Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

GEREZA KITETE – NKASI LAANZA UZALISHAJI WA ZAO LA MAHARAGE

$
0
0

Mkuu wa Gereza Kitete – Nkasi, SP. Job Lwesya(katikati) akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) kukagua mashamba ya maharage ya Gereza Kitete – Nkasi alipofanya ziara ya kikazi katika Gereza hilo leo januari 27, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiangalia moja ya jembe la trekta la Gereza hilo alipotembelea Gereza Kitete – Nkasi leo Januari 27, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akizungumza na Maafisa na askari wa Gereza Kitete – Nkasi alipofanya ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua shughuli mbalimbali za uzalishaji mali katika Gereza hilo.
Maafisa na askari wa Gereza Kitete – Nkasi wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(hayupo pichani)alipotembelea Gereza hilo leo januari 27, 2019 (Picha zote na Jeshi la Magereza).



Na ASP. Lucas Mboje, Nkasi

KATIKA kuelekea kwenye mpango wa kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa magerezani Gereza la Kilimo Kitete – Nkasi limeanza uzalishaji wa maharage ambapo katika msimu huu wa mwaka 2018/2019 tayari limelima zao hilo.

Akizungumza leo mara baada ya kutembelea Gereza hilo, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amesema kuwa ameridhishwa na hatua mbalimbali zinazoendelea katika kufanikisha mpango mkakati wa uzalishaji wa chakula kwa wingi katika maeneo yakimkakati pamoja na uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa na vitendea kazi.

“Ni lazima tuhakikishe kuwa jukumu hili tulilopewa linatekelezwa ipasavyo hivyo, Mkuu wa Gereza pamoja na timu yako hakikisheni mnaongeza bidii ya kazi kwa kutumia rasilimali zilizopo ikiwemo nguvu kazi ya wafungwa ili kufikia malengo ya hekari 300 za zao la maharge mlizopewa kwani msimu bado unaruhusu”. Alisema Kamishna Jenerali Kasike.

Aidha, Kamishna Jenerali Kasike amesema kuwa Jeshi litaangalia uwezekano wa kuliwezesha Gereza Kitete zana mbalimbali za kilimo kama vile trekta, ambazo zitarahisisha kufanikisha malengo ya kimkakati ili kuongeza uzalishaji wa chakula cha wafungwa.

Ameongeza kuwa Gereza Kitete – Nkasi ni miongoni mwa magereza 10 ya kimkakati ambayo tayari yameainishwa katika mpango mkakati wa Jeshi la Magereza katika kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa. Magereza mengine ni Songwe, Mollo, Arusha, Idete, Kiberege, Kitengule, Pawaga, Kitai na Gereza Ludewa.

Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike amewaasa viongozi wa Jeshi hilo pamoja na watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia vitengo(Ugavi na Uhasibu) katika vituo vyao kuzingatia suala la uadilifu na amewataka kujiepushe na vitendo vyote vya ubadhilifu wa mali za umma ili kuwezesha kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza Kitete, SP. Job Lwesya alisema kuwa katika msimu wa Kilimo wa mwaka 2018/2019 gereza hilo limelima ekari 114 za maharage na kwa sasa linaendelea na maandalizi ya mashamba mengine ili kufikia malengo waliyopewa ya kulima hekari 300 za maharage.

Aidha, aliongeza kuwa gereza hilo linayo ardhi ya kutosha na yenye rutuba hivyo wamejipanga kimkakati katika kuhakikisha kuwa wanazalisha mazao mbalimbali kwa wingi kwa ajili ya chakula wafungwa.

Gereza Kitete – Nkasi lina eneo lenye ukubwa wa ekari 3,742 ambazo zinafaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula ikiwemo zao la maharage, mahindi na Arizeti. Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1989 kwa lengo la kuwahifadhi wahalifu pamoja na kuwapatia wafungwa programu za urekebishaji ili wamalizapo vifungo vyao waweze kuwa raia wema.

NMB YAFUTA TOZO MBALIMBALI KWA WATEJA

$
0
0


Meneja Mwandamizi wa NMB, Bidhaa za Amana - Stephen Adili (kulia) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Akaunti na Malipo - Michael Mungure na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha huduma kwa Wateja - Abella Tarimo.
Meneja Mwandamizi wa NMB, Bidhaa za Amana - Stephen Adili (kulia) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Akaunti na Malipo - Michael Mungure na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha huduma kwa Wateja - Abella Tarimo.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja - Abella Tarimo (kushoto) wa Benki ya NMB akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Akaunti na Malipo - Michael Mundure na kulia ni Meneaja Mwandamizi wa Bidhaa za Amana wa Benki ya NMB - Stephen Adili.



NA SALUM MKANDEMBA

KATIKA kuharakisha kasi ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, ikiwemo kuchagiza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki, Benki ya NMB imetangaza kufuta tozo mbalimbali kuanzia Februari mwaka huu.

Kufutwa kwa tozo hizo na kufungua milango ya huduma bure za kibenki ‘free banking,’ kumetangazwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Akaunti wa NMB, Michael Mungure, alipoongea na wanahabari.

Mungure alibainisha kuwa, baada ya tafiti za kina, zilizojikita katika kujua kiini cha kutoongezeka kwa idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki, hivyo kuachwa na kasi ya maendeleo kuelekea Uchumi wa Kati, wameamua kuja na ‘free banking.’

Alizitaja baadhi ya tozo zilizofutwa kuwa ni pamoja na ile ya kufungua akaunti kwa mteja mmoja mmoja (Individuals Account), ada ya kila mwezi (monthly maintenance fees), makato ya miamala (transactions fees) na kufufua akaunti ya zamani (dormant account).

“Hii tozo ya miamala tuliyofuta na ambayo itatumika kuanzia Februari mwaka huu ni ya kuhamisha fedha kutoka akaunti moja ya NMB kwenda akaunti nyingine ya NMB, lakini pia kutakuwa na huduma bure zilizotajwa hapo juu, pamoja kuuliza salio,” alisema Mungure.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Bidhaa za Amana wa NMB. Stephen Adili, aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa ya kufutwa kwa tozo hizo kwa kufungua na kutumia huduma za NMB, ambazo zinapatikana kirahisi kidijitali pia.

“Kuanzia sasa tunataka wateja wetu na Watanzania kwa ujumla, waje wafungue akaunti kwa wingi na hakutakuwa na makato kama tulivyoainisha, fursa ambayo itaharakisha ustawi wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,” alisema Adili.

TAARIFA KUHUSU UTEUZI WA WENYEVITI NA WAJUMBE WA BODI ZA GST NA STAMICO

TAASISI YA USTAWI WA JAMII INAKARIBISHA MAOMBI YA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2019/2020

MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ABEBA MAONO YANAYOLENGA KUTOA HUDUMA BORA

$
0
0



 *Asema ndoto yake ni kuona TANESCO inajiendesha kwa faida,kutoa gawio kwa Serikali


*Aelezea mkakati wao ni kuendelea kuboresha huduma ya umeme, agusia miundombinu

*Akerwa na tabia ya kuchoma moto katika maeneo ambayo miundombinu yao inapita


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), Dk.Tito Mwinuka amewahimiza watumishi wote wa shirika hilo kutoa huduma bora ,sahihi na kwa wakati kwa wateja wao huku akieleza ndoto yake ni kuona shirika hilo linajiendesha kwa faida na kutoa gawio kwa Serikali.

Dk.Mwinuka ameeleza hayo mjini Arusha, wakati anazungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini baada ya kukamilika kwa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya umeme inayotokelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.John Magufuli .

Ziara hiyo imefanyika katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro na miongoni mwa miradi ambayo wahariri wameona ilivyotekelezwa ni ile iloyopo kwenye TEDAP.

Akifafanua zaidi wakati anajibu baadhi ya maswali ya wahariri hao.Dk.Mwinuka amesema pamoja na kuwepo kwa pongezi nyingi zinatokana na kuwepo kwa huduma bora zinazotolewa na shirika hilo lakini bado amesisitiza kwa watumishi wote wa TANESCO kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja.

"Tunataka kuona TANESCO inatoa huduma nzuri na hiyo iwe kwa nchi nzima.Tunataka mteja anapokwenda TANESCO au kokote ambako tunatoa huduma basi apate huduma nzuri,sahihi na kwa wakati pamoja na kuheshimiwa.Hivyo niendelee kutoa rai kwa watumishi wa ngazi zote tuliyopo tutoe huduma nzuri,"amesisitiza.

Alipoulizwa kuhusu ndoto yake ,Dk.Mwinuka amejibu kuwa ndoto yake ni kuona TANESCO inajiendesha na kufanya kazi zake kwa faida na kwamba wanakwenda vizuri huku akifafanua kwa miaka miwili sasa shirika hilo linajiendesha bila kupewa ruzuki.

