Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109610 articles
Browse latest View live

Fanyeni kazi kwa kuzingatia Masharti na Maadili ya kazi Zenu-Rais Magufuli.

0
0
Paschal Dotto-MAELEZO 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewataka Majaji, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri wapya walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, kufanya kazi kwa kuzingatia masharti ya kazi zao ili kuweza kutoa haki na kuwatumikia wananchi. 

“Nawapongeza sana Majaji sita mahakama ya Rufani 15 mahakama kuu , Wakuu wa Wilaya wawili na Wakurugenzi wa halmashauri 10 mulioapishwa leo kikubwa kafanyeni kazi kwa kuzingatia masharti ya kazi zenu, kwa Majaji kasimamieni haki ili wananachi waweze kuondokana na dhuluma, lakini kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kasimamieni mapato nchi inahitaji mapato siyo mkaanze mabishano, uongozi ni kufanya kazi kwa ushirikiano kwa hiyo sidhani kama nitapata malalamiko”, Rais Magufuli 

Rais Rais Magufuli aliwasisitiza Majaji sita wa Mahakama ya Rufani na Majaji 15 wa Mahakama kuu kwenda kuchapa kazi kwani Serikali inahitaji wananchi wapate haki inayotakiwa na itakuwa njia bora kwa wananchi kujua haki zao. 

Aidha Rais Magufuli alisema kuwa kuna sehemu hapa Tanzania ambazo imekuwa na dhuluma kubwa akitolea mfano Halmashauri ya Mufindi ambako tukio la ubakaji lilifanyika na mtuhumiwa aliachiwa huru. 

“Unapotazamwa na watu wengi na kupimwa, unapopewa kazi ya kusimamia haki hii ni kazi ngumu sana kwa sababu ina lawama kubwa kwa mfano niliona kwenye Televisheni wamama wakilalamika kwa Waziri Mkuu Mtaafu Mzee Pinda kuwa kuna mtuhumiwa mmoja huko Mufindi Iringa alifanya matukio 11 ya ubakaji lakini akaachiliwa huru, vitu hivi vinawaumiza watanzania kwa bahati nzuri Mhe, Jaji naye aliiona video hiyo mimi nilipoona nilimuagiza mzee pinda amwambie Mkuu wa Mkoa amshike huyu mtuhumiwa”, Alisema Rais Magufuli. 

Katika tukio hilo amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro kulifanyia uchukunguzi tukio hilo lifanyiwe kazi kwa upande wa polisi huku akitoa maagizo kwa Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma kufuatilia mahakama ya Iringa kuona kama ushahidi unaotolewa unatosha . 

Akitoa nasaha kwa wateule hao, Makamu wa Rais Samiah Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa wilaya zote mbili Mwanga na Tarime kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi kama walivyoapa mbele ya Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

“Nawapongeza Wakuu wapya wa Wilaya hizi mbili lakini nawaomba mkazifanyie kazi changamoto zilizoko katika wilaya zenu, kwa mwanga watu wanapigana ngumi nadhani utaenda kuyarekebisha haya, lakini kwa Wilaya ya Tarime kuna vishawishi vingi sana vya rushwa pamoja ya unyayasaji wa kijinsia, Ubakaji na kupigwa kwa wanawake kwa hiyo kayafanyie kazi haya.”, alisema Makamu wa Rais. 

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ametoa kongole kwa Rais Magufuli kwa kuteua majaji sita wa Mahakama ya Rufani na 15 wa Mahakama Kuu kuwa hatua hiyo itaongeza ufanisi katika utoaji haki nchini. 

Aidha katika kuongeza ufanisi wa kushikiliza mashauri mbalimbali hapa nchini Prof. Kabudi alipenyeza suala la kuwepo kwa mahakama zinazotembea MOBILE COURT ili kuweza kuwafikia wananchi kwa urahisi. 

“Mhe. Rais nashukuru kwa kunipa hao 15 wa Mahakama kuu na sita wa Mahakama ya Rufani kwani sasa idadi ya majaji imeongezeka kutoka majaji 66 mpaka majaji 81 kwa Mahakama kuu baada ya hawa uliowapisha leo”, Jaji Mkuu Prof. Juma 

Akielezea mahitaji ya majaji katika mahakama ya Tanzania Prof. Juma alisema bado Majaji wanahitajika ili kukidhi hali ya sasa ya kuwahudumia wananchi, aliongeza kuwa bado kuna umuhimu wa kuongeza Majaji ikiwezekana wawe na idadi ya majaji 100 mpka 150 kwa sababu kwa sasa wananchi wamezidi kuzijua haki zao. 

Jaji Mkuu alisema mahakama inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mahakama za mwanzo 12 ambazo zitazinduliwa hivi karibuni,Miradi 36 ya ujenzi itakayozinduliwa Juni mwaka huu, pamoja na Mahakama 28 za Wilaya nchini. 

UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA

0
0
WAKATI Tamasha la Pasaka likijiandaa kuwasha moto katika Jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka  Alex Msama ametoa mwito kwa wasanii mbalimbali nchini wakiwamo wa muziki wa Injili kuhakikisha wanafuata na kuheshimu Sheria za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Msama amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia msimu mpya wa Tamasha la Pasaka ambalo linatarajia kuanza Aprili 21,2019.Amefafanua tamasha hilo litaanzia Katika Jiji la Dar es Salaam na kauli mbiu ya tamasha hilo inasema Umoja na upendo huduma amani ya nchi yetu.

Kuhusu wasanii kufuata Sheria za BASATA, Msama ametoa mwito kwa wasanii kuiheshimu Baraza hilo na kwamba wasanii ambao watashiriki ni wale ambao wamejisajili na kutambuliwa kisheria.

Kuhusu tamasha hilo amesema BASATA tayari wametoa  maelekezo yenye lengo kuhakikisha tamasha hilo linafanikiwa. "Siku zote usipokuwa na msimamizi huwezi kufanya vizuri, Wasanii wengi wanakuwa na dharau, bila BASATA tamasha hili lingekuwa limekufa siku nyingi", amesema Msama

Katika hatua nyingine, Msama amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo na wasanii kutoka mataifa ya nje, kuhakikisha nao wanapata mualiko ili  washiriki tamasha hilo.

"Wasanii wote ambao watashiriki ni wale wanaoiheshimu BASATA, ni vema wasanii wakahakikisha wanafuata sheria katika kufanya kazi zao za sanaa", amesema Msama .Msama muda si mrefu wataanza kutaja majina ya wasanii ambao watashiri tamasha hilo na kueleza kwa mwaka huu tamasha hilo litafanyika pia katika Jiji la Dodoma.

