Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI KANYASU AONESHA WASI WASI UGAWAJI WA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI

0
0
NA LUSUNGU HELELA-MOROGORO
Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Constantine Kanyasu ameahidi kulifanyia kazi suala la kugawa miche  ya miti bure kwa Wananchi  ili wakaipande iliyooteshwa na Kurugenzi ya Uzalishaji miche ya miti   kuwa utaratibu huo hauwezi kuleta matokeo yaliyokusudiwa na Serikali.

Imeelezwa kuwa uzoefu uliopo unaonesha kuwa vitu vingi ambavyo Serikali imekuwa ikivigawa bure kwa Wananchi bila wananchi hao kuchangia gharama yoyote vitu hivyo hushindwa kuthaminiwa. Kanyasu alitoa kauli hiyo jana   mkoani  Morogoro wakati alipotembelea ofisi za  Kurugenzi hiyo kwa lengo la kujua imejipangaje kuzalisha miche za miti yenye ubora  ikiwemo ya mbao pamoja na ya  matunda ambayo itasambazwa nchi nzima.

Alisema utaratibu huo itabidi uangaliwe upya kwa vile ni ngumu kwa wananchi walio wengi kuitunza  kwa sababu hawasikii uchungu na walio wengi hujikuta wakiitupa au kuiacha bila kuimwagilia hadi inakufa. ''Ukichukua miche leo halafu ukaipeleka mkoani Shinyanga ukagawa bure yote italiwa na ng'ombe na vivyo hivyo ukaipeleka Dodoma  yote itakufa kwa vile haitamwagiliwa maji  kwa sababu ni ya bure'' Amesisitiza

 Alisema siku zote kitu cha bure hakithaminiwi, hivyo lazima kila Mwananchi achangie kidogo  lakini isiwe bure kabisa. Hata hivyo, Kanyasu alisema miche ya miti  inaweza kutolewa bure kwa taasisi za umma kama vile shule ila  kwa makubaliano maalumu lakini sio kwa wananchi.

Aidha, Aliitaka Kurugenzi hiyo ijiendeshe kibiashara badala ya kujikita kutoa huduma kwa wananchi
Katika hatua nyingine, Kanyasu aliiagiza  Kurugenzi hiyo ifungue  utalii wa bustani wa miti na maua  katika jiji la Dodoma ambao ni moja ya aina ya  utalii unaopendwa sana hasa na Wanamazingira. Alisema miji kama Arusha pamoja na Mwanza imeanzisha utalii huo licha ya kuwa kumekosekana mwongozo wa kuziboresha bustani hizo lakini hata hivyo watalii wengi wamekuwa wakimiminika katika bustani hizo.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu( wa pili kulia) akiangalia na huku akipewa maelezo na Afisa Misitu, John Mtika  kuhusu hatua za miche ya miti ya miembe inavyokua wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea  ofisi za  Kurugenzi ya Uzalishaji miche ya Miti mkoani Morogoro kwa lengo la kujua imejipangaje kuzalisha miche za miti yenye ubora  ikiwemo ya mbao pamoja na ya  matunda ambayo itasambazwa nchi nzima Kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi hiyo, Edgar Masunga pamoja na watumishi wengine.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza na na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzalishaji miche ya Miti, Edgar Masunga pamoja  na Afisa Misitu, John Mtika ( kushoto) mara baada Naibu Waziri huyo alipotembelea bustani za miti mbalimbali katika Kurugenzi ya Uzalishaji Miche ya Miti iliyopo mkoani Morogoro.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu (katikati) akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzalishaji miche ya Miti, Edgar Masunga, wakati alipokuwa akikagua jana  bustani mbalimbali za miche inayooteshwa na Kurugenzi hiyo mkoani Morogoro, Kulia ni Afisa misitu wa Kurugenzi hiyo, Fandey Mashimba
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu  akizungumza na Watumishi wa kurugenzi hiyo wakati alipotembelea.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akipanda mti ambao upo hatarini kupotea ambapo kwa sasa nchini Tanzania miti ya aina hiyo inapatikana mkoani Lindi pekee. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA]

Waziri Mbarawa azindua Bodi ya Taifa ya Maji

0
0
 Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akimkabidhi nyenzo za kutendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Taifa Profesa Hudson Hamis Ngotagu.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na Katibu Mkuu, Profesa Kitila Mkumbo pamoja na Wenyeviti wa Bodi za Maji Tanzania.

SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KILITEX-ARUSHA

0
0
Na Saidina Msangi, WFM, Dodoma

Serikali iliwalipa stahili zote Watumishi wa Kiwanda cha nguo cha KILITEX kilichopo mkoani Arusha baada ya kufungwa kutokana na tatizo la ukosefu wa mtaji na malimbikizo ya madeni.

Hayo yamebainishwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, alipokua akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalaum Mhe. Catherine Magige, aliyeuliza ni lini Serikali itawalipa wafanyakazi 545 wa KILITEX ambao bado wanadai pensheni baada ya kiwanda hicho kufungwa ilihali mwajiri wao hakuwasilisha michango yao kwenye Mfuko wa Kijamii wa PPF.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, kwa mujibu wa kumbukumbu na nyaraka za ufilisi, taratibu za ufilisi zilikamilika na wafanyakazi hao walilipwa stahiki zao kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni  namba 46 ya mwaka 1931. 

