Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live

Wasanii waagizwa kuwasilisha Mkataba na kampuni za simu

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewaagiza wasanii walioingia mikataba na kampuni za simu au mawakala kwa ajili ya kutumia kazi zao kama miito ya simu lakini hawajalipwa stahiki zao, wawasilishe katika ofisi hizo kwa ajili ya kupatiwa haki zao kuanzia 2016 hadi 2018

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, ameyasema hayo kumaliza kikao na wasanii na mawakala waliokuwa wakijadili kuhusu kutokuwapo na mgawanyo sawa wa malipo ya miito ya simu baina ya wasanii wa muziki, kampuni za simu na mawakala wanaouza kazi za wasanii na kufanya wasanii hao kupoteza haki zao.

Katika kikao hicho, walikubaliana malipo kuwa kwa kipindi cha miezi sita ya kutafuta suluhu ya kudumu, malipo ya kazi za wasanii, mawakala, kampuni za simu na mtoa huduma yawe 50 kwa 50 kabla ya kuja na mfumo rasmi.

“TCRA tumekutana na wadau wote ili kupata muafaka na hatimaye pasiwepo na malalamiko tena kutoka upande wowote na tukakubaliana kuwa kampuni za simu ziwasiliane na wasanii moja kwa moja badala ya kuishia kwa mawakala,” amesema.

Amesema wamekubaliana kuwa upo uwezekano wa msanii kusaini makubaliano ya kutumiwa kwa kazi zake kama miito ya simu kwenye kampuni husika ya simu moja kwa moja na endapo atataka kutumia wakala afanye hivyo.

Pia walikubaliana kuwa kampuni za simu ziwasilishe TCRA mgawanyo halisi wa gharama za utayarishaji wa kazi hizo za wasanii ambazo hutumika kama miito ya simu.

Mhandisi Kilaba, amesema azimio lingine ni TCRA kuangalia uhalisia wa mikataba inayoingiwa baina ya kampuni za simu na mawakala au wasanii kuona kama ni rafiki katika mazingira ya biashara ya miito ya simu kuangalia unufaika kwa wasanii.

Kilaba amesema June mwaka huu, tutakuwa tumeshaangalia namna ya gharama watakazokuwa wanalipana kati ya kampuni za simu, mawakala na wasanii.

Aidha amesema mwaka jana walikuwa na kikao kwa ajili ya kujadili wanafanya nini na walikutana na mitandao yote ya simu. Lengo kufahamu nini kinaendelea katika kazi za wasanii wanazozitumia.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi mwafaka waliyofikia katika mapato yatokanayo na miito ya simu kwa miziki ya wasanii.
 Wadau wa muziki wa wakijadili mwafaka wa mgawanyo wa mapato yatokanayo na miito ya simu.
 Msanii Abdul Nasibu (Diamond Platinum) akichangia Mada ya mapato yatokanayo na miito ya simu katika mkutano ulioitishwa na TCRA.
 Mkutano kati ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA)   na Wadau wa muziki wakiwa katika mkutano wa kujadili kufikia mwafaka wa mgawanyo wa mapato yatokanayo na miito ya simu.
Wadau wa muziki wakijadili mwafaka wa mgawanyo wa mapato yatokanayo na miito ya simu.

INTRODUCING: SALAMA - Vitali Maembe

MHANDISI WA WILAYA NA MKANDARASI WALIOMDANGANYA NAIBU WAZIRI WA MAJI ,JUMA AWESO WATUPWA MAHABUSU .

$
0
0
Askari Polisi akiwa amewashikilia ,Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Monduli,Charles Saidea (kulia) na Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions mara baada ya Naibu Waziri kuamuru wakamatwe kutokana na kubainika kufanya udanganyifu katika mradi huo. 
Mhadisi wa Maji wa wilaya ya Monduli,Charles Saidea akiingia kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli. 

Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions akiingia kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli. 

Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions pamoja na Mhandis wa Maji wa wilaya ya Monduli ,Charles Saidea wakiwa kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli. 
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliji,Juma Aweso akitizama namna mafundi wakiunganisha Bomba za Maji katika mradi unaopeleka maji katika Kata ya Sopeko kikiwemo kijiji cha Lendikinya wilayani Monduli katika mkoa wa Arusha.
 Mafundi wakiendelea na uunganishaji wa Bomba za kupeleka Maji katika kijiji cha Lendikinya wilayani Monduli mkoa wa Arusha. 
 Mhadisi wa Maji wa wilaya ya Monduli Charles Seidea akimueleza Naibu Waziri wa Maji ,Juma Aweso kuhusu namna mradi huo ulivyotekelezwa katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli. 

 Baadhi ya Wananchi katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Juma Aweso (hayupo pichani) alipotembelea mradi huo kujionea maendeleo yake. 

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Monduli ,Julius Kalanga pamoja na wananchi wakienda kujionea namna mkandarasi alivyopitisha Bomba za Plastiki kwenye Korongo badala ya Bomba za Chuma. 


 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso akitizama Bomba za Plastiki zilizopitishwa katika Makorongo badala ya Bomba za Chuma katika mradi wa maji wa kusaidia vijiji 10 vya kata ya Sopeko wilayani Monduli. 

 Baadhi ya Bomba za Plastiki zikiwa zimepita kwenye Korongo badala ya Bmba za Chuma . 
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Lendenyika wakishuhudia wakati watalaamu hao wakichukuliwa katika gari la Polisi.




Anaandika Dixon Busagaga,Monduli.

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso ameamuru kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Monduli ,Charles Saidea na Mkandarasi kutoka kampuni ya Meru Constructions ,Ayo Jeremia kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika miradi wa maji inayoendelea katika vijiji 10 vya Halmashauri ya wilaya ya Monduli .

Waziri Aweso ametoa agizo hilo katika kijiji cha Lendinyika wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Monduli kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maji katika vijiji 10 vya Halmashauri hiyo,ziara ambayo hata hivyo alilazimika kuikatisha mara baada ya kubaini kuwepo kwa taarifa zinazo kinzana na taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji wenye thamani ya Sh Bil 1 na Mil 79 .

Mbali na uwepo wa dosari nyingi za kiufundi ,mradi huo unaotajwa kukamilika kwa asilimia 85 bado haujaanza kutoa maji huku Mkandarasi akieleza kuidai Serikali sehemu ya fedha za mradi hu jambo ambalo Mhandisi alionekana kupinga uwepo wa madai hayo.

Hoja ya kuwepo kwa Mabomba ya plastiki yaliyopita katika Makorongo iliibuliwa na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Lendikinya Lemta Naisikie baada ya kutaka kujua kama ni sahihi kwa mkandarasi kupitisha Bomba hizo katika sehemu za wazi badala ya bomba za chuma.

“Swali langu ni moja ,Bomba zilizotandazwa kuleta maji katika kisima kuu ,kuna sehem za Makorongo zote zimewekwa hii bomba la mpira ,hii naona ni changamoto afadhali ingewekwa bomba la chuma na maeneo mengine kuna mawe tungeomba mkandarasi atandaze bomba la chuma ili zisilete athari baadae”alisema Naisikie.

Baada ya kutolewa kwa hoja hiyo Naibu Waziri ,Aweso aliamua kutembelea baadhi ya Makorongo na kujionea Bomba la Plastiki likiwa limepita juu badala ya Bomba la Chuma ndipo akaamua kutoa maelekezo .

“Viongozi wenu wote wanazungumzia swala la maji ,Lendikinya ni moja ya vijiji vyenye changamoto kubwa sana ya maji ,Mbunge wenu amepiga sana kelele kuhusu maji kwa wananchi wa Monduli,sasa sisi leo tumekuja hapa tumeona kuna mradi wa zaidi ya sh Bil 1 na Mil 79 lakini mradi uko zaidi ya asilimia 80 lakini maji kwa wananchi hakuna .”alisema Aweso 

“Unawauliza wataalamu wetu wakupe taarifa zile sahihi ,hawakupi ,leo mwananchi huyu wa kawaida kabisa anakupa taarifa sahihi mahala ambapo yalitakiwa kuwekwa mabomba ya chuma yameweka mabomba ya plastiki na hakuna usimamizi wa iana yoyote .”aliongeza Aweso.

