Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

OHOOOO....! DALA DALA YACHOMOKA TAIRI NA KUPARAMIA MTARO.

$
0
0
 Baadhi ya Wananchi wakishuhudia ajali ya Daladala ambalo lilichomoka tairi na kuingia mtaroni eneo la Mlango mmoja, Mwanza  kama lionekanavyo pichani,hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.
 


Mchango wa biashara za mtandaoni katika ukuaji wa biashara Afrika

$
0
0

Mchango wa biashara za mtandaoni katika ukuaji wa biashara Afrika

Waafrika milioni 400 wanatumia intaneti.

Mahitaji ya Waafrika ni sawa na kwingineko duniani kote. Wanahitaji bidhaa nzuri, bora na zenye bei nafuu.

Licha ya kutazamwa kwa mitazamo tofauti na mataifa mengi yaliyoendelea duniani, Afrika imeonyesha kuwa shughuli nyingi zinaweza kufanyika na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kwa miaka kadhaa sasa makampuni makubwa kutoka Ulaya, Marekani na Asia yamefungua matawi ya biashara zao na kufanikiwa. Vilevile, maelfu ya biashara mpya zimekuwa zikianzishwa na kufungua fursa nyingi katika sekta mbalimbali.

Afrika ni ya pili kwa kuwa na watumiaji wengi wa mtandao wa intaneti ukiachana na China, ambapo kwa sasa ina watumiaji wa mtandao wa intaneti takribani milioni 400, ambapo idadi ya Waafrika wote ni zaidi ya bilioni 1.2.
Idadi hiyo kubwa ya Waafrika wanaotumia intaneti imekuja na fursa ya biashara ya mtandaoni ambayo imekuwa ikifanyika kwa miaka takribani 20 sasa katika nchi za Marekani na Ulaya. Aina hii ya biashara inahusisha uuzaji na ununuzi wa bidhaa kutoka kwa wauzaji tofuati kwa njia ya mtandao katika sehemu moja.

Katika mahojiano yaliyofanywa hivi karibuni baina ya mmojawapo wa waanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia, Bw. Sacha Poignonnec na kampuni ya McKinsey & Company ameelezea kuwa mwanzoni ilikuwa ni vigumu kufanya uamuzi wa kufanya biashara Afrika kutokana na changamoto na ugumu ambao waliambiwa wangekutana nao.

“Wakati tunaanza shughuli zetu kwa mara ya kwanza kabisa jijini Lagos nchini Nigeria, tulifungua tovuti yetu hakuna aliyekuwa anatujua lakini wateja walinunua simu za mkononi. Nilishangazwa sana na ile shauku ya wateja kununua bidhaa, tena za gharama ya juu. Cha kustaajabisha zaidi tulifanikiwa kuuza bidhaa na kuzipeleka mpaka walipo wateja. Kwa kweli, ilitia moyo kuona mambo mazuri yakitokea kuliko mabaya tuliyoyasikia,” alielezea Bw. Poignonnec.

“Nina matumaini makubwa na biashara ya mtandaoni Afrika kwasababu kitu cha upekee kuhusiana na bara hili ni kwamba tayari nusu ya idadi ya watu wake wameunganishwa. Kati ya watu zaidi ya bilioni 1.2, milioni 400 wanatumia mtandao wa intaneti. Idadi hii ni ya pili duniani ukiachana na China. Hata hivyo, mbali na idadi hiyo bado kuna mazingira magumu ya usambazaji wa bidhaa na huduma. Hii imekuwa ni changamoto kubwa kwa wateja pale wanapohitaji kufanya manunuzi. Lakini, kwa sababu ya matumizi ya simu za mkononi na intaneti, wateja hivi sasa wanao uwezo wa kuzifikia huduma katika njia iliyo rahisi zaidi,” aliongezea.

Bw. Poignonnec aliendelea mbele zaidi kwa kuelezea kuwa tabia za wateja wanaopatikana Afrika hazitofautiani na sehemu zingine. Mahitaji ni yaleyale. Wanahitaji bidhaa nzuri na bora ambazo zinapatikana kwa bei nafuu. Siku zote wateja wanahitaji kuokoa muda na gharama. Katika maeneo mengi ambayo tunafanya shughuli zetu tunawasaidia wateja kuwa na machaguo mengi ya kununua bidhaa kitu ambacho hakipo katika maeneo wanayoishi.

Katika kipindi cha miaka takribani sita tangu Jumia ianze kufanya shughuli zake barani Afrika changamoto kubwa iliyokumbana nayo ni mfumo wa uendeshaji.

Ameelezea kuwa kwa anayeifahamu Afrika vizuri ni kwamba haina mfumo mzuri wa anwani za makazi katika majiji yake mengi. Hivyo basi kwa watoa huduma kama wao ili kuwafikia wateja vizuri ni lazima washirikiane na wauzaji wa nyumbani ambao ndiyo wanayafahamu vizuri maeneo yao. Kwa mfano, mteja anaweza kuagiza bidhaa lakini anwani ya mahali anapoishi inaweza kuwa ni kwa kuelezea majengo yanayopatikana karibu au shughuli maarufu zinazopatikana eneo alilopo.

Kwa hiyo, endapo ukishirikiana na wauzaji sahihi wanaopatikana kwenye eneo hilo na wenye ufahamu sahihi wa maeneo yao utaweza kuwafikia wateja wote kwa urahisi. Lakini mfumo huu pia nao changamoto zake, vingenevyo uwe na mfumo mzuri wa uendeshaji ambao tumeutengeneza. Tunatumia nyenzo na mifumo ya kiteknolojia ambayo tunawapatia ili waweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, kama vile malipo baada ya bidhaa kufika pamoja na huduma mpaka alipo mteja.