“Baadhi ya wafanyakazi walilipwa mafao ya kiinua mgongo kwa mkupuo na wengine walirejeshewa michango yao kwa kadiri walivyochangia baada ya Mfilisi kushindwa kulipa riba, adhabu na malimbikizo ya michango kwenye mfuko wa Pensheni wa PPF”, alisema Dkt. Kijaji.

Alisema Kiwanda hicho kilisimamisha shughuli za uzalishaji mwaka 1994 na kuwekwa chini ya ufilisi na PSRC mwaka 1995.

Aidha akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlimba, Mhe. Suzan Kiwanga, alietaka kufahamu ni lini wafanyakazi 11075 wa Shirila la Reli la Tanzania na Zambia- TAZARA waliostaafishwa kwa lazima miaka 55 mwaka 2005, watalipwa mafao yao.

Alisema Serikali imefuatilia madai hayo na takwimu sahihi ni wastaafu 271 walistaafishwa na madai yao yanashughulikiwa ili waweze kulipwa mafao yao.

KAMPUNI YA KENYA KUNUNUA TANI LAKI MOJA ZA KOROSHO GHAFI TANZANIA

0
0
Serikali ya Tanzania kupitia Bodi ya Taifa ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko imesaini mkataba wa mauzo ya korosho ghafi kiasi cha tani laki moja kwa Kampuni ya Kenya ya INDO Power Solutions kwa malipo ya Shilingi bilioni 418.

Mkataba huo umesainiwa jijini Arusha tarehe 30 Januari 2019 kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo Dkt. Hussein Mansoor kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Bw. Brian Mutembei, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya INDO Power Solutions ya nchini Kenya.

Tukio hilo la kihistoria lilishuhudiwa na Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria,  Joseph Kakunda, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Innocent Bashungwa, Naibu Waziri wa Kilimo, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, Dkt. Evaristo Longopa, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,

Viongozi wengine walioshuhudia ni Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu, Prof. Sifuni Mchome, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Joseph Buchweshaija, Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, Prof. Siza Tumbo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Edwin Rutaberuka, Mkurugenzi wa TanTrade, Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini na Waandishi wa Habari.

Awali wakizungumza kabla ya kusainiwa kwa Mkataba huo Mawaziri hao wakiongozwa na Prof. Kabudi, kwa pamoja walipongeza kwa dhati uamuzi wa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali kununua korosho kutoka kwa wakulima ili kuepusha wakulima hao kuuza korosho zao kwa bei ya chini kwa watu wasio kuwa na nia njema kwa wakulima. Itakumbukwa kuwa, mwezi Novemba 2018, Rais Magufuli alitoa maelekezo kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo waratibu zoezi la ununuzi wa korosho kutoka kwa wakulima kwa shilingi 3,300 kwa kilo moja.

Kwa upande wake Prof. Kabudi alisema kuwa anampongeza Rais Magufuli kwa uamuzi huo wa Serikali kununua korosho yote ili wakulima wapate bei inayolingana na jasho lao ambao hatimaye umezaa matunda kwa faida na maendeleo ya nchi.

Naye Kakunda alieleza kuwa Bw. Mutembei ni mnunuzi wa kwanza kati ya wengi ambao walikuwa kwenye mazungumzo na Serikali kuhusu ununuzi wa korosho hizo. Kakunda alisema katika majadiliano Serikali iliangalia kufanya biashara ya faida ambayo itawezehsa kulipa gharama mbalimbali ikiwemo gharama za upakiaji na upakuaji, malipo kwenye Serikali za Mtaa na michango mingine ya kijamii kwa mujibu wa makubaliano. Hivyo aliwataka watanzania na wenye viwanda kutokuwa na wasiwasi kwani Serikali ina nia njema ya kuwaletea maendeleo wananchi hususan kupitia sekta ya kilimo cha korosho.

“Wakulima wa Korosho wanatakiwa kumshukuru Rais Magufuli kwa uamuzi wake ambao unalinda maslahi ya mkulima na umewawezesha kuuza korosho zao kwa faida. Nawakaribisha wafanyabiasha makini kuja nchini kwani Serikali ipo tayari kuwasikiliza watu wa aina hiyo na kufanya nao biashara” alisema Kakunda.

Kwa upande wake, Bashungwa alieleza kuwa katika msimu wa korosho wa mwaka 2018/2019 tayari zimekusanywa tani 213,159 ambazo kati ya hizo tani 126,194 zimehakikiwa na tayari wakulima wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani wamelipwa fedha zao kwa zaidi ya asilimia 95.5. Bashungwa aliongeza kuwa, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha Wakulima wote kulipwa fedha zao hadi kufikia tarehe 05 Februari 2019.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Balozi wa Kenya nchini, Kazungu alisema kuwa kusainiwa kwa mkataba huo ni faraja kubwa kwake katika historia ya mahusiano kati ya Tanzania na Kenya ambayo yanaendelea kuimarika siku hadi siku. Aidha, alieleza kuwa mkataba huo ni mfano mzuri wa kuimarika kwa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hususan katika masuala ya kilimo na biashara.

Kwa upande wake, mnunuzi wa korosho hizo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Indo Power Solutions, Bw. Mutembei alisema amekuja kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kumwinua mkulima wa Tanzania na kwamba anawataka wale wote wanaobeza jitihada hizo za Rais Magufuli kuacha mara moja huku akilaani kitendo cha baadhi ya wafanyabiashara kuendelea kuwakandamiza wakulima kwa kununua mazao yao kwa bei ndogo wanazopanga wao huku wakijua wazi kuwa wakulima hao wametumia gharama kubwa katika uzalishaji wa mazao hayo.

