Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAANZA KUTUMIA MFUMO MPYA WA SERIKALI GePG


MAONESHO YA PICHA ZA HABARI DUNIANI YAZINDULIWA LEO ALIANCE FRANCAIS JIJINI DAR

0
0
 Mtayarishaji wa Mashindano ya upigaji picha kutoka World Press, Sophie Boshouwers akizumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kabla ya kufunguliwa Maonesho ya Picha Duniani katika Ukumbi wa Aliance Francai's
Mkuu wa Idara ya Mission katika Ubalozi wa Falme za Uholanzi nchini,Lianne Houben akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Maonesho kwa siku ya wapiga picha za Habari Duniani yanayofanyika leo Aliance Francai's
Kaimu Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Hbari Wanawake(TAMWA),Davis Lumala akiongelea ushiriki wa TAMWA katika Maonesho hayo kabambe
Mkurugenzi wa kituo cha Utamduni cha watu wa Ufaransa nchini Tanzania,Aliance Francais ,Frederic Tiberti akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kituo chake kujihusisha na Maonesho mbalimbali.
 Mtayarishaji wa Mashindano ya upigaji picha kutoka World Press, Sophie Boshouwers akitoa maelezo kwa moja ya waandishi wa Habari


TAKUKURU YAIOMBA MAHAKAMA KWENDA GEREZANI KUMHOJI MTUHUMIWA ALIYEISABABISHA SERIKALI HASARA YA BILIONI MBILI

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwenda gerezani kumuhoji mshtakiwa Alloyscious

Mandago katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni mbili inayomkabili yeye na wenzake wanne.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa Mandago anashtakiwa pamoja na mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takriban Sh. Milioni saba kwa dakika, Mohamed Yusufali.

Wakili wa Serikali kutoka Takukuru Leonard Swai Maombi hayo amewasilisha maombi leo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa. 

Wakili Swai alidai, wapo hatua za mwisho za kukamilisha taarifa ili kuwasomea washtakiwa maelezo ya mashahidi(Commital). pia aliiomba mahakama kumuhoji mshtakiwa huyo akiwa gerezani.

Mahakama imeridhia mshtakiwa huyo kuhojiwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 8, mwaka huu itakapikuja kwa ajili ya kutajwa. Mbali na Yusufali na Mandago washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni 

Isaack Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif ambapo wanakabiliwa na mashtaka 39 likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni mbili. 

WAKULIMA KAPUNGA WAMPIGIA MAGOTI RAIS Dkt MAGUFULI,WAMWOMBA KUINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI NA UVAMIZI WA MASHAMBA

0
0
  WAKULIMA wa kijiji cha Kapunga kilichopo wilaya ya Mbarali mkoani mbeya wameiomba Serikali kuingilia kati kuwaondoa kwa nguvu wavamizi wa mashamba yao na maeneo ya kijiji chao kinyume cha sheria.

Wamesemaa kuwa mashamba hayo ambayo wanayamiliki kiharali yamevamiwa na taasisi inayotambuliwa kama umoja wa wakristo Tanzania UWATA kinyume na taratibu na kusababisha uwepo mgogoro kati yao na wananchi wa kijiji cha kapunga.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii jana wilayani humo kwaniaba ya wenzake mmoja wa wahanga wa mashamba hayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM tawi la Mapogolo Kapunga Sekelaga Sandube alisema kuna umuhimu wa serikali kuu kuingilia kati kwani serikali ya mkoa na wilaya pamoja na juhudi kadhaa kuchukuwa lakini imeshindikana wavamizi kuondoka.

Amesema awali baada ya wavamizi hao kuingia walilipoti ofisi ya kijiji cha kapunga na baadae wilayani ambapo kote huko viongozi mbali na kushughulikia tatizo hilo lakini wameshindwa kuwaondoa wavamizi hao hali iliyosababisha wao kushindwa kuendelea na kilimo katika maeneo hao.

"Ndugu Mwandishi mgogoro umechukua miaka zaidi ya 10 na tumehangaika katika ofisi zote za serikali kwa maana kijiji hadi mkoa na mbaya tumefika hadi kwa Waziri mwenye dhamana na ardhi na kutoa maagizo kwa maandishi ya kuelekeza kuondolewa kwa wavamizi hao mara moja lakini viongozi wa wilaya wameshindwa kutekeleza agizo hilo hadi sasa. "alisema Sandube

Nakuongeza kuwa kutokana na viongozi kushindwa kutekeleza maagizo ya waziri na ofisi ya serikali ya mkoa ndio maana tunaiomba serikali kuu hususani mh Rais Dkt John Magufuli kumaliza mgogoro huo.

