Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live

MKUU WA WILAYA KAKONKO KANALI NDAGALA AHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULENI KUPATA ELIMU

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewataka wananchi wenye watoto walemavu kuacha kuwaficha ndani na badala yake wahakikishe wanapeleka shule ili wapate elimu kama watoto wengine.

Aidha amewataka wazazi wote waliowahifadhi watoto wao katika kituo cha Watoto wenye ulemavu Kakonko kuwatembelea na kuwapa huduma zinazo stahiki kwa kuwa na wao wanahaki ya kuthaminiwa kama watoto wengine.

Maagizo hayo aliyatoa jana wilayani Kakonko wakati akikabidhi baiskeli saba za watu wenye ulemavu zilitotolewa na Shirika lisilo la kiserikali Help age International linalosaidia wazee na makundi maalumu yenye uhitaji kwaajili ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu waliokuwa wameshindwa kwenda shule.

Amesema wapo watu wengi wenye ulemavu lakini sasa hivi ni wasomi wakubwa na wanazisaidia familia zao na kulisaidia Taifa, kuwa mlemavu ni jambo la kawaida hivyo wazazi wanatakiwa kuwaibua watoto wengine waweze kupata elimu na sio kuwanyanyapaa.

" Ulemavu sio ugonjwa, leo unaweza kuwa mzima kesho ukapata ajali na bado ukawa mlemavu, hivyo tunatakiwa kuwajali na kuwalinda walemavu bila ubaguzi wowowte kwani hata wao wanahitaji huduma za muhimu kama watu wengine", amesema Kanali Ndagala.

Aidha aliyaomba mashirika mengine ya wakimbizi kuendelea kutoa misaada katika Wilaya hiyo, kwa kuwa wanauhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa na miundombinu mbali mbali ilikusaidia Wilaya hiyo inainuka na kusonga mbele.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Help age Kigoma Fredi Kianda alisema Baiskeli hizo walizozitoa zina thamani ya shilingi milioni tisa na laki nane na hiyo ni hatua ya awali wataendelea kufanya uchunguzi kwa makundi yanayo hitaji msaada ili waweze kuleta msaada.

Amesema awali walianza kwa kutoa magodoro 600 kwa wazee wasio jiweza na shirika hilo litaendelea kutoa misaada hoyo ilikuhakikisha makundi ya walemavu na wasiojiweza wanapata misaada na wanaishi vizuri.

Shirika la help age shirika linalo husika kusaidia wazee na watu wenye mahitaji mbalimbali pamoja na walemavu walifanya uchunguzi na kufanya tathimini na kubaini watoto saba wenye ulemavu wa viungo na kuamua kuleta vifaa kwaajili ya kuwasaidia watoto wanaaandikishwa Shuleni.

Zoezi lingine la kufanya uchunguzi kuendelea kuchunguza wazeee na Watu wenye ulemavu lomezinduliwa rasmi na wataendelea kupita vijijini kuwabaini wote pamoja na watoto wenye ulemavu waliofichwa.


 

TAEC YAENDESHA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA CEDHA JIJINI ARUSHA

0
0

Wanafunzi 53 kutoka katika Kituo cha Elimu ya Maendeleo ya Afya ( CEDHA) cha Jijini Arusha, walimu na Baadhi ya Wafanyakazi wa Tume ya Nguvu za Atomiki wakiwa katika picha ya Pamoja wakati wa hitimisho la mafunzo ya udhibiti na matumizi salama ya vyanzo vya mionzi




Na. Vero Ignatus, Arusha

Tume ya Nguvu za Atomiki nchini imeendesha mafunzo kwa wanafunzi 53 wa kituo cha elimu ya maendeleo ya Afya CEDHA juu ya matumizi ya mionzi

Mafunzo hayo yamefanyika makao makuu ya ofisi ya TAEC iliyopo Jijini Arusha kwa siku tatu yakiwa na lengo la kujifunza maswala mbalimbali yahusuyo faida, matumizi udhibiti na madhara yatokanayo na mionzi mahala pa kazi pamoja na sheria zake

Mafunzo yameendeshwa na TAEC kupitia wataalamu wake wafuatao

Bw Eng. John Ben Ngatunga - Mtafiti
Bw Simon Mdoe- Mtafiti
Bw Jerome Mwimanzi- Mtafiti
Bw Siwidhani Ndovi- Mtafiti

Kwa mujibu wa TAEC lengo kuu la mafunzo hayo ni kutoa elimu ya matumizi salama ya vyanzo vya mionzi ili kujifunza maswala mbalimbali yahusuyo faida, matumizi, udhibiti na sheria zake ili kuwawezesha wanafunzi hao kuelewa matumizi salama ya teknoljia ya Nyuklia na kujilinda pindi watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi hapo.

Peter Ngamilo ni Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka TAEC ameeleza Kutokana na ufuatiliaji wa Mara kwa mara ambao unaambatana na ukaguzi unaofanywa na TAEC ,mpaka hivi sasa hakuna athari zozote zilizojitokeza kwenye maeneo ya kazi isipokuwa tu kuna baadhi ya vituo vichache ambavyo vimekuwa vikikiuka utaratibu na tayari imeshavichukulia hatua za Kisheria.

Hatua mojawapo iliyochukuliwa na TAEC ni pamoja na kuvifungia ili visitoe huduma ambayo itapelekea kusababisha athari za madhara ya mionzi kwa Wafanyakazi na mazingira yanayozunguka

TAEC inapenda kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali ili kupata elimu hiyo juu ya yanayohusu udhibiti usalama wa mionzi na matumizi sahihi ya teknolojia ya nyuklia hapa nchini

Mkataba Kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na MOI Kuwanufaisha Wananchi

0
0

NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

WIZARA ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) leo Mjini Unguja, imesaini mkataba na Taasisi ya Mifupa MOI. Mkataba huo wa ambao umerasimisha SMZ kuleta wagonjwa wake kupata matibabu katika Taasisi hiyo badala ya kuwapeleka nje ya nchi kama ambavyo imekuwa ikifanyika.

Katika tukio hilo, Utiaji wa saini wa mkataba umefanywa na katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Bi. Asha Ali Abdulla pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface huku likishuhudiwa na Mwanasheria wa MOI, Suleiman Mgerwa pamoja na Mwanansheria wa Wizara ya Afya Zanzibar Bi Shufaa Nassoro Ali.

Akizungumza katika tukio hilo, Katibu Wizara ya Afya Zanzibar Bi Asha Abdula amesema Serikali ya Zanzibar imeamua kurasimisha ushirikiano na Taasisi ya MOI kwani imekuwa ikitumia gharama kubwa kupeleka wagonjwa nje ya nchi wakati huduma hizo zinapatikana hapa Tanzania.