Pia aliwataka wafanyabiashara kufuata taratibu na sheria katika kufanya biashara kama Serikali zinavyoelekeza na kuacha kuchanganya biashara na siasa.

Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Nafaka, Dkt. Mansoor alieleza kufurahishwa na tukio hilo ambalo limekuja wakati mwafaka wakati nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikijiandaa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi utakaofanyika jijini humo hivi karibuni. Aidha alisema kuwa, kwa kiasi kikubwa tukio hilo limeiinua Bodi yake na kwamba anatoa wito kwa wafanyabiasha wengine wa ndani na nje ya Tanzania kuja nchini na kushirikiana na Bodi hiyo ili kuwakomboa wakulima wengi Zaidi.

Mkataba huo umesainiwa wakati baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Tanzania wakiwa jijini Arusha kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 1 Februari 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Taifa ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Dkt. Hussein Mansoor (kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya INDO Power Solutions ya nchini Kenya, Bw. Brian Mutembei (kulia) wakisaini Mkataba wa mauziano ya korosho ghafi kiasi cha tani laki moja kwa malipo ya Shilingii bilioni 418. Wanaoshuhudia tukio hilo muhimu ni Prof. Palamagamba Kabudi (wa pili kushoto), Waziri wa Katiba na Sheria, Joseph Kakunda (kushoto), Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Innocent Bashungwa (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Kilimo na Dan Kazungu, Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa mikutano uliopo Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha tarehe 30 januari 2019. Mawaziri hao wapo jijini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Dkt. Mansoor na Bw. Mutembei wakibadilishana Mkataba huo mara baada ya kusaini 
Prof. Kabudi akizungumza kabla ya kuanza kwa tukio hilo la kihistoria la kusainiwa mkataba wa ununuzi wa tani laki moja za korosho ghafi 
Kakunda nae akizungumza 
Dkt. Bashungwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) 
Balozi wa Kenya nchini, Kazungu akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya kusainiwa mkataba wa ununuzi wa tani laki moja za korosho kutoka Tanzania 
Bw. Mutembei nae akieleza furaha yake katika kukamilisha ununuzi wa korosho kutoka Tanzania 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Joseph Buchweshaija akizungumza kwa ufupi kuhusu hafla hiyo ya uwekaji saini mkataba wa ununuzi wa korosho. Wengine katika picha ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,  Prof. Florens Luoga ( kulia walioketi) akifuatiwa na Prof. Sifuni Mchome, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria na Dkt. Evaristo Longopa, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali 
Mkutano ukiendelea. Kushoto ni Mkurugenzi wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MABALOZI WATATU WAPYA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 31 Januari, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi kutoka nchi 3 ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Balozi wa kwanza kukutana na Makamu wa Rais, alikuwa Mhe. Gaber Mohamed Abulwafa Balozi mpya wa Misri hapa nchini ambaye alifika kwa lengo la kujitambulisha na pia kuzungumzia mambo mbali mbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchini  mbili ambao ulianzishwa na waliokuwa marais wa nchi hizi, Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais Gamal Abdel Nasser Hussein wa Misri.

“Misri itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala ya Elimu, Afya na masuala ya teknolojia ya ujenzi wa miundombinu yenye tija kwa mataifa haya mawili” alisema Balozi huyo.

Mwisho Balozi huyo mpya wa Misri aliahidi kusimamia miradi yote ambayo ipo kwenye makubaliano baina ya Serikali hizi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais alimpongeza na kumkaribisha Tanzania pamoja na kumhakikishia ushirikiano mzuri katika kazi zake akiwa hapa nchini na kumueleza kuwa kwa miaka mingi uhusiano kati ya Misri na Tanzania umezidi kuimarika.

Balozi wa Pili kukutana na kuzungumza na Makamu wa Rais alikuwa Mhe. Francisca Pedros, Balozi mpya wa Spain hapa nchini ambaye Makamu wa Rais alimpongeza kwa kuwa Balozi wa kwanza mwanamke kuteuliwa kuja kuitumikia nchi yake hapa nchini.

Balozi wa Tatu kukutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Makamu wa Rais ni Balozi wa Ethiopia nchini Mhe. Yonas Yosef Sanbe ambaye alimueleza Makamu wa Rais furaha yake ya kuwa hapa na kuona namna mahusiano ya nchi hizi mbili yameboreka ambapo alisema kuwa

“nafarijika kuona namna ambavyo wanawake wanapewa nafasi za juu katika uongozi katika nchi hizi mbili”

Makamu wa Rais pamoja na mambo mengine alimpongeza Balozi huyo wa Ethiopia kwa kuwa Balozi wa kwanza mwenye makazi yake hapa Tanzania.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Mohamed Abulwafa (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi mpya wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Mohamed Abulwafa (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Spain nchini Mhe. Francisca (kushoto) aliyefika kujitambulisha ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi mpya wa Spain nchini Mhe. Francisca Pedros (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi mpya wa Spain nchini Mhe. Francisca Pedros(kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Ethiopia nchini Mhe. Yonas Yosef Sanbe aliyefika kujitambulisha leo Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi mpya wa Ethiopia nchini Mhe. Yonas Yosef Sanbe aliyefika kujitambulisha leo Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS MAZISHI YA MKE WA MUFTI

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mazishi ya mke wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakary Bin Zubeir yaliyofanyika Kwamndolwa, Korogwe mkoani Tanga.