Akizungumzia chanzo cha uvamizi wa maeneo hayo Sandube amesema kwa makusudi huku wakiwa wanajuwa wanachokifanya ni kinyume cha sheria ardhi ya vijiji sura 114 ya 2002 uongozi wa serikali ya kijiji cha Ukwavila uligawa maeneo ya kijiji cha kapunga na kusababisha migogoro inayoendelea hadi sasa.

Naye Katibu wa umoja wa kilimo cha umwagiliaji Mpunga mmoja (SKIMU) Emmanuel Mwansanga Alisema mgogoro huo umewsatori kutokana na miundombinu kuharibiwa zikiwemo mbegu ambazo zilikuwa zimepandwa kwa ajili ya maandalizi ya kilimo cha msimu huu.

" Jumla ya hekari 62 ambazo ni mali ya sisi kama wakulima na zaidi ya heri 600 ambazo ndani yake zilitakiwa zigawiwe kwa vijana wa kijiji. nazo zimevamiwa."Amesema Mwansanga

Aliongeza kuwa hekari hizo 600 zilitengwa kutona na maagizo ya Rais Dkt Magufuli aliyoyatoa mwaka 2016 kupitia Waziri William Lukuvi nakwamba nazo zimevamiwa huku viongozi wakishndwa kusimamia maagizo yaliyotolewa.

Kwaupande wake Mtendaji wa kijiji cha Kapunga Jackson Mbilinyi alikiri kuwepo kwa uvamizi huo na migogoro ya ardhi nakwamba wao kama viongozi walijaribu kushughulikia tatizo.

Kwaupande wake Daimon Simwandiya ambaye anadaiwa ni mmoja wa wavamizi wa mashamba hayo akizungumza kwa njia ya simu alisema wao waliyapata maeneo hayo kihalali mwaka 2002 na wakapewa hati ya kimila 2013.

Alipoulizwa kwanini Serikali ya kijjji cha Ukwavila ikawape mashamba kwenye kijiji cha Kapunga amesema wao ni watanzania wanahaki ya kulima popote hata Dar es Salaam wanaweza wakalima.

Naye mkuu wa Wilaya ya Mbarali akizungumzia sakata hilo alisema hana taarifa mgogoro wa uvamizi na kama hao watu waende ofisni kwake.

"Mimi sina taarifa hiii kwamba kuna mgogoro na anachofahamu yeye kwamba kulikuwa na mgogoro wa mpaka ambao mkuu wa mkoa wa mbeya alishaumaliza "amesema Mkuu huyo wa wilaya.
 
Mwenyekiti wa CCM tawi la Mapogolo Kapunga Sekelaga Sandube  

Tutasimamia na kutekeleza maagizo ya viongozi katika sekta ya Madini-STAMICO

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Shirika la Taifa la Madini (Stamico) limesema kuwa litaendelea kusimamia sekta ya madini katika kutoa utaalam kwa wachimbaji wadogo katika kuhakikisha wanakua ikiwa ni pamoja kuongeza Pato la Taifa.

Akizungumza katika katika mahojiano na Michuzi Blog katika Mkutano wa Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam ,Kaimu Mkurugenzi wa Uchorongaji na Utafiti Alex Rutagwelela amesema kuwa Stamico iko wazi katika kuhudumia wachimbaji wa Madini wadogo masaa 24.

Amesema kuwa wana mtambo wa uchorongaji ambapo wachimbaji wadogo ni wakati mwafaka wa kutumia kwa gharama nafuu.

"Wachimbaji wa madini wadogo watumie shirika lao katika ushauri ili kuweza kuchimba kisasa na kuchimba kimazoea wa bila mafanikio" amesema Rutagwelela.

Rutagwelela amesema kuwa mkutano wa Madini ulikuwa na maelekezo ya viongozi wakuu wa nchi hivyo kazi yetu ni kutekeleza maagizo ili sekta ya madini iwe nguzo ya uchumi kutokana na rasilimali zilizopo ziendelezwe kwa maendeleo.

Aidha amesema kuwa Stamico imekuwa ikitembelea wachimbaji wadogo wa madini kuwataka kushirikiana katika kuwapa ushauri.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC)Dkt. Samuel Gwamaka amesema kuwa suala uchimbaji wa madini linakwenda na mazingira.