Kuna fursa nyingi endapo waafrika wataamua kuitumia ipasavyo fursa ya biashara kwa njia ya mtandaoni. Tofauti na nchi za Marekani na Ulaya ambapo biashara nyingi huanzia madukani na kuhamia mtandaoni, kwa Afrika wafanyabiashara wengi wanaanzia mtandaoni na kisha hufungua maduka. Sababu kubwa ni kwamba hakuna gharama kufanya biashara mtandaoni.

Ili kujiunga na Jumia kuifanya biashara yako iwepo mtandaoni hauhitaji gharama yoyote kujiunga, hakuna malipo ya kila mwezi au pango la duka, fursa ya kujitangaza na kutafuta masoko ni bure, kuna fursa kubwa ya kuwafikia wateja wengi waliopo maeneo mbalimbali ndani ya muda mfupi pamoja na uhakika wa bidhaa kuwafikia wateja mpaka pale walipo.

Hivyo basi kama mfanyabiashara unaweza ukaanza kidogokidogo mtandaoni, ukawekeza ile faida ndogo unayoipata, baada ya hapo unakua kiasi ambacho unaweza kufungua duka kubwa na kuajiri watu wengi zaidi.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 30,2019

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA EAC

$
0
0
Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (aliyekaa mbele), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha maandalizi kabla ya kushiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kilichofanyika jijini Arusha tarehe 29 Januari 2019. Pamoja na mambo mengine kikao cha Makatibu Wakuu kilipokea na kujadili taarifa mbalimbali zilizowasilishwa kwao na wajumbe wa ngazi ya Wataalam. Kikao cha Makatibu Wakuu kitafuatiwa na kikao cha Baraza la Mawaziri kitakachofanyika tarehe 30 Januari 2019 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 1 Februari 2019. 
Bw. Stephen Mbundi (katikati), Kiongozi wa kikao cha ngazi ya wataalam ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoa taarifa kwa Makatibu Wakuu. Wengine katika picha ni Dkt. Yamungu Kayandabila (kushoto), Naibu Gavana na Bw. Bernard Haule, Kaimu Mkurugenzi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Evaristo Longopa (wa pili kulia) akichangia jambo wakati wa kikao cha maandalizi ya ushiriki wa Tanzania kwenye kikao cha Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wengine katika picha ni Prof. Sifuni Mchome (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Joseph Buchweshaija, Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara na Prof. Siza Tumbo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo. 
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Aziz Mlima (kulia) akifuatilia kikao hicho akiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina KH. Shaaban 
Wajumbe ambao ni Wataalam kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakifuatilia kikao 
Kikao kikiendelea 
Wajumbe wengine wakiwa kwenye kikao 
Wajumbe wa kikao wakifuatilia kikao 
Wajumbe kutoak Wizara, Idara na Taasisi za Serikali walioshiriki kikao 
Wajumbe wengine nao wakifuatilia kikao 
Wataalam wa masuala mbalimbali kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali wakiwa kwenye kikao 
Wataalam wakinukuu masuala mbalimbali yaliyokuwa yanajadiliwa kwenye kikao hicho 
Kikao kikiendelea 
Kikao kikiendelea 

WAKENYA WATUA NCHINI KUJIFUNZA MIRADI YA MAJI TAKA

$
0
0


Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA). 

Ujumbe huo ulilenga kutembelea na kujionea miradi ya majitaka maeneo ya Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi maalum ya Maji Taka inayotekelezwa katika maeneo yasiyopimwa na yenye msongamano. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutoka Kampuni ya majisafi na majitaka Nairobi (NCWSC) na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundi vya jamii wapo nchini kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti Rahimu Seif Gassi (kulia) kiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutokea upande wa Maji na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundu vya jami wapo nchini kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza.

Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Moja ya Choo cha kisasa vinavyojenga na Shirika la CCI kwa kusaidiana na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) ili kuwawezesha wananchi wanaoishi katika maeneo yasiyo rasmi.
Moja ya chemba za vyoo vya kisasa.
Muonekano wa Choo cha zamani ambacho wakazi wa Vingunguti walivyokuwa wakitumia.
Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam akionyesha namna mabomba ya vyoo yalivyopita.
Wageni wakiendelea na ziara.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti jijini Dar es Salaam, Rahimu Seif Gassi (kulia) kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Wananchi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam akiwakaribisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Wananchi wakimsikiliza mwenyekiti.
Bi Kellen Muchira kutoka Shirika la Caritas Switzerland lililopo nchini Kenya akizungumza machache juu ya jinsi walivyoweza kufika Tanzania kujifunza namna ya Shirika la CCI na DAWASA wanavyoweza kushirikiana kuwasaidia wakazi wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi kukusanya Maji Taka.
Afisa Miradi wa Akiba Mahirani Trust ya nchini Kenya, Patriki Njoroge akieleza machache mbele ya wakazi wa Vinguti jijini Dar es Salaam wakati walipofika Tanzania kujifunza namna ya Shirika la CCI na DAWASA wanavyoweza kushirikiana kuwasaidia wakazi wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi kukusanya Maji Taka.
Makazi wa Vingunguti akisoma risara mbele ya wageni.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Mhandisi Charles Makoye akiwaelezea juu ya mradi wa kuchakata maji Taka uliopo Toangoma wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) huku wakiwa wamelenga eneo la Vingunguti na Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye miradi ya maji Taka.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) (mwenye shati jeupe) akiwaonyesha chemba ya mradi wa kuchataka Maji Taka iliopo Toangoma jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Mhandisi Charles Makoye (Kulia) akiendelea kutoa maelezo.
Wageni wakiwa katika picha ya pamoja.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE AHITIMISHA ZIARA YAKE MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI, MKOANI RUVUMA