" Malengo yetu ni kuhakikishia TANESCO tunafanya kazi zetu na kutengeneza faida na hii imeanza kuleta tija,ni mwaka wa pili tunajiendesha bila ruzuku ya Serikali na hiki ndicho tunachosisitiza tuwe shirika ambalo linapata faida na hatimaye tutoe gawio kwa Serikali," amefafanua Dk.Mwinuka.

Kuhusu madeni ,Dk.Mwinuka ameweka wazi TANESCO ilikuwa inadaiwa madeni makubwa ambayo yaliionekana sugu lakini kupitia mikakati yao wamedhamiria kulipa madeni hayo na kwamba kwa sasa wamefanikiwa kwani deni haliongezeki na hivyo wanatarajia kuyamaliza.

"Kutokana na hali iliyokuwepo miaka ya nyuma TANESCO ilijikuta inadaiwa ,hivyo tunaendelea kulipa madeni ya nyuma," amesema na kusisitiza pamoja na muelekeo mzuri wa shirika hilo bado wamejipanga kutoa huduma ikiwemo ya kuhakikisha nchi yetu inakuwa na umeme wa uhakika na kuendelea kutatua changamoto zilizopo.

Kuhusu miradi ya Miradi ya Kuimarisha mifumo ya Usambazaji Umeme nchini(TEDAP) Dk.Mwinuka amesema wamefanikiwa kuitekeleza miradi hiyo kwa mikoa ya Arusha,Kimanjaro na Dar es Salaam na kwamba uwepo wa miradi hiyo imeleta tija kubwa.Alipoulizwa iwapo TANESCO itapeleka mradi wa TEDAP katika mikoa mingine ,Dk.Mwinuka amesema kuwa "Ni kweli tunatamani kuipeleka miradi hiyo nchi nzima maana tumeona faida yake kwa mikoa ambayo tuimeitekeleza.

"Pamoja na kutamani TEDAP itekelezwe na kwenye mikoa mingine lakini changamoto kubwa ni fedha.Hata hivyo pamoja na changamoto hiyo TANESCO tumejiongeza kwani kwa kutumia fedha zetu za ndani tumeutekeleza mradi wa TEDAP eneo la Dege Kigamboni.Hivyo tutaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa umeme," amesema Dk.Mwinuka.

Pamoja na mambo mengine wahariri walitaka kufahamu kuhusu uchomwaji moto maeneo ambayo imepita miundombinu ya TANESCO,amejibu kuwa ni kweli kuna mikoa uchomaji moto umeshika kasi na kuitaja baadhi ya mikoa hiyo ni Lindi,Mtwara na Songea ambako huko ndiko mto unaonekana kuwaka sana.

" Wananchi wasichome moto katika maeneo ambayo miundombinu ya umeme, ni jukumu letu sote kuhakikisha tunailinda na kuitunza miundombinu yetu ya umeme ambayo uwekezaji wake katika kutekeleza miradi ya umeme inatumia gharama kubwa.Tuitunze miundombinu yetu,"amesema Dk.Mwinuka.

Wakati huo huo Dk.Mwinuka amezungumzia namna ambavyo wakati mwingine TANESCO inatupiwa lawama katika jambo ambalo huenda halikusababishwa na Shirika hilo.Ametoa mfano unapotokea moto lawama mara nyingi zinaelekezwa TANESCO hata kama chanzo cha moto ni mteja wao.

"Mtu anaweka pasi kwenye umeme,halafu anapomaliza kunyoosha nguo hazimi swichi ya umeme,ikitokea bahati mbaya kukatokea moto lawama zinakwenda TANESCO wakati sababu za moto ni mteja.Hata hivyo hatuwezi kukwepa moja kwa moja ,hivyo sote tunaotumia umeme kuchukua tahadhari kuondoa hizi lawama," amesema Dk. Mwinuka na kuwaomba wateja wao kuwa sehemu ya kuondoa tatizo la moto.

Kuhusu TANESCO kutumia magrupu ya WhatsApp kutoa taarifa kuhusu umeme kwa wateja wao,amesema magrupu hayo yanasaidia sana kutoa taarifa kwa haraka na uhakika.Ametoa rai kwa TANESCO kwa wilaya na mikoa yote nchini kuhakikisha kunakuwa na magrupu hayo na kuhakikisha wananchi wengi wanajiunga nayo kwa lengo la kutoa na kupokea taarifa zinazohusu umeme nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kushoto), akiwa na Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Shirika hilo anayeshughhulikia usambazaji na huduma kwa wateja, Mhandisi Raymond Seya, (wakwanza kulia), Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona, wakati akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya wahariri wa vyombo vya habari waliokuwa wakitembelea mradi wa ukarabati na uimarishaji miundombinu ya umeme, TEDAP, na ule wa Kenya-Tanzania Power Interconnection Project (KTPIP) TII jijini Arusha.
Dkt. Mwinuka na wasaidizi wake, wakiwa na wahariri.
Dkt, Mwinuka akisikilzia kwa makini maoni na maswali kutoka kwa wahariri
Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akifungua kikao hicho.

Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Stella Hiza, akijitambulisha. Picha na
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Arusha

WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KICHACHA MKOANI KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAJENGEA MADARASA

$
0
0


Na Rhoda Ezekiel,Kigoma

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Kichacha katika Kijiji cha Kichacha Kata ya Kasanda wilayani Kakonko mkoani Kigoma wameipongeza Serikali kwa kuwajengea madarasa na kuwatoa chini ya mti walikokuwa wakisomea awali.

Pongezi hizo wamezitoa jana baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala kutembelea shule hiyo na kukuta watoto wakiwa katika vyumba vya madarasa tofauti na awali walipokuwa wakisomea katika nyumba ya miti.

Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo Kulwa Anania amesema walikuwa wakipata wakati mgumu pindi mvua zilipokuwa zikinyesha kwani walikuwa hawaendi shule kwa kuwa walikuwa hawana eneo zuri la kusomea na ilikuwa ikisababisha kushuka kwa ufaulu katika masomo.

Amesema wanaipongeza Serikali kwa kutatua changamoto yao waliokuwa nayo na sasa wanaendelea kusoma vizuri katika mazingira mazuri na wanaipongeza serikali kwa jitihada wanazo zifanya.Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Kichacha Emanuel Siwija amesema kwa mwaka 2017/2018 walipokea jumla ya Sh. milioni 42 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na vyoo matundu manne na ofisi moja, ambapo mpaka sasa ujenzi huo umekamilika na wanafunzi wanatumia vyumba hivyo.

Amesema awali wanafunzi hao walianza kusomea chini ya mti ,na baadae wakajenga kijumba cha miti kwa ajili ya kujihifadhi na 2018 ndipo walipopata madarasa na mpaka sasa upungufu ni mdogo.Ameongeza kwa mwaka jana wao kama shule kwa matokeo ya darasa la nne wameshika nafasi ya pili katika Wilaya na wanaendelea kupambana kuhakikisha wanafunzi wote wanafaulu kwa kuwa nyenzo za kufundishia wanazo na Serikali imetoa madawati kupitia Mkuu wa Wilaya.

Akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za maendeleo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, amesema wao kama Serikali wamejitahidi sana kuhakikisha suala la upungufu wa vyumba vya darasa linapungua na kuhakikisha Wanafunzi wanapata elimu na katika mazingira bora ya kusomea .

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha watoto wote wanapata elimu, na kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali kuchangia shughuli za maendeleo bila kujali itikadi zao.

Aidha Mkuu huyo alitoa mwito kwa Wananchi wa Wilaya hiyo kuwapuuza Wale wote wanaowashawishi wananchi kuacha kujitolea katika shughuli za maendeleo kwa kuwa maendeleo yote yanaletwa na Wananchi kwa kushirikiana na Serikali.


Shule ya msingi Kichacha ilivyokuwa mwaka 2017

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kichacha katika Kijiji cha Kichacha Kata ya Kasanda wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Kanali Ndagala ametembeea shule hiyo na kukuta watoto wakiwa katika vyumba vya madarasa tofauti na awali walipokuwa wakisomea katika nyumba ya miti.
Shule ya msingi Kichacha ilivyo sasa 

OSCAR KAMBONA: KIONGOZI MAHIRI, MTANASHATI NA RAFIKI KIPENZI WA MWALIMU NYERERE ALIYEISHIA KUWA ADUI YAKE MKUBWA!!!

$
0
0
1. Usuli

Jioni ya Ijumaa ya tarehe 13.8.1925, huku mvua kubwà na radi kali zikirindima kijijini Kwambe, wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma, alizaliwa mtoto wa kiume akiwa buheri wa afya. Wazazi wa mtoto huyo, Rev. DAVID KAMBONA na Bi. MARIAM KAMBONA, wakampa mtoto huyo jina la OSCAR SATHIEL DAVID KAMBONA. Mvua na radi hiyo, kwa mujibu wa mila za kijijini hapo, "nyumbi hii, bombi hii", ilikuwa ni baraka na ishara kuwa mtoto huyo atakujakuwa wa kipekee.

