Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

MWEZI WA RAMADHANI SABABU YA AFCON 2019 KUSOGEZWA MBELE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF limetoa taarifa ya kusogeza  mbele tarehe ya kuanza kwa michuano ya  Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2019 yatakayofanyika nchini Misri;..

Hatua hii inakuja baada ya Shirikisho hilo kutaarifiwa na waandaaji wa michuano ya AFCON , Misri, kwamba tarehe iliyopangwa awali inaingiliana na mwezi wa mtukufu wa Ramadhan hivyo inaweza kuathiri viwango vya wachezaji wa kiislam,  Mwezi mtukufu wa Ramadhani unatarajiwa kuanza Jumapili ya Mei 5 na kukamilika Jumanne ya Juni 4,

Awali, AFCON 2019, ilipangwa kuanza Juni 14 na kumalizika Julai 13 lakini sasa imesogezwa mbele kwa takribani wiki moja, ambapo itaanza Juni 21 na kumalizika Julai 19.

CAF imeripoti kwamba droo ya michuano hiyo ya kwanza kabisa kushirikisha timu 24, itafanyika xcsdAprili 12 mwaka huu, majuma machache baada ya mechi za mwisho za kufuzu zitakazofanyika mwezi Machi.

Misri ilipata haki ya kuandaa michuano hiyo baada ya waandaaji wa awali, Cameroon kushindwa kuiridhisha CAF kwa maandalizi yake.

WASANII JISAJILINI MPATE HAKI ZENU ZA MSINGI-BASATA

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Arusha. 

Wito umetolewa kwa wasanii nchini kujisajili katika Baraza na sanaa nchini ili waweze kutambulika, kupata haki zao msingi, na wawe na uhuru wa kufanya kazi

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Katibu wa Shughuli za Sanaa Kanda ya Kaskazini Flora Mgonja ambapo amewataka wasanii kufahamu kuwa sanaa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na wanatakiwa kuithamini, kuipenda na kuilinda

Amesema sheria namba 23 ya mwaka 1984 iliyoanzishwa kwa mujibu wa Bunge na kanuni mpya ya Februari 2018 inamtambua msanii, inaelezea sababu ya msanii kusajiliwa, pia zimeweka wazi kwamba hakuna msanii yeyote ambae anaweza kufanya kazi zake bila kusajiliwa Basata

Kwa mujibu wa Kanuni za Baraza la sanaa la Taifa, 23-(1)Mtu yeyote hatoruhusiwa kufanya kazi ya sanaa ya aina yeyote kwa mujibu wa sheria inayohusika na sanaa, kufanya biashara ya kazi za sanaa bila kusajiliwa na Baraza

Amesema kuwa Baraza la sanaa la Taifa lipo tayari kuwasaidia pele watakapokuwa wamesajiliwa na kutambuliwa ili kuweza kuwapa huduma kwa mujibu wa sheria na taratibu.'' Tuna dawati la sheria pale ofisini kwetu hawalijui wasanij wengi, wanadhukumiwa mikataba, wanashindwa kupata fidia zao kwasababu hawajasajiliwa, leo unakuja kusema kazi yangu imechukuliwa wakati hujasajiliwa''

Amesema kwa sasa wameanza kutoa elimu kwanza kwa wasanii mbalimbali katika kanda zote sita nchini ambapo kila mmoja wapo anatakiwa kutambua kwamba anatakiwa ajisajili kwenye Baraza la sanaa la Taifa.''Hatuwezi kuwabana tukakimbikia kwenye sheria, tunamuda ambao tumejiwekea kuhakikisha kwamba msanii ajitambue kwamba ni lazima nisa jiliwe kwenye Baraza la sanaa la Taifa"Alisema

Amesema wanapoelekea itafikia mahala ambapo washehereshaji (MC) wote,Dj, kufanya kazi bila kuwa na cheti kutoka Basata kwani wasanii wote wanatakiwa wawepo kwenye Data base.Amewataka kufahamu kuwa kujisajili kwao ni fursa, kwani baraza hilo linanafasi ya kumsaidia msanii pale anapopata mialiko mbalimbali ya kwenda nje ya nchi kufanya matamasha nchi za nje 

Amesema kwa sasa msanii hawezi kupita uwanja wa ndege bila barua kutoka Basata kama anakwenda nje ya nchi kwa mujibu wa kanuni na sheria za Baraza la sanaa la Taifa

'' Lazima msanii apate barua na ada yake ni shilingi 50,000Msanii anapoondoka nchini kwenda nje ya nchi anatakiwa aondoke na kibali kutoka basata ambacho ni shilingi 50,000 akiwa na tatizo lolote nchi husika zinawasikiana lakini akiondoka. Kiholela hawezi kusaidika''alisisitiza

Ameainisha garama za kujisajili kwa msanii ni shilingi 45,000, mchanganuo wake fomu 5000, usajili 20,000, kibali cha mwaka 20,000 ambapo jumla yake ni 45,000 .Sambamba na hayo amesisitiza kuwa usajili kwa msanii binafsi ni mara moja kwa mwaka, ila kibali cha mwaka kinalipiwa kila mwaka mpya unapoaanza.
Mratibu wa shughuli za sanaa Kanda ya Kaskazini Flora Mgonja akiwa katika ofisi ya Utamaduni Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus
Kutoka kulia ni Mratibu wa shughuli za Sanaa Kanda ya Kaskazini (BAATA) Flora Mgonja, akiwa na Msimamizi wa maendeleo ya sanaa Kanda ya Kaskazini - BASATA. Picha na Vero Ignatus
Kutoka kulia ni Afisa michezo na Utamaduni Jiji la Arusha Benson B. Maneno, Mratibu wa shughuli za sanaa Kanda ya Kaskazini (BASATA) Flora Mgonja na Msimamizi wa maendeleo ya sanaa Kanda ya Kaskazini -BASATA

BIKOSPORTS YAWAKABIDHI KOCHA ZAHERA NA MAKAMBO KUTOKA YANGA TUZO ZAO

$
0
0

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya BikoSports  kupitia kwa afisa uhusiano wao Geof Lea,leo  imekabidhi tuzo kwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera na mshambuliaji wa timu hiyo Heritier Makambo ambao walikuwa wameshinda tuzo hizo.

Makambo na alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba 2018 wakati kocha Mwinyi Zahera alifanikiwa kushinda tuzo ya Kocha Bora wa mwezi huo huo Disemba ikiwa ni mara ya tatu anashinda tuzo hiyo.

Shirikisho la soka Tanzania TFF liliingia mkataba wa udhamini na kampuni ya BikoSports kwa ajili ya kutoa zawadi na tuzo kwa washindi wa mchezaji bora wa mwezi na kocha bora sambamba na zawadi ya Tsh Milioni 1 kila mmoja kwa kipindi chote cha msimu wa Ligi Kuu 2018/2019 kilichosalia.


