Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU TIDO MHANDO.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii. 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Imemuachia huru Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Tido Mhando, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Hukumu hiyo imesomwa leo Januari 25.2019 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao dhidi ya mshtakiwa Tido. 

Katika kesi hiyo Tido ameshtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka wakati akiongoza shirika hilo ambapo anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na moja la kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. Milioni 800

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Shaidi amesema, upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake watano wameshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa kuwa kweli alitenda makosa hayo. 

Akiuchambua ushahidi huo, Hakimu Shaidi amesema miongoni mwa mambo mengi yaliyozungumzwa yalikuwa ni suala la mikataba.Amesema katika ushahidi wao, wa mkataba ulionyesha kulikuwa na sahihi ya Tido na Channel 2 lakini hakuna sahihi ya Mwanasheria Mkuu, Bodi wala mamlaka nyingine.

Ameongeza, Mshtakiwa Tido akiwa kama Mkurugenzi alikuwa ana wajibu wa kufata taratibu za zabuni na hivyo ili kitu kiwe mkataba lazima kipitie hatua lakini mkataba huo anaodaiwa kusaini Tido na Channel 2 hakuwa na sifa ya kuwa mikataba.

Akiendelea kuuchambua ushahidi huo Hakimu Shaidi amesema, ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hauelezi mahali ambapo malipo yamefanyikia, sababu malipo yamefanyika kwa mikataba ambayo haina vigezo.Upande wa mashitaka unadai mkataba huo haukufuata utaratibu wa kisheria.

" Kweli mkataba kuitwa mkataba ili ukamilike lazima kuwepo na watu ambao wanahusika na lazima kuwepo na mwanasheria hivyo mkataba huo sio halali bali ni makubaliano ya awali, " alisema.Baada ya uchambuzi huo, Hakimu Huruma alisema mshitakiwa huyo hakuna sehemu ilithibitisha kwamba ulikuwa ni mkataba hivyo anamwachia huru.

Miongoni mwa mashahidi wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi katika kesi hiyo ni ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

Katika kesi hiyo, inadaiwa Juni 16 mwaka Jana, huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume cha Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

Katika shtaka la pili, Tido anadaiwa kusaini makubaliano ya utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl.

Katika shtaka la tatu, anadaiwa Agosti 11 na Septemba mwaka Jana, akiwa Dubai, Tido alitumia vibaya madaraka yake kwa kusaini mkataba wa makubaliano ya ununuzi, usambazaji na kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.

Pia Tido anadaiwa, kutumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa makubaliano kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT Broadcast Infrastructure) kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI.

Katika shtaka la mwisho Tido anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16 mwaka huu akiwa UAE, aliisababishia TBC hasara ya Sh 887,122,219.19.

WAJUMBE UMOJA WA WABUNGE WANAWAKE TANZANIA WAKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SHIRIKA LA UMOJA WA KIMATAIFA LA WANAWAKE JIJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Wajumbe kutoka Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) na ugeni kutoka Shirika la Umoja wa kimataifa la wanawake ulioongozwa na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa kimataifa la wanawake Kanda ya Afrika Mashariki na Kati yenye makazi yake Nairobi, Dkt. Izeduwa Derex Briggs kikao kilichofanyika leo tarehe 25 Januari, 2019 katika ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Margaret Sitta akiongoza kikao cha pamoja cha Wajumbe kutoka Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) na ugeni kutoka Shirika la Umoja wa kimataifa la wanawake  (UN Women) kilichofanyika leo tarehe 25 Januari, 2019 katika ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa kimataifa la wanawake Kanda ya Afrika Mashariki na Kati yenye makazi yake Nairobi, Dkt. Izeduwa Derex Briggs akizungumza na Wajumbe kutoka Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (hawapo kwenye picha) kikao kilichofanyika leo tarehe 25 Januari, 2019 katika ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe kutoka Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) wakiwa katika kikao cha pamoja na ugeni kutoka Shirika la Umoja wa kimataifa la wanawake (UN Women) kilicholenga kufahamiana, kubadilishana uzoefu na kujua shughuli mbali mbali zinazofanywa na Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) kikao kilichofanyika leo tarehe 25 Januari, 2019 katika ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) na ugeni kutoka Shirika la Umoja wa kimataifa la wanawake ulioongozwa na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa kimataifa la wanawake Kanda ya Afrika Mashariki na Kati yenye makazi yake Nairobi, Dkt. Izeduwa Derex Briggs (wanne kulia mbele) kikao kilichofanyika leo tarehe 25 Januari, 2019 katika ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia mbele ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Margaret Sitta na Mjumbe Mhe. Salma Kikwete (wa pili kulia mbele)

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WAZIRI KIGWANGALLA ATUA NCHINI HISPANIA, AUNGURUMA

$
0
0
Na Mwandishi wetu-Hispania

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla amewaita Wawekezaji kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii wakati aliposhiriki kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika.

Kongamano hilo limefanyika jana katika jiji la Madrid nchini Hispania
likiwa limeandaliwa na Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UNWTO)kwa
kushirikiana na Taasisi za Casa Afrika pamoja na Taasisi yamaonesho ya
Biashara ya Madrid (IFEMA) na kushirikisha nchi mbali mbali duniani.

Katika Kongamano hilo, Waziri Kigwangalla alipata fursa ya kuwa mmoja wa wazungumzaji ambapo amewahakikishia Wawekezaji wenye nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania kwamba ni sehemu salama ukizingatia hali ya amani na utulivu iliyopo nchini lakini pia kuna vivutio vingi vya utalii na fursa za kuwekeza.

"Nawakaribisheni nyote, Njooni Tanzania muwekeze kufuatia uwepo wa
mazingira na miundombinu bora kwa ajili uwekezaji katika sekta ya utalii
pamoja na viwanda" Alisema

Waziri Kigwangalla pia alitumia nafasi hiyo kwa kuutangaza ukanda mpya wa kusini mwa Tanzania ambao umejaliwa kuwa na vivutio vya Utalii vya kipekee vinavyopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mikumi pamoja Pori la Akiba Selous.

Katika hatua nyingine , Waziri Kigwangalla wakati akizungumza katika
kongamano hilo aliwaeleza washiriki hao kuhusu juhudi mbalimbali
zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Tanzania,John Pombe Magufuli kwa kutaja mifano michache kama vile kufufua kampuni yandege (ATCL) kwa kununua ndege mpya sita pamoja kujenga chanzo kikubwa cha kuzalisha umeme katika mto Rufiji.

Alisema serikali ya Tanzania pia inaendelea na mradi wa kisasa wa ujenzi wa njia mpya ya kisasa ya reli (Standard Gauge) pamoja na kuboresha
miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo.

Alibainisha kuwa kutokana na juhudi hizo zilizochukuliwa na Serikali hiyo,
sekta ya utalii itaweza kusonga mbele ikiwa pamoja na kurahisisha usafiri
kwa watalii pamoja na wawekezaji kwa ujumla.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa kongamano la 10 la Uwekezaji navBiashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour) lililofanyika Janakatika jiji la Madrid nchini Hispania ambapo katika Kongamano hilo WazirivKigwangalla alitumia fursa hiyo kuwaita Wawekezaji kuja nchini kwa ajili yavkuwekeza katika sekta ya Utalii na viwanda.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (mbele ) akiwa ni miongoni mwa washiriki akifuatilia kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour)  lililofanyika Jana  katika jiji la Madrid nchini Hispania ambapo katika Kongamano hilo Waziri Kigwangalla alitumia fursa hiyo kuwaita Wawekezaji kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii na viwanda.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiwa ni miongoni mwa Wazungumzaji  kwenye kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour) lililofanyika jana katika jiji la Madrid nchini Hispania ambapo katika Kongamano hilo Waziri Kigwangalla alitumia fursa hiyo  kuwaita Wawekezaji kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii na viwanda.