Wakati huo huo Msama amesema katika kipindi cha tamasha la Pasaka watatumia pia nafasi hiyo kuendelea kumuombea Rais  Dk.John Magufuli, Makamu wa  Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali ya Awamu ya Tano.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya Tamasha la Pasaka jijini Dar es salaam,ambalo linatarajiwa kuanza kurindima Aprili 21,2019.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Alex Msama akitoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha hilo ambalo kwa kawaida hufanyika kila mwaka,mbele ya waandishi wa habari leo, jijini Dar es salaam,kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo Jimmy Charles.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama alipokuwa akizungumza nao leo jijini Dar kuhusu maendeleo ya maandalizi ya tamasha na ujumbe muhimu kwa wasanii/waimbaji watakaoshiriki tamasha hilo.

SHAUKU NA KUOGOFYA: Haya ndio madaraja ya kushangaza zaidi?

0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

INGAWA Ulimwenguni kuna madaraja mengi makubwa na ya kila aina ila kuna madaraja yanatambuliwa kuwa ya kushangaza zaidi. Kwenye Nchi ya Uingereza kuna madaraja kadhaa ya kuogofya ikiwemo daraja la Queen Elizabeth II ambalo linaunganisha pia nchi Scotland na Wales.

Kumekuwa na maoni kwamba baadhi ya madaraja yamekuwa ni ya kuogofya kwa maumbo na miundo yake, Mfano tu, Mamlaka nchini Italia imeagiza ukaguzi wa madaraja yote baada daraja la Morandi kubomoka na kupelekea vifo vya watu 43 mwezi wa nane mwaka jana. 

Mtandao wa ClickMechanic umefanya utafiti na kutoa orodha ya madaraja ya kushangaza, kuogofya na ambayo huwapa ugumu zaidi madereva kuendesha vyombo vya usafiri na madaraja hayo ni pamoja na:

1. Daraja la Eshima Ohashi nchini Japan

Daraja hili lina urefu wa mita 1,700 na limejengwa katika urefu wa kwenda juu (kutoka usawa wa bahari) karibu mita 45 na hivyo kuwezesha meli kubwa kupita chini. Mwinuko wa Daraja hilo ni wa kushangaza na kustaajabisha upatapo nafasi kulitembelea. Daraja la Eshima Ohashi linaunganisha majiji ya Matsue na Sakaiminato huku mwinuko wake wa karibu asilimia 6.1 inafanya ujihisi unapandisha mlima hivi. Pamoja na kuwa na urefu(kwa umbali) wa mita 1,700 na kimo cha urefu kwenda juu karibu mita 45 hakulifanyi kuwa daraja kubwa zaidi ingawa linaruhusu Meli kupita chini yake.


2. Daraja la Storseisundet nchini Norway,

Daraja hili lina muonekano wa kushangaza kutokana na upepo na mawimbi makubwa toka baharini huleta ugumu kwa madereva kuendesha. Unapokuwa upande wa kulia, unaweza kuhisi daraja hilo halijakamilika au muundo wake umeishia karibu tu. Inawezekana ndio daraja ambalo picha zake zimetumika zaidi. Daraja hili linaunganisha peninsula ya Romsdal na kisiwa cha Averøya kilichopo kwenye Bahari ndogo ya Norway. Muundo wake wa nusu duara wenye umbali wa mita 260 za urefu huweza kukufanya ufikiri daraja halijakamilika katika upande wake wa pili.

3. Daraja la Millau Creissels nchini Ufaransa

Hili ni daraja refu kwenda juu zaidi ulimwenguni kwa kimo cha mita zipatazo 343. Wakati mwingine madereva na vyombo vya usafiri hujikuta wakipita kwenye mawingu wanapokatiza kwenye daraja hilo kutokana na urefu wake. Lilichora na mbunifu kutoka Uingereza Lord Norman Foster na mchoro kufanyiwa kazi na Mhandisi mfaransa Michel Virlogeux. Mwaka 2006 Daraja hilo lilishinda Tuzo ya Muundo bora duniani kutoka kwenye Chama cha Kimataifa cha Madaraja na Wahandisi Miundo kuonesha jinsi gani limeshinda yote kwa Ubunifu uliotumika.


4. Daraja la Hong Kong–Zhuhai–Macau nchini China.

Ni daraja refu zaidi ulimwenguni linalokatiza Baharini, kwa kuwa na umbali unaofikia maili 34 huku likiunganisha majiji matatu liyopo kwenye Mto Pearl Delta. Daraja hili limekamilika mwaka jana na kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Daraja la Jiaozhou lenye urefu wa maili 26 pia la nchini China.

Daraja la Hong Kong–Zhuhai–Macau ni muunganiko wa madaraja matatu, njia ya chini ya bahari na likiunganisha visiwa vinne ambavyo ni vya kujengwa. Ujenzi wake umetumia nadharia na muundo kama wa daraja la Chesapeake kwenye ufukwe wa Virginia. Kuna Vibali 10,000 vya magari vimetolewa kupita katika daraja hili kutoka Hong Kong kwenda Zhuhai. Haitoshi, magari yanayoingia jiji la Hong Kong na Macau kutoka sehemu nyingine hupaswi kulipia vibali vya kila siku.


5. Daraja la Nanpu nchini China.

Daraja lenye viunga na mipishano kama chakula cha tambi ni maarufu duniani kote. Daraja la Nanpu lipo Shanghai linadhihirisha mchanyato wa ubunifu na uhandisi uliotamalaki. Mzunguko na kunesa kwa daraja huweza kumfanya dereva kupata kizunguzungu wakati wa kupita katika daraja hili. Nanpu limejengwa kwa namna ya kupunguza matumizi makubwa ya ardhi hivyo basi ni daraja mzunguko wa kuvutia na kustaajabisha.

YANGA DHIDI YA BIASHARA KOMBE LA ASFC KUPIGWA IJUMAA HII

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mchezo wa Hatua ya 32 bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup -ASFC) kati ya Yanga na Biashara United kupigwa Ijumaa wiki hii.

Mechi hiyo ya kuingia hatua ya 16 bora utazikutanisha timu hizo katik dimba la Uwanja wa Taifa.

Kuelekea mchezo huo, makocha wamejizatiti kuhakikisha hawapotezi huku Kocha Mkuu wa Timu ya Biashara United, Amri Said amesema Yanga akiwaonya Yanga kuwa mechi hiyo haitakuwa nyepesi kwao.

Said amesema kuwa kikosi chake kimejipanga kuondoka na matokeo Uwanja wa Taifa kwani anaamini wana uwezo mzuri wa kupata matokeo mbele ya Yanga.

Said amesema hana mashaka na uwezo wa wachezaji wake kutokana na maandalizi ambayo anayafanya kikubwa anachofikiria ni kupata ushindi kwenye mchezo wake na anamini dakika 90 zitaamua.

"Yanga kuondoka na ushindi kwenye mechi hiyo wasifikiri ni kazi, mechi hii ni zaidi ya fainali ukiangalia zaidi ni mtoano hivyo ni lazima wachezaji waonyeshe upambanaji kwenye mchezo wetu,” amesema Said.