INTRODUCING: Official Video: ANITHA CHA WOTE - NA WEWE

TAASISI YA DORIS MOLLEL YAENDESHA MAFUNZO YA 'KANGAROO' KWA WAUGUZI NCHINI

$
0
0
 Baadhi ya Wauguzi kutoka hospital mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa warsha ya kuelimishana namna ya kuwasaidia wakina mama wanaojifungua watoto kabla ya wakati (Watoto Njiti) hasa katika kipindi cha kumuwezesha mtoto kupata joto lake (Kangaroo), iliyofanyika hivi karibuni jijiji Dar es salaam. Warsha hiyo ilioendeshwa na Taasisi ya Doris Mollel iliyojikitaka katika kusaidia wakinamama na watoto njiti nchini. 
Muuguzi Selina Pemba kutoka Mkoani Shinyanga akitoa somo kwa Wauguzi wenzake namna wanavyotakiwa kuwaelekeza wazazi ubebaji wa mtoto akiwa mdogo, wakati wa warsha ya kuelimishana namna ya kuwasaidia wakina mama wanaojifungua watoto kabla ya wakati (Watoto Njiti) hasa katika kipindi cha kumuwezesha mtoto kupata joto lake (Kangaroo), iliyofanyika hivi karibuni jijiji Dar es salaam.
 Muuguzi Bridgiter Cheyo kutoka Mkoani Pwani, akionyesha namna ya kumfunga Mama anayekuwa amemuweka Mtoto kifuani wakati wa Kangaroo. 
 Muuguzi Cleopatra Mtei kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye ndiye aliyekuwa akiongoza Mafunzo hayo, akizungumza jambo wakati wa warsha ya kuelimishana namna ya kuwasaidia wakina mama wanaojifungua watoto kabla ya wakati (Watoto Njiti) hasa katika kipindi cha kumuwezesha mtoto kupata joto lake (Kangaroo), iliyofanyika hivi karibuni jijiji Dar es salaam.

WANAFUNZI WOTE TUSIIME WALIOFANYA MTIHANI KIDATO CHA NNE MWAKA JANA WAFAULU MTIHANI ,KUENDELEA KIDATO CHA TANO

$
0
0
Na Ripota Wetu

WANAFUNZI wote 272 wa Shule ya Sekondari ya Tusiime ya Tabata Dar es Salaam, waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana wamefaulu kwenda kidato cha tano huku 204 kati yao wakipata daraja la kwanza na la pili.

Kwa mujibu wamatokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), wanafunzi 86 wa shule hiyo wamepata daraja la kwanza na 118 daraja la pili.

Matokeo hayo yanaonyesha kuwa wanafunzi wengine 60 wamepata daraja la tatu na wanafuni nane daraja la nne lakini wote wamefanikiwa kupata alama za kuendelea na kidato cha tano.

Mkuu wa Taaluma shuleni hapo, John Kishefu alisema matokeo hayo ni mazuri sana hasa ikizingatiwa idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa nao ambayo ni kubwa kuliko shule nyingi zilizofanya mtihani huo.

Kishefu alisema miaka yote Tusiime huwa haichagui wanafunzi wa vipaji maalum kama zinavyofanyaa baadhi ya shule bali huchukua wa aina zote hata wale wenye uwezo mkubwa na mdogo darasani na kuwaandaa vizuri.

“Sisi hatuchagui mwanafunzi, unaweza kukuta amekuja hapa akiwa na uwezo mdogo sana lakini timu mahiri ya walimu waliopo hapa wanamtengeneza hadi anapata daraja la kwanza au la pili hilo nji jambo la kawaida hapa Tusiime,” alisema Kishefu

Kishefu alisema matokeo hayo mazuri ni mwendelezo ya matokeo kama hayo kwa shule za Tusiime kuanzia shule ya msingi na kidato cha pili ambapo wamekuwa wakifaulisha kwa alama za juu.

“Matokeo haya yamewafurahisha hata wazazi wengi ambao wamekuwa wakitupigia simu na kutupongeza. Tulikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi lakini tumemudu kuwapeleka kidato cha tano wote hii si kazi rahisi,” alisema Kishefu

“Wanafunzi wetu wengi wamepata alama A za kutosha sana kwenye masomo mbalimbali na siku ya leo (jana) simu zetu zilikuwa busy wazazi wanapiga kuelezea namna walivyofurahishwa na matokeo haya,” alisema Kishefu

Akizungumzia matokeo hayo, Mkurugenzi wa shule hizo, Albert Katagira, alisema matokeo hayo mazuri yanatokana na dhamira waliyonayo kama taasisi kuhakikisha vijana wa Tanzania wanapata elimu bora katika mazingira yaliyo safi na salama.

“Napenda kuwathibitishia wadau wote wa elimu kuwa shule za Tusiime zimejipanga kuendelea kutoa elimu bora hapa nchini na hivyo tumewekeza vya kutosha katika miundombinu, zana za kufundishia, motisha kwa wafanyakazi na ushirikiano mzuri baina yetu, serikali na wazazi, haya yote kwa pamoja ndiyo yametufikisha kwenye matokeo haya,” alisema

Alisema shule hizo zimejipanga kuendelea kufanya vizuri kwa kuimarisha mifumo ya utoaji wa elimu na huduma katika shule hizo ili kuwajengea watoto uwezo na kuwapa maarifa stahiki na aliwataka wazazi waendelee kuwaamini na kuwapa ushirikiano katika azma yao hiyo ya kutoa elimu bora kwa vijana.

SBL yazindua kampeni ya ‘Usitumie Kilevi na Kuendesha Chombo cha Moto’ jijini Mwanza

$
0
0



Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha,kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha na kulia ni Mrakibu wa Polisi Mwandamizi Audax Majaliwa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha(kushoto) akimshukuru Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam alipozindua mafunzo kwa wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha. 


Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha, akiwasilisha mada ya kuepuka kunywa na kuendesha kwa wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.
Wadau wa usafiri jijini Mwanza wakifuatilia mada wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha inayofanywa na kampuni ya Bia ya Serengeti.


Mwanza, Januari 25, 2019-Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kampeni inayolenga kutoa elimu kwa umma juu ya unywaji wa kistaarabu, ikiwa ni moja ya hatua muhimu inayochukuliwa na kampuni hiyo kuzuia ajali nyingi zinazosababishwa na madereva wanaoendesha wakiwa wametumia vilevi

Kampeni hiyo inayobeba ujumbe wa, “Usitumie Kilevi na Kuendesha Chombo cha Moto’ imezinduliwa jijini Mwanza leo na ilianza na kongamano lililojadili unywaji wa kistaarabu ambalo liliwaleta pamoja wadau kama vile Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, Mamlakka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), madereva, abiria, na wadau wengine katika sekta ya usafirishaji

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika hoteli ya Gold Crest, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) mkoani Mwanza Mkaddam Hamis Mkaddam, alisema kwa kulishirikisha jeshi la Polisi kampuni ya SBL imeiunga mkono serikali katika kuelimisha umma juu ya unywaji wa kistaarabu na kusisitiza umuhimu wa kutatua tatizo hilo.

Mkaddam alisema baadhi ya watu na haswa madereva hunywa kiasi kikubwa cha pombe pasipo kujali madhara yanayoweza kusababishwa na kitendo hicho na kuonya kuwa vitendo vya aina hiyo vinaweza kusababisha ajali mbaya.

“Sote tunafahamu kuwa matumizi ya vileo yana uhusiano mkubwa na uendeshaji mmbovu ambao unaweza husababisha ajali mbaya za barabarani zenye athari kubwa kwa jamii zetu. Athari zake siyo tu zinawagusa watumiaji wa vilevi bali hata maisha ya wengine na kusababisha upotevu wa maisha na ulemavu kwa watu ambao wangeweza kuchangia uchumi wa nchi,” alisema Mkaddam.

Alisema pamoja na kusababisha vifo visivyotarajiwa na majeraha, unywaji usiokuwa wa kistaarabu una maadhara makubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwa kiasi kikubwa cha fedha kinatumika kwa ajili ya huduma, madawa na vifaa tiba kwa waathirika wa ajali za barabarani na hivyo kuwa ni mzigo kwa Serikali.