TAARIFA YA UTEUZI DIWANI WANAWAKE VITI MAALUM

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA KUAPISHWA KWA RAIS WA CONGO DRC

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Congo imeandika historia mpya kwa kukabidhiana madaraka kwa upendo na ana imani Viongozi wataendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo na maslahi mapana ya nchi yao.

Makamu wa Rais ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameyasema hayo mara baada ya sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Felix Tshisekedi.

“Linalofurahisha ni kwamba ni mara ya kwanza kwa nchi hii ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanya uchaguzi wa kidemokrasia na kukabidhiana madaraka kwa usalama kabisa” alisema Makamu wa Rais.

 Uchaguzi huo uliofanyika Desemba 30, 2018, Mhe. Felix Tshisekedi alipata takribani kura milioni 7 sawa na asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa ambapo wagombea wenzake kama Martin Fayulu alipata ailimia 34 sawa na kura milioni 6.4, Bw. Emmanuel Ramazani Shadary alipata asilimia 23 sawa na takribani kura milioni 4.4.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeandika historia kwa mara ya kwanza tangu ilipopata uhuru kwa kukabidhiana madaraka kwa njia ya Amani. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Damas Ndumbaro pamoja na viongozi wengine wakati wa sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uwanja mkuu wa michezo mjini Kinshasa, wengine pichani ni Rais Felix Tshisekedi pamoja na Joseph Kabila.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Damas Ndumbaro pamoja na viongozi wengine wakati wa sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uwanja mkuu wa michezo mjini Kinshasa

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA CWT TAIFA

$
0
0
PMO 9013 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Taifa, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 25, 2019. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais , Deus Seif, Mweka Hazina , Abubakar Allawi, Katibu Mkuu, Christopher Banda na Wapili kulia ni Rais wa CWT , Leah Ulaya.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MAWAZIRI UGANDA NA TANZANIA KUJADILI BOMBA LA MAFUTA GHAFI

$
0
0
Kikao cha Nne cha Mawaziri mbalimbali kutoka Uganda na Tanzania wanaohusika na utekelezaji wa mradi wa bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania kinatarajiwa kufanyika leo jijini Kampala ambapo Mawaziri hao wanatarajiwa kupata taarifa za majadiliano yaliyokuwa yakifanyika kati ya Timu ya Kitaifa ya Majadiliano (GNT) ya Tanzania na Uganda ambayo yalianza Januari 21, 2019.

Kutoka Tanzania Mawaziri watakaohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.

Aidha Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pia watahudhuria kikao hicho, hii ni baada ya kufanya kikao jana na Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali nchini Uganda wanaohusika na utekelezaji wa mradi huo hivyo Makatibu Wakuu hao ndio wataokawasilisha taarifa  kwa Mawaziri kuhusu majadiliano ya wataalam wa pande zote.

Kabla ya kufanya kikao na Mawaziri wa Uganda, Mawaziri hao kutoka Tanzania mapema leo walifanya kikao  na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali nchini Tanzania walio katika  Timu ya Kitaifa ya Majadiliano ya Mradi huo ili kupata taarifa ya awali ya hatua ya majadiliano.

Baada ya kupata taarifa ya hatua ya majadiliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili, Mawaziri hao watajadili taarifa hiyo na endapo wataiafiki, hatua nyingine za majadiliano zitaendelea  ambazo  sasa zitahusisha Serikali ya Uganda na Tanzania na wawekezaji wa mradi ambao ni kampuni ya Total E&P  ya Ufaransa, Tullow Oil ya Uingereza, CNOOC ya China na kampuni za Mafuta za Taifa za Tanzania na Uganda.

Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania litakuwa na urefu wa kilometa 1445.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati), Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi ( wa pili kushoto), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ( wa pili kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (wa kwanza kulia) wakiwa katika kikao na wataalam wa Tanzania (hawapo pichani) wanaohusika na majadiliano ya mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
 Wataalam kutoka Taasisi mbalimbali nchini Tanzania walio katika Timu ya Kitaifa ya Majadiliano (GNT) ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania wakiwa katika kikao na Mawaziri kutoka Tanzania (hawapo pichani) wanaohudhuria mkutano kuhusu mradi huo unaofanyika jijini Kampala-Uganda.
 Kikao kati ya Mawaziri  na Wataalam mbalimbali kutoka Tanzania  waliohudhuria Mkutano kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi unaofanyika jijini Kampala-Uganda.
 Watendaji mbalimbali kutoka Tanzania wakiwa katika kikao na Mawaziri kutoka Tanzania wanaohudhuria Mkutano kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi unaofanyika jijini Kampala Uganda.
Watendaji mbalimbali kutoka Tanzania wakiwa katika kikao na Mawaziri kutoka Tanzania wanaohudhuria Mkutano  kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi unaofanyika jijini Kampala Uganda.

WAZIRI BITEKO AMALIZA MGOGORO KATI YA KAMPUNI YA BEAL NA MTL

$
0
0

Waziri wa Madini, Doto Biteko amemaliza mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Barrick Exploration Africa Limited (BEAL) na Megagems Tanzania Limited (MTL) uliodumu kwa muda mrefu. MTL ambaye ni mlalamikiji alikuwa anadai kulipwa kiasi cha Dola za Marekani 10,000 na Kampuni ya BEAL.

Akisuluhisha mgogoro huo Waziri Biteko ameitaka Kampuni ya BEAL kumlipa mlalamikaji kwa kuwa vibali vyote vinaonesha kuwa anastahili kulipwa. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 25 Januari, 2019 jijini Dodoma katika Ofisi ya Waziri wa Madini, Doto Biteko.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akishuhudia Mwakilishe wa Kampuni ya Barrick Exploration African Limited (BEAL), Janet Lekashingo akipeana mkono na mmiliki wa kampuni ya Megagems Tanzania Limited (MTL) baada ya kufikia mwafaka wa mgogoro wao wa MTL kulipwa haki yake.
 Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa (wa kwanza kushoto) akifatilia  kikao cha kusuluhisha mgogoro kati ya Kampuni ya Barrick Exploration Africa Limited (BEAL) na Megagems Tanzania Limited (MTL). Wengine katika picha ni Mwanasheria wa Wizara, Godfrey Nyamsenda (wa pili kushoto), Mwanasheria wa Novelty Advocate Joseph Asenga na Mmiliki wa Kampuni ya MTL, Suleiman Nasib.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Barrick Exploration African Limited (BEAL), Janet Lekashingo akimkabidhi Waziri wa Madini, Doto Biteko nyaraka kwa ajili ya kupitia kabla ya kumaliza Mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Barrick Exploration Africa Limited (BEAL) na Megagems Tanzania Limited (MTL).
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akipitia nyaraka iliyokabidhiwa kwake na Mwakilishe wa Kampuni ya Barrick Exploration African Limited (BEAL), Janet Lekashingo (hayupo pichani) kabla ya kumaliza mgogoro kati ya Kampuni ya Barrick Exploration Africa Limited (BEAL) na Megagems Tanzania Limited (MTL). 


