Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109610 articles
Browse latest View live

Ubalozi wa Ujerumani kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto.

0
0
Daktari Bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Vivian Mlawi akimweleza  Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera maendeleo ya afya ya mtoto aliyefanyiwa  upasuaji wa bila kufungua kifua na kuzibwa matundu ya moyo katika kambi   maalum ya matibabu inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo kwa watoto wa  JKCI, Israel na Ujerumani.
 Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini,  Jörg Herrera akiangalia uzibuaji wa mishipa ya moyo iliyoziba jinsi unavyofayika  katika kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Israel na Ujerumani. Jumla ya watoto 20 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua.
 Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuuguzi  Robert Mallya akimweleza Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera kuhusu mendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI, Israel na Ujerumani. Katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel Simon Fisher na kulia ni Afisa Mipango wa JKCI Vida Mushi.
 Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na wafanyakazi wa JKCI , Israel na Ujerumani mara baada ya kumalizika kwa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo ili kuona maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI, Israel na Ujerumani. Jumla ya watoto 20 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua.
Balozi  Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo ili kuona maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI, Israel na Ujerumani. Jumla ya watoto 20 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua katika kambi hiyo ya siku tano.Picha na JKCI.


========  ==========  ============ ========

Ubalozi wa Ujerumani kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto.


Ubalozi wa Ujerumani nchini umeahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuleta wataalamu wa magonjwa ya moyo ikiwa ni njia moja wapo ya kubadilishana uzoefu na ujuzi katika kutoa huduma za matibabu ya kibingwa kwa watoto wenye matatizo ya moyo.

Ahadi hiyo imetolewa leo na Kaimu Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Jörg Herrera alipofanya ziara ya kutembelea Taasisi hiyo ili kuona maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI, Israel na Ujerumani.

Mhe. Balozi Herrera alisema madaktari kutoka nchini Ujerumani wanauzoefu wa kutosha wa kufanya upasuaji kwa watoto wenye umri mdogo kuanzia siku moja, hivyo ujio wao utakuwa na manufaa kwa madaktari wa JKCI kwa kuweza kubadilishana ujuzi wa kazi wa kutoa matibabu ya kibingwa kwa watoto.

“Katika kambi hii kuna daktari kutoka Ujerumani mwenye uwezo wa kumfanyia upasuaji wa bila kufungua kifua mtoto mwenye umri wa siku moja, ujuzi huu ukisambazwa kwa madaktari wengi utasaidia kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo wanaopoteza maisha katika umri mdogo,” alisema Mhe. Herrera.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema kambi ya madaktari kutoka nchini Israel na Ujerumani imeweza kuokoa maisha kwa watoto ambao wamefanyiwa upasuaji na kuongeza ufanisi kwa wataalamu wa magonjwa ya moyo.

Aidha Prof. Janabi aliushukuru ubalozi wa Ujerumani kwa kuendelea kushirikiana na JKCI na kutuma wataalamu wake ambao wamekuja hapa nchini kutoa huduma ya matibabu kwa watoto.

“Ujuzi tunaoendelea kuupata kutoka kwa wataalamu mbalimbali wa magonjwa ya moyo kupitia kambi maalum za matibabu ikiwemo madaktari kutoka nchini Ujerumani zinatusaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya moyo,” alisema Prof. Janabi.

Jumla ya watoto 20 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo kuziba na kutopitisha damu vizuri wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua katika kambi hiyo na hali zao zinaendelea vizuri huku wengine wakiruhusiwa kurudi nyumbani.

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZINDUA BODI YA PILI YA USHAURI YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashidi Mohamed ameishauri Bodi ya mpya ya Ushauri ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuangalia uwezekanao wa kuvitumia vifaa vya Tiba vilivyopo kwa ajili ya kazi nyengine za Tafiti za Kisayansi. Amesema Wizara ya Afya inavyo vifaa vingi vya Tiba ambavyo havijatumika kikamilifu na vinaweza kusaidia kwa shughuli nyengine mbali mbali za maendeleo zikiwemo za Utafiti.

Waziri Hamad alieleza hayo katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Pili ya Ushauri ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyofanyika jengo jipya la Ofisi hiyo eneo la Maruhubi.
Alisema kitu muhimu kwa Bodi hiyo ni kuongeza ubunifu na kuzaa mawazo mapya ambayo yataweza kusaidia kuongeza matumizi kwa baadhi ya vifaa ambavyo vimekuwa vikitumika kwa muda mchache na uwezo wa kutumika ni mkubwa.