Said amesema, anafahamu Yanga ina timu nzuri na ni kubwa na anawafahamu na kuwaheshimu wapinzani wao ila haliwapi shaka kwani mpira unachezwa Uwanjani.

Biashara United imeweka kambi katika moja ya viunga vya Jiji la Dar es Salaam wakisubiri mtanange hao baada ya kumaliza kucheza na Azam kwenye mechi ya Ligi uliomalizika kwa wao kupoteza kwa matokeo ya 2-1.

CLIFFORD NDIMBO ATEULIWA NA CAF

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Shirikisho la  Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Cliford Ndimbo kuwa Ofisa wa habari wa CAF.

Ndimbo  ameteuliwa CAF kuwa OfisA Habari wa CAF katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika utakaopigwa Afrika Kusini.

Ndimbo atakuwa Ofisa  kwenye mchezo namba 99 kati ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Mchezo huo utachezwa Ijumaa, Februari 1, nchini Afrika Kusini Uwanja wa Tshwane-Loftus Versfeld ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ndimbo anaungana na vigogo wengine kutoka katika Shirikisho la mpira wa miguu Nchini (TFF) kupata nafasi ya kusimamia michezo kadhaa ya Kimataifa.

WASENEGAL KUAMUA NANI MBABE AL AHLY VS SIMBA JUMAMOSI HII

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Waamuzi kutoka nchini Senegal wanatarajiwa kuamua mchezo wa Kundi D wa Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Al Ahly dhidi ya Misri  dhidi Simba ya Tanzani.

Mchezo huo wa tatu wa Kundi D utachezwa Jumamosi ya  wiki hii kwenye Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewataja waamuzi hao kuwa Utachezwa na mwamuzi Maguette Ndiaye atakayekuwa wa mwamuzi wa kati akisaidiwa na washika vibendera Djibril Camara na El Hadji Malick Samba wakati mezani atakuwepo  Daouda Gueye.  

Simba wamesafiri leo kuelekea Nchini Misri kwenda kujiandaa na mchezo huo wakiwa ugenini na wakisafiri na wachezaji 20 sambamba na benchi la Ufundi na viongozi wengine.

Kwenye mchezo huo Simba wataendelea kuwakosa wachezaji wake nyota Nahodha John Bocco ambaye anauguza majeraha baada ya kuumia kwenye mchezo wao dhidi ya JS Saoura, Erasto Nyoni aliyeumia kwenye kombe la Mapinduzi sambamba na Shomari Kapombe aliyeumia akiwa na timu ya Taifa.

Katika michezo miwili iliyopita Simba walifanikiwa kuondoka na alama 3 wakiwa nyumbani dhidi ya JS Saoura baada ya kuwafunga goli 3-0 na kupoteza mchezo wa pili kwa goli 5-0 dhidi ya As Vita kutoka DR Congo.

Smba anashinda nafasi ya tatu katika Kundi D akiwa alama sawa na As Vita wakitofautiana magoli ya kufunga na Kufungwa na nafasi ya kwanza ikiongozwa na Al Ahly wenye alama nne wakishinda mechi moja na kutoa sare na JS Saoura akishika nafasi ya nne akiwa na alama moja

Mechi hizo zinatarajiwa kuwa zimempa nafasi kocha Patrick Aussems kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mechi dhidi ya AS Vita kuelekea mechi ya Jumamosi na Al Ahly.

RAIS DKT.MAGUFULI AWAAPISHA MAJAJI 6 WA MAHAKAMA YA RUFANI NA MAJAJI 15 WA MAHAKAMA KUU TANZANIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Winnie Korosso Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es Salaam. Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Sahel Barke Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es Salaam. Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Lugano Samson Mwandambo Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es Salaam Januari 29, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Dkt. Mary Levira Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Ignus Paul Kitusi Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Rehema Kerefu Sameji Kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. John Rugalema Kahyoza Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bi. Susan Bernard Mkapa Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Fahamu Hamidu Mtulya Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Cyprian Phocas Mkeha Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Willbard Richard Mashauri Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Dunstan Beda Ndunguru Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Seif Mwinshehe Kulita Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bi. Upendo Elly Madeha Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam Januari 29, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Yohane Bokobora Masara Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Mustapha Kambona Ismail Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Athumani Matuma Kirati Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Zepherine Nyalugenda Galeba Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bw. Dkt. Ntemi Nimilwa Kilikamajenga Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Bi. Dkt. Juliana Laurent MasaboKuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapish Dkt. Lilian Mihayo Mongella Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kuu . Hafla iliyofanyika Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu Wakiapa kiapo cha uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwaapisha  Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Wakuu wa Wilaya  wapya 2 wa Wilaya ya Mwanga  na Tarime pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri 10 Wakiapa kiapo cha uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwaapisha Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani na  Majaji 15 Mahakama Kuu Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,201
Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu Wakitia saini hati za  kiapo cha uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwaapisha  Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha  Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani na Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu ,Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa TAMISEMI Seleman JaffO, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani  mara baada ya kuwaapisha Majaji hao na Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu ,Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa TAMISEMI Seleman JaffO, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu,Watumishi mbalimbali wa Mahakama mara baada ya kuwaapisha Majaji hao. Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa TAMISEMI Seleman JaffO, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu na Viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya Dini  mara baada ya kuwaapisha Majaji hao. Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa TAMISEMI Seleman JaffO, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani Majaji wapya 15 wa Mahakama Kuu, Wakuu wa Wilaya 2 na Wakurugenzi 10 wa Halmashauri, Mara baada ya kuwaapisha Majaji. Ikulu Jijini  Dar es salaam. Januari 29,2019.
Wakuu wa Wilaya  wapya 2 wa Wilaya ya Mwanga  na Tarime pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri 10 wakiwa katika hafla ya uwaapisho wa Majaji 6 wa Mahakama ya Rufani na Majaji 15 wa Mahakama Kuu .Ikulu Jijini  Dar es Salaam Januari 29,2019.
PICHA NA IKULU

OFISA TRA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA YA SHILINGI MILIONI 10

0
0
Na Karama Kenyunko globu ya Jamii

OFISA Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kituo cha Gerezani Kariakoo, Dar es Salaam, Charles Kapongo  amefikishwa katika Mahakama ya Wilayaya Ilala akikabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya Sh. milioni 10.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali kutoka Takukuru, Dumas Muganyizi amedai  mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule kuwa,  Januari 25, mwaka huu katika maeneo ya ofisi za TRA zilizopo Gerezani Kariakoo ndani ya Wilaya ya Ilala,  mshtakiwa alitenda kosa. 

Imedaiwa siku hiyo mshtakiwa Kapongo akiwa mwajiriwa na TRA, alipokea rushwa ya USD ,4200 Ambazo ni Sawa na Sh.  milioni 10, kutika kwa Naibu Magala ambaye ni mwajiriwa wa kampuni ya Ushauri  ya Hakha Business Accounting.

