Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

EALA BEGINS SENSITISATION OF STAKEHOLDERS IN REGION

$
0
0
East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: February 1st, 2019: The East African Legislative Assembly (EALA) has commenced sensitization activities in the Partner States with legislators targeting various stakeholders in the outreach programme.


The sensitization activities, been carried out by the EALA local chapters in the Partner States, is shall run over six days (Feb 1-6th, 2019).  The sensitization programme is anchored on the theme: “EAC Integration Agenda: Accessing the gains and assessing the Challenges”.


The sensitization activities target Parliamentarians, youth groups, representatives of the business community and local government authorities. Other groups include the women organisations, learning institutions and media in the respective Partner States.  The sensitisation activities are to run simultaneously in the Partner States.


EALA will work with the respective Ministries of EAC in the Partner States to identify and access the target stakeholders. The week-long sensitization activities will include; presentations as well as questions and answers to select representatives of the stakeholders groups, public addresses (Baraza) where possible and courtesy calls to the Regional Commissioners, Governors and District leaders among other opinion leaders in respective Partner States.  


The overall objectives of the sensitization programme are:

(i)             to sensitize EAC citizens on the overall integration process,
(ii)            to promote liaison with EAC National Assemblies and key stakeholders,
(iii)           to create awareness among the EAC populace on the gains and challenges of integration,
(iv)          to enhance mutual relationships and sustainable networking between EALA and EAC populace,
(v)           to EAC populace on the role of EALA in the integration process.

   A number of benefits are expected to be arrived at when done. Such include;
(i)             sensitization of EAC citizenry on the overall integration process,
(ii)            promotion of liaison with EAC National Assemblies and key stakeholders,
(iii)           creation of awareness among the EAC populace on the gains and challenges of integration,
(iv)          enhancement of mutual relationships and sustainable networking between EALA and EAC populace,
(v)           informed EAC populace on the role of EALA in the integration process.

The EAC which turns two decades later this year has realized a number of economic achievements.  The establishment of the Customs Union, has led to increase of intra-regional trade through establishment of the single customs territory where importers clear their goods at the point of entry and revenues are collected at that point and remitted to the destination Partner State.  Also in place, is the one stop border post leading to integrated land border management systems where customs and other government agencies of both neighboring countries work in the same office and clearance procedures are done at once at the point of entry. 

Other developments include the improved issuance of travel documents to facilitate travel within the region by EAC citizens and harmonization of educational curricula, examinations, standards, certification and accreditation of educational and training institutions to facilitate recognition of academic qualifications. 


Challenges currently been addressed, include the existence of Non-Tariff Barriers, which call for sustained efforts to remove them and consolidated efforts to ensure peace and security given the heightened terrorist attacks as well as instability which threatens the very impact of the region’s security and economic performance.

Sensitization is a key component of regional Assembly’s work and the EALA’s Strategic Plan anticipates a people-centered approach to widening and deepening of the integration agenda. 


Mashindano ya kuogelea ya Taliss-IST kufanyika Februari 9 na 10

$
0
0
Dar es Salaam. Mashindano ya kuogelea ya Taliss-IST yamepangwa kufanyika kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga kwa siku mbili kuanzia Februari 9.

Mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji wenye umri tofauti kwa mujibu wa meneja wa klabu ya Taliss-IST, Hadija Shebe.

Hadija alisema kuwa wanatarajia kupata ushindani mkubwa katika mashindano hayo ambayo yameandaliwa kwa ajili kupima maendeleo na uwezo wa waogeleaji baada ya kufanya mazoezi.

Alisema kuwa klabu yao imejipanga kuendesha mashindano yenye ushidani mkubwa chini ya usimamizi wa Chama Cha Kuogelea nchini (TSA).

Alifafanua kwa wanatarajia kupata waogeleaji kutoka mikoa mbalimbali ikiwa pamoja na Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Zanzibar.

“Haya mashindano ya kupima maendeleo ya waogeaji wenye umri tofauti na maandalizi yake yamekwisha kamilika. Waogeleaji watashindana katika staili tano tofauti na vile vile kushindana kwenye ‘relay’,” alisema Hadija.

Alisema kuwa kila klabu inatakiwa kuorodhesha majina ya waogeleaji wake wakiwa na umri na aina ya mashindano ambayo wanatakiwa kushindana ili kuwawezesha kuandaa programu kamili ya mashindano hayo.

Staili ambazo waogeleaji watashindania ni Backstroke, Butterfly, Freestyle, Breaststroke na Individual Medley (IM).

Waogeleaji watakuwa katika makundi ya umri tofauti ikiwa pamoja na chini ya miaka nane (8), 9 na 10, 11 na 12, 13 na 14 na wenye miaka kuanzia 15 na zaidi.

Washindi kwa upande wa wanawake na wanaume watazwadiwa medali ikiwa pamoja na dhahabu, fedha na shaba wakati washindi wa kwanza, kwa makundi ya umri watazawadiwa vikombe.

TAARIFA KWA UMMA: SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2019

NAIBU WAZIRI NDITIYE AKABIDHI KOMPYUTA SHULE ZA SEKONDARI MPANDA

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amekabidhi kompyuta 25 kwa shule za sekondari Mpanda mkoani Katavi kwa lengo la kukuza kiwango cha ufaulu na kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) shuleni kwa kuwawezesha waalimu kutumia kufundishia na wanafunzi kujifunzia
Nditiye amewataka waalimu na wanafunzi wa shule hizo kuhakikisha kuwa kompyuta zilizotolewa zinatumika kwa nia njema kutoa elimu kwa watoto wetu kwa kuwa sasa dunia ni kijiji. 