"Tumekuwa tukipeleka wagonjwa wengi nje ya nchi kwa matibabu hususani hawa wa mifupa, sasa tunafahamu kwamba wenzetu hawa wa MOI wameboresha sana huduma zao hivyo tumeamua wagonjwa wetu waende MOI badala ya kwenda nje, naamnini Mashirikiano hayo haya yatakuwa yenye tija kwa wananchi wetu" alisema bi Asha.

Bi Asha ameongeza kwamba wagonjwa wamekuwa wakienda MOI kupata huduma kwa kipindi kirefu lakini mkataba huu unafanya ushirikiano uwe rasmi na wagonjwa wapokelewe na kupata huduma kwa namna bora zaidi.

" Hili sio jambo jipya, wagonjwa wetu wanakuja huko kupata huduma na tunashukuru kwamba mmekuwa mkiwahudumia vyema, mkataba huu utaboresha namna mnavyowapokea na hata kama kutakuwa na changamoto yoyote kwa mgonjwa tutajadiliana na kuangalia nini cha kufanya kwani mambo sasa yamekuwa rasmi" Alisema Bi Asha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema ni heshma kubwa kwa MOI kuingia mkataba na Wizara ya Afya ya Zanzibar ikiwa ni ishara tosha kwamba Serikali ya Zanziba imetambua maboresho yaliyofanyika MOI pamoja na huduma za ubora wa hali ya juu zinazotolewa.

"Tunawashukuru sana kwa Kuona kwamba huu ni muda muafaka wa kuingia makubaliano nasi, tunawashukuru sana kwa kutambua ubora wa huduma zetu, tunawaahidi kwamba wagonjwa watakaofika kwetu tutahakikisha wanapata huduma bora na kwa wakati kama ambavyo mnatarajia" alisema Dkt Boniface

Dkt Boniface amesema kwamba huduma zinazopatikana MOI kwa sasa ni sawa na zile zinazotolewa katika mataifa yaliyoendelea hivyo wagonjwa kutoka Zanziba watapata huduma nzuri tena kwa wakati.

"Ndugu Katibu Mkuu tumeboresha sana huduma zetu, tuna kitengo cha kisasa cha radiolojia, maabara na wodi za kisasa (Executive ) hivyo tunaamini wagonjwa kutoka Zanziba na watanzania wataendelea kupata huduma bora" Alisema Dkt Boniface

Hatua hii ni itapelekea wagonjwa kutoka Visiwani Zanziba kupata huduma za kibingwa katika Taasisi ya MOI na hivyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kimekuwa kikitumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Bi Asha Ali Abdulla akikabidhiana mkataba wa Matibabu kwa wagonjwa kutoka Zanzibar na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Bonifece katika Hafla iliyofanyika Zanzibar leo (Picha na MOI)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Bi Asha Ali Abdulla akitia saini mtaba wa wagonjwa kutoka Zanziba kupata huduma za kibingwa MOI
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitia saini mtaba wa wagonjwa kutoka Zanziba kupata huduma za kibingwa MOI
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani ) katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika Zanziba leo
Mwanasheria wa MOI Bwana Suleimani Mgerwa akitia saini Mkataba huo
Mwanasheria wa Wizara ya Afya Zanziba Bi Shufaa Nassoro Ali akitia sini Mkataba huo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanziba Bi Asha Ali Abdulla akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani ) katika hafla ya utiaji saini leo Zanziba

WIZARA YA MADINI YAMLILIA MGUNDUZI WA MADINI YA TANZANITE

TAKUKURU TEMEKE YASHINDA KESI MBILI MAHAKAMA WILAYA YA TEMEKE

UKATILI DHIDI YA WATOTO HAUKUBALIKI, HAUVUMILIKI, TUWALINDE WATOTO- TGNP

0
0
TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wadau wa haki za wanawake, watoto na usawa wa kijinsia tunatoa salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza watoto Mkoani Njombe kutokana na matukio ya mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikina.

Vitendo hivi ni vitendo ambavyo havikubaliki katika jamii kwani ni kinyume cha Azimio la ulimwengu juu ya haki za binadamu (Universal Declaration of Human Rights) la tarehe 10 Desemba 1948. Kifungu cha 3 kinachotamka kwamba “Kila mtu ana haki ya kuishi, haki ya uhuru na haki ya kulinda nafsi yake. Na ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Ibara ya 14 imetamka juu ya Haki ya kuishi sambamba na sheria ya Haki ya kuishi ya mwaka 1984.

Jamii inawajibu wa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya mtoto na. 21 ya mwaka 2009 na mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA), unaolenga kupunguza kiwango cha ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii yetu kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Matukio kama haya yamesababisha vifo vya wananchi (wanawake, wanaume, wazee na watoto) wasio na hatia kama vile mauaji ya vikongwe, watu wenye ualibino na sasa yanafanyika kwa watoto ambao hawana ulemavu. 

TGNP Mtandao, tunatambua jitihada za serikali ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa katika kukabiliana na suala hili, na kamati ya kuchunguza mauaji haya tayari imeundwa. Kwetu sisi tunaona ni jitihada nzuri pamoja na kwamba upelelezi unaendelea, tunashauri yafuatayo:-

Kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, ilete majibu hayaka iwezekanvyo, na taarifa ya uchunguzi ifanyiwe kazi kwa wakati ili kutokomeza kabisa mauaji haya.

Serikali na vyombo vya dola visimamie kikamilifu sheria ya kudhibiti uchawi na. 12 ya mwaka 1998(The Witchcraft Act). Ambayo imeainisha adhabu kwa watu wanaoendesha vitendo vya kishirikiana vinavyoweza kudhuru wengine.

Tunalitaka jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola kuhakikisha watoto wanakuwa salama kwa kuimarisha ulinzi katika maeneo yote yanayotajwa kuwa sio salama katika mkoa wa Njombe ili kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo kikamilifu.

Tunaitaka jamii kutoa ulinzi wa mtoto kwani ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha ustawi wa watoto. Pia, serikali na wadau kuzijengea uwezo kamati za ulinzi wa watoto ili waweze kutimiza majukumu yao ikiwemo kubaini maeneo hatarishi katika kijiji/ mtaa na kupanga mikakati ya kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Imetolewa na


Lilian Liundi
Mkurugenzi Mtendaji
TGNP Mtandao.