Wakili Flora Anaendeleaje kudai kuwa,  fedha hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kushawishi kupunguza makadirio ya kodi ya kampuni hiyo,  kutoka Sh 45,571,664 kwenda Sh.  milioni nane kitendo ambacho ni kinyume na maadili yake ya kazi.

Hata hivyo,  mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kufanikiwa kukamilisha masharti yaliyowekwa Na Mahakama ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini kati yao mmoja atoke kwenye taasisi yoyote inayotambulika Na wote wametakiwa kusaini bondi ya Sh.  Milioni tano.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa Februari 11.2019
 FISA Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kituo cha Gerezani Kariakoo, Dar es Salaam, Charles Kapongo akifishwa katika Mahakama ya Wilayaya Ilala akikabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya Sh. milioni 10.


RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA KILIMO MALIASILI MIFUGO NA UVUVI ZANZIBAR

0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar, kuhusiana na maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara hiyo,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kulia Mshauri wa Rais Masuala ya Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Abdulrahman Mwinyijumbe, mkutano huo umefanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 /RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasi, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, kuhusiana na Maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara hiyo,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Kilimo Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma, wakiwa katika ukumbi wa mikutano Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Kilimo, Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar. Mhe. Rashid Ali Juma, akiwasilisha ripoti ya Maendeleo ya Miradi mbalimbali ya Wizara yake ,wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hayuko pichani na kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu)
 VIONGOZI wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar, wakifuatilia taarifa ya maendeleo ya Miradi ya Wizara hiyo, wakati ikiwasilishwa na Waziri wa Kilimo Maliasi, Mifugo na Uvuvi.Mhe. Rashid Ali Juma, wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Bi. Maryam Juma Sadalla, akichangia wakati wa mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein,kuzungumzia maendeleo ya Miradi ya Wizara hiyo, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, katika ukumbi wa mikutano Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

0
0
Spika wa Bunge Job Ndugai  (kulia) akimwapisha Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea , Bungeni jijini Dodoma, Januari 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana  na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho  ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018, Bungeni jijini Dodoma, Januari 29 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kiembe Samaki, Ibrahim Raza kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Januari 29, 2019.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi kutoka jimbo la Kilwa Kusini waliotembelea Bunge kwa mwaliko wa Mbunge wao  Selemani Bungara, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Januari 29, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Januari 29, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Januari 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS MAGUFULI AKEMEA TABIA YA MA-DC KUTUMIA VIBAYA SHERIA NA MAMLAKA WALIYONAYO YA KUWEKA WATU NDANI

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ametoa onyo kwa  Wakuu  Wilaya nchini  kuacha  kutumia vibaya sheria na mamlaka waliyopewa ya kuweka watu ndani.

Ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za  kuwaapisha majaji 15 wa Mahakama Kuu na Majaji sita wa Mahakama ya Rufaa ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza umuhimu kwa wakuu wa wilaya nchini kutotumia sheria na mamlaka ya kuweka mtu ndani kwani sio haki pale unapomuweka mtu ndani bila kumfikisha mahakamani.

Rais Magufuli ameeleza hivi"Wakuu wa Wilaya msitumie vibaya sheria na mamlaka ya kumuweka mtu ndani.Unamuweka mtu ndani halafu unamtoa kwa madai amejifunza bila kumpeleka mahakamani,hii sio fair kabisa.

"Viongozi wengi wamezungumzia hii tabia na mimi naomba niirudie wakuu wa wilaya acheni kuweka watu ndani.Hivi na Mkuu wa Mkoa naye akiamua kuweka mtu ndani itakuaje,si itakuwa vurugu,"amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa kwanza saa nyingine kumuweka mtu ndani huenda isilete tija kwani sio kila jambo unataka kumuweka mtu ndani,mengine unatakiwa kutoa maelelezo tu na ikawa na matokeo mazuri zaidi.

Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kuelezea sababu za kumuondoa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro Aaron Mbogho ambaye amemuhamishia Kitengo cha Wadudu kwani yeye(Mbogho) ni mtalaam wa wadudu.

"Akiwa wilayani Mwanga yaliyokuwa yanatokea wote tumesikia,viongozi wamewekwa ndani na unapofuatilia unaona chanzo ni yeye.Katika mazungumzo yake amekuwa akisema kuwa yeye ndio mtalaam wa wadudu peke yake nchini Tanzania.

" Hivyo huenda na watu nao anawaona kama wadudu,hivyo nimeona kwa kuwa ni mtalaam katika eneo hili basi acha aende huko akachunguze vizuri wadudu,"amesema Rais Magufuli .

Kampuni ya Utalii ya Wengert Windrose Safari yatoa mamilioni kwa vijiji 12 Longido

0
0
Mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe akiwa na baadhi ya viongozi wa vijiji na wafanyakazi wa kampuni ya Wingert Windrose Safaris baada ya kukabidhiwa hundi.

Na Ripota Wetu,Arusha.

Arusha.Kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Wengert Windrose Safaris imetoa kiasi cha sh 36 milioni kwa Vijiji 12 vinavyozunguka kitalu cha uwindaji cha Lake Natron North wilayani Longido ili kuchangia huduma na miradi ya maendeleo.

Meneja mahusiano ya kampuni hiyo, Clarence Msafiri alimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Longido,Frank Mwaisumbe mfano wa hundi kwa niaba ya vijiji hivyo kisha kukabidhi hundi halisi yenye thamani ya Sh 3 milioni kwa kila kijiji.

Vijiji vilivyonufaika na fedha hizo ni Mairowa,Magadini,Gelai,Wosiwosi,Ngoswaki na Matale A, Origrai,Matele B,Lumbwa ,Ilnjakitsapukin ,Kimwati na Alaililai ambapo pia kampuni hiyo imetoa fedha nyingine kiasi cha dola 5000 zaidi ya sh 11 milioni kuchangia huduma za jamii kupitia ada ya kitalu chake cha uwindaji.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya, Mwaisumbe aliwataka viongozi wa vijiji kusimamia vizuri matumizi ya fedha hizo hasa katika kipindi hiki ambacho ujenzi wa madarasa unaendelea kwa kasi ili kutoa nafasi kwa watoto wa jamii hiyo ya wafugaji kupata fursa ya elimu.

