Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

TaESA yajengea uwezo wa kutafuta ajira wanafunzi 500 ATC

$
0
0
WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA), imewajengea uwezo na kuwapa mbinu za kutafuta ajira pindi wanapomaliza masomo zaidi ya wanafunzi 500 wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).

Huduma zinazotolewa na TaESA ni kuunganisha watafuta kazi na waajiri, kutoa mafunzo kuhusu mbinu za usaili ambayo huwajengea uwezo wa kujiamini, kutoa ushauri kuhusu masuala ya ajira na kutoa taarifa za soko la ajira.

Akizungumza mjini Arusha Afisa Kazi Mwandamizi wa TaESA na Mratibu wa Mafunzo hayo kwa wanafunzi Peter Ugata alisema, Tanzania na dunia kwa sasa kuna changamoto zinazohusiana na Soko la Ajira. Alisema hatua hiyo imechangiwa na mahitaji ya Waajiri kuhamia kwa watu wenye ujuzi wa ziada mbali ya na weledi wa kusomea, kwani mara nyingi ujuzi wa ziada hausomewi.

“Changamoto zilizopo zimeletwa na mabadiliko ya dunia ya utanfawazi ambapo watu, huduma na bidhaa ziko huru kutoka sehemu moja hadi nyingine. “Ili kukabiliana na hali hiyo nchi mbalimbali duniani zilianzisha huduma za Ajira kupitia Sera, Sheria, Kanuni na maazimio ya Shirika la Kazi Duniani (ILO),” alisema.

Akifafanua namna huduma za ajira zinavyotolewa Ugata alisema Wakala husajili na kutunza taarifa za watafuta kazi kwa kutumia Kanzidata iliyopo. “Wakala huoanisha sifa za mtafuta kazi kulingana na mahitaji ya kazi husika kama yalivyoanishiwa na mwajiri, lakini pia wakala unaoanisha ujuzi, uzoefu, elimu na sifa nyingine za watafuta kazi na mahitaji ya sifa za kazi za mwajiri,” alisema Ugata.

Anazitaja baadhi ya faida za kutumia TaESA ni Waajiri kupewa ushauri mzuri kuhusu mwenendo wa soko la Ajira na mahitaji na aina ya watu na ujuzi utaokamsaidia kuleta tija. “TaESA itamuwezesha mwajiri kupata wafanyakazi kazi waadilifu na waaminifu katika kazi, wabunifu na wakujituma kazini , lakini pia kuiwezesha serikali kupata takwimu za uamuzi na mipango kwa haraka,” alisema Ugata.

TaESA inafanya kazi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu. 
Afisa Kazi kutoka TaESA Emma Mangesho akiwajengea uwezo na kuwapa mbinu Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kuhusu namna bora ya kutafuta kazi 
Meneja wa Karakana ya uchomeleaji Chuo cha Ufundi Arusha Expedito Miliaso akiwaonyesha maofisa wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA), vifaa vipya vya uchomeleaji wanavyotumia wanafunzi wa Chuo hicho kwa ajili ya mafunzo. 
Maofisa wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) kutoka Dar es Salaam na Arusha wakiangalia kifaa maalumu cha uchomeleaji ndani ya Karakana ya Chuo cha Ufundi Arusha anayewaonyesha ni Meneja wa Karakana ya uchomeleaji Expedito Miliaso. 
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), wakimsikiliza Afisa Kazi wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESO) kutoka Dar es Salaam Emma Mangesho akifundisha namba bora ya uandishi wa barua za kuomba ajira.
Afisa Kazi wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESO) kutoka Dar es Salaam Emma Mangesho akifundisha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), mbinu za kuomba ajira ikiwamo namna bora ya uandishi wa barua za kuomba kazi. 
Afisa Kazi Mwandamizi kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) na Mratibu wa mafunzi Peter Ugata akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) wakati wa kuwajengea uwezo wa namna bora ya kutafuta kazi.
 

Wateja 100 wa Benki ya NMB wajishindia shs 100,000/- kila mmoja shindano la 'MastaBata'

$
0
0
JUMLA ya wateja 100 wa Benki ya NMB wamejishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- kila mmoja na wengine sita wakijishindia simu janja 'Samsung S9+' zenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kila moja. Idadi ya wateja hao imefikiwa leo baada ya kuchezeshwa droo ya tano ya shindano la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata' na wateja wengine 20 kujipatia kitita hicho.

Droo ya tano imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam katika Tawi la NMB Oyster Plaza na kupatikana kwa washindi hao 20 chini ya uangalizi wa Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdallah Hemedy.

Akizungumza katika droo hiyo Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi Benki ya NMB, Manfredy Kayala Alisema wateja 20 wamepigiwa simu na kujulishwa ushindi wao na fedha walizojishindia zitaingizwa kwenye akaunti zao ndani ya saa 24 tangu kuchezeshwa kwa droo hiyo.Alisema kupatikana kwa washindi wa leo kunatimiza idadi ya wateja 100 hadi sasa ambao wamejishindia shilingi 100,000 kila mmoja, huku kukiwa na wengine 6 walionyakuwa simu aina ya Samsung S9+' droo iliyopita.

Alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia zawadi hizo.

Hata hivyo, aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika na shindano zima.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Oyster Plaza, Hildegard Mng'ong'o akizungumza leo kwenye droo ya tano ya Masta Bata iliyochezeshwa katika tawi hilo. 


Remida Mosi (kulia) kutoka Benki ya NMB kitengo cha Kadi akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tano ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata'. Kushoto ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdallah Hemedy na Florence Mchau kutoka kitengo cha kadi cha NMB (katikati). 

Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi Benki ya NMB, Manfredy Kayala (kulia) akizungumza leo kwenye droo ya tano ya shindano la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata'. Kushoto droo hiyo ikiendelea kuchezeshwa. 
Remida Mosi (kulia) kutoka Benki ya NMB kitengo cha Kadi akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tano ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata'. Kushoto ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdallah Hemedy na Florence Mchau kutoka kitengo cha kadi cha NMB (katikati). 

UJENZI WA NJIA NNE MOROGORO ROAD ENEO LA MBEZI WASHIKA KASI

$
0
0
--
Wakandarasi wakiendelea na ujenzi wa Roound about ya Msigani kama inavyoonekana katika picha Barabara ya Morogoro Road katika Mfumo wa njia nane
Under Pass Mpya kabisa iliyojengwa kwenda Maramba mawili katika eneo la kituo cha Daladala Mbezi
Under Pass Inavyooekana kwa juu
Wafanyabishara walioamuliwa kuondoka katika eneo la ujenzi wa barabara wakiwa wamerejea kiasi cha kumkwamisha mkandarasi kufanya kazi kwa ufanisi

TGNP MTANDAO YAENDESHA WARSHA KWA WAHARIRI KUHUSU BAJETI YA MRENGO WA KIJINSIA

$
0
0


TGNP Mtandao imeendesha warsha kwa Wahariri na baadhi ya waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa ajili ya kuwaongezea uelewa na uwezo kuhariri na kuripoti masuala ya kijinsia.

Warsha hiyo ya siku moja imefanyika leo Jumamosi Januari 19,2019 katika ofisi za TGNP Mtandao zilizopo jijini Dar es salaam.

Akifungua warsha,Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema mafunzo hayo yawawezesha wahariri na waandishi wa habari kuhamasisha uingizwaji wa masuala ya kijinsia katika mipango,miongozo na sera za serikali.

"Tumekutana hapa kwa ajili ya kukumbushana dhana kuu za jinsia na umuhimu wa kuzingatia masuala ya jinsia kwa maendeleo lakini pia kuweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti masuala ya kijinsia katika vyombo vya habari kwani tunaamini vyombo vya habari ni muhimu kwa maendeleo ya jamii",alisema Liundi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akizungumza wakati akifungua warsha ya wahariri kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia katika ukumbi wa ofisi za TGNP Mtandao jijini Dar es salaam. Picha zote na Kadama Malunde - na Frankius Cleophace Malunde1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akielezea kuhusu dhana nzima ua bajeti yenye mrengo wa kijinsia.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.

Regina Mziwanda wa BBC Swahili akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Warsha inaendelea..
Mhariri wa gazeti la Majira,Imma Mbuguni akichangia hoja ukumbini.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - na Frankius Cleophace Malunde1 blog

KLABU ZA FEMA ZACHANGIA UFAULU WA WANAFUNZI MASHULENI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

KATIKA kusherekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa shirika lisilo la kiserikali la FEMINA, mchango wa shirika hilo umeonekana kwa vijana hasa kwa kuonesha juhudi zao za kuwafikia vijana nchini kote na kuwapa elimu kuhusiana na afya ya uzazi, uwezeshaji kiuchumi pamoja na ushiriki katika masuala ya uraia.