$
0
0
Mkuu wa Magereza Mkoani Ruvuma, ACP. Alexander Nyefwe akimwelezea Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) juu ya wadudu wanaoshambulia mahindi katika shamba hilo hata hivyo tayari wamekwishapiga dawa za kuzuia wadudu hao.
Askari wa Gereza Kitai, Sajini Edga Mwakibinga akiimarisha ulinzi ndani ya mashamba ya mahindi wakati wafungwa wakiendelea na kazi ya palizi katika mashamba hayo ya Gereza, januari 29, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akizungumza na Wafungwa wa Gereza la Kitai waliokuwa wakiendelea na kazi ya palizi katika mashamba ya mahindi baada ya kumaliza kukagua mashamba hayo, januari 29, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani)akiangalia miundombinu inayotarajiwa kutumika katika kilimo cha umwagiliaji katika mashamba ya gereza Kitai ili kufikia malengo ya mpango mkakati wa kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike mashine ya kuzalisha nishati ya umeme wa maji katika Gereza la Kitai ambapo kwa sasa mashine hiyo haifanyi kazi kutokana na baadhi ya vifaa kuungua.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Pololeti Kamando(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa pili toka kushoto) alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, januari 29, 2019. Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa huo(Picha na Jeshi la Magereza).
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) akipokea taarifa ya Magereza Mkoa kwa Mkuu wa Magereza Mkoani Ruvuma, ACP. Alexander Nyefwe kabla ya kutembelea Gereza Mahabusu Songea na Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai lililopo Wilaya ya Mbinga, januari 29, 2019.
Mkuu wa Gereza Kitai – Nkasi, SSP Sylivester Shija akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike alipowasili gerezani hapo katika ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua mashamba ya mahindi ya Gereza hilo, januari 29, 2019.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WIZARA YA KILIMO MALIASILI MIFUGO NA UVUVI ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar,kuhusiana na maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara hiyo,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kulia Mshauri wa Rais Masuala ya Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Abdulrahman Mwinyijumbe, mkutano huo umefanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasi, Mifugo na Uvuvi Zanzibar,kuhusiana na Maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara hiyo,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Kilimo Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma, wakiwa katika ukumbi wa mikutano Ikulu Zanzibar.
WAZIRI wa Kilimo, Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar. Mhe. Rashid Ali Juma, akiwasilisha ripoti ya Maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara yake ,wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hayuko pichani na kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu)
VIONGOZI wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar, wakifuatilia taarifa ya maendeleo ya Miradi ya Wizara hiyo, wakati ikiwasilishwa na Waziri wa Kilimo Maliasi, Mifugo na Uvuvi.Mhe. Rashid Ali Juma, wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Bi. Maryam Juma Sadalla, akichangia wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein,kuzungumzia maendeleo ya Miradi ya Wizara hiyo, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, katika ukumbi wa mikutano Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MAAGIZO YA NAIBU WAZIRI NDUGULILE KWA MAAFISA USTAWI WA JAMII NCHINI


Korosho Yaingiza Serikali fedha za Kigeni Zaidi ya Tsh. Trilioni Moja

$
0
0

Zao la Korosho katika kipindi kilichoishia Januari 2018 liliingizia Taifa fedha za kigeni shilingi 1,136,609,586,722 ikilinganishwa na mazo mengine ya biashara.

Akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Maftaha Abdallah Nachuma, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omari Mgumba, amesema licha mchango huo katika uchumi wa Taifa, zao la korosho limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo Serikali imekuwa ikizitafutia ufumbuzi ikiwemo kuongeza bei ya korosho na kutafuta masoko ya uhakika.

Mhe. Mgumba amezitaja changamoto hizo kuwa ni kuyumba kwa bei ya korosho katika soko la dunia kutokana na zao hilo kuuzwa likiwa ghafi yaani bila kuongezwa thamani, tija ndogo katika uzalishaji, baadhi ya wakulima kutotumia miche bora na matumizi hafifu ya pembejeo ikiwemo viuadudu kama salfa na wakulima kutozingatia kanuni bora za kilimo katika uzalishaji.

Aidha, Mhe. Mgumba amezitaja changamoto nyingine kuwa uvunaji na uhifadhi hafifu wa korosho, uwezo mdogo wa maghala ya kuhifadhia korosho na baadhi ya wakulima kuchanganya zao hilo na mawe na mchanga kwa ajili ya kuongeza uzito wakati wa mavuno.

“Katika kukabiliana na changamoto hizo, Serikali imeboresha mfumo wa uuzaji wa korosho kwa kuimarisha usimamaizi na ukaguzi kuanzia ngazi ya vyama vya msingi, maghala makuu, maghala aya hifadhi na kutoa elimu, kurejesha kwa kiwanda cha BUCCO cha mkoani Lindi cha ubanguaji wa korosho, ujenzi wa maghala matatu ya kuhifadhia korosho katika mikoa ya Lindi, Pwani na Tanga ili kuongeza kiwango cha uhifadhi na ubora wa korosho pamoja na kuzalisha miche bora 10,000,000 na kuisambaza kwa wakulima bure,”alisema Mgumba.