Hata hivyo Waziri wa Afya aliitaka Bodi ya Ushauri ya Maabara ya Mkemia Mkuu kutoa kipaumbele suala la rasilimali watu kwa kuwatafutia masomo wafanyakazi wanaosimamia mashine za maabara hiyo kwani Teknolojia inabadilika kwa haraka sana. Aliitaka Bodi kujiandaa kutoa elimu kwa wananchi na muhimu zaidi ni kuipeleka kwa wananfuzi wa Skuli ili waelewe umuhimu wa Sayansi tunayoendelea nayo katika maendeleo ya Taifa.

Katika kujenga utashi wa kisiasa, Waziri wa Afya ameishauri Bodi hiyo kutoa elimu kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na makundi mengine ya kisiasa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Aidha amesisitiza umuhimu kwa Bodi kusimamia matumizi bora ya mashine ya maabara hiyo ili ziweze kudumu muda mrefu ujao.

Alisema Serikali imetumia fedha nyingi kununu mashine za maabara hiyo, ikiwemo ya kuchunguza vinasaba vya watoto wanaozaliwa ambayo kwa miaka mingi ilikosekana Zanzibar. BMwenyekiti wa mpya wa Bodi hiyo Dk. Haji Mwemvura Haji alimuhakikishia Waziri wa Afya kwamba watayafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipolifungua jengo hilo hivi karibuni.

Dk. Mwemvura alimshukuru Mwenyekiti wa kwanza wa Bodi hiyo Dk. Yussuf Nuhu kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.

Akitoa shukrani zake, Mwenyekiti aliemaliza muda Dk. Yussuf Nuhu aliishauri Serikali kuandaa utaratibu kwa taasisi zinazoendesha tafiti za kisayansi kufanyakazi kwa pamoja kwani baadhi ya taasisi hizo zina mashine za kisasa lakini zimekuwa hazitumiki kikamilifu na zinaweza kusaidia katika taasisi nyengine.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dk. Haji Mwemvura akimkaribisha Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed kuzindua Bodi hiyo katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Mkemia Mkuu Maruhubi.
  Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati akiizindua rasmi Bodi hiyo katika Ofisi ya Mkemia Mkuu Maruhubi.
  Mwenyekiti mstaafu wa Bodi ya Ushauri ya Maabara ya Mkemia Mkuu Dk. Yussuf Nuhu (kulia) na Mkemia Mkuu wa Serikali Dk. Slim Rashid wakimsikiliza Waziri wa Afya wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jengo la Ofisi ya Mkemia Mkuu Maruhubi.
Picha ya pamoja ya Waziri wa Afya na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya uzinduzi uliofanyika Ofisi ya Mkemia Mkuu Maruhubi. Picha na Makame Mshenga.

TBA WAPEWA WIKI MBILI KUPELEKA FEDHA ZA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SIMIYU

0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwa Injini mkuu wa TBA Simiyu Bw. Likimaitare Naunga wakati akipotembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Simiyu. Kulia ni Mkuu wa mkoa huo Bw. Anthony Mtaka.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsalimia ndugu wa mgonjwa aliyelazwa (jina halijafahamika) katika hospitali teule ya Somanda alipotembelea hospitali kuona hali ya utaoaji huduma za afya. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Bi. Juliana Mahongo na Daktari zamu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati alipotembelea wodi za Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu. Kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa Dkt. Mageda Kihulya, Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Bi. Happines Lugiko na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitembelea ujenzi wa jengo la uchunguzi na mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Simiyu. Waliongozana nae ni viongozi waandamizi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo Anthony Mtaka.



Na WAMJW-SIMIYU


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameiagiza wakala wa ujenzi (TBA) kupeleka fedha za ujenzi zilizotolewa na Serikali katika ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu kuhakikisha zinafika ndani ya wiki mbili.

Agizo hilo limetolewa leo wakati alipotembelea ujenzi wa jengo la Uchunguzi na jengo la Mama na Mtoto na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huo huku sababu kubwa inayopelekea kusuasua ikitajwa ni fedha kidogo zilizopokelewa na wakala wa ujenzi wa mkoa wa Simiyu kiasi cha Shilingi Milioni 430 wakati serikali imetoa Bilioni 1.064 kwa ajili ya ujenzi huo.

“Ninawashngaa TBA kwanini wanakaa na fedha wakati wanajua mradi wa ujenzi unaendelea huku, serikali imetoa Bilioni 1.064 ili zitumike katika ujenzi wa Hospitali hii lakini TBA wameleta milioni 430 tu, hizo fedha zingine ziko wapi?”. Alihoji waziri Ummy.

Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy ameahidi kushughulikia suala hilo na kuahidi fedha hizo zitafika katika mradi huo ndani ya wiki mbili ili ziweze kusaidia kuongeza kasi ya ujenzi wa majengo hayo ambapo yanatarajiwa kukabidhiwa na kuanza kutoa huduma kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Kwa upande wake Injinia mkuu wa TBA anayesimamia ujenzi huo Bw. Likimaitare Naunga amesema fedha zilizoletwa katika mradi huo hazitoshi na ndiyo sababu kubwa inayochangia kusuasua kwa mradi huo huku akitaka wakala wa ujenzi (TBA) kuhakikisha fedha hizo zinafika mapema ili zisaidie kuongeza kasi ya mradi na kufikia lengo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka amemuahidi Waziri Ummy kuwa atasimamia kwa karibu upatikanaji wa fedha hizo zilizopo TBA zinafika katika mradi na kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda uliopangwa ili huduma muhimu za kibingwa zianze kutolewa Hopitalini hapo.

Wakati huo huo waziri Ummy ametembelea Hospitali teule ya Somanda iliyopo wilayani Bariadi na kuonekana kutoridhishwa na huduma zinazotolewa katika jengo la Mama na Mtoto ambapo alishuhudia huduma mbaya zinazotolewa kwa akinamama wajawazito na watoto wachanga.

Pia Waziri Ummy ameshangazwa baada ya kuona hakuna chumba cha kuhifadhia watoto wenye uhitaji wa huduma maalum kama huduma za joto kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda (Njiti) na kuitaka Hospitali hiyo kuwa na chumba hicho muhimu.

Aidha, Waziri Ummy ameshangazwa na kutokuwepo kwa huduma za upasuaji katika jengo hilo huku sababu ikitajwa kutokuwepo kwa Sinki, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa akinamama wajawazito wanaofika kupata huduma hospitalini hapo.

Kufuatia hali hiyo waziri huyo ametoa siku tatu kwa uongozi wa Hospitali hiyo chini ya Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mageda Kihulya kuhakikisha wananunua sinki hilo na huduma za upasuaji zianze kutolewa mara moja katika jengo hilo.

Waziri Ummy yupo Mkoani hapa katika ziara ya kikazi ya kutembelea mikoa ya Simiyu, Geita na Shinyanga ili kuweza kuona hali ya miundombinu na utoaji huduma katika hospitali za rufaa za mikoa.

SIMANJIRO YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 35.4

0
0
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya sh35.4 bilioni kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi akisoma rasimu ya mpango huo wa bajeti alisema umezingatia vipaumbele sita. 

Myenzi alitaja vipaumbele hivyo kuwa ni sekta ya elimu, afya, maji, utawala bora, maendeleo ya jamii, kilimo, mifugo na uvuvi. Alisema katika rasimu hiyo ya bajeti, sh17.5 bilioni ni mishahara, sh827.4 ni ruzuku ya uendeshaji ofisi, sh16 bilioni ni miradi ya maendeleo na mapato ya ndani sh1.8 bilioni. 

Alisema kwa vile Simanjiro ni miongoni mwa halmashauri zilizo kwenye mazingira magumu, wamewasilisha maombi maalum kwenye vipaumbele ambavyo havikutengewa fedha. Alisema kupitia maombi hayo wanatarajia kukamilisha madarasa 42 ya shule za msingi, madarasa 77 ya sekondari na nyumba 74 za walimu na watumishi wa elimu. 

Alisema wanatarajia kukamilisha zahanati sita na vituo vya afya viwili na kujenga vituo tisa vya afya na zahanati nne kwenye maeneo ya Msitu wa Tembo, Emboreet na Moipo. "Pia tunatarajia kukamilisha jengo jipya la makao makuu ya wilaya, umaliziaji wa miradi ya maji vijijini na nyumba mbili za watumishi wa afya," alisema Myenzi. 

Diwani wa kata ya Endiamtu, Philemon Oyogo alisema wamepitisha bajeti hiyo ila serikali kuu inapaswa kufikisha fedha kwani kwenye bajeti ya mwaka jana hawakuwaletea fedha zote. Diwani wa kata ya Naberera, Haiyo Yamati alipongeza bajeti hiyo ila alitarajia sekta ya mifugo kutengewa fedha nyingi zaidi. Diwani wa kata ya Mirerani, Thomas Yohana alisema shule mpya ya sekondari Songambele itanufaika kupitia bajeti hiyo. Katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2018/2019 halmashauri hiyo ilipitisha bajeti ya sh22.6 bilioni. 
 Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakipitia rasimu ya mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 35.4 kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred Myenzi akisoma rasimu ya mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 35.4 kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani lililopitisha bajeti ya shilingi bilioni 35.4 kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.  

SINGIDA UNITED YAAGA MICHUANO YA SPORTPESA

0
0
Wachezaji wa timu ya Bandari wakishangilia baada ya kufanikiwa kupata goli lililowapelekea hatua ya nusu fainali ya Michuano ya Sportpesa leo katika Uwanjwa wa Taifa Jijini Dar es Salaam.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

TIMU ya Singida United ya Tanzania imepoteza mchezo wake wa hatua ya robo fainali kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Bandari uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.