2. Elimu Chini ya Mwembe

KAMBONA, tofauti na watoto wengine, hakusomea shuleni elimu ya awali bali alifundishwa na wazazi wake pamoja na mjomba wake ambao wote walikuwa walimu. Mafunzo hayo ya awali yalikuwa yakifanyika chini ya mwembe huku chai na mihogo vikiwa pembeni.

3. Elimu ya "Middle School"

Baadae KAMBONA alipelekwa shule ya Kati ya Mt. Barnabas, Liuli. Akiwa shuleni hapo, KAMBONA alikuwa kipanga na "aliwatimulia vumbi" wanafunzi wote kwa miaka yote alipokuwa shuleni hapo.

4. Alliance Sec. School

KAMBONA alifaulu vizuri mitihani yake na akachaguliwa kujiunga na "Alliance Sec. School", Idodomia ambayo baadae ikajaitwa Mazengo Sec. School. Almanusra KAMBONA asiendelee na masomo kwani baba yake hakuwa na uwezo wa kulipa £ 30 kwa mwaka. Uwezo wa KAMBONA "kutema yai" ndio uliomponya kwani alifanikiwa kumshawishi Askofu kumlipia ada hiyo baada ya kusali Sala ya Baba Yetu kwa Kiingereza!.

5. Tabora Boyz Sec. School

KAMBONA alisoma shule hii pamoja na J. Lusinde, E. Mzena, B. Ngwilulupi, A. Nsekela, A. Nyirenda na K. Chiume. Ni akiwa shuleni hapo ndipo kwa mara ya kwanza, KAMBONA alionana na NYERERE aliyekuwa akifundisha St. Marys, Tabora.

6. Ualimu Alliance Sec. School

Baadae, KAMBONA alienda kufundisha shule hii na akakutana na J. Lusinde na K. Chiume na baadae akawa "Schoolmaster".

7. KAMBONA akutana na NYERERE tena

KAMBONA alikutana na NYERERE kwa mara ya 2 kwenye Mkutano wa taifa wa waalimu mwaka 1954.

8. KAMBONA Ajiunga TANU

Mwaka 1955, KAMBONA alijiunga na TANU iliyozaliwa tarehe 7.7.1954 na akaonesha bidii kubwa huku akifanya kazi kwa kujitolea kwani TANU haikuwa na fedha. Bidii yake ilipelekea kuwa Katibu Mkuu wa TANU.

9. KAMBONA Awaingiza TANU Watanganyika 100,000

KAMBONA alitembea nchi nzima kwa miezi 6 akionana na Machifu na wanavijiji na kufanikiwa kuingiza wanachama 10,000. Baadae akiendelea na harakati hizo na baada ya miezi 12 akawa ameingiza wanachama 100,000. Viongozi wenzake wa TANU walimpongeza sana kwani TANU ikawa inaenea kwa kasi sana.

10. KAMBONA Afungua Akaunti ya Kwanza ya TANU

KAMBONA alikuwa na mawazo ya kimaendeleo kwani kutokana na michango ya wanachama aliweza kufungua akaunti ya kwanza ya TANU. Kwa hakika, hili lilikuwa ni jambo la kihistoria.

11. KAMBONA afuma "Governor's Scholarship" kusomea Sheria, UK

Mwaka 1957, KAMBONA alipata fursa ya kwenda UK kusomea LLB kwa miaka 3 na hivyo akaenda huko.

12. KAMBONA Awa Mtangazaji wa 1 wa Kiswahili BBC 1957

Tarehe 27.6.1957, KAMBONA aliweka historia kwa kutangaza Kiswahili BBC kwa mara ya 1 akisema-: "Hapa ni London, kwa mara ya kwanza BBC inawaletea habari kwa Kiswahili wananchi wa Afrika Mashariki. Asalaam Aleikhum".

13. KAMBONA awa Mwenyekiti wa TANU London

Kutokana na talanta yake kubwa ya uongozi, KAMBONA alichaguliwa kuwa Kiongozi wa wanafunzi chuoni na Mwenyekiti wa Tawi la TANU, London.

14. KAMBONA na NYERERE Washeachumba Chuoni London
Kati ya tarehe 26.6.1959 na 7.8.1959, NYERERE alikwenda UK kwa matayarisho ya uhuru wa Tanganyika na akalala chumba kimoja na KAMBONA ambaye walikuwa "wameshibana" sana. Katika "Press Conference" ya 1991 KAMBONA alisema- "TANU haikuwa na hela hivyo ili kubana matumizi, nikakaa na NYERERE room yangu chuoni na hii ilisaidia tuwe na muda mwingi wa majadiliano".

15. KAMBONA Amuoa MISS Tanganyika

Tarehe 19.11.1960, KAMBONA alimuoa Miss Tanganyika mrembo, Bi. FLORA MORIYO toka Kilimanjaro. Harusi hiyo ya kukata na shoka ilifanyika St. Paul Cathedral, London na kuhudhuriwa na wageni waalikwa 400. NYERERE alikuwa ndiye msimamizi aliyemsindikiza Bi. FLORA altareni. Ilikuwa ni harusi ya kwanza ya watu weusi kanisani hapo na ilitoka kwenye magazeti mbalimbali ya Ulaya.

16. KAMBONA Arejea Bongo

KAMBONA alirejea Bongo kuendelea na harakati za uhuru akihudumu kama Waziri wa Elimu na Katibu Mkuu wa TANU.

17. KAMBONA Awa Waziri wa 1 wa Mambo ya Nje

Katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Tanganyika, KAMBONA aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi.

18. KAMBONA Kipenzi cha 2 cha Wananchi baada ya NYERERE

KAMBONA alipendwa sana nchini kwani alikuwa msomi, mwanasiasa hodari, mtanashati na vijana wengi walimuiga staili yake ya nywele "KAMBONA Style". Kwa hakika, KAMBONA alipendwa sana.

19. KAMBONA- Kiongozi PEKEE Aliyewakabili Waasi, 1964

Usiku wa tarehe 19.1.1964, askari wa kambi ya Colito(Lugalo) waliasi wakidai marupurupu na nafasi za juu za vyeo kwa Waafrika. Rais NYERERE na Mh. RASHID MFAUME KAWAWA walitoroshwa na mlinzi wao, PETER BWIMBWO usiku wa manani hadi Kigamboni na kufichwa kwenye nyumbaya Mzee KIZWEZWE.

Mawaziri wote walibanisha makwao baada ya kupigiwa simu na Mh. J. LUSINDE, Waziri wa Mambo ya Ndani, kuhofia usalama wao. KAMBONA ndiye pekee aliyeingia "fronti" kwani si tu raia waliokuwa wakimpenda bali pia askari. Waasi walionekana kutulia baada ya mambo yao kuwekwa sawa lakini baada ya Rais NYERERE kuibukia Ikulu toka mafichoni baada ya siku 3, waasi "wakalianzisha" tena hivyo ikabidi maasi hayo yalizimwe kwa msaada wa Waingereza na baadae Wanaijeria.

20. KAMBONA Ashuhudia mchakato wa Muungano 1964

KAMBONA alikuwa ni mmoja wa mawaziri wachache sana waliokuwa wakijua mchakato wote wa muungano kwa undani na pia alishuhudia utiaji saini hati za muungano huko Zenji, tarehe 22.4.1964 kati ya Rais NYERERE na Rais wa Zanzibar, Mh. ABEID AMAN KARUME.

21. KAMBONA Atofautiana na NYERERE Mfumo wa Chama Kimoja

Baada ya ziara ya China 1965, NYERERE alivutiwa na "alikuwaameoza" kwa siasa za China na mfumo wao wa siasa hivyo akaunda Tume tarehe 28.1.1964 ili ipendekeze mfumo gani unaifaa nchi yetu. Tume hiyo ilikuwa chini ya Mh. KAWAWA ikapendekeza mfumo wa chama kimoja. KAMBONA, ambaye daima alikuwa hapepesi macho wala hayumbishwi, aliweka kunji na kutosaini ripoti hiyo na badala yake akatayarisha ripoti yake ya kutaka mfumo wa vyama vingi na NYERERE akahuzunishwa sana na msimamo huo wa KAMBONA. 

Kipindi hiki NYERERE aliishamuondoa KAMBONA kwenye wizara zile nyeti.

22. NYERERE "Amchana" kiaina KAMBONA 77 ya 1966

Tarehe 7.7.1966, NYERERE, akihutubia Taifa katika sherehe za 77, NYERERE alitumia mafumbo "kumpa za uso" KAMBONA ambapo alisema viongozi  wanaonekana kujipatia mali nyingi kiajabu hawafai hata kidogo.