Akizungumza na waandishi wa habari katika warsha uliowakutanisha, Mkurugenzi wa Habari wa FEMINA Amabilis Batamula amesema kuwa miaka 20 ya shirika hilo imekuwa ya mafanikio makubwa kwani tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999 vijana wengi wamenufaika na wanaendelea kulea vijana wapya na kusema kuwa programu zote zitakuwa endelevu.

Akieleza maeneo ambayo wao kama FEMINA wanayafanyia kazi Amabilisi amesema kuwa wanajiegemeza katika maeneo makuu matatu ambayo ni kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia ambayo ilianza kutolewa mwaka 1999 kwa kutoa elimu kuhusia na ugonjwa wa UKIMWI na baadae stadi za maisha na taarifa kuhusu afya ya uzazi na kwa sasa katika shule wanatumia mbinu ya kusubiri pamoja na kufikia huduma za afya.

Pia eneo jingine ambalo wanaliegemea ni uwezeshaji wa kiuchumi kwa vijana ambapo huwapa taarifa za fursa zinazowazunguka vijana hao na sio pesa wala mitaji na hiyo ni katika kuwasaidia kwa kuwajengea wigo wa kujitegemea na katika hilo hushirikiana na wadau mbalimbali wa kimaendeleo katika kupata taarifa ambazo wao huzichakata.

Ameeleza kuwa FEMINA pia hutoa elimu kwa vijana kuhusu kushiriki mambo mbalimbali ya kijamii kama mikutano ya kata, vijiji na Wilaya pamoja na kujitolea katika nafasi mbalimbali kama vile kufanya usafi katika hospitali, masoko na kujitolea damu na hiyo ni pamoja na kupiga vita tamaduni potovu ikiwa ni pamoja na ukeketaji na ndoa za utotoni.

Amabilisi amesema kuwa lazima wazazi pamoja na walezi wawe wawazi kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha kuhusiana na afya ya uzazi pamoja na kukabiliana na changamoto katika ukuaji wao.

Kuhusiana na mchango wa FEMINA katika klabu za FEMA kote nchini Afisa ufuatiliaji na tathimini kutoka FEMINA Martha Samwel amesema kuwa ufaulu kwa shule zenye klabu za FEMA uameongezeka na hiyo ni kutokana na mirejesho wanayoipata kutoka kwa walimu na walezi wa klabu hizo kwani kupitia klabu hizo wanafunzi wamekuwa wakielimishana na kuhimizana kuhusu masomo na katika baadhi ya maeneo wanafunzi watoro darasani wamerudi shule kutokana na nguvu ya klabu za FEMA.

"Kuna baadhi ya shule zimekuwa na misimamo yao ambapo wanakauli mbiu zao za kutoruhusu mwanaklabu ya FEMA afeli darasani, hii inawapa nguvu na ari ya wao kusoma zaidi na hatimaye kufanya vizuri katika masomo yao" ameeleza Martha.

Aidha amesema kuwa mafanikio waliyoyapata kwa miaka 20 ni makubwa sana hasa kwa kuwafikia vijana wengi Tanzania kote na kutoe elimu ambayo imewasaidia kwa kiasi kikubwa hivyo wanajivunia kuwa sehemu ya maisha kwa vijana hao.

Pia amewashauri vijana wengine kujiunga na klabu za FEMA ili waweze kupata elimu ya afya na ujinsia pamoja na elimu ya ujasiriamali ambayo itawasaidia katika kujenga taifa na kujenga nchi ya viwanda kwa kuwa wao ndio nguvu kazi ya taifa.
Mkurugenzi wa Masuala ya Habari katika shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya vijana la Femina Hip, Amabilis Batamula (kulia) akizungumza kuhusiana na miaka 20 ya shirika hilo wakati wa semina na wanahabari, jijini Dar es Salaam juzi. Picha na Joseph Zablon

MIAKA 20 YA FEMINA YAWAFIKIA VIJANA NCHINI KOTE

$
0
0
Na Agnes Francis, Blogu ya jamii

WAKATI shirika lisilo la Kiserikali la FEMINA likitimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake wameeleza kujivunia kwao kwa kufanikiwa kuwafikia vijana wengi zaidi katika kila Wilaya iliyopo Tanzania bara na baadhi ya shule za Visiwani Zanzibar na kutoa elimu ambayo imewasaidia na wengi wao kutoa mirejesho chanya kwa shirika hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa habari wa FEMINA Amabilisi Batamula amesema kuwa hadi sasa kuna klabu zaidi ya 2300 ambazo zimesajiliwa na zinapata majarida, pia kuna muunganiko wa klabu zaidi ya 2900 ambazo ni muunganiko wa klabu za Wilaya, Mikoa na Kanda pamoja na klabu za FEMA za walimu walezi wa klabu hizo zipatazo 38.

Batamula amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shirika hilo wamekuwa wakijikita katika utoaji wa elimu kwa vijana kuhusiana na afya ya uzazi na ujinsia kwa kuwapa stadi za maisha na huwafundisha mbinu ya kusubiri hadi watakapotimiza malengo yao bila kujihusisha na masuala la ngono.

Amesema kuwa FEMINA huwasaidia vijana katika kujikwamua kiuchumi na hiyo ni kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kupata taarifa na wao huzichakata na kuwapa vijana kupitia majarida na kusema kuwa hutoa taarifa kwa vijana juu ya fursa zinazowazunguka na sio kuwapatia fedha wala mitaji.

Pia amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shirika hilo wamekuwa wanawahimiza vijana kushiriki katika mikutano mbalimbali ya vijiji, kata na Wilaya pamoja na kujua haki na wajibu wao katika jamii na kujitolea katika masuala ya kijamii kama vile kufanya usafi katika hospitali, masoko na kujitolea damu pamoja na kupinga tamaduni potofu zikiwemo mimba za utotoni na ukeketaji.

"Wana klabu wa FEMA jijini Dodoma wamekuwa na utaratibu wa kujitolea damu katika hospitali mbalimbali na hata tatizo la damu likitokea wana klabu hutafutwa na kushiriki zoezi hilo ambalo huokoa maisha ya wengi." ameeleza Batamula.

Kuhusiana na njia wanazotumia kuwafikia vijana kote nchini ameeleza kuwa, FEMINA huwafikia vijana hao kupitia jarida la FEMA linalotoka mara nne kwa mwaka na kusambazwa katika shule zote za sekondari zilizosajiliwa kama wana klabu, pia amesema kuwa wanawafikia vijana hao kupitia vipindi vya redio na televisheni na vipindi vingi hufanyika vijijini ili kuwafikia vijana wengi zaidi.

Amabilisi amesema kuwa lazima wazazi pamoja na walezi wawe wawazi kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha kuhusiana na afya ya uzazi pamoja na kukabiliana na changamoto katika ukuaji wao.

Kuhusiana na mchango wa FEMINA katika klabu za FEMA kote nchini Afisa ufuatiliaji na tathimini kutoka FEMINA Martha Samwel amesema kuwa ufaulu kwa shule zenye klabu za FEMA uameongezeka na hiyo ni kutokana na mirejesho wanayoipata kutoka kwa walimu na walezi wa klabu hizo kwani kupitia klabu hizo wanafunzi wamekuwa wakielimishana na kuhimizana kuhusu masomo na katika baadhi ya maeneo wanafunzi watoro darasani wamerudi shule kutokana na nguvu ya klabu za FEMA.

"Kuna baadhi ya shule zimekuwa na misimamo yao ambapo wanakauli mbiu zao za kutoruhusu mwanaklabu ya FEMA afeli darasani, hii inawapa nguvu na ari ya wao kusoma zaidi na hatimaye kufanya vizuri katika masomo yao" ameeleza Martha.Aidha amesema kuwa mafanikio waliyoyapata kwa miaka 20 ni makubwa sana hasa kwa kuwafikia vijana wengi Tanzania kote na kutoe elimu ambayo imewasaidia kwa kiasi kikubwa hivyo wanajivunia kuwa sehemu ya maisha kwa vijana hao.

Pia amewashauri vijana wengine kujiunga na klabu za FEMA ili waweze kupata elimu ya afya na ujinsia pamoja na elimu ya ujasiriamali ambayo itawasaidia katika kujenga taifa na kujenga nchi ya viwanda kwa kuwa wao ndio nguvu kazi ya taifa.

BODI YA WAKUREGENZI DAWASA KUENDELEA KUKAGUA UTOAJI HUDUMA YA MAJI KWA WANANCHI WA DAR NA PWANI

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA),Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ametembelea mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini na kushiriki upandaji wa miti pembezoni mwa chanzo cha Mto Ruvu.