Mchezo huo ulioanza majira ya saa 8 mchana ukiwa  ni mechi ya Ufunguzi wa michuano ya Sportpesa inapoteza dhidi ya Bandari na kupunguza idadi ya wawakilishi kutoka Tanzania. mashindano hayo.

Singida United imepoteza mchezo huo na inakuwa ni timu ya kwanza kuondolewa kwenye hatua ya robo fainali kutoka Tanzania na kuifanya Bandari kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.


Mchezo unaoendelea kwa sasa ni kati ya Yanga na KK Sharks Uwanja wa Taifa ili kumpata mshindi atakayetinga hatua ya nusu fainali ya mashindano haya.

Mshindi wa SportPesa Cup atapata fursa ya kucheza na timu ya Everton ambayo nayo inadhaminiwa na kampuni ya SportPesa na msimu huu mshindi atafuatwa nyumbani na Everton wenyewe.

TAZAMA TANZANIA SAFARI CHANNEL

YANGA YAONDOLEWA MICHUANO YA SPORTPESA

0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

Timu ya Yanga imekuwa timu ya pili kuondolewa kwenye michuano ya Sportpesa baada ya kukubali kichapo cha goli 3-2 kutoka kwa Kariobang Sharks.

Mchezo huo wa pili ulizikutanisha timu hizo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na KK Sharks kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.

Ilichukua dakika 10 kwa KK Sharks kuandika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Duke Abuye.Yanga waliendelea kupambana kupata goli la kusawazisha wakishindwa nafasi walizozipata na kuwapa nafasi wapinzani wao kufanya mashmbulizi ya mara kwa mara langoni mwao.

Katika dakika ya 37 mchezaji wa KK Sharks anaipatia timu yake goli la pili na kuelekea mapumziko wakiwa wanaongoza kwa jumla ya goli 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kutafuta namna ya kufanya marekebisho ya makosa ya kipindi cha kwanza kwa kusaka magoli ya kusawazisha.

Mshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe anaipatia Yanga goli la kwanza kwenye dakika ya 86 ya kipindi cha pili na haikuchukua mda mrefu Duke Abuye wa KK Sharks anaiandikia Timu yake goli la 3 dakika za nyongeza na kupeleka simanzi zaidi kwa Yanga.

Dakika ya 90+5 Tambwe anaipatia timu yake goli la 2 na kupelekea matokeo kuwa 3-2. Mpaka dakika 90 za mtanange huo unamalizika Yanga inakuwa timu ya pili baada ya Singida United kuaga mashindano hayo kwa jumla ya goli 3-2.

Michuano hiyo inaendelea tena kesho kwa Gor Mahia kuumana na Mbao Fc huku Simba wakishuka dimbani kuvaana na AFC Leopard na mshindi wa michuano hii atacheza na timu ya Everton kutoka Ligi Kuu Uingereza zote zikiwa ni timu zinazodhaminiwa na kampuni ya ubashiri Sportpesa.
Wachezaji wa Kariobang Sharks wakiwa wanashaangalia baada y kufanikiwa kuiondoa Yanga kwenye hatua ya robo fainali ya Michuano ya Sportpesa leo katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

TAARIFA MAALUM KWA WADAU WOTE WA ZAO LA MUHOGO NCHINI


MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 23, 2019

Introducing Nakutunza inaruhusiwa Official Video by Maarifa Feat Madee

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 22.01.2019

DC JOKATE ALIA NA UKOSEFU WA MAJI KISARAWE

0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo amemuomba Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso kuhakikisha Wilaya hiyo inapata Maji yakutosha kutokana nakuwepo changamoto kubwa ya upatikanaji wa Maji hayo.
Akizungumza na Watendaji wa Wilaya hiyo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso - Jokate ameshukuru kuwepo mradi wa Maji unaotoka Ruvu Juu, amesema mradi huo umekaa kimkakati kutokana na Wilaya hiyo kuwa na Viwanda vingi.
Hata hivyo, Jokate amesema maendeleo ya Wilaya ya Kisarawe yamekwamishwa kwa ukosefu wa Maji Safi na Salama hivyo kuna nia yakuhakikisha Maji hayo yanapatikana.
‘’Haileti maana kama Kisarawe haina Miundombinu yakuwezesha Viwanda mbalimbali kustawi, hata uwepo wa Bandari na Kiwanja cha Ndege’’, amesisitiza Jokate.
‘’Watu wengi wamekuwa na imani Kisarawe kuwa sio eneo la Makazi, wengi wanaishi Gongo la Mboto, Chanika kutokana nakukosekana huduma ya maji’’, ameeleza Jokate.
Jokate ameshukuru kuwepo ziara ya Naibu Waziri wa Maji ambapo amemuomba kuangalia kwa umakini miradi hiyo, Je inatekelezwa ipasavyo?
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso akisisitiza jambo wakati alipowasili katika Ofoisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya ziara yake yakutembelea miradi mbalimbali ya Maji Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo akizungumza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso wakati wa ziara yake yakutembelea miradi mbalimbali ya Maji Wirani Kisarawe Mkoa wa Pwani.