Akitoa salam kwa niaba yake amesema “Rais Dkt. Magufuli aliweka nia ya dhati kushiriki mazishi haya ila kwa bahati mbaya leo ana mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha ambapo yeye ni Mwenyekiti.” 

“Mheshimiwa Rais amenituma nije nikupe pole wewe, watoto, familia na wote walioguswa na msiba huu. Mheshimiwa Rais anawaombea kwa Mungu ili mpate utulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na nguzo katika familia. Haya yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu.”

Waziri Mkuu ameshiriki mazishi hayo ya mke wa Mufti, Bibi Hidaya Omar leo (Alhamisi, Januari 31, 2019).

Kadhalika, Waziri Mkuu amewasihi wafiwa na waombolezaji wote waendelee kuwa watulivu na kumuombea marehemu kila mmoja kwa imani yake ili Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema.

Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum akizungumza kwa niaba ya familia amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumtuma Waziri Mkuu amuwakilishe katika mazishi hayo. Pia amewashukuru watu wote waliojitokeza kwa ajili ya kuifariji familia kutokana na msiba walioupata.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo niWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo, Mhe. Salma Kikwete, Mhe. Hawa Ghasia, Mhe. Mary Chatanda ,Mhe. Mkuu wa Mkoa wa TangaMartine Shigelana Masheikh wa Mikoa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika mazishi ya Hidaya Omar, mke wa Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubier  yaliyofanyika katika kijiji cha Kwamdolwa wilayani Korogwe, Januari 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akishiriki katika sala ya jeneza  wakati wa mazishi ya Hidaya Omar, Mke wa Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubeir  (kushoto kwa Waziri Mkuu) yaliyofanyika katika kijiji cha Kwamdolwa wilayani Korogwe, Januari 31, 2019. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Sheikh Mohammed Kigoda aliyeongoza sala hiyo na kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Alhad Mussa Salum. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubeir  baada ya kushiriki katika mazishi ya Hidaya Omar, mke wa Mufti ,yaliyofanyika  katika kijiji cha Kwamdolwa wilayani Korogwe, Januari 31, 2019. Katikati ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.

TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (rtd) Nicodemus Elias Mwangela amewataka Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) kukamilisha miradi ya ujenzi wanayo pewa ndani ya muda wa makubaliano ya mikataba.

Brig. Jen. (rtd) Mwangela ameyasema hayo jana wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa na ya Katibu ya Katibu Tawala Mkoa kati ya TBA na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.

“TBA mna sifa nzuri ya kujenga majengo ya serikali kwa kuzingatia ubora unaotakiwa na kwa gharama nafuu lakini kuna wakati kunakuwa na kusita katika kuwapa kazi kutokana na historia yenu ya kuchelewesha kukamilisha miradi mnayopewa ya ujenzi”, ameeleza Brig. Jen. (rtd) Mwangela.

Ameongeza kuwa TBA wamechelewesha ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ujenzi wa Hospitali ya Mji wa Tunduma hivyo ucheleweshaji huo usirudie katika mikataba hiyo miwili waliyopewa kwani hatasita kuvunja mikataba hiyo endapo wataonyesha ucheleweshaji.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila ameishukuru serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuupatia Mkoa wa Songwe kiasi cha shilingi bilioni 26.8 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali mkoani hapa.

Kafulila amesema serikali imekuwa ikitoa fedha za miradi mbalimbali lakini kasi ya utoaji wa fedha na matumizi ya fedha hizo kwenye miradi husika imekuwa haiendani na hivyo kusababisha kuchelewa kukamilika kwa miradi hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwa amini na kuwapa miradi hiyo miwili yenye thamani ya shilingi bilioni moja na kuahidi kuikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Mhandisi Cosmas amesema hapo awali walikuwa na changamoto kama vile ukosefu wa maji, umeme na baadhi ya vifaa lakini wamesha zifanyia kazi changamoto hizo hivyo watamaliza miradi hiyo Juni 30, 2019 kama walivyokubaliana katika Mikataba.
 Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila akisaini mikataba ya Ujenzi wa nyumba za Mkuu wa Mkoa na ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, ambapo Wakala wa Majengo (TBA) wamekubali kukamilisha ujenzi huo kwa muda wa miezi mitano na kwa gharama ya shilingi bilioni moja.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila na Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas wakisaini mkataba wa ujenzi wa nyumba za Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa, wa Kwanza Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Rtd) Nicodemus Mwangela.

BODI YA USHAURI NFRA YATEMBELEA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA MKOANI MANYARA, YAMTAKA MKANDARASI KUONGEZA KASI YA UJENZI

0
0
Na Mathias Canal, NFRA-Babati
Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imetembelea eneo la Mradi wa ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa Mkoani Manyara na kuipongeza kampuni ya Unia Araj Realizacje Sp.o.o) chini ya msimamizi wa utekelezaji wa mradi huo ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kasi waliyoanza nayo ya ujenzi.


Kampuni hiyo ambayo imeanza ujenzi huo tarehe 15 Disemba 2018 katika Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara katika kipindi hicho imetekeleza mradi huo kwa kasi nzuri, Imesema Bodi hiyo.