Mwamunyange amepanda mti sambamba na wajumbe wa bodi kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji vya mto Ruvu ikiwa ndio chanzo kikubwa kinachozalisha maji kwa asilimia 88 katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.Akiwa katika ziara yake ya siku ya pili, Mwamunyange ametembelea mtambo huo ikiwa ni mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo.

Mwamunyange ametembelea mtambo huo akiwa ameongozana na wajumbe wa bodi ya DAWASA kuona namna uzalishaji maji unavyoanzia na kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wahandisi wa Mamlaka hiyo.Akizungumza baada ya kumaliza kutembelea mtambo huo, Mwamunyange amesema kiwango kikubwa cha uwekezaji kimefanyika na wataalamu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata maji.

Mwamunyange amesema jitihada kubwa za serikali zinafanyika kuhakikisha wananchi wote wanapata maji hususani kwenye maeneo yaliyokuwa hayana maji kwa kipindi chote kikubwa wananchi wawe wavumilivu kwakuwa DAWASA wanafanya kazi kuwapelekea maji.Baada ya kuwasili katika mtambo huo Mwamunyange alipata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi wa mtambo huo na kuwataka wafanye kazi kwa juhudi kubwa ili kutimiza adhma ya serikali ya kufikia asilimia 95 ya wananchi wote ifikapo 2020.

Mwamunyange amesema, anafahamu kuna changamoto mbalimbali za wafanyakazi ila amewaahidi atazifanyia kazi atakapokutana na Sekretarieti ya DAWASA.Mbali na kutembelea mtambo wa Ruvu Chini, Mwamunyange ametembelea Tenki la maji la Changanyikeni, Busta pampu zilizofungwa Makongo kwa ajili kusukuma maji na maunganisho mapya Salasala.

Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi itaendelea kwenye maeneo mengine tofauti kwa ajili ya kujifunza na kuona namna DAWASA wanavyotoa huduma ya maji kwa wananchi wa Dar esSalaam na Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Mhandisi Arone Joseph walipotembelea mtambo wa Ruvu Chini ikiwa ni ziara ya siku tatu.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka (DAWASA) Jenerali Davis Mwamunyange akipanda miti pembezoni mwa chanzo cha Mto Ruvu wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Mamlaka hiyo.

UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020.

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

UMOJA wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Tanzania kwa upande wa Zanzibar, leo umezindua rasmi kamati ndogo ndogo nne zitakazokuwa na majukumu mbali mbali ya kufanisha kwa ufanisi kazi za umoja huo kwa mwaka 2019/2020.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi alizitaja kamati zilizozinduliwa kuwa ni pamoja na Kamati ya Uchumi, Mipango na Fedha, Kamati ya Mawasiliano kwa Umma, Kamati ya Elimu,Malezi na Mafunzo pamoja na Kamati ya Mahusiano na Taasisi za Wanawake ndani na nje ya Nchi.

Alisema kuwanzishwa kwa kamati hizo ni matarajio makubwa zaidi ni kuwafikia Wanawake na Vijana pamoja na makundi mbali mbali yaliyopo katika jamii na watoto ili kushinda Uchaguzi ujao mwaka 2020.

Katika maelezo yake Makamu Mwenyekiti huyo aliwasisitiza Wajumbe wote wa Kamati hizo kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika utekelezaji wa majukumu ya msingi ya UWT pamoja na CCM kwa ujumla.

“Wanawake ni Jeshi kubwa tena la ukombozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, nasaha zangu kwenu ni kwamba tutumie nafasi hii kuhakikisha tunawafikia wanawake wote hasa waliopo Vijijini na Pembezoni kwa nia ya kuwaweka karibu na kufanya nao shughuli zetu za kisiasa.

Pia Wanawake wa UWT lazima tupate Sauti zetu kila mmoja kwa nafasi yake ndani ya Umoja Wetu kuyasema mambo mema yanayotekelezwa na CCM chini ya Viongozi wetu Wakuu ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wanaoendelea kusimamia kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.”, alisema Makamu Mwenyekiti Thuwayba Kisasi.

Aliwataka Wanawake nchini kushirikiana katika malezi ya Watoto ili waweze kukuwa wakiwa katika malezi na maadili bora yatakayowasaidia kupambana na changamoto za mmomonyoko wa maadili.Awali akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo , alieleza kuwa UWT imejipanga kufanya kazi zake Kisayansi zaidi kwa lengo la kufanikisha kwa wakati malengo waliyojiwekea ndani ya Umoja huo.

Aidha alifafanua kuwa Kamati hizo zilizozinduliwa zitakuwa ni chachu ya kubuni miradi mipya ya kiuchumi itakayoongeza kipato ndani ya UWT pamoja na kupatikana fursa ya mahusiano mazuri na Taasisi mbali mbali za Wanawake Duniani.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati tekelezaji WUT Taifa Ndugu Lucy Mwakembe alisema Umoja huo utaendelea kupanga mikakati mbali mbali ya kimaendeleo ili kujiinua kiuchumi.
MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi akizungumza na Wajumbe wa Kamati ndogo ndogo za Umoja huo mara baada ya kuzinduliwa.
NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo akitoa ufafanuzi wa majukumu mbali mbali ya Kamati hizo ambazo ni nne zilizozinduliwa kutokana na Matakwa ya Kanuni ya Umoja huo.
BAADHI ya Wajumbe wa Kamati ndogo ndogo za UWT Zanzibar zilizozinduliwa leo wakiwa katika Kikao cha Awali cha utambulisho wa Kamati hizo, huko Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui.
Picha ya Pamoja ya Wajumbe wote wa Kamati Nne za UWT zilizozinduliwa.




MKUTA YAWAPATIA WACHIMBAJI ELIMU YA KIFUA KIKUU NA UKIMWI

$
0
0
ILI kutokomeza maambukizi ya kifua kikuu, HIV na Silikosis, kwenye migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wachimbaji 13,328 wamepatiwa elimu ya kujikinga kupitia shirika la mapambano ya kifua kikuu na ukimwi (Mkuta). Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la Mapambano ya kifua kikuu na ukimwi Tanzania (Mkuta) Thobias Magati aliyasema hayo wakati akizungumzia kazi za huduma ya jamii kwa mwaka jana. 

Magati alisema katika watu hao 13,328 waliofikiwa, wanaume walikuwa 11,307 wanawake 1,804 na watoto ni 217 na wagonjwa waliogundulika ni 123. Alisema uwezeshaji ni mdogo kwao kwani hawana wafadhili ila mwaka jana waliwezeshwa na Kibong'oto OHSC kufikia wagonjwa wengi. "Uwezeshaji ndiyo mdogo ila wameweza kufungua matawi ya Mkuta kwenye maeneo ya kitalu B (Opec) na kitalu D ambayo yapo kwenye migodi inayowazunguka ili kusaidia shughuli za uibuaji," alisema Magati. 

Alisema wanafanya hayo ili kufikia malengo ya tamko la kisiasa la umoja wa mataifa la kutokomeza kifua kikuu ifikapo mwaka 2022. Alisema endapo kuna asasi au taasisi yeyote itakayokuwa inataka kuonana nao wawasiliane nao kupitia namba za simu 0789564832 au barua pepe ya mkutaclubmirerani@gmail.com watawapata. Katibu wa Mkuta, Benjamin Kaba alisema wanakabiliwa na changamoto ya wagonjwa wengi wa kifua kikuu, gharama ya ufuatiliaji na kutopata vipimo kwa wakati. 

Kaba alisema changamoto nyingine ni wachimbaji wengi wanaugua ugonjwa wa Silikosis na Pneumonia ambayo yanahitaji kufanyiwa utafiti wa kina zaidi na mabadiliko ya ukuta yamesababisha wagonjwa kushindwa kutoka kwenda kupata huduma.  Alisema changamoto nyingine ni kuhamahama kwa wagonjwa kwenda migodi mingine ya Kitwai, Lemshuku, Mwajanga, Landanai na Kimwengani. 

Alisema wana mikakati mingi yakufanikisha mipango yao ila wanakwamishwa kutokana na ukata unaowakabili kwani hawana mfadhili wa kukisaidia kikundi hicho chenye wanachama 58. Mjumbe wa Mkuta, Mwasiti Ntandu alitoa wito kwa serikali kuiangalia Mirerani kwa jicho la pekee kwani magonjwa ya kifua kikuu na Silikosis inayosababishwa na ulanga imewaathiri watu wengi. Ntandu alisema baadhi ya wachimbaji wamewaacha wajane na yatima kutokana na kuugua maradhi hayo ambayo yanaweza kutibika. 
 Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la Mkuta la Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Thobias Chacha Magati akielezea mikakati ya asasi yao. 
Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la Mkuta la Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Thobias Chacha Magatiakisoma kanuni na sheria za Mkuta. 
Wanachama wa shirika lisilo la kiserikali la Mkuta wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakifurahia pamoja baada ya taarifa ya utekelezaji wa huduma kwa jamii ya mwaka jana. 