Msemaji wa bikosports Tanzania, Geoffrey Lea picha ya kwanza akikabidhi tuzo kwa mchezaji bora wa mwezi Desemba Elichia Makambo.
Msemaji wa bikosports Tanzania, Geoffrey Lea akimkabidhi tuzo kocha bora wa mwezi Desemba,Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera zinazodhaminiwa na Bikosports.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera (kulia) na mchezaji bora wa mwezi Desemba Elichia Makambo wakiwa katika picha ya pamoja.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera akifanya mahojiano na baadhi ya waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa tuzo yake kama kocha bora wa mwezi Desemba zinazodhaminiwa na Bikosports.

CCM Z’BAR YATOA VIFAA TIBA KWA HOSPITALI YA KIVUNGE

$
0
0

MWENYEKITI wa Kikundi cha Hamasa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Ndugu Shaaban Ali Othman (kushoto) akimkabidhi Daktari dhamana Tamim Hamad Said(kulia) Friji mbili za kuhifadhi dawa za hospitali zilizotolewa na kikundi cha hamasa cha vijana wa Afisi Kuu CCM Zanzibar.

MWENYEKITI wa Kikundi cha Hamasa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Ndugu Shaaban Ali Othman (wa pili kushoto) akizungumza mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja, Daktari dhamana Tamim Hamad Said (wa kwanza kushoto) pamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Haji Machano Juma(wa kwanza kulia) wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba vilivyotolewa na kikundi cha hamasa.


BAADHI ya vijana wa kikundi cha hamasa cha Afisi Kuu ya CCM Zanzibar wakisikiliza kwa makini nasaha za viongozi mbali mbali wa CCM, UVCCM na Hospitali ya Wilaya Kivunge katika hafla ya makabidhiano ya Vifaa Tiba iliyofanyika leo Tarehe 30/01/2019.(PICHA NA IS-HAKA OMAR


………………………….

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

VIJANA mbali mbali nchini wameshauriwa kuendeleza utamaduni wa kujitolea katika kuisaidia jamii katika masuala mbali mbali ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kimaendeleo.

Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Kikundi cha Hamasa cha Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Ndugu Shaaban Ali Othman wakati akikabidhi Friji(Jokofu) mbili zilizotolewa na kikundi hicho na kukabidhi Uongozi wa Hospitali ya Kivunge ya Wilaya Kaskazini ‘A’ Unguja.

Amesema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kusaidia uhifadhi wa vifaa tiba vya hospitali hiyo hasa dawa za matumizi ya binadamu zinazohitaji hali ya baridi muda wote.

Ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuvitunza na kuvitumia katika matumizi yaliyokusudiwa ili vitoe huduma endelevu kwa wananchi mbali mbali wanaofika hopitalini hapo kwa ajili ya matibabu.

Pamoja na hayo amebainisha kuwa vifaa hivyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na viongozi wa CCM ambao ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wanaotekeleza kwa kasi mipango ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi wote.

Ameeleza kwamba vijana nchini wana wajibu wa kutekeleza kwa vitendo masuala mbali mbali ya kijamii kwa lengo la kuwasaidia wananchi wanaokabiliwa na changamoto katika mazingira wanayoishi.

Katika maelezo yake Mwenyekiti huyo Shaaban,amesema endapo vijana wa Zanzibar wataweka mbele dhana ya uzalendo,umoja, mshikamano na kuelekezana mambo mema ya kuisaidia jamii, itasaidia Zanzibar kuwa nchi bora zaidi duniani iliyopiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Awali Katibu wa Kikundi hicho cha Hamasa, Suleiman Mohamed Rashid amefafanua kuwa kikundi hicho kitaendelea kusaidia masuala mbali mbali ya kijamii katika maeneo mbali mbali yaliyopo katika Wilaya zote za Unguja na Pemba. Amesema Chama Cha Mapinduzi kipo mstari wa mbele kushughulikia changamoto zinazoikabili jamii katika maeneo ya mijini na vijijini.

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Daktari Dhamana wa Hospitali hiyo Tamim Hamad Said, amesema uongoizi wa hospitali hiyo umefurahi kupokea vifaa hivyo kwani vilikuwa ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya taasisi hiyo.

Dr.Tamim ameahidi kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa hasa kuhifadhi dawa na vifaa mbalimbali vinavyotumika katika matibabu ili wananchi wapate huduma bora za Afya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ndugu Pandu Salum Sungura amesema vijana wa mkoa huo wapo imara katika kuunga mkono juhudi za vijana wenzao wa kikundi cha hamasa kutoka Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, kilichoonyesha mfano bora wa kutoa vifaa hivyo kwa hospitali ili viwasaidie wananchi wa Mkoa huo.

Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, Katibu Msaidizi wa Taasisi hiyo Ndugu Khamis Salum Abdi amesema Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kusimamia na kutekeleza Ilani yake ya Mwaka 2015/2020 kwa ufanisi mkubwa kwa lengo la kumaliza kero zinazoikabili jamii.

Amesema suala la kuwapelekea wananchi maendeleo halina itikadi za kisiasa hivyo kila mwananchi, kikundi pamoja na taasisi yoyote wana wajibu wa kutatua changamoto za wananchi.

KADETFU NA BUKOBA DC WAINGIA MAKUBALIANO RASMI YA KUFANYA KAZI PAMOJA

$
0
0
 
Anaandika Abdullatif Yunus - Kagera.

Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Kagera Development and Credit Revolving Fund (KADETFU) lenye Makao Makuu yake Manispaa ya Bukoba, limeiingia makubaliano rasmi na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ya kufanya pamoja Shughuli mbalimbali za Kimaendeleo kwa Kushirikiana pande zote mbili.

Hapo awali KADETFU wamekuwa wakifanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kwa ushirikiano mkubwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwa Muda mrefu pasina kuwepo Mkataba wa Maelewano, licha ya kuwa shughuli hizo zikiwemo za Kijamii zimekuwa zikifanikiwa kwa kiwango Kikubwa kama yalivyo matarajio yao.

Miongoni mwa shughuli zilizotekelezwa na KADETFU kwa kushirikiana na Halmashauri ya Bukoba ni pamoja na Kujengeana uwezo Kati ya Wataalamu wa pande zote mbili (KADETFU na Halmashauri), kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali, kusaidiana katika shughuli za Kazi, Kuwajengea wananchi uwezo katika masuala ya mipango na bajeti, Masuala ya Upashanaji Habari, Ununuzi wa mashine ya Kusaga iliyopo katika Kata ya Rubale, ununuzi wa Injini ya gari la Halmashauri, kuibua miradi n.k

Hata hivyo kwa Mkataba waliokabidhiana Januari 30, 2019 mbele ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani, mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Madiwani, una lenga kuendelea kushirikiana kwa pande zote mbili katika Miradi ya Utawala Bora na Uwajibikaji, kujenga uwezo kwa Kamati za Kata kwa kutafuta Wafadhili wa Kuendesha semina kwa Wafanyakazi na watumishi, lakini pia kuanzisha Mradi wa pamoja wa Kulinda haki za watoto wa kike katika masuala ya mimba za utotoni, ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia n.k ambapo mradi huu unatarajiwa pia kulishirikisha Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la jinsia.