Mradi huo katika Kanda ya Arusha (Babati), pamoja na Dodoma, Makambako, Mbozi, Shinyanga, Songea, Sumbawanga na Mpanda. utagharimu Dola za Kimarekani Milioni 55, ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ikiwa ni sehemu ya kiasi cha milioni 110 kilichotolewa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Akizungumza na mkandari wa mradi huo Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mhandisi Eustance Kangole alisema kuwa kampuni hiyo inapaswa kuongeza kasi zaidi ya ujenzi ili kukamilisha kwa muda uliopangwa.


Alisema kuwa Hifadhi ya Chakula inayohitajika kukidhi mahitaji ya dharula kwa miezi mitatu ni zaidi ya tani 500,000 ukilinganisha na tani 150,000 iliyokuwa inahitajika miaka ya 1992 Wakala ulipoanzishwa.


Pia, technologia ya vihenge itawezesha Wakala kutumia teknolojia ya kisasa na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji, Itawezesha Wakala kuhifadhi chakula kwa muda mrefu Zaidi, itasaidia kupunguza upotevu wa zao la mahindi baada ya kuvuna (posthaverst loss) na kuongeza soko la mahindi nchini na kuimarisha usalama wa nafaka inayohifadhiwa kwa kudhibiti sumukuvu (Aflatoxin) kwa mahindi yaliyohifadhiwa.


Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Eustance Kangole na katibu wake ambaye pia ni Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba imefanya ziara hiyo mara baada ya kikao kazi cha 33 cha Bodi hiyo Jijini Dodoma kilichofanyika kwa lengo la kujadili masuala muhimu ya Wakala ikiwemo utekelezaji wa mkataba wa mauzo ya mahindi Tani 36,000 kwa Shirika la Chakula Duniani (WFP) sambamba na kujadili maendeleo ya Mradi wa Vihenge na Maghala ya kisasa.


Vihenge 8 vinatarajiwa kujenzgwa Kanda ya Arusha katika eneo la (Babati) vyenye uwezo wa kuhifadhi nafaka Tani 25,000 ambapo pia yatajengwa maghala 2 yenye uwezo wa kuhifadhi nafaka Tani 15,000 hivyo kuwa na jumla ya Tani 40,000.


Baada ya mradi kukamilika Wakala utakuwa umeongeza uwezo wa kuhifahi kwa Tani 250,000 zaidi (vihenge vya kisasa 190,000 MT na maghala 60,000 MT) jambo ambalo litakuwa chachu na mafanikio yenye tija katika kuunga mkono Juhudi za utendaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.


Kupatikana kwa Mradi huo nchini ni jitihada za Serikali ambazo zitapelekea ukuaji wa uchumi nchini na kuchangia kuwezesha Tanzania ya viwanda ambapo kutawezesha maghala ya Wakala kuweza kuhifadhi akiba ya Chakula ambayo itaendana na mahitaji halisi ya dharura kulinganisha na ongezeko la watu nchini.


Wajumbe wa Bodi ya ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakikagua eneo la Mradi wa ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa Mkoani Manyara unaojengwa na kampuni ya Unia Araj Realizacje Sp.o.o) chini ya msimamizi wa utekelezaji wa mradi huo ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)





SHISHY BABY AMTOLEA UVIVU DIAMOND, AMTAKA AMUOE ZARI

0
0
UMEMSIKIA alichosema Shishy Baby ? Iko hivi leo bwana amemtolea uvivu msanii maarufu nchini Nasseb Abdull a.k.a Diamond kwa kumwambia ni vema akamuoa Zarinah Hassan a.k.a Boss Lady. 

Shishy amesema hayo leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam baada ya kutakiwa kusalimia wasanii na wageni waalikwa walioko viwanjani hapo. 

“Diamond naomba nikwambie hivi, binafsi natamani sana umuoe Zari…ni mwanamke anayejua kusuka mipango, ni mjasiriamali , ni mbunifu na anao uwezo mkubwa katika mambo ya ujasiriamali. 

“Wakati ule ulivyomuacha Wema na kwenda kwa Zari tukasema sio tatizo.Hivyo nitumie nafasi hiii kukuomba leo kuwa natama umuoe Zari maana huyu anakufaa sana,”amesema Shishy Baby. 

Hata hivyo Shishy Baby wakati anaeleza hayo Diamond alikuwa kimya akimsikiliza tu na baada ya kumaliza kuzungumza mshehereshaji wa shughuli hiyo alisema kuwa Shishy alikuwa anatania tu ili kufurahisha wageni waalikwa. 

MTENDAJI MKUU TEMESA AKAGUA MASHINE YA KISASA YA KUKAGUA MAGARI KARAKANA YA MT. DEPOT

0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe (wa pili kushoto) akimpa maelezo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) wakati alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo. Kushoto ni Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe  (wa pili kushoto) wakati alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo ili kurahisisha utendaji kazi. Kushoto ni Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.
Gari linaonekana likiwa limenyanyuliwa juu na mashine ya kisasa (3D Wheel Allignment) tayari kwa kuanza kukaguliwa, mashine hiyo ya kisasa imefungwa katika karakana ya TEMESA Mt. Depot Keko Jijini Dar es Salaam. Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA una mpango wa kufunga mashine nyingine kama hizo katika karakana za mkoa wa Mwanza na Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akikagua maboksi maalumu ya kuhifadhia mtambo wa kuongozea taa za magari (traffic light controller) katika karakana ya Mt. Depot kikosi cha Umeme. Kushoto ni Kaimu meneja wa kikosi hicho Mhandisi Pongeza Semakuwa na wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO - (TEMESA)

MC PILIPILI ASEMA ANAMSUBIRI DIAMOND KISHA ZAMU YAKE

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

MSHEHERESHAJI aliyekuwa kwenye ubora wake kwa sasa nchini Tanzania Emmanuel Mathias a.k.a MC Pilipili amesema kwa sasa anasubiri Nassib Abdull aoe na kisha naye afuatie. 