Amesema kuwa mazingira ndio yanamzunguka mwanadamu hivyo lazima yalindwe na kusimamiwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico) Alex Rutagwelela akizungumza na waandishi habari katika mkutano wa Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza kuhusiana na Baraza hilo katika usimamiaji wa Mazingira katika Sekta ya madini katika mkutano wa Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico) Said Mtuwa akitoa maelezo kwa wadau wa Madini walipotembelea sehemu ya maonesho ya mkutano wa Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAJUMBE WA BODI YA MISHAHARA NA MASLAHI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi  katika Utumishi wa Ummam, kwenye  Makazi ya Waziri Mkuu jiji Dar es salaam, Januari 24, 2019. Kutoka kushoto ni  Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula, Mjumbe wa Bodi, George Mlawa na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya  Mishahara na Maslahi  katika Utumishi  wa Umma, George Mlawa baada ya mazungumzo na wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 24, 2019. Wengine kutoka kushoto ni  Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WANANCHI WAVAMIA HIFADHI ZA MISTU NA KUENDESHA UHARIBIFU

0
0
 NA TIGANYA VINCENT
TAMKO lilitolewa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kuruhusu baadhi ya vijiji na vitongoji vilivyopo katika maeneo ya hifadhi vitambulike rasmi limetafasiri vibaya mkoani Tabora na baadhi ya wananchi kwa kuanza kuvamia na kulima na kuchunga mifugo katika maeneo ya Hifadhi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa Wakala wa Huduma  za Mistu Tanzania Kanda ya Magharibi Valentitne Msusa wakati uzinduzi wa kampeni ya upandaji  miti  Mkoa wa Tabora yenye la kuhifadhi mazingira ya kuifanya Tabora kuwa ya kijani. Alisema  kuanzia wiki iliyopita makundi ya yameingia kutoka mkoa wa Singida na kuvamilia mistu ya Uyui, Igombe Mkuu na Mistu ya Fila na wengine wameingia na kuanza kuandaa mashamba mapya kwa ajili ya kilimo.

Msusa alisema kuwa Rais hakuelekeza watu waingie katika maeneo ya Hifadhi ya kufyeka miti na kusema kinachoendelea ni kitendo kinachokiuka maelekezo ya Rais kwa kuwa hakusema watu wakaanzishe mashamba mapya ya ndani ya Hifadhi. “Jamii nawaomba acheni kuingia katika Hifadhi ya kuanzisha mashamba mapya hayo sio maelekezo ya Mheshimiwa Rais … kwani vitendo hivyo vinahatarisha chanzo cha maji ya Mkoa wa Tabora”alisema.

Alisema watu watakaokutwa ndani ya hifadhi wakianzisha mashamba mapya na kuendesha shughuli za ufugaji watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa wanakiuka maelekezo ya Rais na Sheria. Meneja huyo wa Kanda ya Magharibi wa TFS aliwataka watu wote ambao walishaondolewa siku za nyuma katika maeneo ya Hifadhi wasidiriki kurudi kwani watachukuliwa hatua.

Msusa aliitaka jamii kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanalinda na kuhifadhi maeneo yote ya Hifadhi za Mistu ili yasivamiwe na watu na kuendesha uharibifu. Aidha alisema TFS inatarajia  kupanda miti katika maeneo yote ya Hifadhi ambayo  uharibifu ulifanyika ikikwemo katika Wilaya ya Nzega kama mkakati wa kuhifadhi na kutunza mazingira.

Awali viongozi wa dini Mkoani Tabora wameitaka jamii kuunga mkono juhudi za Serikali za upandaji na utunzaji miti kwa ni muhimu katika ujenzi wa uchumi wa kati kuelekea ujenzi wa viwanda nchini. Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Magharibi Kati Isaac Laiser alisema kuwa upandaji wa miti ni jukumu la kila mtu na mtu anayekataa kupanda miti hamgomei Mkuu wa Mkoa bali anaigomea Serikali.

Aliongeza kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya ujenzi wa kati kuelekea ujenzi wa viwanda na utunzaji wa mazingira na kuongeza kuwa vitu vina uhusiano mkubwa. Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi alisema jambo la uhifadhi wa mazingira wananchi wote kwa kuwa ni maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwa aliumba ili wanadamu wayatunze na kuyahifadhi mazingira.

Alisema suala la upandaji miti halina dini , kabila, siasa kwa kuwa miti ni muhimu kwa watu wote. Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwaagiza viongozi kuanzia ngazi za Vitongoji hadi Mkoa kusimamia zoezi la upandaji kiti katika maeneo yao na kiongozi atakayeshindwa kutekeleza jukumu hilo atakuwa haina sifa ya kuwa kiongozi.
 Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Tabora wakiwa katika maandamano ya kuunga mkono kampeni za upandaji miti na utunzaji mazingira jana.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi akitoa maoni yake jana wakati wa kampeni za uzinduzi wa upandaji miti kwa mkoa wa Tabora kwa mwaka huu.
 Askofu wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Magharibi Kati Isaac Laiser akitoa maoni yake jana wakati wa kampeni za uzinduzi wa upandaji miti kwa mkoa wa Tabora kwa mwaka huu
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua kampeni rasmi za upandaji miti mkoani humo kwaka huu.
 Askofu wa Kanisa la Anglican Tabora Dkt. Elias Chakupewa akipanda mti kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora jana 
 Baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti mkoani Tabora wakisikiliza jana hotuba za viongozi mbalimbali.
 Meneja wa Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania Kaznda ya Magharibi Valentine Msusa akieleza jana uharibifu ambao umeanza kufanywa katika mistu ya hifadha.
Wanakwaya wa chuo cha Ualimu Tabora wakiimba wimbo maalumu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti mkoani Tabora jana.