Itakumbukwa pia KADETFU chini ya ufadhili wa Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS), wametekeleza Mradi wa Ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa Jamii (UUJ) katika sekta ya Elimu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, lengo hasa likiwa ni kuwawezesha Wananchi kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ya Elimu katika maeneo yao, mradi ulioanza Julai hadi Desemba 2018.
 Mkurugenzi wa Shirika la KADETFU  Bwana. Yusto Muchuruza na Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Bukoba Mheshimiwa Murshidi Ngeze, wakikabidhiana Mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi pamoja kati ya Kadetfu na Halmashauri hiyo Januari 30, 2018 katika Ukumbi wa Chemba.
 Bwana Yusto Mchuruza Mkurugenzi wa KADETFU akitoa maelezo machache kabla ya Kukabidhiana mkataba kati ya KADETFU na Halmashauri ya Bukoba wa kushirikiana kufanya Shughuli mbalimbali kwenye Halmashauri hiyo.
 Wajumbe wa Kamati ya Ufatiliaji wa uwajibikaji  wa watumishi wa umma, wakizungumza na Mkuu wa shule ya Msingi ya Ntoma iliyopo Kata Kanyangereko Wilayani Bukoba, juu ya Matumizi ya fedha za Shule hiyo.
 Afsa Mipango wa Wilaya ya Bukoba Bwana Julian Tarimo akitoa semina elekezi kwa wafanyakazi wa KADETFU katika maana ya ushirikiano uliopo kati ya pande zote mbili.

WAZIRI UMMY ATOA MABATI 200 KUSAIDIA UJENZI SHULE TANO ZA SEKONDARI JIJINI TANGA

$
0
0

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Mabati 200 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Mabati 200 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Hamis Mkoba
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Mabati 200 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Hamis Mkoba
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Mabati 200 Naibu Meya wa Jiji la Tanga Mohamed Haniu baada ya kumkabidhi Mkurugenzi wa Jiji hilo Daudi Mayeji

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya kukabidhi mabati 200 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule tano Jijini Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa





WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametoa mabati 200 yenye thamani yash.milioni 4.2 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule tano za Sekondari Jijini Tanga.

Halfa ya makabidhiano hayo yalifanyika mjini Tanga kwenye shule ya Msingi Mwakidila ambapo Mkurugenzi wa Jiji hilo alipokea mabati hayo ikiwa ni mkakati wa Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga kusaidia kuondosha changamoto ya uhaba wa madarasa.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi mabati hayo, Waziri Ummy aliwashauriwa wazazi na walezi kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya watoto wao jambo ambalo linaweza kuwasaidia kufanya vizuri kwenye masomo yao.

“Ndugu zangu wazazi na walezi hakikisheni mnafuatilia maendeleo ya watoto wenu wanapokuwa shuleni kwani nyie pia mnaweza kuchangia ufaulu wa mtoto wako “Alisema. idha pia Waziri Ummy amehaidi kuchangia ujenzi wa madarasa kwenye shule ya Sekondari Kange ili kuchochea ukuaji wa sekta ya elimu kwa mkoa wa Tanga .

“Lakini pia niwashukuru watendaji wa Shirika la Tawode kwa kujitoa katika kuchangia maendeleo ya Jamii ya Tanga kwa kutafuta wafadhili mbalimbali wa ndani na nje ya mkoa huu”Alisema 

WANANCHI,SERIKALI WAONDOA CHANGAMOTO WANAFUNZI WA SEKONDARI KUTEMBEA UMBALI MREFU KATA YA OLDONYOWASI

$
0
0
Na Woinde Shizza ,Globu ya jamii Arusha

WANAFUNZI ambao wamemaliza masomo elimu ya darasa la saba mwaka 2018 na kufanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari wanaoishi Kata ya Odonyowasi katika Halmashauri ya Arusha, wameepukana na adha ya kutembea umbali mrefu baada ya Serikali  kuwapangia Sekondari ya Oldonyowasi ambayo ni
mpya na ipo ndani ya kata hiyo.

 Kabla ya kukamilika kwa sekondari hiyo wanafunzi wanaosoma masomo ya sekondari kutoka ndani ya kata hiyo walikuwa wakitembea umbali wa kilometa 16 kwenda na kurudi shuleni katika Shule ya Sekondari ya Oldonyosambu.Umbali huo ulikuwa changamoto kubwa kwa wanafunzi ikiwemo ya wengi wao kutofanya vizuri kwenye masomo na wengine kuacha shule.

Hivyo wazazi, walezi na wananchi wa Kata hiyo waliweka mkakati kuhakikisha wanaondoa changamoto hiyo ya wanafunzi kutembea umbali mrefu.Waliamua kuchangishana fedha pamoja na kuomba msaada wa wadau wa maendeleo wakiwamo TANAPA na Serikali kupitia mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Akizungumza leo Januari 30, 2019, Mwenyekiti wa Kijiji cha Oldonyowas Geophray Ayoa amesema ujenzi wa sekondari hiyo mpya ya Oldonyowas, ulianza mwaka 2018 baada ya wazazi kukerwa na changamoto  zinazowakabili watoto wao, hasa ya kutembea umbali mrefu kwenda kupata elimu ya sekondari. "Ujenzi ulianza kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na TANAPA kwa kujenga vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu na vyoo pamoja na samani za ofisi na za madarasa kwa gharama ya Sh.milioni 70 huku TANAPA wakitoa Sh.milioni 50 na wananchi Sh.milioni 15,"amesema.

Aidha ameipongeza Serikali kupitia mradi wa TASAF awamu ya III,  kwa kuunga mkono juhudi za wananchi wa Oldonyowas,  kwa kuongezea nguvu na  kufanikiwa kujenga vyumba viwili vya madarasa na ofisi ndogo ya walimu, nyumba ya walimu yenye sehemu mbili (2 in 1), vyoo na jengo la utwala pamoja
na kununua  samani za ofisi na madarasa.Jumla ya Sh.milioni 229.4 zimetumika."Tayari imeanza kupokea wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza."

Pia amesema wananchi wa Oldonyowas wamekwenda mbali zaidi na kukusanya nguvu na kujenga jengo la  maabara za masomo ya Sayansi, jengo lililogharimu Sh.milioni 45 ambapo wananchi wamechangia Sh.100,000 kwa kila familia na kwamba jengo lipo hatua za umaliziaji.