MC Pilipili amesema anafahamu ‘Caple’inayosumbua nchini Tanzania ni yake na ile ya Diamond. “Nasubiri tu Diamond afanye mambo yake pale Uwanja wa Taifa na baada ya hapo name nifanye yangu. na Diamond. 

MC Pilipili amesema hayo wakati mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla wanaofuatilia nyendo zake wanakumbuka namna ambavyo amemwaga chozi hadharani wakati anamvisha pete ya uchumba mpenzi wake. 

MAKONDA AWACHANA ‘LIVE’ WASANII KISA... STEVE NYERERE

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

AMEWACHANA!Ndivyo unavyoweza kuelezea kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda baada ya kuamua kuwachana ‘Live’ baadhi ya wasanii ambao wanamdharau na kumkejeli Steve Nyerere. 

Akizungumza leo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam Makonda amesema wasanii ni vema wakajenga tabia ya kuheshimiana.”Nimeamua kukutana na wasanii na nikamuomba Steve Nyerere anisaidie kuwaambia lakini baadhi yenu mnasema Steve ndio nani. 

“Mbona mnapokua na matatizo yenu au mnapopatwa na misiba mnamwambia Steve Nyerere aje kwangu aniambie.Tuheshimiane hata kama tulisoka wote lakini hatufanani , hivyo lazima tujenge kuheshimiana,”amesema Makonda. 

Makonda hakusita kuwaambia wasanii hao kuwa kuna baadhi yoa hata wanapokamatwa wanaomba msaada wa Steve Nyrere afikishe ujumbe kwake na leo hii anamuomba amsaidie kuwaambia anataka kukutana na wasanii wanamkejeli. 

Makonda amesema kwake yeye hana msanii mkubwa wala mdogo na hivyo ataamua tu amtumie msanii gani kwenye jambo la aina gani. “Kwangu wasanii wote mnayo nafasi sawa, asitokee mmoja wenu akajiona kwanu anayo nafasi kubwa kuliko mwingine.Ndio maana nasema kila mmoja amheshimu mwenzake na kujenga utamaduni wa kupenda ili mambo yaende,”amesema Makonda. 

Ametumia nafasi hiyo kuwahamiza wasanii kuwa wamoja kwani kinyume na hapo hakuna ambacho watafanikiwa.”Naomba muwe wa moja na nitafurahi mkiwa wamoja na kujadili mambo yenu. Acheni majungu.” 

Pamoja na mambo mengine Makonda ametumia nafasi hiyo kuelezea mikakati mbalimbali ambayo ameipanga kwa ajili ya kuwainua wasanii huku akiwataka kuangalia namna ya kutatua changamoto ambazo zinawakabili wasanii. 

Pia Makonda amewataka wasanii wa fani zote kujitathimini na kutambua thamani yao ili kuondoa malalamiko yaliyopo kabla na maada ya kufanyika kwa chaguzi mbalimbali nchini. 

Pia amesema ni wakati sahihi wa kuangalia suala la bima ya afya kwa wasanii na kutumia nafasi hiyo kuwaleza lengo la kukutana nao ni kutaka kuwasikiliza zaidi wao ili kuwa na ukurasa mpya wa wasanii wa tasnia zote. 


KHADIJA KOPA AMWAMBIA MAKONDA WANAMUZIKI WA TAARAB HAWATHAMINIWI…ATOA NENO

0
0

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii 

MWANAMUZIKI  maarufu katika Muziki wa Taarab nchini Khadija Kopa amesema anasikitishwa na kitendo cha wasanii wa muziki huo kutopewa kipaumbele kama ilivyo kwa wasanii wengine wakiwamo wa Bongo Fleva na waigizaji filamu. 

Kopa amesema hayo leo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam baada ya Makonda kuamua kukutana na wasanii wa fani mbalimbali. 

“Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam naomba niseme umenigusa sana kwenye hili la wasanii kuwa wamoja. Ni jambo muhimu kwa wasanii kuwa na umoja imara.Umoja ambao unazungumziwa uwe wa wasanii wote bila ya kuwapo ubaguzi. 

“Nitoe kilio changu hasa kwa Serikali, wanamuziki wa taarab wanakufa lakini hakuna hata ushiriki wa Serikali wakati akitoa msanii wa muziki wa Bongo Fleva au waigizaji wa filamu wanathaminiwa na tunaona.Hivyo nitoe rai nasi tunastahili kuthaminiwa na kushirikishwa katika mambo mbalimbali,”amesema Kopa. 

Amefafanua anashindwa kuelewa namna ambavyo jamii inawachukulia wanamuziki wa taarabu nchini”Sijui wanamuziki wa taarab tunaonekana ni watu maskini sana au sijui kuna nini?Tunastahili kuthaminiwa.” 

MSANII BI KIDIDE ATOA OMBI KWA RC MAKONDA

0
0

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii 

MSANII Bi Kidide amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwa amekuwa katika sanaa kwa zaidi ya miaka 25 lakin hakuna ambacho amenufaika nacho na hivyo anamuomba amsaidie. 