“Ajali hizi pia ni mzigo kwa vyombo vyetu vya utekelezaji wa sheria kwa kuwa maofisa wanalazimika kuzishughulikia wakati zinaweza kuzuilika ambazo zinasabishwa na madereva wanaondesha wakiwa wametumia vilevi,” Mkaddam aliongeza.

Akizungumzia namna kampeni hiyo itaisadia jamii, mkuu huyo wa usalama barabarani alisema, “sote kwa pamoja ikiwamo sisi polisi, madereva, jamii na wadau wengine tuna jumuku la kutafuta suluhisho la kumaliza tatizo la kutumia vilevi na kuendesha vyombo vya moto. Ninayo furaha kuona SBL pamoja na kwamba biashara yao ni kuuza vilevi, wameona wanawajibu wa kuhimiza unywaji wa kistarabu”.

Kampeni hii inalenga kuwafikia vijana na watu wengine na kuwaeliisha juu ya madhara ya unywaji usiokuwa wa kistaarabu huku ikiwataka kubadili tabia kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL John Wanyancha alisema kampeni ya unywaji wea kistaarabu inalenga kuielimisha jamii kuwa wanywaji wanapaswa kunywa kwa kiasi na kuhakikisha unywaji wao hauna madhara kwao na kwa watu wanaowazunguka.

“SBL imedhamiria kuungana na serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa jamii na haswa madereva ambao wanakunywa na kuendesha vyombo vya moto wanaelimishwa juu ya madhara ya vitendo hivyo na kutakiwa kubadilisha tabia,” alisema Wanyancha. 

WAZIRI UMMY MWALIMU AKUTANA NA MKURUGENZI WA UN WOMEN KANDA YA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA

$
0
0
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekutana na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) kwa lengo la kumpa taarifa ya Mkutano wa 63 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake duniani utakaofanyika Mjini New York Mwezi Machi Mwaka huu.

Aidha Waziri Afya pamoja na Kiongozi huyo walifanya mazungumzo na kubadilishana mawazo kuhusu maeneo ambayo shirika la UN Women linayafanyia kazi kwa kushirikiana na serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Katika kikao cha muda mfupi ofisni kwa Waziri Ummy kiongozi huyo pia alimwalika Waziri Ummy kushiriki katika Mkutano wa Afrika wa kujenga msimamo wa pamoja ambao ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkutano wa 63 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake duniani utakaofanyika Jijini Cairo mwezi Februari mwaka huu.

Bi. Derex-Briggs pia ameitaka Tanzania kuhakikisha inaingiza masuala ya Jinsia katika taarifa yake itakayotoa katika Mkutano wa kimataifa wa Jukwaa la Juu la Kisiasa (High Level Political Forum) utakaofanyika Mwezi Julai ,9-18 Jijini New York Marekani mwaka huu.

Wakati huohuo Waziri Ummy Mwalimu amemwambia Mkurugenzi huyo kuwa Wizara yake imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Shirika la UN Women na kusema vipaumbele vyake kama Waziri mwenye dhamana imekuwa ni kuhakikisha wanawake wote wanapata huduma ya kujifungua salama katika vituo vya Afya.

Aidha Waziri Mwalimu amesema maeneo mengine ya kipaumbele kwasasa ni uwezeshaji wanawake kiuchumi, juhudi za kuhakikisha kunakuwepo uwakilishi wanawake katika maamuzi ya kisiasa unaendelea kufikia 50/50 lakini pia kupunguza mimba na ndoa za utotoni ambazo ni kikwazo kwa wasichana wengi kufikia ndoto zao.

Kuhusu suala la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi Waziri Ummy amesema kuna asilimia 4 ya fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri zimekuwa zikitolewa kwa ajili kuwazesha wanawake kiuchumi lakini kuna idadi dogo ya wanawake wanaojitokeza kuomba mikopo hiyo.

Katika sula la uwezeshaji wa wanawake kisiasa Waziri Ummy bado kuna changamoto ambazo zinahitaji kufanyia kazi ili wanawake waweze kujitokeza kwa wingi kushiriki katika masuala ya kisiasa kwani uwakilishi wanaume bungeni bado ni mkubwa ukilinganisha na wanawake.

Naye mwakilishi wa shirika la UN Women Nchini Tanzania Bi. Hodan Addou amemwahakikishia Waziri Umy kuwa Shirika lake litaendelea kuchangia katika Maendeleo ya Wanawake Nchini kwani mpaka sasa limechangia katika Maeneo yote ya vipaumbelea kwa kushirikiana na Wizara.

Aidha Bi. Derex-Briggs anaitembelea Tanzania kwa ziara ya kikazi tayari ametembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu na amekuwa Jijini Dodoma kutembelea Bunge la Tanzania ambapo amepata fursa ya kuongea na baadhi ya wabunge wanawake na kubadilishana nao mawazo kuhusiana na mstakabali wa masuala ya wanawake.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam wa kwanza kulia ni Bi. Hodan Addou Mwakilishi wa Shirika hilo hapa Nchini.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam wa kwanza kulia ni Bi. Hodan Addou Mwakilishi wa Shirika hilo hapa Nchini. 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiagana na mgeni wake ambaye ni Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake(UN Women) ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.


TANZANIA,BOSNIA NA HERZEGOVINA KUANZISHA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA

$
0
0
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Balozi Modest J. Mero (kulia) na Mwakilishi wa Kudumu wa Bosnia na Herzegovina katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ivica Dronjic wakiweka saini Makubaliano ya kuanzisha Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bosnia na Herzegovina. Makubaliano hayo ambayo yatazingatia Mkataba wa Vienna wa masuala ya mahusiano ya kidiplomasia wa Mwaka 1961 uliwekwa saini New York, Marekani tarehe 25 Januari 2019. 
Afisa wa Ubalozi, Bibi Lilian Mukasa akitoa maelekezo ya namna Waheshimiwa Mabalozi watakavyosaini Makubaliano ya kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi zao. 
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Balozi Modest J. Mero (kulia) na Mwakilishi wa Kudumu wa Bosnia na Herzegovina katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ivica Dronjic wakibadilishana Nyaraka ya Makubaliano baada ya wawili hao kuweka saini. 

DKT KINGWANGALA ATEMBELEA MAONESHO YA UTALII,HISPANIA

$
0
0
Mhe. Kigwangalla kifuatilia maelezo kutoka kwa mdau wa utalii wa Tanzania Bw. Denis Lebouteux alipotembelea banda la Tanzania wakati wa maonesho ya FITUR 2019.
Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii akiongea na wadau wa utalii wakampuni ya Tanganyika Expedition Bw. Oscar Gabaldon (Kushoto) na Denis Lebouteux (katikati) punde alipowasili katika banda la Tanzania.
Waziri Kigwangalla akiwa na wadau wa utalii wa Tanzania.
Wadau wa Utalii akiongea na wadau wa utalii punde alipowasili katika banda la Tanzania.


Na: Augustina Makoye

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla ametembelea banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Feria 

Internacionale de Turismo (FITUR) yanayofanyika Madrid nchini Spain na kuzungumza na wadau wa utalii kutoka Tanzania wanaoshitiki maonesho hayo.

Waziri Kigwangalla amesema kuwa hii ni mara yake ya kwanza kuhudhuria maonesho ya Kimataifa ya utalii na amefurahi sana kukutana na kuongea na washiriki kutoka Tanzania na hivyo kupata uzoefu na kujifunza mambo mengi pamoja na changamoto zilizopo kwa Tanzania kushiriki maonesho ya Kimataifa.

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ndiyo inayoratibu ushiriki wa Tanzania katika maonesho haya ambapo jumla ya makampuni binafsi manne (4) ya watoa huduma za utalii yanashiriki pamoja na Taasisi mbili (2) za serikali ambazo TTB Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Waziri Kigwangala yupo nchini Hispania kuhudhuria kongamano la kumi la uwekezaji katika sekta ya utalii na biashara linalofanyika katika eneo la Feria de Madrid yanapofanyika maonesho ya Fitur 2019.

KIKAO CHA MAWAZIRI WA TANZANIA NA UGANDA WANAOHUSIKA NA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI CHAFANYIKA KAMPALA

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wamefanya kikao kati yao na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali nchini Tanzania walio katika Timu ya Kitaifa ya Majadiliano ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.