Papmoja na kuishukuru Serikali kupitia TANAPA na mradi wa TASAF kwa kusaidia ujenzi sambamba na kukamilisha usajili, amewashukuru  wananchi wa Oldonyowas kwa kuchangia maendeleo ndani ya kata yao,  pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kutoa elimu bila malipo mpaka
kidato cha nne, fursa inayowawezesha watoto wengi kuendelea na shule pindi wanapomaliza elimu ya msingi. 
Sehemu ya picha ikionesha Vyumba viwili vya madarasa na ofisi ndogo ya walimu, jengo linalojengwa na wananchi kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Taifa - TANAPA.
 Picha ikionesha wanafunzi wa shule ya Oldonyowas wakiwa darasani

TAFITI ZABAINI ASILIMIA 72 VIFO VYA MIFUGO HUSABABISHWA NA MAGONJWA MBALIMBALI

$
0
0
Woinde Shizza Globu  ya jamii Arusha

TAFITI zinaonesha kuwa asilimia 72 ya vifo vya mifugo nchini, hutokana na magonjwa mbalimbali yakiwamo magonjwa yanayotokana na kupe na ndorobo, na kulisababishia taifa hasara ya Sh.bilioni 63 kwa mwaka huku takribani asilimia 70 ya ndama wanaozaliwa hufa kila mwaka kutokana na wafugaji walio wengi kutokuwa na muamko wa kuogesha mifugo yao.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Arusha , Dk.Wilson Mahera  wakati wa kukabidhi za viuatilifu vya kuua wadudu na  dawa ya kuogeshea mifugo.Baadhi ya viuatilifu ni vya kuulia wadudu aina ya kupe, mgao huo ni kutokana na mpango wa Serikali ya Awamu ya tano wenye lengo la kuhamasisha wafugaji kuogesha mifugo yao ili kuwa na ufugaji wenye tija.

Amesema neema hiyo kwa wafugaji imetokana na  Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoa jumla ya lita 75 za viuatilifu aina ya 'Paranex' yenye kiini cha 'Alphacypermethtrin yenye uwezo wa kuua wadudu ya kupe kwa ajiki ya wafugaji wa vijiji vitano vya halmashauri ya Arusha."Inaonekana wafugaji hawana mwamko wa kuosha mifugo yao, kupitia Serikali ya Kijiji na  wajumbe wa kamati za uendeshaji majosho, ni vema kukafanyika uhamasishaji ili na usimamizi mzuri ili kila mfugaji anufaike na huduma hii,"amesema Dk.Mahera.

Ili kuzuia vifo hivyo na hasara kubwa inayoligharimu Taifa, Serikali imeanza kuwawezesha wafugaji kwa kutoa dawa za kuogeshea mifugo ili  kuzuia magonjwa yanayoenezwa na kupe, hivyo ni lazima  kuhamasisha wafugaji kuogesja  ng'ombe kupitia majosho yaliyo katika maeneo yao.

Aidha Dk.Mahera amewataka wajumbe wa kamati  hizo kushirikiana na Serikali ya kijiji chini ya usimamizi wa maofisa mifugo wa ngazi zote, kusimamia vema utoaji wa huduma hiyo kwa wafugaji kwa kuhamasisha na kuwahimiza wafugaji kuogesha mifugo yao,  pamoja na kusimamia fedha za mapato na matumizi ili
mradi huo uwe endelevu.

Amefafanua Serikali inatoa dawa hizo kama mtaji wa kuanzia kutoa huduma ya kuogesha mifugo na mapato yatakayopatikana, yatumike kuendeleza huduma hiyo kwa wafugaji katika maeneo yao huku akiwahimiza kushirikiana na Serikali ya Kijiji pamoja na maofisa mifugo katika maeneo yao.

Kwa upande wake Daktari wa mifugo katika Halmashauri ya Arusha Dkt. Linus Prosper ametaja  bei elekezi iliyotolewa na Serikali  ya kuendesha huduma hiyo ya kuogesha mifugo kwa kufafanua bei ya ng'ombe mmoja kwa muosho mmoja ni Sh.50 na kwa mbuzi na kondoo Sh.10 kwa mbuzi na kondoo kwa muosho mmoja.

Pia Serikali Serikali imefafanua gharama hizo zinaweza kubadilika, kulingana na gharama halisi za uendeshaji wa josho katika eneo husika kutegemea uamuzi Kamati ya Uendeshaji wa Josho husika.Aidha Dk. Linus amezitaja kamati nne za majosho, zilizokabidhiwa dawa  za kuogesha mifugo  ambazo ni Kamati ya Josho la Engutukoit kata ya Oldonyowas, Oloitushula kata ya Musa, kidali na Engalaoni kata ya Mwandet huku kila Josho likipata lita 10 za dawa.

Hata hivyo wajumbe wa kamati hizo wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwakumbuka wafugaji, kwani kwa miaka mingi sasa, Serikali ilikua kama imewasahau na kuahidi kwenda kuhamasisha wafugaji kujitokeza kuogesha mifugo yao,  kwa gharama nafuu ambazo hapo awali wafugaji wengi walikua
wanashindwa kuzimudu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Josho la Oloitushula kata ya Musa, Manase Meoki, licha ya kuishuru Serikali kwa kuwakumbuka wafugaji, amesema kuwa uwepo wa dawa hizo, zilizotolewa na Serikali utawasaidia kupunguza gharama kubwa walizokuwa wakizitumia pamoja na kuepuka kuuziwa dawa zisizofaa na kuwataka wananchi wenzake kuunga mkono jitihada hizi za Serikali.

Halmashauri ya Arusha ina jumla ya majosho 18, majosho  nane  kati ya hayo ndio yanatoa huduma, majosho matano hayatoi huduma kutokana na uhalisia wa maeneo yalipo  tayari kumeshakuwa miji na kuwa katika makazi ya watu hivyo hayatumiki kwa sasa, huku majosho matano yakihitaji ukarabati
kutokana na uchakavu uliotokana na kujengwa muda mrefu.
 Picha ikionesha Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera akimkabidhi mmoja wa mjumbe wa kamati ya uendeshaji josho (jina halikuweza kupatikana) box lenye lita kumi za dawa.
Picha baadhi ya wajumbe wa Kamati za Uendeshaji Majosho, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa dawa za kuogeshea mifugo.

SOT, PRALENA KUCHANGISHA MILIONI 45

$
0
0
NA ANDREW CHALE

Taasisi ya Michezo ya watu wenye Ulemavu wa Akili Tanzania, Special Olympics inahitaji shilingi milioni 45 kwa ajili ya kuisaidia timu ya Taifa inayotarajia kushiriki michezo ya Dunia itakayofanyika mwezi Machi mwaka huu, Abu Dhabi Falme za Kiarabu (UAE).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays alisema fedha hizo ni kwa ajili ya tiketi za kwenda na kurudi sambamba na kambi ya maandalizi kuelekea katika michezo hiyo.

Rays alisema kambi ya maandalizi kwa siku 14 inahitaji shilingi milioni 10.5 huku tiketi kwa ajili ya kwenda na kurudi Abu Dhabi ni sh.milioni 34.5.