UGONJWA WA MALARIA WAPUNGUA KWA KIASI KIKUBWA KWA AKINAMAMA WAJAWAZITO NA WATOTO

0
0
Mtaalamu wa magonjwa ya Damu, Vinasaba na Saratani Professa Lucio Luzatto wa Chuo cha MUHAS akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Wageni waalikwa na wafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia. Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akiwasiliasha mada ya 'Malaria kwa akinamama wajawazito na Watoto' katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mtaalam wa Masuala ya Dawa wa Chuo cha MUHAS, Prof. Omary Minzi akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wageni waalikwa na wafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Andrew Barnabas Pembe akifatilia kwa makini mada. Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha MUHAS, Dkt Bill Ngasala akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wageni waalikwa na wafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia. Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Julie Makani (kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya ugonjwa wa Siko Seli unavyoendana na ungonjwa wa Malaria. Mtafiti wa Malaria wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu kilichopo Bombo Hospitali, Tanga, Deus Ishengoma akizungumzia ukata wa fedha unavyonyongonyesha tafiti bunifu. Mmoja ya mdau wa masuala ya afya akiuliza swali... Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma MUHAS na Mloganzila, Hellen Mtui akitoa shukrani zake za pekee kwa wote walioweza kushiriki katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Muhadhara huo, Prof. Lyamuya akihitimisha kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Utafiti umeonyesha ugonjwa wa Malaria kwa akinamama wajawazito na watoto umepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na awali. Kwa upande wa Zanzibar ugonjwa wa Malaria umepungua kwa kiwango kikubwa hivyo ni vyema Tanzania Bara kuendelea kupambana ili ifikapo 2030 tatizo la ugonjwa wa Malaria kwa jamii limekwisha. 

Hayo ameyabainisha Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma wakati akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni 'Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya malaria Tanzania' lililofanyika jijini leo Dar es Salaam. 

Amesema kuwa kadili mama mjamzito anavyotumia vizuri dawa za kujikinga na ugonjwa wa Malaria wakati akiwa amepata ujauzito ndivyo anavyoweza kuepukana na ugonjwa huo. "Kawaida mama mjamzito anapofika wiki ya 13 huwa anapewa dawa za kuzuia Ugonjwa wa Malaria kwa ajili ya yeye na kumkimkinga mtoto, hivyo akizitumia sawa sawa kwa kufuata maelekezo ya dokta pindi anapojifungua huwa salama," amesema. 


Prof Kamuhabwa amesema kuwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyofanyika katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam imeonyesha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria yamepungua chini ya asilimia moja jambo linaloletea faraja kubwa. 


"Tafiti ni jukumu letu kubwa na tunaangalia magonjwa ya kipaumbele katika nchi na Malaria ni ugonjwa wa kipaumbe maana unaathiri akinamama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 5 hivyo hatuna budi kupambana zaidi" amesema. Amesema kwa sasa MUHAS wanaendesha tafiti nyingine ya dawa mbadala ya Malaria kwa akinamama wajawazito na watoto maana dawa ile ya awali SP imeonyesha kuwaletea sugu akina mama. 

"Tunafanya tafiti huko Rufiji ya dawa mbadala ya kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria ambapo Shirika la Afya Duniani limetutaka tufanyie utafiki katika nchi mbali mbali dunia japo wenzetu Kenya na Uganda matokeo yameonyesha dawa hiyo inafanya vizuri lakini kabla hapa kwetu hatujaanza kuitumia lazima nasi tufanye utafiki ila matokeo ya awali yanaonyesha dawa hii inafanya vyema. Dawa wanayoifanyia utafiti inamchanganyiko wa mseto na dawa nyingine ili kupata mbadala na kuachana na SP kwa ajili ya kinga ya akina mama wajawazito na watoto ila tunamalizia utafiti ili tuje tutoe matokeo ifikapo machi mwaka huu. 

Kwa upade wake Mtafiti wa Malaria wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilichopo Bombo Hospitali, Tanga, Deus Ishengoma ameiomba serikali kuwasaidia watafiti ili waweze kuibua tafiti zinazotoa majibu tofauti kwa jamii ambapo ka sasa ambapo tafiti nyingi zimekuwa zikigharimiwa na mashirika ya nje jambo linalowanyima uhuru kwa kufanya tafiti za kigunduzi. 

"Serikali iliahidi kutoa asilimia moja ya pato la Taifa ili kuwawezesha watafiti nchi nzima ili waibue tafiti za kigunduzi, lakini mpaka leo kimya... tambueni fedha tunazopewa na mashirika ya nje zinakuwa zimelenga kile wanachokitaka wao na tufanye tofauti na tungewezeshwa kufanya tafiti za kigunduzi zingeleta tija kwa jamii, mfano kubuni mbinu mpya za kukabili Ugonjwa wa Malaria katika maeneo yenye Malaria kubwa kule Kanda ya Ziwa, Kigoma na Kusini mbinu ziwe tofauti, vile vile maeneo yenye maambukizi kidogo kama Dodoma, Kilimanjaro, Arusha na Manyara na kuelekea ukanda wa nyanda za juu kusini mwa Tanzania napo kukawa na mbinu tofauti," Amesema Ishengoma. 

Pia ameomba jamii kutumia vema vyandarua wanavyopewa ili kuzuia wasiumwe na mbu na kuachana na mila potofu zinazoweza kudhoofisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria ikiwemo kusema kuwa vyandarua vinazalisha kunguni, vinapoteza hamu ya unyumba kwa wapenzi na wengine wanafugua kuku. 

Awali akifungua kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambapo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, Prof Andrew Barnabas Pembe amewaomba watafiti kujitokeza kwa wingi kufanya tafiti zitakazoleta matokeo Chanya katika jamii yetu. "Niwaombe watafiti wote kujitokeza kwa wingi kuungana na Chuo chetu Cha MUHAS ili tufanye tafiti zenye tija ili kuweza kutatua matatizo mbali mbali kwa jamii," amesema. 

Kongamano hilo la pili limehudhuriwa na watalaamu kutoka Wizara ya Afya, Shirika la Afya Duniani (WHO), SIDA Tanzania, Kituo cha Utafiti Ifakara, Mradi wa Taifa wa kuzuia Malaria pamoja na Vyuo mbali mbali na wadau wa Afya.

VIKWAZO VISIVYO RASMI KATIKA BIASHARA BADO NI CHANGAMOTO NCHI ZA EAC

0
0

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Vikwazo visivyo rasmi Usalama utekelezaji wake bado ni changamoto ya kufikia malengo ya kibiashara kwenye nchi za ukanda wa Afrika mashariki katika sekta ya biashara ambapo baraza la biashara limewataka viongozi wa jumuiya hiyo kulingalia na kuchukuwa hatua za maksudi kulitolea tamko.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa Ofisi za Baraza la biashara Afrika mashariki(EABC) jijini hapa Mwenyekiti wa baraza la mawaziri kwenye jumuiya hiyo amesema suala hilo ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa na wakuu wa jumuiya hiyo kesho jijini hapa watakapokutana ili kuondoa changamoto hiyo.

Amesema kuwa changamoto ya vikwazo vya kiusalama na mtangamano wa kibiashara bado umekuwa changamoto kwenye Boda zetu na kuwafanya wafanyabiashara kutoenda na muda hivyo kuchelewesha maendeleo tunatarajia wakuu wan chi zetu watalijadili ili kuwezesha kuondoa changamoto hizo.