Amefafanua kuwa lengo ni tupate wanafunzi mahiri kwa kompyuta hizo kutumika na wanafunzi wengine kwenye shule mbali mbali kwa kuziunganisha kompyuta hizo kwenye mtandao ili mwalimu mmoja aweze kufundisha wanafunzi wengi wengine wa shule nyingine
“Kumbukeni hapo zamani wanafunzi wa mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma ilikuwa inatoa wanafunzi wenye ufaulu mzuri, hivyo tuwarithishe wanafunzi wetu,” amesisitiza Nditiye
Kompyuta hizo zimetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambao una dhamana ya kuhakikisha wananchi waishio vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara wana wasiliana kwa kuzipatia kampuni za simu za mkononi ruzuku ya kujenga minara ili kufikisha huduma za mawasiliano maeneo mbali mbali nchini

Nditiye amekabidhi kompyuta 25 zenye thamani ya shilingi milioni 46 kwa Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi kwa niaba ya waalimu na wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo mjini humo kwa kuwa aliiomba Serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu  ili shule hizo ziweze kupatiwa kompyuta hizo.

“Nimeanza kumsumbua Nditiye zaidi ya mwaka mmoja na nusu kuomba kompyuta, unaweza kuona kompyuta ni chombo chepesi ila sio hivyo kwa kuwa ni chombo muhimu na kitatunza siri,” amesema Kapufi
Pia, ameongeza kuwa tunalotekeleza hapa ni upendo na na litaenda kufuta ujinga wa watoto wetu kwenye shule za sekondari kwa kutumia kompyuta hizi. Vile vile ameishukuru Serikali kwa ahadi ya mafunzo ya kompyuta ambayo yatatolewa kwa waalimu wa shule ili kuwawezesha namna ya kutumia na kufanyia matengenezo madogo madogo kompyuta hizo ambapo ameahidi kuwa atakwenda yeye mwenyewe binafsi kukabidhi kompyuta hizo kwa kila shule

 Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka UCSAF Mhandisi Albert Richard amesema kuwa UCSAF imekuwa ikitoa kompyuta hizo kwenye shule mbali mbali nchini kupitia mradi wa kuunganisha shule ujulikanao kama “School Connectivity”. Richard amesema kuwa ni imani yao kuwa kompyuta hizo zitatumika kwa malengo yaliyopangwa kwa nia ya kuwasaidia wanafunzi kusoma na waalimu kufundishia. Ameongeza kuwa UCSAF itatoa mafunzo kwa waalimu wa shule za sekondari za Mpanda ya namna ya kutumia kompyuta hizo kufundushia pamoja na waalimu wao wenyewe kuweza kuzifanyia matengenezo madogo madogo kompyuta hizo pale zinapoharibika.

Akizungumza kwa niaba ya waalimu wa shule za sekondari za Mpanda, Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Mpanda, Enelia Lutungulu amesema kuwa shule za msingi na sekondari zina uhitaji mkubwa sana wa kompyuta kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia na TEHAMA ambapo kazi nyingi zinahitaji mawasiliano kwa kutumia kompyuta
“Shule hizi zina uhitaji mkubwa wa kompyuta kwa kuwa baadhi ya shule kompyuta zinazotumika ni za waalimu binafsi na hivyo kuleta ugumu wa utendaji wa kazi wa kila siku ukizingatia upokeaji na utoaji wa taarifa ni wa kila mara,” amefafanua Lutungulu.

Ameongeza kuwa kompyuta hizo zitakuwa kichocheo cha kuongeza na kurahisisha ufanisi wa kazi katika shughuli mbali mbali zikiwemo za uchapishaji wa mitihani ndani ya shule, ukusanyaji na uhifadhi wa data za kielimu katika shule, utoaji rahisi na wa haraka wa taarifa kwa kutumia TEHAMA, kupokea miongozo na maagizo mbali mbali ya kikazi kwa kutumia mawasiliano ya barua pepe, kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ikiwemo TEHAMA na mawasiliano katika kazi za kila siku. Makabidhiano ya kompyuta hizo yamehudhuriwa na wakuu wa shule za sekondari, viongozi na wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Mpanda na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya hiyo

Akiwasilisha taarifa ya mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Abdallah Malela amemuomba Nditiye kuipatia mkoa huo ofisi ya TTCL ya ngazi ya mkoa tofauti na hali ilivyo sasa ambapo ipo ofisi ya TTCL ya ngazi ya wilaya. Pia, ameongeza kuwa mkoa upatiwe usafiri wa ndege kwa kuwa ina kiwanja kizuri na kuna wateja wa kutosha