Aidha Rays alisema ili kufanikisha kushiriki katika michezo hiyo wameomba ridhaa ya Taasisi ya PRALENA Network Ltd ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa fedha hizo kupitia mfumo wa simu za mkononi.


Naye mwakilishi wa PRALENA, Thabit Said alisema ili kufanikisha upatikaji wa fedha hizo wametengeneza mifumo mbalimbali ambayo wadau watachangia fedha.Said alisema mfumo huo utatumika kwa kila anayeguswa katika mitandao ya simu ya Tigopesa, M-Pesa na Airtel Money.

“Tunawaomba wadau katika jamii, kusaidia kupatikana kwa fedha hizo kupitia Tigopesa, M-Pesa na Airtel Money kupitia namba ya kampuni 123123 na kumbukumbu namba ni 60024833555,” alisema Said.

Said aliweka bayana kauli mbiu ya ufanikishwaji wa fedha hizo ni ‘Ushindi wao ni ushindi wetu’. 
 Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati wa  kuchangisha  fedha za tiketi. Kulia ni Mwakilishi wa taasisi ya PRALENA, Bi. Irine Victor  na kushoto ni Mjumbe wa bodi ya SOT, Makuburi Ally.

 Mwakilishi wa PRALENA, Thabit Said akizungumza  namna ya mifumo mbalimbali ambayo wadau watachangia fedha ili kukusanya kiasi hicho cha Sh. Milioni 45.

WATUMISHI TASAF WAOANISHA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI NA USIMAMIZI THABITI WA SERIKALI.

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga(aliyesimama)akitia nasaha za ufunguzi wa Kikao kazi cha watumishi wa taasisi hiyo jijini DSM.

Mkurugenzi wa Programu za TASAF,Bw. Amadeus Kamagenge (aliyeshika kipaza sauti) akitoa mada kwenye kikao kazi cha Watumishi wa Taasisi hiyo juu kukamilika kwa awamu ya kwanza na maandalizi ya awamu ya pili ya Mpango wa kunusuru kaya maskini-PSSN.

Mmoja wa Maafisa Ufuatiliaji wa TASAF akisoma taarifa ya pamoja ya utekelezaji wa maafisa hao kwenye kikao kazi kilichoanza hapo jana jijini DSM.

Baadhi ya Watumishi wa TASAF akiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa taasisi hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji Bw. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani kwenye kikao kazi ambacho hufanyika kila mwaka kujadili utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa taasisi hiyo wanaohudhuria kikao kazi kinachojadili utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo jijini DSM.
 
 
Na Estom Sanga- DSM.

Wafanyakazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF wamekiri kuwa usimamizi na miongozo thabiti inayotolewa na Serikali imechangia kwa kiwango kikubwa kufanikiwa kutekelezwa kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na Umaskini.

Akifungua kikao kazi cha Wafanyakazi wa Mfuko huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga amesema mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo yamechangia jitihada za Serikali za kukuza na kuboresha maisha ya wananchi hususani wale ambao wamekuwa wakiishi katika dimbwi la umaskini na kuamsha ari ya wao kujiletea maendeleo.

Bwana Mwamanga amewaasa Watumishi hao wa TASAF kutobweteka na mafanikio yaliyopatikana katika kuwahudumia Walengwa wa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini badala yake waongeze jitihada zaidi ili lengo la Serikali la kupambana na adui umaskini liwe la mafanikio endelevu na makubwa zaidi kupitia Mpango huo.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amebainisha kuwa maelekezo ya Serikali katika kusimamia na kuboresha utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa awamu ya pili yakiwemo ya kuwashirikisha Walengwa Kufanya kazi yatazingatiwa ili kukuza kipato cha Walengwa hao na kuwawezesha kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa taifa na kuboresha huduma za kijamii kwenye maeneo yao.

Bwana Mwamanga amesema kuwa kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika awamu yake ya kwanza , kumekuwa na mahitaji kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao Mpango huo haujawafikia wakitaka wajumuishwe kwenye huduma za Mpango huo ambapo amesisitiza kuwa maelekezo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa Wananchi wenye uhitaji na kuwa na vigezo vya kujumuishwa kwenye Mpango wapate huduma hiyo kazi ambayo amesema itatekelezwa katika awamu ijayo ya Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini.

Katika awamu ya kwanza ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini takribani kaya Milioni Moja na Laki Moja zimeandikishwa na kuendelea kupata huduma za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF -ambayo ni sawa na asilimia 70 ya vijiji/shehia huku asilimia 30 ya vijiji/shehia ikisalia kutokana na ufinyu wa raslimali fedha.

Akitoa taarifa ya kukamilika kwa Awamu ya Kwanza ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na Maandalizi ya Sehemu ya Pili ya Mpango huo inayotarajiwa kuanza hivi karibuni, Mkurugenzi wa Programu za Jamii wa TASAF, Bwana Amadeus Kamagenge ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwenye awamu ya kwanza kuwa ni pamoja na kuanzisha Masjala ya Walengwa zaidi ya Milioni Sita huku kazi ya kuhaulisha fedha ikitekelezwa kwa mafanikio makubwa kwa Walengwa tangu mwaka 2014.

Aidha amesema Serikali kupitia TASAF imefanikiwa kuhamasisha Wananchi ambao walikuwa wakiishi katika umaskini mkubwa kurejesha matumaini kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali kwa kutumia sehemu ya ruzuku huku wakitekeleza masharti ya Mpango hususani yanayolenga katika sekta za Elimu na Afya na hivyo kujiongezea uwezo wa kukabiliana na kero ya umaskini.

KARIBUNI KWENYE MAONESHO YA AFYA BURE COLOSSSEUM HOTEL

$
0
0

Karibu katika Maonyesho ya Afya yatakayofanyika katika Hoteli ya Colosseum iliyopo Masaki siku ya Jumapili, tarehe 03/02/2019 kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi jioni.

Pata nafasi ya kukutana na mabingwa katika kada zaidi ya 15 zikiwemo Lishe, Mazoezi, Ugonjwa wa Kisukari, Magonjwa ya Moyo, Afya ya Meno, Afya ya Akili, Msongo wa Mawazo, Matumizi ya Pombe na Ulevi, Madawa ya Kulevya, Afya ya Uzazi, Mahusiano, nk. Pia kutakuwa na walimu waliobobea katika malezi ya watoto watakaofundisha watoto Juu ya kutunza Afya zao!

Hakuna kiingilio! Karibu sana!

NMB yasaidia madawati Sekondari ya Magawa na vifaa vya ujenzi Zahanati ya Nganje, Mkuranga

$
0
0
Na Ripota wetu, Mkuranga

BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa viti na madawati 50 kwa Shule ya Sekondari Magawa pamoja na baadhi ya vifaa vya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nganje Wilaya ya Mkuranga vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 10.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa NMB, Bi. Vicky Bishubo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Mh. Subira Hamisi Mgalu (MB) katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari Magawa wilayani Mkuranga.