Ametoa kauli hiyo leo wakati Makonda alipokutana na wasanii wa fani mbalimbali kwa lengo la kujadiliana nao mambo mbalimbali yanayohusu sanaa. 

“Mkuu wangu wa Mkoa wa Dar es Salaam naomba nikwambie tu nipo kwenye sanaa kwa miaka 25 sasa lakini hakuna ambacho nimenufaika nacho.Naomba unisaidie name mambo yawe sawa,”amesema Bi. Kidide. 

Bi Kidide pia amemuomba Makonda kuhakikisha wasanii wanapata bima ya afya ambayo ni muhimu kwa wasanii wa tasnia mbalimbali.

NYOSHI EL-SAADAT , PATCHO MWAMBA WAOMBA WAWE RAIA WA TANZANIA

0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

WANAMUZIKI wa dansi wenye uraia wa nchi ya Congo ambao wapo nchini Tanzania wameomba wapatiwe vibali vya uraia kwani wameka nchini kwa muda mrefu. 

Wametoa ombi hilo kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaa Paul Makonda ambaye aliamua kukutana na wasanii wa tasnia mbalimbali kuzungmza nao na kusikia changamoto zinazowakabili. 

Mwanamuziki maarufu katika muziki wa dansi nchini Nyoshi El-Saadat amesema amekuwa nchini Tanzania kwa miaka 25 sasa lakini bado wanaendelea kusumbuliwa na imefika mahali wanajificha juu ya dali. 

“Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tunaomba utusaidie kwenye hili la uraia.Tunaomba tuwe raia wa Tanzania, ni nchi ambayo tumeishi miaka mingi.Mimi nipo Tanzania kwa zaidi ya miaka 25 , nimebahatika kupata watoto 12, sasa leo hii naenda wapi zadi ya kubaki katika nchi nzuri ya Tanzania,”amesema Nyosh-Elsaadat 

Kwa upande wake mwanamuziki na mugizaji wa filamu nchini Patcho Mwamba ametoa ombi kwa Makonda la kutaka aangalie namna ya kuwasadia wapate uraia wa Tanzania. 

“Tunakuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda utusaidie kwenye hili la uraia.tupo nchini kwa muda mrefu tukiendelea na maisha yetu. “Nikienda Congo nikikaa siku tatu tu au wiki moja narudi nchini Tanzania.Kule Congo tulikuwa tunakula mbwa, hivyo sitaki tena kula mbwa.Tusaidie kwenye suala la uraia mkuu wetu wa mkoa,”amesema Patcho Mwamba. 

Wakati huo huo wanamuziki hao wamezungumzia kushuka kwa mapato kutokana na shughuli za muziki kuzuiliwa kwa kupiga mwisho saa sita usiku. Wasema wategemea muziki kuishi na kuendesha maisha yao kupitia muziki wa dansi na wanasomesha watoto pamoja na maisha mengine.


SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)

0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani alipomtembelea leo tarehe 31 Januari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Katikati ni Meneja Masoko na Utafiti Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndg. Itandula Kambalagi.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani alipomtembelea leo tarehe 31 Januari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulid Banyani (wa pili kulia) walipomtembelea leo tarehe 31 Januari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MAKONDA AWACHANA ‘LIVE’ WASANII KISA... STEVE NYERERE

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

AMEWACHANA!Ndivyo unavyoweza kuelezea kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda baada ya kuamua kuwachana ‘Live’ baadhi ya wasanii ambao wanamdharau na kumkejeli Steve Nyerere. 

Akizungumza leo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam Makonda amesema wasanii ni vema wakajenga tabia ya kuheshimiana.”Nimeamua kukutana na wasanii na nikamuomba Steve Nyerere anisaidie kuwaambia lakini baadhi yenu mnasema Steve ndio nani. 

“Mbona mnapokua na matatizo yenu au mnapopatwa na misiba mnamwambia Steve Nyerere aje kwangu aniambie.Tuheshimiane hata kama tulisoka wote lakini hatufanani , hivyo lazima tujenge kuheshimiana,”amesema Makonda. 

Makonda hakusita kuwaambia wasanii hao kuwa kuna baadhi yoa hata wanapokamatwa wanaomba msaada wa Steve Nyrere afikishe ujumbe kwake na leo hii anamuomba amsaidie kuwaambia anataka kukutana na wasanii wanamkejeli. 

Makonda amesema kwake yeye hana msanii mkubwa wala mdogo na hivyo ataamua tu amtumie msanii gani kwenye jambo la aina gani. “Kwangu wasanii wote mnayo nafasi sawa, asitokee mmoja wenu akajiona kwanu anayo nafasi kubwa kuliko mwingine.Ndio maana nasema kila mmoja amheshimu mwenzake na kujenga utamaduni wa kupenda ili mambo yaende,”amesema Makonda. 

Ametumia nafasi hiyo kuwahamiza wasanii kuwa wamoja kwani kinyume na hapo hakuna ambacho watafanikiwa.”Naomba muwe wa moja na nitafurahi mkiwa wamoja na kujadili mambo yenu. Acheni majungu.” Pamoja na mambo mengine Makonda ametumia nafasi hiyo kuelezea mikakati mbalimbali ambayo ameipanga kwa ajili ya kuwainua wasanii huku akiwataka kuangalia namna ya kutatua changamoto ambazo zinawakabili wasanii. 