Kikao hicho kinachofanyika Kampala – Uganda ni cha maandalizi kabla ya kufanyika kikao na Mawaziri wa Uganda wanaohusika na mradi huo baadaye leo.

Kikao cha Mawaziri wa Tanzania na Uganda wanaohusika na mradi huo kinafanyika kufuatia majadiliano ya wataalam wa nchi hizi mbili yaliyoanza tarehe 21/1/2019 na kufuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zinazosimamia mradi kutoka Tanzania na Uganda kilichofanyika Januari 24/2019 Kutoka kushoto ni Januari Makamba Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, William Lukuvi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Merdad Kalemani Waziri wa Nishati, Profesa Paramagamba Kabudi Waziri wa Sheria na Katiba Mawaziri kutoka Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wanaohudhuria kikao kuhusu maandalizi ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania,ambapo 
majadiliano ya wataalam wa nchi hizi mbili yaliyoanza tarehe 21/1/2019 na kufuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zinazosimamia mradi kutoka Tanzania na Uganda kilichofanyika Januari 24/2019 nchini Uganda. 


Mawaziri kutoka Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Jahuri ya Uganda wakiwa katika mkutano kuhusu maandalizi ya ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania unaofanyika leo nchini Uganda.
Baadhi ya wataalam wakiwa katika mkutano huo.
Makatibu wakuu wa wizara mbalimbali kutoka nchini Tanzania wakihudhuria mkutano huo.
Baadhi ya maofisa kutoka Tanzania wakihudhuria mkutano huo. 

RC MWANRI ATOA ONYO KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA WANAOCHUKUA FEDHA KWA MAMA MJAMZITO

$
0
0
Na Amisa Mussa

MKUU  wa  Mkoa  wa  Tabora  Aggrey Mwanri ameahidi kuwashughulikia wataalam wa afya wanaowatoza fedha  wajawazito wakati kutaka kujifungua.

 Pamoja na mambo mengine amesema kwa sasa wanaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za afya pamoja na kupunguza vifo vya mama na mtoto mkoani humo.

Akizungumza katika kampeni za  Bima ya Afya ya Jamii(CHF) iliyoboreshwa pamoja na Kampeni ya  Jiongeze Tuwavushe salama ,Mwanri ametumia kampeni hizo kuwanyooshea vidole baadhi ya watoa huduma za afya ambao wanawatoza fedha wanawake wajazito wanakwenda kujifungua katika vituo vya afya na zahanati.

Mwanri amesema hatosita kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi wa afya atakayebainika kumtoza fedha mama mjamzito.

Katika hatua nyingine Mwanri ametoa onyo kwa wakurugenzi wa  Halmashauri  za  Wilaya  mkoani humo ambao  wamezembea  kuwasajili  wazee  na  kufungua  madirisha  maalum ya  kuwahudumia  katika hospitali  na zahanati zilizopo kwenye maeneo yao.

Kuhusu uzinduzi  wa  kampeni  hizo  imekwenda  pamoja na  Serikali ya  Mkoa  wa  Tabora  kupokea  magari  madogo  nanne ya kubeba wagonjwa kutoka Shirika  Care  International kupitia  mradi  wa  Tamani yenye  thamani  ya zaidi ya Sh.Milioni 184.

Dkt. Mahiga amwakilisha Rais Dkt Magufuli Jukwaa la Uchumi Duniani

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Kulia) akichangia Mjadala wa Changamoto za Usalama na uhaba wa Chakula Duniani tarehe 24 Januari 2019 Davos, Uswisi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine akizungumza na Rais wa WEF, Mhe. Borge Brende tarehe 25 Januari 2019 Davos, Uswisi
Mhe. Waziri Mahiga akifanya mazungumzo na  Bi. Rachel Samren, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Millicom (Millicom International Cellular S.A) tarehe 25 Januari 2019 Davos, Uswisi.




Tanzania imesisitiza umuhimu wa kukabili uhaba wa chakula kwa kuzalisha mazao kwa kutumia utalaamu wa kisasa kwa kuwpatia wakulima pembejeo na masoko ya uhakika ya chakula cha ziada.


Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) wakati wa kuchangia mjadala unaohusu uhakika wa chakula na changamoto za uhaba wa chakula duniani katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum-WEF) unaofanyika Davos, Uswisi kuanzia tarehe 22 hadi 25 Januari 2019.


Mhe. Mahiga alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika jukwaa hilo ambalo kaulimbiu ya mwaka huu ni Kutengeneza Mazingira ya Utandawazi wa Dunia kwa ajili ya Mapinduzi ya Kisasa ya Nne ya Viwanda “Shaping a Global Architecture in the Age of the Fourth Industrial Revolution”.


Katika mkutano huo, ajenda kuu zilizojadiliwa ni pamoja na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, Agenda ya Afrika ya Maendeleo, Hali ya Ulinzi na Usalama Pembe ya Afrika, changamoto za biashara ya kimataifa, ushirikiano wa Bara la Ulaya na Afrika katika ajenda mpya ya maendeleo.


Tanzania ilialikwa kuchangia mjadala unaohusu uhakika wa chakula na changamoto za uhaba wa chakula duniani pamoja na ajenda ya uwezeshaji wa mawasiliano ya simu za mkononi. Katika ajenda hiyo, Tanzania ilitoa wito wa umuhimu wa teknolojia katika kuboresha utaalamu katika sekta ya kilimo kwa ajili ya kuwawezesha wakulima wadogo waliopo vijijini.


Hili ni Jukwaa la pekee ambalo linakutanisha kwa pamoja Viongozi wa Serikali kutoka mabara yote duniani, Taasisi na Mashirika ya Kimataifa, Viongozi wa Makampuni Makubwa ya Kibiashara kwa ajili ya kujadili maendeleo na mwelekeo wa uchumi duniani.


Kando ya Mkutano huo, Mhe. Dkt. Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa mashirika na makampuni ambayo yapo Tanzania na yanayohitaji kupanua wigo kama vile Tigo na General Electric na makampuni yanayotafuta fursa za kuwekeza Tanzania. Aidha, alikutana na Rais wa WEF, Mhe. Borge Brende ambapo aliahidi kushawishi wawekezaji kuwekeza Tanzania na kuandaa Jukwaa la wawekezaji wa kimataifa la Tanzania ili waweze kuwekeza Tanzania.


Viongozi wengine waliokutana na Waziri Mahiga ni pamoja na; Bw. Scott Strazik, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gesi yenye Makao makuu yake Atlanta, Georgia- Marekani; Bw. Richard Hatchett, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kupambana na magonjwa ya Mlipuko (Coalition for Epidermic Preparedness Innovations); Bi. Rachel Samren, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Millicom ambayo TIGO ni Tawi la Kampuni hiyo, na Bw. Mohamed Al-Beity, Mtanzania aliyetambuliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani kwa mradi wa kutangaza Utalii wa Tanzania kwa njia ya Mtandao (Tanzania Digital Tourism).



Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma

 26 Januari 2019


Mtazamo hasi umefanya wagonjwa wa Ukoma kunyanyapaliwa –Waziri Ummy Mwalimu

$
0
0
 Waziri Ummy Mwalimu baada ya kutoa tamko la maadhimisho ya siku ya ukoma Duniani ambayo itafanyika kesho akiwakabidhi waathirika wa ukoma chakula kwenye makazi yaliyopo Nunge wilayani Kigamboni.Siku ya ukoma Kitaifa itafanyika kesho makazi ya watu waishio na ukoma Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,,Jinsia Wazee na Watoto akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rachel Mhando,Viongozi wa wizara pamoja na wazee hao wakitoa ujumbe wa kuashiria kuondoa unyanyapaa dhidi ya waathirika wa ukoma.
 Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwapa mikono waathirika wa ugonjwa wa mikono wanaoishi makazi ya Nunge wilayani Kigamboni ikiwa ni ishara ya kuondoa unyanyapaa kwa waathirika wa ukoma
 Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwapa mikono waathirika wa ugonjwa wa mikono wanaoishi makazi ya Nunge wilayani Kigamboni ikiwa ni ishara ya kuondoa unyanyapaa kwa waathirika wa ukoma

 Waziri Ummy Mwalimu akitoa tamko la siku ya ukoma Duniani ambapo aliwasisitiza wananchi kujenga tabia ya kuchunguza miili yao pamoja na watoto kama kuna mabaka rangi ya shaba  yasiyo na hisia na kuwahi hospitalini mara waonapo dalili hizo.
 Mwaathirika wa ugonjwa wa Ukoma Vumilia Chambuso akitoa Shukrani kwa Waziri wa Afya,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu mara baada ya kutoa tamko la maadhimisho ya Siku ya Ukoma katika makazi ya Ninge Jijini Dar es Salaam.
 Askari akimuongoza mtuhumiwa anayedaiwa kuuza maeneo katika makazi ya Nunge baada ya kutajwa na mmoja ya mkazi wa makazi ya Nunge. 
Kamishina Msaidizi wa Idara ya Ustawi wa Jamii Rabikila Mushi akitoa taarifa kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika makazi ya Nunge.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema jamii imekuwa na mtazamo hasi na kufanya wagogonjwa wa ukoma umekuwa kuogopwa na kuweka unyanyapaa na kufanya wagonjwa hao kuogopwa kuwa tegemezi na kutothaminiwa.