Akifafanua zaidi juu ya msaada huo, Bi. Vicky Bishubo alisema viti na madawati 50 yaliyotolewa kwa Shule ya Sekondari Magawa vina thamani ya shilingi milioni 5, huku mbao 520 na misumari iliyotolewa kwenye ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nganje inathamani ya shilingi milioni 5.

Aidha aliongeza kuwa Benki ya NMB inazipa kipaumbele changamoto za sekta ya elimu na afya nchini Tanzania kutokana na umuhimu wa sekta hizo, kwa kile kuwa kama nguzo kuu ya maendeleo kwa taifa na hata nchi yoyote duniani.

"..Tunatambua juhudi za Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ya kusimamia elimu na afya kwa nguvu zote kwa kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari, na pia kuboresha utoaji wa huduma za afya mijini na vijijini; tunaipongeza Serikali kwa hilo."

Alisema Serikali inafanya mambo makubwa katika sekta hizo, lakini NMB kama wadau wanawajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo kwa kusaidia jamii kwani kupitia jamii ndio imeifanya benki kuendelea kufanya vizuri.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Mh. Subira Hamisi Mgalu (MB) akipokea msaada huo aliishukuru Benki ya NMB kwa ukarimu wao wa kuijali jamii na kuziomba taasisi zingine zifuate nyayo za NMB katika kuisaidia jamii kwa mambo mbalimbali.

"...Nawashukuru, nawashukuru sana kwa kujitoa kwenu kwa jamii nimekuwa nikishuhudia mkisaidia jamii kupitia sekta mbalimbali, huu ni mfano wa kuigwa kwa kweli endeleeni kuisaidia jamii nasi tunaahidi kuunga mkono shughuli zenu," alisema Bi. Mgalu.


Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa NMB, Bi. Vicky Bishubo akikabidhi sehemu ya mbao 520 na misumari kwa Naibu Waziri wa Nishati, Mh. Subira Hamisi Mgalu (MB) ikiwa ni mchango wao katika ujenzi wa Zahanati ya Nganje iliyopo wilayani Mkuranga. Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 5. Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid (kushoto) na Meneja wa Tawi la NMB Mkuranga, Joseph Iramba (kulia).

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Magawa wakiwa wamekalia madawati hayo mara baada ya kukabidhiwa na Benki ya NMB.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa NMB, Bi. Vicky Bishubo akikabidhi sehemu ya madawati na viti 50 kwa Naibu Waziri wa Nishati, Mh. Subira Hamisi Mgalu (MB) kusaidia Shule ya Sekondari Magawa. Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 5. Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid (kushoto) na Meneja wa Tawi la NMB Mkuranga, Joseph Iramba (kulia).

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Magawa wakibeba meza na viti mara baada ya kukabidhiwa na NMB.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa NMB, Bi. Vicky Bishubo akizungumza katika hafla hiyo.

Naibu Waziri wa Nishati, Mh. Subira Hamisi Mgalu (MB) akiishukuru NMB kwa msaada wake.

NAMTUMBO WAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2019/2020

$
0
0
NA YEREMIAS NGERANGERA,NAMTUMBO.

Baraza maalumu la madiwani pamoja na Baraza la wafanyakazi katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma limepitisha Rasimu ya mpango wa bajeti 2019/2020 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo.

Akisoma rasimu ya bajeti hiyo kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo Ofisa mipango wa Halmashauri TeklaNyoni alisema kuwa mapendekezo ya bajeti hiyo imezingatia dira ya Halmashauri ,mwelekeo wa Halmashauri pamoja na miongozo mbalimbali iliyotolewa na serikali na kulenga kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi 2015-2020

Awali Tekla alitoa taarifa kwa waheshimiwa madiwani na kisha kwenye baraza la wafanyakazi kuwa pamoja na mambo mengine mapendekezo ya bajeti hizo zimezingatia vipaumbele vilivyoibuliwa na wananchi kutoka katika vijiji na kisha kuwasilisha vipaumbele hivyo ofisi ya mkurugenzi.

Aliwathibitishia waheshimiwa madiwani pamoja na baraza la wafanyakazi katika vikao tofauti kuwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo imekasimia kuwa na bajeti ya shilingi 24,212,575,600.ambapo kati ya fedha hizo shilingi 1,765,714,100 sawa na asilimia 7 zitatumika kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi 18,371,513,00 sawa na asilimia 76kwa ajili ya mishahara na shilingi 2,658,621,500 kwa ajili ya shughuli za maendeleo ambapo ni sawa na asilimia 11 ya fedha kisiwa na jumla ya shilingi 1,416,727,000 sawa na asilimia 6 kuwa ni makusanyo ya Ndani ya Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Daniel Nyambo aliwataka waheshimiwa madiwani kupitia mapendekezo ya bajeti hizo kwa umakini na kuazingatia mahitaji ya vipaumbele hizo katika maeneo yenye uhitaji badala ya kila diwani kulalamikia kuingizwa vipaumbele vyake kwanza.

Hata hivyo aliwataka madiwani hao kufahamu kwamba fedha hata siku moja haitoshelezi mahitaji na kinachotakiwa katika halmashauri hiyo ni kujipanga ili kukamilisha miradi hiyo kwa kuzingatia mahitaji ya eneo husika na sio vinginevyo.

Nyambo pia aliwataka madiwani wenzake kuunda kamati ya kupitia pendekezo la chanzo kipya cha mapato kinachopendekezwa cha kuwa na mnada wa ng`ombe katika Halmashauri hiyo ili kujiridhisha kama chanzo hicho cha mapato kinaweza kusaidia Halmashauri hiyo kuinua mapato kulingana na Ng`ombe waliopo na kujihadhari na chanzo hicho kutoa mwanya wa wafugaji kuingiza mifugo yao katika Halmashauri hiyo 

Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Evance Nachimbinya aliwaomba waheshimiwa madiwani kuhamasisha wananchi kwenye maeneo yao kuibua miradi ya maendeleo kama kujenga vyoo vya shule zahanati na kuanza kuitekeleza mpaka hatua ya boma na Halmashauri itashughulika vifaa vya viwandani ili kukamilisha miradi hiyo alisema mkurugenzi huyo.

Lakini pia mkurugenzi huyo aliwataka madiwani hao kuhamasisha wananchi wao kuhusu kulima mazao kwa wingi ili wapate chakula cha ziada na biashara ili halmashauri iweze kupata mapato yatakayoiwezesha halmashauri kukamilishia umaliziaji wa miradi ya wananchi wake.