23. KAMBONA Ajiuzulu u-Waziri na U-Katibu Mkuu TANU 1967

Tarehe 9.6.1967, KAMBONA alibwaga manyanga kwa kujiuzulu U-Katibu Mkuu wa TANU na Uwaziri wa Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini ambapo alitaja sababu za kiafya kuwa ndizo zilipelekea achukue uamuzi huo.

24. KAMBONA Atorokea Kenya, 1967 ki-James Bond !!

Kwakuwa KAMBONA alikuwa ni mtoto wa mjini, alitonywa kwamba kuna mpango wa kumkamata na kumsweka kizuizini.

Hivyo, usiku wa kuamkia tarehe 26.7.1967, KAMBONA, mkewe, watoto wake 2 na msaidizi wa kazi walifunga virago na ku-drive hadi Kenya kwa staili ya "James Bond"! Watu wengi walipigwa butwaa ni kwq vipi aliweza kutoroka bila kubambwa!.

Usiku wa siku hiyo jijini Nairobi, KAMBONA na familia yake walikwea "pipa" East African Airways Flight 720 kwenda "Kwa Mama, huku, huku nyuma ikadaiwa alitoroka na mamilioni ya fedha!.

25. NYERERE Aelezea "Kusepa" kwa KAMBONA

Siku chache baada ya KAMBONA "kula kona", NYERERE, akiongea na viongozi wa TANU Morogoro, alisema : "Itachukua muda mrefu kufahamu sababu za Bw. KAMBONA kujiuzulu, lakini jambo moja ni dhahiri; KAMBONA amenidanganya mimi, TANU, TZ na Afrika".

26. KAMBONA Ajitetea UK

Baada ya kusikia vijineno kwamba amesepa na mamilioni, tarehe 6.9.1967, KAMBONA alikanusha vikali na kuitaka serikali ya Tanzania iwasiliane na ya Kenya kupata uthibitisho kitu ambacho serikali ya TZ  hakikufanyika.

27. OTTIN na MATTIYA KAMBONA "Wasukumiziwa Ndani",1967

Hawa wadogo zake KAMBONA walionja "joto ya jiwe" kwani walinyakwa usiku tarehe 30.12.1967 na kuwekwa kizuizini, Ukonga.

Familia zao zikasambaratika vibaya sana kufuatia kukamatwa kwao. OTTIN alikuwa ni "Journalist" na MATTIYA alikuwa mfanyakazi Wizara ya Kilimo. OTTIN alikuwa amemuoa raia wa Martinique na walikuwa na watoto 2 wadogo na MATTIYA alikuwa amemuoa Mgambia wakiwa na mtoto wa miezi 3 tu. Wanawake hao walifukuziliwa mbali na kurudishwa makwao pamoja na watoto wao!.

28. KAWAWA "Amchana" KAMBONA Bungeni, 1968

Jumanne ya tarehe 23.1.1968, KAWAWA, 2nd VP, alilitaarifu Bunge:

"Wote mnajua kwamba Bw. KAMBONA aliikimbia nchi mwaka jana, 1967. Kabla hajaondoka, tarehe 6.12.1966, TZS 500.000/= ziliingizwa kwenye akaunti yake toka benki moja ya Uingereza. Uchunguzi wa BOT toka KAMBONA atoroke umeonesha kuwa tangu Juni 1965 na Desemba 1966, KAMBONA aliingiza katika akaunti yake jijini Dsm TZS 896,800/=. Kambona pia alikuwa anamiliki majumba mengi (Nyumba Magomeni-Plot No. 21,39 31), (Kunduchi bichi-Plot No.28), (Msasani bichi -Plot No. 92), (Morogoro-Plot No. 89) ns (Songea-Plot No.21)".

29. KAMBONA Amchana NYERERE nchini Nigeria, 1968

Baada ya TZ kuitambua Biafra, serikali ya Rais YAKUB GOWON ilikasirishwa sana hivyo ilimwalika KAMBONA aichafue TZ . Kwahakika, "jipu likawa limepata mkunaji" Hivyo, KAMBONA akaenda na kutoa muadhara Lagos tarehe 14.6.1968 ambapo "alimchana" vilivyo Rais NYERERE na kumwita dikteta. KAMBONA akaonesha kukosa uzalendo kwa taifa lake pale alipozomoka, bila ushahidi, kwamba TZ imepeleka vifaa vya kijeshi Biafra badala ya Zimbabwe!.

30. TANU "Yamfyekelea mbali" KAMBONA

NEC ya TANU iliyokuwa ikiketi Tanga, tarehe 19.10.1968, ilimvua uanachama KAMBONA pamoja na wabunge wengine 8 "Vichwa-maji" waliohoji uhalali wa TANU kuwa juu ya Bunge. Wabunge hao ni W. Mwakitwange, M. Choga, S. Kibuga, J. Bakampenja, E. Anangisye, G. Kaneno na Dr. F. Masha.

31. NYERERE "Amchana" tena KAMBONA, 1969

Tarehe 12.1.1969 kwenye sherehe za Mapinduzi Znz, NYERERE "alimuwakia" KAMBONA na kusema- "KAMBONA ni mwizi na mhuni kisiasa.

32. KAMBONA Akejeliwa Mashuleni na Majeshini

Nyimbo nyingi za kumkejeli KAMBONA zilitungwa majeshini na mashuleni lakini zilizokuwa maarufu ni hizi 2:

1. KAOMBONA Kaolewa wapi....? Kwa Wazungu...Kisa nini?...Tamaa ya Mali!

2. Alimselema ...alija, akija KAMBONA chinja... chinjilia mbali..!!.

33. KAMBONA Adaiwa ni _"Mastermind"_wa Uhaini, 1969

Mwaka 1969, KAMBONA alidaiwa kuwa "Mastermind" wa uhaini. Mashitaka yalikuwa kwamba washtakiwa 7 wakishirikiana na KAMBONA kati ya Machi 1968 na Octoba 1969, walitaka kumuua Rais NYERERE na kuipindua serikali. Washtakiwa hao 7  ni (Bibi Titi Mohamed , Michael Kamaliza, Gray Mattaka, John na Eliya Chipaka, Capt A. Milinga na W. Chacha). 

Kesi ilianza kurindima Jumatatu tarehe 6.6.1970 na ilisikilizwa na Jaji  Mkuu Georges na iliendeshwa na AG Mark Bomani. Wanafunzi wa Sekondari Tambaza(F.V Arts akiwepo Othman Chande, Jaji Mkuu wa 7) walikuwa wakijongo vipindi kwenda kortin kushuhudia kesi hii iliyokuwa na mvuto wa aina yake.

 Washtakiwa wote walitiwa hatiani kasoro A. Milinga na KAMBONA ambaye hakuwepo.  M. Kamaliza na mwenzake walipigwa "mvua" 10 na wengine walifungwa maisha na Bibi Titi akapata msamaha 1972.

34. OTTIN MATTIYA Waachiwa 1978

Tarehe 5.2.1978, katika kusheherekea mwaka 1 wa kuzaliwa CCM, NYERERE, akitumia ibaracya 45 ya Katiba, aliwaachia huru OTTIN na MATTIYA pamoja na JOSEPH KASELABANTU( Mwasisi wa TANU).

OTTIN na MATTIYA, baada ya kugundua familia zao hazipo,  wakaona Bongo hamna ishu nao wakaamua pia kusepa. Walivuka mpaka wa TZ na Kenya usiku Kininja kwani mpaka huo ulikuwa umefungwa kutokana na uhasama bainavya TZ na Kenya na wakaelekea UK.

35. NYERERE NA KAMBONA walikuwa majirani Msasani

Baada ya KAMBONA kuondoka nchini 1967, nyumba yake ikawa inakaliwa na Rais MILTON OBOTE kwa takribani miaka 10 baada ya kupinduliwa na Nduli IDD AMIN, 1971.

36. Vyama Vingi vyaanzishwa Bongo, KAMBONA ataka kurejea

Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992, KAMBONA akiwa London alisema, ije mvua, lije jua,  anarejea kwenye Taifa lake. Serikali ikamuonya kuwa asithubutu na akijifanya fyatu au kichwa-maji akatia pua yake tu Bongo, "hakuna rangi ataacha kuiona".

37. KAMBONA Aitunishia msuli serikali, Atinga Bongo

KAMBONA aliamua kuwa kama "Mbwai, mbwai tu" hivyo akaonesha "Shoo za kibabe" na kurejea nchini akisafiria nyaraka za Umoja wa Mataifa zilizotolewa na serikali ya UK. Aliporejea hakukamatwa na badala yake, tarehe 4.9.1992, serikali ilimpa miezi 3 aweke sawa uraia wake kwakuwa ni Mmalawi! Miezi hiyo iliisha tarehe 4.12.1992 na serikali "ikaufyata" kwani haikumfanya kitu chochote!.

