Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live

POLISI TANZANIA YAITAMBIA MASHUJAA

$
0
0
Na Jeshi la Polisi
Timu ya mpira wa miguu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi daraja la kwanza Tanzania bara imesema mwaka huu ni mwaka wao wa kuhakikisha kuwa wanafanyaa vizuri ili kupanda na kucheza ligi kuu Tanzania.
Akizungumza na gazeti hili Afisa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo Frank Lukwaro amesema msimu huu wamejipanga ikiwemo kuwashirikisha wadau muhimu katika kuleta mafanikio ya ushindi hususani katika mzunguko wa pili unatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki huku timu hiyo ikiwakaribisha wababe wa Simba timu ya Mashujaa kutoka Kigoma.
Lukwaro amesema mashabiki wa mkoa wa Kilimanjaro hivi sasa wameungana pamoja katika kuhakikisha kuwa timu inapata ushindi katika kila mechi iliyosalia ili kujiweka katika nafasi za juu katika kundi B.
Amesema pamoja na kujitokeza kwa wingi uwanjani lakini pia wamekuwa wakitoa ushauri wa nini cha kufanya  kwa ushirikiano wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro KRFA na wafadhili wa timu hiyo kampuni ya Lodhia na Busega Mazao.
‘Hivi sasa timu yetu inacheza vizuri kulingana na usajili makini walioufanya katika dirisha dogo na mwalimu Mbwana Makata ameimarisha kikosi chake vilivyo ndio maana uwanja sasa unajaa mashabiki na hamasa ni kubwa tofauti na hapo awali’ Alisema Lukwaro. Kwa upande wake kocha Mbwana Makata akizungumzia mchezo ujao dhidi ya Mashujaa amesema kikosi chake kipo imara na ana imani kuwa wataibuka na ushindi katika mchezo huo.
Makata amesema kila mechi katika mzunguko wa pili anaipa umuhimu mkubwa hivyo amewajenga kisaikolojia wachezaji wake kujituma na kufuata maelekezo aliyowapa ili kuibuka na ushindi.
Mpaka sasa timu hiyo ipo nafasi ya saba katika msimamo wa kundi B ikiwa imejikusanyia alama 14 katika michezo 11 baada ya kushinda michezo mitatu, kutoka suluhu michezo mitano na kupoteza michezo mitatu.


WADAU WA AFYA KUTAFUTA UFUMBUZI MATUMIZI SAHIHI YA TAKWIMU KWA WATOA HUDUMA WA SEKTA YA HIYO

$
0
0
 Mkurugenzi wa chuo cha madaktari wasaidizi  Ifakara mkoani Morogoro Prof. Frola Kessy akielezea changamoto ya  wahudumu wa afya katika kutoa takwimu sahihi na namna ya kuepuka na changamoto hiyo katika mkutano wa wadau wa afya mkoani Morogoro.
 Wadau wa afya na wakufunzi kutoka vyuo  mbalimbali hapa nchini ikiwemo chuo kikuu cha Mzumbe, chuo kikuu cha Dodoma, kituo cha kimataifa cha mafunzo ya afya Ifakara na chuo kikuu cha Mhimbili  wakifatilia kwa umakini mjadala wa namna takwimu zinazokusanywa jinsi ambavyo zinavyoshindwa kutumiwa ipasavyo na wahudumu wa afya.
 Mtakwimu mkuu ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEM) Yasinta Kijuu akiwasilisha kwa wadau wa afya namna ambavyo serikali iliona mifumo ya takwimu usivyotumiwa ipasavyo  na kuangalia jinsi   ya kutatua changamoto hiyo  katika mkutano wa wadau wa afya uliofanyika mkoani Morogoro ambapo alisema  mwaka 2016 ndipo mchakato wa kutatua changamoto hiyo ya matumizi ya takwimu  ulianza.
 Wadau wa afya wakimfatilia kwa umakini katika mkutano wa wadau wa afya mkoani Morogoro mkufunzi wa chuo kikuu Mzumbe Dr,Mackfallen Anasel akizungumzuia jinsi ambavyo mitaala ya kufundishia inahitaji marekebisho katika swala la ukusanyaji na matumizi ya takwimu  ili wahitimu  wa vyuo waelewe  matumizi sahihi ya takwimu hizo .
Makamu  mkuu wa chuo taaluma,utafiti na ushauri kutoka chuo cha serikali za mitaa  Hombolo Dodoma  Dr, Michael Msendekwa akitoa ushauri wa jinsi gani ya kufikia utoaji wa huduma sahihi za afya kwa wananchi na jinsi ya kuodoa vikwazo vinavyo kwamisha  matumizi sahihi ya takwimu katika kutoa maamuzi  katika kikao cha wadau wa afya mkoani Morogoro.