“Kama unafanya biashara hakuna usalama wa uhakika basi hapo hakuna uhakika hivyo tumeliona tumeliona hilo na miongoni mwa mambo tulioweka kujadiliwa ni hilo la usalama na vikwazo visivyo rasmi katika biashara kuondolewa na kupatiwa ufumbuzi”alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo la biashara kwenye Jumuiya ya Afrika mashariki Nick Nesbitt amesema kwa miongo miwili baraza hilo limepiga hatua kubwa kuelekea kwenye nchi hizo kuwa na nguvu ya kiuchumi kutokana na fursa nzuri za kibiashara na kuwataka wakuu kuona umuhimu wa kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika nchi hizo

Ameeleza kuwa vikwazo visivyo rasmi ni moja ya changamoto kubwa ya kufikia malengo ya kukuza biashara katika ukanda wetu kwani ukuaji wake umekuwa bado hauendani na ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara(SADC) hivyo mikakati inahitajika kufikia japo asilimia 40

Nae Mkurugenzi wa Baraza hilo la biashara Afrika mashariki ameeleza mafanikio na changamoto mbali mbali zinazolikabili baraza hilo kwa miongo miwili kuwa ni changamoto za kiusalama na vikwazo visivyo rasmi kwa wafanyabiashara wanavyokumbana navyo kuelekea kwenye mtangamano wa kibiashara.

Amesema kuna mafanikio mengi yamepatikana ndani ya miaka hii 20 ya uwepo wa EABC na kuwashukuru wakuu kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya kibiashara katika muingiliano wan chi moja kwenda nyingine

Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza la wafanyabiashara nchini Tanzania Samuel Nyanchae amesema kuwa vikwazo visivyo kodi bado ni changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wa nchi hizo na kuwataka wakuu hao kuendelea kuona njia nzuri ya kuhuisha maazimio yake kufikia malengo tarajiwa.

“Naona maadamu vimetakiwa viondolewe naomba utekelezaji wake ukazingatiwa ili kuondoa changamoto yake kwa wana biashara wan chi zetu kwani kuna baadhi ya nchi zetu bado wapo chini katika utekelezaji wa vikwazo hivyo visivyo rasmi”alisisitiza Nyanchae.


MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARI 1,2019

KIKOSI CHA IGP SIRO CHATUA NJOMBE KUWASAKA WAUAJI WA WATOTO

0
0


NJOMBE 

Ikiwa siku moja imepita tangu naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi amuagize IGP Siro kutuma kikosi maalumu cha kiintelinsia kuongeza nguvu katika uchunguzi wa watekaji na wauaji wilayani Njombe , Hatimae hii leo kikosi hicho kimewasili mkoani Njombe kikiongozwa na Kamisha wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi nchini Nsato Marijani. 

Akizungumza katika mkutano wa dharura na wananchi katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Njombe mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka wakati akitamburisha kikosi hicho kilichosheheni wataalamu mbalimbali kutoka vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama nchini amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini wahusika wamaovu hayo huku akidai hakuna mtu atakae achwa salama kama amehusika na mauaji. 

Katika mkutano huo pia Olesendeka amemuagiza kamanda wa polisi mkoa wa Njombe RPC Rennata Mzinga kumkamata mara moja aliyekuwa mratibu wa tiba mbadala na asilia mkoa wa Njombe Matias Gambishi ambaye pia ni afisa afya wa mkoa huo baada ya kulalamikiwa na waganga wataalamu wa tiba asili na mbadala kuwa amekuwa chanzo cha kusababisha migogoro katika chama chao pamoja kufanya usajiri holela wa waganga hao. 

Nae kamanda wa kikosi hicho maalumu Nsato Marijani ambaye Kamisha wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi nchini anapata wasaha wa kuzungumza na wananchi ambapo anasema kikosi hicho kimekuja kwa kazi ya kuwasaka wahusika wa mauaji na kwamba kitawasaka popote walipo kwa heri ama shari. 

Kwa upande wananchi wanapongeza serikali kwa kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto.

“BENKI YA NMB, WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI ZAJA NA MIKAKATI YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MAZIWA NCHINI”

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Benki ya NMB na menejimenti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi 
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao na maafisa kutoka Benki ya NMB na menejimenti wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (hawapo pichani) kuhusu uwekezaji katika sekta ya maziwa 
Meneja Mwandamizi kutoka Benki ya NMB idara ya kilimo Bw. Carol Nyagaro akimuelezea Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anyeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) juu ya uwekezaji wa sekta ya maziwa na Benki ya NMB 

……………………… 

Na. Edward Kondela 

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel ameitaka Benki ya NMB kushirikiana na wizara hiyo katika kukuza sekta ya maziwa nchini kwa kuwa bado kuna mwitikio mdogo wa wananchi kunywa maziwa kutokana na taarifa iliyotolewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP) 

Prof. Gabriel amebainisha hayo leo (31.01.2019) Jijini Dodoma, akiwa kwenye kikao na maafisa kutoka idara ya kilimo ya Benki ya NMB, waliofika ofisini kwake kumwelezea mikakati ya Benki ya NMB ambayo imekuwa ikifanya tafiti na wadau wa sekta ya maziwa lengo likiwa ni kutaka kuwekeza katika sekta hiyo. 

“Kwa takwimu ambazo zimetolewa na Shirika la Chakula Duniani ni kwamba kwa wastani angalau mtu anatakiwa walau atumie lita mia mbili kwa mwaka za maziwa lakini kwa bahati mbaya kwa watanzania wastani ni lita arobaini na saba tu, bado tuna kazi kubwa sana.” Alisema Prof Gabriel 

Prof. Gabriel amesema Benki ya NMB inapaswa kuwa na ushirikiano na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Dawati la Sekta Binafsi ambalo limekuwa likiwaunganisha wadau wa sekta ya mifugo na uvuvi, ili kuhakikisha mazao yatokanayo na ng’ombe yakiwemo maziwa yanatumika ipasavyo. 

Katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa pia na watendaji wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu mkuu huyo pia amesema ni wakati muafaka kwa Benki ya NMB kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kuhakikisha inawaletea maendeleo wafugaji, hususan wafugaji wadogo ambao wamefanikiwa pamoja na wafugaji ambao watakuwa tayari kubadilika na kuingia katika ufugaji wa kisasa na kuachana na ufugaji wa kuhamahama. 

Aidha Prof. Gabriel amesisitiza umuhimu wa kufanyika kwa tafiti kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Benki ya NMB kupitia idara ya kilimo ili tafiti hizo ziweze kufanyiwa kazi na kuleta matokeo chanya kwa wafugaji. 