Mwaisumbe alisema anaishukuru sana, Kampuni ya Wengert kwa kuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika wilaya hiyo, kutokana na kujitoa kuchangia shughuli nyingi za maendeleo katika wilaya hiyo.“Naishukuru kampuni hii kwa kuonesha uzalendo na kuheshimu makubaliano kusaidia vijiji na naamini mtaendelea kushirikiana katika kuhakikisha Longido tunakua na uhifadhi endelevu unaozingatia ustawi wa jamii inazunguka maliasili zetu,”alisema Mwaisumbe

Meneja Mahusiano wa kampuni ya Wenget Windrose Safaris Limited,Clarence Msafiri alisema wataendelea kushirikiana na vijiji vinavyowazunguka kuchangia huduma za jamii.Msafiri alisema licha ya fedha hizo, kampuni hiyo pia itaendelea kutoa ajira kwa vijana wa jamii inayowazunguka lakini pia tayari wametoa kiasi cha dola 5000 sawa ni Sh 11.5 milioni ambayo ni malipo kwaajili ya kila kitalu kila mwaka.

Msafiri alitaja vijiji vilivyonufaika kuwa ni Mairowa,Magadini,Gelai,Wosiwosi,Ngoswaki na Matale A,vijiji vingine ni Origra,Matele B,Lumbwa ,Ilnjakitsapukin ,Kimwati na Alaililai.Akizungumza kwa niaba ya vijiji hivyo, Diwani wa Kata ya Mundarara ,Alais Mushao alisema mchango wa uhifadhi ni muhimu katika kuinua na kuchangia shughuli za maendeleo na kuitaka kampuni hiyo kufanya kazi zake kwa kutunza mazingira ili rasilimali hizo zinufaishe vizazi vijavyo.

Kampuni ya Wingert Windrose Safaris ni kati ya kampuni zinazomilikiwa na taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) ambayo pia inamiliki kampuni ya Mwiba Holdings iliyowekeza hifadhi ya Makao na Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) ambayo imewekeza maeneo kadhaa nchini.

Angalia Coppa Italia kupitia StarTimes, Napoli mikononi mwa AC Milan, Juve kwa Atalanta

0
0
Robo fainali ya Coppa Italia msimu huu imekaa kama shindano la 8 bora ya Serie A ambapo Fiorentina timu pekee nje ya nane bora katika msimamo wa ligi ya Serie A msimu huu.

Shughuli inaanzia jijini Milan ambapo wenyeji AC Milan watawakaribisha Napoli katika dimba la San Siro saa 4:45 Usiku. Napoli inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya Serie A nyuma ya Juventus ambao wamezidi wamezidi kuimarika siku za hivi karibuni. Licha ya Napoli kuwa na kikoso kizuri bado hawajaweza kushindana na Juventus, na Kombe la Coppa Italia ndio nafasi yao wazi zaidi kushinda taji mwaka huu japo haitakuwa rahisi.

AC Milan wao wana muda mrefu zaidi wakiwa hawajashinda Kombe japo walishinda taji la Super Coppa Italiana mwaka 2016 huku wakiwa hawajashinda ligi wa Kombe la Shirikisho. Wenzao Inter Milan watakuwa nyumbani pia dhidi ya Lazio siku ya Alhamisi saa 5:00 Usiku.Kesho Jumatano, Fiorentina watakuwa nyumbani dhidi ya Roma na mechi itachezwa saa 2:15 Usiku kwa saa za Afrika mashariki.

Cristiano Ronaldo aliwapatia Juventus ushindi katika Supercoppa dhidi ya Milan wiki mbili zilizopita na Dybala kumwagia sifa kibao baada ya mechi. “Tunafahamu umuhimu wa Cristiano Ronaldo na ukubwa wa mchango wake kila siku. Mara zote nimekuwa nikisema yeye na Messi wako kwenye kiwango sawa. Mimi nina bahati ya kucheza nao wote”

Juventus watakuwa ugenini dhidi ya Atalanta siku ya Jumatano saa 4:45 Usiku na michezo yote hii itakuwa MUBASHARA kupitia ST World Football pekee.

WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO MAZITO KWA MAAFISA USTAWI WA JAMII

0
0
*Awataka wajiepushe na rushwa wafanye kazi kwa bidii, weledi na uadilifu
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa  amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa watekeleze majukumu yao kwa bidii, weledi, uadilifu na wasijihusishe na vitendo vya rushwa.

Amesema maafisa hao wanatakiwa watumie mbinu shirikishi ambazo zinahusisha jamii yenyewe na wataalamu ambao ni watoa huduma ngazi ya jamii (Community Case Worker) ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumanne, Januari 29, 2019) kwenye Mkutano wa Mwaka wa Kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, jijini Dodoma.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka maafisa hao wahakikishe kwamba haki za msingi za makundi hayo zinapatikana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo katika kutoa huduma ya taaluma yao.

Amesema taaluma ya Ustawi wa Jamii imepewa dhamana ya kuwa mlinzi wa mtoto, kumhudumia na kusimamia haki zake, hivyo amewatakawazuie na watokomeze aina zote za ukatili kwa watoto, wazee na wenye ulemavu.

Waziri Mkuu amesema jukumu hilo pia linahusisha watoto waliopo kwenye mazingira hatarishi na wanaoishi na kufanya kazi mitaani, wazee, wanawake wasio na uwezo na watu wenye ulemavu.

Amesema pamoja na mafanikio makubwa ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imeyapata ni muhimu wakaendelea kuongeza nguvu na weledi ili kutorudi nyuma katika kujenga msingi wa kuimarisha ustawi wa makundi maalumu.

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza maafisa hao wakasimamie utekelezaji wa mkakati wa  Mkono kwa Mkono, Familia kwa Familia, Kaya kwa Kaya kupitia huduma ya kuzuia ukatili ngazi ya familia wenye lengo la kuzuia ukatili ndani ya familia ili ulete matokeo tarajiwa.

“Tambueni umuhimu wenu na kwamba jamii inawategemea kutekeleza majukumu yenu kikamilifu ili kupunguza matatizo ya kijamii kwa wale wenye uhitaji wakiwemo watoto, watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye migogoro na akina mama wanaonyanyaswa na makundi mengine.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewashukuru wadau wa maendeleo kwa namna wanavyoshirikiana na Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo likiwemo suala la uimarishaji wa huduma za ustawi wa jamii nchini.

Amesema anatambua mchango mkubwa kutoka kwa shirika la UNICEF, USAID, UN WOMEN, UNFPA, John Snow Inc, Pact, HelpAge International, World Vision, Save the Children, Plan International na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine wameendelea kushirikiana na Serikali kuinua kiwango cha utoaji huduma za ustawi wa jamii nchini.

“Ninapenda kuwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Magufuli, ipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi ili tuweze kufikia malengo ya maendeleo endelevu ifikapo 2030.”

Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Uadilifu, Weledi na Uwajibikaji katika Utoaji wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ni Nguzo katika kuelekea Uchumi wa Kati wa Viwanda.”

Waziri Mkuu amepongeza kwa kuanzisha utamaduni huo wa kukutana Watendaji wa Sekta ya Ustawi wa Jamii kwa kuwa hiko ni kiashiria kwamba kuna mabadiliko katika utendaji kwa kuzingatia kuwa mkutano huu haujawahi kufanyika toka mwaka 2006.