TAMASHA SAUTI ZA BUSARA YATOA OFFA MAALUM KWA WATANZANIA

$
0
0
Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya tamasha la Sauti za Busara kuanza, Mwenyekiti wa Busara Promotions Simai Mohammed Said amewataka watanzania na wakaazi wa Zanzibar kwa ujumla kuchangamkia fursa zinazo tokana na tamasha hilo. 

“Kuna offa maalum kwa ajili ya watanzania ambayo ni ya chini kabisa ukilinganisha na kile wanacholipa wageni kutoka sehemu zingine kuingia kwenye tamasha,” alisema Simai. 

Alisema fursa zinazo tokana tamasha hili haipatikani mahali popote na wanaofaidika zaidi ni wakazi wa mitaa ambao bado wanashindwa kutumia hizo fursa kikamilifu . 

"Kuna nyakati ambazo watu wanauliza maswali mengi kuhusu tamasha laSauti za Busara na wengine wanakwenda mbali hadi kusema kuwa ni tamasha kwa watalii wakati wao ndio wenyeji," alisema Bw Simai .Mwenyekiti wa Bodi zaidi aliongeza: 'Hakika hakuna haja ya kuangalia mbali sana kupata majibu ya maswali kama hayo; Kwa miaka 16 iliyopita muda huu umekuwa msimu wa juu kwa biashara ya utalii kulingana idadi ya wageni wanaokuja Zanzibar’. 

Kulingana na yeye kuna dalili kwamba hoteli zote za Zanzibar zimejaa kikamilifu na Jiji la Zanzibar kwa ujumla ipo katika hali ya matarajio.Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elizabeth Jacobsen kwa upande wake atakuwa akihudhuria tamasha kwa mara ya kwanza na anatarajia mengi kutoka kwenye tamasha hilo hususan fursa zinazopatikana kwenye tamasha. 

“Tunaendelea kusaidia shughuli za kitamaduni kama Sauti za Busara kwa sababu tunaelewa thamani ya shughuli hizo. Tunaona hii ni jukwaa muhimu la kujieleza bure, kukuza tamaduni zetu, weledi na utaalamu katika sekta ya kitamaduni ya Tanzania "alisema Balozi huyo wa Norway, ambaye alianza majikumu yake la kidiplomasia mnamo Septemba 2018. 

Pia aliwahimiza wafanyabiashara ambao ni walengwa wakuu wa tamasha kuunga mkono tukio hilo kwa namna ya uwajibikaji kwa jamii.Julia Bishop ambaye ni makamu wa Mwenyekiti kwa upande wake alisema amejionea mwenyewe jinsi tamansha la Sauti za Busara linavyo badilisha maisha ya wasanii hususan wale chipukizi wasiojulikana kabisa. 

“Kwa mtu ambaye hajawahi kufika Zanzibar kabla ni vigumu kufikiria ukubwa wa tukio hili, ubora wa maonyesho, utaalamu na msisimko ambayo hupatikana ndani ya Stone Town, "alisema.Kulingana na yeye, ukweli kwamba makundi madogo ambayo haijulikani sana kupata fursa sawa na nyota wa muziki kwenye jukwa moja yenyewe ni hatua ya kubadili maisha. 

Tamasha la Sauti za Busara linadhaminiwa na Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na Zambia, Umoja wa Ulaya, Africalia, Ubalozi wa Ufaransa, Ubalozi wa Ujerumani, Pro Helvetia, Zanlink, Mozeti, Shirika la Ndege la Ethiopia, African Movie Channel, Zanzibar Media Corporation, TV-E, E-FM, Madinat Al Bahaar, Golden Tulip na wengine wengi. 

Sauti za Busara ni tamasha la muziki la Kiafrika linalofanyika kila mwaka, mwezi Februari mjini Zanzibar, Tanzania katika eneo la Ngome Kongwe (Old Fort) sambamba na matukio mengine ya kuvutia yanayofanyika kwa wakati mmoja maeneo ya Stone Town- ikiwemo Carnival Street Parade, Swahili Encounters, Movers & Shakers na Busara Xtra. 

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI, BALOZI WA SWEDEN JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg alipomtembelea leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
pika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg baada ya kumtembelea na kufanya nae mazungumzo leo tarehe 30 Januari, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MAJINA WAUAJI WATOTO NJOMBE YABAINIKA-WAZIRI LUGOLA.