38. KAMBONA aeleza sababu za kutoroka, 1967:

Baada ya kurejea nchini, KAMBONA alikata kiu ya wote waliotaka kujua kilichopelekea asepe "Kwa Mama" ni nini ambapo alitiririka:
"Mimi na NYERERE tumetoka mbali. Sisi ndio tuliokuwa Viongozi wakuu wa TANU; Yeye Mwenyekiti, mimi Katibu Mkuu. NYERERE aliporudi toka China 1965 alitaka kuleta sera za China na mfumo wa chama kimoja. Nikapingana nae.."

39. KAMBONA Aeleza alichokuwa akifanya UK

Wiki 2 baada ya kurejea nchini, KAMBONA alitiririka kitu alichokuwa akifanya nchini Uingereza kwa miaka 25 aliyoishi huko ambapo alisema- "I did business. I used to go to the Arab countries but this did not last. I then depended on income support from Britain. Every Tuesday You take your book to the Post office...

40. KAMBONA atishia "Kumwaga ugali na mboga" kuhusu NYERERE

Badala ya kushugulikia uraia, KAMBONA akaendeleza bifu lake na NYERERE ambapo alisema anataka kufanya mkutano mkubwa viwanja vya Jangwani ili aeleze ufisadi wa NYERERE. Mapadri na masheikh walimsihi sana lakini akashikilia msimamo wake.

41. KAMBONA Ambwelambwela Jangwani,1992

Tarehe 21.11.1992, viwanja vya Jangwani viliweka rekodi kutokana na umati mkubwa wa "wapenda ubuyu" uliojitokeza toka mida ya mchana kulisikia Jabali hilo litaeleza nini kuhusu Baba wa Taifa, Mwalimu NYERERERE.

KAMBONA aliwaboa sana 90% ya waliohudhuria kwani alidai, bila ushahidi, kuwa NYERERE, AMIR JAMAL na KAWAWA wameficha mamilioni ya fedha mabenki ya Ulaya. KAMBONA akaenda mbali na kudai NYERERE ni Mtutsi, KAWAWA na MKAPA ni watu wa Msumbiji na MALECELA ni Mcongoman!. Ikaonekana ni hekaya za Abunuwasi na hadithi za Esopo tu!.

42. NYERERE Amjibu KAMBONA

NYERERE, siku chache baadaye akiwa Msasani, aling'aka- "Mimi ni lofa. I dont have a single penny abroad, I can assure you. Kama RASHID na AMIR hawawekwi kundi la watu waaminifu duniani, labda neno uaminifu ni neno tu, halina maana. Hawa ni waaminifu sana. Pia, mimi sipendi kuhusishwa na mambo ya kijingajinga. Ni makosa kushindana na kundi la wapumbavu. Kambona alete ushahidi maana "any blessed fool could stand up there" na kusema chochote".

43. MAWAKILI wamchimba Mkwara-Mbuzi KAMBONA

Baada ya KAMBONA kutoa kashfa dhidi ya viongozi hao mashuhuri nchini, mawakili wa Viongozi hao walimpa siku 14 toka tarehe 8.12.1992 kuomba radhi au kutoa ushahidi.

KAMBONA aliwajibu kuwa _"Mtu mzima hatishiwi nyau"_na akachekesha watu pale alipodai _"Nondo" zake kuhusu "bank accounts" za viongozi hao amezisahau UK!.

44. KAMBONA Aunda TADEA

KAMBONA aliunda chama cha TADEA ambacho hakikuleta upinzani wowote wa maana.

45. KAMBONA afariki London, 1997

KAMBONA alifariki jijini London mwaka 1997 na mwili wake kuletwa nchini na kupokelewa na ndugu zake na kiongozi wa serikali, Mh. J.M. KIKWETE, Waziri wa Mambo ya Nje. Rafiki yake NYERERE hawakuwahi kuonana toka atoroke mwaka 1967 na wala hakwenda kwenye mazishi yake.

46. RAIS KIKWETE Akutana na Mke wa KAMBONA, 2007

Tarehe 28.6.2007 katika hotel ya Kilimanjaro Kempisk, Rais wa awamu ya nne, Mh. JK alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 50 ya BBC KISWAHILI. Mh. JK, akiwa na mcheshi na mwenye bashasha kama kawaida yake, alikutana na kusalimiana na Bi. FLORA KAMBONA ambaye alikuwa mgeni mahsusi kwani mmewe, KAMBONA ndiye aliyekuwa Mtangazaji wa 1 wa BBC Kiswahili, 1957.

46. MWISHO:

Huyu ndiye OSCAR SATIEL DAVID KAMBONA aliyekuwa chanda na pete na Mwalimu NYERERE lakini mwisho wakawa maadui wasio na mfanowe!.

Tafakuri Tunduizi:

ATIKALI HII YA KUKATA NA SHOKA ina Tafakuri Tunduizi 100!!!

Taasisi ya Dk Ntuyabaliwe yakabidhi maktaba Tandale Magharibi

$
0
0
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi amezindua Maktaba ya Shule ya Msingi Tandale Magharibi na kutoa wito kwa wanafunzi kuitumia vyema maktaba hiyo kujenga maarifa.
Aidha amewataka wanafunzi kuilinda maktaba hiyo kama chanzo cha maarifa na weledi.
Maktaba hiyo imewezeshwa na taasisi hiyo kufuatia shindano la Andika Chalenge kwa shule za serikali nchini.
Aliwataka pia wazazi kutekeleza jukumu lao la kushawishi watoto kusoma vitabu na kutumia maktaba na kuwa weledi katika masomo kwa kujisomea.
Akizindua maktaba hiyo ambayo Taasisi iliikarabati, kuweka mashubaka pamoja na vitabu vya aina mbalimbali, Mwenyekiti wa Taasisi, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi amesema amejisikia furaha kutimiza ahadi ya kukabidhi maktaba kwa shule hiyo iliyotoa mshindi.
Katika  shindano hilo la uandishi la Andika Challenge ambalo linafanyika mikoa yote Tanzania na kushirikisha wanafunzi wote wa shule za msingi za serikali kuanzia darasa la 4 mpaka la 7 ambapo wanafunzi huandika hadithi na kutuma kwa sanduku la posta 163 Dar es salaam, washindi huzawadiwa tuzo na shule aliyotoka husaidiwa kuwa na maktaba.
Shule ya Msingi Tandale Magharibi imepata maktaba hiyo baada ya mwanafunzi wake Nuurat Venance kushinda shindano la kutunga hadithi lililowashindanisha wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo, jijini Dar es salaam.  Hivi sasa shindano hilo linawashindanisha wanafunzi  wote wa shule za msingi hapa nchini.
Alisema baada ya mshindi kupatikana mwaka jana ambaye alitoka katika shule hiyo, taasisi ilibaki na changamoto ya kuwezesha kupatikana kwa maktaba, na anapoifungua maktaba hiyo anafurahishwa kuwa taasisi imetekeleza ahadi yake kwa mshindi wa shindano hilo.
Jacqueline Mengi akizungumza katika makabidhiano hayo alisema kwamba nia kubwa wa shindano hilo ni kusaidia watoto kujua kusoma na kuandika na pia kuwa wabunifu na kutumia ubunifu wao kusonga mbele.
Alisema pamoja na serikali kuwezesha elimu bure, wao kama taasisi wanatoa mchango wao ambao utasaidia kuimarishwa kwa tabia ya kusoma na kujipatia maarifa kutoka katika maktaba.
Alisema taasisi ya Dk Ntuyabaliwe iliyoanzishwa kwa ajili ya kumuenzi baba yake ambaye alikuwa anapenda sana kujisomea vitabu na kuwahimiza watoto wake akiwemo yeye kujifunza kusoma,  kwa sasa inaendesha shindano hilo la Andika Challenge ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanajijenga katika ubunifu na matumizi wa lugha ya Kiswahili kwa kutunga hadithi zao wenyewe.