Nditiye amepokea changamoto hizo na kuielekeza Bodi ya TTCL na menejimenti yake kufungua ofisi ya Shirika hilo lenye hadhi ya mkoa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja. Pia, ameuhakikishia uongozi wa mkoa na wananchi wa Katavi kuwa Serikali inaleta gari la zimamoto kwenye uwanja huo na huduma za usafirishaji utaanza kutolewa kwa wananchi na wadau wa mkoa huo. Pia, Nditiye alitembelea na kukagua kiwanja hicho cha ndege na kuona hali ya kiwanja na miundombinu yake.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akikabidhi kompyuta kwa Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (wa pili kulia) kwa ajili ya shule za sekondari mjini humo. Wakishuhudia, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela (wa pili kushoto)
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa viongozi wa Mkoa wa Katavi, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na waalimu wa sekondari (hawapo pichani) kuhusu ukuaji na maendeleo wa sekta ya Mawasiliano nchini. Kulia kwake ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard akitoa maelezo ya kompyuta walizotoa kwa shule za sekondari za Mpanda. Walioketi wakimsikiliza, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na  katikati ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi.
 Afisa Elimu wa Shule za Sekondari wa Manispaa ya Mpanda, Enelia Lutungulu akisoma risala ya shukrani kwa Serikali kwa niaba ya waalimu na wanafunzi wa shule kwa kuzipatia shule hizo kompyuta 25. Walioketi wakimsikiliza wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na  katikati ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi.
 Waalimu wa shule za sekondari, viongozi na watendaji wa mkoa wa Katavi na Manispaa ya Mpanda wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati akiwahutubia kabla ya kukabidhi kompyuta kwa ajili ya shule za sekondari za Mpanda.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akisisitiza jambo kwa Afisa Usalama Msaidizi wa Uwanja wa Ndege wa Katavi, Fredrick Valentine(wa kwanza kulia) wakati akikagua miundombinu na hali ya uwanja huo akiwa ziarani mkoani humo. Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (wa tatu kulia) akifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyesimama mbele amefunga mikono) akiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wa shule za sekondari, viongozi na watendaji wa mkoa wa Katavi na Manispaa ya Mpanda. Wan ne kulia ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi na wa tano kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela

POLISI TANZANIA YAICHAPA MASHUJAA 1-0

$
0
0
 Mshambuliaji wa timu ya Polisi Tanzania Edga Mfumakule akionyesha umahiri wa kusakata kabumbu wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza dhidi ya Mashujaa ya Kigoma katika uwanja wa Ushirika Moshi ambapo Polisi walishinda 1-0 (Picha na Jeshi la Polisi).
 Santos Marcelino wa Polisi Tanzania akitamba mbele ya walinzi  wa Mashujaa ya Kigoma wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza katika uwanja wa Ushirika Moshi ambapo Polisi walishinda 1-0.
 Santos Marcelino wa Polisi Tanzania akiwatoka walinzi wa Mashujaa ya Kigoma wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza katika uwanja wa Ushirika Moshi ambapo Polisi walishinda 1-0.
Kikosi cha timu ya Polisi Tanzania kilichoanza dhidi ya Mashujaa ya Kigoma wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza katika uwanja wa Ushirika Moshi ambapo Polisi walishinda 1-0 (Picha na Jeshi la Polisi).

MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA YABAINIKA

$
0
0
Dixon Busagaga, Globu ya Jamii - Moshi

WAFANYABIASHARA  wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi wamebuni mbinu mpya za kusafirisha Dawa hizo kwa kutumia magari ya Kifahari yakiwemo Toyota Land Cruser ,Toyota Alphasad,Toyota Vanguard huku wengine wakilazimka kuzifanyia mabadiliko gari aina ya Toyota Noah ili kurahisisha ubebaji wa Mirungi kwa kificho.

Hata hivyo tayari jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limebaini mbinu hizo baada ya kufanikiwa kukamata gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 443 DET lililokuwa limebeba kilogramu 102 za Mirungi likielekea Kondoa mkoani Dodoma.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah alithibitisha kukamatwa kwa gari hilo majira ya saa 6:30 za usiku katika kizuizi cha askari eneo la Kwa Wasomali likielekea njia ya Arusha.

“Tumeendelea na zoezi la kukamata wasafirishaji w Dawa za kulevya ,tumekamata kwa mara nyingine gari aina ya Noah ,hili gari limetokea maeneo ya mkoani Kilimanjaro ,linaelekea mkoani Dodoma katika wilaya ya Kondoa “alisema Kamanda Issah.
“Hili gari limebadilishwa badilishwa ndani  ,ukilitizama limejengewa vyumba maeneo tofauti tofauti kwa ajili ya kuekea Mirungi,Bampa la mbele lina vyumba ,ndani kumetobolewa na kuchomelewa vizuri ,yaani limefanyiwa mabadiliko makubwa kwa ajili ya shughul ihii ya usafirishaji wa Mirungi,ukikagua kwa mashaka huwezi gundua kwa mara moja”aliongeza Kamanda Issah.

Alisema hadi sasa watu wawili wanashikiliwa huku akiwataja majina kuwa ni Simoni Boaa mkazi wa Babati  na aliyekuwa dereva wa gari hilo na Abushil Abdalah mkazi wa Kondoa  na kwamba taratibu zikikamilika watafikishwa mahakamani huku akitoa onyo kwa wafanyabiashara wa Mirungi walioshindwa kuacha biashara hiyo .
  




KESI YA MALINZI NA WENZAKE YAPANGIWA HAKIMU MWINGINE

$
0
0
HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Hakimu  Mkazi Kisutu,  Maira Kasonde aliyepangwa kuendelea kusikiliza kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili  aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na  wenzake Wanne ameomba kupewa muda wa kupitia jalada la kesi hiyo ili kuangalia ushahidi na vielelezo vilivyotolewa na upande wa mashtaka katika shauli hilo kabla ya kutoa maamuzi. 