SHULE YA SEKONDARI ANNA MKAPA YADAIWA KUTUMIA MAJI YA MUWSA KINYUME NA UTARATIBU

$
0
0
Mwenyekiti w Serikali ya Mtaa wa Fonga ilipo shule ya Sekondari ya Anna Mkapa akitizama kwa karibu wizi wa maji ulivyofanyika katika shule hiyo. 
Bomba likiwa limeunganishwa moja kwa moja mara baada ya kuondolewa Mita ya shule hiyo iliyokuwa ikitumika kuhesabu unit za maji yanayotumika katika shule ya Anna Mkapa.
Fundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) akifungua kipande cha Bomba kilichounganishwa kwa ajili ya kufanikisha wizi wa maji mara baada ya kuondoa Mita hiyo .
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi wakiwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Fonga,Mama Kimambo ,wajumbe wa serikali ya mtaa pamoja na Diwani wa kata jirani ya Bomambuzi Juma Raibu wakishuhudia namna ambavyo Bomba la maji limeunganishwa katika maungio ya Mita ili kufanikisha wizi wa maji .


Anaandika Dixon Busagaga ,Moshi 

SHULE ya Sekondari ya Anna Mkapa iliyopo kata ya Pasua katika Manispaa ya Moshi imebainika kufanya udanganyifu kwa kushiriki kitendo cha kuiba Maji ya Mamlaka ya Majisafi na Mazingira mjini Moshi (MUWSA) kinyume cha sheria.

Mbali na wizi huo wa maji uliofanywa na wahusika kwa kuunganisha bomba katika maungio ya Mita za Maji pia Mamlaka imebaini kupotea kwa Mita ya kusoma kiwango cha Maji kinachotumika iliyotolewa na MUWSA kwa shule hiyo ambayo ilipaswa kuwepo katika Bomba hilo lililounganishwa kinyemela.

Tukio hilo lilibainika jana usiku majira ya saa 3:30 baada ya wafanyakazi wa MUWSA kufanya operesheni ya kushtukiza katika shule baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema waliotoa taarifa kwa Mamlaka juu ya wizi huo.

Akizungumza katika eneo la tukio ,Afisa Habari wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Rashid Nachan alisema kilichofanyika ni wizi na kwamba wahusika wanachangia kuhujumu uchumi wa nchi.

“Kinachoonekana hapa dhahiri ni kwamba uongozi wa shule unafahamu kinachoendelea ,kwa sababu hawezi kuja mtu kutoka nje kufanya kitendo cha kutondoa Mita na kuweka Bomba la moja kwa moja bila uongozi wa shule kufahamu ,atakuwa anafanya kwa faida ya nani sasa “alihoji Nachan.

Alisema kinachoonekana Shule ya Anna Mkapa imefanya kitendo hicho kwa muda mrefu na kwamba kimekuwa kikifanyika majira ya usiku na ikifika asubuhi hurudishia Mita kama kawaida mara baada ya Maji kujaa katika Matenki yaliyopo shuleni hapo. “Hatua tunazoenda kuchukua kwa sasa ni kufungua shauri Polisi dhidi ya wahusika kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ikiwa ni pamoja na kufanya mahesabu na kuandaa Bili ya kiasi cha Maji yaliyoibiwa kwa muda wote “alisema Nachan.

Alipulizwa juu ya mada ya wizi wa maji ,Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Anna Mkapa ,Sindato Seiya alikiri kufanyika wizi wa maji katika shule hiyo huku akitupi mpira kwa Mlinzi na Fundi wa miundombinu ya Maji wa shule hiyo.

“Nimeiona sehemu yenyewe ,na toka jana usiku huyu fundi ametafutwa na hapokei simu hadi sasa maana yake anajua mwenyewe ni kitu gani amefanya,hapa shule kuna wafanyakazi wa asubuhi hadi saa tisa na anakabidhiwa shule mlizni wa mchana ambaye pia anakabidhi kwa mlinzi wa usiku hao ndio wanaweza kujua hili suala”alisema Mwl,Seiya.

Alisema yupo tayari kwa hatua zitakazochukuliwa kutokana na kwamba yeye anafahamu wamekuwa wakilipa Bili za Maji kwa njia ya hundi kila mwezi na kwamba wizi wa maji uliofanyika hajui wahusika wamefanya kwa faida ya nani.