Naibu Waziri Mgumba ameongeza kuwa mikakati mingine ni pamoja na kuimarisha mnyororo wa thamani katika zao la korosho ili kuongeza uzalishaji, kuimarisha usambazaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati, kutoa huduma za ugani pamoja na kuweka mazingira wezeshi na kuwajengea uwezo wabanguaji wa ndani kwa lengo la kuongeza thamani ya korosho inayozalishwa nchini.

Akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye aliyetaka kujua hatua zilichukuliwa na Serikali kuhusu vitendo vya rushwa katika kuhakiki ununuzi wa Korosho, Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga alisema kuwa wote waliojihusisha na vitendo hivyo hatua kali zilichukuliwa dhidi yao ikiwemo kusimamishwa kazi.

Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa na dhamira ya dhati ya kuwainua wakulima nchini ikiwemo wa korosho kwa kuongeza bei ya korosho na kusimamia ununuzi wake. Jambo ambalo limekuwa kichocheo kwa wakulima wengi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Tanga kujikita katika kilimo hicho.

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli mwishoni mwaka 2018 alisema Serikali itanunua korosho kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo. Jambo ambalo lilifanyiwa kazi na wakulima wa zao hilo wanafurahia bei hiyo na kutambua kuwa Serikali inawajali.

AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII NA TAMISEMI

WAZIRI MHAGAMA AWASILISHA RASMI BUBGENI MUSWADA WA VYAMA VYA SIASA

$
0
0

*Wabunge waanza kuuchambua,Halima Mdee ataka Bunge kuchukua tahadhari


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana na Ajira amewasilisha rasmi Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ambapo baada ya kuwasilisha wabunge mbalimbali wameuchambua na kutoa maoni yao.

Hata hivyo baadhi ya wabunge hasa wa Vyama vya Upinzani ambao wamechangia mjadala kuhusu muswada huo wametilia shaka baadhi ua vipengele na kuomba Bunge kuviangalia kwa umakini mkubwa.

Wakati anawasilisha Muswada huo wa Marekebisho ya Sheria vya Vyama vya Siasa Waziri Mhaga ameliambia Bunge leo mjini Dodoma na lengo la muswada huo ni kuwa na sheria ya vyama vya siasa ambayo itamuwezesha Msajili wa Vyama vya Siasa kutekeleza majukumu yake vuzuri.

Amefafanua baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye muswada huo ambapo kabla ya hapo aliweka wazi mchakato wa muswada huo ulianza rasmi mwaka 2013 na ilipofika mwaka 2014 ulisimama kupisha mchakato wa Katiba Mpya na mwaka 2015 mchakato ukasimamishwa kupisha uchaguzi Mkuu.

"Muswada wa marebisho ya  Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018 unalenga kufanya mabadiliko mbalimbali kwa lengo la kumuwezesha Msajili wa Vyama vya siasa kufanya shughuli zake kwa ufanisi." Kama nilivyotangulia kueleza awali mchakato ulianza mwaka 2013 wakati ukusanyaji wa maoni na ilipofika mwaka 2014 ulisimama kwa ajili ya mchakato wa Katiba mpya na mwaka 2015 ulisimama kupisha uchaguzi mkuu.Muswada huu ninaouwasilisha leo hii umegawanyika sehemu kuu mbili,"amesema Waziri Mhagama.

Amefafanua muswada huo unampa nafasi Msajili wa Vyama vya Siasa kutekeleza majukumu yake ambapo akatumia nafasi hiyo kuelezea hatua kwa hatua vipengele vilivyomo kwenye muswada huo kikiwemo kipengele kinachovitaka vyama vya siasa kuheshimu Katiba ya nchi pamoja na alama kuu za Taifa.

Pia kuna vipengele ambavyo vinatoa maelekezo ya vyama vya siasa namna ya kupata viongozi wake pamoja na hatua zinazotakiwa kufuatwa kwa anayetaka kuanzisha chama cha siasa.

 Katika kipengele cha kuanzisha chama cha siasa moja ya sharti ni kwa anayeanzisha kuwa raia wa kuzaliwa wa Tanzania ambacho kinakwenda sambamba na uraia wa wazazi.Kipengele hicho kimeonekana kuibuq mjadala Bungeni.
 
Pamoja na mambo mengine muswada huo kwa mujibu wa Waziri Mhagama amesema  unaweka maelekezo ya jina la chama cha siasa kutofafana na chama kingine ili kuepuka migongano kati ya chama na chama.
Pia amesema muswada unaweka maelekezo ya jina la chama cha siasa kutofafana na chama kingine.Pia muswada huo una kipengele ambacho kinataka vyama vya siasa kuwasilisha orodha ya majina ya viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na kuwepo orodha ya wanachama kwa lengo la kumuwezesha msajili kuwa na kumbukumbu ya vyama husika.