WAZIRI WA MAJI PROF. MBARAWA AONGOZA ZOEZI LA KUOTESHA MITI 600 MJI WA SERIKALI, IHUMWA DODOMA

$
0
0
Watumishi wa Wizara ya Maji wamepanda miti katika eneo la Ihumwa kwenye mji wa serikali zoezi lililoongozwa na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa.
Jumla ya miti 600 imepandwa na watumishi wa Wizara pamoja na viongozi akiwemo Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Emmanuel Kalobelo, Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo.
Profesa Mbarawa ameelekeza teknolojia ya kisasa ya umwagiliaji itumike ili miti yote ilipandwa ikue. Amesema kuwa zipo teknolojia mbali mbali za umwagiliaji ambazo wataalamu wetu wanatakiwa kuzijua na kuzitumia.
Zoezi la upandaji miti kwenye kiwanja cha Wizara liliwahusisha wataalamu wa misitu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambayo imetoa miti hiyo ikiwa ni kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani.
Awali, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Kalobelo alisema kuwa, tayari Wizara ya Maji ina kisima kitakachotumika katikaumwagiliaji wa miti na bustani za wizara hivyo miti iliyopandwa itatunzwa kama inavyotakiwa.
Kwa mujibu wa TFS kwa jiji la Dodoma wastani wa asilimia 35 ya miti inayopandwa ndiyo hukua hivyo uangalizi wa karibu ni muhimu kuhakikisha miti yote iliyopandwa inakua. Jumla ya watumishi 300 walishiriki zoezi la upandaji miti katika mji wa Serikali - Ihumwa kwenye kiwanja cha Wizara.
 Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akiotesha mti katika mji wa Serikali, eneo la Wizara ya Maji, Ihumwa jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akiotesha mti katika mji wa serikali, eneo la wizara yake, Ihumwa jijini Dodoma. Profesa Mkumbo amesema miti iliyooteshwa itatunzwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa na tayari maji ya uhakika yapo.
 Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Emmanuel N.M Kalobelo akiotesha mti katika eneo la wizara yake, mji wa serikali Ihumwa jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo (kulia) akikagua eneo la kuotesha miti, katika kiwanja cha Wizara ya Maji, mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma. Kushoto, ni Mhandisi Tamin Katakweba, mmoja kati ya timu ya wizara iliyopo katika neno la ujenzi.
Viongozi wa Wizara ya Maji, kati, Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (Mb), kulia, Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo na kushoto Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Emmanuel N.M Kalobelo, pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maji baada ya kukamilisha kazi ya kuotesha miti 600, katika mji wa serikali Ihumwa jijini Dodoma.

Halmashauri 33 zavuka malengo ya Ukusanyaji wa mapato

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Halmashauri 33  kati ya halmashauri 185 zimeweza kukusanya mapato ya ndani kwa kiwango cha asilimia 50 na zaidi ya makisio ya mwaka wa fedha 2018/19 huku  halmashauri 21 zikiwa zimefanya vibaya kwa kusanya chini ya asilimi 20 ya makisio yake kwa mwaka. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemeni Jafo alipokuwa  akitoa taarifa ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa robo ya pili ya mwaka.

Alisema katika Halmashauri 33 zilizokusanya asilimia 50 na zaidi zimo Halmashauri za  Majiji tatu zikiongozwa na Jiji la Dodoma, Manispaa ni mbili zikiongozwa na manispaa ya Iringa, Halmashauri za Miji nane zikizongozwa na Mji wa Geita na Halmashauri za Wilaya ni ishirini zikiongozwa na Halmashauri ya Wilaya ya Geita. “Uchambuzi unaonyesha kuwa Katika Majiji 6, Jiji la Dodoma linaongoza kwa kukusanya asilimia 59 ya makisio na Jiji la Tanga limekuwa la mwisho kwa kukusanya asilimia 33 ya makisio” alisema.

Aidha Manispaa ya Iringa imeongoza katika kundi la Manispaa kwa kukusanya asilimia 64 ya makisio ambapo Manispaa ya Lindi imekuwa ya mwisho katika kundi hili kwa kukusanya asilimia 20 ya makisio.
Jafo aliongeza kuwa kwa upande wa Halmashauri za Miji, Halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kwa kukusanya asilimia 84 ya makisio na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho katika kundi hili kwa kukusanya asilimia 9 tu ya makisio.

Alisema Katika kundi la Halmashauri za Wilaya, Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeongoza kwa kukusanya asilimia 78 ya makisio ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 6 tu ya makisio.Kwa kuzingatia wingi wa makusanyo ya mapato ya  Halmashauri Jafo alibainisha Halmashauri iliyoongoza kwa kuwa ni Jiji la Dodoma ambalo limekusanya Shilingi Bilioni 40.12 na halmashauri iliyokusanya kiasi kidogo cha fedha ni halmashauri ya Wilaya ya Momba ambayo imekusanya shilingi milioni 105.04.

Waziri Jafo pia alibainisha Mkoa ambao Halmashauri zake zimekusanya mapato kwa kuzingatia wingi wa mapato kuwa ni Mkoa wa Dar es salaam ambao kwa jumla halmashauri zake zimekusanya shilingi bilioni 77.4 na Mkoa wa Mwisho ni Katavi ambao halmashauri zake zimekusanya shilingi bilioni 2.4 tu.

Alisema katika Mkoa uliokusanya vizuri kwa kuzingatia asilimia ya makusanyo ni  Mkoa wa Geita Halmashauri zake zimekusanya asilimia  56.4 ya makisio ya mwaka ukifuatiwa kwa karibu na Mkoa wa Dodoma uliokusanya asilimia 55.9 ya makisio yake na Mkoa wa mwisho kwa kigezo hicho ni Mkoa wa Mtwara ambao umekusanya asilimia 15 ya makisio yake ya mwaka.

Wakati huo huo Waziri Jafo amewataka wakurugenzi wote ambao Halmashauri zao hazikufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwa kukusanya chini ya asilimia kumi ya makisio yake kwa kipindi cha nusu mwaka kujieleza na kujitathimini na kuhakikisha wanaongeza bidii katika suala la ukusanyaji wa mapato.

“Halmashauri 9 kati ya 10 zilizofanya vibaya katika mwaka wa fedha uliopita zimefanikiwa kufanya vizuri katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2018/19 kwa kukusanya zaidi ya asilimia 20 ya makisio yake” alisema .
Waziri Jafo pia aliwaagiza Wakurugenzi wote kuhakikisha takwimu zote za mapato katika mfumo wa LGRCIS zinafanyiwa usuluhisho na kutumwa katika mfumo wa IFMS(Epicor)  kwani taarifa zote za mapato na matumizi ya fedha zinatakiwa kutolewa kupitia mfumo huo.

Ulinganifu huu wa taarifa za mapato umelenga kuonesha jinsi kazi za ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa inavyoendelea kusimamiwa vyema na takwimu hizi zinazotolewa ni kwa mujibu wa taarifa zilizofanywiwa usuluhisho na kutumwa katika mfumo wa IFMS(Epicor).

Katika mwaka wa fedha 2018/19 Halmashaurti zilipangiwa kukusanya shilingi bilioni 735.6 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani na hadi kufikia Disemba 31,2018 Halmashauri zimekusanya shilingi bilioni 300 sawa na asilimia 41 ya makisio.

Kwa kipindi cha kwa mwaka 2017/18 halmashauri zilipanga kukusanya shilingi bilioni 687.3 na hadi  kufikia Disemba,2017 halmashauri hizo zilikuwa zimekusanya  sh bilioni 281.3 sawa na asilimia 41 ya makisio.
Takwimu hizi zinabainisha kuwa kuna ongezeko la Shilingi bilioni 18.7 kwa mwaka wa fedha 2018/19 ikilinganishwa na makusanyo kwa kipindi kama hiki kwa mwaka wa fedha 2017/18.


NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWATAKA KAZI SACCOS KUWA NA MIRADI YENYE TIJA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana) Mhe. Anthony Mavunde ameutaka uongozi wa Kazi SACCOS kubuni miradi yenye tija ili kuboresha mfuko wao na kuleta manufaa kwa wanachama wake. Ametoa rai hiyo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wanachama wa SACCOS hiyo uliofanyika Januari 19, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za TAKWIMU Jijini Dodoma.

Ameutaka uongozi wa chama hicho kubuni miradi ya kimkakati inayotekelezeka na kuendana na mazingira, na hali ya kiuchumi ya eneo husika. “Ni vyema uongozi kuangalia fursa za kiuchumi zilizopo Dodoma ili kuanzisha miradi itakayoendana na hali halisi ya kiuchumi pamoja na kukikwamua chama chenu kuendelea kuwa na tija,” alisisitiza Mavunde.