“Ningependa sekta hii ya mifugo, iwe pia na tafiti nyingi zinafanyika, sasa tukifanya hizo tafiti tutaweza kuleta mabadiliko chanya na yenye uhakika katika maendeleo ya wafugaji kwa sababu lengo siyo tu kufanya jambo, lakini liwe jambo ambalo linaweza kugusa maisha ya wafugaji.” Alisema Prof. Gabriel 

Katika kikao hicho pia Katibu Mkuu Prof. Gabriel ameshauri uwepo wa mahusiano ya karibu kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Benki ya NMB na taasisi za elimu ya juu, ili kuhakikisha tafiti ambazo zimekuwa zikifanywa na wanafunzi ziweze kutumika katika kuleta mabadiliko na kuleta manufaa kwa wafugaji, badala ya tafiti hizo kuwekwa katika maktaba za vyuo hivyo pekee. 

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB kutoka idara ya kilimo Bw. Carol Nyagaro amesema kutokana na kasi ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli pamoja na utendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewalazimu benki hiyo kubadili mtazamo wa namna ya kutafuta wateja wapya kupitia sekta mbalimbali. 

“Kutokana na kasi ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli na uongozi mzima wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwetu inajenga mazingira mazuri ya kufanya biashara, pia kuchangia maendeleo ya jamii na kuweza kutengeneza wateja wa siku zijazo.” Alisema Bw. Ngayaro 

Aidha Bw. Nyagaro amesema Benki ya NMB kupitia idara ya kilimo inafikiria pia kuwekeza katika sekta ya samaki ambayo imekuwa ikifanya vizuri kiuchumi katika siku za hivi karibuni. 

Bw. Nyagaro amemueleza pia Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel, kuwa Muunganiko wa Vyama vya Ushirika Vikuu vya Maziwa Duniani unatarajia kufanya mkutano wake hapa nchini Tarehe 25 na 26 Mwezi Februari mwaka 2019 kwa kushirikiana na Benki ya NMB lengo kuu likiwa ni kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika sekta ya maziwa hapa nchini. 

Amefafanua kuwa muunganiko huo wenye nchi wanachama 95 ambao unafanya biashara ya takriban Dola za Marekani Bilioni 200 kwa mwaka, umeichagua Tanzania kwa ajili ya kufanya majadiliano kwa kuhusisha wadau wa sekta ya mifugo ili kuwekeza katika sekta ya maziwa. 

Amesema mkutano huo pia utaainisha mambo ambayo tayari yalishafanyiwa tafiti kwa ajili ya utekelezaji wa mipango hiyo.

TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (rtd) Nicodemus Elias Mwangela amewataka Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) kukamilisha miradi ya ujenzi wanayo pewa ndani ya muda wa makubaliano ya mikataba.

Brig. Jen. (rtd) Mwangela ameyasema hayo jana wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa na ya Katibu ya Katibu Tawala Mkoa kati ya TBA na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.

“TBA mna sifa nzuri ya kujenga majengo ya serikali kwa kuzingatia ubora unaotakiwa na kwa gharama nafuu lakini kuna wakati kunakuwa na kusita katika kuwapa kazi kutokana na historia yenu ya kuchelewesha kukamilisha miradi mnayopewa ya ujenzi”, ameeleza Brig. Jen. (rtd) Mwangela.

Ameongeza kuwa TBA wamechelewesha ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ujenzi wa Hospitali ya Mji wa Tunduma hivyo ucheleweshaji huo usirudie katika mikataba hiyo miwili waliyopewa kwani hatasita kuvunja mikataba hiyo endapo wataonyesha ucheleweshaji.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila ameishukuru serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuupatia Mkoa wa Songwe kiasi cha shilingi bilioni 26.8 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali mkoani hapa.

Kafulila amesema serikali imekuwa ikitoa fedha za miradi mbalimbali lakini kasi ya utoaji wa fedha na matumizi ya fedha hizo kwenye miradi husika imekuwa haiendani na hivyo kusababisha kuchelewa kukamilika kwa miradi hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwa amini na kuwapa miradi hiyo miwili yenye thamani ya shilingi bilioni moja na kuahidi kuikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Mhandisi Cosmas amesema hapo awali walikuwa na changamoto kama vile ukosefu wa maji, umeme na baadhi ya vifaa lakini wamesha zifanyia kazi changamoto hizo hivyo watamaliza miradi hiyo Juni 30, 2019 kama walivyokubaliana katika Mikataba.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila akisaini mikataba ya Ujenzi wa nyumba za Mkuu wa Mkoa na ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, ambapo Wakala wa Majengo (TBA) wamekubali kukamilisha ujenzi huo kwa muda wa miezi mitano na kwa gharama ya shilingi bilioni moja.

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila na Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas wakisaini mkataba wa ujenzi wa nyumba za Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa, wa Kwanza Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Rtd) Nicodemus Mwangela.

TAASISI YA WANAWAKE WAHASIBU TANZANIA (TAWCA) YAMWAGA VITABU VYA HESABU SHULE YA SEKONDARI TURIANI WILAYA YA KINONDONI

0
0

Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na Mwanyekiti wa bodi ya Tanzania Association of Women Certified Accountants (TWCA) wanawake wahasibu kushoto na Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TWCA) wa pili kutoka kushoto na wenzao wakikabidhi vitabu mbalimbali vya mahesabu kwa Angalo Izungo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam ikiwa ni msaada walioutoa kwa shule hiyo kwa ajili ya watoto wanaosoma masomo ya hesabu.
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na Mwanyekiti wa bodi ya Taasisi ya Tanzania Association of Women Certified Accountants (TWCA) wanawake wahasibu kushoto na Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TWCA) wa pili kutoka kushoto na wenzao wakikabidhi boksi la vitabu mbalimbali vya mahesabu kwa Angalo Izungo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam na mmoja wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo ikiwa ni msaada walioutoa kwa shule hiyo kwa ajili ya watoto wanaosoma masomo ya hesabu.
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na Mwanyekiti wa bodi ya Taasisi ya wanawake wahasibu Tanzania Association of Women Certified Accountants(TWCA) akikabidhi vitabu vya hesabu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Turiani Wilayani Kinondoni kushoto ni Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWCA) na wanachama wenzao wakishuhudia tukio hilo.
Wanawake wahasibu kutoka taasisi ya Tanzania Association of Women Certified Accountants (TAWCA)wakiwa katika picha na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kukabidhi msaada wa vitabu hivyo.

Wanawake wahasibu kutoka taasisi ya Tanzania Association of Women Certified Accountants (TAWCA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi vitabu hivyo.

......................................................................................................

TAASISI ya wanawake wahasibu Tanzania Association of Women Certified Accountants (TAWCA) wametoa msaada wa vitabu mbalimbali vya hesabu na masomo ya biashara vyenye thamani ya Sh.milioni 8.5 kwa Shule ya Sekondari Turiani jijini Dar es Salaam.