VIONGOZI WA UUGUZI MOI WATOA MSAADA WA KIJAMII WODINI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi MOI, Fidelis Minja (Kulia) akiwakabidhi dawa na zawadi nyingine wazazi wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wanatibiwa katika Taasisi hiyo. Wengine ni viongozi kutoka kwenye kurugenzi hiyo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Baadhi ya viongozi wakiandaa dawa pamoja na zawadi nyingine kabla ya kukabidhiwa
Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi MOI akijadiliana na viongozi wa kurugenzi yake kabla ya kutoa msaada kwa watoto
Viongozi wa kurugenzi ya Uuguzi wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
Viongozi wa kurugenzi ya Uuguzi wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi Fidelis Minja akizungumza na waandishi wa habari (Pichani hawapo)

NA KHAMISI MUSSA

Viongozi wa kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Mifupa MOI leo wametoa msaada wa kijamii pamoja na dawa kwa watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi wanaopata huduma katika Taasisi ya MOI wodi 5A. Msaada huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kujitolea kwa wale wenye mahitaji maalumu pamoja na kuhamsisha huduma bora kwa wateja

Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi wa MOI Bwana Fidelis Minja amesema imekuwa ni utamaduni wa kurugenzi hiyo kufanya shughuli za kijamii kwa lengo la kuonyesha mfano kwa jamii na pia kuwaunga mkono wanajamii ambao hujitolea kwa ajili ya watu wenye uhitaji hususani wagonjwa

“Sisi kama viongozi wa Kurugenzi hii ya Uuguzi tumeamua tutoe msaada kwa Watoto hawa wenye vichwa vikubwa pamoja na kuwapatia dawa ambazo tumenunua kwa kuchangishana fedha zetu, pamoja na msaada huu tutawahudumia na kuwapa faraja wazazi wao. Tunaamini hili ni jambo jema kama ambavyo wengine wamekuwa wakifanya” Alisema bwana Minja

Bwana Minja ameongeza kwamba hii ni sehemu ya utakelezaji wa mpango mkakati wa Taasisi ya MOI ambao pamoja na mambo mengine unaelekeza juu ya uboreshwaji wa huduma za uuguzi pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja yaani ‘Customer care’

“Tumefanya hivi ikiwa ni sehemu ya kuonyesha kwa vitendo kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali yetu pamoja na kazi kubwa inayofanywa na kiongozi wetu wa MOI Dkt Respicious Boniface ambaye amejitoa kwa dhati kuboresha hali ya utoaji huduma kwa wateja” Alsiema Bwana Minja

Kwaupande wake muwakilishi wa wazazi wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi Bi Zuena Ally amesema anaishukuru Serikali kwa kuboresha huduma na pia anawashukuru wauguzi ambao watoa msaada pamoja na dawa kwaajili ya Watoto

“Nawashukuru sana kwa kuteletea dawa, tulizoea kuona watu kutoka nje ndio wanatuletea msaada lakini leo mmekuja nyie, Mungu awabariki sana kwa moyo wa upendo.Mtoto wangu anaendelea vizuri nashukuru sana kwa huduma nzuri” Alisema Bi Zuena.

Taasisi ya MOI ipo kwenye utekelezaji wa mpango mkakati wake wa miaka 5 ambao pamoja na mambo mengine umejikita katika kuboresha huduma kwa wagonjwa. 

MAGEREZA KUMI (10) YA KIMKAKATI KUZALISHA CHAKULA CHA WAFUNGWA, GEREZA SONGWE LIKIWEMO

$
0
0
Na ASP Lucas Mboje, Mbeya
KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amesema kuwa Jeshi la Magereza limeanza utekelezaji wa mpango wa miaka mitano wa kuelekea kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa magerezani katika magereza kumi (10) ya kimkakati likiwemo Gereza Songwe, lililopo Mkoani Mbeya ambalo limelima hekari 750 za zao la mahindi.
Akizungumza na wanahabari leo mara baada ya kukagua mashamba ya mahindi katika Gereza la Kilimo Songwe, Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike amesema kuwa lengo la ziara yake ni kujionea hali halisi ya ufanikishaji wa jukumu walilopewa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wanazalisha chakula kwa wingi cha wafungwa waliopo magerezani.
Amesema kuwa Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa ambayo imeingizwa katika utekelezaji wa mpango huo wa uzalishaji chakula cha wafungwa ambapo kila Gereza la kimkakati limepangiwa malengo ya kulima mazao mbalimbali ya chakula cha wafungwa ikiwemo mahindi, maharage na mpunga.
“Mpango huu ni lazima tuufanikishe, hivyo tayari tumekwishajipanga na nguvu kazi ya wafungwa inatumika ipasavyo katika kufanya kazi katika magereza hayo kama mlivyojionea leo hapa Gereza Songwe, pia tunajitahidi kusimamia rasilimali nyinginezo tulizonazo katika maeneo yetu ya magereza ili tuweze kutekeleza ipasavyo maelekezo ya Serikali”. Alisisitiza Jenerali Kasike.
Aidha, Jenerali Kasike ameongeza kuwa kwa sasa Jeshi hilo linakusanya rasilimali zilizopo na kutoa kipaumbele katika magereza yakimkakati, ambapo katika kukidhi mahitaji ya nguvu kazi ya wafungwa, tayari wafungwa kutoka sehemu mbalimbali nchini wamehamishiwa katika magereza yenye mkakakati ili kuongeza nguvu kazi yakutosha katika maeneo hayo yenye uzalishaji.
Akisoma taarifa ya Magereza Mkoa kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Mkuu wa Magereza Mkoani Mbeya, SACP. Luhende Makwaia amesema kuwa Mkoa huo una jumla ya magereza matano ambayo yanatekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo miradi ya kilimo, likiwemo Gereza Songwe.
Kuhusu msongamano wa wahalifu, SACP. Luhende Makwaia amesema kuwa magereza yote ya mkoa wa mbeya yanakabiliwa na tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu kutokana na ongezeko la uhalifu unaotokana na kuongezeka kwa idadi ya watu pamoja na kukosekana kwa gereza moja la wilaya katika mkoa huo.
Mkoa wa Mbeya una jumla ya wilaya sita(6) ambazo ni Mbeya mjini, Mbeya Vijijini, Chunya, Rungwe, Mbarali, na Kyela. Katika wilaya hizo ni wilaya tano(5) tu zina magereza, wilaya moja(1) ya chunya hakuna gereza hali inayochangia uwepo wa msongamano wa wahalifu katika mkoa. Aidha, katika magereza matano yaliyopo hupokea na kuhifadhi wafungwa na mahabusu katika mkoa huo.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkuu wa Gereza Songwe, SSP. Peter Anatory alipowasili katika Gereza la Kilimo Songwe leo Januari 25, 2019 kwa ziara ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa Jeshi hilo pamoja na kukagua mashamba ya kimkakati katika kuelekea kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa magerezani.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua moja ya mashamba ya mahindi ya Gereza Songwe alipofanya ziara ya kikazi katika Gereza hilo kabla ya kuendelea na ziara yake Mkoani Rukwa leo Januari 25, 2019.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akitoa maelekezo kwa Maafisa Waandamizi wa Magereza Mkoani Mbeya alipotembelea na kukagua mashamba ya mahindi ya Gereza Songwe.
 Muonekano wa mashamba ya mahindi katika Gereza la Kilimo yakiwa yamestawi kama inavyoonekana katika picha.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiangalia zao la mhindi ambalo linakaribia kukauka katika eneo la mradi wa Kilimo cha umwagiliaji cha Gereza Songwe. 
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Jeremia Minja (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya.(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Serikali Itaendelea Kushirikiana na Sekta Binafsi-Dkt Abbasi.

$
0
0
Mwandishi wetu-MAELEZO 


SERIKALI itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kutoa fursa kwa watu wengi kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mingi kwa mapana, katika Taasisi za serikali na Taasisi binafsi. 