Hakimu Maira ambaye amepangwa kusikiliza kesi hiyo baada ya hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Wilbard Mashauri kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ametoa ombi hilo leo Februari 4, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutolewa maamuzi. 

Mapema wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leornard Swai amedai, kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya uamuzi na kueleza kuwa imepata hakimu mpya baada ya Mashauri kuteuliwa kuwa Jaji hivyo kutokana na hali hiyo washtakiwa wanapaswa kukiri kama wanataka waanze upya au waendelee walipoishia. 

Hakimu Kasonde amesema kuwa ni kweli kesi hiyo ilikuwa kwa Hakimu Mashauri ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Jaji,  hivyo anahitaji kupata muda wa kupitia jalada, kusoma ushahidi pamoja na kuangalia vielelezo vilivyotolewa katika kesi hiyo ili awe katika nafasi nzuri ya kujua kitu gani anatakiwa kufanya.

"Ninahitaji nipate muda wa kupitia na kuangalia ushahidi kama unaeleweka na vielelezo vilivyotolewa pia hivyo kwa sasa sipo katika nafasi nzuri ya kuendelea kuisikiliza, " alisema. 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 19, mwaka huu.  

Mbali na Malinzi, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa  Selestine(46) na Mhasibu wa TFF,  Nsiande  Mwanga(27), Meneja wa  Ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya.

Washtakiwa hao Kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtaka 30 katika  kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 na Sh 43,100,000.

WATATU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA MIRUNGI

$
0
0
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii.
WATU watatu wakazi wa Jijini Dar es Salaam, leo Februari 4, 2019 wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za kukutwa na mirungi yenye uzito wa kilogramu 45.22.

Washtakiwa hao, Juma Hussein, Mwanaidi Mohamed na Salama Tunzamali, wamesomewa mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtega wa Mahakama hiyo.

Mapema,  akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Faraji Nguka amedai  katika shtaka la kwanza la kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi inadaiwa, Januari 18 mwaka huu, huko  Kariakoo eneo La Mtambani Hussein na Mohamed. walisafirisha mirungi yenye uzito wa kilogramu 30.24.
Aidha mshtakiwa Tunzamali anadaiwa, siku na mahali hapo, alisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi yenye uzito wa kilogramu 14.98.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande kwa kuwa ujazo wa wa dawa waliokamatwa nao Hussein na Tunzamali hauna dhamana huku mshtakiwa Mohamed akibahatika kusomewa masharti ya dhamana ambayo Pia hakuweza kuyatimiza.

 Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa  hadi Februari 19, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

KITUO CHA AFYA IKWIRIRI CHAPOKEA MSAADA WA VIFAA TIBA

$
0
0
Kituo cha afya Ikwiriri Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa dawa ambazo hupelekwa kidogo ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa katika kituo hicho huku tatizo la vifo vinavyotokana na uzazi vikiendelea kutokea katika kituo hicho.
Mganga mkuu wa kituo cha afya Ikwiriri, Yahya Mohamed ametoa taarifa hiyo baada ya kupokea msaada wa vifaa tiba mbalimbali ikiwemo dawa za kusaidia kina mama wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua na vifaa vya upasuaji kwa kina mama wanaopata uzazi pingamizi kutoka katika kikundi cha maombi cha Our God is Good cha Jijini Dar Es Salaam.
Amesema kituo hicho kwa sasa kinahudumia idadi kubwa ya wagonjwa hasa wasiokuwa na uwezo hivyo wakati mwingine kulazimika kutoa huduma ya matibabu bure kwani hawawezi kumwacha mgonjwa apoteze maisha kwa sababu tu hana fedha za kulipia
Kwa upande wake mratibu wa zoezi hilo kutoka OGG Liku Madaki ameelezea kuwa  lengo la msaada huo ni kuutaka uongozi wa kituo hicho kuitumia kwa lengo lililokusudiwa ili kuokoa maisha ya wana Ikwiriri na Rufiji kwa ujumla,mbali na vifaa na dawa amesema wamepeleka zawadi mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa:
Baadhi ya wagonjwa  kituoni hapo mbali na wakishukuru kwa msaada huo,ambapo pia wameiomba serikali kuboresha kituo hicho kwa kuhakikisha kinapata vifaa na dawa kulingana na idadi ya wagonjwa ili kuwapunguzia umbali wa kufuata huduma ya matibabu Utete ambako kuna hospitali ya wilaya.
 Baadhi ya Wadau wa Maendeleo kutoka katika kikundi cha maombi cha Our God is Good cha Jijini Dar Es Salaam,wakijadiliana jambo kala ya kuanza shughuli yao ya kukabidhi msaada waoo vifaa tiba na vitu vingine kwa kituo hicho cha Afya. 
 Baadhi ya Wadau wa Maendeleo kutoka katika kikundi cha maombi cha Our God is Good cha Jijini Dar Es Salaam,wakikabidhi msaada waoo vifaa tiba na vitu vingine kwa Uongozi wa kituo hicho cha Afya. 