Anasema kwa msimu huu mashindano hayo yanaendelea na kwamba vigezo vinavyostahili kufanywa na wanafunzi kuanzia darasa la 4 hadi la 7.
Ikiamini kwamba kusoma na kuandika ndio njia pekee ya kukabiliana na wanafunzi wanaomaliza shule bila kujua kuandika Jacquline alisema kwa sasa wamewezesha shule 7 kuwa na maktaba, wanafunzi 4,406 kusaidia mambo mbalimbali na vitabu takaribani 20,827 kuwafikia wanafunzi.
Mapema Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa alisema kitendo cha kukabidhi maktaba kwa shule hiyo, Taasisi ya Dk Mtuyabaliwe imekuwa ikiunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais John Magufuli za kuboresha elimu nchini.
Wakitoa shukrani kwa niaba ya shule, Mwalimu Mkuu Doris Msigalo na Mwakilishi wa Wazazi  Sudi Makamba wameishukuru Taasisi na kusisitiza kuwa wataitumia na kuitunza vizuri maktaba hiyo.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akisalimiana na Mwakilishi wa Wazazi na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa,  Sudi Makamba mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Tandale Magharibi kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tandale Magharibi mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akiuliza maswali kwa wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akiimba pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba  lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya tukio la kuzindua maktaba  lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akikata utepe kufungua maktaba mpya ya shule ya msingi Tandale Magharibi iliyojengwa na taasisi hiyo jijini Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa juma. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwalimu Mkuu  wa shule hiyo, Doris Msigalo (katikati), Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa (wa kwanza kulia) pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akikata utepe kufungua maktaba mpya ya shule ya msingi Tandale Magharibi iliyojengwa na taasisi hiyo katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa, Mwakilishi wa Wazazi  Sudi Makamba, viongozi wa bodi ya shule pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa wakipitia baadhi ya vitabu vilivyotolewa na taasisi hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Tandale Magharibi kujisomea na kuongeza maarifa.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akimkabidhi moja ya kitabu mwanafunzi  Nuurat Venance aliyeshinda shindano la kutunga hadithi “Andika Challenge” lililowashindanisha wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo, jijini Dar es salaam na kupelekea shule yake kujengewa maktaba na taasisi hiyo.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akipewa mkono wa pongezi na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa mara baada ya kuonyesha picha za muonekano wa jengo la maktaba ya shule ya msingi Tandale Magharibi lilivyokuwa awali.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi akimkumbatia mwanafunzi  Nuurat Venance aliyeshinda shindano la kutunga hadithi “Andika Challenge” lililowashindanisha wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo, jijini Dar es salaam na kupelekea shule yake kujengewa maktaba na taasisi hiyo.
 Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Tandale Magharibi, Doris Msigalo akitoa neno la shukrani Muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi mara baada ya kuwakabidhi jengo jipya la maktaba shuleni hapo.
Muasisi na mwenyekiti wa  taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi  katika picha ya pamoja na uongozi wa Shule ya msingi Tandale Magharibi na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kufungua maktaba mpya iliyojengwa na taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi  akisalimiana na Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandrah aliyemwakilisha mtoto wake aliyesoma shule ya msingi Tandale Magharibi kushiriki halfa ya uzinduzi wa maktaba mpya shuleni hapo.Katikati ni Dj wa Diamond Platnumz Romy Jones.
Muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi  katika picha ya pamoja na Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandrah (wa pili kulia), Dj wa Diamond Platnumz Romy Jones (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Grace Mtesigwa (kulia) pamoja na dada wa Diamond Patnumz, Esma Platnumz.
Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Tandale Magharibi wakipiga ‘Selfie’ na Muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi  mara baada ya kufungua maktaba mpya shuleni hapo.

Naibu Waziri Shonza Awapongeza Waandaaji wa Mbio za Riadha Mirerani

$
0
0
Na Lorietha Laurence-WHUSM,Mirerani.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo  Mhe. Juliana Shonza   amewapongeza waandaji na waratibu wa mbio za riadha Mirerani (Mirerani Marathon) na kuahidi kuwa serikali itashirikiana nao kwa ukaribu kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa katika kuendeleza mchezo huo yanafanikiwa.
Hayo ameyasema jana Mji Mdogo wa Mirerani, wakati wa ufunguzi wa mbio fupi zilizoandaliwa na Mratibu Charles Mnyalu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya CRDB na Shirika la Bima la Zanzibar.
Mhe. Juliana Shonza ameeleza kuwa kupitia mbio hizo  za riadha kwa kiasi kikubwa zitasaidia  katika kutangaza fursa zinazopatikana Mirerani yakiwemo madini ya Tanzanite.
“Kupitia mashindano haya ya riadha yatasaidia katika kuutangaza mji huu wa Mirerani ambao ni mji pekee duniani ambapo madini ya Tanzanite yanapatikana, na hivyo kufungua fursa ya utalii wa madini nchini” amesema Mhe. Juliana Shonza.
Aidha aliwasihi  Maafisa Michezo kutokaa ofisini na badala yake kutoka nje na kushirikiana na wadau katika kusaka na kuendeleza vipaji mashuleni  ili kuwa na wachezaji wazuri watakaowakilisha nchi katika mashindano mbalimbali.
Vilevile Mhe. Shonza aliongeza kwa kueleza kuwa sera ya michezo inaeleza kuwa michezo ni suala jumuishi hivyo ni jukumu la wadau kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa inakuzwa na kuendelezwa.
Naye Mratibu wa mbio hizo Bw. Charles Mnyalu amesema kuwa lengo la mbio hizo ni kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John magufuli za kulinda rasilimali madini ya Tanzanite ikiwemo kuzungushia ukuta machimbo ya mirerani yaliyopo Wilayani Simanjiro.
Mashindano ya riadha Mirerani (Mirerani Marathon) yalihusisha mbio za kilomita 3, 5 na 21, ambapo washindi katika kilomita 21 walikuwa ni Bw. Faraji Damasi kwa upande wa wanaume huku wanawake waliongozwa na Failuna Matanga.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Katikati) akiponyeza kitufe kuashiria kuanza kwa mashindano ya riadha yaliyofanyika jana Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akimaliza mbio fupi za kilomita 5 wakati wa ufunguzi wa ponyeza wa mashindano ya riadha yaliyofanyika jana Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiongea na washiriki wa mbio fupi za riadha zilizofanyika jana Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza(kulia) akimpa mkono wa pongezi mshindi wa riadha za kilomita 21 kwa upande wa wanawake Bi. Failuna Matanga katika mashindano ya riadha yaliyofanyika jana Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza(kulia) akimpa mkono wa pongezi mshindi wa riadha za kilomita 21 kwa upande wa wanaume Bw. Faraji Damas katika mashindano ya riadha yaliyofanyika jana Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Mirerani).

Uganda na Tanzania zakubaliana kumaliza majadiliano ya Bomba la Mafuta mwezi Juni mwaka huu

$
0
0
Na Teresia Mhagama, Kampala
Serikali za Uganda na Tanzania zimekubaliana kuwa, majadiliano mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa mradi wa Bomba la mafuta Ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania yakamilike ifikapo mwezi Juni mwaka huu  ili kuendelea na hatua ya ujenzi wa bomba hilo.

Hayo yalielezwa kwa nyakati tofauti jijini Kampala na Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt Medard Kalemani na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Irene Muloni mara baada ya kufanyika kikao cha Mawaziri mbalimbali kutoka Uganda na Tanzania wanaohusika na mradi huo.

“ Kwa ujumla tumejipanga kuwa, majadiliano yote ya mradi na maandalizi mengine ya mradi kati ya pande zote mbili  yakamilike mwezi Juni mwaka huu ili ujenzi wa mradi pia uanze mwezi Juni  na tunataka kukamilisha mradi huu ndani ya miezi 36 mara baada ya ujenzi kuanza,” alisema Dkt Medard Kalemani. 

Dkt Kalemani alisema kuwa,  kwa ujumla, mradi ulishaanza kutekelezwa kwa kufanyika kazi za awali ikiwemo tathmini ya mazingira  ambayo kwa upande wa Tanzania imekamilika na upatikanaji wa eneo kutapojengwa matenki matano yatakayohifadhi mafuta lita laki tano kila moja  mkoani Tanga ambapo taratibu za ujenzi zinaendelea.

 Aliongeza kuwa, mradi huo unatekelezwa hatua kwa hatua hivyo kuna kazi zinazoendelea kufanyika wakati  majadiliano yakiendelea ikiwemo kazi za utafiti wa kijiokemia, kijiolojia na kijiotekniko na kuna kazi zitakazofuata baada ya majadiliano kukamilika.

Vilevile alisema kuwa, mara baada ya kumalizika kwa majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Uganda, hatua itakayofuata ni majadiliano ya kimkataba kati ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji wa mradi ambao ni kampuni ya Total E&P  ya Ufaransa, Tullow Oil ya Uingereza na CNOOC ya China na pia  Serikali ya Uganda itafanya  majadiliano husika na wawekezaji hao.

Akizungumzia kikao hicho cha Mawaziri, Dkt Kalemani alisema kuwa, mara baada ya kusainiwa kwa mkataba wa mradi huo mwaka 2017, kulikuwa na masuala mengi ya kujadili lakini katika vikao mbalimbali vya ngazi ya Mawaziri, wameendelea kukubaliana katika masuala mengi yatakayowezesha mradi kusonga mbele.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Irene Muloni alisema kuwa  mazungumzo kati ya pande hizo mbili yamefanyika vizuri na yale waliyokubaliana, kila pande unaenda kuyawasilisha katika uongozi wa juu wa nchi kabla ya kuendelea na hatua nyingine za majadiliano.

“Kwa ujumla kuna majadiliano mbalimbali yaliyo mbele yetu ikiwemo majadiliano kuhusu ubia wa kampuni (shareholding agreement) ambayo tunatarajia yakamilike mwezi Juni ili kuweza kuanza ujenzi wa mradi,” alisema Muloni.