Mkutano huo wa siku tatu unajumuisha Maafisa Ustawi wa Jamii 164 kutoka mikoa yote Tanzania Bara, wadau wa maendeleo, wawakilishi wa wazee, watoto waishio katika mazingira hatarishi waliohitimu mafunzo ya VETA pamoja na watoto waliokuwa wakiishi mitaani ambao kwa sasa wameunda kikundi cha burudani. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Mwaka  wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Januari 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza mtoto, Hussein Jailal (kushoto) wakati alipotoa ushuhuda kwa niaba ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara, uliofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Januari 29, 2019.


Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Januari 29, 2019.
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipoingia kwenye ukumbi wa  Mikutano wa Jakaya Kikwete jijiniDodoma kufungua mkutano huo, Januari 29, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti cha kuzaliwa mtoto, Faisal Rashidi Haroun kabla ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara, Kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Januari 29, 2019. Kushoto ni Mama Mzazi wa mtoto huyo, Habiba Mohammed.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Fundi Mkuu wa Karakana ya Vifaa Visaidizi vya Wenye Ulemavu iliyopo eneo la Sabasaba jijini Dodoma, Bw. Mwita Marwa Maki baada ya kuvutiwa na baiskeli za magurudumu matatu zilifungwa mota ambazo zimebuniwa na zinatengenezwa na karakana hiyo. Tukio hilo lilifanyika kwenye viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, kabla ya Waziri Mkuu kufungua Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara, Januari 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CHUO CHA BANDARI KUDAHILI WANAFUNZI KIDIJITALI

0
0
Chuo cha Bandari kitaanza kudahili wanafunzi wapya kupitia mfumo wake mpya wa kidijitali ujulikanao kama Student’s Information Management System (SIMS). Mfumo huo wa kidijitali uliozinduliwa jana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe utawezesha chuo hicho kuwadahili wanafunzi kidijitali.

Mbali na hayo, mfumo huo ambao ulibuniwa na kutengenezwa na wafanyakazi wa TPA kitengo cha TEHAMA, pia utatumika kukokotoa matokeo ya mitihani na kuanda taarifa ya mwisho wa mwaka wa mafunzo yaani ‘final year transcript’. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tovuti ya mfumo huo mpya, Waziri Kamwelwe alisema uwepo wa mfumo huo utasaidia kudhibiti udanganyifu uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wasiokuwa waaminifu.

Mhandisi Kamwelwe ameongeza kwamba awali wakati udahili ulipokuwa ukifanywa kwa kujaza fomu kwa mkono ‘manual’, kulikuwa na tatizo la uchakachuaji wa vyeti na upotevu wa pesa.  “Wakati wa application manual (kujisajili kupitia mikono) kuna fomu za maombi zilikuwa zinapotea na kulikuwa na upotevu wa pesa pamoja na tatizo la kuchapisha vyeti feki na baadhi ya wanafunzi kutohudhuria mafunzo ipasavyo,” amesema.

Mhandisi ameongeza kwamba kipindi hicho kuna baadhi ya wanafunzi waliishia kusajiliwa tu na baada ya miaka miwili unamkuta mtaani na cheti lakini kwa uwepo wa mfumo, hayo mambo hakuna tena. Kwa upande wake Mkuu wa Bodi ya Magavana ya Chuo hicho, Mhandisi Deusdedit Kakoko alimshukuru Waziri kwa kutenga muda na kuja kuwazindulia tovuti hiyo ambayo ni muhimu mno kwa chuo hicho. 

Mhandisi Kakoko ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA amesema kwamba waziri ana mambo mengi lakini kutokana na umuhimu wa jambo hilo, ameamua kuja kuzindua mfumo huo ambao ni muhimu kwa wanafunzi na chuo kwa ujumla. “Uwepo wa mfumo huu, utarahisisha utendaji kazi wetu kama chuo na kudhibiti wale wote waliokuwa wakitumia mianya ya kutokuwepo kwa mifumo hiyo, kufanya udanganyifu,” amesema.

Akizungumzia faida za mfumo huo, mmoja wa wafanyakazi wa TPA ambaye ameshiriki kubuni mfumo huo, Rainer Mwashu alisema utarahisisha zoezi la udahili wanafunzi na kupata taarifa zao kwa urahisi wakati wowote zikihitajika. “Kupitia mfumo huu, mwanafunzi ataweza kujisajili kwa ajili ya mwaka wa masomo popote pale alipo…amesema na kuongeza kwamba,…kwasasa taarifa zote za wanafunzi wa chuo hiki zitapatikana kidijitali kupitia mfumo huu.” Mbali ya hayo, pia mfumo huo utatumika kuzalisha taarifa ya mwisho ya matokeo ‘final year transcript’, na utawezesha kuoana kwa mifumo ya ndani na nje ya taasisi kama vile NACTE, NECTA na GePG.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa tovuti hiyo. Wengine picha ni Mkuu wa Chuo kushoto, Dkt. Joseph Kakeneno, pembeni ya Waziri ni Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo Cha Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko na Mjumbe wa bodi hiyo, Dkt. Eliamini Kasembe.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe katikati mara baada ya kukata riboti kuashiria uzinduzi wa tovuti hiyo. Wengine pichani ni Mkuu wa Chuo cha Bandari, Dkt. Joseph Kakeneno, kushoto, Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo Cha Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko, wa pili kulia na Mjumbe wa bodi hiyo, Dkt. Eliamini Kasembe 
  

MAKONDA AWAAGIZA WAKUU WA WILAYA KUHAKIKISHA UGAWAJI WA VITAMBULISHO VILIVYOTOLEWA NA RAIS MAGUFULI UNAMALIZIKA KABLA YA MWEZI MACHI

0
0
* Atoa tahadhari katika kipindi hiki cha mvua
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaagiza wakuu wa Wilaya zote 5 kuhakikisha hadi kufikia Mosi, Machi mwaka huu kila mfanyabiashara ndogondogo anakuwa na Kitambulisho cha utambuzi kilichotolewa na Rais Dkt. John Magufuli na kuwataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo ambayo haina malipo.

 Makonda amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya kata na kueleza kuwa baada ya Tarehe 01/03/2019 mfanyabiashara yeyote atakayekutwa bila kitambulisho, leseni ya manispaa au vielelezo vya kulipa kodi toka TRA atajikuta mikononi mwa vyombo vya dola kama muhujumu Uchumi.

Sambamba na hayo Makonda  amegawa vitambulisho vya wafanyabiashara ndogondogo kwa Wakuu wa Wilaya na kufanya mkoa huo kuwa kinara kwa kupokea takribani vitambulisho 175,0000 kutoka kwa Rais Magufuli.