SPIKA NDUGAI AFANYA MAZUNGUMZO NA MSTAAFU (MDAU WA MAENDELEO) JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mstaafu (Mdau wa Maendeleo), Injinia, Rajabu Rukombe (katikati) wakati alipomtembela ofisini kwake kwa ajili ya kumgawia vitabu ambavyo Mhe. Spika pia atawapatia viongozi mbali mbali wa kitaifa, vitabu vyenye maudhui makuu matatau (3), ikiwemo kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuonyesha jitihada na umuhimu wa uchumi wa viwanda pia tufanye nini kufikia lengo la viwanda kikao kilichofanyika leo tarehe 4 Februari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni mwanae Injinia, Ndg. Rukombe Rukombe.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipokea vitabu kutoka kwa Mstaafu (Mdau wa Maendeleo), Injinia, Rajabu Rukombe (katikati) alipomtembela leo tarehe 4 Februari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Vyenye maudhui makuu matatau (3), ikiwemo kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuonyesha jitihada na umuhimu wa uchumi wa viwanda pia tufanye nini kufikia lengo la viwanda, Kulia ni mwanae Injinia, Ndg. Rukombe Rukombe
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mstaafu (Mdau wa Maendeleo), Injinia, Rajabu Rukombe (kushoto) alipomtembelea leo tarehe 4 Februari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Lengo likiwa ni kumgawia vitabu ambavyo Mhe. Spika pia atawapatia viongozi mbali mbali wa kitaifa, vyenye maudhui makuu matatau (3), ikiwemo kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuonyesha jitihada na umuhimu wa uchumi wa viwanda  pia tufanye nini kufikia lengo la Tanzania ya viwanda. Kulia ni mwanae Injinia, Ndg. Rukombe Rukombe
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN MGENI RASMIN SIKU YA SHERIA ZANZIBAR ZILIZOFANYIKA KISIWANI PEMBA WETE

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa Meza Kuu wamesimama ukipigwa wimbo wa Taifa kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe Haroun Ali Suleiman.
 WAHESHIMIWA Majaji na Mahakimu na Wananchi wakihudhuria hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, zilizofanyika Kisiwani Pemba Wilaya ya Wete ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, wakiwa katika ukumbi wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, zilizofanyika Wilaya ya Wete Pemba.
 BAADHI ya Mawaziri Makatibu Wakuu na Wananchi wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, zilizofanyika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba.
 MWAKILISHI wa Chama Cha Wanasheria Zanzibar Mhe. Omar Said Shaban, akitowa salamu za Wanasheria Zanzibar wakati wa hafla ya Maafdhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar.
  JAJI Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akihutubia wakati wa hafla ya Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizindua Kitabu cha Zanzibar ya Law, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba, kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sheria Katiba Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe Haroun Ali Suleiman.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha Kitabu cha Zanzibar ya Law baada ya kukizindua katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, zilizofanyika Kitaifa Kisiwani Pemba Wilaya ya Wete, kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe. Haroun Ali Suleimin.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba.
 JAJI Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akiongoza maandamano ya Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar wakielekea katika ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba, wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar,kulia Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar Mhe. Abdulhakim Ameir Issa na kushoto Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar Mhe. Abraham Mwampashi.

Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Maonyesho ya Wiki ya Sheria

$
0
0
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kati ya Taasisi inayoshiriki maonesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea katika Viwanja vya Nyerere 'Suare' Jijini Dodoma. Wananchi mbalimbali wa rika tofauti wamefika katika Banda hili wakiwa na shinda mbalimbali au kupatiwa elimu kuhusu utendaji na majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mbali ya Wananchi wapo viongozi ambao wamefika katika Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Viongozi hao ni pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali Dr. Fidelice Mafumiko.
Watoto hawa walikuwa sehemu ya wananchi waliotembelea Banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali. kutoka kushoto Christina, Christian ( darasa la 11 A) Catherine Mutambuzi ( darasa la 11A), Proscovia Christian ( darasa la V1B) na Prisca Christian (111A) wanaosoma shule la St. Ignatius ya Jijini Dodoma walimuuliza maswali mbalimbali Wakili wa Serikali Anna Mkongwa ambaye aliwajibu wa ufasaha maswali yao .
Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Obadia Kajungu akitoa maelezo kuhusu majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Dr. Fidelice Mafuniko ( aliyevaa koti)wakati alipofika kwenye Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mkemia Mkuu alifuatana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Jinai na Huduma za Vinasaba Bw. David Elias.
Mwakilishi wa Mkazi wa Bank ya Dunia nchini Tanzania B.i Bella Bird akipata maelezo kutoka kwa Wakili wa Serikali Obadia Kajungu kuhusu Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati Bi Bird alipotembelea Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Dodoma wengine katika picha ni wanafunzi Godliver Adrian (Msalato) na Auxarus Chambulila ( Mzumbe) ambao wamepangiwa Banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama sehemu ya mafunzo yao. Wanafunzi hawa na wengine waliotembelea Banda hili wameonyesha nia yao ya kuwa wanasheria. Picha na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Kesi ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 14 kufanyiwa marekebisho

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)  kesho, inatarajia kufanyia marekebisho hati ya mashtaka dhidi ya kesi ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 14 inayomkabili mfanyabiashara  maarufu aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takribani Sh. Milioni Saba kwa dakika, Mohamed Yusufali na mfanyakazi wake Arital Maliwala. Kwa kumuongeza mshtakiwa mmoja. 