TUMIENI TAALUMA ZENU KATIKA SEKTA YA JAMII -WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

AIRTEL KUENDELEA KUSHIKIANA NA JESHI LA POLISI

$
0
0
Na Jeshi la Polisi.
Kampuni  ya  simu za mkononi ya Airtel imelipongeza  Jeshi la Polisi  kwa ushirikiano mkubwa wanaoipatia  katika suala zima la ulinzi wa  raia na mali zao jambo ambalo linawezesha kampuni  ya Airtel kuendelea kutoa huduma kwa watanzania.
 Mkurugenzi  Mtendaji  wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Sunil Colaso  alitoa shukrani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro  na Mkoa wa kipolisi Kinondoni kwa kusaidia kuwakamata na kuwafikisha mahakamani  wahalifu  waliotaka kuiba fedha  zaidi ya shilingi  bilioni moja  kutoka kampuni simu ya Airtel.
Aliongeza kuwa Kampuni yake itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mawasiliano ili wananchi waendelee kupata huduma ya ulinzi na  usalama.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro alimpongeza Mkurugenzi  Mtendaji  wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Sunil Colaso  kwa kuleta mrejesho wa kazi nzuri inayofanywa  na Jeshi la Polisi na kuongeza kuwa ni watu wachache wanaokuwa tayari kuleta mrejesho wa kazi nzuri inayofanywa na  Jeshi la Polisi.
Vilevile,   IGP Sirro aliwataka maofisa wote wa Polisi kuiga mfano wa Kamanda wa mkoa wa Kipolisi Kindondoni ili kujenga na kulinda taswira nzuri ya Jeshi la Polisi kwa kuwa kazi yao ni kuhakikisha wahalifu wote wanashughulikiwa  kwa mujibu wa sheria.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Sunil Colaso pamoja na maofisa wa kampuni hiyo walipofika ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa lengo la kutoa shukrani na pongezi kwa Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa kufanikisha kuwakamata wahalifu waliotaka kuiba zaidi ya shilingi bilioni moja kutoka Airtel.      
( Picha na Jeshi la Polisi.)

WAZIRI MKUU AMJULIA HALI MBUNGE WA MISUNGWI, CHARLES KITWANGA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga ambaye amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa matibabu, Januari 30, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole, Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Mkunda ambaye anamuuguza mwanae, Tunu Kikula aliyelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa matibabu, Januari 30, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari na wauguzi wa Kitengo cha Kusafisha Damu katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma wakati alipowajulia hali wagonjwa  hospitalini hapo, Januari 30, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani, Bungeni jijini Dodoma, Januari 30, 2019. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Januari 30, 2019. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Kiembe Samaki, Ibrahim Raza, Mbunge wa Kwimba, Shanif Mansoor na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Januari 30, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Mwanne Nchemba kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Januari 30, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (wapili kulia), Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwako (kushoto), Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (wapili kushoto) na Mbunge wa Igunga,  Dkt. Dalaly Kafumu , kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Januari 30, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ADO yataka wabunge kujadili sheria ya weledi

$
0
0
Na Mwandishi Wetu.
Taasisi ya Jukwaa la Katiba (ADO) imesema kuwa sheria ya vyama siasa baadhi ya wabunge waache kumhusisha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na sheria kwani yeye ndio aliyepigania uhuru na kufanya nchi ina amani. Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Habibu Mchange amesema kuwa  wabunge watumie weledi katika kujadili sheria hiyo kwani serikali ndio iliyopeleka ili vyama vya siasa viendeshwe kwa demokrasia na sio kama ilivyo kwa sasa.

Mchange amesema vyama vinajiendesha kwa kuwa na watu wale wale lakini sheria hiyo baada ya kupita na kuwa mswada kutakuwa na ukomo wa viongozi. Amesema kuwa kama wadau wanawajibu wa kuzungumza hali inayoendelea bungeni kwa masilahi mapana ya Taifa. Aidha amesema kuwa sheria ya vyama vya siasa haimpi nguvu msajili wa vyama kama yeye bali kazi hiyo inafanywa na ofisi ya msajili nchi nzima.

Amesema kuwa vyama vya siasa vimekuwa vikipewa fedha lakini haijowi pamoja na watu wengine wakichangia lakini zinatumika bila kuingiliwa na mtu yoyote hali hii inawafanya wanachama kukosa haki ndani ya vyama vyao hasa vyama vya upinzani. "Tunataka watu wajadili vitu vyenye hoja kwa mstakabali wa Taifa na kuondoa masuala ambayo yalikuwa katika vyama siasa vya kufanya visihojiwe katika matumizi ya fedha na madaraka ya viongozi wa wakuu".amesema Mchange.

Mchange amesema kuwa ndani ya sheria hiyo imeondoa kuwepo kwa vikundi vya ulinzi  katika vyama ambapo vikundi hivyo vimekuwa vikifanya visivyo kwa kuwadhuru wasio na hatia.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jukwaa la Katiba (ADO) Habibu Mchange akizungumza na waandishi habari juu ya wabunge kujadili sheria ya vyama siasa kwa kuangalia masilahi mapana ya Taifa.

PRECISION AIR YAWA MSHIRIKA WA MASHINDANO YA KILIMANJARO MARATHONI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Shirika la ndege linaloongoza Tanzanaia Precision Air limetangaza kuwa msafirishaji rasmi wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon.


Taarifa hiyo imetolewa na Meneja Masoko na Mahusiano wa shirika hilo Hillary Mremi kuwa wameamua kushiriki katika mashindano ya mwaka huu ili kuweza kuwezesha washiriki na watu wengine wanaoenda kufuatilia kupata fursa ya kwenda kwa bei rahisi.