Tanzania kufaidika na mradi wa kuzalisha takwimu zinazohusiana na Jinsia

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Izeduwa Derex-Briggs  juu ya mradi  wa kuzalisha takwimu zinazohusiana na jinsia Ofisini kwake Jijini Dodoma.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa  akifafanaua jambo kwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Izeduwa Derex-Briggs(kulia kwake )  na Mwakilishi wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN WOMEN) Bi. Hodan Addou(wa Tatu kulia) juu ya mradi  wa kuzalisha takwimu zinazohusiana na jinsia Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akiongoza kikao cha kujadili juu ya mradi  wa kuzalisha takwimu zinazohusiana na jinsia.Kikao hicho kimeudhuriwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Izeduwa Derex-Briggs(kulia kwake )  na Mwakilishi wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN WOMEN) Bi. Hodan Addou.Mradi huo wa miaka mitatu ambapo Tanzania itapata bilioni mbili ili kuzalisha takwimu zinazohusiana na jinsia.
 Wajumbe kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifuatilia kikao kati yao na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Izeduwa Derex-Briggs(kulia kwake )  na Mwakilishi wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN WOMEN) Bi. Hodan Addou ) juu ya mradi  wa kuzalisha takwimu zinazohusiana na jinsia leo  Jijini Dodoma.
Wajumbe kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifuatilia kikao kati yao na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Izeduwa Derex-Briggs(kulia kwake )  na Mwakilishi wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN WOMEN) Bi. Hodan Addou ) juu ya mradi  wa kuzalisha takwimu zinazohusiana na jinsia leo  Jijini Dodoma. Picha zote na DAUDI MANONGI, DODOMA



WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA MPONDE WILAYANI LUSHOT

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao alichokiitisha cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha Chai cha Mponde katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga kilichowajumuisha Naibu Mawaziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF na Msajili wa Hazina. Kikao hicho kilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 24, 2019. (Picha ba Ofisi ya Waziri Mkuu)

MADAKTARI BINGWA WA JKCI WAFANYA UPASUAJI KWA WATOTO WALIOZALIWA NA MATATIZO YA MOYO

0
0
Madaktari bingwa wa upasuaji wa kufungua kifua kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia upasuaji mtoto ambaye mishipa yake ya damu safi na damu chafu imekinzana kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Shirika la Healing Little Heart la nchini Uingereza wakati wa Camp maalum ya upasuaji wa kufungua kifua kwa watoto waliozaliwa na matatizo ya moyo leo katika Taasisi hiyo. Jumla ya watoto nane wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi hiyo na hali zao zinaendelea vizuri.

IDARA YA UHAMIAJI YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA KUONDOSHWA NCHINI WAHAMIAJI WALOWEZI

WAZIRI MBARAWA ATAKA MRADI WA VISIMA KIMBIJI NA MPERA KUMALIZIKA HARAKA

0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo mafupi toka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mamlaka ya Maji safi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Lydia Ndibalema (wa pili toka kushoto) juu ya mradi wa visima vya Kimbiji na Mpera uliopo Kimbiji, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa Kimbiji na Mpera Mhandisi Shiyenze (wa nne toka nne) Bunyese mara baada ya kutembelea katika kisima cha K-17, K-11 na K-3 ambavyo vipo katika hatua ya mwisho ili wananchi waweze kupatiwa maji safi na salama.
Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa wasimamizi pamoja na mkandarasi wanaosimamia miradi ya Mradi wa Kimbiji katika kisima cha K-17, K-11 na K-3 ambavyo vipo katika hatua ya mwisho ili wananchi waweze kupatiwa maji safi na salama.
Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Pro. Makame Mbarawa akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizia ziara yake ya kutembelea mradi wa Kimbiji na Mpera katika kisima cha K-17, K-11 na K-3 ambavyo vipo katika hatua ya mwisho ili wananchi waweze kupatiwa maji safi na salama. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. Waziri wa Maji na Unwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amewataka wataalamu wanaokabidhiwa majukumu kufanya kazi kwa wakati na kukamilisha miradi ili huduma zifike kwa wananchi. Ameyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa Visima 20 vya Kimbiji na Mpera vyenye jumla ya thamani ya Bilioni 23.