Wakili wa Serikali kutoka Takukuru,  Leornard Swai ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu kuwa,  kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa na pia walitarajia kufanyia mabadiliko hati ya mashtaka  hata hivyo wamekwama kidogo hivyo wanaomba shauli hilo lije kesho ili wafanye mabadiriko hayo. 

Kufuatia maelezo hayo Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi kesho kwa ajili ya kufanyika kwa mabadiliko hayo. 

Yusufali na mfanyakazi wake Maliwala wanaokabiliwa na mashtaka 601 likiwemo hilo la kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh.  bilioni 14.

Katika mashtaka hayo, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi, kuwasilisha taarifa za mwezi za mahesabu ya uongo kwa Mamalaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), kukwepa kodi na kuisababishia serikali hasara ya sh. 14,987,707,044.58.


Katika shtaka la kuisababishia serikali hasara, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa la kusabisha hasara ambayo imetokana na kukwepa kodi ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008 hadi 2015 kupitia kampuni ya Pamplant ltd iliyokuwa inamilikiwa na mshtakiwa Yusufali ambapo mshtakiwa Paliwala alikuwa mfanyakazi wake.

Inadaiwa kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo wakiwa wanatumia stakabadhi za kughushi pamoja na kutumia makampuni ya kughushi wakidai kuwa wamenunua vitu kutoka katika makampuni mbalimbali wakati wakijua baadhi ya kampuni hizo ni za kughushi huku zikiwa hazijasajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brella).

Pia imedaiwa kampuni hizo zina majina ya kampuni ambazo hazapo brella na zina namba  za usajili ambazo brella haijazifikia huku pia wakiwa wanaghushi stakabadhi za malipo.

MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akizungumza Bungeni nakuiomba  Serikali  kutoa tamko kuhusu ambazo imeshachukua kuhusu hali ya mauaji ya watoto Mkoani  Njombe kabla ya Bunge hilo kuhairishwa wiki hii.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akijibu maswali mbalimbali ya wabunge leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile akijibu hoja mbalimbali za Wabunge leo Bungeni  Jijini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Waziri wa  Katiba  na Sheria Mhe.Palamagamba  Kabudi  akiteta Jambo na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko  leo  Bungeni  Jijini Dodoma.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, wakifuatilia mijadala inayo endelea Bungeni Mjini Dodoma Februari 4/2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mwenye suti nyeusi, akisalimiana na Mbunge wa kuteuliwa, Abdalah Bulembo. kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 4, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Shinyanga.Azza Hamad, Bungeni jijini Dodoma, Februari 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wema Sepetu ndani ya Filamu ya Enemy Cops

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya jamii
MCHAMBUZI wa filamu nchini Zamaradi Mketema atambulisha ujio wa filamu yake mpya inayoitwa jina la Cops Enemy. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Zamaradi amesema filamu hiyo ina ubora kutokana na kuweka vionjo mbalimbali ambapo havikuwepo katika filamu zingine. Amesema uandaji  wa Filamu hiyo umegharimu  Sh.milioni 200 hadi kukamilika kwa filamu hiyo.

"Tumeshirikisha wasanii wa nchi tofauti Tanzania akiwemo msanii Wema Sepetu,Aunt Ezekiel na kwa nchi ya Nigeria akiwemo Van Vicker.

Aidha amesema filamu hiyo imeandaliwa  zaidi ya miaka miwili kutokana na kupatikana kwa watayarishaji (DIRECTOR) kutoka Australia ambae ni mahiri na ambaye ataungana na  Neema Ndepanya ambae ni Meneja wa Msanii Wema Sepetu. Zamaradi amefafanua zaidi filamu hiyo itawezwa kuangaliwa na rika za watu wazima kutokana na maudhui mengine si sahihi kwa mtoto kutazama .

Pia Zamaradi ametoa wito kwa wasanii kutengeneza filamu ambazo zitaweza kuingia kwenye tuzo za nchi za nje na kuifanya tasnia kuongeza uwigo wa kupata masoko nje za nchi. Kwa upande wake mtayarishaji wa filamu hiyo hapa nchini Neema Ndepanya amesema filamu ya Cops Enemy ni nzuri na ina mafundisho mengi kutokana na maudhui mengi kugusa hadhira katika jamii nyingi nje na ndani ya nchi.

Ndepanya ameeleza kuwa filamu imewapa vipaumbele kwa watu wote ambao wanaojua lugha ya Kiswahili na Kingereza kuwepo kwa mandishi yanayotafsiri maongezi katika filamu hiyo (Subtitle)

Pia ameeleza uwezo wa Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walionyesha kwenye filamu hiyo kutokana na kutumia lugha ya kiswahili zaidi ambapo uwezo wa Wema Sepetu ni wazi anajulikana kwa ustadi wake wa kutumia lugha ya kingereza hivyo kwa mara ya kwanza ametumia lugha ya Kiswahili zaidi.

"Wema Sepetu bado anatumikia adhabu yake aliyopangiwa na bodi ya filamu hivyo kuzinduliwa kwa filamu hiyo hakutoathiri chochote isipokua alipewa nafasi ya kufanya kazi zake ambazo adhabu hiyo kabla ya kutolewa alikua akiziandaa ndio maana wema Sepetu ametajwa kwenye tuzo za Sinema Zetu na kisheria ana haki ya kushiriki kutokana na tuzo hizo zilishamtangaza kabla ya kupewa adhabu hiyo" amesema Ndepanya.