Aidha  Makonda amesema baada ya 01/03/2019 serikali ya Mkoa itawaingiza wafanyabiashara hao katika mfumo wa kisasa (Database) utakaowezesha serikali kuwafikia na kuwapa mafunzo ya namna kukuza biashara zao ili waweze kufikia uchumi wa Kati.

Pamoja na hayo amewatahadharisha watendaji wanaowatoza kiasi kikubwa cha fedha za vitambulisho tofauti na bei elekezi ya sh. 20,000 huku akiwahimiza wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo waliyopewa na Rais.

Mbali na Vitambulisho  Makonda ametoa miezi miwili kwa Wakurugenzi wa Manispaa kuhakikisha Leseni za wafanyabiashara zinaingizwa katika mfumo mmoja ikiwa ni pamoja na kuharakisha utoaji wa leseni ili kupunguza usumbufu kwa wananchi.

Vilevile ametoa tahadhari kwa wakazi wa Dar es Salaam kuchukua hatua katika kipindi hiki cha mvua kwa kuhakikisha wanafuatilia matangazo yanayotolewa na mamlaka ya hali ya hewa pamoja na kutojenga mabondeni pamoja na kuhama maeneo hatarishi ili kubaki salama.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (kulia) akimkabidhi kasha la vitambulisho  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kushoto) leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam Abubakar Kunenge.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na watendaji wa Mkoa katika kikao kilichowakutanisha na kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo jijini hapo.
 Watendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia mkutano uliowakutanisha na Mkuu wa Mkoa na kujadili changamoto na namna ya kuzitatua, leo jijini Dar es Salaam.

CLIFFORD NDIMBO ATEULIWA NA CAF

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Shirikisho la  Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Cliford Ndimbo kuwa Ofisa wa habari wa CAF. Ndimbo  ameteuliwa CAF kuwa OfisA Habari wa CAF katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika utakaopigwa Afrika Kusini.

Ndimbo atakuwa Ofisa  kwenye mchezo namba 99 kati ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Asec Mimosas ya Ivory Coast. Mchezo huo utachezwa Ijumaa, Februari 1, nchini Afrika Kusini Uwanja wa Tshwane-Loftus Versfeld ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ndimbo anaungana na vigogo wengine kutoka katika Shirikisho la mpira wa miguu Nchini (TFF) kupata nafasi ya kusimamia michezo kadhaa ya Kimataifa.

YANGA DHIDI YA BIASHARA KOMBE LA ASFC KUPIGWA ALHAMISI WIKI HII

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mchezo wa Hatua ya 32 bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup -ASFC) kati ya Yanga na Biashara United kupigwa Alhamisi wiki hii. Mechi hiyo ya kuingia hatua ya 16 bora utazikutanisha timu hizo katik dimba la Uwanja wa Taifa.

Kuelekea mchezo huo, makocha wamejizatiti kuhakikisha hawapotezi huku Kocha Mkuu wa Timu ya Biashara United, Amri Said amesema Yanga akiwaonya Yanga kuwa mechi hiyo haitakuwa nyepesi kwao. Said amesema kuwa kikosi chake kimejipanga kuondoka na matokeo Uwanja wa Taifa kwani anaamini wana uwezo mzuri wa kupata matokeo mbele ya Yanga.

Said amesema hana mashaka na uwezo wa wachezaji wake kutokana na maandalizi ambayo anayafanya kikubwa anachofikiria ni kupata ushindi kwenye mchezo wake na anamini dakika 90 zitaamua. "Yanga kuondoka na ushindi kwenye mechi hiyo wasifikiri ni kazi, mechi hii ni zaidi ya fainali ukiangalia zaidi ni mtoano hivyo ni lazima wachezaji waonyeshe upambanaji kwenye mchezo wetu,” amesema Said.

Said amesema, anafahamu Yanga ina timu nzuri na ni kubwa na anawafahamu na kuwaheshimu wapinzani wao ila haliwapi shaka kwani mpira unachezwa Uwanjani. Biashara United imeweka kambi katika moja ya viunga vya Jiji la Dar es Salaam wakisubiri mtanange hao baada ya kumaliza kucheza na Azam kwenye mechi ya Ligi uliomalizika kwa wao kupoteza kwa matokeo ya 2-1

NAIBU WAZIRI MABULA ASHANGAZWA NA H/JIJI LA DODOMA KUSHINDWA KUDAI BILIONI SITA ZA WADAIWA KODI YA ARDHI

0
0
Na Munir Shemweta,  DODOMA 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula ameshangazwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kujikita zaidi katika kuuza viwanja huku ikiacha kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wadaiwa wa kodi ya ardhi kinachofikia bilioni sita. 

Awali Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi  alisema jiji lake limeongoza katika kukusanya mapato ambapo lilifanikiwa kukusanya bilioni saba na kati ya hizo bilioni nne nukta nane zinatokana na kodi ya ardhi. 

Akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya jiji la Dodoma katika mfulukizo wa ziara zake za kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi  leo tarehe 28 januari 2018 Dkt Mabula alisema pamoja na jiji kukusanya fedha nyingi katika idara ya ardhi kupitia uuzaji viwanja lakini  linapaswa kuhakikisha madeni ya wadaiwa sugu yanakusanywa ili kuepuka ulimbikizaji madeni. 

Naibu Waziri wa Ardhi alisema pamoja na jiji hilo kufanya vizuri lakini yeye anachelewa kulipa pongezi kutokana na kushindwa kukusanya kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wadaiwa wa kodi ya ardhi sambamba na kushindwa kutoa ilani za madai kwa wadaiwa hao jambo linaloikosesha serikali mapato mengi. 

Kufuatia hali hiyo Dkt Mabula ameipa halmashauri hiyo ya jiji la Dodoma wiki mbili kuhakikisha inampatiwa orodha ya wadaiwa wa kodi ya ardhi waliopatiwa ilani za madai na kitu gani kimefanyika kwa wale watakaokaidi kulipa. 

Amelitaka jiji hilo pamoja na kuuza viwanja lakini linapaswa kuhakiisha linakusanya madeni na taarifa za wadaiwa wote wa kodi ya ardhi zinaingia katika vikao vya uchumi na mipango vya madiwani lengo ni kutoa nafasi ya ufuatiliaji kutoka kwa madiwani. 

"Dodoma ni uso na jicho la nchi kutokana na uamuzi uliotolewa wa kuwa makao makuu ya nchi  na watumishi mnatakiwa  kufanya kazi kwa bidii kama vile mko katika makao makuu ya nchi" alisema Dkt Mabula 

Aidha,  Naibu Waziri wa Ardhi amewataka watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo wenye madeni ya kodi ya ardhi kuwa wa kwanza kulipa madeni kabla ya kuanza kudhughulika na wadaiwa sugu kwa kuwa  wanatakiwa kuwa mfano.