 Akizungumza baada ya ziara hiyo, Prof Mbarawa amesema kuwa visima 12 vya Kimbiji tayari vimeshakamilika katika uchimbaji kilichobaki ni kupima wingi wa maji na ubora wake. (Pump test) Mbarawa amesema, kwenye visima hivyo viwili vipo tayari kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi ili wapate maji safi na salama. “ Kulikua na changamoto kidogo ya Mkandarasi ila kwa sasa kila kitu kipo sawa, anayesubiriwa ni Mshauri (Consultant) kwa ajili ya kuja kushauri kuhusu upimaji wa wingi wa maji na ubora ili tuendelee na mchakato wa huduma ya maji kwa wananchi,” amesema Mbarawa. 

“Visima nane kati ya 20 vilivyopo Mpera vipo katika hatua ya Kati ya uchimbaji na nawashauri DAWASA kumaliza kwanza visima vya Kimbiji ili baadae wahamie hivyo vya Mpera, “amesema Mbarawa ameutaka uongozi wa DAWASA kuharakisha katika manunuzi na kumpata Mkandarasi ili kufikia mwishoni mwa Mei mwaka huu wananchi wa Kimbiji na Kigamboni waweze kupata maji. 

Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mamlaka ya Maji safi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Lidya Ndibalema amesema mradi huu ulikuwa na thamani ya Bilioni 23 mpaka sasa wameshatumia bilioni 17 n kikubwa kwa visima vya Kimbiji ni Mshauri (Consultant) ni kuja kutoa maelekezo katika Pump Test.

 Ndibalema amesema tayari ujenzi wa tanki la Kibada upo katika hatua ya manunuzi na wamefuata maelekezo kama tuliyoagizwa na serikali na ikishakamilika tutaanza mchakato wa kuanza ujenzi. 

 Mradi wa Kimbiji na Mpera unazalisha maji takribani milioni 250 kwa siku ikiwa ni nusu ya maji yanayozalishwa kwa Mkoa mzima wa Dar es Salaam Lita Milioni 504, na mradi huo utawanufaisha wananchi wote kwa Ukanda wa Kusini mwa Dar es Salaam yakiwemo maeneo ya Kigamboni, Kibada, Mkuranga, Temeke, Mtoni Kijichi na maeneo mengine yasiyokuwa na mtandao wa maji wa DAWASA kwa ukanda huo.

SERIKALI YATOA BILIONI 2.5 KWA AJILI YA UJENZI WA JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA

0
0
NA WAMJW-SHINYANGA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa kiasi cha shilingi bilioni 2.5 zitakazotumika katika ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, lengo likiwa ni kutoa huduma za kibingwa kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea ujenzi wa Hospitali hiyo na kukuta jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na Utawala likiwa limekamilika.

Waziri Ummy amesema fedha hizo zitafika katika Hospitali hiyo ndani ya wiki mbili ili ziweze kuchochea kasi ya ujenzi na lengo ifikapo mwezi Septemba 2019 Hospitali hiyo ianze kutoa huduma za afya.

“Ninaahidi kutoa shilingi bilioni 2.5 ndani ya wiki mbili ziweze kutumika katika ujenzi wa jengo la mama na mtoto, lengo la serikali ni kuhakikisha kila mama mjamzito anapofika Hospitalini kujifungua atoke akiwa salama yeye na kichanga chake”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amefikia uamuzi huo baada ya kupokea ripoti ya mkoa kuhusu vifo vitokanavyo na uzazi kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mfaume Rashid, ambapo kwa mwaka 2016/2017 kulikua na vifo 73, na mwaka 2017/2018 vikiwa ni vifo 56, hali ambayo Waziri huyo ameonekana kutoridhishwa nayo.

Hata hivyo Waziri Ummy ameahidi kuongeza fedha zingine kiasi cha shilingi bilioni 3 ndani ya mwezi mmoja, zitakazotumika katika ujenzi wa jengo kwa ajili ya huduma za uchunguzi ikiwemo huduma za maabara, X-ray na CT-Scan pia jengo hilo litakua na vyumba vitatu vya upasuaji.

Waziri Ummy amesisitiza ujenzi wa jengo hilo utumike wa mfumo wa Force Account ambao utahakikisha wananchi wanashiriki kwa asilimia 100 katika kufanikisha ujenzi huo na huduma za afya zianze kutolewa mapema.

Wakati huo huo, Waziri Ummy ametembelea kituo cha afya cha Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga kuona hali ya miundombinu ya kituo hicho na utoaji wa huduma za afya huku kwa kiasi kikubwa akionekana kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa majengo ya huduma mbalimbali.