Kikao cha Kupitisha mapendekezo ya bajeti 2019-2020 kilikuwa cha siku moja ambapo kilitanguliwa na baraza la wafanyakazi na kisha baraza la madiwani la Halmashauri hiyo .
Tekla Nyoni akiwasilisha mpango wa bajeti wa Halmashuri hiyo kwenye kikao cha baraza la wafanyakazi katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

BREAKING NEWZZZZ: SPIKA NDUGAI AMSHUSHUA MBUNGE WA KIGOMA MJINI ZITTO KABWE KWA UWONGO

Kesi ya uchochezi dhidi ya vigogo wa Chadema yapata Hakimu mpya

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii 

KESI ya uchochezi inayowakabili vigogo tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama wao, Freeman Mbowe inayounguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepangwa kuendelea kusikilizwa kwa Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina.

Hatua hiyo imekuja baada ya hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi Wilbard Mashauri kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Aidha, rufaa iliyokatwa na upande wa serikali kupinga uamuzi mdogo wa Mahakama Kuu wa kuendelea na usikilizwaji wa rufaa ya kufutiwa dhamana kwa Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Rufani Februari 18, mwaka huu.

Mapema, wakili wa Serikali, Wankyo Simon ameeleza mahakamani hapo kuwa, kesi hiyo leo Januari 31.2019 imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba rufaa iliyopo Mahakama ya Rufani bado haijasikilizwa, hivyo aliomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, wakili wa utetezi, Profesa Abdallah Safari ameieleza mahakama kuwa rufaa imepangwa kusikilizwa Februari 18, 2019.Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 14, mwaka huu na kuwaeleza washitakiwa walio nje kwa dhamana kuwa dhamana zao zinaendelea Mbowe na Matiko wamerudishwa rumande.

Novemba 23, mwaka jana Jaji Mashauri akiwa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alifuta dhamana ya Mbowe na Matiko kwa sababu walikiuka masharti ya dhamana.Baada ya maamuzi hayo, washitakiwa wakiwakilishwa na Wakili wao Peter Kibatala walikata rufaa Mahakama Kuu kupinga maamuzi ya mahakama hiyo ya kufuta dhamana.

Hata hivyo, baada ya mahakama Kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika kusikiliza mapingamizi ya pande zote iliamua kuanza usikilizaji wa rufaa hiyo.Upande wa serikali ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi ulikata rufaa kupinga maamuzi yaliyotolewa na kuiomba mahakama hiyo kuacha kuendelea kusikiliza rufaa hiyo kwa sababu haina mamlaka.

Kufuatia hayo, Jaji Rumanyika alisema mahakama yake imefungwa mikono hivyo anasitisha usikilizwaji wa rufani hiyo hadi hapo itakapotolewa uamuzi katika Mahakama ya Rufani.

Mbali na Mbowe na Matiko washtakiwaa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu ambao wote walikuwepo mahakamani.

Katika kesi ya msingi, washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018 maeneo ya Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa chama wao, Freeman Mbowe akizungumza jambo na Mh.Lazaro Nyarandu.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Chadema wakijadiliana jambo
Baada ya Hakimu kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 14, 

PAKA A.K.A NYAU AINGIA UKUMBI WA MIKUTANO WA MPINGO HOUSE

$
0
0
*Ni wakati tukio la utiwaji saini wa mkataba wa ushirikiano kati ya TFS na NLUPC


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAKATI mjadala ukiendelea kuhusu tukio la bundi kutumia Bungeni, leo hii katika tukio la utiwaji saini wa mkataba wa ushirikiano kati ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi(NLUPC) Paka a.k.a Nyau ameingia katika ukumbi wa mikutano wa Mpingo House jijini Dar es Salaam.

Paka huyo aliingia ukumbini hapo saa sita kasoro dakika tano ikiwa ni dakika chache kabla ya tukio la utiwaji saini kufanyika ambapo haijulikani alitokea wapi.Wakati anaingia ukimbini Paka huyo alianza kupiga kelele za milio ule maaruf wa Nyauuuu...nyau...nyau... kwa staili yao kama ambavyo tumezoea kuusikia masikioni.

Baada ya kuingia ukumbini hakuwa na makeke kwani baada kufika alikwenda kukaa pembeni ya ukutano na kisha akajituliza tuli.

Baadhi ya waandishi waliokuwa ukumbini hapo walijikuta wakianza kucheka kutokana na Paka huyo kuingia.Kwa kuwa hakuna na vurugu yoyote kilichobaki ikawa ni kumuangalia na kwa huu ni ulimwengu wa teknolojia ,kilichofuata ikawa ni kumpiga picha(kama unavyoona hapo pichani).

Hata hivyo baadhi ya waandishi waliamua kumfuata ili kumuondoa mahali alipo lakini aligoma kuondoka.Wakati Paka huyo akiwa mkutanoni hapo waliokuwa meza kuu na wale wa viti vilivyokuwabna baadae akaamua kusogea.

Hivyo wakati wa utiwaji saini mkataba huo aliondoka ukumbini na baada ya tukio kukamilika akarejea tena.

Ujio wake kwa mara ya pili ulisababisha baadhi ya waandishi kujiuliza na maswali kuhusu Paka huyo ambapo baadhi yao wakajikuta wakizungumzia tukioa Bundi kutua Bungeni ambapo Spika wa Bunge Job Ndugai aliamua kuelezea tukio hilo na kwamba kwa Dodoma Bundi wa usiku ndio mwenye madhara na si bundi anayeonekana mchana.

Haifahamiki Paka aliyeingia ukumbi wa mikutano wa Mpingo House leo alikuwa na mkakati gani.Hiyo itabaki kuwa siri ya Paka mwenyewe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ajumuika pamoja na Wafanyabiashara wa Jijini Mwanza katika Hafla ya Jioni

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia) akitambulishwa kwa Mkuu wa Wilaya Ilemela, Severine Lalika aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella katika hafla ya jioni iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja na Wafanyabiashara wa Jijini Mwanza, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Gold Crest, Januari 29, 2019. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay pamoja na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akijumuika pamoja na Wateja na Wafanyabiashara wa Jijini Mwanza katika Hafla ya Jioni iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Gold Crest, Januari 29, 2019, Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dkt. Severline Laika, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay na Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, Dkt. Anthony Dialo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akiznumza katika hafla hiyo na kumtambilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa baadhi ya wateja na wafanyabiashara wa jijini Mwanza waliohudhulia hafla hiyo, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Gold Crest, Januari 29, 2019, jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiznumza katika hafla hiyo ambapo aliwashukru wateja na wafanyabiashara wa jijini Mwanza kwa kuendelea kutumia huduma za benki hiyo na kuwaahidi huduma bora zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza jambo na aliyekuwa Mkurugezi wa Benki ya CRDB tawi la Mwanza, Calystus Wambura baada ya kuagwa rasmi na Mameneja wa Benki hiyo wa Kanda ya Ziwa.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akimpongeza aliyekuwa Mkurugezi wa Benki ya CRDB tawi la Mwanza, Calystus Wambura baada ya kuagwa rasmi na Mameneja wa Benki hiyo wa Kanda ya Ziwa.