VOA SWAHILI: Duniani Leo January 22nd, 2019

BBC HARDtalk 21/01/2019 Tundu Lissu MP

RELI TV: LAZIMA TUWAPELEKE MADEREVA WETU NJE YA NCHI,TRENI TUNAWASHA NOVEMBER MWAKA HUU 2019


CCM PANGANI YAMTUNUKU TUZO YA SHUKRANI RAIS DKT MAGUFULI KWA UAMUZI WAKE WA KURIDHIA KUTIA SAINI UJENZI WA BARABARA YA TANGA-,PANGANI HADI BAGAMOYO

0
0


CHAMA Cha Mapinduzi wilaya ya Pangani kimemtunuku tunzo ya shukrani Rais John Magufuli kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni .

Akikabidhi tunzo hiyo hapo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya wa Umoja wa wanawake wa chama hicho UWT Taifa Jesca Mbogo wakati akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za maendeleo wilayani humo

Mwenyekiti CCM wilayani humo Hamis Mnegero alisema kuwa wameamua kutoa tunzo hiyo kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Rais Magufuli kutoka na kufanikiwa kutekeleza ndoto ya siku nyingi ya kuwa na barabara ya kiwango cha lami wilayani humo.

“Tunajua kuna juhudi kubwa ambazo zilikuwa zimechukuliwa na marais waliotangulia lakini ndoto hizo hazikuweza kutimia lakini kwa juhudi kubwa za Rais wa awamu ya tani tumeona ujenzi huo sasa unakwenda kufanyika”alisema Mnegero.

Alisema kuwa barabara hiyo ilikuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa wilaya hivyo anaamini kwa kuanza kwa ujenzi huo kutaweza kufufua matumaini mapya kwa wilaya hiyo.

Kwa upande wake Naibu Katibu mbogo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inajitahidi kuboresha mazingira bora katika sekta mbalimbali ili kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa ya kupata maendeleo na unafuu wa maisha.

“Kama mnavyoona utekelezaji wa sera ya elimu bure pamoja na uboreshwaji wa huduma za afya hii yote ni kuhakikisha mtoto wa kitanzania anakuwa na afya bora lakini anapata fursa ya elimu bora”alisema Naibu Katibu huyo. 
Naibu Katibu Mkuu Mbogo yupo mkoani Tanga kwa ziara ya siku tatu kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali pamoja na kuzungumza na wanachama wa UWT mkoani hapa
 Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero akizungumza na waandishi wa habari hatua yao ya kumtunuku tunzo ya shukrani Rais John Magufuli kutokana na uamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
 Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero akizungumza na waandishi wa habari hatua yao ya kumtunuku tunzo ya shukrani Rais John Magufuli kutokana na uamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa.
 Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero katikati akimkabidhi tuzo  ya shukrani ya  Rais John Magufuli ,Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah 
 Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero katikati akimkabidhi tuzo  ya shukrani ya  Rais John Magufuli ,Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah 
 Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kushoto akitazama tuzo aliyotunukiwa Rais Dkt John Magufuli ya Shukrani na  Chama cha Mapinduzi wilaya ya Pangani kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibun katikati ni Mwenyekiit wa CCM wilaya ya Pangani Hamisi Mnegero kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
 Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kushoto akitazama tuzo aliyotunukiwa Rais Dkt John Magufuli ya Shukrani na  Chama cha Mapinduzi wilaya ya Pangani kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibun katikati ni Mwenyekiit wa CCM wilaya ya Pangani Hamisi Mnegero kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah


MKANDARASI ANAYESIMAMIA MRADI WA MAJI BOGA WILAYANI KISARAWE AONDOLEWA

0
0
 Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii .

 Mkandarasi wa Kampuni ya Mazongela Bulding Limited aliyekuwa anasimamia mradi wa Maji katika Kata ya Boga Wilayani Kisarawe ameondolewa kuendelea kusimamia ujenzi wa mradi huo baada yakubainika kusuasua kwa muda. 
 Kampuni hiyo ya ujenzi iliyo chini ya Mkandarasi, Salum Suleiman Ally ameondolewa kuendelea na ujenzi wa mradi huo licha yakutengewa zaidi ya Shilingi Milioni 536/- ambazo angelipwa katika utekelezaji wake. 
 Akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na Wananchi wa Kata ya Boga wilayani humo wakati akitembelea miradi mbalimbali ya Maji, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso amesema Mkandarasi huyo hafai kutokana na kuwaumiza Wananchi hao kwa muda mrefu, ambapo ameagiza asipewe kazi yoyote katika Halmashauri hiyo ya Kisarawe. 
 ‘’Changamoto kubwa katika Wilaya hii ya Kisarawe kuwaweka Wakandarasi wasio na uwezo kusimamia miradi mbalimbali ya Maji, wengi wanapatikana Kindugu hii haiwezekani’’, amesema Mhe. Aweso. Mhe. 
Aweso amewaasa Watendaji wa Wizara hiyo Wilayani humo, kukataa Wakandarasi wasio na uwezo, badala yake amewataka kuchukua Wandarasi wenye uwezo, hata hivyo Aweso amewataka Watendaji hao kuhakikisha Mkandarasi mwengine anapatikana kwa haraka ili kutekeleza mradi huo kwa haraka. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo ameiomba Serikali kupitia Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso kuwachukulia hatua kali Wakandarasi ambao watashindwa kutekeleza miradi yao ipasavyo kutokana na Wilaya hiyo kukumbwa na kero kubwa ya Maji. 
 ‘’Kuna Miji mikubwa kama Nairobi imeundwa mwaka mmoja na Wilaya yetu lakini wao wana maendeleo sisi bado tupo nyuma’’, amesema Jokate. 
Naye Diwani wa Kata ya Boga, Inadi Chachaka amekili kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa Maji katika Kata hiyo, ambapo pia amemuomba Naibu Waziri kwa kushirikiana na Watendaji wake Wilayani Kisarawe kusimamia ipasavyo miradi hiyo ikiwemo Mradi wa Maji katika Kata ya Boga.
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo akisisitiza jambo kwa Naibu wa Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso wataki walipotembelea mradi wa maji eneo la Mnarani, Kisarawe.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso pamoja na Watendaji wengine wa Wizara ya Maji wakiangalia mradi wa maji wa Kata ya Boga, Wilayani Kisarawe baada kuambiwa umesuasua kwa muda kutokana na Mkandarasi anayetekeleza mradi kushindwa kusimamia ipasavyo licha yakutengewa zaidi ya Shilingi Milioni 536/-
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso akishuhudia Shimo lililochimbwa kwa kile lilichoelezwa ni utekelezaji wa mradi wa maji, Kata ya Boga, Kisarawe.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo wakimsikiliza Mhandisi wa Wilaya ya Kisarawe, Majid Mtili katika kutembelea utekelezaji wa mradi wa maji, Kata ya Chole.

LTSP YATOA MAFUNZO KWA MABARAZA YA ARDHI YA KIJIJI KUPUNGUZA MLUNDIKANO KESI ZA ARDHI ULANGA

0
0
Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kupitia mpango wake wa kuwezesha umilikishaji Ardhi(TLSP) imetoa mafunzo kwa mabaraza ya ardhi ya Vijiji 56 vilivyopo katika wilaya za Ulanga ,Kilombero na Malinyi Mkoani Morogoro ili kukabiliana na migogoro ya ardhi na namna bora ya kuisuruhisha. 

Mratibu wa mafunzo hayo JAMES BALELE amesema utafiti uliofanywa na mradi huo umebaini migogoro mingi ya ardhi imekuwa haimaliziki kutokana na uelewa mdogo wa wasuluishi,ufinyu wa vitendea kazi pamoja na miongozo ya kisheria. 

Awali akifunga mafunzo hayo ,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga, FADHILI FURAHA ameishukuru wizara ya Ardhi kupitia mpango wake wa uwezeshwaji na umilikishaji Ardhi TLSP kwa kutoa mafunzo hayo yatakayo punguza migogoro kwa wananchi huku mwanasheria wa halmashauri hiyo DEVOTA KISEMBO akaeleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo mabaraza hayo ya ardhi.
Mafunzo kwa Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji katika Wilaya ya Ulanga katika kijiji cha Mavimba yakiendelea ikiwa ni sehemu ya hafla ya kuhitimisha mafunzo haya kwa wajumbe wa mabaraza wilayani humo.
Mwezeshaji kutoka Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi (LTSP) ambaye ndie mratibu wa mafunzo hayo yanayoendeshwa na LTSP akitoa salamu za utangulizi kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa Ulanga ambaye ndie alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo
Mgeni Rasmi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa Ulanga Fadhili Furaha akitoa salamu kwa washiriki wa warsha hiyo ya mafunzo.
Mmoja wa wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kijiji akichangia hoja mara baada ya mgeni rasmi kuwasili katika hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo ya mabaraza ya ardhi ya kijiji Ulanga. 
Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo.