Kuhusu uhaba wa watumishi wa kada za afya Waziri huyo ameahidi kutatua changamoto hiyo hali inayopelekea kuwepo kwa msongamano wa wagonjwa.

Aidha, Waziri Ummy amehitimisha ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na kuridhishwa kwa kiasi kikubwa na hali ya utoaji wa huduma za afya hasa katika jengo la huduma za mama na mtoto na pia katika jengo la kuhifadhia watoto wachanga wenye uhitaji wa uangalizi maalumu (NICU).

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ambalo limekamilika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneka na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Albert Msosela.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akioneshwa ramani ya majengo ya kituo cha afya cha Kambarage na Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Lusajo Mwakajoko wakati alipotembelea kituo hicho leo kilichopo manispaa ya Shinyanga.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto mchanga aliyezaliwa katika kituo cha afya cha Kambarage mjini Shinyanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipanda mti wa kumbukumbu katika kituo cha afya cha Kambarage kilichopo katika manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiangalia kichanga kilicholazwa katika chumba maalum cha uangalizi wa watoto mahututi na wale waliozaliwa kabla ya siku (njiti) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni daktari bingwa wa watoto Dkt. Mwita Ngutunyi.

MADAKTARI WA MAGONJWA YA MOYO WAPATA MAFUNZO YA UZIBUAJI WA VALVU YA MOYO KWA NJIA YA MTANDAO

0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA)Bw. Charles Kiondo akizungumza na daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI Dr. Tatizo Waane kulia mara baada ya kumalizika mafunzo hayobyaliyofanyika leo kwa njia ya Video katikati ni Dr. Delillah Kimambo kutoka JKCI na Dr Kilalo Mjema kutoka Hospitali ya Agha Khan na kushoto ni Katibu Mkuu Mstaafu wa Utumishi Joseph Rugiyamheto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA)Bw. Charles Kiondo akisikiliza mjadala wakati wa mafunzo kwa njia ya mtandao yaliyoendeshwa kwa pamoja na Hospitali Continental ya India pamoja na wakala hiyo yaliyofanyika jijini Dar es salaam yakishirikisha wataalam na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na taasisi zingine kulia ni Balozi Ulisubisya Mpoki na katikati ni Katibu Mkuu Mstaafu Utumishi Joseph Rugiyamheto.

...................................................................................................

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) imeendesha mafunzo ya uzibuaji valvu ya Moyo kwa njia Video na Hospitali ya Continental ya nchini India ili kubadilishana uzoefu na wataalam wa nchini.

Akizungumza katika mafunzo ya uzibuaji wa Valvu ya Moyo Mkurugenzi Mkuu wa wakala hiyo Charles Senkondo amesema kuwa katika mkutano huo watalaam wamepata uzoefu kutoka kwa Mkuu wa Cath Lab ya Hospitali ya Continental ya nchini India Profesa Bharath Purohit. Senkondo amesema kuwa tangu kuanza kwa mkutano kwa njia ya Mtandao kada mbalimbali zimepata mafunzo katika Mada zinazoandaliwa na taasisi hiyzo kwa kushirikiana na wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao TaGLA. Amesema wakala hiyo ndio inaongoza kwa nji za Afrika katika uendeshaji wa mafunzo.

Aidha amesema kuwa eneo hilo la uzibuaji valvu ya Moyo umekuwa na mwitikio mkubwa kwa upande wa madaktari wetu katika kupata uzoefu wa Hospitali ya Continental ya nchini India. Daktari Bingwa wa Moyo Dkt.Tatizo Waene amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu katika Sekta ya Afya kwa watalaam kupata ujuzi zaidi kutoka kwa wabobezi wa masuala ya magonjwa ya moyo na pia mafunzo hayo yanapunguza hata gharama za matibabu kwakuwa wataalamu wengi wanapopata mafunzo wanapata uzoefu na kufanya kazi nzuri ya kutibu wagonjwa HAYO hapahapa nyumbani.

Dr. Tatizo Waane ameongeza kuwa kuna kila sababu ya kuwa na mipango mahsusi kati ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Walala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) ili kufanya uchambuzi ulio makini na wenye tija wakati wa kuwapata washiriki wa mafunzo hayo ili kupata uwiano wa kada zote jambo ambalo litawezesha wataalam hao kupata weledi wa namna ya kukabili magonjwa ya moyo kwa uwiano mzuri
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) na Katibu Mkuu Mstaafu Utumishi Joseph Rugiyamheto wakimsikiliza Dr. Bharath Purohit kutoka Hospitali ya Continental ya india wakati akitoa mafunzo ya uzibuaji wa valvu ya moyo kwa njia ya video leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Mstaafu Utumishi Joseph Rugiyamheto akichangia jambo wakati wa mafunzo kwa njia ya video huku Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) akifuatilia mjadala huo.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya washiriki wakifuatilia mjadala huo ulifanyika kwa njia ya video.