Waziri Mhagama pia amesema muswada huo una kipengele ambacho kinaeleza kuwa  ni marufuku kwa vyama vya siasa kuwa na vikundi vya ulinzi ambapo kipengele hicho nacho kimeibua mjadala kwani wakati Mbunge wa Kawe Halima Mdee(Chadema) wakati anachangia ameonesha kutoridhishwa na uwepo wa kipengele hicho na kuomba Bunge na Kamati ya Katiba na Sheria kuangalia upya kipengele hicho.
Wakati huo huo Mdee wakati anacgangia muswada huo amesema si kweli kwamba wabunge wa vyama vya upinzani pamoja na vyama vya siasa nchini vinaukataa muswada huo kwani mwaka 2009 walipeleka muswada Bungeni kutaka sheria ya vyama vya siasa kufanyiwa marekebisho.

"Kambi ya upinzani bungeni mwaka 2009 tulipeleka muswada bungeni ili kuhakikisha sheria ya vyama siasa inafanyiwa marekebisho lakini ikakataliwa.Hatujawahi kuogopa kukaguliwa jana,leo na kesho,tuache kutumia propaganda katika jambo la Nchi.

"Watu hapa wanasema tusijadili mambo madogo,hivi kujadili jambo linalovunja Katiba ni dogo?Ibara ya 8 C ya muswada huu kinavunja Katiba," amesema Mdee na kufafanua kuna vipengele ambavyo vinaleta ubaguzi na hilo ni huko ni kuvunja Katiba ya nchi.

Amezungumzia pia kipengele ambacho kinataka kuwepo na orodha ya viongozi wa ngazi mbalimbali kwa kupeleka orodha hiyo kwa Msajili sambamba na kuorodhesha majina ya wanachama jambo ambalo ni gumu hasa kwa kuzingatia mwanachama anaweza kujiunga leo na kesho akatoka kwenye chama husika.

Pia ameonesha mashaka na kipengele cha kuzuia vyama vya siasa kuwa na vikundi vya ulinzi ambapo anasema kipengele hicho hakubaliani nacho .

CSI 2018 Social Impact: Highlights from Somalia, Tanzania, and Uganda

OPERESHENI JESHI LA POLISI KILIMANJARO YAKAMATA KILO 400 YA MIRUNGI NDANI YA SIKU SITA.

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga, Moshi.

OPERESHENI ya kukamata Dawa za kulevya inayoendelea mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kukamata kilogramu 320 na Dawa za kulevya aina ya Mirungi zikiwa kwenye gari aina ya Toyota Alphasad lenye namba za usajili T 308 DMC ikisafirishwa kuelekea mkoani Arusha.

Hili ni tukio la pili ndani ya siku sita kwa Jeshi la Polisi kufanikiwa kukamata kiasi kikubwa cha Dawa za Kulevya aina ya Mirungi ambapo tukio la karibuni kikosi cha Pikipiki cha jeshi hilo kilifanikiwa kunasa kilogramu 80 za Mirungi iliyokuwa ikisafirishwa kwa kutumia pikipiki kutoka nchi jirani ya Kenya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi,Hamis Issah alithibitisha kukamatwa kwa Dawa hizo za kulevya katika eneo la KIA zikiwa njiani kusafirishwa kuelekea Arusha kutokea nchi jirani ya Kenya .

“Tulipata taarifa uwepo wa gari nyeusi ambayo mwendo wake ulitiliwa shaka na askari wetu ,na kila walipokuta askari ilikuwa ikiwasha taa huku ikiwa mwendo wa kasi,ndipo katika kituo cha KIA askari walizuia magari yote na kufanikiwa kuikamata hiyo gari”alisema Kamanda Issah.

“Wale watu waliokuwa kwenye hii gari baada ya kuona askari wanawafuata walikimbia na kupanda pikipiki zilizokuwa pembeni yake na kutokomea kwa uelekeo wa Arusha na hata hii gari inaonekana uelekeo wake ulikuwa ni huko huko Arusha na tumefanikiwa kuikamata.”aliongeza Kamanda Issah.

Alisema gari lililokuwa limebeba mzigo huo wa dawa zakulevya litakuwa chini ya jeshi la Polisi huku akitoa wito kwa mmiliki wa gari hilo kujitokeza mwenyewe kabla hatua za kufuatilia katika vyombo vingine vya dola kuanza .

Katika tukio la hivi karibuni Polisi walikamata Majani ya Miringi yaliyokuwa yamefungwa katika vifurushi vidogo vidogo zaidi ya 50 na kisha kuwekwa kwenye mfuko mmmoja mkubwa maarufu kama Kiroba huku wahusika wakitumia pikipiki maarufu kama Bodaboda.

Alisema kundi la wasafirishaji wa Dawa hizo za kulevya ambao wamekuwa wakisafirisha kutoka nchi ya Kenya kupitia mpaka wa Holili pindi linapoingia barabarani limeonekana kuwa tishio na hatari kwa usalama wa watu wengine barabarani kwa namna wanavyoendesha pikipiki zao.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah akiwa ameshikilia dawa za kulevya aina ya mitungi baada ya kukamatwa katika eneo la KIA.
 Magunia yenye Dawa za kulevya aina ya Mirungi yakipimwa katika mzani mara baada ya kukamatwa yakisafirishwa kuelekea mkoani Arusha.
 Gari aina ya Toyota Alphasad lenye namba za s usajili T 308 DMC lilikuwa kumbeba dawa hizo aina ya Mitungi kilogramu 380.