Mashindano haya Kilimanjaro Marathon si tu kwamba yanasaidia kuinua vipaji vya wanariadha hapa nyumbani,lakini pia yanatangaza utalii kwa nchi yetu na Shirika la Precision Air kama wadau wakubwa wa utalii nchini wameamua kushiriki katika tukio hilo.

“Kilimanjaro Marathoni ni moja kati mbio za riadha zilizofanikiwa sana katika Ukanda wa Afrika Mashariki na ni furaha kubwa kwetu kua sehemu ya mashindano haya. Tukiwa kama shirika la Ndege linaloongoza Tanzania na tukiwa na safari zinazoiunganisha Kilimanjaro na Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Nairobi na Entebbe tumejizatiti kutoa usafiri wa anga wa haraka, uhakika na nafuu kwa wale wote wanaopanga kushiriki.” 

“ Tuna wasihii wale wanaopanga kuhudhuria Kilimanjaro Marathon mwaka huu, kuchangamkia fursa ya punguzo la nauli kwa safari zetu zote za ndani ya nchi, ambapo wanaweza kujipatia tiketi ya kwenda tu, kwa nauli ya kuanzia SH.90,000/-. Kupitia safari zetu 6 kati ya Dar es Salaam – Kilimanjaro, safari tatu kati ya Nairobi-Kilimanjaro, safari moja kati ya Mwanza – Kilimanjaro na safari moja kati ya Entebbe – Kilimanjaro abiria wetu watakua na uhuru mkubwa wakuchagua muda wa safari wakati wakipanga safari zao,"alisema Mremi

Mashindano ya Kilimanjaro Marathon ambayo yalianzishwa mwaka 2003 na kampuni ya Wild Frontiers yakiwa na lengo la kuutangaza utalii Tanzania yameendelea kukua na kuwa moja ya matukio makubwa ya kimichezo katika ukanda wa Africa Mashariki na Afrika nzima kwa ujumla. 

Akizungumzia udhamini wa Precision Air, Mkurugenzi wa Mbio hizo, John Addison amesema wanayofuraha kulikaribisha shirika hilo kama mshirika rasmi wa mashindano hayo. 

“Ushirikiano tunaopata kutoka kwa mashirika ya nyumbani kama Precision Air umesaidia kwa kiwango kikubwa kukuza hadhi ya mashindano haya na kuwezesha watu wengi zaidi kushiriki ikiwa ni pamoja na wanariadha na mashabiki watakao safari kuelekea Kilimanjaro kwa gharama nafuu kwa ajili ya kushiriki riadha pamoja na kusheherekea.” Alieleza Bw. Addison.

Meneja Masoko na Mahusiano wa Shirika la ndege linaloongoza Tanzanaia Precision Air Hillary Mremi akizungumza na waandishi wa habari kuelekea  mashindano Kilimanjato Marathoni na ushirika wao katika kusafirisha washiriki kwa bei nafuu.

KNCV, Muhimbili waboresha huduma kwa wagonjwa wa kifua kikuu

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imekabidhiwa jengo la wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) lililokarabatiwa na mradi wa TB unaofadhiliwa na USAID chini ya Shirika la KNCV ili kusaidia wagonjwa wengi kutibiwa kwa wakati mmoja katika hospitali hiyo tofauti na awali.

Awali, wataalam wa Muhimbili walikuwa wakitoa huduma kwa wagonjwa sita hadi 10 kwa siku na kwa wiki walikuwa wakitibiwa wagonjwa 30 hadi 40. Lakini hivi sasa baada ya ukarabati wa jengo hilo wagonjwa 10 watakuwa wakilazwa kwa wakati mmoja na wangine 50 wa nje watakuwa wakitibiwa kila siku.

 Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko huo, Dkt. Vishnu Mahamba amesema ukarabati wa jengo hilo umegharimu TSh. milioni 69 na kwamba wametoa msaada wa ukarabati ili kuhakikisha wagonjwa wa kifua kikuu wanapata huduma bora.

Akizungumzia msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru alishukuru mfuko huo kwa kusaidia ukarabati wa jengo hilo  kwani litakuwa na manufaa kwa wagonjwa mbalimbali wanaotibiwa katika hospitali hiyo.

Pia, Prof. Museru aliagiza jengo hilo lianze kutumika mara moja baada ya kukabidhiwa kwa uongozi wa hospitali hiyo na kwamba wataalam wanapaswa kuweka mahitaji muhimu vikiwamo vitanda pamoja na vifaa vingine ili kuanza mara moja kwa huduma za matibabu.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani wa Muhimbili, Dkt. Amina Mgunya amesema kwamba jengo hilo watalitumia kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa ndani na nje wa kifua kikuu na wa kifua kikuu sugu.