Pia ametoa shukrani za dhati kwa mmiliki wa filamu hiyo zamaradi Mketema kwa kuweza kumuamini na kulifanikisha hilo kwani ameweza kujifunza vingi jinsi ya kuandaa filamu kwa viwango vya hali ya juu kutoka kwa watayarishaji wa nchini Australia na Nigeria.
Mchambuzi wa filamu nchini, Zamaradi Mketema akizungumza na waandishi wa habari wakati akitambulisha ujio mpya wa filamu yake ya Cops Enemy jijini Dar es Salaam.

WATU WENYE ULEMAVU WAPEWA ELIMU YA SERA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

$
0
0
Na Farida Ramadhani, WFM, Mwanza
Wizara ya Fedha na Mipango imeanza kutoa elimu ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa watu wenye ulemavu wa kusikia (Viziwi) kwa lengo la kuwajengea uwezo na kushirikishwa katika Huduma Jumuishi za Fedha.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dionisia Mjema, ameeleza kuwa mafunzo hayo yameanza mkoani Mwanza na yanatarajia kuwafikia makundi maalumu yote na wananchi wa hali ya chini ili  kuwawezesha kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya kuinua maisha yao na kuchangia katika uchumi wa nchi.

“Miongoni mwa malengo ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ni kuangalia makundi maalum kwa kujua changamoto zao na kuona namna ya kuzitatua na namna  makundi hayo yanaweza kujiunga kwenye vikundi (solidarity groups) kwa ajili ya kupatiwa mikopo ili kujishughulisha katika shughuli za kiuchumi”, alisema Bi. Dionisia.

Mjema alisema Sera hiyo inalenga kuongeza utoaji wa huduma bora na jumuishi za kifedha  kwa wananchi wa kipato cha chini na makundi maalum  ili  kuongeza  ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

Alisema Serikali inatambua umuhimu wa Huduma Ndogo za Fedha katika kukuza uchumi wa nchi na kuwa, ili kuboresha usimamizi na udhibiti wa Sera hiyo, imetunga Sheria ya  Huduma Ndogo za Fedha  mwaka 2018 ambayo inatoa mwongozo na kusimamia utekelezaji wa Sera pamoja na kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha nchini.  

Mjema alitoa wito kwa watu wenye ulemavu kushiriki shughuli za maendeleo kwa kuwa fursa zipo nyingi na wana nafasi kubwa katika jamii.

Naye Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi nchini (TAMAVITA), Kelvin Nyema, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuandaa mafuzo hayo, kwa kuwa anaamini mafunzo hayo yataongeza uelewa kwa wenye ulemavu wa kusikia ambao wengi walikuwa hawana uelewa wa masuala mbalimbali ya kifedha.

Nyema alisema changamoto kubwa inayowakabili ni mawasiliano ambayo inasababisha wasishirikishwe katika shughuli mbalimbali za maendeleo na za kijamii.

“Mawasiliano ni changamoto kubwa kwetu viziwi, ni kikwazo hata katika kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo, ukizingatia lazima tuwe na wakalimani”, alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi mkoani Mwanza (CHAVITA) Jones George, ameiomba Serikali kuweka mazingira wezeshi kwa wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) kupata mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Alisema hali ya watu wenye ulemavu wa kusikia ni ngumu, hawana elimu yoyote ya masuala ya fedha na hawajui waanzie wapi huku akibainisha kuwa kuna wakati wanaogopa kukopa kwa dhana kuwa wakikopa watafungwa.
 Baadhi ya washiriki wa Semina ya Elimu ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa makundi maalum wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango , Jijini Mwanza.
 Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dionisia Mjema, akiwasilisha mada kwa watu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) ambapo alitoa wito kwa walemavu wote nchini kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuwawezesha kiuchumi, wakati wa Semina ya Elimu ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa makundi maalum iliyoandaliwa na wizara hiyo, mkoani Mwanza.
 Mmoja wa washiriki akielezea changamoto za watu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) kwa kutumia lugha ya alama, likiwemo suala la mawasiliano,  katika Semina ya Elimu ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa makundi maalum iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango, mkoani Mwanza.
Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dionisia Mjema (Watatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi wa wizara hiyo pamoja na  Washiriki wa Semina ya Elimu ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa makundi maalum iliyoandaliwa na Wizara hiyo,  mkoani Mwanza.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

WATU WENYE ULEMAVU WAPEWA ELIMU YA SERA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

$
0
0
Na Farida Ramadhani, WFM, Mwanza

Wizara ya Fedha na Mipango imeanza kutoa elimu ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa watu wenye ulemavu wa kusikia (Viziwi) kwa lengo la kuwajengea uwezo na kushirikishwa katika Huduma Jumuishi za Fedha.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dionisia Mjema, ameeleza kuwa mafunzo hayo yameanza mkoani Mwanza na yanatarajia kuwafikia makundi maalumu yote na wananchi wa hali ya chini ili kuwawezesha kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya kuinua maisha yao na kuchangia katika uchumi wa nchi.

“Miongoni mwa malengo ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ni kuangalia makundi maalum kwa kujua changamoto zao na kuona namna ya kuzitatua na namna makundi hayo yanaweza kujiunga kwenye vikundi (solidarity groups) kwa ajili ya kupatiwa mikopo ili kujishughulisha katika shughuli za kiuchumi”, alisema Bi. Dionisia.