Akizungumza katika mjadala wa Clouds Media katika kipindi cha The Big Breakfast chenye kauli mbiu ya The power of Man yaani Nguvu ya Pamoja kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi alisema kuwa serikali inaendelea na jukumu la ujenzi wa nchi kwa kushirikiana na sekta binafsi. 

“Tunatambua na kuheshimu nguvu ya wengi kama kauli mbiu hii inavyoeleza, katika dhana ya maendeleo kuna mengi Serikali inafanya ili kutekeleza azma yake kwa wananchi, mfano Ujenzi wa madaraja mbalimbali nchini, Miradi ya Maji, Miradi ya Umeme, Ujenzi wa vituo vya afya na Hospitali na kulete ndege, kwetu sisi haya ni maendeleo makubwa sana”, Dkt. Abbasi. 

Katika dhana ya Nguvu ya pamoja, Dkt. Abbasi alisema kuwa kauli mbiu hii inaonesha namna gani sasa haya mambo ambayo Serikali inafanya yanawafikia wananchi na kuwanufaisha popote walipo. 

Dkt.Abbasi alieleza kuwa katika mjadala wa nguvu ya pamoja dhana ya maendeleo ina nadharia mbili ambazo wasomi wanazijadili duniani kote ikiwa ni moja ya miongozo ya maenedeleo duniani, huku wakiamini katika nadharia ya maendeleo ni watu na wengine wakiamini katika nadharia ya maendelo ni vitu. 

“nilichokisema ni kwamba duniani kuna mjadala mkubwa sana katika suala la maendeleo, wapo wanaoamini kwamba maendeleo ni watu kwa mambo yanafanyika moja kwa moja na yanagusa watu, wapo wanaoamini kwamba maendeleo ni vitu kwamba huwezi kuwaendeleza watu bila kuwajengea miundombinu kama vile barabara, reli, umeme na maji”, Dkt Abbasi. 

Katika kuunga mkono kauli mbiu ya nguvu ya pamoja, Dkt Abbasi alieleza kuwa katika nadharia mbili za maendeleo Serikali inaamini katika nadharia zote yaani maendeleo ni vitu kwani inatekeleza miradi mbalimbali kama barabara, Umeme, Maji, Afya na elimu, huku ikiwawezesha wananchi kupata elimu bure, dawa katika vituo vya afya na umeme, ambao kwa sasa unafika mpaka vijijini kwa maana ya maendeleo ni watu. 

Aidha Dkt Abbasi alieleza kuwa kauli mbiu ya Nguvu ya pamoja kutoka Clouds Media ni moja ya njia kubwa katika kutimiza malengo la wananchi kwa kutekeleza na kusimamia miradi mbalimbali ambayo ndiyo inawawezesha wananchi kufanya shughuli zao za maendeleo. 

Kwa upande wa sekta ya habari Dkt.Abbasi alieleza kuwa Serikali inafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na sekta binafsi katika sekta hiyo muhimu pamoja na sekta zingine ambazo zinawezesha wananchi kujikwamua kimaendeleo. 

“Serikali ndiyo mwezeshaji mkuu wa sekta mbalimbali, Sekta haiwezi kufanya kazi nchini bila Serikali kuiwezesha kwa hiyo katika dhana hiyo hiyo ya Nguvu ya pamoja Serikali inashiriki kwa nguvu zote”, Dkt Abbasi. 

Dkt. Abbasi aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuheshimu uwepo wa sekta binafsi katika sekta ya habari kwani mpaka sasa imewezesha upatikanaji wa leseni kwenye majarida na mageti 202, Vituo vya Televisheni 35 na Redio 160. 

Alieleza pia kuwa nguvu ya pamoja ni pamoja na watendaji wa Serikali kushirikiana na sekta binafsi ili kuwawezesha kupata huduma mara moja pale inapohitajika kwa sababu watakuwa wanatenda jambo la kuwafanya wengi kupata ajira katika sekta hizo. 

“Ukiangalia uanzishwaji wa viwanda ni lazima kuna mtendaji alijituma kutoa leseni, maendeleo ya biashara mbalimbali, kilimo na sekta zingine ni lazima upate leseni ni hata kwenye sekta ya habari hii inamaana kuwa mtendaji wa Serikali unapoharakisha kwa kufuata sheria na taratibu kuhakikisha mtu anapata leseni ya kuanzisha kiwanda, Biashara kubwa au gazeti utakuwa umeajiri watu wengi bila kujua na hii ndiyo the power of man (Nguvu ya pamoja)”, Alisisitiza Dkt. Abbasi. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu na Mumiliki wa Clouds media Group Joseph Kusaga aliahidi kushirikiana na Serikali katika kutangaza maendeleo ya nchi hasa kwenye sekta ya usafiri wa anga (shirika la ndege la Tanzania AirTanzania) pamoja na sekta ya utalii katika kampeni mbalimbali zitakazokuwa zinatangazwa Clouds Media.

Naibu Waziri wa Afya Azindua bidhaa ya kikombe hedhi jijini Dar

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile akizungumza katika hafla ua uzinduzi wa bidhaa ya kikombe hedhi na teknolojia ya simu ya mkononi ya mzunguko wa hedhi iliyozalishwa na Kampuni ya AnuFlo Industries Ltd. Jijini Dar es Salaam
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii 

NAIBU Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile amesema elimu ya hedhi bado ni changamoto hapa nchini, kwa sababu hakuna mfumo rasmi wa elimu hiyo na wengi hawaelewi kuhusu mzunguko.

Dk. Ndungulile ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa bidhaa ya kikombe hedhi na teknolojia ya simu ya mkononi ya mzunguko wa hedhi iliyoanzishwa na Kampuni ya AnuFlo Industries Ltd. Jijini Dar es Salaam

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema, elimu inatakiwa kutolewa ili kusaidia jamii kujua kuhusiana na mzunguko wa hedhi kwa sababu kuna baadhi ya wanafunzi wanakosa masomo wakiwa katika hali hiyo kwa kuhofia kuwa wapo tofauti na wengine.

Amesema,  elimu hiyo inatakiwa kutolewa kwa wanaume pia kwani nao wanapaswa  kuujua juu ya mzunguko huu, tusiishie kwenye mzunguko wa mpira tu," amesema Dk.Ndungulile
Amebainisha kuwa asilimia 50 ya watanzania wanaguswa na watoto hili hasa wasichana wenye umri  wa kati ya 15 hadi 18 asilimia 27 kwani  wengi wao ni wajawazito au ameshakuwa na mtoto.

 Amesema  takwimu Hizo ambazo hizo sio nzuri kwa nchi yetu, zimechangiwa zaidi na ukosefu wa elimu ya hedhi, na kuwashaurii kwa wadau mbalimbali waendelee kutoa elimu hiyo.


Aidha Dk. Ndungulile ametaja changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya hedhi salama kuwa bado ni kubwa kiasi ambacho mtu anaweza kupata maambukizi ya maradhi kama hajatumia vifaa salama.

"Mimi kama daktari nalielewa sana jambo hili kwa upana, linaashilia kuwa kijana amepevuka na linaumuhimu katika ukomo wa hedhi, ambapo ndiyo mwisho wa kupata mtoto, kwa hiyo elimu hii ni muhimu kwa kila mmoja," alisema Dk.Ndungulile

Ameongeza kuwa,  wakitokea wajasiliamali kama hawa tunahakikisha tunawashika mkono  kuhakikisha wanatimiza malengo yao.
Naye,  Mkurugenzi wa Kampuni ya Anuflo, Flora Njelekela amesema tafiti za hedhi salama nchini zinaonesha, kuwa asilimia 65 ya wanawake nchini kupata hedhi kila mwezi huku asilimia 82 ya Wasichana na wanawake akiwa hawana uelewa juu ya afya na hedhi salama.