CAF WAIONDOA ISMAILIA KWENYE MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeiondoa timu ya Ismailia nchini Misri kutokana na mashabiki wake kuwafanyia vurugu timu ya Club African Ya Tunisia.

Maamuzi hayo yamekuwa baada ya CAF kupokea ripoti ya mchezo namba 96 kati ya Ismailia na Club African uliochezwa Januari 18 mwaka huu nchini Misri ikielezea vurugu zilizotokea kwenye mchezo huo.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa mashabiki wa timu ya Ismilia walianza kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi wa mchezo huo pamoja na timu ya Club African hususani katika dakika ya 86 ya mechi hiyo.

Baada ya kushindwa kuendelea na mchezo huo kutokana na vurugu za mashabiki wa Ismailia, mwamuzi aliamua kusimamisha mchezo huo na kuzitaka timu zote kuingia vyumbani na walipelekwa wakisindikizwa na walinzi.

Katika kanuni ya 12, kifungu cha 3 kinaeleza kuwa kama mwamuzi atalazimika kusimamisha mchezo au kuumaliza basi timu iliyohusika na vurugu itahesabiwa imepoteza mechi au ikiwemo na kuondolewa kwenye michuano.

Baada ya kamati kukutana na kuipitia ripoti ya kamisaa wa mchezo huo, wamefikia maamuzi ya kuiondoa timu hiyo katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na kufuta matokeo yote kwa zile timu ambazo walishacheza nazo.

Ismailia ilikua katika kundi C wakiwa sambamba na Timu ya Tp Mazembe, Club African na Cs Constatinios na kwa sasa zinasalia timu tatu.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE KUANZA ZIARA YA KIKAZI BAADHI YA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia vazi la kiraia) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Songwe leo Januari 24, 2019 tayarri kwa ziara ya kikazi katika baadhi ya mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwemo Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi na Ruvuma.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(vazi la kiraia) akisalimiana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya mapema alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Songwe leo Januari 24, 2019 kwa ziara ya kikazi katika baadhi ya mikoa ya nyanda za juu kusini.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati vazi la kiraia) akiteta jambo na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo mara baada ya kuwasili jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mbeya, SACP. Luhende Makwaia(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya awali ya Uaskari Magereza – Kiwira, ACP. Mathias Mkama(wa pili toka kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mbeya, ACP. Lyzek Mwaseba 
. Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akisalimiana na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Chocha Peter(kushoto) alipokutananaye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Songwe leo Januari 24, 2019.

TANESCO YAPONGEZWA KWA KUIMARISHA HUDUMA ZAKE ARUSHA

0
0

Mkurugenzi kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Bw. Sailesh Pandit
Meneja Uendeshaji wa kiwanda cha Sunflag Bw. Magessa Charles(kulia), akifafanua jambo kuhusu utengenezaji wa nguo
Wafanyakazi wa kiwanda cha A -Z wakiwa kazini
Meneja Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, anayeshughulikia miradi, Mhandisi Emmanuel G. Munirabona(kulia), akizungumza na Mkurugenzi kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Bw. Sailesh Pandit.Picha zote nz Vero Ignatus




Na.Vero Ignatus, Arusha

Shirika la umeme nchini Tanzania TANESCO limepongezwa kwa kuimarisha huduma zake kwa wateja wa wakubwa na wale wa kati jijini Arusha
Akizungumza Mkurugenzi kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Bw. Sailesh Pandit amesema huduma za TANESCO zimeimarika kiasi kwamba ameshawishika kufungua viwanda vingine vitatu Jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga

“Zamani tulikuwa na shida sana miaka miwili mitatu iliyopita, power cut (kukatika kwa umeme), sasa hivi hamna ni mara chache sasa labda ikitokea kwenye gridi ya taifa hapo hatuna ha kufanya, lakini sasa hivi hatuna tatizo la umeme kabisa.” Alisema Bw. Sailesh ambaye kwa mwezi anailipa TANESCO kiasi cha kati ya shilingi milioni 500 hadi 600 kama bili ya umeme.

Akizungumzia ushirikiano wa kikazi kutoka kwa wafanyakazi wa TANESCO na kiwanda chake, Bw. Sailesh amesema, hakuwahi kuuona ushirikiano huo miaka ya nyuma ila ndio ameanza kuona hivi sasa ambapo inawatia moyo wao kama wawekezaji na kuona wanaifikia Tanzania ya viwanda

“Kwakweli sina cha kusema au kibaya chochote, namna ninavyofanya kazi nao ni very friend manner, mimi ninaweza kumpigia simu Injinia hata saa nane usiku, sina umeme ata respond simu yako hapo hapo na kuchukua hatua wakati kipindi cha nyuma haikuwa hiovyo.” Hali kadhalika uongozi wa kiwanda cha nguo Sunflag, nao umetoa pongezi kwa TANESCO kwa kusema kuwa huduma zimeboreka na kwamba kuna matatizo madogomadogo tu.