Lengo la mkutano hilo lilikuwa ni kupeana taarifa za uendeshaji wa chama, kufanya uchaguzi wa viongozi wapya katika bodi ya uongozi na kamati ya usimamizi pamoja na kujadili namna bora ya kuendelea kuboresha Chama hicho ili kuendelea kuwa na tija kwa wanachama wake.

Aidha aliwatoa hofu wanachama kwa kueleza kuwa, uwepo wa vyama hivi ni kisheria na kikanuni za utumishi wa umma na kuwataka kuviheshimu ili kuendelea kuwa wanachama hai. “Ieleweke kuwa ukiwa katika chama hiki, bado upo katika utaratibu na kanuni za utumishi wako hivyo muendelee kufanya vyema katika chama ili kujipatia heshima ndani na nje ya ofisi yako,” alisema Mavunde.

Aliwapongeza viongozi pamoja na wanachama wote kwa mchango wanaoutoa kwa ofisi yake kuzingatia mchango wa Chama kwa watumishi wote. “Ninashawishika na kuona mchango wenu kwetu kama ofisi, kwani mmechangia kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wetu, ambao vinginevyo wangeshindwa kutoa huduma bora yenye tija kwa wadau wetu kutokana na changamoto za kifedha huwenda ingechangia kuwaingiza katika matendo ya utovu wa nidhamu kama vile rushwa”,alisisitiza Mavunde.

Pia aliwataka viongozi wa Ofisi yake kuendelea kuunga mkono jitihada hizo ambazo chama kimezionesha hususani uanzishwaji wa miradi ikiwemo ikiwemo kuwekeza katika viwanda. Naye Omari Sama mwenyekiti wa chama hicho aliunga mkono maagizo hayo kwa kuanzisha miradi endelevu itakayoleta maendeleo ya kiuchumi kwenye chama, kuongeza wanachama na kukifanya chama hiko kitambulike zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa ofisi hiyo, Peter Kalonga aliuasa uongozi mpya kuendelea kutoa elimu ya ushirika kwa wanachama ili kuweza kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Kazi SACCOS Ltd walipokutana Januari 19, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za TAKWIMU Jijini Dodoma.
 Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Dorothy Uwiso akichangia jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Kazi SACCOS Ltd walipokutana Januari 19, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za TAKWIMU Jijini Dodoma.
 Sehemu ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Kazi SACCOS Ltd wakimkaribisha mgeni rasmi wa mkutano huo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akifuatilia Taarifa ya Utekelezaji ya Bodi ya Uongozi wa Kazi SACCOS LTD wakati wa mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Kazi SACCOS Omari Sama akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya Bodi ya Uongozi wa Kazi SACCOS LTD wakati wa Mkutano Mkuu wa SACCOSS hiyo Januari 19, 2019 Ukumbi wa TAKWIMU Dodoma.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu  Peter Kalonga akiwasilisha salamu za Katibu Mkuu wa ofisi hiyo ambaye ndio Mlezi wa Chama wakati wa mkutano huo.
 Baaadhi ya wanachama wa Kazi SACCOS wakifuatili uwasilishwaji wa mada kutoka kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Kazi SACCOS Omari Sama (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.
 Afisa Kazi Wilaya ya kinondoni  Yusuf Nzugile akichangia mada wakati wa mkutano huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu Wanachama wa Kazi SACCOS Januari 19, 2019.Jijini Dodoma.

RAIS DKT. SHEIN AWATAKA WAHITIMU WA VYUO VIKUU KUANZISHA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI ILI WAPATE KUJIAJIRI

$
0
0
Na Ramadhan Ali Maelezo 19/01/2019
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali imeanzisha na kuimarisha Mfuko wa Wajasiriamali ili kuwawezesha vijana kiuchumi katika kukabiliana na tatizo la ajira linalozikabili nchi nyingi duniani ikiwemo Zanzibar.

Amewashauri vijana wanaomaliza Vyuo Vikuu na Elimu ya juu nchini kuunda vikundi vya Ujasiriamali na kufuatilia taarifa za mfuko huo katika Wizara ya Kazi, Uwezesdhaji, Wazee, Vijana na Watoto ili kuitumia fursa iliyopo ya kupatiwa mikopo kwa lengo la kuweza kujiajiri wenyewe.

Dk. Shein alieleza hayo katika Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Bi. Riziki Pembe Juma katika Kempasi ya Chuo hicho Chukwani.

Alisema lengo la kuanzishwa Mfuko huo mwishoni mwa mwaka 2013 ni kuwasaidia wajasiriamali wakiwemo vijana wanaomaliza vyuo na elimu ya juu na wananchi wengine wanaopendelea kujiendeleza kimaisha kwa njia ya kujiajiri wenyewe.

”Kuanzia mwezi Januari hadi Septemba 2018  jumla ya mikopo 441 yenye thamani ya shilingi 685 milioni ilishatolewa kwa vikundi mbali mbali vya ujasiriamali Unguja na Pemba na mikopo zaidi itaendelea kutolewa mwaka huu,” alisema Rais wa Zanzibar.

Alieleza kufurahishwa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Al-Sumait kuanzisha mafunzo maalumu kwa wanafunzi katika mwaka wao wa mwisho wa masomo yenye lengo la kuwapata taaluma na ujuzi unaohitajika katika kukabiliana na soko la ajira na alivishauri Vyuo Vikuu vyengine viliopo Zanzibar kuiga mpango huo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alikipongeza Chuo hicho kwa kazi nzuri ya kuzalisha walimu wenye sifa za juu za kufundisha skuli mbali mbali na wataalamu wengine walioajiriwa katika Taasisi za Serikali na binafsi.

Hata hivyo aliushauri uongozi wa Chuo Kikuu cha  Al Sumait wakati wanajiandaa kuanzisha shahada ya Uzamili ya ‘Islamic Sheria’ kuwa waangalifu na kukaa pamoja na Kamisheni ya Mipango ya Zanzibar ili kupata ushauri na kujua vipaumbele vinavyohitajika katika mahitaji ya taaluma nchini.

Aidha Dk. Shein alipendekeza Vyuo Vikuu vitatu viliopo Zanzibar hivi sasa, Abdulrahman Al-Sumait, SUZA na Zanzibar University cha Tunguu kuunda Kamati ya pamoja kukaa na kubadilishana mawazo kuhusu aina ya programu wanazoanzisha ili kuepuka kuanzisha programu zisizokuwa na uhalisia.

Akizungumza katika mahafali hayo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al-Sumait Professa Amran Rasli aliwanasihi wanafunzi waliomaliza na wanaoendelea na masomo chuoni hapo kuweka umuhimu wa kulipa madeni ya mikopo waliochukua kwa ajili ya masomo.

Aliwakumbusha wanafunzi kuwa deni ni amana na kulipa deni ni ibada hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwa makini na madeni anayodaiwa bila kuangalia kuwa ni deni la Serikali ama la mtu binafsi.

Alisema katika kukiimarisha chuo hicho, wameanzisha programu ya kusomesha wanafunzi wa chekechea ili kuhudumia jamii inayoishi karibu kwa lengo la kujenga umoja na  ushirikiano kati ya chuo na jamii.

Alizitaja hatua nyengine wanazoendelea kuzifanya ni kuimarisha miundombinu, nyenzo, taratibu na sera kwa ajili ya huduma, maslahi na mazinguira mazuri ya wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho.   

Jumla ya Wahitimu 571 wakiwemo 226 wa shahada ya kwanza, 277 wa stashahada na 68 wa cheti walitunukiwa shahada na vyeti vyao baada ya kuhitimu masomo katika taaluma ya ualimu ambapo asilimia 33 ni wahitimu wanawake.
 Gwaride la Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Abrahman Al-Sumait yakingia uwanjani wakati wa Mahafali ya 18 yaliyofanyika kempasi yao, Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Bendi ya Jeshi la Polisi ikitumbuiza katika Mahafali ya 18 ya Chuo Kiuu cha Abdulrahman Al- Sumait kiliopo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Professa Amran Rasli akimkabidhi zawadi mwanafunzi Bora wa mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Al-Sumait, Thuwein Thabit Mzee.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al- Sumait Dk. Abdulrahman Almuhilan akiwatunuku vyeti wahitimu mbali mbali katika Mahafali ya 18 Chuo hicho.
 Baadhi ya wahitimu wa shahada ya kwanza wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al- Sumait wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma (hayupo pichani) katika Mahafali ya 18 ya Chuo hicho yaliyofanyika Chukwani, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  Baadhi ya waalikwa waliohudhuria Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al- Sumait Chukwani Mjini Zanzibar wakifuatilia mahafali hayo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma akiwahutubia wahitimu na wahadhiri pamoja na waalikwa waliohudhuria mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait kiliopo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Picha na Makame Mshenga.     