Uamuzi wa (TAWCA) kutoa msaada huo kwenye shule hiyo ni kuwahamasisha wanafunzi hasa wa kike kupenda masomo ya hesabu nchini ili baadae waje kuongeza idadi ya watalaamu wahasibu nchini.

Akizungumza leo shuleni hapo wakati wa tukio la kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania Tumaini Lawrence amesema wanawake wahasibu nchini wameona haja ya kushiriki kwa vitendo kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo yanayohosu hesabu na ndio maana wameamua kutoa msaada huo wenye lengo la kuwahamasisha wanafunzi wa kike nchini kupenda hesabu.

“Wanawake wahasibu nchini kwa umoja wetu tumeamua kuchangishana fedha ili kufanikisha msaada huu kwa ajili ya wanafunzi wa Sekondari ya Turiani.Tumekuja kuwahamasisha wasome kwa bidi masomo ya hesabu na biashara ili tuongeze idadi ya wahasibu na hawa wahasibu wa kike katika nchi yetu ambapo kwa sas idadi yao ni chini ya asilimia 25 ya wahasibu wote.

“Kuna dhana ambayo inajengeka kuwa masomo ya hesabu ni kwa ajili ya wanafunzi wa kiume tu lakini sisi wahasibu wanawake ambao ndio mama zenu tunawaambia wanafunzi kuwa somo la hesabu ni la wote.Hivyo wanafunzi wa kike jitahidi kusoma hesabu na masomo ya biashara,”amesema Lawrence.

Kuhusu mikakati ya taasisi ya wahasibu nchini, Lawrence amesema ni kuendelea kuhamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya hesabu na huku akitoa ushauari kwa wazazi na walezi kuwajengea uwezo wa kujiamini watoto hao.

“Naomba nisieleweke vibaya ila wahasibu wanawake wakiwa kwenye maeneo yao ya kazi wanakuwa waaminifu sana.Kwa kutambua hilo ni jukumu letu kuwatia moyo wanafunzi wa kike nchini kupenda hesabu,” Lawrence. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo Neema Kiure Mssusa amesema ni faraja kwao kufika shuleni hapo kuzungumza na wanafunzi hao.

“Tumefika shuleni hapa kwa lengo la kumsha ari kwa wanafunzi wetu wa kike kusoma masomo ya biashara.Tunawaambia hesabu haikimbiliki, hivyo wasome kwa bidi kwani tunaona faida ya kusoma hesabu maana wanawake wahasibu kila mmoja yupo kwenye taasisi anafanya kazi yake vizuri,”amesema

Ameongeza wao kuwa wahasibu kumetokana na msingi mzuri ambao uliwekwa na walimu wao kuanzia ngazi ya chini , hivyo wanaamini wanafunzi wa kike watasoma kwa bidi masomo ya hesabu.

Wakati huo huo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Turiani jijini Dar es Salaam Angalo Izungo amesema anashukuru kupata msaada huo na kwamba wahasibu hao wanawake wameonesha upendo wa dhati kwa shule yao. Amefafanua changamoto kubwa iliyopo shuleni hapo ni vitabu vya masomo ya hesabu na biashara pamoja a uhaba wa walimu , hivyo baada ya kupata vitabu ombi lao ni Serikali kuwapatia walimu kwani waliopo ni wawili tu na wanafunzi walionao ni 506.

“Tunao walimu wawili tu wa masomo ya hesabu hapa shuleni kwetu, hivyo tunashukuru kwa msaada huu.Tunaomba Serikali yetu ituongezee walimu wa masomo ya hesabu shuleni kwetu, wanafunzi wetu wanapenda hesabu sana,”amesema Izungo.

MTENDAJI MKUU TEMESA AKAGUA MASHINE YA KISASA YA KUKAGUA MAGARI KARAKANA YA MT. DEPOT

0
0


Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe (wa pili kushoto) akimpa maelezo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) wakati alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo. Kushoto ni Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe (wa pili kushoto) wakati alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo ili kurahisisha utendaji kazi. Kushoto ni Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.

Pichani, gari linaonekana likiwa limenyanyuliwa juu na mashine ya kisasa (3D Wheel Allignment) tayari kwa kuanza kukaguliwa, mashine hiyo ya kisasa imefungwa katika karakana ya TEMESA Mt. Depot Keko Jijini Dar es Salaam. Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA una mpango wa kufunga mashine nyingine kama hizo katika karakana za mkoa wa Mwanza na Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akikagua maboksi maalumu ya kuhifadhia mtambo wa kuongozea taa za magari (traffic light controller) katika karakana ya Mt. Depot kikosi cha Umeme. Kushoto ni Kaimu meneja wa kikosi hicho Mhandisi Pongeza Semakuwa na wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe. PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO – (TEMESA)

SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KILITEX-ARUSHA

0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji



Na Saidina Msangi, WFM, Dodoma 

Serikali iliwalipa stahili zote Watumishi wa Kiwanda cha nguo cha KILITEX kilichopo mkoani Arusha baada ya kufungwa kutokana na tatizo la ukosefu wa mtaji na malimbikizo ya madeni. 

Hayo yamebainishwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, alipokua akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalaum Mhe. Catherine Magige, aliyeuliza ni lini Serikali itawalipa wafanyakazi 545 wa KILITEX ambao bado wanadai pensheni baada ya kiwanda hicho kufungwa ilihali mwajiri wao hakuwasilisha michango yao kwenye Mfuko wa Kijamii wa PPF. 

Dkt. Kijaji alisema kuwa, kwa mujibu wa kumbukumbu na nyaraka za ufilisi, taratibu za ufilisi zilikamilika na wafanyakazi hao walilipwa stahiki zao kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni namba 46 ya mwaka 1931. 

“Baadhi ya wafanyakazi walilipwa mafao ya kiinua mgongo kwa mkupuo na wengine walirejeshewa michango yao kwa kadiri walivyochangia baada ya Mfilisi kushindwa kulipa riba, adhabu na malimbikizo ya michango kwenye mfuko wa Pensheni wa PPF”, alisema Dkt. Kijaji. 

Alisema Kiwanda hicho kilisimamisha shughuli za uzalishaji mwaka 1994 na kuwekwa chini ya ufilisi na PSRC mwaka 1995. 

Aidha akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlimba, Mhe. Suzan Kiwanga, alietaka kufahamu ni lini wafanyakazi 11075 wa Shirila la Reli la Tanzania na Zambia- TAZARA waliostaafishwa kwa lazima miaka 55 mwaka 2005, watalipwa mafao yao. 

Alisema Serikali imefuatilia madai hayo na takwimu sahihi ni wastaafu 271 walistaafishwa na madai yao yanashughulikiwa ili waweze kulipwa mafao yao.

WAFANYABIASHARA WANAOINGIZA BIDHAA KUPITIA NJIA ZA PANYA ILI KUKWEPA USHURU KUKIONA-RPC WANKYO

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI .

JESHI la polisi mkoani Pwani, limeweka bayana kuendelea kukaza uzi, katika kupambana na wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa kwa njia za magendo kwa lengo la kukwepa ushuru na kuisababishia serikali kukosa mapato. 

Kutokana na kuchukua hatua hiyo jeshi hilo, limefanikiwa kukamata madumu 86 ya mafuta ya kula ambayo hayajalipiwa ushuru yakiwa yamehifadhiwa ndani ya stoo ya mfanyabiashara Mmas Athumani (35) mkazi wa Kongowe Kibaha mkoani hapo. 

Akieleza juu ya suala hilo, kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP) Wankyo Nyigesa alisema, madumu hayo yamefikia jumla ya madumu 107 ya mafuta ya kula yaliyokamatwa katika kipindi cha wiki moja. 

“Taarifa tumezipata kutoka kwa raia wema, ambapo walieleza mafuta hayo yameingizwa nchini kupitia Bagamoyo na kukwepa ushuru wa serikali kisha kusafirishwa kwa njia za panya hadi kwenye stoo hiyo eneo la Kongowe “alifafanua Wankyo. 

Alitaja mafuta ni dumu moja lita 20 aina ya jenau, madumu 26 ya lita 20 aina ya MTRA pamoja na madumu 59 ya lita 20 aina ya oki. Aidha Wankyo alisema, pia limekamata mifuko 18 ya sukari ambayo imeingizwa nchini kutoka nchi jirani kwa kukwepa ushuru. 

Wakati huo huo, wanamsaka mfanyabiashara mmoja ambae kwa sasa jina linahifadhiwa aliyetoroka baada ya kuona maafisa wa polisi wakimfatilia na kutelekeza madumu 21 ya mafuta ya kupikia aina ya Micogold yenye ujazo wa lita 20 kila moja ambayo hayajalipiwa ushuru eneo la Magomeni Bagamoyo. 

Kamanda huyo alitoa wito kwa wafanyabiashara, kuacha kujihusisha na biashara za magendo na ukwepaji wa ushuru katika biashara wanazofanya .
Wankyo aliwapa salamu kwamba, watambue hawapo salama kwani jeshi hilo limejipanga vilivyo kwenye KUTINDUA mitandao yote ya wafanyabiashara wanaoingiza mali za magendo na ukwepaji ushuru kupitia bandari bubu. 

CGP – PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA ENEO LA UJENZI OFISI ZA WIZARA MAMBO YA NDANI, WIZARA YA ELIMU NA OFISI YA WAZIRI MKUU AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU, JIJINI DODOMA

0
0

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akitembelea maeneo ya mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma yanapojengwa majengo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana na Walemavu, leo januari 31, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akimsikiliza Msimamizi Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi cha Magereza katika mradi huo, ACP. Aron Lunyungu alipotembelea katika eneo la ujenzi wa Ofisi Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana na Walemavu, leo januari 31, 2019.
Ujenzi wa majengo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana na Walemavu, leo januari 31, 2019 ukiendelea katika hatua mbalimbali kama inavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akisaini kitabu cha ukaguzi katika ujenzi wa Ofisi Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana na Walemavu, leo januari 31, 2019(Picha na Jeshi la Magereza). 



…………………….. 

Na ASP. Lucas Mboje, Dodoma 

KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike leo januari 31, 2019 ametembelea maeneo ya mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma yanapojengwa majengo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana na Walemavu ambapo amekiagiza Kikosi cha ujenzi cha Jeshi la Magereza kinachoshiriki katika ujenzi wa ofisi hizo kuzingatia ubora katika ujenzi wa majengo hayo. 

Kamishna Jenerali Kasike amewataka pia Maafisa na askari wanaoshiriki katika ujenzi wa ofisi hizo kuongeza kasi ya ujenzi kama ambavyo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alivyoagiza lakini wazingatie viwango vya ubora katika ujenzi huo. 

“Hakikisheni ujenzi unafanyika usiku na mchana kama tulivyokwishajipanga lakini zingatieni viwango vya ubora katika ujenzi”. Amesisitiza Jenerali Kasike. 

Aidha, Kamishna Jenerali Kasike amemtaka Msimamizi Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi cha Magereza katika mradi huo, ACP. Aron Lunyungu pamoja na Mhandisi Mradi, SSP. Alfred Bundala kuhakikisha kuwa wanakusanya mahitaji yote muhimu katika eneo la ujenzi ili kufanikisha kasi ya ujenzi huo. 

Ujenzi wa majengo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi ulitarajiwa kukamilika mapema ifikapo tarehe 31 Januari 2019 lakini kutokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa nje ya uwezo wa Kikosi cha ujenzi cha Jeshi la Magereza, ujenzi huo umechelewa kukamilika kwa wakati na hatua za ukamilishaji zinaendelea kwa kasi ya kuridhisha.

SPIKA WA BUNGE AKIMUAGA MHE. KITWANGA UWANJA WA NDEGE JIJINI DODOMA WAKATI AKIPELEKWA JIJINI DAR ES SALAAM KWA MATIBABU ZAIDI

0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akiagana na Mbunge wa Misugwi Mhe. Charles Kitwaga katika Uwanja wa Ndege wa Jijini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa  matibabu zaidi. Kulia kwa Spika ni Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula na kushoto kwa Spika ni Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.

PICHA NA BUNGE

MAHAKIMU MAHAKAMA ZA MWANZO, WAJUMBE MABARAZA YA KATA WAPIGWA MSASA

0
0
MAHAKIMU wa Mahakama za Mwanzo na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata katika Wilaya za Nyamagana na Ilemela wametakiwa kutambua mipaka na majukumu yao ya usimamizi wa haki ili kuleta suluhu na kupunguza migogoro kwenye vyombo vya juu vya kutoa haki kwa jamii.

Pia watendaji wa kata, mitaa, vijiji na vitongoji wameonywa na kutakiwa kuacha kupora majukumu ya mabaraza ya kata kwa kusilikiza mashauri na kuyatolea maamuzi, kwani wanakiuka kwa kuwa mabaraza yapo kwa mujibu wa sheria.

Rai hiyo ilitolewa jana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Jaji Sam Rumanyika wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo mahakimu na wajumbe hao wa mabaraza ya kata yaliyoandaliwa na Chuo cha  Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).

Alisema mafunzo hyo ni utekelezaji wa agizo la  Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma baada ya ziara yake mkoani Tabora mwaka jana, alipokea malalamiko ya utendaji usioridhisha wa Mabaraza ya Kata na alishuhudia maamuzi mengi ya mabaraza hayo kutothibitishwa na Mahakama za Mwanzo kwa mujibu wa sheria ya uanzishwaji wake.

Alisema kutokana na uwezo wa mabaraza hayo katika kutatua migogoro kuwa bado ni kizungumkuti (changamoto) na sababu ya kutowezeshwa katika hali ya uelewa na mazingira, alielekeza zifanyike juhudi za kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata juu ya majukumu ya mabaraza, mamlaka husika kuyalinda ili kuimarisha mfumo wa utoaji haki.