Dkt. Mgunya amesema mbali na ukarabati wa jengo hilo, pia wagonjwa watakuwa wakipatiwa matibabu yote Muhimbili badala ya kupelekwa Hospitali ya Kibong’oto mkoani Kilamanjaro kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Kuanzia sasa wagonjwa wa kifua kikuu watakuwa wakipatiwa matibabu yote Muhimbili badala ya kupelekwa Kibong’oto kwa ajili ya matibabu zaidi,” amesema Dkt. Mgunya.

Naye Mkuu wa Idara ya Huduma za Uuguzi Muhimbili, Yassin Munguatosha amesema wamepokea agizo la Prof. Museru na kwamba agizo hilo watalitekeleza maramoja ili kuhakikisha wagonjwa wa kifua kikuu wanapatiwa matibabu katika jengo hilo.

Mbali na ukarabati wa jengo hilo, pia, Muhimbili imekarabati jengo lingine ambalo wataalam wa ugonjwa wa kifua kikuu watakuwa wanalitumia kutoa huduma.

Wagonjwa wa kifua kikuu wamekuwa wakionwa na wataalam katika Kituo cha Magonjwa Yanayoambukiza kwa njia ya hewa (IDC) na baadaye kupelekwa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

 Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akikata utepe ikiwa ishara ya kufungua  jengo la wagonjwa wa kifua kikuu lililokarabatiwa na mradi wa TB unaofadhiliwa na USAID chini ya Shirika la KNCV. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili, Dkt. Hedwiga Swai, katikati ni Ofisa Mradi wa Shirika la KNCV, Irene Mauya na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la KNCV, Dkt. Vishnu Mahamba.
  Ofisa Mradi wa Shirika la KNCV, Irene Mauya akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru wa tatu kutoka kushoto. Wengine ni wataalam wa MNH wakimsikiliza ofisa huyo.
  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani wa Muhimbili, Dkt. Amina Mgunya akitoa maelezo kwa Prof. Museru wa pili kushoto kuhusu matumizi ya jengo hilo.
 Mkuu wa Kitengo cha Majengo Muhimbili, Injinia Gama Kimoto akimweleza Prof. Museru kuhusu ukarabati wa jengo litakalotumiwa na wataalam wa kifua kikuu wakati wa kutoa tiba. Jengo hilo limekarabatiwa na Muhimbili.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru akizungumza na wataalam wa MNH  na maofisa mradi wa Shirika la KNCV kuhusu ukarabati na matumizi ya jengo hilo baada ya kukabidhiwa leo.
 Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa MNH na maofisa mradi wa Shirika la KNCV. Nyuma ni jengo la wagonjwa wa kifua kikuu lililokarabatiwa na KNCV

BENO KAKOLONYA AMEANDIKA BARUA YA KUVUNJA MKATABA- LUKUMAY

$
0
0
Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii
Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kuwa tayari wameshamalizana na golikipa wao Beno Kakolanya ingawa wamepokea barua ya kuvunja mkataba.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo Samwel Lukumay amesema kwamba mlinda mlango Beno Kakolanya haidai klabu hiyo katika kipindi hiki baada ya kumaliziwa stahiki zake ambazo amekuwa akizidai.

Lukumay amesema ingawa wameweza kumaliza kumlipa stahiki zake zote, uongozi kwa  siku ya jana umepokea barua kutoka kwa mwanasheria wa Beno wakihitaji kuvunja mkataba wake jambo ambalo amedai uongozi utakaa na kulijadili kwa undani kwani mchezaji alishalipwa stahiki zake kabla ya madai hayo ya kuvunja mkataba.

Amesema kwamba kimsingi hadi kufikia sasa mchezaji ni wa Yanga hivyo kama dhamira yake ni kuvunja mkataba basi ni vizur taratibu zikafuatwa.

Aidha amesema kwamba swala la yeye na kocha mkuu wa klabu Mwinyi Zahera ni jambo ambalo mchezaji alipaswa kuwasiliana na uongozi au kocha mwenyewe ili kulipatia ufumbuzi jambo ambalo hakulifanya.

Kwa mujibu wa Lukumay amesema kwamba katika usajili wa msimu uliopita Beno amesaini mkataba wa miaka miwili hivyo bado angali na mkataba wa muda mrefu kusalia ndani ya klabu hiyo.

HOSPITALI YA KANDA MBEYA YATIMIZA NDOTO ZA UPENDO TABELA MLEMAVU WA MACHO KUTOKA MBOZI

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt Paul Lewala(mwenye Miwani) akimkabidhi Vifaa vya ushonaji kwa Ndg Upendo Tebela Mlemavu wa Macho kutoka wilayani Mbozi.  Kushoto ni Katibu wa Hospitali Ms Mryiam Msalale na Muuguzi Mkuu Petro Seme(mwenye Kaunda suti)

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda mbeya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Dkt Paul Lewala(mwenye Miwani), Katibu wa Hospitali Ms Mryiam Msalale, Muuguzi Mkuu Petro Seme(mwenye Kaunda suti) na wafanyakazi katika picha ya pamoja na Ndugu Upendo Tebela.