Bilioni 3.5 kujenga makazi ya Askari Dodoma

$
0
0
Jumla ya nyumba Mia Moja za Makazi ya Askari zimeanza kujengwa  mkoani Dodoma  ikiwa ni Mpango  wa  serikali  kukabiliana na changamoto za makazi ya  Askari Polisi watakaohamia hivi karibuni baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kutekeleza agizo la kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani hapa

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama kutembelea eneo la Medeli Mashariki ambapo Awamu ya Kwanza ya mradi huo ukihusisha nyumba 30, Ujenzi wa Shule ya Awali, Ujenzi wa Kantini, Ujenzi wa Viwanja vya Michezo tayari imeshaanza

“Ujenzi wa nyumba hizi unakwenda sambamba na ujenzi wa nyumba kama hizi katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha askari wanaishi sehemu safi na lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha ujenzi wa nyumba kama hizi  kote nchini unafanyika kwa gharama nyepesi na tukitumia wataalamu wa ujenzi waliopo serikalini na katika Jeshi la Polisi..” alisema Masauni

“…..mradi huu utakua na awamu tatu ambapo mwezi April mwaka jana, awamu ya kwanza ilianza na kutarajiwa kukamilika April mwaka huu huku awamu zilizobakia zikitarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu na  hadi kufikia mwaka kesho katikati awamu zote zitakua zimekamilika” aliongeza Masauni

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Mussa Zungu amewapongeza Viongozi wa wizara na Jeshi la Polisi kwa mradi huo huku akishauri miradi mingine wajenge maghorofa ili kuweza kuitumia ardhi waipatayo kwa matumizi mengine sambamba na ujenzi wa makazi ya askari.

“Nawapongeza kwa kutumia mapato yenu wenyewe ya ndani kuanzisha miradi mikubwa kama hii na sisi wajumbe wa kamati tumeridhishwa na hatua hizi za kukabiliana na makazi ya wapiganaji wetu wanaotulinda usiku na mchana na nchi yetu kuendelea kuwa na amani,” alisema Zungu

Jumla ya gharama ya mradi huo wa nyumba Mia  Moja za Makazi ya Askari Polisi ni Bilioni Mia Tatu na Laki Tano ambazo zinatokana na Mfuko wa Tuzo na Tozo ikiwemo malipo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na askari polisi na faini zinazotozwa na askari kwenye makosa mbalimbali.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akitoa maelezo ya Ujenzi wa Nyumba mia moja kwa ajili ya makazi ya askari polisi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Medeli, jijini Dodoma zinapojengwa nyumba hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Zungu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Mussa Zungu akimuuliza maswali Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) wakati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea eneo la Medeli, jijini Dodoma zinapojengwa nyumba mia moja kwa ajili ya makazi ya askari polisi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) akiongozana na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Medeli,jijini Dodoma zinapojengwa nyumba mia moja(pichani) kwa ajili ya makazi ya askari polisi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akiwaongoza  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Ihumwa ,jijini Dodoma yanapojengwa Makao Makuu ya wizara hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Baadhi ya nyumba  zinazojengwa katika eneo la Medeli ikiwa ni mkakati maalumu wa Serikali ya Awamu ya Tano kujenga makazi ya askari polisi nchi nzima ili kuwaondolea askari changamoto za makazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAANZA KUUGEUKIA UTALII WA FUKWE

$
0
0
NA LUSUNGU HELELA- KIBAHA
Wizara  ya Maliasili na Utalii, imeanza kuyatambua na kuainisha maeneo kwa ajili ya utalii wa Fukwe katika Kisiwa cha Mafia mkoani Kibaha kwa ajili ya kuhamasisha Wawekezaji kuchangamkia fursa ya ujenzi wa Hoteli za kitalii ili kuwavutia watalii kutembelea katika kisiwa hicho.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwaka jana kwa Wizara hiyo  kuwa ianzishe Kurugenzi ya Fukwe itakayokuwa na jukumu la kusimamia na kuendeleza  Fukwe zote nchini.

Lengo likiwa ni kuhakikisha mapato yatokanayo na sekta ya Utalii kupitia Utalii wa Fukwe yanaongezeka kwa mfano Kisiwa cha Mafia ni cha tano duniani kwa uzuri wa vivutio vya utalii na rasilimali bahari na  cha pili barani Afrika, Hivyo kina sifa kemkem za kuongeza pato la Taifa zaidi.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya siku mbili kisiwani humo ya kutembelea Fukwe pamoja na magofu ya kale,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu  amesema Wizara imejipanga kikamilifu kwa ajili kuwasaidia  Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye Fukwe kwa ajili ya utalii.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Kanyasu alitembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii vilivyopo kisiwani humo ukiwemo Msitu wa Mlola, Magofu na fukwe katika kijiji cha Kanga  pamoja na maeneo ya uwekezaji ya Ras Mlundo Jojo, Banja, Rasini Kanga na Tembo Unyama.

Hata hivyo, Baada ya ziara hiyo Naibu Waziri huyo alisema kuwa baadhi ya wamiliki wa maeneo hayo ya fukwe yamefanya kuwa mashamba ilhali ni kivutio kikubwa cha utalii ambapo baadhi ya nchi zimekuwa ziikingiza fedha nyingi za kigeni kupitia utalii wa fukwe.

Aidha, Kanyasu amewataka wananchi wanaomiliki maeneo karibu na Fukwe kuyatumia kwa ajili ya utalii wa fukwe  badala ya kuyageuza kuwa  mashamba.

Amesema kuwa watalii walio wengi kutoka nje za nchi mara baada ya kutembelea Hifadhi za Taifa kama vile Serengeti Mikumi, husafiri kwenda Msumbiji au Zanziba' kwa ajili ya kutembelea Fukwe ilhali kuna fukwe nzuri mbali na Kisiwa cha Mafia ambazo hazijaweza kuendelezwa

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo, Shaib Nnunduma alieleza kuwa wilaya yake inawakaribisha Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika wilaya hiyo na kuahidi kuwa atatoa ushirikiano wa kutosha.

Aliongeza kuwa Wilaya hiyo tayari imeshatenga maeneo kwa ajili ya Wawekezaji kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli za kiutalii katika maeneo ya ufukweni.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ( watatu kulia)  akiwa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama akipewa maelezo na Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi, Maliasili na Utalii, Juma Hassan kuhusu eneo la fukwe lililotengwa kwa ajili ya  uwekezaji  wa  ujenzi wa Hoteli za kitaliii wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kwa ajili ya kuhamasisha utalii wa Fukwe katika wilaya ya Mafia mkoani Kibaha. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mafia, Mohammed Kongo wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea maeneo ya fukwe ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwaka jana kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa 
ianzishe Kurugenzi ya Fukwe 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Constantine Kanyasu akishuka kwenye ndege  ndogo wakati alipowasili  wilayani Mafia mkoani Kibaha  kwa ajili ya kutembelea maeneo ya fukwe kwa ajili ya uwekezaji wa Utalii
 Baadhi ya rasilimali bahari maarufu kwa jina la  Matumbawe ambayo ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika kisiwa cha Mafia mkoani Kibaha
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu (  kulia)  akiwa ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Mafia pamoja na kamati ya ulinzi na usalama  wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya fukwe yanayofaa kwa ajili ya uwekezaji lengo likiwa ni kuhasisha utalii wa fukwe 
 Moja ya magogfu ya kale lililojengwa karne ya 18 ambalo linapatikana pembezoni mwa fukwe katika kisiwa cha Mafia mkoani Kibaha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mafia. Erick Mapunda akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu kabla hya kufanya ziara ya kutembelea maeneo ya fukwe kwa ajili ya uwekezaji wa utalii.  

  (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)

Mtumishi wa TANROADS kizimbani kwa tuhuma za Rushwa

$
0
0
Na Emanuel Madafa, Mbeya 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Mkoa wa Mbeya, imemfikisha Mahakamani mtumishi wa Wakala wa Barabarani(TANROADS) kwa tuhuma za kupokea rushwa ya shilingi 597,000.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Kiyano, alisema mtumishi huyo akiwa msimamizi wa mzani wa kupima magari uliopo eneo la Uyole Jijini Mbeya, alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mtumishi wa Kampuni ya Kichina iitwayo Chongqing Foreign Trade Economic Corporation.

Amesema Kesi hiyo namba CC. 189/ 2018 imefunguliwa katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya, chini ya kifungu cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 dhidi ya mtumishi huyo wa umma Zabron Zebeda Kenan.

Ameeleza kuwa mtumishi huyo wa Kampuni ya Kichina, Onesphory Ngonyani, inasemekana alitoa kiasi hicho cha fedha ili gari aina ya Howo lenye namba za usajili T 755BZC na Tela namba T587BPY lililokuwa halina kibali cha mzigo wenye upana usio wa kawaida(Abnomal Wide Loard) lipite kwenye mzani huo bila ya kukamatwa.