 
 

MASAUNI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA NJOMBE KUHUSU UTEKWAJI NA MAUAJI YA WATOTO

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi  kuhusu matukio ya utekwaji na kuuliwa kwa watoto katika Mkoa wa Njombe, ambapo aliwaasa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika juhudi za kukomesha matukio hayo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri akizungumza na wananchi  kuhusu matukio ya utekwaji na kuuliwa kwa watoto katika Mkoa wa Njombe, ambapo aliahidi kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kukomesha matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto.
Mkazi wa Njombe, Alex Msupilo akimuuliza maswali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kukagua leseni za waganga wa tiba asilia ambao wamekua wakitajwa kufanya tiba chonganishi zinazopelekea kutokea kwa matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto katika mkoa huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika kikao kidogo kilichohusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe na baadhi ya wananchi lengo ikiwa ni kujadili juu ya matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto mkoani hapo.

MBUNGE ATAKA KUFAHAMU HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUKOMESHA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kusini Merndrad Kigola kupitia Chama Cha 
Mapinduzi (CCM), ameitaka Serikali kueleza ni hatua gani inazochukua ili 
kukomesha mauaji ya watoto katika Mkoa wa Njombe.

Akiuliza swali hilo leo Januari 30, 2019 bungeni Mjijini Dodoma, Kigola ameuliza ni mkakati gani uliopo katika kukomesha mauaji hayo ambayo yamesababisha hofu kubwa kwa wananchi wa Mkoa huo.

Akijibu swali hilo , Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amesema kuna hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za kukomesha mauaji hayo na tayari tangu Januari 28 mwaka huu Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni yupo mkoani Njombe ambako amekutana na kamati za ulinzi na usalama ya mkoa wakiendelea na vikao vya ndani.

"Tunaamini wote wanaojihusisha na vitendo hivyo watapatikana na sheria 
itachukua mkondo wake. Tunayo orodha ya maji ya watu ambao wanahusika na matukio hayo na sababu za kufanya hivyo ni mambo ya imani za kishirikiana,"amesema Lugola huku akisisitiza wanaofanya matukio hayo ya mauaji hayo waache mara moja.

Kwa kukumbusha tu wakati Serikali ikiendelea kuchukua hatua dhidi ya kuwasaka watu waliohusika na mauaji hayo, idadi ya watoto waliouliwa 
imefikia 13 kutokana na taarifa mbalimbali ambazo zimetolewa.

Wakati huohuo Lugola amezungumzia hatua ambazo Serikali inazichukua ili 
kupunguza msongamano wa mahabusu katika magereza nchini.Amesema hayo leo wakati anajibu swali aliloulizwa kuhusu hatua ambazo Serikali inachukua katika gereza la Mlele ambalo idadi ya mahubusu imekuwa kubwa.

"Kuna hatua ambazo Serikali inachukua maeneo yote ya magereza ambayo yanayonekana kuzidiwa na idadi ya mahabusu.Kwa gereza la Mlele naomba nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa hatua ambazo anazochukua za kufanikisha ujenzi wa gereza la Mlele,"ameseme Lu
gola.

HALOTEL YAREJESHA FAIDA KWA JAMII

$
0
0

KATIKA kuhakikisha inatekeleza agizo la Serikali ya kurejesha faida kwa jamii Kampuni ya Simu ya Halotel imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kiasi cha zaidi ya Sh Milioni 20 kwa ajili ya kuwawezesha vijana wa mkoa huo kujiajiri kupitia sekta ya ujenzi.

Mbali na fedha hizo, Halotel pia imekabidhi vifaa mbalimbali vya hospitali kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa vikiwemo vitanda, neti, mashuka na aproni vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sita katika Hospitali ya Makole iliyopo Dodoma mkoani humo.

Akikabidhi misaada hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilithi Mahenge mbele ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Tanzania Nguyen Van Son alisema pamoja na mambo mengine, misaada hiyo imelenga kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano.

Son alisema katika kuhakikisha inaunga mkono jitihada hizo za Serikali, Kampuni hiyo ya simu ya Halotel imekuwa mstari wa mbele kurudisha faida kwa kile inachokipata kwa kuisaidia jamii mambo mbalimbali kwa lengo la kukabiliana na changamoto zinazowazunguka.

Alisema hatua hiyo imelenga kutoa shukrani kwa wananchi kwa hatua yao ya kuwaunga mkono kwa kutumia huduma za kampuni hiyo iliyosambaa nchi nzima ikitoa huduma mbalimbali na hasa katika maeneo na hasa vijijini.“Tunaamini misaada hii itakwenda kuwa chachu ya maendeleo katika sekta ya afya na ujenzi, hususani kwa kuwawezesha vijana kujiajri katika sekta za ujenzi unaoendana na kukua kwa mji wa Dodoma” alisema Son.

Aidha aliishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi na rafiki yaliyowavutia kuweza kwenye Sekta ya Mawasiliano nchini na kuongeza kuwa dhamira yao ni kuendeleza ushirikiano na kuhakikisha kuwa huduma za mawasiliano zinakuwa za viwango, ubora na gharama nafuu kwa mtumiaji.

Aidha akizungumza wakati wa makabidhiano ya misaada hiyo, mbali na kuipongeza Halotel kwa hatua hiyo, alizitaka kampuni zingine kuiga mfano huo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali linayozitaka kampuni za simu kurejesha sehamu ya faida kwa jamii.