SERIKALI KUPITIA TANESCO YAANZA KUTEKELEZA MRADI WA UMEME WA KENYA-TANZANIA POWER INTERCONNECTION

0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Monduli

MRADI wa umeme wa Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK tayari umeanza kutekelezwa ambapo kazi ya kutengeneza misingi ya kusimika minara (towers) imeanza, Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Peter Kigadye amewaambia wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kambi ya wakandarasi iliyoko kijiji cha Nanja kilichoko barabara ya Bababti-Arusha wilayani Munduli leo Januari 22, 2019.

Mradi huo ni sehemu moja ya mradi mzima wa regional power connection ambao lengo lake ni kuunganisha mfumo wa umeme wa Tanzania na Afrika Mashariki (East Africa Power Pool) kwa upande wa Kaskazini, na baadaye utekelezaji wa sehemu nyingine ya tatu ambayo itakuwa inaunganisha mifumo ya nxchi Kusini mwa Afrika, kupitia chombo kinachoitwa Southern Africa Power Pool (SAPP)

“Tanzaania tumebarikiwa tutakuwa na sehemu tatu ya kwanza ni mradi wa Backborn ambao umejengwa katikati ya nchi yetu na ulikuwa na kilomita 670 inaanzia Shinyanga hadi Iringa, sehemu ya pili ni kuunga kutoka Singida hadi mpakani na Kenya kuna kituo kimoja kinaitwa Isinya, jumla hapo kuna kilomita 510.7 na hizo ndio kilomita za mradi tunazoanza kuutekeleza hivi sasa.” Alisema Mhandisi Kigadye.
 
“Baada ya hapo sehemu ya tatu ni kuanzia Iringa kwenda Kusini ambapo kuna mradi utakaoitwa Zambia Interconector ambako kuna kilomita nyingine 624 kwahiyo Tanzania tutakuwa tumekamilisha ule mkongo wa msongo wa kilovoti 400.” Alisema Mhandisi Kigadye.Akielezea zaidi kuhusu kuunganiushwa kwa umeme kwenye nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini Mhandisi Kigadye alisema, “ Lengo ni kuunganisha nchi yetu na ukanda nchi za Kikanda kuanzia Kaskazini kuungana na Kenya na Kusini kuungana na Zambia.”

Alisema mradi wa Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK, utakamilika Aprili 2020, wakati ule Zambia Connector utakamilika mwaka 2022 tutakuwa tumemaliza mikongo hii mitatu (3)na nchi yetu itakuwa tayari kushiriki kwenye biashara ya umeme Kikanda.Akifafanua zaidi kuhusu mradi huo wa Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK Mhandisi Kigadye alisema sehemu ya kwanza itahusu ujenzi wa njia za kusafirisha umeme (transmission lines) na ujenzi wa vituo vya kupozea umeme.

Mradi mzima una urefu wa kilomita 510 na umegawanyika kwenye sehemu nne, ambazo ni Isinya Kenya hadi Namanga Kilomita kilomita 96, sehemu ya pili unahusu Namanga-Arusha Kilomita 114, sehemu ya tatu Arusha-Babati kilomita 150, na Bababti-Singida kilomita 150.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayehusika na Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona, alisema tayari vifaa vya kutekeleza ujenzi wa mradi huo vimewasili kwa kiasi kikubwa cha kazi kuanza.

Akieleza zaidi Mhandisi Manirabona alibainisha kuwa kila kitu kiko sawa na wananchi wote ambao wako kwenye sehemu mradi unakopita, tayari Serikali imeshawalipa fidia na ndiyo maana mkandarasi anaendelea na kazi.
Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayehusika na Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona, akifafanua mambo mbalimbali yahusuyo utekelezaji wa mradi huo leo Januari 22, 2019
Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Peter Kigadye, akifafanua jambo kwa wahariri eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha leo Januari 22, 2019
Vifaa viko site tayari
Vifaa viko site tayari
Zege linamwaga kwenye msingi wa kusimika mnara wa kupitisha nyaya za umeme mkubwa
Eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kisongo.






Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayehusika na Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona (kushoto), akimsikiliza Mhandisi Mshauri Mradi wa umeme wa Kenya-Tanzania Interconnection-Lot2(KTPIP-Lot2), Gilles Allard kutoka kampuni ya Intec, kwenye eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme kinachojengwa eneo la Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha Januari 22, 2019.
Mhandisi Herini Mhina. Meneja wa TANESCO jijini Arusha.
Mhandisi Peter Kigadye
Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayehusika na Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona (kushoto), akiwa na Meneja Mkazi, Mradi wa Kenya-Tanzania Interconnection Project-Lot2 SBU Power Bouygues ya Ufaransa, Christophe Batholome
Mhandisi Mshauri Mradi wa umeme wa Kenya-Tanzania Interconnection-Lot2(KTPIP-Lot2), Gilles Allard kutoka kampuni ya Intec
Mhariri wa gazeti la Majira, Bw. Imma Mbuguni akizungumza jambo.