 


















VODACOM TANZANIA WAZINDUA KITUO CHA KUTOA HUDUMA MAKAMBAKO

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Makambako Bw Paul Malala, akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kituo cha kutoa huduma cha Vodacom Tanzania jijini Makambako, Njombe jana. (Kushoto) ni Mteja wa Vodacom Emmanuel Gadau, Meneja Mauzo wa Njombe, Humphrey Mutabiirwa na Msimamizi wa Maduka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Yasinta Hussein. Vodacom Tanzania imelenga kuongeza upatikanaji wa huduma ili kuwezesha maendeleo ya jamii.
Msimamizi wa Duka, Mussa Ndazi, akielezea juu ya huduma mbali mbali zitakazo tolewa katikaa kituo kipya cha Vodacom Tanzania kilichozinduliwa jijini Makambako, Njombe jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Makambako Bw Paul Malala. Vodacom Tanzania imelenga kusogeza huduma zake ili kuwezesha maendeleo ya jamii.

CHUO CHA BANDARI KUFUNDISHA KISASA ZAIDI, MTAMBO WA KUFUNDISHIA WANUNULIWA

$
0
0
Chuo cha Bandari ambacho kipo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kimejipanga kupokea mitambo ya kisasa ya kufundishia ili kukifanya kiwe cha kisasa zaidi. Kwa kuanzia, TPA imeshaingia mkabata wa kununua mtambo mkubwa wa kufundishia uendeshaji wa vyombo vyote vya kupakia na kupakua mizigo bandarini yaani ‘full Mission Crane Training Simulator’.

Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo hicho, Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema kwamba mtambo huo, unaotarajiwa kugharimu takribani Shs.1.5bn ni wa kisasa na wenye manufaa makubwa zaidi kwa Chuo.
“Mtambo huu utafungwa ndani ya miezi sita kuanzia sasa na kuanza kutumika mwanzoni mwa mwaka ujao wa fedha,” amesema Mhandisi Kakoko.

Mhandisi Kakoko ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, amesema kwamba Mamlaka itaendelea kuwekeza katika vifaa ili kukifanya Chuo hicho kiwe cha kisasa zaidi. Aidha, Chuo kimezindua tovuti pamoja na mfumo wa TEHAMA ‘Students Information Management System’ amesema Mhandisi Kakoko na kuongeza kwamba juhudi hizi zinalenga kuimarisha na kusimamia ubora wa huduma zitolewazo na Chuo.

Kwa upande, Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Joseph Kakeneno amesema kwamba Chuo kinakusudia kutoa Stashahada za juu na Shahada ya kwanza ya kuongeza ujuzi wa utendaji kazi ‘Competence Based’. Dkt. Kakeneno amesema kwamba shahada hizo wanazotarajia kuzianzisha katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, ni katika taaluma zinazohusiana na huduma za meli, maji na menejimenti ya shughuli za bandari. Amesema kwamba kwasasa Chuo kina karakana nne (4) za mafunzo kwa vitendo, moja kwa kila fani ya ‘Mechanical, Civil, Automotive, Eletrical na mabara moja ya kompyuta na maktaba moja.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo cha Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko akihutubia wageni wakati wa mhafali ya Chuo cha Bandari
 Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo cha Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko akimpa zawadi Waziriwa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe, C, Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo cha Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko, R, na Mkuu wa Chuo cha Bandari Dkt Joseph Kakeneno.
 Wanafunzi waliomaliza masomo yao wakiwa katika mahaafali hayo

MAJAJI, MAHAKIMU NA MAKADHI ZANZIBAR WAPEWA MAFUNZO YA NAMNA YA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA FEDHA HARAMU

$
0
0
Na Ramadhani Ali - Maelezo  
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amesema tatizo la Utakatishaji  Fedha haramu linahitaji mashirikiano ya pamoja katika kukabiliana nalo kwani linahatarisha Maendeleo ya Mataifa mengi duniani. Amesema tatizo hilo linapelekea taifa kupoteza heshma yake na kutoaminika mbele ya mashirika na jamii ya kimataifa na kuzorotesha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Jaji Makungu alieleza hayo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo Majaji, Mahakimu na Makadhi wa Zanzibar namna ya kushughulikia masuala ya fedha haramu yanayofanyika Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi. Amesema utakatishaji fedha haramu ni vitendo vya aibu na vinahatarisha mfumo mzima wa fedha katika nchi, sheria na usalama hatimae nchi kupoteza washirika wake wa maendeleo.

Alisema kwa kutambua ukubwa wa tatizo hilo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikifanya juhudi mbali mbali ikiwemo kutunga sheria ya kukabiliana na vitendo hivyo viovu. Aliwaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa jitihada za pamoja zinazochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupambana na tatizo hilo zimeleta mafanikio makubwa.

Alisema vitendo vya uhalifu na dawa za kulevya, ambavyo ni miongoni mwa mambo yanayopelekea utakatishaji wa fedha haramu vimekua vikidhibitiwa na kupungua kwa kiasi kikubwa. Amekipongeza Kitengo cha kudhibiti fedha haramu Tanzania kwa juhudi kubwa wanazochukua kutoa elimu kwa wadau wa kada mbali mbali nchini ili kufahamu athari zinazotokana na vitendo hivyo na njia za kupambana navyo.

Akimkaribisha Jaji Mkuu kufungua mafunzo hayo, Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu Tanzania Onesmo Makombe amesema vitendo vya utakatishaji wa fedha haramu vinadhoofisha ukuaji wa uchumi wa nchi. Aliishauri jamii ya Watanzania kuungana kupiga vita vitendo vya utakatishaji fedha haramu ili nchi iendelee kuaminika na kujenga imani mbele ya jamii ya kimataifa.

Alimuhakikishia Jaji Mkuu wa Zanzibar kwamba Kitengo cha kudhibiti Fedha Haramu Tanzania kitaendelea kutoa taaluma  ndani ya pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha tatizo hilo linapungua na hatimae kuondoka moja kwa moja.
 Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu Tanzania Onesmo Makombe akitoa maelezo kwa Majaji, Mahakimu na Makadhi wa Zanzibar wanaoshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya fedha haramu yanayofanyika Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi.
 Baadhi ya Mjaji, Mahakimu na Makadhi wa Zanzibar wanaoshiriki mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo kuhusu kushughulikia masuala ya fedha haramu wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi.
 Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akifungua Mkutano wa siku mbili wa kuwajengea uwezo Majaji, Mahakimu na Makadhi wa Zanzibar juu ya kushughulikia masuala ya fedha haramu yanayofanyika Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Mkungu (kati kati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji, Mahakimu na Makadhi baada ya kufungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo kuhusu utakatishaji fedha haramu katika Chuo cha Utalii Maruhubi
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images