Ummy ameyasema hayo wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani ambayo hufanyika Jumapili ya mwisho ya Januari iliyofanyika katika makazi ya Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Amesema tunaadhimisha miaka 60 ya uwepo wa Shirika la Ujerumani linaloshughulikia masuala ya Kifua kikuu na Ukoma (GLRA). Shirika hili limekuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali kuhakikisha Ukoma unatokomezwa kwa kufadhili shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa vyombo vya usafiri kwa waratibu wa Kifua kikuu na Ukoma nchi nzima.


Ummy Siku ya Ukoma Duniani inatupa fursa ya kutathmini mwelekeo wa jitihada zetu nchini na zile za kimataifa katika kupambana na ugonjwa huu kwa kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu ni “Tutokomeze Ubaguzi, Unyanyapaa na Chuki dhidi ya Waathirika wa Ukoma.

Aidha amesema waathirika wengi wa Ukoma wananyanyapaliwa na kubaguliwa katika maeneo mengi, takriban asilimia 50 ya wagonjwa wa Ukoma hupatwa na sonona na huishi maisha ya huzuni na wasi wasi mkubwa.

Amsema wadau na wananchi wote wanahimizwa kuungana na kuongeza nguvu katika kupinga matukio vyote vya ubaguzi na unyanyapaa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hakuna sheria kandamizi kwa watu walioathirika na ugonjwa wa Ukoma. Kwa kufanya kazi pamoja na kupinga kwa nguvu zote vitendo hivi itatusaidia kupiga hatua mbele kuelekea kutokomeza Ukoma.

Ummu amesema nchi imefikia viwango vya utokomezaji wa Ukoma kitaifa mwaka 2006 kwa kiwango cha chini cha mgonjwa mmoja (1) kati ya watu 10,000, na kwa mujibu wa takwimu za Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma (NTLP) za mwaka 2017, jumla ya wagonjwa wapya 1,933 waligunduliwa na hivyo kufanya kiwango cha ugunduzi kuwa watu wane (4) kwa kila watu 100,000 na nchi kuwa . miongoni mwa nchi 22 zenye wagonjwa wengi wa Ukoma duniani nchi nyingine ni pamoja na India, Indonesia, Brazil, Ethiopia, Msumbiji, Nigeria na DRC Kongo.

Amesema mikoa 10 iliyogundulika na wagonjwa wapya wa Ukoma wengi zaidi kila mwaka na kuchangia karibia 80% ya wagonjwa wote ni Mikoaya Lindi, Rukwa, Mtwara, Morogoro,Pwani,Tanga,Geita,Dodoma,Tabora na Kigoma na Wilaya 20 ambazo hazijafikia lengo la utokomezaji ugonjwa ni Liwale, Lindi vijijini, Nachingwea, Ruangwa, Nanyumbu, Masasi mjini, Pangani, Mkinga, Korogwe, Mvomero, Kilombero, Morogoro vijijini, Ulanga, Shinyanga Manispaa, Mafia, Rufiji, Kilwa, Chato, Nkasi, na Mpanda.

Ametoa rai kwa jamii, wazazi na walezi kuwa sote tujenge tabia ya kuchunguza miili yetu na ya watoto wetu endapo utaona mojawapo ya dalili za Ukoma ambazo ni baka au mabaka mwilini yenye rangi ya shaba na hayana hisia, vijinudu kwenye ngozi au mishipa ya fahamu kuvimba na dalili zingine nyingine ni ganzi kwenye mikono na miguu unashauriwa kwenda kwenye kituo cha tiba kilicho karibu nawe kwa uchunguzi bila kuchelewa.

Ugonjwa wa Ukoma unatibika. Mgonjwa aliyeanza tiba hawezi kuambukiza mtu mwingine na hivyo hakuna sababu ya kumtenga na anaweza kuendelea na shughuli za kawaida za maisha.

"Nachukua nafasi hii kwa niaba ya serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuyashukuru mashirika mbali mbali ya ndani na nje yanayounga mkono juhudi zetu za kutokomeza Ukoma nchini”amesema Ummy

TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO SIKU YA UKOMA DUNIANI

$
0
0
 Waziri Ummy Mwalimu akitoa tamko la siku ya ukoma Duniani ambapo aliwasisitiza wananchi kujenga tabia ya kuchunguza miili yao pamoja na watoto kama kuna mabaka rangi ya shaba  yasiyo na hisia na kuwahi hospitalini mara waonapo dalili hizo.



==========   =========   ==============  ==============



TAMKO LA MHE. UMMY MWALIMU (MB) WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA UKOMA DUNIANI TAREHE 27/01/2019
KIGAMBONI, DAR ES SALAAM

Ndugu wanahabari,
Siku ya Ukoma Duniani huadhimishwa ulimwenguni kote kila Jumapili ya mwisho ya mwezi Januari. Kwa mwaka huu, siku hii itaadhimishwa tarehe 27 Januari, 2019.

Lengo kuu la maadhimisho haya ni kukumbusha umma wa watanzania juu ya ugonjwa huu. Ni dhahiri kuwa ugonjwa wa Ukoma umekuwa ukiogopwa sana katika jamii yetu toka enzi na enzi hasa kutokana na ukweli kwamba unasababisha ulemavu wa kudumu mwilini na kufanya waathirika kuwa tegemezi na kutothaminiwa.

Sanjali na madhimisho haya, hapa Tanzania tunaadhimisha miaka 60 ya uwepo wa Shirika la Ujerumani linaloshughulikia masuala ya Kifua kikuu na Ukoma (GLRA). Shirika hili limekuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali kuhakikisha Ukoma unatokomezwa kwa kufadhili shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa vyombo vya usafiri kwa waratibu wa Kifua kikuu na Ukoma nchi nzima.
 
Ndugu wanahabari,
Siku ya Ukoma Duniani inatupa fursa ya kutathmini mwelekeo wa jitihada zetu nchini na zile za kimataifa katika kupambana na ugonjwa huu. Kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu ni “TUTOKOMEZE UBAGUZI, UNYANYAPAA NA CHUKI DHIDI YA WAATHIRIKA WA UKOMA”. Ni kweli kuwa waathirika wengi wa Ukoma wananyanyapaliwa na kubaguliwa katika maeneo mengi, takriban asilimia 50 ya wagonjwa wa Ukoma hupatwa na sonona na huishi maisha ya huzuni na wasi wasi mkubwa. Haya yote husababishwa na mtazamo hasi wa jamii dhidi ya waathirika wa ugonjwa wa Ukoma. Mtazamo huu hasi ndio kikwazo kikubwa katika vita ya kutokomeza Ukoma duniani na hapa nchini.

Serikali, wadau na wananchi wote wanahimizwa kuungana na kuongeza nguvu katika kupinga matukio vyote vya ubaguzi na unyanyapaa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hakuna sheria kandamizi kwa watu walioathirika na ugonjwa wa Ukoma. Kwa kufanya kazi pamoja na kupinga kwa nguvu zote vitendo hivi itatusaidia kupiga hatua mbele kuelekea kutokomeza Ukoma.