Meneja Mkazi, Mradi wa Kenya-Tanzania Interconnection Project-Lot2 SBU Power Bouygues ya Ufaransa, Christophe Batholome(kulia), akibadilishana mawazo na Meneja wa TANESCO jijini Arusha, Mhandisi Herini Mhina, (katikati) na Msimamizi wa ujenzi kutoka Tanesco.


Mashimo manne ya nguzo nne za mnara (tower) moja. mafundi wanasubiri kumwaga zegu.

Mafundi wakiwa wamesimama mbele ya moja ya shimo litakalotumika kusimika mnara (tower). Kwa kawaida Mnara mmoja nashikiliwa na nguzo nne, hili shimo ni la kusimika nguzo moja kati ya hizo.
Mhandisi Kigadye akifafanua jambo eneo la uchimbaji na usimikazji minara ambapo kazi ya kumimina zege kwenye mashimo imeanza
Waandishi na wahariri wakinukuu taarifa muhimu eneo la utendaji huko wilayani Monduli.
Mafundi wakiwa kazini.

NAIBU WAZIRI DK MABULA ARIDHISHWA NA UJENZI WA NHC KATIKA MJI WA SERIKALI MTUMBA

0
0
Na Munir Shemweta, Dodoma
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa ofisi za wizara katika mji wa serikali ya Mtumba mkoani Dodoma unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Dk Mabula alitoa kauli hiyo leo tarehe 22 Januari 2019 wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa ofisi za Serikali katika mji wa Mtumba mkoani Dodoma unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo liko chini ya Wizara yake.
Alisema kazi inayofanywa na shirika la Nyumba la Taifa kujenga ofisi za Serikali katika mji huo kwa sasa unaenda kwa kasi na unatia moyo jambo linalooonesha kuwa mradi wa ujenzi wa ofisi hizo utakamilika katika muda uliopangwa.
Katika mradi huo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia kampuni yake ya ujenzi inajenga ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Fedha na Uchumi, Wizara ya Nishati pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara.
Aidha, Dk Mabula amefurahishwa na ufuatialiaji wa ujenzi wa ofisi hizo unaofanywa na Wizara ya Fedha pamoja na Viwanda na Biashara na kueleza kuwa hatua hiyo inalifanya Shirika hilo kufanya kazi kulingana na mahitaji ya wateja wake.
Alibainisha kuwa, pamoja na changamoto ya kukatika umeme lakini NHC imejitahidi na kilichomfurahisha ni kuwepo vifaa vyote vya ujenzi kwenye eneo la ujenzi jambo linalompa faraja kuwa hakuna kitakachokwamisha ujenzi kukamilika kwa wakati
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amepongeza jitihada znazofanywa na Rais John Pombe Magufuli za kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Dodoma na kubainisha kuwa hatua hiyo inatimiza ndoto ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Emma Lyimo alilisifu Shirika la Nyumba la Taifa kwa kasi kubwa wanayoendelea nayo kwenye ujenzi wa ofisi ya Wizara yake na kubainisha kuwa pamoja na kuchelewa kuanza ujenzi lakini kasi wanayoenda nayo ana imani ujenzi utakamilika kwa wakati.
Naye Msimamizi wa ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo la Makazi Mhandisi Grace Musita alisema, ujenzi wa ofisi umefikia asilimia sabini na tano na anatarajia utakamilika katika tarehe iliyopangwa kwa kuwa wamefikia hatua nzuri ya kukamika.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akiangalia maendeleo ya Ujenzi ya Ofisi ya Wizara ya Nishati katika mji wa Serikali wa Mtumba, kushoto ni Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Elisante Ulomi na katikati ni meneja mradi Haikameni Mlekio.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akioneshwa moja ya kifaa kitakachotumika katika Ujenzi ya Ofisi ya Wizara ya Nishati katika mji wa Serikali wa Mtumba mkoani Dodoma, kulia ni Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Elisante Ulomi na kushoto ni meneja mradi Haikameni Mlekio.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akimsikiliza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Viwanda na Bisahara Emma Lyimo (Kulia) wakati alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Viwanda na Biashara katika mji wa Serikali wa Mtumba mkoani Dodoma, kushoto ni Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Hassan Mohamed.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akiongozwa na Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Grace Musita kukagua ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mji wa Serikali eneo la Mtumba Dodoma .
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula katikati akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mji wa Serikali wa Mtumba kutoka kwa meneja mradi wa Shirika la Nyumba Haikameni Mlekio wakati alipofanya ziara, kushoto ni Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Grace Musita.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mji wa Serikali wa Mtumba kutoka kwa meneja mradi wa Shirika la Nyumba Haikameni Mlekio (kulia) wakati alipofanya ziara, kushoto ni Mhandisi wa ujenzi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Grace Musita. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Viewing all 109610 articles
Browse latest View live




Latest Images