Pia Makonda amewataka wasanii wa fani zote kujitathimini na kutambua thamani yao ili kuondoa malalamiko yaliyopo kabla na maada ya kufanyika kwa chaguzi mbalimbali nchini. 

Pia amesema ni wakati sahihi wa kuangalia suala la bima ya afya kwa wasanii na kutumia nafasi hiyo kuwaleza lengo la kukutana nao ni kutaka kuwasikiliza zaidi wao ili kuwa na ukurasa mpya wa wasanii wa tasnia zote.

DIAMOND AWAONYA WASANII WANAOTOA RUSHWA WASIKIKE

0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii. 

MSANII maarufu katika muziki wa kizazi kipya nchini Nasseb Abdull a.k.a Diamond ameahidi kuwasaidia wanamuziki wa taarab nchini huku akitoa onyo kwa wale wasanii ambao wanatoa fedha ili nyimbo zao zipigwe kwenye redio na Televisheni ya Wasaf. 

Diamond ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza mbele ye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye ameamua kuwaita wasanii wa tasnia mbalimbali kuzungumza nao. 

Amesema amesikia anatambua nafasi ya wasanii kushirikiana na kusaidiana katika kuhakikisha kazi zao za sanaa zinasonga mbele, hivyo ametumia nafasi hiyo kuahadi nyimbo za taraab kupigwa kwenye Redio ya Wasaf pamoja na Wasaf TV. 

“Nimesikia mama yangu Khadija Kopa amezungumzia kuhusu muziki wa taarab, naomba nimwambie nyimbo za taarab tutazipiga bila tatizo lolote, tunaomba watuleteee tu. 

“Pia naomba niseme hapa kuna wasanii ambao wanatoa fedha Wasaf ili nyimbo zao zipigwe.Hili sitaki kuona likienda na msanii nikisikia analeta fedha kwa ajili ya nyimbo yake ipigwe nitamfungia,”amesema Diamond. 

Amefafanua lengo la kuanzisha Wasafi TV na Wasaf FM ni kuwasaidia wasanii wote na hivyo hataki kusikia habari ya msanii kutoa rushwa ili nyimbo zake zipigwe.

MAKONDA BWANA…AWAPA MBINU NYOSH EL-SAADAT, PATCHO MWAMBA WAKITAKA KUWA WATANZANIA

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewapa mbinu wanamuziki Nyoshi El-Saadat na Patcho Mwamba namna ya kufanya ili wawe raia wa Tanzania. 

Makonda ametoa kauli hiyo leo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam baada ya wanamuziki hao kutoa ombi mbele yake kuwa wanaomba kuwa raia wa Tanzania kwani wamekaa muda mrefu. 

Amesema amesikia ombi la wanamuziki hao lakini ili waweze kuupata uraia ni vema wakaandika maombi maalumu kwenye baruana kisha kuiwasilisha katika mamlaka husika ili kuondokana na changamoto ya kuishi maisha ya kujificha. 

“Niwaombe wanamuziki Nyoshi El-Saadat na Patcho Mwamba andekeni barua kwa kutaja majina yenu, mnakoishi na kazi ambayo mnafanya kisha leteni.Mkifanya ivyo itakuwa rahisi kupata uhalali wa maombi yenu kushughulikiwa. 

“Mnapoishi kwa kujificha maana yake msababisha hata watoto wenu nao kuishi kwa kujificha jambo ambalo kwangu naona si nzuri sana.Andikeni barua ambayo itaweka kila kitu kuhusu ninyi,naamini mtafanikiwa tu,”amesema Makonda. 

Kabla ya Makonda kutoa maelekezo hayo kwa wanamuziki hao ambao ni raia wa Congo lakini wamekuwepo nchini Tanzania kwa muda mrefu, waliamua kutoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa huo kuwa wapo nchini kwa miaka mingi lakini changamoto kubwa iliyopo ni aina ya maisha ya kujifichaficha ambayo wanaishi.

MFUMO MBOVU WA KUUZA KAZI ZA FILAMU WAMKERA WEMA SEPETU

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

STAA mwenye umaarufu wake katika tasnia ya uigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu ametoa ombi la kuwepo kwa soko la uhakika la kuuza kazi zao za filamu. 

Wema ametoa amesema hay oleo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda baada ya kuwaita wasanii wa fani mbalimbali kukuta naye ili kusikiliza changamoto za wasanii. 

Amesema changamoto kubwa ambayo inawakabili waigizaji wa filamu ni kutokuwa na soko maalumu kwa ajili ya kuuza kazi zao na kwamba eneo hilo likipatiwa ufumbuzi wataifanya kazi hiyo ya sanaa kwa uhuru. 

“Tunaomba Mkuu wa Mkoa utusaidie kupata mfumo ambao utatuwezesha kuuza zetu bila kuwepo kwa matatizo.Kwa sasa ni changamoto ni nyingi kiasi cha kukatisha tamaa.Hivyo natumai utatusaidia katika kutatua changamoto ya mfumo wa uuzaji wa kazi za filamu,”amesema Wema. 

Wema wakati anazungumzia changamoto ya soko la filamu nchini ,Makonda alikuwa akiliza kwa makini na wakati anajibu kuhusu ombi la muigizaji huyo ameahidi kutafuta umbuzi. Makonda aliamua kuwaita wasanii wa tasnia mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha anasikiliza changamoto za wasanii hao na kisha kuzitafutia ufumbuzi wake.

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images