MGUNDUZI WA MADINI YA TANZANITE MZEE NGOMA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, Jummane Ngoma amefariki dunia leo Jumatano Januari 30, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mtoto wa marehemu, Hassan Ngoma amesema, “Ni kweli Mzee amefariki leo jioni hii hapa Muhimbili,” amesema Ngoma 
Hassan amesema kinachofanyika kwa sasa ni kuuhifadhi mwili wa baba yake kisha baadaye watatoa taarifa rasmi ikiwamo utaratibu wa msiba utakuwa wapi na mazishi yatafanyika wapi baada ya kikao cha familia.

Aprili 6 mwaka jana, Rais John Magufuli akizindua ukuta wa mgodi wa Tanzanite, Mirerani mkoani Manyara alimzawadia Sh100 milioni kama shukrani kwa mchango wake kwa kugundua madini hayo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wenginme wakimsikiliza Mzee Jumanne Ngoma akitoa shukurani zake kwa kutambuliwa na serikali na kupewa shilingi milioni 1000 na Rais kama ahsante yake wakati wa sherehe za kuzindua rasmi ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara  Aprili 6, 2018. Picha na Maktaba 

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI,JANUARI 31,2019

Tigo yatoa zawadi kwa Mawakala waliofanya vizuri mwishoni mwa mwaka 2018

$
0
0
 Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed, akifurahia jambo na mshindi wa jumla wa Promosheni ya Chifu wa Mawakala Vicky Ibrahim wakati akimkabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 20 jijijini Dar es Salaam jana.

 Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed, (kushoto) akimkabidhi Said Khatibu (kulia)  ambaye ni mmoja kati wa mawakala watano wa Tigo Pesa watano walioibuka washindi wa shilingi milioni 2 kutoka kanda ya Pwani katika Promosheni ya mwisho wa mwaka 2018 inayojulikana kama Chifu wa Mawakala. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Bidhaa Tigo Pesa James Sumari.

 Washindi wa Promosheni ya Chifu wa Mawakala kutoka kanda ya Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa huduma ya Tigo Pesa kutoka kampuni ya Tigo muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi zao za fedha taslimu.

Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed, (kushoto) akimkabidhi Hajira Saidi(kulia)  ambaye ni mmoja kati wa mawakala watano wa Tigo Pesa watano walioibuka washindi wa shilingi milioni 2 kutoka kanda ya Pwani katika Promosheni ya mwisho wa mwaka 2018 inayojulikana kama Chifu wa Mawakala. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Bidhaa Tigo Pesa James Sumari.


 Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed, (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kutoa zawadi za fedha taslimu kwa washindi kutoka kanda ya Pwani wa Promosheni ya mwisho wa mwaka inayojulikana kama Chifu wa Mawakala. Kulia ni Mkuu wa Bidhaa wa Tigo Pesa James Sumari.



Kampuni ya Tigo Tanzania, imetoa zawadi ya fedha taslimu kwa mawakala wake wa Tigo Pesa waliofanya vizuri katika promosheni ya mwisho wa mwaka 2018 inayojulikana kama “Wakala Chief Promotion”.


Kupitia promosheni hiyo, wakala aliyefanya vizuri kuliko wote nchini, amepokea zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 20 wakati mawakala wengine wanaofuatia kwa kufanya vizuri kutoka kanda nne wakipokea jumla ya shilingi milioni 40.


Akiongea wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi zao, Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed alisema promosheni hiyo imewekwa maalum kwa ajili ya kuwashukuru na kuwazadia mawakala wanaofanya vizuri katika kipindi cha mwisho wa mwaka.


Hussein alisema, washindi 20 kutoka kanda nne ambazo ni Pwani, Kusini, Kaskazini na Kanda ya Ziwa walipatikana ambapo kila kanda ilitoa washindi watano ambao kila mmoja alijinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni mbili wakati mshindi wa jumla akiondoka na shilingi milioni 20.


“Jumla ya mawakala 90,000 walishiriki katika promosheni hii ya nchi zima iliyoanza tarehe 1 Disemba na kumalizika tarehe 31 Disemba 2018,” alisema


Kwa upande wake Mkuu wa Bidhaa Huduma za Kifedha kwa njia ya Simu, James Sumari aliongeza kwa kuwashukuru Mawakala kwa mchango wao mkubwa katika kufikisha huduma za kifedha kwa wantanzania


“Tunayofuraha kutoa mchango unaowezesha wananchi wengi kufikiwa na huduma za kifedha. Kupitia huduma ya Tigo Pesa, tumewawezesha mamilioni ya Watanzania kutuma na kupokea fedha na kufanya malipo mbali mbali kwa urahisi na kwa usalama. Tigo Pesa ni zaidi ya suluhisho kwa malipo na huduma rahisi za kifedha, ni sehemu ya maisha,” alisema Sumari.