Ndugu wanahabari,
Pamoja na kwamba nchi yetu ilifikia viwango vya utokomezaji wa Ukoma kitaifa mnamo mwaka 2006 kwa kiwango cha chini ya mgonjwa 1 kati ya watu 10,000, Ukoma bado unaendelea kuwa tatizo la kiafya miongoni mwa jamii nchini kwetu. Kwa mujibu wa takwimu za Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma (NTLP) za mwaka 2017, jumla ya wagonjwa wapya 1,933 waligunduliwa na hivyo kufanya kiwango cha ugunduzi kuwa watu 4 kwa kila watu 100,000. Takwimu hizi zinaifanya Tanzania kuendelea kuwa miongoni mwa nchi 22 zenye wagonjwa wengi wa Ukoma duniani nchi nyingien ni pamoja na India, Indonesia, Brazil, Ethiopia, Msumbiji, Nigeria na DRC Kongo. Hivi sasa bado kuna mikoa kumi ambayo inagundua wagonjwa wapya wa Ukoma wengi zaidi kila mwaka na kuchangia karibia 80% ya wagonjwa wote. Mikoa hiyo ni pamoja na: Lindi, Rukwa, Mtwara, Morogoro, Pwani; Tanga, Geita, Dodoma, Tabora na Kigoma.

Aidha, bado zipo wilaya 20 ambazo kiwango cha ukubwa wa tatizo la Ukoma lipo juu sana na bado hazijafikia lengo la utokomezaji, nazo ni Liwale,  Lindi vijijini, Nachingwea, Ruangwa, Nanyumbu, Masasi mjini,  Pangani, Mkinga, Korogwe,  Mvomero, Kilombero, Morogoro vijijini, Ulanga, Shinyanga manispaa,  Mafia, Rufiji, Kilwa, Chato, Nkasi,  na Mpanda.

Ndugu wanahabari, 
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI inatekeleza shughuli mbali mbali katika kuhakikisha Ukoma unatokomezwa  kabisa. Shughuli hizo ni pamoja na :
·       Kuhakikisha dawa za kutibu Ukoma zinaendelea kupatikana wakati wote na bila malipo yoyote,
·       Kuendesha kampeni za uibuaji wa wagonjwa wapya ngazi ya jamiikwa kuwashirikisha watoa huduma ngazi ya jamii ( Leprosy Elimination Campaigns) hasa katika wilaya zenye kiwango kikubwa cha wagonjwa wa Ukoma,
·       Kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu dalili za Ukoma na upatikanaji wa huduma kwa kutumia vifaa vya habari, Elimu na mawasiliano kama vile vipeperushi, mabango na mikanda ya video,
·       Utekelezaji wa shughuli za kuzuia ulemavu unaotokana na Ukoma ikiwemo kutathmini wagonjwa wenye vidonda, kufanya upasuaji maalum, huduma za kitaalam za macho na utoaji wa viungo bandia pamoja na viatu maalum.

Ndugu wanahabari,
Pamoja na hatua zinazochukuliwa na serikali na mafanikio zipo changamoto kubwa mbili ambazo ni jamii kuendelea kushikilia imani potofu juu ya Ukoma kuwa ni ugonjwa wa kurithi au kulogwa; na wagonjwa kuchelewa kujitokeza kupata matibabu hadi wanapopata ulemavu. Ukoma ni ugonjwa wa kuambukizwa unaosababishwa na vimelea vinavyoshambulia mishipa ya fahamu na huambukizwa kwa njia ya hewa pekee.

Nitoe rai kwa jamii, wazazi na walezi kuwa sote tujenge tabia ya kuchunguza miili yetu na ya watoto wetu. Endapo utaona mojawapo ya dalili za Ukoma ambazo ni baka au mabaka mwilini yenye rangi ya shaba na hayana hisia, vijinudu kwenye ngozi au mishipa ya fahamu kuvimba. Dalili nyingine ni ganzi kwenye mikono na miguu. Unashauriwa kwenda kwenye kituo cha tiba kilicho karibu nawe kwa uchunguzi bila kuchelewa. Hii itawawezesha wataalam wa afya kuchunguza na kubainisha kama mgonjwa ana Ukoma ili apate tiba sahihi mapema na hivyo kuzuia maambukizi na ulemavu wa kudumu unaoweza kuzuilika.

Ugonjwa wa Ukoma unatibika. Mgonjwa aliyeanza tiba hawezi kuambukiza mtu mwingine na hivyo hakuna sababu ya kumtenga na anaweza kuendelea na shughuli za kawaida za maisha.

Tiba ya Ukoma inapatikana nchini kote na hutolewa bila malipo kwa wagonjwa wote.
Nirudie tena kuwa, pale tunapoona mabadiliko yoyote yanajitokeza kwemye miili yetu twende mapema katika vituo vyetu vya huduma kuchunguzwa ili tupate matibabu stahili.

Ndugu wanahabari,
Aidha, napenda kuwashukuru watoa huduma katika vituo vya huduma za afya kote nchini kwa juhudi wanazofanya kila siku kuhakikisha ugonjwa huu si tatizo la kiafya tena nchini. Pia wanahabari kwa kuendelea kuendelea kuelimisha jamii kuhusu magonjwa mbalimbali.

Pia nachukua nafasi hii kwa niaba ya serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuyashukuru mashirika mbali mbali ya ndani na nje yanayounga mkono juhudi zetu za kutokomeza Ukoma nchini kama vile Norvatis Foundation ya Uswisi, Germany Leprosy and Tuberculosis Relief Association (GLRA) ya Ujerumani, Nippon Foundation chini ya  Sasakawa Memorial Health Initiative ya Japani na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa michango yao ya hali na mali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukoma hapa nchini Tanzania.
“TUTOKOMEZE UBAGUZI, UNYANYAPAA NA CHUKI DHIDI YA WAATHIRIKA WA UKOMA”.

Asanteni kwa kunisikiliza!

  

DAWASA YAAHIDI KUWAPA MAJI WAKAZI WA GOBA NA VITONGOJI VYAKE IFIKAPO FEBRUARI MOSI

$
0
0



Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akiwa ameongozana na msimamizi wa miradi alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akipata maelezo toka kwa msimamizi wa miradi mara alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Moja ya mita za maji ambazo zimeshasafungwa kwa wakazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salam.  
Ziara ikiendelea...

Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (kulia) akijibu hoja za mkazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam Waziri wakati alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu.

Mkazi wa Goba Kizudi jijini Dar es Salaam Waziri akitoa shukrani zake za pekee mbele ya wanahabari kwa Serikali jinsi ambavyo imepanga kuwapatia maji.
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa (kulia) akijibu hoja za mkazi wa Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam Waziri wakati alipofanya ziara katika Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwahakikishia wakazi hao kupatiwa maji ifikapo Februari Mosi mwaka huu.


Mkazi wa Goba Kinzudi akimshukuru waziri kufika eneo lao na kusikiliza changamoto zao. 
 
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
 
Serikali imewathibitishia wakazi wa kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam uhakika wa kupata maji safi na salama kuanzia Februari mosi Mwaka huu. Akizungungumza baada ya kufanya ziara katika maeneo hayo, Waziri wa Maji na Umwangiliaji Profesa Makame Mbarawa amesema Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA ) imepeleka vijana wapatao 50 kukamilisha mradi wa usambazaji maji katika maeneo hayo.
 
 Amesema vifaa vyote vimefikishwa katika eneo hilo na vijana wameanza kazi rasmi. "Kuanzia Ijumaa Februari mosi maji katika maeneo haya yataanza kutoka na kila mwananchi atapata maji safi na salama hivyo naomba muendelee kuwa wavumilivu wakati shughuli ya uunganishwaji mabomba inaendelea," amesema Profesa Mbarawa. 
 
Amesema katika mitaa ya Kinzudi na kwa Ubarikio zilizopo katika kata hizo wanatarajia kuunganisha wateja wapya mia saba (700) ambao wanatarajia kuongeza mapato ya DAWASA. "Tunakiri kukosea kwa kuwa hakukuwa na haja ya mradi huo kuchelewa kutokana na kutekeleza miradi mingi kwa wakati mmoja na sasa tumekubaliana kuwekeza nguvu katika mradi mmoja na utakapokamilika tunahamia mwingine kwa wingi," amesema. 
 