Amesema, ukosefu bidhaa hedhi salama hulazimisha msichana mmoja kati ya 10 kukosa masomo kwa siku tatu hadi tano kila mwezi ambazo ni sawa na asilimia 20 ya siku za masomo kwa mwaka.

Njelekela amesema  kutokana na uhaba wa bidhaa hizo,  garama takwimu, na tafiti zilizofanywa kuhusiana na hedhi salama ndiyo maana Kampuni yake ikajikita katika kuzalisha kikombe cha hedhi, kwa sababu ni salama ni hakina madhara, kinadumu kwa muda mrefu na Pia kitawafanya wanafunzi wasome kwa raha.

Alisema kikombe hedhi hicho,  kimekuja kukabiliana na tatizo la uchafuzi wa mazingira, kwa sababu kitatumika kwa kipindi cha miaka mitano na  pia kinawekwa kwa masaa 12 asubuhi hadi jioni ndiyo mtu anakitoa.
Mkurugenzi huyo amesema hiyo imetengenezwa kwa kuzingatia ubunifu makini na teknolojia za kisasa kwani kimetengenezwa kwa asilimia 100 ya LFGB medical silicone ambayo haileti Madhara 

Kwa upande wake, Muwakilishi wa Ofisa  Elimu Mkoa, Maimuna Mtanda amesema kikombe hicho kitaondoa suala la utorosho shuleni , sio kwamba wanafunzi hawapendi kwenda shule ni kutokana na kutokuwepo na mazingira rafiki ya wao wakiwa kwenye hedhi.


Naye, Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana, Jangwani, Jackline Shio alisema walikuwa wanapata changamoto katika kipindi cha hedhi , kutokana na gharama za taulo za kike kuwa kubwa ila Flora ameweza kulitatua tatizo hilo kwa kuwaletea kikombe cha hedhi.

Mwanafunzi huyo alitoa pendekezo kuwa elimu hiyo iendelee kutolewa ili kuokoa wanafunzi wanaokosa masomo, kipindi ambacho wanakuwa na hali hiyo.



HALMMASHAURI YA MJI KONDOA YAPONGEZWA KWA KUZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI

$
0
0
Na: Sekela Mwasubila,Halmashauri yamKondoa Mji

Halmashauri ya wa Mji Kondoa imepongezwa kwa kufanya uzinduzi wa baraza la wafanyakazi ikiwa ni halmashauri ya pili katika mkoa wa Dodoma kufanya hivyo.

Pongezi hizo zilitolewa na Katibu Tawala wa Wilaya Andrea Mwani wakati akizindua baraza hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi Kondoa Mjini.

Alisema kuwa uwepo wa baraza hilo ikawe chombo cha kusema katika kufikisha matakwa ya watumishi na kuimarisha ushirikiano na mwajili na kuwa anauhakika katika baraza hilo wajumbe watawasilisha wanayoona yatafaa katika kushirikiana na mwajiri kutatua changamoto za kazini.

”Mnaweza mkaona katika uongozi huu wa awamu ya tano jinsi Mheshimiwa Rais anavyofanya mabadiliko ya kuiendeleza nchi na wakuyafanya haya ni sisi wafanyakazi hivyo kila mmoja awajibike katika eneo lake na kujitathmini ili tuendane na upepo uliopo.”Alisema Mwani

Aidha alisisitiza wafanyakazi kufanyakazi na kutimiza majukumu yao walioajiliwa nayo kwa asilimia zote pamoja na melekezo wanayopewa kwani kwa kufanya hivyo wanamsaidia Mheshimiwa Rais, Mkuu wa Wilaya, Halmashauri na wananchi wanaowahudumia.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Mji Kondoa Msoleni Dakawa alisema kuwa baraza limeanzishwa baada ya kuona umuhimu wa wafanyakazi kwa kuwa katika serikali mfanyakazi ndio mzalishaji na mtekelezaji wa maagizo na ahadi zinazotolewa na serikali.

“Niombe kwa wakati mwingine kwa umoja huu tuliouonyesha na vyama vya wafanyakazi tuendelee nao iwe wakati wa shida na raha kwani lengo ni kuhakikisha mambo yanaenda nai tuna wajibu wa kupambana kama anavyofanya Mheshimiwa Rais lengo likiwa kuwahudumia wananchi na kuwapatia haki zao watumishi.” Alisisitiza Dakawa

Naye mwakilishi wa vyama vya wafanyakazi ambaye ni Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma Bwana Mchenya John alisema kuwa baraza la wafanyakazi ni chombo muhimu cha maamuzi kwa halmashauri na kuwataka wajumbe wa baraza kuacha uoga na kujadili mambo yatakayowasaidia kuendesha halmashauri na maslahi ya watumishi.

“Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kulitolea maamuzi suala la kikokotoo kwani liliwakatisha taama sana wafanyakazi na nilishakuja hapa mwaka jana nikapata fursa ya kuongea na wafanyakazi na nashukuru walinielewa na kuwa watulivu wakati wote wa mpito hadi Mheshimiwa Rais alipolitolea maamuzi.”Alimaliza Bwana Mchenya.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kondoa Andrea Mwani akiongea wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Mji wa Kondoa. 
Wajumbe wa baraza la wafanyakazi Kondoa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa baraza hilo.

MUIGIZAJI MKONGWE SALOME NONGE ( MAMA ABDULI) AFARIKI DUNIA.

$
0
0
Muigizaji Mkongwe Salome Nonge (Mama Abduli) enzi za uhai wake.

TANZANIA DRAMA & FILM ACTORS ASSOCIATION (TDFAA)

TAARIFA KWA WAIGIZAJI(M) ( KINONDONI /UBUNGO)

Kamati ya Matukio Maadili na mikataba 
Inawajulisha waigizaji wote .wadau wa filamu na wa Tanzania,Kuwa Muigizaji Mkongwe Salome Nonge (Mama Abduli).

Amefariki mchana huu nyumban kwakeMbrahati na msiba upo hapo taratibu za Mazishi tutawajulisha baada ya kikao

Asante.

Imetolewa Leo tar 25/Jan/2019
Masoud kaftany
Afisa Habari , Chama cha waigizaji TDFAA (M) Kinondoni / Ubungo

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-AMEN

TDC GLOBAL LAUNCH AND INVESTMENT CONFERENCE


WATUMISHI WA UMMA MSIWEKE VIKWAZO KWA WAFANYABIASHARA WA MIPAKANI– PROFESA KAMUZORA

$
0
0

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Profesa Faustine Kamuzora akizungumza na  na baadhi ya  wavuvi katika mwalo wa Kabindi Kashenye   wakati wa ziara yake Wilayani Missenyi.

Na Sylvester Raphael
“Mipaka kati ya nchi moja na nyingine ni fursa ya kiuchumi kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo wakifanya biashara kulingana na masoko yaliyopo katika nchi hizo. Wananchi wanaoishi katika mipaka wanatakiwa kutumia mipaka kufanya biashara na kutajirika kwa kufuata sheria za nchi na jukumu letu Serikali ni kuhakikisha wananchi hawa wananufaika na siyo kuwa kikwazo kwao na mipaka kuonekana si mahala pazuri pa kuishi.”

Msistizo huo ulitolewa na Profesa Faustine Kamuzora Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera wakati akitembelea mipaka ya Tanzania na Uganda iliyopo Mkoani Kagera Wilayani Missenyi (Kabindi- Kashenye, Mtukula na Bugango) pia Murongo Wilayani Kyerwa Januari 22 hadi 23, 2019 alipokutana na wananchi na watumishi katika mipaka hiyo ili kuona namna bora ya wananchi wanaoishi mipakani wanavyoweza kunufaika na mipaka hiyo huku Serikali ikiwawekea mazingira mazuri ya kibiashara.