Vilevile alisema kuwa, Timu za Majadiliano ya Kitaifa kutoka Uganda na Tanzania (GNT) bado zina kazi kubwa ya kufanya na wanaamini kuwa wataendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Uganda na Tanzania wanafurahia mradi huo muhimu.

Mawaziri kutoka Tanzania waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi,  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati), Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Irene Muloni (kulia) na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi (kushoto) wakiwa katika kikao cha majumuisho cha Mawaziri wanaohusika na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania kilichofanyika jijini Kampala-Uganda.
 Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali nchini Tanzania wakifuatilia kikao cha majumuisho cha Mawaziri wanaohusika na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania kilichofanyika jijini Kampala-Uganda. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.
 Watendaji mbalimbali kutoka nchini Tanzania wakiwa katika kikao cha majumuisho cha Mawaziri wanaohusika na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania kilichofanyika jijini Kampala-Uganda.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba  na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Nzinyagwa Mchany wakifuatilia kikao cha majumuisho cha Mawaziri wanaohusika na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania kilichofanyika jijini Kampala-Uganda.

UTUNZAJI MAJALADA YA ARDHI CHAMWINO WAMVURUGA NAIBU WAZIRI MABULA

$
0
0
Na Munir Shemweta, DODOMA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekasirishwa na jinsi halmashauri ya wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma inavyotunza majalada ya Ardhi katika halmashauri hiyo.

Dkt Mabula alikutana na kadhia hiyo mwishoni mwa wiki alipotembelea masijala ya ardhi katika halmashauri hiyo akiwa katika mfululizo wa ziara zake kutembelea halmashauri mbalimbali nchini kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.

Dkt Mabula alisema, utunzaji wa majalada ya ardhi katika halmashauri ya Chamwino hauzingatii taratibu za kutunza majalada jambo linaloweza kutoa nafasi kwa baadhi ya nyaraka kupotea na wakati mwingine watumishi wasiokuwa waaminifu kuyahujumu

Wakati wa ukaguzi wa majalada ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Chamwino Dkt Mabula alibaini majalada mengi yakiwa hayana maelekezo kutoka kwa afisa mmoja kwenda kwa mwingine jambo linaloonesha kuwa utendaji kazi katika sekta hiyo hauna maelekezo yoyote.

‘’mawasiliano ya ofisi lazima yaonekane kutoka kwa ofisa mmoja kwenda kwa mwingine na hapa kuna index namba lakini haitumiki na huwezi kujua aliyepokea nyaraka kwa mara ya kwanza nani hapo lazima migogoro isiishe.’’ Alisema Mabuila.

Dkt Mabula alisema, utunzaji majalada ya ardhi usiozingatia taratibu kwa kiasi kikubwa ndiyo chanzo cha migogoro mingi ya ardhi katika maeneo mbalimbali kwa kuwa ni rahisi kucheza na majalada kwa nia ya kufanya udanganyifu.

Naibu waziri wa Ardhi alitoa maagizo kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi Christopher Sanga na Afisa Ardhi Mteule wa halmashauri hiyo ambaye anahudumu pia wilaya ya Kongwa Letare Shoo kuhakikisha upungufu uliopo katika majalada ya ardhi yanarekebishwa kabla mwezi machi mwaka huu na ukifika muda huo atarajea kuona kama maagizo yake yametekelezwa.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameagiza kufikia machi mwaka huu 2019 viwanja vyote vya halmashauri ya Chamwino viwe vimepimwa na kupatiwa hati na Mkurugenzi wake ahakikishe halmashauri inalipa kodi ya pango la ardhi kwa viwanja inavyomiliki.

Pia ameitaka halmashauri ya Chamwino kuhakikisha wadaiwa wote wa kodi ya pango la ardhi wanapelekewa ilani za madai na watakaoshindwa kutii wafikishwe kwenye mabaraza ya ardhi na kusisitiza kuwa suala hilo halitakiwi kufanywa kisiasa ili kuja na matokeo chanya.

Katika hatua nyingine Dkt Mabula aliitaka idara ya ardhi katika halmashauri wilaya ya Chamwino kuhakikisha hakuna mmiliki wa kiwanja anayejenga katika halmashauri hiyo bila kuwa na kibali cha ujenzi ili kuepuka ujenzi holela.

Naibu Waziri Mabula alisema anataka halmashauri ya Chamwino kuwa na mji uliopangika na mfano kwa halmashauri nyingine na kusisitiza anachotaka ni wengine kujifunza kwenye halmashauri hiyo hasa ikizingatiwa Ikulu iko Chamwino.

Katika kutekeleza hilo amewataka watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo kuwa na maadili katika kazi zao ili kuepuka utoaji kiwanja kimoja kwa zaidi ya mtu mmoja jambo linalotokea kwa baadhi ya halmashauri na kuleta migogoro.
 Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiangalia moja ya majalada ya ardhi aliyokagua katika halmashauri ya wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wakati wa uhamasishaji ulipaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi, kushoto kwa waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamuga na kulia ni Afisa Ardhi Mteule Letare Shoo.
 Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma (hawapo pichani) Mwishoni mwa wiki wakati akihamasisha ulipaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
 Watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wakimsikiliza Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula mwishoni mwa wiki wakati akihamasisha ulipaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
 Mkuu wa wilaya ya Chamwinop mkoa wa Dodoma Vumilia Nyamuga akizungumza wakati Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula alipofanya ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika wilaya hiyo mwishoni mwa wiki.
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akioneshwa sehemu ndani ya jengo jipya la halmashauri ya wilaya ya Chamwino na Mkuu wa Idara ya ardhi Christopher Sanga alipowasili kukagua ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamuga.

GARI INAUZWA.

$
0
0
 Make : Toyota Allion
Mileage : 58,800Km
Condition : Good condition,Original Seats ,Ac,New Tyres.
Price : 9.5M
Location : Makumbusho
Engine : CC1790
Contacts : 076 61 12445
 






Wawekezaji kutoka Austria wavutiwa na mazingira ya uwekezaji nchini

$
0
0
Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Austria wenye makazi yake Nairobi, Kenya. Bw. Kurt Muellauer akifungua Kongamano la Biashara lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na Wenyeviwanda Tanzania (TCCIA) na Ubalozi wa Austria. Kongamano hilo nimwendelezo wa jitihada za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambao unawakilisha pia nchini Austria na wadau mbalimbali katika kutekeleza diplomasia ya uchumi. Pamoja na mambo mengine kampuni 8 kati 16 zinatarajiwa kufanya ziara jijini Dodoma tarehe 29 Januari kwa lengo la kukutana na Mawaziri wa Kilimo; Nishati; Fedha na Mipango; Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto na Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Kongamano hilo limefanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. 
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa TIC, Bw. John Mnali, pamoja na wadau wengine wakimsikiliza kwa makini Bw.Muellauer (hayupo pichani). 
Baadhi ya wawekezaji kutoka Austria nao wakifuatilia kongamano hilo. 
Kaimu Rais wa Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na Wenyeviwanda Tanzania (TCCIA), Bw. Octavian Mshiu, akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo, ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji nchini na kuunga mkono Sera ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ya Uchumi wa Viwanda nchini. 
Juu na chini wadau wakiendelea kufuatilia mada mbalimbali wakati wa kongamano
Afisa wa Uhamasishaji Uwekezaji (TIC), Bi. Diana Ladislaus akizungumzia fursa za uwekezaji nchini wakati wa kongamano hilo. 
Kongamano likiendelea. 
Tunataka tushirikiane ili tuweze kuwekeza nchini Tanzania 
Majadiliano yanayoonesha dalili ya kuzaa matunda ya ushirikiano kati ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Austria 

RATIBA YA MATUKIO KATIKA WIKI YA SHERIA NCHINI JANUARI 31-FEB 06,2019

Balozi Seif azindua mradi wa maji safi na Salama Shule ya msingi Mangapwani

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameonya kwamba Serikali haitosita kumuwajibisha na hata kumpelekea Mahakamani Mtendaji ye yote wa Halmashauri ya Wilaya atakayebainika kuhusika na ubabaishaji wa matumizi ya Fedha za Mfuko wa Jimbo zinazotengwa kwa ajili ya kuendeleza Miradi ya Wananchi.

Alisema zipo hitilafu zinazojitokeza kuzorotesha uendelezaji wa Miradi ya Wananchi Majimboni ambazo husababishwa na baadhi ya Watendaji wa Halmashauri za Wilaya zikionyesha kuzunguukwa na mazingira ya utapeli hasa katika matumizi ya Fedha.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati alipozindua Rasmi Mradi wa Maji safi na salama katika Skuli ya Msingi Mangapwani ambao pia utasaidia kusambaza huduma hiyo katika vijiji jirani vinavyoizunguuka Skuli hiyo.