Aidha,Mkuu huyo amesema , Taasisi hiyo inaendelea kumtafuta mtumishi wa Kampuni ya Kichina, Onesphory Ngonyani kwani alifanikiwa kutoroka baada ya kutoa hongo hiyo, huku gari yake aina ya Toyota Carina lenye namba  T108 BQH likishikiliwa na ofisi hiyo ya TAKUKURU.

"Baada ya kutoa fedha hiyo Ngonyani alitoweka na kukimbilia Mahali pasipo julikana ambapo tulifanikiwa kumamata gari anayo tumia hivyo tunamtaka afike na achukue gari lake "Alisema Kiyabo.

Hata hivyo, alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa gari hiyo, iliponunuliwa haikubadilishwa umiliki wake hivyo kuna fedha ya serikali inatakiwa kulipwa kama ada ya kuhamisha umiliki na endapo ataendelea kujificha chombo hicho cha moto kitapigwa mnada ili kufidia gharama za serikali.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Takukuru Mbeya amesema katika roho ya Tatu ya mwaka 2018/2019 taasisi hiyo imeendelea kuchambua mifumo katika utendaji wa serikali ,mashirika ya umma na sekta binafsi kwa lengo la kuzuia mianya ya rushwa .

TIMU 128 ZA WAENDESHA BODABODA ZAPAMBANA KATIKA MICHUANO YA USALAMA BARABARANI(KAMANDA CUP)

$
0
0
 Mrakibu wa jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha elimu Tanzania, Abel Swai. (Kushoto) akifafanua jambo   kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kiraia ya Haki elimu Tanzania,   Dkt. John Kalage , (katikati) na Meneja Uhusiana na Mawasikiano wa GSM Tanzania, Matina Nkurlu wakati wa hafla ya uzinduzi mashindano ya Usalama barabarani ‘Kamanda Cup’  katika viwanja vya Tanganyika Pakers  jijini Dar es Salaam.Jumla ya timu 128 za waendesha bodaboda wa mkoa wa Dar es Salaam zinashiriki , Lengo la michuoano hiyo ni kutoa elimu kwa madereva wa vyombo vyamoto,  mashindano hayo yameandaloiwa na jeshi la Polisi kwa udhaminiwa na kamapuni ya GSM Tanzania.
Meneja Uhusiana na Mawasikiano wa GSM Tanzania, Matina Nkurlu  akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi mashindano ya Usalama barabarani ‘Kamanda Cup’  katika viwanja vya Tanganyika Pakers  jijini Dar es Salaam.Jumla ya timu 128 za waendesha bodaboda wa mkoa wa Dar es Salaam zinashiriki , Lengo la michuoano hiyo ni kutoa elimu kwa madereva wa vyombo vya moto,  mashindano hayo.
  Mrakibu wa jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha elimu Tanzania, Abel Swai. (Kushoto)  akikabidhiwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kiraia ya Haki elimu Tanzania,   Dkt. John Kalage boksi lenye  vipeperushi vyenye ujumbe wa usalama barabarabani   wakati wa hafla ya uzinduzi wa  mashindano ya Usalama barabarani ‘Kamanda Cup’  uliofanyika kwenye  viwanja vya Tanganyika Pakers  jijini Dar es Salaam.Jumla ya timu 128 za waendesha bodaboda wa mkoa wa Dar es Salaam zinashiriki , Lengo la michuano hiyo ni kutoa elimu kwa madereva wa vyombo vyamoto,  mashindano hayo.
 Kamishina Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Operesheni Kikosi cha Usalma barabarani Makao Makuu ,Abdi Issango, ( Kulia )  akiongozwa na Mrakibu wa jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha elimu Tanzania, Abel Swai (wapili kulia) kwenda kuzindua michuoano ya  Usalama barabarani” Kamanda Cup” inayofanyika  kwenye  viwanja vya Tanganyika Pakers  jijini Dar es Salaam.Jumla ya timu 128 za waendesha bodaboda wa mkoa wa Dar es Salaam zinashiriki , Lengo la michuoano hiyo ni kutoa elimu kwa madereva wa vyombo vyamoto,  mashindano hayo.
  Kamishina Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Operesheni Kikosi cha Usalama barabarani Makao Makuu ,Abdi Issango, ( Kulia ) akisalimiana na  Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa GSM ,Matina Nkurlu.  Wakati wa uzinduzi wa michuoano ya  Usalama barabarani” Kamanda Cup” inayofanyika  kwenye  viwanja vya Tanganyika Pakers  jijini Dar es Salaam.Jumla ya timu 128 za waendesha bodaboda wa mkoa wa Dar es Salaam zinashiriki , Lengo la michuoano hiyo ni kutoa elimu kwa madereva wa vyombo vyamoto,  mashindano hayo yameandaloiwa na jeshi la Polisi kwa udhaminiwa na kamapuni ya GSM Tanzania.Kushoto ni Mrakibu wa jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha elimu Tanzania, Abel Swai.





WAHITIMU WA USTAWI WA JAMII KISANGARA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

$
0
0
 Wahitimu wa taaluma ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kilichoko wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na miiko ya taaluma yao ili kujitofautisha na watumishi wengine kutokana na elimu waliyoipata.

Rai hiyo imetolewa na Kamishina wa Ustawi wa Jamii Kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Dkt. Naftali B. Ng’ondi wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kwa wahitimu kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Dkt. Ng’ondi amesema kuwa wataalam mbalimbali wamekuwa wakivamia kazi za Ustawi wa Jamii kwa kudhani kuwa ni kazi holela kuweza kufanywa na mtu yeyote na  kuwakumbusha wahitimu kuwa kazi za ustawi wa jamii ni muhimu na inapaswa kufanywa na wataalam wenye weledi wanatoa huduma kwa kuzingatia maadili na miiko ya kazi.

 Amekipongeza Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kwa kuonesha mafanikio chanya kwani kmwaka wa masomo 2016/2017 wakati chuo kinaanza kulikuwa na wanafunzi 56 tu. Lakini kwa mwaka wa masomo 2018/2019 chuo kimedahili wanafunzi 158 ambapo  wanafunzi wa kike ni 115 na wa kiume ni 43 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100 katika udahili ukilinganisha na mwaka 2016/17.

Kamishna Ngondi amepongeza jitihada uongozi wa Chuo kwa kufanikisha usajili wa kudumu Chuo na mtaala kutolea mafunzo na huduma bora inayotolewa na Chuo katika kusimamia mafunzo na kuongeza nyenzo mbalimbali za kutolea mafunzo kama kompyuta na projector jambo ambalo limekuwa chachu ya ongezeko la udahili wa wanafunzi.

“Wizara inatambua changamoto zilizopo za uchakavu na miundombinu ya madarasa na mabweni hiyo tutaendelea kuimarisha na kukarabati majengo ya chuo ili kuwa na mazingira bora zaidi ya kusomea na kujifunzia”.alisema Dkt. Ng’ondi.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Anna Mwingira amewapongeza wazazi  na walezi kwa kuthamini utoaji wa fursa sawa kwa wasichana na Mtoto wa kike na kuwezesha udahili wa wanafunzi wa kike kufikia asilimia 73 ukilinganisha na asilimi 43 ya wavulana, ongezeko ambalo ni takribani ni mara mbili zaidi ya wavulana.

“Hii ni dalili njema kuwa jamii inaendelea kuelewa azma ya Serikali ya kuwawezesha wanawake ili kuwapa mbinu na stadi za kuweza kutoa mchango katika kufikia uchumi wa kati na wa viwanda’’ aliongeza.

Aidha Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa jamii Kisangara Anna Mwingira alieleza kuwa awali kuanzia mwaka 1986 hadi mwaka 2012 chuo kilikuwa kinatoa mafunzo kwa ngazi ya cheti katika fani ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya mtoto (ECD, Non NTA level). Kuanzia Julai 2012 mafunzo katika fani ya ustawi wa jamii pia yalianza kutolewa katika ngazi ya cheti kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, American International Health Alliance (AIHA) na Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama (Institute of Social Work D’SALAAM – ISW).

 Mwingira ameleza kuwa Chuo kina usajili wa kudumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) uliopatikana mnamo tarehe 29/3/2017 na Na.  REG/BTP/009 kwa kozi ya Ustawi wa Jamii ngazi ya Astashahada hadi ngazi ya Diploma na kwa sasa Chuo kinatoa mafunzo katika fani ya ustawi wa Jamii ngazi ya Cheti na Diploma (NTA Level 4, 5 and 6) na fani ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (ECD) ambayo inasimiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Chuo kinaendesha amsomo kwa kutumia mtaala wake wa fani ya ustawi wa jamii, ambao ulikamilika mwaka 2016/2017.