“Mabaraza ya Kata kazi yake ni kutoa uamuzi wa mashauri ya jinai na madai yaliyoanishwa na adhabu zake ni ndogo, lakini yamewekwa kando na wasimamizi (serikali za mitaa).Kwa kuwa yapo kisheria katika muundo wa kutoa haki,yawezeshwe kimiundombinu, vitendea na uelewa wa mambo,”alisema Jaji Rumanyika.

 Aliongeza kuwa ; “Inasikitika kuona mpangilio wa majalada hasa ya ardhi, muundo na ujengaji wa hoja katika kufikia maamuzi na si wingi wa migogoro.Faraja ni lengo la sheria ya mabaraza inayolenga kudumisha suluhu na kupunguza mashauri ikizingatiwa asilimia 70 yanafunguliwa kila siku.Ni imani yangu mabaraza yakijengewa uwezo yatapunguza mzigo na nafuu itapatikana kwenye vyombo vingine.”

Jaji Rumanyika alidai licha ya mabaraza ya kata kuwepo kisheria yameharibiwa na kimsingi utendaji wake si mbaya sana, si mbaya, kutokana na uwezo usioridhisha wa kutatua migororo kwa jinsi rekodi za maamuzi yao zilivyo, hivyo yakiwezeshwa yatakuwa na sura nzuri.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha IJA, Taaluma, Tafiti na Ushauri Fahamu Mtulya alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata kubadilisha uzoefu katika changamoto za utoaji haki na kuzitatua.

Alisema kuwa imedhihirika kuwepo kwa changamoto nyingi kwenye mabaraza hayo na hivyo chuo kiliona umuhimu wa kutoa mafunzo ya uwezeshaji ya kuwajengea uwezo wajumbe wa mabaraza hayo na mahakimu ili kupunguza ama kuondoa changamoto hizo ambazo zimekuwa nyingi nchini.

“Utendaji wa mabaraza hayo si mzuri kwa mujibu wa utafiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria hasa mabaraza ya ardhi ambapo Jaji Mkuu Profesa Juma akiwa tabora alipokea malalamiko mengi na maamuzi yanayotolewa hayazingatii maadili na mienendo ya utumishi,”alisema  Mtulya.

Alisema kuwa si wote wanafahamu mamlaka zao ( mahakimu na wajumbe wa mabaraza) hivyo chuo kiliamua kubeba jukumu la kuwaelimisha na kuwaunganisha ili wajione ni wasimamizi wa haki nchini.

Alieleza kuwa nia na lengo la mabaraza ni kufanya usuluhishi wa migogoro midogo midogo ili jamii iishi salama kwa amani zaidi, hivyo baada ya kupata mafunzo (elimu) hayo mahakimu na wajumbe wa mabaraza ya kata watakuwa mabalozi wa utoaji haki isiyo na shaka.

Kwa mujibu wa Mtulya wanalenga kuwakumbusha muundo na ukomo mamlaka ya Mahakama za Mwanzo, muundo wa Mabaraza ya Kata,mashauri katika mahakama hizo,namna ya kusuluhisha mashauri kwenye mabaraza ya kata na mamlaka ya usimamizi ya Mahakama za Mwanzo kwenye mabaraza hayo .

“Zipo sheria zinawapa mamlaka wajumbe wa mabaraza ya kata kusikiliza baadhi ya mashauri na kuyatolea maamuzi pia kuna sheria mahakimu wanapewa mamlaka ya kuwasimamia wajumbe wa mabaraza ya kata.Pia yapo aina ya mashauri yanayotakiwa kusikilizwa na Mahakama za Mwanzo na mabaraza yana ukomo wa kazi zao pia,”alifafanua Mtulya
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uongozi Lushoto (IJA), Taaluma, Tafiti na Ushauri Fahamu Mtulya akizungumza na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo pamoja na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata wa Wilaya za Nyamagana na Ilemela (hapo pichani) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika juzi jijini Mwanza.Kutoka kulia wa pili ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Jaji Sam Rumanyika na kulia ni Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Kingwele Omari na kushoto ni Mhadhiri wa IJA Dk. Alexander Saba.
 Kaimu MKuu wa Chuo cha Uongozi Lushoto (IJA),Taaluma, Tafiti na Ushauri Fahamu Mtulya akisistiza jambo kwa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo wa Wilaya za Nyamagana na Ilemela na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata (hawapo pichani) kutoka kwenye wilaya hizo mbili wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo.Mtulya aliteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. 
 Wajumbe wa Mabaraza ya Kata wakiwa pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Jaji Sam Mpaya Rumanyika, wa tatu kutoka kulia.Wa pili kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uongozi Lushoto (IJA) Fahamu Mtulya na wa pili kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Mwanza Kingwele Omari.Kushoto ni Mhadhiri wa IJA Dk. Alexander Saba.
 Mgeni rasmi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo pamoja na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Mwanza, Jaji Sam Mpaya Rumanyika (wa tano kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja, wanne kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha IJA Fahamu Mtulya, wa tatu kushoto ni Mhadhiri wa chuo hicho Dk. Alexander Sana na wa nne kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Mwanza  Kingwele Omari.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uongozi Lushoto (IJA), Taaluma, Tafiti na Ushauri Fahamu Mtulya akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu mkakati wa chuo hicho kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata yatakayowawezesha kutimiza wajibu na majukumu yao kwa weledi. Picha zote na Baltazar Mashaka

RC MAKONDA AWATAFUTIA WASANII MKOPO WA BILIONI 2 BILA RIBA.

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda katika kujali na kunusuru kazi za Wasanii amewatafutia mkopo wa Shilingi Bilioni 2 bila riba zitakazotolewa kwenye Halmashauri za Mkoa huo kupitia fungu la mkopo wa 10% zinazotolewa kwa Vijana, Walemavu na kinamama  kwa lengo la kuwawezesha wasanii kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuziingiza sokoni.

RC Makonda amesema wasanii wengi wamejikuta wakizalisha kazi nzuri lakini wanakosa mitaji ya kuingiza kazi zao sokoni kutokana na kukosa mitaji jambo linalowapelekea wenye pesa kutumia fursa hiyo kunyonya kazi za wasanii na mwisho wa siku wanazidi kudidimia.

Aidha RC Makonda amesema hadi kufikia mwezi March 01 mkopo huo utakuwa tayari na ameshazielekeza halmashauri kutoa fedha hizo huku akiwasihi wasanii kuchangamkia fursa hiyo.

Hayo yote yamejiri wakati wa kikao baina ya RC Makonda na Wasanii kilicholenga kutatua kero za wasanii wa tasnia mbalombali.
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live




Latest Images