Hii ni kutokana na uongozi wa Mkoa wa Kagera kuweka azma ya mwaka 2019 kuwa mwaka wa kodi kwa wafanyabiashara wote wakubwa na wadogo kuhakikisha wanalipa kodi stahiki na rafiki ambayo itawafanya kuendelea kufanya biashara zao na kunufaika. Katika hali hyo Profesa Kamuzora anasema lazima Serikali  kuyajua matatizo wanayokumbana nayo wafanyabiashara na kuyafanyia kazi ili wananchi wanufaike na fursa zilizopo katika mazingira yao.

Mara baada ya kutembelea Mwalo wa Kabindi Kashenye Wilayani Missenyi mpakani mwa Tanzania na Uganda upande wa Ziwa Victoria na kuongea na wananchi wa Mwalo huo ambao ni wavuvi walimweleza Profesa Kamuzora kuwa kuna shida ya soko la samaki wakati mwingine viwanda vilivyopo Bukoba vinapata samaki wa kutosha na havinunui samaki wao jambo ambalo linawatia hasara au kulazimika kuuza samaki kwa bei ndogo wakati katika nchi jirani ya Uganda kuna soko zuri la samaki na kwa bei nzuri lakini hawaruhusiwi kuuza huko.

Profesa Kamuzora baada ya kusikilza kilio chao aliwaeleza kuwa ndiyo maana alimua kutembelea mipaka ili aone changamoto zilizopo ili Serikali iweze kuzifanyia kazi ambapo alisisitiza kuwa maana ya kuwa mpakani unatakiwa kucheza na fursa za nchi zote mbili ili utajirike. Profesa Kamuzora aliwaeleza wavuvi hao kuwa Serikali itaangalia namna bora ya kuona nchi jirani Uganda kama kuna bei nzuri ya samaki wavuvi waruhusiwe kuuza huko kwa kufuata sheria na kulipa ushuru wa Serikali lakini pia kutoa  changamoto katika viwanda vya ndani ili vitoe bei nzuri kwa wavuvi.

Pia Profesa Kamuzora alisisitiza kuwa wananchi wanaokaa mipakani wanatakiwa kunufaika na mipaka hiyo kwani likitokea jambo baya mfano vita au magonjwa wao ndiyo wa kwanza kudhurika tofauti na katikati mwa nchi kwa hiyo ni vizuri hata fursa za biashara ziwanufaishe kwani wananchi hao ni ndugu bali mipaka iliwekwa tu Wakoloni lakini bado wao wana mahusiano makubwa.

Katika hatua nyingine Profesa Kamuzora alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kupima viwanja haraka iwezekanavyo katika eneo la Kabindi Kashenye ili kuwe na mji uliopangika na wananchi hasa wanaojihusisha na uvuvi katika eneo hilo waweze kuwa na makazi bora lakini pia na wawekezaji ambao wangependa kuwekeza katika eneo hilo wakute viwanja vilivyopimwa ili paweze kuchangamka kama upande wa pili wa nchi jirani Kasensero.

Profesa Kamuzora akiwa katika mpaka wa Mtukula ambapo alipata fursa kuongea na watumishi wa idara zote za Serikali zinaotoa huduma katika mpaka huo aliwaeleza watumishi hao kuwa wanatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wananchi wanaojishughulisha na biashara katika mpaka huo bali wawe wabunifu katika kazi zao na kutekeleza sheria lakini wakiongozwa na busara kubwa katika kutatua changamoto mbalimbali za kuwasaidia wananchi kutumia fursa ya mpaka kufanya biashara.

“Sisi watumishi wa umma tusiwe kikwazo kwa watu wetu kuwa mpakani ni fursa kubwa ya wananchi wetu kutajirika, ukienda nchi nyingine wananchi wa mipakani ndiyo matajiri kwasababu wamepewa fursa ya kufanya biashara katika pande zote mbili lakini kwa kuzingatia matakwa ya sheria. Sisi tuwe mwangaza na njia kwao badala ya kuwa vikwazo ili tuinue uchumi wao.” Aliwaasa watumishi wa Mtukula Profesa Kamuzora

Aidha, Profesa Kamuzora alisema kuwa baada ya kutembelea mipaka hasa Mtukula, Bugango na Murongo changamoto kubwa aliyoiona ni upande wa pili wa nchi jirani Uganda wafanyabiashara kuchangamkia fursa karibu na mipaka kwa kuanzisha miji na vituo vya biashara wakati huku upande wa Tanzania kukiwa hakuna kilichoendelezwa na kupelekea Watanzania kunufaisha wenzao wa nchi jirani kwa kununua bidhaa huko.

Profesa Kamuzora anasema kuwa kunatakiwa kufanyanyika upembuzi wa kina kuona kwanini nchi jirani wanatambua fursa za mipaka lakini sisi upande wa Tanzania bado.  Mfano Mtukula maduka ya bidhaa mbalimbali yapo upande wa pili wakati huku Tanzania hakuna, hivyo hivyo Bugango Waganda wana maduka makubwa ya bidhaa lakini Tanzania hakuna na Murongo upande wa Uganda Kikagati kuna mji wa kibiashara lakini Tanzania hakuna, mipaka yote Watanzania wanavuka kutafuta manunuzi nchi jirani.

Profesa Kamzora akiongea na watumishi na Viongozi mbalimbali katika Wilaya hizo mbili za Missenyi na Kyerwa alisema kuwa kuna haja ya Serikali kuangalia upya mifumo ya kodi pia kufanya utafiti kwanini wenzetu wanapata fursa ya kufungua biashara mipakani lakini Watanzania hawafanyi hivyo wakati mwingine wanakwenda kufungua biashara upande wa nchi jirani lakini si upande wa Tanzania.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mipakani aliokutana nao Profesa Kamuzora walimweleza kuwa upande wa nchi jirani Uganda kodi zao ni nafuu katika kufungua biashara ukilinganisha na Tanzania na ndiyo maana maduka na biashara zianaanzishwa upande wa pili kuliko upande wa Tanzania. Pia walimweleza kuwa katika upande wa Tanzania mipakani Miundombinu kama umeme maji na pengine barabara nzuri za rami zilicheleweshwa kufika katika mipaka hiyo jambo ambalo linakwamisha sana kibiashara.

Vilevile wafanyabisaha walimweleza Profesa kamuzora kuwa upande Tanzania kuna mamlaka nyingi ambazo zinasimamia sheria zinazofanana na kuleta usumbufu mkubwa kwao mfano TFDA, TBS na nyinginezo ambazo kama zingepunguzwa au kuunganishwa majukumu yake ingeweza kuondoa usumbufu na Watanzania wakaweza kufungua au kuwekeza  kibiashara katika upande wa Tanzania.

Profesa Kamuzora aliwashauri viongozi na Watendaji wa Halmashauri za Wilaya zilizopo mipakani  kuona namna bora ya kuzibaini na kuzichambua chanagamoto mbalimbali zilizopo mipakani na kuishauri Serikali kwani wao ndiyo wanaishi katika maeneo husika kuliko viongozi waliopo Dodoma na Dar es Saam ili changamoto hizo zifanyiwe kazi kulingana na uhalisia.