Naye mmoja wa wahitimu Immaculate Kinama na Elizaberth Kawishe kwa wakati tofauti walibainisha kuwa wamejengewa weledi kwani wanayo maarifa, mbinu na stadi za kuwawezesha kufanya majukumu yao kwa umahiri katika kusaidia wahitaji kama vile watu wenye ulemavu, wazee, watoto na makundi yote yenye uhitaji maalum katika jamii.

Taaluma ya ustawi wa jamii msingi wake ni haki na ustawi katika jamii ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma na kubaguliwa ama kutengwa katika huduma mbalimbali za maendeleo ya jamii husika. Pia, taaluma hii ni muhimu katika kuwasaidia watu walio katika makundi tete mfano wanaonyanyaswa, wanaonyanyapaliwa na maskini sana ili waweze kufaidika na rasilimali au huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu, afya, shughuli za kiuchumi, burudani na shughuli mbalimbali katika jamii na kupata habari kwa mfano kwa watu wasiosikia.

Haya ni Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii kisangara baada ya kupita miaka 33 bila kusanyiko la mahafali. Wahitimu 158 wametunukiwa vyeti katika ngazi ya Astashahada wakiwa na wajibu wa  kuwezesha huduma za ustawi wa jamii katika ngazi ya kata, mashule ya awali, msingi sekondari, na maeneo mengine kama vile Ofisi za Polisi, Mahakama, Magereza na katika jamii kwa ujumla.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto (Idara kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. Naftali B. Ng’ondi akimtunuku cheti kwa mmoja wa wanafunzi wahitimu wa Astashahada ya Ustawi wa Jamii Esher Reubeni katika Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Kilimajaro.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali B. Ng’ondi akiwahutubia wahitimu na halaiki ya watu waliohudhuria kusanyiko la mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara mkoani Kilimanjaro.
 Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kilichoko Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Anna Mwingira akieleza mafanikio ya Chuo  hicho katika Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Kilimajaro.
 Baadhi ya  ndugu na jamaa wa wahitimu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi katika Mahafali ya Chuo cha hichoa ambaye ni Kamishina wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali B. Ng’ondi katika Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Kilimanjaro.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. Naftali B. Ngondi akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara wakati wa Mahafali ya kwanza ya Chuo hicho. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

AFISA ELIMU ASIMAMISHWA KAZI ARUSHA

$
0
0
Na Vero Ignatus, Arusha. 

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemsimamisha kazi Ofisa elimu wa mkoa huo Gift Kyando kwa madai ya kuzuia wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza huku akilazimisha kila darasa kuwa na wanafunzi 40 tu.  Pia anadaiwa kusababisaha wanafunzi hao kukosa nafasi za masomo kwa kukataa kusajiliwa kwa shule mbili mpya za Oldonyowasi na Losikito kwa madai ya kukoda mahabara.

Gambo amesema kitendo hicho ni cha kukwamisha juhudi za serikali kupitia ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuwa uamuzi aliouchukua Ofisa huyo haukumuhusisha kiongozi yeyote yule wa serikali ngazi ya wilaya au mkoa. Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha Dk. Wilson Mahera amesema kitendo hicho alichokifanya  ofisa huyo kiliwachanganya na kusababisha ugomvi kati yao na   wazazi wa wanafunzi hao 

Amesema ofisa huyo angesababisha wanafunzi 6,819 kukosa elimu  wakati yapo madarasa ambayo yaliachwa na wanafunzi waliohitimu kidato cha nne ambayo yangeweza kutumiwa na wanafunzi hao
'' Madarasa yaliyopo yangeweza kuchukua wanafunzi  kwa kipindi kifupi wapatao 55 kwa darasa moja '' alisema Mahera

Dkt. Mahera amesema kuhusu mapokezi  wanafunzi kati ya shule 4239 wameshapokelewa katika shule 28 za halmashauri ya Arusha wakiwemo  wavulana 1,853 na wasichana 2,386 ambao ni sawa na asilimia 62 huku waliobakia wakiendelea kuripoti na wengine wakichukua fomu za kujiunga. 

Kwa upande wake Mwenyakiti wa CCM mkoa Loata Sanare amesema alichokiona ni hujuma za waziwazi kwa ofisa huyo  dhidi ya serikali na kutaka kuzuia wanafunzi wasianze masomo. Sanare anasema alianza kupokea simu za malalamiko kutoka kwa wazazi wawanafunzi hao na alipompigia ofisa elimu huyo alimjibu majibu ambayo hayakumridhisha ndipo alipoamua kuwasikiana na mkuu wa mkoa. 

SERIKALI YATOA MAAGIZO KWA WAFUGAJI

$
0
0


Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akizungumza na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Singida kabla ya kuanza ziara ya uhamasishaji wa kuogesha ng'ombe katika kijiji cha Mgori.
Bw.Rashid Mandoa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Singida akitoa taarifa kwa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega.
Bw.Elia Digha,Mwenyekiti wa halmashauri ya Singida akitoa ujumbe kwa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega (hayupo pichani)kuhusu kuweka mikakati katika sekta ya mifugo nchini.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akikagua ng'ombe katika kijiji cha Mgori kilichopo Singida vijijini alipokuwa ameenda kuzindua zoezi la uhamasishaji wa kuogesha mifugo.
Baadhi ya ng'ombe wakisubiri kuogeshwa dawa katika josho la Mgori katika hamshauri ya wilaya ya Singida vijini ambapo Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alizindua zoezi la uhamasishaji wa kuogesha mifugo.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akichanganya dawa za kudhibiti magonjwa ya mifugo katika kijiji cha Mgori kwa ajili ya kuhamasisha kuogesha ng'ombe katika majosho yalipo nchini ambapo Serikali imeamua kutoa dawa bure kwa wafugaji.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akisaidiana na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo katika josho lenye dawa ambazo zimetolewa bure na Serikali zoezi hilo la uzinduzi katika mkoa wa Singida lilifanyika katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya Singida vijijini.Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog



Na.Alex Sonna,Singida

Serikali imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya mifugo pamoja na kudhibiti magonjwa ya mifugo huku ikiwahimiza wafugaji kuzingatia matumizi ya majosho yenye dawa.

Akizungumza na wafugaji Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega wakati wa zoezi la uhamasishaji wa uogeshaji wa ngo’mbe kanda ya kati mkoani Singida, katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya Singida vijijini.

Katika uhamasishaji huo waziri Ulega aliwataka wafugaji kufanya zoezi la uogeshaji wa mifugo uliyoanzishwa uwe wenye tija na endelevu, kwa vile hivi sasa hakuna sababu za kushindwa kuogesha mifugo yao katika majosho yenye dawa ya kudhibiditi kupe.

Aidha amesema kuwa kwa sasa serikali katika zoezi hili, imetoa dawa bure kwa halmashauri zote nchini, na kukarabati majosho yote yaliyokuwa hayafanyi kazi, ili wafungaji waweze kuogesha mifugo yao , kukinga ugonjwa hatari unaoenezwa na kupe, ambao unaoongozwa katika vifo vya ng’ombe hapa nchini.

"Mwanzo shughuli hizo zilikuwa zikifanywa kwa ,kutofuata taratibu nzuri za makusanyo yalikuwa yakitoka kwa wafugaji walipokuwa wakipata huduma za kuongesha mifugo yao, hazikuwa na taarifa ya mapato na matumizi na hivyo kushindwa kuwa na utaratibu endelevu wa shughuli hiyo, majosho mengi yalisimama kufanya kazi"amesema Ulega

Katika kampeni hii ya uhamamishaji wa uongeshaji wa mifugo tozo imepunguwa ambapo hivi sasa kila ng’ombe ana ogeshwa katika majosho ni shilingi 50 tu, huko nyuma uogeshaji ulikuwa unatozwa wastani wa shilingi mia 2 kwa kila ngo’mbe na kwa mbuzi ilikuwa shilingi 10.

“Nyie wafugaji msikalie rasialimali hii ya mifugo mliokuwa mnayo, kwani ni uchumi mkubwa sana mliyokuwa nayo kwenu na pia kwa Taifa ili kuongeza mapato, yanayotokana na mifugo yenu”amesisitiza Ulega.Aidha alifafanua kuwa ufungaji kwa kufuata taratibu za ufugaji wa kisasa na kibiashara kwa kuvuna mifugo inapozidi katika eneo uliyokuwa nayo, itakusaidia kupata kipato katika kuboresha maisha yako na ya familia.

Uhamasishaji huu unafuatia uzinduzi wa kampeni ya uogeshaji wa mifugo,iliyofanywa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina katikati ya mwezi jana katika kijiji cha Buzirayombo halmashauri ya chato.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images