Kwa upande wao wakazi wa Mtaa hiyo wameishukuru serikali kwa kuwaahidi kupata maji kwani wamekuwa wakiteseka kwa kutumia muda mrefu kutafuta maji. Mmoja wa wakazi hayo Juma Saidi amesema wamechimba mitaro ili wapatiwe huduma hiyo ambapo kwa sasa wanaishukuru DAWASA kuwatua mzigo huo. "Huku kwetu maji yamekuwa ni lulu maana yanauzwa shilingi 500 kwa ndoo jambo linalotufanya kuhangaike hata kuyapata," amesema.

UWT YAWATAKA VIONGOZI KUJENGA MSHKAMANO KUTATUA KERO ZA JAMII

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Wananchama na viongozi wa Umoja wa Wanawake nchini (UWT) wametakiwa kujenga mshikamano na umoja sanjari na kuhamasisha wenzao kuungana kwa pamoja kujenga maendeleo na kuibua kero mbali mbali ili ziweze kupatiwa ufumbuzi na serikali.

Akiongea kwenye kikao cha majumuisho kilichoshirikisha mikoa ya Singida,Manyara,Tanga,Kilimanjaro na wenyeji Arusha Katibu mkuu wa umoja huo Queen Mlonzi amewaambia kuwa upendo ndio silaha kuu ya wanawake katika kukabiliana na majukumu ya ujenzi wa taifa na Familia hivyo mafunzo waliotoa ni shemu ya kujenga jamii.

Amewataka wanawake kujenga na kuacha kupeleka maneno huko na huko kwani wao ni sehemu ya taifa na wanamchango mkubwa wa kuisaidia nchi kufikia malengo tarajiwa ya uchumi wa kati mbali na changamoto mbali mbali wanazokutana nazo.

“Kwenye ziara hii tumekutana na changamoto mbali mbali za migogoro ya wananchi ikiwemo lishe duni,elimu,ukekektaji na ndoa za utotoni haya tumeyafundisha kwenye semina zetu kote tulipo pita nyie viongozi mkawe mabalozi wazuri wa kuhubiri na kuyafanyia kazi hizi changamoto kwenye jamii zenu zinazowazunguka”alisisitiza Mlonzi.

Kwa Upande wake Naibu Katibu mkuu wa umoja huo Jesca Mbogo amesema kuwa wanawake Kote nchini wanawajibu wa kuhakikisha lishe duni inakuwa historia ndani ya mikoa yetu hadi ngazi za familia kwa kuishi kwa upendo na kuwajali wenzetu pindi tunapoona wana matatizo tuwasaidie kwa hali na mali.

Amesema kuwa tukiishi kwa mshikamano na umoja tutafikia kwenye malengo ya uzalendo utakaopelekea kuona mchango wa maendeleo kwenye taifa letu tuishi kwa kuhubiri upendo ili kuweza kuitunza amani yetu na umoja wetu kama wanawake na mwisho wa siku taifa liendelee.

Ameinyooshea kidole baadhi ya halmashauri kushindwa kutoa mikopo kwa kina mama kwa wakati hali inayowafanya kushindwa kuzichangamkia fursa za kimaendeleo hivyo kuwataka kuwapatia mikopo wakinamama na vijana kwa wakati na kuwafuta huko walipo 

“Ziara hizi ambazo tumefanya semina mbali mbali kuhusiana na masuala ya Ukeketaji,Elimu,Lishe duni na Ndoa za utotoni ambazo zipo kwenye jamii yetu ili kuondoa changamoto na kuweza kuisaidia serikali kufikia malengo ya maendeleo kwani ukimueleimisha mwanamke ambaye ana usawishi mkubwa kwenye jamii utakuwa umeielimisha jamii nzima”alisema Mbogo.

Awali mbunge wa viti maalum Catherine Mgige alitoa Pikipiki Saba kwa viongozi wa umoja huo kwa lengo la kuwawezesha viongozi hao kuwafikia wananchini na wananchama hadi vijijini ambao ndio malengo ya serikali kuwafikia wananchi wa hali ya chini kuweza kuwainua kiuchumi.

Amesema kuwa pikipiki hizo ziwe chachu ya ushindi wa chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mapema mwishoni mwa mwaka huu wakitanguliza mshikamano kama wanachama wa chama cha mapinduzi kwani umoja ni ushindi na mshikamano unahitajika bila kuyapa nafasi makundi kutugawanya.

Nae mwenyekiti wa Umoja huo mkoani hapa Jasmin Bachu amewataka wanachama wa umoja huo kutembea vifua mbele kwa kazi inayofanywa na serikali ya Awamu ya tano chini ya Dkt.John Magufuli na kujipanga kuisaidia katika kuhakikisha malengo ya serikali yanatimia na wao kama mkoa na umoja huo wamejipanga kuyasemea yote yanayofanywa na serikali hii.

Amesema kuwa wanawake wa mkoa wa Arusha wamejipanga kutekeleza maagizo yote yaliotolewa na viongzo wao wa ngazi ya taifa na kuyafanyia kazi kwa umoja wao na mshikamano na kuacha kusemana kwa kupeleka maneno upande huu na huu ambapo aliwaomba wenzao wa mikoa mingine kuja kujifunza Arusha na wao pia wataenda kujifunza kwao kwa lengo la kufikia kwenye umoja.

“Kwa dhati nisema kuwa wanawake wenzangu wa mkoa wa Arusha tumejipanga kuhakikisha umoja na mshikamano utakaopelekea ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa ili yote mlio yasema kwenye ziara yenu viongozi wangu tutyafanyia kazi kwa vitendo na tutayaishi katika maisha yetu”alisema Bachu

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AKAGUA MASHAMBA YA MAHINDI GEREZA MOLLO, MKOANI RUKWA

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akikagua mashamba ya mahindi katika Gereza la Kilimo Mollo, Mkoani Rukwa mara baada ya kuwasili leo januari 26, 2019(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Gereza Mollo, SSP. Francis Nkurushi  akimuongoza Mkuu wa Jeshi hilo kujionea mashamba ya kimkakati katika mpango wa kuelekea kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa magerezani.

 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akitoa maelekezo kwa watendaji wa Jeshi hilo wakati akikagua moja ya mashamba ya mahindi ya Gereza Mollo, Mkoani Rukwa alipofanya ziara ya kikazi katika Gereza hilo leo januari 26, 2019.


 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akikagua moja ya ghala la kuhifadhia mahindi yanayozalishwa katika Gereza Mollo.


Mashamba ya mahindi katika Gereza la Kilimo Mollo yakiwa yamestawi kama inavyoonekana katika picha. Gereza hilo katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 limelima jumla ya hekari 825 za zao la mahindi.

. Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Mkuu wa Magereza Mkoani Rukwa, ACP. Jail Mwamgunda alipotembelea Gereza Mollo leo Januari 26, 2019.


Maafisa na askari wa Gereza Mollo wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(hayupo pichani)alipotembelea Gereza hilo leo januari 26, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza).





Wanahabari shirikini kuijenga NHIF- Mziray

$
0
0
 Meneja Mahusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Anjela Mziray akisisitiza jambo kwenye kikao kazi cha wanachama wa vyama vya waandishi wa habari mikoa ya Mtwara na Lindi.
 Meneja Uhusiano wa NHIF, Anjela Mziray akifafanua jambo, kulia kwake ni Kaimu Meneja wa Mkoa wa Mtwara, Gidion Katondo na Meneja wa Mkoa wa Lindi Bw. Emmanuel Mwikwabe, Kulia ni Wenyeviti wa Mtwara, Martina Ngulumbi na Christopher Lilai.
 Washiriki wa kikao kazi wakifuatilia mada juu ya shughuli zinazofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
 Wanachama wa vyama vya waandishi wa habari mikoa ya Lindi na Mtwara wakifuatilia ufafanuzi wa     hoja mbalimbali.
 Sehemu ya wanachama hao wakifuatilia mada.
Meneja wa Mkoa wa Lindi Bw. Emmanuel Mwikwabe akiwasilisha mada ya maboresho yaliyofanywa na Mfuko.