Vile vile,  Dkt Mabula ameitaka halmashauri ya jiji la Dodoma kusimamia mji usichafuke ili kuepuka kuwa na jiji la ajabu na kulitaka kusimamia vyema utoaji vibali vya ujenzi sambamba na  kuhakikisha ukaguzi na unafanyika na kuwa na watu wa kuwapa taarifa maeneo yanayojengwa kiholela ili kudhibiti wanakiuka sheria za ujenzi na kusisitiza  huu siyo wakati wa kuleana na cha msingi ni kupanga mji vizuri. 

Pia Naibu Waziri wa Ardhi alikumbana na tatizo la utunzaji majalada ya ardhi usiozingatia taratibu kama alivyokuta katika halmashauri mbalimbali alizozitembelea na kuagiza upungufu uliojitokeza kurekebishwa haraka iwezekanavyo. 

Mkuu wa Idara ya Ardhi, Mipango Miji na Maliasili katika halmashauri ya jiji la Dodoma Joseph Mafuru alisema jiji hilo katika mwaka uliopita limefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 7. 196 ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni  4. 8 zimetoka katika kodi ya pango la ardhi na katika kipindi cha kuanzia januari mwaka huu tayari  imekusanya shilingi bilioni 1. 194 

Mkuu huyo wa idara ya ardhi alisema halmadhauri hiyo ina jumla ya migogoro 2136 na kati ya hiyo 1541 ishapatiwa ufumbuzi huku migogoro 595 ikiendelea kutatuliwa. 

Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Dodoma Edward Mpogolo alisema halmashauri ya jiji la Dodoma imekuwa ikifanya kazi nzuri lakini imekuwa ikukambana na baadhi ya changamoto Kama ucheleweshaji ulipaji fidia  katika baadhi ya maeneo yaliyo twaliwa na serikali kwa ajili ya shughuli mbalimbali.

Ametolea mfano wa sehrmu ya eneo la Iyumbu mkoani Dodoma ambalo  limetwaliwa kwa ajili ya shughuli mbalimbaki kama vile  barabara na eneo la  kuzikia (makaburi). 

Alisema,  hali hiyo inawafanya wananchi ambao maeneo yao yamechukuliwa kutojua hatma ya malipo yao na hivyo kuwafanya kuishi kwa mashaka. 
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumaba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimpa maelekezo Mtunza kumbukumbu wa halmashauri ya jiji la Dodoma Rashid Chikawe katika ofisi za idara ya ardhi wakati alipofanya ukaguzi katika majalada ya ardhi kwenye jiji hilo leo tarehe 28 Januari 2019 kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi. wa pili kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Dodoma Edward Mpogolo

 Watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya jiji la Dodoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipofanya ziara katika halamashauri hiyo kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi.
 - Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwasili katika halamashauri ya jiji la Dodoma kuzungumza na watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI)

ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU NIDA DICKSON MAIMU SASA AFUNGULIWA MASHTAKA 100,APANDISHWA KIZIMBANI

0
0
Na Karama Kenyunko globu ya Jamii, 
BAADA ya kuachiwa huru na kukamatwa tena jana mchana,  aliyekuwa  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake watano wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka 100 mapya yakiwemo mashtaka 25 ya utakatishaji fedha.

Wakili wa Serikali Wankyo Saimon akisaidiana na Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amewataja washtakiwa wengine mbali na Maimu kuwa ni Meneja Biashara wa (NIDA), Aveln Momburi,
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers,  Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.


Katika mashtaka hayo ambayo yamesomwa mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally,  washtakiwa wanakabiliw Na mashtaka 22 ya kughushi, mashtaka 43 ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri, mashtaka mawili ya kula njama, mashtaka 25 ya kutakatisha fedha na mashtaka matano ya kuisababishia hasara NIDA.

Pia washtakiwa wanakabiliwa Na mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la matumizi mabaya ya madara lipo moja ambalo linamkabili  Maimu na Sabina. 

Katika shtaka la kwanza la kula njama Maimu, Ndege na Ntalima wanadaiwa, kati ya Julai 19, 2011 na Agosti 31,2015 wakiwa maeneo tofauti tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam walikula njama ya kufanya udanganyifu wa Sh bilioni 1.175 dhidi ya NIDA.

Pia Maimu anatuhumiwa kutakatisha fedha kiasi cha sh bilioni 1,175,785,600.93  kati Julai 19,2011 na Agosti 31, 2015  ambapo anadaiwa kujihusisha moja kwa moja kuhamisha fedha hizo huku akijua ni zao la kosa la kughushi.

Katika shtaka jingine,  Maimu na  Raymond wanatuhumiwa November 7, 2011 wakiwa Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni jijini Dar es Salama walitumia madaraka yao vibaya na kusababisha  huo cha sheria  (Law School) Dar es Salaam na Kampuni ya Gotham International Ltd kupata faida ya Sh .899,935,494.

Imedaiwa kati ya Novemba 12, 2011 na Mei 12, 2015, Maimu na Momburi wakiwa makao makuu ya NIDA, Kinondoni akiwa Mkurugenzi na Meneja wa biashara walishindwa kusimamia ujenzi wa jengo lililopo plonti namba 39A na kuikuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh 402,210,885.02.

Aidha imeendelea kudaiwa kuwa kati ya Julai 19,2011 na Agosti 12, 2011,  washtakiwa Maimu na Ntalima wakiwa Makao Makuu ya NIDA walitumia nyaraka ya uongo kwa nia ya kumdanganya mwajiri wao kuwa walitumia stakabadhi ya malipo namba 0034 na namba 0035 kuilipa Kampuni ya Aste Insurance Brokers Ltd dola za Marekani 10,300.00.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za Uhujumu uchumi,  hadi Mahakama Kuu kwa kupata kibali kutoka kwa DPP. 

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeshakamilika na tayari wamewasalisha maelezo ya mashahidi Mahakama Kuu.

Katika kesi hiyo washtakiwa, Momburi na Raymond wao hawajapatikana na kosa la kutakatisha fedha, kwa hiyo mashtaka yao yanadhaminika, hivyo upande wa utetezi uliiomba mahakama kuwapatia washtakiwa hao dhamana. 

upande wa mashtaka ulieleza kuwa dhamana iko wazi kwa washtakiwa hao, lakini si hapa ni Mahakama Kuu kama wanataka wanaweza kupeleka maombi ya dhamana Mahakama Kuu.

"Njia pekee ni wapeleke maombi yao Mahakama Kuu yakasikilizwe na kutolewa uamuzi kwa sababu sisi hatuna Mamlaka ya kusikiliza kesi hii," amsema hakimu Ally 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi February 12 mwaka huu, ambapo washtakiwa watasomewa maelezo ya mashahidi (Committal)
Viewing all 109610 articles
Browse latest View live


Latest Images