Vicky Ibrahim ambaye ni mshindi mkubwa katika promosheni hiyo kutoka Kanda ya Pwani mkoa wa Dar es Salaam alisema, shilingi milioni 20 alizojishindia zitamsaidia kupanua biashara yake hiyo ya Tigo Pesa huku akiishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo.


“Ninayo furaha kubwa kupokea zawadi hii ambayo kimsingi sikuitarajia. Nitatumia fedha hizi kupanua biashara yangu na kutatua matatizo yangu binafsi ambayo yanahitaji fedha,” alisema.


MKUTANO MAALUM WA 38 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza kama kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye Kikao Maalum cha 38 cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kinachofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 30 Januari 2019 ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 1 Februari 2019. Wengine katika picha ni Kapt. Mstaafu, Mhe. George Mkuchika (kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maejimenti ya Utumishi wa Umma na Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango. Anayeonekana nyuma ya Mhe. Mkuchika ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe. 
Mawaziri hao wakipitia nyaraka mbalimbali wakati wa kikao hicho 
Mwenyekiti wa Kikao Maalum cha 38 cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda, Mhe. Kirunda Kivejinja (wa pili kulia), ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza hilo. 
Ujumbe wa Burundi ukiwa kwenye kikao hicho cha Baraza la Mawaziri 
Ujumbe wa Kenya nao ukifuatilia kikao 
Mjumbe kutoka Sudan Kusini (kushoto) akiwa katika meza moja na ujumbe wa Rwanda wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri 
Ujumbe wa Uganda nao ukifuatilia kikao 
Wajumbe wa Tanzania wakiongozwa na Mawaziri wakifuatilia kikao. Kulia ni Naibuu katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bibi Amina KH. Shaaban 
Dkt, Aloyce Nzuki, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii akiwa na Bw. Stephen Mbundi, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima (kushoto) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao cha Baraza la Mawaziri 

Wajumbe wengine wa Tanzania


====================================================




KUHUSU MKUTANO MAALUM WA 38 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Mkutano Maalum wa 38 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unafanyika jijini Arusha kwa lengo la kujadili na kukubabaliana na agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 1 Februari, 2019.

Mkutano huo ambao unaongozwa na Mwenyekiti kutoka Jamhuri ya Uganda ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Kirunda Kivejinja utajadili agenda mbalimbali muhimu ambazo ni pamoja na ripoti ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, taarifa kuhusu masuala ya miundombinu, forodha na biashara na ripoti ya kamati ya utawala na fedha.

Agenda zingine ni taarifa ya Baraza kwa Wakuu wa Nchi kuhusu utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yanayofiwa kwenye mikutano ya Wakuu hao wa Nchi na Kalenda ya Matukio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2019.

Mkutano huo wa Mawaziri ulitanguliwa na vikao vya Maafisa Waandamizi kutoka nchi wanachama kilichofanyika tarehe 28 Januari kikifuatiwa na kikao cha Kamati ya Uratibu chini ya Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama kilichofanyika tarehe 29 Januri 2019.

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo unaongozwa na Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuwahusisha pia Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), Waziri wa , Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Waziri Fedha na Mipango, Mhe. Kapt. Mstaafu George Mkuchika (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Joseph Kakunda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara na Mhe. Innocent Bashungwa, Naibu Waziri wa Kilimo. 

Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inaundwa na nchi sita za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini imeendelea kuhakikisha wananchi katika nchi hizo wananufaika na Jumuiya hiyo hususan katika nyanja za biashara, ulinzi na usalama, viwanda, kilimo, miundombinu na huduma za kijamii. 


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Arusha.
30 Januari 2019



IFAHAMU MIKAKATI YA JESHI LA MAGEREZA TANZANIA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, Kamishna Jenerali Phaustine Kasike amesema wanaendelea na mpango wa kuhamisha wafungwa kutoka kwenye magereza yasiyo na shughuli za kilimo na kuwahamishia kwenye Magereza ya kilimo ili kufikia malengo ya kimkakati ya kuzalisha chakula kwa ajili ya kutosheleza wafungwa na mahabusu wote hapa nchini. Ameyasema hayo mara baada ya kukagua shamba la mahindi la Gereza la Kitai lililopo katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ambapo gereza hilo pia ni miongoni mwa magereza 10 hapa nchini, ambayo yameteuliwa kwenye mpango mkakati wa mradi wa kilimo kwa ajili ya chakula cha wafungwa na mahabusu.
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live




Latest Images