchi hizo Tatu wameazimia kuwa, mradi huo utekelezwe kwa kasi usiku na mchana bila kuwa na visingizio na kama kuna muda uliopotezwa na mkandarasi wa mradi, ufidiwe kwa njia mbalimbali ikiwemo kuongeza nguvu kazi.

Aidha, ili kuongeza usimamizi katika mradi huo, Mawaziri hao ambao kwa kawaida hukutana kila baada ya miezi Sita, wameamua kufanya vikao vya dharura kila itakapohitajika ili kuhakikisha kuwa yale wanayoaagiza yanatekelezwa kwa ufanisi.
Viewing all 109935 articles
Browse latest View live




Latest Images