“Mimi nashauri Mkuu wa Wilaya Pamoja na Wakurugenzi mliopo mipakani kukaa chini na kuzichambua changamoto hizi na kutuletea Mkoani ili nasi tuzipeke mahali panapohusika Serikali ni sikivu itazifanyia kazi. Mfano huwezi kuelewa mpaka ufike huku hata mimi nikiwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu nilikuwa napokea mengi lakini baada ya kufika huku na kujionea ndiyo nimeelewa zaidi. Ibueni nyinyi tuleteeni mkoani ili tuyasukume ili sheria zifanye kazi kulingana uhalisia.” Profesa Kamuzora alisistiza

Profesa Faustine Kamuzora aliyeteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera tarehe 8 Januari, 2019 na kuapishwa Januari 9, 2019 aidha, aliripoti Mkoani Kagera tarehe 10, Januari, 2019 anasema baada ya kukabidhi ofisi sasa ameanza kazi rasmi Mkoani Kagera lakini akianza na kujifunza kwa kupitia mipaka na kuona changamoto zake na kuona namna bora ya kuweka ustawi wa wananchi katika kufanya biashara zao bila bughudha.

IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA YATAKIWA KUFUATILIA UTUNZAJI WA NYARAKA KWENYE TAASISI ZA UMMA

$
0
0
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa imetakiwa kufanya ufuatiliaji wa utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu katika taasisi zote za umma kwa lengo la kuondoa tatizo la uvujaji wa siri za serikali.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dodoma, yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu kwa kina majukumu ya idara hiyo na kujiridhisha namna idara hiyo inavyotekeleza majukumu yake ya kila siku.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ndiyo inayohusika na masuala yote ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka hivyo inatakiwa ijiwekee utaratibu wa kufanya ufuatiliaji wa namna ya nyaraka zinavyotunzwa na kushauri namna bora ya utunzaji wa nyaraka hizo.
“Tujenge tabia ya kufanya ufuatiliaji wa Miongozo tunayoitoa ili kuona kama inatekelezwa inavyotakiwa kwani tusipofanya hivyo taasisi zinafanya inavyotaka na matokeo yake ni kuvuja kwa siri za serikali,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amemtaka Mkurugenzi wa idara hiyo kuwa mkali na kuchukua hatua za kinidhamu kwa taasisi zote za umma zinazoshindwa kutekeleza ipasavyo jukumu la utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka na hatimaye kusababisha siri za serikali kuvuja. 
Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameipongeza idara hiyo kwa kutumia njia za kisasa za TEHAMA katika kutunza kumbukumbu na nyaraka na kuwataka kuongeza kasi ya kuzihifadhi nyaraka hizo kidigitali ili kuimarisha usalama wake.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi ameyataja majukumu ya idara yake kuwa ni pamoja na kuweka mifumo ya utunzaji kumbukumbu na nyaraka katika taasisi za umma, kutoa ushauri juu ya utunzaji bora wa kumbukumbu na nyaraka na kuratibu mipango ya kutunza na kuhifadhi kumbukumbu muhimu katika taasisi za umma, kuweka na kusimamia viwango vya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka katika taasisi za umma.
Bw. Msiangi ameendelea kutaja majukumu mengine kuwa ni kukusanya na kuhifadhi nyaraka zenye umuhimu kitaifa ili kulinda urithi andishi wa nchi yetu, kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Miongozo ya kutunza na kuteketeza kumbukumbu katika taasisi za umma, kufanya tathmini ya kumbukumbu tuli (majalada yaliyofungwa) ili kutambua majalada yenye umuhimi wa kudumu kwa ajili ya kuyahifadhi, kuhifadhi nyaraka kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kurahisisha upatikanaji na kulinda nakala halisi na kukusanya, kutunza na kuhifadhi kumbukumbu za vitu vya Waasisi wa Taifa.  
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ilianza kutekeleza majukumu yake kama idara inayojitegemea kuanzia mwezi Julai, 2015 baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne kupitisha muundo wa Idara tarehe 12 Februari, 2015. Hata hivyo idara hii inaanzia mwaka 1963 wakati Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipotoa Waraka Na.7 wa Mwaka 1963 ulioelekeza kutunza, kuhifadhi na kuteketeza nyaraka za Serikali.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipata ufafanuzi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi kuhusu mifumo ya TEHAMA inavyofanya kazi katika utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka alipofanya ziara ya kikazi kuhimiza uwajibikaji katika idara hiyo jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishiriki kutoa nakala ya nyaraka ili kuihifadhi katika mfumo wa TEHAMA alipofanya ziara ya kikazi katika Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji. Anayemsaidia kutoa ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya kumbukumbu na nyaraka zilizohifadhiwa katika majalada kwa ajili ya rejea ya kiofisi alipofanya ziara ya kikazi katika Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji jijini Dodoma. 
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipata maelezo kutoka kwa  Mtunza Kumbukumbu Msaidizi, Bi. Joyce Maro juu ya kumbukumbu zilizohifadhiwa katika Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa alipofanya ziara ya kikazi katika Idara hiyo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji jijini Dodoma.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza namna bora ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka za serikali ili kuondokana na tatizo la uvujaji wa siri za serikali alipofanya ziara ya kikazi kuhimiza uwajibikaji katika Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa alipofanya ziara ya kikazi kuhimiza uwajibikaji katika idara hiyo jijini Dodoma.

BANDARI YAIFUNGA SIMBA NA KUTINGA FAINALI YA SPORTESA

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

TIMU ya Simba imekubali kichapo cha goli  2-1 toka kwa timu ya Bandari ya nchini Kenya kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Sportpesa.

Mechi hiyo ya nusu fainali ya kwanza ulikuwa n baina ya Bandari ya Kenya na Simba ambao mpaka dakika 90 mchezo huo unamalizikaBandari walifanikiwa kutinga hatua ya fainali.

Mchezo ulianza kwa Simba kuandika goli la kwanza katika dakika ya 44 kupitia kwa mshambuliaji wake wa Kimataifa Meddie Kagere na kuipeleka Simba mapumziko wakiwa kifua mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Bandari kutafuta goli la kusawazisha na katika dakika ya 58 Bandari wanapata penati inayofungwa na mchezaji William Wadri   na kupelekea matokeo kuwa 1-1.

Kwenye dakika ya 72, mchezaji Lugogo aliyeingia kwenye kipindi cha pili anaiandikia Bandari goli la pili akimalizia mpira ulipanguliwa na kipa Aishi Manula baada ya kupigwa Kona.

Mpaka dakika 90 zinamalizika Simba wanakuwa wameondolewa kwenye hatua ya nusu fainali na kwa sasa watakuwa wanasubiri timu itakayotolewa kwenye nusu fainali ya pili baina ya Mbai Fc na Kariobang na kucheza nae mshindi wa tatu.

Nusu fainali ya  michuano ya Sportpesa itachezwa siku ya Jumapili katika Uwanja wa Taifa ikifuatiw ana fainali itakayoanza majira ya saa 10 alasiri na mshindi wa mchezo huo atakutana na timu ya Everton ya Uingereza sambamba na kitita cha dola 30,000.
 Mchezaji wa timu ya Bandari William Wodry akijaribu kumtoka kiungo wa Simba James Kotei katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Sportesa iliyomalizika kwa Simba kuondolewa kwa jumla ya goli 2-1.
 Beki wa kati wa Simba Pascal Wawa akiwa amemtoka mchezaji wa Bandari Abdalla Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Sportesa iliyomalizika kwa Simba kuondolewa kwa jumla ya goli 2-1.



Golikipa wa Simba Aishi Manula akiwa ameruka juu na nkuudaka mpira uliokuwa umeelekzwa langoni mwake katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Sportesa iliyomalizika kwa Simba kuondolewa kwa jumla ya goli 2-1.