“Nitoe wito kwa kampuni zingine za simu za mkononi ziige mfano wa Halotel wa kurudisha shukrani kwa wananchi” alisema Nditiye na kuwataka wananchi kuthamini mchango wa mawasiliano katika maisha yao ya kila siku kwa uchumi na maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilithi Mahenge, pamoja na kuipongeza Halotel alisema msaada huo umekuja wakati muafaka hususani wakati huu ambao mkoa huo unaendelea na mikakati yake ya kuwasaidia vijana.
“Vijana wa Dodoma mtanufaika na Serikali kuhamia Dodoma, kupitia fedha hizi tumeona tuanzishe kikundi cha vijana ili waweze kuanzisha kiwanda cha kufyatua matofali na mradi huo utakuwa na vijana wa kutoka Jeshi la Kujenga Taifa ili wawasaidie ili baadae vijana waweze kuanzisha na kuendeleza viwanda vyao,” amesema Dkt. Mahenge.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Makole Dkt Geogre Matiko, aliishukuru Halotel kwa msaada huo na kwamba kutokana na mahitaji mbalimbali yaliyopo katika hospitali hiyo ya Makole huku akizitaka taasisi zingine kuiga mfano huo.
Alisema pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuinua sekta ya afya, bado kuna changamoto baadhi ambazo kama wadau watajitokeza na kusaidia kama ambavyo Halotel imefanya, zitaweza kupungua ama kuisha kabisa.


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akikabidhi vifaa mbali mbali vya hospitali vilivyotolewa na kampuni ya Halotel kwa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Makole, Dodoma Dkt. George Matiko ( wa pili kushoto) Mkurugenzi wa kampuni ya Halotel, Nguyen Van Son (wa pili kulia) kwa niaba ya Serikali kutoka kwa kampuni ya Halotel kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizarani Mhandisi Dkt. Maria Sasabo

Mkurugenzi wa kampuni ya Halotel, Nguyen Van Son(wa kwanza kushoto) akikabidhi hundi ya shilingi milioni 20.6 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilithi Mahenge (wa kwanza kulia) kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kufyatua matofali cha kikundi cha vijana wa Dodoma, akishuhudia makabidhiano ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati).  

Sheria ya Ardhi ya Kilimo Itapunguza Migogoro ya Wakulima

$
0
0
Na Bashiri Salum, Dodoma
Sheria ya Ardhi ya Kilimo Itapunguza Migogoro ya Wakulima
Sehemu kubwa ya ardhi inayotumika kwa shughuli za kilimo nchini haitambuliki kama ni ardhi ya kilimo kisheria hivyo kuwa ni chanzo cha migogoro hasa vijijini. 

Akiongea wakati wa kikao kazi cha maandalizi ya sheria ya kuanisha kulinda na kusimamia matumizi ya ardhi ya kilimo kilichofanyika katika ukumbi wa  chuo cha wakulima Bihawana hivi karibuni, Mkurungenzi wa Idara ya Usimamiaji na Mipango ya Ardhi Bwana Paulo Tarimo amesema sehemu ya ardhi inayotumiwa kwa shughuli za kilimo imekuwa ikipangiwa matumizi mengine hivyo kuwa chanzo cha migogoro hapa nchini.

Aidha tafiti za kisayansi zinaonesha kwamba zipo ikolojia mbalimbali za kilimo hapa nchini lakini  ardhi inayofaa kwa kilimo imekuwa ikipangiwa matumizi mbalimbali bila kujali mahitaji ya ardhi ya kilimo kwa matumizi ya sasa na ya baadaye alisistiza Bwana Tarimo.  Hata hivyo amesisitiza kwamba idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kwa kasi lakini ardhi haiongezeki, hivyo jitihada za dhati zinatakiwa kuchukuliwa ili  kuanisha kulinda na kusimamia ardhi hiyo kwa manufaa mapana ya kuimarisha uzalishaji na uwekezaji katika kilimo.

Aidha  amebainisha kwamba Wizara ya Kilimo kupitia Idara ya  Mipango na Matumizi ya Aridhi ya Kilimo  imekutana mara kadhaa kuandaa rasimu ya sheria ya kuainisha, kulinda na kusimamia matumizi ya ardhi ya kilimo ili kupunguza migogoro ya aridhi ambayo imekuwa ikisababishwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa matumizi mengine yasikuwa ya kilimo katika ardhi hiyo. 'migogoro mingi ya ardhi ipo vijijini ambayo inasababishwa na muingiliano wa matumizi ya ardhi ya kilimo na matumizi mengine yasiyokuwa na kilimo hivyo sheria hiyo itasaidia ardhi ya kilimo  kutambuliwa kuwa ni maalum kwa  shughuli za kilimo."

Hata hivyo ameendelea kueleza  kwamba sheria hii itakuwa na manufaa kwa wakulima na wawekezaji kwa sababu italinda  rutuba ya udongo na kuleta uendelevu wa matumizi ya ardhi hiyo kwa kuwa watumiaji watalazimika kuitumia ardhi  kwa misingi ya kanuni za kilimo bora zitakazokuwa zimeainishwa

''Sehemu kubwa ya ardhi inayotumika kwa shughuli za kilimo haitumiki kwa kupewa matunzo ya kutosha ili kuiwezesha kutumika kwa muda mrefu bila ya kuathiri rutuba na ubora wake''. aliendelea kueleza Bwana Tarimo
sheria hii ni muhimu kwa kuwa itasaidia   kuwekwa katika madaraja yatakayoainisha idadi na uwezo wa kimtaji na kiteknolojia wa wakulima wadogo, wa kati na wakubwa. Hii itaongeza tija na ufanisi katika kusimamia na kuratibu uendelezaji wa rasilimali ardhi ya kilimo nchini. 
hata hivyo uaandaaji wa rasimu ya muswada huo ulitokana na  marekebisho ambayo yalitolewa awali na kikao cha baraza la mawaziri kilicho fanyika hivi karibuni
Aidha kikao hicho kilijumuisha wadau mbalimbali ambapo matokeo ya kikao kazi hicho yatajadiliwa katika ngazi mbambali kabla ya kupelekwa katika baraza la mawaziri
Kikosi kazi  kinachoshughulikia rasimu ya muswada wa sheria ya ardhi ya Kilimo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha kazi hiyo iliyokuwa inafanyika katika ukumbi wa chuo cha wakulima Bihawana hivi karibuni.