Mjema alisema Sera hiyo inalenga kuongeza utoaji wa huduma bora na jumuishi za kifedha kwa wananchi wa kipato cha chini na makundi maalum ili kuongeza ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

Alisema Serikali inatambua umuhimu wa Huduma Ndogo za Fedha katika kukuza uchumi wa nchi na kuwa, ili kuboresha usimamizi na udhibiti wa Sera hiyo, imetunga Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha mwaka 2018 ambayo inatoa mwongozo na kusimamia utekelezaji wa Sera pamoja na kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha nchini.

Mjema alitoa wito kwa watu wenye ulemavu kushiriki shughuli za maendeleo kwa kuwa fursa zipo nyingi na wana nafasi kubwa katika jamii.

Naye Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi nchini (TAMAVITA), Kelvin Nyema, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuandaa mafuzo hayo, kwa kuwa anaamini mafunzo hayo yataongeza uelewa kwa wenye ulemavu wa kusikia ambao wengi walikuwa hawana uelewa wa masuala mbalimbali ya kifedha.

Nyema alisema changamoto kubwa inayowakabili ni mawasiliano ambayo inasababisha wasishirikishwe katika shughuli mbalimbali za maendeleo na za kijamii.

“Mawasiliano ni changamoto kubwa kwetu viziwi, ni kikwazo hata katika kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo, ukizingatia lazima tuwe na wakalimani”, alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi mkoani Mwanza (CHAVITA) Jones George, ameiomba Serikali kuweka mazingira wezeshi kwa wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) kupata mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Alisema hali ya watu wenye ulemavu wa kusikia ni ngumu, hawana elimu yoyote ya masuala ya fedha na hawajui waanzie wapi huku akibainisha kuwa kuna wakati wanaogopa kukopa kwa dhana kuwa wakikopa watafungwa.
Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dionisia Mjema, akiwasilisha mada kwa watu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) ambapo alitoa wito kwa walemavu wote nchini kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuwawezesha kiuchumi, wakati wa Semina ya Elimu ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa makundi maalum iliyoandaliwa na wizara hiyo, mkoani Mwanza.
Mmoja wa washiriki akielezea changamoto za watu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) kwa kutumia lugha ya alama, likiwemo suala la mawasiliano, katika Semina ya Elimu ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa makundi maalum iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango, mkoani Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Elimu ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa makundi maalum wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango , Jijini Mwanza.
Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dionisia Mjema (Watatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi wa wizara hiyo pamoja na Washiriki wa Semina ya Elimu ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa makundi maalum iliyoandaliwa na Wizara hiyo, mkoani Mwanza. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

MAKATIBU WA WABUNGE MAJIMBONI WAPATIWA MAFUNZO

$
0
0
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Bunge Ndugu Jane Kajiru akifungua mafunzo  kwa makatibu wa waheshimiwa wabunge majimboni kwa ajili ya kujengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao.mafunzo hayo yametolewa  na Ofisi ya Bunge chini ya mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kushoto kwake  ni Mratibu wa Mradi wa LSP II Ndugu Mary Lasway.
 Mtaalamu kutoa Chuo cha Utumishi wa Umma , Ndugu Dorah Chenyambuga akitoa mada kuhusu utunzaji wa nyaraka, uendeshaji wa ofisi, ufuatiliaji na tathimini kwa makatibu wa waheshimiwa wabunge majimboni. Mafunzo hayo yametolewa  na Ofisi ya Bunge chini ya mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
 Baadhi ya makatibu wa waheshimiwa wabunge majimboni wakipatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo.mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma yametolewa  na Ofisi ya Bunge chini ya mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP II) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

RC Mongella acharuka fedha za vitambulisho vya wajasiriamali

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Severine Lalika (kushoto) vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo ikiwa ni awamu ya pili ya ugawaji wa vitambulisho hivyo.Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt Philis Nyimbi (kushoto) vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Sengerema, Mwl. Emmanuel Kipole kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Magu, Dkt. Philemon Sengati (kushoto) vitambulisho kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Kwimba, Senyi Ngaga vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Ukerewe, Mwl. Cornel Magembe (kushoto) vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wilayani humo.

BMG Habari
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amewaonya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaotumia mbinu chafu za udanganyifu ili kupatiwa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo na kisha kuvigawa kwa wafanyakazi wao.

Mongella ametoa onyo hilo mapema leo Februari 04, 2019 wakati akizungumza kwenye zoezi la kuwakabidhi Wakuu wa Wilaya vitambulisho elfu 55 ikiwa ni awamu ya pili ya zoezi hilo ambapo awamu ya kwanza Mkoa Mwanza ulipata vitambulisho elfu 25.

Amesema wale tayari wote waliohusika kwenye udanganyifu wa aina hiyo katika awamu ya kwanza ya ugawaji vitambulisho hivyo wamebainika na sheria itachukuliwa dhidi yao huku akiwa mkali kwenye suala la fedha zinazokusanywa kwenye zoezi hilo ambapo kila mfanyabiashara mdogo anachangia shilingi elfu 20 kwa mwaka ili kupata kitambulisho.
Tazama BMG Online TV hapa chini

Kangomba ni Rushwa-Waziri Mkuchika

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images