Wachezaji wa Bandari wakishangilia baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya fainali kwa kuwafunga Simba goli 2-1.

JAJI MKUU AWATAKA WASAJILI WA MAHAKAMA NCHINI KUHAKIKISHA KESI ZOTE ZENYE DOSARI HAZIINGI KWENYE MFUMO WA MAHAKAMA

$
0
0
Na Karama Kenyunko globu ya Jamii. 
JAJI Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma amewataka wasajili wa mahakama zote nchini kuhakiksha kesi zenye dosari haziingii kwenye Mfumo wa mahakama yoyote hapa nchini.

Profess Juma, ameyasema hayo leo Aprili 25.2019 Jijini Dar e Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhudu maadhimisho ya wiki na siku ya sheria nchini, Ambayo hufanyika kila mwanzoni mwa mwaka yanayoashiria kuanza rasmi kwa mwaka wa Mahakama. 

Amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu Mahakama ya Rufaa pamoja na mahakama Kuu kutupilia mbali mashauri mbalimbali yanayopelekwa ambapo amebainisha kuwa hali hiyo inatokanana  na dosari zinazojitokeza kwe kesi hizo.

Amesema, watu wengi wanalalamikia Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu kutupilia mbali Mashauri kwa sababu ya dosari zinazojitokeza na kujiuliza kama Mahakama haiko makini ama la.

Muhimbili wa mahakama upo wazi sana, kila kitu tunachokifanya kinapimika, unapofungua kesi unapewa muda wa kujibu, unaleta mashahidi, kesi inarekodiwa, hukumu inatolewa,"Hatupendezwi na malalamiko ya jumla jumla kwani kuna mfumo wa kupokea malalamiko, sisi tupo wazi na 

Huwezi kuwazuia Wanasiasa wasizungumze ndio kazi yao, sisi tunafanya kazi kimya kimya na ukitaka majibu utayakuta katika nyaraka" amesema Jaji Profesa Juma.Aidha amemsifu Msajili aliyesimama kidete kukataa kusajili kesi yenye dosari, nampongeza kwa ujasiri, tuna Majaji wachache hatutaki kuwapangia kesi nyingi kisha wazifute" amesema Jaji Mkuu. 

Kwa upande mwingine, aJi profesa Juma amewata wananchi ambao wamezoea kubeba mabango ya malalamiko, siku kilele cha wiki ya sheria waache kufanya hivyo na badala yake watumie wiki ya sheria kutafuta suluhu ya malalamiko hayo,ambayo mwaka huu Kitaifa itafanyikia jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square kuanzia Januari 31 na kuitimishwa Februari 6.2019 jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamuhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya kilele hicho ambacho kauli mbiu yake itakuwa ni, Utoaji wa Haki kwa wakati: wajibu wa Mahakama na wadau.

Pamoja na mambo mengine Jaji Profesa Juma amesema mashauri mengi ya kesi yanachelewa kumalizika kutokana na uelewa mdogo wa wannchi ikiwa ni pamoja na kutokufahamu miongozo ya mashauri mbalimbali paomja na haki zao.

Achilia mbali hayo pia amebainsha mafanikio ambayo wameweza kuyapata tofuati na miaka mingine ikiwa ni pamoja na kuanzisha matumizi ya usajili wa mashauri kwa njia ya elektroniki huku akisema kuwa licha ya njia hizo bado kasi ya mawakili kisajili mashauri bado ni ndogo
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani).
Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. John Kahyoza (kushoto) na Mtendaji wa Makhakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha (Kulia) wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Maadhimisho ya Wiki na Siku ya Sheria nchini.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akizungumza wakati wa Mkutano wa Jaji Mkuu na Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki na Siku ya Sheria nchini.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari wakati wa mkutano kati yao na Jaji Mkuu wa Tanzania.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati akizungumza wakati wa Mkutano huo. Kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi.

Tanzania yashinda Tuzo Maonesho ya Kimataifa ya Utalii, India

$
0
0

Picha ya pamoja ya washiriki baada ya kupokea Tuzo ya ushindi wa kwanza kwa upande wa Banda bora la maonesho lilipambwa kwa unadhifu na kuvutia watu wengi [The Winner of Best Decoration Award] katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Mwaka 2019 Jijini Mumbai, India tarehe 25 Januari, 2019. 
Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Utalii wa India, Mhe. K. J. Alphons akiwa katika banda la Tanzania. Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akiwa na washiriki wengine katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Mwaka 2019 Jijini Mumbai, India tarehe 23 Januari, 2019
Wageni mbalimbali wanatembelea banda la Tanzania ili kupata maelezo kuhusu vivutio vya utalii nchini. 
Wageni katika banda la Tanzania wakipata maelezo kuhusu fursa na vivutio vya utalii nchini. 


Ubalozi wa Tanzania, New Delhi, Taasisi za Serikali na kampuni binafsi mbalimbali za utalii nchini zimeshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Mwaka 2019 nchini India yajulikanayo kama OTM 2019 [Outbound Travel Mart-2019] kwa lengo la kutangaza na kutafuta fursa mpya za soko la utalii nchini humo.

Maonesho hayo maarufu na makubwa kabisa katika ukanda wa Asia-Pasifiki yalianza tarehe 23 Januari, 2019 na yamemalizika leo tarehe 25 Januari, 2019, Maonesho haya hufanyika kila mwaka katika Jiji la Mumbai na kushirikisha taasisi mbalimbali za utalii duniani.

Taasisi za Serikali zinazoshiriki ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Kituo cha Kutangaza Utalii wa Zanzibar India [Zanzibar Tourism Promotion Centre]. Kwa upande wa kampuni binafsi ni Leopard Tours, Zara Tours, Ngarawa Hotel and Resort, DOTCOM Safaris Ltd na Jackal Adventures.

Katika Maonesho hayo, Banda la Tanzania limeibuka Mshindi wa Kwanza kwa upande wa Banda bora lilopambwa kwa unadhifu na kuvutia watu wengi [The winner of Best Decoration Award].

Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda amesema kuwa maonesho hayo ni fursa adhimu kwa nchi kutangaza vivutio vya utalii ambapo wafanyabiashara wapatao 15,000 wanaojishughulisha na masuala ya utalii walishiriki kutoka katika mataifa zaidi ya 50 duniani. Washiriki wamepata fursa ya kupeana taarifa muhimu kuhusu mwelekeo na maendeleo ya biashara ya utalii katika maeneo mbalimbali duniani, vivutio vipya pamoja na kufanya biashara.

Akiwa katika maonesho hayo, Balozi Luvanda alieleza kuwa maonesho yalisaidia washiriki kukutana na wadau na kuanzisha uhusiano wa kibiashara unaotarajiwa kufungua soko la utalii nchini baada ya wadau hao kupata maelezo ya kutosha kuhusu vivutio vilivyopo nchini na faida zake. Kwa ujumla, India ina soko kubwa la utalii. Tunategemea idadi ya watalii kutoka India wanaokwenda Tanzania itaongezeka mara dufu baada ya kuanza kwa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania [Air Tanzania] moja kwa moja kutoka Tanzania kuja India ambapo zinategemewa kuanza kabla ya mwezi wa Juni 2019.

‘Nachukua fursa hii kwa dhati kuwapongeza sana Maafisa wote walioshiriki katika Banda letu la Tanzania la Maonesho kwa kazi nzuri iliyowezesha ushindi huo wa kwanza kwa upande wa Banda bora lilopambwa kwa unadhifu na kuvutia watu wengi [The winner of Best Decoration Award]”, alisema Balozi Luvanda.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
25 Januari 2019
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images