WAZIRI WA MADINI AFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA TEITI

$
0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko, Januari 29, 2019, alikutana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi asilia (TEITI), Ludovick Utouh, ofisini kwake Jijini Dodoma. Lengo likiwa ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu ya TEITI nchini.
Mkutano ukiendelea
Waziri wa Madini Doto Biteko akiagana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi asilia (TEITI), Ludovick Utouh alipofika ofisini kwake Jijini Dodoma. Lengo likiwa ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu ya TEITI nchini.
Waziri wa Madini Doto Biteko(wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi asilia (TEITI), Ludovick Utouh(wa pili kushoto)  alipofika ofisini kwake Jijini Dodoma. Lengo likiwa ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu ya TEITI nchini. Wa kwanza kushoto ni Naibu waziri wa Madini, Staslaus Nyongo 

WAZIRI KAIRUKI AKUTANA NA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki amekutana na watumishi wa ofisi yake kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Magufuli kushika wadhifa huo mpya. Waziri Kairuki amekutana na watumishi hao mapema hii leo (Januari 30, 2019) katika Ofisi hiyo Jijini Dodoma na kuzungumza nao ikiwa ni sehemu ya kufahamiana na kujua ofisi hiyo.

Mkutano huo uliohudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama pamoja na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde pamoja na Makatibu wakuu wa Ofisi hiyo Bi.Maimuna Tarishi anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu pamoja na Dorothy Mwaluko anayeshughulikia Sera, Uratibu na Uwekezaji.

Kairuki waliwataka watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa umoja na uzalendo ili kujilete maendeleo nchini na kuahidi kushirikiano nao kwa kipindi chote atakachokuwa katika Ofisi hiyo. “Kipekee ninawashukuru viongozi na watumishi wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mapokezi mazuri na  hii ni ishara ya umoja wenu na ninaahidi kushirikiana na watendaji wote katika utekelezaji wa majukumu tuliyonayo  kwa maslahii mapana ya ofisi yetu na Taifa kwa ujumla,”alisisitiza Kairuki

Naye Waziri wa Nchi wa ofisi hiyo Mhe.Jenista Mhagama alipongeza watumishi wa Ofisi yake kwa kuendelea kutekeleza majukumu na kuwataka kuwa na uzalendo na weledi wa hali ya juu. “Ninachoweza kusema tutaendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa kazi za kila siku kwa kuzingatia kuwa hii ni familia moja yenye nia moja ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais ili kujiletea maendeleo katika nchi yetu,”alisema Mhagama.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki wakati alipokutana na watumishi wa Ofisi yake Januari 30, 2019 Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde wakati wa mkutano huo na watumishi wa ofisi yake Januari 30, 2019.
 Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Dorothy Mwaluko.
 Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo alipokutana nao Januari 30, 2019 katika Ofisi hiyo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa ofisi yake walipokutana nao mapema hii leo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na watendaji wa Ofisi yake (hawapo pichani) walipokutana kuzungumza nao Jijini Dodoma, kulia ni Waziri wa Nchi ofisi hiyo, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama na wa kwanza kushoto ni Naibu wake Mhe. Anthony Mavunde.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Mhe.Jenista Mhagama pamoja na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde wakiwa katika ofisi hiyo walipokutana na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu hii leo.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akizungumza jambo wakati wa mkutano wao na Mawaziri wa Nchi wa Ofisi hiyo walipokutana Januari 30, 2019 Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akizungumza jambo na Viongozi wa Ofisi hiyo alipokutana nao ofisini kwake hii leo, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nchi ofisi hiyo anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde.


Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakisubiri kuzungumza na Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki alipokutana nao kujadili masula ya ofisi yao Januari 30, 2019.

MKUU OPERESHENI MAALUM JESHI LA POLISI NCHINI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KIKOSI CHA KUPAMBANA NA UHALIFU MKOA WA MTWARA

$
0
0
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, akizungumza na kikosi Maalum cha kupambana na uhalifu katika viwanja vya Kikosi cha kutuliza Ghasia Mkoa wa Mtwara, baada ya kuwasili katika ziara yake ya kikazi akitokea mkoani Ruvuma. (Picha na Jeshi la Polisi) 
Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, akishiriki mazoezi ya pamoja na kikosi maalum cha kupambana na uhalifu Mkoa wa Mtwara baada ya kuwasili katika ziara yake  mkoani humo.
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas aliesimama katikati, akimsikiliza Mkaguzi wa Polisi INSP, Idd Kimia wa kushoto kwake wakati akiangalia utayali wa kikosi cha kupambana na uhalifu Mkoa wa Mtwara  ambacho hakipo pichani. 
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas katikati na kulia kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara ACP Joseph M.Konyo wakiwa katika picha ya pamoja na kikosi maalum cha kupambana na Uhalifu mkoani humo. (Picha na Jeshi la Polisi).
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images