Alisema wapo baadhi ya Watendaji ndani ya Halmashauri za Wilaya wakionyesha udhaifu wa kuzorotesha Miradi ya Wananchi waliyoianzisha ilhali fedha zinazotengwa kuitekeleza Miradi hiyo huwa tayari zimeshaidhinishwa na kutiwa saini na Viongozi wanaouhusika.

Balozi Seif alisema kuanzia sasa atalazimika kufuatilia changamoto zote anazowasilishiwa zinazohusiana na kadhia hiyo na hatosita kumchukulia hatua za kinidhamu mtendaji atakayebainika kuhusika na hadaa yoyote hasa ile inayohusiana na masuala ya Fedha.

Aliwataka Wananchi wa Mangapwani kutoa taarifa mapema pale yanapojitokeza matatizo ya kiufundi katika uendeshaji wa Mradi huo wa Maji safi na salama na kuacha tabia ya kuwatumia Mafundi wa vichochoroni wanaoweza kuleta athari zaidi ya kiufundi kwenye mradi huo muhimu kwa ustawi wa Jamii.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza na kuwashukuru Wananchi wa Vijiji vya Mangapwani, Kiomba Mvua, Vuga Mkadini na Matetema kwa jitihada zao za kujisogezea huduma mbali mbali za Kijamii na Maendeleo kwenye maeneo yao.

Katika ziara hiyo Balozi Seif akiwa pia Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alipata wasaa wa kukagua Mradi wa Kisima cha Maji safi kilichochimbwa kupitia Fedha za Mfuko wa Mbunge hapo Mangapwani, Jengo linalotarajiwa kuwa Skuli ya Msingi la Kiomba Mvua, Jengo la Skuli ya Msingi Vuga Mkadini pamoja na Mradi wa Umeme uliopo katika Kijiji cha Matetema.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua Rasmi Mradi wa Huduma ya Maji safi na salama uliopo Skuli ya Msingi Mangapwani utaosambaza pia katika Vijiji Jirani vinavyoizunguuka Skuli hiyo.
 Balozi Seif akitoa onyo kwa Mtendaji ye yote wa Halmashauri ya Wilaya atakayebainika kuzorotesha uendelezaji wa Miradi ya Wananchi ndani ya Majimbo.
 Balozi Seif  akikemea ucheleweshwaji wa Mradi wa Maji safi katika Kijiji cha Mangapwani uliofanywa na Mhandisi wa Mradi huo unaotekelezwa kupitia Fedha za Mfuko wa Mbunge wa Jimbo la Mahonda.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balaozi Seif akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Skuli ya Msingi ya Kiomba Mvua unafanywa na Wananchi wenyewe. Picha na – OMPR – ZNZ.

MAHAKAMA YAITAKA UPANDE WA MASHTAKA KESI YA WEMA SEPETU UNAKAMILIKA KWA WAKATI

$
0
0
Na Karama Kenyunko globu ya Jamii. 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha kuwa upelelezi katika kesi inayomkabili msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu, unakamilika kwa wakati, ili kesi iweze kuendelea.

Uamuzi huo umetolewa leo, Januari 28, 2019 na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa na upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

"Nataka upande wa mashtaka mkamilishe kwa wakati upelelezi ili kesi iweze kuendelea, kwa sababu ni kesi ya muda mrefu tangu ilipofunguliwa Mahakamani hapa Novemba mwaka jana na mpaka sasa upelelezi bado, ?" Alihoji.

Hakimu Kasonde ameaihirisha kesi hiyo hadi Februari 13, 2019 kesi hiyo itakapotajwa na kuwataka upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha upelelezi wao kwa wakati.

Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006. alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Novemba Mosi, 2018, kujibu shtaka hilo la kuchapisha video ya ngono na kuisambaza kwenye mtandao ya kijamii. 

Katika kesi ya msingi, Wema anadaiwa kuwa Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kusambaza  katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha kamati ya uongozi cha kujadili ratiba za shughuli za Bunge katika Mkutano wa kumi na nne (14) kilichofanyika leo tarehe 28 Januari, 2019 katika ofisi ya Bunge jijini Dodoma, ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa kumi na nne (14) wa Bunge la 11 unaotegemewa kuanza kesho tarehe 29 Januari, 2019 Bungeni Jijini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akizungumza  na wajumbe wa kamati ya uongozi wakati wa kikao cha kujadili ratiba za shughuli za Bunge katika Mkutano wa kumi na nne (14) kilichofanyika leo tarehe 28 Januari, 2019 katika ofisi ya Bunge jijini Dodoma. Ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa kumi na nne (14) wa Bunge la 11 unaotegemewa kuanza kesho tarehe 29 Januari, 2019 Bungeni Jijini Dodoma.

Wajumbe kamati ya uongozi wakiwa kwenye kikao cha kujadili ratiba za shughuli za Bunge katika Mkutano wa kumi na nne (14) kilichofanyika leo tarehe 28 Januari, 2019 katika ofisi ya Bunge jijini Dodoma,  ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa kumi na nne (14) wa Bunge la 11 unaotegemewa kuanza kesho tarehe 29 Januari, 2019 Bungeni Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MATUKIO YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wabunge wa Viti Maalum, Amina Makilagi (katikati) na Fatma Toufiq kwenye viwanja vya Bunge jijjini Dodoma  Januari 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Longido Dkt. Stephen Kiruswa, nje ya jengo la utawata Bungeni jijjini Dodoma  Januari 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YAWEKA MIPANGO MADHUBUTI YA KUBORESHA HUDUMA NA MAZINGIRA KWA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0

Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mh Rais Dr.John Pombe Magufuli imeweka mipango madhubuti ya kuboresha huduma na mazingira katika makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu likiwemo kubwa la uwezeshwaji kiuchumi kupitia asilimia 2% ya mapato ya ndani ya Halmashauri na Manispaa nchini.

Hayo yamesemwa jana katika Hotel ya Hyatt Regency na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde kwa niaba ya Mh Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya HAJI MANARA FOUNDATION* ambapo Mavunde alitumia nafasi hiyo kuelezea mipango Serikali katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata fursa sawa katika masuala ya siasa,kijamii na ushiriki katika ustawi na ujenzi wa Taifa Tanzania.

Mavunde alichukua fursa hiyo kumpongeza sana Mwanzilishi wa Taasisi hiyo Ndg Haji Manara kwa uamuzi na utayari kusaidia watu wenye mahitaji na kuahidi kwamba Serikali itatoa kila ushirikiano kwa Taasisi hiyo katika kutimiza majukumu yake hasa katika kutoa elimu kwa jamii juu ya nafasi ya watu wenye ulemavu katika Jamii.

Akizungumza katika hafla hiyo,Ndg Haji Manara ambaye pia jana alizindua perfume yake iendayo kwa jina la De La Boss,amesema Taasisi hiyo ni itasaidia kuwajengea uwezo watu wenye Ualbino pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuepukana na dhana potofu juu ya watu wenye ualbino,ambapo pia alibainisha kwamba

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh Paul Makonda ametumia nafasi hiyo kumpongeza Haji Manara kwa ubunifu mkubwa na kuitaka jamii kuwaunga mkono watu wanaoleta mabadiliko na fikra mpya na sio kuwavunja moyo kwa majungu na maneno yasiyofaa.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde kwa niaba ya Mh Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa Majaliwa akimpongeza Haji Manara kwa kuzindua taasisi yake ya HAJI MANARA FOUNDATION pamoja manukato 'perfume' yake iliojulikana kwa jina  la De La Boss
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde kwa niaba ya Mh Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza jamo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi wa taasisi ya HAJI MANARA FOUNDATION pamoja manukato 'perfume' yake iliojulikana kwa jina la De La Boss,iliofanyika jana jijini Dar
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde kwa niaba ya Mh Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa akiizindua manukato 'perfume' ya De La Boss mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika ukumbini humo kushuhudia tukio hilo lililofanyika jana jijini Dar.
Sehemu ya Meza kuu ikifurahia jambo
Msanii nyota wa Bongofleva almaarufu Diamond Platnumz akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa taasisi ya HAJI MANARA FOUNDATION pamoja manukato 'perfume' yake iliojulikana kwa jina la De La Boss,ambapoo viongozi mbalimbali wa serikali na wadau walihuduhuria tukio hilo adhimu kabisa.
Haji Manara akilishwa keki wakati wa uzinduzi wa taasisi ya HAJI MANARA FOUNDATION pamoja manukato 'perfume' yake iliojulikana kwa jina la la De La Boss,ambapoo viongozi mbalimbali wa serikali na wadau walihuduhuria tukio hilo adhimu kabisa.

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI AKUTANA NA WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, George Kakunda (kulia) akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi.Sarah Cooke,alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, George Kakunda (kulia) akimkaribisha mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke,alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Uingereza.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, George Kakunda (wapili kulia) aikiwa katika picha ya pamoja na wageni.

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images