“Nina kila sababu ya kuwashukuru TANESCO kipindi cha nyuma kila mtu ni shahidi tulikuwa na matatizo kwenye eneo hili la upatikanaji wa umeme lakini pia ushirikiano haukuwa mzuri sana, lakini kwa sasa, panapotokea tatizo response ya TANESCO panapotokea tatizo ni ni very fast na very incouraging mtu atakayewanyooshea kidole itakuwa ni sababu zake mwenyewe.”

Alipongeza pia mfumo wa utoaji taarifa, ambapo hata kama kuna katizo la umeme wamekuwa wakipata taarifa mapema na wao kama kiwanda hujipanga na hivyo kuondoa usumbufu.Aidha uongozi wa kiwanda cha A to Z pamoja na kuponegza kuimarika kwa upatikanaji wa umeme, wao bado kuna wakati umeme unapungua nguvu (fluctuation) na hivyo kusababisha mitambo yao kusimama kufanya kazi

“Lakini kwa ujumla kumekuwa na maendeleo mazuri ya hali ya umeme ukilinganisha na kipindi cha nyuma, wito wetu ni kufanyia kazi mapungufu hayo,” Alisema Afisa Mterndaji Mkuu wa A to Z, Bw.Viral Shah.

Akizungumzia mapungufu hayo, Meneja Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, anayeshughulikia miradi, Mhandisi Emmanuel G. Munirabona, alisema wao kama shirika watafuatilia kwa kina kujua hasa nini chanzo cha tatizo hilo.

“Tumefanya maboresho makubwa ya mitambo yetu ikiwa ni pamoja na kupanua vituo sita vya kupoza umeme jijini Arusha, ambavyo vimewezesha wateja wakubwa kufunguwa laini zinazojitegemea ili kuondoa uwezekano wa kukatika kwa umeme na hivyo kuathiri shughuli za uendeshaji

Jiji la Arusha ni miongoni mwa miji mitatu ambayo ilikuwa kwenye mpango wa kukarabati na kuimarisha miundombinuya umeme (TEDAP), ambapo Shirika hilo lilifanya ukarabati mkubwa wa njia za kusafirisha umeme lakini pia kufanya upanuzi wa vituo vya kupoza umeme.

INTRODUCING Official Video:ACHA TULEWE - Y-TONY

INTRODUCING Proffesor Jay ft Victoria Kimani-Woman

ARUMERU YAENDELEA KUUNGWA MKONO NA WADAU,YAKABIDHIWA AWAMU YA KWANZA YA MIFUKO 100 YA SARUJI

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro  ameendelea kuungwa mkono na wadau wa Maendeleo Kwa kukabidhiwa awamu ya kwanza ya Mifuko 100 ya Saruji kutoka katika Kampuni ya Farm Acces Ltd kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi 100 Arumeru.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa saruji hiyo Ndugu Muro mbali na kushukuru Kwa msaada huo , amepongeza jitihada zinazofanywa na  kampuni hiyo ambayo bado haijaanza uzalisha wa Dawa za mifugo lakini wameweza kuchangia mifuko 100 Kwa awamu ya kwanza na kuwataka wadau wengine kuunga mkono juhudi Za ujenzi wa vyumba vya madarasa .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Dkt. Saimoni amepongeza juhudi zinazofanywa  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru chini ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli na kusisitiza kutoa msaada zaidi pindi watakapoanza uzalishaji kiwandani hapo.

Wadau hao wa maendeleo Waliahidi kuchangia mifuko 200 ya Saruji na kwa Awamu ya kwanza wamemkabidhi Dc Muro mifuko 100 ya saruji na kuahaidi ndani ya muda mfupi watamkabidhi tena Mkuu wa Wilaya mifuko 100 mingine iliyobakia.

Dc Muro anaendelea na ziara yake ya kuhamasisha, na kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule mbalimbali Za sekondari katika Wilaya ya Arumeru Kwa lengo la kumaliza changamoto ya madarasa kuanzia shule Za msingi, sekondari na kidato Cha tano na sita .
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro  ameendelea kuungwa mkono na wadau wa Maendeleo Kwa kukabidhiwa awamu ya kwanza ya Mifuko 100 ya Saruji kutoka katika Kampuni ya Farm Acces Ltd kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi 100 Arumeru.
 
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images