Na Grace Michael, Mtwara 

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewahimiza waandishi wa habari kushirikiana nao katika kuendelea kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa bima ya afya pamoja na kushiriki kuulinda Mfuko huo ili uweze kudumu na kunufaisha wengi. 

Rai hiyo imetolewa na Meneja Mahusiano wa NHIF, Anjela Mziray wakati wa kikao kazi kilichofanyika mkoani Mtwara kikihusisha wanachama wa vyama vya waandishi wa habari katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. 

“Nawaomba sana ndugu zangu tuendelee kushirikiana katika kuhakikisha tunahamasisha wananchi kupitia vyombo vyetu ili waelewe na kutumia huduma za Mfuko huu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu lakini pia ili Mfuko uendelee kuwa imara tuendelee kuunganisha nguvu katika kuulinda Mfuko wetu,” alisema Mziray. 

Alisema kuwa endapo wanahabari watashiriki vyema juhudi za Mfuko za kufikisha taarifa kwa wananchi zinazohusiana na umuhimu wa kutumia huduma za matibabu kwa mfumo wa bima, wananchi wengi wataweza kujiunga na hatimaye kuwa na uhakika wa kupata matibabu. 

“Kwa sasa bima ya afya ndio suluhisho kwa huduma za matibabu kwa wananchi wetu na ili wafanikiwe kujiunga ni lazima tuhakikishe tunawafikia kwa njia mbalimbali ikiwemo ya elimu na uhamasishaji hivyo kama ambavyo mmekuwa wadau wazuri wa Mfuko tangu mwanzo tuendelee kuwafikia wananchi wetu kupitia program mbalimbali za uelimishaji,” alisema Bi. Mziray. 

Kwa upande wa wanachama wa vyama vya waandishi wa habari katika Mikoa ya Lindi na Mtwara, wameupongeza Mfuko kwa juhudi kubwa ambazo umefanya hususan za kuanzisha mpango wa Ushirika Afya ambao utawasaidia kwa kiwango kikubwa wakulima ambao awali hawakuwa na fursa hiyo. 

“Mfuko umekuwa ni mkombozi mkubwa kwa afya za wananchi wengi tukiwemo na sisi waandishi wa habari, mfano mzuri sisi wa Mkoa wa Lindi na Mtwara ni wanufaika na tumeweka kipaumbele sana katika suala hili kwa kuwa tunafahamu kabisa kuwa gharama za matibabu ni kubwa na bila bima ya afya ni ngumu mtu kumudu gharama hizo, hivyo niendelee pia kuwahamasisha wanahabari wa mikoa mingine kuhakikisha wanajiunga na Mfuko lakini pia kuendelea na uhamasishaji,” alisema Katibu wa Chama cha Waandishi wa Mkoa wa Lindi Bw. Christopher Lilai. 

Mfuko umesema unaendelea na maboresho mbalimbali ya huduma zake ikiwemo kuongeza wigo wa wanachama kupitia makundi mbalimbali lakini pia upatikanaji wa huduma za matibabu kirahisi kupitia uimarishaji wa mifumo wa TEHAMA.

SPIKA NDUGAI BADO KUNA TATIZO KATIKA VIPIMO SAHIHI UNUNUZI MAZAO

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa (APNAC) pamoja na wawezeshaji wa semina (hawapo kwenye picha), wakati wa semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma. 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akifungua semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika (wa pili kushoto) wakati wa semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph kakunda na kushoto ni Katibu wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa, Mhe. Daniel Mtuka
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Cpt. George Mkuchika wakati wa semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa vipimo na mizani, Dkt. Ludovick Manenge akizungumza na wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa (APNAC) wakati wa semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma. 
Mjumbe wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa (APNAC) na Mbunge wa Mufundi, Mhe. Cosato Chumi akizungumza jambo wakati wa semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma. 
Wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa kupambana na Rushwa wakiwa katika semina ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa sheria ya wakala wa vipimo na mizani iliyofanyika leo tarehe 26 Januari, 2019 katika hoteli ya Dodoma Jijini Dodoma.PICHA NA OFISI YA BUNGE)


Na.Alex Sonna,Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano La Tanzania Job Ndugai amesema bado kuna tatizo kubwa katika vipimo sahihi wakati wa ununuzi wa mazao kutoka kwa wakulima licha ya kuwepo kwa Sheria ya vipimo.

Hayo ameyasema leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua Semina ya wabunge juu ya changamoto na mafanikio ya sheria ya vipimo ikiwa ni pamoja na wabunge hao kutoa michango yao katika semina hiyo jinsi ya kupambana na rushwa katika vipimo.

Wabunge hao ni wanachama wa hiari wa chama cha kupambana na vitendo vya rushwa APNAC ambao hutoa michango juu ya kupambana na rushwa na kuifikisha panapo husika.Spika amesema kuwa wakulima wamekuwa wakinyonywa sana na baadhi ya wafanyabisha kwa kutumia vipimo ambavyo si sahihi ikiwemo ufungaji wa mazao kwa njia ya lumbesa.

“Rasilimali nyingi zimekuwa zikipotea kutokana na ufungashaji kwa njia ya lumbesa , na nyinginezo ambazo si rasmi tufikie wakati tuwe na sheria kali zaidi kwani wakulima wetu wamenyonywa na kupunjwa vya kutosha” amesema Ndugai

Akitolea ufafanuzi kuhusiana na vipimo vya magari ya mizigo Spika alishangazwa kuona kuwa magari hayo licha ya kupita katika mizani mbalimbali lakini bado yanzuiwa sehemu Fulani kwa sababu ya kutakiwa kupimwa tena.

Aidha amesema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwakera wananchi kwani hawaelewi nini tatizo mpaka kuwepo kwa vipimo kila sehemu na kufanya msururu wa magari kuwa mkubwa kusubiri kupimwa.“Kama ni magari ya mizigo inawezekana wakaongeza njiani lakini kama wale wanaosafirisha mafuta kweli jamani tuliangalie na hilo tuliangalie” amesisitiza

Spika Ndugai amesema kuwa hali hiyo ni chimbuko la rushwa kwani kama mfanyabishara anayesafirisha mafuta ameshapima vituo vyote hakuna sababu ya kumzuiakwani uwezekano wa kuongeza ujazo wa mafuta njiani ni mdogo.

Awali akitoa taarifa ya awali kwa wabunge wanachama wa chama cha wabunge wanapambana na rushwa (APNAC) Katibu wa APNAC Daniel Mtuka alisema APNEC iliundwa mwaka 2000.Hata hivyo amesema kuwa madhumuni ya kuundwa kwake ni kupambana na rushwa mara baada ya kuona vitendo vya rushwa vinazidi.

Pia amesema kuwa wabunge waliokuwepo kipindi hicho waliona kuna umuhimu wa kuanzisha kikundi cha wabunge ambao watapambana na rushwa.Spika Ndugai amesema kuwa APNAC ilifanikiwa mwaka 2007 kushiriki kuandaa sheria namba 11 ya TAKUKURU ambapo sheria hiyo ilikuwa na vifungu vine tu lakini sasa vipo 24

Amesema kuwa bado Sheria ya Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa inahitaji marekebisho zaidi. Alisema kutokana na hali hiyo APNAC ilita mawazo wakati wa mchakato wa Bunge la katiba ambao alisema ungewabana zaidi wanaokamatwa na vitendo vya rushwa.

“Tumeweza kutoa marekebisho mengi juu ya Sheria ya TAKUKURU na mengi yameweza kusaidia nchi yetu lakini bado tunaona ipo haja ya kuendelea kutoa mawazo yetu.Kwa upande wa vipimo Waziri wa Biashara na Viwanda Josph Kakunda amesema kuwa bado kuna changamoto kubwa katika suala la vipimo.Hata hivyo amesema kuwa kumekuwa na udanganyifu mkubwa kwa wafanyabiashara na madalali wanunuapo amzao toka kwa wakulima .

“Vipimo kama vya Lumbesa, Madebe na hata vikopo bado vimekuwa vikitumika katika sehemu nyingi hapa nchini ingawa tunavikataa” amesema
Amesema kuwa Wizara yake imeweza kujenga vituo vya msoko katika mipaka ili wakulima waweze kuuza mazao yao kihalali na uzito unaotakiwa.
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live




Latest Images